• SACKED

    Fadlu Davids ameondoka Simba SC

    Uamuzi umefanywa na kukubaliwa, faili lake limefungwa.

    Kocha huyo raia wa Afrika Kusini alikeisha ifahamisha klabu hiyo msimamo wake baada ya kupoteza imani na kutojihisi salama tena kufuatia matamshi ya vitisho kutoka kwa baadhi ya viongozi wa juu wa klabu ya Simba SC Tanzania.

    FADLU anaona kwa usalama wake binafsi haupo na amepoteza kujiamini ndani ya klabu hiyo.
    Kocha FADLU ataondoka pamoja na benchi lake lote la ufundi isipokuwa kocha Seleman Abdallah Matola

    Thank you Fadlu

    Ozil Kiiza Morris
    Kita A Kita
    SACKED Fadlu Davids ameondoka Simba SC Uamuzi umefanywa na kukubaliwa, faili lake limefungwa. ✍️ Kocha huyo raia wa Afrika Kusini alikeisha ifahamisha klabu hiyo msimamo wake baada ya kupoteza imani na kutojihisi salama tena kufuatia matamshi ya vitisho kutoka kwa baadhi ya viongozi wa juu wa klabu ya Simba SC Tanzania. FADLU anaona kwa usalama wake binafsi haupo na amepoteza kujiamini ndani ya klabu hiyo. Kocha FADLU ataondoka pamoja na benchi lake lote la ufundi isipokuwa kocha Seleman Abdallah Matola Thank you Fadlu Ozil Kiiza Morris Kita A Kita
    0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·68 Visualizações
  • Ameandika Mtangazaji wa kabumbu Nazareth Upete

    Sikutaka kuandika update yoyote ya Fadlu kwa Jana kwa sababu Simba walikuwa na mechi ngumu, muhimu na serious zaidi ambayo isingekuwa vyema kuandika chochote chenye mapelekeo yoyote hasi kwa mtu yoyote anayehusiana na Simba SC.

    THE SAGA…!
    Tarehe 07/09 siku 3 kabla ya Simba Day kuna mtu ninayemwamini sana kutoka Morocco alinipatia taarifa ya Fadlu kuridhiana na klabu ya Raja Casablanca kwenda kuhudumu hapo…!

    Pamoja na kutoachana vyema sana na Raja akiwa Kocha msaidizi haikuwarudisha nyuma huku inaelezwa Wydad pia waliulizia upatikanaji wake lakini mkataba wa Raja ulikuwa na sababu nyingi za kuridhiwa kuliko kukataliwa.

    Tarehe 11 baada ya Simba Day, Wydad walikuwa serious kuulizia taarifa za Fadlu kwa baadhi ya watu hususani mwenendo wake kwenye maeneo yote ya msingi…! Wakataka kuingilia kati deal.

    Bado Ofa ya Raja ikasimama kiume…! Fadlu yupo tayari kuibeba Ofa ya Raja na project yao ya #BringBackCasablanca⚽️

    Wakati hali ikiwa hivyo inaelezwa mmoja wa wasaidizi wake anataka kusalia Msimbazi akiamini project yao italipa punde!

    Inaelezwa Fadlu anahisi kuna vitu havipo sawa na zigo la lawama analitupa kwa uongozi wa timu huku yeye akitafuta mlango wa kutokea!

    Kwa sasa kuna urafiki wa mashaka baina ya pande mbili na Simba wamefanya kila kitu kumbakisha ila msimamo wa Fadlu umebebwa mazima na Ofa za waManga pale Morocco

    95% mechi ya Jana ilikuwa ya mwisho kwa Fadlu kama Kocha wa Simba na sasa kilichobaki ni yeye tu awalipe Simba SC kuvunja mkataba ingali analazimisha wamruhusu aende Free!

    MTAZAMO WANGU!?
    Simba hawatakuwa na Pengo kuondoka kwa Fadlu…! Amefanya kazi nzuri ila makocha ni wengi sana barani Afrika! Kikubwa ni kutuliza Kichwa wakati wa uchaguzi wa Kocha na kuachana na % za maslahi.

    Fadlu ni Kocha mzuri ila kwa mtazamo wangu pengo linazibika…! Bahati nzuri hajacheza mechi yoyote ya Ligi…! Yoyote atakayekuja ni rahisi tu kuendeleza kitu bora kwa sababu wachezaji Quality yao sio ya kubeza!

    Salaaam!
    Ameandika Mtangazaji wa kabumbu Nazareth Upete ✍️ Sikutaka kuandika update yoyote ya Fadlu kwa Jana kwa sababu Simba walikuwa na mechi ngumu, muhimu na serious zaidi ambayo isingekuwa vyema kuandika chochote chenye mapelekeo yoyote hasi kwa mtu yoyote anayehusiana na Simba SC. THE SAGA…! Tarehe 07/09 siku 3 kabla ya Simba Day kuna mtu ninayemwamini sana kutoka Morocco alinipatia taarifa ya Fadlu kuridhiana na klabu ya Raja Casablanca kwenda kuhudumu hapo…! Pamoja na kutoachana vyema sana na Raja akiwa Kocha msaidizi haikuwarudisha nyuma huku inaelezwa Wydad pia waliulizia upatikanaji wake lakini mkataba wa Raja ulikuwa na sababu nyingi za kuridhiwa kuliko kukataliwa. Tarehe 11 baada ya Simba Day, Wydad walikuwa serious kuulizia taarifa za Fadlu kwa baadhi ya watu hususani mwenendo wake kwenye maeneo yote ya msingi…! Wakataka kuingilia kati deal. Bado Ofa ya Raja ikasimama kiume…! Fadlu yupo tayari kuibeba Ofa ya Raja na project yao ya #BringBackCasablanca⚽️ Wakati hali ikiwa hivyo inaelezwa mmoja wa wasaidizi wake anataka kusalia Msimbazi akiamini project yao italipa punde! Inaelezwa Fadlu anahisi kuna vitu havipo sawa na zigo la lawama analitupa kwa uongozi wa timu huku yeye akitafuta mlango wa kutokea! Kwa sasa kuna urafiki wa mashaka baina ya pande mbili na Simba wamefanya kila kitu kumbakisha ila msimamo wa Fadlu umebebwa mazima na Ofa za waManga pale Morocco ✍️ 95% mechi ya Jana ilikuwa ya mwisho kwa Fadlu kama Kocha wa Simba na sasa kilichobaki ni yeye tu awalipe Simba SC kuvunja mkataba ingali analazimisha wamruhusu aende Free! MTAZAMO WANGU!? Simba hawatakuwa na Pengo kuondoka kwa Fadlu…! Amefanya kazi nzuri ila makocha ni wengi sana barani Afrika! Kikubwa ni kutuliza Kichwa wakati wa uchaguzi wa Kocha na kuachana na % za maslahi. Fadlu ni Kocha mzuri ila kwa mtazamo wangu pengo linazibika…! Bahati nzuri hajacheza mechi yoyote ya Ligi…! Yoyote atakayekuja ni rahisi tu kuendeleza kitu bora kwa sababu wachezaji Quality yao sio ya kubeza! Salaaam!
    0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·57 Visualizações
  • Ofa ya klabu ya £25m ya Real Betis ilikubaliwa na Man United Kuhusu kumsajili Antony na tayari Man United ilimpa ruhusa Antony kusafiri kuelekea Spain

    Lakini saa chache baadae Real Betis imebadilishaa msimamo wake na kujiondoa kwenye mazungumzo wakidai kuwa mshahara wa Antony ni mkubwa hivyo hawataweza vinginevyo Man United wapungize Bei ya Antony au Antony apunguze Mshahara wake. .

    Source Ben Jacobs

    #SportsElite
    🚨 Ofa ya klabu ya £25m ya Real Betis ilikubaliwa na Man United Kuhusu kumsajili Antony na tayari Man United ilimpa ruhusa Antony kusafiri kuelekea Spain Lakini saa chache baadae Real Betis imebadilishaa msimamo wake na kujiondoa kwenye mazungumzo wakidai kuwa mshahara wa Antony ni mkubwa hivyo hawataweza vinginevyo Man United wapungize Bei ya Antony au Antony apunguze Mshahara wake. 🥴🇧🇷. Source Ben Jacobs #SportsElite
    0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·382 Visualizações
  • Msimamo wa La Liga kwa sasa
    🚨🚨Msimamo wa La Liga kwa sasa 👇👇👇👇
    0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·90 Visualizações


  • Mchezaji Marcus Rashford ameendelea kubaki na msimamo wake wa kutaka kujiunga na Club ya Barcelona katika msimu huu wa kiangazii Richa ya kuwa timu ya Juventus, bayern Munich, Chelsea na Liverpool kuonekana zinamwitajii lakn ameendelea kusimamia msimamo wake wa kwenda club ya Barcelona


    #SportsElite
    Mchezaji Marcus Rashford ameendelea kubaki na msimamo wake wa kutaka kujiunga na Club ya Barcelona katika msimu huu wa kiangazii Richa ya kuwa timu ya Juventus, bayern Munich, Chelsea na Liverpool kuonekana zinamwitajii lakn ameendelea kusimamia msimamo wake wa kwenda club ya Barcelona #SportsElite
    0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·431 Visualizações
  • Nguvu inayo badilisha mtu .

    Warumi 12:2
    [2]*Wala msiifuatishe namna ya dunia hii;
    *bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu*

    Kama ukiwachukua watu wasili wanao waza sawa tunategemea matokeo yatakuwa sawa.

    Iko nguvu inaitwa neno la Mungu inayo weza badilisha mtu kama tu mtu akijua jinsi Mungu anavyo taka aenende .

    Kiwango chako cha kumjua Mungu katika neno lazima kiendane na matokeo kwani chochote apandacho mtu ndicho atakacho vuna.

    Wagalatia 6:7
    [7]Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.


    faida za kulijua neno kama nguvu inayo badilisha mtu .

    1.INATUHAKIKISHIA KUFNIKIWA.

    Mungu amehakikisha kila anaye mjua sawa sawa na neno anampa nguvu ya kufanikiwa.

    Zaburi 1:1-2
    [1]Heri mtu yule asiyekwenda
    Katika shauri la wasio haki;
    Wala hakusimama katika njia ya wakosaji;
    Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

    [2]Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,
    Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

    Lazma uamue kuishi maisha yasiyo na mizaa kabisa na dhambi kwa kulifuata neno kama mwongozo wako hapo ndipo utampendeza Mungu na Mungu atajihakikishia kukuwazia mema na mafanikio.

    Isaya 55:8-9
    [8] *Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.*
    .
    [9]Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.

    Mawazo ya mungu ni kuona ndoa yako inafanikiwa toka ujana wako mpaka uzee.

    Mawazo ya Mungu nikuona biashara yako inashine kuliko jana .

    Mawazo ya Mungu ni kukuona ukiishi maisha ya mafanikio na furaha siku zote za maisha yako .

    Yeremia 29:11
    [11] *Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.*

    Tatizo lako ni moja umeichukulia mzaa dhambi na kufanya mawazo ya Mungu kwako yasitimie .

    Acha dhambi acha mzaa na zinaa kutoka kusema hii ndo zambi yetu vijana anza kuichukia totally maisha yako yatabadilika totally na Mungu atakuhakikishia mafanikio siku zote.

    Mafanikio ni hakika na kweli kabisa kwa mtu anaye kaa na neno, mtu ambaye katika kila jambo anajibu na kulitazama neno linasema nini lazima apokee mafanikio makubwa zaidi.

    2.inatusaidia kutoka katika mawazo na fikra hasi

    Mtu hawezi kufanikiwa zaidi ya vile anavyo amini .

    Mtu awezi kupokea uponyaji zaidi ya vile anavyo hitaji.

    Kiwango cha mafanikio yako kinaamuliwa na kiwango cha imani yako .

    Marko 9:23
    [23]Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.

    Ukiweza kuwekeza katika neno neno litakupa matokeo ya mwilini kwani neno litakusaidia kujua jinsi gani watu walio tembea na mungu walifanikiwa .

    Utaacha kuona haiwezekani kila jambo utaanza kuona inawezekana kila jambo kwani utajua yeye anasemaji.

    Wafilolipi 4:13
    *Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu*

    Ko ni neno litabadilisha msimamo wako juu ya mawazo hasi juu ya mafanikio .

    Kwa maana mtu hawezi kuwa zaidi ya anavyo jiona.

    Mithali 23:7
    [7] *Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo*.
    Akuambia, Haya, kula, kunywa;
    Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.

    Neno pekee ndilo linaweza badilisha namna unavyo jiona na jinsi unavyo amini ili upokee mambo makubwa .

    Usidanganyikee mtu hawezi kupokea zaidi ya ufunuo alio upata katika neno husika .

    Nimatumaini yangu utaanza kuongeza imani katika neno ili upate nguvu ibadilishayo mtu .

    Take care, naitwa sylvester natokea kutoka (build new eden)

    Karubu tujifunze pamoja neno la Mungu .kupitia group la watsap

    https://chat.whatsapp.com/IxkPEsnxi02ExNGrlmbWR4

    #restore men position
    #build new position
    Nguvu inayo badilisha mtu . Warumi 12:2 [2]*Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; *bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu* Kama ukiwachukua watu wasili wanao waza sawa tunategemea matokeo yatakuwa sawa. Iko nguvu inaitwa neno la Mungu inayo weza badilisha mtu kama tu mtu akijua jinsi Mungu anavyo taka aenende . Kiwango chako cha kumjua Mungu katika neno lazima kiendane na matokeo kwani chochote apandacho mtu ndicho atakacho vuna. Wagalatia 6:7 [7]Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. faida za kulijua neno kama nguvu inayo badilisha mtu . 1.INATUHAKIKISHIA KUFNIKIWA. Mungu amehakikisha kila anaye mjua sawa sawa na neno anampa nguvu ya kufanikiwa. Zaburi 1:1-2 [1]Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. [2]Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Lazma uamue kuishi maisha yasiyo na mizaa kabisa na dhambi kwa kulifuata neno kama mwongozo wako hapo ndipo utampendeza Mungu na Mungu atajihakikishia kukuwazia mema na mafanikio. Isaya 55:8-9 [8] *Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.* . [9]Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Mawazo ya mungu ni kuona ndoa yako inafanikiwa toka ujana wako mpaka uzee. Mawazo ya Mungu nikuona biashara yako inashine kuliko jana . Mawazo ya Mungu ni kukuona ukiishi maisha ya mafanikio na furaha siku zote za maisha yako . Yeremia 29:11 [11] *Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.* Tatizo lako ni moja umeichukulia mzaa dhambi na kufanya mawazo ya Mungu kwako yasitimie . Acha dhambi acha mzaa na zinaa kutoka kusema hii ndo zambi yetu vijana anza kuichukia totally maisha yako yatabadilika totally na Mungu atakuhakikishia mafanikio siku zote. Mafanikio ni hakika na kweli kabisa kwa mtu anaye kaa na neno, mtu ambaye katika kila jambo anajibu na kulitazama neno linasema nini lazima apokee mafanikio makubwa zaidi. 2.inatusaidia kutoka katika mawazo na fikra hasi Mtu hawezi kufanikiwa zaidi ya vile anavyo amini . Mtu awezi kupokea uponyaji zaidi ya vile anavyo hitaji. Kiwango cha mafanikio yako kinaamuliwa na kiwango cha imani yako . Marko 9:23 [23]Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. Ukiweza kuwekeza katika neno neno litakupa matokeo ya mwilini kwani neno litakusaidia kujua jinsi gani watu walio tembea na mungu walifanikiwa . Utaacha kuona haiwezekani kila jambo utaanza kuona inawezekana kila jambo kwani utajua yeye anasemaji. Wafilolipi 4:13 *Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu* Ko ni neno litabadilisha msimamo wako juu ya mawazo hasi juu ya mafanikio . Kwa maana mtu hawezi kuwa zaidi ya anavyo jiona. Mithali 23:7 [7] *Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo*. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe. Neno pekee ndilo linaweza badilisha namna unavyo jiona na jinsi unavyo amini ili upokee mambo makubwa . Usidanganyikee mtu hawezi kupokea zaidi ya ufunuo alio upata katika neno husika . Nimatumaini yangu utaanza kuongeza imani katika neno ili upate nguvu ibadilishayo mtu . Take care, naitwa sylvester natokea kutoka (build new eden) Karubu tujifunze pamoja neno la Mungu .kupitia group la watsap https://chat.whatsapp.com/IxkPEsnxi02ExNGrlmbWR4 #restore men position #build new position
    Like
    1
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·1KB Visualizações
  • Unaweza Kuwa Baba bora na Bado Ukapoteza Familia Yako
    Kwa sababu katika ulimwengu wa sasa, juhudi haimaanishi chochote ikiwa wewe ni mwanaume.
    Unaamka mapema.
    Nenda kazini.
    Unalipa kodi.
    Ubaki mwaminifu.
    Unaiombea familia.
    Bado-
    unawapoteza.
    Sio kwa sababu umeshindwa.
    Lakini kwa sababu ubaba wa kisasa umejengwa kama mtego.
    Unafanya kila kitu sawa ...
    na bado kuishia vibaya.
    Anaondoka. Watoto wanafuata. Nyumba inakuwa kumbukumbu.
    Unaendelea kulipa bili.
    Anaendelea kubadilisha simulizi.
    Na ikiwa unathubutu kupaza sauti yako?
    Wewe ni "sumu."
    Wewe "huna msimamo."
    Wewe ndiye "sababu aliondoka."
    Umelipia mpiga filimbi-
    lakini bado anaamuru wimbo.
    Ulifuata sheria. Lakini hilo ndilo tatizo.
    Kwa sababu ukifuata sheria, wewe si kiongozi.
    Ikiwa wewe ni mwaminifu, unakuwa rahisi.
    Uliambiwa umlinde.
    Kwa hivyo ulifanya.
    Uliambiwa utoe.
    Kwa hivyo ulifanya.
    Uliambiwa ukae mwaminifu.
    Kwa hivyo ulifanya.
    Na sasa?
    Umeachana.
    Una huzuni.
    Unaweza kutupwa.
    Mahakama inasema, "Wewe si baba."
    Lakini uharibifu tayari umefanywa.
    Moyo wako? Imevunjwa.
    Jina lako? Iliyotiwa rangi.
    Mkoba wako? Bado kuwajibika.
    Wanaiita “kwa manufaa ya mtoto.”
    Mtoto hatakuruhusu umuone... tangu 2019.
    Wakati huo huo, anatabasamu kwa ukimya.
    Kwa sababu tayari alishinda.
    Uongo huo ulifanya kazi.
    Mfumo ulimsaidia.
    Na jamii ikamshangilia.
    Wewe?
    Uko kwenye mtaala wako wa nne.
    Na hakuna mtu aliyepiga makofi ulivyo nusurika.
    Tuzungumze ukweli.80% ya talaka huanzishwa na wanawake.
    Uchunguzi wa DNA 1 kati ya 3 hurejea kuwa hasi.
    Maelfu ya wanaume wako korokoroni—si kwa uhalifu—
    lakini kwa kutoweza kuendelea na malipo yaliyoidhinishwa na mahakama...
    kwa watoto ambao hata si wao.
    Acha hiyo marinate.
    Unapoteza familia yako ... na bado wanakulaumu.
    "Labda alimuonya."
    "Alichagua uzuri, sio akili."
    "Hakujitambua vya kutosha."
    Kweli?
    Kwa hivyo wakati watu wa Mungu-
    Mchungaji Chris Oyakhilome, Benny Hinn,Kenneth Copeland—
    kuishia kutengana au kuachwa...
    hawakumsikia Mungu? Hawakuwa na kasi ya kutosha?
    Hawakuwa na macho ya kiroho?
    Au labda…
    labda tu…
    walioa wanawake ambao walikuwa wataalamu wa kuficha asili yao halisi.
    Hadi siku moja -
    waliamka, na kubadili.
    Hakuna onyo.
    Hakuna majuto.
    "Nimebadilika tu."
    Wanawake wa kisasa hawakuacha kwa kudanganya.
    Wanaondoka kwa sababu rekodi yako ya matukio imekwisha.
    Hujawa mtu wa njozi haraka vya kutosha.
    Hukuweza kumudu kifurushi cha maisha laini kwa ratiba.
    Kwa hiyo "hupunguza hasara zao" na kupiga risasi mitaani.
    Ulikuwa mzuri.
    Lakini ulikuwa hautoshi.
    Sio tajiri wa kutosha.
    Sio furaha ya kutosha.
    Haielekezi vya kutosha.
    Na sasa watoto wamekwenda.
    Nyumba ni kimya.
    Moyo wako umechoka.
    Na yote unayosikia ni:
    "Wanaume wa kweli hupigania familia zao."
    Kana kwamba haujatoa damu ukijaribu.
    Niseme wazi.

    Unaweza kuwa baba bora -
    na bado kupoteza.
    Sio kwa sababu haukupenda vya kutosha.
    Lakini kwa sababu upendo haujalishi tena.
    Sio kama wewe ni mwanaume.
    Wacha wapiganaji na wataalam wafurike maoni.
    Wacha wanawake waseme "sio sote."
    Waache wakanushaji waje wakibembea.

    Lakini wanaume halisi wanajua.
    Wameishi.
    Wamemwaga damu.
    Wamezika ndoto.
    Usiseme chochote.
    Andika tu "Kupitia" na uendelee.

    #ubaba
    #uanaume
    #maumivu kimya
    #utapeli wa ubaba
    #mahakama ya familia
    Unaweza Kuwa Baba bora na Bado Ukapoteza Familia Yako Kwa sababu katika ulimwengu wa sasa, juhudi haimaanishi chochote ikiwa wewe ni mwanaume. Unaamka mapema. Nenda kazini. Unalipa kodi. Ubaki mwaminifu. Unaiombea familia. Bado- unawapoteza. Sio kwa sababu umeshindwa. Lakini kwa sababu ubaba wa kisasa umejengwa kama mtego. Unafanya kila kitu sawa ... na bado kuishia vibaya. Anaondoka. Watoto wanafuata. Nyumba inakuwa kumbukumbu. Unaendelea kulipa bili. Anaendelea kubadilisha simulizi. Na ikiwa unathubutu kupaza sauti yako? Wewe ni "sumu." Wewe "huna msimamo." Wewe ndiye "sababu aliondoka." Umelipia mpiga filimbi- lakini bado anaamuru wimbo. Ulifuata sheria. Lakini hilo ndilo tatizo. Kwa sababu ukifuata sheria, wewe si kiongozi. Ikiwa wewe ni mwaminifu, unakuwa rahisi. Uliambiwa umlinde. Kwa hivyo ulifanya. Uliambiwa utoe. Kwa hivyo ulifanya. Uliambiwa ukae mwaminifu. Kwa hivyo ulifanya. Na sasa? Umeachana. Una huzuni. Unaweza kutupwa. Mahakama inasema, "Wewe si baba." Lakini uharibifu tayari umefanywa. Moyo wako? Imevunjwa. Jina lako? Iliyotiwa rangi. Mkoba wako? Bado kuwajibika. Wanaiita “kwa manufaa ya mtoto.” Mtoto hatakuruhusu umuone... tangu 2019. Wakati huo huo, anatabasamu kwa ukimya. Kwa sababu tayari alishinda. Uongo huo ulifanya kazi. Mfumo ulimsaidia. Na jamii ikamshangilia. Wewe? Uko kwenye mtaala wako wa nne. Na hakuna mtu aliyepiga makofi ulivyo nusurika. Tuzungumze ukweli.80% ya talaka huanzishwa na wanawake. Uchunguzi wa DNA 1 kati ya 3 hurejea kuwa hasi. Maelfu ya wanaume wako korokoroni—si kwa uhalifu— lakini kwa kutoweza kuendelea na malipo yaliyoidhinishwa na mahakama... kwa watoto ambao hata si wao. Acha hiyo marinate. Unapoteza familia yako ... na bado wanakulaumu. "Labda alimuonya." "Alichagua uzuri, sio akili." "Hakujitambua vya kutosha." Kweli? Kwa hivyo wakati watu wa Mungu- Mchungaji Chris Oyakhilome, Benny Hinn,Kenneth Copeland— kuishia kutengana au kuachwa... hawakumsikia Mungu? Hawakuwa na kasi ya kutosha? Hawakuwa na macho ya kiroho? Au labda… labda tu… walioa wanawake ambao walikuwa wataalamu wa kuficha asili yao halisi. Hadi siku moja - waliamka, na kubadili. Hakuna onyo. Hakuna majuto. "Nimebadilika tu." Wanawake wa kisasa hawakuacha kwa kudanganya. Wanaondoka kwa sababu rekodi yako ya matukio imekwisha. Hujawa mtu wa njozi haraka vya kutosha. Hukuweza kumudu kifurushi cha maisha laini kwa ratiba. Kwa hiyo "hupunguza hasara zao" na kupiga risasi mitaani. Ulikuwa mzuri. Lakini ulikuwa hautoshi. Sio tajiri wa kutosha. Sio furaha ya kutosha. Haielekezi vya kutosha. Na sasa watoto wamekwenda. Nyumba ni kimya. Moyo wako umechoka. Na yote unayosikia ni: "Wanaume wa kweli hupigania familia zao." Kana kwamba haujatoa damu ukijaribu. Niseme wazi. Unaweza kuwa baba bora - na bado kupoteza. Sio kwa sababu haukupenda vya kutosha. Lakini kwa sababu upendo haujalishi tena. Sio kama wewe ni mwanaume. Wacha wapiganaji na wataalam wafurike maoni. Wacha wanawake waseme "sio sote." Waache wakanushaji waje wakibembea. Lakini wanaume halisi wanajua. Wameishi. Wamemwaga damu. Wamezika ndoto. Usiseme chochote. Andika tu "Kupitia" na uendelee. #ubaba #uanaume #maumivu kimya #utapeli wa ubaba #mahakama ya familia
    Like
    Love
    2
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·2KB Visualizações
  • “Sisi tumeitwa na serikali tumekuja kusikiliza ila msimamo wa Klabu upo wazi na unafahamika ila hapa tumekuja kusikiliza na tutayabeba yale ambayo tuna uwezo nayo ambayo hatuna uwezo nayo tutayaacha, ilipofikia sio suala la maslahi ya mpira wa Tanzania bali maslahi ya Klabu yetu kwanza” - Alex Ngai, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Yanga SC.

    “Sisi tumeitwa na serikali tumekuja kusikiliza ila msimamo wa Klabu upo wazi na unafahamika ila hapa tumekuja kusikiliza na tutayabeba yale ambayo tuna uwezo nayo ambayo hatuna uwezo nayo tutayaacha, ilipofikia sio suala la maslahi ya mpira wa Tanzania bali maslahi ya Klabu yetu kwanza” - Alex Ngai, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Yanga SC.
    0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·843 Visualizações
  • Balozi wa Afrika Kusini Nchini Marekani , Ebrahim Rasool ambaye ametimuliwa na Nchi ya Marekani kutokana na kukosoa sera za Donald Trump, amerejea Afrika Kusini kwa ufakhari mkubwa na kupokewa kwa shangwe na mamia ya Wananchi waliofurika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town Nchini Afrika Kusini.

    Balozi huyo na mkewe, Rosieda, waliwasili jana katika Uwanda wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town baada ya kusafari kutoka Nchini Marekani kupitia Qatar na wamekaribishwa vyema na kwa shangwe na mamia ya Wafuasi wao. Mapema mwezi huu, Balozi Rasool alitangazwa na Serikali ya Marekani kuwa ni Mtu asiyetakiwa kuweko Nchini humo baada ya kukosoa sera za Donald Trump, hatua ambayo inaonesha wazi jinsi madai ya uhuru wa kusema yasivyothaminiwa Nchini Marekani licha ya majigambo makubwa ya Nchi Marekani ya kupigania haki za Binadamu na demokrasia.

    Akiwahutubia mamia ya Mashabiki wake kwenye Uwanja wa Ndege wa Cape Town, Balozi Rasool amesema kwamba ingawa ametakiwa kuondoka huko Marekani lakini jambo hilo limeshindwa kufikia lengo lake kwani Viongozi wa Marekani wanadhani wamemdhalilisha wakati yeye anaona fakhari kwa maneno aliyotoa na Wananchi wa Afrika Kusini nao wanajivunia msimamo huo ndio maana wamejitokea kwa mamia kumpokea kishujaa.

    "Unaporejea nyumbani na kupokewa kwa shangwe na umati kama huu wa watu, mtu unaona fakhari na unajivunia msimamo wako." alisema Rasool.

    Alipoulizwa iwapo diplomasia imeshindwa, amesema ukweli kwamba matamshi yake yamemfanya Trump na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio kuwa makini na hatua ya Serikali ya Marekani ya kumtangaza kuwa ni Mtu asiyetakiwa nchini humo ni ushahidi kwamba ujumbe wake umefika ngazi za juu kabisa za serikali ya Marekani.

    Balozi wa Afrika Kusini 🇿🇦 Nchini Marekani 🇺🇸, Ebrahim Rasool ambaye ametimuliwa na Nchi ya Marekani kutokana na kukosoa sera za Donald Trump, amerejea Afrika Kusini kwa ufakhari mkubwa na kupokewa kwa shangwe na mamia ya Wananchi waliofurika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town Nchini Afrika Kusini. Balozi huyo na mkewe, Rosieda, waliwasili jana katika Uwanda wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town baada ya kusafari kutoka Nchini Marekani kupitia Qatar na wamekaribishwa vyema na kwa shangwe na mamia ya Wafuasi wao. Mapema mwezi huu, Balozi Rasool alitangazwa na Serikali ya Marekani kuwa ni Mtu asiyetakiwa kuweko Nchini humo baada ya kukosoa sera za Donald Trump, hatua ambayo inaonesha wazi jinsi madai ya uhuru wa kusema yasivyothaminiwa Nchini Marekani licha ya majigambo makubwa ya Nchi Marekani ya kupigania haki za Binadamu na demokrasia. Akiwahutubia mamia ya Mashabiki wake kwenye Uwanja wa Ndege wa Cape Town, Balozi Rasool amesema kwamba ingawa ametakiwa kuondoka huko Marekani lakini jambo hilo limeshindwa kufikia lengo lake kwani Viongozi wa Marekani wanadhani wamemdhalilisha wakati yeye anaona fakhari kwa maneno aliyotoa na Wananchi wa Afrika Kusini nao wanajivunia msimamo huo ndio maana wamejitokea kwa mamia kumpokea kishujaa. "Unaporejea nyumbani na kupokewa kwa shangwe na umati kama huu wa watu, mtu unaona fakhari na unajivunia msimamo wako." alisema Rasool. Alipoulizwa iwapo diplomasia imeshindwa, amesema ukweli kwamba matamshi yake yamemfanya Trump na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio kuwa makini na hatua ya Serikali ya Marekani ya kumtangaza kuwa ni Mtu asiyetakiwa nchini humo ni ushahidi kwamba ujumbe wake umefika ngazi za juu kabisa za serikali ya Marekani.
    Love
    Like
    3
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·1KB Visualizações
  • Taarifa kwa umma kutoka katika klabu ya Yanga SC kuhusu msimamo wao kufuatia kughairisha kwa mchezo wao dhidi ya klabu ya Simba SC.

    - Kupewa alama tatu kwa sababu walifuata taratibu zote za mchezo huku kamati ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara ikichukua uamuzi wa kughairisha mchezo huo bila kufuata kanuni.

    - Yanga SC haitacheza mchezo mwingine shidi ya klabu ya Simba SC msimu huu Ligi Kuu Tanzania Bara (labda wakutane kombe la Shirikisho FA).

    - Klabu ya Simba SC walikuwa na haki ya kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa lakini hakufuata utaratibu wa kupewa haki hiyo kama kutoa taarifa kwa Afisa wa Uwanja, klabu ya Yanga SC ili waandaliwe mazingira ya wao kutumia Uwanja huo.

    Taarifa kwa umma kutoka katika klabu ya Yanga SC kuhusu msimamo wao kufuatia kughairisha kwa mchezo wao dhidi ya klabu ya Simba SC. - Kupewa alama tatu kwa sababu walifuata taratibu zote za mchezo huku kamati ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara ikichukua uamuzi wa kughairisha mchezo huo bila kufuata kanuni. - Yanga SC haitacheza mchezo mwingine shidi ya klabu ya Simba SC msimu huu Ligi Kuu Tanzania Bara (labda wakutane kombe la Shirikisho FA). - Klabu ya Simba SC walikuwa na haki ya kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa lakini hakufuata utaratibu wa kupewa haki hiyo kama kutoa taarifa kwa Afisa wa Uwanja, klabu ya Yanga SC ili waandaliwe mazingira ya wao kutumia Uwanja huo.
    Like
    1
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·650 Visualizações
  • Ijumaa, tarehe 28 Februari, haikuwa siku rahisi kwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alipofanya ziara katika Ikulu ya White House, Marekani. Kabla hata ya mzozo wa maneno kati yake na mwenyeji wake, Rais Donald Trump, pamoja na Makamu wa Rais JD Vance, tayari kulikuwa na ishara za mivutano.

    Trump alimkaribisha Zelensky mlangoni na kusema kwa utani: “Leo amevalia kweli kweli,” kauli ambayo iliwafanya baadhi ya waandishi wa habari kuiona kama kejeli badala ya pongezi. Wakati huo, Zelensky alikuwa amevalia fulana nyeusi ya mikono mirefu, vazi ambalo amekuwa akilivaa mara kwa mara tangu Ukraine ivamiwe na Urusi mwaka 2022.

    Baadaye, Trump alipompokea Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, alionekana kutazama mavazi yake kwa makini kutoka juu hadi chini, kisha kunong’ona maneno yanayoweza kutafsiriwa kama pongezi kwa suti rasmi aliyovaa Starmer.

    Mjadala kuhusu mavazi ya Zelensky ulizidi kupamba moto wakati wa mkutano wa waandishi wa habari. Brian Glenn, mwandishi kutoka Real America’s Voice—chombo cha habari kinachopendelea mrengo wa kulia—alimtupia swali la moja kwa moja:

    “Kwa nini hauvai suti? Upo katika ofisi ya juu kabisa katika nchi hii, na umegoma kuvaa suti – je, unamiliki hata suti?”

    Kwa utulivu, Zelensky alijibu kwa mshangao mdogo:

    “Nitavaa suti vita hivi vitakapomalizika. Labda suti kama yako, labda bora zaidi, au pengine ya bei nafuu kuliko yako,” alisema kwa utani huku akionyesha msimamo wake wa kuendelea kuvaa mavazi ya kijeshi.

    Swali hilo la Glenn liliibua mjadala mkali mitandaoni. Wengine walimuunga mkono, wakisema kwamba kiongozi wa taifa anapaswa kuvaa mavazi rasmi anapokutana na viongozi wengine, ilhali wengine waliona swali hilo kuwa la dhihaka na lisilo na umuhimu.

    Miongoni mwa waliomkosoa Glenn ni mwandishi maarufu wa Uingereza, Piers Morgan, ambaye pia ni rafiki wa karibu wa Trump. Morgan aliandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter):

    “Swali la kipuuzi. Elon Musk havai suti anapoingia Ikulu.”

    Historia pia inaonyesha kuwa si Zelensky pekee aliyeingia Ikulu ya Marekani bila suti. Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Winston Churchill, alifanya hivyo katika moja ya ziara zake rasmi.
    Ijumaa, tarehe 28 Februari, haikuwa siku rahisi kwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alipofanya ziara katika Ikulu ya White House, Marekani. Kabla hata ya mzozo wa maneno kati yake na mwenyeji wake, Rais Donald Trump, pamoja na Makamu wa Rais JD Vance, tayari kulikuwa na ishara za mivutano. Trump alimkaribisha Zelensky mlangoni na kusema kwa utani: “Leo amevalia kweli kweli,” kauli ambayo iliwafanya baadhi ya waandishi wa habari kuiona kama kejeli badala ya pongezi. Wakati huo, Zelensky alikuwa amevalia fulana nyeusi ya mikono mirefu, vazi ambalo amekuwa akilivaa mara kwa mara tangu Ukraine ivamiwe na Urusi mwaka 2022. Baadaye, Trump alipompokea Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, alionekana kutazama mavazi yake kwa makini kutoka juu hadi chini, kisha kunong’ona maneno yanayoweza kutafsiriwa kama pongezi kwa suti rasmi aliyovaa Starmer. Mjadala kuhusu mavazi ya Zelensky ulizidi kupamba moto wakati wa mkutano wa waandishi wa habari. Brian Glenn, mwandishi kutoka Real America’s Voice—chombo cha habari kinachopendelea mrengo wa kulia—alimtupia swali la moja kwa moja: “Kwa nini hauvai suti? Upo katika ofisi ya juu kabisa katika nchi hii, na umegoma kuvaa suti – je, unamiliki hata suti?” Kwa utulivu, Zelensky alijibu kwa mshangao mdogo: “Nitavaa suti vita hivi vitakapomalizika. Labda suti kama yako, labda bora zaidi, au pengine ya bei nafuu kuliko yako,” alisema kwa utani huku akionyesha msimamo wake wa kuendelea kuvaa mavazi ya kijeshi. Swali hilo la Glenn liliibua mjadala mkali mitandaoni. Wengine walimuunga mkono, wakisema kwamba kiongozi wa taifa anapaswa kuvaa mavazi rasmi anapokutana na viongozi wengine, ilhali wengine waliona swali hilo kuwa la dhihaka na lisilo na umuhimu. Miongoni mwa waliomkosoa Glenn ni mwandishi maarufu wa Uingereza, Piers Morgan, ambaye pia ni rafiki wa karibu wa Trump. Morgan aliandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter): “Swali la kipuuzi. Elon Musk havai suti anapoingia Ikulu.” Historia pia inaonyesha kuwa si Zelensky pekee aliyeingia Ikulu ya Marekani bila suti. Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Winston Churchill, alifanya hivyo katika moja ya ziara zake rasmi.
    Like
    Love
    2
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·1KB Visualizações
  • #SportsElite
    Msimamo wa Ligi ya @championshiptz ya @nbc_tanzania
    #SportsElite 🇹🇿 Msimamo wa Ligi ya @championshiptz ya @nbc_tanzania
    0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·1KB Visualizações
  • Msimamo wa EPL
    Msimamo wa EPL
    Love
    1
    · 1 Comentários ·0 Compartilhamentos ·624 Visualizações
  • Msimamo wa Laliga
    Msimamo wa Laliga
    Haha
    1
    · 1 Comentários ·0 Compartilhamentos ·768 Visualizações
  • Msimamo wa NBC
    Msimamo wa NBC
    Like
    1
    · 1 Comentários ·0 Compartilhamentos ·617 Visualizações
  • TBT ya Haji Manara

    "September 2007 nikiwa kijana Mdogo na nikiwa kiongozi wa Chama changu na hapo ni fresh from School kule Beijing China.
    Kipindi hicho nna madini ya hatari kuhusu taaluma ya Propaganda na Uenezi,enzi ambazo nilikuwa naweza kukuaminisha Jiwe ni Keki

    Enzi ambazo nilikuwa naweza kuwavusha hata kuku barabarani kwa maneno tu,
    Ni zile zile zama nilizowaaminisha Barcelona haichomoki kwa Mkapa, tena Barcelona kweli ya Xavi ,Iniesta na kina Messi.
    Taaluma iliyonipa ujasiri wa kusema na kuamini tutafuzu kwa AFCON ya 2019 kule Misri,wakati huo tukiwa chini kwenye msimamo wa kundi letu, na Nchi nzima ikiwa imejikatia tamaa ya kwenda Cairo.

    Bila kusahau one day kule Paris France niliposahau Passport hotelini na siku hiyo tulisimamishwa na Manjagu njiani nikiwa na wenzangu ambao walikuwa Kamil Gado,
    Nikazuga kama naitoa kwenye mfuko wa koti, Askari wakaniamini kabla ya kuwaonyesha ,wakaturuhusu kilaini kabisa,inaitwa Blue Propaganda

    Yes: Pembeni yangu katika hiyo picha ni Marehemu Captain Barongo aliyekuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es salaam,
    Na hii ilikuwa sherehe ya harusi ya DC wa Temeke hivi sasa Mh Sixtus Mapunda ambae wakati huo alikuwa Katibu wa Umoja wa Vijana ( UV CCM ) Mkoa huu.
    Hadi leo tumebaki marafiki wakubwa na hakosi mwaliko wowote kwangu

    Nb: Usicheke ukubwa wa koti,miaka ile ilikuwa ndio fashion na wenyewe tuliyaita Majumba "

    TBT ya Haji Manara "September 2007 nikiwa kijana Mdogo na nikiwa kiongozi wa Chama changu na hapo ni fresh from School kule Beijing China. Kipindi hicho nna madini ya hatari kuhusu taaluma ya Propaganda na Uenezi,enzi ambazo nilikuwa naweza kukuaminisha Jiwe ni Keki 😀😀😀 Enzi ambazo nilikuwa naweza kuwavusha hata kuku barabarani kwa maneno tu😀😀😀, Ni zile zile zama nilizowaaminisha Barcelona haichomoki kwa Mkapa, tena Barcelona kweli ya Xavi ,Iniesta na kina Messi. Taaluma iliyonipa ujasiri wa kusema na kuamini tutafuzu kwa AFCON ya 2019 kule Misri,wakati huo tukiwa chini kwenye msimamo wa kundi letu, na Nchi nzima ikiwa imejikatia tamaa ya kwenda Cairo. Bila kusahau one day kule Paris France niliposahau Passport hotelini na siku hiyo tulisimamishwa na Manjagu njiani nikiwa na wenzangu ambao walikuwa Kamil Gado, Nikazuga kama naitoa kwenye mfuko wa koti, Askari wakaniamini kabla ya kuwaonyesha ,wakaturuhusu kilaini kabisa,inaitwa Blue Propaganda 😀😀😀 Yes: Pembeni yangu katika hiyo picha ni Marehemu Captain Barongo aliyekuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Na hii ilikuwa sherehe ya harusi ya DC wa Temeke hivi sasa Mh Sixtus Mapunda ambae wakati huo alikuwa Katibu wa Umoja wa Vijana ( UV CCM ) Mkoa huu. Hadi leo tumebaki marafiki wakubwa na hakosi mwaliko wowote kwangu 🙏🙏 Nb: Usicheke ukubwa wa koti,miaka ile ilikuwa ndio fashion na wenyewe tuliyaita Majumba 😀😀😀"
    0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·2KB Visualizações
  • Mfalme wa Nchi ya Jordan , Abdullah II amekataa pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump la kutaka kuwahamishia Wapalestina Nchini mwake baada ya mazungumzo na Rais Donald Trump wa Marekani, ambaye alishauri Wakazi wa Gaza wapatao milioni mbili (2) kuondolewa kutoka katika eneo lililoharibiwa na vita.

    Katika mkutano na Rais Trump, Mfalme Abdullah alijitolea kuchukua hadi Watoto 2,000 kutoka Gaza, hasa wale wanaohitaji matibabu ya dharura, ikiwemo Watoto wa saratani. Kupitia mtandao wa X, Mfalme Abdullah alisema, "Msimamo wa Jordan ni msimamo wa pamoja wa mataifa ya Kiarabu."

    Sanjari na hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit, alikosoa pendekezo hilo, akisema kuwa ni lisilokubalika katika ukanda huo, huku Nchi ya China ikisisitiza kuwa Gaza ni ardhi ya Wapalestina.

    Mfalme wa Nchi ya Jordan 🇯🇴, Abdullah II amekataa pendekezo la Rais wa Marekani 🇺🇸 Donald Trump la kutaka kuwahamishia Wapalestina Nchini mwake baada ya mazungumzo na Rais Donald Trump wa Marekani, ambaye alishauri Wakazi wa Gaza wapatao milioni mbili (2) kuondolewa kutoka katika eneo lililoharibiwa na vita. Katika mkutano na Rais Trump, Mfalme Abdullah alijitolea kuchukua hadi Watoto 2,000 kutoka Gaza, hasa wale wanaohitaji matibabu ya dharura, ikiwemo Watoto wa saratani. Kupitia mtandao wa X, Mfalme Abdullah alisema, "Msimamo wa Jordan ni msimamo wa pamoja wa mataifa ya Kiarabu." Sanjari na hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit, alikosoa pendekezo hilo, akisema kuwa ni lisilokubalika katika ukanda huo, huku Nchi ya China 🇨🇳 ikisisitiza kuwa Gaza ni ardhi ya Wapalestina.
    Like
    1
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·894 Visualizações
  • #SportsEliteMsimamo wa Ligi ya @championshiptz ya @nbc_tanzania
    #SportsElite🇹🇿Msimamo wa Ligi ya @championshiptz ya @nbc_tanzania
    Love
    1
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·741 Visualizações
  • Rais wa Marekani , Donald Trump ameonya kuwa kama kundi la Hamas (Gaza) hawatawaachilia mateka wote wa Nchi ya Israel kufikia Jumamosi ya Wiki hii basi Dunia itashuhudia mashambulizi halisi katika eneo hilo. Onyo la Trump linakuja siku moja baada ya Kundi la Wapiganaji wa Hamas kuvunja makubaliano ya usitishwaji vita na Israel kwa kugoma kuendelea na zoezi la kuwaachia huru mateka wa Israel mpaka watakapotoa taarifa nyingine.

    Uamuzi huo wa Hamas umekuja siku chache baada ya Viongozi wake Wakuu kufanya ziara Nchini Iran na kukutana na Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khemenei ambaye aliwapongeza kwa kuendelea kusimama imara dhidi ya Israel. Trump wiki iliyopita alionya kuwa Gaza haitofaa kuwa eneo la kuishi chini ya Uongozi wa Hamas na kupendekeza kwamba Marekani ingependa kulichukua eneo hilo na kulisimamia huku Wakazi wa eneo hilo wakihamishiwa Nchi za Misri na Jordan .

    Rais huyo wa Marekani alisema Marekani ipo tayari kulinunua eneo hilo na kulimiliki na kuahidi kwamba Marekani italijenga na kulifanya kuwa eneo zuri la mfano Mashariki ya Kati. Kiufupi kundi la Hamas wanacheza na moto kwa sasa, Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz ameviagiza Vikosi vya Israel kukaa tayari kwa mashambulizi mapya iwapo Kundi hilo la Hamas likigoma kutii maelekezo ya kuachia mateka.

    Marekani ndio imekuwa Nchi inayoipa misaada mikubwa ya kibinadamu na kiuchumi Gaza pamoja na kuizuia Israel kutokuifutilia mbali Gaza kwa miaka mingi sasa ambapo Hamas imekua ikifanya uchokozi. Ikumbukwe Trump ni kati ya Viongozi wa Marekani ambaye ana msimamo mkali mno dhidi ya kundi la Hamas na tokea kuanza kwa mapigano Oktoba 7 mwaka 2023 Trump alisema Israel inachopaswa kufanya ni kulifutilia mbali kundi hilo.

    Rais wa Marekani 🇺🇸, Donald Trump ameonya kuwa kama kundi la Hamas (Gaza) hawatawaachilia mateka wote wa Nchi ya Israel 🇮🇱 kufikia Jumamosi ya Wiki hii basi Dunia itashuhudia mashambulizi halisi katika eneo hilo. Onyo la Trump linakuja siku moja baada ya Kundi la Wapiganaji wa Hamas kuvunja makubaliano ya usitishwaji vita na Israel kwa kugoma kuendelea na zoezi la kuwaachia huru mateka wa Israel mpaka watakapotoa taarifa nyingine. Uamuzi huo wa Hamas umekuja siku chache baada ya Viongozi wake Wakuu kufanya ziara Nchini Iran 🇮🇷 na kukutana na Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khemenei ambaye aliwapongeza kwa kuendelea kusimama imara dhidi ya Israel. Trump wiki iliyopita alionya kuwa Gaza haitofaa kuwa eneo la kuishi chini ya Uongozi wa Hamas na kupendekeza kwamba Marekani ingependa kulichukua eneo hilo na kulisimamia huku Wakazi wa eneo hilo wakihamishiwa Nchi za Misri 🇪🇬 na Jordan 🇯🇴. Rais huyo wa Marekani alisema Marekani ipo tayari kulinunua eneo hilo na kulimiliki na kuahidi kwamba Marekani italijenga na kulifanya kuwa eneo zuri la mfano Mashariki ya Kati. Kiufupi kundi la Hamas wanacheza na moto kwa sasa, Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz ameviagiza Vikosi vya Israel kukaa tayari kwa mashambulizi mapya iwapo Kundi hilo la Hamas likigoma kutii maelekezo ya kuachia mateka. Marekani ndio imekuwa Nchi inayoipa misaada mikubwa ya kibinadamu na kiuchumi Gaza pamoja na kuizuia Israel kutokuifutilia mbali Gaza kwa miaka mingi sasa ambapo Hamas imekua ikifanya uchokozi. Ikumbukwe Trump ni kati ya Viongozi wa Marekani ambaye ana msimamo mkali mno dhidi ya kundi la Hamas na tokea kuanza kwa mapigano Oktoba 7 mwaka 2023 Trump alisema Israel inachopaswa kufanya ni kulifutilia mbali kundi hilo.
    Like
    1
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·916 Visualizações
  • Kwa mujibu wa Tovuti ya The Guardian, Wananajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) wameripotiwa kuuawa katika operesheni za siri Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo . Kuuawa kwa Wanajeshi hao katika operesheni hiyo kunapingana na msimamo wa Serikali ya Rwanda inayodai Askari wake hawahusiki wala kushiriki katika mzozo unaoendelea kati ya kundi la M23 na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo .

    Taarifa hiyo iliyochapishwa na tovuti ya The Guardian imedai kuwa vyanzo mbalimbali vya kijasusi, kijeshi na kidiplomasia vinasema idadi ya Wanajeshi wa RDF waliouawa ni kubwa, huku wakidai walikuwa wakisaidia mashambulizi yanayofanywa na Waasi wa M23 ndani ya DR Congo.

    Picha za Setilaiti zilizopigwa katika makaburi ya kijeshi yaliyoko Jijini Kigali, Nchini Rwanda, zimethibitisha kuonekana kwa makaburi mapya yasiyopungua 600 yaliyopatikana tangu Waasi wa M23, wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, walipoanza operesheni zao ndani ya DR Congo miaka mitatu iliyopita.

    Kwa mujibu wa Tovuti ya The Guardian, Wananajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda 🇷🇼 (RDF) wameripotiwa kuuawa katika operesheni za siri Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Kuuawa kwa Wanajeshi hao katika operesheni hiyo kunapingana na msimamo wa Serikali ya Rwanda inayodai Askari wake hawahusiki wala kushiriki katika mzozo unaoendelea kati ya kundi la M23 na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Taarifa hiyo iliyochapishwa na tovuti ya The Guardian imedai kuwa vyanzo mbalimbali vya kijasusi, kijeshi na kidiplomasia vinasema idadi ya Wanajeshi wa RDF waliouawa ni kubwa, huku wakidai walikuwa wakisaidia mashambulizi yanayofanywa na Waasi wa M23 ndani ya DR Congo. Picha za Setilaiti zilizopigwa katika makaburi ya kijeshi yaliyoko Jijini Kigali, Nchini Rwanda, zimethibitisha kuonekana kwa makaburi mapya yasiyopungua 600 yaliyopatikana tangu Waasi wa M23, wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, walipoanza operesheni zao ndani ya DR Congo miaka mitatu iliyopita.
    0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·613 Visualizações
Páginas impulsionada