NANI MWAMBA KATI YA SIMBA NA YANGA ?
A. REKODI ZA YANGA:
1. Kama kuna timu imewahi kuinyanyasa SIMBA, basi ni YANGA. Hakuna timu imeifunga SIMBA mara nyingi toka ianzishwe 8.8.1936 kama YANGA.
2. YANGA imetwaa ubingwa wa Ligi mara 30, SIMBA mara 22 ie Mama Samia ataondoka madarakani 2030 SIMBA ikiwa haijavunja rekodi hii hata ikishinda mfululizo!
3. YANGA imeshinda mechi nyingi zaidi za ligi kuliko SIMBA.
4. YANGA imefunga magoli mengi ya Ligi kuliko SIMBA. YANGA ndio imefungwa mabao machache zaidi mechi za watani.
5. YANGA imeshinda mechi nyingi za watani kuliko SIMBA. Mechi 4 za mwisho, SIMBA kafa zote!
6. YANGA ndio ilishinda pambano la kwanza la watani (Juni 7, 1965)
7. YANGA imetoa mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi ya ligi kwa misimu mingi (Kitwana Manara).
8. YANGA imetoa mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi kwa msimu mmoja (MOHAMMED HUSSEIN "MMACHINGA")
9. YANGA imetoa Mchezaji Bora kuwahi kutokea nchini (SUNDAY MANARA "COMPUTER").
10. YANGA ilitoa mchezaji wa _"Kombaini ya Afrika 1973"_ (MAULID DILUNGA)1973. Kamba za SIMBA kuwa nao walitoa mchezaji (OMAR MAHADHI ziliumbuliwa baada ya kubainika MAHADHI alijiunga SIMBA 1975. 1973 MAHADHI alikuwa African Sports!)
11. YANGA ndio timu iliyoshinda pambano la Kihistoria na Bora kuliko yote ya watani (Nyamagana 10.8.1974: 2-1)
12. YANGA ndio timu pekee iliyofika fainali kombe la 2 kwa ukubwa Afrika (CAF Confederation cup 2023). SIMBA ilifika fainali 1993 kwenye kombe lililokuwa la 3 kwa hadhi ie "Caf cup". Kombe hili lilikuwa nyuma ya Kombe la Klabu Bingwa na Kombe la Washindi). Kwenye fainali, YANGA ilikosa kombe kwa Kanuni ya goli la ugenini (2-2) ila SIMBA ilikandwa kiduwanzi 2-0.
13. YANGA ndio timu pekee nchini iliyowahi kuingia "TOP 5" ya kinyang'anyiro cha timu bora Afrika (2023).
14. YANGA ndio timu pekee iliyotwaa ubingwa nje ya nchi (1993 & 1999)
15. YANGA ndio timu iliyoalikwa Ikulu na Marais wengi kuliko timu yeyote (Novemba 11, 1969 ilialikwa na Rais Nyerere, Februari 4, 1993 ilialikwa na Rais Mwinyi na Juni 4, 2023 ilialikwa na Rais Samia).
16. YANGA ndiyo timu pekee nchini iliyowahi kualikwa kwenye sherehe za uhuru wa Taifa jingine (Malawi Julai 7, 2023).
17. YANGA iliweka rekodi (2023) ya kuwa timu ya kwanza nchini kushinda mechi nyingi zaidi nje ya nchi michuano ya Afrika
*NB:* Mashabiki maandazi wa SIMBA wanalialia eti YANGA inapata mafanikio kwaajili GSM anadhamini timu nyingi. Huu ni Upuuzi wa kiwango cha SGR! Kwani GSM alikuepo 1960s, 1970s, 1980s, nk ?
B. REKODI MUJARAB ZA SIMBA:
1. Bw. Ramadhani Ali, Mnazi kindakindaki wa SIMBA, aliweka rekodi ya watani baada ya kumkabidhi mkewe, Bi Mwajuma Sadiki Ali kwa mnazi wa Yanga, Bw. Juma Gobe, magomeni Juni 1, 1968 baada ya Yanga kuitandika SIMBA 5-0. Hao jamaa walikuwa wamepinga kabla ya mechi kuwa timu itakayofungwa, aliyefungwa atamgawa mkewe !.
2. SIMBA ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kuweka mpira kwapani mechi ya watani (Machi 3, 1969)
3. Mnazi wa Simba wa Tabora aliandika rekodi ya kujiua kwa kujitumbukiza kwenye pipa la mafuta baada ya SIMBA kufungwa 2-1 Nyamagana 10.8.1974. Timu ya SIMBA ilionesha ubinadamu ilipoenda Tabora kuhani msiba. Abdallah Kibaden "King" ndiye aliyekabidhi ubani.
4. Nicco Njohole wa SIMBA aliliaibisha Taifa baada ya kupigwa umeme 1979 Nchumbiji kwa kukojoa uwanjani!
5. Mwaka 1987, Kiongozi 1 wa SIMBA alienda kwa Idd Pazi, kipa wa PILSNER wakakubaliana ampe Tshs 50,000 ili afungishe kwenye mechi ya kwanza. SIMBA ilikiwa inachungulia kaburi. Kiongozi huyo akampa Tshs 25,000/= tu, hakumalizia. SIMBA ikatandikwa 2-0.
6. Kwenye mechi ya pili, PAZI aliitwa nyumbani kwa Mwenyekiti Yusuph Hazzali Ilala. Akamkuta na kapteni Malota Soma. Wakamsihi sana afungishe kwani ye ni "mwana" ila hawakumpa fedha. PAZI akamsimulia JAMHURI KIHWELU ambaye alikataa ujinga huo. Dakika ya 10 tu, Zicco wa Kilosa akafunga. Kabla ya HT, PAZI akaachia mpira uingie wavuni lakini JAMHURI akaenda kuuokolea kwenye chaki! Kipindi cha pili PAZI akaachia goli, SIMBA iliyopachikwa jina "Guluguja" kwa kufungwafungwa, ikaambulia sare !
7. Mwaka 1987, SIMBA ilikuwa inashika mkia. Kwenye mechi ya mwisho dhidi ya Bingwa mtetezi Tukuyu stars, ilitakiwa kutoa sare 5-5 ili inusurike kushuka daraja. Na kweli ikala njama na Tukuyu stars zikatoka sare 5-5. FAT ikaishia tu kuzionya!
8. SIMBA imenusurika kushuka daraja mara 3 mfululizo (1987, 1988 & 1989).
9. Novemba 30, 1993, SIMBA ililazimika kutia kiberiti makontena 5 ya Khanga zilizoandikwa _"SIMBA BINGWA CAF 1993"_ baada ya kufilimbwa 2-0 na Stela Abidjan.
10. Manazi wa SIMBA waliandika rekodi ya kung'oa viti Oktoba 1, 2016.
11. SIMBA ililiaibisha Taifa kwa uchawi kwa kuwasha moto uwanjani mbungi dhidi ya Orlando Pirates Aprili 25, 2022 na Caf kuilima faini $ 10,000
12. Manazi wa SIMBA waliweka rekodi ya kulipiga mawe basi lao toka Ntwara hadi Dsm kote lilikopita baada ya kuchalazwa 2-1 na Azam Mei 8, 2023 uwanja wa Nangwanda Sijaona.
13. SIMBA ina tabia za Mbwa koko- Mbwa koko hubweka nyumbani tu. SIMBA haijawahi kutwaa kombe nje ya nchi. SIMBA hutia aibu sana mechi za kimataifa nje ya nchi, inategemea Bongo _"Kwa Mkapa Hatoki Mtu"_!
14. Manazi wa SIMBA walifanya tukio la hovyo kuwahi kutokea katika Historia ya mpira wa miguu. Hassan Dalali aliwahi kusimulia kwa uchungu :
_"Simba tulipofungwa na Azzam 2-1, mashabiki wetu walifanya tukio la hovyo kupita kiasi. Walienda Kariakoo wakanunua mapera wakala. Zikaja coaster 3 nyumbani kwangu. Wakaanza kupiga mawe nyumba yangu. Haraka nikaificha familia yangu. Wakaingia wakaanza kunya sebuleni na kwingine. Nikawauliza wamemaliza? Nikawaambia waende uani kuna jaba la maji wakajisafishe. Walinisikitisha sana kwani walienda hadi chumba maalum nikako swalia wakanya. Nilihuzunika sana. Siku ya pili nikaenda klabuni nikajiuzulu"