• Read more
    Tunatumia sehemu kubwa ya maisha yetu kungoja kuliko kuishi. Tunangoja tumalize shule. Tunangoja tupate kazi. Tunangoja tusome tena. Tunangoja tupate kazi nzuri. Tunangoja mchumba abadilike. Tunangoja tupendwe. Tunangoja ndoa. Tunangoja tujenge. Tunangoja tupate watoto. Tunangoja tupandishwe cheo. Tunangoja kipato kitulie. Tunangoja watoto wasome. Mara tumezeeka. Tunangoja muujiza. Tunangoja kufa. Tunakufa kweli. Hatujaishi.
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·22 Views
  • Read more
    Alhamdulillah mashallah tumeiona Tena Leo ime siku ya KUTOA sadaka tulishe watoto wetu kwa kidogo tulicho barikiwa kwenye maisha yetU Watoto wanauhitaji WA UNGA NA MCHELE MCHELE KG 100 =200,000/TZSH UNGA KG 50 = 55000/tzsh 0655987549 Mixx but Yas/call Moza MohamedIjumaa nyongine Leo nzuri Alhamdulillah mashallah tumeiona Tena Leo ime siku ya KUTOA sadaka tulishe watoto wetu kwa kidogo tulicho barikiwa kwenye maisha yetU Watoto wanauhitaji WA UNGA NA MCHELE MCHELE KG 100 =200,000/TZSH UNGA KG 50 = 55000/tzsh 0655987549 Mixx but Yas/call Moza Mohamed
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·106 Views
  • Read more
    2. BABELI Kigeographia Babeli hii leo ipo Iraq Babeli Nchi hii ambayo ilikuwa na mwanzo wake huko Mesopotamia inarejelewa katika Maandiko yote. Katika maandishi mengi ya kale inafafanuliwa kuwa kitovu cha wafanyabiashara na biashara. Wakati wa Yoshua mwanamume wa Israeli alisimulia jinsi alivyopata vazi la kipekee, “joho nzuri kutoka Babeli, vipande vya fedha mia mbili, na kipande cha dhahabu, uzani wake shekeli hamsini” (Yoshua 7:21). Babiloni pia likawa makao ya maelfu ya Waisraeli wakati wa utekwa. Nebukadneza II alikuwa amevamia Yerusalemu na jeshi lake na kuchukua sehemu kubwa ya watu hadi ufalme wake. Aliteketeza hekalu lililojengwa na Sulemani na kuharibu jumba la kifalme kando ya kila jengo kubwa la Yerusalemu.
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·157 Views
  • Read more
    KUTOKA SINGIDA BLACK STARS ✍️ HII NI KWENU WACHAMBUZI WOTE WENYE USHABIKI KULIKO UCHAMBUZI Singida Black stars Sc ni Timu yenye utaratibu wake na mipango yake juu ya kuiongoza Timu yake kwa misingi yake Timu yetu haipangiwi na wala hatupelekeshwi na maneno ya mitandaoni katika kuiendesha Timu Yetu, Tunaomba Mfahamu kuwa kila mchezaji Tuliyemsajili anatufaa na anafaa kuipambania Nembo ya Timu yetu Katika kikosi chetu chenye jumla ya wachezaji 33 wote wakiwa wazima wa Afya na Fitness nzuri kocha wetu na Benchi letu la Ufundi lina uhuru wa Kumchagua Mchezaji yeyote akaanza katika kikosi cha kwanza katika mchezo wowote Rejea michezo Yetu Mitatu ya nyuma kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Yanga sc Tulicheza michezo 3 dhidi ya Kagera Sugar, KMC Fc, na JKT Tanzania Katika mchezo wetu dhidi ya Kagera sugar tulianzisha wachezaji wengi wa kimataifa na Tulipata sare ya goli 2-2 mchezo uliofuata tukacheza dhidi ya KMC FC na wachezaji wengi wa kimataifa walianza pia tukafungwa goli 2 bila Benchi la ufundi kikafanya mabadiliko kadhaa kwenye mchezo uliofuata dhidi ya JKT Tanzania Na tukapata ushindi kwenye moja ya Viwanja ambavyo Timu zote za ligi kuu hakuna iliyopata ushindi Baada ya Benchi la Ufundi kuridhika na vipaji vya wachezaji wetu wa ndani waliotupa Ushindi wa mchezo wa JKT Tanzania wakaridhishwa kwamba wachezaji wale wanafaa baadhi yao kuanza kwenye mchezo dhidi ya Yanga, kwa upande wa Timu yetu Tumefurahi Timu ilicheza vizuri kwa nidhamu ya hali ya juu na mchezo ukaisha kwa goal 2-1 Sasa baada ya mchezo ule wameibuka watu wanaojiita wachambuzi kwa vivuli vya ushabiki wao na roho zao mbaya na umaskini uliowajaa wanataka kutupangia Kikosi chetu kitu Ambacho kwetu hakikubaliki hata kidogo Ni mfano uone mwanaume Ameoa wake 4 alafu wewe jirani yake unataka kumpangia kwamba Leo kalale kwa mwanamke huyu na utapikiwa na huyu hilo haliwezekani Abadani SISI HATUPANGIWI MAISHA NA VITAKATAKA KAMA NYINYI
    0 Comments ·0 Shares ·291 Views
  • Read more
    "Tangu nilipokutana nawe (Hamisa), nilijua kuwa wewe ni wangu wa milele. Wewe ni ushindi wangu mkubwa, ndoto yangu nzuri zaidi imetimia." "Mwaka jana, nilipiga shuti muhimu zaidi-sio uwanjani, lakini kwa goti moja. Na uliposema NDIYO, Dunia yangu ilibadilika milele." — Aziz Ki, Mchezaji wa klabu ya Yanga SC.
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·148 Views
  • Read more
    Tarehe 24 Novemba 2009, ikiwa ni siku chache kabla ya Sikukuu ya Thanksgiving, John Jones aliamua kwenda kuchunguza mapango na ndugu zake. Alikuwa baba wa mtoto mmoja na mke wake alikuwa mjamzito wa mtoto wao wa pili. Alikuwa mchungaji wa kanisa, mwenye tabia nzuri, aliyependwa na familia yake. Alikuwa na uzoefu mdogo wa kuingia mapangoni, lakini aliamini hana cha kuhofia. Akiwa na kaka yake, Josh Jones, na marafiki wachache, waliamua kuchunguza sehemu mpya ya Nutty Putty Cave—pango maarufu lililokuwa na njia nyembamba na hatari. Walikuwa na matumaini ya kujifurahisha tu, lakini hakuna aliyejua kuwa hii ingekuwa safari ya kifo cha kutisha.
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·234 Views
  • Read more
    #PART1 Katika maisha, kuna mafanikio, kuna mapenzi, na kuna maumivu. Lakini maumivu gani yanaweza kuwa makali zaidi ya baba kugombana na damu yake mwenyewe? Hii ni stori ya 50 Cent, mwanamuziki, mfanyabiashara, na mtu aliye role model wa mamilioni ya wanaume duniani. Jamaa aliinuka kutoka mitaa ya ghetto, akapambana, akawa milionea. Lakini pamoja na pesa zote, hakununua upendo wa mtoto wake wa kwanza. Miaka ya nyuma, 50 Cent alikuwa baba mwenye furaha. Alikuwa anampenda mtoto wake kupita maelezo. Ilikuwa siyo tu kwa sababu ni damu yake, bali pia alitaka kuhakikisha kijana wake anakuwa na maisha bora zaidi. Aliamua kumuandalia mtoto wake maisha mazuri. Akampeleka kwenye shule nzuri ya mpira wa kikapu. Akalipia kila kitu, kutoka ada mpka mavazi. Mtoto akapewa kila alichohitaji, maisha ya kifahari yakawa sehemu yake ya kila siku. Lakini kitu kimoja hakikumpenda. Mpira wa kikapu haukumpenda. Dogo akaamua kuachana na basketball. Baba yake hakukasirika, akamwambia "Sawa mwanangu, kama siyo mpira, basi komaa na shule."
    0 Comments ·0 Shares ·580 Views
  • Read more
    Rais wa Marekani 🇺🇸, Donald Trump, ameshitua Watu Duniani baada ya kutangaza nia yake ya kuchukua udhibiti wa Ukanda wa Gaza ulioharibiwa na vita na kuufanyia maendeleo ya kiuchumi baada ya Wapalestina kuhamishiwa maeneo mengine. Hatua hiyo inaweza kubadili sera za Marekani za miongo kadhaa kuhusu mgogoro wa Israel na Palestina. Katika mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, Rais huyo alitangaza mpango huu bila kutoa maelezo ya kina. Kabla ya tangazo hilo, Trump alipendekeza kuwa zaidi ya Wapalestina milioni mbili (2) wa Gaza wahamishiwe Nchi jirani. Alikitaja kisiwa hicho kidogo, ambacho kwa sasa kina makubaliano dhaifu ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas, kuwa “eneo la kubomolewa.” Pendekezo hili linakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Washirika na Wapinzani wa Marekani. Pia linaibua maswali kuhusu ikiwa Saudi Arabia itashiriki katika juhudi mpya za Marekani za kuleta uhusiano wa kawaida kati ya Israel na mataifa ya Kiarabu. - Hatua ya Marekani kuchukua ushawishi wa moja kwa moja Gaza itapingana na msimamo wa muda mrefu wa Washington na Jumuiya ya kimataifa, ambao unaona Gaza kama sehemu ya Taifa la baadaye la Palestina pamoja na Ukingo wa Magharibi. "Marekani itachukua Ukanda wa Gaza, na tutafanya nao kazi nzuri sana. Tutakuwa na umiliki wake na kuhakikisha tunasafisha mabomu na silaha zote hatari zilizobaki." "Tutaendeleza Gaza, kuunda maelfu ya ajira, na kuifanya iwe sehemu ambayo Mashariki ya Kati yote itajivunia. Ninaona umiliki wa muda mrefu na ninaamini italeta utulivu mkubwa katika eneo hilo." amesema Donald Trump. “nyumbani kwa watu wa dunia.” Aliielezea Gaza kama eneo lenye uwezo wa kuwa “Riviera ya Mashariki ya Kati.” - Donald Trump baada ya kuulizwa nani ataishi Gaza baada ya kuitengeneza Trump hakujibu moja kwa moja kuhusu mamlaka au mchakato wa kuchukua eneo hilo la Gaza baada ya kuulizwa Marekani ina mamlaka gani ya kuichukua Gaza, ambalo lina urefu wa maili 25 (km 45) na upana wa hadi maili 6 (km 10) na historia ya vurugu. Serikali za awali za Marekani, ikiwemo ile ya Trump katika muhula wake wa kwanza, ziliepuka kutuma Wanajeshi Gaza.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·375 Views
  • Read more
    𝐏𝐑𝐄𝐒𝐒💬 "Maandalizi yetu kwa ujumla yapo vizuri,tumejiandaa vizuri kwenda kucheza mchezo wetu dhidi ya KenGold" "Wamesajili wachezaji wengi wazoefu ukilinganisha na mzunguko wa kwanza, na kwetu sisi hiki ni kitu kizuri maana mechi itakuwa nzuri sana maana wana wachezaji wazoefu na wachezaji wanaojua" Mshery #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·492 Views
  • nzuri hii
    nzuri hii
    Like
    1
    · 1 Comments ·0 Shares ·145 Views
  • Read more
    Shirika la habari la New York Post imeripoti kuwa Rais wa Marekani 🇺🇸, Donald Trump amesitisha ufadhili wa kifedha kwenye mifuko inayopambana na virusi vya ukimwi Duniani kwa muda wa miezi mitatu. Zuio hilo litasababisha wasiwasi mkubwa wa upatikanaji wa dawa za kupambana na ugonjwa huo hatari kwa Wagonjwa takribani milioni (25) waliokuwa wanufaika na dawa hizo. Baadhi ya mifuko mikubwa iliyokuwa ikipokea fedha ikiwemo PEPFAR na Shirika la USAID yataathirika na zuio hilo. Zuio hilo ni moja ya mazuio ya Donald Trump ya utoaji fedha nje kwa ajili ya misaada ambao unafanyiwa mapitio na Serikali yake kuona tija yake ili kuona kama kuna haja ya kuendelea na ufadhili. Waathirika wakubwa katika zuio hilo ni bara la Afrika ambako idadi ya maambukizi na Wagonjwa bado ni kubwa huku hali ya umasikini kuweza kumudu gharama za dawa ikiwa sio nzuri. Trump anaendelea na sera ambazo zinatajwa kugusa makundi mbalimbali ulimwenguni kwa kila namna. Ikumbukwe kwamba Marekani ndio Nchi linaloongoza kwa kutoa misaada Duniani ikiwemo ya kugharamia udhibiti wa magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa hatari wa UKIMWI, malaria na kifua kikuu.
    0 Comments ·0 Shares ·645 Views
  • Read more
    Rais wa Marekani 🇺🇸, Donald Trump alienda kwenye Kanisa moja Anglican Nchini humo linalofahamika kama Episcopal Church, alienda kwa dhumuni la Ibada ya kushukuru ila alipofika Askofu wa Kanisa hilo Bi Marrian Edgar Budde kwenye hotuba yake akasema manano yafuatayo: “Rais Trump tunakuomba kwa jina la Mungu uwe na huruma kwa Watu wa Mapenzi ya Jinsia moja na Wahamiaju haramu, wanaogopa sana” akamaliza Askofu huyo. Rais Trump hakuridhishwa na hotuba hiyo na wakati anaondoka akasema maneno yafuatayo: “Haikuwa hotuba nzuri, haivutii, inachafua taswira ya Kanisa lake au ninyi Waandishi mnaona inavutia, binafsi sikuipenda, haivutii na ni kweli haivutii haina maana” - Donald Trump, Rais wa Marekani 🇺🇸. Msimamo wa Trump dhidi ya Mapenzi ya Jinsia moja ni mkali saaana.
    0 Comments ·0 Shares ·387 Views
  • Read more
    Rais wa Marekani 🇺🇸, Donald Trump alienda kwenye Kanisa moja Anglican Nchini humo linalofahamika kama Episcopal Church, alienda kwa dhumuni la Ibada ya kushukuru ila alipofika Askofu wa Kanisa hilo Bi Marrian Edgar Budde kwenye hotuba yake akasema manano yafuatayo: “Rais Trump tunakuomba kwa jina la Mungu uwe na huruma kwa Watu wa Mapenzi ya Jinsia moja na Wahamiaju haramu, wanaogopa sana” akamaliza Askofu huyo. Rais Trump hakuridhishwa na hotuba hiyo na wakati anaondoka akasema maneno yafuatayo: “Haikuwa hotuba nzuri, haivutii, inachafua taswira ya Kanisa lake au ninyi Waandishi mnaona inavutia, binafsi sikuipenda, haivutii na ni kweli haivutii haina maana” - Donald Trump, Rais wa Marekani 🇺🇸. Msimamo wa Trump dhidi ya Mapenzi ya Jinsia moja ni mkali saaana.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·386 Views
  • Read more
    MACHACHE KUHUSU MFALME MKWASI ZAIDI DUNIANI KUNA HISTORIA ambazo ukitaka kuandika unaweza kuchukua siku mbili za kutafakari uanze wapi na au uishie wapi.....Mfalme Sulemani ni mmoja wapo............. Mama wa Sulemani (BATH-SHEBA) alikuwa tayari ni mke wa mtu (URIA MHITI) huyu URIA alikuwa askari wa mfalme DAUDI. so mfalme DAUDI aliponogewa na penzi la BATH SHEBA akafanya mbinu za kifo cha URIA vitani. ......umewahi kuwaza kwamba unahangaika na familia moja tu dhidi ya mtu anayetajwa kuwa na wenza 700 na masuria 300...hujahesabu watoto, wajakazi, shangazi, mjomba, wajukuu, nk wanaovinjari kila siku katika hemaya zake........tunaambiwa kwamba chakula kilicholiwa kwa siku moja kilikuwa magunia 240 ya unga, magunia 480 ya chakula, ng'ombe kumi kwa nyama choma, ng'ombe ishirini wa mchuzi, kondoo mia moja, ndege na wanyama wengine wa aina mbalimbali .......... unahangaika kutafuta mufu wa dhahabu ilihali mwenzako anapokea tani 30 za dhahabu kila mwaka .........Kwa mwaka mmoja pekee alikuwa anapokea tani si chini ya 30 ya vipande bora vya dhahabu ukiachilia mbali Vito na Madini mengine....kila nakshi na chombo ndani ya nyumba ya Sulemani ilikua ni DHAHABU tupu maana nyakati hizo madini ya fedha yalithaminishwa kwa kiwango cha vumbi dhidi ya dhahabu.... Jumba la Hukumu la Sulemani lilikuwa kubwa na lilijengwa na mwerezi na kuzungushwa na pembe zilizofunikwa na dhahabu na kusimamiwa na simba ........... Katika ukuta kulikuwa kumewekwa ngao 500 za dhahabu .................hata vyombo vya kunywea na sahani zilizokuwa kwenye nyumba hii kuu zilikuwa za “dhahabu”. Shaba “ haikuwa kitu cha kuhesabiwa katika siku za Sulemani”.................Pia alianzisha shamba la kifalme na mbuga yenye maziwa bandia, shamba la maua na matunda Wana-ikiolojia wamepata ushahidi dhabiti wa majengo ya Sulemani kote nchini hasa Hazori, Megido na Gezeri, mabaki ambayo yanatoa ushahidi wa ukweli wa 1 Wafalme 9:15. Megido ni muhimu kwa vibanda vyake vya magari ya farasi 450. Jeshi kubwa la Sulemani lilihitaji jengo lenye vibanda 4,000 vya farasi na vilijengwa karibu na mipaka ya Israeli na kulindwa na waendeshaji magari ya farasi.. Sulemani alipata faida kwani Israeli ilikuwa sehemu nzuri katikati mwa bara la Asia na Afrika. Alitawala njia za kaskazini na kusini na kwa usaidizi wa Wafoeniki, alijenga meli nyingi pale Esion-geberi ili zitumike kubeba shaba iliosafishwa na bidhaa zingine. Meli hizi zilifanya safari ya kusini hadi Ethiopia, Yemen na India Arabian mara moja kila miaka mitatu, na kuleta dhahabu, fedha, na pembe, nyani na tausi Sulemani pia aliendeleza viwanda vya kusafisha chuma, pamoja na kuchimba madini katika Araba, kusini mwa Bahari ya Chumvi, na kiwanda kikubwa cha kuyeyusha vyuma cha Esion-geberi, mahali ambapo palikuwa bandari karibu na Bahari ya Shamu. Kwa Mujibu wa wanahistoria.. Mansa Musa mfalme wa Mali empire... Ndio Binadamu alie wahi kuwa tajir Dunia nzima mpaka leo hamna mtu alie wahi fikia Utajir wake.. (wakati anaenda hiji macca alipitia misri .. Na kusabisha uchumi wao kuyumba kutokana na dhahabu alizo tumia Pale misri)... UKWELI NI KWAMBA MANSA MUSA aliyetawala kati ya mwaka 1312-1337 na utajiri wake ulikadiriwa kufikia USD billion 400 ILIHALI Mfalme Sulemani alikuwa na utajiri unaokadiriwa kufikia dollar za kimarekani trillion 2.1.......Mansa Kankan Mussa ni tajiri wa kwanza katika kipindi cha baada ya Yesu. Wenyewe wanaita Anno Domino (AD) Hata Nathaniel Rothchild Family ( zikiwepo rockerfeller, morgan na du pont family yaani FAMILI NZIMA) Utajiri wao haufikii hata theluthi ya Mfalme Sulemani (dola bilioni 600 tu) Wingi wa wake za Sulemani unahalasiha kutapanyika kwa kiazazi chake karibu kote duniani, yasemekana hata hawa wahabeshi wa Somalia, Watusi wa Rwanda na wa Iraq wa Tanzania ni mbegu yake huyo jamaa baada ya kumgaragaza malkia wa Ethiopia ( QUEEN OF SHEBA) alivyompelekea kiasi kikubwa cha dhahabu kutoka Afrika kwa ajili ya kupamba hekalu alilokamilisha. Usiulizd iwapo alikua anatozwa kodi kwani yeye ndie alikuwa mtawala wa himaya yake kwahiyo asingeweza kutozwa kodi...na utawala wake ulidumu kwa miaka 40 Uchaguzi wa Busara wa Sulemani kwa kumwomba Bwana “Moyo adili wa kuwahukumu watu wako” ulisababisha idhini ya Bwana na utoaji wa "moyo wa hekima na ufahamu" na kuongezewa "utajiri na heshima " Mhhhhhh...............yumkini kama nilivyosema si rahisi sana kumsimulia Sulemani na kuna vyanzo vingi ambavyo kila mtu anaweza kuibuka na chake walau nimeokoteza kwa vyanzo vya uhakika na kwa kuwa ni simulizi tutaendelea kuimani tu maana HATUKUWEPO................ Mada hii itaendelea kuboreshwa kwa kadri ya vyanzo vingine.... ..
    Love
    Like
    3
    · 0 Comments ·0 Shares ·716 Views
  • Read more
    PATA BLUETICK YAKO KWA TSHS 1,300 TU KATIKA INSTAGRAM NA FACEBOOK! 🙌 Kampuni ya Meta inayosimamia Mtandao wa Instagram, Facebook na WhatsApp imeanzisha Mfumo wa Discount (Punguzo la Bei) kwa Account za Biashara (Business Accounts) katika Huduma yake ya Meta Verified (Huduma ya Blue tick za Kulipia). Sasa Mtu/Kampuni yenye Account Instagram inaweza Kupata tick ya Blue kwa Ada ya Tshs 1,300 tu! (Elfu Moja na Mia Tatu) kwa Mwezi wa Kwanza, kisha Tshs 19,500 kwa Mwezi unaofuata. Huduma ya Meta Verified ni huduma nzuri ikiwa unapenda Kulinda Brand yako Mtandaoni kwani utawapa Mashabiki au Wateja urahisi wa kufahamu ipi ni Account yako Rasmi. ZINGATIA: Ofa ya Punguzo la Bei ya tiki hizi ipo kwa Account za Biashara pekee katika Instagram na kwa Watumiaji wa Facebook wenye Account zilizo katika Professional Mode. (Si Account zote zinaweza Kuwa na Discount hii).
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·395 Views
  • Read more
    NJIA MPYA YA KUJIINGIZIA PESA FACEBOOK KUPITIA POSTS ZA MAANDISHI, VIDEO NA REELS. October 2, 2024 Facebook Walizindua Programu Mpya waliyoipa Jina “Content Monetization” ambayo imezijumuisha kwa Pamoja category ambazo mwanzo zilijitegemea, Category hizo zilikuwa, ⬜️ Ads On Reels ⬜️ InStream Ads ⬜️ Performance Bonus Category hizi kwasasa zimejumuishwa kwa Pamoja na Kupewa Jina “Content Monetization” ambapo Mtu yeyote kwasasa mwenye Page ya Facebook au Account ambayo iko “on Professional Mode” iliyo na Video, Picha, Post au Maudhui yoyote ambayo yatakuwa yanafaa Kulipwa basi Facebook watapachika Matangazo yao na Mhusika ataanza Kulipwa kwa Ukubwa zaidi kuliko Mwanzo. Malipo ni kila Tarehe 21-23 ya Kila Mwezi na kiwango cha Chini cha Kutoa Pesa ni $100 (Tshs 271,500), yaani ikiwa Page au Account yako haijafikisha Kiwango hicho hutoruhusiwa Kutoa mpaka utakapofikisha au kupita kiwango hicho na Ni rahisi kufikisha ikiwa unatengeneza Video zaidi na zinatazamwa zaidi. Hii Itawapa Motisha zaidi Content Creators kutengeneza Video zaidi katika Platform hiyo. Mfumo huu kwasasa unatolewa kwa Mualiko Pekee, ikiwa Una Page au Account yenye Video au Posts zilizo tazamwa zaidi fuata hatua zifuatazo hapo chini kuomba Mualiko wa Kuunganishwa na Programu hii BURE. ⬜️ Ingia >> hapa https://creators.facebook.com/tools/facebook-content-monetization ⬜️ Chagua >> I'm Interested ⬜️ Jaza Taarifa zako ⬜️ Sehemu ya Email Address, Weka Email yako yoyote iliyo hewani (Ni Vizuri ukitumia uliyo Link katika Account yako) ⬜️ Sehemu ya Facebook Account URL, Weka Link ya Account au Page yako unayohitaji Iwe na Programu hiyo. ⬜️ Sehemu ya Other Social Media Accounts, Weka Link ya Account yako katika Mtandao Mwingine (Hasa Instagram). 🔗 Baadae Bofya LET'S DO THIS Utapokea Email ya Uthibitisho baada ya Siku kadhaa ikiwa Account au Page yako imeruhusiwa Kutumia Programu hiyo. Programu hii ni Programu nzuri na Bora zaidi kwa Content Creators wadogo, Wakubwa na Wanaochipukia (Upcoming Creators). Ni Programu Rafiki kwa kila Mmoja, itakusaidia Kupata Chochote kupitia Kazi zako.
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·619 Views
  • Read more
    OPERATION ENTEBBE -2 Tayari zilikuwa zimepita siku tatu tangu ndege ya Air France Flight 139 kuondoka Tel Aviv na hatimaye kutekwa baada ya kuruka jijini Athens iliposimama kuchukua abiria. Lakini pia zilikuwa zimepita siku mbili tangu ndege hii kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda. Katika siku zote mbili hizi tangu ndege hii itue uwanjani hapa, rais wa Uganda Idd Amin Nduli Dadaa alikuwa anafika uwanjani hapo kila siku “kuwajulia hali” mateka hao. Kwa muda wa siku hizi zote mbili tangu ndege itue uwanjani hapo, magaidi hawa walioiteka ndege kwa kushirikiana na jeshi la Uganda kuchunguza majina ya kila abiria kama ambavyo yalikuwa yameandikwa kwenye pasport. Lengo lao la kufanya hivi ilikuwa ni kujaribu kufahamu uraia wa kila mateka waliye naye. Baada ya kufanya uchambuzi huu wa passport zote, hatimaye siku hii ya tatu, yaani tarehe 29 June 1976 kiongozi wa magaidi hawa Wilfred Bose akiwa na karatasi mkononi aliingi ndani ya terminal ambayo walikuwa wanaitumia kuwahifadhi mateka na kisha akaanza kusoma majina ya kila abiria. Alichokuwa anakifanya ni kusoma majina ya mateka ambao passport zao zilionyesha walikuwa ni raia wa Israel. Lakini pia alisoma majina ya mateka wengine ambao licha ya passport zao kuonyesha kuwa hawakuwa raia wa Israel lakini walikuwa na majina ya kiyahudi. Pamoja na hao pia mateka wote ambao walikuwa na uraia pacha na uraia huo mmojawapo ukiwa ni Israel basi nao waliunganishwa kwenye list hii. Baada ya kuwatenganisha raia wote wa Israel na kuwaweka kwenye chumba kingine peke yao hapo hapo kwenye terminal, kuna mwanadada raia wa Ufaransa aliyeitwa Jocelyne Monier yeye jina lake halikuitwa kwenye ile list ya wanaotakiwa kutengwa kwenye chumba kingine (Waisrael na Wayahudi). Lakini ‘boyfriend’ wake alikuwa ni Muisrael na aliitwa jina na kutengwa na wengine katika kile chumba kingine. Mwanadada huyu ili kuonyesha kumtia moyo mpenzi wake na kupinga huu ubaguzi uliokuwa unafanywa na hawa magaidi, kwa hiari yake alijipeleka kwenye chumba cha mateka wa Kiisrael. Si mwanadada huyu pekee ambaye alifanya kitendo hiki cha ushujaa, lakini pia kulikuwa na mwanamama mwingine aliitwa Janet Almog (rai wa Marekani) na mateka mwingine aliyeitwa Jean-Jacques Mimouni (raia wa Ufaransa) nao kwenye kuonyesha hali ya kuwaunga mkono wenzao waliotengwa kwenye chumba kingine na kupinga ubaguzi uliokuwa unafanywa na maharamia hawa, nao walijipeleka kwa hiari yao kwenye chumba ambacho mateka hao walikibatiza jina “Chumba cha Waisrael”, ambacho mateka wote walijua fika kwamba kuna jambo baya maharamia hao walikuwa wamepanga kulifanya. Licha ya maharamia kwa kushirikiana na jeshi la Uganda kufanya uchambuzi huu wa kina kuhusu uraia wa kila mateka waliye naye, lakini walifanya kosa kubwa sana ambalo lilkuja kuwagharimu sana hapo baadae. Kwenye uchambuzi wao wote huu walioufanya walishindwa kumng’amua mateka mmoja mwanajeshi wa Israel ambaye alikuwa ana uraia pacha na siku hiyo alikuwa anatumia passport ambayo sio ya Israel. Mateka huyu alikuja kuwa muhimu sana huko mbeleni kuwapatia Mossad Intelijensia mujarabu kabisa kuhusu watekaji, jengo wanaloshikilia mateka, na namana wanavyoshirikiana na jeshi la Uganda. Siku iliyofuata yaani June 30, maharamia haya wakawaachia mkupuo wa kwanza wa mateka wasio raia wa Israel au wayahudi. Katika mkupuo huu wa kwanza waliachia mateka 48 ambao walikuwa ni wazee, watoto na akina mama wenye watoto wadogo. Baada ya mkupuo huu wa kwanza wa kuwaachia mateka hawa wachache, maharamia wakaweka wazi matakwa yao ili waweze kuachia mateka wengine. Kwanza kabisa walitaka walipwe fedha kiasi cha dola za Kimarekani milioni 5. Na pili walitakakuachiwa kwa wafungwa 53 wenye asili ya kipalestina wanaotuhumiwa kwa ugaidi, ambao kati yao 40 walikuwa kwenye jela za Israel na 13 katika nchi nyingine za Ulaya. Watekaji hawa wakatoa ‘ultimutum’ kwamba kama matakwa yao hayatatekelezwa ndani ya masaa ishirini na nne yajayo (mpaka tarehe 1 July saa 8 mchana) basi wataanza kuua raia wa Israel mmoja baada ya mwingine. Dunia nzima ni kama ilisimama kwa masaa kadhaa kutokana na sintofahamu iliyogubika kila mahali. Sintofahamu hii ililetwa na ukweli kwamba, ilikuwa inajulikana wazi kwa miaka yote kwamba Israel wana sera ya kutofanya mazungumzo au makubaliano na Magaidi. Kwahiyo kila mtu alikuwa nafahamu kuwa kuna uwezekano mkubwa ndani ya masaa 24 yajayo ulimwengu ukashuhidia watu zaidi ya 200 wakichinjwa kama kuku. NCHINI ISRAEL: KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI Nchini Israel kikao cha dharura cha baraza la mawaziri kilikuwa kimeitishwa na waziri Mkuu Yitzhak Rabin kujadili kuhusu hatua za kuchukua kuokoa raia wake ambao wameshikiliwa mateka huko uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda. Hali ya kikao ilikuwa tete sana kutokana na kila dakika waliyokuwa wanaitumia kujadili ndivyo ambavyo walikuwa wanaikaribia saa 8 mchana ya tarehe 1 July. Walipowasilana na Ujerumani na Ufaransa ambao nao walikuwa na baadhi ya wafungwa wa Kipalestina ambao watekaji walitaka waachiwe… walipowaomba ushirikiano wao kuhusu kukabali kuachia hao wafungwa, Ujerumani na Ufaransa walikataa katakata kuachia hata mfungwa mmoja wa Kipalestina ambaye alikuwa kwenye magereza zao. Sintofahamu ilizidi kuongezeka. Masaa yalizidi kuyoyoma. Saa 8 mchana ya tarehe 1 July ilizidi kukaribia. Harufu ya damu ilikuwa inabisha hodi mlangoni kwao. Licha ya weledi wao wote walionao lakini mbele yao waliona giza. Inapaswa kukumbukwa kwamba Idd Amin aliwahi kupatiwa mafunzo ya weledi wa kijeshi nchini Isarel (Special Force Training). Kwa hiyo baraza la mawaziri likamuagiza Baruch Bar-Lev, kamanda mstaafu wa IDF ambaye alihusika kumpatia mafunzo ya kijeshi Amin kipindi yuko Israel na kufanikiwa kujenga naye ukaribu. Baraza la Mawaziri likamuagiza Baruck (marafiki zake humuita “Burka”) kufanya mawasiliano na Rais huyo wa Uganda ili kujaribu kumuomba awashawishi magaidi wanaoshikilia mateka kwenye uwanja wake wa ndege wa Entebbe wawaachie mateka hao bila masharti magumu. Kupitia kwa Burka, Israel ilifikia mpaka hatua ya kumuahidi Idd Amin kuwa kama atafanikisha kuachiwa kwa mateka hao basi watatumia ushawishi walionao kuhakikisha kuwa Amin anatunukiwa tuzo ya amani ya Nobel. Lakini Amin hakulegeza msimamo, akaendelea kuwasisitiza kuwa hakuna namna nyingine yeyote ambayo mateka hao wataachiwa bila masharti yaliyotolewa na watekaji kutimizwa. Baada ya juhudi hii ya kumuhonga ‘tuzo’ kugonga mwamba, Waziri Mkuu wa Israel akawasiliana na serikali ya Marekani na kuwaomba wamshawishi Rais wa Misri Anwar Sadat ambaye alikuwa anaheshimiana sana na Amin ili amshawishi kuwaamuru magaidi yaliyoko uwanjani kwake Entebbe waachiemateka bila masharti magumu. Amin bado akashikilia msimamo kwamba hakuna mateka atakayeachiwa pasipo masharti yaliyotolewa kutimizwa. Juhudi hizi za kumshawishi Amin zilikula muda mwingi sana na hatimaye wakajikuta tayari kulikuwa kumekucha asubuhi. Mbele yao kulikuwa kumebakia masaa chini ya manane kabla ya damu ya zaidi ya watu 200 kumwagika. Baraza la mawaziri la Israel likamuomba Amin aongee na watekaji wakubali kusogeza siku mbele ili kuipa serikali ya Israel muda wakutosha kushughulikia lojistiki na kushawishi Ujerumani na Ufaransa ili waweze kutimiza sharti la kuachiwa kwa wafungwa wa kipalestina 53 wanaotuhumiwa kwa ugaidi. Rais Idd Amin baada ya kushawishiwa sana akakubali ombi hili na akaieleza serikali ya Israel kwamba ni siku tatu tu pekee zinaongezwa, yaani ikimaanisha kwamba siku zitaongezwa mpaka tarehe 4 July, saa 8 mchana. Serikali ya Israel ikakubliana na hili. Mchana wa siku hiyo, serikali ilitoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari wakilaani vitendo vya kigaidi na hususani matukio ya utekeji wa raia wasio na hatia, na pia ikaendelea kusisitiza kuhusu sera yake ya kutojadili na magaidi. Lakini taarifa hii ikamalizia kwa kueleza kuwa kwa kujali zaidi uhai wa zaidi ya raia 200 ambao bado wanashikiliwa na magaidi hayo, na kujali maumivu ambayo familia zao na taifa zima linapitia, wamekubali kutimiza sharti la magaidi hao la kuwalipa fedha za kimarekani dola milioni tano pamoja na kuachiwa kwa wafungwa wa kipalestina 53 wenye tuhuma za ugaidi. Ilikuwa ni moja ya matukio machache ambayo yaliishangaza dunia kwa Israel kukubali kushindwa hadharani. Kwa upande wa maadui wa Israel hii ilikuwa ni sherehe kubwa kwao. Na kwa upande wa Isarel na maswahiba zake hii iikuwa ni maombolezo makubwa. Amin na wenzake kule Uganda walikuwa wanasherehekea baada ya taarifa hii kutolewa kwa vyombo vya habari. Walihsi kabisa harufu ya ushindi inanukia kwenye pua zao. Kitu ambacho walikuwa hawafahamu ilikuwa ni kwamba, Israel walikuwa wanawafanyia ‘mchezo’ wa kisaikolojia ili Amin, jeshi lake na watekaji wajiamini kwa kuona kuwa ushindi umeegemea upande wao na hatimaye wajisahau kutokana na kujiamini huku. NYUMA YA PAZIA Huko Tel aviv, makamanda wa IDF na maafisa wa Mossad walikuwa wamekusanyika katika conference room ya mako makuu ya wizara ya ulinzi kuweka mkakati wa oparesheni ya uokozi (rescue mission) wa mateka wanaoshikiliwa katika uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda. Kati ya watu muhimu ambao walikuwepo kwenye kikao hiki alikuwa ni Waziri Mkuu Rabin na Ehud Barak ambaye kipindi hicho alikuwa kamanda wa ngazi za juu kwenye jeshi anayeongoza kitengo cha Intelijensia ya jeshi (Military Intelligence). Moja kati ya vitu muhimu ambavyo viliwasaidia ilikuwa ni taarifa ya intelijensia iliyoletwa na Mossad kwamba uwanja wa ndege wa Entebbe ulijengwa na kampuni ya Kiisrael inayoitwa Solel Boneh. Kwahiyo muwakilishi kutoka katika kampuni hii ya ujenzi naye akaitwa kikaoni kwa ajili ya kuwasilisha michoro kuhusu jengo lote na uwanja wa ndege wa Entebbe ulivyo. Lakini pia wakati huo huo kulikuwa na maafisa wa Mossad ambao walikuwa ufaransa kuwahoji wale mateka ambao walikuwa wameachiwa awali. Mtu muhimu zaidi ambaye alitoa taarifa nzuri kwa Mossad alikuwa ni yule afisa wa jeshi niliyemuelezea awali kwamba alikuwa na uraia wan chi mbili (Israel na Ufaransa) na siku hii alikuwa ametumia passport ya nchi ya ufaransa hivyo watekaji walimuachia pamoja na wenzake wa kundi la kwanza lile la watu 48. Bwana huyu alitoa taarifa muhimu zaidi kuhusu kilichokuwa kinaendelea katika uwanja wa ndege wa Entebbe, kwa kuwa yeye tofauti na wenzake kutokana na uzoefu wake wa jeshi alikuwa aliweza kuwaeleza Mossad kuhusu ni salaha za namna gani watekaji walikuwa nazo, kulikuwa na ndege za aina gani za kijeshi pale uwanjani (Idd Amin aliamuru Air Force ya Uganda kulinda uwanja huo masaa 24), pia aliweza kuwaeleza kuhusu ‘rotation’ ya ulinzi ya jeshi la Uganda pamoja na taarifa nyingine muhimu ambazo abiria wengine wasingeweza kuzitilia maanani au kkuzieleza kwa ufasaha. Baada ya kupata intelijensia ya kutosha, mkakati wa awali ambao ulipendekezwa na jeshi ulikuwa ni kutumia ndege ya kijeshi na kisha kudondosha makomando kwenye ziwa Viktoria na kutoka hapo watatumia boti za mpira kuvuka mpaka nchi kavu na hatimaye kuelekea uwanja wa ndege ambao haukuwa mbali sana na ziwa Viktoria. Mkakati huu ulikuwa ni mzuri lakini ulihairishwa baada ya kupewa taarifa kuwa ziwa Viktoria lilikuwa na mamba wengi na ingeweza kuhatarisha uhai wa hawa makomando kabla hata ya kufika kwenye uwanja wa ndege. Kwahiyo ilikuwa dhahiri kwamba mkakati wowote ambao utawekwa ni lazima uwe wa kuvamia kutokea nchi kavu na ikiwezekana kutoka nchi jirani. Changamoto kubwa zaidi ilikuwa ni usafiri. Yaani kwamba oparesheni hii ilikuwa si tu kwamba makomando wanaotumwa kutekeleza wanaenda kupambana na magaidi wanne tu walioteka ndege, bali ilikuwa ni kana kwamba wanaenda kupambana na jeshi zima la Uganda. Kwa hiyo kikosi cha makomando ambacho kitatumwa kwenda huko lazima kiwe na watu wengi wa kutosha na pia lazima wachukue silaha nzito za kutosha. Ili kufaniskisha safari yenye makomando wengi hivi na vifaa vizito ilikuwa ni lazima kutumia ndege kubwa za kijeshi zenye uwezo mkubwa pia na hakukuwa na chaguo zuri zaid ya kutumia ndege za kijeshi za LOCKHEED C-130 HERCULES. Sasa changamoto ilikuwa inakuja kwamba huwezi kurusha dege kubwa kama hii kwenda na kurudi kutoka Israel mpaka Uganda bila kujaza mafuta tena japo mara moja. Katika kipindi hiki bado Israel walikuwa hawajawa na uwezo wa kufanya ‘Aerial Refuel’, yaani ndege kujazwa mafuta kwa kutumia ndege nyingine ikiwa angani. Lakini pia ilikuwa ni lazima madege hayo yakikaribia Uganda yaruke chini chini ili kukwepa kudunguliwa na kuikwepa rada ya kijeshi. Kwa hiyo ilikuwa ni lazima kupata nchi ndani ya afrika Mashariki ambao watakubali madege hayo ya kijeshi ya Israel kutua kwenye uwanja wake wa ndege na kujaza mafuta lakini pia kujiandaa na kuanzisha operation kutokea hapo na pia anga lao kutumika kuanzisha shambulizi la kijeshi kuelekea Uganda. Sasa japokuwa nchi zote za Afrika Mashariki zilikuwa hazikubaliana na kitendo cha Rais wa Uganda kushirikiana na watekaji, lakini hakukuwa na hata nchi moja ambayo ilikuwa iko tayari kuingia kwenye mzozo na Idd Amin kwa kuruhusu viwanja vya vya ndege kutumika na ndege za jeshi la Israel au wanajeshi kujiandaa kuvamia Entebbe au pia kuruhusu anga lao kutumia na jeshi la Israel. Ndipo hapa ambapo kwa haraka sana siku hiyo hiyo Waziri Mkuu Rabin akamtuma Ehud Barak na maafisa wachache wa Mossad kwenda Kenya kushawishi serikali ya Mzee Jomo Kenyatta iruhusu ndege za jeshi la Isarel kutumia kiwanja chao cha ndege. Ehud barak na wenzake hawakwenda tu moja kwa moja kwa Mzee Kenyatta, bali kwanza walienda kwa Waziri wa kilimo wa kipindi hicho Bw. Bruce McKenzie ambaye huyu aliwahi kuwa afisa wa Idara ya ujasusi ya Uingereza, MI6 na pia alikuwa swahiba mkubwa wa Ehud Barak. Kwa hiyo Israel ikamtumia Bruce McKenzie kumshawishi Mzee Jomo Kenyatta kuruhusu anga la Kenya na viwanjavya ndege kutumiwa na makomando wa Israel na ndege zao. Ehud Barak na maafisa wa Mossad hawakuishia hapa tu, bali pia walifanya vikao vya siri na wafanyabiashara wakubwa nchini Kenya wenye asili ya Israel na wale ambao walikuwa na ‘marafiki’ wa Israel kuwaomba watumie ushawishi wao wa kisiasa na kiuchumi wasaidie kumshawishi Kenyatta kukubali ombi la seriakli ya Israael viwanja vyao kutumika na ndege za kijeshi za Israel na makondo wake. Baada ya mashinikizo haya kutoka kila upande, Mzee Kenyatta hakuwa na chaguo linguine zaidi ya kukubali ombi lao. Bwana huyu McKenzie pia alikuwa na ndege yakebinafsi, na Ehud Barak akaona fursa. Walitumia ndege hii ya kiraia kuruka mpaka Uganda mijini Entebbe na kukatiza juu ya anga la uwanja wa ndege wa Entebbe na walipokuwa wanapita juu ya anga la uwanja wa ndege, Ehud Barak akatumia fursa hii kupiga picha kila eneo la uwanja. Kwa kuwa hii ilikuwa ni ndege ya kiraia, jeshi la Uganda hawakushughulika nayo. Picha hizi zilizopigwa na Ehud Barak zilikuja kuwa na umuhimumkubwa katika maandalizi ya mwisho ya oparesheni ya makomando wa Isarel Kuvamia uwanja huu. Mpaka kufikia hapa maandalizi yote muhimu yalikuwa yamekamilika. WAKATI HUO HUO Upande wa watekaji kule Uganda walikuwa wanasubria mifwedha yao dola milioni 5 za kimarekani. Rais Idd Amin naye baada ya kufikia makubaliano na Israel kuwa masharti ya fedha na wafungwa wa kipalestina kuachiwa tarehe 4 July, naye ‘akarelax’ na akaona huo ndio muda wa kutekeleza majukumu Mengine akisubiria tarehe 4 July ifike. Katika kipindi hiki Idd amin ndiye alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwa kuzingatia utaratibu wa uenyekiti kuzunguka kwa kila nchi kwa mwaka mmoja mmoja na wiki hii alikuwa anatakiwa kwenye kikao cha Umoja wa Afrika kilichokuwa kinafanyika Mauritius. Kwa hiyo Amin akafunga safari kuelekea Mauritius kwenda kukabidhi kijiti cha Uenyekiti. Ehud Barak aliposikia taarifa hii, kwa kutumia akili yake kubwa ya kuzaliwa aliyojaliwa na uzoefu wake wa ujasusi, aliona fursa adhimu kabisa hapa. Akawasiliana na walioko kikaoni huko Tel Aviv na kuwaeleza taarifa ambazo awali wote hawakuielewa. Ehud Barak: “Idd Amin akiwa ndani ya Uganda huwa anatumia Mercedes Limousine katika msafara wake” Waziri Mkuu Rabin: “Ok! Limefanyaje?’ Ehud Barak: “Nataka mtafute gari kama hiyo… Mercedes Limousine” Waziri Mkuu Rabin: “la kazi gani?” Ehud Barak: “siku ambayo kikosi cha makomando wakipanda kwenye ndege kutoka huko Israel kwenda Uganda, gari hilo nataka pia lipakiwe ndani ya ndge!” Kwa dakika kadhaa wote ambao walikuwa wanamsikiliza pale kikaoni kupitia simu hakuna ambaye alielewa nini hasa Ehud Barak alikuwa anapendekeza. Yalikuwa yamebaki masaa machache tu ambapo, weledi, ushujaa na uzalendo uliotukuka ulikuwa unaedna kudhihirika. Itaendelea #TheBOLD_JF
    0 Comments ·0 Shares ·1K Views
  • Read more
    "Wolper aliwahi kuniomba hela ya mtaji nikachukua milioni 30 nikampa ila cha kusikitisha akaenda kula pesa hizo na bishoo mmoja mwenye sura nzuri nzuri anaitwa Rich Mitindo. Alipokuwa China nikawa naona anapiga picha nyingi nyingi na jamaa, nilipomuuliza akawa anajibu "hakuna kitu babe huyu ni mdogo wangu tu" - Harmonize, Msanii wa muziki Tanzania.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·476 Views
  • Read more
    *FAHAMU MAAJABU YA WANAWAKE YALIYOWASHINDA HATA WANA FALSAFA KUELEWA* Wanawake ni binadamu wa ajabu sana katika uso huu wa Dunia yaani hawa watu ni next level, Manabii na busara zao zote walishindwa kuwaelewa wakaishia kushauri ya kwamba tuishi nao kwa akili. Sasa najiuliza ni jambo gani unaweza kufanya nao bila kutumia akili?, hapa ndipo napata ushahidi kwamba kumbe wanawake walishindikana tangu zama za mwanzo kabisa!. Wanasaikolojia wanasema kuwa kama utamuoa/kuishi na mwanamke mwenye miaka 25 basi itakuchukua miaka 25 mingine kumuelewa huyo mwanamke angalau kwa 90% maana hawa kila siku hubadilika na kuwa wapya kimatendo na kifikra. Mwanamke unaweza mnunulia BMW X6 akatoka nayo kwenda kutembea, akiwa njiani akaombwa lift na kijana akampa akipitia sheli hela ya mafuta ikawa haitoshi, yule kijana akaamua kumuongeza ata elfu 20 basi mwanamke huweza kubadili mawazo na kumuona yule kijana ni bora kisa tu kachangia mafuta kuliko wewe uliyenunua BMW X6. Mfano akitoka hapo akapitia supermarket kununua bidhaa labda akapungukiwa kiasi mfano anadaiwa elfu 20, na yule kijana akasema hiyo ntalipa mimi basi basi hapo atasahau zile zawadi zote huwa unambebea na hiyo elfu 20 inaweza kumfanya awaze kumtunuku yule kijana penzi. Mwanamke unaweza mpa hela akanunue nyama kilo 5 buchani, mwenye bucha akimuongeza robo tu hilo litamfurahisha kiasi kwamba anaweza kumpa mwenye bucha penzi na akusahau wewe ulieyota hela ya nyama kilo 5. Mwanamke unaweza kumnunulia nguo, weaving, mafuta, perfume na urembo mzuri akavutia ila akipita mtaani akasifiwa na mwanaume kuwa kapendeza inaweza kuwa chanzo cha kumtunuku penzi na akakusahu wewe uliyegharamika na kufanya asifiwe!. Mwanamke unaweza kumpa mimba na ukamhudumia mwanzo mwisho na familia ukalea kwa juhudi zako zote ila siku mkikosana anakwambia niache na watoto wangu, apo ashasahau kuwa wewe ndiye uliyempa mimba na kumlea yeye na watoto!. Mchukue rafiki yako mwende bar, wewe uwe na laki 5 na yeye awe na elfu 30 kisha mkae meza moja na muagize unywaji, wewe agiza soda na yeye aagize bia. halafu baada ya nusu saa iteni warembo utaona wewe na laki 5 yako unapitwa tu ila yeye mwenye slfu 30 anaibuka kidedea kisa kaweza kumudu gharama ya bia, Hao ndio wanawake ndugu! Mwanamke ndiye kiumbe pekee anayeweza kukupenda bila sababu ama kukuchukia bila sababu tofauti na viumbe wengine. Mwanamke ndiye mwigizaji mkubwa ulimwenguni, anaweza kulia kwa furaha na akacheka kwa huzuni, bado hujawajua tu wanawake! Mwanamke akisema ndio humaanisha hapana, na akisema hapana humaanisha ndio, pia anaweza kucheka bila kujua sababu lakini pia anaweza kulia pasipo sababu ya msingi ya kumfanya alie, hivyo chunga sana usijejichanganya!. Mwanamke hupendi vutu vigumu na vyenye hatari mfano wanaume wenye nguvu, mlevi, muhuni (playboy), jambazi, mgomvi anayeogopwa hata na wanaume wenzie ila ukimuuliza anakuambia mie napenda kuwa na mwanaume mpole mwenye hofu ya Mungu tifauti na sisi wanaume tunavyopenda vitu vipole na vinyenyekevu na vyenye ukarimu, sasa wewe jifanye kumuamini mwanamke! Jinsi unavyozidi kumpenda na kumthibutishia upendo wa dhati ndivyo unavyozidi kujiweka mbali nayeye, mwanamke hupenda migogoro isiyo na maana, ukijua hili ndoa haitokusumbua. Mwanamke hupendi utulivu kamwe!, usipomchokoa atakuchokoa tuu na usipomuendesha lazima akuendeshe yeye, Hawa viumbe hawana hiyana aisee!. Mwanamke hupendi vitu vikubwa wala vidogo, kiufupi hana chaguo maalumu. Ukimnunulia gari sio garantii ya yeye kutulia nawewe bali anaweza kukusaliti hata na muosha gari wako. Ukimjengea nyumba nzuri na kumuwekea kila kitu sio njia ya kumteka kimahaba kwani anaweza kumtunuku penzi ata mtunza bustani wa nyumba yako. Mwanamke hapendi ukweli, Ukimpa ukweli akija mwenye uongo basi we andika maumivu. Unaweza kuwa na elfu 50 ukamueleza ukweli kuwa "mke wangu leo hali mbaya chukua hii elfu 30,"... akatokea jamaa akamuongopea kuwa "Chukua hii elfu 15 ngoja nimesahau ATM card yangu nyumbani ikifuka saa 10 jioni ntakutumia laki 2 kwenye simu", Usishangae mkeo akakusaliti hata kabla ya hiyo saa 10 na iyo laki 2 asiione katu!. Unamuoa hana ishu akiwa kwao amekaa tu, unaamua kumfungulia biashara hata ya duka unamjazia kila kitu. anatokea mshikaji mmoja kumuunga pale dukani kila siku na kumuachia soda tu na hicho kinakuwa kigezo tosha cha kuona mshikaji anamjali kwa kumuachia ya soda kila siku kuliko wewe uliyemfungulia duka zima na kinachofuata ni usaliti tu. Yapo mengi mno kuliko hayo ila kwa leo naishia hapo... ukiweza shea kwenye groups zingine. 😂🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽 Wamekuwa viumbe walioshindikana kwa Maana nyingine 😅👀 *ni mawazo tu wadau msijenge chuki*🏃🏽
    0 Comments ·0 Shares ·1K Views
  • Read more
    SAKATA LA JASUSI SERGEI SKRIPAL NA MWANAE NI UTEKELEZAJI WA OPERATION SARLISBURY ILIYOTEKELEZWA NA RUSSIA, KIMSIMGI NI VITA KATI YA URUSI NA NATO KUJIBU MAPIGO YA UCHAGUZI WA MAREKANI MWAKA 2016. Na mhariri wako Comred Mbwana Allyamtu Sakata la jaribio la mauaji ya jasusi au mpelelezi, ndumilakuwili wa Urusi na Uingereza, Sergei Skripal na binti yake Yulia katika kitongoji cha Salisbury jijini London nchini Uingereza linachukua sura mpya kila siku. Wawili hao walipatikana wakiwa hawajitambui katika eneo la maduka liitwalo Maltings mwanzoni mwa Machi. Taarifa kutoka kwa polisi wa Uingereza ambao hushughulikia matukio ya kigaidi wanaamini kuwa jasusi huyo na mwanaye, walivuta hewa iliyokuwa na kemikali yenye sumu iitwayo novichok. Kemikali hii hushambulia mfumo wa mfahamu na inasemekana ilitengenezwa katika maabara moja huko Urusi na ilitumika wakati wa Vita vya Pili vya Dunia mwaka 1935 hadi 1945. Kemikali hiyo iliachwa mlangoni mwa nyumba ambayo amekuwa akiishi jasusi huyo na mwanaye katika eneo hilo la Salisbury. Mashirika makubwa ya habari nchini Uingereza yameipa umuhimu habari hii ambapo Machi 30, yalitangaza kuwa binti wa Skripal, Yulia hakuwa katika hali tete kiafya. Kufuatia tukio hilo Serikali ya Uingereza chini ya Waziri Mkuu, Theresa May iliitupia lawama Serikali ya Urusi kwa kuhusika na uovu huo na ili kuonyesha kuwa imechukia iliamua kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi wapatao 23. Urusi imekanusha kuhusika na uovu huo na ikaahidi kuwa kwa kila hukumu itakayotolewa nayo itajibu kwa ukubwa huohuo au zaidi ya hapo, na ikajibu kwa kutoa hukumu ya kisasi kwa kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa Uingereza na kufunga kituo cha Lugha na Utamaduni cha Uingereza, British Council na imeitaka Uingereza kuwaondoa wanadiplomasia wake wengine wapatao 50 katika kipindi cha mwezi mmoja. Ili kuonyesha mshikamano na Uingereza nchi nyingine za Ulaya Magharibi na Australia zimewafukuza wanadiplomasia wa Urusi wanaofikia 150 huku Marekani ikiongoza kwa kufunga ubalozi mdogo wa Urusi katika Jiji la Seattle na kuwafukuza wanadiplomasia 60 kutoka nchi hiyo. Urusi nayo haikubaki kimya, Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov ametangaza kuwafukuza wanadiplomasia 60 wa Marekani na vilevile kufunga ubalozi wa Marekani katika mji wa Saint Petersburg na kuahidi kuwa kila nchi iliyohusika na kufukuza wanadiplomasia wake itaadhibiwa vilivyo. Kwa ujumla nchi karibu 23 na Umoja wa Kujihami wa nchi za Ulaya Magharibi (Nato) kote ulimwenguni zimeonyesha kukerwa na vitendo vya Urusi kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi tofautitofauti, kama vile kuvamia Ukraine na kulichukua jimbo la Krimea, kuitungua ndege ya Malaysia na kuingilia uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka 2016. Siyo mara ya kwanza nchi hizi kuingia katika mzozo wa kidiplomasia kwani mwaka 1986 Ronald Reagan aliyekuwa Rais wa Marekani, aliamuru wanadiplomasia 80 wa Shirikisho la Urusi (USSR) wafukuzwe nchini humo na mwaka 2016, Rais Barak Obama aliwatimua wanadiplomasia 35 kutoka nchi hiyo kwa tuhuma za kudukua kompyuta za chama cha Democratic kwa nia ya kumhujumu mgombea wake wa Rais, Hillary Clinton. Mwaka 2006 Skripal alihukumiwa kifungo cha miaka 13, nchini Urusi katika kesi ambayo iliendeshwa katika mahakama ya siri, alipewa haki ya ukimbizi na ukazi nchini Uingereza mwaka 2010 baada ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa katika mtindo ambao ulitumika enzi za vita baridi kuhusiana na shughuli za kijasusi. Kulingana na nyaraka za kumbukumbu ambazo vyombo vya habari vya Uingereza vilizipata kutoka makumbusho ya taifa ya Uingereza mwaka 2015, zinaonyesha kuwa Serikali ya Urusi imekuwa ikiichunguza Uingereza muda mrefu lakini kisa kinachojulikana sana ni kile kilichopewa jina la Cambridge Four, ambapo kitengo cha ujasusi cha shirikisho la Urusi (USSR), KGB, katika miaka ya 1930 kabla ya vita vya pili vya dunia kiligundua kuwa Serikali ya Uingereza ilikuwa ikitumia Chuo Kikuu cha Cambridge kama sehemu maalumu ya kuwapata majasusi wachanga wakiwa masomoni. KGB waliwafuata wanafunzi wanne wa wakati huo ambao ni Anthony Blunt, Donald Duart Maclean, Kim Phillby na Guy Burgess. Wasomi hao ambao kwa bahati nzuri kwao KGB walipomaliza masomo yao waliingia kufanya kazi katika Mashirika ya Ujasusi ya Uingereza, MI5 na MI6, na wakawa ni majasusi ndumilakuwili. Walifanya kazi yao hadi mwaka 1964 ambapo Anthony Blunt ambaye alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Ujasusi wa ndani, MI5, alikiri kuwa jasusi ndumilakuwili ili asishtakiwe na habari hiyo ilikuja kutolewa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo, Magreth Thatcher alipokuwa akihutubia Bunge mwaka 1979. Donald Duart Maclean, Kim Phillby na Guy Burgess wao walitimkia Urusi na Serikali ya Uingereza ikawa imekubali yaiishe. Kwa hiyo Urusi imekuwa hailali usingizi wakati wote wa miaka ya vita baridi kati ya nchi za Ulaya Mashariki na Magharibi miaka ya 1945 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1990, imekuwa ikiingiza wapelelezi wake maeneo mbalimbali katika nchi hizo ili kupata habari nyeti kuhusiana na masuala mbalimbali katika nyanja za uchumi, biashara hasa ya silaha na teknolojia yake na hivi karibuni kuingilia mambo ya siasa za uchaguzi huko Marekani. Ukiangalia kisa cha safari hii hakina tofauti sana kile alichofanyiwa Jasusi mwingine wa Urusi Novemba 2006, Alexander Litvinenko ambaye aliwekewa kemikali iitwayo Polonium 210 katika kikombe cha chai katika mgahawa mmoja jijini London. Litvinenko alitoroka Urusi baada ya kutofautiana na wenzake katika shirika la kijasusi la nchi hiyo FSB, ambapo aliutuhumu uongozi wa juu wa nchi hiyo kuigeuza nchi hiyo kuwa Taifa la kimafia. akiwa nchini Uingereza, alifanya kazi kama mwandishi wa habari, vitabu na mshauri wa mambo ya usalama. Akiwa Uingereza aliandika vitabu viwili, Blowing up Russia: Terror from within na Lubyanka Criminal Group ambapo aliituhumu idara hiyo ya kijasusi kwa vitendo vya mauaji na matumizi ya mabomu na mauaji ya mwandishi wa habari, Anna Politkovskaya kwa amri kutoka kwa Rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin. Litvinenko akiwa mahututi kitandani hospitalini jijini London aliwatamkia ndugu zake kuwa alikuwa na uhakika kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin ndiye aliyeamuru auawe. Serikali ya Uingereza ya wakati huo chini ya Waziri Mkuu, Tony Blair ilifanya upelelezi na kugundua kuwa jasusi huyo siku chache kabla ya kupata mkasa huo alikuwa ametembelewa na jasusi mwingine mstaafu wa FSB ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara, Andrey Lugovoy. Serikali ya Uingereza iliitaka Urusi imsalimishe kwake ili afanyiwe mahojiano lakini Urusi ilikataa kwa maelezo kuwa Katiba ya nchi hiyo inakataza raia wake kupelekwa nchi nyingine kufanyiwa mashtaka ya jinai. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulififia kwa muda. Serikali ya Uingereza kwa matukio yote haya imekuwa ikiituhumu serikali ya Urusi kwa kile inachoeleza kuwa kemikali hizo haziwezi kuwa mikononi mwa mtu binafsi bila kuwa na kibari cha mamlaka za juu za nchi hiyo. Wakati Kim Phillby alipokimbilia Urusi baada ya kushtukia kuwa wenzake walikuwa wanaelekea kumgundua kuwa ni ndumilakuwili, Ofisa mmoja wa ngazi ya juu ndani ya KGB wakati huo alimsifu kuwa alikuwa jasusi mwenye thamani kubwa wa karne iliyopita. Urusi imekuwa ikitoa ulinzi wa kiwango cha juu kwa majasusi ndumilakuwili ambao wamefanikiwa kuingia nchini humo baada ya mambo kwenda kombo huko kwao. Marekani nayo haikuwahi kupona kwa taasisi zake za kijasusi kuingiliwa na wenzao wa Urusi. Mwaka 2001 Shirika la Ujasusi wa Ndani, FBI, lilimkamata Robert Hanssen ambaye alikuwa mtumishi wake kwa kupeleka taarifa za siri za nchi hiyo kwa Urusi tangu mwaka 1979 kwa kulipwa fedha na almasi. Kwa sehemu kubwa shughuli za ujasusi zimekuwa zikifanywa kwa njia ya teknolojia (Artificial Intelligence) ambapo mitambo ya kompyuta na setelaiti na kamera zenye nguvu za kunasa picha hutumika na pale ambapo haiwezekani, inabidi kutumia binadamu (human intelligence) ili kupata habari ambazo ni siri na mataifa karibu yote duniani yameuweka ujasusi kama ni kosa la uhaini kwa yeyote atakayejihusisha nao.
    0 Comments ·0 Shares ·1K Views
More Results