• Ukraine Import Data – Decode Shipments & Market Dynamics

    Unlock powerful trade insights with Ukraine Import Data from Import Globals – track shipments, spot traits, and stay beforehand in global markets.
    With Import Globals, get entry to real-time Ukraine Import Data to decode market dynamics and make smarter enterprise selections instantly.

    Contact No: +91-9999887320
    Email: [email protected]
    Website: https://www.importglobals.com/
    Page: https://www.importglobals.com/Ukraine-Import-Data

    #ukraineimportdata #importglobals
    Ukraine Import Data – Decode Shipments & Market Dynamics Unlock powerful trade insights with Ukraine Import Data from Import Globals – track shipments, spot traits, and stay beforehand in global markets. With Import Globals, get entry to real-time Ukraine Import Data to decode market dynamics and make smarter enterprise selections instantly. Contact No: +91-9999887320 Email: [email protected] Website: https://www.importglobals.com/ Page: https://www.importglobals.com/Ukraine-Import-Data #ukraineimportdata #importglobals
    www.importglobals.com
    Import Globals is a leading Global Import Export Trade Data Provider for 100+ Countries. Get the Latest Import Export Data, and Customs Import Export Data Online.
    0 Commenti ·0 condivisioni ·432 Views
  • Rais wa Nchi ya Ukraine , Volodymyr Zelensky, ametabiri kuea Rais wa Urusi , Vladimir Putin, "atakufa hivi karibuni" huku kukiwa na tetesi kuwa afya ya Kiongozi huyo wa Urusi inazorota. Zelensky alitoa kauli hiyo katika mahojiano na Waandishi wa habari Jijini Paris, Ufaransa baada ya kukutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kusema kuwa "Putin atakufa hivi karibuni, na hilo ni jambo la uhakika."

    Picha za Putin zilizochunguzwa kwa muda zimezua uvumi kuhusu hali yake ya afya, hasa baada ya kuonekana na macho mekundu na alama ya ajabu kwenye mkono wake. Aidha, picha zingine zimeonyesha kovu shingoni mwake, likizua dhana kuwa huenda alipitia upasuaji wa saratani ya tezi dume.

    Ripoti za awali zilidai kuwa Putin alikuwa akifuatana mara kwa mara na Daktari bingwa wa saratani, huku uvujaji wa taarifa za kijasusi za Marekani ukionyesha kuwa alikuwa akipokea tiba ya saratani. Sanjari na hayo, amekuwa akionekana akiwa na miguu isiyo imara, akishika meza kwa nguvu, au akitikisa mguu wake mara kwa mara, hali inayoongeza mashaka kuhusu afya yake.

    Rais wa Nchi ya Ukraine 🇺🇦, Volodymyr Zelensky, ametabiri kuea Rais wa Urusi 🇷🇺, Vladimir Putin, "atakufa hivi karibuni" huku kukiwa na tetesi kuwa afya ya Kiongozi huyo wa Urusi inazorota. Zelensky alitoa kauli hiyo katika mahojiano na Waandishi wa habari Jijini Paris, Ufaransa 🇫🇷 baada ya kukutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kusema kuwa "Putin atakufa hivi karibuni, na hilo ni jambo la uhakika." Picha za Putin zilizochunguzwa kwa muda zimezua uvumi kuhusu hali yake ya afya, hasa baada ya kuonekana na macho mekundu na alama ya ajabu kwenye mkono wake. Aidha, picha zingine zimeonyesha kovu shingoni mwake, likizua dhana kuwa huenda alipitia upasuaji wa saratani ya tezi dume. Ripoti za awali zilidai kuwa Putin alikuwa akifuatana mara kwa mara na Daktari bingwa wa saratani, huku uvujaji wa taarifa za kijasusi za Marekani 🇺🇸 ukionyesha kuwa alikuwa akipokea tiba ya saratani. Sanjari na hayo, amekuwa akionekana akiwa na miguu isiyo imara, akishika meza kwa nguvu, au akitikisa mguu wake mara kwa mara, hali inayoongeza mashaka kuhusu afya yake.
    0 Commenti ·0 condivisioni ·1K Views
  • Rais wa Marekani , Donald Trump ametupilia mbali madai kwamba Nchi ya Urusi imekataa mapendekezo ya Nchi yake ya Marekani ya kusitisha mapigano Nchini Ukraine . Kiongozi huyo wa Marekani alionyesha kwa ufanisi kuwa ni mapema kujadili kuimarisha vikwazo vya Nchi ya Marekani dhidi ya Urusi.

    "Yeye (Rais wa Urusi Vladimir Putin ) hakukataa chochote. Na wana vikwazo," - Donald Trump aliwaambia Waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani (White House), akijibu swali ikiwa Marekani inapaswa kuimarisha vikwazo dhidi ya Urusi kwa sababu madai ya Putin kukataa usitishaji vita Nchini Ukraine.

    "Wana takriban vikwazo zaidi kuliko mtu yeyote," aliongeza

    Putin na Trump walipiga simu mnamo Machi 18, 2025 wakijadili wazo la kusitisha mapigano kwa siku thelathini katika mzozo wa Ukraine, njia za kuzuia kuongezeka zaidi kwa mvutano na masuala kadhaa ya kimataifa, Kremlin ilisema. Kulingana na maelezo yake ya wito huo, Kiongozi huyo wa Urusi aliunga mkono mpango wa Rais wa Marekani wa kusitisha mapigano ya nishati na miundombinu Nchini Ukraine.

    Ikulu ya White House ilisema katika usomaji huo kwamba Viongozi hao wawili pia walikubaliana kuanza mazungumzo ya kiufundi "juu ya utekelezaji wa usitishaji vita wa baharini katika Bahari Nyeusi, usitishaji kamili wa mapigano na amani ya kudumu."

    Rais wa Marekani 🇺🇸, Donald Trump ametupilia mbali madai kwamba Nchi ya Urusi 🇷🇺 imekataa mapendekezo ya Nchi yake ya Marekani ya kusitisha mapigano Nchini Ukraine 🇺🇦. Kiongozi huyo wa Marekani alionyesha kwa ufanisi kuwa ni mapema kujadili kuimarisha vikwazo vya Nchi ya Marekani dhidi ya Urusi. "Yeye (Rais wa Urusi Vladimir Putin ) hakukataa chochote. Na wana vikwazo," - Donald Trump aliwaambia Waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani (White House), akijibu swali ikiwa Marekani inapaswa kuimarisha vikwazo dhidi ya Urusi kwa sababu madai ya Putin kukataa usitishaji vita Nchini Ukraine. "Wana takriban vikwazo zaidi kuliko mtu yeyote," aliongeza Putin na Trump walipiga simu mnamo Machi 18, 2025 wakijadili wazo la kusitisha mapigano kwa siku thelathini katika mzozo wa Ukraine, njia za kuzuia kuongezeka zaidi kwa mvutano na masuala kadhaa ya kimataifa, Kremlin ilisema. Kulingana na maelezo yake ya wito huo, Kiongozi huyo wa Urusi aliunga mkono mpango wa Rais wa Marekani wa kusitisha mapigano ya nishati na miundombinu Nchini Ukraine. Ikulu ya White House ilisema katika usomaji huo kwamba Viongozi hao wawili pia walikubaliana kuanza mazungumzo ya kiufundi "juu ya utekelezaji wa usitishaji vita wa baharini katika Bahari Nyeusi, usitishaji kamili wa mapigano na amani ya kudumu."
    0 Commenti ·0 condivisioni ·795 Views
  • "Sijui kama mnaona jinsi Trump na Marekani yake wanavyocheza na Dunia kupitia ugomvi au migogoro ya Dunia ili kuipatia faida Marekani kwa kisingizio cha kutafuta amani huku nyuma ya pazia Marekani ikipata faida kupitia migogoro au vita.

    Tazama Makubaliano ya Madini pale Ukraine
    Ambapo Marekani watafaidika na Rasilimali za madini za Ukraine, yani ili Marekani waisadie Ukraine ni lazima Ukraine kuipatia madini yake Marekani

    Congo nayo inakaribia kusaini mkataba wa kuipatia Marekani madini ili Marekani iipatie ulinzi hapo tunazungumzia rasimali za Congo amabzo zinaenda kutumika kama faida kwa Marekani kisa tu ni ugomvi wa Afrika wenyewe kwa wenyewe na hapo hapo Trump katupiga Bao

    Huko Gaza napo mpango wa kuwahamisha wakazi wa Gaza kwa kisingizio cha kuijenga upya Gaza umeiva, Trump haijengi Gaza bure anafahamu fika kuwa chini ya ardhi ya Gaza kuna utajiri mkubwa wa maliasili ya Gesi na mafuta

    Huyo ndiye Trump mfanyabiashara kutoka White House ambaye anaenda sambamba na ule msemo unaosema "no free lunch in America" yaani hakuna chakula cha mchana cha bure Marekani, ukiona unapewa cha bure ujue badae utalipia tu!!" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa Siasa.

    "Sijui kama mnaona jinsi Trump na Marekani yake wanavyocheza na Dunia kupitia ugomvi au migogoro ya Dunia ili kuipatia faida Marekani kwa kisingizio cha kutafuta amani huku nyuma ya pazia Marekani ikipata faida kupitia migogoro au vita. Tazama Makubaliano ya Madini pale Ukraine Ambapo Marekani watafaidika na Rasilimali za madini za Ukraine, yani ili Marekani waisadie Ukraine ni lazima Ukraine kuipatia madini yake Marekani Congo nayo inakaribia kusaini mkataba wa kuipatia Marekani madini ili Marekani iipatie ulinzi hapo tunazungumzia rasimali za Congo amabzo zinaenda kutumika kama faida kwa Marekani kisa tu ni ugomvi wa Afrika wenyewe kwa wenyewe na hapo hapo Trump katupiga Bao Huko Gaza napo mpango wa kuwahamisha wakazi wa Gaza kwa kisingizio cha kuijenga upya Gaza umeiva, Trump haijengi Gaza bure anafahamu fika kuwa chini ya ardhi ya Gaza kuna utajiri mkubwa wa maliasili ya Gesi na mafuta Huyo ndiye Trump mfanyabiashara kutoka White House ambaye anaenda sambamba na ule msemo unaosema "no free lunch in America" yaani hakuna chakula cha mchana cha bure Marekani, ukiona unapewa cha bure ujue badae utalipia tu!!" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa Siasa.
    0 Commenti ·0 condivisioni ·870 Views
  • Rais wa Marekani , Donald Trump ametoa siri kuwa Ofisi yake imepokea barua kutoka kwa Rais wa Ukraine , Volodymyr Zelensky, ikisema yuko tayari kwa mazungumzo na Russia na kusaini makubaliano ya madini adimu.

    “Ukraine iko tayari kukaa kwenye meza ya mazungumzo haraka iwezekanavyo ili kuleta amani ya kudumu. Hakuna anayetaka amani zaidi ya Waukraine,” Trump amesema katika hotuba yake bungeni usiku wa kuamkia leo huku akinukuu barua hiyo.

    “Mimi na timu yangu tuko tayari kufanya kazi chini ya uongozi thabiti wa Rais Trump ili kupata amani ya kudumu’,” Trump alinukuu maneno ya Zelenskyy.

    “Si hilo lingekuwa jambo zuri?” aliuliza. “Ni wakati wa kukomesha huu upuuzi. Ni wakati wa kusitisha mauaji. Ni wakati wa kumaliza vita hivi visivyo na maana. Ukitaka kumaliza vita, lazima uzungumze na pande zote mbili,” amesema Trump.

    Kauli hiyo ya Trump imekuja siku chache baada ya mvutano mkali kati yake na Zelenskyy katika Ofisi ya Oval iliyoko Ikulu ya White House, hali iliyosababisha Marekani kusitisha msaada muhimu wa kijeshi kwa Ukraine.

    Rais wa Marekani 🇺🇸, Donald Trump ametoa siri kuwa Ofisi yake imepokea barua kutoka kwa Rais wa Ukraine 🇺🇦, Volodymyr Zelensky, ikisema yuko tayari kwa mazungumzo na Russia 🇷🇺 na kusaini makubaliano ya madini adimu. “Ukraine iko tayari kukaa kwenye meza ya mazungumzo haraka iwezekanavyo ili kuleta amani ya kudumu. Hakuna anayetaka amani zaidi ya Waukraine,” Trump amesema katika hotuba yake bungeni usiku wa kuamkia leo huku akinukuu barua hiyo. “Mimi na timu yangu tuko tayari kufanya kazi chini ya uongozi thabiti wa Rais Trump ili kupata amani ya kudumu’,” Trump alinukuu maneno ya Zelenskyy. “Si hilo lingekuwa jambo zuri?” aliuliza. “Ni wakati wa kukomesha huu upuuzi. Ni wakati wa kusitisha mauaji. Ni wakati wa kumaliza vita hivi visivyo na maana. Ukitaka kumaliza vita, lazima uzungumze na pande zote mbili,” amesema Trump. Kauli hiyo ya Trump imekuja siku chache baada ya mvutano mkali kati yake na Zelenskyy katika Ofisi ya Oval iliyoko Ikulu ya White House, hali iliyosababisha Marekani kusitisha msaada muhimu wa kijeshi kwa Ukraine.
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·704 Views
  • Ijumaa, tarehe 28 Februari, haikuwa siku rahisi kwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alipofanya ziara katika Ikulu ya White House, Marekani. Kabla hata ya mzozo wa maneno kati yake na mwenyeji wake, Rais Donald Trump, pamoja na Makamu wa Rais JD Vance, tayari kulikuwa na ishara za mivutano.

    Trump alimkaribisha Zelensky mlangoni na kusema kwa utani: “Leo amevalia kweli kweli,” kauli ambayo iliwafanya baadhi ya waandishi wa habari kuiona kama kejeli badala ya pongezi. Wakati huo, Zelensky alikuwa amevalia fulana nyeusi ya mikono mirefu, vazi ambalo amekuwa akilivaa mara kwa mara tangu Ukraine ivamiwe na Urusi mwaka 2022.

    Baadaye, Trump alipompokea Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, alionekana kutazama mavazi yake kwa makini kutoka juu hadi chini, kisha kunong’ona maneno yanayoweza kutafsiriwa kama pongezi kwa suti rasmi aliyovaa Starmer.

    Mjadala kuhusu mavazi ya Zelensky ulizidi kupamba moto wakati wa mkutano wa waandishi wa habari. Brian Glenn, mwandishi kutoka Real America’s Voice—chombo cha habari kinachopendelea mrengo wa kulia—alimtupia swali la moja kwa moja:

    “Kwa nini hauvai suti? Upo katika ofisi ya juu kabisa katika nchi hii, na umegoma kuvaa suti – je, unamiliki hata suti?”

    Kwa utulivu, Zelensky alijibu kwa mshangao mdogo:

    “Nitavaa suti vita hivi vitakapomalizika. Labda suti kama yako, labda bora zaidi, au pengine ya bei nafuu kuliko yako,” alisema kwa utani huku akionyesha msimamo wake wa kuendelea kuvaa mavazi ya kijeshi.

    Swali hilo la Glenn liliibua mjadala mkali mitandaoni. Wengine walimuunga mkono, wakisema kwamba kiongozi wa taifa anapaswa kuvaa mavazi rasmi anapokutana na viongozi wengine, ilhali wengine waliona swali hilo kuwa la dhihaka na lisilo na umuhimu.

    Miongoni mwa waliomkosoa Glenn ni mwandishi maarufu wa Uingereza, Piers Morgan, ambaye pia ni rafiki wa karibu wa Trump. Morgan aliandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter):

    “Swali la kipuuzi. Elon Musk havai suti anapoingia Ikulu.”

    Historia pia inaonyesha kuwa si Zelensky pekee aliyeingia Ikulu ya Marekani bila suti. Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Winston Churchill, alifanya hivyo katika moja ya ziara zake rasmi.
    Ijumaa, tarehe 28 Februari, haikuwa siku rahisi kwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alipofanya ziara katika Ikulu ya White House, Marekani. Kabla hata ya mzozo wa maneno kati yake na mwenyeji wake, Rais Donald Trump, pamoja na Makamu wa Rais JD Vance, tayari kulikuwa na ishara za mivutano. Trump alimkaribisha Zelensky mlangoni na kusema kwa utani: “Leo amevalia kweli kweli,” kauli ambayo iliwafanya baadhi ya waandishi wa habari kuiona kama kejeli badala ya pongezi. Wakati huo, Zelensky alikuwa amevalia fulana nyeusi ya mikono mirefu, vazi ambalo amekuwa akilivaa mara kwa mara tangu Ukraine ivamiwe na Urusi mwaka 2022. Baadaye, Trump alipompokea Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, alionekana kutazama mavazi yake kwa makini kutoka juu hadi chini, kisha kunong’ona maneno yanayoweza kutafsiriwa kama pongezi kwa suti rasmi aliyovaa Starmer. Mjadala kuhusu mavazi ya Zelensky ulizidi kupamba moto wakati wa mkutano wa waandishi wa habari. Brian Glenn, mwandishi kutoka Real America’s Voice—chombo cha habari kinachopendelea mrengo wa kulia—alimtupia swali la moja kwa moja: “Kwa nini hauvai suti? Upo katika ofisi ya juu kabisa katika nchi hii, na umegoma kuvaa suti – je, unamiliki hata suti?” Kwa utulivu, Zelensky alijibu kwa mshangao mdogo: “Nitavaa suti vita hivi vitakapomalizika. Labda suti kama yako, labda bora zaidi, au pengine ya bei nafuu kuliko yako,” alisema kwa utani huku akionyesha msimamo wake wa kuendelea kuvaa mavazi ya kijeshi. Swali hilo la Glenn liliibua mjadala mkali mitandaoni. Wengine walimuunga mkono, wakisema kwamba kiongozi wa taifa anapaswa kuvaa mavazi rasmi anapokutana na viongozi wengine, ilhali wengine waliona swali hilo kuwa la dhihaka na lisilo na umuhimu. Miongoni mwa waliomkosoa Glenn ni mwandishi maarufu wa Uingereza, Piers Morgan, ambaye pia ni rafiki wa karibu wa Trump. Morgan aliandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter): “Swali la kipuuzi. Elon Musk havai suti anapoingia Ikulu.” Historia pia inaonyesha kuwa si Zelensky pekee aliyeingia Ikulu ya Marekani bila suti. Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Winston Churchill, alifanya hivyo katika moja ya ziara zake rasmi.
    Like
    Love
    2
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·1K Views
  • Nikueleze kwa kifupi sana kiini cha mgogoro. Kabla ya mwaka 1991 Ukraine ilikua sehemu ya Urusi kupitia muungano wa kisovieti wa USSR. Baada ya USSR kufa ndipo taifa la Ukraine likazaliwa pamoja na mataifa mengine 14 yaliyokua majimbo ya Urusi.

    Lakini usisahau mwaka 1949 umoja wa kujihami wa nchi za magharibi (NATO) ulianzishwa dhidi ya Urusi (USSR). Makubaliano yao ni kwamba ikiwa Urusi itamgusa mmoja wao basi wote watamvamia. Marekani akiwa kinara.

    Kuanguka kwa USSR kukafanya mataifa 15 mapya kuzaliwa. Baadhi ya Mataifa hayo yakawa na hofu kuwa Urusi inaweza kurudi kuyakalia kimabavu. Kwahiyo yakaomba kujiunga NATO kwa usalama wao. Estonia, Latvia na Lithuania zikapata uanachana wa NATO chap kwa haraka. Ukraine ilipoomba uanachama Urusi ikakataa, kwa sababu ya strategic position ya Ukraine ambayo inaiweka Urusi hatarini.

    Ukraine ilipokosa uanachama NATO ikamua kujilinda kwa kusuka mpango wa nyuklia. Marekani na Urusi zikashtuka. Kwa kutambua hatari ya nyuklia zikamsihi sana Ukraine aachane na mpango huo. Mwaka 1994 ukaandaliwa mkataba uitwao Budapest memorundum, huko Hungary. Mkataba huo ulihusisha nchi 4. Urusi na Ukraine zilisaini kwamba hakuna atakayemvamia mwenzake. Marekani na Uingereza zikasaini kwamba atakayemvamia mwenzake watampiga bila huruma. Pia Marekani na Uingereza zitagharamia fedha na vifaa vyote vya vita. Mkataba ukasainiwa na Ukraine ikasitisha mpango wake wa nyuklia.

    Lakini Mwaka 2014 Urusi ikaivamia Ukraine na kuchukua jimbo lake la Crimea kimabavu. Marekani na Uingereza hazikuipiga Urusi kama mkataba wa Budapest unavyosema. Ukraine akalalamika lakini akapuuzwa. Kwenye vita inayoendelea sasa, Urusi ameshajitwalia majimbo manne Donetsk, Luhansk, Zaporizhzhia na Kherson lakini Marekani na Uingereza ziko kimya.

    Ukraine inaona imesalitiwa. Mkataba wa Budapest ulikua kiini macho. Laiti Ukraine ingekataa kusaini na kuendelea na mpango wake wa nyuklia, leo Urusi isingethubutu kuigusa. Lakini Waliomdanganya sasa wamemgeuka na wanamfokea. Ukraine ingeyajua maneno ya Mzee Jomo Kenyatta "Learn to fight your own battle" isingeachana na mpango wake wa nyuklia mwaka 1994. Wangejifunza kupigana vita yao wenyewe bila kutegemea mtu.!
    (Malisa GJ)

    Nikueleze kwa kifupi sana kiini cha mgogoro. Kabla ya mwaka 1991 Ukraine ilikua sehemu ya Urusi kupitia muungano wa kisovieti wa USSR. Baada ya USSR kufa ndipo taifa la Ukraine likazaliwa pamoja na mataifa mengine 14 yaliyokua majimbo ya Urusi. Lakini usisahau mwaka 1949 umoja wa kujihami wa nchi za magharibi (NATO) ulianzishwa dhidi ya Urusi (USSR). Makubaliano yao ni kwamba ikiwa Urusi itamgusa mmoja wao basi wote watamvamia. Marekani akiwa kinara. Kuanguka kwa USSR kukafanya mataifa 15 mapya kuzaliwa. Baadhi ya Mataifa hayo yakawa na hofu kuwa Urusi inaweza kurudi kuyakalia kimabavu. Kwahiyo yakaomba kujiunga NATO kwa usalama wao. Estonia, Latvia na Lithuania zikapata uanachana wa NATO chap kwa haraka. Ukraine ilipoomba uanachama Urusi ikakataa, kwa sababu ya strategic position ya Ukraine ambayo inaiweka Urusi hatarini. Ukraine ilipokosa uanachama NATO ikamua kujilinda kwa kusuka mpango wa nyuklia. Marekani na Urusi zikashtuka. Kwa kutambua hatari ya nyuklia zikamsihi sana Ukraine aachane na mpango huo. Mwaka 1994 ukaandaliwa mkataba uitwao Budapest memorundum, huko Hungary. Mkataba huo ulihusisha nchi 4. Urusi na Ukraine zilisaini kwamba hakuna atakayemvamia mwenzake. Marekani na Uingereza zikasaini kwamba atakayemvamia mwenzake watampiga bila huruma. Pia Marekani na Uingereza zitagharamia fedha na vifaa vyote vya vita. Mkataba ukasainiwa na Ukraine ikasitisha mpango wake wa nyuklia. Lakini Mwaka 2014 Urusi ikaivamia Ukraine na kuchukua jimbo lake la Crimea kimabavu. Marekani na Uingereza hazikuipiga Urusi kama mkataba wa Budapest unavyosema. Ukraine akalalamika lakini akapuuzwa. Kwenye vita inayoendelea sasa, Urusi ameshajitwalia majimbo manne Donetsk, Luhansk, Zaporizhzhia na Kherson lakini Marekani na Uingereza ziko kimya. Ukraine inaona imesalitiwa. Mkataba wa Budapest ulikua kiini macho. Laiti Ukraine ingekataa kusaini na kuendelea na mpango wake wa nyuklia, leo Urusi isingethubutu kuigusa. Lakini Waliomdanganya sasa wamemgeuka na wanamfokea. Ukraine ingeyajua maneno ya Mzee Jomo Kenyatta "Learn to fight your own battle" isingeachana na mpango wake wa nyuklia mwaka 1994. Wangejifunza kupigana vita yao wenyewe bila kutegemea mtu.! (Malisa GJ)
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·1K Views
  • "Nimetazama Interview ya Rais wa Marekani na Rais wa Ukraine pale Oval Office ndani ya Ikulu ya Marekani, nimekuja kugundua Rais wa Ukraine anahisi anajadiliana na Mwanasiasa mwenzake ila anachosahau Trump ni Mfanyabiashara na hawezi kufanya kitu cha bure ambacho Taifa lake Marekani halinufaiki na chochote, ndio maan anamsukumia sana kuwa amalizane na Urusi wasaini mkataba wa amani.

    Pale Ukraine kuna madini adimu sana duniani, Mrusi hapigani Kichwa kichwa ndio maana maeneo ya Donbass na Zaporizhia yanabaki kuwa maeneo ya Kimkakati sana kwa Mrusi, hata Marekani hawapo kichwa kichwa maana Secretary Rubio wa Marekani alimwambia Rais wa Ukraine akubali kusaini mkataba wa madini ili wao waendelee kumlinda, Mrusi na Mmarekani wapo rada sana eneo lile na kila mmoja yupo Kitalaam.

    Kwa akili ya kawaida Marekani hataki kuendelea kugharamikia vita hivyo bila faida.

    Juzi kuna website nilisoma ya taarifa za Kiuchunguzi ni kuwa Marekani, China na Urusi kwasasa wapo meza moja na wazo lao kubwa wamekubaliana juu ya MULTIPOLAR WORLD ORDER ambapo Mataifa zaidi ya mawili yanakuwa na nguvu sawa ama yanakaribiana, kwa ufupi sana mataifa haya matatu yanataka kuitawala dunia bila kugusana.

    Ndio maana Trump alivyoingia madarakani akapush agenda chap ya BRICS kuachana na wazo lao la kuibadili dola ya Marekani kuwa sio sarafu rasmi kwenye umoja wao, ndio maana alipoingia wamerudi mezani kwa mengi ikiwemo Trump na Putin wote kukiri kuwa watashirikiana na Trump atasafiri kuelekea Urusi kwenye sherehe za Mei 9, ambapo watakutana Marais wote watatu yani Putin, Xi Jinping na Trump.

    Kifupi sana Marekani ya Donald Trump ina Approach tofauti sana, ndio maana hata Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Stearmer alipofika White House kukutana na Trump kwenye mazungumzo yao akalisifia sana Jeshi la Uingereza ila kuna sehemu akampiga kwa kumwambia huwezi kuichukua Urusi peke yako, hata leo amesisitiza Ukraine wakubali amani nje na hapo bila msaada wake hawamuwezi Mrusi, huyo ndio Donald Trump" - Farhan JR, Mchambuzi.

    "Nimetazama Interview ya Rais wa Marekani na Rais wa Ukraine pale Oval Office ndani ya Ikulu ya Marekani, nimekuja kugundua Rais wa Ukraine anahisi anajadiliana na Mwanasiasa mwenzake ila anachosahau Trump ni Mfanyabiashara na hawezi kufanya kitu cha bure ambacho Taifa lake Marekani halinufaiki na chochote, ndio maan anamsukumia sana kuwa amalizane na Urusi wasaini mkataba wa amani. Pale Ukraine kuna madini adimu sana duniani, Mrusi hapigani Kichwa kichwa ndio maana maeneo ya Donbass na Zaporizhia yanabaki kuwa maeneo ya Kimkakati sana kwa Mrusi, hata Marekani hawapo kichwa kichwa maana Secretary Rubio wa Marekani alimwambia Rais wa Ukraine akubali kusaini mkataba wa madini ili wao waendelee kumlinda, Mrusi na Mmarekani wapo rada sana eneo lile na kila mmoja yupo Kitalaam. Kwa akili ya kawaida Marekani hataki kuendelea kugharamikia vita hivyo bila faida. Juzi kuna website nilisoma ya taarifa za Kiuchunguzi ni kuwa Marekani, China na Urusi kwasasa wapo meza moja na wazo lao kubwa wamekubaliana juu ya MULTIPOLAR WORLD ORDER ambapo Mataifa zaidi ya mawili yanakuwa na nguvu sawa ama yanakaribiana, kwa ufupi sana mataifa haya matatu yanataka kuitawala dunia bila kugusana. Ndio maana Trump alivyoingia madarakani akapush agenda chap ya BRICS kuachana na wazo lao la kuibadili dola ya Marekani kuwa sio sarafu rasmi kwenye umoja wao, ndio maana alipoingia wamerudi mezani kwa mengi ikiwemo Trump na Putin wote kukiri kuwa watashirikiana na Trump atasafiri kuelekea Urusi kwenye sherehe za Mei 9, ambapo watakutana Marais wote watatu yani Putin, Xi Jinping na Trump. Kifupi sana Marekani ya Donald Trump ina Approach tofauti sana, ndio maana hata Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Stearmer alipofika White House kukutana na Trump kwenye mazungumzo yao akalisifia sana Jeshi la Uingereza ila kuna sehemu akampiga kwa kumwambia huwezi kuichukua Urusi peke yako, hata leo amesisitiza Ukraine wakubali amani nje na hapo bila msaada wake hawamuwezi Mrusi, huyo ndio Donald Trump" - Farhan JR, Mchambuzi.
    0 Commenti ·0 condivisioni ·1K Views
  • Mazungunzo kati ya Rais wa Marekani , Donald Trump na Rais wa Ukraine , Volorymyr Zelensky yameishia njiani baada ya kushindwa kuelewana kuhusu hatima ya vita ya Russia dhidi ya Ukraine. Ilianza kama utani wakati wa kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance na Waandishi wa Habari.

    Kila upande ulianza kuelezea kile ambacho wamejadiliana kuhusiana na makubaliano yaliyokuwa yanatarajiwa kutiwa saini. Awali Trump alieleza kuwa makubaliano hayo ni pamoja na kusaini mkataba unaoiruhusu Marekani kuchimba madini adimu (rare minerals) katika ardhi ya Ukraine.

    Wakati mrejesho wa hatua iliyofikiwa kuhusu makubaliano hayo ya mkataba wa madini mambo yalikuwa sawa ila yakaanza kwenda mrama pale Trump alipohamisha mada na kuingia suala la kupata mwafaka wa mzozo kati ya Ukraine na Russia ya Vladimir Putin.

    Trump kwenye suala hilo alienda moja kwa moja na kumtaka Rais Zelensky, kuingia makubaliano na Russia ya kumaliza vita hivyo, la sivyo Marekani itajindoa katika mazungumzo hayo na haitoendelea kuifadhili tena wala kuipatia misaada Ukraine. Wawili hao walikatizana mara kwa mara wakati wa majibizano yao kwa namna isiyo ya kawaida ndani ya Marekani (White House).

    Mazungunzo kati ya Rais wa Marekani 🇺🇸, Donald Trump na Rais wa Ukraine 🇺🇦, Volorymyr Zelensky yameishia njiani baada ya kushindwa kuelewana kuhusu hatima ya vita ya Russia 🇷🇺 dhidi ya Ukraine. Ilianza kama utani wakati wa kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance na Waandishi wa Habari. Kila upande ulianza kuelezea kile ambacho wamejadiliana kuhusiana na makubaliano yaliyokuwa yanatarajiwa kutiwa saini. Awali Trump alieleza kuwa makubaliano hayo ni pamoja na kusaini mkataba unaoiruhusu Marekani kuchimba madini adimu (rare minerals) katika ardhi ya Ukraine. Wakati mrejesho wa hatua iliyofikiwa kuhusu makubaliano hayo ya mkataba wa madini mambo yalikuwa sawa ila yakaanza kwenda mrama pale Trump alipohamisha mada na kuingia suala la kupata mwafaka wa mzozo kati ya Ukraine na Russia ya Vladimir Putin. Trump kwenye suala hilo alienda moja kwa moja na kumtaka Rais Zelensky, kuingia makubaliano na Russia ya kumaliza vita hivyo, la sivyo Marekani itajindoa katika mazungumzo hayo na haitoendelea kuifadhili tena wala kuipatia misaada Ukraine. Wawili hao walikatizana mara kwa mara wakati wa majibizano yao kwa namna isiyo ya kawaida ndani ya Marekani (White House).
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·871 Views
  • Kikao cha mazungumzo ya kumaliza mzozo wa Nchi ya Ukraine na Nchi ya Urusi kinaendelea Nchini Saudi Arabia 🇸 ambapo Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Urusi chini ya Sergie Lavrov na Marekani chini ya Marco Rubio. Hata hivyo, Ukraine na Umoja wa Ulaya (EU) hawajashirikishwa huku Ukraine upande wake inapinga kikao hicho kuwa makubaliano yoyote haitayatambua.

    Katika kusisitiza hilo Ukraine imeendelea kusisitiza kwamba itaendelea kupigana vita kwa kutegemea Ulaya sio Marekani kama mwanzo huku Rais wa Nchi hiyo Volodmiry Zelensky akisema Ukraine ni Taifa huru, hivyo haliwezi kuamuliwa mambo yake na Marekani, itautetea uhuru wake hadi tone la mwisho. Marekani imejibu kwa kusema inaitaka Ukraine irejeshe haraka deni lote la usaidizi wa vita lililotolewa na Marekani tangu Februari 2022 Oparesheni ya Urusi ilipoanza.

    Kikao hiki kinachoendelea ni hatua muhimu kuelekea mkutano wa Rais Putin na Rais Trump uliopangwa mwezi Mei katika sherehe za Mashujaa wa Urusi utakaofanyika Jijini Moscow, Urusi ambapo pia mkutano huo utamwalika Rais wa China Xi Ping kama Mgeni mwalikwa muhimu.

    Kikao cha mazungumzo ya kumaliza mzozo wa Nchi ya Ukraine 🇺🇦 na Nchi ya Urusi 🇷🇺 kinaendelea Nchini Saudi Arabia 🇸 ambapo Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Urusi chini ya Sergie Lavrov na Marekani 🇺🇸 chini ya Marco Rubio. Hata hivyo, Ukraine na Umoja wa Ulaya (EU) hawajashirikishwa huku Ukraine upande wake inapinga kikao hicho kuwa makubaliano yoyote haitayatambua. Katika kusisitiza hilo Ukraine imeendelea kusisitiza kwamba itaendelea kupigana vita kwa kutegemea Ulaya sio Marekani kama mwanzo huku Rais wa Nchi hiyo Volodmiry Zelensky akisema Ukraine ni Taifa huru, hivyo haliwezi kuamuliwa mambo yake na Marekani, itautetea uhuru wake hadi tone la mwisho. Marekani imejibu kwa kusema inaitaka Ukraine irejeshe haraka deni lote la usaidizi wa vita lililotolewa na Marekani tangu Februari 2022 Oparesheni ya Urusi ilipoanza. Kikao hiki kinachoendelea ni hatua muhimu kuelekea mkutano wa Rais Putin na Rais Trump uliopangwa mwezi Mei katika sherehe za Mashujaa wa Urusi utakaofanyika Jijini Moscow, Urusi ambapo pia mkutano huo utamwalika Rais wa China 🇨🇳 Xi Ping kama Mgeni mwalikwa muhimu.
    0 Commenti ·0 condivisioni ·856 Views
  • Rais wa Urusi , Vladimir Putin amewaalika Rais China , Xi Jinping na Rais wa Marekani , Donald Trump kuhudhuria sherehe maarufu za Ushindi wa Urusi katika vita kuu ya pili ya Dunia (Russia’s Victory Parade) zitakazofanyika tarehe 9 Mwezi May Jijini Moscow Nchini Urusi. Mwaliko huu unatokana na ombi la Rais Donald Trump la tarehe 11 Feb 2025 alipoomba kuzuru Moscow kwa lengo la kumaliza mgogoro wa Ukraine, Kikao kilichotokana na ombi hili kilifanywa kwa njia ya simu ambapo pamoja na mambo mengine, Trump alimhakikishia Putin kwamba Marekani itaacha ufadhili wa kijeshi kwa Ukraine na pia Ukraine itaachia sehemu ya ardhi yake iliyotwaliwa kama dhamana ya usalama wake dhidi ya Moscow.

    Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Washington katika taarifa yake ilikazia na kusisitiza kile alichokizungumza Trump na Moscow na kwamba Marekani inakusudia kumaliza tofauti zao kidunia. Utawala wa Trump umekuwa na juhudi kubwa kumaliza mizozo mikubwa duniani ambayo Ikulu hiyo ilikuwa ikifadhili na kuanzisha uchokozi kwa muda mrefu, Ukiachiliambali mgogoro wa Ukraine, pia Washington inashughulika kumaliza mgogoro wa Mashariki ya Kati huko Gaza ambapo mamia ya watu wameuawa kwa ufadhili wa Marekani hiyohiyo.

    Rais wa Urusi 🇷🇺, Vladimir Putin amewaalika Rais China 🇨🇳, Xi Jinping na Rais wa Marekani 🇺🇸, Donald Trump kuhudhuria sherehe maarufu za Ushindi wa Urusi katika vita kuu ya pili ya Dunia (Russia’s Victory Parade) zitakazofanyika tarehe 9 Mwezi May Jijini Moscow Nchini Urusi. Mwaliko huu unatokana na ombi la Rais Donald Trump la tarehe 11 Feb 2025 alipoomba kuzuru Moscow kwa lengo la kumaliza mgogoro wa Ukraine, Kikao kilichotokana na ombi hili kilifanywa kwa njia ya simu ambapo pamoja na mambo mengine, Trump alimhakikishia Putin kwamba Marekani itaacha ufadhili wa kijeshi kwa Ukraine na pia Ukraine itaachia sehemu ya ardhi yake iliyotwaliwa kama dhamana ya usalama wake dhidi ya Moscow. Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Washington katika taarifa yake ilikazia na kusisitiza kile alichokizungumza Trump na Moscow na kwamba Marekani inakusudia kumaliza tofauti zao kidunia. Utawala wa Trump umekuwa na juhudi kubwa kumaliza mizozo mikubwa duniani ambayo Ikulu hiyo ilikuwa ikifadhili na kuanzisha uchokozi kwa muda mrefu, Ukiachiliambali mgogoro wa Ukraine, pia Washington inashughulika kumaliza mgogoro wa Mashariki ya Kati huko Gaza ambapo mamia ya watu wameuawa kwa ufadhili wa Marekani hiyohiyo.
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·958 Views
  • Marais wa Urusi , V. Putin na yule wa Marekani , D.Trump walizungumza leo hii kwa muda saa moja na nusu kuhusu kumaliza vita Nchini Ukraine , kuboresha uhusiano kati ya Marekani na Urusi, na uwezekano wa kubadilishana Wafungwa.

    Aidha, Putin alimwalika Trump kwenda Mjini Moscow Nchini Urusi na akasema yuko tayari kuwakaribisha Maafisa wa Marekani kwa mazungumzo. Hii ilikuwa simu ya kwanza ya Putin na Rais wa Marekani aliyeko madarakani tangu Februari 2022, alipoongea na Biden muda mfupi kabla ya kutuma Wanajeshi Nchini Ukraine.

    Toa maoni yako
    #MvanoHabari
    #MvanoMtangazaji
    #M33
    Marais wa Urusi 🇷🇺, V. Putin na yule wa Marekani 🇺🇸, D.Trump walizungumza leo hii kwa muda saa moja na nusu kuhusu kumaliza vita Nchini Ukraine 🇮🇱, kuboresha uhusiano kati ya Marekani na Urusi, na uwezekano wa kubadilishana Wafungwa. Aidha, Putin alimwalika Trump kwenda Mjini Moscow Nchini Urusi na akasema yuko tayari kuwakaribisha Maafisa wa Marekani kwa mazungumzo. Hii ilikuwa simu ya kwanza ya Putin na Rais wa Marekani aliyeko madarakani tangu Februari 2022, alipoongea na Biden muda mfupi kabla ya kutuma Wanajeshi Nchini Ukraine. Toa maoni yako #MvanoHabari #MvanoMtangazaji #M33
    0 Commenti ·0 condivisioni ·1K Views
  • Kwa mujibu wa wa kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un , migogoro inayochochewa na Marekani katika sehemu mbalimbali za dunia, "inazidi kuongeza hatari ya kuzuka kwa vita vya dunia vipya vyenye athari kubwa sio tu kwa amani na usalama wa kimataifa bali pia nyanja nyingine zote za shughuli za binadamu."

    Pia Kim alitoa maoni kwamba mwaka 2025, mzozo wa Ukraine utasalia kuwa moja ya "mhimili mkuu wa hali ya wasiwasi ya kimataifa," nyingine ikiwa hali katika Ukanda wa Gaza na Syria "ambayo imekuwa uwanja wa migogoro ya kijiografia na makabiliano ya kimataifa mwaka jana."

    Katika hatua nyingine Kim alisema Marekani na nchi za Magharibi zinaelezea mzozo wa Ukraine kwa kushindwa kuishinda Urusi kimkakati, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alisema, kama ilivyonukuliwa na Shirika la Habari la Korea (KCNA).

    Katika mkutano katika Wizara ya Ulinzi, kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 77 ya Jeshi la Wananchi wa Korea, alidai kwamba Marekani imepofushwa na tamaa mbaya huku akiionyesha wasiwasi mkubwa juu ya tabia ya kutojali ya Marekani na kundi la Magharibi kwa makusudi kuendeleza vita vya muda mrefu kwa ndoto isiyoweza kutekelezwa ili kukabiliana na kurudi kwa kimkakati kwa Urusi," shirika la habari lilibainisha.

    Kim alidokeza kuwa Pyongyang imekuwa ikipinga kila mara "kitendo chochote cha kunyima haki ya kimataifa na kuvuruga amani na usalama duniani." Aliongeza kuwa nchi yake "itaunga mkono kila wakati na kuhimiza sababu ya haki ya jeshi la Urusi na watu kutetea uhuru wao, usalama na uadilifu wa eneo kwa kuzingatia ari ya mkataba juu ya ushirikiano wa kimkakati wa kina kati ya DPRK na Urusi."
    (Zungu)

    Kwa mujibu wa wa kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un , migogoro inayochochewa na Marekani katika sehemu mbalimbali za dunia, "inazidi kuongeza hatari ya kuzuka kwa vita vya dunia vipya vyenye athari kubwa sio tu kwa amani na usalama wa kimataifa bali pia nyanja nyingine zote za shughuli za binadamu." Pia Kim alitoa maoni kwamba mwaka 2025, mzozo wa Ukraine utasalia kuwa moja ya "mhimili mkuu wa hali ya wasiwasi ya kimataifa," nyingine ikiwa hali katika Ukanda wa Gaza na Syria "ambayo imekuwa uwanja wa migogoro ya kijiografia na makabiliano ya kimataifa mwaka jana." Katika hatua nyingine Kim alisema Marekani na nchi za Magharibi zinaelezea mzozo wa Ukraine kwa kushindwa kuishinda Urusi kimkakati, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alisema, kama ilivyonukuliwa na Shirika la Habari la Korea (KCNA). Katika mkutano katika Wizara ya Ulinzi, kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 77 ya Jeshi la Wananchi wa Korea, alidai kwamba Marekani imepofushwa na tamaa mbaya huku akiionyesha wasiwasi mkubwa juu ya tabia ya kutojali ya Marekani na kundi la Magharibi kwa makusudi kuendeleza vita vya muda mrefu kwa ndoto isiyoweza kutekelezwa ili kukabiliana na kurudi kwa kimkakati kwa Urusi," shirika la habari lilibainisha. Kim alidokeza kuwa Pyongyang imekuwa ikipinga kila mara "kitendo chochote cha kunyima haki ya kimataifa na kuvuruga amani na usalama duniani." Aliongeza kuwa nchi yake "itaunga mkono kila wakati na kuhimiza sababu ya haki ya jeshi la Urusi na watu kutetea uhuru wao, usalama na uadilifu wa eneo kwa kuzingatia ari ya mkataba juu ya ushirikiano wa kimkakati wa kina kati ya DPRK na Urusi." (Zungu)
    0 Commenti ·0 condivisioni ·1K Views
  • Putin sasa anazunguka huku na kule akitafuta suluhu ya amani, lakini Ukraine naye amegoma kusalimu amri.

    Katika ramani ya dunia, mababe wawili wamebaki, Marekani na China.

    Marekani bado inatawala masoko ya dunia, ina silaha za kisasa, na inafanya kila kitu kuhakikisha inabaki juu.

    China inakuja kwa kasi, ikitumia siasa za uchumi badala ya vita. Wanajua kuwa kushinda vita vya sasa, sio kwa mabomu tu bali kwa pesa na teknolojia.

    Urusi? Imebanwa. Vita na Ukraine imeichosha. Mipango ya kupanua mipaka imekufa. Na sasa dunia inajiuliza Putin anaweza kushindwa?

    Hii dunia ina kanuni moja kubwa, Usimwamini mtu. Na hata kama ukimwamini mtu, basi huyo mtu awe wewe mwenyewe.

    Ukraine alifanya kosa ambalo sasa linamgharimu. Aliamini ahadi za mataifa makubwa bila kuhakikisha ana kinga yake mwenyewe. Akasahau kuwa siasa za dunia haziongozwi na ahadi, bali na nguvu.

    Hili liwe somo kwa kila taifa linalotegemea misaada kutoka nje. Leo wanakupenda, kesho wakishapata wanachotaka, wanakusahau.

    Na dunia ilivyo sasa, muda wowote inaweza kulipuka. Mataifa yanapimana nguvu, migogoro inaongezeka, na tunakaribia kuona enzi mpya ya vita vya madaraka kati ya Marekani na China.

    Ukraine, Anajifunza kwa uchungu kuwa historia haimsahau mjinga.
    Putin sasa anazunguka huku na kule akitafuta suluhu ya amani, lakini Ukraine naye amegoma kusalimu amri. Katika ramani ya dunia, mababe wawili wamebaki, Marekani na China. Marekani bado inatawala masoko ya dunia, ina silaha za kisasa, na inafanya kila kitu kuhakikisha inabaki juu. China inakuja kwa kasi, ikitumia siasa za uchumi badala ya vita. Wanajua kuwa kushinda vita vya sasa, sio kwa mabomu tu bali kwa pesa na teknolojia. Urusi? Imebanwa. Vita na Ukraine imeichosha. Mipango ya kupanua mipaka imekufa. Na sasa dunia inajiuliza Putin anaweza kushindwa? Hii dunia ina kanuni moja kubwa, Usimwamini mtu. Na hata kama ukimwamini mtu, basi huyo mtu awe wewe mwenyewe. Ukraine alifanya kosa ambalo sasa linamgharimu. Aliamini ahadi za mataifa makubwa bila kuhakikisha ana kinga yake mwenyewe. Akasahau kuwa siasa za dunia haziongozwi na ahadi, bali na nguvu. Hili liwe somo kwa kila taifa linalotegemea misaada kutoka nje. Leo wanakupenda, kesho wakishapata wanachotaka, wanakusahau. Na dunia ilivyo sasa, muda wowote inaweza kulipuka. Mataifa yanapimana nguvu, migogoro inaongezeka, na tunakaribia kuona enzi mpya ya vita vya madaraka kati ya Marekani na China. Ukraine, Anajifunza kwa uchungu kuwa historia haimsahau mjinga.
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·1K Views
  • Marekani, Alitoa msaada wa miezi mitatu tu, kisha akaanza kulegeza kamba. Kwa sasa, Marekani imechoshwa na vita vya Ukraine.

    Wameona haina faida ya kuendelea kutoa silaha zisizoleta matokeo ya haraka.

    Uingereza, Ipo kama haipo. Iliahidi mengi, lakini imetulia kimya huku Waukraine wakiteketea kwenye moto wa kivita.

    Ulaya, Inajifanya ina wasiwasi, lakini ukweli ni kwamba kila nchi inajitazama yenyewe kwanza.

    Ukraine yuko peke yake.

    Na hapa ndipo tujiulize. Je, kweli Ukraine aliangamiza kila kitu?

    Inawezekana hana mabomu ya nyuklia tena, lakini ana akili, ana wataalamu, ana formula za kuyatengeneza.

    Na kama historia ni mwalimu, basi ni suala la muda tu kabla ya Ukraine kuamua kuchukua mkondo mpya.
    Vita vya Ukraine vimekuwa mzigo mzito kwa Urusi. Jeshi lake limepoteza askari wengi, uchumi wake umebanwa, na nguvu yake ya kijeshi imetetereka.
    Marekani, Alitoa msaada wa miezi mitatu tu, kisha akaanza kulegeza kamba. Kwa sasa, Marekani imechoshwa na vita vya Ukraine. Wameona haina faida ya kuendelea kutoa silaha zisizoleta matokeo ya haraka. Uingereza, Ipo kama haipo. Iliahidi mengi, lakini imetulia kimya huku Waukraine wakiteketea kwenye moto wa kivita. Ulaya, Inajifanya ina wasiwasi, lakini ukweli ni kwamba kila nchi inajitazama yenyewe kwanza. Ukraine yuko peke yake. Na hapa ndipo tujiulize. Je, kweli Ukraine aliangamiza kila kitu? Inawezekana hana mabomu ya nyuklia tena, lakini ana akili, ana wataalamu, ana formula za kuyatengeneza. Na kama historia ni mwalimu, basi ni suala la muda tu kabla ya Ukraine kuamua kuchukua mkondo mpya. Vita vya Ukraine vimekuwa mzigo mzito kwa Urusi. Jeshi lake limepoteza askari wengi, uchumi wake umebanwa, na nguvu yake ya kijeshi imetetereka.
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·938 Views
  • Muda ukasonga. Dunia ikabadilika. Mataifa yakaanza kuweka mbele maslahi yao, na Ukraine akajikuta akilia peke yake kwenye uwanja wa vita.

    Aliyeahidi kumlinda Urusi ndiye huyo anayemshambulia kwa mabomu, vifaru na ndege za kivita.

    Kwa miaka mingi, Vladimir Putin alikuwa anaangalia ramani ya dunia akijiuliza, "Mbona Crimea na Donbas zipo nje ya milki yangu?"

    Halafu, ghafla mwaka 2014, Urusi ikaamua kumng'ata Ukraine kwa mara ya kwanza.

    Crimea ikachukuliwa, na dunia ikakaa kimya. Hakukuwa na hatua kubwa zilizochukuliwa na Marekani wala Uingereza. Ukraine akaanza kuona dalili za usaliti.

    Mwaka 2022, Urusi ikarudi tena, safari hii kwa nguvu kubwa zaidi.
    Tishio la silaha za nyuklia lililomfanya Ukraine kuwa mbabe, halikuwepo tena. Hakuwa na kinga tena, alikuwa mtu mwepesi wa kushambuliwa.

    Na hapa ndipo Ukraine alipogundua kosa lake kubwa aliamini makaratasi kuliko mabavu.
    Muda ukasonga. Dunia ikabadilika. Mataifa yakaanza kuweka mbele maslahi yao, na Ukraine akajikuta akilia peke yake kwenye uwanja wa vita. Aliyeahidi kumlinda Urusi ndiye huyo anayemshambulia kwa mabomu, vifaru na ndege za kivita. Kwa miaka mingi, Vladimir Putin alikuwa anaangalia ramani ya dunia akijiuliza, "Mbona Crimea na Donbas zipo nje ya milki yangu?" Halafu, ghafla mwaka 2014, Urusi ikaamua kumng'ata Ukraine kwa mara ya kwanza. Crimea ikachukuliwa, na dunia ikakaa kimya. Hakukuwa na hatua kubwa zilizochukuliwa na Marekani wala Uingereza. Ukraine akaanza kuona dalili za usaliti. Mwaka 2022, Urusi ikarudi tena, safari hii kwa nguvu kubwa zaidi. Tishio la silaha za nyuklia lililomfanya Ukraine kuwa mbabe, halikuwepo tena. Hakuwa na kinga tena, alikuwa mtu mwepesi wa kushambuliwa. Na hapa ndipo Ukraine alipogundua kosa lake kubwa aliamini makaratasi kuliko mabavu.
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·1K Views
  • Miaka ya 90, Ukraine alikuwa mbabe sana. Taifa hili lilikuwa lina nguvu za kijeshi ambazo ziliwafanya majirani zake kusita hata kufikiria kulivamia.

    Sababu?

    Lilikuwa na zaidi ya mabomu 1,000 ya nyuklia. Haya si mabomu ya kawaida, ni silaha za maangamizi ambazo zingeweza kuifuta dunia katika sekunde chache.

    Lakini kama ilivyo kwa kila hadithi ya usaliti, Ukraine alifanya kosa moja kubwa, aliamini watu wengine badala ya kujilinda mwenyewe.

    Marekani, Urusi na Uingereza walimfuata kwa heshima kubwa, wakampigia magoti na kumwambia.

    "Tafadhali, haribu mabomu yako. Dunia itakuwa mahali salama zaidi, na sisi tutakuwa walinzi wako. Hatutakuacha."
    Ukraine akakubali. Akayaangamiza mabomu yake yote ya nyuklia. Mikataba iliwekwa. Ahadi zikaandikwa kwa kalamu na kutiwa muhuri.

    Ukraine akaamini kabisa kuwa usalama wake hauwezi kutikiswa tena.
    Miaka ya 90, Ukraine alikuwa mbabe sana. Taifa hili lilikuwa lina nguvu za kijeshi ambazo ziliwafanya majirani zake kusita hata kufikiria kulivamia. Sababu? Lilikuwa na zaidi ya mabomu 1,000 ya nyuklia. Haya si mabomu ya kawaida, ni silaha za maangamizi ambazo zingeweza kuifuta dunia katika sekunde chache. Lakini kama ilivyo kwa kila hadithi ya usaliti, Ukraine alifanya kosa moja kubwa, aliamini watu wengine badala ya kujilinda mwenyewe. Marekani, Urusi na Uingereza walimfuata kwa heshima kubwa, wakampigia magoti na kumwambia. "Tafadhali, haribu mabomu yako. Dunia itakuwa mahali salama zaidi, na sisi tutakuwa walinzi wako. Hatutakuacha." Ukraine akakubali. Akayaangamiza mabomu yake yote ya nyuklia. Mikataba iliwekwa. Ahadi zikaandikwa kwa kalamu na kutiwa muhuri. Ukraine akaamini kabisa kuwa usalama wake hauwezi kutikiswa tena.
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·753 Views
  • Rais Donald Trump wa Marekani amemuandikia barua ya mwaliko kwenye Ikulu ya Marekani White House Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akimuomba aende wiki ijayo wakajadili hali ya Mashariki ya Kati na maslahi yao ya pamoja katika ukanda huo (mgogoro wa Palestina na Israel).

    Kwa mwaliko huo, Benjamin Netanyahu atakuwa kiongozi Mkuu wa kwanza wa nje kufanya ziara rasmi Marekani baada ya Trump kushinda tena Urais wa Taifa hilo. Ikumbukwe maandalizi ya mkutano wa Trump na Putin pia yanaendelea ili kumaliza vita vya Ukraine.

    Rais Donald Trump wa Marekani amemuandikia barua ya mwaliko kwenye Ikulu ya Marekani White House Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akimuomba aende wiki ijayo wakajadili hali ya Mashariki ya Kati na maslahi yao ya pamoja katika ukanda huo (mgogoro wa Palestina na Israel). Kwa mwaliko huo, Benjamin Netanyahu atakuwa kiongozi Mkuu wa kwanza wa nje kufanya ziara rasmi Marekani baada ya Trump kushinda tena Urais wa Taifa hilo. Ikumbukwe maandalizi ya mkutano wa Trump na Putin pia yanaendelea ili kumaliza vita vya Ukraine.
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·686 Views
  • Rais Donald Trump wa Marekani amemuandikia barua ya mwaliko kwenye Ikulu ya Marekani White House Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akimuomba aende wiki ijayo wakajadili hali ya Mashariki ya Kati na maslahi yao ya pamoja katika ukanda huo (mgogoro wa Palestina na Israel).

    Kwa mwaliko huo, Benjamin Netanyahu atakuwa kiongozi Mkuu wa kwanza wa nje kufanya ziara rasmi Marekani baada ya Trump kushinda tena Urais wa Taifa hilo. Ikumbukwe maandalizi ya mkutano wa Trump na Putin pia yanaendelea ili kumaliza vita vya Ukraine.

    Rais Donald Trump wa Marekani amemuandikia barua ya mwaliko kwenye Ikulu ya Marekani White House Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akimuomba aende wiki ijayo wakajadili hali ya Mashariki ya Kati na maslahi yao ya pamoja katika ukanda huo (mgogoro wa Palestina na Israel). Kwa mwaliko huo, Benjamin Netanyahu atakuwa kiongozi Mkuu wa kwanza wa nje kufanya ziara rasmi Marekani baada ya Trump kushinda tena Urais wa Taifa hilo. Ikumbukwe maandalizi ya mkutano wa Trump na Putin pia yanaendelea ili kumaliza vita vya Ukraine.
    Like
    3
    · 1 Commenti ·0 condivisioni ·484 Views
  • Uingereza na Ukraine zimesaini makubaliano ya miaka 100, huku Uingereza ikiahidi kuipa mkopo kwa ajili ya ununuzi wa silaha na vifaa vya kijeshi vya dola bilioni 2.6 [trilioni 6.5] kwa ajili ya kupambana na uvamizi wa Urusi.

    Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer amesema mkopo huo hautalipwa na Ukraine bali kutoka kwenye mali za Urusi zilizozuiliwa.
    Uingereza na Ukraine zimesaini makubaliano ya miaka 100, huku Uingereza ikiahidi kuipa mkopo kwa ajili ya ununuzi wa silaha na vifaa vya kijeshi vya dola bilioni 2.6 [trilioni 6.5] kwa ajili ya kupambana na uvamizi wa Urusi. Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer amesema mkopo huo hautalipwa na Ukraine bali kutoka kwenye mali za Urusi zilizozuiliwa.
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·639 Views
Pagine in Evidenza