• Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo , Felix Tshisekedi ameitaka Nchi ya Marekani kununua madini moja kwa moja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akiitaja ndio "mmiliki halisi" wa rasilimali hizo na sio Nchi Rwanda .

    Tshisekedi amesema kuwa anaanza kwa kutoa ofa hiyo kwa Marekani kwanza huku akitoa pendekezo hilo pia liko wazi kwa mataifa ya Umoja Ulaya (EU) na wanunuzi wengine wanaotafuta na kununua madini kutoka Nchini Rwanda kwa sasa.

    Rais huyo amewaonya Mataifa yanayonunua madini kutoka Nchini Rwanda kuwa wanachukua madini yaliyoibwa kutoka Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, kwahiyo wanatakiwa kununua kwa mmiliki halali. Ikumbukwe kwamba Nchi ya Rwanda ni moja ya kati ya Nchi zinauza madini mengi barani Afrika kwa Mataifa ya Ulaya, Marekani na Asia.

    Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo 🇨🇩, Felix Tshisekedi ameitaka Nchi ya Marekani 🇺🇸 kununua madini moja kwa moja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akiitaja ndio "mmiliki halisi" wa rasilimali hizo na sio Nchi Rwanda 🇷🇼. Tshisekedi amesema kuwa anaanza kwa kutoa ofa hiyo kwa Marekani kwanza huku akitoa pendekezo hilo pia liko wazi kwa mataifa ya Umoja Ulaya (EU) na wanunuzi wengine wanaotafuta na kununua madini kutoka Nchini Rwanda kwa sasa. Rais huyo amewaonya Mataifa yanayonunua madini kutoka Nchini Rwanda kuwa wanachukua madini yaliyoibwa kutoka Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, kwahiyo wanatakiwa kununua kwa mmiliki halali. Ikumbukwe kwamba Nchi ya Rwanda ni moja ya kati ya Nchi zinauza madini mengi barani Afrika kwa Mataifa ya Ulaya, Marekani na Asia.
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·15 Views
  • Zambia wana Laptop zao zinaitwa NEO, Rwanda wana MARA Phones na Satelite , Uganda wana Simu zao zinaitwa SIMI, Kenya wana Laptop zao zinaitwa TAIFA Wana Starlink pia wana Satelite yao, Tanzania tuna nini ?
    Zambia wana Laptop zao zinaitwa NEO, Rwanda wana MARA Phones na Satelite , Uganda wana Simu zao zinaitwa SIMI, Kenya wana Laptop zao zinaitwa TAIFA Wana Starlink pia wana Satelite yao, Tanzania tuna nini ?
    Like
    Wow
    2
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·125 Views
  • Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeomba msaada wa kijeshi kutoka Nchini Chad katika jitihada zake za kupambana na Waasi wa kundi la M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda . Waziri anayeshughulikia masuala ya kikanda wa DR Congo alikutana na Rais wa Chad, Mahamat Idriss Deby Itno, Jumanne akimuwakilisha Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi, kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Rais wa Chad na kusasishwa kwenye wa mtandao wa Facebook.

    Maelezo ya kina ya mazungumzo yao hajawekwa wazi. Mmoja wa Maafisa wa Chad anayeyefahamu mazungumzo hayo alisema Chad inalibeba ombi la kuombwa msaada na DR Congo, lakini bado haijafanya maamuzi kuhusu ombi hilo. Chanzo kutoka Ofisi ya Rais DR Congo C kimeiambia BBC kuwa kuwa Nchi hiyo imeomba msaada wa kijeshi na kidiplomasia kutoka Nchini Chad.

    Hata hivyo chanzo hicho ambacho hakijataka kutambulishwa kwa sababu za ndani, hakijatoa maelezo zaidi. Msemaji wa Serikali ya Chad, Gassim Cherif, hakujibu ombi la kutoa maoni yake kuhusu hili, kwa mujibu wa Reuters. Kwa upande wake, Msemaji wa Rais Tshisekedi, Tina Salama, alisema hana taarifa yoyote kuhusu suala hilo.

    Wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad aliiambia Reuters kuwa kupeleka msaada wa kijeshi DR Congo ni "taarifa za tetesi" bado haijathibitishwa rasmi.
    (BBC)

    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 imeomba msaada wa kijeshi kutoka Nchini Chad 🇹🇩 katika jitihada zake za kupambana na Waasi wa kundi la M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda 🇷🇼. Waziri anayeshughulikia masuala ya kikanda wa DR Congo alikutana na Rais wa Chad, Mahamat Idriss Deby Itno, Jumanne akimuwakilisha Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi, kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Rais wa Chad na kusasishwa kwenye wa mtandao wa Facebook. Maelezo ya kina ya mazungumzo yao hajawekwa wazi. Mmoja wa Maafisa wa Chad anayeyefahamu mazungumzo hayo alisema Chad inalibeba ombi la kuombwa msaada na DR Congo, lakini bado haijafanya maamuzi kuhusu ombi hilo. Chanzo kutoka Ofisi ya Rais DR Congo C kimeiambia BBC kuwa kuwa Nchi hiyo imeomba msaada wa kijeshi na kidiplomasia kutoka Nchini Chad. Hata hivyo chanzo hicho ambacho hakijataka kutambulishwa kwa sababu za ndani, hakijatoa maelezo zaidi. Msemaji wa Serikali ya Chad, Gassim Cherif, hakujibu ombi la kutoa maoni yake kuhusu hili, kwa mujibu wa Reuters. Kwa upande wake, Msemaji wa Rais Tshisekedi, Tina Salama, alisema hana taarifa yoyote kuhusu suala hilo. Wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad aliiambia Reuters kuwa kupeleka msaada wa kijeshi DR Congo ni "taarifa za tetesi" bado haijathibitishwa rasmi. (BBC)
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·210 Views
  • Rais wa Rwanda , Paul Kagame ameweka wazi kuwa hana hofu na vitisho vya vikwazo vinavyotolewa na Mataifa ya Magharibi dhidi ya Nchi yake akisisitiza kuwa Rwanda itachukua hatua zozote zinazohitajika kulinda maslahi yake, akizungumza na Gazeti la Jeune Afrique, Kagame amezungumzia kwa kina mzozo kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na shinikizo kutoka Ulaya na Marekani .

    Kagame amesisitiza kuwa hatakubali mashinikizo yanayoelekezwa kwa Rwanda kwa lengo la kuidhoofisha akisema Nchi yake inayo haki ya kujilinda dhidi ya vitisho vyovyote vya nje ambapo Mataifa ya Magharibi yanaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono kundi la Waasi wa M23 wanaopigana mashariki mwa DR Congo jambo ambalo Rwanda imekanusha mara kadhaa.

    Kauli Kagame inakuja wakati mvutano kati ya Rwanda na DR Congo ukiendelea huku mataifa ya Magharibi yakitoa wito wa mazungumzo ya amani lakini licha ya hivyo Rwanda imeendelea kusisitiza kuwa haitakubali kushinikizwa kwa njia yoyote ikibainisha kuwa hatua zake zitalenga kulinda usalama wa Taifa lake kwa gharama yoyote.
    (DW Swahili)

    Rais wa Rwanda 🇷🇼, Paul Kagame ameweka wazi kuwa hana hofu na vitisho vya vikwazo vinavyotolewa na Mataifa ya Magharibi dhidi ya Nchi yake akisisitiza kuwa Rwanda itachukua hatua zozote zinazohitajika kulinda maslahi yake, akizungumza na Gazeti la Jeune Afrique, Kagame amezungumzia kwa kina mzozo kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 pamoja na shinikizo kutoka Ulaya na Marekani 🇺🇸. Kagame amesisitiza kuwa hatakubali mashinikizo yanayoelekezwa kwa Rwanda kwa lengo la kuidhoofisha akisema Nchi yake inayo haki ya kujilinda dhidi ya vitisho vyovyote vya nje ambapo Mataifa ya Magharibi yanaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono kundi la Waasi wa M23 wanaopigana mashariki mwa DR Congo jambo ambalo Rwanda imekanusha mara kadhaa. Kauli Kagame inakuja wakati mvutano kati ya Rwanda na DR Congo ukiendelea huku mataifa ya Magharibi yakitoa wito wa mazungumzo ya amani lakini licha ya hivyo Rwanda imeendelea kusisitiza kuwa haitakubali kushinikizwa kwa njia yoyote ikibainisha kuwa hatua zake zitalenga kulinda usalama wa Taifa lake kwa gharama yoyote. (DW Swahili)
    Love
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·157 Views
  • Wapiganaji wa kundi la Waasi wa M23 na Askari wanaodhaniwa kuwa ni Rwanda wameendelea kusonga mbele katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo . Hayo ni kwa mujibu wa vyanzo vya eneo hilo pamoja na vya mashirika ya kibinadamu. Miji iliyotekwa ni Ihusi na Kalehe, iliyoko karibu kiliomita sitini (60) kutoka Mji wa Bukavu.

    Katika taarifa, Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeitisha mkutano wa dharura wa mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutathmini hali hiyo na "kutathmini hali na matokeo ya kitendo hiki kipya cha uchokozi", ikitoa wito wa vikwazo.

    Rais wa Burundi , Evariste Ndayishimiye amesema yeyote atakayeishambulia Nchi yake naye atashambuliwa. Wakati huo huo, Viongozi wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Nchini DR Congo na ule wa Kanisa la Kristo la DR Congo umekutana na kundi la Waasi wa M23 Mjini Goma katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kusaka amani na mazungumzo. Walikutana na kiongozi wa kisiasa wa kundi la M23 Corneille Nangaa.
    (DW Swahili)

    Wapiganaji wa kundi la Waasi wa M23 na Askari wanaodhaniwa kuwa ni Rwanda 🇷🇼 wameendelea kusonga mbele katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Hayo ni kwa mujibu wa vyanzo vya eneo hilo pamoja na vya mashirika ya kibinadamu. Miji iliyotekwa ni Ihusi na Kalehe, iliyoko karibu kiliomita sitini (60) kutoka Mji wa Bukavu. Katika taarifa, Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeitisha mkutano wa dharura wa mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutathmini hali hiyo na "kutathmini hali na matokeo ya kitendo hiki kipya cha uchokozi", ikitoa wito wa vikwazo. Rais wa Burundi 🇧🇮, Evariste Ndayishimiye amesema yeyote atakayeishambulia Nchi yake naye atashambuliwa. Wakati huo huo, Viongozi wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Nchini DR Congo na ule wa Kanisa la Kristo la DR Congo umekutana na kundi la Waasi wa M23 Mjini Goma katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kusaka amani na mazungumzo. Walikutana na kiongozi wa kisiasa wa kundi la M23 Corneille Nangaa. (DW Swahili)
    Love
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·216 Views
  • "Unajua hadithi hiyo, sihitaji kuirudia. Tuna
    angalau makubaliano matano na serikali za Congo tangu Mwaka 2007 na hakuna hata mmoja wao ambaye ameheshimu toka DRC. Wanamgambo wa mauaji ya kimbari bado wanaishi Congo. Kuifanya Rwanda kuwa tatizo ni njia ya kuficha tatizo halisi na kuandika upya historia kwa kumbadilisha mhasiriwa kuwa Mnyongaji“

    "Halafu kuna kutokubaliana kwa wazi na udanganyifu kwa upande wa nchi , kama Ubelgiji, ambazo ni sehemu ya historia na tatizo. Serikali ya DRC inaajiri mamluki, kama kila mtu anavyojua.Wanatoka wapi? Kutoka Ulaya. Je, umewahi kusikia kuhusu nchi moja ya Ulaya wanalaumu wale raia wao ambao wanahusika, pamoja na serikali pia. Nani aliwaajiri?Hakuna. Na bado wanaendelea kurudia kwamba kila kitu ni makosa ya Rwanda. ” - Paul Kagame, Rais wa Rwanda kupitia AJ

    "Unajua hadithi hiyo, sihitaji kuirudia. Tuna angalau makubaliano matano na serikali za Congo tangu Mwaka 2007 na hakuna hata mmoja wao ambaye ameheshimu toka DRC. Wanamgambo wa mauaji ya kimbari bado wanaishi Congo. Kuifanya Rwanda kuwa tatizo ni njia ya kuficha tatizo halisi na kuandika upya historia kwa kumbadilisha mhasiriwa kuwa Mnyongaji“ "Halafu kuna kutokubaliana kwa wazi na udanganyifu kwa upande wa nchi , kama Ubelgiji, ambazo ni sehemu ya historia na tatizo. Serikali ya DRC inaajiri mamluki, kama kila mtu anavyojua.Wanatoka wapi? Kutoka Ulaya. Je, umewahi kusikia kuhusu nchi moja ya Ulaya wanalaumu wale raia wao ambao wanahusika, pamoja na serikali pia. Nani aliwaajiri?Hakuna. Na bado wanaendelea kurudia kwamba kila kitu ni makosa ya Rwanda. ” - Paul Kagame, Rais wa Rwanda 🇷🇼 kupitia AJ
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·150 Views
  • Mahakama ya ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) imeanza kusikiliza shauri la Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo dhidi ya Nchi ya Rwanda , ambalo limefunguliwa kwenye mahakama hiyo iliyoko Jijini Arusha Nchini Tanzania .

    Aidha, DR Congo ilifungua kesi dhidi ya Rwanda, Agosti 21 2023, ikiituhumu Nchi hiyo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu. Kupitia kesi namba 007/2023, DR Congo inadai kuwa Nchi ya Rwanda inahusika na mgogoro unaeondelea Mashariki mwa Nchi hiyo hasa Mkoa wa Sud-Kivu.

    Mahakama ya ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) imeanza kusikiliza shauri la Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 dhidi ya Nchi ya Rwanda 🇷🇼, ambalo limefunguliwa kwenye mahakama hiyo iliyoko Jijini Arusha Nchini Tanzania 🇹🇿. Aidha, DR Congo ilifungua kesi dhidi ya Rwanda, Agosti 21 2023, ikiituhumu Nchi hiyo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu. Kupitia kesi namba 007/2023, DR Congo inadai kuwa Nchi ya Rwanda inahusika na mgogoro unaeondelea Mashariki mwa Nchi hiyo hasa Mkoa wa Sud-Kivu.
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·193 Views
  • Rais wa Nchi ya Rwanda , Paul Kagame ameendelea kukanusha madai kuwa wao kuwa ndiyo chanzo cha mgogoro wa Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kusema kuwa huo ni mgogoro wa ndani ya DR Congo na hautoki nje ya Congo na suluhu lazima itoke kwa Serikali ya Nchi hiyo.

    Ikumbukwe kwamba Rais Paul Kagame alihudhuria mkutano wa Marais wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika Febuari 8,2025 uliojadili namna gani ya kurudisha usalama Nchini DR Congo ambapo Waasi wa kundi la M23 wameiteka Mkoa wa Kivu Kaskazini.

    Rais wa Nchi ya Rwanda 🇷🇼, Paul Kagame ameendelea kukanusha madai kuwa wao kuwa ndiyo chanzo cha mgogoro wa Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 kwa kusema kuwa huo ni mgogoro wa ndani ya DR Congo na hautoki nje ya Congo na suluhu lazima itoke kwa Serikali ya Nchi hiyo. Ikumbukwe kwamba Rais Paul Kagame alihudhuria mkutano wa Marais wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika Febuari 8,2025 uliojadili namna gani ya kurudisha usalama Nchini DR Congo ambapo Waasi wa kundi la M23 wameiteka Mkoa wa Kivu Kaskazini.
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·150 Views
  • Hii joint meeting imehudhuriwa na viongozi karibu wote wa SADC na EAC kwa kutambua umuhimu wake kwa usalama eneo la maziwa makuu.

    Viongozi hawa wanajua kuwa usalama wa eneo hili ni muhimu kwa ustawi wa kanda nzima, hasa ikizingatiwa mizozo ya muda mrefu kama ile ya Mashariki mwa DRC.

    Lakini pia hata viongozi ambao nchi zao zimekuwa kwenye msuguano kwenye mgogoro wa Congo wamehushuria. Paul Kagame wa Rwanda na Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini wamehudhuria pia.

    Wote tunakumbuka kwamba hivi karibuni Kagame na Ramaphosa walikuwa kwenye uhasama hawa kwa sababu ya tuhuma zinazoelekewa kwa Rwanda kwamba wanawaunda mkono M23, kundi la waasi linalohusishwa na kuvuruga amani Mashariki mwa DRC.

    Hata hivyo, Tshisekedi ameshindwa kuona umuhimu wa mkutano huu mpaka kumtuma mwakilishi badala yake?

    Hii inaashiria kutokuwa na ushirikiano wa kutosha au kutokubaliana na juhudi za kutatua mgogoro huu kwa njia ya kidiplomasia.

    Is this a sign of deeper political divisions within the DRC or a strategic move to maintain sovereignty?..
    Hii joint meeting imehudhuriwa na viongozi karibu wote wa SADC na EAC kwa kutambua umuhimu wake kwa usalama eneo la maziwa makuu. Viongozi hawa wanajua kuwa usalama wa eneo hili ni muhimu kwa ustawi wa kanda nzima, hasa ikizingatiwa mizozo ya muda mrefu kama ile ya Mashariki mwa DRC. Lakini pia hata viongozi ambao nchi zao zimekuwa kwenye msuguano kwenye mgogoro wa Congo wamehushuria. Paul Kagame wa Rwanda na Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini wamehudhuria pia. Wote tunakumbuka kwamba hivi karibuni Kagame na Ramaphosa walikuwa kwenye uhasama hawa kwa sababu ya tuhuma zinazoelekewa kwa Rwanda kwamba wanawaunda mkono M23, kundi la waasi linalohusishwa na kuvuruga amani Mashariki mwa DRC. Hata hivyo, Tshisekedi ameshindwa kuona umuhimu wa mkutano huu mpaka kumtuma mwakilishi badala yake? Hii inaashiria kutokuwa na ushirikiano wa kutosha au kutokubaliana na juhudi za kutatua mgogoro huu kwa njia ya kidiplomasia. Is this a sign of deeper political divisions within the DRC or a strategic move to maintain sovereignty?..
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·251 Views
  • Kwa mujibu wa Tovuti ya The Guardian, Wananajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) wameripotiwa kuuawa katika operesheni za siri Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo . Kuuawa kwa Wanajeshi hao katika operesheni hiyo kunapingana na msimamo wa Serikali ya Rwanda inayodai Askari wake hawahusiki wala kushiriki katika mzozo unaoendelea kati ya kundi la M23 na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo .

    Taarifa hiyo iliyochapishwa na tovuti ya The Guardian imedai kuwa vyanzo mbalimbali vya kijasusi, kijeshi na kidiplomasia vinasema idadi ya Wanajeshi wa RDF waliouawa ni kubwa, huku wakidai walikuwa wakisaidia mashambulizi yanayofanywa na Waasi wa M23 ndani ya DR Congo.

    Picha za Setilaiti zilizopigwa katika makaburi ya kijeshi yaliyoko Jijini Kigali, Nchini Rwanda, zimethibitisha kuonekana kwa makaburi mapya yasiyopungua 600 yaliyopatikana tangu Waasi wa M23, wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, walipoanza operesheni zao ndani ya DR Congo miaka mitatu iliyopita.

    Kwa mujibu wa Tovuti ya The Guardian, Wananajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda 🇷🇼 (RDF) wameripotiwa kuuawa katika operesheni za siri Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Kuuawa kwa Wanajeshi hao katika operesheni hiyo kunapingana na msimamo wa Serikali ya Rwanda inayodai Askari wake hawahusiki wala kushiriki katika mzozo unaoendelea kati ya kundi la M23 na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Taarifa hiyo iliyochapishwa na tovuti ya The Guardian imedai kuwa vyanzo mbalimbali vya kijasusi, kijeshi na kidiplomasia vinasema idadi ya Wanajeshi wa RDF waliouawa ni kubwa, huku wakidai walikuwa wakisaidia mashambulizi yanayofanywa na Waasi wa M23 ndani ya DR Congo. Picha za Setilaiti zilizopigwa katika makaburi ya kijeshi yaliyoko Jijini Kigali, Nchini Rwanda, zimethibitisha kuonekana kwa makaburi mapya yasiyopungua 600 yaliyopatikana tangu Waasi wa M23, wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, walipoanza operesheni zao ndani ya DR Congo miaka mitatu iliyopita.
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·198 Views
  • Rwanda inalichukulia jeshi la Burundi kama tishio jingine la usalama katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya demokrasi ya Congo (DRC).

    Nchi inayopakana na Rwanda na DRC imekuwa na maelfu ya wanajeshi huko kwa miaka mingi.

    Walikwenda kuwafuatilia waasi wa Burundi lakini sasa wanasaidia jeshi la Kinshasa katika vita dhidi ya M23.

    Uhusiano kati ya Rwanda na Burundi ni mbaya.

    Nchi hizi mbili zina muundo wa kikabila unaofanana lakini kinyume na Rwanda, Hutu ndiyo wanaoshikilia madaraka nchini Burundi.

    Nchi zote mbili zimekashifiana kwa kudai kujaribu kuangusha serikali zao.

    Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, ametoa onyo kali kwenye mitandao ya kijamii.

    "Ikizidi, Rwanda itaendelea na mashambulizi," aliandika, "Najua vita vitafika Burundi… Siku moja atataka kuingia Burundi - hatutakubaliana na hilo. Vita vitapanuka."

    Tishio hili litakuwa kubwa zaidi ikiwa M23 itaendelea na mashambulizi kutoka Goma kuelekea mkoa wa Kivu kusini karibu na mpaka wa Burundi, ambapo vikosi vyake viko.

    "Kile kinachotafutwa na Burundi hapa ni kuokoa utawala wake," alisema Bw. Stearns.

    "Burundi inahofia kuwa kama vikosi vya Rwanda vitaimarisha ushawishi wao katika eneo la Kivu kusini, inaweza kuteteresha serikali ya Bujumbura. Kile kilicho hatarini hapa ni kuzima uasi huu kabla haujaingilia karibu zaidi."

    Wengine wanahofia kurudi kwa vita mbili zilizoshambulia eneo hilo mwishoni mwa miaka ya 1990, ambazo zilihusisha nchi tisa na kusababisha vifo vya mamilioni ya watu.

    Mara hii, mapigano ya moja kwa moja kati ya majeshi mawili yanaweza kupelekea mgogoro wa DRC kuvuka nje ya mipaka yake.
    (BBC Swahili)

    Rwanda inalichukulia jeshi la Burundi kama tishio jingine la usalama katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya demokrasi ya Congo (DRC). Nchi inayopakana na Rwanda na DRC imekuwa na maelfu ya wanajeshi huko kwa miaka mingi. Walikwenda kuwafuatilia waasi wa Burundi lakini sasa wanasaidia jeshi la Kinshasa katika vita dhidi ya M23. Uhusiano kati ya Rwanda na Burundi ni mbaya. Nchi hizi mbili zina muundo wa kikabila unaofanana lakini kinyume na Rwanda, Hutu ndiyo wanaoshikilia madaraka nchini Burundi. Nchi zote mbili zimekashifiana kwa kudai kujaribu kuangusha serikali zao. Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, ametoa onyo kali kwenye mitandao ya kijamii. "Ikizidi, Rwanda itaendelea na mashambulizi," aliandika, "Najua vita vitafika Burundi… Siku moja atataka kuingia Burundi - hatutakubaliana na hilo. Vita vitapanuka." Tishio hili litakuwa kubwa zaidi ikiwa M23 itaendelea na mashambulizi kutoka Goma kuelekea mkoa wa Kivu kusini karibu na mpaka wa Burundi, ambapo vikosi vyake viko. "Kile kinachotafutwa na Burundi hapa ni kuokoa utawala wake," alisema Bw. Stearns. "Burundi inahofia kuwa kama vikosi vya Rwanda vitaimarisha ushawishi wao katika eneo la Kivu kusini, inaweza kuteteresha serikali ya Bujumbura. Kile kilicho hatarini hapa ni kuzima uasi huu kabla haujaingilia karibu zaidi." Wengine wanahofia kurudi kwa vita mbili zilizoshambulia eneo hilo mwishoni mwa miaka ya 1990, ambazo zilihusisha nchi tisa na kusababisha vifo vya mamilioni ya watu. Mara hii, mapigano ya moja kwa moja kati ya majeshi mawili yanaweza kupelekea mgogoro wa DRC kuvuka nje ya mipaka yake. (BBC Swahili)
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·286 Views
  • #PART5

    Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite.

    Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo.

    Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba.

    Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay.

    April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha.

    March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa.

    Kumekua na jitihada mbalimbali za kumaliza mgogoro wa DRC kwa njia za kidiplomasia ikiwemo mkutano wa viongozi wakuu wa SADC na EAC uliofanyika leo jijini Dar.

    #MyaTake:
    1. Congo imeponzwa na ukarimu wake. Wakati wa vita vya Rwanda, Congo ilipokea Watutsi wengi na kuwapa hifadhi, akiwemo Kagame. Baada ya utawala wa Habyarimana kuangushwa Wahutu nao wakakimbilia Congo na kupewa hifadhi. Sasa hicho kimekua kigezo cha Rwanda kuingiza majeshi Congo kila mara kwa madai ya kuwatafuta Wahutu wa FDLR. Kwa lugha rahisi vita ya ndugu wawili (Wahutu na Watutsi) iliyopaswa kupiganwa Rwanda sasa inapiganwa Congo.

    2. Congo inateswa na mipaka ya kikoloni. Laiti wakati wa kuchora mipaka jamii yote ya Watutsi ingewekwa Rwanda, leo kusingekuwa na Banyamulenge Congo, kwahiyo Watutsi wasingepata sababu ya kuishi Congo na kujifanya raia. Ni sawa na kukuta Wamasai 1,000 pale Longido, halafu uambiwe kati yao wapo wa Kenya. Utawajuaje? Utawatofautishaje?

    3. Congo inateswa na rasilimali zake. Kama eneo la Kivu lisingekuwa na utajiri, mgogoro usingekuwa mkubwa kama ulivyo. Rejea #Part1 kujua utajiri uliopo Kivu. Kumbuka bila Kivu dunia haina laptop wala smartphones kwa sababu 80% ya coltan yote duniani inatoka Kivu.

    4. Rwanda na Uganda ni Keyplayers kwenye mgogoro wa Congo. Kwa miaka mingi majeshi yao yameigeuza Congo shamba la bibi. Waondoe majeshi yao Congo.

    5. Viongozi wengi wa M23 ni Wanyarwanda. Huu ni udhibitisho kuwa Rwanda ni kinara kwenye mgogoro huu.

    6. Congo ni kubwa sana na hivyo inakosa jeshi imara la kutosha kulinda mipaka yake yote. Congo ni kubwa mara 90 ya Rwanda. Wapo wanaoshauri igawanywe kama njia ya kutatua mgogoro. Kama ambavyo Yugoslavia iligawanywa na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.

    7. Kiongozi wa sasa wa M23 Corneille Nangaa alikua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi 2019 na ndiye aliyemtangaza Tshisekedi kuwa Rais kwa ushindi wa 38%. Lakini alilaumiwa kupunguza kura za Martin Fayulu aliyepata 34%. Huenda kuna ahadi alipewa haikutimizwa ndio maana akaungana na Waasi.

    Sababu hizo hapo juu zikifanyiwa kazi, mgogoro wa Congo unaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Mnaopenda kujifunza zaidi, naandika Kitabu. Get ready to have your copy. MWISHO.!

    (Malisa GJ )

    #PART5 Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite. Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo. Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba. Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay. April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha. March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa. Kumekua na jitihada mbalimbali za kumaliza mgogoro wa DRC kwa njia za kidiplomasia ikiwemo mkutano wa viongozi wakuu wa SADC na EAC uliofanyika leo jijini Dar. #MyaTake: 1. Congo imeponzwa na ukarimu wake. Wakati wa vita vya Rwanda, Congo ilipokea Watutsi wengi na kuwapa hifadhi, akiwemo Kagame. Baada ya utawala wa Habyarimana kuangushwa Wahutu nao wakakimbilia Congo na kupewa hifadhi. Sasa hicho kimekua kigezo cha Rwanda kuingiza majeshi Congo kila mara kwa madai ya kuwatafuta Wahutu wa FDLR. Kwa lugha rahisi vita ya ndugu wawili (Wahutu na Watutsi) iliyopaswa kupiganwa Rwanda sasa inapiganwa Congo. 2. Congo inateswa na mipaka ya kikoloni. Laiti wakati wa kuchora mipaka jamii yote ya Watutsi ingewekwa Rwanda, leo kusingekuwa na Banyamulenge Congo, kwahiyo Watutsi wasingepata sababu ya kuishi Congo na kujifanya raia. Ni sawa na kukuta Wamasai 1,000 pale Longido, halafu uambiwe kati yao wapo wa Kenya. Utawajuaje? Utawatofautishaje? 3. Congo inateswa na rasilimali zake. Kama eneo la Kivu lisingekuwa na utajiri, mgogoro usingekuwa mkubwa kama ulivyo. Rejea #Part1 kujua utajiri uliopo Kivu. Kumbuka bila Kivu dunia haina laptop wala smartphones kwa sababu 80% ya coltan yote duniani inatoka Kivu. 4. Rwanda na Uganda ni Keyplayers kwenye mgogoro wa Congo. Kwa miaka mingi majeshi yao yameigeuza Congo shamba la bibi. Waondoe majeshi yao Congo. 5. Viongozi wengi wa M23 ni Wanyarwanda. Huu ni udhibitisho kuwa Rwanda ni kinara kwenye mgogoro huu. 6. Congo ni kubwa sana na hivyo inakosa jeshi imara la kutosha kulinda mipaka yake yote. Congo ni kubwa mara 90 ya Rwanda. Wapo wanaoshauri igawanywe kama njia ya kutatua mgogoro. Kama ambavyo Yugoslavia iligawanywa na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe. 7. Kiongozi wa sasa wa M23 Corneille Nangaa alikua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi 2019 na ndiye aliyemtangaza Tshisekedi kuwa Rais kwa ushindi wa 38%. Lakini alilaumiwa kupunguza kura za Martin Fayulu aliyepata 34%. Huenda kuna ahadi alipewa haikutimizwa ndio maana akaungana na Waasi. Sababu hizo hapo juu zikifanyiwa kazi, mgogoro wa Congo unaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Mnaopenda kujifunza zaidi, naandika Kitabu. Get ready to have your copy. MWISHO.! (Malisa GJ ✍️)
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·898 Views
  • "Congo hawawezi kutuambia tukae kimya wakati wanasababisha matatizo makubwa ya kiusalama dhidi yetu, hakuna wa kutuambia tukae kimya, tumeongea na Congo mara nyingi tumewaita tukae tuongee hawataki"

    "Mimi naomba tusiwe na vikao vingi sana kama ambavyo tayari tumeshakuwa navyo, hatuwezi kila siku kukaa kujadili matatizo maana kinachoendelea pale ni vita ya Kikabila ni suala la kutambuana, kujadiliana na kuwapa haki yao, tutumie kikao hiki kupata suluhu ya kudumu na sio matatizo yatokee Congo kisha ubaya anapewa Rwanda” - Paul Kagame, Rais wa Rwanda akiongea kwenye mkutano wa EAC na SADC.

    "Congo hawawezi kutuambia tukae kimya wakati wanasababisha matatizo makubwa ya kiusalama dhidi yetu, hakuna wa kutuambia tukae kimya, tumeongea na Congo mara nyingi tumewaita tukae tuongee hawataki" "Mimi naomba tusiwe na vikao vingi sana kama ambavyo tayari tumeshakuwa navyo, hatuwezi kila siku kukaa kujadili matatizo maana kinachoendelea pale ni vita ya Kikabila ni suala la kutambuana, kujadiliana na kuwapa haki yao, tutumie kikao hiki kupata suluhu ya kudumu na sio matatizo yatokee Congo kisha ubaya anapewa Rwanda” - Paul Kagame, Rais wa Rwanda 🇷🇼 akiongea kwenye mkutano wa EAC na SADC.
    Haha
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·198 Views
  • Kwenye kikao cha pamoja kati ya Jumuiya mbili za SADC na ile ya EAC, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo , Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, ambaye alihudhuria kwa njia ya Mtandao, aliweka wazi matakwa yake kwenye mkutano huo ambapo alisema baadhi ya mambo yakiwemo yafuatayo:

    - Nchi ya Rwanda iambiwe ukweli, ionywe na iachane na uvamizi wake huko Mjini Goma.

    - Vikosi vya Rwanda viondoke mara moja kwenye maeneo ya DR Congo ambayo wanayamiliki pasipo uhalali.

    - Kufunguliwa kwa Uwanja wa Ndege wa Mjini Goma kwa ajili ya misaada ya kibinadamu.

    - Kurejesha Mji wa Goma kwa Mamlaka ya Serikali ya DR Congo.

    Kwenye kikao cha pamoja kati ya Jumuiya mbili za SADC na ile ya EAC, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo 🇨🇩, Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, ambaye alihudhuria kwa njia ya Mtandao, aliweka wazi matakwa yake kwenye mkutano huo ambapo alisema baadhi ya mambo yakiwemo yafuatayo: - Nchi ya Rwanda 🇷🇼 iambiwe ukweli, ionywe na iachane na uvamizi wake huko Mjini Goma. - Vikosi vya Rwanda viondoke mara moja kwenye maeneo ya DR Congo ambayo wanayamiliki pasipo uhalali. - Kufunguliwa kwa Uwanja wa Ndege wa Mjini Goma kwa ajili ya misaada ya kibinadamu. - Kurejesha Mji wa Goma kwa Mamlaka ya Serikali ya DR Congo.
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·160 Views
  • #PART12

    Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite.

    Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo.

    Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba.

    Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay.

    April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha.

    March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa.!
    (Malisa GJ)

    #PART12 Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite. Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo. Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba. Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay. April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha. March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa.! (Malisa GJ)
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·715 Views
  • Jumuiya ya kimataifa inafuatilia kwa karibu hali inayoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), huku mashirika ya haki za binadamu yakilaani uhalifu wa kivita unaofanywa na pande zote dhidi ya raia.

    Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa maelfu ya watu wamelazimika kuyakimbia makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea, huku ukatili dhidi ya wanawake na watoto ukiongezeka kwa kiwango cha kutisha.

    Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetangaza kuwa inafuatilia kwa karibu mzozo huu na imeonya kuwa yeyote anayehusika na uhalifu wa kivita, dhidi ya binadamu, au mauaji ya halaiki hatosazwa na mkono wa sheria.

    Mgogoro wa DRC ni wa muda mrefu na wenye mizizi mirefu. Tangu miaka ya 1990, taifa hili limepitia machafuko ya mara kwa mara, yakichochewa na rasilimali za madini,ukosefu wa utawala thabiti, na uhusiano tata wa kisiasa kati ya mataifa jirani, hususan Rwanda na Uganda.

    M23, kundi la waasi linalotajwa kupokea msaada kutoka nje, limeendelea kushikilia maeneo muhimu, hususan Goma, na hata kutishia kuuteka mji wa Kinshasa.

    Katika mazingira haya, kama ungekuwa Rais wa DRC, Félix Tshisekedi, ungefanya nini?

    Kwa mtazamo wangu, suluhisho pekee ni mazungumzo na diplomasia.

    Historia imeonyesha kuwa vita dhidi ya makundi ya waasi kama M23 si rahisi kushinda kwa nguvu za kijeshi pekee.

    Licha ya msaada wa kijeshi kutoka kwa MONUSCO (Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC) na majeshi ya kikanda kama vile EACRF (East African Community Regional Force), kundi hili limeendelea kuwa tishio kubwa kwa utawala wa Tshisekedi.

    Ikiwa Rais Tshisekedi ataendelea kulazimisha suluhisho la kijeshi bila mpango wa mazungumzo, hatari ipo kwamba mapigano yatapanuka zaidi, na hata kutishia utulivu wa taifa kwa ujumla.

    Hatua muhimu kwa sasa ni kuitisha mazungumzo ya dhati na kutafuta njia ya kidiplomasia ya kumaliza mgogoro huu kabla hali haijazidi kuwa mbaya.
    Jumuiya ya kimataifa inafuatilia kwa karibu hali inayoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), huku mashirika ya haki za binadamu yakilaani uhalifu wa kivita unaofanywa na pande zote dhidi ya raia. Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa maelfu ya watu wamelazimika kuyakimbia makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea, huku ukatili dhidi ya wanawake na watoto ukiongezeka kwa kiwango cha kutisha. Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetangaza kuwa inafuatilia kwa karibu mzozo huu na imeonya kuwa yeyote anayehusika na uhalifu wa kivita, dhidi ya binadamu, au mauaji ya halaiki hatosazwa na mkono wa sheria. Mgogoro wa DRC ni wa muda mrefu na wenye mizizi mirefu. Tangu miaka ya 1990, taifa hili limepitia machafuko ya mara kwa mara, yakichochewa na rasilimali za madini,ukosefu wa utawala thabiti, na uhusiano tata wa kisiasa kati ya mataifa jirani, hususan Rwanda na Uganda. M23, kundi la waasi linalotajwa kupokea msaada kutoka nje, limeendelea kushikilia maeneo muhimu, hususan Goma, na hata kutishia kuuteka mji wa Kinshasa. Katika mazingira haya, kama ungekuwa Rais wa DRC, Félix Tshisekedi, ungefanya nini? Kwa mtazamo wangu, suluhisho pekee ni mazungumzo na diplomasia. Historia imeonyesha kuwa vita dhidi ya makundi ya waasi kama M23 si rahisi kushinda kwa nguvu za kijeshi pekee. Licha ya msaada wa kijeshi kutoka kwa MONUSCO (Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC) na majeshi ya kikanda kama vile EACRF (East African Community Regional Force), kundi hili limeendelea kuwa tishio kubwa kwa utawala wa Tshisekedi. Ikiwa Rais Tshisekedi ataendelea kulazimisha suluhisho la kijeshi bila mpango wa mazungumzo, hatari ipo kwamba mapigano yatapanuka zaidi, na hata kutishia utulivu wa taifa kwa ujumla. Hatua muhimu kwa sasa ni kuitisha mazungumzo ya dhati na kutafuta njia ya kidiplomasia ya kumaliza mgogoro huu kabla hali haijazidi kuwa mbaya.
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·459 Views

  • Katika uteuzi huo, pia wamemteua Meya wa Jiji la Goma pamoja na Wakuu wa Wilaya mbalimbali.

    Hatua hii inakuja wakati maeneo kama Walikale, Lubero, na Beni bado yako chini ya udhibiti wa serikali ya DRC inayoongozwa na Félix Tshisekedi.

    M23, kundi la waasi lenye silaha nzito na za kisasa, linadai kuwa linapigania haki za jamii ya Watutsi wa Congo.

    Jamii ya Watutsi waishio Congo mara nyingi hutengwa, huku serikali ya DRC ikiwatambua kama Wanyarwanda wanaoishi nchini humo.

    Taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa, zikiwemo Umoja wa Mataifa na serikali ya DRC, zinadai kuwa kundi hili linaungwa mkono na Rwanda kwa maslahi ya kiuchumi na kisiasa.

    Hata hivyo, M23 wamekanusha vikali tuhuma hizo, wakisisitiza kuwa hawapokei msaada wa kijeshi kutoka Rwanda na kwamba wanapigana kwa maslahi yao wenyewe..

    Katika uteuzi huo, pia wamemteua Meya wa Jiji la Goma pamoja na Wakuu wa Wilaya mbalimbali. Hatua hii inakuja wakati maeneo kama Walikale, Lubero, na Beni bado yako chini ya udhibiti wa serikali ya DRC inayoongozwa na Félix Tshisekedi. M23, kundi la waasi lenye silaha nzito na za kisasa, linadai kuwa linapigania haki za jamii ya Watutsi wa Congo. Jamii ya Watutsi waishio Congo mara nyingi hutengwa, huku serikali ya DRC ikiwatambua kama Wanyarwanda wanaoishi nchini humo. Taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa, zikiwemo Umoja wa Mataifa na serikali ya DRC, zinadai kuwa kundi hili linaungwa mkono na Rwanda kwa maslahi ya kiuchumi na kisiasa. Hata hivyo, M23 wamekanusha vikali tuhuma hizo, wakisisitiza kuwa hawapokei msaada wa kijeshi kutoka Rwanda na kwamba wanapigana kwa maslahi yao wenyewe..
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·228 Views
  • Inaripotiwa kuwa zaidi ya Wafungwa mia moja (100) wa kike walibakwa na kisha kuchomwa moto wakiwa hai wakati wa hali ya machafuko ilipotokea baada ya Wafungwa kutoroka Gerezani Jijini Goma, Nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo .

    Kulingana na ripoti mpya kutoka kwa Umoja wa Mataifa, mamia ya Wafungwa walitoroka katika Gereza la Munzenze Jumatatu iliyopita, baada ya Wapiganaji wa kundi la Waasi la M23 kuuteka Mji huo wa Goma.

    Ripoti hiyo inaeleza kwamba kati ya Wanawake 165 na 167 walivamiwa na kunyanyaswa na Wafungwa wa kiume walipovunja Gereza. Wengi wa Wanawake hao waliuawa baada ya Wafungwa hao kuchoma moto jela. Jiji hilo la Goma lina ukubwa na Watu zaidi milioni moja (1), lilitekwa na kundi la Waasi la M23, linalodaiwa kuungwa mkono na Rwanda , lilipovamia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

    Inaripotiwa kuwa zaidi ya Wafungwa mia moja (100) wa kike walibakwa na kisha kuchomwa moto wakiwa hai wakati wa hali ya machafuko ilipotokea baada ya Wafungwa kutoroka Gerezani Jijini Goma, Nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo 🇨🇩. Kulingana na ripoti mpya kutoka kwa Umoja wa Mataifa, mamia ya Wafungwa walitoroka katika Gereza la Munzenze Jumatatu iliyopita, baada ya Wapiganaji wa kundi la Waasi la M23 kuuteka Mji huo wa Goma. Ripoti hiyo inaeleza kwamba kati ya Wanawake 165 na 167 walivamiwa na kunyanyaswa na Wafungwa wa kiume walipovunja Gereza. Wengi wa Wanawake hao waliuawa baada ya Wafungwa hao kuchoma moto jela. Jiji hilo la Goma lina ukubwa na Watu zaidi milioni moja (1), lilitekwa na kundi la Waasi la M23, linalodaiwa kuungwa mkono na Rwanda 🇷🇼, lilipovamia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
    0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·180 Views
  • #PART11

    Baada ya Ntaganda kupelekwa The Heague, M23 iliongozwa na Sultan Makenga, Mtutsi wa Rutshuru huko Kivu Kaskazini. Mwaka 1990 Makenga akiwa na miaka 17 tu alienda Rwanda kujiunga na kikundi cha waasi RPF kilichokuwa kinaongozwa na Jenerali Fredy Rwigyema. Sultan Makenga akiwa askari wa RPF alipigana msituni dhidi ya serikali ya kihutu ya Juvenile Habyarimana.

    Baada RPF ilishika dola, Askari wote wa RPF waliingizwa katika jeshi la Rwanda akiwemo Sultan Makenga. Alihudumu katika jeshi hilo kwa muda mrefu hadi kufikia cheo cha Kanali kabla ya kurudi "nyumbani" Congo, kujiunga na kikundi cha waasi cha CNDP. Baada ya mkataba wa amani wa March 23, 2009 Sultan Makenga alikuwa miongoni mwa askari 600 wa CNDP waliokataa kujiunga na jeshi la Congo (FARDC).

    Mwaka 2012 Bosco Ntaganda alipojitoa kwenye jeshi la Congo na kuunga kikundi cha waasi cha M23, Sultan Makenga alikua wa kwanza kujiunga. Baada ya Ntaganda kujisalimisha, Makenga akapewa uongozi wa M23. Akaongoza kuanzia 2013 hadi 2016 alipotoweka ghafla. Haijulikani alipo, japo inasemekana alienda Rwanda na hakurudi tena.

    Baada ya Makenga kutoweka katika mazingira ya "kutatanisha" M23 ikawa na viongozi ambao hawakuwa mashuhuri sana hadi 2022 ilipompata Corneille Nangaa. Huyu alikua Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi nchini Congo (CENI) na ndiye aliyemtangaza Tshikeshedi kuwa mshindi wa kiti cha Urais wa Congo kwenye uchaguzi wa December 30 mwaka 2018.

    Katika mambo yanayoshangaza na kufanya vita ya Congo kuonekana ngumu, ni jinsi Nangaa alivyotoka kuwa Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, hadi kuanzisha coalition ya vikundi vya waasi, Congo River Alliance (CRA) kikiwemo M23. Jenerali Nangaa ndiye aliyeongoza M23 kuutwaa mji wa Goma January 2025, na kuyafurusha majeshi ya serikali. Nangaa ametangaza nia ya kumuondoa madarakani Rais Tshisekedi, ambaye mwaka 2018 ni Nangaa huyohuyo aliyemtangaza Tshikeshedi kuwa Rais.

    August 2024 Mahakama ya kijeshi mjini Kinshasa ilimhukumu Nangaa adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa kosa la uhaini. Hukumu hiyo ilitolewa bila yeye kuwepo mahakamani (death sentence in absentia). Nangaa amesema ikiwa M23 itashika dola, wale waliomhukumu ndio watanyongwa kwa niaba yake.!
    (Malisa GJ)

    #PART11 Baada ya Ntaganda kupelekwa The Heague, M23 iliongozwa na Sultan Makenga, Mtutsi wa Rutshuru huko Kivu Kaskazini. Mwaka 1990 Makenga akiwa na miaka 17 tu alienda Rwanda kujiunga na kikundi cha waasi RPF kilichokuwa kinaongozwa na Jenerali Fredy Rwigyema. Sultan Makenga akiwa askari wa RPF alipigana msituni dhidi ya serikali ya kihutu ya Juvenile Habyarimana. Baada RPF ilishika dola, Askari wote wa RPF waliingizwa katika jeshi la Rwanda akiwemo Sultan Makenga. Alihudumu katika jeshi hilo kwa muda mrefu hadi kufikia cheo cha Kanali kabla ya kurudi "nyumbani" Congo, kujiunga na kikundi cha waasi cha CNDP. Baada ya mkataba wa amani wa March 23, 2009 Sultan Makenga alikuwa miongoni mwa askari 600 wa CNDP waliokataa kujiunga na jeshi la Congo (FARDC). Mwaka 2012 Bosco Ntaganda alipojitoa kwenye jeshi la Congo na kuunga kikundi cha waasi cha M23, Sultan Makenga alikua wa kwanza kujiunga. Baada ya Ntaganda kujisalimisha, Makenga akapewa uongozi wa M23. Akaongoza kuanzia 2013 hadi 2016 alipotoweka ghafla. Haijulikani alipo, japo inasemekana alienda Rwanda na hakurudi tena. Baada ya Makenga kutoweka katika mazingira ya "kutatanisha" M23 ikawa na viongozi ambao hawakuwa mashuhuri sana hadi 2022 ilipompata Corneille Nangaa. Huyu alikua Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi nchini Congo (CENI) na ndiye aliyemtangaza Tshikeshedi kuwa mshindi wa kiti cha Urais wa Congo kwenye uchaguzi wa December 30 mwaka 2018. Katika mambo yanayoshangaza na kufanya vita ya Congo kuonekana ngumu, ni jinsi Nangaa alivyotoka kuwa Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, hadi kuanzisha coalition ya vikundi vya waasi, Congo River Alliance (CRA) kikiwemo M23. Jenerali Nangaa ndiye aliyeongoza M23 kuutwaa mji wa Goma January 2025, na kuyafurusha majeshi ya serikali. Nangaa ametangaza nia ya kumuondoa madarakani Rais Tshisekedi, ambaye mwaka 2018 ni Nangaa huyohuyo aliyemtangaza Tshikeshedi kuwa Rais. August 2024 Mahakama ya kijeshi mjini Kinshasa ilimhukumu Nangaa adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa kosa la uhaini. Hukumu hiyo ilitolewa bila yeye kuwepo mahakamani (death sentence in absentia). Nangaa amesema ikiwa M23 itashika dola, wale waliomhukumu ndio watanyongwa kwa niaba yake.! (Malisa GJ)
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·594 Views
  • Nchi ya Rwanda imesema kuwa mbinu za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ya kutaka kukomesha mikataba ya Rwanda kimataifa sio suluhisho kwa mzozo wa mashariki mwa DR Congo.

    Hii imekuja baada ya Serikali ya DR Congo kuandikia barua vilabu vya Arsenal FC, PSG na FC Bayern wakivitaka visitishe mikataba na Rwanda kwa madai kuwa Nchi hiyo inaunga mkono Waasi wa kundi la M23 na kuwa makubaliano hayo "yana damu".

    Nchi ya Rwanda 🇷🇼 imesema kuwa mbinu za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 ya kutaka kukomesha mikataba ya Rwanda kimataifa sio suluhisho kwa mzozo wa mashariki mwa DR Congo. Hii imekuja baada ya Serikali ya DR Congo kuandikia barua vilabu vya Arsenal FC, PSG na FC Bayern wakivitaka visitishe mikataba na Rwanda kwa madai kuwa Nchi hiyo inaunga mkono Waasi wa kundi la M23 na kuwa makubaliano hayo "yana damu".
    Like
    1
    · 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·289 Views
Αναζήτηση αποτελεσμάτων