• Rais wa Rwanda , Paul Kagame amesema kuwa hajui kama Wanajeshi wa Nchi yake wako mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambako mapigano kati ya kundi la Waasi la M23 na Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yanaendelea.

    Rais huyo ameyaomba hayo jana Februari 3, alipohojiwa na Mwandishi Larry Madowo wa CNN aliyetaka kufahamu ikiwa hadi kufikia jana kulikuwa na Vikosi vya kijeshi vya Rwanda Nchini Kongo. Licha ya kuwa Amiri Jeshi Mkuu amesema hajui.

    "Sijui. Ni kweli mimi ni Amiri Jeshi Mkuu ila kuna vitu vingi ambavyo sivifahamu, ila kama utaniuliza kama kuna tatizo Kongo linaloihusu Rwanda na kwamba Rwanda inapaswa kufanya chochote ili kujilinda nitakwambia asilimia mia moja," Paul Kagame, Rais wa Rwanda.

    Majibu ya Kagame yanakuja katika kipindi ambacho sehemu kubwa ya Jumuiya ya kimataifa inaamini kuwa Rwanda inawaunga mkono Waasi wa M23, waliodai kuuteka Mji wa Goma mashariki mwa Kongo wiki iliyopita.

    Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaamini kuwa takribani Wanajeshi 3,000 - 4,000 wa Rwanda wanawasimamia na kuwaunga mkono wapiganaji wa M23 mashariki mwa DR Congo. Ikinukuu Shirika la Afya Ulimwenguni, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu katika ripoti ya Jumatatu ilidai kuwa kufikia tarehe 31 Januari, takribani miili 900 imepatikana kutoka mitaani.

    Rais wa Rwanda 馃嚪馃嚰, Paul Kagame amesema kuwa hajui kama Wanajeshi wa Nchi yake wako mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambako mapigano kati ya kundi la Waasi la M23 na Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 馃嚚馃嚛 yanaendelea. Rais huyo ameyaomba hayo jana Februari 3, alipohojiwa na Mwandishi Larry Madowo wa CNN aliyetaka kufahamu ikiwa hadi kufikia jana kulikuwa na Vikosi vya kijeshi vya Rwanda Nchini Kongo. Licha ya kuwa Amiri Jeshi Mkuu amesema hajui. "Sijui. Ni kweli mimi ni Amiri Jeshi Mkuu ila kuna vitu vingi ambavyo sivifahamu, ila kama utaniuliza kama kuna tatizo Kongo linaloihusu Rwanda na kwamba Rwanda inapaswa kufanya chochote ili kujilinda nitakwambia asilimia mia moja," Paul Kagame, Rais wa Rwanda. Majibu ya Kagame yanakuja katika kipindi ambacho sehemu kubwa ya Jumuiya ya kimataifa inaamini kuwa Rwanda inawaunga mkono Waasi wa M23, waliodai kuuteka Mji wa Goma mashariki mwa Kongo wiki iliyopita. Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaamini kuwa takribani Wanajeshi 3,000 - 4,000 wa Rwanda wanawasimamia na kuwaunga mkono wapiganaji wa M23 mashariki mwa DR Congo. Ikinukuu Shirika la Afya Ulimwenguni, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu katika ripoti ya Jumatatu ilidai kuwa kufikia tarehe 31 Januari, takribani miili 900 imepatikana kutoka mitaani.
    0 Comments 0 Shares 392 Views
  • MAANA YA 'HANSARD' ZA BUNGE

    NENO "Hansard" ni maarufu sana katika shughuli za Bunge nchini Tanzania, na pia katika nchi zote za Jumuiya ya Madola (Commonwealth Countries). Hutamkwa kwa haraka, "han-sadi."

    Maana yake ni Kumbukumbu Rasmi za Majadiliano katika mijadala na hoja kati ya Wabunge na Serikali , ambayo hufanyika ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri.

    Kimsingi, ni mtiririko wa nukuu mbalimbali za hoja za wabunge (ambao ni wawakilishi wa wananchi) na Mawaziri (ambao ni Serikali), katika mijadala yao kwa ruksa ya Spika wa Bunge.

    Ni mtiririko wa nukuu ya majadiliano ya wabunge wakati wote wa vikao vya Bunge la Jamhuri, ambapo kila baada ya vikao husika majadiliano hayo huchapishwa na huhifadhiwa kama kumbukumbu mahsusi, hususan kwa ajili ya matumizi katika kumbukumbu za historia.

    Aidha, Hansard ni jina la heshima kutokana na kazi ya mwandishi na mchapishaji wa nyaraka na vitabu wa nchini Uingereza, Thomas Curson Hansard, ambaye alikuwa mwandishi na mchapishaji wa kwanza wa kumbukumbu za Bunge la Uingereza kule Westminster, mjini London.

    Kutokana na kazi hiyo ya mwandishi huyo, Thomas Hansard, ndipo majadiliano ya wabunge wa Uingereza yakapewa jina la Hansard.

    Hiyo ni kwa vile kila baada ya vikao husika vya wabunge, majadiliano yao yalikuwa tayari yamechapishwa na kusomwa na wao wenyewe, na pia watu wengine, kuhusiana na kile kilichokuwa kinajadiliwa na wabunge ndani ya Bunge.

    PICHA: Thomas Curson Hansard, ambaye alifariki mwaka 1833 akiwa na umri wa miaka 57.
    MAANA YA 'HANSARD' ZA BUNGE NENO "Hansard" ni maarufu sana katika shughuli za Bunge nchini Tanzania, na pia katika nchi zote za Jumuiya ya Madola (Commonwealth Countries). Hutamkwa kwa haraka, "han-sadi." Maana yake ni Kumbukumbu Rasmi za Majadiliano katika mijadala na hoja kati ya Wabunge na Serikali , ambayo hufanyika ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri. Kimsingi, ni mtiririko wa nukuu mbalimbali za hoja za wabunge (ambao ni wawakilishi wa wananchi) na Mawaziri (ambao ni Serikali), katika mijadala yao kwa ruksa ya Spika wa Bunge. Ni mtiririko wa nukuu ya majadiliano ya wabunge wakati wote wa vikao vya Bunge la Jamhuri, ambapo kila baada ya vikao husika majadiliano hayo huchapishwa na huhifadhiwa kama kumbukumbu mahsusi, hususan kwa ajili ya matumizi katika kumbukumbu za historia. Aidha, Hansard ni jina la heshima kutokana na kazi ya mwandishi na mchapishaji wa nyaraka na vitabu wa nchini Uingereza, Thomas Curson Hansard, ambaye alikuwa mwandishi na mchapishaji wa kwanza wa kumbukumbu za Bunge la Uingereza kule Westminster, mjini London. Kutokana na kazi hiyo ya mwandishi huyo, Thomas Hansard, ndipo majadiliano ya wabunge wa Uingereza yakapewa jina la Hansard. Hiyo ni kwa vile kila baada ya vikao husika vya wabunge, majadiliano yao yalikuwa tayari yamechapishwa na kusomwa na wao wenyewe, na pia watu wengine, kuhusiana na kile kilichokuwa kinajadiliwa na wabunge ndani ya Bunge. PICHA: Thomas Curson Hansard, ambaye alifariki mwaka 1833 akiwa na umri wa miaka 57.
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 421 Views
  • BAPHOMET: SANAMU LA SHETANI LILILOLETA UTATA NCHINI MAREKANI.

    Binadamu tangu zama za kale amekuwa akijenga, kuchonga na kuweka sanamu za aina nyingi kwa sababu mbalimbali.
    Baadhi hutumiwa kuwaenzi watu maarufu na kuwakumbuka, na nyingine huabudiwa kama miungu. Kwa muda mrefu hata hivyo imekuwa ni nadra kuona sanamu ambayo moja kwa moja inahusishwa na shetani au ibilisi. Lakini ukifika Marekani, mambo ni tofauti. Kuna sanamu moja kubwa ya shaba ambayo inahusishwa na ushetani. Ni sanamu ya, Baphomet ni kiumbe mwenye kichwa kinachofanana na cha mbuzi lakini ameongezwa maungo ya ajabu. Ni kiumbe mwenye mabawa, na kwenye sanamu hiyo inayotumiwa kwa sasa huoneshwa akiwa na watoto wawili wanaotabasamu.

    Sanamu inayotumiwa kwa sasa ina urefu wa karibu futi 9, na iligharimu $100,000 (£64,000) kuitengeneza. Sanamu hii imekuwa ikitumiwa kuwapiga vita wale walio na imani za Kikristo kiislamu na imani nyingine zenye kumcha Mungu mmoja. Ni sanamu hii ambayo imekuwa ikitumiwa kuendesha vita dhidi ya kuwekwa kwa sanamu za Kikristo na dini nyingine katika majengo maarufu, bustani na maeneo ya umma nchini Marekani. Agosti 17, sanamu hiyo ya kiumbe anayefahamika kama Baphomet ilipelekwa katika jimbo la Arkansas anakotoka Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton. Wanaotumia sanamu hiyo ni watu wa kundi linalofahamika kama Satanic Temple (Hekalu la Shetani) ambalo ni kundi la 'kidini' na kisiasa ambalo hupinga kuingizwa kwa dini katika masuala ya Serikali.

    Kundi hilo liliandaa maandamano ya watu 150 waliyojumuisha waabudu shetani, watu wasioamini Mungu yupo, na Wakristo pia.
    Maandamano hayo yalifanyika nje ya jengo lililo Makao Makuu ya jimbo la Arkansas katika mji wa Little Rock. Walikuwa wamekerwa na hatua ya kuweka sanamu ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu katika uwanja wa Makao Makuu hayo. Satanic Temple walisema sanamu hiyo inakiuka Sheria ya Kwanza ya Marekebisho ya Katiba nchini Marekani ambayo huzungumzia uhuru na haki za kidini. "Ikiwa utakubaliana na kuwepo kwa sanamu ya dini moja basi kunafaa kuwa na uhuru kwa wengine kuweka sanamu za kidini, na ukizuia basi kusiwe na sanamu yoyote ile," mwanzilishi mwenza wa tawi la Satanic Temple katika jimbo la Arkansas, Ivy Forrester, alinukuliwa na wanahabari siku hiyo ya maandamano.

    Ndoto yao ni kuwa na sanamu ya kudumu, lakini siku hiyo hawakuruhusiwa na sheria kuiweka kwa muda mrefu. Kuna sheria ya Arkansas ya mwaka 2017 inayohitaji sanamu ya kuwekwa maeneo ya Serikali iwe na udhamini wa Mbunge ambaye atawasilisha mswada iidhinishwe kupitia Bunge. Sanamu hiyo ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu ilidhaminiwa na mwanasiasa wa Republican, Seneta Jason Rapert. Hata hivyo, chini ya saa 24 baada ya kuwekwa, mwanamume mmoja alivurumisha gari na kuugonga mnara huo na kuubomoa. Maandamano ya Satanic Temple Arkansas yalisababisha kuandaliwa kwa maandamano mengine ya kuwapinga yaliyoandaliwa na makundi ya Kikristo na Wanachama wa Republican. Wakristo walikuwa wamebeba karatasi zilizokuwa na ujumbe kutoka kwenye Biblia. Satanic Temple waliwasilisha ombi la kushirikishwa kwenye kesi ya kupinga mnara huo wa Amri Kumi za Mungu iliyowasilishwa na shirika la haki za kiraia la American Civil Liberties Union, lakini kundi hilo limewasilisha ombi kutaka wasishirikishwe kwenye kesi hiyo.

    Sanamu hiyo ya Baphomet ilizinduliwa mara ya kwanza katika mji wa Detroit, Michigan. Mipango ya kuuweka nje ya Makao Makuu ya jimbo la Oklahoma ambapo kulikuwa kumewekwa mnara mwingine wa Amri Kumi za Mungu mwaka 2015. Mnara huo ulizinduliwa Julai 25 Mwaka huo, ambapo kupitia taarifa yao, Satanic temple walisema: "Tulichagua Baphomet kwa sababu ni kiumbe ambaye huhusishwa na Shetani na maana inayohusishwa naye inafaa sana akiwekwa kando na Sanamu inayowakilisha dini nyingine." Sherehe ya kuizindua ilikuwa ya faragha, na ukumbi uliotumiwa uliwekwa siri kubwa kwani Wakristo walikuwa wameandamana awali kuipinga mjini. Picha zilizopakiwa kwenye Facebook zilionyesha uzinduzi wake ulifanyika karibu na Mto wa Detroit. Kabla ya uzinduzi huo kufanyika, waumini takriban 200 walihudhuria ibada ya misa katika kanisa la St. Joseph mjini humo kupinga sanamu hiyo. Wengine 50 walifanya maombi mjini katika eneo ambalo awali Satanic Temple walikuwa wamepanga kuuzindulia mnara huo hapo.

    Mwanamume yule yule aliyeuharibu mnara wa Arkansas anadaiwa kufanya vivyo hivyo na kuubomoa mnara mwingine kama huo wa Amri Kumi za Mungu nje ya Makao Makuu ya jimbo la Oklahoma.
    Satanic Temple walisitisha juhudi zao za kutaka kuweka sanamu ya Baphomet huko baada ya Mahakama ya Juu ya Oklahoma kuamua kwamba Sanamu ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu ilikuwa imewekwa kinyume cha sheria, hivyo wakawa wameshinda vita bila kupigana. Mahakama ilisema ni kinyume cha sheria kutumia mali ya umma kwa manufaa ya dini yoyote ile.

    Jina hili Baphomet, asili yake ni enzi ya kukomesha uasi katika Kanisa Katoliki katika miaka ya 1100, kwa Kiingereza "Inquisition", na kuteswa kwa wapiganaji wa kidini kwa jina la "Knights Templar" waliokuwa wanateswa ili wafichue siri zao na wakubali kuifuata dini kwa mujibu wa viongozi wa kanisa wa wakati huo. Kwa mujibu wa waandishi wa enzi za vita vya kidini maarufu kama Crusade, wapiganaji hao walikiri kumuabudu Mungu wa wapagani kwa jina la Baphometh.

    Baadhi ya wasomi hata hivyo huamini kwamba "Baphometh" ni upotoshaji wa jina "Mahomet" - ambalo hutumiwa kumrejelea Nabii Muhammad, jambo linalozua utata zaidi. Lakini kadiri miaka ilivyosonga na mafumbo na siri kuhusu Utata wa Knights Templar kuzidi, ndivyo ufafanuzi wa neno hilo na maana yake ulivyozidi kutofautiana. Moja ya tafsiri ya neno hilo inapatikana katika kitabu cha "Da Vinci Code" cha ,Dan Brown, ambapo, neno Baphomet limefafanuliwa na kutafsiriwa kama "Sophia" au busara.

    Picha maarufu zaidi ya Baphomet ilichorwa na mzungu wa Ufaransa aitwaye , Eliphas Levi, mwaka 1856 katika kitabu chake cha Transcendental Magic: Its Doctrine and Ritual. Alichora kiumbe mwenye mabawa na mwenye pembe na mwenge ulio katikati ya pembe hizo kichwani. Kuna mchoro pia wa pembe nane kwenye paji la uso. Mikononi kumeandikwa maneno ya Kilatino SOLVE (tenganishwa) na COAGULA (fungamanisha) - ambazo ni nguvu za kuunganisha na kutenganisha ambazo zilitwaliwa kutoka kwa Mungu. Mchoro wa Levi ulihamasisha zaidi sanamu inayotumiwa na Satanic Temple.

    Ni jinsia mbili kwa pamoja, nusu mnyama na nusu binadamu.anapiga saluti ya vidole viwili Sanamu hiyo ina vidole viwili vilivyoelekezwa juu mkono wa kulia na viwili vinavyoelekezwa chini mkono wa kushoto, maana yake "kama ilivyo juu, na chini iwe pia". Maneno hayo na ishara hiyo ya vidole ni maarufu miongoni mwa wenye kuamini katika mizungu na mafumbo. Chanzo chake ni kazi za kale za msomi Hermes Trismegistus, ambaye vitabu vyake vilikuwa maarufu sana enzi ya Kipindi cha mwamko wa sanaa na mageuzi ya kidini, maarufu kama "Renaissance and Reformation" barani Ulaya. Maneno hayo pia hutumiwa kuhusiana na sayansi, vitu vyote na Mungu, lakini Levi aliandika kwamba kwa kutumia ishara hiyo, Baphomet wake alikuwa anaashiria kuwiana sawa kwa fadhila na haki. Lakini maana yake halisi ni kwamba ,shetani anatawala duniani na Mungu anatawala juu.

    Lucien Greaves, msemaji wa Satanic Temple anasema "lengo lao ni kwamba watoto watatazama kazi hiyo ya sanaa kama kwa usalama, ni sanamu isiyofaa kuzua wasiwasi wowote. "Sura ya mbuzi huyo haioneshi chochote. Si ya kishetani wala ya kutisha - kama wanavyodai baadhi ya watu - ukiitazama bila kuongozwa na mzigo wa utamaduni."
    "Sifikiri watoto wanaokutana na sanamu hii watatiwa hofu na propaganda wanaweza wasione chochote cha kuwatia wasiwasi," anasema Greaves. "Lakini si kwamba tunapinga kuwaingiza watoto kwenye mitazamo ya kidini. Mara nyingi watoto hulazimishwa kuingia kwenye dini. Hilo ni jambo hatutaki kulifanya kamwe."

    Kwenye tumbo la Baphomet kuna ishara ya kale ya Kigiriki ya nyoka wawili walio kwenye fimbo - fimbo ambayo ilibebwa na Hermes na maafisa wa kueneza matangazo au kutoa matangazo rasmi waliotumiwa kutoa matamko rasmi. Ishara hiyo kwenye sanamu hiyo inaashiria biashara, mashauriano na kutendeana, na iliingizwa kwenye Baphomet na Levi. "Kwetu ni ishara ya maridhiano ya vitu viwili tofauti - kwa mfano kuwa na sanamu ya Kishetani karibu na sanamu ya Kikristo," anasema Greaves. "Tunafikiri ni ujumbe wenye nguvu sana kuwa na sanamu hii ikiwa karibu na sanamu ya Amri Kumi za Mungu. Unaweza kuwa na mambo mawili tofauti kwa pamoja bila mzozo." Baphomet wa Levi alikuwa ni mwenye maziwa, lakini "tuliyaondoa maziwa hayo" anasema Greaves. Anasema hatukutaka wajipachike kwenye mdahalo kuhusu jinsia ya kiumbe huyo wao jambo ambalo lingewafanya watu kupoteza maana halisi. Badala yake anasema watoto wawili, mvulana na msichana, ndio wanaowakilisha jinsia. Kwa maana iliyojificha Greaves anashindwa kusema kwamba watoto hao wawili wa kike na kiume wanawakilisha ulimwengu wote na hawa ni Adam na Hawa,

    Kwenye paji la uso la Baphomet na kwenye kiti cha enzi alichokikalia kuna mchoro wa nyota ya pembe tano, ishara ambayo mara nyingi hutambuliwa kama ishara ya shetani. Mara nyingi huonekana ikiwa imepinduliwa. Msalaba wa Peter pia hupinduliwa. Greaves anasema lengo lao ni kuwafanya watu wabadilishe mtazamo wao na kuacha kuongozwa na waliyofunzwa na utamaduni wao. Waangazie mambo kwa kuzingatia ushahidi uliopo. Anasema mtazamo huo huwazuia watu kuchukua msimamo huru kuhusu masuala kama vile ndoa za wapenzi wa jinsia moja na haki za kutoa mimba pamoja na huduma nyingine za uzazi wa mpango. "Mwenge wa maarifa ndio kama upembe wa kati na inatukuza juhudi za kutafuta elimu na maarifa. Tunathamini hilo sana," anasema Greaves.

    Levi mwenyewe aliandika kwamba mwenge wa maarifa uolikuwa unawaka katikati ya pembe za Baphomet ni mwanga wa kusawazisha vitu vyote. Ni taswira ya roho iliyo juu ya vitu vyote vinavyoonekana, kama zilivyo ndimi za moto, ingawa bado imeunganishwa na vitu hivyo, mfano moto unavyoendelea kung'aa juu ya mafuta au kijiti. Kulikuwa na mpango wa kuongeza maandiko kwenye mchoro wa nyota ya pembe tano ya moja ya nguzo saba kuu za Satanic Temple: "moyo wa huruma, busara na haki unafaa daima kuongoza zaidi ya neno lililoandikwa au kutamkwa." Nyuma ya sanamu hiyo, kutakuwa na nukuu kutoka kwa kitabu cha Cain chake Lord Byron unaosema: "Kisha, nani alikuwa Ibilisi? Yule hangekuruhusu wewe uishi milele, au yule ambaye angelikuumba uishi milele, katika raha na nguvu za elimu na maarifa?"

    Kwa mujibu wa tovuti yao Satanic Temple wanaamini kwamba "kimsingi watu kuteseka au kuumia ni vibaya, na chochote kile kinachopunguza madhila na mateso ni kizuri." Hawaamini katika kutenda mabaya. Wanasema: "Huwa tunakumbatia kukufuru kama njia halali ya kujieleza na kuonyesha uhuru wa mtu binafsi dhidi ya imani za kitamaduni zisizo na tija." "Msimamo wa Satanic Temple ni kwamba dini inaweza, na inafaa kutenganishwa na ushirikina. Hivyo basi, huwa hawaendelezi imani katika Shetani binafsi. "Kukumbatia jina la Shetani ni kukumbatia mtazamo wa kutumia fikira na kujiondoa kutoka katika mfumo wa kuamini katika nguvu za kipekee za kutoka nje ya dunia na utamaduni uliopitwa na wakati wenye msingi wake katika ushirikina."
    BAPHOMET: SANAMU LA SHETANI LILILOLETA UTATA NCHINI MAREKANI. Binadamu tangu zama za kale amekuwa akijenga, kuchonga na kuweka sanamu za aina nyingi kwa sababu mbalimbali. Baadhi hutumiwa kuwaenzi watu maarufu na kuwakumbuka, na nyingine huabudiwa kama miungu. Kwa muda mrefu hata hivyo imekuwa ni nadra kuona sanamu ambayo moja kwa moja inahusishwa na shetani au ibilisi. Lakini ukifika Marekani, mambo ni tofauti. Kuna sanamu moja kubwa ya shaba ambayo inahusishwa na ushetani. Ni sanamu ya, Baphomet ni kiumbe mwenye kichwa kinachofanana na cha mbuzi lakini ameongezwa maungo ya ajabu. Ni kiumbe mwenye mabawa, na kwenye sanamu hiyo inayotumiwa kwa sasa huoneshwa akiwa na watoto wawili wanaotabasamu. Sanamu inayotumiwa kwa sasa ina urefu wa karibu futi 9, na iligharimu $100,000 (£64,000) kuitengeneza. Sanamu hii imekuwa ikitumiwa kuwapiga vita wale walio na imani za Kikristo kiislamu na imani nyingine zenye kumcha Mungu mmoja. Ni sanamu hii ambayo imekuwa ikitumiwa kuendesha vita dhidi ya kuwekwa kwa sanamu za Kikristo na dini nyingine katika majengo maarufu, bustani na maeneo ya umma nchini Marekani. Agosti 17, sanamu hiyo ya kiumbe anayefahamika kama Baphomet ilipelekwa katika jimbo la Arkansas anakotoka Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton. Wanaotumia sanamu hiyo ni watu wa kundi linalofahamika kama Satanic Temple (Hekalu la Shetani) ambalo ni kundi la 'kidini' na kisiasa ambalo hupinga kuingizwa kwa dini katika masuala ya Serikali. Kundi hilo liliandaa maandamano ya watu 150 waliyojumuisha waabudu shetani, watu wasioamini Mungu yupo, na Wakristo pia. Maandamano hayo yalifanyika nje ya jengo lililo Makao Makuu ya jimbo la Arkansas katika mji wa Little Rock. Walikuwa wamekerwa na hatua ya kuweka sanamu ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu katika uwanja wa Makao Makuu hayo. Satanic Temple walisema sanamu hiyo inakiuka Sheria ya Kwanza ya Marekebisho ya Katiba nchini Marekani ambayo huzungumzia uhuru na haki za kidini. "Ikiwa utakubaliana na kuwepo kwa sanamu ya dini moja basi kunafaa kuwa na uhuru kwa wengine kuweka sanamu za kidini, na ukizuia basi kusiwe na sanamu yoyote ile," mwanzilishi mwenza wa tawi la Satanic Temple katika jimbo la Arkansas, Ivy Forrester, alinukuliwa na wanahabari siku hiyo ya maandamano. Ndoto yao ni kuwa na sanamu ya kudumu, lakini siku hiyo hawakuruhusiwa na sheria kuiweka kwa muda mrefu. Kuna sheria ya Arkansas ya mwaka 2017 inayohitaji sanamu ya kuwekwa maeneo ya Serikali iwe na udhamini wa Mbunge ambaye atawasilisha mswada iidhinishwe kupitia Bunge. Sanamu hiyo ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu ilidhaminiwa na mwanasiasa wa Republican, Seneta Jason Rapert. Hata hivyo, chini ya saa 24 baada ya kuwekwa, mwanamume mmoja alivurumisha gari na kuugonga mnara huo na kuubomoa. Maandamano ya Satanic Temple Arkansas yalisababisha kuandaliwa kwa maandamano mengine ya kuwapinga yaliyoandaliwa na makundi ya Kikristo na Wanachama wa Republican. Wakristo walikuwa wamebeba karatasi zilizokuwa na ujumbe kutoka kwenye Biblia. Satanic Temple waliwasilisha ombi la kushirikishwa kwenye kesi ya kupinga mnara huo wa Amri Kumi za Mungu iliyowasilishwa na shirika la haki za kiraia la American Civil Liberties Union, lakini kundi hilo limewasilisha ombi kutaka wasishirikishwe kwenye kesi hiyo. Sanamu hiyo ya Baphomet ilizinduliwa mara ya kwanza katika mji wa Detroit, Michigan. Mipango ya kuuweka nje ya Makao Makuu ya jimbo la Oklahoma ambapo kulikuwa kumewekwa mnara mwingine wa Amri Kumi za Mungu mwaka 2015. Mnara huo ulizinduliwa Julai 25 Mwaka huo, ambapo kupitia taarifa yao, Satanic temple walisema: "Tulichagua Baphomet kwa sababu ni kiumbe ambaye huhusishwa na Shetani na maana inayohusishwa naye inafaa sana akiwekwa kando na Sanamu inayowakilisha dini nyingine." Sherehe ya kuizindua ilikuwa ya faragha, na ukumbi uliotumiwa uliwekwa siri kubwa kwani Wakristo walikuwa wameandamana awali kuipinga mjini. Picha zilizopakiwa kwenye Facebook zilionyesha uzinduzi wake ulifanyika karibu na Mto wa Detroit. Kabla ya uzinduzi huo kufanyika, waumini takriban 200 walihudhuria ibada ya misa katika kanisa la St. Joseph mjini humo kupinga sanamu hiyo. Wengine 50 walifanya maombi mjini katika eneo ambalo awali Satanic Temple walikuwa wamepanga kuuzindulia mnara huo hapo. Mwanamume yule yule aliyeuharibu mnara wa Arkansas anadaiwa kufanya vivyo hivyo na kuubomoa mnara mwingine kama huo wa Amri Kumi za Mungu nje ya Makao Makuu ya jimbo la Oklahoma. Satanic Temple walisitisha juhudi zao za kutaka kuweka sanamu ya Baphomet huko baada ya Mahakama ya Juu ya Oklahoma kuamua kwamba Sanamu ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu ilikuwa imewekwa kinyume cha sheria, hivyo wakawa wameshinda vita bila kupigana. Mahakama ilisema ni kinyume cha sheria kutumia mali ya umma kwa manufaa ya dini yoyote ile. Jina hili Baphomet, asili yake ni enzi ya kukomesha uasi katika Kanisa Katoliki katika miaka ya 1100, kwa Kiingereza "Inquisition", na kuteswa kwa wapiganaji wa kidini kwa jina la "Knights Templar" waliokuwa wanateswa ili wafichue siri zao na wakubali kuifuata dini kwa mujibu wa viongozi wa kanisa wa wakati huo. Kwa mujibu wa waandishi wa enzi za vita vya kidini maarufu kama Crusade, wapiganaji hao walikiri kumuabudu Mungu wa wapagani kwa jina la Baphometh. Baadhi ya wasomi hata hivyo huamini kwamba "Baphometh" ni upotoshaji wa jina "Mahomet" - ambalo hutumiwa kumrejelea Nabii Muhammad, jambo linalozua utata zaidi. Lakini kadiri miaka ilivyosonga na mafumbo na siri kuhusu Utata wa Knights Templar kuzidi, ndivyo ufafanuzi wa neno hilo na maana yake ulivyozidi kutofautiana. Moja ya tafsiri ya neno hilo inapatikana katika kitabu cha "Da Vinci Code" cha ,Dan Brown, ambapo, neno Baphomet limefafanuliwa na kutafsiriwa kama "Sophia" au busara. Picha maarufu zaidi ya Baphomet ilichorwa na mzungu wa Ufaransa aitwaye , Eliphas Levi, mwaka 1856 katika kitabu chake cha Transcendental Magic: Its Doctrine and Ritual. Alichora kiumbe mwenye mabawa na mwenye pembe na mwenge ulio katikati ya pembe hizo kichwani. Kuna mchoro pia wa pembe nane kwenye paji la uso. Mikononi kumeandikwa maneno ya Kilatino SOLVE (tenganishwa) na COAGULA (fungamanisha) - ambazo ni nguvu za kuunganisha na kutenganisha ambazo zilitwaliwa kutoka kwa Mungu. Mchoro wa Levi ulihamasisha zaidi sanamu inayotumiwa na Satanic Temple. Ni jinsia mbili kwa pamoja, nusu mnyama na nusu binadamu.anapiga saluti ya vidole viwili Sanamu hiyo ina vidole viwili vilivyoelekezwa juu mkono wa kulia na viwili vinavyoelekezwa chini mkono wa kushoto, maana yake "kama ilivyo juu, na chini iwe pia". Maneno hayo na ishara hiyo ya vidole ni maarufu miongoni mwa wenye kuamini katika mizungu na mafumbo. Chanzo chake ni kazi za kale za msomi Hermes Trismegistus, ambaye vitabu vyake vilikuwa maarufu sana enzi ya Kipindi cha mwamko wa sanaa na mageuzi ya kidini, maarufu kama "Renaissance and Reformation" barani Ulaya. Maneno hayo pia hutumiwa kuhusiana na sayansi, vitu vyote na Mungu, lakini Levi aliandika kwamba kwa kutumia ishara hiyo, Baphomet wake alikuwa anaashiria kuwiana sawa kwa fadhila na haki. Lakini maana yake halisi ni kwamba ,shetani anatawala duniani na Mungu anatawala juu. Lucien Greaves, msemaji wa Satanic Temple anasema "lengo lao ni kwamba watoto watatazama kazi hiyo ya sanaa kama kwa usalama, ni sanamu isiyofaa kuzua wasiwasi wowote. "Sura ya mbuzi huyo haioneshi chochote. Si ya kishetani wala ya kutisha - kama wanavyodai baadhi ya watu - ukiitazama bila kuongozwa na mzigo wa utamaduni." "Sifikiri watoto wanaokutana na sanamu hii watatiwa hofu na propaganda wanaweza wasione chochote cha kuwatia wasiwasi," anasema Greaves. "Lakini si kwamba tunapinga kuwaingiza watoto kwenye mitazamo ya kidini. Mara nyingi watoto hulazimishwa kuingia kwenye dini. Hilo ni jambo hatutaki kulifanya kamwe." Kwenye tumbo la Baphomet kuna ishara ya kale ya Kigiriki ya nyoka wawili walio kwenye fimbo - fimbo ambayo ilibebwa na Hermes na maafisa wa kueneza matangazo au kutoa matangazo rasmi waliotumiwa kutoa matamko rasmi. Ishara hiyo kwenye sanamu hiyo inaashiria biashara, mashauriano na kutendeana, na iliingizwa kwenye Baphomet na Levi. "Kwetu ni ishara ya maridhiano ya vitu viwili tofauti - kwa mfano kuwa na sanamu ya Kishetani karibu na sanamu ya Kikristo," anasema Greaves. "Tunafikiri ni ujumbe wenye nguvu sana kuwa na sanamu hii ikiwa karibu na sanamu ya Amri Kumi za Mungu. Unaweza kuwa na mambo mawili tofauti kwa pamoja bila mzozo." Baphomet wa Levi alikuwa ni mwenye maziwa, lakini "tuliyaondoa maziwa hayo" anasema Greaves. Anasema hatukutaka wajipachike kwenye mdahalo kuhusu jinsia ya kiumbe huyo wao jambo ambalo lingewafanya watu kupoteza maana halisi. Badala yake anasema watoto wawili, mvulana na msichana, ndio wanaowakilisha jinsia. Kwa maana iliyojificha Greaves anashindwa kusema kwamba watoto hao wawili wa kike na kiume wanawakilisha ulimwengu wote na hawa ni Adam na Hawa, Kwenye paji la uso la Baphomet na kwenye kiti cha enzi alichokikalia kuna mchoro wa nyota ya pembe tano, ishara ambayo mara nyingi hutambuliwa kama ishara ya shetani. Mara nyingi huonekana ikiwa imepinduliwa. Msalaba wa Peter pia hupinduliwa. Greaves anasema lengo lao ni kuwafanya watu wabadilishe mtazamo wao na kuacha kuongozwa na waliyofunzwa na utamaduni wao. Waangazie mambo kwa kuzingatia ushahidi uliopo. Anasema mtazamo huo huwazuia watu kuchukua msimamo huru kuhusu masuala kama vile ndoa za wapenzi wa jinsia moja na haki za kutoa mimba pamoja na huduma nyingine za uzazi wa mpango. "Mwenge wa maarifa ndio kama upembe wa kati na inatukuza juhudi za kutafuta elimu na maarifa. Tunathamini hilo sana," anasema Greaves. Levi mwenyewe aliandika kwamba mwenge wa maarifa uolikuwa unawaka katikati ya pembe za Baphomet ni mwanga wa kusawazisha vitu vyote. Ni taswira ya roho iliyo juu ya vitu vyote vinavyoonekana, kama zilivyo ndimi za moto, ingawa bado imeunganishwa na vitu hivyo, mfano moto unavyoendelea kung'aa juu ya mafuta au kijiti. Kulikuwa na mpango wa kuongeza maandiko kwenye mchoro wa nyota ya pembe tano ya moja ya nguzo saba kuu za Satanic Temple: "moyo wa huruma, busara na haki unafaa daima kuongoza zaidi ya neno lililoandikwa au kutamkwa." Nyuma ya sanamu hiyo, kutakuwa na nukuu kutoka kwa kitabu cha Cain chake Lord Byron unaosema: "Kisha, nani alikuwa Ibilisi? Yule hangekuruhusu wewe uishi milele, au yule ambaye angelikuumba uishi milele, katika raha na nguvu za elimu na maarifa?" Kwa mujibu wa tovuti yao Satanic Temple wanaamini kwamba "kimsingi watu kuteseka au kuumia ni vibaya, na chochote kile kinachopunguza madhila na mateso ni kizuri." Hawaamini katika kutenda mabaya. Wanasema: "Huwa tunakumbatia kukufuru kama njia halali ya kujieleza na kuonyesha uhuru wa mtu binafsi dhidi ya imani za kitamaduni zisizo na tija." "Msimamo wa Satanic Temple ni kwamba dini inaweza, na inafaa kutenganishwa na ushirikina. Hivyo basi, huwa hawaendelezi imani katika Shetani binafsi. "Kukumbatia jina la Shetani ni kukumbatia mtazamo wa kutumia fikira na kujiondoa kutoka katika mfumo wa kuamini katika nguvu za kipekee za kutoka nje ya dunia na utamaduni uliopitwa na wakati wenye msingi wake katika ushirikina."
    0 Comments 0 Shares 914 Views
  • #jewajua
    -
    LILITH -
    Kadri Ya Masimulizi Ya Jewish Yana Eleza Lilith Ali Kuwa Mke Wa Kwanza Wa Adam,
    Simulizi Inasema Adam Na Lilith Wali umbwa Siku Moja Na Waliishi Pamoja Eden. -

    Lakini Lilith Alikuwa Mwanamke Jeuri Sana., ali kuwa Hana Heshima Kwa Adam, alikuwa ana taka haki sawa (Wanao Amini Hadithi Hii Wana Dai Lilith Ndio chanzo cha wanawake kudai haki sawa). -

    Maisha Ya Eden Yali kuwa Ya Manyanyaso Sana kwa Adam, Adam Alikua Ana lalamika sana kwa Mungu, Mwisho Lilith Ali mtoroka Adam pale Eden Na Kwenda Huko mbali. -

    Kuondoka Kwa Lilith kuli mfanya Adam Aishi kwa mawazo na kukosa Raha, Hadithi ina simulia Mwenyezi Mungu Ali Watuma Mara kadhaa Malaika Waka mrudishe Lilith lakini haku taka kurudi (Chanzo cha kiburi). -

    Mara Baada ya siku nyingi kupita Huku Adam akionekana mwenye mawazo ndipo ali muumba Eva kutoka kwenye ubavu wa Adam (Sababu za kumuumba kutoka kwenye ubavu ili hasiwe Jeuri kama Lilith). -

    Waliishi maisha ya furaha sana pale Eden, LILITH Ali ingiwa na wivu huko alipo kuwa (Wanao Amini Hadithi Hii Wana sema ndo chanzo cha wanawake kuwa na wivu) Lilith Ali jibadilisha na kuwa nyoka na kwenda kumdanganya Eva ale Tunda. -

    Kilicho fuata kila mtu ana fahamu... Baada ya Lilith kufanya hayo Mungu ali mtuma malaika Mikael aka mfulumushe Lilith, Basi Lilith Ali Pata kichapo kimoja kizito sana, Lilith Ali sukumiwa makonde mazito, Basi Lilith Ali fyekelewa mbali na kukimbilia kusiko julikana. -

    Nime eleza kwa Kifupi sana ili kutoa tu Muongozo, kuna mengi nime acha, Kuna kitabu kinaitwa DEMON LILITH kina maelezo mengi na Wana husianisha na uumbaji unao 0ngelewa kwenye kitabu cha mwanzo yaani Wana Nukuu vifungu. -
    Mimi Nahisi hii ni simulizi ya kuonyesha jinsi shetani alivyo kwa upande wangu nasoma ili kujifunza tu. -

    Kwenye hadithi Kuna mabaya mengi sana kafanya Lilith kwa mfano kuuwa watoto wadogo wengi sana, Ni Vizuri Uka Pata kitabu uka soma. -

    Nini Maoni yako kuhusu Lilith?
    .
    .
    .
    .
    .
    #jewajua - LILITH - Kadri Ya Masimulizi Ya Jewish Yana Eleza Lilith Ali Kuwa Mke Wa Kwanza Wa Adam, Simulizi Inasema Adam Na Lilith Wali umbwa Siku Moja Na Waliishi Pamoja Eden. - Lakini Lilith Alikuwa Mwanamke Jeuri Sana., ali kuwa Hana Heshima Kwa Adam, alikuwa ana taka haki sawa (Wanao Amini Hadithi Hii Wana Dai Lilith Ndio chanzo cha wanawake kudai haki sawa). - Maisha Ya Eden Yali kuwa Ya Manyanyaso Sana kwa Adam, Adam Alikua Ana lalamika sana kwa Mungu, Mwisho Lilith Ali mtoroka Adam pale Eden Na Kwenda Huko mbali. - Kuondoka Kwa Lilith kuli mfanya Adam Aishi kwa mawazo na kukosa Raha, Hadithi ina simulia Mwenyezi Mungu Ali Watuma Mara kadhaa Malaika Waka mrudishe Lilith lakini haku taka kurudi (Chanzo cha kiburi). - Mara Baada ya siku nyingi kupita Huku Adam akionekana mwenye mawazo ndipo ali muumba Eva kutoka kwenye ubavu wa Adam (Sababu za kumuumba kutoka kwenye ubavu ili hasiwe Jeuri kama Lilith). - Waliishi maisha ya furaha sana pale Eden, LILITH Ali ingiwa na wivu huko alipo kuwa (Wanao Amini Hadithi Hii Wana sema ndo chanzo cha wanawake kuwa na wivu) Lilith Ali jibadilisha na kuwa nyoka na kwenda kumdanganya Eva ale Tunda. - Kilicho fuata kila mtu ana fahamu... Baada ya Lilith kufanya hayo Mungu ali mtuma malaika Mikael aka mfulumushe Lilith, Basi Lilith Ali Pata kichapo kimoja kizito sana, Lilith Ali sukumiwa makonde mazito, Basi Lilith Ali fyekelewa mbali na kukimbilia kusiko julikana. - Nime eleza kwa Kifupi sana ili kutoa tu Muongozo, kuna mengi nime acha, Kuna kitabu kinaitwa DEMON LILITH kina maelezo mengi na Wana husianisha na uumbaji unao 0ngelewa kwenye kitabu cha mwanzo yaani Wana Nukuu vifungu. - Mimi Nahisi hii ni simulizi ya kuonyesha jinsi shetani alivyo kwa upande wangu nasoma ili kujifunza tu. - Kwenye hadithi Kuna mabaya mengi sana kafanya Lilith kwa mfano kuuwa watoto wadogo wengi sana, Ni Vizuri Uka Pata kitabu uka soma. - Nini Maoni yako kuhusu Lilith? . . . . .
    0 Comments 0 Shares 635 Views
  • Maisha sio mbio ya kushindana na wengine, bali ni safari ya kugundua uwezo wako na kufikia malengo yako kwa wakati unaofaa

    Furahia kila hatua, jifunze kutokana na kila uzoefu na endelea kusonga mbele kwa matumaini na moyo thabiti huku ukikumbuka kwamba changamoto ni sehemu ya maisha na zinatufanya kuwa imara zaidi

    #JamiiForums

    #Manukuu ya JF

    #Maisha

    #Nukuu ya Asubuhi
    Maisha sio mbio ya kushindana na wengine, bali ni safari ya kugundua uwezo wako na kufikia malengo yako kwa wakati unaofaa Furahia kila hatua, jifunze kutokana na kila uzoefu na endelea kusonga mbele kwa matumaini na moyo thabiti huku ukikumbuka kwamba changamoto ni sehemu ya maisha na zinatufanya kuwa imara zaidi #JamiiForums #Manukuu ya JF #Maisha #Nukuu ya Asubuhi
    Like
    Love
    2
    0 Comments 0 Shares 486 Views
  • FADLU NI KOCHA WA KISASA HANA KIKOSI CHA KWANZA.

    Nimemnukuu mchambuzi na mtangazaji mahari wa kabumbu nchini Nazareth Upete kupitia kipindi cha Bao la Asubuhi, amesema makocha wengi wa kisasa Duniani hawana First Eleven yaani kikosi cha kwanza.

    Hili linaangukia kwa kocha mkuu wa klabu ya Simba Fadlu Davids, ambaye amekuwa hatabiriki katika kikosi chake cha kwanza huku watu wengi wakionekana kutoelewa namna anavyobadilisha wachezaji wake wa kikosi cha kwanza.

    Upete pia aliendelea kusema, licha ya hayo lakini kumekuwa na wachezaji ambao wamekuwa wakianza mara zote kama ilivyo kwa Che Malone, Abdulrazack Hamza na Moussa Camara.

    Uchambuzi huu unayonyesha wana Simba wanapaswa kujipiga kifua kuwa wamepata bonge moja la kocha na wataraji kuwa na kikosi kipana katika klabu yao.

    Mnyama ndiye kinara wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara na alimpasua vibaya mno Singida Fountain Gate katika dimba lake la CCM Liti, Singida.

    #paulswai
    馃毃 FADLU NI KOCHA WA KISASA HANA KIKOSI CHA KWANZA. Nimemnukuu mchambuzi na mtangazaji mahari wa kabumbu nchini Nazareth Upete kupitia kipindi cha Bao la Asubuhi, amesema makocha wengi wa kisasa Duniani hawana First Eleven yaani kikosi cha kwanza. Hili linaangukia kwa kocha mkuu wa klabu ya Simba Fadlu Davids, ambaye amekuwa hatabiriki katika kikosi chake cha kwanza huku watu wengi wakionekana kutoelewa namna anavyobadilisha wachezaji wake wa kikosi cha kwanza. Upete pia aliendelea kusema, licha ya hayo lakini kumekuwa na wachezaji ambao wamekuwa wakianza mara zote kama ilivyo kwa Che Malone, Abdulrazack Hamza na Moussa Camara. Uchambuzi huu unayonyesha wana Simba wanapaswa kujipiga kifua kuwa wamepata bonge moja la kocha na wataraji kuwa na kikosi kipana katika klabu yao. Mnyama ndiye kinara wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara na alimpasua vibaya mno Singida Fountain Gate katika dimba lake la CCM Liti, Singida. #paulswai
    Like
    4
    1 Comments 0 Shares 432 Views
  • #Breaking: Hamas iko tayari kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza kufuatia kutangazwa kwa mapatano kati ya Lebanon na Israel, AFP inaripoti, ikimnukuu mwakilishi wa harakati hiyo......
    #Breaking: Hamas iko tayari kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza kufuatia kutangazwa kwa mapatano kati ya Lebanon na Israel, AFP inaripoti, ikimnukuu mwakilishi wa harakati hiyo......
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 387 Views
  • NUKUU YA LEO: “Kadri unavyokua kwenye matatizo, kitu cha muhimu zaidi ni kukabiliana nayo na si kuyakimbia.
    NUKUU YA LEO: “Kadri unavyokua kwenye matatizo, kitu cha muhimu zaidi ni kukabiliana nayo na si kuyakimbia.
    Like
    4
    1 Comments 0 Shares 202 Views
  • NUKUU YA LEO: “Hakuna anayekutazama kwa umakini na utulivu kama yule ambaye haamini katika uwezo wako
    NUKUU YA LEO: “Hakuna anayekutazama kwa umakini na utulivu kama yule ambaye haamini katika uwezo wako
    Love
    Like
    5
    1 Comments 0 Shares 195 Views