• 𝐏𝐑𝐄𝐒𝐒

    "Nadhani tumeboresha mambo mengi tangu nilipokuja, na bila shaka tunahitaji kuwa makini zaidi katika safu ya ushambuliaji. Katika mechi za mwisho, tulifunga mabao mengi na tulipata nafasi nyingi mbele ya goli. Hii ni moja ya nguvu zetu, lakini tunapaswa kuwa na umakini zaidi katika kumalizia na kujaribu kufunga mabao zaidi, kwa sababu tunataka kuwa bora katika kila kitu tunachofanya" Sead Ramovic

    #timuyawananchi
    #daimambelenyumamwiko
    𝐏𝐑𝐄𝐒𝐒💬 "Nadhani tumeboresha mambo mengi tangu nilipokuja, na bila shaka tunahitaji kuwa makini zaidi katika safu ya ushambuliaji. Katika mechi za mwisho, tulifunga mabao mengi na tulipata nafasi nyingi mbele ya goli. Hii ni moja ya nguvu zetu, lakini tunapaswa kuwa na umakini zaidi katika kumalizia na kujaribu kufunga mabao zaidi, kwa sababu tunataka kuwa bora katika kila kitu tunachofanya" Sead Ramovic #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko
    Like
    1
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·645 Views
  • 𝐏𝐑𝐄𝐒𝐒

    "Tunahitaji kujaribu kucheza kati ya mistari. Tunapaswa kucheza katika nafasi ndogo nyuma ya safu ya ulinzi. Tunahitaji kuwasambaza ili tuweze kupata nafasi kati ya mistari. Kwa ujumla, itakuwa mechi ngumu tena, lakini kama ninavyosema kila wakati, sisi ni timu bora zaidi nchini Tanzania. Tumeshinda taji mara tatu, na tunataka kushinda tena" Sead Ramovic

    #timuyawananchi
    #daimambelenyumamwiko
    𝐏𝐑𝐄𝐒𝐒💬 "Tunahitaji kujaribu kucheza kati ya mistari. Tunapaswa kucheza katika nafasi ndogo nyuma ya safu ya ulinzi. Tunahitaji kuwasambaza ili tuweze kupata nafasi kati ya mistari. Kwa ujumla, itakuwa mechi ngumu tena, lakini kama ninavyosema kila wakati, sisi ni timu bora zaidi nchini Tanzania. Tumeshinda taji mara tatu, na tunataka kushinda tena" Sead Ramovic #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko
    Like
    1
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·657 Views
  • #PART2

    Baada ya mipaka ya Wakoloni walioangukia Rwanda na Burundi waliendelea kujiita Watutsi, lakini walioangukia Congo hawakujiita Watutsi, kwa sababu ya kukwepa ubaguzi. Ili wasitengwe wakajitambulisha kwa eneo wanalotoka, safu za Milima ya Mulenge. Kwahiyo wakajiita Banyamulenge, yani watu kutoka Mulenge. Lakini ukweli ni Watutsi, wametengwa na wenzao kwa mipaka ya wakoloni.

    Ni sawa na wamassai wa Tanzania na wale wa Kenya. Ni jamii moja ila wametengwa na mipaka ya Wakoloni. Huku Tanzania Wamasai ni wengi kuliko Kenya, lakini serikali ya Kenya haiwezi kuwafukuza wa Kenya waje Tanzania. Itakua dhambi ya ubaguzi. Mipaka ilipowekwa waliojikuta Kenya wakawa raia wa Kenya hivyo, hali kadhalika waliojikuta Tanzania.

    Watutsi wa Congo pamoja na kujiita Banyamulenge, bado wakikumbana na ubaguzi. Hawakupata ushirikiano kutoka kwa jamii nyingine za Kivu. Kwahiyo wakajikuta wameongeza "bond" na Watutsi wa Rwanda. Kukawa na mwingiliano mkubwa kati ya Watutsi wa Rwanda na wale wa Congo (Banyamulenge).

    Mwaka 1959, mfalme wa mwisho wa Rwanda, Mutara III, aliuawa kwa sumu. Baada ya kifo chake, Rwanda iliingia katika machafuko ambapo Wahutu waliokuwa zaidi ya 80% waliwashambulia Watutsi, wakiwatuhumu kupendelewa na Wakoloni wa Kibelgiji. Maelfu ya Watutsi walikimbilia Kivu kwa ajili ya usalama wao. Walipofika huko, waliungana na wenzao (Banyamulenge), idadi ikaongezeka.

    Mwaka 1962, Rwanda ilipata uhuru, na Gregoire Kayibanda akawa Rais. Kwa mara ya kwanza, Wahutu walishika madaraka baada ya utawala wa kifalme wa Watutsi kwa miaka mingi. Kayibanda alikakandamiza Watutsi na kupendelea Wahutu wenzake. Watutsi wengi walikimbilia uhamishoni, hasa maeneo ya Kivu. Wakaenda kuungana na wenzao (Banyamulenge).

    Mwaka 1973, Kayibanda alipinduliwa na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Juvénal Habyarimana, ambaye alijiapiza kuwatokomeza Watutsi. Kwa miaka 21 ya utawala wake, Watutsi waliteswa vikali. Waliondolewa kwenye nafasi za kijeshi, mashirika ya umma, na siasa. Wengi walifungwa gerezani au kuuawa. Hali hii iliwafanya Watutsi wengi zaidi kukimbia Rwanda na kuelekea maeneo mbalimbali ikiwemo Kivu. Walioenda Kivu wakaenda kuongeza idadi ya Banyamulenge.!
    (Malisa GJ)

    #PART2 Baada ya mipaka ya Wakoloni walioangukia Rwanda na Burundi waliendelea kujiita Watutsi, lakini walioangukia Congo hawakujiita Watutsi, kwa sababu ya kukwepa ubaguzi. Ili wasitengwe wakajitambulisha kwa eneo wanalotoka, safu za Milima ya Mulenge. Kwahiyo wakajiita Banyamulenge, yani watu kutoka Mulenge. Lakini ukweli ni Watutsi, wametengwa na wenzao kwa mipaka ya wakoloni. Ni sawa na wamassai wa Tanzania na wale wa Kenya. Ni jamii moja ila wametengwa na mipaka ya Wakoloni. Huku Tanzania Wamasai ni wengi kuliko Kenya, lakini serikali ya Kenya haiwezi kuwafukuza wa Kenya waje Tanzania. Itakua dhambi ya ubaguzi. Mipaka ilipowekwa waliojikuta Kenya wakawa raia wa Kenya hivyo, hali kadhalika waliojikuta Tanzania. Watutsi wa Congo pamoja na kujiita Banyamulenge, bado wakikumbana na ubaguzi. Hawakupata ushirikiano kutoka kwa jamii nyingine za Kivu. Kwahiyo wakajikuta wameongeza "bond" na Watutsi wa Rwanda. Kukawa na mwingiliano mkubwa kati ya Watutsi wa Rwanda na wale wa Congo (Banyamulenge). Mwaka 1959, mfalme wa mwisho wa Rwanda, Mutara III, aliuawa kwa sumu. Baada ya kifo chake, Rwanda iliingia katika machafuko ambapo Wahutu waliokuwa zaidi ya 80% waliwashambulia Watutsi, wakiwatuhumu kupendelewa na Wakoloni wa Kibelgiji. Maelfu ya Watutsi walikimbilia Kivu kwa ajili ya usalama wao. Walipofika huko, waliungana na wenzao (Banyamulenge), idadi ikaongezeka. Mwaka 1962, Rwanda ilipata uhuru, na Gregoire Kayibanda akawa Rais. Kwa mara ya kwanza, Wahutu walishika madaraka baada ya utawala wa kifalme wa Watutsi kwa miaka mingi. Kayibanda alikakandamiza Watutsi na kupendelea Wahutu wenzake. Watutsi wengi walikimbilia uhamishoni, hasa maeneo ya Kivu. Wakaenda kuungana na wenzao (Banyamulenge). Mwaka 1973, Kayibanda alipinduliwa na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Juvénal Habyarimana, ambaye alijiapiza kuwatokomeza Watutsi. Kwa miaka 21 ya utawala wake, Watutsi waliteswa vikali. Waliondolewa kwenye nafasi za kijeshi, mashirika ya umma, na siasa. Wengi walifungwa gerezani au kuuawa. Hali hii iliwafanya Watutsi wengi zaidi kukimbia Rwanda na kuelekea maeneo mbalimbali ikiwemo Kivu. Walioenda Kivu wakaenda kuongeza idadi ya Banyamulenge.! (Malisa GJ)
    Like
    1
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·665 Views
  • Siku ya Jana 18, January na leo 19, January 2025 nimefuatilia kwa ukaribu na Umakini Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Mwaka 2025 uliofanyika Dodoma Hakika umekua wa kipekee na Uliovutia kwa Maandalizi mazuri, Hongera sana Kwa Waandaaji wakiongozwa na Dk @samia_suluhu_hassan Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuli ya muungano wa Tanzania.

    Pamoja na mambo mengine yaliyojadiliwa kwenye Mkutano huu nimeshuhudia Matukio Matatu Muhimu,

    Mosi, Uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Dkt Steven Wasira
    Pili, Marekebisho ya Baadhi ya vipengele muhimu vya Katiba ya CCM ikiwemo kuongezeka kwa wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM kutoka nafasi 6 paka 10 yaani nafasi 5 Zanzibar na Nafasi 5 Bara,
    Tatu, Uteuzi na Uidhinishwaji wa Majina ya wagombea wa Nafasi ya Urais Tanzania na Zanzibar Uchaguzi Mkuu 2025 Yaani Dkt @samia_suluhu_hassan kwa Tanzania na Dkt @dr.hmwinyi Zanzibar

    Nne, kupendekeza na kupitisha Jina la Mgombea mwenza (Makamu wa Rais) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt @nchimbie

    Matukio yote haya Manne yameendelea kuthibitisha kwamba CCM ni chama kilichokomaa Kidemocrasia na Ndio chama pekee kinachofaa kuiongoza nchi hii kwa Amani na Utulivu (Hasa ukizingatia yanayoendelea huko upande wa Pili Mmh)

    Lakini pia imendelea kuthibitisha kiasi Gani chama cha Mapinduzi @ccmtanzania kina hazina ya Watu wanaoweza kuiongoza chama na Serikali wakati wowote ule kuanzia Chama chenyewe na Jumuia zake zote @wazazi_ccm_tz @uwt_taifa , na @uvccm_tz , Hakika CCM idumu milele, Hongera Mwenyekiti @samia_suluhu_hassan kwa Uongozi na Malezi Bora kwa Chama

    Itoshe Kusema @ccmtanzania inatosha na ni kwa matakwa ya kikatiba tu lakini ingewezekana TUSIFANYE UCHAGUZI TUMUACHE MAMA NA SAFU YAKE WAENDELEE KUFANYA KAZI YA KUIJENGA TANZANIA, Kwa Hali inayoendelea na Mfarakano wa huko kwa Majirani naona kabisa ni kupoteza muda. Ni kwasababu ni Takwa la kikatiba tu na CCM tunaheshimu Katiba lakini isingekua Hilo Basi Mama @samia_suluhu_hassan Angeachwa na Safu yake aendelee kuchapa kazi, Aendeleze kazi ya kuijenga Tanzania iliyotukuka

    Hongera Mama @samia_suluhu_hassan, Hongera Dkt @dr.hmwinyi, Hongera Dkt @nchimbie kwa kuaminiwa Tena

    #kaziiendelee

    @ccmtanzania @uvccm_tz @uvccm_tanga
    Siku ya Jana 18, January na leo 19, January 2025 nimefuatilia kwa ukaribu na Umakini Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Mwaka 2025 uliofanyika Dodoma Hakika umekua wa kipekee na Uliovutia kwa Maandalizi mazuri, Hongera sana Kwa Waandaaji wakiongozwa na Dk @samia_suluhu_hassan Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuli ya muungano wa Tanzania. Pamoja na mambo mengine yaliyojadiliwa kwenye Mkutano huu nimeshuhudia Matukio Matatu Muhimu, Mosi, Uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Dkt Steven Wasira Pili, Marekebisho ya Baadhi ya vipengele muhimu vya Katiba ya CCM ikiwemo kuongezeka kwa wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM kutoka nafasi 6 paka 10 yaani nafasi 5 Zanzibar na Nafasi 5 Bara, Tatu, Uteuzi na Uidhinishwaji wa Majina ya wagombea wa Nafasi ya Urais Tanzania na Zanzibar Uchaguzi Mkuu 2025 Yaani Dkt @samia_suluhu_hassan kwa Tanzania na Dkt @dr.hmwinyi Zanzibar Nne, kupendekeza na kupitisha Jina la Mgombea mwenza (Makamu wa Rais) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt @nchimbie Matukio yote haya Manne yameendelea kuthibitisha kwamba CCM ni chama kilichokomaa Kidemocrasia na Ndio chama pekee kinachofaa kuiongoza nchi hii kwa Amani na Utulivu (Hasa ukizingatia yanayoendelea huko upande wa Pili Mmh🙌😂) Lakini pia imendelea kuthibitisha kiasi Gani chama cha Mapinduzi @ccmtanzania kina hazina ya Watu wanaoweza kuiongoza chama na Serikali wakati wowote ule kuanzia Chama chenyewe na Jumuia zake zote @wazazi_ccm_tz @uwt_taifa , na @uvccm_tz , Hakika CCM idumu milele, Hongera Mwenyekiti @samia_suluhu_hassan kwa Uongozi na Malezi Bora kwa Chama Itoshe Kusema @ccmtanzania inatosha na ni kwa matakwa ya kikatiba tu lakini ingewezekana TUSIFANYE UCHAGUZI TUMUACHE MAMA NA SAFU YAKE WAENDELEE KUFANYA KAZI YA KUIJENGA TANZANIA, Kwa Hali inayoendelea na Mfarakano wa huko kwa Majirani naona kabisa ni kupoteza muda. Ni kwasababu ni Takwa la kikatiba tu na CCM tunaheshimu Katiba lakini isingekua Hilo Basi Mama @samia_suluhu_hassan Angeachwa na Safu yake aendelee kuchapa kazi, Aendeleze kazi ya kuijenga Tanzania iliyotukuka Hongera Mama @samia_suluhu_hassan, Hongera Dkt @dr.hmwinyi, Hongera Dkt @nchimbie kwa kuaminiwa Tena #kaziiendelee @ccmtanzania @uvccm_tz @uvccm_tanga
    0 Commentarios ·0 Acciones ·690 Views
  • SOMA HII.. Rekodi ya gari lenye kasi zaidi Duniani ya vunjwa JE gari ilo Lina uwezo kiasi Gani..

    Wiki hii katika ulimwengu wa magari: Bugatti imeweka rekodi mpya ya gari la wazi lenye kasi kubwa zaidi duniani, Cadillac imezindua gari lake jipya aina ya SUV (gari maridadi) linalotumia umeme. Gari hilo la kampuni ya Xiaomi limevunja rekodi ya Porsche, huku Donald Trump akimteua Mkurugenzi mtendaji wa kwanza wa kampuni ya magari ya Hyundai ambaye sio raia wa Korea

    Kampuni ya Bugatti ilivunja rekodi ya gari la wazi na la kasi zaidi duniani kwa kusajili kasi ya kilomita 91.453 kwa saa. Rekodi hii iliwekwa na Bugatti Mistral W16 barabarani nchini Ujerumani mbele ya wamiliki maarufu wa magari.

    Ingawa muundo wake kwa kawaida unafanana na ule wa Chiron Supercar Mistral inaonekana tofauti kabisa na ilitengenezwa kwa dhana za Bugatti na mifano ya miundo ya jadi.

    Injini ya Mistral ina nguvu ya horse power 1600. Bugatti hapo awali ilikuwa imetumia injini hii katika mfano wa "Chiron Super Sport" na kurekodi kasi ya 482.8 km / kwa saa mnamo 2019.

    Mistral ni mfano wa mwisho wa Bugatti ambayo ina injini yenye silinda kumi na sita. Bugatti ilizindua gari hili mnamo 2022 na ni magari 99 tu ya aina yake yaliyotengenezwa.

    Wakati huo huo wakati Mistral ilizinduliwa, vyombo vya habari vilitangaza bei yake ya msingi kama euro milioni tano (karibu dola milioni tano na elfu 300), lakini Bugatti inasema thamani ya gari iliyovunja rekodi wiki iliyopita ni euro milioni 14 (karibu dola milioni 14 na milioni 700).

    Mmiliki wa mistral hii, ambayo imetajwa " kushikilia rekodi ya ulimwengu", ni mfanyabiashara wa Uingereza mwenye asili ya India aitwaye Reuben Singh. Bwana Singh ana mifano mingine ya Bugatti katika kampuni yake ya magari ambayo pia yamevunja rekodi ya kasi.

    Rekodi hiyo iliwekwa na Andy Wallace, dereva rasmi wa Bugatti, ambaye ameshinda shindano la magari la saa 24 . Baada ya kuweka rekodi ya mzunguko mwingine zaidi , aliondoka na mmiliki gari hilo kwenye barabara ya mashindano, na Bugatti inasema Singh alikuwa "dereva mweye kasi zaidi duniani" bada ya kuzunguka mzunguko mmoja mbele ya magari mengine.

    Rekodi ya awali ya gari la wazi zaidi duniani ilikuwa 427.4 km / kwa saa, ambayo iliwekwa na Hennessy Venom GT Spyder mwaka 2016.

    Cadillac itaongeza SUV (gari maridadi) jipya la umeme linaloitwa "Vistiq" kwenye bidhaa zake kuanzia mwaka ujao. Vistic ni muundo wa tano wa umeme wa gari la Cadillac.

    Vipengele vya gari hili ni sawa na mfano wa Lyric na ina safu tatu za viti kama Escalade.

    Vistic ina motors mbili za umeme ambazo hutoa jumla ya nguvu za horse power 615. Gari huharakisha kutoka sifuri hadi maili 60 kwa saa kwa sekunde 3.7 .

    Ina sauti 23 tofauti mbali na vifaa vya mfumo ambao unafuta kelele za kusumbua.

    Vistic pia ina vifaa vya mfumo wa "Super Cruise" wa GM, ambao unamruhusu dereva kuondoa mikono yake kwenye usukani kwenye njia fulani.

    Katika hali hii, dereva lazima awe makini na wakati gari linatambua kuwa anaondoa macho yake barabarani, humuonya.

    Cadillac inasema kuwa tofauti na magari mengi yenye viti vitatu, imetoa huduma nyingi kwa abiria watatu. Wana mahali pa kuweka kikombe, wanaweza kuchaji simu zao na kubadilisha hali ya hewa ndani ya gari kwa kuongeza joto au baridi. Paa la juu ya safu ya tatu limetengenezwa kwa glasi.
    SOMA HII.. Rekodi ya gari lenye kasi zaidi Duniani ya vunjwa JE gari ilo Lina uwezo kiasi Gani.. Wiki hii katika ulimwengu wa magari: Bugatti imeweka rekodi mpya ya gari la wazi lenye kasi kubwa zaidi duniani, Cadillac imezindua gari lake jipya aina ya SUV (gari maridadi) linalotumia umeme. Gari hilo la kampuni ya Xiaomi limevunja rekodi ya Porsche, huku Donald Trump akimteua Mkurugenzi mtendaji wa kwanza wa kampuni ya magari ya Hyundai ambaye sio raia wa Korea Kampuni ya Bugatti ilivunja rekodi ya gari la wazi na la kasi zaidi duniani kwa kusajili kasi ya kilomita 91.453 kwa saa. Rekodi hii iliwekwa na Bugatti Mistral W16 barabarani nchini Ujerumani mbele ya wamiliki maarufu wa magari. Ingawa muundo wake kwa kawaida unafanana na ule wa Chiron Supercar Mistral inaonekana tofauti kabisa na ilitengenezwa kwa dhana za Bugatti na mifano ya miundo ya jadi. Injini ya Mistral ina nguvu ya horse power 1600. Bugatti hapo awali ilikuwa imetumia injini hii katika mfano wa "Chiron Super Sport" na kurekodi kasi ya 482.8 km / kwa saa mnamo 2019. Mistral ni mfano wa mwisho wa Bugatti ambayo ina injini yenye silinda kumi na sita. Bugatti ilizindua gari hili mnamo 2022 na ni magari 99 tu ya aina yake yaliyotengenezwa. Wakati huo huo wakati Mistral ilizinduliwa, vyombo vya habari vilitangaza bei yake ya msingi kama euro milioni tano (karibu dola milioni tano na elfu 300), lakini Bugatti inasema thamani ya gari iliyovunja rekodi wiki iliyopita ni euro milioni 14 (karibu dola milioni 14 na milioni 700). Mmiliki wa mistral hii, ambayo imetajwa " kushikilia rekodi ya ulimwengu", ni mfanyabiashara wa Uingereza mwenye asili ya India aitwaye Reuben Singh. Bwana Singh ana mifano mingine ya Bugatti katika kampuni yake ya magari ambayo pia yamevunja rekodi ya kasi. Rekodi hiyo iliwekwa na Andy Wallace, dereva rasmi wa Bugatti, ambaye ameshinda shindano la magari la saa 24 . Baada ya kuweka rekodi ya mzunguko mwingine zaidi , aliondoka na mmiliki gari hilo kwenye barabara ya mashindano, na Bugatti inasema Singh alikuwa "dereva mweye kasi zaidi duniani" bada ya kuzunguka mzunguko mmoja mbele ya magari mengine. Rekodi ya awali ya gari la wazi zaidi duniani ilikuwa 427.4 km / kwa saa, ambayo iliwekwa na Hennessy Venom GT Spyder mwaka 2016. Cadillac itaongeza SUV (gari maridadi) jipya la umeme linaloitwa "Vistiq" kwenye bidhaa zake kuanzia mwaka ujao. Vistic ni muundo wa tano wa umeme wa gari la Cadillac. Vipengele vya gari hili ni sawa na mfano wa Lyric na ina safu tatu za viti kama Escalade. Vistic ina motors mbili za umeme ambazo hutoa jumla ya nguvu za horse power 615. Gari huharakisha kutoka sifuri hadi maili 60 kwa saa kwa sekunde 3.7 . Ina sauti 23 tofauti mbali na vifaa vya mfumo ambao unafuta kelele za kusumbua. Vistic pia ina vifaa vya mfumo wa "Super Cruise" wa GM, ambao unamruhusu dereva kuondoa mikono yake kwenye usukani kwenye njia fulani. Katika hali hii, dereva lazima awe makini na wakati gari linatambua kuwa anaondoa macho yake barabarani, humuonya. Cadillac inasema kuwa tofauti na magari mengi yenye viti vitatu, imetoa huduma nyingi kwa abiria watatu. Wana mahali pa kuweka kikombe, wanaweza kuchaji simu zao na kubadilisha hali ya hewa ndani ya gari kwa kuongeza joto au baridi. Paa la juu ya safu ya tatu limetengenezwa kwa glasi.
    Like
    1
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·471 Views
  • Ramovic kama kawaida yake na 4-2-3-1 , wakiwa na umiliki wa mpira wanaswitch na kuwa 2-3-2-3 (CBs wawili nyuma then Kibwana na Yao wanasogea juu mstari mmoja na Aucho huku Duke na Aziz Ki kama namba 10 wawili nyuma ya Pacome , Mzize na Dube walitengeneza uwiano mzuri eneo la mbele wakiwa na mpira kivipi ?

    Yanga kama dakika 30 za kwanza waliutembeza mpira kwa uharaka sana (Decision Making , runners walikuwa wengi eneo la mbele , walipata nafasi kubwa kwenye mpira (Pacome na Mzize) mda mwingi FBs wa Yanga walikuwa pembeni zaidi kwenye chaki….dhumuni ni kutafuta mapana ya uwanja na kuitanua block ya Mashujaa nafasi kwa wale namba 10 wawili + Pacome na Mzize ambao walikuwa wanaingia kwenye Half spaces zikaanza kufunguka .

    Mashujaa kwenye plan ya kuzuia wakiwa chini kwenye “Mid Block” then wakipora mpira haraka sana wanatengeneza mashambulizi kwa kushtukiza (Offesive Transition) na walinufaika na makosa ya safu ya ulinzi kutoka kwa Yanga (Goli la Ulomi “Defense line kusinzia , goli la pili makosa ya golikipa) .

    Mashujaa kuna nyakati kwenye kiungo walicheza vizuri sana , Pasi sahihi , movements lakini pia walitengeneza namba nzuri ya wachezaji (Overloads) ….. kulikuwa na nafasi kubwa kati ya kiungo cha Yanga na walinzi .

    Prince Dube anafunga “Hattrick” ya kwanza msimu huu NBCPL …. Ni mchezo wake bora sana tangia ajiunge na Yanga .

    Kibwana Shomari amecheza game bora sana , Duke akiwa na mali ni ngumu kuchukua …. Wale viungo wa Mashujaa wametoa game bora dhidi ya Yanga . Pacome

    FT : Yanga 3-2 Mashujaa

    Ramovic kama kawaida yake na 4-2-3-1 , wakiwa na umiliki wa mpira wanaswitch na kuwa 2-3-2-3 (CBs wawili nyuma then Kibwana na Yao wanasogea juu mstari mmoja na Aucho huku Duke na Aziz Ki kama namba 10 wawili nyuma ya Pacome , Mzize na Dube walitengeneza uwiano mzuri eneo la mbele wakiwa na mpira kivipi ? Yanga kama dakika 30 za kwanza waliutembeza mpira kwa uharaka sana (Decision Making , runners walikuwa wengi eneo la mbele , walipata nafasi kubwa kwenye mpira (Pacome na Mzize) mda mwingi FBs wa Yanga walikuwa pembeni zaidi kwenye chaki….dhumuni ni kutafuta mapana ya uwanja na kuitanua block ya Mashujaa nafasi kwa wale namba 10 wawili + Pacome na Mzize ambao walikuwa wanaingia kwenye Half spaces zikaanza kufunguka . Mashujaa kwenye plan ya kuzuia wakiwa chini kwenye “Mid Block” then wakipora mpira haraka sana wanatengeneza mashambulizi kwa kushtukiza (Offesive Transition) na walinufaika na makosa ya safu ya ulinzi kutoka kwa Yanga (Goli la Ulomi “Defense line kusinzia , goli la pili makosa ya golikipa) . Mashujaa kuna nyakati kwenye kiungo walicheza vizuri sana , Pasi sahihi , movements lakini pia walitengeneza namba nzuri ya wachezaji (Overloads) ….. kulikuwa na nafasi kubwa kati ya kiungo cha Yanga na walinzi . Prince Dube anafunga “Hattrick” ya kwanza msimu huu NBCPL …. Ni mchezo wake bora sana tangia ajiunge na Yanga . Kibwana Shomari 👏 amecheza game bora sana , Duke akiwa na mali ni ngumu kuchukua …. Wale viungo wa Mashujaa wametoa game bora dhidi ya Yanga . Pacome 👍 FT : Yanga 3-2 Mashujaa
    0 Commentarios ·0 Acciones ·640 Views
  • MSIKIE KOCHA FADLU ::

    Fadlu Davids, amesisitiza nidhamu ya kiufundi na kiakili, akisema: “Tunajua ubora wa Yanga, lakini tunajiandaa kimkakati. Lazima tuwe makini kwa kila dakika, kujenga mashambulizi kwa kasi na kudhibiti safu ya ulinzi kwa umakini mkubwa.”

    Fadlu anaamini kutumia fursa chache zinazopatikana ni muhimu, akiongeza kwa kusema: “Katika mechi kama hizi, nafasi ni chache, hivyo tunahitaji kuwa bora katika kumalizia.”
    #paulswai
    🎙️ MSIKIE KOCHA FADLU :: Fadlu Davids, amesisitiza nidhamu ya kiufundi na kiakili, akisema: “Tunajua ubora wa Yanga, lakini tunajiandaa kimkakati. Lazima tuwe makini kwa kila dakika, kujenga mashambulizi kwa kasi na kudhibiti safu ya ulinzi kwa umakini mkubwa.” Fadlu anaamini kutumia fursa chache zinazopatikana ni muhimu, akiongeza kwa kusema: “Katika mechi kama hizi, nafasi ni chache, hivyo tunahitaji kuwa bora katika kumalizia.” #paulswai
    Like
    1
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·235 Views

  • MAXIMUM POINTS!

    Simba inakusanya alama 3 dhidi ya Dodoma jiji kwa ushindi wa 1-0 na kufikisha jumla ya alama 12 kwenye michezo minne (4).

    Kitu chanya ni kwamba Simba ina wastani wa kufunga kila mchezo na haija ruhusu bao lolote mpaka sasa..safu ya ulinzi inayoanzia kwenye kiungo cha uzuiaji mpaka kwa mlinda mlango imeonekana kutulia kwa haraka zaid licha ya kuwa na maingizo mapya. Kwenye mbio za ubingwa hili ni eneo muhimu sana.

    Ateba anazidi kujitanabaisha kuwa ndio chaguo la kwanza kwenye ushambuliaji kwa perfomance zake, hakua na goal leo lakin alikua na majaribio ya kutosha.

    Bado mwalimu Fadlu anafanya majaribio kadhaa kwenye maeneo kadhaa lakini muelekeo wa timu yake kwa sasa ni muelekeo sahihi.
    #paulswai
    MAXIMUM POINTS! Simba inakusanya alama 3 dhidi ya Dodoma jiji kwa ushindi wa 1-0 na kufikisha jumla ya alama 12 kwenye michezo minne (4). Kitu chanya ni kwamba Simba ina wastani wa kufunga kila mchezo na haija ruhusu bao lolote mpaka sasa..safu ya ulinzi inayoanzia kwenye kiungo cha uzuiaji mpaka kwa mlinda mlango imeonekana kutulia kwa haraka zaid licha ya kuwa na maingizo mapya. Kwenye mbio za ubingwa hili ni eneo muhimu sana. Ateba anazidi kujitanabaisha kuwa ndio chaguo la kwanza kwenye ushambuliaji kwa perfomance zake, hakua na goal leo lakin alikua na majaribio ya kutosha. Bado mwalimu Fadlu anafanya majaribio kadhaa kwenye maeneo kadhaa lakini muelekeo wa timu yake kwa sasa ni muelekeo sahihi. #paulswai
    Love
    1
    · 1 Commentarios ·0 Acciones ·524 Views

  • KAMA UNAELEWA SAYANSI YA MPIRA UTAMUELEWA FADLU, SIMBA YA JANA

    Sayansi ya mpira inasema kabla ya mechi msome sana mpinzani, wazungu wanaita game guiding, lakini pia wakati wa mchezo, ile mechi inaanza tu shika peni na karatasi noti vitu muhimu kwa mpinzani, amekuja kujaje.

    Itasaidia kukupa ABC kudili naye, kutambua ulipo ubora wake & ulipo udhaifu wake. Unaweza kuvunja mitego yake, vunja. Kuna eneo yeye ni bora sana, wewe boresha ilipo nguvu yako kwa lengo la kuudhibiti ubora wake.

    Davids Fadlu kaichukua Simba ambapo moja kati ya eneo lilikuwa linavuja sana ni safu ya ulinzi. Kutoruhusu goli mechi mbili za Ligi Kuu NBC haiwezi kutumika kama guarantee ya kwenda kujilipua ugenini mchezo wa CAF mtoano mbele ya Waarabu.

    Nidhamu ya kwanza ya kimbinu kama mpango kazi, inakulazimu plan A iwe ni kuziba mianya kwa namba kubwa. Sio tena kazi ya mabeki pekee hiyo bali kazi ya timu. System ni mid-block.

    Ilikuwa ni rahisi kumuona mtu kama deep playmaker Deborah Fernandes Mavambo akicheza zaidi chini kuliko ilivyozoeleka. Game Aproach ilimhitaji acheze hivyo.

    Plan A ya kuzima mashambulizi ya mpinzani ilitiki, Plan B ya counter attack ikakataa.Mutale&Balua wakimezwa. Kwenye football kawaida inatokea, kimoja kukubali, kingine kukataa.

    Take away:Bora nusu kitu kuliko kukosa kabisa.
    #paulswai
    KAMA UNAELEWA SAYANSI YA MPIRA UTAMUELEWA FADLU, SIMBA YA JANA Sayansi ya mpira inasema kabla ya mechi msome sana mpinzani, wazungu wanaita game guiding, lakini pia wakati wa mchezo, ile mechi inaanza tu shika peni na karatasi noti vitu muhimu kwa mpinzani, amekuja kujaje. Itasaidia kukupa ABC kudili naye, kutambua ulipo ubora wake & ulipo udhaifu wake. Unaweza kuvunja mitego yake, vunja. Kuna eneo yeye ni bora sana, wewe boresha ilipo nguvu yako kwa lengo la kuudhibiti ubora wake. Davids Fadlu kaichukua Simba ambapo moja kati ya eneo lilikuwa linavuja sana ni safu ya ulinzi. Kutoruhusu goli mechi mbili za Ligi Kuu NBC haiwezi kutumika kama guarantee ya kwenda kujilipua ugenini mchezo wa CAF mtoano mbele ya Waarabu. Nidhamu ya kwanza ya kimbinu kama mpango kazi, inakulazimu plan A iwe ni kuziba mianya kwa namba kubwa. Sio tena kazi ya mabeki pekee hiyo bali kazi ya timu. System ni mid-block. Ilikuwa ni rahisi kumuona mtu kama deep playmaker Deborah Fernandes Mavambo akicheza zaidi chini kuliko ilivyozoeleka. Game Aproach ilimhitaji acheze hivyo. Plan A ya kuzima mashambulizi ya mpinzani ilitiki, Plan B ya counter attack ikakataa.Mutale&Balua wakimezwa. Kwenye football kawaida inatokea, kimoja kukubali, kingine kukataa. Take away:Bora nusu kitu kuliko kukosa kabisa. #paulswai
    Like
    1
    · 0 Commentarios ·0 Acciones ·970 Views
  • Nikicheki muda Ni saa 4 usiku Napiga Dua namshukuru mungu
    Kwa kunilinda Hii Siku na Wenye #Bifu
    Naomba Tena Atulinde huu usiku #Mrefu
    Mungu Mimi kwako si #Mkamilifu
    Najua nakosea Nina mengi #Madhaifu
    Kwa wema wako nioshe niwe #Nadhifu
    Nakusifu kwa mdomo maana hujaniumba #BuBu
    Wape Tumaini wenye matatizo yanayo #Wasibu
    Wagonjwa mahospitali wema wako #Ukawatibu
    Wategemee Dua na sio sangoma Wala #Chifu
    Waombewe na watumishi mashekh wakina #Sharifu
    Wasirogane kwa kuvunjiana Nazi na #Madafu
    Nashukuru kwa hii pumzi inayoingia kwenye #Mapafu
    Nitimize sakramenti takwa Mimi nilie #Mkristu
    Niepushe Na zinaa niogope kufungua #Zipu
    Niepushe Na tamaa nisipende Sana #Chipu
    Niwe mwema ndugu zangu nisiwachezee #Rafu
    Niiheshimu ndoa nilale chumbani niogee #Bafu
    Kesho nijalie riziki yangu niingojee kwa #Safu
    Nisishawishike na ulevi nikaja lala #Club
    Ee mungu tulinde Huu usiku na kila #Tabu
    Dua zetu zipokee kwako ndo liliko #Jawabu
    Nikicheki muda Ni saa 4 usiku Napiga Dua namshukuru mungu🎤 Kwa kunilinda Hii Siku na Wenye #Bifu Naomba Tena Atulinde huu usiku #Mrefu Mungu Mimi kwako si #Mkamilifu Najua nakosea Nina mengi #Madhaifu Kwa wema wako nioshe niwe #Nadhifu Nakusifu kwa mdomo maana hujaniumba #BuBu Wape Tumaini wenye matatizo yanayo #Wasibu Wagonjwa mahospitali wema wako #Ukawatibu Wategemee Dua na sio sangoma Wala #Chifu Waombewe na watumishi mashekh wakina #Sharifu Wasirogane kwa kuvunjiana Nazi na #Madafu Nashukuru kwa hii pumzi inayoingia kwenye #Mapafu Nitimize sakramenti takwa Mimi nilie #Mkristu Niepushe Na zinaa niogope kufungua #Zipu Niepushe Na tamaa nisipende Sana #Chipu Niwe mwema ndugu zangu nisiwachezee #Rafu Niiheshimu ndoa nilale chumbani niogee #Bafu Kesho nijalie riziki yangu niingojee kwa #Safu Nisishawishike na ulevi nikaja lala #Club Ee mungu tulinde Huu usiku na kila #Tabu Dua zetu zipokee kwako ndo liliko #Jawabu
    0 Commentarios ·0 Acciones ·2K Views
  • Sukari ndo utamu wa kitumbua..
    Nahodha kuzamisha meli utamu wa mua..
    Utamu wa asali compare na halua..
    Utamu wa mapenzi hasa ukiyajua..
    Utamu wa chumvi kwenye chakula..
    Kuramba chumvi chumvini utapata safura..
    Utamu wa simba iwepo Yanga..
    Utamu wa game zao zinaanza kuchezwa kwa waganga..
    Utamu wa smartphone uwe na emcee bando..
    Ila utamu wa YESU muulize Rose muhando..
    Utamu wa supu chapati mbili..
    Utamu wa chipsi kidogo na pilipili..
    Utamu wa kijiti upate cha Arushwa .
    Kisiwe kibichi kiwe kimekaushwa..
    Utamu wa kigodoro kubambia..
    Utamu wake adi mke wa mtu unamkamatia..
    Sukari ndo utamu wa kitumbua.. Nahodha kuzamisha meli utamu wa mua.. Utamu wa asali compare na halua.. Utamu wa mapenzi hasa ukiyajua.. Utamu wa chumvi kwenye chakula.. Kuramba chumvi chumvini utapata safura.. Utamu wa simba iwepo Yanga.. Utamu wa game zao zinaanza kuchezwa kwa waganga.. Utamu wa smartphone uwe na emcee bando.. Ila utamu wa YESU muulize Rose muhando.. Utamu wa supu chapati mbili.. Utamu wa chipsi kidogo na pilipili.. Utamu wa kijiti upate cha Arushwa . Kisiwe kibichi kiwe kimekaushwa.. Utamu wa kigodoro kubambia.. Utamu wake adi mke wa mtu unamkamatia..
    0 Commentarios ·0 Acciones ·525 Views
  • HIP Hop Hisia Nyingi Ma balz Mingi Napokuwa Narap..
    Najiona Zaidi Dingi Demu Kiganja Napigi Safu..
    Umenipa Nini Hip Hop Nafanya Vingi Juu Yako..
    Bila Shilingi Me Mbavu Najiamini Nikiwa Kwako..
    Nilishakana Kubana Pua Wote Mashoga Bongo Wanazingua..
    Siko Dom Arusha Nakichafua Nakwako Ndo Nimeshatua..
    Hip Hop Nikupe Nini Usiwafate Maemce Shilingi..
    HIP Hop Hisia Nyingi Ma balz Mingi Napokuwa Narap.. Najiona Zaidi Dingi Demu Kiganja Napigi Safu.. Umenipa Nini Hip Hop Nafanya Vingi Juu Yako.. Bila Shilingi Me Mbavu Najiamini Nikiwa Kwako.. Nilishakana Kubana Pua Wote Mashoga Bongo Wanazingua.. Siko Dom Arusha Nakichafua Nakwako Ndo Nimeshatua.. Hip Hop Nikupe Nini Usiwafate Maemce Shilingi..
    0 Commentarios ·0 Acciones ·532 Views
  • Wachezaji wa Afrika wanaosaka heshima na historia Ulaya

    Picha,Ademola Lookman (atachuana na mchezaji mwenzake wa Nigeria, Victor Boniface (kulia) katika fainali ya Ligi ya Europa siku ya Jumatano.

    Mashindano makubwa ya vilabu barani Ulaya yanafikia kilele chake na wachezaji kadhaa wa Kiafrika wanatarajia kuandika historia.

    Kuna uwakilishi mkubwa kutoka Afrika katika fainali zote tatu za Ulaya, timu sita zinazoshiriki zote zina Waafrika katika safu zao za kwanza.

    Kuna wachezaji wa Afrika ambao wametoa mchango muhimu na ambao utawawekea historia katika muda wa wiki moja na nusu ijayo.
    #Sports view
    Wachezaji wa Afrika wanaosaka heshima na historia Ulaya Picha,Ademola Lookman (atachuana na mchezaji mwenzake wa Nigeria, Victor Boniface (kulia) katika fainali ya Ligi ya Europa siku ya Jumatano. Mashindano makubwa ya vilabu barani Ulaya yanafikia kilele chake na wachezaji kadhaa wa Kiafrika wanatarajia kuandika historia. Kuna uwakilishi mkubwa kutoka Afrika katika fainali zote tatu za Ulaya, timu sita zinazoshiriki zote zina Waafrika katika safu zao za kwanza. Kuna wachezaji wa Afrika ambao wametoa mchango muhimu na ambao utawawekea historia katika muda wa wiki moja na nusu ijayo. #Sports view
    Like
    5
    · 0 Commentarios ·1 Acciones ·617 Views
  • Manchester United wanataka takriban asilimia 75 ya pauni milioni 75 walizolipa Borussia Dortmund kwa winga wa Uingereza Jadon Sancho, 24, ambaye atahitaji kupunguzwa mshahara wake wa pauni 275,000 kwa wiki ikiwa klabu hiyo ya Bundesliga itakamilisha dili la kumsaini tena(Sun)

    RB Leipzig wamempa mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sesko mwenye umri wa miaka 20 - ambaye anahusishwa na kuhamia Arsenal - nyongeza ya muda wa kandarasi ya mwaka mmoja. (Fabrizio Romano)

    Sheffield United ingelazimika kulipa kiasi cha tarakimu sita kwa kiungo wa kati wa Brazil Vinicius Souza kwa klabu ya zamani ya Lommel iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 angeanza katika mechi dhidi ya Tottenham Jumapili (Sun)

    THCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
    Bayern Munich na Ajax wanaendelea kupigania sahihi ya Erik ten Hag, 54, kwa imani kwamba atafutwa kazi kama meneja wa Manchester United mwishoni mwa msimu huu(Mirror)

    Kipa wa Uhispania David Raya, 28, anasema hajafanya mazungumzo yoyote na Arsenal kuhusu iwapo watafanya uhamisho wake wa mkopo kutoka Brentford kuwa wa kudumu. (Express)

    Meneja wa Tottenham Ange Postecoglou ataweka kipaumbele kumsaini mshambuliaji mpya na kiungo wa safu ya ulinzi huku akipanga kuwaachilia wachezaji wengi msimu wa joto (Mirror)

    Ipswich wanasema wanafanya kila linalowezekana kusalia na meneja Kieran McKenna huku kukiwa na nia ya kumchukua kocha huyo kutoka kwa Brighton , Chelsea na Manchester United .(Teamtalk)

    THCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
    Mkufunzi wa Chelsea Mauricio Pochettino anasema atafurahi kusalia na 80-85% ya kikosi chake msimu ujao(football.london)

    Mwenyekiti mwenza wa Arsenal Josh Kroenke amewaambia mashabiki "klabu haitasimama tuli" inapotafuta wachezaji ili kusaidia kupata taji la Uingereza na Ulaya(Goal)

    West Ham wanakaribia kumsajili mlinzi mwenye umri wa miaka 18 Mwingereza Luis Brown kutoka Arsenal(Caught Offside..##Sports view
    Manchester United wanataka takriban asilimia 75 ya pauni milioni 75 walizolipa Borussia Dortmund kwa winga wa Uingereza Jadon Sancho, 24, ambaye atahitaji kupunguzwa mshahara wake wa pauni 275,000 kwa wiki ikiwa klabu hiyo ya Bundesliga itakamilisha dili la kumsaini tena(Sun) RB Leipzig wamempa mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sesko mwenye umri wa miaka 20 - ambaye anahusishwa na kuhamia Arsenal - nyongeza ya muda wa kandarasi ya mwaka mmoja. (Fabrizio Romano) Sheffield United ingelazimika kulipa kiasi cha tarakimu sita kwa kiungo wa kati wa Brazil Vinicius Souza kwa klabu ya zamani ya Lommel iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 angeanza katika mechi dhidi ya Tottenham Jumapili (Sun) THCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES Bayern Munich na Ajax wanaendelea kupigania sahihi ya Erik ten Hag, 54, kwa imani kwamba atafutwa kazi kama meneja wa Manchester United mwishoni mwa msimu huu(Mirror) Kipa wa Uhispania David Raya, 28, anasema hajafanya mazungumzo yoyote na Arsenal kuhusu iwapo watafanya uhamisho wake wa mkopo kutoka Brentford kuwa wa kudumu. (Express) Meneja wa Tottenham Ange Postecoglou ataweka kipaumbele kumsaini mshambuliaji mpya na kiungo wa safu ya ulinzi huku akipanga kuwaachilia wachezaji wengi msimu wa joto (Mirror) Ipswich wanasema wanafanya kila linalowezekana kusalia na meneja Kieran McKenna huku kukiwa na nia ya kumchukua kocha huyo kutoka kwa Brighton , Chelsea na Manchester United .(Teamtalk) THCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES Mkufunzi wa Chelsea Mauricio Pochettino anasema atafurahi kusalia na 80-85% ya kikosi chake msimu ujao(football.london) Mwenyekiti mwenza wa Arsenal Josh Kroenke amewaambia mashabiki "klabu haitasimama tuli" inapotafuta wachezaji ili kusaidia kupata taji la Uingereza na Ulaya(Goal) West Ham wanakaribia kumsajili mlinzi mwenye umri wa miaka 18 Mwingereza Luis Brown kutoka Arsenal(Caught Offside..##Sports view
    Like
    Love
    6
    · 5 Commentarios ·0 Acciones ·556 Views