• Victor Osimhen tayari ameshatia sahihi Galatasaray Mpaka 2029,na pia Victor Osimhen ndiye mchezaji mwenye gharama na anayelipwa mshahara mkubwa kwenye historia ya soka la uturukii

    #SportsElite
    Victor Osimhen tayari ameshatia sahihi Galatasaray Mpaka 2029,na pia Victor Osimhen ndiye mchezaji mwenye gharama na anayelipwa mshahara mkubwa kwenye historia ya soka la uturukii #SportsElite
    0 Kommentare ·0 Anteile ·131 Ansichten
  • Lionel Messi ameweka rekodi mpya kama mfungaji bora wa mabao mengi zaidi katika historia ya soka bila penalti.

    Mabao kutoka kwa mchezo wa kawaida (bila penalti):
    1️⃣ Lionel Messi – mabao 764
    2️⃣ Cristiano Ronaldo – mabao 763

    Ufanisi wa Messi unazidi kudhihirisha ubora wake wa kipekee ndani ya uwanja.

    #SportsElite
    Lionel Messi ameweka rekodi mpya kama mfungaji bora wa mabao mengi zaidi katika historia ya soka bila penalti. 🐐 Mabao kutoka kwa mchezo wa kawaida (bila penalti): 1️⃣ Lionel Messi – mabao 764 🔝 2️⃣ Cristiano Ronaldo – mabao 763 Ufanisi wa Messi unazidi kudhihirisha ubora wake wa kipekee ndani ya uwanja. #SportsElite
    0 Kommentare ·0 Anteile ·120 Ansichten
  • Asante Aishi Manula muda wote uliokuwa sehemu ya kikosi cha Mnyama. Historia yako itadumu milele. #NguvuMoja

    #paulswai
    Asante Aishi Manula muda wote uliokuwa sehemu ya kikosi cha Mnyama. Historia yako itadumu milele. #NguvuMoja #paulswai
    Love
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·492 Ansichten
  • La kihistoria! Lionel Andrés Messi Cuccittini sasa ndiye mfungaji bora na mtoa asisti wa muda wote katika klabu ya Inter Miami, akiwa na mabao 52 na pasi 29 za mabao!

    🏟 Mechi: 63
    ⚽️ Mabao: 52
    Pasi za mabao: 29

    Takwimu za Messi katika taaluma yake:

    Mechi: 1108
    ⚽️ Mabao: 868
    Pasi za mabao: 385
    Mchango wa goli kwa kila mechi: 1.13

    Bila shaka, ni mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea.

    #SportsElite
    La kihistoria! 🤯 Lionel Andrés Messi Cuccittini sasa ndiye mfungaji bora na mtoa asisti wa muda wote katika klabu ya Inter Miami, akiwa na mabao 52 na pasi 29 za mabao! 🐐 🏟 Mechi: 63 ⚽️ Mabao: 52 🎯 Pasi za mabao: 29 Takwimu za Messi katika taaluma yake: ✅ Mechi: 1108 ⚽️ Mabao: 868 🅰️ Pasi za mabao: 385 🔥 Mchango wa goli kwa kila mechi: 1.13 Bila shaka, ni mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea. 🐐 #SportsElite
    0 Kommentare ·0 Anteile ·220 Ansichten
  • OFFICIAL Chelsea ni timu ya kwanza katika historia kushinda michuano minne tofauti ya UEFA.

    UEFA Europa Conference
    UEFA Champions League
    UEFA Europa League
    UEFA Cup Winner's Cup

    #SportsElite
    🏆💣 OFFICIAL Chelsea ni timu ya kwanza katika historia kushinda michuano minne tofauti ya UEFA. 🏆 UEFA Europa Conference 🏆🏆 UEFA Champions League 🏆🏆 UEFA Europa League 🏆🏆 UEFA Cup Winner's Cup #SportsElite
    Love
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·474 Ansichten
  • 14 /21 Yesu ni vyote zaidi ya vyote.

    *Petro kauliza tumeacha vyote tumekufuata wewe tutapata nini?*

    Ndipo Petro aka mwambia, “Na sisi tulioacha kila kitu tukakufuata tutapata nini?”

    *Swali hili no swali gumu na kila aliye itwa na Mungu huanza kuliuliza lakini ukitulia vizuri utagundua yesu alimjibu Petro kwa vizuri sana.*

    28 Yesu akawajibu, “Ninawahakikishia kwamba, katika dunia mpya, wakati mimi Mwana wa Adamu nitakapoketi kwenye kiti changu cha utukufu cha enzi, ninyi mlionifuata pia mtaketi katika viti vya enzi kumi na viwili, mkiyahukumu yale makabila kumi na mawili ya Israeli.


    Utapata vyote vya duniani kisha uzima ule wa milele.

    29 Na kila mtu aliyeacha nyumba au ndugu zake au dada zake au baba au mama au watoto wake au mashamba kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia zaidi ya hayo, na atarithi uzima wa milele.

    *Kumbe kadiri unavyo acha kwa ajiri ya injiri ndivyo unavyo pata.*

    Na hili linatimia pale mfalme alipo omba hekima ya kuamua na kuongoza Mungu akampa vyote zaidi ya vyote.

    *Watu wa Mungu ni muhimu sana kujua kuwa kama Mungu amekutenga kwa ajiri ya kazi yake pia hawezi kukuacha hivi hivi lazima tu atakubaliki zaidi .*

    Kumbe kuhimu sana ni utii wa lile kusudi ulilopewa na Mungu .

    Najua hata wewe unajiuliza swali lile lile kuwa nitapata nini nikimfuata Yesu utapata vyote vya duniani kisha mbinguni uzima wa milele na kutawala na Kristo.

    *Walio kubali kumfuata yesu ndio wanapaswa kuitwa vichwa na wala si mkia kwa kuwa yesu ni kichwa cha kanisa kumbe hata sisi ni vichwa mara zote .Ko ni wewe tu kuamua kumfuata yeye ambaye ni zaidi ya vyote.*

    Maandiko yanasema mjue sana Mungu ndipo mema ya kufuate ,kumbe ili yakufuate kuna kanuni yake lazima umjue sana na kumjua ndiko kumuishi (kumfuata ).

    *Ok ni vyema jion hii ukamtaka Yesu ambaye ni vyote zaidi ya vyote ili awe Bwana na mwokozi wa maisha yako na akabadilisha historia yako yote.*

    Ahsante sana naitwa sylvester Mwakabende (build new eden) .

    #build new eden
    #restore men position
    14 /21 Yesu ni vyote zaidi ya vyote. *Petro kauliza tumeacha vyote tumekufuata wewe tutapata nini?* Ndipo Petro aka mwambia, “Na sisi tulioacha kila kitu tukakufuata tutapata nini?” *Swali hili no swali gumu na kila aliye itwa na Mungu huanza kuliuliza lakini ukitulia vizuri utagundua yesu alimjibu Petro kwa vizuri sana.* 28 Yesu akawajibu, “Ninawahakikishia kwamba, katika dunia mpya, wakati mimi Mwana wa Adamu nitakapoketi kwenye kiti changu cha utukufu cha enzi, ninyi mlionifuata pia mtaketi katika viti vya enzi kumi na viwili, mkiyahukumu yale makabila kumi na mawili ya Israeli. Utapata vyote vya duniani kisha uzima ule wa milele. 29 Na kila mtu aliyeacha nyumba au ndugu zake au dada zake au baba au mama au watoto wake au mashamba kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia zaidi ya hayo, na atarithi uzima wa milele. *Kumbe kadiri unavyo acha kwa ajiri ya injiri ndivyo unavyo pata.* Na hili linatimia pale mfalme alipo omba hekima ya kuamua na kuongoza Mungu akampa vyote zaidi ya vyote. *Watu wa Mungu ni muhimu sana kujua kuwa kama Mungu amekutenga kwa ajiri ya kazi yake pia hawezi kukuacha hivi hivi lazima tu atakubaliki zaidi .* Kumbe kuhimu sana ni utii wa lile kusudi ulilopewa na Mungu . Najua hata wewe unajiuliza swali lile lile kuwa nitapata nini nikimfuata Yesu utapata vyote vya duniani kisha mbinguni uzima wa milele na kutawala na Kristo. *Walio kubali kumfuata yesu ndio wanapaswa kuitwa vichwa na wala si mkia kwa kuwa yesu ni kichwa cha kanisa kumbe hata sisi ni vichwa mara zote .Ko ni wewe tu kuamua kumfuata yeye ambaye ni zaidi ya vyote.* Maandiko yanasema mjue sana Mungu ndipo mema ya kufuate ,kumbe ili yakufuate kuna kanuni yake lazima umjue sana na kumjua ndiko kumuishi (kumfuata ). *Ok ni vyema jion hii ukamtaka Yesu ambaye ni vyote zaidi ya vyote ili awe Bwana na mwokozi wa maisha yako na akabadilisha historia yako yote.* Ahsante sana naitwa sylvester Mwakabende (build new eden) . #build new eden #restore men position
    0 Kommentare ·0 Anteile ·839 Ansichten
  • Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) limetangaza zawadi zitakazotolewa kwa Washiriki wa michuano ya Kombe la Dunia la Klabu (FIFA CLUB WORLD CUP), ambapo bingwa wa michuano hiyo atapata dola milioni 125 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 300 za kitanzania huku kukitarajiwa kutolewa jumla ya dola bilioni 1 kwa klabu 32 zitakavyoshiriki na dola milioni 250 zitatolewa kwa mashirikisho kwa ajili kukuza mpira wa miguu kwa ngazi ya klabu Duniani.

    Shirikisho hilo limepanga kutoa dola milioni 250 ili kusaidia maendeleo ya mpira wa miguu kwa kiwango cha kimataifa ambapo fedha hizi zitatumika kusaidia klabu ndogo, kuboresha miundombinu, kuwekeza katika mafunzo ya Wachezaji na Makocha pamoja na kuimarisha ushirikiano wa klabu kimataifa.

    Aidha, pango huu unalenga kuhakikisha kuwa maendeleo ya mpira wa miguu hayaishii kwa klabu kubwa pekee, bali pia yanawanufaisha hadi klabu dogo na kuinua mpira wa Duniani kote. FIFA pia imesisitiza kuwa, mapato yote ya mashindano haya yatasambazwa kwa klabu bila kugusa akiba yake, ambayo inatumiwa kwa maendeleo ya mpira wa miguu kupitia Vyama (211) Wanachama wa FIFA.

    Mfumo huu ni mkubwa zaidi katika historia ya mpira wa miguu, ukiwa na mechi saba (7) kwenye hatua ya makundi na mfumo wa mchujo.

    Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) limetangaza zawadi zitakazotolewa kwa Washiriki wa michuano ya Kombe la Dunia la Klabu (FIFA CLUB WORLD CUP), ambapo bingwa wa michuano hiyo atapata dola milioni 125 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 300 za kitanzania huku kukitarajiwa kutolewa jumla ya dola bilioni 1 kwa klabu 32 zitakavyoshiriki na dola milioni 250 zitatolewa kwa mashirikisho kwa ajili kukuza mpira wa miguu kwa ngazi ya klabu Duniani. Shirikisho hilo limepanga kutoa dola milioni 250 ili kusaidia maendeleo ya mpira wa miguu kwa kiwango cha kimataifa ambapo fedha hizi zitatumika kusaidia klabu ndogo, kuboresha miundombinu, kuwekeza katika mafunzo ya Wachezaji na Makocha pamoja na kuimarisha ushirikiano wa klabu kimataifa. Aidha, pango huu unalenga kuhakikisha kuwa maendeleo ya mpira wa miguu hayaishii kwa klabu kubwa pekee, bali pia yanawanufaisha hadi klabu dogo na kuinua mpira wa Duniani kote. FIFA pia imesisitiza kuwa, mapato yote ya mashindano haya yatasambazwa kwa klabu bila kugusa akiba yake, ambayo inatumiwa kwa maendeleo ya mpira wa miguu kupitia Vyama (211) Wanachama wa FIFA. Mfumo huu ni mkubwa zaidi katika historia ya mpira wa miguu, ukiwa na mechi saba (7) kwenye hatua ya makundi na mfumo wa mchujo.
    0 Kommentare ·0 Anteile ·880 Ansichten
  • Jeshi la Nchi ya Uganda limesema limewaua Wapiganaji 242 wa kundi la Waasi Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linalojulikana kama CODECO baada ya kushambulia kambi ya Jeshi hilo la Uganda mpakani mashariki mwa DR Congo mapema wiki hii ambapo madai yamepingwa na Kundi hilo.

    Msemaji wa Jeshi la Uganda, Chris Magezi, amesema mamia ya Wapiganaji wa kundi la CODECO walishambulia kituo cha kijeshi cha Uganda People's Defence Forces (UPDF) katika eneo la Fataki, Mkoani Ituri, siku ya Jumatano na Alhamisi. Jeshi hilo lilijibu mashambulizi hayo mara zote mbili, likiwaangamiza Wapiganaji 31 siku ya kwanza na 211 siku ya pili, Magezi alisema katika chapisho kwenye akaunti yake ya Mtandao wa X Ijumaa usiku na kuongeza kuwa askari mmoja wa UPDF aliuawa na wengine wanne kujeruhiwa.

    Msemaji wa CODECO, Basa Zukpa Gerson, alipinga taarifa ya jeshi Jumamosi, akisema kundi hilo lilipoteza wapiganaji wawili tu na kwamba idadi ya vifo vya Wanajeshi wa UPDF ilikuwa juu zaidi. Chanzo kimoja cha Umoja wa Mataifa ambacho hakikutaka kutajwa jina kilisema Waasi 70 na Wanajeshi wa Uganda 12 waliuawa.

    Kulikuwa na mapigano zaidi kati ya pande hizo mbili asubuhi ya Jumamosi, alisema Msemaji wa CODECO na kiongozi mmoja wa jamii za kiraia wa eneo hilo. Wapiganaji wa CODECO wanasema lengo lao ni kuwalinda Wakulima wa Lendu dhidi ya Wafungaji wa Hema, ambao kihistoria wamekuwa wakigombana kuhusu ardhi.

    Kundi hilo ni moja ya makundi mengi ya Waasi yanayopigania ardhi na rasilimali za madini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo Waasi wa M23 wameongeza mashambulizi mwaka huu na kupata mafanikio makubwa. Uganda ilituma wanajeshi DR Congo mwaka 2021 kusaidia Serikali kupambana na kundi lingine la Waasi, Allied Democratic Forces (ADF), ambalo lina uhusiano na Islamic State na linafanya mashambulizi ya kikatili kwenye baadhi ya Vijiji.

    Jeshi la Nchi ya Uganda 🇺🇬 limesema limewaua Wapiganaji 242 wa kundi la Waasi Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 linalojulikana kama CODECO baada ya kushambulia kambi ya Jeshi hilo la Uganda mpakani mashariki mwa DR Congo mapema wiki hii ambapo madai yamepingwa na Kundi hilo. Msemaji wa Jeshi la Uganda, Chris Magezi, amesema mamia ya Wapiganaji wa kundi la CODECO walishambulia kituo cha kijeshi cha Uganda People's Defence Forces (UPDF) katika eneo la Fataki, Mkoani Ituri, siku ya Jumatano na Alhamisi. Jeshi hilo lilijibu mashambulizi hayo mara zote mbili, likiwaangamiza Wapiganaji 31 siku ya kwanza na 211 siku ya pili, Magezi alisema katika chapisho kwenye akaunti yake ya Mtandao wa X Ijumaa usiku na kuongeza kuwa askari mmoja wa UPDF aliuawa na wengine wanne kujeruhiwa. Msemaji wa CODECO, Basa Zukpa Gerson, alipinga taarifa ya jeshi Jumamosi, akisema kundi hilo lilipoteza wapiganaji wawili tu na kwamba idadi ya vifo vya Wanajeshi wa UPDF ilikuwa juu zaidi. Chanzo kimoja cha Umoja wa Mataifa ambacho hakikutaka kutajwa jina kilisema Waasi 70 na Wanajeshi wa Uganda 12 waliuawa. Kulikuwa na mapigano zaidi kati ya pande hizo mbili asubuhi ya Jumamosi, alisema Msemaji wa CODECO na kiongozi mmoja wa jamii za kiraia wa eneo hilo. Wapiganaji wa CODECO wanasema lengo lao ni kuwalinda Wakulima wa Lendu dhidi ya Wafungaji wa Hema, ambao kihistoria wamekuwa wakigombana kuhusu ardhi. Kundi hilo ni moja ya makundi mengi ya Waasi yanayopigania ardhi na rasilimali za madini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo Waasi wa M23 wameongeza mashambulizi mwaka huu na kupata mafanikio makubwa. Uganda ilituma wanajeshi DR Congo mwaka 2021 kusaidia Serikali kupambana na kundi lingine la Waasi, Allied Democratic Forces (ADF), ambalo lina uhusiano na Islamic State na linafanya mashambulizi ya kikatili kwenye baadhi ya Vijiji.
    Like
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·629 Ansichten
  • Historia ya Wazazi wa Jackie Chan inavutia zaidi hadi Jackie Chan aliamua kuandaa "Documentary" maalum kwa ajili ya kueleza Wazazi wake walivyokutana na walikuwa wanafanya kazi gani.

    Katika kipindi chote Jackie Chan alichoishi na Wazazi wake hakuwahi kufahamu Wazazi wake walikutana vipi pamoja na kazi halisi za awali za Wazazi wake mpaka hapo Baba yake alipokuwa ana umri wa miaka 80 akaamua kumwambia ukweli maana aliamini umri wake umeenda sana hivyo muda wowote anaweza kufariki bila kumueleza ukweli Jackie Chan.

    Baba Mzazi wa Jackie Chan, Charles Chan (1914 - 2008) siku moja akiwa barabarani kwenye gari na Jackie Chan alifunguka kuwa tangu zamani alikuwa Mpelelezi (Shushushu) kwenye Serikali ya China na Mama yake Jackie Chan, Lee-Lee Chan (1916-2002) alikuwa muuza madawa ya kulevya, siku moja katika "operation" ya kukamata Wauza madawa Charles Chan alimkamata Lee-Lee Chan lakini baada ya kumfikisha kwenye vyombo vya dola walijikuta wamependana na wakafunga ndoa.

    Hadithi hii ilimshitua sana Jackie Chan kwani amekua akijua kwamba Baba yake ni Mpishi na amewahi kuwa Mpishi kwenye ubalozi wa Ufaransa - Hong Kong, pamoja na ubalozi wa Marekani Nchini Australia .

    Taarifa nyingine iliyomshitua zaidi ni pale alipoambiwa kuwa kuwa jina la Baba yake sio Chan bali ni Fang Daolong, hivyo kama asingebadili jina, Jackie Chan hivi sasa angefahamika kama Jackie Fang, Baba Jackie Chan alikuwa "Spy" kwenye Serikali ya China iliyokuwa ikiundwa na Chama cha Kuomintang, mwaka 1949 baada ya vita kali ya wenyewe kwa wenyewe Chama cha Kikomunisti kikiongozwa na Mao Zedong kiliipindua Serikali ya Kuomintang kikachukua Nchi hapo ilibidi Baba Jackie Chan abadili jina kwa sababu ya kuficha utambulisho wake maana kulikuwa na vita kubwa baina ya vyama hivyo na baadhi ya makachero wa Kuomintang walikuwa wakikamatwa na kuuawa.

    Historia ya Wazazi wa Jackie Chan imeelezwa kwa urefu kwenye "Documentary" iliyoandaliwa na Jackie Chan "Traces of the Dragon: Jackie Chan and His Lost Family" (2003)

    "Baba alikua jasusi na Mama alikua Muuza madawa na mcheza kamari. Walikutana na wakaoana baada ya Baba yangu kumkamata Mama"

    "Tangu nilipokua Mdogo nilikua najua Baba yangu anafanya kazi ya upishi kwenye Ubalozi wa Marekani mpaka alipotimiza miaka 80 na akaniambia kazi yake ya kweli. Nilishtuka, nilishtuka"

    " Kwahiyo kuna siku moja nilikua naendesha gari nikiwa na Baba yangu ghafla, Baba akageuka na kusema: 'Jackie, Mimi ni Mzee sana na huenda nisiamke kesho. Kuna kitu lazima nikuambie, ni siri' kisha akasema: kwa kweli wewe sio Jackie Chan, jina lako unaitwa Fong.'

    "Nikahisi kupatwa na mshtuko, kwangu ilikua kitu cha kustaajabisha. Kwa haraka nikamuambia asiendelee kuongea nikampigia rafiki yangu ili tutengeneze documentary ya stori ya Baba yangu. Ilituchukua miaka 3 ya kumfata Baba yangu na kuongea nae kuhusu stori yote."

    " Nilihisi mimi ndiye Mwanae wa pekee lakini nilishtuka baada ya kujua kwamba nina ndugu zangu wanne kwa Wazazi wangu. Kaka zangu wawili, upande wa Baba na Dada zangu wawili upande wa Mama. Alilazimika kunificha yote hayo kwa sababu ya kazi yake, baba alikua jasusi. Nilivutiwa sana baada ya kujua kwamba Baba yangu alikua mpole sana. Miaka yote ile nilidhania ni Mpishi. Nimetengeneza movie kupitia hii stori." - Jackie Chan

    Historia ya Wazazi wa Jackie Chan inavutia zaidi hadi Jackie Chan aliamua kuandaa "Documentary" maalum kwa ajili ya kueleza Wazazi wake walivyokutana na walikuwa wanafanya kazi gani. Katika kipindi chote Jackie Chan alichoishi na Wazazi wake hakuwahi kufahamu Wazazi wake walikutana vipi pamoja na kazi halisi za awali za Wazazi wake mpaka hapo Baba yake alipokuwa ana umri wa miaka 80 akaamua kumwambia ukweli maana aliamini umri wake umeenda sana hivyo muda wowote anaweza kufariki bila kumueleza ukweli Jackie Chan. Baba Mzazi wa Jackie Chan, Charles Chan (1914 - 2008) siku moja akiwa barabarani kwenye gari na Jackie Chan alifunguka kuwa tangu zamani alikuwa Mpelelezi (Shushushu) kwenye Serikali ya China na Mama yake Jackie Chan, Lee-Lee Chan (1916-2002) alikuwa muuza madawa ya kulevya, siku moja katika "operation" ya kukamata Wauza madawa Charles Chan alimkamata Lee-Lee Chan lakini baada ya kumfikisha kwenye vyombo vya dola walijikuta wamependana na wakafunga ndoa. Hadithi hii ilimshitua sana Jackie Chan kwani amekua akijua kwamba Baba yake ni Mpishi na amewahi kuwa Mpishi kwenye ubalozi wa Ufaransa 🇫🇷 - Hong Kong, pamoja na ubalozi wa Marekani 🇺🇸 Nchini Australia 🇦🇺. Taarifa nyingine iliyomshitua zaidi ni pale alipoambiwa kuwa kuwa jina la Baba yake sio Chan bali ni Fang Daolong, hivyo kama asingebadili jina, Jackie Chan hivi sasa angefahamika kama Jackie Fang, Baba Jackie Chan alikuwa "Spy" kwenye Serikali ya China iliyokuwa ikiundwa na Chama cha Kuomintang, mwaka 1949 baada ya vita kali ya wenyewe kwa wenyewe Chama cha Kikomunisti kikiongozwa na Mao Zedong kiliipindua Serikali ya Kuomintang kikachukua Nchi hapo ilibidi Baba Jackie Chan abadili jina kwa sababu ya kuficha utambulisho wake maana kulikuwa na vita kubwa baina ya vyama hivyo na baadhi ya makachero wa Kuomintang walikuwa wakikamatwa na kuuawa. Historia ya Wazazi wa Jackie Chan imeelezwa kwa urefu kwenye "Documentary" iliyoandaliwa na Jackie Chan "Traces of the Dragon: Jackie Chan and His Lost Family" (2003) "Baba alikua jasusi na Mama alikua Muuza madawa na mcheza kamari. Walikutana na wakaoana baada ya Baba yangu kumkamata Mama" "Tangu nilipokua Mdogo nilikua najua Baba yangu anafanya kazi ya upishi kwenye Ubalozi wa Marekani mpaka alipotimiza miaka 80 na akaniambia kazi yake ya kweli. Nilishtuka, nilishtuka" " Kwahiyo kuna siku moja nilikua naendesha gari nikiwa na Baba yangu ghafla, Baba akageuka na kusema: 'Jackie, Mimi ni Mzee sana na huenda nisiamke kesho. Kuna kitu lazima nikuambie, ni siri' kisha akasema: kwa kweli wewe sio Jackie Chan, jina lako unaitwa Fong.' "Nikahisi kupatwa na mshtuko, kwangu ilikua kitu cha kustaajabisha. Kwa haraka nikamuambia asiendelee kuongea nikampigia rafiki yangu ili tutengeneze documentary ya stori ya Baba yangu. Ilituchukua miaka 3 ya kumfata Baba yangu na kuongea nae kuhusu stori yote." " Nilihisi mimi ndiye Mwanae wa pekee lakini nilishtuka baada ya kujua kwamba nina ndugu zangu wanne kwa Wazazi wangu. Kaka zangu wawili, upande wa Baba na Dada zangu wawili upande wa Mama. Alilazimika kunificha yote hayo kwa sababu ya kazi yake, baba alikua jasusi. Nilivutiwa sana baada ya kujua kwamba Baba yangu alikua mpole sana. Miaka yote ile nilidhania ni Mpishi. Nimetengeneza movie kupitia hii stori." - Jackie Chan
    Like
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·1KB Ansichten
  • Rais wa Nchi ya Iran , Ayatollah Ali Khamenei, amesema kuwa vitisho vya Nchi ya Marekani dhidi ya Taifa lake havisaidii lolote na havitaleta matokeo yoyote kama Rais Donald Tramp anavyofikiria. Kiongozi huyo amesema hayo baada ya Rais Trump kuonya uwezekano wa hatua za kijeshi kuchukuliwa dhidi ya Iran.

    "Wamarekani wanapaswa kuelewa kwamba vitisho havitafanikiwa wanapokabiliana na Iran. Wao (Marekani) na wengine wanapaswa kufahamu kuwa wakifanya lolote baya dhidi ya taifa la Iran, watajibiwa kwa nguvu kubwa." alisema Rais Khemenei

    Mnamo Machi 7, Rais Trump alisema kuwa alimwandikia barua Rais Khamenei, akimtaka kuanzisha mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, huku akionya kuwa kuna uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi iwapo Iran itakataa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, alisema Alhamisi wiki hii kuwa barua hiyo ilikuwa zaidi ya tishio, ingawa pia ilionesha uwezekano wa mazungumzo.

    "Tunachunguza kwa kina maudhui ya barua hiyo, na tutajibu rasmi katika siku chache zijazo” alisema Waziri huyo

    Kulingana na ripoti ya tovuti ya habari ya Marekani, Axios, ikimnukuu Afisa wa Serikali ya Trump na vyanzo vingine vikisema, barua hiyo inaweka muda wa miezi miwili wa kufikia makubaliano mapya ya nyuklia. Hata hivyo, haijabainishwa ni lini muda huo utaanza au kuisha. Kwa muda mrefu, Rais Khamenei amepuuza wito wa Rais Trump wa mazungumzo ya moja kwa moja, akisema kuwa Rais huyo wa Marekani anajaribu kudanganya ulimwengu kwa kuonesha kuwa Marekani iko tayari kwa mazungumzo huku Iran ikionekana kutotaka kushiriki.

    Ikumbukwe kwamba Trump ambaye alianza muhula wake wa pili Januari 2025, amerudisha sera yake ya shinikizo la juu dhidi ya Iran. Wakati wa kipindi chake cha kwanza, Trump aliiondoa Marekani kwenye makubaliano ya kihistoria ya nyuklia ya 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu ulimwenguni na akairejeshea Tehran vikwazo vikubwa vya kiuchumi.

    Rais wa Nchi ya Iran 🇮🇷, Ayatollah Ali Khamenei, amesema kuwa vitisho vya Nchi ya Marekani 🇺🇸 dhidi ya Taifa lake havisaidii lolote na havitaleta matokeo yoyote kama Rais Donald Tramp anavyofikiria. Kiongozi huyo amesema hayo baada ya Rais Trump kuonya uwezekano wa hatua za kijeshi kuchukuliwa dhidi ya Iran. "Wamarekani wanapaswa kuelewa kwamba vitisho havitafanikiwa wanapokabiliana na Iran. Wao (Marekani) na wengine wanapaswa kufahamu kuwa wakifanya lolote baya dhidi ya taifa la Iran, watajibiwa kwa nguvu kubwa." alisema Rais Khemenei Mnamo Machi 7, Rais Trump alisema kuwa alimwandikia barua Rais Khamenei, akimtaka kuanzisha mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, huku akionya kuwa kuna uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi iwapo Iran itakataa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, alisema Alhamisi wiki hii kuwa barua hiyo ilikuwa zaidi ya tishio, ingawa pia ilionesha uwezekano wa mazungumzo. "Tunachunguza kwa kina maudhui ya barua hiyo, na tutajibu rasmi katika siku chache zijazo” alisema Waziri huyo Kulingana na ripoti ya tovuti ya habari ya Marekani, Axios, ikimnukuu Afisa wa Serikali ya Trump na vyanzo vingine vikisema, barua hiyo inaweka muda wa miezi miwili wa kufikia makubaliano mapya ya nyuklia. Hata hivyo, haijabainishwa ni lini muda huo utaanza au kuisha. Kwa muda mrefu, Rais Khamenei amepuuza wito wa Rais Trump wa mazungumzo ya moja kwa moja, akisema kuwa Rais huyo wa Marekani anajaribu kudanganya ulimwengu kwa kuonesha kuwa Marekani iko tayari kwa mazungumzo huku Iran ikionekana kutotaka kushiriki. Ikumbukwe kwamba Trump ambaye alianza muhula wake wa pili Januari 2025, amerudisha sera yake ya shinikizo la juu dhidi ya Iran. Wakati wa kipindi chake cha kwanza, Trump aliiondoa Marekani kwenye makubaliano ya kihistoria ya nyuklia ya 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu ulimwenguni na akairejeshea Tehran vikwazo vikubwa vya kiuchumi.
    0 Kommentare ·0 Anteile ·1KB Ansichten
  • "Kupitia kituo cha Wasafi, Kamishna wa mchezo wa Simba na Yanga wa raundi ya kwanza Khalid Bitebo ameomba radhi kuwa aliteleza sio kweli kwamba Yanga walifanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Mkapa kwenye Derby iliyopita, kifupi ameomba radhi kuwa alijichanganya.

    Na huo ndio ukweli ulio wazi kuwa kwenye historia ya Derby hakuna aliyewahi kufanya mazoezi siku moja kabla ya mchezo pale hata Mimi siku ya kwanza ya sakata hili niliripoti kuwa Yanga alifanya mazoezi pale ila sio kweli hawakufanya, Simba na Yanga hata mechi yao iwe Mwanza au Kigoma hawafanyi mazoezi kwenye uwanja wa game, inaenda mbali hadi pitch feeling wanakwepa.

    Wakongwe wa Simba na Yanga pia wakanikumbusha zamani kwanza walikuwa wote wanapakimbia Dar Es Slaaam sio Mgeni wala Mwenyeji wa mechi, mwingine anaenda Pemba mwingine Morogoro, mara Zanzibar mwingine Pemba, timu zinakutana Mjini Mzizima hapa siku ya mbungi na inapigwa kwelikweli ndio utaratibu wao.

    Kwakuwa Kamishna wa mchezo ameomba radhi nadhani ni muhimu ila sio lazima basi na wale waliounga mkono, wakaaminisha Umma kuwa Yanga alifanya mazoezi pale wakaomba radhi pia, ni muhimu ila sio lazima ni katika kuweka kumbukumbu tu sawa, tunakubaliana?" - Farhan JR, Mchambuzi.

    "Kupitia kituo cha Wasafi, Kamishna wa mchezo wa Simba na Yanga wa raundi ya kwanza Khalid Bitebo ameomba radhi kuwa aliteleza sio kweli kwamba Yanga walifanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Mkapa kwenye Derby iliyopita, kifupi ameomba radhi kuwa alijichanganya. Na huo ndio ukweli ulio wazi kuwa kwenye historia ya Derby hakuna aliyewahi kufanya mazoezi siku moja kabla ya mchezo pale hata Mimi siku ya kwanza ya sakata hili niliripoti kuwa Yanga alifanya mazoezi pale ila sio kweli hawakufanya, Simba na Yanga hata mechi yao iwe Mwanza au Kigoma hawafanyi mazoezi kwenye uwanja wa game, inaenda mbali hadi pitch feeling wanakwepa. Wakongwe wa Simba na Yanga pia wakanikumbusha zamani kwanza walikuwa wote wanapakimbia Dar Es Slaaam sio Mgeni wala Mwenyeji wa mechi, mwingine anaenda Pemba mwingine Morogoro, mara Zanzibar mwingine Pemba, timu zinakutana Mjini Mzizima hapa siku ya mbungi na inapigwa kwelikweli ndio utaratibu wao. Kwakuwa Kamishna wa mchezo ameomba radhi nadhani ni muhimu ila sio lazima basi na wale waliounga mkono, wakaaminisha Umma kuwa Yanga alifanya mazoezi pale wakaomba radhi pia, ni muhimu ila sio lazima ni katika kuweka kumbukumbu tu sawa, tunakubaliana?" - Farhan JR, Mchambuzi.
    Like
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·964 Ansichten
  • "Kumbe sasa naanza kupata picha kamili ya sakata hili, nakumbushwa kuwa kwenye historia ya Derby ya Kariakoo, huwa wote wawili hawafanyi mazoezi pale uwanjani siku moja kabla ya mchezo, uwe Mgeni au uwe Mwenyeji huruhusiwi kuugusa uwanja, imekuwa hivyo kwenye historia ya mechi zao na uwanja unalindwa, kila mmoja anapaswa kufanya mazoezi anapofanyiaga, japo hii haipo kikanuni hii kitu ndio nimejua leo, imenishangaza sana.

    Maswali yanakuja, kama mchakato huu haupo Kikanuni na walikuwa wanafuata wote wawili, je walikuwa wanasimamiwa na nani wote wawili kutekeleza kanuni hii mficho? Maana hata mechi ya raundi ya kwanza Mgeni Yanga hakusogea kabisa kwa Mkapa, nimetumiwa picha kuwa walifanya mazoezi Kigamboni, hili sakata

    Ligi ina kanuni au utaratibu au makubaliano ambayo hatuyajui ama? Rasmi nimefunga mikono yangu, siandiki tena hii kitu kumbe ina mambo mengi sana, tunaweza kukomaa na Kanuni kumbe wala watu hawapo huko kwenye karatasi zetu" - Farhan JR, Mchambuzi.

    "Kumbe sasa naanza kupata picha kamili ya sakata hili, nakumbushwa kuwa kwenye historia ya Derby ya Kariakoo, huwa wote wawili hawafanyi mazoezi pale uwanjani siku moja kabla ya mchezo, uwe Mgeni au uwe Mwenyeji huruhusiwi kuugusa uwanja, imekuwa hivyo kwenye historia ya mechi zao na uwanja unalindwa, kila mmoja anapaswa kufanya mazoezi anapofanyiaga, japo hii haipo kikanuni hii kitu ndio nimejua leo, imenishangaza sana. Maswali yanakuja, kama mchakato huu haupo Kikanuni na walikuwa wanafuata wote wawili, je walikuwa wanasimamiwa na nani wote wawili kutekeleza kanuni hii mficho? Maana hata mechi ya raundi ya kwanza Mgeni Yanga hakusogea kabisa kwa Mkapa, nimetumiwa picha kuwa walifanya mazoezi Kigamboni, hili sakata🙌😀 Ligi ina kanuni au utaratibu au makubaliano ambayo hatuyajui ama? Rasmi nimefunga mikono yangu, siandiki tena hii kitu kumbe ina mambo mengi sana, tunaweza kukomaa na Kanuni kumbe wala watu hawapo huko kwenye karatasi zetu" - Farhan JR, Mchambuzi.
    Like
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·626 Ansichten
  • Orodha ya Watayarishaji bora kwenye historia ya muziki wa Tanzania.

    1. P Funk
    2. Master Jay
    3. Miika Mwamba
    4. Bonny Love
    5. Prof Ludigo

    6. Bizzman
    7. Enrico
    8. Marco Chali
    9. Hermy B
    10. Lamar

    11. Man Walter
    12. Alain Mapigo
    13. Said Comorean
    14. Ambrose Dunga
    15. Pancho Latino

    16. J Ryder
    17. T Touch
    18. Kameta
    19. Mona Gangster
    20. Shaddy Clever

    21. Complex
    22. Manecky
    23. Abbah
    24. KGT
    25. Bob Junior

    26. Mensen Selekta
    27. Duke
    28. S2Kezzy
    29. Laizer
    30. Abby Daddy

    31. Bonga
    32. Emma The Boy
    33. Nahreel
    34. Mangustino
    35. Kidbway

    36. Shirko
    37. Fundi Samuel
    38. Ali Baucha.

    Panga orodha yako Watayarishaji wa tano bora wa muda wote.
    Orodha ya Watayarishaji bora kwenye historia ya muziki wa Tanzania. 1. P Funk 2. Master Jay 3. Miika Mwamba 4. Bonny Love 5. Prof Ludigo 6. Bizzman 7. Enrico 8. Marco Chali 9. Hermy B 10. Lamar 11. Man Walter 12. Alain Mapigo 13. Said Comorean 14. Ambrose Dunga 15. Pancho Latino 16. J Ryder 17. T Touch 18. Kameta 19. Mona Gangster 20. Shaddy Clever 21. Complex 22. Manecky 23. Abbah 24. KGT 25. Bob Junior 26. Mensen Selekta 27. Duke 28. S2Kezzy 29. Laizer 30. Abby Daddy 31. Bonga 32. Emma The Boy 33. Nahreel 34. Mangustino 35. Kidbway 36. Shirko 37. Fundi Samuel 38. Ali Baucha. Panga orodha yako Watayarishaji wa tano bora wa muda wote.
    Like
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·855 Ansichten
  • Ijumaa, tarehe 28 Februari, haikuwa siku rahisi kwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alipofanya ziara katika Ikulu ya White House, Marekani. Kabla hata ya mzozo wa maneno kati yake na mwenyeji wake, Rais Donald Trump, pamoja na Makamu wa Rais JD Vance, tayari kulikuwa na ishara za mivutano.

    Trump alimkaribisha Zelensky mlangoni na kusema kwa utani: “Leo amevalia kweli kweli,” kauli ambayo iliwafanya baadhi ya waandishi wa habari kuiona kama kejeli badala ya pongezi. Wakati huo, Zelensky alikuwa amevalia fulana nyeusi ya mikono mirefu, vazi ambalo amekuwa akilivaa mara kwa mara tangu Ukraine ivamiwe na Urusi mwaka 2022.

    Baadaye, Trump alipompokea Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, alionekana kutazama mavazi yake kwa makini kutoka juu hadi chini, kisha kunong’ona maneno yanayoweza kutafsiriwa kama pongezi kwa suti rasmi aliyovaa Starmer.

    Mjadala kuhusu mavazi ya Zelensky ulizidi kupamba moto wakati wa mkutano wa waandishi wa habari. Brian Glenn, mwandishi kutoka Real America’s Voice—chombo cha habari kinachopendelea mrengo wa kulia—alimtupia swali la moja kwa moja:

    “Kwa nini hauvai suti? Upo katika ofisi ya juu kabisa katika nchi hii, na umegoma kuvaa suti – je, unamiliki hata suti?”

    Kwa utulivu, Zelensky alijibu kwa mshangao mdogo:

    “Nitavaa suti vita hivi vitakapomalizika. Labda suti kama yako, labda bora zaidi, au pengine ya bei nafuu kuliko yako,” alisema kwa utani huku akionyesha msimamo wake wa kuendelea kuvaa mavazi ya kijeshi.

    Swali hilo la Glenn liliibua mjadala mkali mitandaoni. Wengine walimuunga mkono, wakisema kwamba kiongozi wa taifa anapaswa kuvaa mavazi rasmi anapokutana na viongozi wengine, ilhali wengine waliona swali hilo kuwa la dhihaka na lisilo na umuhimu.

    Miongoni mwa waliomkosoa Glenn ni mwandishi maarufu wa Uingereza, Piers Morgan, ambaye pia ni rafiki wa karibu wa Trump. Morgan aliandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter):

    “Swali la kipuuzi. Elon Musk havai suti anapoingia Ikulu.”

    Historia pia inaonyesha kuwa si Zelensky pekee aliyeingia Ikulu ya Marekani bila suti. Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Winston Churchill, alifanya hivyo katika moja ya ziara zake rasmi.
    Ijumaa, tarehe 28 Februari, haikuwa siku rahisi kwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alipofanya ziara katika Ikulu ya White House, Marekani. Kabla hata ya mzozo wa maneno kati yake na mwenyeji wake, Rais Donald Trump, pamoja na Makamu wa Rais JD Vance, tayari kulikuwa na ishara za mivutano. Trump alimkaribisha Zelensky mlangoni na kusema kwa utani: “Leo amevalia kweli kweli,” kauli ambayo iliwafanya baadhi ya waandishi wa habari kuiona kama kejeli badala ya pongezi. Wakati huo, Zelensky alikuwa amevalia fulana nyeusi ya mikono mirefu, vazi ambalo amekuwa akilivaa mara kwa mara tangu Ukraine ivamiwe na Urusi mwaka 2022. Baadaye, Trump alipompokea Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, alionekana kutazama mavazi yake kwa makini kutoka juu hadi chini, kisha kunong’ona maneno yanayoweza kutafsiriwa kama pongezi kwa suti rasmi aliyovaa Starmer. Mjadala kuhusu mavazi ya Zelensky ulizidi kupamba moto wakati wa mkutano wa waandishi wa habari. Brian Glenn, mwandishi kutoka Real America’s Voice—chombo cha habari kinachopendelea mrengo wa kulia—alimtupia swali la moja kwa moja: “Kwa nini hauvai suti? Upo katika ofisi ya juu kabisa katika nchi hii, na umegoma kuvaa suti – je, unamiliki hata suti?” Kwa utulivu, Zelensky alijibu kwa mshangao mdogo: “Nitavaa suti vita hivi vitakapomalizika. Labda suti kama yako, labda bora zaidi, au pengine ya bei nafuu kuliko yako,” alisema kwa utani huku akionyesha msimamo wake wa kuendelea kuvaa mavazi ya kijeshi. Swali hilo la Glenn liliibua mjadala mkali mitandaoni. Wengine walimuunga mkono, wakisema kwamba kiongozi wa taifa anapaswa kuvaa mavazi rasmi anapokutana na viongozi wengine, ilhali wengine waliona swali hilo kuwa la dhihaka na lisilo na umuhimu. Miongoni mwa waliomkosoa Glenn ni mwandishi maarufu wa Uingereza, Piers Morgan, ambaye pia ni rafiki wa karibu wa Trump. Morgan aliandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter): “Swali la kipuuzi. Elon Musk havai suti anapoingia Ikulu.” Historia pia inaonyesha kuwa si Zelensky pekee aliyeingia Ikulu ya Marekani bila suti. Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Winston Churchill, alifanya hivyo katika moja ya ziara zake rasmi.
    Like
    Love
    2
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·948 Ansichten
  • PART 3

    Chini ya saa mbili, majengo muhimu ya nchi hii yenye nguvu duniani yalishambuliwa, na kuua karibu watu 3,000 na kujeruhi maelfu kadhaa. Mashambulio haya, ambayo ni mabaya zaidi katika historia ya kisasa, yaliuacha ulimwengu wote kwa mshtuko mkubwa.
    PART 3 Chini ya saa mbili, majengo muhimu ya nchi hii yenye nguvu duniani yalishambuliwa, na kuua karibu watu 3,000 na kujeruhi maelfu kadhaa. Mashambulio haya, ambayo ni mabaya zaidi katika historia ya kisasa, yaliuacha ulimwengu wote kwa mshtuko mkubwa.
    Like
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·739 Ansichten
  • PART 2

    Kwa mara ya pili katika historia yake, Marekani ilikumbwa na shambulio la ndani, hali ambayo ilishuwa wengi wakati Marekani ni mojawapo ya nchi zenye nguvu duniani ambapo ni vigumu kupenya na kufanya shambulizi kubwa kama hilo.
    PART 2 Kwa mara ya pili katika historia yake, Marekani ilikumbwa na shambulio la ndani, hali ambayo ilishuwa wengi wakati Marekani ni mojawapo ya nchi zenye nguvu duniani ambapo ni vigumu kupenya na kufanya shambulizi kubwa kama hilo.
    Like
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·761 Ansichten
  • (B)
    Dr. Harold Frederick Shipman alizaliwa mnamo 1946 huko Nottingham, Uingereza.

    Alikua katika familia yenye maisha ya kawaida, lakini kitu kimoja kilimtofautisha na watoto wengine—upendo wake kwa mama yake.

    Mama yake, Vera, alikuwa kila kitu kwake. Lakini alipofikisha miaka 17, alishuhudia kitu ambacho pengine kingemuumba kuwa mtu wa kutisha zaidi katika historia ya madaktari.

    Mama yake aligunduliwa kuwa na saratani ya mapafu.

    Katika miezi ya mwisho ya ugonjwa wake, alikuwa akipewa dawa za kupunguza maumivu—morphine—na Harold kijana aliona jinsi dawa hizo zilivyomfanya mama yake awe mtulivu kabla ya kufariki.

    Ilikuwa ni tukio lililobadilisha maisha yake.

    Lakini hakuna aliyefikiria kwamba tukio hili lingekuwa chanzo cha wimbi la vifo visivyoelezeka.
    (B) Dr. Harold Frederick Shipman alizaliwa mnamo 1946 huko Nottingham, Uingereza. Alikua katika familia yenye maisha ya kawaida, lakini kitu kimoja kilimtofautisha na watoto wengine—upendo wake kwa mama yake. Mama yake, Vera, alikuwa kila kitu kwake. Lakini alipofikisha miaka 17, alishuhudia kitu ambacho pengine kingemuumba kuwa mtu wa kutisha zaidi katika historia ya madaktari. Mama yake aligunduliwa kuwa na saratani ya mapafu. Katika miezi ya mwisho ya ugonjwa wake, alikuwa akipewa dawa za kupunguza maumivu—morphine—na Harold kijana aliona jinsi dawa hizo zilivyomfanya mama yake awe mtulivu kabla ya kufariki. Ilikuwa ni tukio lililobadilisha maisha yake. Lakini hakuna aliyefikiria kwamba tukio hili lingekuwa chanzo cha wimbi la vifo visivyoelezeka.
    Like
    2
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·1KB Ansichten
  • (A)
    Katika jamii, daktari ni mtu unayemwamini zaidi unapokuwa unaumwa au dhaifu.

    Ni mtu anayeshika maisha yako mikononi mwake na kufanya kila awezalo kuhakikisha unabaki hai.

    But vipi yule unayemtegemea ndio anayekuua taratibu, bila hata wewe kujua?

    Huyu ni Harold Shipman, daktari aliyekuwa muuaji wa kutisha zaidi katika historia ya Uingereza—pengine duniani kote.

    Muuaji hatari aliyejificha kwenye taaluma ya tiba.

    Thread
    (A) Katika jamii, daktari ni mtu unayemwamini zaidi unapokuwa unaumwa au dhaifu. Ni mtu anayeshika maisha yako mikononi mwake na kufanya kila awezalo kuhakikisha unabaki hai. But vipi yule unayemtegemea ndio anayekuua taratibu, bila hata wewe kujua? Huyu ni Harold Shipman, daktari aliyekuwa muuaji wa kutisha zaidi katika historia ya Uingereza—pengine duniani kote. Muuaji hatari aliyejificha kwenye taaluma ya tiba. Thread 🧵
    Like
    Wow
    2
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·1KB Ansichten
  • 6. BONDE LA ELAH

    Bonde hili linajulikana kwa kuandaa moja ya pambano maarufu katika historia.

    Goliathi, jitu la Mfilisti, alitoa changamoto kwa jeshi la Israeli kutuma mtu wa kupigana naye mahali hapa.

    Watu wote wa Sauli walimwogopa yule shujaa mkubwa ambaye alikuwa na urefu wa zaidi ya futi nane. Mchungaji kijana Daudi alisimama na kujitolea kwenda kinyume naye. Jitu lilishindwa na Israeli wakashinda jeshi la Wafilisti.
    6. BONDE LA ELAH Bonde hili linajulikana kwa kuandaa moja ya pambano maarufu katika historia. Goliathi, jitu la Mfilisti, alitoa changamoto kwa jeshi la Israeli kutuma mtu wa kupigana naye mahali hapa. Watu wote wa Sauli walimwogopa yule shujaa mkubwa ambaye alikuwa na urefu wa zaidi ya futi nane. Mchungaji kijana Daudi alisimama na kujitolea kwenda kinyume naye. Jitu lilishindwa na Israeli wakashinda jeshi la Wafilisti.
    0 Kommentare ·0 Anteile ·728 Ansichten
  • Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Nchi ya Uganda (UPDF), Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amesema Uganda inatoa saa (24) vikosi vyote vilivyopo katika Mji wa Bunia Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuacha kuuwa Raia wa kabila la Bahima (ambalo asili yake ni kutoka Nchini Uganda) lasivyo Jeshi lake litashambulia Mji huo.

    Kainerugaba ametoa kauli hiyo Februari 15 katika mtandao wake wa X. Huku akielezwa kuwa na historia ya kuchapisha maoni ya uchochezi kuhusu sera za kigeni mara kwa mara. Alisema ana mamlaka ya Rais Yoweri Museveni, ambaye pia ni Baba yake Mzazi ambako hata hivyo, alipotafutwa Msemaji wa Jeshi la Uganda alisema hawezi kuzungumzia suala hilo.

    Hata hivyo, kabla ya kusasisha ujumbe huo kwenye mtandao wa X, Jenerali huyo alikuwa alieleza bila kutoa ushahidi, kwamba Watu kutoka kabila la Bahima walikuwa wakiuawa huko Nchini DR Congo.

    Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Nchi ya Uganda 🇺🇬 (UPDF), Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amesema Uganda inatoa saa (24) vikosi vyote vilivyopo katika Mji wa Bunia Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 kuacha kuuwa Raia wa kabila la Bahima (ambalo asili yake ni kutoka Nchini Uganda) lasivyo Jeshi lake litashambulia Mji huo. Kainerugaba ametoa kauli hiyo Februari 15 katika mtandao wake wa X. Huku akielezwa kuwa na historia ya kuchapisha maoni ya uchochezi kuhusu sera za kigeni mara kwa mara. Alisema ana mamlaka ya Rais Yoweri Museveni, ambaye pia ni Baba yake Mzazi ambako hata hivyo, alipotafutwa Msemaji wa Jeshi la Uganda alisema hawezi kuzungumzia suala hilo. Hata hivyo, kabla ya kusasisha ujumbe huo kwenye mtandao wa X, Jenerali huyo alikuwa alieleza bila kutoa ushahidi, kwamba Watu kutoka kabila la Bahima walikuwa wakiuawa huko Nchini DR Congo.
    Like
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·751 Ansichten
Suchergebnis