• Nguvu inayo badilisha mtu .

    Warumi 12:2
    [2]*Wala msiifuatishe namna ya dunia hii;
    *bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu*

    Kama ukiwachukua watu wasili wanao waza sawa tunategemea matokeo yatakuwa sawa.

    Iko nguvu inaitwa neno la Mungu inayo weza badilisha mtu kama tu mtu akijua jinsi Mungu anavyo taka aenende .

    Kiwango chako cha kumjua Mungu katika neno lazima kiendane na matokeo kwani chochote apandacho mtu ndicho atakacho vuna.

    Wagalatia 6:7
    [7]Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.


    faida za kulijua neno kama nguvu inayo badilisha mtu .

    1.INATUHAKIKISHIA KUFNIKIWA.

    Mungu amehakikisha kila anaye mjua sawa sawa na neno anampa nguvu ya kufanikiwa.

    Zaburi 1:1-2
    [1]Heri mtu yule asiyekwenda
    Katika shauri la wasio haki;
    Wala hakusimama katika njia ya wakosaji;
    Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

    [2]Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,
    Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

    Lazma uamue kuishi maisha yasiyo na mizaa kabisa na dhambi kwa kulifuata neno kama mwongozo wako hapo ndipo utampendeza Mungu na Mungu atajihakikishia kukuwazia mema na mafanikio.

    Isaya 55:8-9
    [8] *Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.*
    .
    [9]Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.

    Mawazo ya mungu ni kuona ndoa yako inafanikiwa toka ujana wako mpaka uzee.

    Mawazo ya Mungu nikuona biashara yako inashine kuliko jana .

    Mawazo ya Mungu ni kukuona ukiishi maisha ya mafanikio na furaha siku zote za maisha yako .

    Yeremia 29:11
    [11] *Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.*

    Tatizo lako ni moja umeichukulia mzaa dhambi na kufanya mawazo ya Mungu kwako yasitimie .

    Acha dhambi acha mzaa na zinaa kutoka kusema hii ndo zambi yetu vijana anza kuichukia totally maisha yako yatabadilika totally na Mungu atakuhakikishia mafanikio siku zote.

    Mafanikio ni hakika na kweli kabisa kwa mtu anaye kaa na neno, mtu ambaye katika kila jambo anajibu na kulitazama neno linasema nini lazima apokee mafanikio makubwa zaidi.

    2.inatusaidia kutoka katika mawazo na fikra hasi

    Mtu hawezi kufanikiwa zaidi ya vile anavyo amini .

    Mtu awezi kupokea uponyaji zaidi ya vile anavyo hitaji.

    Kiwango cha mafanikio yako kinaamuliwa na kiwango cha imani yako .

    Marko 9:23
    [23]Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.

    Ukiweza kuwekeza katika neno neno litakupa matokeo ya mwilini kwani neno litakusaidia kujua jinsi gani watu walio tembea na mungu walifanikiwa .

    Utaacha kuona haiwezekani kila jambo utaanza kuona inawezekana kila jambo kwani utajua yeye anasemaji.

    Wafilolipi 4:13
    *Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu*

    Ko ni neno litabadilisha msimamo wako juu ya mawazo hasi juu ya mafanikio .

    Kwa maana mtu hawezi kuwa zaidi ya anavyo jiona.

    Mithali 23:7
    [7] *Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo*.
    Akuambia, Haya, kula, kunywa;
    Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.

    Neno pekee ndilo linaweza badilisha namna unavyo jiona na jinsi unavyo amini ili upokee mambo makubwa .

    Usidanganyikee mtu hawezi kupokea zaidi ya ufunuo alio upata katika neno husika .

    Nimatumaini yangu utaanza kuongeza imani katika neno ili upate nguvu ibadilishayo mtu .

    Take care, naitwa sylvester natokea kutoka (build new eden)

    Karubu tujifunze pamoja neno la Mungu .kupitia group la watsap

    https://chat.whatsapp.com/IxkPEsnxi02ExNGrlmbWR4

    #restore men position
    #build new position
    Nguvu inayo badilisha mtu . Warumi 12:2 [2]*Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; *bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu* Kama ukiwachukua watu wasili wanao waza sawa tunategemea matokeo yatakuwa sawa. Iko nguvu inaitwa neno la Mungu inayo weza badilisha mtu kama tu mtu akijua jinsi Mungu anavyo taka aenende . Kiwango chako cha kumjua Mungu katika neno lazima kiendane na matokeo kwani chochote apandacho mtu ndicho atakacho vuna. Wagalatia 6:7 [7]Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. faida za kulijua neno kama nguvu inayo badilisha mtu . 1.INATUHAKIKISHIA KUFNIKIWA. Mungu amehakikisha kila anaye mjua sawa sawa na neno anampa nguvu ya kufanikiwa. Zaburi 1:1-2 [1]Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. [2]Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Lazma uamue kuishi maisha yasiyo na mizaa kabisa na dhambi kwa kulifuata neno kama mwongozo wako hapo ndipo utampendeza Mungu na Mungu atajihakikishia kukuwazia mema na mafanikio. Isaya 55:8-9 [8] *Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.* . [9]Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Mawazo ya mungu ni kuona ndoa yako inafanikiwa toka ujana wako mpaka uzee. Mawazo ya Mungu nikuona biashara yako inashine kuliko jana . Mawazo ya Mungu ni kukuona ukiishi maisha ya mafanikio na furaha siku zote za maisha yako . Yeremia 29:11 [11] *Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.* Tatizo lako ni moja umeichukulia mzaa dhambi na kufanya mawazo ya Mungu kwako yasitimie . Acha dhambi acha mzaa na zinaa kutoka kusema hii ndo zambi yetu vijana anza kuichukia totally maisha yako yatabadilika totally na Mungu atakuhakikishia mafanikio siku zote. Mafanikio ni hakika na kweli kabisa kwa mtu anaye kaa na neno, mtu ambaye katika kila jambo anajibu na kulitazama neno linasema nini lazima apokee mafanikio makubwa zaidi. 2.inatusaidia kutoka katika mawazo na fikra hasi Mtu hawezi kufanikiwa zaidi ya vile anavyo amini . Mtu awezi kupokea uponyaji zaidi ya vile anavyo hitaji. Kiwango cha mafanikio yako kinaamuliwa na kiwango cha imani yako . Marko 9:23 [23]Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. Ukiweza kuwekeza katika neno neno litakupa matokeo ya mwilini kwani neno litakusaidia kujua jinsi gani watu walio tembea na mungu walifanikiwa . Utaacha kuona haiwezekani kila jambo utaanza kuona inawezekana kila jambo kwani utajua yeye anasemaji. Wafilolipi 4:13 *Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu* Ko ni neno litabadilisha msimamo wako juu ya mawazo hasi juu ya mafanikio . Kwa maana mtu hawezi kuwa zaidi ya anavyo jiona. Mithali 23:7 [7] *Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo*. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe. Neno pekee ndilo linaweza badilisha namna unavyo jiona na jinsi unavyo amini ili upokee mambo makubwa . Usidanganyikee mtu hawezi kupokea zaidi ya ufunuo alio upata katika neno husika . Nimatumaini yangu utaanza kuongeza imani katika neno ili upate nguvu ibadilishayo mtu . Take care, naitwa sylvester natokea kutoka (build new eden) Karubu tujifunze pamoja neno la Mungu .kupitia group la watsap https://chat.whatsapp.com/IxkPEsnxi02ExNGrlmbWR4 #restore men position #build new position
    Like
    1
    0 Reacties 0 aandelen 559 Views
  • Unaweza Kuwa Baba bora na Bado Ukapoteza Familia Yako
    Kwa sababu katika ulimwengu wa sasa, juhudi haimaanishi chochote ikiwa wewe ni mwanaume.
    Unaamka mapema.
    Nenda kazini.
    Unalipa kodi.
    Ubaki mwaminifu.
    Unaiombea familia.
    Bado-
    unawapoteza.
    Sio kwa sababu umeshindwa.
    Lakini kwa sababu ubaba wa kisasa umejengwa kama mtego.
    Unafanya kila kitu sawa ...
    na bado kuishia vibaya.
    Anaondoka. Watoto wanafuata. Nyumba inakuwa kumbukumbu.
    Unaendelea kulipa bili.
    Anaendelea kubadilisha simulizi.
    Na ikiwa unathubutu kupaza sauti yako?
    Wewe ni "sumu."
    Wewe "huna msimamo."
    Wewe ndiye "sababu aliondoka."
    Umelipia mpiga filimbi-
    lakini bado anaamuru wimbo.
    Ulifuata sheria. Lakini hilo ndilo tatizo.
    Kwa sababu ukifuata sheria, wewe si kiongozi.
    Ikiwa wewe ni mwaminifu, unakuwa rahisi.
    Uliambiwa umlinde.
    Kwa hivyo ulifanya.
    Uliambiwa utoe.
    Kwa hivyo ulifanya.
    Uliambiwa ukae mwaminifu.
    Kwa hivyo ulifanya.
    Na sasa?
    Umeachana.
    Una huzuni.
    Unaweza kutupwa.
    Mahakama inasema, "Wewe si baba."
    Lakini uharibifu tayari umefanywa.
    Moyo wako? Imevunjwa.
    Jina lako? Iliyotiwa rangi.
    Mkoba wako? Bado kuwajibika.
    Wanaiita “kwa manufaa ya mtoto.”
    Mtoto hatakuruhusu umuone... tangu 2019.
    Wakati huo huo, anatabasamu kwa ukimya.
    Kwa sababu tayari alishinda.
    Uongo huo ulifanya kazi.
    Mfumo ulimsaidia.
    Na jamii ikamshangilia.
    Wewe?
    Uko kwenye mtaala wako wa nne.
    Na hakuna mtu aliyepiga makofi ulivyo nusurika.
    Tuzungumze ukweli.80% ya talaka huanzishwa na wanawake.
    Uchunguzi wa DNA 1 kati ya 3 hurejea kuwa hasi.
    Maelfu ya wanaume wako korokoroni—si kwa uhalifu—
    lakini kwa kutoweza kuendelea na malipo yaliyoidhinishwa na mahakama...
    kwa watoto ambao hata si wao.
    Acha hiyo marinate.
    Unapoteza familia yako ... na bado wanakulaumu.
    "Labda alimuonya."
    "Alichagua uzuri, sio akili."
    "Hakujitambua vya kutosha."
    Kweli?
    Kwa hivyo wakati watu wa Mungu-
    Mchungaji Chris Oyakhilome, Benny Hinn,Kenneth Copeland—
    kuishia kutengana au kuachwa...
    hawakumsikia Mungu? Hawakuwa na kasi ya kutosha?
    Hawakuwa na macho ya kiroho?
    Au labda…
    labda tu…
    walioa wanawake ambao walikuwa wataalamu wa kuficha asili yao halisi.
    Hadi siku moja -
    waliamka, na kubadili.
    Hakuna onyo.
    Hakuna majuto.
    "Nimebadilika tu."
    Wanawake wa kisasa hawakuacha kwa kudanganya.
    Wanaondoka kwa sababu rekodi yako ya matukio imekwisha.
    Hujawa mtu wa njozi haraka vya kutosha.
    Hukuweza kumudu kifurushi cha maisha laini kwa ratiba.
    Kwa hiyo "hupunguza hasara zao" na kupiga risasi mitaani.
    Ulikuwa mzuri.
    Lakini ulikuwa hautoshi.
    Sio tajiri wa kutosha.
    Sio furaha ya kutosha.
    Haielekezi vya kutosha.
    Na sasa watoto wamekwenda.
    Nyumba ni kimya.
    Moyo wako umechoka.
    Na yote unayosikia ni:
    "Wanaume wa kweli hupigania familia zao."
    Kana kwamba haujatoa damu ukijaribu.
    Niseme wazi.

    Unaweza kuwa baba bora -
    na bado kupoteza.
    Sio kwa sababu haukupenda vya kutosha.
    Lakini kwa sababu upendo haujalishi tena.
    Sio kama wewe ni mwanaume.
    Wacha wapiganaji na wataalam wafurike maoni.
    Wacha wanawake waseme "sio sote."
    Waache wakanushaji waje wakibembea.

    Lakini wanaume halisi wanajua.
    Wameishi.
    Wamemwaga damu.
    Wamezika ndoto.
    Usiseme chochote.
    Andika tu "Kupitia" na uendelee.

    #ubaba
    #uanaume
    #maumivu kimya
    #utapeli wa ubaba
    #mahakama ya familia
    Unaweza Kuwa Baba bora na Bado Ukapoteza Familia Yako Kwa sababu katika ulimwengu wa sasa, juhudi haimaanishi chochote ikiwa wewe ni mwanaume. Unaamka mapema. Nenda kazini. Unalipa kodi. Ubaki mwaminifu. Unaiombea familia. Bado- unawapoteza. Sio kwa sababu umeshindwa. Lakini kwa sababu ubaba wa kisasa umejengwa kama mtego. Unafanya kila kitu sawa ... na bado kuishia vibaya. Anaondoka. Watoto wanafuata. Nyumba inakuwa kumbukumbu. Unaendelea kulipa bili. Anaendelea kubadilisha simulizi. Na ikiwa unathubutu kupaza sauti yako? Wewe ni "sumu." Wewe "huna msimamo." Wewe ndiye "sababu aliondoka." Umelipia mpiga filimbi- lakini bado anaamuru wimbo. Ulifuata sheria. Lakini hilo ndilo tatizo. Kwa sababu ukifuata sheria, wewe si kiongozi. Ikiwa wewe ni mwaminifu, unakuwa rahisi. Uliambiwa umlinde. Kwa hivyo ulifanya. Uliambiwa utoe. Kwa hivyo ulifanya. Uliambiwa ukae mwaminifu. Kwa hivyo ulifanya. Na sasa? Umeachana. Una huzuni. Unaweza kutupwa. Mahakama inasema, "Wewe si baba." Lakini uharibifu tayari umefanywa. Moyo wako? Imevunjwa. Jina lako? Iliyotiwa rangi. Mkoba wako? Bado kuwajibika. Wanaiita “kwa manufaa ya mtoto.” Mtoto hatakuruhusu umuone... tangu 2019. Wakati huo huo, anatabasamu kwa ukimya. Kwa sababu tayari alishinda. Uongo huo ulifanya kazi. Mfumo ulimsaidia. Na jamii ikamshangilia. Wewe? Uko kwenye mtaala wako wa nne. Na hakuna mtu aliyepiga makofi ulivyo nusurika. Tuzungumze ukweli.80% ya talaka huanzishwa na wanawake. Uchunguzi wa DNA 1 kati ya 3 hurejea kuwa hasi. Maelfu ya wanaume wako korokoroni—si kwa uhalifu— lakini kwa kutoweza kuendelea na malipo yaliyoidhinishwa na mahakama... kwa watoto ambao hata si wao. Acha hiyo marinate. Unapoteza familia yako ... na bado wanakulaumu. "Labda alimuonya." "Alichagua uzuri, sio akili." "Hakujitambua vya kutosha." Kweli? Kwa hivyo wakati watu wa Mungu- Mchungaji Chris Oyakhilome, Benny Hinn,Kenneth Copeland— kuishia kutengana au kuachwa... hawakumsikia Mungu? Hawakuwa na kasi ya kutosha? Hawakuwa na macho ya kiroho? Au labda… labda tu… walioa wanawake ambao walikuwa wataalamu wa kuficha asili yao halisi. Hadi siku moja - waliamka, na kubadili. Hakuna onyo. Hakuna majuto. "Nimebadilika tu." Wanawake wa kisasa hawakuacha kwa kudanganya. Wanaondoka kwa sababu rekodi yako ya matukio imekwisha. Hujawa mtu wa njozi haraka vya kutosha. Hukuweza kumudu kifurushi cha maisha laini kwa ratiba. Kwa hiyo "hupunguza hasara zao" na kupiga risasi mitaani. Ulikuwa mzuri. Lakini ulikuwa hautoshi. Sio tajiri wa kutosha. Sio furaha ya kutosha. Haielekezi vya kutosha. Na sasa watoto wamekwenda. Nyumba ni kimya. Moyo wako umechoka. Na yote unayosikia ni: "Wanaume wa kweli hupigania familia zao." Kana kwamba haujatoa damu ukijaribu. Niseme wazi. Unaweza kuwa baba bora - na bado kupoteza. Sio kwa sababu haukupenda vya kutosha. Lakini kwa sababu upendo haujalishi tena. Sio kama wewe ni mwanaume. Wacha wapiganaji na wataalam wafurike maoni. Wacha wanawake waseme "sio sote." Waache wakanushaji waje wakibembea. Lakini wanaume halisi wanajua. Wameishi. Wamemwaga damu. Wamezika ndoto. Usiseme chochote. Andika tu "Kupitia" na uendelee. #ubaba #uanaume #maumivu kimya #utapeli wa ubaba #mahakama ya familia
    Like
    Love
    2
    0 Reacties 0 aandelen 1K Views
  • “Sisi tumeitwa na serikali tumekuja kusikiliza ila msimamo wa Klabu upo wazi na unafahamika ila hapa tumekuja kusikiliza na tutayabeba yale ambayo tuna uwezo nayo ambayo hatuna uwezo nayo tutayaacha, ilipofikia sio suala la maslahi ya mpira wa Tanzania bali maslahi ya Klabu yetu kwanza” - Alex Ngai, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Yanga SC.

    “Sisi tumeitwa na serikali tumekuja kusikiliza ila msimamo wa Klabu upo wazi na unafahamika ila hapa tumekuja kusikiliza na tutayabeba yale ambayo tuna uwezo nayo ambayo hatuna uwezo nayo tutayaacha, ilipofikia sio suala la maslahi ya mpira wa Tanzania bali maslahi ya Klabu yetu kwanza” - Alex Ngai, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Yanga SC.
    0 Reacties 0 aandelen 740 Views
  • Balozi wa Afrika Kusini Nchini Marekani , Ebrahim Rasool ambaye ametimuliwa na Nchi ya Marekani kutokana na kukosoa sera za Donald Trump, amerejea Afrika Kusini kwa ufakhari mkubwa na kupokewa kwa shangwe na mamia ya Wananchi waliofurika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town Nchini Afrika Kusini.

    Balozi huyo na mkewe, Rosieda, waliwasili jana katika Uwanda wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town baada ya kusafari kutoka Nchini Marekani kupitia Qatar na wamekaribishwa vyema na kwa shangwe na mamia ya Wafuasi wao. Mapema mwezi huu, Balozi Rasool alitangazwa na Serikali ya Marekani kuwa ni Mtu asiyetakiwa kuweko Nchini humo baada ya kukosoa sera za Donald Trump, hatua ambayo inaonesha wazi jinsi madai ya uhuru wa kusema yasivyothaminiwa Nchini Marekani licha ya majigambo makubwa ya Nchi Marekani ya kupigania haki za Binadamu na demokrasia.

    Akiwahutubia mamia ya Mashabiki wake kwenye Uwanja wa Ndege wa Cape Town, Balozi Rasool amesema kwamba ingawa ametakiwa kuondoka huko Marekani lakini jambo hilo limeshindwa kufikia lengo lake kwani Viongozi wa Marekani wanadhani wamemdhalilisha wakati yeye anaona fakhari kwa maneno aliyotoa na Wananchi wa Afrika Kusini nao wanajivunia msimamo huo ndio maana wamejitokea kwa mamia kumpokea kishujaa.

    "Unaporejea nyumbani na kupokewa kwa shangwe na umati kama huu wa watu, mtu unaona fakhari na unajivunia msimamo wako." alisema Rasool.

    Alipoulizwa iwapo diplomasia imeshindwa, amesema ukweli kwamba matamshi yake yamemfanya Trump na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio kuwa makini na hatua ya Serikali ya Marekani ya kumtangaza kuwa ni Mtu asiyetakiwa nchini humo ni ushahidi kwamba ujumbe wake umefika ngazi za juu kabisa za serikali ya Marekani.

    Balozi wa Afrika Kusini 馃嚳馃嚘 Nchini Marekani 馃嚭馃嚫, Ebrahim Rasool ambaye ametimuliwa na Nchi ya Marekani kutokana na kukosoa sera za Donald Trump, amerejea Afrika Kusini kwa ufakhari mkubwa na kupokewa kwa shangwe na mamia ya Wananchi waliofurika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town Nchini Afrika Kusini. Balozi huyo na mkewe, Rosieda, waliwasili jana katika Uwanda wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town baada ya kusafari kutoka Nchini Marekani kupitia Qatar na wamekaribishwa vyema na kwa shangwe na mamia ya Wafuasi wao. Mapema mwezi huu, Balozi Rasool alitangazwa na Serikali ya Marekani kuwa ni Mtu asiyetakiwa kuweko Nchini humo baada ya kukosoa sera za Donald Trump, hatua ambayo inaonesha wazi jinsi madai ya uhuru wa kusema yasivyothaminiwa Nchini Marekani licha ya majigambo makubwa ya Nchi Marekani ya kupigania haki za Binadamu na demokrasia. Akiwahutubia mamia ya Mashabiki wake kwenye Uwanja wa Ndege wa Cape Town, Balozi Rasool amesema kwamba ingawa ametakiwa kuondoka huko Marekani lakini jambo hilo limeshindwa kufikia lengo lake kwani Viongozi wa Marekani wanadhani wamemdhalilisha wakati yeye anaona fakhari kwa maneno aliyotoa na Wananchi wa Afrika Kusini nao wanajivunia msimamo huo ndio maana wamejitokea kwa mamia kumpokea kishujaa. "Unaporejea nyumbani na kupokewa kwa shangwe na umati kama huu wa watu, mtu unaona fakhari na unajivunia msimamo wako." alisema Rasool. Alipoulizwa iwapo diplomasia imeshindwa, amesema ukweli kwamba matamshi yake yamemfanya Trump na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio kuwa makini na hatua ya Serikali ya Marekani ya kumtangaza kuwa ni Mtu asiyetakiwa nchini humo ni ushahidi kwamba ujumbe wake umefika ngazi za juu kabisa za serikali ya Marekani.
    Love
    Like
    3
    0 Reacties 0 aandelen 982 Views
  • Taarifa kwa umma kutoka katika klabu ya Yanga SC kuhusu msimamo wao kufuatia kughairisha kwa mchezo wao dhidi ya klabu ya Simba SC.

    - Kupewa alama tatu kwa sababu walifuata taratibu zote za mchezo huku kamati ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara ikichukua uamuzi wa kughairisha mchezo huo bila kufuata kanuni.

    - Yanga SC haitacheza mchezo mwingine shidi ya klabu ya Simba SC msimu huu Ligi Kuu Tanzania Bara (labda wakutane kombe la Shirikisho FA).

    - Klabu ya Simba SC walikuwa na haki ya kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa lakini hakufuata utaratibu wa kupewa haki hiyo kama kutoa taarifa kwa Afisa wa Uwanja, klabu ya Yanga SC ili waandaliwe mazingira ya wao kutumia Uwanja huo.

    Taarifa kwa umma kutoka katika klabu ya Yanga SC kuhusu msimamo wao kufuatia kughairisha kwa mchezo wao dhidi ya klabu ya Simba SC. - Kupewa alama tatu kwa sababu walifuata taratibu zote za mchezo huku kamati ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara ikichukua uamuzi wa kughairisha mchezo huo bila kufuata kanuni. - Yanga SC haitacheza mchezo mwingine shidi ya klabu ya Simba SC msimu huu Ligi Kuu Tanzania Bara (labda wakutane kombe la Shirikisho FA). - Klabu ya Simba SC walikuwa na haki ya kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa lakini hakufuata utaratibu wa kupewa haki hiyo kama kutoa taarifa kwa Afisa wa Uwanja, klabu ya Yanga SC ili waandaliwe mazingira ya wao kutumia Uwanja huo.
    Like
    1
    0 Reacties 0 aandelen 551 Views
  • Ijumaa, tarehe 28 Februari, haikuwa siku rahisi kwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alipofanya ziara katika Ikulu ya White House, Marekani. Kabla hata ya mzozo wa maneno kati yake na mwenyeji wake, Rais Donald Trump, pamoja na Makamu wa Rais JD Vance, tayari kulikuwa na ishara za mivutano.

    Trump alimkaribisha Zelensky mlangoni na kusema kwa utani: “Leo amevalia kweli kweli,” kauli ambayo iliwafanya baadhi ya waandishi wa habari kuiona kama kejeli badala ya pongezi. Wakati huo, Zelensky alikuwa amevalia fulana nyeusi ya mikono mirefu, vazi ambalo amekuwa akilivaa mara kwa mara tangu Ukraine ivamiwe na Urusi mwaka 2022.

    Baadaye, Trump alipompokea Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, alionekana kutazama mavazi yake kwa makini kutoka juu hadi chini, kisha kunong’ona maneno yanayoweza kutafsiriwa kama pongezi kwa suti rasmi aliyovaa Starmer.

    Mjadala kuhusu mavazi ya Zelensky ulizidi kupamba moto wakati wa mkutano wa waandishi wa habari. Brian Glenn, mwandishi kutoka Real America’s Voice—chombo cha habari kinachopendelea mrengo wa kulia—alimtupia swali la moja kwa moja:

    “Kwa nini hauvai suti? Upo katika ofisi ya juu kabisa katika nchi hii, na umegoma kuvaa suti – je, unamiliki hata suti?”

    Kwa utulivu, Zelensky alijibu kwa mshangao mdogo:

    “Nitavaa suti vita hivi vitakapomalizika. Labda suti kama yako, labda bora zaidi, au pengine ya bei nafuu kuliko yako,” alisema kwa utani huku akionyesha msimamo wake wa kuendelea kuvaa mavazi ya kijeshi.

    Swali hilo la Glenn liliibua mjadala mkali mitandaoni. Wengine walimuunga mkono, wakisema kwamba kiongozi wa taifa anapaswa kuvaa mavazi rasmi anapokutana na viongozi wengine, ilhali wengine waliona swali hilo kuwa la dhihaka na lisilo na umuhimu.

    Miongoni mwa waliomkosoa Glenn ni mwandishi maarufu wa Uingereza, Piers Morgan, ambaye pia ni rafiki wa karibu wa Trump. Morgan aliandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter):

    “Swali la kipuuzi. Elon Musk havai suti anapoingia Ikulu.”

    Historia pia inaonyesha kuwa si Zelensky pekee aliyeingia Ikulu ya Marekani bila suti. Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Winston Churchill, alifanya hivyo katika moja ya ziara zake rasmi.
    Ijumaa, tarehe 28 Februari, haikuwa siku rahisi kwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alipofanya ziara katika Ikulu ya White House, Marekani. Kabla hata ya mzozo wa maneno kati yake na mwenyeji wake, Rais Donald Trump, pamoja na Makamu wa Rais JD Vance, tayari kulikuwa na ishara za mivutano. Trump alimkaribisha Zelensky mlangoni na kusema kwa utani: “Leo amevalia kweli kweli,” kauli ambayo iliwafanya baadhi ya waandishi wa habari kuiona kama kejeli badala ya pongezi. Wakati huo, Zelensky alikuwa amevalia fulana nyeusi ya mikono mirefu, vazi ambalo amekuwa akilivaa mara kwa mara tangu Ukraine ivamiwe na Urusi mwaka 2022. Baadaye, Trump alipompokea Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, alionekana kutazama mavazi yake kwa makini kutoka juu hadi chini, kisha kunong’ona maneno yanayoweza kutafsiriwa kama pongezi kwa suti rasmi aliyovaa Starmer. Mjadala kuhusu mavazi ya Zelensky ulizidi kupamba moto wakati wa mkutano wa waandishi wa habari. Brian Glenn, mwandishi kutoka Real America’s Voice—chombo cha habari kinachopendelea mrengo wa kulia—alimtupia swali la moja kwa moja: “Kwa nini hauvai suti? Upo katika ofisi ya juu kabisa katika nchi hii, na umegoma kuvaa suti – je, unamiliki hata suti?” Kwa utulivu, Zelensky alijibu kwa mshangao mdogo: “Nitavaa suti vita hivi vitakapomalizika. Labda suti kama yako, labda bora zaidi, au pengine ya bei nafuu kuliko yako,” alisema kwa utani huku akionyesha msimamo wake wa kuendelea kuvaa mavazi ya kijeshi. Swali hilo la Glenn liliibua mjadala mkali mitandaoni. Wengine walimuunga mkono, wakisema kwamba kiongozi wa taifa anapaswa kuvaa mavazi rasmi anapokutana na viongozi wengine, ilhali wengine waliona swali hilo kuwa la dhihaka na lisilo na umuhimu. Miongoni mwa waliomkosoa Glenn ni mwandishi maarufu wa Uingereza, Piers Morgan, ambaye pia ni rafiki wa karibu wa Trump. Morgan aliandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter): “Swali la kipuuzi. Elon Musk havai suti anapoingia Ikulu.” Historia pia inaonyesha kuwa si Zelensky pekee aliyeingia Ikulu ya Marekani bila suti. Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Winston Churchill, alifanya hivyo katika moja ya ziara zake rasmi.
    Like
    Love
    2
    0 Reacties 0 aandelen 934 Views
  • #SportsElite
    Msimamo wa Ligi ya @championshiptz ya @nbc_tanzania
    #SportsElite 馃嚬馃嚳 Msimamo wa Ligi ya @championshiptz ya @nbc_tanzania
    0 Reacties 0 aandelen 893 Views
  • Msimamo wa EPL
    Msimamo wa EPL
    Love
    1
    1 Reacties 0 aandelen 462 Views
  • Msimamo wa Laliga
    Msimamo wa Laliga
    Haha
    1
    1 Reacties 0 aandelen 580 Views
  • Msimamo wa NBC
    Msimamo wa NBC
    Like
    1
    1 Reacties 0 aandelen 473 Views
  • TBT ya Haji Manara

    "September 2007 nikiwa kijana Mdogo na nikiwa kiongozi wa Chama changu na hapo ni fresh from School kule Beijing China.
    Kipindi hicho nna madini ya hatari kuhusu taaluma ya Propaganda na Uenezi,enzi ambazo nilikuwa naweza kukuaminisha Jiwe ni Keki

    Enzi ambazo nilikuwa naweza kuwavusha hata kuku barabarani kwa maneno tu,
    Ni zile zile zama nilizowaaminisha Barcelona haichomoki kwa Mkapa, tena Barcelona kweli ya Xavi ,Iniesta na kina Messi.
    Taaluma iliyonipa ujasiri wa kusema na kuamini tutafuzu kwa AFCON ya 2019 kule Misri,wakati huo tukiwa chini kwenye msimamo wa kundi letu, na Nchi nzima ikiwa imejikatia tamaa ya kwenda Cairo.

    Bila kusahau one day kule Paris France niliposahau Passport hotelini na siku hiyo tulisimamishwa na Manjagu njiani nikiwa na wenzangu ambao walikuwa Kamil Gado,
    Nikazuga kama naitoa kwenye mfuko wa koti, Askari wakaniamini kabla ya kuwaonyesha ,wakaturuhusu kilaini kabisa,inaitwa Blue Propaganda

    Yes: Pembeni yangu katika hiyo picha ni Marehemu Captain Barongo aliyekuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es salaam,
    Na hii ilikuwa sherehe ya harusi ya DC wa Temeke hivi sasa Mh Sixtus Mapunda ambae wakati huo alikuwa Katibu wa Umoja wa Vijana ( UV CCM ) Mkoa huu.
    Hadi leo tumebaki marafiki wakubwa na hakosi mwaliko wowote kwangu

    Nb: Usicheke ukubwa wa koti,miaka ile ilikuwa ndio fashion na wenyewe tuliyaita Majumba "

    TBT ya Haji Manara "September 2007 nikiwa kijana Mdogo na nikiwa kiongozi wa Chama changu na hapo ni fresh from School kule Beijing China. Kipindi hicho nna madini ya hatari kuhusu taaluma ya Propaganda na Uenezi,enzi ambazo nilikuwa naweza kukuaminisha Jiwe ni Keki 馃榾馃榾馃榾 Enzi ambazo nilikuwa naweza kuwavusha hata kuku barabarani kwa maneno tu馃榾馃榾馃榾, Ni zile zile zama nilizowaaminisha Barcelona haichomoki kwa Mkapa, tena Barcelona kweli ya Xavi ,Iniesta na kina Messi. Taaluma iliyonipa ujasiri wa kusema na kuamini tutafuzu kwa AFCON ya 2019 kule Misri,wakati huo tukiwa chini kwenye msimamo wa kundi letu, na Nchi nzima ikiwa imejikatia tamaa ya kwenda Cairo. Bila kusahau one day kule Paris France niliposahau Passport hotelini na siku hiyo tulisimamishwa na Manjagu njiani nikiwa na wenzangu ambao walikuwa Kamil Gado, Nikazuga kama naitoa kwenye mfuko wa koti, Askari wakaniamini kabla ya kuwaonyesha ,wakaturuhusu kilaini kabisa,inaitwa Blue Propaganda 馃榾馃榾馃榾 Yes: Pembeni yangu katika hiyo picha ni Marehemu Captain Barongo aliyekuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Na hii ilikuwa sherehe ya harusi ya DC wa Temeke hivi sasa Mh Sixtus Mapunda ambae wakati huo alikuwa Katibu wa Umoja wa Vijana ( UV CCM ) Mkoa huu. Hadi leo tumebaki marafiki wakubwa na hakosi mwaliko wowote kwangu 馃檹馃檹 Nb: Usicheke ukubwa wa koti,miaka ile ilikuwa ndio fashion na wenyewe tuliyaita Majumba 馃榾馃榾馃榾"
    0 Reacties 0 aandelen 1K Views
  • Mfalme wa Nchi ya Jordan , Abdullah II amekataa pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump la kutaka kuwahamishia Wapalestina Nchini mwake baada ya mazungumzo na Rais Donald Trump wa Marekani, ambaye alishauri Wakazi wa Gaza wapatao milioni mbili (2) kuondolewa kutoka katika eneo lililoharibiwa na vita.

    Katika mkutano na Rais Trump, Mfalme Abdullah alijitolea kuchukua hadi Watoto 2,000 kutoka Gaza, hasa wale wanaohitaji matibabu ya dharura, ikiwemo Watoto wa saratani. Kupitia mtandao wa X, Mfalme Abdullah alisema, "Msimamo wa Jordan ni msimamo wa pamoja wa mataifa ya Kiarabu."

    Sanjari na hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit, alikosoa pendekezo hilo, akisema kuwa ni lisilokubalika katika ukanda huo, huku Nchi ya China ikisisitiza kuwa Gaza ni ardhi ya Wapalestina.

    Mfalme wa Nchi ya Jordan 馃嚡馃嚧, Abdullah II amekataa pendekezo la Rais wa Marekani 馃嚭馃嚫 Donald Trump la kutaka kuwahamishia Wapalestina Nchini mwake baada ya mazungumzo na Rais Donald Trump wa Marekani, ambaye alishauri Wakazi wa Gaza wapatao milioni mbili (2) kuondolewa kutoka katika eneo lililoharibiwa na vita. Katika mkutano na Rais Trump, Mfalme Abdullah alijitolea kuchukua hadi Watoto 2,000 kutoka Gaza, hasa wale wanaohitaji matibabu ya dharura, ikiwemo Watoto wa saratani. Kupitia mtandao wa X, Mfalme Abdullah alisema, "Msimamo wa Jordan ni msimamo wa pamoja wa mataifa ya Kiarabu." Sanjari na hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit, alikosoa pendekezo hilo, akisema kuwa ni lisilokubalika katika ukanda huo, huku Nchi ya China 馃嚚馃嚦 ikisisitiza kuwa Gaza ni ardhi ya Wapalestina.
    Like
    1
    0 Reacties 0 aandelen 757 Views
  • #SportsEliteMsimamo wa Ligi ya @championshiptz ya @nbc_tanzania
    #SportsElite馃嚬馃嚳Msimamo wa Ligi ya @championshiptz ya @nbc_tanzania
    Love
    1
    0 Reacties 0 aandelen 605 Views
  • Rais wa Marekani , Donald Trump ameonya kuwa kama kundi la Hamas (Gaza) hawatawaachilia mateka wote wa Nchi ya Israel kufikia Jumamosi ya Wiki hii basi Dunia itashuhudia mashambulizi halisi katika eneo hilo. Onyo la Trump linakuja siku moja baada ya Kundi la Wapiganaji wa Hamas kuvunja makubaliano ya usitishwaji vita na Israel kwa kugoma kuendelea na zoezi la kuwaachia huru mateka wa Israel mpaka watakapotoa taarifa nyingine.

    Uamuzi huo wa Hamas umekuja siku chache baada ya Viongozi wake Wakuu kufanya ziara Nchini Iran na kukutana na Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khemenei ambaye aliwapongeza kwa kuendelea kusimama imara dhidi ya Israel. Trump wiki iliyopita alionya kuwa Gaza haitofaa kuwa eneo la kuishi chini ya Uongozi wa Hamas na kupendekeza kwamba Marekani ingependa kulichukua eneo hilo na kulisimamia huku Wakazi wa eneo hilo wakihamishiwa Nchi za Misri na Jordan .

    Rais huyo wa Marekani alisema Marekani ipo tayari kulinunua eneo hilo na kulimiliki na kuahidi kwamba Marekani italijenga na kulifanya kuwa eneo zuri la mfano Mashariki ya Kati. Kiufupi kundi la Hamas wanacheza na moto kwa sasa, Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz ameviagiza Vikosi vya Israel kukaa tayari kwa mashambulizi mapya iwapo Kundi hilo la Hamas likigoma kutii maelekezo ya kuachia mateka.

    Marekani ndio imekuwa Nchi inayoipa misaada mikubwa ya kibinadamu na kiuchumi Gaza pamoja na kuizuia Israel kutokuifutilia mbali Gaza kwa miaka mingi sasa ambapo Hamas imekua ikifanya uchokozi. Ikumbukwe Trump ni kati ya Viongozi wa Marekani ambaye ana msimamo mkali mno dhidi ya kundi la Hamas na tokea kuanza kwa mapigano Oktoba 7 mwaka 2023 Trump alisema Israel inachopaswa kufanya ni kulifutilia mbali kundi hilo.

    Rais wa Marekani 馃嚭馃嚫, Donald Trump ameonya kuwa kama kundi la Hamas (Gaza) hawatawaachilia mateka wote wa Nchi ya Israel 馃嚠馃嚤 kufikia Jumamosi ya Wiki hii basi Dunia itashuhudia mashambulizi halisi katika eneo hilo. Onyo la Trump linakuja siku moja baada ya Kundi la Wapiganaji wa Hamas kuvunja makubaliano ya usitishwaji vita na Israel kwa kugoma kuendelea na zoezi la kuwaachia huru mateka wa Israel mpaka watakapotoa taarifa nyingine. Uamuzi huo wa Hamas umekuja siku chache baada ya Viongozi wake Wakuu kufanya ziara Nchini Iran 馃嚠馃嚪 na kukutana na Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khemenei ambaye aliwapongeza kwa kuendelea kusimama imara dhidi ya Israel. Trump wiki iliyopita alionya kuwa Gaza haitofaa kuwa eneo la kuishi chini ya Uongozi wa Hamas na kupendekeza kwamba Marekani ingependa kulichukua eneo hilo na kulisimamia huku Wakazi wa eneo hilo wakihamishiwa Nchi za Misri 馃嚜馃嚞 na Jordan 馃嚡馃嚧. Rais huyo wa Marekani alisema Marekani ipo tayari kulinunua eneo hilo na kulimiliki na kuahidi kwamba Marekani italijenga na kulifanya kuwa eneo zuri la mfano Mashariki ya Kati. Kiufupi kundi la Hamas wanacheza na moto kwa sasa, Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz ameviagiza Vikosi vya Israel kukaa tayari kwa mashambulizi mapya iwapo Kundi hilo la Hamas likigoma kutii maelekezo ya kuachia mateka. Marekani ndio imekuwa Nchi inayoipa misaada mikubwa ya kibinadamu na kiuchumi Gaza pamoja na kuizuia Israel kutokuifutilia mbali Gaza kwa miaka mingi sasa ambapo Hamas imekua ikifanya uchokozi. Ikumbukwe Trump ni kati ya Viongozi wa Marekani ambaye ana msimamo mkali mno dhidi ya kundi la Hamas na tokea kuanza kwa mapigano Oktoba 7 mwaka 2023 Trump alisema Israel inachopaswa kufanya ni kulifutilia mbali kundi hilo.
    Like
    1
    0 Reacties 0 aandelen 727 Views
  • Kwa mujibu wa Tovuti ya The Guardian, Wananajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) wameripotiwa kuuawa katika operesheni za siri Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo . Kuuawa kwa Wanajeshi hao katika operesheni hiyo kunapingana na msimamo wa Serikali ya Rwanda inayodai Askari wake hawahusiki wala kushiriki katika mzozo unaoendelea kati ya kundi la M23 na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo .

    Taarifa hiyo iliyochapishwa na tovuti ya The Guardian imedai kuwa vyanzo mbalimbali vya kijasusi, kijeshi na kidiplomasia vinasema idadi ya Wanajeshi wa RDF waliouawa ni kubwa, huku wakidai walikuwa wakisaidia mashambulizi yanayofanywa na Waasi wa M23 ndani ya DR Congo.

    Picha za Setilaiti zilizopigwa katika makaburi ya kijeshi yaliyoko Jijini Kigali, Nchini Rwanda, zimethibitisha kuonekana kwa makaburi mapya yasiyopungua 600 yaliyopatikana tangu Waasi wa M23, wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, walipoanza operesheni zao ndani ya DR Congo miaka mitatu iliyopita.

    Kwa mujibu wa Tovuti ya The Guardian, Wananajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda 馃嚪馃嚰 (RDF) wameripotiwa kuuawa katika operesheni za siri Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 馃嚚馃嚛. Kuuawa kwa Wanajeshi hao katika operesheni hiyo kunapingana na msimamo wa Serikali ya Rwanda inayodai Askari wake hawahusiki wala kushiriki katika mzozo unaoendelea kati ya kundi la M23 na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 馃嚚馃嚛. Taarifa hiyo iliyochapishwa na tovuti ya The Guardian imedai kuwa vyanzo mbalimbali vya kijasusi, kijeshi na kidiplomasia vinasema idadi ya Wanajeshi wa RDF waliouawa ni kubwa, huku wakidai walikuwa wakisaidia mashambulizi yanayofanywa na Waasi wa M23 ndani ya DR Congo. Picha za Setilaiti zilizopigwa katika makaburi ya kijeshi yaliyoko Jijini Kigali, Nchini Rwanda, zimethibitisha kuonekana kwa makaburi mapya yasiyopungua 600 yaliyopatikana tangu Waasi wa M23, wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, walipoanza operesheni zao ndani ya DR Congo miaka mitatu iliyopita.
    0 Reacties 0 aandelen 521 Views
  • #PART3

    Hivyo, wale waliokuwa hawana ushahidi wa moja kwa moja wakaanza kuhamishwa.

    Lakini wale waliokuwa na rekodi ya ugaidi wa kiwango cha juu, wakabaki.
    Kwa Trump, Guantanamo lilikuwa muhimu.

    Lilikuwa sehemu ya kuhakikisha magaidi hawana sehemu ya kujificha.

    Hapa hakuna kesi.
    Hakuna mawakili.
    Hakuna upendeleo.

    Ukiingia, unasahau kama kuna dunia nje.

    Mateso yanayotokea ndani ya gereza hili ni siri kubwa ya Marekani.

    Lakini waliowahi kutoka, au maafisa wa zamani wa CIA na FBI, wamesema kwamba mateso ya Guantanamo yanaweza kumfanya mtu mwenye msimamo mkali wa kidini aseme Yesu alikuwa Muislam na Muhammad alikuwa Myahudi.
    #PART3 Hivyo, wale waliokuwa hawana ushahidi wa moja kwa moja wakaanza kuhamishwa. Lakini wale waliokuwa na rekodi ya ugaidi wa kiwango cha juu, wakabaki. Kwa Trump, Guantanamo lilikuwa muhimu. Lilikuwa sehemu ya kuhakikisha magaidi hawana sehemu ya kujificha. Hapa hakuna kesi. Hakuna mawakili. Hakuna upendeleo. Ukiingia, unasahau kama kuna dunia nje. Mateso yanayotokea ndani ya gereza hili ni siri kubwa ya Marekani. Lakini waliowahi kutoka, au maafisa wa zamani wa CIA na FBI, wamesema kwamba mateso ya Guantanamo yanaweza kumfanya mtu mwenye msimamo mkali wa kidini aseme Yesu alikuwa Muislam na Muhammad alikuwa Myahudi.
    0 Reacties 0 aandelen 792 Views
  • Rais wa Marekani , Donald Trump, ameshitua Watu Duniani baada ya kutangaza nia yake ya kuchukua udhibiti wa Ukanda wa Gaza ulioharibiwa na vita na kuufanyia maendeleo ya kiuchumi baada ya Wapalestina kuhamishiwa maeneo mengine. Hatua hiyo inaweza kubadili sera za Marekani za miongo kadhaa kuhusu mgogoro wa Israel na Palestina.

    Katika mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, Rais huyo alitangaza mpango huu bila kutoa maelezo ya kina.

    Kabla ya tangazo hilo, Trump alipendekeza kuwa zaidi ya Wapalestina milioni mbili (2) wa Gaza wahamishiwe Nchi jirani. Alikitaja kisiwa hicho kidogo, ambacho kwa sasa kina makubaliano dhaifu ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas, kuwa “eneo la kubomolewa.”

    Pendekezo hili linakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Washirika na Wapinzani wa Marekani. Pia linaibua maswali kuhusu ikiwa Saudi Arabia itashiriki katika juhudi mpya za Marekani za kuleta uhusiano wa kawaida kati ya Israel na mataifa ya Kiarabu.

    - Hatua ya Marekani kuchukua ushawishi wa moja kwa moja Gaza itapingana na msimamo wa muda mrefu wa Washington na Jumuiya ya kimataifa, ambao unaona Gaza kama sehemu ya Taifa la baadaye la Palestina pamoja na Ukingo wa Magharibi.

    "Marekani itachukua Ukanda wa Gaza, na tutafanya nao kazi nzuri sana. Tutakuwa na umiliki wake na kuhakikisha tunasafisha mabomu na silaha zote hatari zilizobaki."

    "Tutaendeleza Gaza, kuunda maelfu ya ajira, na kuifanya iwe sehemu ambayo Mashariki ya Kati yote itajivunia. Ninaona umiliki wa muda mrefu na ninaamini italeta utulivu mkubwa katika eneo hilo." amesema Donald Trump.

    “nyumbani kwa watu wa dunia.” Aliielezea Gaza kama eneo lenye uwezo wa kuwa “Riviera ya Mashariki ya Kati.” - Donald Trump baada ya kuulizwa nani ataishi Gaza baada ya kuitengeneza

    Trump hakujibu moja kwa moja kuhusu mamlaka au mchakato wa kuchukua eneo hilo la Gaza baada ya kuulizwa Marekani ina mamlaka gani ya kuichukua Gaza, ambalo lina urefu wa maili 25 (km 45) na upana wa hadi maili 6 (km 10) na historia ya vurugu. Serikali za awali za Marekani, ikiwemo ile ya Trump katika muhula wake wa kwanza, ziliepuka kutuma Wanajeshi Gaza.

    Rais wa Marekani 馃嚭馃嚫, Donald Trump, ameshitua Watu Duniani baada ya kutangaza nia yake ya kuchukua udhibiti wa Ukanda wa Gaza ulioharibiwa na vita na kuufanyia maendeleo ya kiuchumi baada ya Wapalestina kuhamishiwa maeneo mengine. Hatua hiyo inaweza kubadili sera za Marekani za miongo kadhaa kuhusu mgogoro wa Israel na Palestina. Katika mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, Rais huyo alitangaza mpango huu bila kutoa maelezo ya kina. Kabla ya tangazo hilo, Trump alipendekeza kuwa zaidi ya Wapalestina milioni mbili (2) wa Gaza wahamishiwe Nchi jirani. Alikitaja kisiwa hicho kidogo, ambacho kwa sasa kina makubaliano dhaifu ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas, kuwa “eneo la kubomolewa.” Pendekezo hili linakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Washirika na Wapinzani wa Marekani. Pia linaibua maswali kuhusu ikiwa Saudi Arabia itashiriki katika juhudi mpya za Marekani za kuleta uhusiano wa kawaida kati ya Israel na mataifa ya Kiarabu. - Hatua ya Marekani kuchukua ushawishi wa moja kwa moja Gaza itapingana na msimamo wa muda mrefu wa Washington na Jumuiya ya kimataifa, ambao unaona Gaza kama sehemu ya Taifa la baadaye la Palestina pamoja na Ukingo wa Magharibi. "Marekani itachukua Ukanda wa Gaza, na tutafanya nao kazi nzuri sana. Tutakuwa na umiliki wake na kuhakikisha tunasafisha mabomu na silaha zote hatari zilizobaki." "Tutaendeleza Gaza, kuunda maelfu ya ajira, na kuifanya iwe sehemu ambayo Mashariki ya Kati yote itajivunia. Ninaona umiliki wa muda mrefu na ninaamini italeta utulivu mkubwa katika eneo hilo." amesema Donald Trump. “nyumbani kwa watu wa dunia.” Aliielezea Gaza kama eneo lenye uwezo wa kuwa “Riviera ya Mashariki ya Kati.” - Donald Trump baada ya kuulizwa nani ataishi Gaza baada ya kuitengeneza Trump hakujibu moja kwa moja kuhusu mamlaka au mchakato wa kuchukua eneo hilo la Gaza baada ya kuulizwa Marekani ina mamlaka gani ya kuichukua Gaza, ambalo lina urefu wa maili 25 (km 45) na upana wa hadi maili 6 (km 10) na historia ya vurugu. Serikali za awali za Marekani, ikiwemo ile ya Trump katika muhula wake wa kwanza, ziliepuka kutuma Wanajeshi Gaza.
    Like
    1
    0 Reacties 0 aandelen 860 Views
  • Rais wa Marekani , Donald Trump ameendelea na msimamo wake na kuweka mkazo kuhusu kuifanya Nchi ya Canada kuwa jimbo la (51) la Nchi ya Marekani. Kupitia ukurasa wake wa mtandao X, Rais huyo amesema kuwa Nchi yake ya Marekani inatumia mabilioni ya fedha na punguzo za ushuru kuihudumia Canada hivyo hakuna haja Nchi hiyo kuendelea kuifaidi Marekani wakati ingeweza kuwa sehemu ya Marekani na kupata unafuu bila kuinyonya Nchi ya Marekani.

    Donald Trump amesema iwapo Nchi ya Canada itakataa mpango huo basi tozo na ushuru wa bidhaa kwa Taifa hilo utapanda mara dufu na kulingana mataifa mengine. Trump amesema iwapo Canada ikijiunga na Marekani hakutakuwa na tozo wala mazuio ya maelfu ya Raia wa Canada wanaoingia Marekani kufanya kazi.

    Ikumbukwe kwamba Nchi za Canada na Mexico ni kati ya mataifa yenye Raia wengi wanaofanya kazi za kujiingizia kipato Nchini Marekani ambao hawana vibali halali vya kazi na uhamiaji (Wahamiaji haramu). Tayari Donald Trump ameshaongea na Viongozi wakuu wa mataifa hayo na kuwapa muda wa siku thelathini (30) kuchukua hatua kwa mapendekezo yake ama utozaji wa tozo na ushuru wa asilimia (25) kwa bidhaa zao uanze mara moja.

    Viongozi wa Nchi hizo wamekiri kupokea maelekezo ya Trump na kuahidi kuchukua hatua ikiwemo kuzuia mipaka yao kuwa njia za Wahamiaji haramu. Waziri Mkuu wa Canada, Justin Tradeau amesema Canada kuwa sehemu ya Marekani haitawezekana licha ya kwamba huenda wakakutana rungu la kiuchumi kisha Wananchi wakaamua wenyewe kupitia uchunguzi (kura).

    Rais wa Marekani 馃嚭馃嚫, Donald Trump ameendelea na msimamo wake na kuweka mkazo kuhusu kuifanya Nchi ya Canada 馃嚚馃嚘 kuwa jimbo la (51) la Nchi ya Marekani. Kupitia ukurasa wake wa mtandao X, Rais huyo amesema kuwa Nchi yake ya Marekani inatumia mabilioni ya fedha na punguzo za ushuru kuihudumia Canada hivyo hakuna haja Nchi hiyo kuendelea kuifaidi Marekani wakati ingeweza kuwa sehemu ya Marekani na kupata unafuu bila kuinyonya Nchi ya Marekani. Donald Trump amesema iwapo Nchi ya Canada itakataa mpango huo basi tozo na ushuru wa bidhaa kwa Taifa hilo utapanda mara dufu na kulingana mataifa mengine. Trump amesema iwapo Canada ikijiunga na Marekani hakutakuwa na tozo wala mazuio ya maelfu ya Raia wa Canada wanaoingia Marekani kufanya kazi. Ikumbukwe kwamba Nchi za Canada na Mexico 馃嚥馃嚱 ni kati ya mataifa yenye Raia wengi wanaofanya kazi za kujiingizia kipato Nchini Marekani ambao hawana vibali halali vya kazi na uhamiaji (Wahamiaji haramu). Tayari Donald Trump ameshaongea na Viongozi wakuu wa mataifa hayo na kuwapa muda wa siku thelathini (30) kuchukua hatua kwa mapendekezo yake ama utozaji wa tozo na ushuru wa asilimia (25) kwa bidhaa zao uanze mara moja. Viongozi wa Nchi hizo wamekiri kupokea maelekezo ya Trump na kuahidi kuchukua hatua ikiwemo kuzuia mipaka yao kuwa njia za Wahamiaji haramu. Waziri Mkuu wa Canada, Justin Tradeau amesema Canada kuwa sehemu ya Marekani haitawezekana licha ya kwamba huenda wakakutana rungu la kiuchumi kisha Wananchi wakaamua wenyewe kupitia uchunguzi (kura).
    Love
    1
    0 Reacties 0 aandelen 859 Views
  • #PART3

    Baadhi ya wanajeshi wa Kitutsi hawakuridhika na ukandamizaji uliofanywa na Habyarimana. Wakajiorganize kupambana. Wakati huo Kagame akiwa askari wa NRA ya Uganda akimsaidia Museveni vita vya msituni. Mwaka 1983 hadi 1985 alienda kozi ya kijeshi TMA, Moduli. Alipohitimu akarudi Uganda kumsaidia Museveni vita vya msituni na hatimaye mwaka 1986 wakafanikiwa kuchukua nchi. NRA ikawa sehemu ya jeshi la Uganda kabla ya kubadilishwa muundo mwaka 1995 kuwa UPDF.

    Kagame akawa mkuu wa intelijensia ya jeshi. Baadae akaenda masomoni Marekani. Akiwa huko RPF ikaanzishwa na Jenerali Fredy Rwigyema kupambana na Serikali ya Habyarimana. Lakini Jenerali Rwigyema akauawa kwa guruneti akiwa uwanja wa vita. Kagame akalazimika kukatisha masomo na kurudi Rwanda kuongoza RPF akishirikiana na Alexis Kanyarwenge. Museveni akampa msaada wa fedha, silaha na chakula. RPF ikaweka kambi Uganda eneo la Kabale, Burundi eneo la Muyinga na Congo maeneo ya Kivu, Uvira na Goma.

    Mwaka 1994, askari wa RPF wakatungua ndege ya Rais Habyarimana ikiwa inakaribia kutua uwanja wa ndege wa Kigali ikitokea Dar es Salaam kwenye mazungumzo ya Amani alikuwa na Rais Cyprien Ntaramira wa Burundi. Wote wawili walikufa papo hapo.

    Kuuawa kwa Rais Habyarimana kuliamsha hasira za Wahutu na kusabisha mauaji ya Kimbari ambapo Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa kikatili kwa kucharangwa mapanga. Hali hiyo ilisababisha Watutsi wengi kukimbia nchi yao. Wapo waliokimbilia Tanzania, Uganda, lakini wengi zaidi walikimbilia eneo la Kivu.

    Kwa kifupi, idadi ya Watutsi eneo la Kivu iliongezeka siku hadi siku. Watutsi walioenda Kivu wengi hawakurudi Rwanda hata baada ya vita kumalizika. Ilikuwa vigumu kutofautisha Mtutsi mwenye asili ya Congo (Banyamulenge) na Mtutsi wa Rwanda, kwa sababu wote wanaongea lugha moja, mila na desturi moja.

    Kwahiyo hisia za Wakongomani kwamba Banyamulenge ni wageni zikaanza kupata nguvu kutokana na uhamiaji mkubwa wa Watutsi maeneo ya Kivu kaskazini na kusini. Wakati huo Congo ikiitwa Zaire Rais Mobutu Sese Seko alikataa kuwatambua Banyamulenge kama raia wake, na akazuia wasipewe vitambulisho vya taifa.
    (Malisa GJ)

    #PART3 Baadhi ya wanajeshi wa Kitutsi hawakuridhika na ukandamizaji uliofanywa na Habyarimana. Wakajiorganize kupambana. Wakati huo Kagame akiwa askari wa NRA ya Uganda akimsaidia Museveni vita vya msituni. Mwaka 1983 hadi 1985 alienda kozi ya kijeshi TMA, Moduli. Alipohitimu akarudi Uganda kumsaidia Museveni vita vya msituni na hatimaye mwaka 1986 wakafanikiwa kuchukua nchi. NRA ikawa sehemu ya jeshi la Uganda kabla ya kubadilishwa muundo mwaka 1995 kuwa UPDF. Kagame akawa mkuu wa intelijensia ya jeshi. Baadae akaenda masomoni Marekani. Akiwa huko RPF ikaanzishwa na Jenerali Fredy Rwigyema kupambana na Serikali ya Habyarimana. Lakini Jenerali Rwigyema akauawa kwa guruneti akiwa uwanja wa vita. Kagame akalazimika kukatisha masomo na kurudi Rwanda kuongoza RPF akishirikiana na Alexis Kanyarwenge. Museveni akampa msaada wa fedha, silaha na chakula. RPF ikaweka kambi Uganda eneo la Kabale, Burundi eneo la Muyinga na Congo maeneo ya Kivu, Uvira na Goma. Mwaka 1994, askari wa RPF wakatungua ndege ya Rais Habyarimana ikiwa inakaribia kutua uwanja wa ndege wa Kigali ikitokea Dar es Salaam kwenye mazungumzo ya Amani alikuwa na Rais Cyprien Ntaramira wa Burundi. Wote wawili walikufa papo hapo. Kuuawa kwa Rais Habyarimana kuliamsha hasira za Wahutu na kusabisha mauaji ya Kimbari ambapo Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa kikatili kwa kucharangwa mapanga. Hali hiyo ilisababisha Watutsi wengi kukimbia nchi yao. Wapo waliokimbilia Tanzania, Uganda, lakini wengi zaidi walikimbilia eneo la Kivu. Kwa kifupi, idadi ya Watutsi eneo la Kivu iliongezeka siku hadi siku. Watutsi walioenda Kivu wengi hawakurudi Rwanda hata baada ya vita kumalizika. Ilikuwa vigumu kutofautisha Mtutsi mwenye asili ya Congo (Banyamulenge) na Mtutsi wa Rwanda, kwa sababu wote wanaongea lugha moja, mila na desturi moja. Kwahiyo hisia za Wakongomani kwamba Banyamulenge ni wageni zikaanza kupata nguvu kutokana na uhamiaji mkubwa wa Watutsi maeneo ya Kivu kaskazini na kusini. Wakati huo Congo ikiitwa Zaire Rais Mobutu Sese Seko alikataa kuwatambua Banyamulenge kama raia wake, na akazuia wasipewe vitambulisho vya taifa. (Malisa GJ)
    Like
    1
    0 Reacties 0 aandelen 947 Views
  • Kwa waliosahau msimamo wa Ligi Kuu ya NBC na Ligi Kuu ya Wanawake.

    Hali ipo hivi

    #paulswai
    馃搱 Kwa waliosahau msimamo wa Ligi Kuu ya NBC na Ligi Kuu ya Wanawake. Hali ipo hivi 馃槑 #paulswai
    Love
    1
    0 Reacties 0 aandelen 793 Views
Zoekresultaten