• Sauti ya Mungu na maelekezo ya Mungu imeandaliwa specific kwa wanadamu.


    Mithali 8:4
    [4]Enyi watu, nawaita ninyi;
    Na sauti yangu ni kwa wanadamu.

    Mwanadamu anaye sikia sauti ya Mungu ndiye anayekuwa mtawala wa kila kitu.

    Mwanzo 1:26
    [26]Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

    Kama ukiweza kuishi katika mapenzi ya Mungu basi yeye ni kila kitu .

    Mtu baada ya kuokoka anaznza kutembea katka kusudi la Mungu,kusikia sauti ya Mungu lazima la atapata zaidi ya vile aombavyo.

    Kanuni ya kupata katokeo unaposikia sauti ya Mungu.

    Mali ni zawadi ,nyumba ni zawadi lakini ili upate izo zawadi lazima ufuate kanuni ya kumcha MUNGU.

    Mithali 8:13
    [13]Kumcha BWANA ni kuchukia uovu;
    Kiburi na majivuno, na njia mbovu,
    Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.

    Kumbz ili ufike kusema unamcha Bwana lazima uwe mtu wa kuchukia uovu kwa moyo wote .

    Na mtu ili awe wake Mungu au afanyike kuwa mwana lazima achukie uovu seriously kabisa.

    Ok naitwa sylvester Mwakabende kutoka (build new eden)

    Kwa mafundisho zaidi unaweza kujiungaletu la watsap.
    https://chat.whatsapp.com/IxkPEsnxi02ExNGrlmbWR4

    #Build new eden
    #Restoremenposition
    Sauti ya Mungu na maelekezo ya Mungu imeandaliwa specific kwa wanadamu. Mithali 8:4 [4]Enyi watu, nawaita ninyi; Na sauti yangu ni kwa wanadamu. Mwanadamu anaye sikia sauti ya Mungu ndiye anayekuwa mtawala wa kila kitu. Mwanzo 1:26 [26]Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Kama ukiweza kuishi katika mapenzi ya Mungu basi yeye ni kila kitu . Mtu baada ya kuokoka anaznza kutembea katka kusudi la Mungu,kusikia sauti ya Mungu lazima la atapata zaidi ya vile aombavyo. Kanuni ya kupata katokeo unaposikia sauti ya Mungu. Mali ni zawadi ,nyumba ni zawadi lakini ili upate izo zawadi lazima ufuate kanuni ya kumcha MUNGU. Mithali 8:13 [13]Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia. Kumbz ili ufike kusema unamcha Bwana lazima uwe mtu wa kuchukia uovu kwa moyo wote . Na mtu ili awe wake Mungu au afanyike kuwa mwana lazima achukie uovu seriously kabisa. Ok naitwa sylvester Mwakabende kutoka (build new eden) Kwa mafundisho zaidi unaweza kujiungaletu la watsap. https://chat.whatsapp.com/IxkPEsnxi02ExNGrlmbWR4 #Build new eden #Restoremenposition
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·656 Views
  • Balozi wa Afrika Kusini Nchini Marekani , Ebrahim Rasool ambaye ametimuliwa na Nchi ya Marekani kutokana na kukosoa sera za Donald Trump, amerejea Afrika Kusini kwa ufakhari mkubwa na kupokewa kwa shangwe na mamia ya Wananchi waliofurika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town Nchini Afrika Kusini.

    Balozi huyo na mkewe, Rosieda, waliwasili jana katika Uwanda wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town baada ya kusafari kutoka Nchini Marekani kupitia Qatar na wamekaribishwa vyema na kwa shangwe na mamia ya Wafuasi wao. Mapema mwezi huu, Balozi Rasool alitangazwa na Serikali ya Marekani kuwa ni Mtu asiyetakiwa kuweko Nchini humo baada ya kukosoa sera za Donald Trump, hatua ambayo inaonesha wazi jinsi madai ya uhuru wa kusema yasivyothaminiwa Nchini Marekani licha ya majigambo makubwa ya Nchi Marekani ya kupigania haki za Binadamu na demokrasia.

    Akiwahutubia mamia ya Mashabiki wake kwenye Uwanja wa Ndege wa Cape Town, Balozi Rasool amesema kwamba ingawa ametakiwa kuondoka huko Marekani lakini jambo hilo limeshindwa kufikia lengo lake kwani Viongozi wa Marekani wanadhani wamemdhalilisha wakati yeye anaona fakhari kwa maneno aliyotoa na Wananchi wa Afrika Kusini nao wanajivunia msimamo huo ndio maana wamejitokea kwa mamia kumpokea kishujaa.

    "Unaporejea nyumbani na kupokewa kwa shangwe na umati kama huu wa watu, mtu unaona fakhari na unajivunia msimamo wako." alisema Rasool.

    Alipoulizwa iwapo diplomasia imeshindwa, amesema ukweli kwamba matamshi yake yamemfanya Trump na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio kuwa makini na hatua ya Serikali ya Marekani ya kumtangaza kuwa ni Mtu asiyetakiwa nchini humo ni ushahidi kwamba ujumbe wake umefika ngazi za juu kabisa za serikali ya Marekani.

    Balozi wa Afrika Kusini 🇿🇦 Nchini Marekani 🇺🇸, Ebrahim Rasool ambaye ametimuliwa na Nchi ya Marekani kutokana na kukosoa sera za Donald Trump, amerejea Afrika Kusini kwa ufakhari mkubwa na kupokewa kwa shangwe na mamia ya Wananchi waliofurika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town Nchini Afrika Kusini. Balozi huyo na mkewe, Rosieda, waliwasili jana katika Uwanda wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town baada ya kusafari kutoka Nchini Marekani kupitia Qatar na wamekaribishwa vyema na kwa shangwe na mamia ya Wafuasi wao. Mapema mwezi huu, Balozi Rasool alitangazwa na Serikali ya Marekani kuwa ni Mtu asiyetakiwa kuweko Nchini humo baada ya kukosoa sera za Donald Trump, hatua ambayo inaonesha wazi jinsi madai ya uhuru wa kusema yasivyothaminiwa Nchini Marekani licha ya majigambo makubwa ya Nchi Marekani ya kupigania haki za Binadamu na demokrasia. Akiwahutubia mamia ya Mashabiki wake kwenye Uwanja wa Ndege wa Cape Town, Balozi Rasool amesema kwamba ingawa ametakiwa kuondoka huko Marekani lakini jambo hilo limeshindwa kufikia lengo lake kwani Viongozi wa Marekani wanadhani wamemdhalilisha wakati yeye anaona fakhari kwa maneno aliyotoa na Wananchi wa Afrika Kusini nao wanajivunia msimamo huo ndio maana wamejitokea kwa mamia kumpokea kishujaa. "Unaporejea nyumbani na kupokewa kwa shangwe na umati kama huu wa watu, mtu unaona fakhari na unajivunia msimamo wako." alisema Rasool. Alipoulizwa iwapo diplomasia imeshindwa, amesema ukweli kwamba matamshi yake yamemfanya Trump na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio kuwa makini na hatua ya Serikali ya Marekani ya kumtangaza kuwa ni Mtu asiyetakiwa nchini humo ni ushahidi kwamba ujumbe wake umefika ngazi za juu kabisa za serikali ya Marekani.
    Love
    Like
    3
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·1χλμ. Views
  • Muungano wa Waasi wa kundi la AFC/M23 umetangaza kutoshiriki mazungumzo ya amani huku wakiituhumu Serikali ya Kinshasa kwa kuendeleza vita. Katika taarifa ya Kundi hilo iliyotolewa Februari 17, 2025, Waasi hao wa M23 wameituhumu Serikali ya Rais Félix Tshisekedi kwa kuendesha mashambulizi ya ardhini kwa kutumia Ndege za kivita wakati wanajua fike wapo kwenye hatua za mwisho kuelekea kwenye mkutano wa amani Nchini Angola .

    Ikumbukwe kwamba Waasi hao wa AFC/M23 walikuwa tayari wameshawateua Wawakilishi wao na kuthibitisha kuwa watatuma Wawakilishi hao Nchini Jijini Luanda, Angola kwa ajili ya mazungumzo ya maani ambayo yamepangwa kufanyika Machi 18, 2025.

    Muungano wa Waasi wa kundi la AFC/M23 umetangaza kutoshiriki mazungumzo ya amani huku wakiituhumu Serikali ya Kinshasa kwa kuendeleza vita. Katika taarifa ya Kundi hilo iliyotolewa Februari 17, 2025, Waasi hao wa M23 wameituhumu Serikali ya Rais Félix Tshisekedi kwa kuendesha mashambulizi ya ardhini kwa kutumia Ndege za kivita wakati wanajua fike wapo kwenye hatua za mwisho kuelekea kwenye mkutano wa amani Nchini Angola 🇦🇴. Ikumbukwe kwamba Waasi hao wa AFC/M23 walikuwa tayari wameshawateua Wawakilishi wao na kuthibitisha kuwa watatuma Wawakilishi hao Nchini Jijini Luanda, Angola kwa ajili ya mazungumzo ya maani ambayo yamepangwa kufanyika Machi 18, 2025.
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·567 Views
  • Margaret Nduta Macharia (37) ambaye ni Raia wa Kenya aliyekamatwa mwaka 2023 Nchini Vietnam na kilogramu mbili (2) za dawa za kulevya aina ya Cocaine, anatarajiwa kunyongwa hadi kufa kesho Jumatatu Machi 17, 2025.

    Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Nation, Margaret aliyepewa hukumu hiyo Machi 6, 2025 alisema alipewa mzigo huo wa dawa za kulevya na Mwanaume mmoja kutoka Nchini Kenya aliyemtaja kwa jina moja la John. Pia, taarifa hiyo inaeleza kuwa alifanikiwa kupita katika Viwanja vitatu (3) vya Ndege bila kukamatwa, kabla ya kugundulika Nchini Vietnam. Viwanja hivyo ni pamoja na Jomo Kenyatta (Kenya), Bole (Ethiopia) na Hamad (Qatar).

    Hata hivyo, Margaret akijitetea Mahakamani Nchini Vietnam alidai hakufahamu kama mzigo ule ulikuwa ni dawa za kulevya. Taarifa kutoka Nchini Vietnam, Margaret atakula chakula chake cha mwisho kesho saa 1:30 usiku na kisha kunyongwa saa 2:30 za usiku.

    Margaret Nduta Macharia (37) ambaye ni Raia wa Kenya 🇰🇪 aliyekamatwa mwaka 2023 Nchini Vietnam 🇻🇳 na kilogramu mbili (2) za dawa za kulevya aina ya Cocaine, anatarajiwa kunyongwa hadi kufa kesho Jumatatu Machi 17, 2025. Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Nation, Margaret aliyepewa hukumu hiyo Machi 6, 2025 alisema alipewa mzigo huo wa dawa za kulevya na Mwanaume mmoja kutoka Nchini Kenya aliyemtaja kwa jina moja la John. Pia, taarifa hiyo inaeleza kuwa alifanikiwa kupita katika Viwanja vitatu (3) vya Ndege bila kukamatwa, kabla ya kugundulika Nchini Vietnam. Viwanja hivyo ni pamoja na Jomo Kenyatta (Kenya), Bole (Ethiopia) na Hamad (Qatar). Hata hivyo, Margaret akijitetea Mahakamani Nchini Vietnam alidai hakufahamu kama mzigo ule ulikuwa ni dawa za kulevya. Taarifa kutoka Nchini Vietnam, Margaret atakula chakula chake cha mwisho kesho saa 1:30 usiku na kisha kunyongwa saa 2:30 za usiku.
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·827 Views
  • PART 7

    Saa 4:28 asubuhi, Mnara wa Kaskazini wa WTC ulianguka, dakika 102 baada ya athari iliyosababishwa na ndege ya shirika la ndege la American Airlines. Mamia ya watu, ambao hawakuweza kuondolewa, ikiwa ni pamoja na waokoaji waliokuwa katika ghorofa, walifukiwa na vifusi vya jengo hilo.
    Minara hiyo inayoanguka pia ilisababisha uharibifu mkubwa kwa majengo yaliyo kuwa karibu, kama mnara wa 7 wa WTC, ambao ulidondoka saa 11:20 jioni.
    PART 7 Saa 4:28 asubuhi, Mnara wa Kaskazini wa WTC ulianguka, dakika 102 baada ya athari iliyosababishwa na ndege ya shirika la ndege la American Airlines. Mamia ya watu, ambao hawakuweza kuondolewa, ikiwa ni pamoja na waokoaji waliokuwa katika ghorofa, walifukiwa na vifusi vya jengo hilo. Minara hiyo inayoanguka pia ilisababisha uharibifu mkubwa kwa majengo yaliyo kuwa karibu, kama mnara wa 7 wa WTC, ambao ulidondoka saa 11:20 jioni.
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·699 Views
  • PART 6

    Saa 3:59 asubuhi, Mnara wa Kusini wa kituo cha Biashara cha World Trade Center (WTC) ulidondoka wenyewe, dakika 55 matukio hayo ya kwanza.
    Ndege ya nne, ya shirika la ndege la United Airlines Flight 93, ilianguka saa 10: 03 asubuhi kwenye chamba moja karibu na Pittsburg, huko Pennsylvania, ikiwa na watu 44, wakiwemo magaidi wanne. Abiria kwenye ndege hiyo waliripotiwa kupigana na watekaji nyara baada ya kuambiwa juu ya mkasa huo kwenye simu zao za rununu. Inaaminika kwamba ndege hii, iliyokuwa ikielekea Washington,ilienda kushambulia Capitol, makao makuu ya Bunge la Marekani.
    PART 6 Saa 3:59 asubuhi, Mnara wa Kusini wa kituo cha Biashara cha World Trade Center (WTC) ulidondoka wenyewe, dakika 55 matukio hayo ya kwanza. Ndege ya nne, ya shirika la ndege la United Airlines Flight 93, ilianguka saa 10: 03 asubuhi kwenye chamba moja karibu na Pittsburg, huko Pennsylvania, ikiwa na watu 44, wakiwemo magaidi wanne. Abiria kwenye ndege hiyo waliripotiwa kupigana na watekaji nyara baada ya kuambiwa juu ya mkasa huo kwenye simu zao za rununu. Inaaminika kwamba ndege hii, iliyokuwa ikielekea Washington,ilienda kushambulia Capitol, makao makuu ya Bunge la Marekani.
    Like
    Love
    2
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·780 Views
  • PART 5

    Lakini saa 3:37 asubuhi huko Virginia, ndege ya tatu, ya shirika la ndege la American Airlines Flight 77, ilianguka katika sehemu ya magharibi ya Pentagon, makao makuu ya wizara ya Ulinzi ya Marekani, ikiwa na watu 64, wakiwemo watu watano wa kujitoa mhanga.
    PART 5 Lakini saa 3:37 asubuhi huko Virginia, ndege ya tatu, ya shirika la ndege la American Airlines Flight 77, ilianguka katika sehemu ya magharibi ya Pentagon, makao makuu ya wizara ya Ulinzi ya Marekani, ikiwa na watu 64, wakiwemo watu watano wa kujitoa mhanga.
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·597 Views
  • PART 4

    2:46 asubuhi, ulimwengu wapigwa na bumbuwazi

    Ilikuwa saa 2:46 asubuhi, saa zahuko New York, wakati Boeing 767 kutoka shirika la ndege la American Airlines Flight 11 ilipoanguka kwenye Mnara wa Kaskazini wa kituo cha Biashara cha World Trade Center , ikiwa na watu 92 , wakiwemo magaidi watano.
    Dakika kumi na saba baadaye, saa 3:03 asubuhi, vituo kadhaa vya televisheni vilikuwa vikitangaza tukio hilo, watu waliona ndege ya shirika la ndege la United Airlines Flight 175 ikigonga Mnara wa Kusini wa jengo hilo la kibiashara. Watu 65 walikuemo, ikiwa ni pamoja na watekaji nyara watano. Wakati moto ukiharibu sakafu za juu za minara hiyo miwili, Andrew Card, mkurugenzi katika ofisi ya rais, alimfahamisha rais George W. Bush: “Ndege ya pili imegonga mnara mwingine na Marekani sasa inashambuliwa. "
    PART 4 2:46 asubuhi, ulimwengu wapigwa na bumbuwazi Ilikuwa saa 2:46 asubuhi, saa zahuko New York, wakati Boeing 767 kutoka shirika la ndege la American Airlines Flight 11 ilipoanguka kwenye Mnara wa Kaskazini wa kituo cha Biashara cha World Trade Center , ikiwa na watu 92 , wakiwemo magaidi watano. Dakika kumi na saba baadaye, saa 3:03 asubuhi, vituo kadhaa vya televisheni vilikuwa vikitangaza tukio hilo, watu waliona ndege ya shirika la ndege la United Airlines Flight 175 ikigonga Mnara wa Kusini wa jengo hilo la kibiashara. Watu 65 walikuemo, ikiwa ni pamoja na watekaji nyara watano. Wakati moto ukiharibu sakafu za juu za minara hiyo miwili, Andrew Card, mkurugenzi katika ofisi ya rais, alimfahamisha rais George W. Bush: “Ndege ya pili imegonga mnara mwingine na Marekani sasa inashambuliwa. "
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·788 Views
  • PART 1

    Miaka ishirini iliyopita, asubuhi ya Septemba 11, 2001 katika pwani ya mashariki mwa Marekani, ndege nne za abiria zilitekwa nyara kwa wakati mmoja na magaidi 19 na kusababisha vifo vya maelfu ya watu baada ya kugonga minara pacha ya kituo cha bisahara cha World Trade Center nchini Marekani.
    PART 1 Miaka ishirini iliyopita, asubuhi ya Septemba 11, 2001 katika pwani ya mashariki mwa Marekani, ndege nne za abiria zilitekwa nyara kwa wakati mmoja na magaidi 19 na kusababisha vifo vya maelfu ya watu baada ya kugonga minara pacha ya kituo cha bisahara cha World Trade Center nchini Marekani.
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·635 Views
  • Maazimio (22) ya Marais wa Nchi Wanachama wa SADC na EAC kwenye mkutano uliofanyika leo hii Jijini Dar Es Salaam, Tanzania , Azimio la (12) limewataka Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Nchi zote Wanachama kukutana ndani ya siku tano (5) na kutoa mwelekeo wa kitalaam kuhusu mambo yafuatayo:

    - Kusitisha mara moja mapigano huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo .

    - Kutoa misaada ya Kibinadamu na kuwasaidia Wahanga wa vita.

    - Kutoa mpango kazi wa ulinzi ndani ya Mji wa Goma na maeneo Jirani.

    - Kuzifungua njia muhimu za mawasiliano kwenye Miji ya Goma - Kibumba- Rumangambo - Kalengera- Rutshuru na Goma - Kiwanja- Rwindi lakini pia matumizi ya Ziwa Kivu kwa ajili ya usafiri.

    - Kuufungua Uwanja wa Ndege wa Mji Goma mara moja.

    Maazimio (22) ya Marais wa Nchi Wanachama wa SADC na EAC kwenye mkutano uliofanyika leo hii Jijini Dar Es Salaam, Tanzania 🇹🇿, Azimio la (12) limewataka Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Nchi zote Wanachama kukutana ndani ya siku tano (5) na kutoa mwelekeo wa kitalaam kuhusu mambo yafuatayo: - Kusitisha mara moja mapigano huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo 🇨🇩. - Kutoa misaada ya Kibinadamu na kuwasaidia Wahanga wa vita. - Kutoa mpango kazi wa ulinzi ndani ya Mji wa Goma na maeneo Jirani. - Kuzifungua njia muhimu za mawasiliano kwenye Miji ya Goma - Kibumba- Rumangambo - Kalengera- Rutshuru na Goma - Kiwanja- Rwindi lakini pia matumizi ya Ziwa Kivu kwa ajili ya usafiri. - Kuufungua Uwanja wa Ndege wa Mji Goma mara moja.
    Like
    2
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·604 Views
  • Kwenye kikao cha pamoja kati ya Jumuiya mbili za SADC na ile ya EAC, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo , Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, ambaye alihudhuria kwa njia ya Mtandao, aliweka wazi matakwa yake kwenye mkutano huo ambapo alisema baadhi ya mambo yakiwemo yafuatayo:

    - Nchi ya Rwanda iambiwe ukweli, ionywe na iachane na uvamizi wake huko Mjini Goma.

    - Vikosi vya Rwanda viondoke mara moja kwenye maeneo ya DR Congo ambayo wanayamiliki pasipo uhalali.

    - Kufunguliwa kwa Uwanja wa Ndege wa Mjini Goma kwa ajili ya misaada ya kibinadamu.

    - Kurejesha Mji wa Goma kwa Mamlaka ya Serikali ya DR Congo.

    Kwenye kikao cha pamoja kati ya Jumuiya mbili za SADC na ile ya EAC, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo 🇨🇩, Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, ambaye alihudhuria kwa njia ya Mtandao, aliweka wazi matakwa yake kwenye mkutano huo ambapo alisema baadhi ya mambo yakiwemo yafuatayo: - Nchi ya Rwanda 🇷🇼 iambiwe ukweli, ionywe na iachane na uvamizi wake huko Mjini Goma. - Vikosi vya Rwanda viondoke mara moja kwenye maeneo ya DR Congo ambayo wanayamiliki pasipo uhalali. - Kufunguliwa kwa Uwanja wa Ndege wa Mjini Goma kwa ajili ya misaada ya kibinadamu. - Kurejesha Mji wa Goma kwa Mamlaka ya Serikali ya DR Congo.
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·528 Views
  • Muda ukasonga. Dunia ikabadilika. Mataifa yakaanza kuweka mbele maslahi yao, na Ukraine akajikuta akilia peke yake kwenye uwanja wa vita.

    Aliyeahidi kumlinda Urusi ndiye huyo anayemshambulia kwa mabomu, vifaru na ndege za kivita.

    Kwa miaka mingi, Vladimir Putin alikuwa anaangalia ramani ya dunia akijiuliza, "Mbona Crimea na Donbas zipo nje ya milki yangu?"

    Halafu, ghafla mwaka 2014, Urusi ikaamua kumng'ata Ukraine kwa mara ya kwanza.

    Crimea ikachukuliwa, na dunia ikakaa kimya. Hakukuwa na hatua kubwa zilizochukuliwa na Marekani wala Uingereza. Ukraine akaanza kuona dalili za usaliti.

    Mwaka 2022, Urusi ikarudi tena, safari hii kwa nguvu kubwa zaidi.
    Tishio la silaha za nyuklia lililomfanya Ukraine kuwa mbabe, halikuwepo tena. Hakuwa na kinga tena, alikuwa mtu mwepesi wa kushambuliwa.

    Na hapa ndipo Ukraine alipogundua kosa lake kubwa aliamini makaratasi kuliko mabavu.
    Muda ukasonga. Dunia ikabadilika. Mataifa yakaanza kuweka mbele maslahi yao, na Ukraine akajikuta akilia peke yake kwenye uwanja wa vita. Aliyeahidi kumlinda Urusi ndiye huyo anayemshambulia kwa mabomu, vifaru na ndege za kivita. Kwa miaka mingi, Vladimir Putin alikuwa anaangalia ramani ya dunia akijiuliza, "Mbona Crimea na Donbas zipo nje ya milki yangu?" Halafu, ghafla mwaka 2014, Urusi ikaamua kumng'ata Ukraine kwa mara ya kwanza. Crimea ikachukuliwa, na dunia ikakaa kimya. Hakukuwa na hatua kubwa zilizochukuliwa na Marekani wala Uingereza. Ukraine akaanza kuona dalili za usaliti. Mwaka 2022, Urusi ikarudi tena, safari hii kwa nguvu kubwa zaidi. Tishio la silaha za nyuklia lililomfanya Ukraine kuwa mbabe, halikuwepo tena. Hakuwa na kinga tena, alikuwa mtu mwepesi wa kushambuliwa. Na hapa ndipo Ukraine alipogundua kosa lake kubwa aliamini makaratasi kuliko mabavu.
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·1χλμ. Views
  • #PART6

    Alipoingia Ikulu Kabila alifuta jina Zaire na kurudisha Congo (Jamhuri ya kidemokrasia). Baadae alifikiria kuiachia Kivu, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini adimu duniani. Akasema "to hell with Lemera Agreement" akautupilia mbali mkataba wa Lemera. Akasema Kivu itabaki Congo na madini ya Kivu yatajenga Congo. Full stop. Ashakuwa Rais utamfanya nini?

    Kagame hakuamini macho yake. Alishawaza jinsi ambavyo Rwanda ingekuwa Dubai ya Afrika kwa rasilimali za Congo. Lakini ghafla aligeukwa na mshirika wake Laurent Désiré Kabila. Akamfuata "Godfather" wake mzee Museveni. Mzee akasema kama katugeuka tumpige. Wakatafuta kikundi cha Waasi wakiunge mkono. Wakapata Rassemblement Congolais pour la Démocratie (RCD), kilichoongozwa na Jenerali Ernest Wamba dia Wamba. Kikundi kikapewa silaha na fedha kikaanza kumshughulikia Kabila.

    RCD ikaanza kuchapana na jeshi la Congo (FARDC) ikiwa na backup ya Rwanda na Uganda. Vita vikapamba moto. Rwanda na Uganda nao wakaingiza majeshi Congo kusaidia waasi wa RCD. Kabila akaona anazidiwa, akaomba msaada Angola na Chad. Nchi hizo zikaleta vikosi vyake Congo. Mapigano yakawa makali sana. Eneo la mashariki mwa Congo likageuka machinjioni. Watu walikufa kwa wingi, mpaka maiti zikatapakaa barabarani bila kuzikwa, zikawa zinadonolewa na ndege.

    Hii iliitwa Vita ya Pili ya Congo (1998–2002), iliyokua mbaya zaidi katika historia ya vita zote Afrika. Imebatizwa jina "Vita Kuu ya Afrika". Inakadiriwa watu laki tano walipoteza maisha huku mamilioni wakikimbia nchi. Mapigano yaliendelea, huku vikosi vya Rwanda na Uganda vikichota madini. Katikati ya mapigano mgongano wa kimaslahi ukajitokeza.

    Jasin Stearns, katika kitabu chake Dancing in the Glory of Monsters, anasema Kagame alishindwa kuelewana na "godfather" wake Museveni juu ya mgawanyo wa mali. Hali hiyo ilifanya kikundi cha RCD kipasuke na kuzaliwa vikundi viwili. Cha kwanza kikajiita RCD-Goma kikiongozwa na Kanali Emile Ilunga (hiki kilisaidiwa na Rwanda) na cha pili kikajiita RCD-Kisangani, kikiongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi (kikisaidiwa na Uganda).
    (Malisa GJ)

    #PART6 Alipoingia Ikulu Kabila alifuta jina Zaire na kurudisha Congo (Jamhuri ya kidemokrasia). Baadae alifikiria kuiachia Kivu, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini adimu duniani. Akasema "to hell with Lemera Agreement" akautupilia mbali mkataba wa Lemera. Akasema Kivu itabaki Congo na madini ya Kivu yatajenga Congo. Full stop. Ashakuwa Rais utamfanya nini? Kagame hakuamini macho yake. Alishawaza jinsi ambavyo Rwanda ingekuwa Dubai ya Afrika kwa rasilimali za Congo. Lakini ghafla aligeukwa na mshirika wake Laurent Désiré Kabila. Akamfuata "Godfather" wake mzee Museveni. Mzee akasema kama katugeuka tumpige. Wakatafuta kikundi cha Waasi wakiunge mkono. Wakapata Rassemblement Congolais pour la Démocratie (RCD), kilichoongozwa na Jenerali Ernest Wamba dia Wamba. Kikundi kikapewa silaha na fedha kikaanza kumshughulikia Kabila. RCD ikaanza kuchapana na jeshi la Congo (FARDC) ikiwa na backup ya Rwanda na Uganda. Vita vikapamba moto. Rwanda na Uganda nao wakaingiza majeshi Congo kusaidia waasi wa RCD. Kabila akaona anazidiwa, akaomba msaada Angola na Chad. Nchi hizo zikaleta vikosi vyake Congo. Mapigano yakawa makali sana. Eneo la mashariki mwa Congo likageuka machinjioni. Watu walikufa kwa wingi, mpaka maiti zikatapakaa barabarani bila kuzikwa, zikawa zinadonolewa na ndege. Hii iliitwa Vita ya Pili ya Congo (1998–2002), iliyokua mbaya zaidi katika historia ya vita zote Afrika. Imebatizwa jina "Vita Kuu ya Afrika". Inakadiriwa watu laki tano walipoteza maisha huku mamilioni wakikimbia nchi. Mapigano yaliendelea, huku vikosi vya Rwanda na Uganda vikichota madini. Katikati ya mapigano mgongano wa kimaslahi ukajitokeza. Jasin Stearns, katika kitabu chake Dancing in the Glory of Monsters, anasema Kagame alishindwa kuelewana na "godfather" wake Museveni juu ya mgawanyo wa mali. Hali hiyo ilifanya kikundi cha RCD kipasuke na kuzaliwa vikundi viwili. Cha kwanza kikajiita RCD-Goma kikiongozwa na Kanali Emile Ilunga (hiki kilisaidiwa na Rwanda) na cha pili kikajiita RCD-Kisangani, kikiongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi (kikisaidiwa na Uganda). (Malisa GJ)
    Like
    2
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·1χλμ. Views
  • #PART3

    Baadhi ya wanajeshi wa Kitutsi hawakuridhika na ukandamizaji uliofanywa na Habyarimana. Wakajiorganize kupambana. Wakati huo Kagame akiwa askari wa NRA ya Uganda akimsaidia Museveni vita vya msituni. Mwaka 1983 hadi 1985 alienda kozi ya kijeshi TMA, Moduli. Alipohitimu akarudi Uganda kumsaidia Museveni vita vya msituni na hatimaye mwaka 1986 wakafanikiwa kuchukua nchi. NRA ikawa sehemu ya jeshi la Uganda kabla ya kubadilishwa muundo mwaka 1995 kuwa UPDF.

    Kagame akawa mkuu wa intelijensia ya jeshi. Baadae akaenda masomoni Marekani. Akiwa huko RPF ikaanzishwa na Jenerali Fredy Rwigyema kupambana na Serikali ya Habyarimana. Lakini Jenerali Rwigyema akauawa kwa guruneti akiwa uwanja wa vita. Kagame akalazimika kukatisha masomo na kurudi Rwanda kuongoza RPF akishirikiana na Alexis Kanyarwenge. Museveni akampa msaada wa fedha, silaha na chakula. RPF ikaweka kambi Uganda eneo la Kabale, Burundi eneo la Muyinga na Congo maeneo ya Kivu, Uvira na Goma.

    Mwaka 1994, askari wa RPF wakatungua ndege ya Rais Habyarimana ikiwa inakaribia kutua uwanja wa ndege wa Kigali ikitokea Dar es Salaam kwenye mazungumzo ya Amani alikuwa na Rais Cyprien Ntaramira wa Burundi. Wote wawili walikufa papo hapo.

    Kuuawa kwa Rais Habyarimana kuliamsha hasira za Wahutu na kusabisha mauaji ya Kimbari ambapo Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa kikatili kwa kucharangwa mapanga. Hali hiyo ilisababisha Watutsi wengi kukimbia nchi yao. Wapo waliokimbilia Tanzania, Uganda, lakini wengi zaidi walikimbilia eneo la Kivu.

    Kwa kifupi, idadi ya Watutsi eneo la Kivu iliongezeka siku hadi siku. Watutsi walioenda Kivu wengi hawakurudi Rwanda hata baada ya vita kumalizika. Ilikuwa vigumu kutofautisha Mtutsi mwenye asili ya Congo (Banyamulenge) na Mtutsi wa Rwanda, kwa sababu wote wanaongea lugha moja, mila na desturi moja.

    Kwahiyo hisia za Wakongomani kwamba Banyamulenge ni wageni zikaanza kupata nguvu kutokana na uhamiaji mkubwa wa Watutsi maeneo ya Kivu kaskazini na kusini. Wakati huo Congo ikiitwa Zaire Rais Mobutu Sese Seko alikataa kuwatambua Banyamulenge kama raia wake, na akazuia wasipewe vitambulisho vya taifa.
    (Malisa GJ)

    #PART3 Baadhi ya wanajeshi wa Kitutsi hawakuridhika na ukandamizaji uliofanywa na Habyarimana. Wakajiorganize kupambana. Wakati huo Kagame akiwa askari wa NRA ya Uganda akimsaidia Museveni vita vya msituni. Mwaka 1983 hadi 1985 alienda kozi ya kijeshi TMA, Moduli. Alipohitimu akarudi Uganda kumsaidia Museveni vita vya msituni na hatimaye mwaka 1986 wakafanikiwa kuchukua nchi. NRA ikawa sehemu ya jeshi la Uganda kabla ya kubadilishwa muundo mwaka 1995 kuwa UPDF. Kagame akawa mkuu wa intelijensia ya jeshi. Baadae akaenda masomoni Marekani. Akiwa huko RPF ikaanzishwa na Jenerali Fredy Rwigyema kupambana na Serikali ya Habyarimana. Lakini Jenerali Rwigyema akauawa kwa guruneti akiwa uwanja wa vita. Kagame akalazimika kukatisha masomo na kurudi Rwanda kuongoza RPF akishirikiana na Alexis Kanyarwenge. Museveni akampa msaada wa fedha, silaha na chakula. RPF ikaweka kambi Uganda eneo la Kabale, Burundi eneo la Muyinga na Congo maeneo ya Kivu, Uvira na Goma. Mwaka 1994, askari wa RPF wakatungua ndege ya Rais Habyarimana ikiwa inakaribia kutua uwanja wa ndege wa Kigali ikitokea Dar es Salaam kwenye mazungumzo ya Amani alikuwa na Rais Cyprien Ntaramira wa Burundi. Wote wawili walikufa papo hapo. Kuuawa kwa Rais Habyarimana kuliamsha hasira za Wahutu na kusabisha mauaji ya Kimbari ambapo Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa kikatili kwa kucharangwa mapanga. Hali hiyo ilisababisha Watutsi wengi kukimbia nchi yao. Wapo waliokimbilia Tanzania, Uganda, lakini wengi zaidi walikimbilia eneo la Kivu. Kwa kifupi, idadi ya Watutsi eneo la Kivu iliongezeka siku hadi siku. Watutsi walioenda Kivu wengi hawakurudi Rwanda hata baada ya vita kumalizika. Ilikuwa vigumu kutofautisha Mtutsi mwenye asili ya Congo (Banyamulenge) na Mtutsi wa Rwanda, kwa sababu wote wanaongea lugha moja, mila na desturi moja. Kwahiyo hisia za Wakongomani kwamba Banyamulenge ni wageni zikaanza kupata nguvu kutokana na uhamiaji mkubwa wa Watutsi maeneo ya Kivu kaskazini na kusini. Wakati huo Congo ikiitwa Zaire Rais Mobutu Sese Seko alikataa kuwatambua Banyamulenge kama raia wake, na akazuia wasipewe vitambulisho vya taifa. (Malisa GJ)
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·985 Views
  • muda mwingi yeye yeye utamkuta anaiongoza camera drone (ndege isiyo na rubani) au anakuwa na peni na karatasi yako muda mwingi anaandika baadhi ya vitu

    huyu ndo mfungua code wa kocha fadlu davies , huyu ndo anampa mifumo na uwezo wa timu inayotarajiwa kucheza na SIMBA , huyu ndo humpa udhaifu na ubora wa timu pinzani inayotarajiwa kucheza na SIMBA huyu ndo anajifungia ndani na kocha fadlu kumpa mrejesho wa perfomance ya mchezaji mmoja mmoja wa SIMBA baada ya kumalizika mazoezi

    Ni bwanamdogo sana ila uwezo wake unatisha sana ukizungumzia mafanikio ya RAJA CASABLANCA msimu uliopita basi moja kati ya waliochangia ni huyu jamaa na raja ikamaliza msimu uliopita ligi ya moroco wakiwa mabingwa na walimaliza msimu bila kufungwa (unbeaten)

    anaitwa MUEEZKAJEE ni mchambuzi wa video wa SIMBA SPORTS CLUB ( video &perfomance analysis) ni kijana mzaliwa wa africa kusini ila uwezo mkubwa sana , hata ile siku anaenda kuuambia uongozi wa RAJA kuwa anaondoka na anamfata kocha fadlu viongozi wa RAJA waliumia sana

    wote kwa pamoja walikuwa raja na msimu uliopita na wakaipa ubingwa namsimu huu wapo SIMBA wanaendelea kuwapa furaha wanasimba.


    #paulswai
    muda mwingi yeye yeye utamkuta anaiongoza camera drone (ndege isiyo na rubani) au anakuwa na peni na karatasi yako muda mwingi anaandika baadhi ya vitu huyu ndo mfungua code wa kocha fadlu davies , huyu ndo anampa mifumo na uwezo wa timu inayotarajiwa kucheza na SIMBA , huyu ndo humpa udhaifu na ubora wa timu pinzani inayotarajiwa kucheza na SIMBA huyu ndo anajifungia ndani na kocha fadlu kumpa mrejesho wa perfomance ya mchezaji mmoja mmoja wa SIMBA baada ya kumalizika mazoezi Ni bwanamdogo sana ila uwezo wake unatisha sana ukizungumzia mafanikio ya RAJA CASABLANCA msimu uliopita basi moja kati ya waliochangia ni huyu jamaa na raja ikamaliza msimu uliopita ligi ya moroco wakiwa mabingwa na walimaliza msimu bila kufungwa (unbeaten) anaitwa MUEEZKAJEE ni mchambuzi wa video wa SIMBA SPORTS CLUB ( video &perfomance analysis) ni kijana mzaliwa wa africa kusini ila uwezo mkubwa sana , hata ile siku anaenda kuuambia uongozi wa RAJA kuwa anaondoka na anamfata kocha fadlu viongozi wa RAJA waliumia sana wote kwa pamoja walikuwa raja na msimu uliopita na wakaipa ubingwa namsimu huu wapo SIMBA wanaendelea kuwapa furaha wanasimba. 👍👍👍👍🦁🦁🦁🦁 #paulswai
    Like
    2
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·1χλμ. Views
  • Rais wa Marekani , Donald Trump amesema mgogoro kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni mkubwa sana. Trump ameyasema hayo jana Januari 30, 2025 akijibu swali la Mwandishi aliyemuuliza kuhusu kinachoendelea baina ya Rwanda na DR Congo, wakati wa mkutano na Waandishi wa habari kuhusu ajali ya Ndege iliyotokea Mjini Washington.

    "Unaniuliza swali kuhusu Rwanda, ni tatizo kubwa sana, nakubali, lakini sidhani kama inafaa kwa sasa kulizungumzia. Lakini ni tatizo kubwa sana," amesema Donald Trump.

    Rais wa Marekani 🇺🇸, Donald Trump amesema mgogoro kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 ni mkubwa sana. Trump ameyasema hayo jana Januari 30, 2025 akijibu swali la Mwandishi aliyemuuliza kuhusu kinachoendelea baina ya Rwanda na DR Congo, wakati wa mkutano na Waandishi wa habari kuhusu ajali ya Ndege iliyotokea Mjini Washington. "Unaniuliza swali kuhusu Rwanda, ni tatizo kubwa sana, nakubali, lakini sidhani kama inafaa kwa sasa kulizungumzia. Lakini ni tatizo kubwa sana," amesema Donald Trump.
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·509 Views
  • MACHACHE KUHUSU MFALME MKWASI ZAIDI DUNIANI

    KUNA HISTORIA ambazo ukitaka kuandika unaweza kuchukua siku mbili za kutafakari uanze wapi na au uishie wapi.....Mfalme Sulemani ni mmoja wapo.............

    Mama wa Sulemani (BATH-SHEBA) alikuwa tayari ni mke wa mtu (URIA MHITI) huyu URIA alikuwa askari wa mfalme DAUDI. so mfalme DAUDI aliponogewa na penzi la BATH SHEBA akafanya mbinu za kifo cha URIA vitani.

    ......umewahi kuwaza kwamba unahangaika na familia moja tu dhidi ya mtu anayetajwa kuwa na wenza 700 na masuria 300...hujahesabu watoto, wajakazi, shangazi, mjomba, wajukuu, nk wanaovinjari kila siku katika hemaya zake........tunaambiwa kwamba chakula kilicholiwa kwa siku moja kilikuwa magunia 240 ya unga, magunia 480 ya chakula, ng'ombe kumi kwa nyama choma, ng'ombe ishirini wa mchuzi, kondoo mia moja, ndege na wanyama wengine wa aina mbalimbali ..........

    unahangaika kutafuta mufu wa dhahabu ilihali mwenzako anapokea tani 30 za dhahabu kila mwaka .........Kwa mwaka mmoja pekee alikuwa anapokea tani si chini ya 30 ya vipande bora vya dhahabu ukiachilia mbali Vito na Madini mengine....kila nakshi na chombo ndani ya nyumba ya Sulemani ilikua ni DHAHABU tupu maana nyakati hizo madini ya fedha yalithaminishwa kwa kiwango cha vumbi dhidi ya dhahabu.... Jumba la Hukumu la Sulemani lilikuwa kubwa na lilijengwa na mwerezi na kuzungushwa na pembe zilizofunikwa na dhahabu na kusimamiwa na simba ........... Katika ukuta kulikuwa kumewekwa ngao 500 za dhahabu .................hata vyombo vya kunywea na sahani zilizokuwa kwenye nyumba hii kuu zilikuwa za “dhahabu”. Shaba “ haikuwa kitu cha kuhesabiwa katika siku za Sulemani”.................Pia alianzisha shamba la kifalme na mbuga yenye maziwa bandia, shamba la maua na matunda

    Wana-ikiolojia wamepata ushahidi dhabiti wa majengo ya Sulemani kote nchini hasa Hazori, Megido na Gezeri, mabaki ambayo yanatoa ushahidi wa ukweli wa 1 Wafalme 9:15. Megido ni muhimu kwa vibanda vyake vya magari ya farasi 450. Jeshi kubwa la Sulemani lilihitaji jengo lenye vibanda 4,000 vya farasi na vilijengwa karibu na mipaka ya Israeli na kulindwa na waendeshaji magari ya farasi..

    Sulemani alipata faida kwani Israeli ilikuwa sehemu nzuri katikati mwa bara la Asia na Afrika. Alitawala njia za kaskazini na kusini na kwa usaidizi wa Wafoeniki, alijenga meli nyingi pale Esion-geberi ili zitumike kubeba shaba iliosafishwa na bidhaa zingine. Meli hizi zilifanya safari ya kusini hadi Ethiopia, Yemen na India Arabian mara moja kila miaka mitatu, na kuleta dhahabu, fedha, na pembe, nyani na tausi

    Sulemani pia aliendeleza viwanda vya kusafisha chuma, pamoja na kuchimba madini katika Araba, kusini mwa Bahari ya Chumvi, na kiwanda kikubwa cha kuyeyusha vyuma cha Esion-geberi, mahali ambapo palikuwa bandari karibu na Bahari ya Shamu.

    Kwa Mujibu wa wanahistoria.. Mansa Musa mfalme wa Mali empire... Ndio Binadamu alie wahi kuwa tajir Dunia nzima mpaka leo hamna mtu alie wahi fikia Utajir wake.. (wakati anaenda hiji macca alipitia misri .. Na kusabisha uchumi wao kuyumba kutokana na dhahabu alizo tumia Pale misri)... UKWELI NI KWAMBA MANSA MUSA aliyetawala kati ya mwaka 1312-1337 na utajiri wake ulikadiriwa kufikia USD billion 400 ILIHALI Mfalme Sulemani alikuwa na utajiri unaokadiriwa kufikia dollar za kimarekani trillion 2.1.......Mansa Kankan Mussa ni tajiri wa kwanza katika kipindi cha baada ya Yesu. Wenyewe wanaita Anno Domino (AD)

    Hata Nathaniel Rothchild Family ( zikiwepo rockerfeller, morgan na du pont family yaani FAMILI NZIMA) Utajiri wao haufikii hata theluthi ya Mfalme Sulemani (dola bilioni 600 tu)

    Wingi wa wake za Sulemani unahalasiha kutapanyika kwa kiazazi chake karibu kote duniani, yasemekana hata hawa wahabeshi wa Somalia, Watusi wa Rwanda na wa Iraq wa Tanzania ni mbegu yake huyo jamaa baada ya kumgaragaza malkia wa Ethiopia ( QUEEN OF SHEBA) alivyompelekea kiasi kikubwa cha dhahabu kutoka Afrika kwa ajili ya kupamba hekalu alilokamilisha.

    Usiulizd iwapo alikua anatozwa kodi kwani yeye ndie alikuwa mtawala wa himaya yake kwahiyo asingeweza kutozwa kodi...na utawala wake ulidumu kwa miaka 40

    Uchaguzi wa Busara wa Sulemani kwa kumwomba Bwana “Moyo adili wa kuwahukumu watu wako” ulisababisha idhini ya Bwana na utoaji wa "moyo wa hekima na ufahamu" na kuongezewa "utajiri na heshima "

    Mhhhhhh...............yumkini kama nilivyosema si rahisi sana kumsimulia Sulemani na kuna vyanzo vingi ambavyo kila mtu anaweza kuibuka na chake walau nimeokoteza kwa vyanzo vya uhakika na kwa kuwa ni simulizi tutaendelea kuimani tu maana HATUKUWEPO................

    Mada hii itaendelea kuboreshwa kwa kadri ya vyanzo vingine....
    ..
    MACHACHE KUHUSU MFALME MKWASI ZAIDI DUNIANI KUNA HISTORIA ambazo ukitaka kuandika unaweza kuchukua siku mbili za kutafakari uanze wapi na au uishie wapi.....Mfalme Sulemani ni mmoja wapo............. Mama wa Sulemani (BATH-SHEBA) alikuwa tayari ni mke wa mtu (URIA MHITI) huyu URIA alikuwa askari wa mfalme DAUDI. so mfalme DAUDI aliponogewa na penzi la BATH SHEBA akafanya mbinu za kifo cha URIA vitani. ......umewahi kuwaza kwamba unahangaika na familia moja tu dhidi ya mtu anayetajwa kuwa na wenza 700 na masuria 300...hujahesabu watoto, wajakazi, shangazi, mjomba, wajukuu, nk wanaovinjari kila siku katika hemaya zake........tunaambiwa kwamba chakula kilicholiwa kwa siku moja kilikuwa magunia 240 ya unga, magunia 480 ya chakula, ng'ombe kumi kwa nyama choma, ng'ombe ishirini wa mchuzi, kondoo mia moja, ndege na wanyama wengine wa aina mbalimbali .......... unahangaika kutafuta mufu wa dhahabu ilihali mwenzako anapokea tani 30 za dhahabu kila mwaka .........Kwa mwaka mmoja pekee alikuwa anapokea tani si chini ya 30 ya vipande bora vya dhahabu ukiachilia mbali Vito na Madini mengine....kila nakshi na chombo ndani ya nyumba ya Sulemani ilikua ni DHAHABU tupu maana nyakati hizo madini ya fedha yalithaminishwa kwa kiwango cha vumbi dhidi ya dhahabu.... Jumba la Hukumu la Sulemani lilikuwa kubwa na lilijengwa na mwerezi na kuzungushwa na pembe zilizofunikwa na dhahabu na kusimamiwa na simba ........... Katika ukuta kulikuwa kumewekwa ngao 500 za dhahabu .................hata vyombo vya kunywea na sahani zilizokuwa kwenye nyumba hii kuu zilikuwa za “dhahabu”. Shaba “ haikuwa kitu cha kuhesabiwa katika siku za Sulemani”.................Pia alianzisha shamba la kifalme na mbuga yenye maziwa bandia, shamba la maua na matunda Wana-ikiolojia wamepata ushahidi dhabiti wa majengo ya Sulemani kote nchini hasa Hazori, Megido na Gezeri, mabaki ambayo yanatoa ushahidi wa ukweli wa 1 Wafalme 9:15. Megido ni muhimu kwa vibanda vyake vya magari ya farasi 450. Jeshi kubwa la Sulemani lilihitaji jengo lenye vibanda 4,000 vya farasi na vilijengwa karibu na mipaka ya Israeli na kulindwa na waendeshaji magari ya farasi.. Sulemani alipata faida kwani Israeli ilikuwa sehemu nzuri katikati mwa bara la Asia na Afrika. Alitawala njia za kaskazini na kusini na kwa usaidizi wa Wafoeniki, alijenga meli nyingi pale Esion-geberi ili zitumike kubeba shaba iliosafishwa na bidhaa zingine. Meli hizi zilifanya safari ya kusini hadi Ethiopia, Yemen na India Arabian mara moja kila miaka mitatu, na kuleta dhahabu, fedha, na pembe, nyani na tausi Sulemani pia aliendeleza viwanda vya kusafisha chuma, pamoja na kuchimba madini katika Araba, kusini mwa Bahari ya Chumvi, na kiwanda kikubwa cha kuyeyusha vyuma cha Esion-geberi, mahali ambapo palikuwa bandari karibu na Bahari ya Shamu. Kwa Mujibu wa wanahistoria.. Mansa Musa mfalme wa Mali empire... Ndio Binadamu alie wahi kuwa tajir Dunia nzima mpaka leo hamna mtu alie wahi fikia Utajir wake.. (wakati anaenda hiji macca alipitia misri .. Na kusabisha uchumi wao kuyumba kutokana na dhahabu alizo tumia Pale misri)... UKWELI NI KWAMBA MANSA MUSA aliyetawala kati ya mwaka 1312-1337 na utajiri wake ulikadiriwa kufikia USD billion 400 ILIHALI Mfalme Sulemani alikuwa na utajiri unaokadiriwa kufikia dollar za kimarekani trillion 2.1.......Mansa Kankan Mussa ni tajiri wa kwanza katika kipindi cha baada ya Yesu. Wenyewe wanaita Anno Domino (AD) Hata Nathaniel Rothchild Family ( zikiwepo rockerfeller, morgan na du pont family yaani FAMILI NZIMA) Utajiri wao haufikii hata theluthi ya Mfalme Sulemani (dola bilioni 600 tu) Wingi wa wake za Sulemani unahalasiha kutapanyika kwa kiazazi chake karibu kote duniani, yasemekana hata hawa wahabeshi wa Somalia, Watusi wa Rwanda na wa Iraq wa Tanzania ni mbegu yake huyo jamaa baada ya kumgaragaza malkia wa Ethiopia ( QUEEN OF SHEBA) alivyompelekea kiasi kikubwa cha dhahabu kutoka Afrika kwa ajili ya kupamba hekalu alilokamilisha. Usiulizd iwapo alikua anatozwa kodi kwani yeye ndie alikuwa mtawala wa himaya yake kwahiyo asingeweza kutozwa kodi...na utawala wake ulidumu kwa miaka 40 Uchaguzi wa Busara wa Sulemani kwa kumwomba Bwana “Moyo adili wa kuwahukumu watu wako” ulisababisha idhini ya Bwana na utoaji wa "moyo wa hekima na ufahamu" na kuongezewa "utajiri na heshima " Mhhhhhh...............yumkini kama nilivyosema si rahisi sana kumsimulia Sulemani na kuna vyanzo vingi ambavyo kila mtu anaweza kuibuka na chake walau nimeokoteza kwa vyanzo vya uhakika na kwa kuwa ni simulizi tutaendelea kuimani tu maana HATUKUWEPO................ Mada hii itaendelea kuboreshwa kwa kadri ya vyanzo vingine.... ..
    Love
    Like
    3
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·1χλμ. Views
  • Nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon aliyewahi kucheza klabu ya FC Barcelona ya Hispania Samuel Eto’o (43) akiwa na Klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi, aliweka rekodi ya Mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa Duniani kati ya mwaka 2011 na 2013.

    Eto’o alikuwa akilipwa pauni 365,000 kwa wiki ambazo ni takribani Shilingi Bilioni 1.1 za Kitanzania na alipewa Ndege binafsi (Private Jet) ambayo aliweza kusafiri kila siku kutoka Makhachkala kwenda Moscow ambapo ni umbali wa (1,910 KM) kwa mujibu wa Mkataba wake.

    Samuel Eto’o hadi anaachana na Klabu hiyo, alikuwa kacheza jumla ya mechi (73), kafunga mabao (36), Pasi saidizi (assist) 16. Cha kushangaza zaidi kwa sasa Klabu hiyo haipo kabisa imefilisika na Juni 2022 ilipoteza rasmi leseni ya Klabu baada ya kupitia matatizo ya kifedha na kushindwa kucheza mchezo wowote.

    Nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon aliyewahi kucheza klabu ya FC Barcelona ya Hispania Samuel Eto’o (43) akiwa na Klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi, aliweka rekodi ya Mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa Duniani kati ya mwaka 2011 na 2013. Eto’o alikuwa akilipwa pauni 365,000 kwa wiki ambazo ni takribani Shilingi Bilioni 1.1 za Kitanzania na alipewa Ndege binafsi (Private Jet) ambayo aliweza kusafiri kila siku kutoka Makhachkala kwenda Moscow ambapo ni umbali wa (1,910 KM) kwa mujibu wa Mkataba wake. Samuel Eto’o hadi anaachana na Klabu hiyo, alikuwa kacheza jumla ya mechi (73), kafunga mabao (36), Pasi saidizi (assist) 16. Cha kushangaza zaidi kwa sasa Klabu hiyo haipo kabisa imefilisika na Juni 2022 ilipoteza rasmi leseni ya Klabu baada ya kupitia matatizo ya kifedha na kushindwa kucheza mchezo wowote.
    Like
    Love
    4
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·593 Views
  • Nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon aliyewahi kucheza klabu ya FC Barcelona ya Hispania Samuel Eto’o (43) akiwa na Klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi, aliweka rekodi ya Mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa Duniani kati ya mwaka 2011 na 2013.

    Eto’o alikuwa akilipwa pauni 365,000 kwa wiki ambazo ni takribani Shilingi Bilioni 1.1 za Kitanzania na alipewa Ndege binafsi (Private Jet) ambayo aliweza kusafiri kila siku kutoka Makhachkala kwenda Moscow ambapo ni umbali wa (1,910 KM) kwa mujibu wa Mkataba wake.

    Samuel Eto’o hadi anaachana na Klabu hiyo, alikuwa kacheza jumla ya mechi (73), kafunga mabao (36), Pasi saidizi (assist) 16. Cha kushangaza zaidi kwa sasa Klabu hiyo haipo kabisa imefilisika na Juni 2022 ilipoteza rasmi leseni ya Klabu baada ya kupitia matatizo ya kifedha na kushindwa kucheza mchezo wowote.

    Nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon aliyewahi kucheza klabu ya FC Barcelona ya Hispania Samuel Eto’o (43) akiwa na Klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi, aliweka rekodi ya Mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa Duniani kati ya mwaka 2011 na 2013. Eto’o alikuwa akilipwa pauni 365,000 kwa wiki ambazo ni takribani Shilingi Bilioni 1.1 za Kitanzania na alipewa Ndege binafsi (Private Jet) ambayo aliweza kusafiri kila siku kutoka Makhachkala kwenda Moscow ambapo ni umbali wa (1,910 KM) kwa mujibu wa Mkataba wake. Samuel Eto’o hadi anaachana na Klabu hiyo, alikuwa kacheza jumla ya mechi (73), kafunga mabao (36), Pasi saidizi (assist) 16. Cha kushangaza zaidi kwa sasa Klabu hiyo haipo kabisa imefilisika na Juni 2022 ilipoteza rasmi leseni ya Klabu baada ya kupitia matatizo ya kifedha na kushindwa kucheza mchezo wowote.
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·555 Views
  • Ndege mzur na mwenyenguvu kama huyu,,,nae anatafta katika rizki yake,,,kwann tusiongeze juhud tuzifikie zetu.
    Ndege mzur na mwenyenguvu kama huyu,,,nae anatafta katika rizki yake,,,kwann tusiongeze juhud tuzifikie zetu.
    Love
    2
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·382 Views
Αναζήτηση αποτελεσμάτων