• Ushirikiano wa RDC – Monaco unakabiliwa na changamoto?

    Ushirikiano kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na klabu ya AS Monaco unaweza kuwa kwenye hatari, ikizingatiwa taarifa zilizotolewa na Gazeti la L’Équipe la Nchini Ufaransa.

    Taarifa hizo zinaonyesha kwamba malalamiko ya "kuficha fedha", "kufurushwa fedha za umma" (Wizi) na "ufisadi" yamewasilishwa katika Tume ya Ufilisi wa Kifedha ya Taifa (PNF) mnamo Septemba 2025.

    Malalamiko haya yanahusu mkataba uliosainiwa kati ya Wizara ya Michezo ya RDC na AS Monaco mwezi Juni mwaka jana.

    Baada ya miezi kadhaa ya uchambuzi, PNF imetuma ripoti rasmi kwa mamlaka za Monaco. Hivyo, sasa kesi hiyo ipo mikononi mwa Mahakama ya Dola la Nchi ya Monaco.

    Hali hii inachukua sura mpya katika uhusiano wa michezo na uwekezaji kati ya RDC na Monaco, huku mashabiki na wanasiasa wakilenga kuona matokeo ya kesi hii.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Ushirikiano wa RDC – Monaco unakabiliwa na changamoto? Ushirikiano kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na klabu ya AS Monaco unaweza kuwa kwenye hatari, ikizingatiwa taarifa zilizotolewa na Gazeti la L’Équipe la Nchini Ufaransa. Taarifa hizo zinaonyesha kwamba malalamiko ya "kuficha fedha", "kufurushwa fedha za umma" (Wizi) na "ufisadi" yamewasilishwa katika Tume ya Ufilisi wa Kifedha ya Taifa (PNF) mnamo Septemba 2025. Malalamiko haya yanahusu mkataba uliosainiwa kati ya Wizara ya Michezo ya RDC na AS Monaco mwezi Juni mwaka jana. Baada ya miezi kadhaa ya uchambuzi, PNF imetuma ripoti rasmi kwa mamlaka za Monaco. Hivyo, sasa kesi hiyo ipo mikononi mwa Mahakama ya Dola la Nchi ya Monaco. Hali hii inachukua sura mpya katika uhusiano wa michezo na uwekezaji kati ya RDC na Monaco, huku mashabiki na wanasiasa wakilenga kuona matokeo ya kesi hii. Toa maoni yako #Habari
    0 Comments 0 Shares 97 Views
  • Umoja wa Ulaya wafadhili euro milioni 81 kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Umoja wa Ulaya (EU) umethibitisha kutoa ufadhili wa Euro milioni 81 kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (RDC), kwa ajili ya kusaidia mpango wa msaada wa kibinadamu katika maeneo ya mashariki ambako mizozo inazidi kuathiri Wananchi.

    Akizungumza kuhusu hatua hii, Msemaji wa Umoja wa Ulaya amesema, “Hii ni hatua yetu ya dhati ya kuhakikisha kwamba jamii zilizo hatarini zinapata msaada wa dharura na huduma za msingi zinazohitajika, hususan kwa wakimbizi na watu waliokumbwa na mizozo.”

    Aidha, Umoja wa Ulaya umesisitiza umuhimu wa kushirikiana na mamlaka za RDC pamoja na mashirika ya misaada ya kibinadamu ili kuhakikisha fedha hizi zinatumika kwa ufanisi na kufikia jamii zinazohitaji zaidi.

    Msemaji huyo aliongeza, “Tutaendelea kushirikiana na washirika wetu wa ndani na kimataifa kuhakikisha kwamba msaada unawafikia walengwa haraka na kwa uwazi, ili kupunguza madhara yanayosababishwa na mapigano yanayoendelea mashariki mwa nchi.”

    Hii ni sehemu ya jitihada kubwa za kimataifa zinazolenga kupunguza mateso ya kibinadamu na kuboresha hali ya maisha kwa familia zinazokabiliwa na mizozo, haswa katika kanda zenye migogoro ya muda mrefu.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Umoja wa Ulaya wafadhili euro milioni 81 kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Umoja wa Ulaya (EU) umethibitisha kutoa ufadhili wa Euro milioni 81 kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (RDC), kwa ajili ya kusaidia mpango wa msaada wa kibinadamu katika maeneo ya mashariki ambako mizozo inazidi kuathiri Wananchi. Akizungumza kuhusu hatua hii, Msemaji wa Umoja wa Ulaya amesema, “Hii ni hatua yetu ya dhati ya kuhakikisha kwamba jamii zilizo hatarini zinapata msaada wa dharura na huduma za msingi zinazohitajika, hususan kwa wakimbizi na watu waliokumbwa na mizozo.” Aidha, Umoja wa Ulaya umesisitiza umuhimu wa kushirikiana na mamlaka za RDC pamoja na mashirika ya misaada ya kibinadamu ili kuhakikisha fedha hizi zinatumika kwa ufanisi na kufikia jamii zinazohitaji zaidi. Msemaji huyo aliongeza, “Tutaendelea kushirikiana na washirika wetu wa ndani na kimataifa kuhakikisha kwamba msaada unawafikia walengwa haraka na kwa uwazi, ili kupunguza madhara yanayosababishwa na mapigano yanayoendelea mashariki mwa nchi.” Hii ni sehemu ya jitihada kubwa za kimataifa zinazolenga kupunguza mateso ya kibinadamu na kuboresha hali ya maisha kwa familia zinazokabiliwa na mizozo, haswa katika kanda zenye migogoro ya muda mrefu. Toa maoni yako #Habari
    0 Comments 0 Shares 166 Views
  • “Wanajifariji kwa kusema kwamba tumetuma meli kubwa ya kivita kuelekea Iran. Ni kweli, meli hiyo ni silaha hatari lakini kilicho hatari zaidi kuliko meli ya kivita ni silaha hadimu inayoweza kuizamisha na kuipeleka chini kabisa ya bahari”

    - Ayatollah Sayyed Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Taifa la Iran.

    Toa maoni yako
    #Habari
    “Wanajifariji kwa kusema kwamba tumetuma meli kubwa ya kivita kuelekea Iran. Ni kweli, meli hiyo ni silaha hatari lakini kilicho hatari zaidi kuliko meli ya kivita ni silaha hadimu inayoweza kuizamisha na kuipeleka chini kabisa ya bahari” - Ayatollah Sayyed Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Taifa la Iran. Toa maoni yako #Habari
    0 Comments 0 Shares 158 Views
  • Katibu Mkuu wa UN asema Afrika lazima iwe na uwawakilishi kamili kwenye meza ya Dunia.

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amesisitiza umuhimu wa bara la Afrika katika maamuzi ya kimataifa, akisisitiza kuwa bara hilo linastahili uwakilishi wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

    Akihutubia kwenye Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) Mjini Addis Ababa, Guterres alisema: “Afrika lazima iwe mezani.”

    Kauli hiyo inatokana na hali ya dunia iliyogawanyika na migogoro mingi, ambapo Guterres alibainisha kuwa Umoja wa Afrika ni mhimili muhimu wa ushirikiano wa kimataifa. Alisisitiza kuwa ukosefu wa uwakilishi wa kudumu wa Afrika katika Baraza la Usalama hauna msingi wa haki wala mantiki: “Huu ni mwaka 2026, si 1946.”

    Aidha, Katibu Mkuu wa UN alitoa wito wa amani na utulivu katika maeneo yaliyo hatarini barani Afrika, ikiwemo Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Pia alisisitiza umuhimu wa mageuzi ya kifedha ya kimataifa na kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, akisema: “Afrika itaendelea kuwa kipaumbele cha Umoja wa Mataifa.”

    Kauli hizi zinaonesha msukumo wa Umoja wa Mataifa kushirikisha bara la Afrika kikamilifu katika maamuzi makuu ya kimataifa, huku likipatiwa nafasi sawa na mataifa mengine katika masuala ya usalama, uchumi, na mazingira.

    Hii ni sehemu ya jitihada zinazoongeza msukumo wa mabadiliko ya kimfumo, na kutoa ishara kwamba dunia inatambua Afrika kama mchezaji muhimu wa kimataifa.

    Toa maoni yako
    #Habari
    Katibu Mkuu wa UN asema Afrika lazima iwe na uwawakilishi kamili kwenye meza ya Dunia. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amesisitiza umuhimu wa bara la Afrika katika maamuzi ya kimataifa, akisisitiza kuwa bara hilo linastahili uwakilishi wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Akihutubia kwenye Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) Mjini Addis Ababa, Guterres alisema: “Afrika lazima iwe mezani.” Kauli hiyo inatokana na hali ya dunia iliyogawanyika na migogoro mingi, ambapo Guterres alibainisha kuwa Umoja wa Afrika ni mhimili muhimu wa ushirikiano wa kimataifa. Alisisitiza kuwa ukosefu wa uwakilishi wa kudumu wa Afrika katika Baraza la Usalama hauna msingi wa haki wala mantiki: “Huu ni mwaka 2026, si 1946.” Aidha, Katibu Mkuu wa UN alitoa wito wa amani na utulivu katika maeneo yaliyo hatarini barani Afrika, ikiwemo Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Pia alisisitiza umuhimu wa mageuzi ya kifedha ya kimataifa na kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, akisema: “Afrika itaendelea kuwa kipaumbele cha Umoja wa Mataifa.” Kauli hizi zinaonesha msukumo wa Umoja wa Mataifa kushirikisha bara la Afrika kikamilifu katika maamuzi makuu ya kimataifa, huku likipatiwa nafasi sawa na mataifa mengine katika masuala ya usalama, uchumi, na mazingira. Hii ni sehemu ya jitihada zinazoongeza msukumo wa mabadiliko ya kimfumo, na kutoa ishara kwamba dunia inatambua Afrika kama mchezaji muhimu wa kimataifa. Toa maoni yako #Habari
    0 Comments 0 Shares 58 Views
  • Mwigizaji wa Nollywood Maurice Sam, mtandaoni yachafukwa baada ya shambulio la risasi.

    Mwigizaji wa filamu za Nollywood, Nigeria, Maurice Sam, amesambaa kwenye vichwa vya habari mtandaoni baada ya taarifa zinazodai kuwa alishambuliwa kwa risasi jana Februari 13, 2026 akiwa kwenye seti ya filamu yake mpya. Tukio hili lilianza kuchipuka mtandaoni baada ya Mwanaharakati maarufu wa mitandao, Very Dark Man, kuposti picha na madai ya kwamba Mwigizaji huyo alikuwa amejeruhiwa vibaya na alikuwa akifikiria kuondoka Nigeria ili kulinda usalama wake.

    Ripoti kutoka tovuti ya Latest Nigerian News inaeleza kuwa baadhi ya picha zilizosambazwa mtandaoni zinaonyesha Gari lililoharibiwa na alama za risasi, jambo lililoashiria hatari kubwa aliyokabiliana nayo Mwigizaji huyo. Mada hii iliibua mjadala mkali miongoni mwa mashabiki, wadau wa filamu, na Watumiaji wa mitandao ya kijamii, huku wengi wakihoji ni nini hasa kilichosababisha tukio hili na kuzingatia juhudi za Maurice Sam kujijenga kibiashara na kupata nafasi kubwa ndani ya tasnia ya Nollywood.

    Mchambuzi mmoja wa tasnia ya filamu alisema: “Ni jambo linalotia wasiwasi kuona msanii chipukizi akikabiliwa na tukio la aina hii. Inaleta mjadala juu ya usalama wa wasanii na hali ya kazi kwenye tasnia ya filamu nchini Nigeria.”

    Hata hivyo, ripoti hizo pia zinaonyesha wazi kuwa hakuna uthibitisho rasmi kutoka kwa Mwigizaji, Polisi, au vyombo vya habari vikuu. Taarifa hizi zinazozagaa zinatokana zaidi na mitandao ya kijamii, na bado hazina uthibitisho wa moja kwa moja wa jeraha lolote lililopatikana.

    Kwa sasa, Maurice Sam yupo salama, ingawa duru zinaeleza kuwa tukio hili limemuathiri kisaikolojia kiasi cha kuanza kufikiria kuachana na uigizaji na kuwekeza katika shughuli nyingine za kibiashara. Tukio hili limeibua mjadala wa kimataifa kuhusu hatari zinazoweza kutokea kwa Wasanii chipukizi, huku wadau wa tasnia wakihimiza tahadhari na uangalizi zaidi kwenye seti za filamu.

    Toa maoni yako
    #Filamu
    #Habari
    Mwigizaji wa Nollywood Maurice Sam, mtandaoni yachafukwa baada ya shambulio la risasi. Mwigizaji wa filamu za Nollywood, Nigeria, Maurice Sam, amesambaa kwenye vichwa vya habari mtandaoni baada ya taarifa zinazodai kuwa alishambuliwa kwa risasi jana Februari 13, 2026 akiwa kwenye seti ya filamu yake mpya. Tukio hili lilianza kuchipuka mtandaoni baada ya Mwanaharakati maarufu wa mitandao, Very Dark Man, kuposti picha na madai ya kwamba Mwigizaji huyo alikuwa amejeruhiwa vibaya na alikuwa akifikiria kuondoka Nigeria ili kulinda usalama wake. Ripoti kutoka tovuti ya Latest Nigerian News inaeleza kuwa baadhi ya picha zilizosambazwa mtandaoni zinaonyesha Gari lililoharibiwa na alama za risasi, jambo lililoashiria hatari kubwa aliyokabiliana nayo Mwigizaji huyo. Mada hii iliibua mjadala mkali miongoni mwa mashabiki, wadau wa filamu, na Watumiaji wa mitandao ya kijamii, huku wengi wakihoji ni nini hasa kilichosababisha tukio hili na kuzingatia juhudi za Maurice Sam kujijenga kibiashara na kupata nafasi kubwa ndani ya tasnia ya Nollywood. Mchambuzi mmoja wa tasnia ya filamu alisema: “Ni jambo linalotia wasiwasi kuona msanii chipukizi akikabiliwa na tukio la aina hii. Inaleta mjadala juu ya usalama wa wasanii na hali ya kazi kwenye tasnia ya filamu nchini Nigeria.” Hata hivyo, ripoti hizo pia zinaonyesha wazi kuwa hakuna uthibitisho rasmi kutoka kwa Mwigizaji, Polisi, au vyombo vya habari vikuu. Taarifa hizi zinazozagaa zinatokana zaidi na mitandao ya kijamii, na bado hazina uthibitisho wa moja kwa moja wa jeraha lolote lililopatikana. Kwa sasa, Maurice Sam yupo salama, ingawa duru zinaeleza kuwa tukio hili limemuathiri kisaikolojia kiasi cha kuanza kufikiria kuachana na uigizaji na kuwekeza katika shughuli nyingine za kibiashara. Tukio hili limeibua mjadala wa kimataifa kuhusu hatari zinazoweza kutokea kwa Wasanii chipukizi, huku wadau wa tasnia wakihimiza tahadhari na uangalizi zaidi kwenye seti za filamu. Toa maoni yako #Filamu #Habari
    0 Comments 0 Shares 246 Views
  • RDC: Majeshi ya Congo na Uganda yatathmini operesheni SHUJAA Beni.

    Luteni Jenerali Ychalingonza Nduru Jacques ameongoza kikao cha tathmini ya operesheni za pamoja za kijeshi kati ya Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF) katika Mji wa Beni, Mkoa wa Nord-Kivu.

    Kikao hicho kilifanyika siku ya Jana Jumanne na kuhudhuriwa pia na Luteni Jenerali Kayanja Muhanga kutoka Uganda pamoja na Makamanda wengine waandamizi wa majeshi ya mataifa hayo mawili. Mkutano huo ni mwendelezo wa kikao kilichofanyika Mjini Kinshasa mwezi Juni 2025, kilicholenga kutathmini operesheni ya kuwasaka Wapiganaji wa kundi la ADF-MTN-ISCARP na kurekebisha mikakati ya kukabiliana na vitisho vipya vya kiusalama.

    Operesheni SHUJAA ni ushirikiano wa kijeshi kati ya Congo na Uganda unaolenga kutokomeza makundi ya Waasi na magaidi yanayohatarisha usalama mashariki mwa Congo, hususan katika maeneo ya Beni, Lubero na Ituri.

    Katika tathmini hiyo, Viongozi hao wa kijeshi wamepongeza mafanikio ya kimkakati yaliyopatikana katika operesheni hizo, wakieleza kuwa mashambulizi kadhaa ya makundi yenye silaha yamezuiwa na miundombinu yao kuvurugwa. Hata hivyo, wamebainisha kuwa bado kuna mashambulizi yanayoendelea katika baadhi ya maeneo, jambo linaloashiria umuhimu wa kuimarisha zaidi operesheni za usalama.

    Maeneo ya Lubero, Beni na Ituri yamekuwa yakikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa makundi yenye silaha, hasa ADF, hali inayosababisha vifo vya Raia na maelfu ya wananchi kulazimika kuyahama makazi yao.

    Viongozi hao wawili wa kijeshi wameisisitiza haja ya kuongeza nguvu katika operesheni za pamoja, kuimarisha uratibu wa kijasusi na kuendelea na mikakati madhubuti ili kurejesha amani ya kudumu katika ukanda huo.

    Tathmini hiyo inatajwa kuwa hatua muhimu katika kuendeleza ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili, huku ikionyesha dhamira ya pamoja ya kukabiliana na vitisho vya usalama vinavyoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Toa maoni yako

    #Habari
    RDC: Majeshi ya Congo na Uganda yatathmini operesheni SHUJAA Beni. Luteni Jenerali Ychalingonza Nduru Jacques ameongoza kikao cha tathmini ya operesheni za pamoja za kijeshi kati ya Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF) katika Mji wa Beni, Mkoa wa Nord-Kivu. Kikao hicho kilifanyika siku ya Jana Jumanne na kuhudhuriwa pia na Luteni Jenerali Kayanja Muhanga kutoka Uganda pamoja na Makamanda wengine waandamizi wa majeshi ya mataifa hayo mawili. Mkutano huo ni mwendelezo wa kikao kilichofanyika Mjini Kinshasa mwezi Juni 2025, kilicholenga kutathmini operesheni ya kuwasaka Wapiganaji wa kundi la ADF-MTN-ISCARP na kurekebisha mikakati ya kukabiliana na vitisho vipya vya kiusalama. Operesheni SHUJAA ni ushirikiano wa kijeshi kati ya Congo na Uganda unaolenga kutokomeza makundi ya Waasi na magaidi yanayohatarisha usalama mashariki mwa Congo, hususan katika maeneo ya Beni, Lubero na Ituri. Katika tathmini hiyo, Viongozi hao wa kijeshi wamepongeza mafanikio ya kimkakati yaliyopatikana katika operesheni hizo, wakieleza kuwa mashambulizi kadhaa ya makundi yenye silaha yamezuiwa na miundombinu yao kuvurugwa. Hata hivyo, wamebainisha kuwa bado kuna mashambulizi yanayoendelea katika baadhi ya maeneo, jambo linaloashiria umuhimu wa kuimarisha zaidi operesheni za usalama. Maeneo ya Lubero, Beni na Ituri yamekuwa yakikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa makundi yenye silaha, hasa ADF, hali inayosababisha vifo vya Raia na maelfu ya wananchi kulazimika kuyahama makazi yao. Viongozi hao wawili wa kijeshi wameisisitiza haja ya kuongeza nguvu katika operesheni za pamoja, kuimarisha uratibu wa kijasusi na kuendelea na mikakati madhubuti ili kurejesha amani ya kudumu katika ukanda huo. Tathmini hiyo inatajwa kuwa hatua muhimu katika kuendeleza ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili, huku ikionyesha dhamira ya pamoja ya kukabiliana na vitisho vya usalama vinavyoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Toa maoni yako #Habari
    0 Comments 0 Shares 209 Views
  • Trump aonya kuhusu makubaliano ya biashara kati ya China na Canada.

    Rais wa Marekani, Donald Trump, ametoa kauli kali akizungumzia uwezekano wa makubaliano ya kibiashara kati ya China na Canada, akionya kuwa hatua hiyo inaweza kuiweka Canada katika hatari kubwa ya kiuchumi.

    Akizungumza katika muktadha wa mijadala ya biashara za kimataifa, Trump alidai kuwa China ina uwezo mkubwa wa kiuchumi na kimkakati ambao unaweza kuathiri vibaya mataifa yanayoingia nayo mikataba bila tahadhari ya kutosha. Kwa mujibu wa Trump, Canada inaweza kujikuta ikidhoofishwa endapo itafanya makubaliano ya karibu na taifa hilo la Asia.

    “Ninasema wazi kabisa, China itaimeza Canada ikiwa watafanya makubaliano kati yao,” alisema Trump.

    Kauli hiyo imeibua mjadala mpana kuhusu uhusiano wa kibiashara kati ya mataifa makubwa na yale ya kati, hasa ikizingatiwa nafasi ya China kama moja ya nguvu kubwa za uchumi duniani. Wachambuzi wa siasa na uchumi wanasema matamshi ya Trump yanaakisi msimamo wake wa muda mrefu wa tahadhari na hata upinzani dhidi ya ushawishi wa China katika biashara za kimataifa.

    Hadi sasa, serikali ya Canada haijatoa tamko rasmi kujibu kauli hiyo, huku China pia ikikaa kimya kuhusu madai hayo. Hata hivyo, mjadala unaendelea kuonyesha jinsi masuala ya biashara na diplomasia yanavyoendelea kuwa nyeti katika uhusiano wa kimataifa, hasa yanapohusisha mataifa yenye maslahi makubwa ya kiuchumi.

    Toa maoni yako
    #Habari
    #Trump #China #Canada #Biashara #UhusianoYaKimataifa
    Trump aonya kuhusu makubaliano ya biashara kati ya China na Canada. Rais wa Marekani, Donald Trump, ametoa kauli kali akizungumzia uwezekano wa makubaliano ya kibiashara kati ya China na Canada, akionya kuwa hatua hiyo inaweza kuiweka Canada katika hatari kubwa ya kiuchumi. Akizungumza katika muktadha wa mijadala ya biashara za kimataifa, Trump alidai kuwa China ina uwezo mkubwa wa kiuchumi na kimkakati ambao unaweza kuathiri vibaya mataifa yanayoingia nayo mikataba bila tahadhari ya kutosha. Kwa mujibu wa Trump, Canada inaweza kujikuta ikidhoofishwa endapo itafanya makubaliano ya karibu na taifa hilo la Asia. “Ninasema wazi kabisa, China itaimeza Canada ikiwa watafanya makubaliano kati yao,” alisema Trump. Kauli hiyo imeibua mjadala mpana kuhusu uhusiano wa kibiashara kati ya mataifa makubwa na yale ya kati, hasa ikizingatiwa nafasi ya China kama moja ya nguvu kubwa za uchumi duniani. Wachambuzi wa siasa na uchumi wanasema matamshi ya Trump yanaakisi msimamo wake wa muda mrefu wa tahadhari na hata upinzani dhidi ya ushawishi wa China katika biashara za kimataifa. Hadi sasa, serikali ya Canada haijatoa tamko rasmi kujibu kauli hiyo, huku China pia ikikaa kimya kuhusu madai hayo. Hata hivyo, mjadala unaendelea kuonyesha jinsi masuala ya biashara na diplomasia yanavyoendelea kuwa nyeti katika uhusiano wa kimataifa, hasa yanapohusisha mataifa yenye maslahi makubwa ya kiuchumi. Toa maoni yako #Habari #Trump #China #Canada #Biashara #UhusianoYaKimataifa
    0 Comments 1 Shares 266 Views
  • WAKAZI WA PAKADJUMA WAKATAA KUONDOKA ENEO LILILOBOMOLEWA, WAKABILIA POLISI LIMETE.

    Hali ya wasiwasi na taharuki imetanda katika eneo la Pakadjuma, Wilaya ya Limete, Jijini Kinshasa, DR Congo, baada ya Wakazi wa eneo hilo kukataa kuondoka katika sehemu iliyobomolewa na mamlaka za Jiji. Hatua hiyo imesababisha makabiliano kati ya Wakazi na vikosi vya polisi vilivyotumwa kutekeleza agizo la kusafisha eneo hilo.

    Kwa mujibu wa mamlaka za Jiji la Kinshasa, Wakazi wa Pakadjuma waliondolewa katika eneo hilo kwa sababu kadhaa, ikiwemo madai kuwa makazi hayo yalijengwa bila kufuata mipango rasmi ya Mji, hali inayoyafanya kutambuliwa kama makazi yasiyo halali. Vilevile, eneo hilo limekuwa likitajwa kuwa hatarishi kiafya kutokana na uchafuzi wa mazingira, taka na mafuriko ya mara kwa mara, hali inayodaiwa kuhatarisha maisha ya Wakazi.

    Hatua ya ubomoaji pia inaelezwa kuwa ni sehemu ya mpango wa upangaji na usafi wa Jiji la Kinshasa, unaolenga kuondoa makazi yaliyojengwa kinyume cha sheria, kurejesha maeneo ya hifadhi na kuboresha miundombinu ya jiji pamoja na usalama wa Wakazi.

    Hata hivyo, Wakazi wa Pakadjuma wamepinga vikali uamuzi huo, wakisema hawajapewa makazi mbadala wala fidia ya kuridhisha. Wengi wao wameendelea kubaki katika eneo hilo licha ya ubomoaji, wakidai hawana sehemu nyingine ya kwenda.

    Mmoja wa wakazi hao amenukuliwa akisema, “Hatuwezi kuondoka hapa bila kupata uhakika wa mahali pa kuishi. Nyumba zetu zimebomolewa na hatujapewa suluhisho lolote.”

    Mvutano uliongezeka pale Polisi walipojaribu kuwasukuma Wakazi kuondoka katika eneo hilo, hali iliyopelekea makabiliano ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili. Mashuhuda wanasema hali ilikuwa ya vurugu kwa nyakati tofauti huku Wakazi wakionyesha hasira zao dhidi ya hatua za mamlaka.

    Kwa upande wake, Afisa mmoja wa usalama aliyekuwepo eneo la tukio amesema, “Tupo hapa kutekeleza maagizo ya kisheria na kuhakikisha usalama wa Raia wote. Tunawahimiza Wakazi kushirikiana na mamlaka ili kuepuka madhara.”

    Hadi sasa, hali bado ni tete katika eneo la Pakadjuma, huku Wakazi wakiendelea kushikilia msimamo wao na mamlaka za Jiji la Kinshasa zikiwa bado hazijatoa tamko rasmi kuhusu mpango wa makazi mbadala au fidia kwa Waathirika wa zoezi hilo.

    Toa maoni yako
    #Habari
    WAKAZI WA PAKADJUMA WAKATAA KUONDOKA ENEO LILILOBOMOLEWA, WAKABILIA POLISI LIMETE. Hali ya wasiwasi na taharuki imetanda katika eneo la Pakadjuma, Wilaya ya Limete, Jijini Kinshasa, DR Congo, baada ya Wakazi wa eneo hilo kukataa kuondoka katika sehemu iliyobomolewa na mamlaka za Jiji. Hatua hiyo imesababisha makabiliano kati ya Wakazi na vikosi vya polisi vilivyotumwa kutekeleza agizo la kusafisha eneo hilo. Kwa mujibu wa mamlaka za Jiji la Kinshasa, Wakazi wa Pakadjuma waliondolewa katika eneo hilo kwa sababu kadhaa, ikiwemo madai kuwa makazi hayo yalijengwa bila kufuata mipango rasmi ya Mji, hali inayoyafanya kutambuliwa kama makazi yasiyo halali. Vilevile, eneo hilo limekuwa likitajwa kuwa hatarishi kiafya kutokana na uchafuzi wa mazingira, taka na mafuriko ya mara kwa mara, hali inayodaiwa kuhatarisha maisha ya Wakazi. Hatua ya ubomoaji pia inaelezwa kuwa ni sehemu ya mpango wa upangaji na usafi wa Jiji la Kinshasa, unaolenga kuondoa makazi yaliyojengwa kinyume cha sheria, kurejesha maeneo ya hifadhi na kuboresha miundombinu ya jiji pamoja na usalama wa Wakazi. Hata hivyo, Wakazi wa Pakadjuma wamepinga vikali uamuzi huo, wakisema hawajapewa makazi mbadala wala fidia ya kuridhisha. Wengi wao wameendelea kubaki katika eneo hilo licha ya ubomoaji, wakidai hawana sehemu nyingine ya kwenda. Mmoja wa wakazi hao amenukuliwa akisema, “Hatuwezi kuondoka hapa bila kupata uhakika wa mahali pa kuishi. Nyumba zetu zimebomolewa na hatujapewa suluhisho lolote.” Mvutano uliongezeka pale Polisi walipojaribu kuwasukuma Wakazi kuondoka katika eneo hilo, hali iliyopelekea makabiliano ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili. Mashuhuda wanasema hali ilikuwa ya vurugu kwa nyakati tofauti huku Wakazi wakionyesha hasira zao dhidi ya hatua za mamlaka. Kwa upande wake, Afisa mmoja wa usalama aliyekuwepo eneo la tukio amesema, “Tupo hapa kutekeleza maagizo ya kisheria na kuhakikisha usalama wa Raia wote. Tunawahimiza Wakazi kushirikiana na mamlaka ili kuepuka madhara.” Hadi sasa, hali bado ni tete katika eneo la Pakadjuma, huku Wakazi wakiendelea kushikilia msimamo wao na mamlaka za Jiji la Kinshasa zikiwa bado hazijatoa tamko rasmi kuhusu mpango wa makazi mbadala au fidia kwa Waathirika wa zoezi hilo. Toa maoni yako #Habari
    0 Comments 0 Shares 228 Views
  • Ubalozi wa RDC Burundi wakanusha taarifa za orodha ya Raia kurudi kwa hiari Uvira.

    Bujumbura, Burundi, Ubalozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (RDC) nchini Burundi umekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa umefungua orodha ya usajili kwa Raia wa Congo wanaotaka kurejea kwa hiari katika Mji wa Uvira, Mkoani Sud-Kivu.

    Taarifa hizo, zilizosambazwa kwa kasi kupitia mitandao ya kijamii hususan makundi ya WhatsApp, zilisababisha idadi ya Raia wa Congo kujitokeza katika majengo ya ubalozi wakiamini kuwa kuna mchakato rasmi wa kurejea unaoendelea.

    Akizungumza, Balozi wa RDC nchini Burundi, Willy Mulamba Mabika, amesema ubalozi hauna mamlaka ya kuandaa au kuruhusu kurejea kwa hiari kwa Wakimbizi.

    “Ubalozi hauna haki ya kufungua mpaka wala kuruhusu kurejea kwa wakimbizi nchini mwao. Jukumu hili ni la Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (HCR), Serikali ya Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kufanyika tathmini ya awali ya hali ya usalama,” amenukuliwa akisema Balozi huyo.

    Kwa mujibu wa taratibu za kimataifa, kurejea kwa hiari kwa Wakimbizi huratibiwa na HCR, hufanyika kwa makubaliano kati ya nchi mwenyeji na nchi ya asili, na hutegemea tathmini ya kiusalama inayohakikisha kurejea kwa usalama, heshima na kwa hiari.

    Hakuna tamko lolote kutoka kwa HCR, Serikali ya Burundi au Serikali ya RDC linalothibitisha kuwepo kwa mpango wa sasa wa kurejesha Wakimbizi wa Congo kutoka Burundi kwenda Uvira. Wachambuzi huru wanasema kujitokeza kwa Raia wa Congo mbele ya ubalozi kunaweza kuakisi hamu ya kurejea nyumbani, inayochochewa na matarajio ya kuimarika kwa hali ya usalama na juhudi zinazoendelea za kurejesha mamlaka ya dola katika eneo la Uvira.

    Ubalozi umehimiza umma kuwa makini dhidi ya taarifa zisizothibitishwa na kuzingatia mawasiliano rasmi pekee kutoka HCR na mamlaka husika.

    “Upotoshaji wa taarifa katika mazingira nyeti ya kibinadamu na kiusalama unaweza kuwaweka watu hatarini bila sababu,” balozi ameongeza.

    Hakuna orodha rasmi iliyofunguliwa katika Ubalozi wa RDC nchini Burundi kwa ajili ya kurejea kwa hiari kwa Raia wa Congo kwenda Uvira; madai hayo hayana msingi na yamekanushwa rasmi.

    Ubalozi wa RDC Burundi wakanusha taarifa za orodha ya Raia kurudi kwa hiari Uvira. Bujumbura, Burundi, Ubalozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (RDC) nchini Burundi umekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa umefungua orodha ya usajili kwa Raia wa Congo wanaotaka kurejea kwa hiari katika Mji wa Uvira, Mkoani Sud-Kivu. Taarifa hizo, zilizosambazwa kwa kasi kupitia mitandao ya kijamii hususan makundi ya WhatsApp, zilisababisha idadi ya Raia wa Congo kujitokeza katika majengo ya ubalozi wakiamini kuwa kuna mchakato rasmi wa kurejea unaoendelea. Akizungumza, Balozi wa RDC nchini Burundi, Willy Mulamba Mabika, amesema ubalozi hauna mamlaka ya kuandaa au kuruhusu kurejea kwa hiari kwa Wakimbizi. “Ubalozi hauna haki ya kufungua mpaka wala kuruhusu kurejea kwa wakimbizi nchini mwao. Jukumu hili ni la Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (HCR), Serikali ya Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kufanyika tathmini ya awali ya hali ya usalama,” amenukuliwa akisema Balozi huyo. Kwa mujibu wa taratibu za kimataifa, kurejea kwa hiari kwa Wakimbizi huratibiwa na HCR, hufanyika kwa makubaliano kati ya nchi mwenyeji na nchi ya asili, na hutegemea tathmini ya kiusalama inayohakikisha kurejea kwa usalama, heshima na kwa hiari. Hakuna tamko lolote kutoka kwa HCR, Serikali ya Burundi au Serikali ya RDC linalothibitisha kuwepo kwa mpango wa sasa wa kurejesha Wakimbizi wa Congo kutoka Burundi kwenda Uvira. Wachambuzi huru wanasema kujitokeza kwa Raia wa Congo mbele ya ubalozi kunaweza kuakisi hamu ya kurejea nyumbani, inayochochewa na matarajio ya kuimarika kwa hali ya usalama na juhudi zinazoendelea za kurejesha mamlaka ya dola katika eneo la Uvira. Ubalozi umehimiza umma kuwa makini dhidi ya taarifa zisizothibitishwa na kuzingatia mawasiliano rasmi pekee kutoka HCR na mamlaka husika. “Upotoshaji wa taarifa katika mazingira nyeti ya kibinadamu na kiusalama unaweza kuwaweka watu hatarini bila sababu,” balozi ameongeza. Hakuna orodha rasmi iliyofunguliwa katika Ubalozi wa RDC nchini Burundi kwa ajili ya kurejea kwa hiari kwa Raia wa Congo kwenda Uvira; madai hayo hayana msingi na yamekanushwa rasmi.
    0 Comments 0 Shares 155 Views
  • "Nani alaumiwe? Anaweza kuwa Injinia Hersi Said mwenyewe. Yanga ilifika fainali za Shirikisho miaka ya karibuni. Yanga ilitolewa robo fainali. Yanga ilitolewa pia makundi. Hersi anajua ndoto za Wanayanga. Huwa wananyanyasika kwa mashabiki wa mtani zao kwa kutofanya vizuri katika michuano ya CAF. Ligi ya Mabingwa.
    .
    Wakati huu wakiwa wamesajili wachezaji wazuri huku akiendelea kumiliki wachezaji mafundi kama kina Pacome Zouzoua, Hersi akaitafutia Yanga kocha mwanafunzi.

    Ukitazama wasifu wa Folz, alikuwa amepita katika klabu kadhaa akiwa kama kocha msaidizi. Hersi na wenzake walikuwa wamecheza kamari kwa kumleta Folz. Hajawahi kuwa kocha mkuu wala kutwaa taji lolote muhimu katika maisha yake ya mpira.

    Unawezaje kutimiza ndoto zako ukiwa na kocha wa namna hii. Katika lugha ya mtaani ya Waingereza tunaweza kusema Hersi na wenzake walikuwa wamecheza kamari. ‘Gambling’. Haukuwa muda wa Yanga kucheza bahati nasibu.

    Ulikuwa muda wa wao kuwa na kocha ambaye ana uzoefu na anaweza kuishi katika falsafa zao. Matokeo yake Yanga wamejiweka katika hatari. Wameshafungwa ugenini na wageni wao wanaweza kuja na mbinu za ajabu. Injinia Hersi na wenzake ambao wanaongoza Yanga sasa hivi hawakufikiria kama wanaweza kuwa katika nafasi hii kwa sasa. Wakati wao wanaiwaza nusu fainali au fainali, tayari wapo hatarini kutofika hata makundi.

    - Edo Kumwembe, Mchambuzi.
    "Nani alaumiwe? Anaweza kuwa Injinia Hersi Said mwenyewe. Yanga ilifika fainali za Shirikisho miaka ya karibuni. Yanga ilitolewa robo fainali. Yanga ilitolewa pia makundi. Hersi anajua ndoto za Wanayanga. Huwa wananyanyasika kwa mashabiki wa mtani zao kwa kutofanya vizuri katika michuano ya CAF. Ligi ya Mabingwa. . Wakati huu wakiwa wamesajili wachezaji wazuri huku akiendelea kumiliki wachezaji mafundi kama kina Pacome Zouzoua, Hersi akaitafutia Yanga kocha mwanafunzi. 😀 Ukitazama wasifu wa Folz, alikuwa amepita katika klabu kadhaa akiwa kama kocha msaidizi. Hersi na wenzake walikuwa wamecheza kamari kwa kumleta Folz. Hajawahi kuwa kocha mkuu wala kutwaa taji lolote muhimu katika maisha yake ya mpira. Unawezaje kutimiza ndoto zako ukiwa na kocha wa namna hii. Katika lugha ya mtaani ya Waingereza tunaweza kusema Hersi na wenzake walikuwa wamecheza kamari. ‘Gambling’. Haukuwa muda wa Yanga kucheza bahati nasibu. Ulikuwa muda wa wao kuwa na kocha ambaye ana uzoefu na anaweza kuishi katika falsafa zao. Matokeo yake Yanga wamejiweka katika hatari. Wameshafungwa ugenini na wageni wao wanaweza kuja na mbinu za ajabu. Injinia Hersi na wenzake ambao wanaongoza Yanga sasa hivi hawakufikiria kama wanaweza kuwa katika nafasi hii kwa sasa. Wakati wao wanaiwaza nusu fainali au fainali, tayari wapo hatarini kutofika hata makundi. - Edo Kumwembe, Mchambuzi.
    0 Comments 0 Shares 1K Views
  • TUJIKUMBUSHE KIDOGO

    Sebastian Coates

    Sebastian Coates alisajiliwa na Liverpool kutoka Nacional mwezi Agosti 2011 baada ya kupigiwa kura kama mchezaji bora chipukizi kwenye Copa America ya mwaka huo.

    Akiwa na urefu wa futi 6 na inchi 6, raia huyo wa Uruguay aliwasili akiwa na sifa ya kuwa na uwezo mkubwa wa kucheza mipira ya juu — pia akiwa hatari katika ulinzi na mashambulizi.

    Alicheza mechi 12 katika msimu wake wa kwanza ndani ya Liverpool, tukio la kukumbukwa likiwa bao la kuvutia alilofunga kwa bicycle kick dhidi ya Queens Park Rangers.

    Katika msimu wa 2012–13, msimu wa kwanza wa Brendan Rodgers kama kocha, Coates alicheza tena mechi 12.

    Hata hivyo, matumaini ya kujikita kikosini chini ya kocha wa kipindi hicho, Rodgers yalizimwa na jeraha lililomharibia msimu uliofuata.

    Baadaye alitolewa kwa mkopo kwenda Sunderland msimu wa 2014–15, na hatimaye akajiunga nao kwa mkataba wa kudumu mwezi Julai 2015.
    👀TUJIKUMBUSHE KIDOGO 👀Sebastian Coates 👉Sebastian Coates alisajiliwa na Liverpool kutoka Nacional mwezi Agosti 2011 baada ya kupigiwa kura kama mchezaji bora chipukizi kwenye Copa America ya mwaka huo. 👉Akiwa na urefu wa futi 6 na inchi 6, raia huyo wa Uruguay aliwasili akiwa na sifa ya kuwa na uwezo mkubwa wa kucheza mipira ya juu — pia akiwa hatari katika ulinzi na mashambulizi. 👉Alicheza mechi 12 katika msimu wake wa kwanza ndani ya Liverpool, tukio la kukumbukwa likiwa bao la kuvutia alilofunga kwa bicycle kick dhidi ya Queens Park Rangers. 👉Katika msimu wa 2012–13, msimu wa kwanza wa Brendan Rodgers kama kocha, Coates alicheza tena mechi 12. 👉Hata hivyo, matumaini ya kujikita kikosini chini ya kocha wa kipindi hicho, Rodgers yalizimwa na jeraha lililomharibia msimu uliofuata. 👉Baadaye alitolewa kwa mkopo kwenda Sunderland msimu wa 2014–15, na hatimaye akajiunga nao kwa mkataba wa kudumu mwezi Julai 2015.
    0 Comments 0 Shares 1K Views
  • Slot: Ekitike tayari ana mchango mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji

    Kocha wa Liverpool, Arne Slot, amesema:

    “Tayari amekuwa na mchango mkubwa kwenye sehemu ya ushambuliaji ya mchezo wetu—si tu kwa kufunga mabao, bali pia kwa kushiriki katika ujenzi wa mashambulizi, akiwa mmoja wa wanaoanzisha hatari.”

    “Jibu rahisi kuhusu anachoweza kuboresha ni uwezo wa kuhimili mechi kwa dakika zote. Natarajia afanye mengi zaidi bila mpira kuliko anavyofanya sasa, ingawa tayari anajitahidi.”

    “Hii ni hali ya kawaida kabisa kwa mchezaji anayehama kutoka ligi tofauti na mtindo wa uchezaji tofauti. Frankfurt hawakuwa wakishambulia kwa presha kama tunavyofanya sisi, na sasa akiwa kwenye ligi mpya, kuna mengi ya kukabiliana nayo.”

    “Ili kuzoea kiwango cha nguvu na kasi bila mpira, kuna hatua ndogo anazopaswa kuchukua.”

    #SportsElite
    🔴 Slot: Ekitike tayari ana mchango mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji 👉Kocha wa Liverpool, Arne Slot, amesema: 🗣️ “Tayari amekuwa na mchango mkubwa kwenye sehemu ya ushambuliaji ya mchezo wetu—si tu kwa kufunga mabao, bali pia kwa kushiriki katika ujenzi wa mashambulizi, akiwa mmoja wa wanaoanzisha hatari.” 🗣️ “Jibu rahisi kuhusu anachoweza kuboresha ni uwezo wa kuhimili mechi kwa dakika zote. Natarajia afanye mengi zaidi bila mpira kuliko anavyofanya sasa, ingawa tayari anajitahidi.” 🗣️ “Hii ni hali ya kawaida kabisa kwa mchezaji anayehama kutoka ligi tofauti na mtindo wa uchezaji tofauti. Frankfurt hawakuwa wakishambulia kwa presha kama tunavyofanya sisi, na sasa akiwa kwenye ligi mpya, kuna mengi ya kukabiliana nayo.” 🗣️ “Ili kuzoea kiwango cha nguvu na kasi bila mpira, kuna hatua ndogo anazopaswa kuchukua.” #SportsElite
    0 Comments 0 Shares 1K Views
  • Moja ya mafundi wa Kibrazil Walioyeyuka Ghafla

    Philippe Coutinho na Thiago Alcântara walitazamwa kama almasi za kisasa kwenye soka wenye vipaji vya kipekee, akili ya uwanjani na mguso wa hatari. Waliwahi kung'aa Ulaya kwa kiwango kikubwa, lakini ghafla moto wao ukapoa.

    Coutinho alizimika Barcelona, Thiago akaelemewa na majeraha Liverpool. Sasa, wanabaki kuwa kumbukumbu tamu za vipaji vilivyo kadiliwa makubwa lakini vikatoweka kabla ya wakati.

    Nadhani Coutinho mnalijua kosa lake

    #SportsElite
    🚨🚨Moja ya mafundi wa Kibrazil Walioyeyuka Ghafla ✊🇧🇷 🌀Philippe Coutinho na Thiago Alcântara walitazamwa kama almasi za kisasa kwenye soka wenye vipaji vya kipekee, akili ya uwanjani na mguso wa hatari. Waliwahi kung'aa Ulaya kwa kiwango kikubwa, lakini ghafla moto wao ukapoa. Coutinho alizimika Barcelona, Thiago akaelemewa na majeraha Liverpool. Sasa, wanabaki kuwa kumbukumbu tamu za vipaji vilivyo kadiliwa makubwa lakini vikatoweka kabla ya wakati. 💔✨ Nadhani Coutinho mnalijua kosa lake 😀 #SportsElite
    0 Comments 0 Shares 876 Views
  • Kuna asilimia nyingi za Marc Casado kuondoka Barcelona Kwanini?

    Barca inabanwa na sheria ya matumizi ya pesa nyingi hivyo kuondoka kwa Casado kutawapa Barca angalau ahueni kwenye sajili zake.

    Vilabu vya Como, Wolves na Real Betis vimeonesha nia ya kumsajili.

    Isingekuwa hii sheria Barca wangekuwa na kikosi kimoja hatari sana

    #SportsElite
    🚨🚨Kuna asilimia nyingi za Marc Casado kuondoka Barcelona Kwanini? Barca inabanwa na sheria ya matumizi ya pesa nyingi hivyo kuondoka kwa Casado kutawapa Barca angalau ahueni kwenye sajili zake. Vilabu vya Como, Wolves na Real Betis vimeonesha nia ya kumsajili. ✍️Isingekuwa hii sheria Barca wangekuwa na kikosi kimoja hatari sana🤕 #SportsElite
    0 Comments 0 Shares 803 Views
  • Rushine De Reuck Kitasa kipya cha Simba,jamaa yuko aggressive,muda wote ananusa hatari na kufika kwenye matukio ili kufanya interception,tackling,clearance n.k.

    Rushine De Reuck Ni dominant kwenye mipira ya juu na chini…jamaa akiwa kwenye siku zake ni ngumu kwa mshambuliaji kukabiliana nae.

    Yote kwa yote ukimtazama akiwa na mali mguuni uta-enjoy…jamaa ni ball-playing defender

    Wana simba hapa mmepata beki,jamaa ana uzoefu mkubwa pia ana uwezo wa kucheza maeneo yote ya nyuma

    Super Signing

    #SportsElite
    🚨🚨Rushine De Reuck Kitasa kipya cha Simba,jamaa yuko aggressive,muda wote ananusa hatari na kufika kwenye matukio ili kufanya interception,tackling,clearance n.k. Rushine De Reuck Ni dominant kwenye mipira ya juu na chini…jamaa akiwa kwenye siku zake ni ngumu kwa mshambuliaji kukabiliana nae. Yote kwa yote ukimtazama akiwa na mali mguuni uta-enjoy…jamaa ni ball-playing defender🙌 Wana simba hapa mmepata beki,jamaa ana uzoefu mkubwa pia ana uwezo wa kucheza maeneo yote ya nyuma🖐️ Super Signing🔥 #SportsElite
    0 Comments 0 Shares 821 Views
  • BREAKING: Yanga wamekamilisha usajili wa kiungo namba 10 wa Stade Malien,Raia wa Mali Lassine Kouma (21)

    Simba walikuwa wa kwanza kuzungumza na Lassine Kouma,Kisha kinda huyo akampigia Simu Diarra ili kujua mazingira ya Tanzania,baada ya Diarra kujua kinda huyo hatari anaelekea Simba akamwambia Eng Heris aingilie haraka na mchakato wa kumsaini kuja Yanga ukaanza rasmi na Leo jioni kila kitu kimekamilika….Lassine Kouma Is now green & Yellow


    #SportsElite
    BREAKING: Yanga wamekamilisha usajili wa kiungo namba 10 wa Stade Malien,Raia wa Mali 🇲🇱 Lassine Kouma (21)✅ Simba walikuwa wa kwanza kuzungumza na Lassine Kouma,Kisha kinda huyo akampigia Simu Diarra ili kujua mazingira ya Tanzania,baada ya Diarra kujua kinda huyo hatari anaelekea Simba akamwambia Eng Heris aingilie haraka na mchakato wa kumsaini kuja Yanga ukaanza rasmi na Leo jioni kila kitu kimekamilika….Lassine Kouma Is now green & Yellow #SportsElite
    0 Comments 0 Shares 1K Views
  • CONFIRMED

    Sunderland imekamilisha usajili wa winga hatari wa kifaransa kutokea Sassuolo, Armand Lauriente mwenye umri wa miaka 26.

    Armand Lauriente amejiunga na miamba hiyo ya uingereza kwa ada ya uhamisho ya €20M.

    Sunderland wapo sokoni kuhemea

    #SportsElite
    CONFIRMED ✅ Sunderland imekamilisha usajili wa winga hatari wa kifaransa kutokea Sassuolo, Armand Lauriente mwenye umri wa miaka 26. Armand Lauriente amejiunga na miamba hiyo ya uingereza kwa ada ya uhamisho ya €20M. Sunderland wapo sokoni kuhemea✍️ #SportsElite
    0 Comments 0 Shares 614 Views
  • Manchester united imeweka wazi bei ya winga wake hatari Antony €58M na sio chini ya hapo.

    United wapo tayari kuachana na Antony na vilabu kadhaa vikubwa vimeonesha nia ya kumuhitaji ikiwemo;

    Newcastle
    Brighton
    Bayer Leverkusen
    RB Leipzig.

    Credit [365Scores]

    #SportsElite
    🚨Manchester united imeweka wazi bei ya winga wake hatari Antony €58M na sio chini ya hapo. United wapo tayari kuachana na Antony na vilabu kadhaa vikubwa vimeonesha nia ya kumuhitaji ikiwemo; 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Newcastle 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Brighton 🇩🇪 Bayer Leverkusen 🇩🇪 RB Leipzig. Credit [365Scores] #SportsElite
    0 Comments 0 Shares 675 Views
  • Inter Miami yahatarisha kupoteza €300M endapo Messi ataondoka!

    Klabu ya Inter Miami inaweza kupata pigo kubwa kifedha ikiwa Lionel Messi ataondoka. Tangu ajiunge, wameingiza €265M kupitia tiketi za mechi na €29.7M kupitia Apple TV

    #SportsElite
    🚨 Inter Miami yahatarisha kupoteza €300M endapo Messi ataondoka! 😮📉 Klabu ya Inter Miami inaweza kupata pigo kubwa kifedha ikiwa Lionel Messi 🇦🇷 ataondoka. Tangu ajiunge, wameingiza €265M kupitia tiketi za mechi na €29.7M kupitia Apple TV 📺🔥 #SportsElite
    0 Comments 0 Shares 943 Views
  • #SportsElite

    - Baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu, hatimaye mshambuliaji hatari wa klabu ya Inter Miami pamoja Nahodha wa timu ya Taifa ya Argentina, Leo Messi.. kupitia katika Ukurasa wake wa Instagram (@leomessi) ‘FIFA BOY’ ame-share picha ya Diogo Jota, ikiwa ni ishara ya KUGUSWA moja kwa moja na msiba huu mzito katika soka. Kudos Legend..!
    .
    .
    - Hakika kwa kuondokewa na mtu kama Diogo Jota, itoshe kusema familia ya mpira tumepata pigo kubwa haswa! 🥹!
    .
    .

    …Endelea kupumzika, Diogo Jota. 🕊
    #SportsElite - Baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu, hatimaye mshambuliaji hatari wa klabu ya Inter Miami pamoja Nahodha wa timu ya Taifa ya Argentina, Leo Messi.. kupitia katika Ukurasa wake wa Instagram (@leomessi) ‘FIFA BOY’ ame-share picha ya Diogo Jota, ikiwa ni ishara ya KUGUSWA moja kwa moja na msiba huu mzito katika soka. Kudos Legend..! 🤝 . . - Hakika kwa kuondokewa na mtu kama Diogo Jota, itoshe kusema familia ya mpira tumepata pigo kubwa haswa! 🥹! . . …Endelea kupumzika, Diogo Jota. 🕊
    0 Comments 0 Shares 1K Views
More Results