OPERATION ENTEBBE -3
Siku ya July 3 mwaka huo 1976 saa 12 na nusu ya jioni takribani masaa kadhaa kabla ya kufikia deadline ya mwisho waliyopewa na watekaji (July 4), Waziri mkuu wa Israel Yitzhak Rabin alitia saini nyaraka ya kuidhinisha oparesheni ya kijeshi ya uokozi (rescue mission) ambayo iliwasilishwa mezani na Meja Jenerali Yekutiel Adam (maarufu kwa jina la “Kuti”) na Brigedia Generali Dan Shomron. Pia kwa mujibu wa nyaraka hiyo iliyosainiwa na Waziri mkuu, Shomron aliteuliwa kuwa Kamanda wa utekelezaji wa Oparesheni.
Baada ya oparesheni hii kuidhinishwa rasmi na Baraza la Mawaziri muda huo nilioutaja hapo juu, Meja Jenerali Yekutiel Adam na Brigedia Generali Dan SHomron walikusuka kikosi cha kijeshi kwa ajili ya kutekeleza oparesheni hiyo kama ifuatavyo;
The Ground Command
Hiki kilikuwa ni kikosi (japo sio kikosi haswa) ambcho kilikuwa na watu wawili tu, Brigedia Generali Dan Shomron na mwakilishi wa jeshi la Anga la Israel Kanali Ami Ayalon na watu wachache wa masasiliano ya jeshi. Kikosi hiki ndicho ambacho kilikuwa na amri ya mwisho juu ya nini wanajeshi walikuwa wanatakiwa kufanya pindi wakakapoanza utekelezaji wa oparesheni.
The Asault Team
Timu hii ilipewa kazi ya kuvamia jengo la uwanja wa ndege ambalo mateka walikuwa wanashikiliwa na kuokoa mateka wote waliomo humo.
Kikosi hiki kilikuwa na wanajeshi 29 ambacho kiliongozwa na Luteni Kanali Yonathan Netanyahu (kaka yake Waziri Mkuu wa sasa wa Israel, Benjamin Netanyahu). Kikosi hiki kilijumuisha makomando wenye weledi wa hali juu kutoka katika kitengo maalumu cha jeshi la Israel kiitwacho SAYERET MATKAL.
Nieleze kidogo kuhusu Sayet Matkal.
Hiki ni kikosi cha weledi maalumu (special force) ndani ya jeshi la Israel la IDF. Makomando wanofuzu kutumika katika kikosi hiki, licha ya kupata mafunzo yote ya kijeshi kama wanajeshi wengine lakini wanaongezewa mafunzo mengine adhimu zaidi kuwafanya waweze kutekeleza oparesheni hata katika mazingira ambayo kwa akili ya kijeshi ya kawaida inaonekana kwamba hakuna uwezekano wa kufanikiwa kwa oparesheni hiyo.
Mfano wa mafunzo haya adhimu ambayo wanapatiwa ni pamoja na ukusanyaji wa intelijensia, kufanya ‘deep recon’ (nimekosa Kiswahili chake) katika uwanja wa vita, upenyezaji wa intelijensia za kimkakati (strategic intelligence) mafunzo adhimu ya counterterrorism pamoja na uokozi wa mateka nje ya mipaka ya Israel.
Kwa namna fulani ili kukielewa kikosi hiki unaweza kukifananisha na kikosi cha SAS kwenye jeshi la nchi ya Uingereza japo vinatofauti fulani bado. Ila kwa ufupi huo ndio muonekano wa Sayeret Matkal na shughuli zake.
The securing Element
Kikosi hiki kiligawanywa katika vikundi vidogo vidogo vitatu ili kuleta ufanisi.
1.Paratroopers – hawa waliongozwa na Kanali Matan Vilnai. Kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha hakuna shughuli zozote zinaendelea ndani ya uwanja wa ndege wa Entebbe qawakati ambao oparesheni hiyo inatekelezwa. Pia walikuwa wanatakiwa kuhakikisha kuwa njia ya kurukia ndege (runway) iko ‘clear’ muda wote. Pamoja na hayo kikosi hiki pia walikuwa ndio wanaowajibika kulinda ndege za kijeshi za Israel muda wote zinatakapo kuwa kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe pamoja na ujazaji mafuta.
2. The Golani Force – kikundi hikicha kijeshi kiliongozwa na Kanali Uri Sagi. Kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa yale madege makubwa aina ya Lockheed Harcules C-130. Pia walitakiwa kuyasogeza madege hayo karibu kabisa na terminal ambayo mateka walikuwepo ili waweze kuwapakia pindi ambapo uokozi ukiwa umefanikiwa. Lakini pia kikundi hiki kilifanya kazi kama ‘kikosi’ cha akiba endapo ambapo kungetoke dharura ya upungufu katika kikosi kingine.
3. The Sayeret Matkal Force – kikosi hiki nacho pia kama ilivyo kwa ‘Assault Team’ ambayo nimeiongelea hapo juu, nacho pia kiliundwa na makomando wa Sayeret Matkal na kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha kuwa hakukuwa na ‘interception’ yoyote kutoka kwenye jeshi la anga la Uganda na kuwa tayari kuwazuia na kuzuia shambulizi lolote la kijeshi ikitokea kwamba wanajeshi wa Uganda walioko uwanja wa ndege wakiomba msaada kutoka kambi ya jeshi iliyoko ndani ya jiji la Entebbe.
Kwa ujumla huo ndio ulikuwa muonekano kamili wa Kikosi kizima na majukumu ya wanajeshi wote waliohusia katika oparesheni ya uokozi kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe.
USIKU WA TAREHE 3 JULY, 1976
Hatimaye siku ya siku ikawadia, saa lililotarajiwa likafika. Ndege nne kubwa aina ya Lockheed Harcules C-130 zikiwa zimebea zaidi ya makomando 200 pamoja na ile gari Mercedes Limousine (pamoja na gari nyingine aina ya Land Rover) ambayo Ehud Barak alipendekeza waje nayo, ziliruka kutoka kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi ulioko eneo la Sharm El Sheikh mpakani kabisa na Misri.
Ndege hizi nne kubwa Lockheed Harcules C-130 zilisindikizwa nyuma na ndege mbili aina ya Boeing 707 ambazo moja ilikuwa imelengwa kutumiwa kama ‘command post’ na nyingine itumike kama hospitali kutibu majeruhi ambao watatokana na mapambano ya risasi ambayo walikuwa wanayategemea kati yao na watekaji pamoja na jeshi la Uganda.
Ndege ziliruka katika njia ya kimataifa kupita Red sea na kwa muda mwingi wa safari yake zililazimika kuruka si zaidi ya mita 30 angani (kuna muda inaelezwa kuwa iliwabidi kuruka mpaka futi 35 kutoka ardhini) ili kuepuka kuonekana na rada za Misi, Sudan na Saud Arabia.
Safari ilikuwa ngumu haswa hasa ukizingatia kuwa ndege kubwa kama zile zikiruka katika usawa wa karibu hivyo na ardhi mtikisiko unakuwa mkubwa haswa ndani ya ndege.
Waliokaribia mchepuko wa kusini wa Red Sea ndege zilikata kona na kupita kusini mwa nchi ya Djibouti. Kutokea hapo walielekea mpaka kutokea kaskazini mashariki mwa Nairobi, Kenya na kisha Somalia na kupita eneo la Ogaden nchini Ethiopia.
Kutoka hapo wakapinda magharibi kufuata bonde la ufa ba mpaka kutokea juu ya ziwa Victoria.
Ikumbukwe kwamba kati ya ndege zile mbili za Boeing 707 zilizokuwa zinafuatia nyuma na zile Harcules nne, moja ambayo ilipangwa itumike kama hospitali ilitua Nairobi, uwanja wa ndege wa Jomo Kenyetta. Ile nyingine ambayo nimeeleza kwamba ilipangwa itumike kama ‘command post’ ilikuwa inaruka kuzunguka uwanja wa ndege wa Entebbe wakati ndege zile za kijeshi zikitua. Ndege hii (command post) haikutua uwanjani na kamanda mkuu wa oparesheni hii Meja Jenerali Yekutiel Adam alikuwa ndani yake kuwaongoza wenzake walipo ardhini.
Mnamo saa 23:00 ndege za kijeshi za Israel zilitua kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe huku milango ya nyuma ya mizigo kwenye ndege ikiwa wazi.
Hapa nieleze kidogo…
Mbinu kuu ambayo jeshi la Israel walikuwa wanataka kuitumia ili kufanikisha Oparesheni hii ilikuwa ni kufanya shambulio la kushtukiza. !
Kivipi?
Katika sehemu iliyopita nilieleza kuwa Ehud Barak baada ya kukusanya intelijensia za kutosha akiwa Kenya, aliwaeleza wenzake kuwa wapakie gari aina ya Mercedes Limousine inayofanana kabisa na ile ambayo inatumiwa na Rais Idd Amin a Uganda ambayo ilikuwa na rangi nyeusi.
Kwa kuwa walifahamu Rais Idd Amin alikuwa safarini nchini Mauritius kukabidhi uenyekiti wa O.A.U, hivyo walitaka kuigiza kana kwamba Idd Amin alikuwa anarejea kutoka safarini na alikuwa anaenda kutembelea mateka pale uwanja wa ndege kama ambavyo ilikuwa kawaida yake. Hii ndio sababu ya wao kwenda na ile gari nyeusi aina ya Mercedes Limousine pamoja na Land Rover… ambavyo ndivyo ilikuwa namna ambavyo Idd Amin alikuwa anapenda kwenda kutembelea pale uwanjani…. Mercedes Limousine ambayo ina mbeba yeye na nyuma yake gari aina ya Land Rover iliyo na walinzi wake.
Kwa hiyo ndege ya kwanza ya jeshi la Israel ilipotua kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe ambao kwa muda huo wa saa tano usiku kulikuwa na giza tupu taa zote za uwanja wa ndege zikiwa zimezimwa. Ndege ilitua ikiwa imefunguliwa mlango wa nyuma wa mizigo, ambako ilitoka gari aina ya Mercedes Limousine ikiongozana na Landa Rover na moja kwa zikaendeshwa kuelekea kwenye geti la Terminal ambayo mateka walikuwa wamehifadhiwa.
Walikuwa wamefaulu kuigiza kabisa msafara wa Idd amin unavyokuwa. Msafara ulikuwa unafanana kabisa na ule wa Idd Amin lakini tofauti ilikuwa kwamba gari hizi ndani yake kuliwa na makomamdo.
Jambo la ajabu ni kwamba walipofika mbele ya geti la Terminal badala ya kuruhusiwa kupita, wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanalinda getini waliinua bunduki zao na kuwanyoosha kuelea magari haya.
Walichokuwa hawakijua makomando hawa ambacho wanajeshi hawa waliokuwa wanalinda hapa uwanjani walikijua ni kwamba, Siku moja ya kabla ya Idd Amin kwenda Mauritus alibadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi kwenda rangi nyeupe.
Kwa hiyo wanajeshi hawa wa Uganda walipoona magari haya walikuwa wanajua fika kuwa huyu hakuwa Rais wao Idd Amin.
Itaendelea
#TheBOLD_JF