Upgrade to Pro

  • OPERATION ENTEBBE -1

    Jina mbadala: Operation Thunderstorm/Operation Yonatan

    Watekelezaji: -MOSSAD
    - IDF (ISRAEL DEFENCE FORCE)
    Kitengo cha Weledi: Sayeret Matkal
    Mwaka wa utekelezaji: July, 1976
    Nchi: Israel/Uganda

    Silaha za kukumbukwa: Lockheed C-130 Hurcules
    Wahusika wa kukumbukwa: - Yonatan Netanyahu (kaka wa Waziri Mkuu wa zamani Benjamin Netanyahu)
    -Ehud Barak (alikuja kuwa Waziri Mkuu miaka ya karibuni)

    MOSAD & IDF: OPERATION ENTEBBE

    Siku ya tarehe 27 June mwaka 1976 ilianza kama siku nyingine yioyote ndani ya uwanja wa ndege wa kimataifa katika mji mkuu wa nchi ya Israel Tel Aviv, uwanja ujulikanao kama Ben Gurion International Airport. Moja kati ya ndege ambayo ilikuwa inafanya safari yake katika siku ya elo ilikuwa ni ndege ya kampuni ya Air Frace ambao walikuwa na ndege yao ya Air France Flight 139 ambayo ni ndege aina ya Airbus A300B4-203 yenye namba ya usajili mkiani F-BVGG (c/n 019).
    Ndege hii ilikuwa inafanya safari yake katika siku ya leo kutoka Tel Aviv na ilikuwa inatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Charles DE Gaulle International Airport jijini Paris, Ufaransa. Baada ya taratibu na protokali zote za uwanja wa ndege kukamilika na abiria wote kukwea kwenye ndege, ndege iliruka kutoka kiwanjani ikiwa na abiria 190 ndani yake pamoja na ‘crew’ ya watu 12 (Marubani na wahudumu) ambamo asilimia kubwa ya abiria walikuwa ni raia wa Israel pamoja na watu wenye asili ya kiyahudi. Ndege iliruka kutoka Tel Aviv mpaka jijini Anthens, Ugiriki ambapo ilichukua abiria wengine wapatao 58. Baada ya hapo ndege iliruka pasipo kujua kwamba kati aya abiria hao 58 waliowachukua Ugiriki ndani yao kulikuwa na abiria wanne ambao walikuwa ni wanachama wawili wa kikundi cha Popular Front For The Liberation of Palestine – External Operations (PFLP-EO) kutoka Plaestina na wanachama wawili wa kikundi cha Revolutionary Cells kutoka nchini Ujerumani.

    Baada ya abiria wote kukamilisha utaratibu na kupanda ndani ya ndege, ndege iliondoka uwanjani Athens mnamo amjira ya saa 6 na dakika 30 mchana kuelekea Paris, Ufaransa.
    Dakika chache baada ya ndege kuruka rubani mkuu wa ndege ambaye ndiye alikuwa ameshikili ‘usukani’ Bw. Michel Bacos akasikia kelele nyuma ya ndege wanakokaa abiria (cabin). Ili kujiridhisha kwamba kila kitu kiko sawa, rubani Michel Bacos akamuagiza msaidizi wake mmoja wapo ambaye ndiye alikuwa injinia wa ndege aende kuangalia nini kilikuwa kinaendelea.
    Mara tu baada ya msaidizi huyo kufungua mlango wa mbele wa chumba cha marubani, alikutana uso kwa uso na bastola usoni mwake iliyoshikiliwa na mtu ambaye mkononi alikuwa amebeba bomu la kurusha kwa mkono. Huku msaidizi huyo akiwa bado ameshikwa na bumbuwazi, mtu huyu mwenye bomu mkononi na bastola (jina lake anaitwa Wilfred Bose raia wa Ujerumani) alimsukuma yule injinia nakumrudisha tena ndani ya chumba cha marubani na kisha yeye mwenyewe pia kuingia.
    Mara tu baada ya kufika ndani ya chumba cha marubani, akawaweka chini ya ulinzi marubani ambao bado walikuwa kwenye mshituko wa mshangao na kisha kumnyanyua rubani msaidizi kutoka kwenye siti yake na kukaa yeye. Baada ya kukaa kwenye siti ya rubani msaidizi kitu cha kwanza alichokifanya haramia huyu Wilfre Bose ni kuchukua microphone ambayo marubani huwa wanatumia kutoa matangazo kwa abria, na baada ya kuiweka microphone akatoa tangazo lake la kwanza, kwa sauti ya utulivu iliyojaa lafudhi nzito ya kijerumani, akawasema; *“..kuanzia sasa ndege hii inaitwa HAIFA 1, badala ya Flight 139..”*
    Haifa ni eneo (mji) maarufu ulipo kaskazini mwa nchi ambayo abiria wengi waliopanda kwenye ndege hiyo walitambua kama Israel lakini watekaji hawa na watu wengine duniani wakitambua kama Palestina.
    Mara tu baada ya tangazo hili kusikika kwenye vipaza sauti vya ndege, abiria wote licha ya kuwa kwenye mshituko mkubwa wa ghafla lakini moja kwa moja waling’amua ni nini kilikuwa kinaendelea. Flight 139 au Haifa 1 kama alivyoibatiza aliyetoa tangazo, ilikuwa imetekwa na maharamia.
    Baada ya Tangazo hili, haramaia Wilfred Bose akamuamuru rubani Michel Bacos kuendesha ndege kuelekea mji wa Bengazhi, nchini Libya.
    Baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Bengazhi nchini Libya, ndege ilitumia karbia masaa saba uwanjani hapo kwa ajili ya kujaza ndege mafuta. Katika masaa hayo saba kuna mwanamama Patricia Martel mwenye asili ya Uingereza lakini akiwa ameolewa nchin Israel miaka michache iliyopita alifanya ‘kituko’ ambacho kilikuja kuwa na manufaa sana baadae. Wakati ambao ndege inaendelea kujaza mafuta kwa masaa yote hayo, huyu mama ambaye ni nesi kwa taaluma, alianza kulalamika juu ya maumivu ya tumbo yaliyopitiliza. Aliwaeleza watekaji kwamba ana ujauzito. Maharamia haya yakaruhusu wahudumu wa ndege wamuhudumie mwananmke mwenzao kwa vile ambavyo wataweza kwa kuzingatia kwamba ana mimba. Baada ya kuhudumiwa kwa karibia saa nzima, Patricia akatumua ujuzi wake wa unesi akafanya alicho kifanya na ghafla akaanza kutoka damu kiduchu sehemu za siri. Baada ya damu hizi kidogo kuanza kumtoka na kulalamika kuwa maumivu yamemzidia ndipo hapa ambapo wahudumu wa ndege wakaripoti kwa maharamia kuwa mimba ilikuwa imetoka.

    Kwa huruma na ili kuepusha taharuki ndani ya ndege maharamia hawa wakamuachia huru mwanamama Patricia Martel hapo uwanja wa ndege mjini Bengazhi ili aweze kupata uangalizi mzuri zaidi wa kidaktari.
    Lakini ukweli ni kwamba Patricia hakuwa na mimba wala hakuwa na maumivu yoyote tumboni, alichokifanya ilikuwa ni uigizaji pamoja na kuchanganya utaalamu wake wa fani ya unesi na kuweza kuwahadaa maharamia hao.
    Baada ya kuachiwa Patricia alikuwa ni mtu wa kwanza muhimu kutumiwa na Mossad kujua taarifa sahihi zaidi kuhusu nini hasa kilikuwa kinaendelea ndani ya ndege, kulikuwa na watekaji wangapi, jinsia zao, silaha zao na vingine vyote ambavyo alifanikiwa kuviona.
    Baada ya hapa Bose akamuamuru tena rubani Michel Bacos kurusha tena ndege angani pasipo kumueleza kuwa wanaeelekea wapi.
    Wakiwa angani ndipo alianza kumpa maagizo wapi hasa anataka waelekee. Upande wa abiria kwenye cabin ambao nao walikuwa wamewekwa chini ya ulinzi na maharamia wengine waliosalia, wao hawaku wanafahamu hata ni wapi walikuwa wanaeleke. Ndege ilikuwa inaruka angani kwa karibia masaa 24. Abiria wengi walianza kuhisi labda ndege ilikuwa inaruka kuelekea China au labda Siberia, na vichwani mwao walikuwa wanajiuliza kwa nini walikuwa wanapelekwa huko.
    Lakini laiti kama wangelijua mahali ambako walikuwa wanapelekwa basi wangetamani ndege hiyo ielekee kweli china.
    Baada ya ya takribani masaa 24 ndege kuwa angani tangu iruke kutoka Bengazhi nchini Libya, hatimaye abiria walisikia ndege ikitua na kugusa Runway ya kiwanja cha ndege mahali fulani dunia walipowasili lakini wakiwa hawafahamu ni mwapi hasa walikuwa.
    Baada ya matairi ya ndege tu kukanyaga lami za runaway na abiria kufungua ‘pazia’ (shutters) kwenye vioo vilivyopo pemnbeni mwa siti zao na kuangalia nje, mara moja wakaelewa wako wapi. Nje uwanjani kwenye lami, kulikuwa kumesimama lijitu la miraba minne lenye ngozi nyeusi tiiii likiwa na walinzi wa kijeshi na wengine waliovalia nguo za kiraia likiwa limezungukwa pande zote na walinzi hao. Mtu huyu mwenye umbo la kutisha kwa kipindi hiki alikuwa anajulikana ulimwenguni kote kutokana na matendo yake na ukatili wake. Kwa kutupa jicho mara moja tu haukuweza kukosea kujua kuwa pale kwenye lami uwanjani, alikuwa amesimama Generali Nduli Idd Amin Dadaa, ‘Field Marshal’. Swali lilokuwepo vichwani mwao lilikuwa limejibiwa tayari, wamepelekwa kwenye ardhi ya moja ya watawala ‘watemi’ na katili kuwahi kutokea juu ya uso wa dunia. Walikuwa nchini Uganda.
    Baada ya ndege kusimama abria wote 248 ambao wengi wao walikuwa ni raia wa Israel na wayahudi, walishushwa kutoka kwenye ndege na moja kwa moja kupelekwa ‘terminal’ ambayo kwa wakati huo ilikuwa haitumiki. Mpaka muda huu wakang’amua kwamba hawakuwa ‘abiria’ tena kama ambavyo waliondoka Tel Aviv, bali sasa walikuwa ni mateka wa maharamia haya ya kijerumani, palestina na jeshi la Uganda.

    Wakati huo huo…
    Nchini Israel katika jamii ya masuala ya usalama walikuwa wako kwenye bumbuwazi kuu, matukio ya dizaini hii huwa ni ya kushtukiza na yanatokea kipindi ambacho ‘haujajiandaa’. Pia kwa kipindi hiki bado Idara ya Ujasusi ya Mossad hawakuwa na Intelejensia ya kutosha za nchi nyingi za kiafrika, akili yao na nguvu yao yote ilikuwa kwenyekudhibiti juhudi za nchi za kiarabu kufuta Israel kutoka kwenye eneo hilo walilopo. Kwa hiyo kitendo cha raia wao wengi kiasi hiki kutekwa na kupelekwa Africa kilikuwa si tu na changamoto ya namana gani wanawaokoa bali pia kulikuwa na changamoto ya uwepo wa Intelijensia ya kutosha kuhusu eneo la Entebbe, Uganda kuweza kufanya oparesheni yoyote ya kijeshi.
    Ndipo hapa ambapo waziri mkuu wa kipindi hicho wa Israel Yitzhak Rabin akaitisha kikao cha maafisa wa ngazi za juu wa jeshi na Mossad na kuwauliza swali moja tu, *“…tunafanyeje?”*

    Itaendelea…
    #TheBold_Jf
    OPERATION ENTEBBE -1 Jina mbadala: Operation Thunderstorm/Operation Yonatan Watekelezaji: -MOSSAD - IDF (ISRAEL DEFENCE FORCE) Kitengo cha Weledi: Sayeret Matkal Mwaka wa utekelezaji: July, 1976 Nchi: Israel/Uganda Silaha za kukumbukwa: Lockheed C-130 Hurcules Wahusika wa kukumbukwa: - Yonatan Netanyahu (kaka wa Waziri Mkuu wa zamani Benjamin Netanyahu) -Ehud Barak (alikuja kuwa Waziri Mkuu miaka ya karibuni) MOSAD & IDF: OPERATION ENTEBBE Siku ya tarehe 27 June mwaka 1976 ilianza kama siku nyingine yioyote ndani ya uwanja wa ndege wa kimataifa katika mji mkuu wa nchi ya Israel Tel Aviv, uwanja ujulikanao kama Ben Gurion International Airport. Moja kati ya ndege ambayo ilikuwa inafanya safari yake katika siku ya elo ilikuwa ni ndege ya kampuni ya Air Frace ambao walikuwa na ndege yao ya Air France Flight 139 ambayo ni ndege aina ya Airbus A300B4-203 yenye namba ya usajili mkiani F-BVGG (c/n 019). Ndege hii ilikuwa inafanya safari yake katika siku ya leo kutoka Tel Aviv na ilikuwa inatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Charles DE Gaulle International Airport jijini Paris, Ufaransa. Baada ya taratibu na protokali zote za uwanja wa ndege kukamilika na abiria wote kukwea kwenye ndege, ndege iliruka kutoka kiwanjani ikiwa na abiria 190 ndani yake pamoja na ‘crew’ ya watu 12 (Marubani na wahudumu) ambamo asilimia kubwa ya abiria walikuwa ni raia wa Israel pamoja na watu wenye asili ya kiyahudi. Ndege iliruka kutoka Tel Aviv mpaka jijini Anthens, Ugiriki ambapo ilichukua abiria wengine wapatao 58. Baada ya hapo ndege iliruka pasipo kujua kwamba kati aya abiria hao 58 waliowachukua Ugiriki ndani yao kulikuwa na abiria wanne ambao walikuwa ni wanachama wawili wa kikundi cha Popular Front For The Liberation of Palestine – External Operations (PFLP-EO) kutoka Plaestina na wanachama wawili wa kikundi cha Revolutionary Cells kutoka nchini Ujerumani. Baada ya abiria wote kukamilisha utaratibu na kupanda ndani ya ndege, ndege iliondoka uwanjani Athens mnamo amjira ya saa 6 na dakika 30 mchana kuelekea Paris, Ufaransa. Dakika chache baada ya ndege kuruka rubani mkuu wa ndege ambaye ndiye alikuwa ameshikili ‘usukani’ Bw. Michel Bacos akasikia kelele nyuma ya ndege wanakokaa abiria (cabin). Ili kujiridhisha kwamba kila kitu kiko sawa, rubani Michel Bacos akamuagiza msaidizi wake mmoja wapo ambaye ndiye alikuwa injinia wa ndege aende kuangalia nini kilikuwa kinaendelea. Mara tu baada ya msaidizi huyo kufungua mlango wa mbele wa chumba cha marubani, alikutana uso kwa uso na bastola usoni mwake iliyoshikiliwa na mtu ambaye mkononi alikuwa amebeba bomu la kurusha kwa mkono. Huku msaidizi huyo akiwa bado ameshikwa na bumbuwazi, mtu huyu mwenye bomu mkononi na bastola (jina lake anaitwa Wilfred Bose raia wa Ujerumani) alimsukuma yule injinia nakumrudisha tena ndani ya chumba cha marubani na kisha yeye mwenyewe pia kuingia. Mara tu baada ya kufika ndani ya chumba cha marubani, akawaweka chini ya ulinzi marubani ambao bado walikuwa kwenye mshituko wa mshangao na kisha kumnyanyua rubani msaidizi kutoka kwenye siti yake na kukaa yeye. Baada ya kukaa kwenye siti ya rubani msaidizi kitu cha kwanza alichokifanya haramia huyu Wilfre Bose ni kuchukua microphone ambayo marubani huwa wanatumia kutoa matangazo kwa abria, na baada ya kuiweka microphone akatoa tangazo lake la kwanza, kwa sauti ya utulivu iliyojaa lafudhi nzito ya kijerumani, akawasema; *“..kuanzia sasa ndege hii inaitwa HAIFA 1, badala ya Flight 139..”* Haifa ni eneo (mji) maarufu ulipo kaskazini mwa nchi ambayo abiria wengi waliopanda kwenye ndege hiyo walitambua kama Israel lakini watekaji hawa na watu wengine duniani wakitambua kama Palestina. Mara tu baada ya tangazo hili kusikika kwenye vipaza sauti vya ndege, abiria wote licha ya kuwa kwenye mshituko mkubwa wa ghafla lakini moja kwa moja waling’amua ni nini kilikuwa kinaendelea. Flight 139 au Haifa 1 kama alivyoibatiza aliyetoa tangazo, ilikuwa imetekwa na maharamia. Baada ya Tangazo hili, haramaia Wilfred Bose akamuamuru rubani Michel Bacos kuendesha ndege kuelekea mji wa Bengazhi, nchini Libya. Baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Bengazhi nchini Libya, ndege ilitumia karbia masaa saba uwanjani hapo kwa ajili ya kujaza ndege mafuta. Katika masaa hayo saba kuna mwanamama Patricia Martel mwenye asili ya Uingereza lakini akiwa ameolewa nchin Israel miaka michache iliyopita alifanya ‘kituko’ ambacho kilikuja kuwa na manufaa sana baadae. Wakati ambao ndege inaendelea kujaza mafuta kwa masaa yote hayo, huyu mama ambaye ni nesi kwa taaluma, alianza kulalamika juu ya maumivu ya tumbo yaliyopitiliza. Aliwaeleza watekaji kwamba ana ujauzito. Maharamia haya yakaruhusu wahudumu wa ndege wamuhudumie mwananmke mwenzao kwa vile ambavyo wataweza kwa kuzingatia kwamba ana mimba. Baada ya kuhudumiwa kwa karibia saa nzima, Patricia akatumua ujuzi wake wa unesi akafanya alicho kifanya na ghafla akaanza kutoka damu kiduchu sehemu za siri. Baada ya damu hizi kidogo kuanza kumtoka na kulalamika kuwa maumivu yamemzidia ndipo hapa ambapo wahudumu wa ndege wakaripoti kwa maharamia kuwa mimba ilikuwa imetoka. Kwa huruma na ili kuepusha taharuki ndani ya ndege maharamia hawa wakamuachia huru mwanamama Patricia Martel hapo uwanja wa ndege mjini Bengazhi ili aweze kupata uangalizi mzuri zaidi wa kidaktari. Lakini ukweli ni kwamba Patricia hakuwa na mimba wala hakuwa na maumivu yoyote tumboni, alichokifanya ilikuwa ni uigizaji pamoja na kuchanganya utaalamu wake wa fani ya unesi na kuweza kuwahadaa maharamia hao. Baada ya kuachiwa Patricia alikuwa ni mtu wa kwanza muhimu kutumiwa na Mossad kujua taarifa sahihi zaidi kuhusu nini hasa kilikuwa kinaendelea ndani ya ndege, kulikuwa na watekaji wangapi, jinsia zao, silaha zao na vingine vyote ambavyo alifanikiwa kuviona. Baada ya hapa Bose akamuamuru tena rubani Michel Bacos kurusha tena ndege angani pasipo kumueleza kuwa wanaeelekea wapi. Wakiwa angani ndipo alianza kumpa maagizo wapi hasa anataka waelekee. Upande wa abiria kwenye cabin ambao nao walikuwa wamewekwa chini ya ulinzi na maharamia wengine waliosalia, wao hawaku wanafahamu hata ni wapi walikuwa wanaeleke. Ndege ilikuwa inaruka angani kwa karibia masaa 24. Abiria wengi walianza kuhisi labda ndege ilikuwa inaruka kuelekea China au labda Siberia, na vichwani mwao walikuwa wanajiuliza kwa nini walikuwa wanapelekwa huko. Lakini laiti kama wangelijua mahali ambako walikuwa wanapelekwa basi wangetamani ndege hiyo ielekee kweli china. Baada ya ya takribani masaa 24 ndege kuwa angani tangu iruke kutoka Bengazhi nchini Libya, hatimaye abiria walisikia ndege ikitua na kugusa Runway ya kiwanja cha ndege mahali fulani dunia walipowasili lakini wakiwa hawafahamu ni mwapi hasa walikuwa. Baada ya matairi ya ndege tu kukanyaga lami za runaway na abiria kufungua ‘pazia’ (shutters) kwenye vioo vilivyopo pemnbeni mwa siti zao na kuangalia nje, mara moja wakaelewa wako wapi. Nje uwanjani kwenye lami, kulikuwa kumesimama lijitu la miraba minne lenye ngozi nyeusi tiiii likiwa na walinzi wa kijeshi na wengine waliovalia nguo za kiraia likiwa limezungukwa pande zote na walinzi hao. Mtu huyu mwenye umbo la kutisha kwa kipindi hiki alikuwa anajulikana ulimwenguni kote kutokana na matendo yake na ukatili wake. Kwa kutupa jicho mara moja tu haukuweza kukosea kujua kuwa pale kwenye lami uwanjani, alikuwa amesimama Generali Nduli Idd Amin Dadaa, ‘Field Marshal’. Swali lilokuwepo vichwani mwao lilikuwa limejibiwa tayari, wamepelekwa kwenye ardhi ya moja ya watawala ‘watemi’ na katili kuwahi kutokea juu ya uso wa dunia. Walikuwa nchini Uganda. Baada ya ndege kusimama abria wote 248 ambao wengi wao walikuwa ni raia wa Israel na wayahudi, walishushwa kutoka kwenye ndege na moja kwa moja kupelekwa ‘terminal’ ambayo kwa wakati huo ilikuwa haitumiki. Mpaka muda huu wakang’amua kwamba hawakuwa ‘abiria’ tena kama ambavyo waliondoka Tel Aviv, bali sasa walikuwa ni mateka wa maharamia haya ya kijerumani, palestina na jeshi la Uganda. Wakati huo huo… Nchini Israel katika jamii ya masuala ya usalama walikuwa wako kwenye bumbuwazi kuu, matukio ya dizaini hii huwa ni ya kushtukiza na yanatokea kipindi ambacho ‘haujajiandaa’. Pia kwa kipindi hiki bado Idara ya Ujasusi ya Mossad hawakuwa na Intelejensia ya kutosha za nchi nyingi za kiafrika, akili yao na nguvu yao yote ilikuwa kwenyekudhibiti juhudi za nchi za kiarabu kufuta Israel kutoka kwenye eneo hilo walilopo. Kwa hiyo kitendo cha raia wao wengi kiasi hiki kutekwa na kupelekwa Africa kilikuwa si tu na changamoto ya namana gani wanawaokoa bali pia kulikuwa na changamoto ya uwepo wa Intelijensia ya kutosha kuhusu eneo la Entebbe, Uganda kuweza kufanya oparesheni yoyote ya kijeshi. Ndipo hapa ambapo waziri mkuu wa kipindi hicho wa Israel Yitzhak Rabin akaitisha kikao cha maafisa wa ngazi za juu wa jeshi na Mossad na kuwauliza swali moja tu, *“…tunafanyeje?”* Itaendelea… #TheBold_Jf
    ·29 Ansichten
  • OPERATION ENTEBBE -2

    Tayari zilikuwa zimepita siku tatu tangu ndege ya Air France Flight 139 kuondoka Tel Aviv na hatimaye kutekwa baada ya kuruka jijini Athens iliposimama kuchukua abiria. Lakini pia zilikuwa zimepita siku mbili tangu ndege hii kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda. Katika siku zote mbili hizi tangu ndege hii itue uwanjani hapa, rais wa Uganda Idd Amin Nduli Dadaa alikuwa anafika uwanjani hapo kila siku “kuwajulia hali” mateka hao.
    Kwa muda wa siku hizi zote mbili tangu ndege itue uwanjani hapo, magaidi hawa walioiteka ndege kwa kushirikiana na jeshi la Uganda kuchunguza majina ya kila abiria kama ambavyo yalikuwa yameandikwa kwenye pasport. Lengo lao la kufanya hivi ilikuwa ni kujaribu kufahamu uraia wa kila mateka waliye naye. Baada ya kufanya uchambuzi huu wa passport zote, hatimaye siku hii ya tatu, yaani tarehe 29 June 1976 kiongozi wa magaidi hawa Wilfred Bose akiwa na karatasi mkononi aliingi ndani ya terminal ambayo walikuwa wanaitumia kuwahifadhi mateka na kisha akaanza kusoma majina ya kila abiria. Alichokuwa anakifanya ni kusoma majina ya mateka ambao passport zao zilionyesha walikuwa ni raia wa Israel. Lakini pia alisoma majina ya mateka wengine ambao licha ya passport zao kuonyesha kuwa hawakuwa raia wa Israel lakini walikuwa na majina ya kiyahudi. Pamoja na hao pia mateka wote ambao walikuwa na uraia pacha na uraia huo mmojawapo ukiwa ni Israel basi nao waliunganishwa kwenye list hii.
    Baada ya kuwatenganisha raia wote wa Israel na kuwaweka kwenye chumba kingine peke yao hapo hapo kwenye terminal, kuna mwanadada raia wa Ufaransa aliyeitwa Jocelyne Monier yeye jina lake halikuitwa kwenye ile list ya wanaotakiwa kutengwa kwenye chumba kingine (Waisrael na Wayahudi). Lakini ‘boyfriend’ wake alikuwa ni Muisrael na aliitwa jina na kutengwa na wengine katika kile chumba kingine. Mwanadada huyu ili kuonyesha kumtia moyo mpenzi wake na kupinga huu ubaguzi uliokuwa unafanywa na hawa magaidi, kwa hiari yake alijipeleka kwenye chumba cha mateka wa Kiisrael. Si mwanadada huyu pekee ambaye alifanya kitendo hiki cha ushujaa, lakini pia kulikuwa na mwanamama mwingine aliitwa Janet Almog (rai wa Marekani) na mateka mwingine aliyeitwa Jean-Jacques Mimouni (raia wa Ufaransa) nao kwenye kuonyesha hali ya kuwaunga mkono wenzao waliotengwa kwenye chumba kingine na kupinga ubaguzi uliokuwa unafanywa na maharamia hawa, nao walijipeleka kwa hiari yao kwenye chumba ambacho mateka hao walikibatiza jina “Chumba cha Waisrael”, ambacho mateka wote walijua fika kwamba kuna jambo baya maharamia hao walikuwa wamepanga kulifanya.

    Licha ya maharamia kwa kushirikiana na jeshi la Uganda kufanya uchambuzi huu wa kina kuhusu uraia wa kila mateka waliye naye, lakini walifanya kosa kubwa sana ambalo lilkuja kuwagharimu sana hapo baadae. Kwenye uchambuzi wao wote huu walioufanya walishindwa kumng’amua mateka mmoja mwanajeshi wa Israel ambaye alikuwa ana uraia pacha na siku hiyo alikuwa anatumia passport ambayo sio ya Israel. Mateka huyu alikuja kuwa muhimu sana huko mbeleni kuwapatia Mossad Intelijensia mujarabu kabisa kuhusu watekaji, jengo wanaloshikilia mateka, na namana wanavyoshirikiana na jeshi la Uganda.
    Siku iliyofuata yaani June 30, maharamia haya wakawaachia mkupuo wa kwanza wa mateka wasio raia wa Israel au wayahudi. Katika mkupuo huu wa kwanza waliachia mateka 48 ambao walikuwa ni wazee, watoto na akina mama wenye watoto wadogo.
    Baada ya mkupuo huu wa kwanza wa kuwaachia mateka hawa wachache, maharamia wakaweka wazi matakwa yao ili waweze kuachia mateka wengine. Kwanza kabisa walitaka walipwe fedha kiasi cha dola za Kimarekani milioni 5. Na pili walitakakuachiwa kwa wafungwa 53 wenye asili ya kipalestina wanaotuhumiwa kwa ugaidi, ambao kati yao 40 walikuwa kwenye jela za Israel na 13 katika nchi nyingine za Ulaya. Watekaji hawa wakatoa ‘ultimutum’ kwamba kama matakwa yao hayatatekelezwa ndani ya masaa ishirini na nne yajayo (mpaka tarehe 1 July saa 8 mchana) basi wataanza kuua raia wa Israel mmoja baada ya mwingine.
    Dunia nzima ni kama ilisimama kwa masaa kadhaa kutokana na sintofahamu iliyogubika kila mahali. Sintofahamu hii ililetwa na ukweli kwamba, ilikuwa inajulikana wazi kwa miaka yote kwamba Israel wana sera ya kutofanya mazungumzo au makubaliano na Magaidi. Kwahiyo kila mtu alikuwa nafahamu kuwa kuna uwezekano mkubwa ndani ya masaa 24 yajayo ulimwengu ukashuhidia watu zaidi ya 200 wakichinjwa kama kuku.

    NCHINI ISRAEL: KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI
    Nchini Israel kikao cha dharura cha baraza la mawaziri kilikuwa kimeitishwa na waziri Mkuu Yitzhak Rabin kujadili kuhusu hatua za kuchukua kuokoa raia wake ambao wameshikiliwa mateka huko uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda.
    Hali ya kikao ilikuwa tete sana kutokana na kila dakika waliyokuwa wanaitumia kujadili ndivyo ambavyo walikuwa wanaikaribia saa 8 mchana ya tarehe 1 July. Walipowasilana na Ujerumani na Ufaransa ambao nao walikuwa na baadhi ya wafungwa wa Kipalestina ambao watekaji walitaka waachiwe… walipowaomba ushirikiano wao kuhusu kukabali kuachia hao wafungwa, Ujerumani na Ufaransa walikataa katakata kuachia hata mfungwa mmoja wa Kipalestina ambaye alikuwa kwenye magereza zao.
    Sintofahamu ilizidi kuongezeka. Masaa yalizidi kuyoyoma. Saa 8 mchana ya tarehe 1 July ilizidi kukaribia. Harufu ya damu ilikuwa inabisha hodi mlangoni kwao. Licha ya weledi wao wote walionao lakini mbele yao waliona giza.
    Inapaswa kukumbukwa kwamba Idd Amin aliwahi kupatiwa mafunzo ya weledi wa kijeshi nchini Isarel (Special Force Training). Kwa hiyo baraza la mawaziri likamuagiza Baruch Bar-Lev, kamanda mstaafu wa IDF ambaye alihusika kumpatia mafunzo ya kijeshi Amin kipindi yuko Israel na kufanikiwa kujenga naye ukaribu. Baraza la Mawaziri likamuagiza Baruck (marafiki zake humuita “Burka”) kufanya mawasiliano na Rais huyo wa Uganda ili kujaribu kumuomba awashawishi magaidi wanaoshikilia mateka kwenye uwanja wake wa ndege wa Entebbe wawaachie mateka hao bila masharti magumu.
    Kupitia kwa Burka, Israel ilifikia mpaka hatua ya kumuahidi Idd Amin kuwa kama atafanikisha kuachiwa kwa mateka hao basi watatumia ushawishi walionao kuhakikisha kuwa Amin anatunukiwa tuzo ya amani ya Nobel.
    Lakini Amin hakulegeza msimamo, akaendelea kuwasisitiza kuwa hakuna namna nyingine yeyote ambayo mateka hao wataachiwa bila masharti yaliyotolewa na watekaji kutimizwa.
    Baada ya juhudi hii ya kumuhonga ‘tuzo’ kugonga mwamba, Waziri Mkuu wa Israel akawasiliana na serikali ya Marekani na kuwaomba wamshawishi Rais wa Misri Anwar Sadat ambaye alikuwa anaheshimiana sana na Amin ili amshawishi kuwaamuru magaidi yaliyoko uwanjani kwake Entebbe waachiemateka bila masharti magumu.
    Amin bado akashikilia msimamo kwamba hakuna mateka atakayeachiwa pasipo masharti yaliyotolewa kutimizwa.
    Juhudi hizi za kumshawishi Amin zilikula muda mwingi sana na hatimaye wakajikuta tayari kulikuwa kumekucha asubuhi. Mbele yao kulikuwa kumebakia masaa chini ya manane kabla ya damu ya zaidi ya watu 200 kumwagika.
    Baraza la mawaziri la Israel likamuomba Amin aongee na watekaji wakubali kusogeza siku mbele ili kuipa serikali ya Israel muda wakutosha kushughulikia lojistiki na kushawishi Ujerumani na Ufaransa ili waweze kutimiza sharti la kuachiwa kwa wafungwa wa kipalestina 53 wanaotuhumiwa kwa ugaidi.
    Rais Idd Amin baada ya kushawishiwa sana akakubali ombi hili na akaieleza serikali ya Israel kwamba ni siku tatu tu pekee zinaongezwa, yaani ikimaanisha kwamba siku zitaongezwa mpaka tarehe 4 July, saa 8 mchana. Serikali ya Israel ikakubliana na hili.
    Mchana wa siku hiyo, serikali ilitoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari wakilaani vitendo vya kigaidi na hususani matukio ya utekeji wa raia wasio na hatia, na pia ikaendelea kusisitiza kuhusu sera yake ya kutojadili na magaidi. Lakini taarifa hii ikamalizia kwa kueleza kuwa kwa kujali zaidi uhai wa zaidi ya raia 200 ambao bado wanashikiliwa na magaidi hayo, na kujali maumivu ambayo familia zao na taifa zima linapitia, wamekubali kutimiza sharti la magaidi hao la kuwalipa fedha za kimarekani dola milioni tano pamoja na kuachiwa kwa wafungwa wa kipalestina 53 wenye tuhuma za ugaidi.
    Ilikuwa ni moja ya matukio machache ambayo yaliishangaza dunia kwa Israel kukubali kushindwa hadharani. Kwa upande wa maadui wa Israel hii ilikuwa ni sherehe kubwa kwao. Na kwa upande wa Isarel na maswahiba zake hii iikuwa ni maombolezo makubwa.
    Amin na wenzake kule Uganda walikuwa wanasherehekea baada ya taarifa hii kutolewa kwa vyombo vya habari. Walihsi kabisa harufu ya ushindi inanukia kwenye pua zao.
    Kitu ambacho walikuwa hawafahamu ilikuwa ni kwamba, Israel walikuwa wanawafanyia ‘mchezo’ wa kisaikolojia ili Amin, jeshi lake na watekaji wajiamini kwa kuona kuwa ushindi umeegemea upande wao na hatimaye wajisahau kutokana na kujiamini huku.

    NYUMA YA PAZIA
    Huko Tel aviv, makamanda wa IDF na maafisa wa Mossad walikuwa wamekusanyika katika conference room ya mako makuu ya wizara ya ulinzi kuweka mkakati wa oparesheni ya uokozi (rescue mission) wa mateka wanaoshikiliwa katika uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda.
    Kati ya watu muhimu ambao walikuwepo kwenye kikao hiki alikuwa ni Waziri Mkuu Rabin na Ehud Barak ambaye kipindi hicho alikuwa kamanda wa ngazi za juu kwenye jeshi anayeongoza kitengo cha Intelijensia ya jeshi (Military Intelligence).
    Moja kati ya vitu muhimu ambavyo viliwasaidia ilikuwa ni taarifa ya intelijensia iliyoletwa na Mossad kwamba uwanja wa ndege wa Entebbe ulijengwa na kampuni ya Kiisrael inayoitwa Solel Boneh.
    Kwahiyo muwakilishi kutoka katika kampuni hii ya ujenzi naye akaitwa kikaoni kwa ajili ya kuwasilisha michoro kuhusu jengo lote na uwanja wa ndege wa Entebbe ulivyo.
    Lakini pia wakati huo huo kulikuwa na maafisa wa Mossad ambao walikuwa ufaransa kuwahoji wale mateka ambao walikuwa wameachiwa awali. Mtu muhimu zaidi ambaye alitoa taarifa nzuri kwa Mossad alikuwa ni yule afisa wa jeshi niliyemuelezea awali kwamba alikuwa na uraia wan chi mbili (Israel na Ufaransa) na siku hii alikuwa ametumia passport ya nchi ya ufaransa hivyo watekaji walimuachia pamoja na wenzake wa kundi la kwanza lile la watu 48.
    Bwana huyu alitoa taarifa muhimu zaidi kuhusu kilichokuwa kinaendelea katika uwanja wa ndege wa Entebbe, kwa kuwa yeye tofauti na wenzake kutokana na uzoefu wake wa jeshi alikuwa aliweza kuwaeleza Mossad kuhusu ni salaha za namna gani watekaji walikuwa nazo, kulikuwa na ndege za aina gani za kijeshi pale uwanjani (Idd Amin aliamuru Air Force ya Uganda kulinda uwanja huo masaa 24), pia aliweza kuwaeleza kuhusu ‘rotation’ ya ulinzi ya jeshi la Uganda pamoja na taarifa nyingine muhimu ambazo abiria wengine wasingeweza kuzitilia maanani au kkuzieleza kwa ufasaha.
    Baada ya kupata intelijensia ya kutosha, mkakati wa awali ambao ulipendekezwa na jeshi ulikuwa ni kutumia ndege ya kijeshi na kisha kudondosha makomando kwenye ziwa Viktoria na kutoka hapo watatumia boti za mpira kuvuka mpaka nchi kavu na hatimaye kuelekea uwanja wa ndege ambao haukuwa mbali sana na ziwa Viktoria.
    Mkakati huu ulikuwa ni mzuri lakini ulihairishwa baada ya kupewa taarifa kuwa ziwa Viktoria lilikuwa na mamba wengi na ingeweza kuhatarisha uhai wa hawa makomando kabla hata ya kufika kwenye uwanja wa ndege. Kwahiyo ilikuwa dhahiri kwamba mkakati wowote ambao utawekwa ni lazima uwe wa kuvamia kutokea nchi kavu na ikiwezekana kutoka nchi jirani.
    Changamoto kubwa zaidi ilikuwa ni usafiri. Yaani kwamba oparesheni hii ilikuwa si tu kwamba makomando wanaotumwa kutekeleza wanaenda kupambana na magaidi wanne tu walioteka ndege, bali ilikuwa ni kana kwamba wanaenda kupambana na jeshi zima la Uganda. Kwa hiyo kikosi cha makomando ambacho kitatumwa kwenda huko lazima kiwe na watu wengi wa kutosha na pia lazima wachukue silaha nzito za kutosha. Ili kufaniskisha safari yenye makomando wengi hivi na vifaa vizito ilikuwa ni lazima kutumia ndege kubwa za kijeshi zenye uwezo mkubwa pia na hakukuwa na chaguo zuri zaid ya kutumia ndege za kijeshi za LOCKHEED C-130 HERCULES. Sasa changamoto ilikuwa inakuja kwamba huwezi kurusha dege kubwa kama hii kwenda na kurudi kutoka Israel mpaka Uganda bila kujaza mafuta tena japo mara moja.
    Katika kipindi hiki bado Israel walikuwa hawajawa na uwezo wa kufanya ‘Aerial Refuel’, yaani ndege kujazwa mafuta kwa kutumia ndege nyingine ikiwa angani. Lakini pia ilikuwa ni lazima madege hayo yakikaribia Uganda yaruke chini chini ili kukwepa kudunguliwa na kuikwepa rada ya kijeshi. Kwa hiyo ilikuwa ni lazima kupata nchi ndani ya afrika Mashariki ambao watakubali madege hayo ya kijeshi ya Israel kutua kwenye uwanja wake wa ndege na kujaza mafuta lakini pia kujiandaa na kuanzisha operation kutokea hapo na pia anga lao kutumika kuanzisha shambulizi la kijeshi kuelekea Uganda.
    Sasa japokuwa nchi zote za Afrika Mashariki zilikuwa hazikubaliana na kitendo cha Rais wa Uganda kushirikiana na watekaji, lakini hakukuwa na hata nchi moja ambayo ilikuwa iko tayari kuingia kwenye mzozo na Idd Amin kwa kuruhusu viwanja vya vya ndege kutumika na ndege za jeshi la Israel au wanajeshi kujiandaa kuvamia Entebbe au pia kuruhusu anga lao kutumia na jeshi la Israel.
    Ndipo hapa ambapo kwa haraka sana siku hiyo hiyo Waziri Mkuu Rabin akamtuma Ehud Barak na maafisa wachache wa Mossad kwenda Kenya kushawishi serikali ya Mzee Jomo Kenyatta iruhusu ndege za jeshi la Isarel kutumia kiwanja chao cha ndege. Ehud barak na wenzake hawakwenda tu moja kwa moja kwa Mzee Kenyatta, bali kwanza walienda kwa Waziri wa kilimo wa kipindi hicho Bw. Bruce McKenzie ambaye huyu aliwahi kuwa afisa wa Idara ya ujasusi ya Uingereza, MI6 na pia alikuwa swahiba mkubwa wa Ehud Barak.

    Kwa hiyo Israel ikamtumia Bruce McKenzie kumshawishi Mzee Jomo Kenyatta kuruhusu anga la Kenya na viwanjavya ndege kutumiwa na makomando wa Israel na ndege zao.
    Ehud Barak na maafisa wa Mossad hawakuishia hapa tu, bali pia walifanya vikao vya siri na wafanyabiashara wakubwa nchini Kenya wenye asili ya Israel na wale ambao walikuwa na ‘marafiki’ wa Israel kuwaomba watumie ushawishi wao wa kisiasa na kiuchumi wasaidie kumshawishi Kenyatta kukubali ombi la seriakli ya Israael viwanja vyao kutumika na ndege za kijeshi za Israel na makondo wake.
    Baada ya mashinikizo haya kutoka kila upande, Mzee Kenyatta hakuwa na chaguo linguine zaidi ya kukubali ombi lao.
    Bwana huyu McKenzie pia alikuwa na ndege yakebinafsi, na Ehud Barak akaona fursa. Walitumia ndege hii ya kiraia kuruka mpaka Uganda mijini Entebbe na kukatiza juu ya anga la uwanja wa ndege wa Entebbe na walipokuwa wanapita juu ya anga la uwanja wa ndege, Ehud Barak akatumia fursa hii kupiga picha kila eneo la uwanja. Kwa kuwa hii ilikuwa ni ndege ya kiraia, jeshi la Uganda hawakushughulika nayo.
    Picha hizi zilizopigwa na Ehud Barak zilikuja kuwa na umuhimumkubwa katika maandalizi ya mwisho ya oparesheni ya makomando wa Isarel Kuvamia uwanja huu.
    Mpaka kufikia hapa maandalizi yote muhimu yalikuwa yamekamilika.
    WAKATI HUO HUO
    Upande wa watekaji kule Uganda walikuwa wanasubria mifwedha yao dola milioni 5 za kimarekani.
    Rais Idd Amin naye baada ya kufikia makubaliano na Israel kuwa masharti ya fedha na wafungwa wa kipalestina kuachiwa tarehe 4 July, naye ‘akarelax’ na akaona huo ndio muda wa kutekeleza majukumu Mengine akisubiria tarehe 4 July ifike.
    Katika kipindi hiki Idd amin ndiye alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwa kuzingatia utaratibu wa uenyekiti kuzunguka kwa kila nchi kwa mwaka mmoja mmoja na wiki hii alikuwa anatakiwa kwenye kikao cha Umoja wa Afrika kilichokuwa kinafanyika Mauritius. Kwa hiyo Amin akafunga safari kuelekea Mauritius kwenda kukabidhi kijiti cha Uenyekiti.
    Ehud Barak aliposikia taarifa hii, kwa kutumia akili yake kubwa ya kuzaliwa aliyojaliwa na uzoefu wake wa ujasusi, aliona fursa adhimu kabisa hapa. Akawasiliana na walioko kikaoni huko Tel Aviv na kuwaeleza taarifa ambazo awali wote hawakuielewa.
    Ehud Barak: “Idd Amin akiwa ndani ya Uganda huwa anatumia Mercedes Limousine katika msafara wake”
    Waziri Mkuu Rabin: “Ok! Limefanyaje?’
    Ehud Barak: “Nataka mtafute gari kama hiyo… Mercedes Limousine”
    Waziri Mkuu Rabin: “la kazi gani?”
    Ehud Barak: “siku ambayo kikosi cha makomando wakipanda kwenye ndege kutoka huko Israel kwenda Uganda, gari hilo nataka pia lipakiwe ndani ya ndge!”
    Kwa dakika kadhaa wote ambao walikuwa wanamsikiliza pale kikaoni kupitia simu hakuna ambaye alielewa nini hasa Ehud Barak alikuwa anapendekeza.
    Yalikuwa yamebaki masaa machache tu ambapo, weledi, ushujaa na uzalendo uliotukuka ulikuwa unaedna kudhihirika.

    Itaendelea
    #TheBOLD_JF
    OPERATION ENTEBBE -2 Tayari zilikuwa zimepita siku tatu tangu ndege ya Air France Flight 139 kuondoka Tel Aviv na hatimaye kutekwa baada ya kuruka jijini Athens iliposimama kuchukua abiria. Lakini pia zilikuwa zimepita siku mbili tangu ndege hii kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda. Katika siku zote mbili hizi tangu ndege hii itue uwanjani hapa, rais wa Uganda Idd Amin Nduli Dadaa alikuwa anafika uwanjani hapo kila siku “kuwajulia hali” mateka hao. Kwa muda wa siku hizi zote mbili tangu ndege itue uwanjani hapo, magaidi hawa walioiteka ndege kwa kushirikiana na jeshi la Uganda kuchunguza majina ya kila abiria kama ambavyo yalikuwa yameandikwa kwenye pasport. Lengo lao la kufanya hivi ilikuwa ni kujaribu kufahamu uraia wa kila mateka waliye naye. Baada ya kufanya uchambuzi huu wa passport zote, hatimaye siku hii ya tatu, yaani tarehe 29 June 1976 kiongozi wa magaidi hawa Wilfred Bose akiwa na karatasi mkononi aliingi ndani ya terminal ambayo walikuwa wanaitumia kuwahifadhi mateka na kisha akaanza kusoma majina ya kila abiria. Alichokuwa anakifanya ni kusoma majina ya mateka ambao passport zao zilionyesha walikuwa ni raia wa Israel. Lakini pia alisoma majina ya mateka wengine ambao licha ya passport zao kuonyesha kuwa hawakuwa raia wa Israel lakini walikuwa na majina ya kiyahudi. Pamoja na hao pia mateka wote ambao walikuwa na uraia pacha na uraia huo mmojawapo ukiwa ni Israel basi nao waliunganishwa kwenye list hii. Baada ya kuwatenganisha raia wote wa Israel na kuwaweka kwenye chumba kingine peke yao hapo hapo kwenye terminal, kuna mwanadada raia wa Ufaransa aliyeitwa Jocelyne Monier yeye jina lake halikuitwa kwenye ile list ya wanaotakiwa kutengwa kwenye chumba kingine (Waisrael na Wayahudi). Lakini ‘boyfriend’ wake alikuwa ni Muisrael na aliitwa jina na kutengwa na wengine katika kile chumba kingine. Mwanadada huyu ili kuonyesha kumtia moyo mpenzi wake na kupinga huu ubaguzi uliokuwa unafanywa na hawa magaidi, kwa hiari yake alijipeleka kwenye chumba cha mateka wa Kiisrael. Si mwanadada huyu pekee ambaye alifanya kitendo hiki cha ushujaa, lakini pia kulikuwa na mwanamama mwingine aliitwa Janet Almog (rai wa Marekani) na mateka mwingine aliyeitwa Jean-Jacques Mimouni (raia wa Ufaransa) nao kwenye kuonyesha hali ya kuwaunga mkono wenzao waliotengwa kwenye chumba kingine na kupinga ubaguzi uliokuwa unafanywa na maharamia hawa, nao walijipeleka kwa hiari yao kwenye chumba ambacho mateka hao walikibatiza jina “Chumba cha Waisrael”, ambacho mateka wote walijua fika kwamba kuna jambo baya maharamia hao walikuwa wamepanga kulifanya. Licha ya maharamia kwa kushirikiana na jeshi la Uganda kufanya uchambuzi huu wa kina kuhusu uraia wa kila mateka waliye naye, lakini walifanya kosa kubwa sana ambalo lilkuja kuwagharimu sana hapo baadae. Kwenye uchambuzi wao wote huu walioufanya walishindwa kumng’amua mateka mmoja mwanajeshi wa Israel ambaye alikuwa ana uraia pacha na siku hiyo alikuwa anatumia passport ambayo sio ya Israel. Mateka huyu alikuja kuwa muhimu sana huko mbeleni kuwapatia Mossad Intelijensia mujarabu kabisa kuhusu watekaji, jengo wanaloshikilia mateka, na namana wanavyoshirikiana na jeshi la Uganda. Siku iliyofuata yaani June 30, maharamia haya wakawaachia mkupuo wa kwanza wa mateka wasio raia wa Israel au wayahudi. Katika mkupuo huu wa kwanza waliachia mateka 48 ambao walikuwa ni wazee, watoto na akina mama wenye watoto wadogo. Baada ya mkupuo huu wa kwanza wa kuwaachia mateka hawa wachache, maharamia wakaweka wazi matakwa yao ili waweze kuachia mateka wengine. Kwanza kabisa walitaka walipwe fedha kiasi cha dola za Kimarekani milioni 5. Na pili walitakakuachiwa kwa wafungwa 53 wenye asili ya kipalestina wanaotuhumiwa kwa ugaidi, ambao kati yao 40 walikuwa kwenye jela za Israel na 13 katika nchi nyingine za Ulaya. Watekaji hawa wakatoa ‘ultimutum’ kwamba kama matakwa yao hayatatekelezwa ndani ya masaa ishirini na nne yajayo (mpaka tarehe 1 July saa 8 mchana) basi wataanza kuua raia wa Israel mmoja baada ya mwingine. Dunia nzima ni kama ilisimama kwa masaa kadhaa kutokana na sintofahamu iliyogubika kila mahali. Sintofahamu hii ililetwa na ukweli kwamba, ilikuwa inajulikana wazi kwa miaka yote kwamba Israel wana sera ya kutofanya mazungumzo au makubaliano na Magaidi. Kwahiyo kila mtu alikuwa nafahamu kuwa kuna uwezekano mkubwa ndani ya masaa 24 yajayo ulimwengu ukashuhidia watu zaidi ya 200 wakichinjwa kama kuku. NCHINI ISRAEL: KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI Nchini Israel kikao cha dharura cha baraza la mawaziri kilikuwa kimeitishwa na waziri Mkuu Yitzhak Rabin kujadili kuhusu hatua za kuchukua kuokoa raia wake ambao wameshikiliwa mateka huko uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda. Hali ya kikao ilikuwa tete sana kutokana na kila dakika waliyokuwa wanaitumia kujadili ndivyo ambavyo walikuwa wanaikaribia saa 8 mchana ya tarehe 1 July. Walipowasilana na Ujerumani na Ufaransa ambao nao walikuwa na baadhi ya wafungwa wa Kipalestina ambao watekaji walitaka waachiwe… walipowaomba ushirikiano wao kuhusu kukabali kuachia hao wafungwa, Ujerumani na Ufaransa walikataa katakata kuachia hata mfungwa mmoja wa Kipalestina ambaye alikuwa kwenye magereza zao. Sintofahamu ilizidi kuongezeka. Masaa yalizidi kuyoyoma. Saa 8 mchana ya tarehe 1 July ilizidi kukaribia. Harufu ya damu ilikuwa inabisha hodi mlangoni kwao. Licha ya weledi wao wote walionao lakini mbele yao waliona giza. Inapaswa kukumbukwa kwamba Idd Amin aliwahi kupatiwa mafunzo ya weledi wa kijeshi nchini Isarel (Special Force Training). Kwa hiyo baraza la mawaziri likamuagiza Baruch Bar-Lev, kamanda mstaafu wa IDF ambaye alihusika kumpatia mafunzo ya kijeshi Amin kipindi yuko Israel na kufanikiwa kujenga naye ukaribu. Baraza la Mawaziri likamuagiza Baruck (marafiki zake humuita “Burka”) kufanya mawasiliano na Rais huyo wa Uganda ili kujaribu kumuomba awashawishi magaidi wanaoshikilia mateka kwenye uwanja wake wa ndege wa Entebbe wawaachie mateka hao bila masharti magumu. Kupitia kwa Burka, Israel ilifikia mpaka hatua ya kumuahidi Idd Amin kuwa kama atafanikisha kuachiwa kwa mateka hao basi watatumia ushawishi walionao kuhakikisha kuwa Amin anatunukiwa tuzo ya amani ya Nobel. Lakini Amin hakulegeza msimamo, akaendelea kuwasisitiza kuwa hakuna namna nyingine yeyote ambayo mateka hao wataachiwa bila masharti yaliyotolewa na watekaji kutimizwa. Baada ya juhudi hii ya kumuhonga ‘tuzo’ kugonga mwamba, Waziri Mkuu wa Israel akawasiliana na serikali ya Marekani na kuwaomba wamshawishi Rais wa Misri Anwar Sadat ambaye alikuwa anaheshimiana sana na Amin ili amshawishi kuwaamuru magaidi yaliyoko uwanjani kwake Entebbe waachiemateka bila masharti magumu. Amin bado akashikilia msimamo kwamba hakuna mateka atakayeachiwa pasipo masharti yaliyotolewa kutimizwa. Juhudi hizi za kumshawishi Amin zilikula muda mwingi sana na hatimaye wakajikuta tayari kulikuwa kumekucha asubuhi. Mbele yao kulikuwa kumebakia masaa chini ya manane kabla ya damu ya zaidi ya watu 200 kumwagika. Baraza la mawaziri la Israel likamuomba Amin aongee na watekaji wakubali kusogeza siku mbele ili kuipa serikali ya Israel muda wakutosha kushughulikia lojistiki na kushawishi Ujerumani na Ufaransa ili waweze kutimiza sharti la kuachiwa kwa wafungwa wa kipalestina 53 wanaotuhumiwa kwa ugaidi. Rais Idd Amin baada ya kushawishiwa sana akakubali ombi hili na akaieleza serikali ya Israel kwamba ni siku tatu tu pekee zinaongezwa, yaani ikimaanisha kwamba siku zitaongezwa mpaka tarehe 4 July, saa 8 mchana. Serikali ya Israel ikakubliana na hili. Mchana wa siku hiyo, serikali ilitoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari wakilaani vitendo vya kigaidi na hususani matukio ya utekeji wa raia wasio na hatia, na pia ikaendelea kusisitiza kuhusu sera yake ya kutojadili na magaidi. Lakini taarifa hii ikamalizia kwa kueleza kuwa kwa kujali zaidi uhai wa zaidi ya raia 200 ambao bado wanashikiliwa na magaidi hayo, na kujali maumivu ambayo familia zao na taifa zima linapitia, wamekubali kutimiza sharti la magaidi hao la kuwalipa fedha za kimarekani dola milioni tano pamoja na kuachiwa kwa wafungwa wa kipalestina 53 wenye tuhuma za ugaidi. Ilikuwa ni moja ya matukio machache ambayo yaliishangaza dunia kwa Israel kukubali kushindwa hadharani. Kwa upande wa maadui wa Israel hii ilikuwa ni sherehe kubwa kwao. Na kwa upande wa Isarel na maswahiba zake hii iikuwa ni maombolezo makubwa. Amin na wenzake kule Uganda walikuwa wanasherehekea baada ya taarifa hii kutolewa kwa vyombo vya habari. Walihsi kabisa harufu ya ushindi inanukia kwenye pua zao. Kitu ambacho walikuwa hawafahamu ilikuwa ni kwamba, Israel walikuwa wanawafanyia ‘mchezo’ wa kisaikolojia ili Amin, jeshi lake na watekaji wajiamini kwa kuona kuwa ushindi umeegemea upande wao na hatimaye wajisahau kutokana na kujiamini huku. NYUMA YA PAZIA Huko Tel aviv, makamanda wa IDF na maafisa wa Mossad walikuwa wamekusanyika katika conference room ya mako makuu ya wizara ya ulinzi kuweka mkakati wa oparesheni ya uokozi (rescue mission) wa mateka wanaoshikiliwa katika uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda. Kati ya watu muhimu ambao walikuwepo kwenye kikao hiki alikuwa ni Waziri Mkuu Rabin na Ehud Barak ambaye kipindi hicho alikuwa kamanda wa ngazi za juu kwenye jeshi anayeongoza kitengo cha Intelijensia ya jeshi (Military Intelligence). Moja kati ya vitu muhimu ambavyo viliwasaidia ilikuwa ni taarifa ya intelijensia iliyoletwa na Mossad kwamba uwanja wa ndege wa Entebbe ulijengwa na kampuni ya Kiisrael inayoitwa Solel Boneh. Kwahiyo muwakilishi kutoka katika kampuni hii ya ujenzi naye akaitwa kikaoni kwa ajili ya kuwasilisha michoro kuhusu jengo lote na uwanja wa ndege wa Entebbe ulivyo. Lakini pia wakati huo huo kulikuwa na maafisa wa Mossad ambao walikuwa ufaransa kuwahoji wale mateka ambao walikuwa wameachiwa awali. Mtu muhimu zaidi ambaye alitoa taarifa nzuri kwa Mossad alikuwa ni yule afisa wa jeshi niliyemuelezea awali kwamba alikuwa na uraia wan chi mbili (Israel na Ufaransa) na siku hii alikuwa ametumia passport ya nchi ya ufaransa hivyo watekaji walimuachia pamoja na wenzake wa kundi la kwanza lile la watu 48. Bwana huyu alitoa taarifa muhimu zaidi kuhusu kilichokuwa kinaendelea katika uwanja wa ndege wa Entebbe, kwa kuwa yeye tofauti na wenzake kutokana na uzoefu wake wa jeshi alikuwa aliweza kuwaeleza Mossad kuhusu ni salaha za namna gani watekaji walikuwa nazo, kulikuwa na ndege za aina gani za kijeshi pale uwanjani (Idd Amin aliamuru Air Force ya Uganda kulinda uwanja huo masaa 24), pia aliweza kuwaeleza kuhusu ‘rotation’ ya ulinzi ya jeshi la Uganda pamoja na taarifa nyingine muhimu ambazo abiria wengine wasingeweza kuzitilia maanani au kkuzieleza kwa ufasaha. Baada ya kupata intelijensia ya kutosha, mkakati wa awali ambao ulipendekezwa na jeshi ulikuwa ni kutumia ndege ya kijeshi na kisha kudondosha makomando kwenye ziwa Viktoria na kutoka hapo watatumia boti za mpira kuvuka mpaka nchi kavu na hatimaye kuelekea uwanja wa ndege ambao haukuwa mbali sana na ziwa Viktoria. Mkakati huu ulikuwa ni mzuri lakini ulihairishwa baada ya kupewa taarifa kuwa ziwa Viktoria lilikuwa na mamba wengi na ingeweza kuhatarisha uhai wa hawa makomando kabla hata ya kufika kwenye uwanja wa ndege. Kwahiyo ilikuwa dhahiri kwamba mkakati wowote ambao utawekwa ni lazima uwe wa kuvamia kutokea nchi kavu na ikiwezekana kutoka nchi jirani. Changamoto kubwa zaidi ilikuwa ni usafiri. Yaani kwamba oparesheni hii ilikuwa si tu kwamba makomando wanaotumwa kutekeleza wanaenda kupambana na magaidi wanne tu walioteka ndege, bali ilikuwa ni kana kwamba wanaenda kupambana na jeshi zima la Uganda. Kwa hiyo kikosi cha makomando ambacho kitatumwa kwenda huko lazima kiwe na watu wengi wa kutosha na pia lazima wachukue silaha nzito za kutosha. Ili kufaniskisha safari yenye makomando wengi hivi na vifaa vizito ilikuwa ni lazima kutumia ndege kubwa za kijeshi zenye uwezo mkubwa pia na hakukuwa na chaguo zuri zaid ya kutumia ndege za kijeshi za LOCKHEED C-130 HERCULES. Sasa changamoto ilikuwa inakuja kwamba huwezi kurusha dege kubwa kama hii kwenda na kurudi kutoka Israel mpaka Uganda bila kujaza mafuta tena japo mara moja. Katika kipindi hiki bado Israel walikuwa hawajawa na uwezo wa kufanya ‘Aerial Refuel’, yaani ndege kujazwa mafuta kwa kutumia ndege nyingine ikiwa angani. Lakini pia ilikuwa ni lazima madege hayo yakikaribia Uganda yaruke chini chini ili kukwepa kudunguliwa na kuikwepa rada ya kijeshi. Kwa hiyo ilikuwa ni lazima kupata nchi ndani ya afrika Mashariki ambao watakubali madege hayo ya kijeshi ya Israel kutua kwenye uwanja wake wa ndege na kujaza mafuta lakini pia kujiandaa na kuanzisha operation kutokea hapo na pia anga lao kutumika kuanzisha shambulizi la kijeshi kuelekea Uganda. Sasa japokuwa nchi zote za Afrika Mashariki zilikuwa hazikubaliana na kitendo cha Rais wa Uganda kushirikiana na watekaji, lakini hakukuwa na hata nchi moja ambayo ilikuwa iko tayari kuingia kwenye mzozo na Idd Amin kwa kuruhusu viwanja vya vya ndege kutumika na ndege za jeshi la Israel au wanajeshi kujiandaa kuvamia Entebbe au pia kuruhusu anga lao kutumia na jeshi la Israel. Ndipo hapa ambapo kwa haraka sana siku hiyo hiyo Waziri Mkuu Rabin akamtuma Ehud Barak na maafisa wachache wa Mossad kwenda Kenya kushawishi serikali ya Mzee Jomo Kenyatta iruhusu ndege za jeshi la Isarel kutumia kiwanja chao cha ndege. Ehud barak na wenzake hawakwenda tu moja kwa moja kwa Mzee Kenyatta, bali kwanza walienda kwa Waziri wa kilimo wa kipindi hicho Bw. Bruce McKenzie ambaye huyu aliwahi kuwa afisa wa Idara ya ujasusi ya Uingereza, MI6 na pia alikuwa swahiba mkubwa wa Ehud Barak. Kwa hiyo Israel ikamtumia Bruce McKenzie kumshawishi Mzee Jomo Kenyatta kuruhusu anga la Kenya na viwanjavya ndege kutumiwa na makomando wa Israel na ndege zao. Ehud Barak na maafisa wa Mossad hawakuishia hapa tu, bali pia walifanya vikao vya siri na wafanyabiashara wakubwa nchini Kenya wenye asili ya Israel na wale ambao walikuwa na ‘marafiki’ wa Israel kuwaomba watumie ushawishi wao wa kisiasa na kiuchumi wasaidie kumshawishi Kenyatta kukubali ombi la seriakli ya Israael viwanja vyao kutumika na ndege za kijeshi za Israel na makondo wake. Baada ya mashinikizo haya kutoka kila upande, Mzee Kenyatta hakuwa na chaguo linguine zaidi ya kukubali ombi lao. Bwana huyu McKenzie pia alikuwa na ndege yakebinafsi, na Ehud Barak akaona fursa. Walitumia ndege hii ya kiraia kuruka mpaka Uganda mijini Entebbe na kukatiza juu ya anga la uwanja wa ndege wa Entebbe na walipokuwa wanapita juu ya anga la uwanja wa ndege, Ehud Barak akatumia fursa hii kupiga picha kila eneo la uwanja. Kwa kuwa hii ilikuwa ni ndege ya kiraia, jeshi la Uganda hawakushughulika nayo. Picha hizi zilizopigwa na Ehud Barak zilikuja kuwa na umuhimumkubwa katika maandalizi ya mwisho ya oparesheni ya makomando wa Isarel Kuvamia uwanja huu. Mpaka kufikia hapa maandalizi yote muhimu yalikuwa yamekamilika. WAKATI HUO HUO Upande wa watekaji kule Uganda walikuwa wanasubria mifwedha yao dola milioni 5 za kimarekani. Rais Idd Amin naye baada ya kufikia makubaliano na Israel kuwa masharti ya fedha na wafungwa wa kipalestina kuachiwa tarehe 4 July, naye ‘akarelax’ na akaona huo ndio muda wa kutekeleza majukumu Mengine akisubiria tarehe 4 July ifike. Katika kipindi hiki Idd amin ndiye alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwa kuzingatia utaratibu wa uenyekiti kuzunguka kwa kila nchi kwa mwaka mmoja mmoja na wiki hii alikuwa anatakiwa kwenye kikao cha Umoja wa Afrika kilichokuwa kinafanyika Mauritius. Kwa hiyo Amin akafunga safari kuelekea Mauritius kwenda kukabidhi kijiti cha Uenyekiti. Ehud Barak aliposikia taarifa hii, kwa kutumia akili yake kubwa ya kuzaliwa aliyojaliwa na uzoefu wake wa ujasusi, aliona fursa adhimu kabisa hapa. Akawasiliana na walioko kikaoni huko Tel Aviv na kuwaeleza taarifa ambazo awali wote hawakuielewa. Ehud Barak: “Idd Amin akiwa ndani ya Uganda huwa anatumia Mercedes Limousine katika msafara wake” Waziri Mkuu Rabin: “Ok! Limefanyaje?’ Ehud Barak: “Nataka mtafute gari kama hiyo… Mercedes Limousine” Waziri Mkuu Rabin: “la kazi gani?” Ehud Barak: “siku ambayo kikosi cha makomando wakipanda kwenye ndege kutoka huko Israel kwenda Uganda, gari hilo nataka pia lipakiwe ndani ya ndge!” Kwa dakika kadhaa wote ambao walikuwa wanamsikiliza pale kikaoni kupitia simu hakuna ambaye alielewa nini hasa Ehud Barak alikuwa anapendekeza. Yalikuwa yamebaki masaa machache tu ambapo, weledi, ushujaa na uzalendo uliotukuka ulikuwa unaedna kudhihirika. Itaendelea #TheBOLD_JF
    ·40 Ansichten
  • Chukua hii.

    Kuna kijiji kimoja huko Nchini Japan kiitwacho Shirakawa, nyumba zake za kihistoria zilizoezekwa kwa kutumia nyasi zinalindwa kwa majanga ya Moto. Wakati moto ukitokea mabomba hayo yaliyokuwa chini ya ardhi zaidi ya sitini (60) yanaibuka juu na kutoa maji kwa "pressure" kubwa hadi kufikia mita thelathini (30).

    Mabomba hayo yamefichwa chini ya Ardhi ili kulinda Nyumba za hizo kihistoria ya kijapani dhidi ya Moto. Mfumo huu hujaribiwa mara mbili (2) kila Mwaka yaani Mwezi Mei na Disemba kupitia kikosi cha zima moto cha eneo hilo. Hata katika hali ya hewa ya mvua, wakati wa kufanya mazoezi hutengeneza upinde wa mvua wenye kuvutia juu ya paa, na kuvutia Watazamaji kutoka Ulimwenguni kote.

    Chukua hii. Kuna kijiji kimoja huko Nchini Japan kiitwacho Shirakawa, nyumba zake za kihistoria zilizoezekwa kwa kutumia nyasi zinalindwa kwa majanga ya Moto. Wakati moto ukitokea mabomba hayo yaliyokuwa chini ya ardhi zaidi ya sitini (60) yanaibuka juu na kutoa maji kwa "pressure" kubwa hadi kufikia mita thelathini (30). Mabomba hayo yamefichwa chini ya Ardhi ili kulinda Nyumba za hizo kihistoria ya kijapani dhidi ya Moto. Mfumo huu hujaribiwa mara mbili (2) kila Mwaka yaani Mwezi Mei na Disemba kupitia kikosi cha zima moto cha eneo hilo. Hata katika hali ya hewa ya mvua, wakati wa kufanya mazoezi hutengeneza upinde wa mvua wenye kuvutia juu ya paa, na kuvutia Watazamaji kutoka Ulimwenguni kote.
    ·111 Ansichten
  • ....Kama unaamini huyo demu uliyonae ndo amani ya moyo wako basi,hata Young Africans ukiwauliza watakwambia Khalid Aucho the Tank , Daktari wa Mpira ndio amani ya Timu yao.

    ......Hakuna shaka yoyote kua Khalid Aucho akiwa eneo la kati kati la timu Yang ndani ya uwanja hata wachezaji wenzake huenjoy, halafu juu yake asimame mzenji Mudathiri Yahya aaah ni Raha mtupu.

    .......hata ukicheki mechi Mbili za mwisho za Champions league dhidi ya Tp mazembe ambazo ndio alirejea Kutoka majeruhi Kuna kitu amekiongeza Kwa hali ya juu tofauti na Ile partnership ya Duke abuya na Mudathiri Kuna kitu kilikua kinapungua hasa kwenye ulinzi,yaani yule cover man Kipindi Yanga wanashambulia alikua anakosekana.

    ......You know what ukubali ukatae Khalid Aucho ndio mbeba maono kunako klabu ya Yanga,atapiga pasi fupi fupi,ataipa timu balance ya kucheza,pia atailinda timu mda inashambulia, kwenye nguvu atatumia nguvu , kwenye akili atatumia akili,ni complete namba six.

    ...... Anaitwa Jinja maestro Khalid Aucho Kutoka pale Kwa Rais museveni Uganda.

    Usisahau kufollow Neliud Cosiah
    ....🎙️Kama unaamini huyo demu uliyonae ndo amani ya moyo wako basi,hata Young Africans ukiwauliza watakwambia Khalid Aucho the Tank , Daktari wa Mpira ndio amani ya Timu yao. ......Hakuna shaka yoyote kua Khalid Aucho akiwa eneo la kati kati la timu Yang ndani ya uwanja hata wachezaji wenzake huenjoy, halafu juu yake asimame mzenji Mudathiri Yahya aaah ni Raha mtupu. .......hata ukicheki mechi Mbili za mwisho za Champions league dhidi ya Tp mazembe ambazo ndio alirejea Kutoka majeruhi Kuna kitu amekiongeza Kwa hali ya juu tofauti na Ile partnership ya Duke abuya na Mudathiri Kuna kitu kilikua kinapungua hasa kwenye ulinzi,yaani yule cover man Kipindi Yanga wanashambulia alikua anakosekana. ......You know what ukubali ukatae Khalid Aucho ndio mbeba maono kunako klabu ya Yanga,atapiga pasi fupi fupi,ataipa timu balance ya kucheza,pia atailinda timu mda inashambulia, kwenye nguvu atatumia nguvu , kwenye akili atatumia akili,ni complete namba six. ...... Anaitwa Jinja maestro Khalid Aucho Kutoka pale Kwa Rais museveni Uganda. Usisahau kufollow Neliud Cosiah
    Like
    1
    ·206 Ansichten
  • Wizara ya Fedha imewatahadharisha wastaafu wote nchini kuwa makini na ujumbe mfupi unaotumwa wa kitapeli, ukionesha mtu aliyetumiwa ujumbe alipigiwa simu na Hazina na hakupatikana, na anahitajika kufika Ofisi za Hazina Ndogo huku ukimtaka apige simu kwa namba zilizoandikwa kwenye ujumbe kwa maelezo zaidi.

    Wizara imesema hakuna zoezi lolote la uhakiki wa mafao linalofanywa na Hazina na huduma za wastaafu hutolewa bure.
    Wizara ya Fedha imewatahadharisha wastaafu wote nchini kuwa makini na ujumbe mfupi unaotumwa wa kitapeli, ukionesha mtu aliyetumiwa ujumbe alipigiwa simu na Hazina na hakupatikana, na anahitajika kufika Ofisi za Hazina Ndogo huku ukimtaka apige simu kwa namba zilizoandikwa kwenye ujumbe kwa maelezo zaidi. Wizara imesema hakuna zoezi lolote la uhakiki wa mafao linalofanywa na Hazina na huduma za wastaafu hutolewa bure.
    ·107 Ansichten
  • Erling Braut Haaland amesaini mkataba na Machester City wa miaka tisa na nusu mpaka 2034 ambao utajumuisha rekodi ya mshahara .

    Mshahara mnono zaidi kuwahi kutokea Man City , na pia mmoja wa mshahara mkubwa katika historia ya Ligi kuu England na Football kiujumla

    Source : @fabriziorom @davidornstein

    Piga hela tu , kuna maisha baada ya kusakata kandanda.!

    #neliudcosih
    Erling Braut Haaland amesaini mkataba na Machester City wa miaka tisa na nusu mpaka 2034 ambao utajumuisha rekodi ya mshahara . Mshahara mnono zaidi kuwahi kutokea Man City , na pia mmoja wa mshahara mkubwa katika historia ya Ligi kuu England na Football kiujumla Source : @fabriziorom @davidornstein Piga hela tu , kuna maisha baada ya kusakata kandanda.! 😀 #neliudcosih
    ·141 Ansichten
  • KUMBE USALITI SIO KATIKA MAPENZI PEKEE? HADI KWENYE SOKA UPO, SAID BAHANUZI ALIPOGEUKA MSALITI.

    Kuna mshikaji wangu niliwahi kumwambia kuwa Neyma Jr kasaliti wapenda soka lakini alikataa, Ila imani Yangu inaniambia Neyma Jr ni miongoni mwa wasaliti wa Soka.

    Kwa kipaji cha Neyma Jr wapenda soka wengi walitaraji makubwa kutoka kwake badala Yake imekuwa kinyume na kwasasa anamalizia soka lake uko Saudia Rabbia.

    Huenda ni muda? Hapana! Yupo wapi Mohamed Ibrahim? Kipaji kikubwa sana cha soka lakini kilipotea gafla mithili ya moto wa mabua.

    Sikuizi nasikia Ramadhani Singano ni imamu wa msikiti! Kiufupi kawa ustadhi ni sawa. Lakini kwa machizi soka ataendelea kudumu na kutambulika kama msaliti. Ramadhani Singano kipaji kikubwa kiasi cha kufananishwa na Laprga kwa kuitwa Messi.

    Kuna wakati huwa tunasema kuhusu muda lakini sio kila jambo tunaweza kuhusianisha na muda, Mambo mengine yanakuwa ni usaliti.

    Tukisema kuhusu muda, Ukweli umetubariki mengi sana lakini kuhusu usaliti umetuacha na maumivu mengi sana.

    Saidi Bahanuzi sio jina geni kabisa kwa watu wa mpira, Miaka ya 2011+ Alikuwa wa moto sana pale mitaa ya Jangwani kariakoo.

    Bahanuzi aliwaka sana, Nakumbuka usajili wake alitokea Lamasia ya bongo Mtibwa Sugar. Wakati ule alikuwa muhimili haswa wa Yanga Afrika.

    Kutokana na ustaa wa Bahanuzi kwa kipindi kile hata baadhi ya masela tuliokuwa tunasoma nao waliokuwa wanaitwa Saidi basi walijiita Bahanuzi.

    Bahanuzi kafanya momenti nyingi sana na Yanga Afrika ila nadhani momenti ya kukosa penati ya maamuzi dhidi ya Al Ahly ndio momenti mbaya zaidi kwake, Maana ilikuwa penati ya maamuzi.

    Leo nimekumbuka jina la Bahanuzi na kujiuliza Yupo wapi? Huenda watu wa soka wanatamani kufahamu alipo fundi wa mpira Saidi Bahanuzi.

    Kwa wakati ule Saidi Bahanuzi aliwaka sana aise, Ilikuwa haiwezi kusemwa Yanga bila kusemwa Yeye lakini cha kushangaza alitoweka Gafla sana kusikojulikana na kuwaacha wapenda soka midomo wazi.

    Kutoka kwa Moja ya Wadau WA Soka

    #neliudcosih
    🚨 KUMBE USALITI SIO KATIKA MAPENZI PEKEE? HADI KWENYE SOKA UPO, SAID BAHANUZI ALIPOGEUKA MSALITI. Kuna mshikaji wangu niliwahi kumwambia kuwa Neyma Jr kasaliti wapenda soka lakini alikataa, Ila imani Yangu inaniambia Neyma Jr ni miongoni mwa wasaliti wa Soka. Kwa kipaji cha Neyma Jr wapenda soka wengi walitaraji makubwa kutoka kwake badala Yake imekuwa kinyume na kwasasa anamalizia soka lake uko Saudia Rabbia. Huenda ni muda? Hapana! Yupo wapi Mohamed Ibrahim? Kipaji kikubwa sana cha soka lakini kilipotea gafla mithili ya moto wa mabua. Sikuizi nasikia Ramadhani Singano ni imamu wa msikiti! Kiufupi kawa ustadhi ni sawa. Lakini kwa machizi soka ataendelea kudumu na kutambulika kama msaliti. Ramadhani Singano kipaji kikubwa kiasi cha kufananishwa na Laprga kwa kuitwa Messi. Kuna wakati huwa tunasema kuhusu muda lakini sio kila jambo tunaweza kuhusianisha na muda, Mambo mengine yanakuwa ni usaliti. Tukisema kuhusu muda, Ukweli umetubariki mengi sana lakini kuhusu usaliti umetuacha na maumivu mengi sana. Saidi Bahanuzi sio jina geni kabisa kwa watu wa mpira, Miaka ya 2011+ Alikuwa wa moto sana pale mitaa ya Jangwani kariakoo. Bahanuzi aliwaka sana, Nakumbuka usajili wake alitokea Lamasia ya bongo Mtibwa Sugar. Wakati ule alikuwa muhimili haswa wa Yanga Afrika. Kutokana na ustaa wa Bahanuzi kwa kipindi kile hata baadhi ya masela tuliokuwa tunasoma nao waliokuwa wanaitwa Saidi basi walijiita Bahanuzi. Bahanuzi kafanya momenti nyingi sana na Yanga Afrika ila nadhani momenti ya kukosa penati ya maamuzi dhidi ya Al Ahly ndio momenti mbaya zaidi kwake, Maana ilikuwa penati ya maamuzi. Leo nimekumbuka jina la Bahanuzi na kujiuliza Yupo wapi? Huenda watu wa soka wanatamani kufahamu alipo fundi wa mpira Saidi Bahanuzi. Kwa wakati ule Saidi Bahanuzi aliwaka sana aise, Ilikuwa haiwezi kusemwa Yanga bila kusemwa Yeye lakini cha kushangaza alitoweka Gafla sana kusikojulikana na kuwaacha wapenda soka midomo wazi. ✍️Kutoka kwa Moja ya Wadau WA Soka 🙌 #neliudcosih
    ·174 Ansichten
  • Kwenye season ya Squid game kuna huyu mwamba the front man , kiongozi wa michezo yote inayofanyika kwenye season ya pili anatambulika kama namba 001 , alikuwa mnafiki kama baba yake yule mzee wa season ya kwanza nayeye alikuwa namba 001

    The front man alikuwa mnafiki , alijifanya ni mwenzao kumbe yeye ndo jambazi kuu na mtunzi wa ile michezo , kuna sehemu alikuwa anajifanyisha hajui kucheza zikiwa zimebaki sekunde chache tu wote wapigwe risasi ! mashabiki wanasema alikuwa mnafiki mpaka alijisahau

    #neliudcosiah
    Kwenye season ya Squid game kuna huyu mwamba the front man , kiongozi wa michezo yote inayofanyika kwenye season ya pili anatambulika kama namba 001 , alikuwa mnafiki kama baba yake yule mzee wa season ya kwanza nayeye alikuwa namba 001 The front man alikuwa mnafiki , alijifanya ni mwenzao kumbe yeye ndo jambazi kuu na mtunzi wa ile michezo , kuna sehemu alikuwa anajifanyisha hajui kucheza zikiwa zimebaki sekunde chache tu wote wapigwe risasi ! mashabiki wanasema alikuwa mnafiki mpaka alijisahau 😀 #neliudcosiah
    ·138 Ansichten
  • Shida ni Kwamba watu hupokea taarifa KWA mihemko ila Tanzania na afrika mashariki hakuna defensive midfield kama khalid aucho na hata wanaocheza ndani ya ligi kuu hakuna na huyu ndo anafanya GUSA ACHIA TWENDE KWAO iwe Tamu San
    Na kocha jana aliona ni vipi akimtoa aucho mechi kadhaa timu inapoteza mvuto jana akaamua amuache asimguse kabisa
    Huyu ni KHALID AUCHO huyu ni JINJA MAESTRO
    Juzi mashabiki wa uganda walicomment kweny ukurasa wake na kumtakia mchezo mwema na wanasema wanataman aucho awaonyeshe nusu ya kiwango chake kweny timu ya taifa wakilinganisha na
    anachokionyesha yanga

    #neliudcosiah
    Shida ni Kwamba watu hupokea taarifa KWA mihemko ila Tanzania na afrika mashariki hakuna defensive midfield kama khalid aucho na hata wanaocheza ndani ya ligi kuu hakuna na huyu ndo anafanya GUSA ACHIA TWENDE KWAO iwe Tamu San Na kocha jana aliona ni vipi akimtoa aucho mechi kadhaa timu inapoteza mvuto jana akaamua amuache asimguse kabisa Huyu ni KHALID AUCHO huyu ni JINJA MAESTRO 💚💛💚💛 Juzi mashabiki wa uganda walicomment kweny ukurasa wake na kumtakia mchezo mwema na wanasema wanataman aucho awaonyeshe nusu ya kiwango chake kweny timu ya taifa wakilinganisha na anachokionyesha yanga #neliudcosiah
    Like
    1
    ·203 Ansichten
  • Nadhani hii Sasa Imevuka kwenye Quality .......

    Khalid Aucho anaweza akawa siyo yule tena in terms of Physically lakin Whenever Aucho is in the Pitch Yanga Africans are safe .

    -Akili ya Mpira
    -Composure
    -Technical Ability
    -Game Passing

    Huyu Mganda anatawala sana Dimba la kati ...Hilal wana watu wagumu na wana kasi lakin Fundi alikua anaokota moja moja pakihitajika Kuvunja kuni anavunja kweli kweli ...

    Juzi Kuna Mashabiki Kutoka Uganda Walicomment kwenye post yake wakimtakia kheri na mechi bora wakaenda mbali zaidi na Kusema ,

    "Tunaomba walau nusu ya Kiwango chako Ndani ya Yanga Sc utuonyeshe Ukiwa na timu yetu ya Uganda Cranes "

    Wanamtambua kama moja ya Viungo bora ambao wamewahi Kuwashuhudia .....Binafsi huyu ni Kipimo halisi cha Kiungo wa Chini au holding Mid ndani ya Ligi yetu .

    THE TANK FOR REASON .

    #neliudcosiah
    Nadhani hii Sasa Imevuka kwenye Quality ....... Khalid Aucho anaweza akawa siyo yule tena in terms of Physically lakin Whenever Aucho is in the Pitch Yanga Africans are safe 🤝. -Akili ya Mpira -Composure -Technical Ability -Game Passing Huyu Mganda anatawala sana Dimba la kati ...Hilal wana watu wagumu na wana kasi lakin Fundi alikua anaokota moja moja pakihitajika Kuvunja kuni anavunja kweli kweli ... Juzi Kuna Mashabiki Kutoka Uganda Walicomment kwenye post yake wakimtakia kheri na mechi bora wakaenda mbali zaidi na Kusema , "Tunaomba walau nusu ya Kiwango chako Ndani ya Yanga Sc utuonyeshe Ukiwa na timu yetu ya Uganda Cranes " Wanamtambua kama moja ya Viungo bora ambao wamewahi Kuwashuhudia .....Binafsi huyu ni Kipimo halisi cha Kiungo wa Chini au holding Mid ndani ya Ligi yetu . THE TANK FOR REASON ✅. #neliudcosiah
    Like
    1
    ·203 Ansichten
  • MOYO SAFI WA SADIO MANÉ NDIO SILAHA YA MAFANIKIO YAKE.

    Sadio Mané amesaidia mambo mengi sana katika Kijiji alichotoka mara Baada ya kupata mafanikio katika soka.

    Sadio Mané amezaliwa katika Kijiji Cha Bambali nchini Senegal,amekulia huko na wanakijiji wengi walimsapoti na kumuombea sana Dua za mafanikio kipindi anaenda rasmi ulaya kujaribu bahati yake katika kazi ya kucheza mpira wa miguu.

    Mungu Si Athumani wala Mzee Nkumilwa kijana akatoboa na maisha yakaanza kuwa safi kwa upande wake,lakini pamoja na yote hakuwasahau watu waliomfanya awe hapo Leo.

    Alianza kukata fungu kwenye Kila mshahara wake wa mwezi kwa ajili ya kusaidia Kijiji chake kutoka kuwa Cha kimasikini mpaka kuwa Cha maisha ya kati kabla ya kuwa Cha kitajiri kabisa.

    Baadae zile pesa alizokuwa anahifadhi kutoka kwenye Kila mshahara wake zilianza kufanya kazi vyema na kufanikisha kukamklisha vitu vifuatavyo:

    1. Alijenga hospital yenye thamani ya €530K sawa na pesa za kitanzania Billion Moja,million mia tatu sabini na mbili,laki tano na Elfu tisini na nne.

    2. Alijenga Shule yenye thamani ya €270K sawa na pesa za kitanzania Million mia sita tisa tisa,laki mbili na Elfu Arobaini na sita.

    3. Pia huwa anatoa kiasi Cha €70 Kwa Kila kaya iliyopo Katika Kijiji hicho kwa mwezi ambayo ni sawa na pesa za kitanzania Laki moja,Elfu themanini na Moja,mia mbili themanini na sita.

    4. Kutoa nguo za bure Kwa watoto wote waliopo ndani ya Kijiji hicho.

    5. Kufanikisha kupeleka internet yenye Kasi ya 4G katika Kijiji hicho.

    6. Kufanikisha kupeleka vituo vya gas katika Kijiji hicho akishirikiana na kampuni ya Oryx.

    7. Kajenga uwanja wa soka pia.

    NDIO MAANA ANAFANIKIWA KILA ANAPOENDA HATA KAMA AKISEMEWA MABAYA KUNA WENGI WAPO NYUMA YAKE WANAMUOMBEA MEMA

    #neliudcosiah
    MOYO SAFI WA SADIO MANÉ NDIO SILAHA YA MAFANIKIO YAKE. Sadio Mané amesaidia mambo mengi sana katika Kijiji alichotoka mara Baada ya kupata mafanikio katika soka. Sadio Mané amezaliwa katika Kijiji Cha Bambali nchini Senegal,amekulia huko na wanakijiji wengi walimsapoti na kumuombea sana Dua za mafanikio kipindi anaenda rasmi ulaya kujaribu bahati yake katika kazi ya kucheza mpira wa miguu. Mungu Si Athumani wala Mzee Nkumilwa kijana akatoboa na maisha yakaanza kuwa safi kwa upande wake,lakini pamoja na yote hakuwasahau watu waliomfanya awe hapo Leo. Alianza kukata fungu kwenye Kila mshahara wake wa mwezi kwa ajili ya kusaidia Kijiji chake kutoka kuwa Cha kimasikini mpaka kuwa Cha maisha ya kati kabla ya kuwa Cha kitajiri kabisa. Baadae zile pesa alizokuwa anahifadhi kutoka kwenye Kila mshahara wake zilianza kufanya kazi vyema na kufanikisha kukamklisha vitu vifuatavyo: 1. Alijenga hospital yenye thamani ya €530K sawa na pesa za kitanzania Billion Moja,million mia tatu sabini na mbili,laki tano na Elfu tisini na nne. 2. Alijenga Shule yenye thamani ya €270K sawa na pesa za kitanzania Million mia sita tisa tisa,laki mbili na Elfu Arobaini na sita. 3. Pia huwa anatoa kiasi Cha €70 Kwa Kila kaya iliyopo Katika Kijiji hicho kwa mwezi ambayo ni sawa na pesa za kitanzania Laki moja,Elfu themanini na Moja,mia mbili themanini na sita. 4. Kutoa nguo za bure Kwa watoto wote waliopo ndani ya Kijiji hicho. 5. Kufanikisha kupeleka internet yenye Kasi ya 4G katika Kijiji hicho. 6. Kufanikisha kupeleka vituo vya gas katika Kijiji hicho akishirikiana na kampuni ya Oryx. 7. Kajenga uwanja wa soka pia. NDIO MAANA ANAFANIKIWA KILA ANAPOENDA HATA KAMA AKISEMEWA MABAYA KUNA WENGI WAPO NYUMA YAKE WANAMUOMBEA MEMA ♥️📌 #neliudcosiah
    Like
    1
    ·233 Ansichten
  • Wakati kuna baadhi ya Wachezaji wanaenda kufanya maombi kwa viongozi wa dini ili kurudisha viwango vyao Mwamba wa uwagadugu anachage tuh nywele nyeusi kwenda nyeupe kiwango kimerudi

    Mechi 2 za mwisho CAF Champions magoli 2, Ki Aziz Kujiamini kumerudi, mashuti yamerudi namuona akiendelea na makali yake ya msimu uliopita

    #muslehelbarcaupdates

    #yangasc #CAFChampionsLeague
    Wakati kuna baadhi ya Wachezaji wanaenda kufanya maombi kwa viongozi wa dini ili kurudisha viwango vyao Mwamba wa uwagadugu anachage tuh nywele nyeusi kwenda nyeupe kiwango kimerudi 😂 Mechi 2 za mwisho CAF Champions magoli 2, Ki Aziz Kujiamini kumerudi, mashuti yamerudi namuona akiendelea na makali yake ya msimu uliopita 🔥 #muslehelbarcaupdates 👽 #yangasc #CAFChampionsLeague
    Like
    2
    1 Kommentare ·172 Ansichten
  • Licha ya jana Klabu ya Yanga SC kushinda mechi yake muhimu dhidi ya timu ngumu ya Al Hilal omdurman lakini kuna huyu mwamba wa kuitwa Jean Claude Giramugisha, hapa kibwana Shomari nahisi usingizi wake ulikuwa wa Mashaka (kuweweseka) maana sio kwa kuburuzwa kule

    Dogo ana speed ya ajabu mpaka nikasema dah huyu sio ndo yule kasongo lakini? achana na speed ana vyenga pia ana pumzi hachoki, Kuna muda akuwa upande wa kushoto kumxhosha kibwana sometime anabadilishana possition na adama Coulibaly, anaenda tena kumnyanyasa Shadrack Boka

    Cha ajabu huyu dogo ni mburundi tuh sijui Tanzania tulicherewa nini kusema huyu dogo ni MUHA wa Kigoma na akatupa faida Tanzania kwenye NT na vilabu

    Oya huyu dogo ni moto

    #muslehelbarcaupdates

    #Alhilalomdurman #CAFChampionsLeague #TotalEnergiesCAFCL
    Licha ya jana Klabu ya Yanga SC kushinda mechi yake muhimu dhidi ya timu ngumu ya Al Hilal omdurman lakini kuna huyu mwamba wa kuitwa Jean Claude Giramugisha, hapa kibwana Shomari nahisi usingizi wake ulikuwa wa Mashaka (kuweweseka) maana sio kwa kuburuzwa kule 🙄 Dogo ana speed ya ajabu mpaka nikasema dah huyu sio ndo yule kasongo lakini? achana na speed ana vyenga pia ana pumzi hachoki, Kuna muda akuwa upande wa kushoto kumxhosha kibwana sometime anabadilishana possition na adama Coulibaly, anaenda tena kumnyanyasa Shadrack Boka 🔥 Cha ajabu huyu dogo ni mburundi tuh sijui Tanzania tulicherewa nini kusema huyu dogo ni MUHA wa Kigoma na akatupa faida Tanzania kwenye NT na vilabu 😂 Oya huyu dogo ni moto 🔥 #muslehelbarcaupdates 👽 #Alhilalomdurman #CAFChampionsLeague #TotalEnergiesCAFCL
    Love
    1
    1 Kommentare ·261 Ansichten
  • KUNA TOFAUTI KATI YA KUWA NA NAMBA YA SIMU NA KUWA NA MAWASILIANO...

    Katika ulimwengu uliojaa miunganisho, ni rahisi kukosea wingi kwa thamani. Tunasherehekea orodha ndefu za anwani, mamia ya wafuasi, na "marafiki" wengi kwenye mitandao ya kijamii. Lakini maisha yanapokuwa mazito, wakati dhoruba za maumivu, hasara, au kutokuwa na uhakika zinapopiga, sio idadi ya majina inayotuokoa. Ni sauti chache zinazojibu tunapopiga simu. Watu ambao ni muhimu sana sio tu maingizo kwenye simu yako. Ndio ambao majina yao yanaonekana mara kwa mara katika kumbukumbu zako za simu, si kwa sababu ya urahisi, lakini kwa sababu uwepo wao unahisi kama nyumbani. Ni wale wanaosikiliza bila hukumu, ambao hukaa hata wakati ukimya ndio unaweza kutoa. Maandiko yanatukumbusha "Rafiki hupenda siku zote, na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu." Urafiki wa kweli haupimwi kwa picha tunazopiga pamoja, karamu tunazohudhuria, au salamu zinazotolewa kwa mazoea. Inapimwa kwa uwepo, kwa mioyo inayosimama kando yako kwenye vivuli, bila kuuliza chochote isipokuwa nafasi ya kutembea nawe.

    Fikiri juu yake. Ni lini mara ya mwisho ulipohitaji mtu wa kumweleza siri zake? Je, ulivinjari watu unaowasiliana nao bila kikomo, au je, moyo wako ulitulia kwa wachache waliochaguliwa? Hayo machache, hapo ndipo hazina ya maisha ilipo. Wakati wa furaha, wengi watasherehekea na wewe. Lakini wakati wa mapambano, ni wale wa kweli tu wanaobaki. Hawahitaji maelezo au maneno kamili. Wanajitokeza tu. Na uwepo wao pekee unakuwa faraja ambayo hukujua unahitaji. Urafiki sio juu ya wangapi unaowajua, lakini jinsi unavyojulikana kwa undani. Linda urafiki huo. Walee. Kuwa sauti hiyo kwa wengine. Kwa sababu katika maisha haya ya muda mfupi, ambapo siku zinaweza kugeuka zisizo na uhakika bila ya onyo, utajiri mkubwa tunaoshikilia sio pesa, lakini mioyo ambayo inatujali kikweli. Basi wapendeni wanao jibu, wanao sikiliza, na wanao kaa. Kwa maana mwishowe, uzito wa maisha huhisi mwepesi unapobebwa na mikono inayokupenda kweli.
    KUNA TOFAUTI KATI YA KUWA NA NAMBA YA SIMU NA KUWA NA MAWASILIANO... Katika ulimwengu uliojaa miunganisho, ni rahisi kukosea wingi kwa thamani. Tunasherehekea orodha ndefu za anwani, mamia ya wafuasi, na "marafiki" wengi kwenye mitandao ya kijamii. Lakini maisha yanapokuwa mazito, wakati dhoruba za maumivu, hasara, au kutokuwa na uhakika zinapopiga, sio idadi ya majina inayotuokoa. Ni sauti chache zinazojibu tunapopiga simu. Watu ambao ni muhimu sana sio tu maingizo kwenye simu yako. Ndio ambao majina yao yanaonekana mara kwa mara katika kumbukumbu zako za simu, si kwa sababu ya urahisi, lakini kwa sababu uwepo wao unahisi kama nyumbani. Ni wale wanaosikiliza bila hukumu, ambao hukaa hata wakati ukimya ndio unaweza kutoa. Maandiko yanatukumbusha "Rafiki hupenda siku zote, na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu." Urafiki wa kweli haupimwi kwa picha tunazopiga pamoja, karamu tunazohudhuria, au salamu zinazotolewa kwa mazoea. Inapimwa kwa uwepo, kwa mioyo inayosimama kando yako kwenye vivuli, bila kuuliza chochote isipokuwa nafasi ya kutembea nawe. Fikiri juu yake. Ni lini mara ya mwisho ulipohitaji mtu wa kumweleza siri zake? Je, ulivinjari watu unaowasiliana nao bila kikomo, au je, moyo wako ulitulia kwa wachache waliochaguliwa? Hayo machache, hapo ndipo hazina ya maisha ilipo. Wakati wa furaha, wengi watasherehekea na wewe. Lakini wakati wa mapambano, ni wale wa kweli tu wanaobaki. Hawahitaji maelezo au maneno kamili. Wanajitokeza tu. Na uwepo wao pekee unakuwa faraja ambayo hukujua unahitaji. Urafiki sio juu ya wangapi unaowajua, lakini jinsi unavyojulikana kwa undani. Linda urafiki huo. Walee. Kuwa sauti hiyo kwa wengine. Kwa sababu katika maisha haya ya muda mfupi, ambapo siku zinaweza kugeuka zisizo na uhakika bila ya onyo, utajiri mkubwa tunaoshikilia sio pesa, lakini mioyo ambayo inatujali kikweli. Basi wapendeni wanao jibu, wanao sikiliza, na wanao kaa. Kwa maana mwishowe, uzito wa maisha huhisi mwepesi unapobebwa na mikono inayokupenda kweli.
    Like
    Love
    2
    ·116 Ansichten
  • "Wolper aliwahi kuniomba hela ya mtaji nikachukua milioni 30 nikampa ila cha kusikitisha akaenda kula pesa hizo na bishoo mmoja mwenye sura nzuri nzuri anaitwa Rich Mitindo. Alipokuwa China nikawa naona anapiga picha nyingi nyingi na jamaa, nilipomuuliza akawa anajibu "hakuna kitu babe huyu ni mdogo wangu tu" - Harmonize, Msanii wa muziki Tanzania.

    "Wolper aliwahi kuniomba hela ya mtaji nikachukua milioni 30 nikampa ila cha kusikitisha akaenda kula pesa hizo na bishoo mmoja mwenye sura nzuri nzuri anaitwa Rich Mitindo. Alipokuwa China nikawa naona anapiga picha nyingi nyingi na jamaa, nilipomuuliza akawa anajibu "hakuna kitu babe huyu ni mdogo wangu tu" - Harmonize, Msanii wa muziki Tanzania.
    Like
    1
    ·151 Ansichten
  • THEIA SAYARI NDOGO ILIYOGONGANA NA DUNIANI.

    ✍🏾Mapande ya sayari inayoitwa Theia ambayo iligongana na Dunia na kusababisha kuundwa kwa Mwezi yamepatikana na Wataalmu Nchini Marekani.Kwa kufafanua zaidi ni wazi kwamba kuna siri nzito Katika Uumbaji,Kweli Mungu ni fundi waungwana,Kwanza Fahamu ya kwamba Asilimia 70% ya Historia ya uuumbaji Haijulikana kisawa Sawa maana Maisha ya Binadamu hayana Umri mrefu sanaa kuzidi Umri wa Dunia maana Umri wa Dunia ni miaka Billion 4.7 na Dunia inatadhamiwa Kuishi miaka Billion 7 Ijayo kabla Haijafa na kusambalatika kama kama Cheche za Mkaa.Theia ni jina la kigiriki lenye maana ya kwamba Mungu wa kike ambapo kulingana na simulizi na imani za wagiri ni kwamba Theia ni moja wa Mungu wa kike waliokuwa wanaishi uko Mwezini.Theia ni moja wa Watoto 7 mama wa Miungu ya uko mwezini yaani Mather of All Goddes uko mwezini hivyo ambaye alifahamika kama Selene huyo Goddess mkuu wa uko mwezini.

    ✍🏾SaSa Hapo mwanzo kulikuwa na Sayari inayofahamika kama Theia ambayo ilikuwa na ukubwa Sawa sawaa na Mars uko ambako NASA wametuma Perseverance Rovers kwenda Kuangalia kama Kulikuwa na maisha Hapo Kale yaani Miaka Billion 3 Iliyopita.Sasa Kuna nadharia kama 4 zinazoelezeaa kutokea Kwa mwezi,Kuna ambao Wanadai ya kwamba Theia ilikuwa iko nje ya Mfumo wa Jua mpaka inakuja kugongana na Dunia Hata Hivyo nadharia hii BADO haijathibika wanasayansi BADO wanafanya Tafiti Mbali Mbali kuliweka Hili sawaa.

    Hata Maji Yaliyopo hapa Duniani Hususani Maji ya kwenye Bahari yalitokea Baada ya Theia Kuparamia na Kuigonga Duniani Ndio Ikasababisha Uwepo wa Bahari kubwa ambazo tunaziona leo hii.Kuna nadharia ya kwanza ambayo Inadai ya kwamba kulikuwa na Moja ya Sayari kubwa Sana, Ambapo Sayari hiyo kulingana na Sababu ambazo hazijawekwa wazi ni kwamba Sayari hiyo kubwa ilikuja Kupasuka pasuka Kwa Kishindo na Kusababisha mgawanyiko ambapo Katika mgawanyiko huo ndio ukapelekea kuwepo Kwa Mwezi Ambapo Mwezi huo ulikuja Kunaswa na Nguvu ya mvutano wa Jua ndio ukabaki ulipo leo lakini Huwenda lisingekuwa Jua Mwezi ungekuwa Umeenda Mbali Sana kuliko ilivyo leo,Wabongo wanasema ya kwamba Mungu ni Fundi kweli (Tunakubaliana ya kwamba Sayari Zote ni Viumbe kama ilivyo Kwa viumbe wengine).

    ✍🏾 kamaa hiyo haitoshi kuna Nadharia ya pili ambayo inaelezea ya kwamba Mwezi uliundwa Wakati mmoja na Wakati Dunia () inaundwa hii Ina maana ya kwamba Dunia na Mwezi viliundwa wakati mmoja Kipindi ambacho Photo planetary Disk Accreted.Kwa kuthibitisha hilo Wakati wa Apollo Project Taasisi kubwa ya Marekani yaani NATIONAL AERONAUTICS AND SPACE ADMINISTRATION (NASA) walipata baadhi ya Ushahidi wa miamba uko mwezini walipoenda uko Mwaka 1969 mpaka mwaka 1972 walikutana na miamba yenye kufanana na ya hapa Duniani na hivyo kuja na Hoja ya kwamba Huenda Dunia na Mwezi viliundwa Wakati mmoja.Kuna baadhi ya chambuzi zinadai ya kwamba Theia ilikuwa ni Earth Trojan yaani Sayari ndogo ambayo ilikuwa ipo Katika mfumo wa kulizunguka JUA yenye Ukubwa wa Km 6,102 sawaa na Mile 3792.Na kulingana na utafiti na Ushahidi wa mwaka 2019 UNAONYESHA ya kwamba Theia ni Sayari ambayo Hakuwa Katika Mfumo wetu wa Jua ILA ni Sayari ambayo Imetoka nje ya Mfumo wa Jua (Solar system Mfumo huu ambao uliatengenezwa miaka 4.6 iliyopita).

    ✍🏾Takribani miaka bilioni 4.5 iliyopita sayari ndogo inayoitwa Theia iligongana na Dunia tukio lililosababisha sayari hiyo kupasuka na baadhi ya mapande yake kuruka kwenye Space na kuundia Mwezi na mapande mengine yalifukiwa chini Duniani ambapo katika utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na wanasayansi kutoka chuo cha Arizona Nchini Marekani wamefanikiwa kuyapata baadhi ya mawe yaliyosalia wakati sayari hiyo ilipogongana na Dunia.ndii maana naungana na Mtaalamu wangu kutoka Marekani alimaarufu kama Bari Katika masuala ya uchambuzi ya kwamba Sayari Huwa zinajizalisha zenyewe ama kuzaliana Zenyewe maana Kwamba Sayari Moja inaweza ikasababisha KUZALIWA KWA Sayari zingine ndio maana Hata baadhi mawe makubwa yaliyoko Angani yenye ukubwa Sawa na Jimbo la Alaska ama Australia ni matokeo ama masalia ya Sayari zilizokufa ama zilizowahi kuwepo miaka Mabilioni iliyopita.

    Maana tufahamu ya kwamba Sayari Huwa zinazaliwa na pia Baada ya miaka Billion 4 mpaka 7 Sayari Huwa zinakufa ndio maana Mtaalamu Bari anazichukuliaa Sayari kama ni VIUMBE Vinavyoishi kama ilivyo Kwa viumbe viumbe Vinginevyo.hivyo Miamba iliyoko mwezini na hapa Duniani Ina Uhusiano Mkubwa na kuonyesha ya kwamba Mwezi na Dunia Zote zimeumbwa wakati Mmoja ama ni matokeo ya Sayari ndogo ya THEIA yenye kutaka kufanana na MARS Kwa ukubwa ilipogngana na Dunia na Kusababisha Kutokea Kwa Mwezi.
    THEIA SAYARI NDOGO ILIYOGONGANA NA DUNIANI. ✍🏾Mapande ya sayari inayoitwa Theia ambayo iligongana na Dunia na kusababisha kuundwa kwa Mwezi yamepatikana na Wataalmu Nchini Marekani.Kwa kufafanua zaidi ni wazi kwamba kuna siri nzito Katika Uumbaji,Kweli Mungu ni fundi waungwana,Kwanza Fahamu ya kwamba Asilimia 70% ya Historia ya uuumbaji Haijulikana kisawa Sawa maana Maisha ya Binadamu hayana Umri mrefu sanaa kuzidi Umri wa Dunia maana Umri wa Dunia ni miaka Billion 4.7 na Dunia inatadhamiwa Kuishi miaka Billion 7 Ijayo kabla Haijafa na kusambalatika kama kama Cheche za Mkaa🤓🤓.Theia ni jina la kigiriki lenye maana ya kwamba Mungu wa kike ambapo kulingana na simulizi na imani za wagiri ni kwamba Theia ni moja wa Mungu wa kike waliokuwa wanaishi uko Mwezini.Theia ni moja wa Watoto 7 mama wa Miungu ya uko mwezini yaani Mather of All Goddes uko mwezini hivyo ambaye alifahamika kama Selene huyo Goddess mkuu wa uko mwezini. ✍🏾SaSa Hapo mwanzo kulikuwa na Sayari inayofahamika kama Theia ambayo ilikuwa na ukubwa Sawa sawaa na Mars uko ambako NASA wametuma Perseverance Rovers kwenda Kuangalia kama Kulikuwa na maisha Hapo Kale yaani Miaka Billion 3 Iliyopita.Sasa Kuna nadharia kama 4 zinazoelezeaa kutokea Kwa mwezi,Kuna ambao Wanadai ya kwamba Theia ilikuwa iko nje ya Mfumo wa Jua mpaka inakuja kugongana na Dunia Hata Hivyo nadharia hii BADO haijathibika wanasayansi BADO wanafanya Tafiti Mbali Mbali kuliweka Hili sawaa. Hata Maji Yaliyopo hapa Duniani Hususani Maji ya kwenye Bahari yalitokea Baada ya Theia Kuparamia na Kuigonga Duniani Ndio Ikasababisha Uwepo wa Bahari kubwa ambazo tunaziona leo hii.Kuna nadharia ya kwanza ambayo Inadai ya kwamba kulikuwa na Moja ya Sayari kubwa Sana, Ambapo Sayari hiyo kulingana na Sababu ambazo hazijawekwa wazi ni kwamba Sayari hiyo kubwa ilikuja Kupasuka pasuka Kwa Kishindo na Kusababisha mgawanyiko ambapo Katika mgawanyiko huo ndio ukapelekea kuwepo Kwa Mwezi Ambapo Mwezi huo ulikuja Kunaswa na Nguvu ya mvutano wa Jua ndio ukabaki ulipo leo lakini Huwenda lisingekuwa Jua Mwezi ungekuwa Umeenda Mbali Sana kuliko ilivyo leo,Wabongo wanasema ya kwamba Mungu ni Fundi kweli (Tunakubaliana ya kwamba Sayari Zote ni Viumbe kama ilivyo Kwa viumbe wengine). ✍🏾 kamaa hiyo haitoshi kuna Nadharia ya pili ambayo inaelezea ya kwamba Mwezi uliundwa Wakati mmoja na Wakati Dunia (🌎) inaundwa hii Ina maana ya kwamba Dunia na Mwezi viliundwa wakati mmoja Kipindi ambacho Photo planetary Disk Accreted.Kwa kuthibitisha hilo Wakati wa Apollo Project Taasisi kubwa ya Marekani yaani NATIONAL AERONAUTICS AND SPACE 🌌 ADMINISTRATION (NASA) walipata baadhi ya Ushahidi wa miamba uko mwezini walipoenda uko Mwaka 1969 mpaka mwaka 1972 walikutana na miamba yenye kufanana na ya hapa Duniani na hivyo kuja na Hoja ya kwamba Huenda Dunia na Mwezi viliundwa Wakati mmoja.Kuna baadhi ya chambuzi zinadai ya kwamba Theia ilikuwa ni Earth Trojan yaani Sayari ndogo ambayo ilikuwa ipo Katika mfumo wa kulizunguka JUA yenye Ukubwa wa Km 6,102 sawaa na Mile 3792.Na kulingana na utafiti na Ushahidi wa mwaka 2019 UNAONYESHA ya kwamba Theia ni Sayari ambayo Hakuwa Katika Mfumo wetu wa Jua ILA ni Sayari ambayo Imetoka nje ya Mfumo wa Jua (Solar system Mfumo huu ambao uliatengenezwa miaka 4.6 iliyopita). ✍🏾Takribani miaka bilioni 4.5 iliyopita sayari ndogo inayoitwa Theia iligongana na Dunia tukio lililosababisha sayari hiyo kupasuka na baadhi ya mapande yake kuruka kwenye Space na kuundia Mwezi na mapande mengine yalifukiwa chini Duniani ambapo katika utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na wanasayansi kutoka chuo cha Arizona Nchini Marekani wamefanikiwa kuyapata baadhi ya mawe yaliyosalia wakati sayari hiyo ilipogongana na Dunia.ndii maana naungana na Mtaalamu wangu kutoka Marekani alimaarufu kama Bari Katika masuala ya uchambuzi ya kwamba Sayari Huwa zinajizalisha zenyewe ama kuzaliana Zenyewe maana Kwamba Sayari Moja inaweza ikasababisha KUZALIWA KWA Sayari zingine ndio maana Hata baadhi mawe makubwa yaliyoko Angani yenye ukubwa Sawa na Jimbo la Alaska ama Australia ni matokeo ama masalia ya Sayari zilizokufa ama zilizowahi kuwepo miaka Mabilioni iliyopita. Maana tufahamu ya kwamba Sayari Huwa zinazaliwa na pia Baada ya miaka Billion 4 mpaka 7 Sayari Huwa zinakufa ndio maana Mtaalamu Bari anazichukuliaa Sayari kama ni VIUMBE Vinavyoishi kama ilivyo Kwa viumbe viumbe Vinginevyo.hivyo Miamba iliyoko mwezini na hapa Duniani Ina Uhusiano Mkubwa na kuonyesha ya kwamba Mwezi na Dunia Zote zimeumbwa wakati Mmoja ama ni matokeo ya Sayari ndogo ya THEIA yenye kutaka kufanana na MARS Kwa ukubwa ilipogngana na Dunia na Kusababisha Kutokea Kwa Mwezi.
    Like
    3
    1 Kommentare ·265 Ansichten
  • MWAKA HUU, USIJARIBU KUTHIBITISHA MTU YEYOTE AMEKOSEA...

    Kuna barabara hatari wengi tunatembea, na wengine kwa sasa wanatembea kwenye barabara hizo bila hata kujua. Ni njia ya matamanio inayochochewa na maumivu, ambayo hupigania kupata kitu ili kudhibiti kuwa watu wengine wamekosea au harakati hiyo na isiyo na mwisho ili kuwaonyesha kuwa unaweza kufanikiwa. Labda walikutilia shaka. Labda walikuumiza, kukataa ndoto zako, au kucheka kwa mapambano yako. Labda, baadhi yao bado wananing'inia wakingojea kusema, "Nilisema." Na sasa, unainuka kila siku ukiendeshwa na sauti hii tulivu inayosema, “Siku moja, wataona. Siku moja nitawaonyesha.” Inahisi heshima, sivyo? Inahisi kama haki. Lakini nakuambia ukweli huu sio uhuru ni gereza. Kuishi maisha yako ili kuthibitisha kuwa mtu amekosea ni kubeba minyororo ya maneno yake na wewe, hata muda mrefu baada ya kuwa ameyasahau. Ni kuyaacha maoni yao yakae kwenye kiti cha enzi cha moyo wako ambapo ni Mungu pekee anayepaswa kutawala. Barabara hii haileti amani. Hata ukifanikisha kila kitu, utupu unabaki. Makofi unayotamani hayatawahi kuwa na sauti ya kutosha kunyamazisha maumivu. Uchungu na kiburi ni masahaba katika safari hii, na hawatakuacha nafasi. Leo nataka kukuambia kuwa kuna njia nyingine. Ni njia ya maana, ya kusudi, na ya kutembea katika hatua na Mungu. Ni njia ambayo hufukuzi tena mizimu ya zamani, lakini badala yake fuata wito na hatima ambayo Mungu ameweka mbele yako.

    Huna haja ya kumuaibisha mtu yeyote kwa sababu mtu kama huyo alisema hivi na hivi kukuhusu. Huna haja ya kuharakisha maana walisema hutaolewa kamwe. Baadhi ya waliofanya hivyo, sasa wanaishi kwa majuto. Baadhi yao walikimbilia ili kuthibitisha kwamba baadhi ya watu walikuwa wamekosea, lakini walipofika huko, iliwabidi watoke nje kwa haraka, kwa sababu badala ya kukosea, waligundua kwamba wao wenyewe walikosea kwa kuthibitisha kuwathibitisha watu wengine kwa haraka. Usiwe na haraka tafuta pesa ili waliosema utazipata wainamishe vichwa vyao kwa aibu. Usiseme unaweza kufanya lolote kuwafanya wale maneno yao; unaweza kuwa unafanya maneno yao yatimie. Hukuumbwa kuishi kwa kuguswa na maumivu. Uliumbwa ili uangaze utukufu wa Mungu. Mruhusu akufundishe jinsi ya kutembea kwa ubora, si kwa kulipiza kisasi, bali kwa kusudi. Mwache atengeneze ndoto zako, si kunyamazisha wakosoaji, bali kuheshimu jina Lake. Hebu auponye moyo wako, si hivyo watajuta, lakini hivyo utafurahi. Umeitwa kwenye maisha ya juu zaidi. Wasahau na chochote walichokisema. Wanaweza maoni yao, lakini Mungu ndiye mwenye kutoa maoni ya mwisho. Bwana asema, “Yasahau mambo ya kwanza; usizingatie yaliyopita. Tazama, ninafanya jambo jipya!”* Leo, Mungu anakuita kwenye maisha bora. Minyororo ya maisha yako ya nyuma haina nguvu tena juu yako. Samehe, achilia. Sio kwa wanastahili, lakini kwa sababu unastahili sababu huru. Usijaribu mtu ye yote amekosea; ishi maisha yako tu."
    MWAKA HUU, USIJARIBU KUTHIBITISHA MTU YEYOTE AMEKOSEA... Kuna barabara hatari wengi tunatembea, na wengine kwa sasa wanatembea kwenye barabara hizo bila hata kujua. Ni njia ya matamanio inayochochewa na maumivu, ambayo hupigania kupata kitu ili kudhibiti kuwa watu wengine wamekosea au harakati hiyo na isiyo na mwisho ili kuwaonyesha kuwa unaweza kufanikiwa. Labda walikutilia shaka. Labda walikuumiza, kukataa ndoto zako, au kucheka kwa mapambano yako. Labda, baadhi yao bado wananing'inia wakingojea kusema, "Nilisema." Na sasa, unainuka kila siku ukiendeshwa na sauti hii tulivu inayosema, “Siku moja, wataona. Siku moja nitawaonyesha.” Inahisi heshima, sivyo? Inahisi kama haki. Lakini nakuambia ukweli huu sio uhuru ni gereza. Kuishi maisha yako ili kuthibitisha kuwa mtu amekosea ni kubeba minyororo ya maneno yake na wewe, hata muda mrefu baada ya kuwa ameyasahau. Ni kuyaacha maoni yao yakae kwenye kiti cha enzi cha moyo wako ambapo ni Mungu pekee anayepaswa kutawala. Barabara hii haileti amani. Hata ukifanikisha kila kitu, utupu unabaki. Makofi unayotamani hayatawahi kuwa na sauti ya kutosha kunyamazisha maumivu. Uchungu na kiburi ni masahaba katika safari hii, na hawatakuacha nafasi. Leo nataka kukuambia kuwa kuna njia nyingine. Ni njia ya maana, ya kusudi, na ya kutembea katika hatua na Mungu. Ni njia ambayo hufukuzi tena mizimu ya zamani, lakini badala yake fuata wito na hatima ambayo Mungu ameweka mbele yako. Huna haja ya kumuaibisha mtu yeyote kwa sababu mtu kama huyo alisema hivi na hivi kukuhusu. Huna haja ya kuharakisha maana walisema hutaolewa kamwe. Baadhi ya waliofanya hivyo, sasa wanaishi kwa majuto. Baadhi yao walikimbilia ili kuthibitisha kwamba baadhi ya watu walikuwa wamekosea, lakini walipofika huko, iliwabidi watoke nje kwa haraka, kwa sababu badala ya kukosea, waligundua kwamba wao wenyewe walikosea kwa kuthibitisha kuwathibitisha watu wengine kwa haraka. Usiwe na haraka tafuta pesa ili waliosema utazipata wainamishe vichwa vyao kwa aibu. Usiseme unaweza kufanya lolote kuwafanya wale maneno yao; unaweza kuwa unafanya maneno yao yatimie. Hukuumbwa kuishi kwa kuguswa na maumivu. Uliumbwa ili uangaze utukufu wa Mungu. Mruhusu akufundishe jinsi ya kutembea kwa ubora, si kwa kulipiza kisasi, bali kwa kusudi. Mwache atengeneze ndoto zako, si kunyamazisha wakosoaji, bali kuheshimu jina Lake. Hebu auponye moyo wako, si hivyo watajuta, lakini hivyo utafurahi. Umeitwa kwenye maisha ya juu zaidi. Wasahau na chochote walichokisema. Wanaweza maoni yao, lakini Mungu ndiye mwenye kutoa maoni ya mwisho. Bwana asema, “Yasahau mambo ya kwanza; usizingatie yaliyopita. Tazama, ninafanya jambo jipya!”* Leo, Mungu anakuita kwenye maisha bora. Minyororo ya maisha yako ya nyuma haina nguvu tena juu yako. Samehe, achilia. Sio kwa wanastahili, lakini kwa sababu unastahili sababu huru. Usijaribu mtu ye yote amekosea; ishi maisha yako tu."
    Like
    Love
    2
    1 Kommentare ·157 Ansichten
  • GHOROFA LA BAYTUL AJAAIB(House of Wonders) ZANZIBAR

    Katika mwaka 1884 Sultan wa zanzibar Sayyid Said walitiliana saini mkataba wa kibiashara na Marekani.

    Wamarekani walijenga kinu cha lifti ya kwanza ya umeme katika Afrika mashariki.

    Pia Marekani iliiwezesha Zanzibar kufaidi kuwa na Taa za Barabarani mapema mno kuliko hata London ambayo London wakati huo bado inatumia Taa za Gesi

    Zanzibar ndio ilikuwa ya kwanza kufunga mitambo ya simu ya Wireless iliyokuwa ikisafirisha mawasiliano kutoka Unguja kwenda Bagamoyo, Rwanda, Barundi, Uganda mpaka Koñgo. Kadhalika kutoka Unguja kwenda Aden mpaka Uingereza.

    Ndio maana kuna sehemu panaitwa WELESI hapo ndipo kilipokuwa kituo cha wireless

    Ni vijana wangapi leo hii wanaojua kwamba Mji wa Zanzibar ulikuwa wa mwanzo kuwasha Taa za umeme Barabarani na Mitaani zikiitwa 'Taa za Stimu' kabla ya London na New york?

    Je wewe kijana wajua meli za Marekani zilikuwa zikitia Nanga katika Bandari ya Zanzibar kuja kununua Mafuta ya Nyangumi kwa ajili ya kwenda kuwashia Taa zao za Barabarani wakati Zanzibar inatumia Umeme"

    Imeandaliwa na Victor Richard.
    GHOROFA LA BAYTUL AJAAIB(House of Wonders) ZANZIBAR Katika mwaka 1884 Sultan wa zanzibar Sayyid Said walitiliana saini mkataba wa kibiashara na Marekani. Wamarekani walijenga kinu cha lifti ya kwanza ya umeme katika Afrika mashariki. Pia Marekani iliiwezesha Zanzibar kufaidi kuwa na Taa za Barabarani mapema mno kuliko hata London ambayo London wakati huo bado inatumia Taa za Gesi Zanzibar ndio ilikuwa ya kwanza kufunga mitambo ya simu ya Wireless iliyokuwa ikisafirisha mawasiliano kutoka Unguja kwenda Bagamoyo, Rwanda, Barundi, Uganda mpaka Koñgo. Kadhalika kutoka Unguja kwenda Aden mpaka Uingereza. Ndio maana kuna sehemu panaitwa WELESI hapo ndipo kilipokuwa kituo cha wireless Ni vijana wangapi leo hii wanaojua kwamba Mji wa Zanzibar ulikuwa wa mwanzo kuwasha Taa za umeme Barabarani na Mitaani zikiitwa 'Taa za Stimu' kabla ya London na New york? Je wewe kijana wajua meli za Marekani zilikuwa zikitia Nanga katika Bandari ya Zanzibar kuja kununua Mafuta ya Nyangumi kwa ajili ya kwenda kuwashia Taa zao za Barabarani wakati Zanzibar inatumia Umeme" Imeandaliwa na Victor Richard.
    Like
    1
    ·121 Ansichten
  • OPERATION ENTEBBE -3

    Siku ya July 3 mwaka huo 1976 saa 12 na nusu ya jioni takribani masaa kadhaa kabla ya kufikia deadline ya mwisho waliyopewa na watekaji (July 4), Waziri mkuu wa Israel Yitzhak Rabin alitia saini nyaraka ya kuidhinisha oparesheni ya kijeshi ya uokozi (rescue mission) ambayo iliwasilishwa mezani na Meja Jenerali Yekutiel Adam (maarufu kwa jina la “Kuti”) na Brigedia Generali Dan Shomron. Pia kwa mujibu wa nyaraka hiyo iliyosainiwa na Waziri mkuu, Shomron aliteuliwa kuwa Kamanda wa utekelezaji wa Oparesheni.
    Baada ya oparesheni hii kuidhinishwa rasmi na Baraza la Mawaziri muda huo nilioutaja hapo juu, Meja Jenerali Yekutiel Adam na Brigedia Generali Dan SHomron walikusuka kikosi cha kijeshi kwa ajili ya kutekeleza oparesheni hiyo kama ifuatavyo;
    The Ground Command
    Hiki kilikuwa ni kikosi (japo sio kikosi haswa) ambcho kilikuwa na watu wawili tu, Brigedia Generali Dan Shomron na mwakilishi wa jeshi la Anga la Israel Kanali Ami Ayalon na watu wachache wa masasiliano ya jeshi. Kikosi hiki ndicho ambacho kilikuwa na amri ya mwisho juu ya nini wanajeshi walikuwa wanatakiwa kufanya pindi wakakapoanza utekelezaji wa oparesheni.
    The Asault Team
    Timu hii ilipewa kazi ya kuvamia jengo la uwanja wa ndege ambalo mateka walikuwa wanashikiliwa na kuokoa mateka wote waliomo humo.
    Kikosi hiki kilikuwa na wanajeshi 29 ambacho kiliongozwa na Luteni Kanali Yonathan Netanyahu (kaka yake Waziri Mkuu wa sasa wa Israel, Benjamin Netanyahu). Kikosi hiki kilijumuisha makomando wenye weledi wa hali juu kutoka katika kitengo maalumu cha jeshi la Israel kiitwacho SAYERET MATKAL.
    Nieleze kidogo kuhusu Sayet Matkal.
    Hiki ni kikosi cha weledi maalumu (special force) ndani ya jeshi la Israel la IDF. Makomando wanofuzu kutumika katika kikosi hiki, licha ya kupata mafunzo yote ya kijeshi kama wanajeshi wengine lakini wanaongezewa mafunzo mengine adhimu zaidi kuwafanya waweze kutekeleza oparesheni hata katika mazingira ambayo kwa akili ya kijeshi ya kawaida inaonekana kwamba hakuna uwezekano wa kufanikiwa kwa oparesheni hiyo.
    Mfano wa mafunzo haya adhimu ambayo wanapatiwa ni pamoja na ukusanyaji wa intelijensia, kufanya ‘deep recon’ (nimekosa Kiswahili chake) katika uwanja wa vita, upenyezaji wa intelijensia za kimkakati (strategic intelligence) mafunzo adhimu ya counterterrorism pamoja na uokozi wa mateka nje ya mipaka ya Israel.
    Kwa namna fulani ili kukielewa kikosi hiki unaweza kukifananisha na kikosi cha SAS kwenye jeshi la nchi ya Uingereza japo vinatofauti fulani bado. Ila kwa ufupi huo ndio muonekano wa Sayeret Matkal na shughuli zake.
    The securing Element
    Kikosi hiki kiligawanywa katika vikundi vidogo vidogo vitatu ili kuleta ufanisi.
    1.Paratroopers – hawa waliongozwa na Kanali Matan Vilnai. Kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha hakuna shughuli zozote zinaendelea ndani ya uwanja wa ndege wa Entebbe qawakati ambao oparesheni hiyo inatekelezwa. Pia walikuwa wanatakiwa kuhakikisha kuwa njia ya kurukia ndege (runway) iko ‘clear’ muda wote. Pamoja na hayo kikosi hiki pia walikuwa ndio wanaowajibika kulinda ndege za kijeshi za Israel muda wote zinatakapo kuwa kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe pamoja na ujazaji mafuta.
    2. The Golani Force – kikundi hikicha kijeshi kiliongozwa na Kanali Uri Sagi. Kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa yale madege makubwa aina ya Lockheed Harcules C-130. Pia walitakiwa kuyasogeza madege hayo karibu kabisa na terminal ambayo mateka walikuwepo ili waweze kuwapakia pindi ambapo uokozi ukiwa umefanikiwa. Lakini pia kikundi hiki kilifanya kazi kama ‘kikosi’ cha akiba endapo ambapo kungetoke dharura ya upungufu katika kikosi kingine.
    3. The Sayeret Matkal Force – kikosi hiki nacho pia kama ilivyo kwa ‘Assault Team’ ambayo nimeiongelea hapo juu, nacho pia kiliundwa na makomando wa Sayeret Matkal na kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha kuwa hakukuwa na ‘interception’ yoyote kutoka kwenye jeshi la anga la Uganda na kuwa tayari kuwazuia na kuzuia shambulizi lolote la kijeshi ikitokea kwamba wanajeshi wa Uganda walioko uwanja wa ndege wakiomba msaada kutoka kambi ya jeshi iliyoko ndani ya jiji la Entebbe.
    Kwa ujumla huo ndio ulikuwa muonekano kamili wa Kikosi kizima na majukumu ya wanajeshi wote waliohusia katika oparesheni ya uokozi kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe.
    USIKU WA TAREHE 3 JULY, 1976
    Hatimaye siku ya siku ikawadia, saa lililotarajiwa likafika. Ndege nne kubwa aina ya Lockheed Harcules C-130 zikiwa zimebea zaidi ya makomando 200 pamoja na ile gari Mercedes Limousine (pamoja na gari nyingine aina ya Land Rover) ambayo Ehud Barak alipendekeza waje nayo, ziliruka kutoka kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi ulioko eneo la Sharm El Sheikh mpakani kabisa na Misri.
    Ndege hizi nne kubwa Lockheed Harcules C-130 zilisindikizwa nyuma na ndege mbili aina ya Boeing 707 ambazo moja ilikuwa imelengwa kutumiwa kama ‘command post’ na nyingine itumike kama hospitali kutibu majeruhi ambao watatokana na mapambano ya risasi ambayo walikuwa wanayategemea kati yao na watekaji pamoja na jeshi la Uganda.
    Ndege ziliruka katika njia ya kimataifa kupita Red sea na kwa muda mwingi wa safari yake zililazimika kuruka si zaidi ya mita 30 angani (kuna muda inaelezwa kuwa iliwabidi kuruka mpaka futi 35 kutoka ardhini) ili kuepuka kuonekana na rada za Misi, Sudan na Saud Arabia.
    Safari ilikuwa ngumu haswa hasa ukizingatia kuwa ndege kubwa kama zile zikiruka katika usawa wa karibu hivyo na ardhi mtikisiko unakuwa mkubwa haswa ndani ya ndege.
    Waliokaribia mchepuko wa kusini wa Red Sea ndege zilikata kona na kupita kusini mwa nchi ya Djibouti. Kutokea hapo walielekea mpaka kutokea kaskazini mashariki mwa Nairobi, Kenya na kisha Somalia na kupita eneo la Ogaden nchini Ethiopia.
    Kutoka hapo wakapinda magharibi kufuata bonde la ufa ba mpaka kutokea juu ya ziwa Victoria.
    Ikumbukwe kwamba kati ya ndege zile mbili za Boeing 707 zilizokuwa zinafuatia nyuma na zile Harcules nne, moja ambayo ilipangwa itumike kama hospitali ilitua Nairobi, uwanja wa ndege wa Jomo Kenyetta. Ile nyingine ambayo nimeeleza kwamba ilipangwa itumike kama ‘command post’ ilikuwa inaruka kuzunguka uwanja wa ndege wa Entebbe wakati ndege zile za kijeshi zikitua. Ndege hii (command post) haikutua uwanjani na kamanda mkuu wa oparesheni hii Meja Jenerali Yekutiel Adam alikuwa ndani yake kuwaongoza wenzake walipo ardhini.
    Mnamo saa 23:00 ndege za kijeshi za Israel zilitua kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe huku milango ya nyuma ya mizigo kwenye ndege ikiwa wazi.
    Hapa nieleze kidogo…
    Mbinu kuu ambayo jeshi la Israel walikuwa wanataka kuitumia ili kufanikisha Oparesheni hii ilikuwa ni kufanya shambulio la kushtukiza. !
    Kivipi?
    Katika sehemu iliyopita nilieleza kuwa Ehud Barak baada ya kukusanya intelijensia za kutosha akiwa Kenya, aliwaeleza wenzake kuwa wapakie gari aina ya Mercedes Limousine inayofanana kabisa na ile ambayo inatumiwa na Rais Idd Amin a Uganda ambayo ilikuwa na rangi nyeusi.
    Kwa kuwa walifahamu Rais Idd Amin alikuwa safarini nchini Mauritius kukabidhi uenyekiti wa O.A.U, hivyo walitaka kuigiza kana kwamba Idd Amin alikuwa anarejea kutoka safarini na alikuwa anaenda kutembelea mateka pale uwanja wa ndege kama ambavyo ilikuwa kawaida yake. Hii ndio sababu ya wao kwenda na ile gari nyeusi aina ya Mercedes Limousine pamoja na Land Rover… ambavyo ndivyo ilikuwa namna ambavyo Idd Amin alikuwa anapenda kwenda kutembelea pale uwanjani…. Mercedes Limousine ambayo ina mbeba yeye na nyuma yake gari aina ya Land Rover iliyo na walinzi wake.
    Kwa hiyo ndege ya kwanza ya jeshi la Israel ilipotua kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe ambao kwa muda huo wa saa tano usiku kulikuwa na giza tupu taa zote za uwanja wa ndege zikiwa zimezimwa. Ndege ilitua ikiwa imefunguliwa mlango wa nyuma wa mizigo, ambako ilitoka gari aina ya Mercedes Limousine ikiongozana na Landa Rover na moja kwa zikaendeshwa kuelekea kwenye geti la Terminal ambayo mateka walikuwa wamehifadhiwa.
    Walikuwa wamefaulu kuigiza kabisa msafara wa Idd amin unavyokuwa. Msafara ulikuwa unafanana kabisa na ule wa Idd Amin lakini tofauti ilikuwa kwamba gari hizi ndani yake kuliwa na makomamdo.
    Jambo la ajabu ni kwamba walipofika mbele ya geti la Terminal badala ya kuruhusiwa kupita, wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanalinda getini waliinua bunduki zao na kuwanyoosha kuelea magari haya.
    Walichokuwa hawakijua makomando hawa ambacho wanajeshi hawa waliokuwa wanalinda hapa uwanjani walikijua ni kwamba, Siku moja ya kabla ya Idd Amin kwenda Mauritus alibadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi kwenda rangi nyeupe.
    Kwa hiyo wanajeshi hawa wa Uganda walipoona magari haya walikuwa wanajua fika kuwa huyu hakuwa Rais wao Idd Amin.

    Itaendelea
    #TheBOLD_JF
    OPERATION ENTEBBE -3 Siku ya July 3 mwaka huo 1976 saa 12 na nusu ya jioni takribani masaa kadhaa kabla ya kufikia deadline ya mwisho waliyopewa na watekaji (July 4), Waziri mkuu wa Israel Yitzhak Rabin alitia saini nyaraka ya kuidhinisha oparesheni ya kijeshi ya uokozi (rescue mission) ambayo iliwasilishwa mezani na Meja Jenerali Yekutiel Adam (maarufu kwa jina la “Kuti”) na Brigedia Generali Dan Shomron. Pia kwa mujibu wa nyaraka hiyo iliyosainiwa na Waziri mkuu, Shomron aliteuliwa kuwa Kamanda wa utekelezaji wa Oparesheni. Baada ya oparesheni hii kuidhinishwa rasmi na Baraza la Mawaziri muda huo nilioutaja hapo juu, Meja Jenerali Yekutiel Adam na Brigedia Generali Dan SHomron walikusuka kikosi cha kijeshi kwa ajili ya kutekeleza oparesheni hiyo kama ifuatavyo; The Ground Command Hiki kilikuwa ni kikosi (japo sio kikosi haswa) ambcho kilikuwa na watu wawili tu, Brigedia Generali Dan Shomron na mwakilishi wa jeshi la Anga la Israel Kanali Ami Ayalon na watu wachache wa masasiliano ya jeshi. Kikosi hiki ndicho ambacho kilikuwa na amri ya mwisho juu ya nini wanajeshi walikuwa wanatakiwa kufanya pindi wakakapoanza utekelezaji wa oparesheni. The Asault Team Timu hii ilipewa kazi ya kuvamia jengo la uwanja wa ndege ambalo mateka walikuwa wanashikiliwa na kuokoa mateka wote waliomo humo. Kikosi hiki kilikuwa na wanajeshi 29 ambacho kiliongozwa na Luteni Kanali Yonathan Netanyahu (kaka yake Waziri Mkuu wa sasa wa Israel, Benjamin Netanyahu). Kikosi hiki kilijumuisha makomando wenye weledi wa hali juu kutoka katika kitengo maalumu cha jeshi la Israel kiitwacho SAYERET MATKAL. Nieleze kidogo kuhusu Sayet Matkal. Hiki ni kikosi cha weledi maalumu (special force) ndani ya jeshi la Israel la IDF. Makomando wanofuzu kutumika katika kikosi hiki, licha ya kupata mafunzo yote ya kijeshi kama wanajeshi wengine lakini wanaongezewa mafunzo mengine adhimu zaidi kuwafanya waweze kutekeleza oparesheni hata katika mazingira ambayo kwa akili ya kijeshi ya kawaida inaonekana kwamba hakuna uwezekano wa kufanikiwa kwa oparesheni hiyo. Mfano wa mafunzo haya adhimu ambayo wanapatiwa ni pamoja na ukusanyaji wa intelijensia, kufanya ‘deep recon’ (nimekosa Kiswahili chake) katika uwanja wa vita, upenyezaji wa intelijensia za kimkakati (strategic intelligence) mafunzo adhimu ya counterterrorism pamoja na uokozi wa mateka nje ya mipaka ya Israel. Kwa namna fulani ili kukielewa kikosi hiki unaweza kukifananisha na kikosi cha SAS kwenye jeshi la nchi ya Uingereza japo vinatofauti fulani bado. Ila kwa ufupi huo ndio muonekano wa Sayeret Matkal na shughuli zake. The securing Element Kikosi hiki kiligawanywa katika vikundi vidogo vidogo vitatu ili kuleta ufanisi. 1.Paratroopers – hawa waliongozwa na Kanali Matan Vilnai. Kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha hakuna shughuli zozote zinaendelea ndani ya uwanja wa ndege wa Entebbe qawakati ambao oparesheni hiyo inatekelezwa. Pia walikuwa wanatakiwa kuhakikisha kuwa njia ya kurukia ndege (runway) iko ‘clear’ muda wote. Pamoja na hayo kikosi hiki pia walikuwa ndio wanaowajibika kulinda ndege za kijeshi za Israel muda wote zinatakapo kuwa kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe pamoja na ujazaji mafuta. 2. The Golani Force – kikundi hikicha kijeshi kiliongozwa na Kanali Uri Sagi. Kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa yale madege makubwa aina ya Lockheed Harcules C-130. Pia walitakiwa kuyasogeza madege hayo karibu kabisa na terminal ambayo mateka walikuwepo ili waweze kuwapakia pindi ambapo uokozi ukiwa umefanikiwa. Lakini pia kikundi hiki kilifanya kazi kama ‘kikosi’ cha akiba endapo ambapo kungetoke dharura ya upungufu katika kikosi kingine. 3. The Sayeret Matkal Force – kikosi hiki nacho pia kama ilivyo kwa ‘Assault Team’ ambayo nimeiongelea hapo juu, nacho pia kiliundwa na makomando wa Sayeret Matkal na kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha kuwa hakukuwa na ‘interception’ yoyote kutoka kwenye jeshi la anga la Uganda na kuwa tayari kuwazuia na kuzuia shambulizi lolote la kijeshi ikitokea kwamba wanajeshi wa Uganda walioko uwanja wa ndege wakiomba msaada kutoka kambi ya jeshi iliyoko ndani ya jiji la Entebbe. Kwa ujumla huo ndio ulikuwa muonekano kamili wa Kikosi kizima na majukumu ya wanajeshi wote waliohusia katika oparesheni ya uokozi kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe. USIKU WA TAREHE 3 JULY, 1976 Hatimaye siku ya siku ikawadia, saa lililotarajiwa likafika. Ndege nne kubwa aina ya Lockheed Harcules C-130 zikiwa zimebea zaidi ya makomando 200 pamoja na ile gari Mercedes Limousine (pamoja na gari nyingine aina ya Land Rover) ambayo Ehud Barak alipendekeza waje nayo, ziliruka kutoka kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi ulioko eneo la Sharm El Sheikh mpakani kabisa na Misri. Ndege hizi nne kubwa Lockheed Harcules C-130 zilisindikizwa nyuma na ndege mbili aina ya Boeing 707 ambazo moja ilikuwa imelengwa kutumiwa kama ‘command post’ na nyingine itumike kama hospitali kutibu majeruhi ambao watatokana na mapambano ya risasi ambayo walikuwa wanayategemea kati yao na watekaji pamoja na jeshi la Uganda. Ndege ziliruka katika njia ya kimataifa kupita Red sea na kwa muda mwingi wa safari yake zililazimika kuruka si zaidi ya mita 30 angani (kuna muda inaelezwa kuwa iliwabidi kuruka mpaka futi 35 kutoka ardhini) ili kuepuka kuonekana na rada za Misi, Sudan na Saud Arabia. Safari ilikuwa ngumu haswa hasa ukizingatia kuwa ndege kubwa kama zile zikiruka katika usawa wa karibu hivyo na ardhi mtikisiko unakuwa mkubwa haswa ndani ya ndege. Waliokaribia mchepuko wa kusini wa Red Sea ndege zilikata kona na kupita kusini mwa nchi ya Djibouti. Kutokea hapo walielekea mpaka kutokea kaskazini mashariki mwa Nairobi, Kenya na kisha Somalia na kupita eneo la Ogaden nchini Ethiopia. Kutoka hapo wakapinda magharibi kufuata bonde la ufa ba mpaka kutokea juu ya ziwa Victoria. Ikumbukwe kwamba kati ya ndege zile mbili za Boeing 707 zilizokuwa zinafuatia nyuma na zile Harcules nne, moja ambayo ilipangwa itumike kama hospitali ilitua Nairobi, uwanja wa ndege wa Jomo Kenyetta. Ile nyingine ambayo nimeeleza kwamba ilipangwa itumike kama ‘command post’ ilikuwa inaruka kuzunguka uwanja wa ndege wa Entebbe wakati ndege zile za kijeshi zikitua. Ndege hii (command post) haikutua uwanjani na kamanda mkuu wa oparesheni hii Meja Jenerali Yekutiel Adam alikuwa ndani yake kuwaongoza wenzake walipo ardhini. Mnamo saa 23:00 ndege za kijeshi za Israel zilitua kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe huku milango ya nyuma ya mizigo kwenye ndege ikiwa wazi. Hapa nieleze kidogo… Mbinu kuu ambayo jeshi la Israel walikuwa wanataka kuitumia ili kufanikisha Oparesheni hii ilikuwa ni kufanya shambulio la kushtukiza. ! Kivipi? Katika sehemu iliyopita nilieleza kuwa Ehud Barak baada ya kukusanya intelijensia za kutosha akiwa Kenya, aliwaeleza wenzake kuwa wapakie gari aina ya Mercedes Limousine inayofanana kabisa na ile ambayo inatumiwa na Rais Idd Amin a Uganda ambayo ilikuwa na rangi nyeusi. Kwa kuwa walifahamu Rais Idd Amin alikuwa safarini nchini Mauritius kukabidhi uenyekiti wa O.A.U, hivyo walitaka kuigiza kana kwamba Idd Amin alikuwa anarejea kutoka safarini na alikuwa anaenda kutembelea mateka pale uwanja wa ndege kama ambavyo ilikuwa kawaida yake. Hii ndio sababu ya wao kwenda na ile gari nyeusi aina ya Mercedes Limousine pamoja na Land Rover… ambavyo ndivyo ilikuwa namna ambavyo Idd Amin alikuwa anapenda kwenda kutembelea pale uwanjani…. Mercedes Limousine ambayo ina mbeba yeye na nyuma yake gari aina ya Land Rover iliyo na walinzi wake. Kwa hiyo ndege ya kwanza ya jeshi la Israel ilipotua kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe ambao kwa muda huo wa saa tano usiku kulikuwa na giza tupu taa zote za uwanja wa ndege zikiwa zimezimwa. Ndege ilitua ikiwa imefunguliwa mlango wa nyuma wa mizigo, ambako ilitoka gari aina ya Mercedes Limousine ikiongozana na Landa Rover na moja kwa zikaendeshwa kuelekea kwenye geti la Terminal ambayo mateka walikuwa wamehifadhiwa. Walikuwa wamefaulu kuigiza kabisa msafara wa Idd amin unavyokuwa. Msafara ulikuwa unafanana kabisa na ule wa Idd Amin lakini tofauti ilikuwa kwamba gari hizi ndani yake kuliwa na makomamdo. Jambo la ajabu ni kwamba walipofika mbele ya geti la Terminal badala ya kuruhusiwa kupita, wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanalinda getini waliinua bunduki zao na kuwanyoosha kuelea magari haya. Walichokuwa hawakijua makomando hawa ambacho wanajeshi hawa waliokuwa wanalinda hapa uwanjani walikijua ni kwamba, Siku moja ya kabla ya Idd Amin kwenda Mauritus alibadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi kwenda rangi nyeupe. Kwa hiyo wanajeshi hawa wa Uganda walipoona magari haya walikuwa wanajua fika kuwa huyu hakuwa Rais wao Idd Amin. Itaendelea #TheBOLD_JF
    ·443 Ansichten
  • OPERATION ENTEBBE -4

    Katika sehemmu iliyopita nilieleza namna ambavyo baada ya madege ya kivita ya Lockheed Harcules C-130 kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe na moja ya ndege hizo kwenda moja kwa moja karibu na geti la Terminal huku mlango wa nyuma ukiwa wazi na kutoka gari aina na Mercides pamoja na Land Rover kufanana kabisa na msafara wa Idd Amin atembeleapo uwanja wa ndege, la kini ajabu ni kwamba walijikuta wakinyooshewa bunduki na wanajeshi waliokuwa wanalinda getini…
    Walikuwa hawana taarifa kuwa Amin alikuwa amebadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi kwenda nyeupe kabla ya safari yake ya kwenda Mauritius kwenye kikao cha O.A.U.
    Tuendelee…
    SEHEMU TA NNE
    Wanajeshi hawa wawili wa Uganda waliokuwa getini walinyanyua bunduki zao aina ya Kalashnikov na hawakuonyesha dalili kwamba labda walikuwa wanataka kufanya ukaguzi wa kawaida tu kabla ya kuwaruhusu, walionyesha dhahiri kabisa kwamba walikuwa wanataka kufanya shambulio.
    Kabla wanajeshi hao wa Uganda kufanya lolote lile, Netanyahu na komando mwingine ambao walikuwa ndani ya gari walitumia weledi wao kufanya uamuzi makini wa haraka kwa kufyatua risasi kutoka kwenye bastola zao zenye ‘silencer’ na mara moja wale wanajeshi wawili wa Uganda walienda chini.
    Lakini moja ya wale wanajeshi wa Uganda waliodondoka chini baada ya kufyatuliwa risasi, hakufa mara moja na alikuwa anajitahidi kuinuka. Hii ilisababisha komando mwingine wa Israel kufyatua risasi lakini safari hii huyu komando wa Israel alifyatua risasi kutoka kwenye bunduki ambayo haina ‘silencer’. Hii iliwashitua wanajeshi wengine wa Uganda waliokuwa nje ya Terminal na kuanza kukimbilia walipokuwa wanasikia milio ya risasi inatokea huku wanafyatua risasi.
    Kwa maneno mengine ilikuwa kwa kiasi fulani walichokuwa wamekipanga makomando wa Israel, kufanya shambulio la kushitukiza lakini mpaka muda huu tayari ile ‘element of surprise’ ilikuwa haipo tena, jeshi la Uganda lilikuwa limeshitukia ‘mchezo’.
    Bila kuchelewa sana, makomando wote walikuwa kwenye zile gari mbili (Mercedes na Land Rover) waliruka nje ya gari na kukimbia kuelekea ndani ya terminal.
    Vichwani mwao walikuwa bado hawajaondokewa na kumbukumbu ya oparesheni kama hii iliyotokea miaka miwili iliyopita nchini Israel kwenye mji wa Ma’a lot ambapowatekaji wa KIpalestina baada ya kushituka kuwa kulikuwa na makomando wa Israel wamefika kufanya uokozi, waliwapiga risasi mateka wao 25 ambao kati yao 22 walikuwa ni watoto wadogo.
    Hivyo Netanyahu na wenzake hawakutaka kitu kama hiki kjitokeze tena… Netenyahu na makomando wenzake wa Syeret Matkal kwa ustadi wa hali ya juu walikimbia na kuingia ndani ya terminal na kuwaacha vile vikosi vingine kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliopo nje ya terminal (kama nilivyoeleza juzi namna kikosi kilivyogawanywa kwenye vikundi vidogo kila kimoja kikipewa jukumu lake).
    Mateka wanaeleza kwamba baada ya mpambano ya risasi kuanza huko nje ya terminal waliwaona watekaji kadhaa wakiongozwa na yule aliyeonekana kama kiongozi wao, Wilfred Bose waliingia ndani ya terminal wakiwa wanahaha kama wamechanganyikiwa wasijue wafanye nini, ilionekana dhahiri kuwa walikuwa hawajajiandaa kwa hili shambulio la ghafla, ilionekana dhahiri kwamba katika akili yao walikuwa wanasubiria Israel kutimiza masharti yao ili waweze kuachia mateka.
    Kuna muda Wilfred Bose alionekana kunyoonya bunduki yake kwa mateka kama vile anawataka kuwamininia risasi lakini alikuwa anashindwa kufanya uamuzi huo. Bose aligeuka ghafla baada ya kusikia kishindo cha mlango wa terminal ukifunguliwa.
    Makomando wa Israel walikuwa wametumia weledi na ustadi wao wa hali ya juu kuingia ndani ya terminal kwa muda sahihi kabla ya Wilfred Bose na wenzake kufanya uamuzi wowote wa kuua mateka.
    Makomando wa Israel walipoingia tu ndani ya terminal, mmoja wao mkononi walikuwa na kipaza sauti aina ya ‘megaphone’ na alikuwa anaongeea kwa nguvu kwa lugha ya kihebrania, “Lay down, Lay down. We are Israel soldiers. Lay down. Lay down!!”.
    Mateka wote wa kiisrael hata wale waliokuwa wamekaa kitako walilala chini, hivyo ndani ya sekunde chache tu kila mtu ambaye alibakia amesimama alikuwa ni halali yao kumtandika risasi.
    Kwa bahati mbaya kulikuwa na mateka kadhaa ambao wwalikuwa hawajui kihebreania sawia na hii iliwagharimu sana. Kwa mfano kulikuwa na kijana wa mika 19 aliyeitwa Jean-Jacques Maimoni, huyu alikuwa amehamia Israel siku si nyingi sana kutokea nchini ufaransa. Lilipotolewa tangazo hilo la kila mtu kulala chini hakuelewa na alibakia akiwa amesimama na alitandikwa risasi na makomando wa Israel pamoja na wale watekaji. Kijana huyu hakuwa peke yake, lakini pia kulikuwa na mateka mwingine aliyeitwa Ida Borochovitch, ambaye alihamia Israel kutoka nchini Urusi.
    Risasi zilirindima kwa takribani dakika mbili nzima na baadae ukimya wa kama sekunde 15 ukatawala na moja wa makomando wa kiisrael akauliza kwa kiebrania, “where are the rest of them?” (“wako wapi wengine?”). Mateka wakaonyesha kidole kwenye chumba kidogo kilichopo pembeni.
    Makomando wakarusha mabomu kadhaa ya kutupa kwa mkono na kisha kuingia ndani ya chumba hicho na kuwamiminia risasi wote ambao walikuwa humo.
    Milio ya risasi ndani ya terminal hatimaye ilikuwa imekoma japo bado huko nje walisikia majibizano ya risasi. Mwanajeshi mmoja wa Israel kati ya wale waliopo ndani ya terminal, kwa sauti ya utulivu kabisa na katika lugha ya kihebrania aliwatangazia mateka, “listen guys, we’ve come to take you home!” (“sikilizeni, tumekuja kuwachukua kuwarudisha nyumbani!”).
    Baada ya hapo makomando walianza kuwatoa mateka kutoka kwenye terminal na kuwapakia kwenye ndege kwa tahadhari kubwa huku wale wenzao wengine wakiendelea kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanarusha risasi kutoka kwenye maeneo ya kujificha ndani ya uwanja wa ndege.
    Wakiwa wanaendelea kuwapakia mateka waliowaokoa kwenye ndege, kumbe kulikuwa na mwanajeshi wa Uganda amebakia juu kwenye mnara wa uongozaji (airport control tower). Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibunui kutoka kwa mtoto wa Idd Amin anasema kwamba mwanajeshi huyu alikuwa ni binamu wa Idd Amin. Kutokea hapo kwenye mnara alimimina risasi mfululizo kwa makomando wa Israel na moja ya risasi hizi ilimpaka Koamando Yonatan Netanyahu ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Matkal iliyopo hapoa na alipoteza uhai pale pale.
    Wanajeshi wa Isarel walijibu mapigo kwa kurusha bomu la roketi ndogo ya begani na kusambaratisha kabisa kiota cha mnara na kumuua mwanajeshi wa Uganda aliyekuwa anawashambulia.
    Baada ya hapo waliwapakia kwenye ndege mateka wote ambao waliokolewa pamoja na miili ya Waisrael ambao walifariki kwenye majibizano hayo ya risasi.
    Kisha ili kuhakikisha kuwa hakuna ndege itakayowafuatia nyuma wakiondoka au kushambuliwa, walilipua ndege zote za jeshi la Uganda ambazo zilikuwa uwanjani hapo.
    Oparesheni yote hii ilichukua takribani dakika 53 ambapo dakika 30 pekee ndio zilikuwa za mapigano na 23 zilizosalia zilikuwa za kupakia mateka walio okolewa na kuondoka.
    Mpaka kufikia mwishio mwa oparesheni, jumla ya watekaji wote 7 walikuwa wameuwawa, pia wanajeshi 45 wa jeshi la Uganda walikuwa wameuwawa pia. Lakini pia ndege za kijeshi 11 aina ya MiG-17 na Mig-21 zililipuliwa na makomando wa Isarel. Ikumbukwe kwamba ndege hizi ndizo zilikuwa ni ndege zote za kijeshi ambazo zilikuwa zinamilikiwa na jeshi la anga la Uganda. Hii inaonyesha moja kati ya mapungufu makubwa ya kiuongozi ya Amin. Hakukuwa na busara yoyote au faida yoyote ya kimkakati kuweka ndege zote za jeshi lako la anga kwenye uwanja wa ndege wa kiraia ili kulinda mateka wa tukio ambalo wengine walikuwa wanaweza kuliona kama tukio la kigaidi na kwa namna Fulani kama ugomvi ambao ulikuwa haumuhusu moja kwa moja.
    Katika mateka wote 106 waliobakia (kumbuka nilieleza kuwa kulikuwa na mikupuo miwili ya mateka wasio wa Kiisrael au asili ya Kiyahudi waliachiwa kwa kupelekwa na ndege ufaransa nchini), kwahiyo kati ya wale 106 waliobakio, mateka watatu waliuwawa muda wa mapambano (hawa ndio wale ambao walikuwa hawaelewi kihebrania kwa ufasaha na kwa hiyo hawakulalala chini kama ilivyoamrishwa na makomando wa Israel), na mateka mmoja bibi wa miaka 74 aliyeitwa Dora Bloch aliachwa akiwa Hospitali mjini Entebbe ambako alipelekwa na Amin siku kadhaa nyuma kutokana na kuhitaji uangalizi maalumu wa kidaktari.
    Kati ya Makomando wa Isarel, ni mmoja tu ndiye aliuwawa tena dakika za mwisho (Yonatan Netanyahu) japo pia kuna makomando wengine kama watano ambao walijeruhiwa. Kifo cha kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Mitkal, Yonatan Netanyahu katika oparesheni hii ndio iliyofanya siku kadhaa baadae oparesheni hii pia kubatizwa jina la OPERATION YONATAN kwa heshima yake na ushujaa wake wa kutoa maisha yake ili kutetea na kuooa roho za raia alioapa kuwalinda.
    Baada ya kila kitu kuwekwa sawa na watu wote kupanda ndani ya ndege, waliruka mpaka Nairobi Kenya kwa mapumziko mafupi ili kutibia wale ambao walijeruhiwa (kama ambavyo nilieleza kuwa ile moja ya Boeing 707 iliyotengwa kama ‘hospitali’ ilibaki Nairobi).
    Baada ya matibabu hapo Nairobi, madege yote yaliruka kurudi Israel. Kwa kifupi operation hii was a big SUCCESS.!
    Japokuwa baada ya ulimwengu mzima kutangaziwa juu ya kilichotokea, juu ya ‘umafia’ uliofanywa na Israel, ulimwengu uligawanyika kila nchi ukiunga mkono upande fulani, lakini nchi nyingi ziliunga mkono Israel kwa matumizi ya jeshi katika nchi nyingine, wengi walimlaumu Amin kwa kushindwa kutumia diplomasia kumaliza mzozo huu. Ajabu ni kwamba mwezi huo wa July, Mkuu wa Majeshi wa Iran moja wa mahsimu wa siku zote wa Israel aliandika barua kwa Waziri mkuu wa Israel kumpongeza kuhusu Oparation hiyo na kumpa pole kwa kifo cha Yonatan Netanyahu akimuita Yonatan kumsifu kuwa ni ‘martyr’.
    Vyovyote vile ambavyo unaweza kuitazama oparesheni hii kwenye jicho la kisiasa ua kidiplomasia, kwamba kama ilikuwa ni sahihi au si sahihi lakini katika jicho la kijeshi na ujasusi hii ni moja ya oparesheni murua kabisa kuwahi kufanyika katika historia ya majeshi duniani. Moja ya manguli wa “ulimwengu wa giza”, Bw. Henry Kissinger aliwahi kutamka kuwa hii ilikuwa ni “an immposible mission”!
    Umaridadi wa oparesheni hii umefanya hata vitengo kadhaa vya weledi vya majeshi mbali mbali kutaka kuiga mfano wake lakini bila mafanikio yoyote. Kwa mfano Wamarekani walijaribu kuiga umaridadi wa Oparesheni hii na kufanya ya kwao iliyoitwa Oparation Eagle Claw baada ya kutokea kwa utekeaji kwenye ubalozi wa Iran lakini oparesheni hiyo ilifeli vibaya.
    Sasa hivi kama wewe ni mwanajeshi katika jeshi fulani kwenye kitengo cha weledi (special force) au labda ni jasusi maalumu, lazima katika hatua fulani ya japo hata ‘darasani’ kwenye makaratasi utafundwa kuhusu Oparetion Entebbe na namna ilivyo tekelezwa.
    Oparesheni hii ilimuacha Amin na aibu kubwa kiasi kwamba akaendelea kufanya vitu ambavyo vilidhihirisha udhaifu wake wa kiungozi. Kwa mfano, yule bibi wa miaka 74 aliyeachwa hospitali mjini Entebbe, aliamuru auwawe kinyama. Lakini pia Amin alisimami kuwawa kwa McKenzie yule waziri wa kilimo wa Kenya ambaye alimsaidia Ehud Barak kumshinikiza Mzee Jomo Kenyetta kuruhusu ndege za jeshi la Israel kutumia viwanja vya ndege vya Kenya wakati wa utekelezaji wa OParesheni hiyo na pia kumsaidi kukusanya Intelijensia kwa kutumia ndege yake binafsi.
    McKenzie aliuwawa kwa bomu lililotegwa kwenye gari yake.
    Pia Amin alisimamia ulipuaji kwa bomu moja ya hoteli kubwa Nairobi kipindi hicho ambayo ilikuwa inaitwa The Norfolk Hotel, ambayo ilimilikiwa na moja ya wayahudi mashuhuri nchini Kenya.
    [6/12, 13:48] The Bold: Licha ya ‘fujo’ zote hizi ambazo Amin alizifanya baada ya jeshi lake kudhalilika kutokana na Oeration Entebbe lakini hatupawsi kusahau kwamba chini ya miaka mitatu baadae, yaani baada ya utekelezaji wa opareshini hii, Idd Amin aliondolewa kwa aibu madarakani na majeshi ya Tanzania na kumfanya akimbie nchi yake.

    ......................MWISHO..............
    #TheBOLD_JF
    OPERATION ENTEBBE -4 Katika sehemmu iliyopita nilieleza namna ambavyo baada ya madege ya kivita ya Lockheed Harcules C-130 kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe na moja ya ndege hizo kwenda moja kwa moja karibu na geti la Terminal huku mlango wa nyuma ukiwa wazi na kutoka gari aina na Mercides pamoja na Land Rover kufanana kabisa na msafara wa Idd Amin atembeleapo uwanja wa ndege, la kini ajabu ni kwamba walijikuta wakinyooshewa bunduki na wanajeshi waliokuwa wanalinda getini… Walikuwa hawana taarifa kuwa Amin alikuwa amebadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi kwenda nyeupe kabla ya safari yake ya kwenda Mauritius kwenye kikao cha O.A.U. Tuendelee… SEHEMU TA NNE Wanajeshi hawa wawili wa Uganda waliokuwa getini walinyanyua bunduki zao aina ya Kalashnikov na hawakuonyesha dalili kwamba labda walikuwa wanataka kufanya ukaguzi wa kawaida tu kabla ya kuwaruhusu, walionyesha dhahiri kabisa kwamba walikuwa wanataka kufanya shambulio. Kabla wanajeshi hao wa Uganda kufanya lolote lile, Netanyahu na komando mwingine ambao walikuwa ndani ya gari walitumia weledi wao kufanya uamuzi makini wa haraka kwa kufyatua risasi kutoka kwenye bastola zao zenye ‘silencer’ na mara moja wale wanajeshi wawili wa Uganda walienda chini. Lakini moja ya wale wanajeshi wa Uganda waliodondoka chini baada ya kufyatuliwa risasi, hakufa mara moja na alikuwa anajitahidi kuinuka. Hii ilisababisha komando mwingine wa Israel kufyatua risasi lakini safari hii huyu komando wa Israel alifyatua risasi kutoka kwenye bunduki ambayo haina ‘silencer’. Hii iliwashitua wanajeshi wengine wa Uganda waliokuwa nje ya Terminal na kuanza kukimbilia walipokuwa wanasikia milio ya risasi inatokea huku wanafyatua risasi. Kwa maneno mengine ilikuwa kwa kiasi fulani walichokuwa wamekipanga makomando wa Israel, kufanya shambulio la kushitukiza lakini mpaka muda huu tayari ile ‘element of surprise’ ilikuwa haipo tena, jeshi la Uganda lilikuwa limeshitukia ‘mchezo’. Bila kuchelewa sana, makomando wote walikuwa kwenye zile gari mbili (Mercedes na Land Rover) waliruka nje ya gari na kukimbia kuelekea ndani ya terminal. Vichwani mwao walikuwa bado hawajaondokewa na kumbukumbu ya oparesheni kama hii iliyotokea miaka miwili iliyopita nchini Israel kwenye mji wa Ma’a lot ambapowatekaji wa KIpalestina baada ya kushituka kuwa kulikuwa na makomando wa Israel wamefika kufanya uokozi, waliwapiga risasi mateka wao 25 ambao kati yao 22 walikuwa ni watoto wadogo. Hivyo Netanyahu na wenzake hawakutaka kitu kama hiki kjitokeze tena… Netenyahu na makomando wenzake wa Syeret Matkal kwa ustadi wa hali ya juu walikimbia na kuingia ndani ya terminal na kuwaacha vile vikosi vingine kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliopo nje ya terminal (kama nilivyoeleza juzi namna kikosi kilivyogawanywa kwenye vikundi vidogo kila kimoja kikipewa jukumu lake). Mateka wanaeleza kwamba baada ya mpambano ya risasi kuanza huko nje ya terminal waliwaona watekaji kadhaa wakiongozwa na yule aliyeonekana kama kiongozi wao, Wilfred Bose waliingia ndani ya terminal wakiwa wanahaha kama wamechanganyikiwa wasijue wafanye nini, ilionekana dhahiri kuwa walikuwa hawajajiandaa kwa hili shambulio la ghafla, ilionekana dhahiri kwamba katika akili yao walikuwa wanasubiria Israel kutimiza masharti yao ili waweze kuachia mateka. Kuna muda Wilfred Bose alionekana kunyoonya bunduki yake kwa mateka kama vile anawataka kuwamininia risasi lakini alikuwa anashindwa kufanya uamuzi huo. Bose aligeuka ghafla baada ya kusikia kishindo cha mlango wa terminal ukifunguliwa. Makomando wa Israel walikuwa wametumia weledi na ustadi wao wa hali ya juu kuingia ndani ya terminal kwa muda sahihi kabla ya Wilfred Bose na wenzake kufanya uamuzi wowote wa kuua mateka. Makomando wa Israel walipoingia tu ndani ya terminal, mmoja wao mkononi walikuwa na kipaza sauti aina ya ‘megaphone’ na alikuwa anaongeea kwa nguvu kwa lugha ya kihebrania, “Lay down, Lay down. We are Israel soldiers. Lay down. Lay down!!”. Mateka wote wa kiisrael hata wale waliokuwa wamekaa kitako walilala chini, hivyo ndani ya sekunde chache tu kila mtu ambaye alibakia amesimama alikuwa ni halali yao kumtandika risasi. Kwa bahati mbaya kulikuwa na mateka kadhaa ambao wwalikuwa hawajui kihebreania sawia na hii iliwagharimu sana. Kwa mfano kulikuwa na kijana wa mika 19 aliyeitwa Jean-Jacques Maimoni, huyu alikuwa amehamia Israel siku si nyingi sana kutokea nchini ufaransa. Lilipotolewa tangazo hilo la kila mtu kulala chini hakuelewa na alibakia akiwa amesimama na alitandikwa risasi na makomando wa Israel pamoja na wale watekaji. Kijana huyu hakuwa peke yake, lakini pia kulikuwa na mateka mwingine aliyeitwa Ida Borochovitch, ambaye alihamia Israel kutoka nchini Urusi. Risasi zilirindima kwa takribani dakika mbili nzima na baadae ukimya wa kama sekunde 15 ukatawala na moja wa makomando wa kiisrael akauliza kwa kiebrania, “where are the rest of them?” (“wako wapi wengine?”). Mateka wakaonyesha kidole kwenye chumba kidogo kilichopo pembeni. Makomando wakarusha mabomu kadhaa ya kutupa kwa mkono na kisha kuingia ndani ya chumba hicho na kuwamiminia risasi wote ambao walikuwa humo. Milio ya risasi ndani ya terminal hatimaye ilikuwa imekoma japo bado huko nje walisikia majibizano ya risasi. Mwanajeshi mmoja wa Israel kati ya wale waliopo ndani ya terminal, kwa sauti ya utulivu kabisa na katika lugha ya kihebrania aliwatangazia mateka, “listen guys, we’ve come to take you home!” (“sikilizeni, tumekuja kuwachukua kuwarudisha nyumbani!”). Baada ya hapo makomando walianza kuwatoa mateka kutoka kwenye terminal na kuwapakia kwenye ndege kwa tahadhari kubwa huku wale wenzao wengine wakiendelea kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanarusha risasi kutoka kwenye maeneo ya kujificha ndani ya uwanja wa ndege. Wakiwa wanaendelea kuwapakia mateka waliowaokoa kwenye ndege, kumbe kulikuwa na mwanajeshi wa Uganda amebakia juu kwenye mnara wa uongozaji (airport control tower). Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibunui kutoka kwa mtoto wa Idd Amin anasema kwamba mwanajeshi huyu alikuwa ni binamu wa Idd Amin. Kutokea hapo kwenye mnara alimimina risasi mfululizo kwa makomando wa Israel na moja ya risasi hizi ilimpaka Koamando Yonatan Netanyahu ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Matkal iliyopo hapoa na alipoteza uhai pale pale. Wanajeshi wa Isarel walijibu mapigo kwa kurusha bomu la roketi ndogo ya begani na kusambaratisha kabisa kiota cha mnara na kumuua mwanajeshi wa Uganda aliyekuwa anawashambulia. Baada ya hapo waliwapakia kwenye ndege mateka wote ambao waliokolewa pamoja na miili ya Waisrael ambao walifariki kwenye majibizano hayo ya risasi. Kisha ili kuhakikisha kuwa hakuna ndege itakayowafuatia nyuma wakiondoka au kushambuliwa, walilipua ndege zote za jeshi la Uganda ambazo zilikuwa uwanjani hapo. Oparesheni yote hii ilichukua takribani dakika 53 ambapo dakika 30 pekee ndio zilikuwa za mapigano na 23 zilizosalia zilikuwa za kupakia mateka walio okolewa na kuondoka. Mpaka kufikia mwishio mwa oparesheni, jumla ya watekaji wote 7 walikuwa wameuwawa, pia wanajeshi 45 wa jeshi la Uganda walikuwa wameuwawa pia. Lakini pia ndege za kijeshi 11 aina ya MiG-17 na Mig-21 zililipuliwa na makomando wa Isarel. Ikumbukwe kwamba ndege hizi ndizo zilikuwa ni ndege zote za kijeshi ambazo zilikuwa zinamilikiwa na jeshi la anga la Uganda. Hii inaonyesha moja kati ya mapungufu makubwa ya kiuongozi ya Amin. Hakukuwa na busara yoyote au faida yoyote ya kimkakati kuweka ndege zote za jeshi lako la anga kwenye uwanja wa ndege wa kiraia ili kulinda mateka wa tukio ambalo wengine walikuwa wanaweza kuliona kama tukio la kigaidi na kwa namna Fulani kama ugomvi ambao ulikuwa haumuhusu moja kwa moja. Katika mateka wote 106 waliobakia (kumbuka nilieleza kuwa kulikuwa na mikupuo miwili ya mateka wasio wa Kiisrael au asili ya Kiyahudi waliachiwa kwa kupelekwa na ndege ufaransa nchini), kwahiyo kati ya wale 106 waliobakio, mateka watatu waliuwawa muda wa mapambano (hawa ndio wale ambao walikuwa hawaelewi kihebrania kwa ufasaha na kwa hiyo hawakulalala chini kama ilivyoamrishwa na makomando wa Israel), na mateka mmoja bibi wa miaka 74 aliyeitwa Dora Bloch aliachwa akiwa Hospitali mjini Entebbe ambako alipelekwa na Amin siku kadhaa nyuma kutokana na kuhitaji uangalizi maalumu wa kidaktari. Kati ya Makomando wa Isarel, ni mmoja tu ndiye aliuwawa tena dakika za mwisho (Yonatan Netanyahu) japo pia kuna makomando wengine kama watano ambao walijeruhiwa. Kifo cha kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Mitkal, Yonatan Netanyahu katika oparesheni hii ndio iliyofanya siku kadhaa baadae oparesheni hii pia kubatizwa jina la OPERATION YONATAN kwa heshima yake na ushujaa wake wa kutoa maisha yake ili kutetea na kuooa roho za raia alioapa kuwalinda. Baada ya kila kitu kuwekwa sawa na watu wote kupanda ndani ya ndege, waliruka mpaka Nairobi Kenya kwa mapumziko mafupi ili kutibia wale ambao walijeruhiwa (kama ambavyo nilieleza kuwa ile moja ya Boeing 707 iliyotengwa kama ‘hospitali’ ilibaki Nairobi). Baada ya matibabu hapo Nairobi, madege yote yaliruka kurudi Israel. Kwa kifupi operation hii was a big SUCCESS.! Japokuwa baada ya ulimwengu mzima kutangaziwa juu ya kilichotokea, juu ya ‘umafia’ uliofanywa na Israel, ulimwengu uligawanyika kila nchi ukiunga mkono upande fulani, lakini nchi nyingi ziliunga mkono Israel kwa matumizi ya jeshi katika nchi nyingine, wengi walimlaumu Amin kwa kushindwa kutumia diplomasia kumaliza mzozo huu. Ajabu ni kwamba mwezi huo wa July, Mkuu wa Majeshi wa Iran moja wa mahsimu wa siku zote wa Israel aliandika barua kwa Waziri mkuu wa Israel kumpongeza kuhusu Oparation hiyo na kumpa pole kwa kifo cha Yonatan Netanyahu akimuita Yonatan kumsifu kuwa ni ‘martyr’. Vyovyote vile ambavyo unaweza kuitazama oparesheni hii kwenye jicho la kisiasa ua kidiplomasia, kwamba kama ilikuwa ni sahihi au si sahihi lakini katika jicho la kijeshi na ujasusi hii ni moja ya oparesheni murua kabisa kuwahi kufanyika katika historia ya majeshi duniani. Moja ya manguli wa “ulimwengu wa giza”, Bw. Henry Kissinger aliwahi kutamka kuwa hii ilikuwa ni “an immposible mission”! Umaridadi wa oparesheni hii umefanya hata vitengo kadhaa vya weledi vya majeshi mbali mbali kutaka kuiga mfano wake lakini bila mafanikio yoyote. Kwa mfano Wamarekani walijaribu kuiga umaridadi wa Oparesheni hii na kufanya ya kwao iliyoitwa Oparation Eagle Claw baada ya kutokea kwa utekeaji kwenye ubalozi wa Iran lakini oparesheni hiyo ilifeli vibaya. Sasa hivi kama wewe ni mwanajeshi katika jeshi fulani kwenye kitengo cha weledi (special force) au labda ni jasusi maalumu, lazima katika hatua fulani ya japo hata ‘darasani’ kwenye makaratasi utafundwa kuhusu Oparetion Entebbe na namna ilivyo tekelezwa. Oparesheni hii ilimuacha Amin na aibu kubwa kiasi kwamba akaendelea kufanya vitu ambavyo vilidhihirisha udhaifu wake wa kiungozi. Kwa mfano, yule bibi wa miaka 74 aliyeachwa hospitali mjini Entebbe, aliamuru auwawe kinyama. Lakini pia Amin alisimami kuwawa kwa McKenzie yule waziri wa kilimo wa Kenya ambaye alimsaidia Ehud Barak kumshinikiza Mzee Jomo Kenyetta kuruhusu ndege za jeshi la Israel kutumia viwanja vya ndege vya Kenya wakati wa utekelezaji wa OParesheni hiyo na pia kumsaidi kukusanya Intelijensia kwa kutumia ndege yake binafsi. McKenzie aliuwawa kwa bomu lililotegwa kwenye gari yake. Pia Amin alisimamia ulipuaji kwa bomu moja ya hoteli kubwa Nairobi kipindi hicho ambayo ilikuwa inaitwa The Norfolk Hotel, ambayo ilimilikiwa na moja ya wayahudi mashuhuri nchini Kenya. [6/12, 13:48] The Bold: Licha ya ‘fujo’ zote hizi ambazo Amin alizifanya baada ya jeshi lake kudhalilika kutokana na Oeration Entebbe lakini hatupawsi kusahau kwamba chini ya miaka mitatu baadae, yaani baada ya utekelezaji wa opareshini hii, Idd Amin aliondolewa kwa aibu madarakani na majeshi ya Tanzania na kumfanya akimbie nchi yake. ......................MWISHO.............. #TheBOLD_JF
    ·594 Ansichten
Suchergebnis