• Rais wa Nchi ya Ukraine , Volodymyr Zelensky, ametabiri kuea Rais wa Urusi , Vladimir Putin, "atakufa hivi karibuni" huku kukiwa na tetesi kuwa afya ya Kiongozi huyo wa Urusi inazorota. Zelensky alitoa kauli hiyo katika mahojiano na Waandishi wa habari Jijini Paris, Ufaransa baada ya kukutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kusema kuwa "Putin atakufa hivi karibuni, na hilo ni jambo la uhakika."

    Picha za Putin zilizochunguzwa kwa muda zimezua uvumi kuhusu hali yake ya afya, hasa baada ya kuonekana na macho mekundu na alama ya ajabu kwenye mkono wake. Aidha, picha zingine zimeonyesha kovu shingoni mwake, likizua dhana kuwa huenda alipitia upasuaji wa saratani ya tezi dume.

    Ripoti za awali zilidai kuwa Putin alikuwa akifuatana mara kwa mara na Daktari bingwa wa saratani, huku uvujaji wa taarifa za kijasusi za Marekani ukionyesha kuwa alikuwa akipokea tiba ya saratani. Sanjari na hayo, amekuwa akionekana akiwa na miguu isiyo imara, akishika meza kwa nguvu, au akitikisa mguu wake mara kwa mara, hali inayoongeza mashaka kuhusu afya yake.

    Rais wa Nchi ya Ukraine 🇺🇦, Volodymyr Zelensky, ametabiri kuea Rais wa Urusi 🇷🇺, Vladimir Putin, "atakufa hivi karibuni" huku kukiwa na tetesi kuwa afya ya Kiongozi huyo wa Urusi inazorota. Zelensky alitoa kauli hiyo katika mahojiano na Waandishi wa habari Jijini Paris, Ufaransa 🇫🇷 baada ya kukutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kusema kuwa "Putin atakufa hivi karibuni, na hilo ni jambo la uhakika." Picha za Putin zilizochunguzwa kwa muda zimezua uvumi kuhusu hali yake ya afya, hasa baada ya kuonekana na macho mekundu na alama ya ajabu kwenye mkono wake. Aidha, picha zingine zimeonyesha kovu shingoni mwake, likizua dhana kuwa huenda alipitia upasuaji wa saratani ya tezi dume. Ripoti za awali zilidai kuwa Putin alikuwa akifuatana mara kwa mara na Daktari bingwa wa saratani, huku uvujaji wa taarifa za kijasusi za Marekani 🇺🇸 ukionyesha kuwa alikuwa akipokea tiba ya saratani. Sanjari na hayo, amekuwa akionekana akiwa na miguu isiyo imara, akishika meza kwa nguvu, au akitikisa mguu wake mara kwa mara, hali inayoongeza mashaka kuhusu afya yake.
    0 Comments ·0 Shares ·83 Views
  • Mchambuzi Farhan JR.

    Nimeona andiko la Waukae @zakazakazi kuhusu TFF kutengeneza Vijana ambalo lilipaswa kuwa jukumu la Klabu na akienda mbali kusema kwamba TFF ndio Shirikisho pekee duniani ambalo lina kituo ambacho kinazalisha na kulea vipaji vya vijana, kwanza kabla ya kupingana nae kuna kitu kwanza nataka kukiweka sawa kwenye eneo hilo.

    Duniani kote Mashirikisho kama TFF yamejikita zaidi kwenye DEVELOPMENT PROJECTS yaani Miradi ya maendeleo kisha wakaachia Mashindano kadhaa yasimamiwe na Bodi zao za Ligi kwa 90% bila kuyaingilia, TFF anachokifanya ni sahihi lakini pia sio sahihi sana kufanya yeye alipaswa kuwa na CLINICS tu ila kuna changamoto sehemu ambayo imeletwa na TFF wenyewe.

    Duniani Klabu zinaweza kuendesha miradi ya Vijana kwasababu kuna kitu kinaitwa FALSAFA ya nchi kwenye mpira, kuanzia mifumo, afya tiba, afya lishe na miundo yote ambayo portifolio hutoka Shirikisho (TFF) Klabu zinaenda kutekeleza mifumo hiyo na kuadjust baadhi ya maeneo halafu Vijana wakienda Clinics za Kitaifa wanaenda kukazia tu.

    Swali linakuja Je Waukaye @zakazakazi FALSAFA ya Tanzania kwenye mpira wa Miguu ni ipi? Iliwasilishwa lini? Anayo nani? Hilo ni Jukumu la TFF ambalo halijatekelezwa, kuna kitu kinaitwa TALENT ID FRAMEWORK ili kupata Vijana je tunayo? Ipoje, anayo nani? Inasemaje? Klabu hazina Mwongozo kutoka kwa TFF? Academy zote nchini zipite humo LAZIMA TFF wafanye wanachoweza, tupo katikati, TFF ASIMAMIE HILO KIKAMILIFU.

    TFF wasiende mbali waende tu hapo Uganda ilipo FUFA, wana Talent ID Framework ambayo Mashirikisho yoote yalipigwa huo Msasa sambamba na Kamati zao tendaji, ndio maana Uganda wapo mbali mno kwenye soka la Vijana kwenye Klabu zao na National Team, kwasababu wana ramani wanaifuata, wameintergrate mfumo wao na FIFA Talent Development Schemes (TDS) je sisi lini tutaforce Klabu zipite humo?

    TFF anajipa majukumu ambayo mengine sio ya kwake, kujadili mikataba ya kibiashara sio Jukumu lake bali Vilabu na Bodi yao, TFF anabaki kama Baba pekee, duniani kote TFF zao zina majukumu yao ukitoa michuano ya FA na Ngao basi Ligi Kuu sio mali yao, TFF ASIMAMIE HASWA JUKUMU LA MAENDELEO NI LAKE.

    Mchambuzi Farhan JR. Nimeona andiko la Waukae @zakazakazi kuhusu TFF kutengeneza Vijana ambalo lilipaswa kuwa jukumu la Klabu na akienda mbali kusema kwamba TFF ndio Shirikisho pekee duniani ambalo lina kituo ambacho kinazalisha na kulea vipaji vya vijana, kwanza kabla ya kupingana nae kuna kitu kwanza nataka kukiweka sawa kwenye eneo hilo. Duniani kote Mashirikisho kama TFF yamejikita zaidi kwenye DEVELOPMENT PROJECTS yaani Miradi ya maendeleo kisha wakaachia Mashindano kadhaa yasimamiwe na Bodi zao za Ligi kwa 90% bila kuyaingilia, TFF anachokifanya ni sahihi lakini pia sio sahihi sana kufanya yeye alipaswa kuwa na CLINICS tu ila kuna changamoto sehemu ambayo imeletwa na TFF wenyewe. Duniani Klabu zinaweza kuendesha miradi ya Vijana kwasababu kuna kitu kinaitwa FALSAFA ya nchi kwenye mpira, kuanzia mifumo, afya tiba, afya lishe na miundo yote ambayo portifolio hutoka Shirikisho (TFF) Klabu zinaenda kutekeleza mifumo hiyo na kuadjust baadhi ya maeneo halafu Vijana wakienda Clinics za Kitaifa wanaenda kukazia tu. Swali linakuja Je Waukaye @zakazakazi FALSAFA ya Tanzania kwenye mpira wa Miguu ni ipi? Iliwasilishwa lini? Anayo nani? Hilo ni Jukumu la TFF ambalo halijatekelezwa, kuna kitu kinaitwa TALENT ID FRAMEWORK ili kupata Vijana je tunayo? Ipoje, anayo nani? Inasemaje? Klabu hazina Mwongozo kutoka kwa TFF? Academy zote nchini zipite humo LAZIMA TFF wafanye wanachoweza, tupo katikati, TFF ASIMAMIE HILO KIKAMILIFU. TFF wasiende mbali waende tu hapo Uganda ilipo FUFA, wana Talent ID Framework ambayo Mashirikisho yoote yalipigwa huo Msasa sambamba na Kamati zao tendaji, ndio maana Uganda wapo mbali mno kwenye soka la Vijana kwenye Klabu zao na National Team, kwasababu wana ramani wanaifuata, wameintergrate mfumo wao na FIFA Talent Development Schemes (TDS) je sisi lini tutaforce Klabu zipite humo? TFF anajipa majukumu ambayo mengine sio ya kwake, kujadili mikataba ya kibiashara sio Jukumu lake bali Vilabu na Bodi yao, TFF anabaki kama Baba pekee, duniani kote TFF zao zina majukumu yao ukitoa michuano ya FA na Ngao basi Ligi Kuu sio mali yao, TFF ASIMAMIE HASWA JUKUMU LA MAENDELEO NI LAKE.
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·164 Views
  • "Msimu uliyopita Zamalek aligomea mechi dhidi ya Al Ahly, Mamlaka za soka nchini Misri zikampa ushindi Al Ahly wa mabao mawili na alama zake tatu kisha wakailima Zamalek alama tatu na timu ikashuka mpaka nafasi ya 12 kama sikosei, Bodi na Chama wala hakikuwaza mara mbili, ni kesi kubwa sana kwenye dunia ya soka kukacha mechi.

    Jana, Al Ahly nae kaleta mbwembwe zile zile za masuala ya Kanuni akagomea mchezo, akasahau kanuni ya kutokea Uwanjani na kucheza mechi ndio kanuni yenye maana zaidi kwenye soka, amejikuta anapoteza alama tatu na mabao matatu kwa Zamalek, Kanuni hii inaweza kusema hivi ila Kanuni nyingine ikawa na maelezo mengine.

    Nikukumbushe tu Al Ahly aliyeadhibiwa ndio Klabu Tajiri zaidi Afrika, Klabu yenye Mashabiki na Wanachama wengi zaidi Afrika, ndio Klabu ya pili kwa Mataji mengi duniani baada ya Real Madrid, ila huko Misri watu hawatazami makunyanzi, ukileta maksudi, Bodi na Chama cha soka zinakufanyia bahati mbaya, Ahly inatajwa pia ina nguvu kubwa sana CAF, sio ya kufikirika ama nadharia ndio uhalisia ila wamepita nayo mapema tu.

    Nawakumbusha tena Watu wangu HAKI huenda na WAJIBU, mfano Tanzania kwa mujibu wa Katiba kuandamana ni haki yako ila unapaswa kutoa taarifa kwa Polisi masaa 72 kabla, umeelewa hapo? Ni haki yako ila huja na Wajibu, Kanuni ili ikulinde hakikisha umetekeleza Wajibu, biashara za Mamlaka za soka duniani ni mpira, kutocheza mpira ni kuzitusi, hazikuachi salama.

    Ni haki yako kuja kufanya mazoezi uwanja wa mechi siku moja kabla ila ni Wajibu wako kunijulisha kuwa nakuja, ili nikuandalie mazingira, huenda narekebisha mfumo wa Umeme? Huenda hali ya usalama sio shwari, huenda nimepulizia dawa za dudu zinaweka kukuathiri, yaani ni HAKI yako ila una WAJIBU wako huu ni mfano tu.

    Mnasemaje Watu wangu wa nchini Yemen haya hayawahusu sana, huko kwenu Kivyenu vyenu Wayemen" - Farhan JR, Mchambuzi.

    "Msimu uliyopita Zamalek aligomea mechi dhidi ya Al Ahly, Mamlaka za soka nchini Misri zikampa ushindi Al Ahly wa mabao mawili na alama zake tatu kisha wakailima Zamalek alama tatu na timu ikashuka mpaka nafasi ya 12 kama sikosei, Bodi na Chama wala hakikuwaza mara mbili, ni kesi kubwa sana kwenye dunia ya soka kukacha mechi. Jana, Al Ahly nae kaleta mbwembwe zile zile za masuala ya Kanuni akagomea mchezo, akasahau kanuni ya kutokea Uwanjani na kucheza mechi ndio kanuni yenye maana zaidi kwenye soka, amejikuta anapoteza alama tatu na mabao matatu kwa Zamalek, Kanuni hii inaweza kusema hivi ila Kanuni nyingine ikawa na maelezo mengine. Nikukumbushe tu Al Ahly aliyeadhibiwa ndio Klabu Tajiri zaidi Afrika, Klabu yenye Mashabiki na Wanachama wengi zaidi Afrika, ndio Klabu ya pili kwa Mataji mengi duniani baada ya Real Madrid, ila huko Misri watu hawatazami makunyanzi, ukileta maksudi, Bodi na Chama cha soka zinakufanyia bahati mbaya, Ahly inatajwa pia ina nguvu kubwa sana CAF, sio ya kufikirika ama nadharia ndio uhalisia ila wamepita nayo mapema tu. Nawakumbusha tena Watu wangu HAKI huenda na WAJIBU, mfano Tanzania kwa mujibu wa Katiba kuandamana ni haki yako ila unapaswa kutoa taarifa kwa Polisi masaa 72 kabla, umeelewa hapo? Ni haki yako ila huja na Wajibu, Kanuni ili ikulinde hakikisha umetekeleza Wajibu, biashara za Mamlaka za soka duniani ni mpira, kutocheza mpira ni kuzitusi, hazikuachi salama. Ni haki yako kuja kufanya mazoezi uwanja wa mechi siku moja kabla ila ni Wajibu wako kunijulisha kuwa nakuja, ili nikuandalie mazingira, huenda narekebisha mfumo wa Umeme? Huenda hali ya usalama sio shwari, huenda nimepulizia dawa za dudu zinaweka kukuathiri, yaani ni HAKI yako ila una WAJIBU wako huu ni mfano tu. Mnasemaje Watu wangu wa nchini Yemen haya hayawahusu sana, huko kwenu Kivyenu vyenu Wayemen😀" - Farhan JR, Mchambuzi.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·241 Views
  • Alhamdulillah MASHALLAH

    napokea iftari kwa AJILI ya ndugu ndugu zetu mayatima wajane mafakir


    Tunaomba swadaka ya kufturisha ndugu waislam wenzetu katika funga hii
    Swadaka ni tiba swadaka ni ibada kubwa zaidi
    ibada

    SUKARI KG 100
    TAMBI
    MCHELE KG 200
    NGANO KG 100

    CHANGIA SADAKA KIDOGO KWA PALE ULIPO BARIKIWA ALLAH ATAKULIPA

    0655987549
    TIGOPESA
    MOZA MOHAMED

    SWADAKA NDIO IBADA KUBWA ZAIDI
    Alhamdulillah MASHALLAH 🤲 napokea iftari kwa AJILI ya ndugu ndugu zetu mayatima wajane mafakir Tunaomba swadaka ya kufturisha ndugu waislam wenzetu katika funga hii Swadaka ni tiba swadaka ni ibada kubwa zaidi ibada SUKARI KG 100 TAMBI MCHELE KG 200 NGANO KG 100 CHANGIA SADAKA KIDOGO KWA PALE ULIPO BARIKIWA ALLAH ATAKULIPA 0655987549 TIGOPESA MOZA MOHAMED SWADAKA NDIO IBADA KUBWA ZAIDI
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·333 Views
  • #SportsElite
    #NBCPREMIERLIGUE
    #Ratibanbc
    #SportsElite #NBCPREMIERLIGUE #Ratibanbc
    Like
    Yay
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·525 Views
  • Issue ya Harold Shipman ilitikisa ulimwengu wa kitabibu.

    Ilizua hofu na maswali mengi—je, kuna wauaji wengine waliyojificha kwenye taaluma ya tiba?

    Serikali ya Uingereza ilibadilisha sheria za matibabu, na hospitali nyingi duniani ziliboresha mifumo yao ili kuhakikisha hakuna daktari mwingine anayeweza kufanya alichofanya Shipman.
    Issue ya Harold Shipman ilitikisa ulimwengu wa kitabibu. Ilizua hofu na maswali mengi—je, kuna wauaji wengine waliyojificha kwenye taaluma ya tiba? Serikali ya Uingereza ilibadilisha sheria za matibabu, na hospitali nyingi duniani ziliboresha mifumo yao ili kuhakikisha hakuna daktari mwingine anayeweza kufanya alichofanya Shipman.
    Like
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·407 Views
  • (A)
    Katika jamii, daktari ni mtu unayemwamini zaidi unapokuwa unaumwa au dhaifu.

    Ni mtu anayeshika maisha yako mikononi mwake na kufanya kila awezalo kuhakikisha unabaki hai.

    But vipi yule unayemtegemea ndio anayekuua taratibu, bila hata wewe kujua?

    Huyu ni Harold Shipman, daktari aliyekuwa muuaji wa kutisha zaidi katika historia ya Uingereza—pengine duniani kote.

    Muuaji hatari aliyejificha kwenye taaluma ya tiba.

    Thread
    (A) Katika jamii, daktari ni mtu unayemwamini zaidi unapokuwa unaumwa au dhaifu. Ni mtu anayeshika maisha yako mikononi mwake na kufanya kila awezalo kuhakikisha unabaki hai. But vipi yule unayemtegemea ndio anayekuua taratibu, bila hata wewe kujua? Huyu ni Harold Shipman, daktari aliyekuwa muuaji wa kutisha zaidi katika historia ya Uingereza—pengine duniani kote. Muuaji hatari aliyejificha kwenye taaluma ya tiba. Thread 🧵
    Like
    Wow
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·469 Views
  • KWENU MNAOJIITA WACHAMBUZI KWA KOFIA ZA USHABIKI NA CHUKI BINAFSI

    kuna kipindi Azam Fc iliwapa wachezaji 5 Simba sports club ili Simba ichukue Ubingwa

    Kuna kipindi kwenye mchezo mmoja Saido ntibanzokiza aliachiwa magoli matano kwenye mechi moja ili Amfikie Fiston kalala Mayele

    Kuna kipindi mchezaji wa Coastal Union alikwepa mpira uliopigwa na saido ili uwe goli

    Mzunguko wa kwanza michezo 2 ya kwanza ya Simba sc dhidi ya Tabora United na Fountain Gate fc wachezaji walifungiwa na kuonekana hawana vibali baada ya wote kucheza na Simba vibali vyao vilikuwepo na walicheza vema na kushinda

    Mzunguko huu wa pili vivyo hivyo Tabora United wachezaji wake Muhimu walikuwa majeruhi na wengine hawakuwa na vibali ila mara tu baada ya kucheza na Simba wachezaji wote walipata vibali na waliokuwa wanaumwa walipona

    Yanga sc ambayo jana imetufunga goli 2 kwa moja ni kikosi hiki hiki kama sikosei ndicho kilichowalamba Tano ni Yanga hii hii ambayo mtoto amezaliwa na amekuwa hajawahi kuona japo Simba ikipata walau Draw dhidi ya yanga kila siku ni vichapo tu

    Nilichogundua mashabiki wengi wa Simba wana wivu sana huwa wanataka wafungwe wao peke yao na Yanga

    Mkiona hapawafai mnaruhusiwa kuhama ligi ila kwa Taarifa za ndaaaaaaani Yanga wamesema popote mtakapohamia na wenyewe watakuja

    Asubuhi mbaya kwenu wabaya wetu
    KWENU MNAOJIITA WACHAMBUZI KWA KOFIA ZA USHABIKI NA CHUKI BINAFSI kuna kipindi Azam Fc iliwapa wachezaji 5 Simba sports club ili Simba ichukue Ubingwa Kuna kipindi kwenye mchezo mmoja Saido ntibanzokiza aliachiwa magoli matano kwenye mechi moja ili Amfikie Fiston kalala Mayele Kuna kipindi mchezaji wa Coastal Union alikwepa mpira uliopigwa na saido ili uwe goli Mzunguko wa kwanza michezo 2 ya kwanza ya Simba sc dhidi ya Tabora United na Fountain Gate fc wachezaji walifungiwa na kuonekana hawana vibali baada ya wote kucheza na Simba vibali vyao vilikuwepo na walicheza vema na kushinda Mzunguko huu wa pili vivyo hivyo Tabora United wachezaji wake Muhimu walikuwa majeruhi na wengine hawakuwa na vibali ila mara tu baada ya kucheza na Simba wachezaji wote walipata vibali na waliokuwa wanaumwa walipona Yanga sc ambayo jana imetufunga goli 2 kwa moja ni kikosi hiki hiki kama sikosei ndicho kilichowalamba Tano ni Yanga hii hii ambayo mtoto amezaliwa na amekuwa hajawahi kuona japo Simba ikipata walau Draw dhidi ya yanga kila siku ni vichapo tu Nilichogundua mashabiki wengi wa Simba wana wivu sana huwa wanataka wafungwe wao peke yao na Yanga Mkiona hapawafai mnaruhusiwa kuhama ligi ila kwa Taarifa za ndaaaaaaani Yanga wamesema popote mtakapohamia na wenyewe watakuja Asubuhi mbaya kwenu wabaya wetu
    0 Comments ·0 Shares ·581 Views
  • Mfalme wa Nchi ya Jordan , Abdullah II amekataa pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump la kutaka kuwahamishia Wapalestina Nchini mwake baada ya mazungumzo na Rais Donald Trump wa Marekani, ambaye alishauri Wakazi wa Gaza wapatao milioni mbili (2) kuondolewa kutoka katika eneo lililoharibiwa na vita.

    Katika mkutano na Rais Trump, Mfalme Abdullah alijitolea kuchukua hadi Watoto 2,000 kutoka Gaza, hasa wale wanaohitaji matibabu ya dharura, ikiwemo Watoto wa saratani. Kupitia mtandao wa X, Mfalme Abdullah alisema, "Msimamo wa Jordan ni msimamo wa pamoja wa mataifa ya Kiarabu."

    Sanjari na hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit, alikosoa pendekezo hilo, akisema kuwa ni lisilokubalika katika ukanda huo, huku Nchi ya China ikisisitiza kuwa Gaza ni ardhi ya Wapalestina.

    Mfalme wa Nchi ya Jordan 🇯🇴, Abdullah II amekataa pendekezo la Rais wa Marekani 🇺🇸 Donald Trump la kutaka kuwahamishia Wapalestina Nchini mwake baada ya mazungumzo na Rais Donald Trump wa Marekani, ambaye alishauri Wakazi wa Gaza wapatao milioni mbili (2) kuondolewa kutoka katika eneo lililoharibiwa na vita. Katika mkutano na Rais Trump, Mfalme Abdullah alijitolea kuchukua hadi Watoto 2,000 kutoka Gaza, hasa wale wanaohitaji matibabu ya dharura, ikiwemo Watoto wa saratani. Kupitia mtandao wa X, Mfalme Abdullah alisema, "Msimamo wa Jordan ni msimamo wa pamoja wa mataifa ya Kiarabu." Sanjari na hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit, alikosoa pendekezo hilo, akisema kuwa ni lisilokubalika katika ukanda huo, huku Nchi ya China 🇨🇳 ikisisitiza kuwa Gaza ni ardhi ya Wapalestina.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·420 Views
  • #PART5

    Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite.

    Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo.

    Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba.

    Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay.

    April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha.

    March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa.

    Kumekua na jitihada mbalimbali za kumaliza mgogoro wa DRC kwa njia za kidiplomasia ikiwemo mkutano wa viongozi wakuu wa SADC na EAC uliofanyika leo jijini Dar.

    #MyaTake:
    1. Congo imeponzwa na ukarimu wake. Wakati wa vita vya Rwanda, Congo ilipokea Watutsi wengi na kuwapa hifadhi, akiwemo Kagame. Baada ya utawala wa Habyarimana kuangushwa Wahutu nao wakakimbilia Congo na kupewa hifadhi. Sasa hicho kimekua kigezo cha Rwanda kuingiza majeshi Congo kila mara kwa madai ya kuwatafuta Wahutu wa FDLR. Kwa lugha rahisi vita ya ndugu wawili (Wahutu na Watutsi) iliyopaswa kupiganwa Rwanda sasa inapiganwa Congo.

    2. Congo inateswa na mipaka ya kikoloni. Laiti wakati wa kuchora mipaka jamii yote ya Watutsi ingewekwa Rwanda, leo kusingekuwa na Banyamulenge Congo, kwahiyo Watutsi wasingepata sababu ya kuishi Congo na kujifanya raia. Ni sawa na kukuta Wamasai 1,000 pale Longido, halafu uambiwe kati yao wapo wa Kenya. Utawajuaje? Utawatofautishaje?

    3. Congo inateswa na rasilimali zake. Kama eneo la Kivu lisingekuwa na utajiri, mgogoro usingekuwa mkubwa kama ulivyo. Rejea #Part1 kujua utajiri uliopo Kivu. Kumbuka bila Kivu dunia haina laptop wala smartphones kwa sababu 80% ya coltan yote duniani inatoka Kivu.

    4. Rwanda na Uganda ni Keyplayers kwenye mgogoro wa Congo. Kwa miaka mingi majeshi yao yameigeuza Congo shamba la bibi. Waondoe majeshi yao Congo.

    5. Viongozi wengi wa M23 ni Wanyarwanda. Huu ni udhibitisho kuwa Rwanda ni kinara kwenye mgogoro huu.

    6. Congo ni kubwa sana na hivyo inakosa jeshi imara la kutosha kulinda mipaka yake yote. Congo ni kubwa mara 90 ya Rwanda. Wapo wanaoshauri igawanywe kama njia ya kutatua mgogoro. Kama ambavyo Yugoslavia iligawanywa na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.

    7. Kiongozi wa sasa wa M23 Corneille Nangaa alikua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi 2019 na ndiye aliyemtangaza Tshisekedi kuwa Rais kwa ushindi wa 38%. Lakini alilaumiwa kupunguza kura za Martin Fayulu aliyepata 34%. Huenda kuna ahadi alipewa haikutimizwa ndio maana akaungana na Waasi.

    Sababu hizo hapo juu zikifanyiwa kazi, mgogoro wa Congo unaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Mnaopenda kujifunza zaidi, naandika Kitabu. Get ready to have your copy. MWISHO.!

    (Malisa GJ )

    #PART5 Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite. Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo. Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba. Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay. April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha. March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa. Kumekua na jitihada mbalimbali za kumaliza mgogoro wa DRC kwa njia za kidiplomasia ikiwemo mkutano wa viongozi wakuu wa SADC na EAC uliofanyika leo jijini Dar. #MyaTake: 1. Congo imeponzwa na ukarimu wake. Wakati wa vita vya Rwanda, Congo ilipokea Watutsi wengi na kuwapa hifadhi, akiwemo Kagame. Baada ya utawala wa Habyarimana kuangushwa Wahutu nao wakakimbilia Congo na kupewa hifadhi. Sasa hicho kimekua kigezo cha Rwanda kuingiza majeshi Congo kila mara kwa madai ya kuwatafuta Wahutu wa FDLR. Kwa lugha rahisi vita ya ndugu wawili (Wahutu na Watutsi) iliyopaswa kupiganwa Rwanda sasa inapiganwa Congo. 2. Congo inateswa na mipaka ya kikoloni. Laiti wakati wa kuchora mipaka jamii yote ya Watutsi ingewekwa Rwanda, leo kusingekuwa na Banyamulenge Congo, kwahiyo Watutsi wasingepata sababu ya kuishi Congo na kujifanya raia. Ni sawa na kukuta Wamasai 1,000 pale Longido, halafu uambiwe kati yao wapo wa Kenya. Utawajuaje? Utawatofautishaje? 3. Congo inateswa na rasilimali zake. Kama eneo la Kivu lisingekuwa na utajiri, mgogoro usingekuwa mkubwa kama ulivyo. Rejea #Part1 kujua utajiri uliopo Kivu. Kumbuka bila Kivu dunia haina laptop wala smartphones kwa sababu 80% ya coltan yote duniani inatoka Kivu. 4. Rwanda na Uganda ni Keyplayers kwenye mgogoro wa Congo. Kwa miaka mingi majeshi yao yameigeuza Congo shamba la bibi. Waondoe majeshi yao Congo. 5. Viongozi wengi wa M23 ni Wanyarwanda. Huu ni udhibitisho kuwa Rwanda ni kinara kwenye mgogoro huu. 6. Congo ni kubwa sana na hivyo inakosa jeshi imara la kutosha kulinda mipaka yake yote. Congo ni kubwa mara 90 ya Rwanda. Wapo wanaoshauri igawanywe kama njia ya kutatua mgogoro. Kama ambavyo Yugoslavia iligawanywa na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe. 7. Kiongozi wa sasa wa M23 Corneille Nangaa alikua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi 2019 na ndiye aliyemtangaza Tshisekedi kuwa Rais kwa ushindi wa 38%. Lakini alilaumiwa kupunguza kura za Martin Fayulu aliyepata 34%. Huenda kuna ahadi alipewa haikutimizwa ndio maana akaungana na Waasi. Sababu hizo hapo juu zikifanyiwa kazi, mgogoro wa Congo unaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Mnaopenda kujifunza zaidi, naandika Kitabu. Get ready to have your copy. MWISHO.! (Malisa GJ ✍️)
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·1K Views
  • #PART12

    Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite.

    Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo.

    Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba.

    Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay.

    April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha.

    March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa.!
    (Malisa GJ)

    #PART12 Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite. Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo. Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba. Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay. April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha. March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa.! (Malisa GJ)
    0 Comments ·0 Shares ·968 Views
  • MADHARA YA KUVUTA SIGARA NA TIBA YAKE
    ✦Magonjwa ya macho
    ✦Kukunjana kwa ngozi
    ✦Magonjwa ya masikio
    ✦Saratani ya ngozi
    ✦Magonjwa ya meno
    ✦Magonjwa ya mapafu,Mifupa,Kucha kungoka kwenye vidole na miguu.
    ✦Magonjwa ya ngozi.

    𝐈𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐰𝐞𝐰𝐞 𝐧𝐢 𝐦𝐮𝐡𝐚𝐧𝐠𝐚 𝐰𝐚 𝐭𝐚𝐭𝐢𝐳𝐨 𝐡𝐢𝐥𝐨 𝐥𝐚 𝐬𝐢𝐠𝐚𝐫𝐚 𝐧𝐚 𝐡𝐚𝐭𝐚 𝐩𝐞𝐦𝐛𝐞,𝐓𝐰𝐚𝐢𝐛 𝐇𝐞𝐫𝐛𝐬 𝐭𝐮𝐧𝐚 𝐬𝐮𝐥𝐮𝐡𝐢𝐬𝐡𝐨 𝐢𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐮𝐧𝐚𝐡𝐢𝐭𝐚𝐣𝐢 𝐤𝐮𝐚𝐜𝐡𝐚 𝐮𝐯𝐮𝐭𝐚𝐣𝐢 𝐰𝐚 𝐚𝐢𝐧𝐚 𝐲𝐨𝐲𝐨𝐭𝐞 𝐧𝐚 𝐩𝐨𝐦𝐛𝐞.

    #𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈𝐀𝐍𝐀_𝐍𝐀𝐒𝐈
    ✦WHATSAP BUSSNESS CATALOGUE
    https://wa.me/c/255767607724

    ✦Instagram:
    https://www.instagram.com/twaibherbs

    ✦Facebook:
    https://www.facebook.com/twaibherbs

    ✦Google/blog.
    https://www.twaibherbs.blogspot.com
    MADHARA YA KUVUTA SIGARA NA TIBA YAKE ✦Magonjwa ya macho ✦Kukunjana kwa ngozi ✦Magonjwa ya masikio ✦Saratani ya ngozi ✦Magonjwa ya meno ✦Magonjwa ya mapafu,Mifupa,Kucha kungoka kwenye vidole na miguu. ✦Magonjwa ya ngozi. 𝐈𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐰𝐞𝐰𝐞 𝐧𝐢 𝐦𝐮𝐡𝐚𝐧𝐠𝐚 𝐰𝐚 𝐭𝐚𝐭𝐢𝐳𝐨 𝐡𝐢𝐥𝐨 𝐥𝐚 𝐬𝐢𝐠𝐚𝐫𝐚 𝐧𝐚 𝐡𝐚𝐭𝐚 𝐩𝐞𝐦𝐛𝐞,𝐓𝐰𝐚𝐢𝐛 𝐇𝐞𝐫𝐛𝐬 𝐭𝐮𝐧𝐚 𝐬𝐮𝐥𝐮𝐡𝐢𝐬𝐡𝐨 𝐢𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐮𝐧𝐚𝐡𝐢𝐭𝐚𝐣𝐢 𝐤𝐮𝐚𝐜𝐡𝐚 𝐮𝐯𝐮𝐭𝐚𝐣𝐢 𝐰𝐚 𝐚𝐢𝐧𝐚 𝐲𝐨𝐲𝐨𝐭𝐞 𝐧𝐚 𝐩𝐨𝐦𝐛𝐞. #𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈𝐀𝐍𝐀_𝐍𝐀𝐒𝐈 ✦WHATSAP BUSSNESS CATALOGUE https://wa.me/c/255767607724 ✦Instagram: https://www.instagram.com/twaibherbs ✦Facebook: https://www.facebook.com/twaibherbs ✦Google/blog. https://www.twaibherbs.blogspot.com
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·590 Views
  • WIKI YA WAZEE WENYE FURAHA.

    PUNGUZA:
    Chumvi.
    Sukari.
    Unga uliokobolewa.
    Bidhaa za maziwa.
    Bidhaa zilizochakatwa.

    VYAKULA VINAVYOHITAJIKA:
    Mboga za majani;
    Mbegu za mikunde;
    Maharage;
    Karanga;
    Mayai;
    Mafuta yaliyosindikwa baridi (Mizeituni, Nazi, …);
    Matunda.

    MAMBO MATATU UNAYOPASWA KUJARIBU KUSAHAU:
    Umri wako.
    Mambo ya zamani.
    Malalamiko yako.

    MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUTHAMINI:
    Familia yako;
    Marafiki zako;
    Mawazo yako chanya;
    Nyumba safi na ya kukaribisha.

    MAMBO MATATU YA MSINGI UNAYOPASWA KUJIFUNZA:
    Daima tabasamu / cheka.
    Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara kwa kasi yako mwenyewe.
    Angalia na kudhibiti uzito wako.

    MTINDO WA MAISHA MUHIMU SITA UNAYOPASWA KUFANYA:
    Usisubiri hadi uwe na kiu kunywa maji.
    Usisubiri hadi uchoke kupumzika.
    Usisubiri hadi uwe mgonjwa kufanya uchunguzi wa matibabu.
    Usisubiri miujiza kumwamini Mungu.
    Usipoteze kamwe kujiamini.
    Kaa chanya na daima tumaini kesho bora.

    KAMA UNA MARAFIKI KATIKA UMRI HUU (47-90 MIAKA), TAFADHALI WATUMIE HII.
    WIKI YA WAZEE WENYE FURAHA.
    WIKI YA WAZEE WENYE FURAHA. PUNGUZA: Chumvi. Sukari. Unga uliokobolewa. Bidhaa za maziwa. Bidhaa zilizochakatwa. VYAKULA VINAVYOHITAJIKA: Mboga za majani; Mbegu za mikunde; Maharage; Karanga; Mayai; Mafuta yaliyosindikwa baridi (Mizeituni, Nazi, …); Matunda. MAMBO MATATU UNAYOPASWA KUJARIBU KUSAHAU: Umri wako. Mambo ya zamani. Malalamiko yako. MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUTHAMINI: Familia yako; Marafiki zako; Mawazo yako chanya; Nyumba safi na ya kukaribisha. MAMBO MATATU YA MSINGI UNAYOPASWA KUJIFUNZA: Daima tabasamu / cheka. Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara kwa kasi yako mwenyewe. Angalia na kudhibiti uzito wako. MTINDO WA MAISHA MUHIMU SITA UNAYOPASWA KUFANYA: Usisubiri hadi uwe na kiu kunywa maji. Usisubiri hadi uchoke kupumzika. Usisubiri hadi uwe mgonjwa kufanya uchunguzi wa matibabu. Usisubiri miujiza kumwamini Mungu. Usipoteze kamwe kujiamini. Kaa chanya na daima tumaini kesho bora. KAMA UNA MARAFIKI KATIKA UMRI HUU (47-90 MIAKA), TAFADHALI WATUMIE HII. WIKI YA WAZEE WENYE FURAHA.
    0 Comments ·0 Shares ·762 Views
  • Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , Félix Tshisekedi na Rais wa Burundi , Evariste Ndayishimiye wamekataa kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioitishwa na Rais wa Kenya , William Ruto, ambao pia ulipangwa kumjumuisha Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye alishasema kuwa yupo tayari kuhudhuria mkutano huo ila kwa kusisitiza, yagusiwe kiini haswa cha ngorongoro uliopo kati ya DR Congo na Waasi.

    Aidha, Tshisekedi amesema kuwa hatoweza kuhudhuria mkutano huo kwa sababu ya ratiba.

    Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩, Félix Tshisekedi na Rais wa Burundi 🇧🇮, Evariste Ndayishimiye wamekataa kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioitishwa na Rais wa Kenya 🇰🇪, William Ruto, ambao pia ulipangwa kumjumuisha Rais wa Rwanda 🇷🇼 Paul Kagame ambaye alishasema kuwa yupo tayari kuhudhuria mkutano huo ila kwa kusisitiza, yagusiwe kiini haswa cha ngorongoro uliopo kati ya DR Congo na Waasi. Aidha, Tshisekedi amesema kuwa hatoweza kuhudhuria mkutano huo kwa sababu ya ratiba.
    0 Comments ·0 Shares ·452 Views
  • Watu mko siriaz na ratiba
    Watu mko siriaz na ratiba🤣🤣
    Haha
    1
    · 1 Comments ·0 Shares ·191 Views
  • Mwaka 2019, Nchini Japan waliweza kupitisha utafiti kwa kuweza kuwaruhusu Wanasayansi kuweza kutengeneza (kuunda) Wanadamu. Mfumo huo ambao unakusanya viungo vya Wanyama na Binadamu ili kuweza kukuza viungo vya Binadamu ndani ya Mnyama kwa njia ya kupandikiza. Watafiti hao wakiongozwa na Mwanasayansi mmoja aitwaye Hiromitsu Nakauchi.

    Utafiti huo unaruhusisha kuingiza "seli" za Binadamu kwenye "viinitete" vya Wanyama (animal embroys) kwa Nguruwe na Panya, ili kuweza kukuza vya Binadamu. Bado kuna wasiwasi wa kimaadili unaweza kujitokeza kuhusu kuchanganya "seli" za kibinadamu na Wanyama haswa kwenye ukuaji wa ubongo.

    Sheria mpya imeruhusu utafiti huo kukuza hadi kuwa Mnyama Binadamu kamili, hivyo kuzua mijadiliano mikali kati ya Sayansi ya matibabu na uumbaji wa Mwenyezi Mungu.

    Mwaka 2019, Nchini Japan 🇯🇵 waliweza kupitisha utafiti kwa kuweza kuwaruhusu Wanasayansi kuweza kutengeneza (kuunda) Wanadamu. Mfumo huo ambao unakusanya viungo vya Wanyama na Binadamu ili kuweza kukuza viungo vya Binadamu ndani ya Mnyama kwa njia ya kupandikiza. Watafiti hao wakiongozwa na Mwanasayansi mmoja aitwaye Hiromitsu Nakauchi. Utafiti huo unaruhusisha kuingiza "seli" za Binadamu kwenye "viinitete" vya Wanyama (animal embroys) kwa Nguruwe na Panya, ili kuweza kukuza vya Binadamu. Bado kuna wasiwasi wa kimaadili unaweza kujitokeza kuhusu kuchanganya "seli" za kibinadamu na Wanyama haswa kwenye ukuaji wa ubongo. Sheria mpya imeruhusu utafiti huo kukuza hadi kuwa Mnyama Binadamu kamili, hivyo kuzua mijadiliano mikali kati ya Sayansi ya matibabu na uumbaji wa Mwenyezi Mungu.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·464 Views
  • Mwaka 2019, Nchini Japan waliweza kupitisha utafiti kwa kuweza kuwaruhusu Wanasayansi kuweza kutengeneza (kuunda) Wanadamu. Mfumo huo ambao unakusanya viungo vya Wanyama na Binadamu ili kuweza kukuza viungo vya Binadamu ndani ya Mnyama kwa njia ya kupandikiza. Watafiti hao wakiongozwa na Mwanasayansi mmoja aitwaye Hiromitsu Nakauchi.

    Utafiti huo unaruhusisha kuingiza "seli" za Binadamu kwenye "viinitete" vya Wanyama (animal embroys) kwa Nguruwe na Panya, ili kuweza kukuza vya Binadamu. Bado kuna wasiwasi wa kimaadili unaweza kujitokeza kuhusu kuchanganya "seli" za kibinadamu na Wanyama haswa kwenye ukuaji wa ubongo.

    Sheria mpya imeruhusu utafiti huo kukuza hadi kuwa Mnyama Binadamu kamili, hivyo kuzua mijadiliano mikali kati ya Sayansi ya matibabu na uumbaji wa Mwenyezi Mungu.

    Mwaka 2019, Nchini Japan 🇯🇵 waliweza kupitisha utafiti kwa kuweza kuwaruhusu Wanasayansi kuweza kutengeneza (kuunda) Wanadamu. Mfumo huo ambao unakusanya viungo vya Wanyama na Binadamu ili kuweza kukuza viungo vya Binadamu ndani ya Mnyama kwa njia ya kupandikiza. Watafiti hao wakiongozwa na Mwanasayansi mmoja aitwaye Hiromitsu Nakauchi. Utafiti huo unaruhusisha kuingiza "seli" za Binadamu kwenye "viinitete" vya Wanyama (animal embroys) kwa Nguruwe na Panya, ili kuweza kukuza vya Binadamu. Bado kuna wasiwasi wa kimaadili unaweza kujitokeza kuhusu kuchanganya "seli" za kibinadamu na Wanyama haswa kwenye ukuaji wa ubongo. Sheria mpya imeruhusu utafiti huo kukuza hadi kuwa Mnyama Binadamu kamili, hivyo kuzua mijadiliano mikali kati ya Sayansi ya matibabu na uumbaji wa Mwenyezi Mungu.
    Like
    Wow
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·435 Views
  • "Natamani kuziona timu zote zinazotoa wachezaji kwenye timu za taifa ziwe zinanufaika na hao wachezaji maana wao ndio wanawatunza hao wachezaji kwa kila kitu na hata mchezaji akiumia timu ya taifa atarudi kwenye klabu yake ili imtibie na wao ndio wanagharamika na hayo matibabu, natakani kuona chama chetu ACA kikipigania hili iwe kama ilivyokuwa kwenye kombe la Dunia pale Qatar kila klabu ilinufaika na wachezaji wao waliokuna timu zao taifa nchini Qatar."

    "Kwa muda mfupi ACA tumepiga kelele angalau hata zile timu ambazo zinazoanzia hatua ya awali na kutolewa kwenye mashindano ya CAF Interclub ziwe zinalipwa sio hadi zifuzu makundi na tumefanikiwa mwaka huu CAF wametoa dollars Elfu 50, tunataka ikiwezekana kila klabu ambayo itakuwa mwanachama wa ACA hata isipocheza haya mashindano ya Afrika iwe inanufaika."- Eng. Hersi Said M/Kiti wa ACA
    "Natamani kuziona timu zote zinazotoa wachezaji kwenye timu za taifa ziwe zinanufaika na hao wachezaji maana wao ndio wanawatunza hao wachezaji kwa kila kitu na hata mchezaji akiumia timu ya taifa atarudi kwenye klabu yake ili imtibie na wao ndio wanagharamika na hayo matibabu, natakani kuona chama chetu ACA kikipigania hili iwe kama ilivyokuwa kwenye kombe la Dunia pale Qatar kila klabu ilinufaika na wachezaji wao waliokuna timu zao taifa nchini Qatar." "Kwa muda mfupi ACA tumepiga kelele angalau hata zile timu ambazo zinazoanzia hatua ya awali na kutolewa kwenye mashindano ya CAF Interclub ziwe zinalipwa sio hadi zifuzu makundi na tumefanikiwa mwaka huu CAF wametoa dollars Elfu 50, tunataka ikiwezekana kila klabu ambayo itakuwa mwanachama wa ACA hata isipocheza haya mashindano ya Afrika iwe inanufaika."- Eng. Hersi Said M/Kiti wa ACA
    Love
    1
    · 1 Comments ·0 Shares ·380 Views
  • "Mimi CAF hawawezi kunifuata kwa sababu nina ratiba ya kuandaa timu kuelekea Robo Fainali, kwahiyo CAF wanaangalia nani hana kazi, ndiyo maana wanamualika yaani Jobless" - Ahmed Ally, Msemaji wa klabu ya Simba SC akijibu swali kuhusu kutokualikwa kwenye droo ya CAF Morocco baada ya Msemaji mwenzie wa klabu ya Yanga SC Ally Kamwe kualikwa.

    "Mimi CAF hawawezi kunifuata kwa sababu nina ratiba ya kuandaa timu kuelekea Robo Fainali, kwahiyo CAF wanaangalia nani hana kazi, ndiyo maana wanamualika yaani Jobless" - Ahmed Ally, Msemaji wa klabu ya Simba SC akijibu swali kuhusu kutokualikwa kwenye droo ya CAF Morocco baada ya Msemaji mwenzie wa klabu ya Yanga SC Ally Kamwe kualikwa.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·419 Views
  • "Mimi CAF hawawezi kunifuata kwa sababu nina ratiba ya kuandaa timu kuelekea Robo Fainali, kwahiyo CAF wanaangalia nani hana kazi, ndiyo maana wanamualika yaani Jobless" - Ahmed Ally, Msemaji wa klabu ya Simba SC akijibu swali kuhusu kutokualikwa kwenye droo ya CAF Morocco baada ya Msemaji mwenzie wa klabu ya Yanga SC Ally Kamwe kualikwa.

    "Mimi CAF hawawezi kunifuata kwa sababu nina ratiba ya kuandaa timu kuelekea Robo Fainali, kwahiyo CAF wanaangalia nani hana kazi, ndiyo maana wanamualika yaani Jobless" - Ahmed Ally, Msemaji wa klabu ya Simba SC akijibu swali kuhusu kutokualikwa kwenye droo ya CAF Morocco baada ya Msemaji mwenzie wa klabu ya Yanga SC Ally Kamwe kualikwa.
    Haha
    Like
    3
    · 1 Comments ·0 Shares ·369 Views
More Results