JAMBAZI MTUKUTU.
Nchini Tanzania, kuna manju 'Dj' fulani wa muziki anayejulikana kwa jina maarufu la 'DJ JD' au kwa kirefu *'DJ John Dilinga'.* Huyu ni moja kati ya maDj wakongwe na mahiri sana tuliobahatika kuwa nao hapa nchini Tanzania. Kwa wale wapenzi na wadau wa muziki wa 'bongofleva' hususani wa miaka ya nyumanyuma kidogo, bila shaka mtakua mnamfahamu Dj huyu.
Kwa muda mrefu nimekuwa nikitamani kufahamu ni kwanini anaitwa John Dilinga..nikiwa nataka kujua kama hilo ni jina lake halisi au ni 'a.k.a'. Maana ni kawaida kuona watu mbalimbali hususani walio kwenye tasnia ya burudani wakitumia majina ya ziada (a.k.a) kuliko majina yao halisi.
Kitu kilichonifanya nianze na DJ JD ni baada ya kugundua kuwa leo ni tarehe 22 Julai. Tarehe ambayo ulimwengu mzima unamtaja bwana mmoja mtukutu sana, aliyewahi kusumbua vichwa vya maofisa usalama wa nchi ya Marekani, akifahamika kama *John Dillinger.* Huyu alikuwa ni moja kati ya wahuni wakubwa nchini Marekani aliyetamba sana katika miaka ya 1930 kwa kujihusisha na matukio ya kihalifu hususani uporaji wa fedha kwenye mabenki.
Tofauti ni kwamba John Dilinga wa Tanzania ni DJ, wakati John Dillinger wa Marekani alikuwa ni jambazi mtukutu.
Utukutu wake ulianza angali ana umri mdogo na hata aliweza kuacha shule ili kwenda kutafuta pesa!! Alianza kama mdokozi wa vitu vidogovidogo lakini tukio lake la kwanza lilikuwa ni *kuiba gari*, kisha 'kwenda misele' kwa mpenzi wake mpya. Siku chache baadae alikuja kukamatwa na mapolisi akiwa anazurula mtaani japokuwa alifanikiwa kuchoropoka na 'kutokomea kusikojulikana'.
Baadae alipata kazi katika jeshi la majini 'navy', akifanya katika meli ya jeshi ya 'USS Uttah'. Baada ya miezi kadhaa John Dillinger alitoroka kazini.
April 1924 akiwa hana shughuli ya kumuingizia kipato, John Dillinger alifunga ndoa na mwanadada Beryl Hovious ambapo walienda kuishi kwenye nyumba ya baba yake ambapo John Dillinger aliahidi kwamba sasa atatulia na kuacha utukutu wote. Lakini wiki chache baada ya ndoa, Dillinger alikamatwa na hata kufikishwa mahakamani kwa kosa la wizi wa kuku, "nadhani alikuwa anatafuta mboga ya kwenda kula na mkewe".
Lakini kwa msaada wa Baba yake, kesi ya Dillinger iliweza kufutwa. Baadae Dillinger aliamua kutoka kwenye nyumba ya baba yake na kwenda kuishi kwenye nyumba ya wazazi wa mwanamke ambapo huko alibahatika kupata kazi kwenye duka la kuuza vifaa vya ujenzi. Akiwa huko, Dillinger alikutana na rafiki yake wa muda mrefu aitwaye *Edgar Singleton,* ambapo walipanga mikakati ya kuiba pesa. Ndipo tarehe 6 septemba 1924 waliiba pesa katika moja ya Grocery japokuwa walikamatwa na kufikishwa mahakamani ambapo John Dillinger alihukumiwa kifungo cha miaka 20 katika Gereza la "Indiana State Reformatory in Pendleton".
Alipokuwa jela, alikutana na wafungwa wengine ambao walimfundisha mbinu nyingine za uhalifu mkubwa hususani uporaji wa fedha kwenye mabenki. Alitumikia kifungo chake hadi mwaka 1933 kwa paroli. Siku chache tu baada ya kutoka jela, John Dillinger alifanya uhalifu mkubwa, safari hii akivamia benki na kuiba pesa benki ingawa alikamatwa na kuhukumiwa kifungo katika gereza la Lima.
Siku chache baada ya Dillinger kuingia jela, wafungwa 12 ambao baadhi yao ni rafiki zake Dillinger, waliweza kutoroka katika gereza la "Indiana State Prison". Hili ni gereza alilowahi kufungwa John Dillinger baada ya kuhamishwa toka kwenye gereza lile la awali.
Miongoni mwa hao waliotoroka, ambao baadhi yao ni marafiki wa Dillinger, walifika katika gereza alilofungwa Dillinger lengo ni kumtorosha rafiki yao. Walimuua askari mmoja na kuchukua funguo kisha kufungua mlango wa selo alilomo Dillinger kisha kutoroka naye. Baada ya kutoroka, John Dillinger na wenzake walielekea mjini Chicago ambapo waliunda genge kubwa la kihalifu *Dillinger Gang*. Genge hili lilipora pesa kwenye mabenki mbalimbali, na ili kuongeza nguvu, walivamia ghala la silaha na kuiba silaha nzitonzito walizozotumia katika shughuli zao za kihalifu.
Wahuni hao walitokea kupata umaarufu mkubwa pale Marekani, hususani huyu Dillinger ambaye alikuwa maarufu sana mithili ya 'nyota wa hollywood' kwani kila siku jina lake lilikuwa likitajwa kwenye vyombo vya habari na kuandikwa magazetini. Sifa nyingine ya genge hili ni kwamba walikuwa watanashati mno wakipendelea kuvaa suti na kofia nyeusi.
Januari 15 1934, Dillinger alivamia benki kuiba pesa. Katika tukio la majibizano ya risasi, Dillinger alimuua askari mmoja aliyejulikana kwa jina la William O'Malley. Yeye alipigwa risasi kadhaa japokuwa hakufa kwasababu alivaa 'bullet proof'.
Baadae, 'Dillinger Gang' walikuja kukamatwa, ambapo Dillinger alipelekwa katika gereza la *crown point* kwa kosa la kumuua Askari. Gereza hilo lilipewa jina la 'escape proof' kwakuwa lilikuwa nj ngumu kutoroka hapo. Umaarufu wake ulipelekea wananchi kufurika mahakamani na gerezani kwa ajili ya kutaka kumuona John Dillinger.
Tarehe 3 Machi 1934, John Dillinger alifanikiwa kutoroka tena katika gereza la *Crown point,* safari hii akitoroka kwa kutumia 'bunduki feki' aliyoichonga kwa kutumia mbao na kuipaka rangi nyeusi. Aliitumia bunduki hiyo kumtisha askari kisha akapora gari la askari na kutoroka nalo. Kitendo hiko kiliwafanya polisi waombe msaada kutoka *FBI* ambao walifanya msako kabambe wa kumkamata John Dillinger.
Alipotoroka, alikimbilia mjini Chicago ambako huko aliunda Genge jipya safari hii akimchukua mtu hatari aliyejulikana kama 'Baby Face Nelson'. Genge hilo liliendelea kufanya matukio mengi ya uporaji wa pesa benki na hata wizi wa silaha. Katika kipindi hiki, John Dillinger alianzisha mahusiano na binti aliyeitwa 'Polly Hamilton' mhudumu wa mgahawa pale Chicago ambaye hapo kabla alikuwa akijihusisha na ukahaba. Ifahamike kuwa kipindi yupo jela, Dillinger alitalikiana na yule mkewe.
MSAKO wa kumpata John Dillinger ulikuwa ukiendelea ambapo FBI walisambaza picha za Dillinger pamoja na kutangaza dau nono kwa yeyote atakayefanikisha upatikanaji wake. FBI walitangaza dau la dola $10,000 kwa yeyote atakayefakiwa kumkamata Dillinger na $5,000 kwa yule atakayetoa taarifa za kupatikana kwake. John Dillinger alisumbua sana vichwa vya maafisa usalama kiasi cha FBI kumtangaza kuwa *"Public Enemy Nō 1".* Ukiona hadi mtu anaitwa Public Enemy Nō 1 ujue huyo alikuwa ni 'kiboko pasua kichwa'.
John Dillinger naye hakuwa nyuma katika kuhakikisha hakamatwi. Unajua alifanyaje??.
Aliamua kufanya operesheni ya uso *"plastic surgery"* ili kubadilisha muonekano wa sura yake. Pia alifanya uperesheni ya kubadilisha alama za vidole yaani 'finger prints'.
Mkuu wa FBI bwana J. Edgar Hoover alimteua bwana Samuel Cowley kuongoza misheni ya kumkamata John Dillinger. Cowley naye aliungana na Afisa *Mervin Purvis* kutoka mjini Chicago. Kwa pamoja walishirikiana na polisi kuhakikisha huyu 'Adui namba moja' anapatikana.
Ilikuwa ni siku ya tarehe 21 Julai 1934 ambapo maafisa usalama walipokea simu kutoka kwa mwanadada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Anna. Binti huyu alitoa taarifa za siri kwamba 'kesho jioni, yeye, John Dillinger pamoja na mpenzi wake, Polly Hamilton, wataenda kuangalia filamu kwenye moja ya majumba ya sinema, akaeleza kwamba watachagua kwenda aidha Biograph Theater au Marbo Theater. Na wakapanga kwamba atavaa vazi la rangi nyekundu ili iwe rahisi kwa maofisa hao kumtambua.
Ilipofika kesho yake, maofisa wakampigia simu Anna Sage ili 'ku-comfirm' ni wapi wataenda kati ya Biograph au Marbo??. Lakini kwakua Anna alikuwa bado hajui ni wapi haswa wataenda, tuliona maofisa usalama wakiongozwa na Marvin Purvis wakijigawa kwenda 'kukava' sehemu zote mbili.
Hatimaye ilipofika majira ya saa 2:30 usiku, Anna, John Dillinger pamoja na Polly Hamilton, walionekana wakiingia kwenye jumba la sinema la *Biograph Theater*. Baada ya kina Dillinger kuingia, tukaona wale maofisa wengine waliokuwepo kule 'Marbo Theater' wakiwasili haraka pale 'Biograph Theater' kwa ajili ya kuongeza nguvu.
Saa 4:30 usiku, baada ya filamu kumalizika, alionekana John Dillinger akiwa na wale warembo wake wawili, mmoja kulia mwingine kushoto, wakiwa wanatoka nje. Wakati wanakuja usawa wa aliposimama ofisa Purvis. Purvis aliwasha sigara yake kama ishara ya wale wenzake kusogea jirani. Wakati anafanya hivyo, kumbe Dillinger alikuwa *'ameshahisi hali ya hatari',* akatoa bastola yake huku akijihami kwa kujaribu kukimbia.
Lakini kabla hajafika mbali, risasi tatu zilifika kwenye mwili wa John Dillinger. Risasi moja ikipenya upande wa nyuma wa shingo na kutokezea kwenye sikio. Dakika chache zilizofuata, hospitali ya Alexian Brothers ilitangaza kifo cha John Dillinger. Na hiyo ndio ikawa mwisho wa mtukutu huyu ambaye alifariki tarehe kama ya leo *22 Julai 1934.* Baada ya kuenea taarifa za kifo chake watu wengi walifurika eneo la tukio angalau waweze kuuona mwili wa John Dillinger.
****
Lakini nafahamu utakuwa unajiuliza yule mwanadada aliyetoa taarifa za siri za kurahisisha kukamatwa kwa John Dillinger ni nani na kwanini alifanya hivyo?!! Baadae nitaeleza kisa hiko. Lakini kwa sasa tuishie hapa.
Ahsante.