Mise à niveau vers Pro

  • “Maandalizi yapo vizuri tunamshukuru mwenyezi Mungu, sisi kama Yanga SC tupo vizuri kabisa kwa mchezo. Tumefanya maandalizi makubwa na yapo sawa tuwaachie tu mashabiki waje uwanjani”

    “Sisi tunataka kwenda robo fainali ya CAF champions League, tunataka tuingie kwenye Top 5 ya klabu bora barani Afrika, kwa mujibu wa taratibu wa renki za klabu kwa ubora barani Afrika tukishinda kesho tunapata point 39 tunataka nafasi ya tano na inakuwa mara ya kwanza klabu ya Tanzania na Afrika mashariki kufika nafasi ya tano, tuna vitu vingi vyakutusukuma kwenda kupambana kesho kupata maatokeo mazuri”

    “Malengo makubwa ambayo viongozi waliyatoa mapema ni kufika tulipofika msimu uliopita yaani tukifika robo fainali tutakuwa tumefikia malengo yetu ya michuano ya kimataifa baada ya hapo gari itakuwa imekata breki ila atakayekuja mbele yeyote yule tutamfokea na kuruka naye sababu itakuwa tayari presha imeshaondoka”

    “Kwanza tumalize mchezo wa kesho kwa wana Yanga njooni tukajaze uwanja,tukamchinje mwarabu, na kuhusu mauzo ya tiketi yanakwenda vizuri” - Ally Kamwe Msemaji wa Klabu ya Yanga SC.

    “Maandalizi yapo vizuri tunamshukuru mwenyezi Mungu, sisi kama Yanga SC tupo vizuri kabisa kwa mchezo. Tumefanya maandalizi makubwa na yapo sawa tuwaachie tu mashabiki waje uwanjani” “Sisi tunataka kwenda robo fainali ya CAF champions League, tunataka tuingie kwenye Top 5 ya klabu bora barani Afrika, kwa mujibu wa taratibu wa renki za klabu kwa ubora barani Afrika tukishinda kesho tunapata point 39 tunataka nafasi ya tano na inakuwa mara ya kwanza klabu ya Tanzania na Afrika mashariki kufika nafasi ya tano, tuna vitu vingi vyakutusukuma kwenda kupambana kesho kupata maatokeo mazuri” “Malengo makubwa ambayo viongozi waliyatoa mapema ni kufika tulipofika msimu uliopita yaani tukifika robo fainali tutakuwa tumefikia malengo yetu ya michuano ya kimataifa baada ya hapo gari itakuwa imekata breki ila atakayekuja mbele yeyote yule tutamfokea na kuruka naye sababu itakuwa tayari presha imeshaondoka” “Kwanza tumalize mchezo wa kesho kwa wana Yanga njooni tukajaze uwanja,tukamchinje mwarabu, na kuhusu mauzo ya tiketi yanakwenda vizuri” - Ally Kamwe Msemaji wa Klabu ya Yanga SC.
    ·93 Vue
  • Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kuzifungia laini za simu 12,896 kutokana na kujihusisha na vitendo vya ulaghai wa mtandaoni kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

    Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabir Bakari amesema matukio ya ulaghai kwa njia ya simu yamepungua kwa asilimia 19 kutoka laini za simu 16,002 Julai na Septemba 2024 hadi 12,896 Oktoba na Desemba 2024, ikiwa ni punguzo la laini 3,106.
    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kuzifungia laini za simu 12,896 kutokana na kujihusisha na vitendo vya ulaghai wa mtandaoni kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabir Bakari amesema matukio ya ulaghai kwa njia ya simu yamepungua kwa asilimia 19 kutoka laini za simu 16,002 Julai na Septemba 2024 hadi 12,896 Oktoba na Desemba 2024, ikiwa ni punguzo la laini 3,106.
    ·54 Vue
  • Jay Melody amemchana Mwijaku kisa madai yake kuwa Diamond Platnumz akifanya collabo na Msanii wa Tanzania basi Msanii huyo anapokea.

    Mwijaku anadai kuwa toka Diamond Platnumz amshirikishe Jay Melody kwenye wimbo wa "Mapozi", Jay Melody amepotea mazima.

    Jay Melody amemchana Mwijaku kisa madai yake kuwa Diamond Platnumz akifanya collabo na Msanii wa Tanzania basi Msanii huyo anapokea. Mwijaku anadai kuwa toka Diamond Platnumz amshirikishe Jay Melody kwenye wimbo wa "Mapozi", Jay Melody amepotea mazima.
    Like
    1
    ·59 Vue
  • "The Unforgetable THROW BACK
    Ilikuwa mwaka 2003 takribani Miaka 22 iliyopita nikiwa naingia kwenye ukumbi wa DIAMOND JUBILEE - UPANGA kwa kusukuma Mkokoteni 'KiZALI LA MENTALI' feat @sir_nature kwenye uzinduzi wa Album yangu ya pili ya MAPINDUZI HALISI ambayo baadae ilikuja kutangazwa na KILIMANJARO MUSIC AWARDS wakati huo (sasa TMA) kuwa album bora ya HIP HOP kwa mwaka 2003, Nilikuwa nimezungukwa na MIILI VIBANDA (Bouncers) pamoja na Producer wangu bora wa muda wote Tanzania @majani187 of BONGO RECORDS na @solothang_aka_ulamaa

    NB: Ni wasanii wachache sana tuliokuwa na uwezo wa kuujaza ukumbi mkubwa wa DIAMOND JUBILEE na ukatapika kisawasawa
    Je wewe ulikuwa wapi kipindi hiki???" - Professor Jay, Msanii wa muziki Hip-hop Tanzania
    "The Unforgetable THROW BACK 🔥🔥🔥 Ilikuwa mwaka 2003 takribani Miaka 22 iliyopita nikiwa naingia kwenye ukumbi wa DIAMOND JUBILEE - UPANGA kwa kusukuma Mkokoteni 'KiZALI LA MENTALI' feat @sir_nature kwenye uzinduzi wa Album yangu ya pili ya MAPINDUZI HALISI ambayo baadae ilikuja kutangazwa na KILIMANJARO MUSIC AWARDS wakati huo (sasa TMA) kuwa album bora ya HIP HOP kwa mwaka 2003, Nilikuwa nimezungukwa na MIILI VIBANDA (Bouncers) pamoja na Producer wangu bora wa muda wote Tanzania @majani187 of BONGO RECORDS na @solothang_aka_ulamaa 👑 NB: Ni wasanii wachache sana tuliokuwa na uwezo wa kuujaza ukumbi mkubwa wa DIAMOND JUBILEE na ukatapika kisawasawa💪💪💪 Je wewe ulikuwa wapi kipindi hiki???" - Professor Jay, Msanii wa muziki Hip-hop Tanzania
    Like
    1
    ·60 Vue
  • Rais Samia Suluhu amemteua Prof. Othman Chande Othman kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kipindi cha pili.

    Rais Samia Suluhu amemteua Prof. Othman Chande Othman kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kipindi cha pili.
    Like
    2
    ·46 Vue
  • Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) leo limetangaza kuahirisha Mashindano ya Mataifa ya Afrika ya TotalEnergies (CHAN) yaliyokuwa yafanyike Kenya, Tanzania, na Uganda kuanzia Februari na sasa yatafanyika Agosti 2025.

    Taarifa ya CAF imekiri kwamba kumekuwa na maendeleo makubwa katika ujenzi na ukarabati wa viwanja vya michezo, maeneo ya mazoezi, hoteli, hospitali, na miundombinu mingine muhimu katika nchi hizo tatu kwa ajili ya mashindano hayo.

    Hata hivyo, wataalamu wa kiufundi na miundombinu wa CAF waliopo Kenya, Tanzania, na Uganda wameishauri CAF kwamba muda zaidi unahitajika ili kuhakikisha miundombinu inafikia viwango vinavyohitajika kwa ajili ya kuandaa mashindano yenye mafanikio.

    Rais wa CAF, Dkt. Patrice Motsepe, amesema: "Ninatoa shukrani za dhati kwa Rais William Ruto wa Kenya, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, na Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa uongozi wao, kujitolea, na maendeleo mazuri yaliyopatikana katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya soka. Nimevutiwa na kazi inayoendelea, na nina uhakika kwamba viwanja vya michezo, maeneo ya mazoezi, hoteli, hospitali, na miundombinu mingine itakidhi viwango vya CAF ifikapo Agosti 2025."

    CAF pia imetangaza kwamba droo ya CHAN Kenya, Tanzania, na Uganda 2024 itafanyika jijini Nairobi, Jumatano, Januari 15, 2025, saa mbili usiku kwa saa za Nairobi.

    Tarehe kamili ya kuanza kwa mashindano hayo mwezi Agosti 2025 itatangazwa na CAF katika siku zijazo.

    #neliudcosiah
    Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) leo limetangaza kuahirisha Mashindano ya Mataifa ya Afrika ya TotalEnergies (CHAN) yaliyokuwa yafanyike Kenya, Tanzania, na Uganda kuanzia Februari na sasa yatafanyika Agosti 2025. Taarifa ya CAF imekiri kwamba kumekuwa na maendeleo makubwa katika ujenzi na ukarabati wa viwanja vya michezo, maeneo ya mazoezi, hoteli, hospitali, na miundombinu mingine muhimu katika nchi hizo tatu kwa ajili ya mashindano hayo. Hata hivyo, wataalamu wa kiufundi na miundombinu wa CAF waliopo Kenya, Tanzania, na Uganda wameishauri CAF kwamba muda zaidi unahitajika ili kuhakikisha miundombinu inafikia viwango vinavyohitajika kwa ajili ya kuandaa mashindano yenye mafanikio. Rais wa CAF, Dkt. Patrice Motsepe, amesema: "Ninatoa shukrani za dhati kwa Rais William Ruto wa Kenya, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, na Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa uongozi wao, kujitolea, na maendeleo mazuri yaliyopatikana katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya soka. Nimevutiwa na kazi inayoendelea, na nina uhakika kwamba viwanja vya michezo, maeneo ya mazoezi, hoteli, hospitali, na miundombinu mingine itakidhi viwango vya CAF ifikapo Agosti 2025." CAF pia imetangaza kwamba droo ya CHAN Kenya, Tanzania, na Uganda 2024 itafanyika jijini Nairobi, Jumatano, Januari 15, 2025, saa mbili usiku kwa saa za Nairobi. Tarehe kamili ya kuanza kwa mashindano hayo mwezi Agosti 2025 itatangazwa na CAF katika siku zijazo. #neliudcosiah
    Like
    1
    ·93 Vue
  • Michuano ya CHAN yahairishwa, badala ya kufanyika Februari 2025 sasa yatafanyika Agosti 2025. Sababu ni kutokamiliaka kwa ujenzi wa miundombinu ya Viwanja katika Nchi wenyeji (Tanzania, Kenya na Uganda).
    Michuano ya CHAN yahairishwa, badala ya kufanyika Februari 2025 sasa yatafanyika Agosti 2025. Sababu ni kutokamiliaka kwa ujenzi wa miundombinu ya Viwanja katika Nchi wenyeji (Tanzania, Kenya na Uganda).
    Like
    Love
    3
    ·146 Vue
  • Jemedari

    Juzi nilipost kuwa yanga watashinda dhidi ya al hilal ya ibenge
    Watu wasio jua mpira wakanibeza kwa sababu yanga akiwa nyumbani alipoteza goli 2-0
    Wakajua akienda kule watakula nyingi zaidi

    Mashabiki na wapenzi wa yanga popote mlipo jipige kifua na mtambe
    Hii ni michuano mikubwa achana na ile ya kojoa ukalale

    Tim Bora Tanzania kwa sasa ni yanga

    Bin kazumary crown media

    #neliudcosiah

    Jemedari 🎤 Juzi nilipost kuwa yanga watashinda dhidi ya al hilal ya ibenge Watu wasio jua mpira wakanibeza kwa sababu yanga akiwa nyumbani alipoteza goli 2-0 Wakajua akienda kule watakula nyingi zaidi Mashabiki na wapenzi wa yanga popote mlipo jipige kifua na mtambe Hii ni michuano mikubwa achana na ile ya kojoa ukalale Tim Bora Tanzania kwa sasa ni yanga 🗣️Bin kazumary crown media #neliudcosiah
    Like
    Love
    2
    ·111 Vue
  • Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linatarajiwa kutoa Tuzo kwa Wachekeshaji bora wa mwaka 2024 kupitia TANZANIA COMEDY AWARDS 2024 zinazotarajiwa kuzinduliwa rasmi 14/2/2024

    Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linatarajiwa kutoa Tuzo kwa Wachekeshaji bora wa mwaka 2024 kupitia TANZANIA COMEDY AWARDS 2024 zinazotarajiwa kuzinduliwa rasmi 14/2/2024
    1 Commentaires ·78 Vue
  • Shida ni Kwamba watu hupokea taarifa KWA mihemko ila Tanzania na afrika mashariki hakuna defensive midfield kama khalid aucho na hata wanaocheza ndani ya ligi kuu hakuna na huyu ndo anafanya GUSA ACHIA TWENDE KWAO iwe Tamu San
    Na kocha jana aliona ni vipi akimtoa aucho mechi kadhaa timu inapoteza mvuto jana akaamua amuache asimguse kabisa
    Huyu ni KHALID AUCHO huyu ni JINJA MAESTRO
    Juzi mashabiki wa uganda walicomment kweny ukurasa wake na kumtakia mchezo mwema na wanasema wanataman aucho awaonyeshe nusu ya kiwango chake kweny timu ya taifa wakilinganisha na
    anachokionyesha yanga

    #neliudcosiah
    Shida ni Kwamba watu hupokea taarifa KWA mihemko ila Tanzania na afrika mashariki hakuna defensive midfield kama khalid aucho na hata wanaocheza ndani ya ligi kuu hakuna na huyu ndo anafanya GUSA ACHIA TWENDE KWAO iwe Tamu San Na kocha jana aliona ni vipi akimtoa aucho mechi kadhaa timu inapoteza mvuto jana akaamua amuache asimguse kabisa Huyu ni KHALID AUCHO huyu ni JINJA MAESTRO 💚💛💚💛 Juzi mashabiki wa uganda walicomment kweny ukurasa wake na kumtakia mchezo mwema na wanasema wanataman aucho awaonyeshe nusu ya kiwango chake kweny timu ya taifa wakilinganisha na anachokionyesha yanga #neliudcosiah
    Like
    1
    ·141 Vue
  • MOYO SAFI WA SADIO MANÉ NDIO SILAHA YA MAFANIKIO YAKE.

    Sadio Mané amesaidia mambo mengi sana katika Kijiji alichotoka mara Baada ya kupata mafanikio katika soka.

    Sadio Mané amezaliwa katika Kijiji Cha Bambali nchini Senegal,amekulia huko na wanakijiji wengi walimsapoti na kumuombea sana Dua za mafanikio kipindi anaenda rasmi ulaya kujaribu bahati yake katika kazi ya kucheza mpira wa miguu.

    Mungu Si Athumani wala Mzee Nkumilwa kijana akatoboa na maisha yakaanza kuwa safi kwa upande wake,lakini pamoja na yote hakuwasahau watu waliomfanya awe hapo Leo.

    Alianza kukata fungu kwenye Kila mshahara wake wa mwezi kwa ajili ya kusaidia Kijiji chake kutoka kuwa Cha kimasikini mpaka kuwa Cha maisha ya kati kabla ya kuwa Cha kitajiri kabisa.

    Baadae zile pesa alizokuwa anahifadhi kutoka kwenye Kila mshahara wake zilianza kufanya kazi vyema na kufanikisha kukamklisha vitu vifuatavyo:

    1. Alijenga hospital yenye thamani ya €530K sawa na pesa za kitanzania Billion Moja,million mia tatu sabini na mbili,laki tano na Elfu tisini na nne.

    2. Alijenga Shule yenye thamani ya €270K sawa na pesa za kitanzania Million mia sita tisa tisa,laki mbili na Elfu Arobaini na sita.

    3. Pia huwa anatoa kiasi Cha €70 Kwa Kila kaya iliyopo Katika Kijiji hicho kwa mwezi ambayo ni sawa na pesa za kitanzania Laki moja,Elfu themanini na Moja,mia mbili themanini na sita.

    4. Kutoa nguo za bure Kwa watoto wote waliopo ndani ya Kijiji hicho.

    5. Kufanikisha kupeleka internet yenye Kasi ya 4G katika Kijiji hicho.

    6. Kufanikisha kupeleka vituo vya gas katika Kijiji hicho akishirikiana na kampuni ya Oryx.

    7. Kajenga uwanja wa soka pia.

    NDIO MAANA ANAFANIKIWA KILA ANAPOENDA HATA KAMA AKISEMEWA MABAYA KUNA WENGI WAPO NYUMA YAKE WANAMUOMBEA MEMA

    #neliudcosiah
    MOYO SAFI WA SADIO MANÉ NDIO SILAHA YA MAFANIKIO YAKE. Sadio Mané amesaidia mambo mengi sana katika Kijiji alichotoka mara Baada ya kupata mafanikio katika soka. Sadio Mané amezaliwa katika Kijiji Cha Bambali nchini Senegal,amekulia huko na wanakijiji wengi walimsapoti na kumuombea sana Dua za mafanikio kipindi anaenda rasmi ulaya kujaribu bahati yake katika kazi ya kucheza mpira wa miguu. Mungu Si Athumani wala Mzee Nkumilwa kijana akatoboa na maisha yakaanza kuwa safi kwa upande wake,lakini pamoja na yote hakuwasahau watu waliomfanya awe hapo Leo. Alianza kukata fungu kwenye Kila mshahara wake wa mwezi kwa ajili ya kusaidia Kijiji chake kutoka kuwa Cha kimasikini mpaka kuwa Cha maisha ya kati kabla ya kuwa Cha kitajiri kabisa. Baadae zile pesa alizokuwa anahifadhi kutoka kwenye Kila mshahara wake zilianza kufanya kazi vyema na kufanikisha kukamklisha vitu vifuatavyo: 1. Alijenga hospital yenye thamani ya €530K sawa na pesa za kitanzania Billion Moja,million mia tatu sabini na mbili,laki tano na Elfu tisini na nne. 2. Alijenga Shule yenye thamani ya €270K sawa na pesa za kitanzania Million mia sita tisa tisa,laki mbili na Elfu Arobaini na sita. 3. Pia huwa anatoa kiasi Cha €70 Kwa Kila kaya iliyopo Katika Kijiji hicho kwa mwezi ambayo ni sawa na pesa za kitanzania Laki moja,Elfu themanini na Moja,mia mbili themanini na sita. 4. Kutoa nguo za bure Kwa watoto wote waliopo ndani ya Kijiji hicho. 5. Kufanikisha kupeleka internet yenye Kasi ya 4G katika Kijiji hicho. 6. Kufanikisha kupeleka vituo vya gas katika Kijiji hicho akishirikiana na kampuni ya Oryx. 7. Kajenga uwanja wa soka pia. NDIO MAANA ANAFANIKIWA KILA ANAPOENDA HATA KAMA AKISEMEWA MABAYA KUNA WENGI WAPO NYUMA YAKE WANAMUOMBEA MEMA ♥️📌 #neliudcosiah
    Like
    1
    ·140 Vue
  • Licha ya jana Klabu ya Yanga SC kushinda mechi yake muhimu dhidi ya timu ngumu ya Al Hilal omdurman lakini kuna huyu mwamba wa kuitwa Jean Claude Giramugisha, hapa kibwana Shomari nahisi usingizi wake ulikuwa wa Mashaka (kuweweseka) maana sio kwa kuburuzwa kule

    Dogo ana speed ya ajabu mpaka nikasema dah huyu sio ndo yule kasongo lakini? achana na speed ana vyenga pia ana pumzi hachoki, Kuna muda akuwa upande wa kushoto kumxhosha kibwana sometime anabadilishana possition na adama Coulibaly, anaenda tena kumnyanyasa Shadrack Boka

    Cha ajabu huyu dogo ni mburundi tuh sijui Tanzania tulicherewa nini kusema huyu dogo ni MUHA wa Kigoma na akatupa faida Tanzania kwenye NT na vilabu

    Oya huyu dogo ni moto

    #muslehelbarcaupdates

    #Alhilalomdurman #CAFChampionsLeague #TotalEnergiesCAFCL
    Licha ya jana Klabu ya Yanga SC kushinda mechi yake muhimu dhidi ya timu ngumu ya Al Hilal omdurman lakini kuna huyu mwamba wa kuitwa Jean Claude Giramugisha, hapa kibwana Shomari nahisi usingizi wake ulikuwa wa Mashaka (kuweweseka) maana sio kwa kuburuzwa kule 🙄 Dogo ana speed ya ajabu mpaka nikasema dah huyu sio ndo yule kasongo lakini? achana na speed ana vyenga pia ana pumzi hachoki, Kuna muda akuwa upande wa kushoto kumxhosha kibwana sometime anabadilishana possition na adama Coulibaly, anaenda tena kumnyanyasa Shadrack Boka 🔥 Cha ajabu huyu dogo ni mburundi tuh sijui Tanzania tulicherewa nini kusema huyu dogo ni MUHA wa Kigoma na akatupa faida Tanzania kwenye NT na vilabu 😂 Oya huyu dogo ni moto 🔥 #muslehelbarcaupdates 👽 #Alhilalomdurman #CAFChampionsLeague #TotalEnergiesCAFCL
    Love
    1
    1 Commentaires ·195 Vue
  • "Wolper aliwahi kuniomba hela ya mtaji nikachukua milioni 30 nikampa ila cha kusikitisha akaenda kula pesa hizo na bishoo mmoja mwenye sura nzuri nzuri anaitwa Rich Mitindo. Alipokuwa China nikawa naona anapiga picha nyingi nyingi na jamaa, nilipomuuliza akawa anajibu "hakuna kitu babe huyu ni mdogo wangu tu" - Harmonize, Msanii wa muziki Tanzania.

    "Wolper aliwahi kuniomba hela ya mtaji nikachukua milioni 30 nikampa ila cha kusikitisha akaenda kula pesa hizo na bishoo mmoja mwenye sura nzuri nzuri anaitwa Rich Mitindo. Alipokuwa China nikawa naona anapiga picha nyingi nyingi na jamaa, nilipomuuliza akawa anajibu "hakuna kitu babe huyu ni mdogo wangu tu" - Harmonize, Msanii wa muziki Tanzania.
    Like
    1
    ·87 Vue
  • Kila la heri @SimbaSCTanzania kwenye mchezo wa leo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

    @CAF_Online @CAFCLCC @ligikuu
    Kila la heri @SimbaSCTanzania kwenye mchezo wa leo wa Kombe la Shirikisho Afrika. @CAF_Online @CAFCLCC @ligikuu
    Like
    2
    1 Commentaires ·111 Vue
  • CAF CONFEDERATION CUP

    FC BRAVOS SIMBA SC
    01:00 usiku
    11 de Novembro

    Ni mechi ya mapema. Itapigwa pale nchini Angola. Wote wawili hapa wana nafasi ya kufuzu. Wanatofautiana pointi tatu tu, Ushindi au sare tu, kwa Simba utaifanya ifuzu moja kwa moja robo fainali. Kila la kheri Mnyama #simbasctanzania

    #paulswai
    CAF CONFEDERATION CUP 🇦🇴 FC BRAVOS 🆚 SIMBA SC 🇹🇿 ⏰ 01:00 usiku 🏟️ 11 de Novembro Ni mechi ya mapema. Itapigwa pale nchini Angola. Wote wawili hapa wana nafasi ya kufuzu. Wanatofautiana pointi tatu tu, Ushindi au sare tu, kwa Simba utaifanya ifuzu moja kwa moja robo fainali. Kila la kheri Mnyama #simbasctanzania 🇹🇿🇹🇿 #paulswai
    Like
    3
    ·213 Vue
  • OPERATION ENTEBBE -4

    Katika sehemmu iliyopita nilieleza namna ambavyo baada ya madege ya kivita ya Lockheed Harcules C-130 kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe na moja ya ndege hizo kwenda moja kwa moja karibu na geti la Terminal huku mlango wa nyuma ukiwa wazi na kutoka gari aina na Mercides pamoja na Land Rover kufanana kabisa na msafara wa Idd Amin atembeleapo uwanja wa ndege, la kini ajabu ni kwamba walijikuta wakinyooshewa bunduki na wanajeshi waliokuwa wanalinda getini…
    Walikuwa hawana taarifa kuwa Amin alikuwa amebadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi kwenda nyeupe kabla ya safari yake ya kwenda Mauritius kwenye kikao cha O.A.U.
    Tuendelee…
    SEHEMU TA NNE
    Wanajeshi hawa wawili wa Uganda waliokuwa getini walinyanyua bunduki zao aina ya Kalashnikov na hawakuonyesha dalili kwamba labda walikuwa wanataka kufanya ukaguzi wa kawaida tu kabla ya kuwaruhusu, walionyesha dhahiri kabisa kwamba walikuwa wanataka kufanya shambulio.
    Kabla wanajeshi hao wa Uganda kufanya lolote lile, Netanyahu na komando mwingine ambao walikuwa ndani ya gari walitumia weledi wao kufanya uamuzi makini wa haraka kwa kufyatua risasi kutoka kwenye bastola zao zenye ‘silencer’ na mara moja wale wanajeshi wawili wa Uganda walienda chini.
    Lakini moja ya wale wanajeshi wa Uganda waliodondoka chini baada ya kufyatuliwa risasi, hakufa mara moja na alikuwa anajitahidi kuinuka. Hii ilisababisha komando mwingine wa Israel kufyatua risasi lakini safari hii huyu komando wa Israel alifyatua risasi kutoka kwenye bunduki ambayo haina ‘silencer’. Hii iliwashitua wanajeshi wengine wa Uganda waliokuwa nje ya Terminal na kuanza kukimbilia walipokuwa wanasikia milio ya risasi inatokea huku wanafyatua risasi.
    Kwa maneno mengine ilikuwa kwa kiasi fulani walichokuwa wamekipanga makomando wa Israel, kufanya shambulio la kushitukiza lakini mpaka muda huu tayari ile ‘element of surprise’ ilikuwa haipo tena, jeshi la Uganda lilikuwa limeshitukia ‘mchezo’.
    Bila kuchelewa sana, makomando wote walikuwa kwenye zile gari mbili (Mercedes na Land Rover) waliruka nje ya gari na kukimbia kuelekea ndani ya terminal.
    Vichwani mwao walikuwa bado hawajaondokewa na kumbukumbu ya oparesheni kama hii iliyotokea miaka miwili iliyopita nchini Israel kwenye mji wa Ma’a lot ambapowatekaji wa KIpalestina baada ya kushituka kuwa kulikuwa na makomando wa Israel wamefika kufanya uokozi, waliwapiga risasi mateka wao 25 ambao kati yao 22 walikuwa ni watoto wadogo.
    Hivyo Netanyahu na wenzake hawakutaka kitu kama hiki kjitokeze tena… Netenyahu na makomando wenzake wa Syeret Matkal kwa ustadi wa hali ya juu walikimbia na kuingia ndani ya terminal na kuwaacha vile vikosi vingine kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliopo nje ya terminal (kama nilivyoeleza juzi namna kikosi kilivyogawanywa kwenye vikundi vidogo kila kimoja kikipewa jukumu lake).
    Mateka wanaeleza kwamba baada ya mpambano ya risasi kuanza huko nje ya terminal waliwaona watekaji kadhaa wakiongozwa na yule aliyeonekana kama kiongozi wao, Wilfred Bose waliingia ndani ya terminal wakiwa wanahaha kama wamechanganyikiwa wasijue wafanye nini, ilionekana dhahiri kuwa walikuwa hawajajiandaa kwa hili shambulio la ghafla, ilionekana dhahiri kwamba katika akili yao walikuwa wanasubiria Israel kutimiza masharti yao ili waweze kuachia mateka.
    Kuna muda Wilfred Bose alionekana kunyoonya bunduki yake kwa mateka kama vile anawataka kuwamininia risasi lakini alikuwa anashindwa kufanya uamuzi huo. Bose aligeuka ghafla baada ya kusikia kishindo cha mlango wa terminal ukifunguliwa.
    Makomando wa Israel walikuwa wametumia weledi na ustadi wao wa hali ya juu kuingia ndani ya terminal kwa muda sahihi kabla ya Wilfred Bose na wenzake kufanya uamuzi wowote wa kuua mateka.
    Makomando wa Israel walipoingia tu ndani ya terminal, mmoja wao mkononi walikuwa na kipaza sauti aina ya ‘megaphone’ na alikuwa anaongeea kwa nguvu kwa lugha ya kihebrania, “Lay down, Lay down. We are Israel soldiers. Lay down. Lay down!!”.
    Mateka wote wa kiisrael hata wale waliokuwa wamekaa kitako walilala chini, hivyo ndani ya sekunde chache tu kila mtu ambaye alibakia amesimama alikuwa ni halali yao kumtandika risasi.
    Kwa bahati mbaya kulikuwa na mateka kadhaa ambao wwalikuwa hawajui kihebreania sawia na hii iliwagharimu sana. Kwa mfano kulikuwa na kijana wa mika 19 aliyeitwa Jean-Jacques Maimoni, huyu alikuwa amehamia Israel siku si nyingi sana kutokea nchini ufaransa. Lilipotolewa tangazo hilo la kila mtu kulala chini hakuelewa na alibakia akiwa amesimama na alitandikwa risasi na makomando wa Israel pamoja na wale watekaji. Kijana huyu hakuwa peke yake, lakini pia kulikuwa na mateka mwingine aliyeitwa Ida Borochovitch, ambaye alihamia Israel kutoka nchini Urusi.
    Risasi zilirindima kwa takribani dakika mbili nzima na baadae ukimya wa kama sekunde 15 ukatawala na moja wa makomando wa kiisrael akauliza kwa kiebrania, “where are the rest of them?” (“wako wapi wengine?”). Mateka wakaonyesha kidole kwenye chumba kidogo kilichopo pembeni.
    Makomando wakarusha mabomu kadhaa ya kutupa kwa mkono na kisha kuingia ndani ya chumba hicho na kuwamiminia risasi wote ambao walikuwa humo.
    Milio ya risasi ndani ya terminal hatimaye ilikuwa imekoma japo bado huko nje walisikia majibizano ya risasi. Mwanajeshi mmoja wa Israel kati ya wale waliopo ndani ya terminal, kwa sauti ya utulivu kabisa na katika lugha ya kihebrania aliwatangazia mateka, “listen guys, we’ve come to take you home!” (“sikilizeni, tumekuja kuwachukua kuwarudisha nyumbani!”).
    Baada ya hapo makomando walianza kuwatoa mateka kutoka kwenye terminal na kuwapakia kwenye ndege kwa tahadhari kubwa huku wale wenzao wengine wakiendelea kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanarusha risasi kutoka kwenye maeneo ya kujificha ndani ya uwanja wa ndege.
    Wakiwa wanaendelea kuwapakia mateka waliowaokoa kwenye ndege, kumbe kulikuwa na mwanajeshi wa Uganda amebakia juu kwenye mnara wa uongozaji (airport control tower). Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibunui kutoka kwa mtoto wa Idd Amin anasema kwamba mwanajeshi huyu alikuwa ni binamu wa Idd Amin. Kutokea hapo kwenye mnara alimimina risasi mfululizo kwa makomando wa Israel na moja ya risasi hizi ilimpaka Koamando Yonatan Netanyahu ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Matkal iliyopo hapoa na alipoteza uhai pale pale.
    Wanajeshi wa Isarel walijibu mapigo kwa kurusha bomu la roketi ndogo ya begani na kusambaratisha kabisa kiota cha mnara na kumuua mwanajeshi wa Uganda aliyekuwa anawashambulia.
    Baada ya hapo waliwapakia kwenye ndege mateka wote ambao waliokolewa pamoja na miili ya Waisrael ambao walifariki kwenye majibizano hayo ya risasi.
    Kisha ili kuhakikisha kuwa hakuna ndege itakayowafuatia nyuma wakiondoka au kushambuliwa, walilipua ndege zote za jeshi la Uganda ambazo zilikuwa uwanjani hapo.
    Oparesheni yote hii ilichukua takribani dakika 53 ambapo dakika 30 pekee ndio zilikuwa za mapigano na 23 zilizosalia zilikuwa za kupakia mateka walio okolewa na kuondoka.
    Mpaka kufikia mwishio mwa oparesheni, jumla ya watekaji wote 7 walikuwa wameuwawa, pia wanajeshi 45 wa jeshi la Uganda walikuwa wameuwawa pia. Lakini pia ndege za kijeshi 11 aina ya MiG-17 na Mig-21 zililipuliwa na makomando wa Isarel. Ikumbukwe kwamba ndege hizi ndizo zilikuwa ni ndege zote za kijeshi ambazo zilikuwa zinamilikiwa na jeshi la anga la Uganda. Hii inaonyesha moja kati ya mapungufu makubwa ya kiuongozi ya Amin. Hakukuwa na busara yoyote au faida yoyote ya kimkakati kuweka ndege zote za jeshi lako la anga kwenye uwanja wa ndege wa kiraia ili kulinda mateka wa tukio ambalo wengine walikuwa wanaweza kuliona kama tukio la kigaidi na kwa namna Fulani kama ugomvi ambao ulikuwa haumuhusu moja kwa moja.
    Katika mateka wote 106 waliobakia (kumbuka nilieleza kuwa kulikuwa na mikupuo miwili ya mateka wasio wa Kiisrael au asili ya Kiyahudi waliachiwa kwa kupelekwa na ndege ufaransa nchini), kwahiyo kati ya wale 106 waliobakio, mateka watatu waliuwawa muda wa mapambano (hawa ndio wale ambao walikuwa hawaelewi kihebrania kwa ufasaha na kwa hiyo hawakulalala chini kama ilivyoamrishwa na makomando wa Israel), na mateka mmoja bibi wa miaka 74 aliyeitwa Dora Bloch aliachwa akiwa Hospitali mjini Entebbe ambako alipelekwa na Amin siku kadhaa nyuma kutokana na kuhitaji uangalizi maalumu wa kidaktari.
    Kati ya Makomando wa Isarel, ni mmoja tu ndiye aliuwawa tena dakika za mwisho (Yonatan Netanyahu) japo pia kuna makomando wengine kama watano ambao walijeruhiwa. Kifo cha kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Mitkal, Yonatan Netanyahu katika oparesheni hii ndio iliyofanya siku kadhaa baadae oparesheni hii pia kubatizwa jina la OPERATION YONATAN kwa heshima yake na ushujaa wake wa kutoa maisha yake ili kutetea na kuooa roho za raia alioapa kuwalinda.
    Baada ya kila kitu kuwekwa sawa na watu wote kupanda ndani ya ndege, waliruka mpaka Nairobi Kenya kwa mapumziko mafupi ili kutibia wale ambao walijeruhiwa (kama ambavyo nilieleza kuwa ile moja ya Boeing 707 iliyotengwa kama ‘hospitali’ ilibaki Nairobi).
    Baada ya matibabu hapo Nairobi, madege yote yaliruka kurudi Israel. Kwa kifupi operation hii was a big SUCCESS.!
    Japokuwa baada ya ulimwengu mzima kutangaziwa juu ya kilichotokea, juu ya ‘umafia’ uliofanywa na Israel, ulimwengu uligawanyika kila nchi ukiunga mkono upande fulani, lakini nchi nyingi ziliunga mkono Israel kwa matumizi ya jeshi katika nchi nyingine, wengi walimlaumu Amin kwa kushindwa kutumia diplomasia kumaliza mzozo huu. Ajabu ni kwamba mwezi huo wa July, Mkuu wa Majeshi wa Iran moja wa mahsimu wa siku zote wa Israel aliandika barua kwa Waziri mkuu wa Israel kumpongeza kuhusu Oparation hiyo na kumpa pole kwa kifo cha Yonatan Netanyahu akimuita Yonatan kumsifu kuwa ni ‘martyr’.
    Vyovyote vile ambavyo unaweza kuitazama oparesheni hii kwenye jicho la kisiasa ua kidiplomasia, kwamba kama ilikuwa ni sahihi au si sahihi lakini katika jicho la kijeshi na ujasusi hii ni moja ya oparesheni murua kabisa kuwahi kufanyika katika historia ya majeshi duniani. Moja ya manguli wa “ulimwengu wa giza”, Bw. Henry Kissinger aliwahi kutamka kuwa hii ilikuwa ni “an immposible mission”!
    Umaridadi wa oparesheni hii umefanya hata vitengo kadhaa vya weledi vya majeshi mbali mbali kutaka kuiga mfano wake lakini bila mafanikio yoyote. Kwa mfano Wamarekani walijaribu kuiga umaridadi wa Oparesheni hii na kufanya ya kwao iliyoitwa Oparation Eagle Claw baada ya kutokea kwa utekeaji kwenye ubalozi wa Iran lakini oparesheni hiyo ilifeli vibaya.
    Sasa hivi kama wewe ni mwanajeshi katika jeshi fulani kwenye kitengo cha weledi (special force) au labda ni jasusi maalumu, lazima katika hatua fulani ya japo hata ‘darasani’ kwenye makaratasi utafundwa kuhusu Oparetion Entebbe na namna ilivyo tekelezwa.
    Oparesheni hii ilimuacha Amin na aibu kubwa kiasi kwamba akaendelea kufanya vitu ambavyo vilidhihirisha udhaifu wake wa kiungozi. Kwa mfano, yule bibi wa miaka 74 aliyeachwa hospitali mjini Entebbe, aliamuru auwawe kinyama. Lakini pia Amin alisimami kuwawa kwa McKenzie yule waziri wa kilimo wa Kenya ambaye alimsaidia Ehud Barak kumshinikiza Mzee Jomo Kenyetta kuruhusu ndege za jeshi la Israel kutumia viwanja vya ndege vya Kenya wakati wa utekelezaji wa OParesheni hiyo na pia kumsaidi kukusanya Intelijensia kwa kutumia ndege yake binafsi.
    McKenzie aliuwawa kwa bomu lililotegwa kwenye gari yake.
    Pia Amin alisimamia ulipuaji kwa bomu moja ya hoteli kubwa Nairobi kipindi hicho ambayo ilikuwa inaitwa The Norfolk Hotel, ambayo ilimilikiwa na moja ya wayahudi mashuhuri nchini Kenya.
    [6/12, 13:48] The Bold: Licha ya ‘fujo’ zote hizi ambazo Amin alizifanya baada ya jeshi lake kudhalilika kutokana na Oeration Entebbe lakini hatupawsi kusahau kwamba chini ya miaka mitatu baadae, yaani baada ya utekelezaji wa opareshini hii, Idd Amin aliondolewa kwa aibu madarakani na majeshi ya Tanzania na kumfanya akimbie nchi yake.

    ......................MWISHO..............
    #TheBOLD_JF
    OPERATION ENTEBBE -4 Katika sehemmu iliyopita nilieleza namna ambavyo baada ya madege ya kivita ya Lockheed Harcules C-130 kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe na moja ya ndege hizo kwenda moja kwa moja karibu na geti la Terminal huku mlango wa nyuma ukiwa wazi na kutoka gari aina na Mercides pamoja na Land Rover kufanana kabisa na msafara wa Idd Amin atembeleapo uwanja wa ndege, la kini ajabu ni kwamba walijikuta wakinyooshewa bunduki na wanajeshi waliokuwa wanalinda getini… Walikuwa hawana taarifa kuwa Amin alikuwa amebadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi kwenda nyeupe kabla ya safari yake ya kwenda Mauritius kwenye kikao cha O.A.U. Tuendelee… SEHEMU TA NNE Wanajeshi hawa wawili wa Uganda waliokuwa getini walinyanyua bunduki zao aina ya Kalashnikov na hawakuonyesha dalili kwamba labda walikuwa wanataka kufanya ukaguzi wa kawaida tu kabla ya kuwaruhusu, walionyesha dhahiri kabisa kwamba walikuwa wanataka kufanya shambulio. Kabla wanajeshi hao wa Uganda kufanya lolote lile, Netanyahu na komando mwingine ambao walikuwa ndani ya gari walitumia weledi wao kufanya uamuzi makini wa haraka kwa kufyatua risasi kutoka kwenye bastola zao zenye ‘silencer’ na mara moja wale wanajeshi wawili wa Uganda walienda chini. Lakini moja ya wale wanajeshi wa Uganda waliodondoka chini baada ya kufyatuliwa risasi, hakufa mara moja na alikuwa anajitahidi kuinuka. Hii ilisababisha komando mwingine wa Israel kufyatua risasi lakini safari hii huyu komando wa Israel alifyatua risasi kutoka kwenye bunduki ambayo haina ‘silencer’. Hii iliwashitua wanajeshi wengine wa Uganda waliokuwa nje ya Terminal na kuanza kukimbilia walipokuwa wanasikia milio ya risasi inatokea huku wanafyatua risasi. Kwa maneno mengine ilikuwa kwa kiasi fulani walichokuwa wamekipanga makomando wa Israel, kufanya shambulio la kushitukiza lakini mpaka muda huu tayari ile ‘element of surprise’ ilikuwa haipo tena, jeshi la Uganda lilikuwa limeshitukia ‘mchezo’. Bila kuchelewa sana, makomando wote walikuwa kwenye zile gari mbili (Mercedes na Land Rover) waliruka nje ya gari na kukimbia kuelekea ndani ya terminal. Vichwani mwao walikuwa bado hawajaondokewa na kumbukumbu ya oparesheni kama hii iliyotokea miaka miwili iliyopita nchini Israel kwenye mji wa Ma’a lot ambapowatekaji wa KIpalestina baada ya kushituka kuwa kulikuwa na makomando wa Israel wamefika kufanya uokozi, waliwapiga risasi mateka wao 25 ambao kati yao 22 walikuwa ni watoto wadogo. Hivyo Netanyahu na wenzake hawakutaka kitu kama hiki kjitokeze tena… Netenyahu na makomando wenzake wa Syeret Matkal kwa ustadi wa hali ya juu walikimbia na kuingia ndani ya terminal na kuwaacha vile vikosi vingine kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliopo nje ya terminal (kama nilivyoeleza juzi namna kikosi kilivyogawanywa kwenye vikundi vidogo kila kimoja kikipewa jukumu lake). Mateka wanaeleza kwamba baada ya mpambano ya risasi kuanza huko nje ya terminal waliwaona watekaji kadhaa wakiongozwa na yule aliyeonekana kama kiongozi wao, Wilfred Bose waliingia ndani ya terminal wakiwa wanahaha kama wamechanganyikiwa wasijue wafanye nini, ilionekana dhahiri kuwa walikuwa hawajajiandaa kwa hili shambulio la ghafla, ilionekana dhahiri kwamba katika akili yao walikuwa wanasubiria Israel kutimiza masharti yao ili waweze kuachia mateka. Kuna muda Wilfred Bose alionekana kunyoonya bunduki yake kwa mateka kama vile anawataka kuwamininia risasi lakini alikuwa anashindwa kufanya uamuzi huo. Bose aligeuka ghafla baada ya kusikia kishindo cha mlango wa terminal ukifunguliwa. Makomando wa Israel walikuwa wametumia weledi na ustadi wao wa hali ya juu kuingia ndani ya terminal kwa muda sahihi kabla ya Wilfred Bose na wenzake kufanya uamuzi wowote wa kuua mateka. Makomando wa Israel walipoingia tu ndani ya terminal, mmoja wao mkononi walikuwa na kipaza sauti aina ya ‘megaphone’ na alikuwa anaongeea kwa nguvu kwa lugha ya kihebrania, “Lay down, Lay down. We are Israel soldiers. Lay down. Lay down!!”. Mateka wote wa kiisrael hata wale waliokuwa wamekaa kitako walilala chini, hivyo ndani ya sekunde chache tu kila mtu ambaye alibakia amesimama alikuwa ni halali yao kumtandika risasi. Kwa bahati mbaya kulikuwa na mateka kadhaa ambao wwalikuwa hawajui kihebreania sawia na hii iliwagharimu sana. Kwa mfano kulikuwa na kijana wa mika 19 aliyeitwa Jean-Jacques Maimoni, huyu alikuwa amehamia Israel siku si nyingi sana kutokea nchini ufaransa. Lilipotolewa tangazo hilo la kila mtu kulala chini hakuelewa na alibakia akiwa amesimama na alitandikwa risasi na makomando wa Israel pamoja na wale watekaji. Kijana huyu hakuwa peke yake, lakini pia kulikuwa na mateka mwingine aliyeitwa Ida Borochovitch, ambaye alihamia Israel kutoka nchini Urusi. Risasi zilirindima kwa takribani dakika mbili nzima na baadae ukimya wa kama sekunde 15 ukatawala na moja wa makomando wa kiisrael akauliza kwa kiebrania, “where are the rest of them?” (“wako wapi wengine?”). Mateka wakaonyesha kidole kwenye chumba kidogo kilichopo pembeni. Makomando wakarusha mabomu kadhaa ya kutupa kwa mkono na kisha kuingia ndani ya chumba hicho na kuwamiminia risasi wote ambao walikuwa humo. Milio ya risasi ndani ya terminal hatimaye ilikuwa imekoma japo bado huko nje walisikia majibizano ya risasi. Mwanajeshi mmoja wa Israel kati ya wale waliopo ndani ya terminal, kwa sauti ya utulivu kabisa na katika lugha ya kihebrania aliwatangazia mateka, “listen guys, we’ve come to take you home!” (“sikilizeni, tumekuja kuwachukua kuwarudisha nyumbani!”). Baada ya hapo makomando walianza kuwatoa mateka kutoka kwenye terminal na kuwapakia kwenye ndege kwa tahadhari kubwa huku wale wenzao wengine wakiendelea kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanarusha risasi kutoka kwenye maeneo ya kujificha ndani ya uwanja wa ndege. Wakiwa wanaendelea kuwapakia mateka waliowaokoa kwenye ndege, kumbe kulikuwa na mwanajeshi wa Uganda amebakia juu kwenye mnara wa uongozaji (airport control tower). Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibunui kutoka kwa mtoto wa Idd Amin anasema kwamba mwanajeshi huyu alikuwa ni binamu wa Idd Amin. Kutokea hapo kwenye mnara alimimina risasi mfululizo kwa makomando wa Israel na moja ya risasi hizi ilimpaka Koamando Yonatan Netanyahu ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Matkal iliyopo hapoa na alipoteza uhai pale pale. Wanajeshi wa Isarel walijibu mapigo kwa kurusha bomu la roketi ndogo ya begani na kusambaratisha kabisa kiota cha mnara na kumuua mwanajeshi wa Uganda aliyekuwa anawashambulia. Baada ya hapo waliwapakia kwenye ndege mateka wote ambao waliokolewa pamoja na miili ya Waisrael ambao walifariki kwenye majibizano hayo ya risasi. Kisha ili kuhakikisha kuwa hakuna ndege itakayowafuatia nyuma wakiondoka au kushambuliwa, walilipua ndege zote za jeshi la Uganda ambazo zilikuwa uwanjani hapo. Oparesheni yote hii ilichukua takribani dakika 53 ambapo dakika 30 pekee ndio zilikuwa za mapigano na 23 zilizosalia zilikuwa za kupakia mateka walio okolewa na kuondoka. Mpaka kufikia mwishio mwa oparesheni, jumla ya watekaji wote 7 walikuwa wameuwawa, pia wanajeshi 45 wa jeshi la Uganda walikuwa wameuwawa pia. Lakini pia ndege za kijeshi 11 aina ya MiG-17 na Mig-21 zililipuliwa na makomando wa Isarel. Ikumbukwe kwamba ndege hizi ndizo zilikuwa ni ndege zote za kijeshi ambazo zilikuwa zinamilikiwa na jeshi la anga la Uganda. Hii inaonyesha moja kati ya mapungufu makubwa ya kiuongozi ya Amin. Hakukuwa na busara yoyote au faida yoyote ya kimkakati kuweka ndege zote za jeshi lako la anga kwenye uwanja wa ndege wa kiraia ili kulinda mateka wa tukio ambalo wengine walikuwa wanaweza kuliona kama tukio la kigaidi na kwa namna Fulani kama ugomvi ambao ulikuwa haumuhusu moja kwa moja. Katika mateka wote 106 waliobakia (kumbuka nilieleza kuwa kulikuwa na mikupuo miwili ya mateka wasio wa Kiisrael au asili ya Kiyahudi waliachiwa kwa kupelekwa na ndege ufaransa nchini), kwahiyo kati ya wale 106 waliobakio, mateka watatu waliuwawa muda wa mapambano (hawa ndio wale ambao walikuwa hawaelewi kihebrania kwa ufasaha na kwa hiyo hawakulalala chini kama ilivyoamrishwa na makomando wa Israel), na mateka mmoja bibi wa miaka 74 aliyeitwa Dora Bloch aliachwa akiwa Hospitali mjini Entebbe ambako alipelekwa na Amin siku kadhaa nyuma kutokana na kuhitaji uangalizi maalumu wa kidaktari. Kati ya Makomando wa Isarel, ni mmoja tu ndiye aliuwawa tena dakika za mwisho (Yonatan Netanyahu) japo pia kuna makomando wengine kama watano ambao walijeruhiwa. Kifo cha kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Mitkal, Yonatan Netanyahu katika oparesheni hii ndio iliyofanya siku kadhaa baadae oparesheni hii pia kubatizwa jina la OPERATION YONATAN kwa heshima yake na ushujaa wake wa kutoa maisha yake ili kutetea na kuooa roho za raia alioapa kuwalinda. Baada ya kila kitu kuwekwa sawa na watu wote kupanda ndani ya ndege, waliruka mpaka Nairobi Kenya kwa mapumziko mafupi ili kutibia wale ambao walijeruhiwa (kama ambavyo nilieleza kuwa ile moja ya Boeing 707 iliyotengwa kama ‘hospitali’ ilibaki Nairobi). Baada ya matibabu hapo Nairobi, madege yote yaliruka kurudi Israel. Kwa kifupi operation hii was a big SUCCESS.! Japokuwa baada ya ulimwengu mzima kutangaziwa juu ya kilichotokea, juu ya ‘umafia’ uliofanywa na Israel, ulimwengu uligawanyika kila nchi ukiunga mkono upande fulani, lakini nchi nyingi ziliunga mkono Israel kwa matumizi ya jeshi katika nchi nyingine, wengi walimlaumu Amin kwa kushindwa kutumia diplomasia kumaliza mzozo huu. Ajabu ni kwamba mwezi huo wa July, Mkuu wa Majeshi wa Iran moja wa mahsimu wa siku zote wa Israel aliandika barua kwa Waziri mkuu wa Israel kumpongeza kuhusu Oparation hiyo na kumpa pole kwa kifo cha Yonatan Netanyahu akimuita Yonatan kumsifu kuwa ni ‘martyr’. Vyovyote vile ambavyo unaweza kuitazama oparesheni hii kwenye jicho la kisiasa ua kidiplomasia, kwamba kama ilikuwa ni sahihi au si sahihi lakini katika jicho la kijeshi na ujasusi hii ni moja ya oparesheni murua kabisa kuwahi kufanyika katika historia ya majeshi duniani. Moja ya manguli wa “ulimwengu wa giza”, Bw. Henry Kissinger aliwahi kutamka kuwa hii ilikuwa ni “an immposible mission”! Umaridadi wa oparesheni hii umefanya hata vitengo kadhaa vya weledi vya majeshi mbali mbali kutaka kuiga mfano wake lakini bila mafanikio yoyote. Kwa mfano Wamarekani walijaribu kuiga umaridadi wa Oparesheni hii na kufanya ya kwao iliyoitwa Oparation Eagle Claw baada ya kutokea kwa utekeaji kwenye ubalozi wa Iran lakini oparesheni hiyo ilifeli vibaya. Sasa hivi kama wewe ni mwanajeshi katika jeshi fulani kwenye kitengo cha weledi (special force) au labda ni jasusi maalumu, lazima katika hatua fulani ya japo hata ‘darasani’ kwenye makaratasi utafundwa kuhusu Oparetion Entebbe na namna ilivyo tekelezwa. Oparesheni hii ilimuacha Amin na aibu kubwa kiasi kwamba akaendelea kufanya vitu ambavyo vilidhihirisha udhaifu wake wa kiungozi. Kwa mfano, yule bibi wa miaka 74 aliyeachwa hospitali mjini Entebbe, aliamuru auwawe kinyama. Lakini pia Amin alisimami kuwawa kwa McKenzie yule waziri wa kilimo wa Kenya ambaye alimsaidia Ehud Barak kumshinikiza Mzee Jomo Kenyetta kuruhusu ndege za jeshi la Israel kutumia viwanja vya ndege vya Kenya wakati wa utekelezaji wa OParesheni hiyo na pia kumsaidi kukusanya Intelijensia kwa kutumia ndege yake binafsi. McKenzie aliuwawa kwa bomu lililotegwa kwenye gari yake. Pia Amin alisimamia ulipuaji kwa bomu moja ya hoteli kubwa Nairobi kipindi hicho ambayo ilikuwa inaitwa The Norfolk Hotel, ambayo ilimilikiwa na moja ya wayahudi mashuhuri nchini Kenya. [6/12, 13:48] The Bold: Licha ya ‘fujo’ zote hizi ambazo Amin alizifanya baada ya jeshi lake kudhalilika kutokana na Oeration Entebbe lakini hatupawsi kusahau kwamba chini ya miaka mitatu baadae, yaani baada ya utekelezaji wa opareshini hii, Idd Amin aliondolewa kwa aibu madarakani na majeshi ya Tanzania na kumfanya akimbie nchi yake. ......................MWISHO.............. #TheBOLD_JF
    ·467 Vue
  • COBRA SNAKEs
    .
    leo ngoja tumuangalie cobra kiundani zaidi maana wameonekana kuwa ni wengi lakini wakitumia majina ya cobra ambao pia wanapatikana sana Bara la Asia na bara la Africa hata hapa TANZANIA WAKO WA KUTOSHAA
    .duniani kote kuna species zaidi ya 10 za cobra
    .
    Sasa neno halisi la COBRA lilipatikana kutoka kwenye lugha ya KIRENO lililoandikwa "COBRA DE CAPELLO," likimanaisha "SNAKE WITH HOOD"
    .
    kwa kiswahili linamaanisha kama nyoka mwenye "kofia" hii kofia ndio kule kuapanuka kwake kwenye shingo
    .ndipo ikatoa maana ya hood yaani covering (Ukitafsiri sana kwa kiswahili unaweza usielewe )
    .
    Sasa baada ya hili neno kutoka ndipo likaanza kutumika hata kwa nyoka ambao hawako kabisaa kwenye jamii ya cobra yaani nyoka wengine wenye hood nao wakaitwa cobra mfano ni KING COBRA yule wa INDIA
    .
    Tuangalia sasa jamii halisi za cobra na wale ambao wanatumia tu jina la cobra
    .
    Jamii ya kwanza ni TRUE COBRA
    .
    kitaalam wanatoka katika genus (NAJA GENUS) na sifa kuu ya cobra hawa kawaida wanakuwa na urefu wa futi 7 - 10 tu na wanameno mafupi sana yaliyopinda ndani
    .
    wanatoa sumu inayoitwa NEUTROXIN VENOM, kiuhalisia sumu hii sio kali sana ila inachofanya iwe kali na kuuwa haraka ni kule cobra kung'ata zaidi ya mara moja hivyo hufanya kiwango cha sumu kuwa kingi
    .
    sasa humu ndio kuna FOREST COBRA in west africa na kuna CAPE COBRA IN SOUTH AFRICA na INDIAN COBRA
    .hawa wote wanakula wadudu na ndege tu kama chakula
    .
    Lakini pia kwenye hii jamii kuna COBRA WANAOTEMA TU SUMU ambayo hufanya mtu awe kipofu ikigusa machoni,
    .kama vile mozambique spiting cobra (Tz wako wengi sana),
    .
    Jamii ya pili ni KING COBRA
    .
    .huyu ndio cobra hatari zaidi duniani kitaalam anaitwa "Hemachatus haemachatus" hata jina halifanani na true cobra.. (fake cobra)
    .Anasifa ya kula NYOKA wengine tu na hali chakula kingine kabisaa na urefu wa futi 15
    .shingo yake sio bapa sana ila anakiwango kikubwa sana cha sumu yaani anang'ata kidogo na unakufa ndani ya dakika chache sana
    .huwa anaishi mwenyewe na yuko bara la Asia tu
    .
    SASA IKITOKEA UMENG'ATWA NA COBRA WAHI HOSPITALI UTAPONA. ila KING COBRA AKIKUNG'ATA HAMNA TIBA..

    The Wildlife Tanzania.
    COBRA SNAKEs . leo ngoja tumuangalie cobra kiundani zaidi maana wameonekana kuwa ni wengi lakini wakitumia majina ya cobra ambao pia wanapatikana sana Bara la Asia na bara la Africa hata hapa TANZANIA WAKO WA KUTOSHAA .duniani kote kuna species zaidi ya 10 za cobra . Sasa neno halisi la COBRA lilipatikana kutoka kwenye lugha ya KIRENO lililoandikwa "COBRA DE CAPELLO," likimanaisha "SNAKE WITH HOOD" . kwa kiswahili linamaanisha kama nyoka mwenye "kofia" hii kofia ndio kule kuapanuka kwake kwenye shingo .ndipo ikatoa maana ya hood yaani covering (Ukitafsiri sana kwa kiswahili unaweza usielewe 😀) . Sasa baada ya hili neno kutoka ndipo likaanza kutumika hata kwa nyoka ambao hawako kabisaa kwenye jamii ya cobra yaani nyoka wengine wenye hood nao wakaitwa cobra mfano ni KING COBRA yule wa INDIA . Tuangalia sasa jamii halisi za cobra na wale ambao wanatumia tu jina la cobra . Jamii ya kwanza ni TRUE COBRA . kitaalam wanatoka katika genus (NAJA GENUS) na sifa kuu ya cobra hawa kawaida wanakuwa na urefu wa futi 7 - 10 tu na wanameno mafupi sana yaliyopinda ndani . wanatoa sumu inayoitwa NEUTROXIN VENOM, kiuhalisia sumu hii sio kali sana ila inachofanya iwe kali na kuuwa haraka ni kule cobra kung'ata zaidi ya mara moja hivyo hufanya kiwango cha sumu kuwa kingi . sasa humu ndio kuna FOREST COBRA in west africa na kuna CAPE COBRA IN SOUTH AFRICA na INDIAN COBRA .hawa wote wanakula wadudu na ndege tu kama chakula . Lakini pia kwenye hii jamii kuna COBRA WANAOTEMA TU SUMU ambayo hufanya mtu awe kipofu ikigusa machoni, .kama vile mozambique spiting cobra (Tz wako wengi sana), . Jamii ya pili ni KING COBRA . .huyu ndio cobra hatari zaidi duniani kitaalam anaitwa "Hemachatus haemachatus" hata jina halifanani na true cobra.. (fake cobra) .Anasifa ya kula NYOKA wengine tu na hali chakula kingine kabisaa na urefu wa futi 15 .shingo yake sio bapa sana ila anakiwango kikubwa sana cha sumu yaani anang'ata kidogo na unakufa ndani ya dakika chache sana .huwa anaishi mwenyewe na yuko bara la Asia tu . SASA IKITOKEA UMENG'ATWA NA COBRA WAHI HOSPITALI UTAPONA. ila KING COBRA AKIKUNG'ATA HAMNA TIBA.. The Wildlife Tanzania.
    ·231 Vue
  • YAJUE MAENEO AMBAYO HURUHUSIWI KUFIKA KAMWE.

    Katika ulimwengu wa leo tunaoishi tunaweza kufanya vitu vingi vinavyotufurahisha ikiwemo kusafiri kwenda maeneo mbalimbali ulimwenguni kwa malengo mbalimbali mfano kibiashara,kiutalii na hata kwa lengo la kuburudika tu.lakini hayo yote yanaweza kufanyika isipokuwa kwa baadhi ya maeneo,yafuatayo ni maeneo manne (4) ambayo huruhusiwi kufika.

    #01.NORTH SENTINEL ISLAND (KISIWA CHA SENTINEL YA KASKAZINI)
    Kisiwa cha NORTH SENTINEL ni sehemu ya visiwa vya ANDAMAN na NICOBAR vilivyopo kwenye bay ya BENGAL kwenye bahari ya hindi kati ya MYANMAR na INDONESIA.Eneo hili ndipo mahali ambapo wakazi wake hawaruhusu mawasiliano kabisa na ulimwengu ulioendelea/mataifa mengine.
    Kuna visa kadhaa vya kuthibitisha 'marufuku' ya kuingia kisiwani huko kutoka kwa wakazi wake.
    -Mwezi DISEMBA mwaka 2004 tsunami ilipopiga kwenye bahari ya hindi waokoaji walihitaji kusaidia wahanga wa kisiwa hiko lakini haikuwa rahisi kutokana na upinzani waliokutana nao kutoka kwa wakazi wa kisiwa hicho,walijaribu kushusha vyakula wakiwa kwenye helikopta ya jeshi la maji la INDIA kilichotokea ni kwamba moja ya helikopta hizo ilishambuliwa na 'shujaa' mmoja wa kisiwa hiko aliepiga mkuki kwenye helikopta kuonesha kuwa watu hao hawakuhitaji msaada wala mawasiliano na mataifa jirani.
    Kimsingi INDIA ndio inayomiliki kisiwa hicho.
    -Kisa kingine ni cha mwaka 1896 cha mfungwa mmoja alietoroka kutoka kwenye gereza lililopo katika kisiwa cha ANDAMAN ambae alikimbilia kwenye kisiwa hiki,siku chache baadae mwili wake ulikutwa pembezoni mwa bahari ukiwa na alama za kupigwa na mishale na huku koo lake likiwa limekatwa.
    Sijui kama wakazi wa kisiwa hiki wanajua kama kuna nchi inaitwa TANZANIA,shughuli wanazofanya kuendesha maisha yao ni uwindaji,uvuvi pia wanakula matunda na asali.
    Huwezi kuamini kuwa maeneo haya hakuna SIMU wala INTANETI.

    #02.ROOM 39 (CHUMBA NAMBA 39)
    Kwa majina mengine huitwa BUREAU 39 au DIVISION 39 au OFFICE 39,jengo hili lipo nchini KOREA KASKAZINI na linakaliwa na tasisi ya siri ya chama cha KOREA KASKAZINI (KOREAN WORKERS' PARTY) lengo lake ni kuchangia uongezekaji wa fedha za kigeni nchini KOREA KASKAZINI,ROOM 39 inaaminika kuendesha shughuli zote zinazohusiana na uingizwaji wa fedha za kigeni nchini humo na mjini PYONGYANG ikiwa pamoja na mahoteli yaliyopo PYONGYANG na uchimbaji wa madini ya ZINC na DHAHABU. Taasisi ya ROOM 39 inaaminika kumiliki baadhi ya makampuni mafano ZOKWANG TRADING na benki ya TAESONG BANK.
    Tasisi hii iliundwa na KIM IL-SUNG miaka ya 1970,kwa mwaka tasisi hii ya siri inasadikika inaiingizia nchi ya KOREA KASKAZINI mapato ya kati ya milioni $500 (dola za kimarekani) mpaka billioni $1 (dola za kimarekani).
    Vyanzo kadhaa vya nchi za magharibi vinaeleza kuwa taasisi hii inaingiza fedha hizo kwa kuendesha shughuli za kihalifu,mfano ripoti moja ya WASHINGTON POST ilieleza ubadhilifu uliotokea katika sekta ya BIMA duniani na kudai kuwa ulifanywa na serikali ya KOREA KASKAZINI kwa kutumia taasisi yake ya KOREA NATIONAL INSURANCE CORP (KNIC).
    Jengo hili la ROOM 39 hakika huruhusiwi kuingia ndani yake,kutokana na sababu za kiusalama hivyo hutaweza kuwemo ndani yake.

    #03.AREA 51
    Hili ni eneo linalomilkiwa na JESHI LA ANGA LA MAREKANI lipo NEVADA.
    Taarifa nyingi na za uhakika kuhusu mambo yanayofanyika katika eneo hili ni 'highly classified' ila tu kuna nadharia kadhaa zinazoeleza mambo yanayofanyika katika eneo hili baadhi ya nadharia hizo ni;
    >Inaaminika kuwa AREA 51 ni mahali wanapofanya tafiti za teknolojia za viumbe wa sayari nyingine (ALLIEN) ambapo jeshi la anga la marekani limehifadhi masalia ya ndege za viumbe hao zilizopata ajali,na pia wanatengeneza ndege kutokana na teknolojia ya ALLIENS.
    >Inaaminika wanaendesha program/mpango wa kutengeneza silaha za kujilinda za awali yaani STRATEGIC DEFENSE INITIATIVE (SDI) na program za silaha nyingine.
    >Inaaminika kuwa ndani ya eneo hilo wanatengeneza teknolojia itakayoweza ku'control' hali ya hewa.
    >Inaaminika kuwa wanafanya program ya kutengeneza teknolojia ya TIME TRAVEL (uwezo wa kumwezesha mtu kurudi wakati uliopita au kwenda wakati ujao,mfano mtu atoke hivi sasa na asafiri kwenda miaka 50 ijayo) na TELEPORTATION (yaani mtu aweze kusafiri kutoka eneo moja hadi jingine pasina usafiri wowote ule na kwa haraka.nadharia hii imeelezwa kwenye filamu/movie/series ya TOMORROW PEOPLE kama ushawahi kuiona basi hivyo ndivyo watu wanavyo teleport).
    >Inaaminika kuwa pengine wanaendesha shughuli zitakazochangia kuwepo kwa serikali moja duniani (ONE WORLD GOVERMENT)
    Moja ya mambo yanayoweza kutumika kama ushahidi juu ya nadharia inayohusisha uwepo wa viumbe kutoka sayari nyingine yaani ALLIENS ndani ya AREA 51 ni baadhi ya watu waliowahi kukiri kuwa wafanyakazi wa AREA 51
    **Mmoja wao ni bwana BOB LAZAR ambae mwaka 1989 alisema kuwa alifanya kazi ndani ya AREA 51 SECTOR FOUR (S-4) ambapo eneo hili lipo chini ya ardhi,bwana BOB LAZAR alisema kuwa alipokuwa ndani ya SECTOR FOUR alifanya kazi na ndege ya anga la juu(spacecraft) ya ALLIENS ambayo inashikiliwa na serikali ya MAREKANI ndani ya AREA 51.
    **Documentary moja iitwayo DREAMLAND iliotoka mwaka 1996 ilioongozwa na BRUCE BURGESS ilijumuisha interview aliofanya na mzee wa umri wa miaka 71 ambae ni injinia (mechanical engeneer) aliekiri kuwa alishawahi kuwa muajiriwa aliefanya kazi ndani ya AREA 51 katika miaka ya 1950,alikiri kuwa alifanya kazi kwenye kitu chenye uwezo wa kupaaa angani kilicho mfano wa sahani kiitwacho "FLYING DISK SIMULATOR" alisema kitu hicho mfano wa sahani kubwa kilitokana na ndege ya anga za juu iliopoata ajali na kilitumika kuwafundishia marubani wa jeshi la MAREKANI,pia alikiri kuwa alifanya kazi na kiumbe kutoka sayari nyingine ambae aliitwa "J-ROD".
    **Mwaka 2004 DAN BURISCH alikiri kufanya kazi ndani ya AREA 51 pamoja na ALLIEN aliefahamika kwa jina la "J-ROD"
    Kuingia katika eneo hili kumezuiwa vikali, na wanajeshi wanaolinda eneo hilo wamepewa mamlaka ya kumfyatulia risasi yeyote atakaeingia ambae hana ruhusa ya kuwepo eneo hilo,Hivyo basi katika eneo hili hautaweza kufika labda uwe mfanyikazi wa humu.
    (KWA WALE WANAOCHEZA SANA VIDEO GAMES AU WALE WALIOWAHI KUCHEZA "GTA SAN ANDREAS" WANAJUA UKIFIKA SEHEMU MOJA INAYOITWA AREA 51 UNASHAMBULIWA KULIKO KAWAIDA)

    #04.ILHA DE QUEIMEDA/SNAKE ISLAND (KISIWA NA NYOKA)
    Kisiwa cha ILHA DE QUEIMEDA kipo umbali wa maili kadhaa kutoka katika pwani ya mji wa SAO PAOLO nchini BRAZIL.
    Kisiwa hiki ni makazi ya nyoka hatari zaidi duniani tena wenye sumu ilio kali kabisa,idadi ya kukadiria ya nyoka waliopo kisiwani humo ni takriban nyoka 4000,nyoka aina ya 'lancehead vipers' wapatikanao kisiwani humo wanakua kwa wastani wa urefu wa SENTIMITA 70 (70 CM) pia wanaweza kufikia hata urefu wa SENTIMITA 118 mpaka 120,vifo vingi vinavyotokea amerika ya kusini miongoni mwao husababishwa na nyoka hawa.
    > Chakula chao cha kawaida mara nyingi ni ndege na imeripotiwa kuwa huwa wanakula mijusi na kula hata nyoka wengine.
    > Nyoka wa aina hii akimng'ata/akimgonga binadamu mara moja basi binadamu anakuwa kwenye hatari ya kufa kwa aslimia 7 (7%) yaani anakuwa na uwezekano wa kufa kwa asilimia 7.
    Moja ya kisa kilichoripitiwa kutokea kisiwani huko ni cha mvuvi mmoja aliekuwa akivua samaki na mara boti yake ikapata tatizo la injini akaamua kuweka makazi kwa muda katika kisiwa hicho pasina kujua hatari iliopo ndani yake, baada ya boti kuonekana ndipo alipopatikana akiwa amekufa huku akiwa na alama za kung'atwa na nyoka.
    Kwa miaka 15 iliopita idadi ya nyoka kisiwani humo imepungua kwa asilimia 15 (15%) kutokana na magonjwa na kupungua kwa uoto ndani ya kisiwa,lakini hii leo bado maelfu ya nyoka bado ndio makazi yao ndani ya kisiwa.Serikali ya BRAZIL imezuia utembeleaji na shughuli za kitalii ndani ya kisiwa hicho isipokuwa kwa wanasayansi na wanajeshi wa majini wa BRAZIL.
    YAJUE MAENEO AMBAYO HURUHUSIWI KUFIKA KAMWE. Katika ulimwengu wa leo tunaoishi tunaweza kufanya vitu vingi vinavyotufurahisha ikiwemo kusafiri kwenda maeneo mbalimbali ulimwenguni kwa malengo mbalimbali mfano kibiashara,kiutalii na hata kwa lengo la kuburudika tu.lakini hayo yote yanaweza kufanyika isipokuwa kwa baadhi ya maeneo,yafuatayo ni maeneo manne (4) ambayo huruhusiwi kufika. #01.NORTH SENTINEL ISLAND (KISIWA CHA SENTINEL YA KASKAZINI) Kisiwa cha NORTH SENTINEL ni sehemu ya visiwa vya ANDAMAN na NICOBAR vilivyopo kwenye bay ya BENGAL kwenye bahari ya hindi kati ya MYANMAR na INDONESIA.Eneo hili ndipo mahali ambapo wakazi wake hawaruhusu mawasiliano kabisa na ulimwengu ulioendelea/mataifa mengine. Kuna visa kadhaa vya kuthibitisha 'marufuku' ya kuingia kisiwani huko kutoka kwa wakazi wake. -Mwezi DISEMBA mwaka 2004 tsunami ilipopiga kwenye bahari ya hindi waokoaji walihitaji kusaidia wahanga wa kisiwa hiko lakini haikuwa rahisi kutokana na upinzani waliokutana nao kutoka kwa wakazi wa kisiwa hicho,walijaribu kushusha vyakula wakiwa kwenye helikopta ya jeshi la maji la INDIA kilichotokea ni kwamba moja ya helikopta hizo ilishambuliwa na 'shujaa' mmoja wa kisiwa hiko aliepiga mkuki kwenye helikopta kuonesha kuwa watu hao hawakuhitaji msaada wala mawasiliano na mataifa jirani. Kimsingi INDIA ndio inayomiliki kisiwa hicho. -Kisa kingine ni cha mwaka 1896 cha mfungwa mmoja alietoroka kutoka kwenye gereza lililopo katika kisiwa cha ANDAMAN ambae alikimbilia kwenye kisiwa hiki,siku chache baadae mwili wake ulikutwa pembezoni mwa bahari ukiwa na alama za kupigwa na mishale na huku koo lake likiwa limekatwa. Sijui kama wakazi wa kisiwa hiki wanajua kama kuna nchi inaitwa TANZANIA,shughuli wanazofanya kuendesha maisha yao ni uwindaji,uvuvi pia wanakula matunda na asali. Huwezi kuamini kuwa maeneo haya hakuna SIMU wala INTANETI. #02.ROOM 39 (CHUMBA NAMBA 39) Kwa majina mengine huitwa BUREAU 39 au DIVISION 39 au OFFICE 39,jengo hili lipo nchini KOREA KASKAZINI na linakaliwa na tasisi ya siri ya chama cha KOREA KASKAZINI (KOREAN WORKERS' PARTY) lengo lake ni kuchangia uongezekaji wa fedha za kigeni nchini KOREA KASKAZINI,ROOM 39 inaaminika kuendesha shughuli zote zinazohusiana na uingizwaji wa fedha za kigeni nchini humo na mjini PYONGYANG ikiwa pamoja na mahoteli yaliyopo PYONGYANG na uchimbaji wa madini ya ZINC na DHAHABU. Taasisi ya ROOM 39 inaaminika kumiliki baadhi ya makampuni mafano ZOKWANG TRADING na benki ya TAESONG BANK. Tasisi hii iliundwa na KIM IL-SUNG miaka ya 1970,kwa mwaka tasisi hii ya siri inasadikika inaiingizia nchi ya KOREA KASKAZINI mapato ya kati ya milioni $500 (dola za kimarekani) mpaka billioni $1 (dola za kimarekani). Vyanzo kadhaa vya nchi za magharibi vinaeleza kuwa taasisi hii inaingiza fedha hizo kwa kuendesha shughuli za kihalifu,mfano ripoti moja ya WASHINGTON POST ilieleza ubadhilifu uliotokea katika sekta ya BIMA duniani na kudai kuwa ulifanywa na serikali ya KOREA KASKAZINI kwa kutumia taasisi yake ya KOREA NATIONAL INSURANCE CORP (KNIC). Jengo hili la ROOM 39 hakika huruhusiwi kuingia ndani yake,kutokana na sababu za kiusalama hivyo hutaweza kuwemo ndani yake. #03.AREA 51 Hili ni eneo linalomilkiwa na JESHI LA ANGA LA MAREKANI lipo NEVADA. Taarifa nyingi na za uhakika kuhusu mambo yanayofanyika katika eneo hili ni 'highly classified' ila tu kuna nadharia kadhaa zinazoeleza mambo yanayofanyika katika eneo hili baadhi ya nadharia hizo ni; >Inaaminika kuwa AREA 51 ni mahali wanapofanya tafiti za teknolojia za viumbe wa sayari nyingine (ALLIEN) ambapo jeshi la anga la marekani limehifadhi masalia ya ndege za viumbe hao zilizopata ajali,na pia wanatengeneza ndege kutokana na teknolojia ya ALLIENS. >Inaaminika wanaendesha program/mpango wa kutengeneza silaha za kujilinda za awali yaani STRATEGIC DEFENSE INITIATIVE (SDI) na program za silaha nyingine. >Inaaminika kuwa ndani ya eneo hilo wanatengeneza teknolojia itakayoweza ku'control' hali ya hewa. >Inaaminika kuwa wanafanya program ya kutengeneza teknolojia ya TIME TRAVEL (uwezo wa kumwezesha mtu kurudi wakati uliopita au kwenda wakati ujao,mfano mtu atoke hivi sasa na asafiri kwenda miaka 50 ijayo) na TELEPORTATION (yaani mtu aweze kusafiri kutoka eneo moja hadi jingine pasina usafiri wowote ule na kwa haraka.nadharia hii imeelezwa kwenye filamu/movie/series ya TOMORROW PEOPLE kama ushawahi kuiona basi hivyo ndivyo watu wanavyo teleport). >Inaaminika kuwa pengine wanaendesha shughuli zitakazochangia kuwepo kwa serikali moja duniani (ONE WORLD GOVERMENT) Moja ya mambo yanayoweza kutumika kama ushahidi juu ya nadharia inayohusisha uwepo wa viumbe kutoka sayari nyingine yaani ALLIENS ndani ya AREA 51 ni baadhi ya watu waliowahi kukiri kuwa wafanyakazi wa AREA 51 **Mmoja wao ni bwana BOB LAZAR ambae mwaka 1989 alisema kuwa alifanya kazi ndani ya AREA 51 SECTOR FOUR (S-4) ambapo eneo hili lipo chini ya ardhi,bwana BOB LAZAR alisema kuwa alipokuwa ndani ya SECTOR FOUR alifanya kazi na ndege ya anga la juu(spacecraft) ya ALLIENS ambayo inashikiliwa na serikali ya MAREKANI ndani ya AREA 51. **Documentary moja iitwayo DREAMLAND iliotoka mwaka 1996 ilioongozwa na BRUCE BURGESS ilijumuisha interview aliofanya na mzee wa umri wa miaka 71 ambae ni injinia (mechanical engeneer) aliekiri kuwa alishawahi kuwa muajiriwa aliefanya kazi ndani ya AREA 51 katika miaka ya 1950,alikiri kuwa alifanya kazi kwenye kitu chenye uwezo wa kupaaa angani kilicho mfano wa sahani kiitwacho "FLYING DISK SIMULATOR" alisema kitu hicho mfano wa sahani kubwa kilitokana na ndege ya anga za juu iliopoata ajali na kilitumika kuwafundishia marubani wa jeshi la MAREKANI,pia alikiri kuwa alifanya kazi na kiumbe kutoka sayari nyingine ambae aliitwa "J-ROD". **Mwaka 2004 DAN BURISCH alikiri kufanya kazi ndani ya AREA 51 pamoja na ALLIEN aliefahamika kwa jina la "J-ROD" Kuingia katika eneo hili kumezuiwa vikali, na wanajeshi wanaolinda eneo hilo wamepewa mamlaka ya kumfyatulia risasi yeyote atakaeingia ambae hana ruhusa ya kuwepo eneo hilo,Hivyo basi katika eneo hili hautaweza kufika labda uwe mfanyikazi wa humu. (KWA WALE WANAOCHEZA SANA VIDEO GAMES AU WALE WALIOWAHI KUCHEZA "GTA SAN ANDREAS" WANAJUA UKIFIKA SEHEMU MOJA INAYOITWA AREA 51 UNASHAMBULIWA KULIKO KAWAIDA) #04.ILHA DE QUEIMEDA/SNAKE ISLAND (KISIWA NA NYOKA) Kisiwa cha ILHA DE QUEIMEDA kipo umbali wa maili kadhaa kutoka katika pwani ya mji wa SAO PAOLO nchini BRAZIL. Kisiwa hiki ni makazi ya nyoka hatari zaidi duniani tena wenye sumu ilio kali kabisa,idadi ya kukadiria ya nyoka waliopo kisiwani humo ni takriban nyoka 4000,nyoka aina ya 'lancehead vipers' wapatikanao kisiwani humo wanakua kwa wastani wa urefu wa SENTIMITA 70 (70 CM) pia wanaweza kufikia hata urefu wa SENTIMITA 118 mpaka 120,vifo vingi vinavyotokea amerika ya kusini miongoni mwao husababishwa na nyoka hawa. > Chakula chao cha kawaida mara nyingi ni ndege na imeripotiwa kuwa huwa wanakula mijusi na kula hata nyoka wengine. > Nyoka wa aina hii akimng'ata/akimgonga binadamu mara moja basi binadamu anakuwa kwenye hatari ya kufa kwa aslimia 7 (7%) yaani anakuwa na uwezekano wa kufa kwa asilimia 7. Moja ya kisa kilichoripitiwa kutokea kisiwani huko ni cha mvuvi mmoja aliekuwa akivua samaki na mara boti yake ikapata tatizo la injini akaamua kuweka makazi kwa muda katika kisiwa hicho pasina kujua hatari iliopo ndani yake, baada ya boti kuonekana ndipo alipopatikana akiwa amekufa huku akiwa na alama za kung'atwa na nyoka. Kwa miaka 15 iliopita idadi ya nyoka kisiwani humo imepungua kwa asilimia 15 (15%) kutokana na magonjwa na kupungua kwa uoto ndani ya kisiwa,lakini hii leo bado maelfu ya nyoka bado ndio makazi yao ndani ya kisiwa.Serikali ya BRAZIL imezuia utembeleaji na shughuli za kitalii ndani ya kisiwa hicho isipokuwa kwa wanasayansi na wanajeshi wa majini wa BRAZIL.
    ·454 Vue
  • *VATICAN CITY......
    Nchi? Mji? Serikali au Kampuni?*

    Nadhani moja kati ya maeneo ambayo yamekuwa tata zaidi kuyaelewa basi ni mji wa Vatican… tukiachilia mbali kuhusu utata/ugumu wa kuelewa mfumo wake wa uendeshaji na historia yake lakini swali jepesi zaidi ambalo kila mtu huwa anahisi analifahamu jawabu lake ni kuhusu utambulisho wa Vatican.!! Ni swali jepesi ambalo karibia kila mtu anadhani ana jawabu sahihi lakini uhalisia ni kwamba asilimia kubwa ya watu wana jawabu lisilo sahihi… kila mtu atakueleza kwamba Vatican ni nchi inayojitegemea lakini hii ni robo tu au thelethi ya jawabu…

    Leo nami niandike kidogo kuhusu eneo hili… na kwenye andishi hili fupi nitaeleza utambulisho wa Vatican ukoje kwa usahihi wake kabisa!

    *Muhimu:* andishi hili halilengi kukosoa au kupinga imani ya mtu yeyote. Tahadhali zote zinazingatiwa ili kulinda heshima ya imani ya kila mtu.

    Tuendelee…

    Vatican City, ndio makao makuu ya Kanisa Katoliki na nyumba ya maisha ya Papa, kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki.
    Vatican ndio nchi ndogo zaidi duniani kiasi kwamba unaweza kuizunguka yote kwa mzingo (circumference) kwa muda wa dakika arobaini tu kwa kutembea kwa miguu.

    Ni ajabu sana kwa namna gani nchi ndogo kiasi hiki imetokea na je ni nchi kama nchi nyingine???

    Jibu la swali hili ni refu sana kiaisi kwamba unaweza hata kusoma darasani kwa mwaka mzima lakini nitajaribu kuweka katika maneno machache sana ya kueleweka kwa wepesi…

    Miaka ya kale sana Papa wa Kanisa Katoliki alikuwa ni mtawala wa nchi ambayo ilikuwa inajiita *Himaya ya Papa (Papal State)* ambayo inarandana kabisa na eneo la sasa la nchi nzima ya Italia. Hii ilikuwa takribani miaka ya 754 mpaka miaka ya 1870.
    Ni katika kipindi hiki ambacho Papa aliteua eneo ndani ya nchi yake Papal State ambalo likajengwa *St. Peters Basilica*, kanisa kubwa zaidi duniani na lenye nakshi adhimu zaidi. Eneo hili ambalo St. Peters Basilica ilijengwa ni eneo fulani hivi la muinuko ambako hapo hapo pia yalijengwa makazi ya Papa kuishi.

    Ikumbukwe kwamba katika kipindi hiki hiki cha uwepo wa himaya ya Papal State pia ilikuwa inapakana na Ufalme wa Italy (Kingdom of Italy) japo kila moja ilikuwa inajitegemea.

    Japokuwa himaya hizi mbili zilikuwa jirani lakini kulikuwa na uhasama fulani kati yao. Hii ilifanya Papa kujenga ukuta mkubwa kuzunguka makazi yake ya kuishi na kanisa la St. Peters Basilica.

    Kadiri miaka ilivyozidi kwenda uhasama kati ya Italy Kingdom na Papal State ulipanuka zaidi na ilifikia hatua Kingdom of Italy wakafanya uamuzi wa kuiteka Papal State na kuifanya makao makuu ya nchi yake (Rome ya sasa).

    Wakati na baada ya uvamizi huu wa Kingdom of Italy kuteka Papal State, Papa mwenyewe alikuwa amejificha ndani ya makazi yake yaliyozungushiwa ukuta ambao nimeeleza awali.
    Ikumbukwe kwamba hata kipindi hiki Kanisa Katoliki tayari lilikuwa na ushawishi mkubwa duniani kwa hiyo Kingdom of Italy walihofia kuingiza majeshi kwa nguvu ndani ya makazi ya Papa na kumkamata kuogopa umaarufu wao kimataifa kudondoka.

    Kwa hiyo majeshi ya Kingdom of Italy yalibakia nje mwa kuta za Vatican kwa miaka mingi sana wakiamini kwamba iko siku Papa atakata tamaa na kujisalimisha.
    Lakini hii haikufua dafu kwani miongo ilipita na Papa hakujisalimisha kwa kutoka nje ya kuta za Vatican. Takribani Mapapa watano kwa muda wa karibia miaka sitini waliishi ndani ya kuta za Vatican katika hali hii. Mapapa hao kwa majina yao walikuwa ni Papa Pius IX, Papa Leo XIII, Papa Pius X, Papa Benedict XV na Papa Pius XI.

    Hali hii ilisababisha Mapapa kutotambua Kingdom of Italy na pia kulalamika mara kwa mara kwa jamii ya kimataifa kwamba wanaishi kama wafungwa ndani ya kuta za Vatican kutokana na ukandamizaji wa Kingdom of Italy na hofu waliyonayo kutoka nje ya kuta za Vatican.

    Hii inatufikisha mpaka miaka ya 1920s wakati wa utawala wa Benito Mussolini akiwa Waziri Mkuu wa Italy.
    Mussolini alichoshwa na malalamiko haya ya Papa na majibizano ya kila mara huku Papa bado akishikilia msimamo wa kutoitambua Italy

    Mussolini mwanasiasa mahiri kama ajulikanavyo akaona fursa hapa ya kuandika jina lake kwenye vitabu vya historia.
    Akapendekeza makubaliano maalumu kwa Papa. Kwamba atafanya yafuatayo;

    1. Italy itatoa ardhi ya Vatican kwa Papa na iwe himaya/nchi iliyo chini ya utawala wa Papa.

    2. Italy itatoa fedha kama fidia kwa Papa kutokana na manyanyaso ya miaka yote.

    Mussolini alihitaji Papa kufanya yafuatayo;

    1. Papa atambue Italy kuwa ni nchi.

    2. Papa asijihusishe wala kutoa maoni yoyote kuhusu masuala ya kisiasa na vita.

    Papa na Mussolini wakafikia makubaliano na mikataba ikasainiwa na hapa ndipo taifa dogo zaidi duniani likazaliwa, Vatican.

    Vatican ikaanza kujiendesha kama taifa linalojitegemea kwa kuwa na sarafu yake, serikali yake, Polisi wake, jela yake (ndio kuna jela Vatican), Posta yake, Plate number zake, Passport zake na kadhalika na kadhalika.

    Vatican si kama nchi nyingine duniani kwa hiyo usidhani kwamba tayari umeielewa Vatican, hicho nilichoeleza ni theluthi tu mkanganyiko wa kuielewa Vatican kama nchi… kunywa tena glass ya maji and relax!! Nitaeleza tena kidogo…

    Ili kuielewa Vatican walau kiduchu kuna watu wawili tunapaswa kuwafahamu;

    1. Papa

    2. Mfalme wa Vatican

    Na pia kuna vitu viwili vya kuvielewa;

    1. The Holy See

    2. Vatican City

    Tuanze kimoja kimoja…

    *1. Papa*
    Hii sihitaji kueleza sana karibia wote tunafahamu. Lakini kwa msingi wa awali kabisa, Papa ni askofu wa Wakatoliki wote waliopo Rome/Vatican lakini kwa kuwa yeye pia ndiye kiongozi wa Wakatoliki wote duniani ndio sababu ya Uaskofu wake kuwa Papa.

    *2. The Holy See*
    Kabla sijaeleza chochote kuhusu Mfalme wa Vatican kwanza nieleze kuhusu The Holy See. Hili ni moja ya mambo magumu zaidi kuyaelewa kuhusu Vatican. Nitaeleza kwa lugha nyepesi na uchache ili tusipasue vichwa kwa mikanganyiko.

    Kwa tafsiri nyepesi Holy See ni 'Throne' ya Papa (nakosa neno zuri la kiswahili, sipendezwi sana na tafsiri ya 'Kiti cha Enzi').

    Ni kwamba, maaskofu wote ndani ya kanisa Katoliki wanakuwa na 'throne' lakini kwa kuwa 'throne' ya Papa ni maalumu (kiongozi wa Wakatoliki wote duniani) kwa hiyo throne yake inakuwa muhimu zaidi na inaitwa 'The Holy See'.
    Mapapa wanabadilika lakini The Holy See iko na itaendelea kuwepo siku zote.

    Yaani kwa mfano Papa anapofariki au kustaafu kama tulivyoona mwaka juzi, Makadinali wanapokusanyika Vatican kwa uhalisia wanaenda kumchagua Kadinali mwenzao ambaye atakalia 'throne' ya 'Holy See'.

    Kwa 'angle' nyingine tunaweza kusema kwamba 'The Holy See' ndiyo sheria na mamlaka yote inayofanya kanisa Katoliki kuwa namna lilivyo. Pia sheria zote za kanisa Katoliki na mfumo wake unatengenezwa na The Holy See (sio Papa).

    Pia tunaweza kusema kwamba Benito Mussolini alipofanya makubaliano na Vatican aliingia mkataba ule na 'The Holy See'.

    Pia unaweza usiamini lakini katika nyanja za sheria za kimataifa 'The Holy See' inatambulika kama mtu/kampuni halisi ambaye amesajiliwa kisheria.

    Labda nitumie lugha nyepesi zaidi ya mfano… ukitaka kuelewa The Holy See, chukulia mfano huu kwamba Holy See ni "Catholic Church Inc." alafu Papa ndiye CEO.

    Nimejitahidi kueleza kwa kifupi na kwa wepesi niwezavyo, kuielewa kwa undani zaidi The Holy See labda tunapaswa kuandaa andishi maalumu mahususi kwa ajili yake tu.

    *3. Mfalme wa Vatican*
    Mfalme wa Vatican ni mtawala mwenye mamlaka yote juu ya nchi ya Vatican na hii inaifanya Vatican kuwa moja kati ya nchi sita pekee duniani zenye wafalme wenye mamlaka kamili (absolute monarchy). Nchi nyingine tano ni Saudi Arabia, Brunei, Oman, Qatar, Oman na Swaziland.

    Hii ndio sababu kwanini Vatican hawawezi kujiunga na Umoja wa Ulaya kwa sababu EU wanakubali nchi zenye mfumo wa kidemokrasia pekee.
    Japokuwa Vatican ina tawi la 'bunge' ambalo linaundwa na makadinali wa Vatican ambayo wanatunga sheria za 'nchi' lakini bado mfalme wa Vatican anauwezo wa kuveto maamuzi yoyote ambayo wamefikia.

    *Swali: Kwanini hatusikii chochote kuhusu Mfalme wa Vatican??*

    Ni kwa sababu Mfalme wa Vatican na Papa ni wajibu na mamlaka mbili tofauti lakini zinakaliwa na mtu mmoja, Papa wa Kanisa Katoliki.

    Hii inatupa kitu kingine cha kipekee kuhusu Vatican.

    Papa anachaguliwa na makadinali wenzake - Demokrasia.
    Lakini Mfalme hachaguliwi.

    Hii inafanya Vatican kuwa nchi pekee kwenye historia ya dunia kuwa na Mfalme mwenye mamlaka kamili ambaye si wa kurithi na anapatikana kidemokrasia (Elected non-heridetary absolute Monarchy).

    Kwa hiyo Papa kulingana na muktadha na mazingira ya suala husika kuna muda anatumia mamlaka yake kama Papa na muda mwingine inampasa kutumia mamlaka yake kama Mfalme wa Vatican.

    Bado kuna mkanganyiko???

    Zingatia mfano huu rahisi; tuseme kwamba kuna kampuni fulani kubwa ya kimataifa inaitwa Aman Enterprises (The Holy See kwa mada yetu). Aman Enterprises wakafanikiwa kuishwishi Tanzania kuwapatia kisiwa cha Mbudya na Bold Enterprises wanakibadilisha kisiwa cha Mbudya kuwa nchi inayojitegemea, labda iitwe Aman Land (Vatican City kwa mfano wetu).
    Sasa CEO wa kampuni Bwana Aman (Papa kwa mada yetu) anahamishiamanya makao makuu ya kampuni mpaka Aman Land. Kwa kuwa Aman Land sasa ni nchi, CEO wa kampuni anakuwa pia mtawala wa nchi hii, Mfalme.

    .
    Kwa hiyo kwa manufaa ya kampuni kutumia 'connection' zake za kimataifa kunufaisha taifa lake la Aman Land ni vyema kutumia mamlaka kama CEO wa Bold Enterprises na kuna muda akihitaji nchi yake ya Aman Land kutunga sheria na taratibu ambazo zitanufaisha kampuni izidi kushamiri ni vyema kutumia mamlaka yake kama Mfalme wa Aman Land.

    Haya ndio mamlaka mawili yaliyo chini ya mtu mmoja ndani ya vatican, Papa na Mfalme wa Vatican.

    Bado kuna mkanganyiko???

    Kama haujaelewa sawia usihofu kwa maana bado kuna hata nchi nyingine duniani bado hawaelewi sawa sawa mfumo mzima wa Vatican.

    Mfano, Umoja wa Mataifa wamekubali The Holy See (corporation) kama mwanachama wake lakini sio Vatican City nchi yenyewe.

    Passports za raia wa Vatican zinatolewa na The Holy See na sio Vatican na zinakubalika kwenye nchi nyingine japokuwa The Holy See kimataifa inatambulika kisheria kama Kampuni inayojitegemea.

    Na hapa tuongee kiduchu pia kuhusu raia wa Vatican. Katika nchi nyingine raia wa wanaongezeka kutokana na kuzaliana lakini hapa Vatican hakuna hilo kutokana na idadi ndogo ya wanaweka kiasi kwamba karibia ni asilimia sufuri. Namna pekee ya kuwa raia wa Vatican ni kwa kupewa uraia na Mfalme wa Vatican ili uishi Vatican kama moja wa wasaidizi wa Papa (ambaye ndiye mfalme). Kwa hiyo siku ukiacha kazi, yaani usaidizi wako kwa Papa ukifikia kikomo, Mfalme wa Vatican (ambayr ndiye Papa) anaondoa uraia wako na unarudi kwenu.

    Katika muda wowote ule raia wa nchi ya Vatican wanakadiriwa kuwa jumla karibia ya 500 ambao ndio idadi ndogo zaidi ya raia kwa nchi na ndogo kushinda hata idadi ya watu wanaoishi kwenye ghorofa moja kwenye nchi nyingi.
    Na raia wote hawa ni wafanyakazi wa Papa/The Holy See ambao wanapewa uraia na Mfalme (ambaye ndiye Papa) ambapo wanafanya kazi kama Makadinali, Wanadiplomasia, walinzi au kazi nyingine za kikanisa.

    Kwa ufupi sana hii ndio picha halisi ya nchi ya Vatican… na hapa ndipo ambapo maisha ya kiroho ya wafuasi zaidi ya Billioni 2 yanapoendeshwa…

    *VATICAN CITY...... Nchi? Mji? Serikali au Kampuni?* Nadhani moja kati ya maeneo ambayo yamekuwa tata zaidi kuyaelewa basi ni mji wa Vatican… tukiachilia mbali kuhusu utata/ugumu wa kuelewa mfumo wake wa uendeshaji na historia yake lakini swali jepesi zaidi ambalo kila mtu huwa anahisi analifahamu jawabu lake ni kuhusu utambulisho wa Vatican.!! Ni swali jepesi ambalo karibia kila mtu anadhani ana jawabu sahihi lakini uhalisia ni kwamba asilimia kubwa ya watu wana jawabu lisilo sahihi… kila mtu atakueleza kwamba Vatican ni nchi inayojitegemea lakini hii ni robo tu au thelethi ya jawabu… Leo nami niandike kidogo kuhusu eneo hili… na kwenye andishi hili fupi nitaeleza utambulisho wa Vatican ukoje kwa usahihi wake kabisa! *Muhimu:* andishi hili halilengi kukosoa au kupinga imani ya mtu yeyote. Tahadhali zote zinazingatiwa ili kulinda heshima ya imani ya kila mtu. Tuendelee… Vatican City, ndio makao makuu ya Kanisa Katoliki na nyumba ya maisha ya Papa, kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki. Vatican ndio nchi ndogo zaidi duniani kiasi kwamba unaweza kuizunguka yote kwa mzingo (circumference) kwa muda wa dakika arobaini tu kwa kutembea kwa miguu. Ni ajabu sana kwa namna gani nchi ndogo kiasi hiki imetokea na je ni nchi kama nchi nyingine??? Jibu la swali hili ni refu sana kiaisi kwamba unaweza hata kusoma darasani kwa mwaka mzima lakini nitajaribu kuweka katika maneno machache sana ya kueleweka kwa wepesi… Miaka ya kale sana Papa wa Kanisa Katoliki alikuwa ni mtawala wa nchi ambayo ilikuwa inajiita *Himaya ya Papa (Papal State)* ambayo inarandana kabisa na eneo la sasa la nchi nzima ya Italia. Hii ilikuwa takribani miaka ya 754 mpaka miaka ya 1870. Ni katika kipindi hiki ambacho Papa aliteua eneo ndani ya nchi yake Papal State ambalo likajengwa *St. Peters Basilica*, kanisa kubwa zaidi duniani na lenye nakshi adhimu zaidi. Eneo hili ambalo St. Peters Basilica ilijengwa ni eneo fulani hivi la muinuko ambako hapo hapo pia yalijengwa makazi ya Papa kuishi. Ikumbukwe kwamba katika kipindi hiki hiki cha uwepo wa himaya ya Papal State pia ilikuwa inapakana na Ufalme wa Italy (Kingdom of Italy) japo kila moja ilikuwa inajitegemea. Japokuwa himaya hizi mbili zilikuwa jirani lakini kulikuwa na uhasama fulani kati yao. Hii ilifanya Papa kujenga ukuta mkubwa kuzunguka makazi yake ya kuishi na kanisa la St. Peters Basilica. Kadiri miaka ilivyozidi kwenda uhasama kati ya Italy Kingdom na Papal State ulipanuka zaidi na ilifikia hatua Kingdom of Italy wakafanya uamuzi wa kuiteka Papal State na kuifanya makao makuu ya nchi yake (Rome ya sasa). Wakati na baada ya uvamizi huu wa Kingdom of Italy kuteka Papal State, Papa mwenyewe alikuwa amejificha ndani ya makazi yake yaliyozungushiwa ukuta ambao nimeeleza awali. Ikumbukwe kwamba hata kipindi hiki Kanisa Katoliki tayari lilikuwa na ushawishi mkubwa duniani kwa hiyo Kingdom of Italy walihofia kuingiza majeshi kwa nguvu ndani ya makazi ya Papa na kumkamata kuogopa umaarufu wao kimataifa kudondoka. Kwa hiyo majeshi ya Kingdom of Italy yalibakia nje mwa kuta za Vatican kwa miaka mingi sana wakiamini kwamba iko siku Papa atakata tamaa na kujisalimisha. Lakini hii haikufua dafu kwani miongo ilipita na Papa hakujisalimisha kwa kutoka nje ya kuta za Vatican. Takribani Mapapa watano kwa muda wa karibia miaka sitini waliishi ndani ya kuta za Vatican katika hali hii. Mapapa hao kwa majina yao walikuwa ni Papa Pius IX, Papa Leo XIII, Papa Pius X, Papa Benedict XV na Papa Pius XI. Hali hii ilisababisha Mapapa kutotambua Kingdom of Italy na pia kulalamika mara kwa mara kwa jamii ya kimataifa kwamba wanaishi kama wafungwa ndani ya kuta za Vatican kutokana na ukandamizaji wa Kingdom of Italy na hofu waliyonayo kutoka nje ya kuta za Vatican. Hii inatufikisha mpaka miaka ya 1920s wakati wa utawala wa Benito Mussolini akiwa Waziri Mkuu wa Italy. Mussolini alichoshwa na malalamiko haya ya Papa na majibizano ya kila mara huku Papa bado akishikilia msimamo wa kutoitambua Italy Mussolini mwanasiasa mahiri kama ajulikanavyo akaona fursa hapa ya kuandika jina lake kwenye vitabu vya historia. Akapendekeza makubaliano maalumu kwa Papa. Kwamba atafanya yafuatayo; 1. Italy itatoa ardhi ya Vatican kwa Papa na iwe himaya/nchi iliyo chini ya utawala wa Papa. 2. Italy itatoa fedha kama fidia kwa Papa kutokana na manyanyaso ya miaka yote. Mussolini alihitaji Papa kufanya yafuatayo; 1. Papa atambue Italy kuwa ni nchi. 2. Papa asijihusishe wala kutoa maoni yoyote kuhusu masuala ya kisiasa na vita. Papa na Mussolini wakafikia makubaliano na mikataba ikasainiwa na hapa ndipo taifa dogo zaidi duniani likazaliwa, Vatican. Vatican ikaanza kujiendesha kama taifa linalojitegemea kwa kuwa na sarafu yake, serikali yake, Polisi wake, jela yake (ndio kuna jela Vatican), Posta yake, Plate number zake, Passport zake na kadhalika na kadhalika. Vatican si kama nchi nyingine duniani kwa hiyo usidhani kwamba tayari umeielewa Vatican, hicho nilichoeleza ni theluthi tu mkanganyiko wa kuielewa Vatican kama nchi… kunywa tena glass ya maji and relax!! Nitaeleza tena kidogo… Ili kuielewa Vatican walau kiduchu kuna watu wawili tunapaswa kuwafahamu; 1. Papa 2. Mfalme wa Vatican Na pia kuna vitu viwili vya kuvielewa; 1. The Holy See 2. Vatican City Tuanze kimoja kimoja… *1. Papa* Hii sihitaji kueleza sana karibia wote tunafahamu. Lakini kwa msingi wa awali kabisa, Papa ni askofu wa Wakatoliki wote waliopo Rome/Vatican lakini kwa kuwa yeye pia ndiye kiongozi wa Wakatoliki wote duniani ndio sababu ya Uaskofu wake kuwa Papa. *2. The Holy See* Kabla sijaeleza chochote kuhusu Mfalme wa Vatican kwanza nieleze kuhusu The Holy See. Hili ni moja ya mambo magumu zaidi kuyaelewa kuhusu Vatican. Nitaeleza kwa lugha nyepesi na uchache ili tusipasue vichwa kwa mikanganyiko. Kwa tafsiri nyepesi Holy See ni 'Throne' ya Papa (nakosa neno zuri la kiswahili, sipendezwi sana na tafsiri ya 'Kiti cha Enzi'). Ni kwamba, maaskofu wote ndani ya kanisa Katoliki wanakuwa na 'throne' lakini kwa kuwa 'throne' ya Papa ni maalumu (kiongozi wa Wakatoliki wote duniani) kwa hiyo throne yake inakuwa muhimu zaidi na inaitwa 'The Holy See'. Mapapa wanabadilika lakini The Holy See iko na itaendelea kuwepo siku zote. Yaani kwa mfano Papa anapofariki au kustaafu kama tulivyoona mwaka juzi, Makadinali wanapokusanyika Vatican kwa uhalisia wanaenda kumchagua Kadinali mwenzao ambaye atakalia 'throne' ya 'Holy See'. Kwa 'angle' nyingine tunaweza kusema kwamba 'The Holy See' ndiyo sheria na mamlaka yote inayofanya kanisa Katoliki kuwa namna lilivyo. Pia sheria zote za kanisa Katoliki na mfumo wake unatengenezwa na The Holy See (sio Papa). Pia tunaweza kusema kwamba Benito Mussolini alipofanya makubaliano na Vatican aliingia mkataba ule na 'The Holy See'. Pia unaweza usiamini lakini katika nyanja za sheria za kimataifa 'The Holy See' inatambulika kama mtu/kampuni halisi ambaye amesajiliwa kisheria. Labda nitumie lugha nyepesi zaidi ya mfano… ukitaka kuelewa The Holy See, chukulia mfano huu kwamba Holy See ni "Catholic Church Inc." alafu Papa ndiye CEO. Nimejitahidi kueleza kwa kifupi na kwa wepesi niwezavyo, kuielewa kwa undani zaidi The Holy See labda tunapaswa kuandaa andishi maalumu mahususi kwa ajili yake tu. *3. Mfalme wa Vatican* Mfalme wa Vatican ni mtawala mwenye mamlaka yote juu ya nchi ya Vatican na hii inaifanya Vatican kuwa moja kati ya nchi sita pekee duniani zenye wafalme wenye mamlaka kamili (absolute monarchy). Nchi nyingine tano ni Saudi Arabia, Brunei, Oman, Qatar, Oman na Swaziland. Hii ndio sababu kwanini Vatican hawawezi kujiunga na Umoja wa Ulaya kwa sababu EU wanakubali nchi zenye mfumo wa kidemokrasia pekee. Japokuwa Vatican ina tawi la 'bunge' ambalo linaundwa na makadinali wa Vatican ambayo wanatunga sheria za 'nchi' lakini bado mfalme wa Vatican anauwezo wa kuveto maamuzi yoyote ambayo wamefikia. *Swali: Kwanini hatusikii chochote kuhusu Mfalme wa Vatican??* Ni kwa sababu Mfalme wa Vatican na Papa ni wajibu na mamlaka mbili tofauti lakini zinakaliwa na mtu mmoja, Papa wa Kanisa Katoliki. Hii inatupa kitu kingine cha kipekee kuhusu Vatican. Papa anachaguliwa na makadinali wenzake - Demokrasia. Lakini Mfalme hachaguliwi. Hii inafanya Vatican kuwa nchi pekee kwenye historia ya dunia kuwa na Mfalme mwenye mamlaka kamili ambaye si wa kurithi na anapatikana kidemokrasia (Elected non-heridetary absolute Monarchy). Kwa hiyo Papa kulingana na muktadha na mazingira ya suala husika kuna muda anatumia mamlaka yake kama Papa na muda mwingine inampasa kutumia mamlaka yake kama Mfalme wa Vatican. Bado kuna mkanganyiko??? Zingatia mfano huu rahisi; tuseme kwamba kuna kampuni fulani kubwa ya kimataifa inaitwa Aman Enterprises (The Holy See kwa mada yetu). Aman Enterprises wakafanikiwa kuishwishi Tanzania kuwapatia kisiwa cha Mbudya na Bold Enterprises wanakibadilisha kisiwa cha Mbudya kuwa nchi inayojitegemea, labda iitwe Aman Land (Vatican City kwa mfano wetu). Sasa CEO wa kampuni Bwana Aman (Papa kwa mada yetu) anahamishiamanya makao makuu ya kampuni mpaka Aman Land. Kwa kuwa Aman Land sasa ni nchi, CEO wa kampuni anakuwa pia mtawala wa nchi hii, Mfalme. . Kwa hiyo kwa manufaa ya kampuni kutumia 'connection' zake za kimataifa kunufaisha taifa lake la Aman Land ni vyema kutumia mamlaka kama CEO wa Bold Enterprises na kuna muda akihitaji nchi yake ya Aman Land kutunga sheria na taratibu ambazo zitanufaisha kampuni izidi kushamiri ni vyema kutumia mamlaka yake kama Mfalme wa Aman Land. Haya ndio mamlaka mawili yaliyo chini ya mtu mmoja ndani ya vatican, Papa na Mfalme wa Vatican. Bado kuna mkanganyiko??? Kama haujaelewa sawia usihofu kwa maana bado kuna hata nchi nyingine duniani bado hawaelewi sawa sawa mfumo mzima wa Vatican. Mfano, Umoja wa Mataifa wamekubali The Holy See (corporation) kama mwanachama wake lakini sio Vatican City nchi yenyewe. Passports za raia wa Vatican zinatolewa na The Holy See na sio Vatican na zinakubalika kwenye nchi nyingine japokuwa The Holy See kimataifa inatambulika kisheria kama Kampuni inayojitegemea. Na hapa tuongee kiduchu pia kuhusu raia wa Vatican. Katika nchi nyingine raia wa wanaongezeka kutokana na kuzaliana lakini hapa Vatican hakuna hilo kutokana na idadi ndogo ya wanaweka kiasi kwamba karibia ni asilimia sufuri. Namna pekee ya kuwa raia wa Vatican ni kwa kupewa uraia na Mfalme wa Vatican ili uishi Vatican kama moja wa wasaidizi wa Papa (ambaye ndiye mfalme). Kwa hiyo siku ukiacha kazi, yaani usaidizi wako kwa Papa ukifikia kikomo, Mfalme wa Vatican (ambayr ndiye Papa) anaondoa uraia wako na unarudi kwenu. Katika muda wowote ule raia wa nchi ya Vatican wanakadiriwa kuwa jumla karibia ya 500 ambao ndio idadi ndogo zaidi ya raia kwa nchi na ndogo kushinda hata idadi ya watu wanaoishi kwenye ghorofa moja kwenye nchi nyingi. Na raia wote hawa ni wafanyakazi wa Papa/The Holy See ambao wanapewa uraia na Mfalme (ambaye ndiye Papa) ambapo wanafanya kazi kama Makadinali, Wanadiplomasia, walinzi au kazi nyingine za kikanisa. Kwa ufupi sana hii ndio picha halisi ya nchi ya Vatican… na hapa ndipo ambapo maisha ya kiroho ya wafuasi zaidi ya Billioni 2 yanapoendeshwa…
    Like
    2
    ·317 Vue
  • JE UNAFAHAMU JINA HALISI LA JOSEPH KABILA ANAITWA "HYPOLITE KANAMBE KAZEMBEREMBE"? NA NI MTOTO WA KUFIKIA WA LAURENT DESIRE KABILA?.

    Kumekuwepo maswali mengi sana ndani ya Kongo DRC na nchi nyingi Afrika juu ya uhalisia wa Joseph Kabila Kabange (JKK) kuhusishwa na Unyarwanda (Rwandese), kumetolewa taarifa nyingi za siri zinazo mtaja JKK kuwa sio mtoto wa kuzaa wa Mzee Laurent Desiree Kabila raisi wa tatu wa Kongo DRC na kiongozi wa zamani wa kundi la uasi la AFDL, aliye uondosha madarakani utawala wa vipindi virefu wa Mobutu Seseseko Kuku Ngwendu wa Zabanga kupitia ile iliyoitwa Operation Banyamrenge/Bahima.

    Joseph Kabila mwenyewe na wafuasi wake wamekuwa wakikanusha hilo na kuhusisha taarifa hizo na njama chafu za kumchafua. Mwaka 2010 kwenye maadhimisho ya miaka kumi ya kifo cha Laurent Desire Kabila, Joseph Kabila mwenyewe alitoa maelezo kuhusiana na taarifa hizo zinazo muhusisha na unyarwanda. Pamoja na maelezo yaliyokanusha ya yeye kuhusishwa na taarifa hizo bado kumekuwepo taarifa na ushahidi mwingi unaoendelea kutolewa kuthibitisha kuwa Joseph Kabila ni Mnyarwanda na sio mtoto wa kuzaa wa Mzee Kabila.

    Moja ya tafiti hizo zinazo zungumzia sintofahamu hii ya Joseph Kabila ni "Waraka" ulio chapishwa na jarida la "Africa Federation" jarada hilo lilipewa jina la (titled) : CONCERNING THE TRUE IDENTITY OF MR. HYPPOLITE KANAMBE ALIAS “JOSEPH KABILA” ndani ya jarida lina mtaja Joseph Kabila kuwa sio mtoto wa kuzaliwa na Kabila mzee, waraka huu unaonesha kuwa mke wa Kabila mzee aliyeitwa Sifa Mahanga alikuwa na watoto sita (6) tu ambao alizaa na mzee Laurent-Desire Kabila. Kati ya watoto hao ambao Sifa Mahanga mke wa mzee Kabila alio zaa nao ni Josephine, Cecile, Masengo, Gloria, Kiki and Maguy. Katika list hiyo Joseph kabila hayumo.

    Je huyu Joseph Kabila Kabangee (JKK) anaye tajwa kuwa sio mtoto wa kuzaa (biological child) wa Mzee Kabila ni nani? Kimsingi huyu Joseph Kabila aliyekuwa rais wa nne wa taifa la Kongo DRC jina lake halisi anaitwa Hypolitte Christopher Kanambe na alizaliwa tarehe 04 June 1971 katika kijiji kidogo cha Hewabora, kilichopo katika mji wa Fizi jimboni Kivu ya kusini (South Kivu Province in the Eastern Congo) huku baba yake akiitwa Christopher Kanambe Kazemberembe na mama yake akiitwa Marcellina Mukambukuje.

    Baba yake alikuwa ni muasi kutoka kabila la Watuttsi aliyepinga utawala wa Juvenal Habyarimana raisi wa Rwanda kipindi hicho. Huyo Christopher Kanambe alikimbia Rwanda yeye na familia yake na kukimbilia nchini Kongo DRC mwaka 1960 baada ya machafuko ya kwanza ya kikabila nchini Rwanda yaliyo anza mwaka 1959, na katika harakati hizo za kutaka kuuondoa utawala wa Juvenal Habyarimana madarakani akafanikiwa kutana na Mzee Laurent Kabila mwaka 1964 aliyekuwa kwenye mapigano ya kumpinga Mobutu Seseseko huko mashariki ya Kongo DRC ,wakawa marafiki chanda na pete kwenye issue zao za kivita.

    Baada ya kukutana na kuendelea na ushirikiano wao kwa makubaliano kwamba Mzee Kabila amsaidie Christopher Kanambe kumuondoa Juvenal Habyalimana madarakani kisha yeye atamsaidia Kabila kumuondosha Mobutu ikulu ya Kinshasa. Walikubaliana hayo kwakua utawala wa Mobutu ulikuwa umewekeza base yake kubwa Rwanda chini ya utawala wa Juvenal Habyalimana (Mtoto wake wa ubatizo) hivyo kufatia sababu hizo Rwanda ilikuwa kikwazo kikubwa kufanikisha mapambano dhidi ya utawala wa Mobutu.

    Mwaka 1977 bwana Christopher Kanambe ambae ndie baba yake wa kumzaa Joseph Kabila alifariki dunia (duru za ndani zinataja Mzee kabila kuhusika, tutalitazama hili baadae) na kwa mujibu wa mila zao na taratibu za kijeshi ilibidi kabila amrithi mke wa Kanambe yani huyo mwanamama Marcellina pamoja na watoto wake wawili mapacha ambao ni Hypolitte na Jenny (wale wa karibu na escape 1 mnakumbuka utajiiri na matanuzi ya huyu dada).

    Baada ya kuchukuliwa na Mzee Kabila wote rasmi wakaanza kuitwa kabila, yani huyo Hypolite na Jenny walibadili majina yao kwa Hypolite kuitwa Joseph kabila na huyo Jenny kuitwa Jennifer Kabila. Ila katika harakati za Mzee Kabila za mapambano yalipo mzidi alikimbilia Tanzania na familia yake ingawaje alikuwa na wanawake 13 na watoto 25 katika sehemu mbalimbali huko Kongo DRC.

    Huyu Joseph Kabila (JKK) a.k.a Hypolite ni mpwa wa mkuu wa majeshi wa zamani wa Rwanda anae aitwaye James kabarebe na hadi mwaka 1996 huyu Hypolite alikuwa ni dereva wake kwenye vita ya Banyamulenge ya kumsaidia Mzee Kabila kumtoa Mobutu madarakani, hilo linathibitishwa na waziri wa mambo ya nje kipindi cha utawala wa Mzee Kabila aliyeitwa Bizima Karaha ambae alikuwa ni mnyarwanda, ambae mara kadhaa Karaha anasema anakumbuka kumuona Kabila akiwa dereva wa Kabarebe mwaka 94 na 95 alikuwa porini na jeshi la kagame la RPF ambalo lilikuwa likimsaidia Mzee Kabila katika vita vya msituni dhidi ya Mobutu.

    Je ni Kwanini Joseph Kabila alipewa uraisi wa Kongo DRC kama hakuwa raia wa Kongo DRC? Katika kujibu swali hilo na kulielewa vizuri ni vyema turejee historia ya kifo cha baba yake Kabila aliyeitwa Christopher Kanambe ambae alikuwa ni mtusi wa Rwanda. plan hii ya kupewa uraisi Joseph Kabila ni plan iliyo injiniwa na Paul Kagame rais wa Rwanda ambae baada ya kuvulugana na Mzee Kabila kufatia kukwama kwa makubaliano ya kile kilichoitwa "Mkataba wa Lemela" ilikuwa ni mpango wa kumuondoa Laurent Kabila duniani na kumuweka mnyarwanda huyu Joseph (Hypolite) mkakati huu ulifanyika kwa umakini wa hali ya juu sana ambapo kijasusi mbinu hizi huitwa "TROJAN HORSE TECHNIC".

    Sasa turejee kwenye habari ya kifo cha BABA YAKE HYPPOLITE........
    Christopher Kanambe Kazemberembe na Mzee Laurent Kabila walikutana na kuanza ushirikiano wao mwaka 1964 kila mmoja akiwa anapambania nchi yake, Kanambe Vs Wahutu (Juvenal Habyarimana) na Kabila Vs Mobutu Seseseko, kufatia mapambano hayo mambo yakawa magumu mwaka 1966 kufatia jeshi la Mobutu kujibu mapigo kwa kusambalatisha uasi wote huko mashariki ya Kongo, kufatia hali hiyo Kanambe na Kabila wakakimbilia Tanzania chini ya mwamvuli wa P.R.P. (Parti de la Revolution du Peuple).

    Baada ya vita ya Moba, Mobutu seseseko alituma watu kumuhonga hela nyingi Christopher Kanambe ambaye ni baba halisi wa Joseph Kabila ili amuue Laurent Kabila lakini mission ilibuma, baada ya mzee Laurent kabila kupenyezewa taarifa hizo, hivyo Kabila akaitisha kikao sehemu iitwayo Nyunzu huko mashariki ya Kongo DRC wanajeshi wake kadhaa wakapatikana na hatia akiwemo Christopher kanambe na wakahukumiwa kifo, lakini kabla ya hukumu ya Christopher Kanambe kutekelezwa aliuwawa na askali wake mwaka 1977 kisha huyo askali nae kuuwawa na walinzi wa Kanambe.

    Baada ya kifo cha Kanambe Laurent Desiree Kabila akamuoa Marcelina mke wa Kanambe na kuwa adopt watoto wake mapacha Jenny na Hypolitte......... Ukweli ni kwamba huyu Hypolite (JKK) alizaliwa Kongo, na baba yake Christopher Kanambe alikuwa ukimbizini akifanya uasi dhidi ya serikali ya wahutu ya Habyarimana, na baada ya kifo chake zilitumika mila za kivu, kurithiwa na mzee Kabila.

    Joseph Kabila, jina lake harisi anaitwa Hyppolite Kanambe Kazemberembe, baba yake wa kufikia Mzee Laurent Kabila alikua na wake zaidi ya 13 na watoto zaidi ya 25 na wengine hawajulikani kwani mzee Kabila hakua na muda wa kuwalea watoto hao kwani kipindi wanaishi Msasani Dar es salaam ambako Hyppolite Kanambe alilazimika kufanya kazi za ufundi, taxi dreva na barman katika Jiji la Dar es salaam na Kigoma kipindi hicho baba yake wa kufikia Laurent Desiree Kabila alikua ana ishi Tanzania huku anapigana vita na Mobutu Sese Seko huko Kongo DRC wakati huo ikiitwa Zaire.

    Mwaka 1995, Hyppolite Kanambe aliamua kurudi kwao Rwanda ambako alipokelewa na mjomba wake James Kabarebe, ambae alikuwa ni mkuu wa intelijensia ya Rwandan Patriotic Army (APR), alimkaribisha Kanambe nyumabni kwake na kumtafutia kazi ya udereva wa ma lori na baadae akawa dereva wake katika jeshi.

    Mwaka 1996, Marekani ilipoandaa shambulio dhidi ya Zaire, kupitia ile iliyoitwa "Operation Banyamrenge" chini ya Paul Kagame, Kagame alimchagua Kanal James Kabarebe kuwa kiongozi mkuu wa Operation hiyo na kuhakikisha Mobutu anapinduliwa.

    Katika kuajilia wanajeshi watakao husika na operation hiyo Banyamrenge Kabarebe aliamua kumweka mpwa wake Hyppolite Kanambe (Joseph Kabila) katika mazoezi ya kijeshi ili baadae ampatie nafasi jeshini, baada ya Hippolyte Kanambe kuhitimu mafunzo aliajiliwa kwenye jeshi la Rwanda kupitia mgongo wa James Kabarebe na alitumika katika jeshi la Rwanda kuanzia mwaka 1995 mpaka 1997, na alitumika pia kama mlinzi wa kagame kuanzia mwaka 1997 mpaka mwaka 1998 alipo rudi Kongo DRC na kuteuliwa kuwa Major General kwenye special Force iliyokuwa ikiendesha operation maalumu huko mashariki ya Kongo DRC.

    Je Kuna uhusiano wowote wa Joseph Kabila kuhusika katika mauaji ya Laurent Desiree Kabila?... Je kuna lolote lile linalohusishwa na ulipaji kisasi cha baba yake marehemu Kanambe Kazemberembe? Au upi uhusiano baina ya "Operation Banyamrenge" na mkakati wa Bahima Platform dhidi ya Joseph kabila na kifo cha Mzee Kabila?... Itaendelea sehemu ya pili.

    Endelea kuwa na mimi katika sehemu ya Pili kupata majibu ya maswali hayo....upate kujua kuwa nchi ya Kongo DRC bado ipo contolled by remote from kigali maana Tshisekedi ni pambo tu.

    Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
    ®Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

    Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
    © Copy rights of this article reserved
    ®written by Comred Mbwana Allyamtu
    JE UNAFAHAMU JINA HALISI LA JOSEPH KABILA ANAITWA "HYPOLITE KANAMBE KAZEMBEREMBE"? NA NI MTOTO WA KUFIKIA WA LAURENT DESIRE KABILA?. Kumekuwepo maswali mengi sana ndani ya Kongo DRC na nchi nyingi Afrika juu ya uhalisia wa Joseph Kabila Kabange (JKK) kuhusishwa na Unyarwanda (Rwandese), kumetolewa taarifa nyingi za siri zinazo mtaja JKK kuwa sio mtoto wa kuzaa wa Mzee Laurent Desiree Kabila raisi wa tatu wa Kongo DRC na kiongozi wa zamani wa kundi la uasi la AFDL, aliye uondosha madarakani utawala wa vipindi virefu wa Mobutu Seseseko Kuku Ngwendu wa Zabanga kupitia ile iliyoitwa Operation Banyamrenge/Bahima. Joseph Kabila mwenyewe na wafuasi wake wamekuwa wakikanusha hilo na kuhusisha taarifa hizo na njama chafu za kumchafua. Mwaka 2010 kwenye maadhimisho ya miaka kumi ya kifo cha Laurent Desire Kabila, Joseph Kabila mwenyewe alitoa maelezo kuhusiana na taarifa hizo zinazo muhusisha na unyarwanda. Pamoja na maelezo yaliyokanusha ya yeye kuhusishwa na taarifa hizo bado kumekuwepo taarifa na ushahidi mwingi unaoendelea kutolewa kuthibitisha kuwa Joseph Kabila ni Mnyarwanda na sio mtoto wa kuzaa wa Mzee Kabila. Moja ya tafiti hizo zinazo zungumzia sintofahamu hii ya Joseph Kabila ni "Waraka" ulio chapishwa na jarida la "Africa Federation" jarada hilo lilipewa jina la (titled) : CONCERNING THE TRUE IDENTITY OF MR. HYPPOLITE KANAMBE ALIAS “JOSEPH KABILA” ndani ya jarida lina mtaja Joseph Kabila kuwa sio mtoto wa kuzaliwa na Kabila mzee, waraka huu unaonesha kuwa mke wa Kabila mzee aliyeitwa Sifa Mahanga alikuwa na watoto sita (6) tu ambao alizaa na mzee Laurent-Desire Kabila. Kati ya watoto hao ambao Sifa Mahanga mke wa mzee Kabila alio zaa nao ni Josephine, Cecile, Masengo, Gloria, Kiki and Maguy. Katika list hiyo Joseph kabila hayumo. Je huyu Joseph Kabila Kabangee (JKK) anaye tajwa kuwa sio mtoto wa kuzaa (biological child) wa Mzee Kabila ni nani? Kimsingi huyu Joseph Kabila aliyekuwa rais wa nne wa taifa la Kongo DRC jina lake halisi anaitwa Hypolitte Christopher Kanambe na alizaliwa tarehe 04 June 1971 katika kijiji kidogo cha Hewabora, kilichopo katika mji wa Fizi jimboni Kivu ya kusini (South Kivu Province in the Eastern Congo) huku baba yake akiitwa Christopher Kanambe Kazemberembe na mama yake akiitwa Marcellina Mukambukuje. Baba yake alikuwa ni muasi kutoka kabila la Watuttsi aliyepinga utawala wa Juvenal Habyarimana raisi wa Rwanda kipindi hicho. Huyo Christopher Kanambe alikimbia Rwanda yeye na familia yake na kukimbilia nchini Kongo DRC mwaka 1960 baada ya machafuko ya kwanza ya kikabila nchini Rwanda yaliyo anza mwaka 1959, na katika harakati hizo za kutaka kuuondoa utawala wa Juvenal Habyarimana madarakani akafanikiwa kutana na Mzee Laurent Kabila mwaka 1964 aliyekuwa kwenye mapigano ya kumpinga Mobutu Seseseko huko mashariki ya Kongo DRC ,wakawa marafiki chanda na pete kwenye issue zao za kivita. Baada ya kukutana na kuendelea na ushirikiano wao kwa makubaliano kwamba Mzee Kabila amsaidie Christopher Kanambe kumuondoa Juvenal Habyalimana madarakani kisha yeye atamsaidia Kabila kumuondosha Mobutu ikulu ya Kinshasa. Walikubaliana hayo kwakua utawala wa Mobutu ulikuwa umewekeza base yake kubwa Rwanda chini ya utawala wa Juvenal Habyalimana (Mtoto wake wa ubatizo) hivyo kufatia sababu hizo Rwanda ilikuwa kikwazo kikubwa kufanikisha mapambano dhidi ya utawala wa Mobutu. Mwaka 1977 bwana Christopher Kanambe ambae ndie baba yake wa kumzaa Joseph Kabila alifariki dunia (duru za ndani zinataja Mzee kabila kuhusika, tutalitazama hili baadae) na kwa mujibu wa mila zao na taratibu za kijeshi ilibidi kabila amrithi mke wa Kanambe yani huyo mwanamama Marcellina pamoja na watoto wake wawili mapacha ambao ni Hypolitte na Jenny (wale wa karibu na escape 1 mnakumbuka utajiiri na matanuzi ya huyu dada). Baada ya kuchukuliwa na Mzee Kabila wote rasmi wakaanza kuitwa kabila, yani huyo Hypolite na Jenny walibadili majina yao kwa Hypolite kuitwa Joseph kabila na huyo Jenny kuitwa Jennifer Kabila. Ila katika harakati za Mzee Kabila za mapambano yalipo mzidi alikimbilia Tanzania na familia yake ingawaje alikuwa na wanawake 13 na watoto 25 katika sehemu mbalimbali huko Kongo DRC. Huyu Joseph Kabila (JKK) a.k.a Hypolite ni mpwa wa mkuu wa majeshi wa zamani wa Rwanda anae aitwaye James kabarebe na hadi mwaka 1996 huyu Hypolite alikuwa ni dereva wake kwenye vita ya Banyamulenge ya kumsaidia Mzee Kabila kumtoa Mobutu madarakani, hilo linathibitishwa na waziri wa mambo ya nje kipindi cha utawala wa Mzee Kabila aliyeitwa Bizima Karaha ambae alikuwa ni mnyarwanda, ambae mara kadhaa Karaha anasema anakumbuka kumuona Kabila akiwa dereva wa Kabarebe mwaka 94 na 95 alikuwa porini na jeshi la kagame la RPF ambalo lilikuwa likimsaidia Mzee Kabila katika vita vya msituni dhidi ya Mobutu. Je ni Kwanini Joseph Kabila alipewa uraisi wa Kongo DRC kama hakuwa raia wa Kongo DRC? Katika kujibu swali hilo na kulielewa vizuri ni vyema turejee historia ya kifo cha baba yake Kabila aliyeitwa Christopher Kanambe ambae alikuwa ni mtusi wa Rwanda. plan hii ya kupewa uraisi Joseph Kabila ni plan iliyo injiniwa na Paul Kagame rais wa Rwanda ambae baada ya kuvulugana na Mzee Kabila kufatia kukwama kwa makubaliano ya kile kilichoitwa "Mkataba wa Lemela" ilikuwa ni mpango wa kumuondoa Laurent Kabila duniani na kumuweka mnyarwanda huyu Joseph (Hypolite) mkakati huu ulifanyika kwa umakini wa hali ya juu sana ambapo kijasusi mbinu hizi huitwa "TROJAN HORSE TECHNIC". Sasa turejee kwenye habari ya kifo cha BABA YAKE HYPPOLITE........ Christopher Kanambe Kazemberembe na Mzee Laurent Kabila walikutana na kuanza ushirikiano wao mwaka 1964 kila mmoja akiwa anapambania nchi yake, Kanambe Vs Wahutu (Juvenal Habyarimana) na Kabila Vs Mobutu Seseseko, kufatia mapambano hayo mambo yakawa magumu mwaka 1966 kufatia jeshi la Mobutu kujibu mapigo kwa kusambalatisha uasi wote huko mashariki ya Kongo, kufatia hali hiyo Kanambe na Kabila wakakimbilia Tanzania chini ya mwamvuli wa P.R.P. (Parti de la Revolution du Peuple). Baada ya vita ya Moba, Mobutu seseseko alituma watu kumuhonga hela nyingi Christopher Kanambe ambaye ni baba halisi wa Joseph Kabila ili amuue Laurent Kabila lakini mission ilibuma, baada ya mzee Laurent kabila kupenyezewa taarifa hizo, hivyo Kabila akaitisha kikao sehemu iitwayo Nyunzu huko mashariki ya Kongo DRC wanajeshi wake kadhaa wakapatikana na hatia akiwemo Christopher kanambe na wakahukumiwa kifo, lakini kabla ya hukumu ya Christopher Kanambe kutekelezwa aliuwawa na askali wake mwaka 1977 kisha huyo askali nae kuuwawa na walinzi wa Kanambe. Baada ya kifo cha Kanambe Laurent Desiree Kabila akamuoa Marcelina mke wa Kanambe na kuwa adopt watoto wake mapacha Jenny na Hypolitte......... Ukweli ni kwamba huyu Hypolite (JKK) alizaliwa Kongo, na baba yake Christopher Kanambe alikuwa ukimbizini akifanya uasi dhidi ya serikali ya wahutu ya Habyarimana, na baada ya kifo chake zilitumika mila za kivu, kurithiwa na mzee Kabila. Joseph Kabila, jina lake harisi anaitwa Hyppolite Kanambe Kazemberembe, baba yake wa kufikia Mzee Laurent Kabila alikua na wake zaidi ya 13 na watoto zaidi ya 25 na wengine hawajulikani kwani mzee Kabila hakua na muda wa kuwalea watoto hao kwani kipindi wanaishi Msasani Dar es salaam ambako Hyppolite Kanambe alilazimika kufanya kazi za ufundi, taxi dreva na barman katika Jiji la Dar es salaam na Kigoma kipindi hicho baba yake wa kufikia Laurent Desiree Kabila alikua ana ishi Tanzania huku anapigana vita na Mobutu Sese Seko huko Kongo DRC wakati huo ikiitwa Zaire. Mwaka 1995, Hyppolite Kanambe aliamua kurudi kwao Rwanda ambako alipokelewa na mjomba wake James Kabarebe, ambae alikuwa ni mkuu wa intelijensia ya Rwandan Patriotic Army (APR), alimkaribisha Kanambe nyumabni kwake na kumtafutia kazi ya udereva wa ma lori na baadae akawa dereva wake katika jeshi. Mwaka 1996, Marekani ilipoandaa shambulio dhidi ya Zaire, kupitia ile iliyoitwa "Operation Banyamrenge" chini ya Paul Kagame, Kagame alimchagua Kanal James Kabarebe kuwa kiongozi mkuu wa Operation hiyo na kuhakikisha Mobutu anapinduliwa. Katika kuajilia wanajeshi watakao husika na operation hiyo Banyamrenge Kabarebe aliamua kumweka mpwa wake Hyppolite Kanambe (Joseph Kabila) katika mazoezi ya kijeshi ili baadae ampatie nafasi jeshini, baada ya Hippolyte Kanambe kuhitimu mafunzo aliajiliwa kwenye jeshi la Rwanda kupitia mgongo wa James Kabarebe na alitumika katika jeshi la Rwanda kuanzia mwaka 1995 mpaka 1997, na alitumika pia kama mlinzi wa kagame kuanzia mwaka 1997 mpaka mwaka 1998 alipo rudi Kongo DRC na kuteuliwa kuwa Major General kwenye special Force iliyokuwa ikiendesha operation maalumu huko mashariki ya Kongo DRC. Je Kuna uhusiano wowote wa Joseph Kabila kuhusika katika mauaji ya Laurent Desiree Kabila?... Je kuna lolote lile linalohusishwa na ulipaji kisasi cha baba yake marehemu Kanambe Kazemberembe? Au upi uhusiano baina ya "Operation Banyamrenge" na mkakati wa Bahima Platform dhidi ya Joseph kabila na kifo cha Mzee Kabila?... Itaendelea sehemu ya pili. Endelea kuwa na mimi katika sehemu ya Pili kupata majibu ya maswali hayo....upate kujua kuwa nchi ya Kongo DRC bado ipo contolled by remote from kigali maana Tshisekedi ni pambo tu. 👉📎Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment. ®Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu. Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu © Copy rights of this article reserved ®written by Comred Mbwana Allyamtu
    Like
    2
    ·363 Vue
Plus de résultats