• “Ukiwa Mwandishi wa Habari una vitu viwili muhimu vya kuchunga navyo ni Ulimi wako na Mikono yako, unapaswa kufahamu unaongea nini ama unaandika kitu gani, nyuma ya mauaji ya Kimbari yalikuwa ni matamshi ya Watangazaji pia ambao walieneza chuki, kwasasa kuna kazi mbili za hatari nazo ni Ualimu na Waandishi wa Habari, hawa wanaweza kutengeneza taifa la Wajinga ama Waelevu.

    Nataka kusema nini? Nataka kusema juu ya kelele na shutuma za Yanga na Singida bado hakuna aliyetupa picha kamili zaidi ni kuwa Mashabiki wanalalamika kwa hisia, Waandishi tunalalamika kwa hisia ila hakuna anayekuja mbele kutoa usahihi, inaitwa Proving beyond reasonable doubt! Nimeona Wadau wanasema TFF haifanyi chochote, lakini wewe umewapa tip gani? Taasisi haifanyi maamuzi kwa hisia, the corporate world works differently from streets.

    Bado kizazi chetu cha Uandishi kuna kitu kinamiss ni INVESTIGATIVE JOURNALISM, binafsi nakiri wazi TUMEFELI sana eneo hili, yaani sote tunalaumu Singida kufanya rotation tunaita kupanga matokeo, tangu lini duniani kubadili kikosi chako ni kupanga matokeo? Ikitokea Coastal kabadili kikosi, ikitokea Simba kabadili ama AZAM? Yani timu inalaumiwa kwa kutumia Wachezaji wake?

    Tunaweza kuwa na hoja ila mpaka sasa hazina mashiko zaidi tunaonekana tunalalama ila tukipelekwa Mahakamani hakuna ambaye atathibitisha chochote, kama kufungwa ni kupanga matokeo mara ya mwisho Simba kumfunga Yanga ndani ya dakika 90 ni lini? Kama kufungwa ni kupanga matokeo lini Singida kamfunga Simba? Kama kufungwa ni kupanga lini Namungo kamfunga Simba lini?

    Sisi WAANDISHI tuna homework tunapaswa kufanya, tutaharibu fikra za Watanzania! Wenzetu Ulaya walipoibua kashfa ya Casciopoli pale Italia walikuja na data, hata UEFA Heated Balls Scandal watu walikuwa na data! Yanga wakisema waende kisheria nani anaweza kuja na hoja za kueleweka? Kama hakuna taarifa sahihi, mifano hai basi tunaongelea hisia, TFF atareact endapo atajitokea Mtu akaattack matter not the subject" - Farhan JR, Mchambuzi.

    “Ukiwa Mwandishi wa Habari una vitu viwili muhimu vya kuchunga navyo ni Ulimi wako na Mikono yako, unapaswa kufahamu unaongea nini ama unaandika kitu gani, nyuma ya mauaji ya Kimbari yalikuwa ni matamshi ya Watangazaji pia ambao walieneza chuki, kwasasa kuna kazi mbili za hatari nazo ni Ualimu na Waandishi wa Habari, hawa wanaweza kutengeneza taifa la Wajinga ama Waelevu. Nataka kusema nini? Nataka kusema juu ya kelele na shutuma za Yanga na Singida bado hakuna aliyetupa picha kamili zaidi ni kuwa Mashabiki wanalalamika kwa hisia, Waandishi tunalalamika kwa hisia ila hakuna anayekuja mbele kutoa usahihi, inaitwa Proving beyond reasonable doubt! Nimeona Wadau wanasema TFF haifanyi chochote, lakini wewe umewapa tip gani? Taasisi haifanyi maamuzi kwa hisia, the corporate world works differently from streets. Bado kizazi chetu cha Uandishi kuna kitu kinamiss ni INVESTIGATIVE JOURNALISM, binafsi nakiri wazi TUMEFELI sana eneo hili, yaani sote tunalaumu Singida kufanya rotation tunaita kupanga matokeo, tangu lini duniani kubadili kikosi chako ni kupanga matokeo? Ikitokea Coastal kabadili kikosi, ikitokea Simba kabadili ama AZAM? Yani timu inalaumiwa kwa kutumia Wachezaji wake? Tunaweza kuwa na hoja ila mpaka sasa hazina mashiko zaidi tunaonekana tunalalama ila tukipelekwa Mahakamani hakuna ambaye atathibitisha chochote, kama kufungwa ni kupanga matokeo mara ya mwisho Simba kumfunga Yanga ndani ya dakika 90 ni lini? Kama kufungwa ni kupanga matokeo lini Singida kamfunga Simba? Kama kufungwa ni kupanga lini Namungo kamfunga Simba lini? Sisi WAANDISHI tuna homework tunapaswa kufanya, tutaharibu fikra za Watanzania! Wenzetu Ulaya walipoibua kashfa ya Casciopoli pale Italia walikuja na data, hata UEFA Heated Balls Scandal watu walikuwa na data! Yanga wakisema waende kisheria nani anaweza kuja na hoja za kueleweka? Kama hakuna taarifa sahihi, mifano hai basi tunaongelea hisia, TFF atareact endapo atajitokea Mtu akaattack matter not the subject" - Farhan JR, Mchambuzi.
    0 Comments ·0 Shares ·109 Views
  • Mkojo wa Sungura wageuka dhahabu Nchini Kenya.

    Kumekukuwa na wimbi kubwa la mahitaji ya mkojo wa Sungura Nchini Kenya huku lita moja (1) ikiuzwa kwa Shilingi elfu moja (1,000) ambazo ni takribani Shilingi 19,885 za Kitanzania hali ambayo imepelekea Wakulima wengi kuvutiwa zaidi kuwekeza katika ufugaji wa Wanyama hao.

    Sanjari na kitoweo cha Sungura kuuzwa kwa kati ya Shilingi elfu moja (1,000) na elfu elfu mbili (2,000) za Kenya (39,790 Tsh) kwa kilo, Wakulima sasa wanapata faida kutokana na mkojo wa Mnyama huyo, ambao hutumika kama mbolea ya asili na dawa ya kuua Wadudu wanaoshambulia mimea.

    Mkojo wa Sungura wageuka dhahabu Nchini Kenya. Kumekukuwa na wimbi kubwa la mahitaji ya mkojo wa Sungura Nchini Kenya 🇰🇪 huku lita moja (1) ikiuzwa kwa Shilingi elfu moja (1,000) ambazo ni takribani Shilingi 19,885 za Kitanzania hali ambayo imepelekea Wakulima wengi kuvutiwa zaidi kuwekeza katika ufugaji wa Wanyama hao. Sanjari na kitoweo cha Sungura kuuzwa kwa kati ya Shilingi elfu moja (1,000) na elfu elfu mbili (2,000) za Kenya (39,790 Tsh) kwa kilo, Wakulima sasa wanapata faida kutokana na mkojo wa Mnyama huyo, ambao hutumika kama mbolea ya asili na dawa ya kuua Wadudu wanaoshambulia mimea.
    0 Comments ·0 Shares ·35 Views
  • "Wakati tunazilaumu Simba Sports na Azam Football Club Kuukosa Ubingwa,tukumbuke pia Mazingira Yao Magumu ya Kushindana

    Parameters za Simba Sports na Azam Fc Kuchukua Ubingwa zimebadilika Kabisa na ni tofauti Washindani wenzao Kwenye Ligi

    Kuna hoja Lazy sana eti Mbona Simba Sports alicheza na Tabora United Dhaifu?

    Kwenye Mechi zote 2 Tabora wana uwezo wa Ku justifie Kwanini walichezesha Vikosi vile na ukawaelewa vizuri tu.

    Mechi ya Kwanza n issue ya Vibali,na mechi ya Pili Heritier Makambo alikuwa na Kadi 3 za njano. Yacouba Sogne alikuwa ni Majeruhi..

    Kuna hoja Lazy nyingine Kwamba mbona Kikosi bora cha Singida Black Stars Kilifungwa 2-0 na KMC ambayo ilifungwa 6-1 na Yanga?

    Kwanza Kwenye hiyo hoja hapo wote tumekubaliana Kwamba Singida Black Stars wamepanga Kikosi Dhaifu

    Pili, Sisi hatusemi Singida Black Stars angepanga Kikosi bora lazima angeshinda dhidi ya Yanga au asingepoteza mechi

    Mbona ile Mechi ya Kwanza Kule Amani Complex Zanzibar Singida Black Stars waliweka Full Mkoko na bado Yanga alishinda 1-0 bao la Paccome ?

    Swali ni Sababu ipi ya Singida Black Stars Kubadilisha wachezaji 6 Kutoka Kwenye Kikosi Kilichomfunga Jkt Tanzania 1-0?

    Mbaya zaidi Kuna wachezaji walichezeshwa Kabisa nje ya Maeneo ya ya asili na wachezaji wenye nafasi zao wakiwa bench

    Singida black stars Dhaifu ilipigwa 2-0 Kipindi Cha Kwanza na Stars bora ilishinda 1-0 Kipindi cha Pili.

    Ligi yetu tukufu inachezewa na watu ambao hawana nia njema na Mpira wetu na Kama tusipotwanga sasa hivi tutakuja Kuula Mbichi" - Wilson Orumo, Mchambuzi.

    "Wakati tunazilaumu Simba Sports na Azam Football Club Kuukosa Ubingwa,tukumbuke pia Mazingira Yao Magumu ya Kushindana Parameters za Simba Sports na Azam Fc Kuchukua Ubingwa zimebadilika Kabisa na ni tofauti Washindani wenzao Kwenye Ligi Kuna hoja Lazy sana eti Mbona Simba Sports alicheza na Tabora United Dhaifu? Kwenye Mechi zote 2 Tabora wana uwezo wa Ku justifie Kwanini walichezesha Vikosi vile na ukawaelewa vizuri tu. Mechi ya Kwanza n issue ya Vibali,na mechi ya Pili Heritier Makambo alikuwa na Kadi 3 za njano. Yacouba Sogne alikuwa ni Majeruhi.. Kuna hoja Lazy nyingine Kwamba mbona Kikosi bora cha Singida Black Stars Kilifungwa 2-0 na KMC ambayo ilifungwa 6-1 na Yanga? Kwanza Kwenye hiyo hoja hapo wote tumekubaliana Kwamba Singida Black Stars wamepanga Kikosi Dhaifu Pili, Sisi hatusemi Singida Black Stars angepanga Kikosi bora lazima angeshinda dhidi ya Yanga au asingepoteza mechi Mbona ile Mechi ya Kwanza Kule Amani Complex Zanzibar Singida Black Stars waliweka Full Mkoko na bado Yanga alishinda 1-0 bao la Paccome ? Swali ni Sababu ipi ya Singida Black Stars Kubadilisha wachezaji 6 Kutoka Kwenye Kikosi Kilichomfunga Jkt Tanzania 1-0? Mbaya zaidi Kuna wachezaji walichezeshwa Kabisa nje ya Maeneo ya ya asili na wachezaji wenye nafasi zao wakiwa bench Singida black stars Dhaifu ilipigwa 2-0 Kipindi Cha Kwanza na Stars bora ilishinda 1-0 Kipindi cha Pili. Ligi yetu tukufu inachezewa na watu ambao hawana nia njema na Mpira wetu na Kama tusipotwanga sasa hivi tutakuja Kuula Mbichi" - Wilson Orumo, Mchambuzi.
    0 Comments ·0 Shares ·76 Views

  • KUTOKA SINGIDA BLACK STARS

    HII NI KWENU WACHAMBUZI WOTE WENYE USHABIKI KULIKO UCHAMBUZI

    Singida Black stars Sc ni Timu yenye utaratibu wake na mipango yake juu ya kuiongoza Timu yake kwa misingi yake

    Timu yetu haipangiwi na wala hatupelekeshwi na maneno ya mitandaoni katika kuiendesha Timu Yetu, Tunaomba Mfahamu kuwa kila mchezaji Tuliyemsajili anatufaa na anafaa kuipambania Nembo ya Timu yetu

    Katika kikosi chetu chenye jumla ya wachezaji 33 wote wakiwa wazima wa Afya na Fitness nzuri kocha wetu na Benchi letu la Ufundi lina uhuru wa Kumchagua Mchezaji yeyote akaanza katika kikosi cha kwanza katika mchezo wowote

    Rejea michezo Yetu Mitatu ya nyuma kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Yanga sc Tulicheza michezo 3 dhidi ya Kagera Sugar, KMC Fc, na JKT Tanzania

    Katika mchezo wetu dhidi ya Kagera sugar tulianzisha wachezaji wengi wa kimataifa na Tulipata sare ya goli 2-2 mchezo uliofuata tukacheza dhidi ya KMC FC na wachezaji wengi wa kimataifa walianza pia tukafungwa goli 2 bila Benchi la ufundi kikafanya mabadiliko kadhaa kwenye mchezo uliofuata dhidi ya JKT Tanzania Na tukapata ushindi kwenye moja ya Viwanja ambavyo Timu zote za ligi kuu hakuna iliyopata ushindi

    Baada ya Benchi la Ufundi kuridhika na vipaji vya wachezaji wetu wa ndani waliotupa Ushindi wa mchezo wa JKT Tanzania wakaridhishwa kwamba wachezaji wale wanafaa baadhi yao kuanza kwenye mchezo dhidi ya Yanga, kwa upande wa Timu yetu Tumefurahi Timu ilicheza vizuri kwa nidhamu ya hali ya juu na mchezo ukaisha kwa goal 2-1

    Sasa baada ya mchezo ule wameibuka watu wanaojiita wachambuzi kwa vivuli vya ushabiki wao na roho zao mbaya na umaskini uliowajaa wanataka kutupangia Kikosi chetu kitu Ambacho kwetu hakikubaliki hata kidogo

    Ni mfano uone mwanaume Ameoa wake 4 alafu wewe jirani yake unataka kumpangia kwamba Leo kalale kwa mwanamke huyu na utapikiwa na huyu hilo haliwezekani Abadani SISI HATUPANGIWI MAISHA NA VITAKATAKA KAMA NYINYI
    KUTOKA SINGIDA BLACK STARS ✍️ HII NI KWENU WACHAMBUZI WOTE WENYE USHABIKI KULIKO UCHAMBUZI Singida Black stars Sc ni Timu yenye utaratibu wake na mipango yake juu ya kuiongoza Timu yake kwa misingi yake Timu yetu haipangiwi na wala hatupelekeshwi na maneno ya mitandaoni katika kuiendesha Timu Yetu, Tunaomba Mfahamu kuwa kila mchezaji Tuliyemsajili anatufaa na anafaa kuipambania Nembo ya Timu yetu Katika kikosi chetu chenye jumla ya wachezaji 33 wote wakiwa wazima wa Afya na Fitness nzuri kocha wetu na Benchi letu la Ufundi lina uhuru wa Kumchagua Mchezaji yeyote akaanza katika kikosi cha kwanza katika mchezo wowote Rejea michezo Yetu Mitatu ya nyuma kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Yanga sc Tulicheza michezo 3 dhidi ya Kagera Sugar, KMC Fc, na JKT Tanzania Katika mchezo wetu dhidi ya Kagera sugar tulianzisha wachezaji wengi wa kimataifa na Tulipata sare ya goli 2-2 mchezo uliofuata tukacheza dhidi ya KMC FC na wachezaji wengi wa kimataifa walianza pia tukafungwa goli 2 bila Benchi la ufundi kikafanya mabadiliko kadhaa kwenye mchezo uliofuata dhidi ya JKT Tanzania Na tukapata ushindi kwenye moja ya Viwanja ambavyo Timu zote za ligi kuu hakuna iliyopata ushindi Baada ya Benchi la Ufundi kuridhika na vipaji vya wachezaji wetu wa ndani waliotupa Ushindi wa mchezo wa JKT Tanzania wakaridhishwa kwamba wachezaji wale wanafaa baadhi yao kuanza kwenye mchezo dhidi ya Yanga, kwa upande wa Timu yetu Tumefurahi Timu ilicheza vizuri kwa nidhamu ya hali ya juu na mchezo ukaisha kwa goal 2-1 Sasa baada ya mchezo ule wameibuka watu wanaojiita wachambuzi kwa vivuli vya ushabiki wao na roho zao mbaya na umaskini uliowajaa wanataka kutupangia Kikosi chetu kitu Ambacho kwetu hakikubaliki hata kidogo Ni mfano uone mwanaume Ameoa wake 4 alafu wewe jirani yake unataka kumpangia kwamba Leo kalale kwa mwanamke huyu na utapikiwa na huyu hilo haliwezekani Abadani SISI HATUPANGIWI MAISHA NA VITAKATAKA KAMA NYINYI
    0 Comments ·0 Shares ·78 Views
  • Tanzania 2️⃣ - 0️⃣ Burkina Faso
    Tanzania 2️⃣ - 0️⃣ Burkina Faso 😂😂
    Like
    1
    · 1 Comments ·0 Shares ·10 Views
  • Mahakama ya ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) imeanza kusikiliza shauri la Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo dhidi ya Nchi ya Rwanda , ambalo limefunguliwa kwenye mahakama hiyo iliyoko Jijini Arusha Nchini Tanzania .

    Aidha, DR Congo ilifungua kesi dhidi ya Rwanda, Agosti 21 2023, ikiituhumu Nchi hiyo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu. Kupitia kesi namba 007/2023, DR Congo inadai kuwa Nchi ya Rwanda inahusika na mgogoro unaeondelea Mashariki mwa Nchi hiyo hasa Mkoa wa Sud-Kivu.

    Mahakama ya ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) imeanza kusikiliza shauri la Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 dhidi ya Nchi ya Rwanda 🇷🇼, ambalo limefunguliwa kwenye mahakama hiyo iliyoko Jijini Arusha Nchini Tanzania 🇹🇿. Aidha, DR Congo ilifungua kesi dhidi ya Rwanda, Agosti 21 2023, ikiituhumu Nchi hiyo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu. Kupitia kesi namba 007/2023, DR Congo inadai kuwa Nchi ya Rwanda inahusika na mgogoro unaeondelea Mashariki mwa Nchi hiyo hasa Mkoa wa Sud-Kivu.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·160 Views
  • "Kuanzia Msimu ujao tunakuja na kanuni ya Golikipa Mmoja tu wakigeni kwenye kila timu haiwezekani kwenye timu moja kuwe na magolikipa wawili wa kigeni haiwezekani hii”

    “Nilikua namtania Rais mwenzangu wa shirikisho aliniambia Mbona kwenye ligi yako kuna wachezaji wa kigeni wengi sana nikamjibu kua siwadekezi watu wavivu, ukiangalia pale Yanga kuna mabeki wengi wakizawa ndio wanacheza hata Siimba pia hivyo hivyo” - W. Karia, Rais wa Shirikisho la Mpira Nchini Tanzania (TFF) kupitia Wasafi FM.

    "Kuanzia Msimu ujao tunakuja na kanuni ya Golikipa Mmoja tu wakigeni kwenye kila timu haiwezekani kwenye timu moja kuwe na magolikipa wawili wa kigeni haiwezekani hii” “Nilikua namtania Rais mwenzangu wa shirikisho aliniambia Mbona kwenye ligi yako kuna wachezaji wa kigeni wengi sana nikamjibu kua siwadekezi watu wavivu, ukiangalia pale Yanga kuna mabeki wengi wakizawa ndio wanacheza hata Siimba pia hivyo hivyo” - W. Karia, Rais wa Shirikisho la Mpira Nchini Tanzania (TFF) kupitia Wasafi FM.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·159 Views
  • "Wakati nakuja Dar nikitokea Kigoma nilimdanganya Mzee (baba yangu). Nilikuwa mwalimu Kigoma, nilimdanganya Mzee kuwa nimepata shule nyingine Dar es Salaam na hapo sikuwa nimepata shule.

    "Mimi mwalimu wa Sekondari nafundisha kuanzia Form One hadi Four. Nilikuwa mwalimu wa Hesabu na Chemistry

    "Kwahiyo nilimwambia Mzee nimepata shule nyingine wanalipa hela nyingi kuliko Kigoma. Akaniruhusu. Ukweli sikuwa na shule na sikujua nafikia wapi"

    "Nilijilipua kwamba nikifika Dar natoboa. Nilikuja na Treni. Sikutaka kupanda basi. Nilikuwa nawacheki washkaji zangu waliopo Dar wote waliniambia hawapo.

    "Nilimcheki dogo mmoja aliniambia yupo Dar anaishi Ubungo. Nilimwambia na Mimi nakuja Dar kuna ishu naifuatilia Gongo la Mboto (nilimdanganya)"- Ndaro, Mchekeshaji (Tanzania) kupitia Clouds TV.

    "Wakati nakuja Dar nikitokea Kigoma nilimdanganya Mzee (baba yangu). Nilikuwa mwalimu Kigoma, nilimdanganya Mzee kuwa nimepata shule nyingine Dar es Salaam na hapo sikuwa nimepata shule. "Mimi mwalimu wa Sekondari nafundisha kuanzia Form One hadi Four. Nilikuwa mwalimu wa Hesabu na Chemistry "Kwahiyo nilimwambia Mzee nimepata shule nyingine wanalipa hela nyingi kuliko Kigoma. Akaniruhusu. Ukweli sikuwa na shule na sikujua nafikia wapi" "Nilijilipua kwamba nikifika Dar natoboa. Nilikuja na Treni. Sikutaka kupanda basi. Nilikuwa nawacheki washkaji zangu waliopo Dar wote waliniambia hawapo. "Nilimcheki dogo mmoja aliniambia yupo Dar anaishi Ubungo. Nilimwambia na Mimi nakuja Dar kuna ishu naifuatilia Gongo la Mboto (nilimdanganya)"- Ndaro, Mchekeshaji (Tanzania) kupitia Clouds TV.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·126 Views
  • #SportsEliteMsimamo wa Ligi ya @championshiptz ya @nbc_tanzania
    #SportsElite🇹🇿Msimamo wa Ligi ya @championshiptz ya @nbc_tanzania
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·152 Views
  • Kwa mujibu wa The Citizens, zaidi ya kampuni tano (5) za kigeni kutoka Nchini Ufaransa na Misri pamoja na Wawekezaji wa ndani ya Tanzania , wameonyesha nia ya kuwekeza katika usafirishaji wa nyaya yaani "cable" kwa lugha ya Kiingereza. Ili kufanikisha hilo sasa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) inakamilisha Kanuni za Usafiri wa Waya za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini za Mwaka, 2024 katika ngazi ya Serikali.

    Kanuni zingine zinazoendelea zinazopendekezwa ni pamoja na Kanuni za LATRA (Utoaji Leseni kwa Waendeshaji Reli) 2024 na Kanuni ya Utoaji Leseni ya Usafiri (Leseni ya Kipekee ya Usafiri wa Umma), 2024. Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa LATRA, Salum Pazzy ameiambia The Citizen kwamba kampuni mbili kutoka Ufaransa na moja kutoka Misri zimejitokeza zikisubiri idhini ya kuwekeza katika sekta hiyo.

    Kampuni hizi zimewasilisha mapendekezo yao na yanasubiri kuidhinishwa kwa kanuni ili kujihakikishia mazingira mazuri kwani usafiri wa waya unaonekana kuwa fursa kubwa ya kiuwekezaji.

    Kwa mujibu wa The Citizens, zaidi ya kampuni tano (5) za kigeni kutoka Nchini Ufaransa 🇫🇷 na Misri 🇪🇬 pamoja na Wawekezaji wa ndani ya Tanzania 🇹🇿, wameonyesha nia ya kuwekeza katika usafirishaji wa nyaya yaani "cable" kwa lugha ya Kiingereza. Ili kufanikisha hilo sasa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) inakamilisha Kanuni za Usafiri wa Waya za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini za Mwaka, 2024 katika ngazi ya Serikali. Kanuni zingine zinazoendelea zinazopendekezwa ni pamoja na Kanuni za LATRA (Utoaji Leseni kwa Waendeshaji Reli) 2024 na Kanuni ya Utoaji Leseni ya Usafiri (Leseni ya Kipekee ya Usafiri wa Umma), 2024. Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa LATRA, Salum Pazzy ameiambia The Citizen kwamba kampuni mbili kutoka Ufaransa na moja kutoka Misri zimejitokeza zikisubiri idhini ya kuwekeza katika sekta hiyo. Kampuni hizi zimewasilisha mapendekezo yao na yanasubiri kuidhinishwa kwa kanuni ili kujihakikishia mazingira mazuri kwani usafiri wa waya unaonekana kuwa fursa kubwa ya kiuwekezaji.
    Like
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·252 Views
  • Na umoja wa klabu zinazodhaminiwa na Azam TV (Media) hatujafurahi hata kidogo .

    NB : Klabu zinazodhaminiwa na Azam TV ni klabu zote za Ligi Kuu Tanzania Bara.

    Na umoja wa klabu zinazodhaminiwa na Azam TV (Media) hatujafurahi hata kidogo 😆. NB : Klabu zinazodhaminiwa na Azam TV ni klabu zote za Ligi Kuu Tanzania Bara.
    0 Comments ·0 Shares ·188 Views
  • Maazimio (22) ya Marais wa Nchi Wanachama wa SADC na EAC kwenye mkutano uliofanyika leo hii Jijini Dar Es Salaam, Tanzania , Azimio la (12) limewataka Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Nchi zote Wanachama kukutana ndani ya siku tano (5) na kutoa mwelekeo wa kitalaam kuhusu mambo yafuatayo:

    - Kusitisha mara moja mapigano huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo .

    - Kutoa misaada ya Kibinadamu na kuwasaidia Wahanga wa vita.

    - Kutoa mpango kazi wa ulinzi ndani ya Mji wa Goma na maeneo Jirani.

    - Kuzifungua njia muhimu za mawasiliano kwenye Miji ya Goma - Kibumba- Rumangambo - Kalengera- Rutshuru na Goma - Kiwanja- Rwindi lakini pia matumizi ya Ziwa Kivu kwa ajili ya usafiri.

    - Kuufungua Uwanja wa Ndege wa Mji Goma mara moja.

    Maazimio (22) ya Marais wa Nchi Wanachama wa SADC na EAC kwenye mkutano uliofanyika leo hii Jijini Dar Es Salaam, Tanzania 🇹🇿, Azimio la (12) limewataka Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Nchi zote Wanachama kukutana ndani ya siku tano (5) na kutoa mwelekeo wa kitalaam kuhusu mambo yafuatayo: - Kusitisha mara moja mapigano huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo 🇨🇩. - Kutoa misaada ya Kibinadamu na kuwasaidia Wahanga wa vita. - Kutoa mpango kazi wa ulinzi ndani ya Mji wa Goma na maeneo Jirani. - Kuzifungua njia muhimu za mawasiliano kwenye Miji ya Goma - Kibumba- Rumangambo - Kalengera- Rutshuru na Goma - Kiwanja- Rwindi lakini pia matumizi ya Ziwa Kivu kwa ajili ya usafiri. - Kuufungua Uwanja wa Ndege wa Mji Goma mara moja.
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·271 Views
  • #PART5

    Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite.

    Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo.

    Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba.

    Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay.

    April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha.

    March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa.

    Kumekua na jitihada mbalimbali za kumaliza mgogoro wa DRC kwa njia za kidiplomasia ikiwemo mkutano wa viongozi wakuu wa SADC na EAC uliofanyika leo jijini Dar.

    #MyaTake:
    1. Congo imeponzwa na ukarimu wake. Wakati wa vita vya Rwanda, Congo ilipokea Watutsi wengi na kuwapa hifadhi, akiwemo Kagame. Baada ya utawala wa Habyarimana kuangushwa Wahutu nao wakakimbilia Congo na kupewa hifadhi. Sasa hicho kimekua kigezo cha Rwanda kuingiza majeshi Congo kila mara kwa madai ya kuwatafuta Wahutu wa FDLR. Kwa lugha rahisi vita ya ndugu wawili (Wahutu na Watutsi) iliyopaswa kupiganwa Rwanda sasa inapiganwa Congo.

    2. Congo inateswa na mipaka ya kikoloni. Laiti wakati wa kuchora mipaka jamii yote ya Watutsi ingewekwa Rwanda, leo kusingekuwa na Banyamulenge Congo, kwahiyo Watutsi wasingepata sababu ya kuishi Congo na kujifanya raia. Ni sawa na kukuta Wamasai 1,000 pale Longido, halafu uambiwe kati yao wapo wa Kenya. Utawajuaje? Utawatofautishaje?

    3. Congo inateswa na rasilimali zake. Kama eneo la Kivu lisingekuwa na utajiri, mgogoro usingekuwa mkubwa kama ulivyo. Rejea #Part1 kujua utajiri uliopo Kivu. Kumbuka bila Kivu dunia haina laptop wala smartphones kwa sababu 80% ya coltan yote duniani inatoka Kivu.

    4. Rwanda na Uganda ni Keyplayers kwenye mgogoro wa Congo. Kwa miaka mingi majeshi yao yameigeuza Congo shamba la bibi. Waondoe majeshi yao Congo.

    5. Viongozi wengi wa M23 ni Wanyarwanda. Huu ni udhibitisho kuwa Rwanda ni kinara kwenye mgogoro huu.

    6. Congo ni kubwa sana na hivyo inakosa jeshi imara la kutosha kulinda mipaka yake yote. Congo ni kubwa mara 90 ya Rwanda. Wapo wanaoshauri igawanywe kama njia ya kutatua mgogoro. Kama ambavyo Yugoslavia iligawanywa na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.

    7. Kiongozi wa sasa wa M23 Corneille Nangaa alikua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi 2019 na ndiye aliyemtangaza Tshisekedi kuwa Rais kwa ushindi wa 38%. Lakini alilaumiwa kupunguza kura za Martin Fayulu aliyepata 34%. Huenda kuna ahadi alipewa haikutimizwa ndio maana akaungana na Waasi.

    Sababu hizo hapo juu zikifanyiwa kazi, mgogoro wa Congo unaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Mnaopenda kujifunza zaidi, naandika Kitabu. Get ready to have your copy. MWISHO.!

    (Malisa GJ )

    #PART5 Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite. Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo. Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba. Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay. April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha. March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa. Kumekua na jitihada mbalimbali za kumaliza mgogoro wa DRC kwa njia za kidiplomasia ikiwemo mkutano wa viongozi wakuu wa SADC na EAC uliofanyika leo jijini Dar. #MyaTake: 1. Congo imeponzwa na ukarimu wake. Wakati wa vita vya Rwanda, Congo ilipokea Watutsi wengi na kuwapa hifadhi, akiwemo Kagame. Baada ya utawala wa Habyarimana kuangushwa Wahutu nao wakakimbilia Congo na kupewa hifadhi. Sasa hicho kimekua kigezo cha Rwanda kuingiza majeshi Congo kila mara kwa madai ya kuwatafuta Wahutu wa FDLR. Kwa lugha rahisi vita ya ndugu wawili (Wahutu na Watutsi) iliyopaswa kupiganwa Rwanda sasa inapiganwa Congo. 2. Congo inateswa na mipaka ya kikoloni. Laiti wakati wa kuchora mipaka jamii yote ya Watutsi ingewekwa Rwanda, leo kusingekuwa na Banyamulenge Congo, kwahiyo Watutsi wasingepata sababu ya kuishi Congo na kujifanya raia. Ni sawa na kukuta Wamasai 1,000 pale Longido, halafu uambiwe kati yao wapo wa Kenya. Utawajuaje? Utawatofautishaje? 3. Congo inateswa na rasilimali zake. Kama eneo la Kivu lisingekuwa na utajiri, mgogoro usingekuwa mkubwa kama ulivyo. Rejea #Part1 kujua utajiri uliopo Kivu. Kumbuka bila Kivu dunia haina laptop wala smartphones kwa sababu 80% ya coltan yote duniani inatoka Kivu. 4. Rwanda na Uganda ni Keyplayers kwenye mgogoro wa Congo. Kwa miaka mingi majeshi yao yameigeuza Congo shamba la bibi. Waondoe majeshi yao Congo. 5. Viongozi wengi wa M23 ni Wanyarwanda. Huu ni udhibitisho kuwa Rwanda ni kinara kwenye mgogoro huu. 6. Congo ni kubwa sana na hivyo inakosa jeshi imara la kutosha kulinda mipaka yake yote. Congo ni kubwa mara 90 ya Rwanda. Wapo wanaoshauri igawanywe kama njia ya kutatua mgogoro. Kama ambavyo Yugoslavia iligawanywa na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe. 7. Kiongozi wa sasa wa M23 Corneille Nangaa alikua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi 2019 na ndiye aliyemtangaza Tshisekedi kuwa Rais kwa ushindi wa 38%. Lakini alilaumiwa kupunguza kura za Martin Fayulu aliyepata 34%. Huenda kuna ahadi alipewa haikutimizwa ndio maana akaungana na Waasi. Sababu hizo hapo juu zikifanyiwa kazi, mgogoro wa Congo unaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Mnaopenda kujifunza zaidi, naandika Kitabu. Get ready to have your copy. MWISHO.! (Malisa GJ ✍️)
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·676 Views
  • #PART12

    Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite.

    Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo.

    Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba.

    Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay.

    April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha.

    March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa.!
    (Malisa GJ)

    #PART12 Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite. Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo. Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba. Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay. April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha. March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa.! (Malisa GJ)
    0 Comments ·0 Shares ·580 Views
  • Chukua hii.

    Kama utakwenda Nchini Japan na kusikia neno "Johatsu" (じょうはつ) tambua kuwa ni Mtu au Watu waliotoweka (kupotea) kutoka kwenye familia zao kutokana na sababu mbalimbali kama vile migogoro kwenye Ndoa, kushindwa kuoa, kukimbia madeni, kufukuzwa kazi na kadhalika. Watu hao huacha maisha yao na kuishi bila kujulikana wapi walipo kwa muda fulani na inaweze kuwa ni ndani ya Nchi ya Japan au nje Nchi yaani mataifa mengine kama vile Tanzania DR Congo , Burundi , Marekani , Mexico , Kenya ,....

    Pamoja na Watu hao kupotea, lakini wanasaidiwa na Makampuni ambayo yamebobea katika kazi hiyo yaani Watu au Mtu anayehitaji huduma hiyo unalipia kisha kuhamishwa usiku. Makampuni hayo maalumu yanajulikana kwa jina la "Wahamishaji Usiku" huwasaidia Watu kupotea (unaweza kusema kujiteka, kujipoteza,...).

    Haya Mashirika au Makampuni husaidia Watu kutoweka kwa kuwahamisha kwa siri sana na mara nyingi kazi hii hufanyika usiku na wanapokupeleka inakuwa ni siri kubwa yaani kuanzia mahali pa kulala, utakula nini, vitambulisho vipya vya kusafiria Kampuni hizo ndizo zinafanya kila kitu kwa mujibu wa mkataba wenu.

    Pia Kampuni hizi zitahakikisha zinasafisha kumbukumbu zote za Mteja na kusahaulika kwenye Jamii, Nyumbani na Nchi kwa ujumla kisha unaanza mwanzo mpya wa kuanzisha maisha mengine kwenye Nchi au mahali walipo kupeleka.

    Chukua hii. Kama utakwenda Nchini Japan 🇯🇵 na kusikia neno "Johatsu" (じょうはつ) tambua kuwa ni Mtu au Watu waliotoweka (kupotea) kutoka kwenye familia zao kutokana na sababu mbalimbali kama vile migogoro kwenye Ndoa, kushindwa kuoa, kukimbia madeni, kufukuzwa kazi na kadhalika. Watu hao huacha maisha yao na kuishi bila kujulikana wapi walipo kwa muda fulani na inaweze kuwa ni ndani ya Nchi ya Japan au nje Nchi yaani mataifa mengine kama vile Tanzania 🇨🇩 DR Congo 🇨🇩, Burundi 🇧🇮, Marekani 🇺🇸, Mexico 🇲🇽, Kenya 🇰🇪,.... Pamoja na Watu hao kupotea, lakini wanasaidiwa na Makampuni ambayo yamebobea katika kazi hiyo yaani Watu au Mtu anayehitaji huduma hiyo unalipia kisha kuhamishwa usiku. Makampuni hayo maalumu yanajulikana kwa jina la "Wahamishaji Usiku" huwasaidia Watu kupotea (unaweza kusema kujiteka, kujipoteza,...). Haya Mashirika au Makampuni husaidia Watu kutoweka kwa kuwahamisha kwa siri sana na mara nyingi kazi hii hufanyika usiku na wanapokupeleka inakuwa ni siri kubwa yaani kuanzia mahali pa kulala, utakula nini, vitambulisho vipya vya kusafiria Kampuni hizo ndizo zinafanya kila kitu kwa mujibu wa mkataba wenu. Pia Kampuni hizi zitahakikisha zinasafisha kumbukumbu zote za Mteja na kusahaulika kwenye Jamii, Nyumbani na Nchi kwa ujumla kisha unaanza mwanzo mpya wa kuanzisha maisha mengine kwenye Nchi au mahali walipo kupeleka.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·366 Views
  • Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Msanii wa muziki wa zamani Ferdnand Ndikuriyo (27) maarufu Chuma cha Chuma kutoka Nchini Burundi , kutumikia kifungo cha miaka mitatu (3) Jela na kulipa faini ya Shilingi 500,000 baada ya kukutwa na hatia ya kuishi Nchini Tanzania bila kibali.

    Hukumu hiyo imetolewa leo, Februari 5, 2025, na Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga, baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa. Ikumbukwe kwamba Chuma cha Chuma alikamatwa kwa kosa hilo Septemba 18, 2024, katika eneo la Las Vegas Casino, Upanga Wilayani Ilala, Jijini Dar es Salaam.

    Hakimu Ruboroga alisema kuwa mshtakiwa ni Mkosaji wa mara ya pili (2) na kwamba anahitaji kupewa adhabu kali ili iwe fundisho kwake na kwa Watu wengine wanaojihusisha na vitendo kama hivyo vya kuingia Nchini Tanzania bila vibali (uhamiaji haramu).

    Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Msanii wa muziki wa zamani Ferdnand Ndikuriyo (27) maarufu Chuma cha Chuma kutoka Nchini Burundi 🇧🇮, kutumikia kifungo cha miaka mitatu (3) Jela na kulipa faini ya Shilingi 500,000 baada ya kukutwa na hatia ya kuishi Nchini Tanzania 🇹🇿 bila kibali. Hukumu hiyo imetolewa leo, Februari 5, 2025, na Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga, baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa. Ikumbukwe kwamba Chuma cha Chuma alikamatwa kwa kosa hilo Septemba 18, 2024, katika eneo la Las Vegas Casino, Upanga Wilayani Ilala, Jijini Dar es Salaam. Hakimu Ruboroga alisema kuwa mshtakiwa ni Mkosaji wa mara ya pili (2) na kwamba anahitaji kupewa adhabu kali ili iwe fundisho kwake na kwa Watu wengine wanaojihusisha na vitendo kama hivyo vya kuingia Nchini Tanzania bila vibali (uhamiaji haramu).
    0 Comments ·0 Shares ·232 Views
  • 𝐏𝐑𝐄𝐒𝐒

    "Tunahitaji kujaribu kucheza kati ya mistari. Tunapaswa kucheza katika nafasi ndogo nyuma ya safu ya ulinzi. Tunahitaji kuwasambaza ili tuweze kupata nafasi kati ya mistari. Kwa ujumla, itakuwa mechi ngumu tena, lakini kama ninavyosema kila wakati, sisi ni timu bora zaidi nchini Tanzania. Tumeshinda taji mara tatu, na tunataka kushinda tena" Sead Ramovic

    #timuyawananchi
    #daimambelenyumamwiko
    𝐏𝐑𝐄𝐒𝐒💬 "Tunahitaji kujaribu kucheza kati ya mistari. Tunapaswa kucheza katika nafasi ndogo nyuma ya safu ya ulinzi. Tunahitaji kuwasambaza ili tuweze kupata nafasi kati ya mistari. Kwa ujumla, itakuwa mechi ngumu tena, lakini kama ninavyosema kila wakati, sisi ni timu bora zaidi nchini Tanzania. Tumeshinda taji mara tatu, na tunataka kushinda tena" Sead Ramovic #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·463 Views
  • Rais Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , Felix Tshisekedi na Paul Kagame wa Rwanda, wanatarajia kukutana Jijini Dar es Salaam, Tanzania, Februari 8, 2025 kujadili mustakabali wa hali ya usalama inayoendelea eneo la Mashariki mwa DR Congo.

    Taarifa iliyotolewa na Rais wa Kenya, William Ruto, wawili hao watakutana katika mkutano wa pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), baada ya Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kuridhia Nchi yake ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo.

    Rais Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩, Felix Tshisekedi na Paul Kagame wa Rwanda, wanatarajia kukutana Jijini Dar es Salaam, Tanzania, Februari 8, 2025 kujadili mustakabali wa hali ya usalama inayoendelea eneo la Mashariki mwa DR Congo. Taarifa iliyotolewa na Rais wa Kenya, William Ruto, wawili hao watakutana katika mkutano wa pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), baada ya Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kuridhia Nchi yake ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo.
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·347 Views
  • "Naona jinsi Media mnatumia nguvu kubwa sana kupotosha watu kwa kila jambo lililofanyika na kwasasa sisemi kitu basi kila mtu anaandika lolote analojisikia ili afuatiliwe na watu. Binafsi upande mnaousimamia ninaujua na ndio sababu sikuongea kupitia media yoyote ile"

    "Naujua mfumo uliopo na kilichofanyika kimefanyika, na hata muandike mabaya kiasi gani kusudi la Mungu bado litasimama. Kwenye zile interviews sina la kuongeza nilishamaliza kila kitu"- Goodluck Gozbert, Msanii wa muziki wa Injili Tanzania.
    "Naona jinsi Media mnatumia nguvu kubwa sana kupotosha watu kwa kila jambo lililofanyika na kwasasa sisemi kitu basi kila mtu anaandika lolote analojisikia ili afuatiliwe na watu. Binafsi upande mnaousimamia ninaujua na ndio sababu sikuongea kupitia media yoyote ile" "Naujua mfumo uliopo na kilichofanyika kimefanyika, na hata muandike mabaya kiasi gani kusudi la Mungu bado litasimama. Kwenye zile interviews sina la kuongeza nilishamaliza kila kitu"- Goodluck Gozbert, Msanii wa muziki wa Injili Tanzania.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·260 Views
  • #PART3

    Baadhi ya wanajeshi wa Kitutsi hawakuridhika na ukandamizaji uliofanywa na Habyarimana. Wakajiorganize kupambana. Wakati huo Kagame akiwa askari wa NRA ya Uganda akimsaidia Museveni vita vya msituni. Mwaka 1983 hadi 1985 alienda kozi ya kijeshi TMA, Moduli. Alipohitimu akarudi Uganda kumsaidia Museveni vita vya msituni na hatimaye mwaka 1986 wakafanikiwa kuchukua nchi. NRA ikawa sehemu ya jeshi la Uganda kabla ya kubadilishwa muundo mwaka 1995 kuwa UPDF.

    Kagame akawa mkuu wa intelijensia ya jeshi. Baadae akaenda masomoni Marekani. Akiwa huko RPF ikaanzishwa na Jenerali Fredy Rwigyema kupambana na Serikali ya Habyarimana. Lakini Jenerali Rwigyema akauawa kwa guruneti akiwa uwanja wa vita. Kagame akalazimika kukatisha masomo na kurudi Rwanda kuongoza RPF akishirikiana na Alexis Kanyarwenge. Museveni akampa msaada wa fedha, silaha na chakula. RPF ikaweka kambi Uganda eneo la Kabale, Burundi eneo la Muyinga na Congo maeneo ya Kivu, Uvira na Goma.

    Mwaka 1994, askari wa RPF wakatungua ndege ya Rais Habyarimana ikiwa inakaribia kutua uwanja wa ndege wa Kigali ikitokea Dar es Salaam kwenye mazungumzo ya Amani alikuwa na Rais Cyprien Ntaramira wa Burundi. Wote wawili walikufa papo hapo.

    Kuuawa kwa Rais Habyarimana kuliamsha hasira za Wahutu na kusabisha mauaji ya Kimbari ambapo Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa kikatili kwa kucharangwa mapanga. Hali hiyo ilisababisha Watutsi wengi kukimbia nchi yao. Wapo waliokimbilia Tanzania, Uganda, lakini wengi zaidi walikimbilia eneo la Kivu.

    Kwa kifupi, idadi ya Watutsi eneo la Kivu iliongezeka siku hadi siku. Watutsi walioenda Kivu wengi hawakurudi Rwanda hata baada ya vita kumalizika. Ilikuwa vigumu kutofautisha Mtutsi mwenye asili ya Congo (Banyamulenge) na Mtutsi wa Rwanda, kwa sababu wote wanaongea lugha moja, mila na desturi moja.

    Kwahiyo hisia za Wakongomani kwamba Banyamulenge ni wageni zikaanza kupata nguvu kutokana na uhamiaji mkubwa wa Watutsi maeneo ya Kivu kaskazini na kusini. Wakati huo Congo ikiitwa Zaire Rais Mobutu Sese Seko alikataa kuwatambua Banyamulenge kama raia wake, na akazuia wasipewe vitambulisho vya taifa.
    (Malisa GJ)

    #PART3 Baadhi ya wanajeshi wa Kitutsi hawakuridhika na ukandamizaji uliofanywa na Habyarimana. Wakajiorganize kupambana. Wakati huo Kagame akiwa askari wa NRA ya Uganda akimsaidia Museveni vita vya msituni. Mwaka 1983 hadi 1985 alienda kozi ya kijeshi TMA, Moduli. Alipohitimu akarudi Uganda kumsaidia Museveni vita vya msituni na hatimaye mwaka 1986 wakafanikiwa kuchukua nchi. NRA ikawa sehemu ya jeshi la Uganda kabla ya kubadilishwa muundo mwaka 1995 kuwa UPDF. Kagame akawa mkuu wa intelijensia ya jeshi. Baadae akaenda masomoni Marekani. Akiwa huko RPF ikaanzishwa na Jenerali Fredy Rwigyema kupambana na Serikali ya Habyarimana. Lakini Jenerali Rwigyema akauawa kwa guruneti akiwa uwanja wa vita. Kagame akalazimika kukatisha masomo na kurudi Rwanda kuongoza RPF akishirikiana na Alexis Kanyarwenge. Museveni akampa msaada wa fedha, silaha na chakula. RPF ikaweka kambi Uganda eneo la Kabale, Burundi eneo la Muyinga na Congo maeneo ya Kivu, Uvira na Goma. Mwaka 1994, askari wa RPF wakatungua ndege ya Rais Habyarimana ikiwa inakaribia kutua uwanja wa ndege wa Kigali ikitokea Dar es Salaam kwenye mazungumzo ya Amani alikuwa na Rais Cyprien Ntaramira wa Burundi. Wote wawili walikufa papo hapo. Kuuawa kwa Rais Habyarimana kuliamsha hasira za Wahutu na kusabisha mauaji ya Kimbari ambapo Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa kikatili kwa kucharangwa mapanga. Hali hiyo ilisababisha Watutsi wengi kukimbia nchi yao. Wapo waliokimbilia Tanzania, Uganda, lakini wengi zaidi walikimbilia eneo la Kivu. Kwa kifupi, idadi ya Watutsi eneo la Kivu iliongezeka siku hadi siku. Watutsi walioenda Kivu wengi hawakurudi Rwanda hata baada ya vita kumalizika. Ilikuwa vigumu kutofautisha Mtutsi mwenye asili ya Congo (Banyamulenge) na Mtutsi wa Rwanda, kwa sababu wote wanaongea lugha moja, mila na desturi moja. Kwahiyo hisia za Wakongomani kwamba Banyamulenge ni wageni zikaanza kupata nguvu kutokana na uhamiaji mkubwa wa Watutsi maeneo ya Kivu kaskazini na kusini. Wakati huo Congo ikiitwa Zaire Rais Mobutu Sese Seko alikataa kuwatambua Banyamulenge kama raia wake, na akazuia wasipewe vitambulisho vya taifa. (Malisa GJ)
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·490 Views
More Results