• Raia wa Marekani wanazidi kuelekeza pesa zao kwenye kamari ya michezo (Betting) badala ya kufanya uwekezaji wa muda mrefu, jambo linalozua wasiwasi kuhusu hali ya kifedha Nchini humo. Utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa katika majimbo ambako kamari ya michezo imehalalishwa, kumekuwa na kupungua kwa akiba na uwekezaji katika mali thabiti kama vile hisa.

    Mwelekeo huu umeambatana na ongezeko la madeni ya kadi za mkopo, alama za chini za mkopo, na kuongezeka kwa kufilisika. Ingawa majimbo yamefaidika na mapato makubwa ya kodi kutoka kwa upanuzi huu wa kamari, athari zake pana za kiuchumi zinaonyesha mwenendo wa kusikitisha.

    Raia wa Marekani 🇺🇸 wanazidi kuelekeza pesa zao kwenye kamari ya michezo (Betting) badala ya kufanya uwekezaji wa muda mrefu, jambo linalozua wasiwasi kuhusu hali ya kifedha Nchini humo. Utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa katika majimbo ambako kamari ya michezo imehalalishwa, kumekuwa na kupungua kwa akiba na uwekezaji katika mali thabiti kama vile hisa. Mwelekeo huu umeambatana na ongezeko la madeni ya kadi za mkopo, alama za chini za mkopo, na kuongezeka kwa kufilisika. Ingawa majimbo yamefaidika na mapato makubwa ya kodi kutoka kwa upanuzi huu wa kamari, athari zake pana za kiuchumi zinaonyesha mwenendo wa kusikitisha.
    0 Kommentare ·0 Anteile ·141 Ansichten
  • PICHA YA SIMBA HUYU NI FUNZO MAISHANI:
    ------------------------------------------------------

    Hivi ndivyo mfalme wa pori anavyoonekana akiwa kwenye siku za mwisho za maisha yake. Jinsi alivyokonda, kujua idadi ya mbavu zake hata huitaji msaada wa calculator.

    Hii picha ilipigwa na "Larry Pannell."

    Alifanikiwa kupata picha ya Simba aliyekuwa kwenye hitimisho la kuvuta pumzi za mwisho. Katika huu ulimwengu wenye mafungamano na dhambi.

    "Larry Pannell" anasema:

    Nilimkuta huyu simba amelala kwenye majani. Akiwa amechoka, miguu ikionekana kumnyima ushirikiano wa kutembea.

    Sikuwa na lakufanya zaidi ya kusimama mita kadhaa. Macho yakifanya ushuhuda wa kutazama, "King of savannah" akipoteza uhai chini ya kivuli cha mti.

    Nikiwa nimesimama kimya. Nilishusha chini camera yangu. Tulitazamana na simba, tukafumba macho yetu pamoja.

    Jinsi mfalme wa nyika alivyokuwa akihangaika kuhema. Pumzi zilionekana kuwa bidhaa hadimu kwenye duka la mapafu yake.

    Kifua chake kilikuwa kikipanda na kushuka. Ishara ya kuonyesha anavuta pumzi za mwisho, kabla ya kukipa ruhusa kifo kiondoke na roho yake.

    Ghafla eneo alilolala Simba ukazaliwa ukimya. Mfalme wa pori akawa haemi wala kutikisika. Mauti ikawa imehitimisha simulizi ya ubabe wake mbugani.

    Hakika maisha ya binadamu na wanyama ni simulizi fupi sana."

    Haijalishi una nguvu kiasi gani. Kuna nyakati zitafika nguvu zitafanya mgomo wa kuishi mwilini mwako. Zitaupisha udhaifu uchukue nafasi ya kukutawala. Udhaifu nao ukikutawala, utayaita maradhi. Bila hiyari utajikuta umekigeuza kitanda kuwa rafiki."

    Kuna shule ya bure hapa: Nguvu tulizonazo ni kitu cha kupita. Hata uzuri umpao kiburi mwanamke una ukomo. Licha ya kujidanganya kwa make up na wanja. Lakini hawezi kuzuia muanguko wa mashavu, uzee unapoanza kumuondoa kwenye kundi la warembo.

    "Chini ya jua kila kitu kina mwanzo na mwisho."

    Hivyo katika maisha tusisahau kuvipa kipaumbele vitu hivi. Utu, wema, ukarimu, heshima, na unyenyekevu.

    Tusaidie wenye maradhi, tuwajali wasiojiweza, na viongozi tusitumie madaraka vibaya.

    Tutende mema tukiamini. Kuna siku pumzi zitamaliza mkataba wa kuishi ndani ya matundu ya pua zetu. Baada ya hapo sisi wote tutalala mauti."

    Imeandikwa na Green Osward
    PICHA YA SIMBA HUYU NI FUNZO MAISHANI: ------------------------------------------------------ Hivi ndivyo mfalme wa pori anavyoonekana akiwa kwenye siku za mwisho za maisha yake. Jinsi alivyokonda, kujua idadi ya mbavu zake hata huitaji msaada wa calculator. Hii picha ilipigwa na "Larry Pannell." Alifanikiwa kupata picha ya Simba aliyekuwa kwenye hitimisho la kuvuta pumzi za mwisho. Katika huu ulimwengu wenye mafungamano na dhambi. "Larry Pannell" anasema: Nilimkuta huyu simba amelala kwenye majani. Akiwa amechoka, miguu ikionekana kumnyima ushirikiano wa kutembea. Sikuwa na lakufanya zaidi ya kusimama mita kadhaa. Macho yakifanya ushuhuda wa kutazama, "King of savannah" akipoteza uhai chini ya kivuli cha mti. Nikiwa nimesimama kimya. Nilishusha chini camera yangu. Tulitazamana na simba, tukafumba macho yetu pamoja. Jinsi mfalme wa nyika alivyokuwa akihangaika kuhema. Pumzi zilionekana kuwa bidhaa hadimu kwenye duka la mapafu yake. Kifua chake kilikuwa kikipanda na kushuka. Ishara ya kuonyesha anavuta pumzi za mwisho, kabla ya kukipa ruhusa kifo kiondoke na roho yake. Ghafla eneo alilolala Simba ukazaliwa ukimya. Mfalme wa pori akawa haemi wala kutikisika. Mauti ikawa imehitimisha simulizi ya ubabe wake mbugani. Hakika maisha ya binadamu na wanyama ni simulizi fupi sana." Haijalishi una nguvu kiasi gani. Kuna nyakati zitafika nguvu zitafanya mgomo wa kuishi mwilini mwako. Zitaupisha udhaifu uchukue nafasi ya kukutawala. Udhaifu nao ukikutawala, utayaita maradhi. Bila hiyari utajikuta umekigeuza kitanda kuwa rafiki." Kuna shule ya bure hapa: Nguvu tulizonazo ni kitu cha kupita. Hata uzuri umpao kiburi mwanamke una ukomo. Licha ya kujidanganya kwa make up na wanja. Lakini hawezi kuzuia muanguko wa mashavu, uzee unapoanza kumuondoa kwenye kundi la warembo. "Chini ya jua kila kitu kina mwanzo na mwisho." Hivyo katika maisha tusisahau kuvipa kipaumbele vitu hivi. Utu, wema, ukarimu, heshima, na unyenyekevu. Tusaidie wenye maradhi, tuwajali wasiojiweza, na viongozi tusitumie madaraka vibaya. Tutende mema tukiamini. Kuna siku pumzi zitamaliza mkataba wa kuishi ndani ya matundu ya pua zetu. Baada ya hapo sisi wote tutalala mauti." Imeandikwa na Green Osward
    Love
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·378 Ansichten
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili hali ya usalama na kibinadamu Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku hali ikizidi kuzorota. Mwakilishi Maalum wa Umoja huo (UN) Nchini DR Congo, Bintou Keita, amesema Waasi wa kundi la M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda sasa wanadhibiti maeneo makubwa ya Mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini na kutishia kupanua mashambulizi yao hadi Mkoani Tshopo na Maniema.

    "Hivi karibuni M23 imesimika utawala wake kwa kuteua gavana, makamu gavana na meya huko Bukavu, Kivu Kusini," amesema Keita.

    Ameeleza kuwa mgogoro huo unahusiana na unyonyaji wa madini mashariki mwa DR Congo na kuzua wasiwasi wa kikanda. Pia amegusia hali mbaya ya kibinadamu, akisema kumekuwa na ongezeko la ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, utekaji nyara na ajira ya kulazimishwa kwa Vijana, wakiwemo Watoto.

    Licha ya makubaliano ya hivi karibuni kati ya Marais wa Rwanda na DR Congo Nchini Qatar , amani bado haijapatikana. Keita ametoa wito wa kuteuliwa kwa mpatanishi wa Umoja wa Afrika ili kuongoza juhudi za kusitisha mapigano.

    Balozi wa DR Congo katika Baraza la Umoja wa kimataifa (UN), Zénon Mukongo Ngay, ameishutumu Rwanda kwa kutotekeleza usitishaji mapigano, huku Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe, akisema Nchi yake itaendelea kuchukua "hatua za ulinzi" mpaka kuwe na mfumo wa kudumu wa usalama.

    Wakati huo huo, imeripotiwa kuwa DR Congo inakabiliwa na janga kubwa zaidi la njaa kuwahi kutokea, ambapo Watu zaidi ya milioni 27.7 wanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na vita na ukosefu wa utulivu mashariki mwa Nchi hiyo.

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili hali ya usalama na kibinadamu Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 huku hali ikizidi kuzorota. Mwakilishi Maalum wa Umoja huo (UN) Nchini DR Congo, Bintou Keita, amesema Waasi wa kundi la M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda 🇷🇼 sasa wanadhibiti maeneo makubwa ya Mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini na kutishia kupanua mashambulizi yao hadi Mkoani Tshopo na Maniema. "Hivi karibuni M23 imesimika utawala wake kwa kuteua gavana, makamu gavana na meya huko Bukavu, Kivu Kusini," amesema Keita. Ameeleza kuwa mgogoro huo unahusiana na unyonyaji wa madini mashariki mwa DR Congo na kuzua wasiwasi wa kikanda. Pia amegusia hali mbaya ya kibinadamu, akisema kumekuwa na ongezeko la ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, utekaji nyara na ajira ya kulazimishwa kwa Vijana, wakiwemo Watoto. Licha ya makubaliano ya hivi karibuni kati ya Marais wa Rwanda na DR Congo Nchini Qatar 🇶🇦, amani bado haijapatikana. Keita ametoa wito wa kuteuliwa kwa mpatanishi wa Umoja wa Afrika ili kuongoza juhudi za kusitisha mapigano. Balozi wa DR Congo katika Baraza la Umoja wa kimataifa (UN), Zénon Mukongo Ngay, ameishutumu Rwanda kwa kutotekeleza usitishaji mapigano, huku Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe, akisema Nchi yake itaendelea kuchukua "hatua za ulinzi" mpaka kuwe na mfumo wa kudumu wa usalama. Wakati huo huo, imeripotiwa kuwa DR Congo inakabiliwa na janga kubwa zaidi la njaa kuwahi kutokea, ambapo Watu zaidi ya milioni 27.7 wanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na vita na ukosefu wa utulivu mashariki mwa Nchi hiyo.
    0 Kommentare ·0 Anteile ·219 Ansichten
  • Rais wa Nchi ya Ukraine , Volodymyr Zelensky, ametabiri kuea Rais wa Urusi , Vladimir Putin, "atakufa hivi karibuni" huku kukiwa na tetesi kuwa afya ya Kiongozi huyo wa Urusi inazorota. Zelensky alitoa kauli hiyo katika mahojiano na Waandishi wa habari Jijini Paris, Ufaransa baada ya kukutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kusema kuwa "Putin atakufa hivi karibuni, na hilo ni jambo la uhakika."

    Picha za Putin zilizochunguzwa kwa muda zimezua uvumi kuhusu hali yake ya afya, hasa baada ya kuonekana na macho mekundu na alama ya ajabu kwenye mkono wake. Aidha, picha zingine zimeonyesha kovu shingoni mwake, likizua dhana kuwa huenda alipitia upasuaji wa saratani ya tezi dume.

    Ripoti za awali zilidai kuwa Putin alikuwa akifuatana mara kwa mara na Daktari bingwa wa saratani, huku uvujaji wa taarifa za kijasusi za Marekani ukionyesha kuwa alikuwa akipokea tiba ya saratani. Sanjari na hayo, amekuwa akionekana akiwa na miguu isiyo imara, akishika meza kwa nguvu, au akitikisa mguu wake mara kwa mara, hali inayoongeza mashaka kuhusu afya yake.

    Rais wa Nchi ya Ukraine 🇺🇦, Volodymyr Zelensky, ametabiri kuea Rais wa Urusi 🇷🇺, Vladimir Putin, "atakufa hivi karibuni" huku kukiwa na tetesi kuwa afya ya Kiongozi huyo wa Urusi inazorota. Zelensky alitoa kauli hiyo katika mahojiano na Waandishi wa habari Jijini Paris, Ufaransa 🇫🇷 baada ya kukutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kusema kuwa "Putin atakufa hivi karibuni, na hilo ni jambo la uhakika." Picha za Putin zilizochunguzwa kwa muda zimezua uvumi kuhusu hali yake ya afya, hasa baada ya kuonekana na macho mekundu na alama ya ajabu kwenye mkono wake. Aidha, picha zingine zimeonyesha kovu shingoni mwake, likizua dhana kuwa huenda alipitia upasuaji wa saratani ya tezi dume. Ripoti za awali zilidai kuwa Putin alikuwa akifuatana mara kwa mara na Daktari bingwa wa saratani, huku uvujaji wa taarifa za kijasusi za Marekani 🇺🇸 ukionyesha kuwa alikuwa akipokea tiba ya saratani. Sanjari na hayo, amekuwa akionekana akiwa na miguu isiyo imara, akishika meza kwa nguvu, au akitikisa mguu wake mara kwa mara, hali inayoongeza mashaka kuhusu afya yake.
    0 Kommentare ·0 Anteile ·276 Ansichten
  • Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi

    CPA Amos Makala kiongozi wa juu wa CCM amesema kuwa Chadema wana mpango wa kununua virusi via Ebola na Mpox ili kuzuia uchaguzi!!

    Maswali yangu kufuatia kauli ya CPA Amos Makala

    1. Hizi taarifa Makala amezipata wapi ?

    2. Idara ya usalama wa taifa (TISS) inataarifa za mpango huu ?, kama hakuna taarifa turejee kwenye swali la kwanza! Kama kuna taarifa hadi sasa ni hatua gani zimechukuliwa?

    3. Makala anatuambia kwa lugha nyingine baadhi ya viongozi wa Chadema wana mpango wa uhaini na kuhujumu uchumi wa nchi je kwanini vyombo vipo kimya kwa watu wenye tuhuma nzito kama hizi ?

    4. Je Makala amepima madhara ya kauli aliyoitoa hadharani ambayo huenda inazua taharuki na hofu kwa wananchi wa Tanzania na kwa wageni amabao wana mpango wa kuitembelea Tanzania kwa siku za usoni ?

    5. Ni hatua gani za kujibu ambazo Chadema wamezichukua hadi sasa ?

    6. Je ni kauli ya maksudi tu ili kuhamisha upepo na mjadala wa chadema ambao utashika kasi kwenye mikutano yao ya hadhara inayoanza hivi punde, kuhusu mpango wao wa no reform no election ?

    7. Je Makala anaweza kuthibitishaje kauli yake kwa Umma ?

    8.Je Chadema watanunulia wapi hivyo virusi, na kumbe vinauzwaga, Makala anaweza kuthibitisha ?

    Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi CPA Amos Makala kiongozi wa juu wa CCM amesema kuwa Chadema wana mpango wa kununua virusi via Ebola na Mpox ili kuzuia uchaguzi!! Maswali yangu kufuatia kauli ya CPA Amos Makala 👇👇👇👇 1. Hizi taarifa Makala amezipata wapi ? 2. Idara ya usalama wa taifa (TISS) inataarifa za mpango huu ?, kama hakuna taarifa turejee kwenye swali la kwanza! Kama kuna taarifa hadi sasa ni hatua gani zimechukuliwa? 3. Makala anatuambia kwa lugha nyingine baadhi ya viongozi wa Chadema wana mpango wa uhaini na kuhujumu uchumi wa nchi je kwanini vyombo vipo kimya kwa watu wenye tuhuma nzito kama hizi ? 4. Je Makala amepima madhara ya kauli aliyoitoa hadharani ambayo huenda inazua taharuki na hofu kwa wananchi wa Tanzania na kwa wageni amabao wana mpango wa kuitembelea Tanzania kwa siku za usoni ? 5. Ni hatua gani za kujibu ambazo Chadema wamezichukua hadi sasa ? 6. Je ni kauli ya maksudi tu ili kuhamisha upepo na mjadala wa chadema ambao utashika kasi kwenye mikutano yao ya hadhara inayoanza hivi punde, kuhusu mpango wao wa no reform no election ? 7. Je Makala anaweza kuthibitishaje kauli yake kwa Umma ? 8.Je Chadema watanunulia wapi hivyo virusi, na kumbe vinauzwaga, Makala anaweza kuthibitisha ?
    0 Kommentare ·0 Anteile ·308 Ansichten
  • Historia ya Wazazi wa Jackie Chan inavutia zaidi hadi Jackie Chan aliamua kuandaa "Documentary" maalum kwa ajili ya kueleza Wazazi wake walivyokutana na walikuwa wanafanya kazi gani.

    Katika kipindi chote Jackie Chan alichoishi na Wazazi wake hakuwahi kufahamu Wazazi wake walikutana vipi pamoja na kazi halisi za awali za Wazazi wake mpaka hapo Baba yake alipokuwa ana umri wa miaka 80 akaamua kumwambia ukweli maana aliamini umri wake umeenda sana hivyo muda wowote anaweza kufariki bila kumueleza ukweli Jackie Chan.

    Baba Mzazi wa Jackie Chan, Charles Chan (1914 - 2008) siku moja akiwa barabarani kwenye gari na Jackie Chan alifunguka kuwa tangu zamani alikuwa Mpelelezi (Shushushu) kwenye Serikali ya China na Mama yake Jackie Chan, Lee-Lee Chan (1916-2002) alikuwa muuza madawa ya kulevya, siku moja katika "operation" ya kukamata Wauza madawa Charles Chan alimkamata Lee-Lee Chan lakini baada ya kumfikisha kwenye vyombo vya dola walijikuta wamependana na wakafunga ndoa.

    Hadithi hii ilimshitua sana Jackie Chan kwani amekua akijua kwamba Baba yake ni Mpishi na amewahi kuwa Mpishi kwenye ubalozi wa Ufaransa - Hong Kong, pamoja na ubalozi wa Marekani Nchini Australia .

    Taarifa nyingine iliyomshitua zaidi ni pale alipoambiwa kuwa kuwa jina la Baba yake sio Chan bali ni Fang Daolong, hivyo kama asingebadili jina, Jackie Chan hivi sasa angefahamika kama Jackie Fang, Baba Jackie Chan alikuwa "Spy" kwenye Serikali ya China iliyokuwa ikiundwa na Chama cha Kuomintang, mwaka 1949 baada ya vita kali ya wenyewe kwa wenyewe Chama cha Kikomunisti kikiongozwa na Mao Zedong kiliipindua Serikali ya Kuomintang kikachukua Nchi hapo ilibidi Baba Jackie Chan abadili jina kwa sababu ya kuficha utambulisho wake maana kulikuwa na vita kubwa baina ya vyama hivyo na baadhi ya makachero wa Kuomintang walikuwa wakikamatwa na kuuawa.

    Historia ya Wazazi wa Jackie Chan imeelezwa kwa urefu kwenye "Documentary" iliyoandaliwa na Jackie Chan "Traces of the Dragon: Jackie Chan and His Lost Family" (2003)

    "Baba alikua jasusi na Mama alikua Muuza madawa na mcheza kamari. Walikutana na wakaoana baada ya Baba yangu kumkamata Mama"

    "Tangu nilipokua Mdogo nilikua najua Baba yangu anafanya kazi ya upishi kwenye Ubalozi wa Marekani mpaka alipotimiza miaka 80 na akaniambia kazi yake ya kweli. Nilishtuka, nilishtuka"

    " Kwahiyo kuna siku moja nilikua naendesha gari nikiwa na Baba yangu ghafla, Baba akageuka na kusema: 'Jackie, Mimi ni Mzee sana na huenda nisiamke kesho. Kuna kitu lazima nikuambie, ni siri' kisha akasema: kwa kweli wewe sio Jackie Chan, jina lako unaitwa Fong.'

    "Nikahisi kupatwa na mshtuko, kwangu ilikua kitu cha kustaajabisha. Kwa haraka nikamuambia asiendelee kuongea nikampigia rafiki yangu ili tutengeneze documentary ya stori ya Baba yangu. Ilituchukua miaka 3 ya kumfata Baba yangu na kuongea nae kuhusu stori yote."

    " Nilihisi mimi ndiye Mwanae wa pekee lakini nilishtuka baada ya kujua kwamba nina ndugu zangu wanne kwa Wazazi wangu. Kaka zangu wawili, upande wa Baba na Dada zangu wawili upande wa Mama. Alilazimika kunificha yote hayo kwa sababu ya kazi yake, baba alikua jasusi. Nilivutiwa sana baada ya kujua kwamba Baba yangu alikua mpole sana. Miaka yote ile nilidhania ni Mpishi. Nimetengeneza movie kupitia hii stori." - Jackie Chan

    Historia ya Wazazi wa Jackie Chan inavutia zaidi hadi Jackie Chan aliamua kuandaa "Documentary" maalum kwa ajili ya kueleza Wazazi wake walivyokutana na walikuwa wanafanya kazi gani. Katika kipindi chote Jackie Chan alichoishi na Wazazi wake hakuwahi kufahamu Wazazi wake walikutana vipi pamoja na kazi halisi za awali za Wazazi wake mpaka hapo Baba yake alipokuwa ana umri wa miaka 80 akaamua kumwambia ukweli maana aliamini umri wake umeenda sana hivyo muda wowote anaweza kufariki bila kumueleza ukweli Jackie Chan. Baba Mzazi wa Jackie Chan, Charles Chan (1914 - 2008) siku moja akiwa barabarani kwenye gari na Jackie Chan alifunguka kuwa tangu zamani alikuwa Mpelelezi (Shushushu) kwenye Serikali ya China na Mama yake Jackie Chan, Lee-Lee Chan (1916-2002) alikuwa muuza madawa ya kulevya, siku moja katika "operation" ya kukamata Wauza madawa Charles Chan alimkamata Lee-Lee Chan lakini baada ya kumfikisha kwenye vyombo vya dola walijikuta wamependana na wakafunga ndoa. Hadithi hii ilimshitua sana Jackie Chan kwani amekua akijua kwamba Baba yake ni Mpishi na amewahi kuwa Mpishi kwenye ubalozi wa Ufaransa 🇫🇷 - Hong Kong, pamoja na ubalozi wa Marekani 🇺🇸 Nchini Australia 🇦🇺. Taarifa nyingine iliyomshitua zaidi ni pale alipoambiwa kuwa kuwa jina la Baba yake sio Chan bali ni Fang Daolong, hivyo kama asingebadili jina, Jackie Chan hivi sasa angefahamika kama Jackie Fang, Baba Jackie Chan alikuwa "Spy" kwenye Serikali ya China iliyokuwa ikiundwa na Chama cha Kuomintang, mwaka 1949 baada ya vita kali ya wenyewe kwa wenyewe Chama cha Kikomunisti kikiongozwa na Mao Zedong kiliipindua Serikali ya Kuomintang kikachukua Nchi hapo ilibidi Baba Jackie Chan abadili jina kwa sababu ya kuficha utambulisho wake maana kulikuwa na vita kubwa baina ya vyama hivyo na baadhi ya makachero wa Kuomintang walikuwa wakikamatwa na kuuawa. Historia ya Wazazi wa Jackie Chan imeelezwa kwa urefu kwenye "Documentary" iliyoandaliwa na Jackie Chan "Traces of the Dragon: Jackie Chan and His Lost Family" (2003) "Baba alikua jasusi na Mama alikua Muuza madawa na mcheza kamari. Walikutana na wakaoana baada ya Baba yangu kumkamata Mama" "Tangu nilipokua Mdogo nilikua najua Baba yangu anafanya kazi ya upishi kwenye Ubalozi wa Marekani mpaka alipotimiza miaka 80 na akaniambia kazi yake ya kweli. Nilishtuka, nilishtuka" " Kwahiyo kuna siku moja nilikua naendesha gari nikiwa na Baba yangu ghafla, Baba akageuka na kusema: 'Jackie, Mimi ni Mzee sana na huenda nisiamke kesho. Kuna kitu lazima nikuambie, ni siri' kisha akasema: kwa kweli wewe sio Jackie Chan, jina lako unaitwa Fong.' "Nikahisi kupatwa na mshtuko, kwangu ilikua kitu cha kustaajabisha. Kwa haraka nikamuambia asiendelee kuongea nikampigia rafiki yangu ili tutengeneze documentary ya stori ya Baba yangu. Ilituchukua miaka 3 ya kumfata Baba yangu na kuongea nae kuhusu stori yote." " Nilihisi mimi ndiye Mwanae wa pekee lakini nilishtuka baada ya kujua kwamba nina ndugu zangu wanne kwa Wazazi wangu. Kaka zangu wawili, upande wa Baba na Dada zangu wawili upande wa Mama. Alilazimika kunificha yote hayo kwa sababu ya kazi yake, baba alikua jasusi. Nilivutiwa sana baada ya kujua kwamba Baba yangu alikua mpole sana. Miaka yote ile nilidhania ni Mpishi. Nimetengeneza movie kupitia hii stori." - Jackie Chan
    Like
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·338 Ansichten
  • VITABU VYENYE NGUVU DUNIANI AMBAVYO HAUTAFUNDISHWA SHULENI: SIRI KUBWA YA UTAJIRI WA ULIMWENGU!

    Je, umefundishwa katika dini yako kuwa Biblia na Quran ndio vitabu pekee vyenye nguvu na maajabu? Ni kweli vitabu hivi ni miongoni mwa vitabu vyenye maajabu, ila kuna baddhi ya vitabu vinavyofichwa kutokana na nguvu zake za kubadili maisha ya watu, kwa utajiri ama wakawa masikini wa kutupwa na hata kuwa wenye mikosi mikubwa.

    Dunia imejawa siri ambazo wachache wanazitumia kujinufaisha na kujitajirisha, huku wakiwadanganya wengine Kuwa ili ufanikiwe basi wafaa upate muda wa kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa, uwe mvumilivu, Ufanye kazi kwa bidii na mambo mengine mengi,
    lakini hawakuambii mambo ya siri wanayoyafanya na vitabu vya siri wanavyosoma ili kukuza utajiri wao na mvuto wao katika ulimwengu.

    Leo hii nimekuletea vitabu vya siri zaidi ya Biblia na Quran, vyenye nguvu sana, na vinavyotumika kubadili maisha ya Matajiri wa dunia hii, na imebakia kuwa siri kwao, wakiificha kwa nguvu zote na kuhakikisha wachache wanaifahamu, huku wengi wakitiwa hofu ya kuiogopa siri hii na kuviona vitabu hivi kama vya mashetani.

    1. The Book of Abramelin the Mage – Kitabu cha kale cha uchawi kinachoeleza njia za kuwasiliana na malaika na nguvu za kichawi. Kitabu hiki kina nguvu za kukufundisha ushirikina na upeo wa juu unaopita uwezo wa kawaida wa mwanadamu.

    2.The Lesser Key of Solomon (Lemegeton) – Kitabu cha uchawi kinachodaiwa kuwa na mafundisho ya mfalme Sulemani kuhusu majini na roho. Ni kitabu kinachosadikika kuandikwa na mfalme wa Israel ajulikanaye kama sulemani, kikiwa kimejaa elimu ya kiroho, na namna ya kuyatumia majini katika shughuli za kila siku bila kutumia nguvu kubwa.

    3.Picatrix – Kitabu cha uchawi wa Kiarabu kinachoeleza jinsi ya kutumia nyota na sayari kwa utajiri. Masomo mengi yanayohusiana na nyota pamoja na bahati, hutolewa katika kitabu hiki cha ajabu. Kuna matamshi ya kiarabu katika kitabu hiki yenye nguvu ya kuleta maajabu usiyotarajia, ambayo sitayasema katika makala hii kwa kuwa sifundishi uchawi, nafunua siri zilizofichwa na mabeberu wachache ili waendelee kuitawala dunia hii kiuchumi na kuwa na nguvu ya ushawishi.

    4.The Kybalion – Kitabu cha Hermeticism kinachofundisha sheria saba za ulimwengu zinazodaiwa kuwa na nguvu za kimetafizikia, zinazoleta mvuto kwa watu wanaokutazama, ushawishi kwa wanaokusikiliza na Nguvu ya fedha.

    5. The Secret (Rhonda Byrne) – Kitabu kinachoelezea sheria ya mvutano (Law of Attraction) na jinsi ya kutumia mawazo kuvutia mafanikio na utajiri. Kitabu hiki ni cha ajabu maana kimejawa na siri zenye uwezo wa Kubadili uchumi wako.

    6. Necronomicon – Ingawa ni kitabu cha kubuniwa na H.P. Lovecraft, kimekuwa na hadithi nyingi zinazodai kuwa kina maelezo ya siri za ulimwengu. Usisome kitabu hiki maana kinaweza kuleta shida maishani mwako bila kupata mwongozo kamili.

    7.The Voynich Manuscript – Kitabu cha ajabu kilichoandikwa kwa lugha isiyojulikana na hakijafasiriwa hadi sasa. Kimekosa tafsiri yake kutokana na ukweli kuwa kiliandikwa katika lugha ambayo haipo hapa duniani, ama ilikuwapo ila imepotea.

    Vitabu hivi ndivyo vinavyowafanya watu kuwa na mvuto, na utajiri mkubwa duniani. Kwa kweli huwezi kuwa na mvuto mkubwa ama utajiri mkubwa duniani pasina kusoma vitabu hivi na kufuata kanuni zake, wenda kama utakuwa tajiri kijijini kwenu lakini si duniani.

    Nikiwa namalizia, kuna Vitabu vyenye nguvu ya kukutajirisha, vyenye nguvu ya kukulaani na hata kukuletea mikosi isiyokoma, ambavyo vimekuwa vikihifadhiwa kwa siri sana, ili kutumiwa na wachache kwa malengo mahususi. Wapo watu kadhaa wanaopinga nguvu ya maandishi katika vitabu wakiidharau na kuyaona maandishi kama herufi za kawaida sana, lakini ukweli ni kuwa kuna nguvu katika vitabu, kuna maajabu katika vitabu na kuna watu waliofunga maisha yao kwa kusoma vifungu fulani kimakosa katika vitabu. Hebu kuwa makini na kila kitabu unachosoma. Hakikisha kwanza kitabu usomacho ni salama, maana kuna vitabu kama vile "Necronomicon, The book of Soyga, The grand Grimoire, n.k" vinavyoweza kukuletea shida na hata mikosi maishani mwako.
    VITABU VYENYE NGUVU DUNIANI AMBAVYO HAUTAFUNDISHWA SHULENI: SIRI KUBWA YA UTAJIRI WA ULIMWENGU! Je, umefundishwa katika dini yako kuwa Biblia na Quran ndio vitabu pekee vyenye nguvu na maajabu? Ni kweli vitabu hivi ni miongoni mwa vitabu vyenye maajabu, ila kuna baddhi ya vitabu vinavyofichwa kutokana na nguvu zake za kubadili maisha ya watu, kwa utajiri ama wakawa masikini wa kutupwa na hata kuwa wenye mikosi mikubwa. Dunia imejawa siri ambazo wachache wanazitumia kujinufaisha na kujitajirisha, huku wakiwadanganya wengine Kuwa ili ufanikiwe basi wafaa upate muda wa kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa, uwe mvumilivu, Ufanye kazi kwa bidii na mambo mengine mengi, lakini hawakuambii mambo ya siri wanayoyafanya na vitabu vya siri wanavyosoma ili kukuza utajiri wao na mvuto wao katika ulimwengu. Leo hii nimekuletea vitabu vya siri zaidi ya Biblia na Quran, vyenye nguvu sana, na vinavyotumika kubadili maisha ya Matajiri wa dunia hii, na imebakia kuwa siri kwao, wakiificha kwa nguvu zote na kuhakikisha wachache wanaifahamu, huku wengi wakitiwa hofu ya kuiogopa siri hii na kuviona vitabu hivi kama vya mashetani. 1. The Book of Abramelin the Mage – Kitabu cha kale cha uchawi kinachoeleza njia za kuwasiliana na malaika na nguvu za kichawi. Kitabu hiki kina nguvu za kukufundisha ushirikina na upeo wa juu unaopita uwezo wa kawaida wa mwanadamu. 2.The Lesser Key of Solomon (Lemegeton) – Kitabu cha uchawi kinachodaiwa kuwa na mafundisho ya mfalme Sulemani kuhusu majini na roho. Ni kitabu kinachosadikika kuandikwa na mfalme wa Israel ajulikanaye kama sulemani, kikiwa kimejaa elimu ya kiroho, na namna ya kuyatumia majini katika shughuli za kila siku bila kutumia nguvu kubwa. 3.Picatrix – Kitabu cha uchawi wa Kiarabu kinachoeleza jinsi ya kutumia nyota na sayari kwa utajiri. Masomo mengi yanayohusiana na nyota pamoja na bahati, hutolewa katika kitabu hiki cha ajabu. Kuna matamshi ya kiarabu katika kitabu hiki yenye nguvu ya kuleta maajabu usiyotarajia, ambayo sitayasema katika makala hii kwa kuwa sifundishi uchawi, nafunua siri zilizofichwa na mabeberu wachache ili waendelee kuitawala dunia hii kiuchumi na kuwa na nguvu ya ushawishi. 4.The Kybalion – Kitabu cha Hermeticism kinachofundisha sheria saba za ulimwengu zinazodaiwa kuwa na nguvu za kimetafizikia, zinazoleta mvuto kwa watu wanaokutazama, ushawishi kwa wanaokusikiliza na Nguvu ya fedha. 5. The Secret (Rhonda Byrne) – Kitabu kinachoelezea sheria ya mvutano (Law of Attraction) na jinsi ya kutumia mawazo kuvutia mafanikio na utajiri. Kitabu hiki ni cha ajabu maana kimejawa na siri zenye uwezo wa Kubadili uchumi wako. 6. Necronomicon – Ingawa ni kitabu cha kubuniwa na H.P. Lovecraft, kimekuwa na hadithi nyingi zinazodai kuwa kina maelezo ya siri za ulimwengu. Usisome kitabu hiki maana kinaweza kuleta shida maishani mwako bila kupata mwongozo kamili. 7.The Voynich Manuscript – Kitabu cha ajabu kilichoandikwa kwa lugha isiyojulikana na hakijafasiriwa hadi sasa. Kimekosa tafsiri yake kutokana na ukweli kuwa kiliandikwa katika lugha ambayo haipo hapa duniani, ama ilikuwapo ila imepotea. Vitabu hivi ndivyo vinavyowafanya watu kuwa na mvuto, na utajiri mkubwa duniani. Kwa kweli huwezi kuwa na mvuto mkubwa ama utajiri mkubwa duniani pasina kusoma vitabu hivi na kufuata kanuni zake, wenda kama utakuwa tajiri kijijini kwenu lakini si duniani. Nikiwa namalizia, kuna Vitabu vyenye nguvu ya kukutajirisha, vyenye nguvu ya kukulaani na hata kukuletea mikosi isiyokoma, ambavyo vimekuwa vikihifadhiwa kwa siri sana, ili kutumiwa na wachache kwa malengo mahususi. Wapo watu kadhaa wanaopinga nguvu ya maandishi katika vitabu wakiidharau na kuyaona maandishi kama herufi za kawaida sana, lakini ukweli ni kuwa kuna nguvu katika vitabu, kuna maajabu katika vitabu na kuna watu waliofunga maisha yao kwa kusoma vifungu fulani kimakosa katika vitabu. Hebu kuwa makini na kila kitabu unachosoma. Hakikisha kwanza kitabu usomacho ni salama, maana kuna vitabu kama vile "Necronomicon, The book of Soyga, The grand Grimoire, n.k" vinavyoweza kukuletea shida na hata mikosi maishani mwako.
    Like
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·326 Ansichten
  • Ahmed Ally, Msemaji wa klabu ya Simba SC

    Anatokea mwehu mmoja anamdhihaki huyu Rais au kikundi cha vijana wa hovyo wanadhihaki Mamlaka za mpira wetu, Hii Nchi uhuru umepitiliza sana

    Wallace Karia, TFF na Bodi ya Ligi Wanapaswa kuheshimiwa, kuenziwa, kutunzwa na kulindwa maana wamefanya kazi kubwa na wanaendelea kufanya kazi kubwa kwenye mpira wetu

    Yote tuliyokua tunayaota kwenye mpira sasa hivi yanatokea, yale tuliyodhani ni magumu kwa Karia yamewezekana

    Na kama haitoshi tunaiona kesho njema ya mpira wa Tanzania chini ya Karia na wenzake

    President @wallacekaria na Uongozi wako wa TFF na Bodi ya ligi msirudi nyuma na msikubali mtu akaturudisha nyuma sasa hivi tunawaza World Cup tunawaza Utawala wa AFCON na Ubingwa Afrika ngazi klabu

    KAMA HUMPENDI KARIA PENDA MAFANIKIO YAKE"

    Ahmed Ally, Msemaji wa klabu ya Simba SC ✍️ Anatokea mwehu mmoja anamdhihaki huyu Rais au kikundi cha vijana wa hovyo wanadhihaki Mamlaka za mpira wetu, Hii Nchi uhuru umepitiliza sana Wallace Karia, TFF na Bodi ya Ligi Wanapaswa kuheshimiwa, kuenziwa, kutunzwa na kulindwa maana wamefanya kazi kubwa na wanaendelea kufanya kazi kubwa kwenye mpira wetu Yote tuliyokua tunayaota kwenye mpira sasa hivi yanatokea, yale tuliyodhani ni magumu kwa Karia yamewezekana Na kama haitoshi tunaiona kesho njema ya mpira wa Tanzania chini ya Karia na wenzake President @wallacekaria na Uongozi wako wa TFF na Bodi ya ligi msirudi nyuma na msikubali mtu akaturudisha nyuma sasa hivi tunawaza World Cup tunawaza Utawala wa AFCON na Ubingwa Afrika ngazi klabu KAMA HUMPENDI KARIA PENDA MAFANIKIO YAKE"
    Like
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·321 Ansichten
  • "Msimu uliyopita Zamalek aligomea mechi dhidi ya Al Ahly, Mamlaka za soka nchini Misri zikampa ushindi Al Ahly wa mabao mawili na alama zake tatu kisha wakailima Zamalek alama tatu na timu ikashuka mpaka nafasi ya 12 kama sikosei, Bodi na Chama wala hakikuwaza mara mbili, ni kesi kubwa sana kwenye dunia ya soka kukacha mechi.

    Jana, Al Ahly nae kaleta mbwembwe zile zile za masuala ya Kanuni akagomea mchezo, akasahau kanuni ya kutokea Uwanjani na kucheza mechi ndio kanuni yenye maana zaidi kwenye soka, amejikuta anapoteza alama tatu na mabao matatu kwa Zamalek, Kanuni hii inaweza kusema hivi ila Kanuni nyingine ikawa na maelezo mengine.

    Nikukumbushe tu Al Ahly aliyeadhibiwa ndio Klabu Tajiri zaidi Afrika, Klabu yenye Mashabiki na Wanachama wengi zaidi Afrika, ndio Klabu ya pili kwa Mataji mengi duniani baada ya Real Madrid, ila huko Misri watu hawatazami makunyanzi, ukileta maksudi, Bodi na Chama cha soka zinakufanyia bahati mbaya, Ahly inatajwa pia ina nguvu kubwa sana CAF, sio ya kufikirika ama nadharia ndio uhalisia ila wamepita nayo mapema tu.

    Nawakumbusha tena Watu wangu HAKI huenda na WAJIBU, mfano Tanzania kwa mujibu wa Katiba kuandamana ni haki yako ila unapaswa kutoa taarifa kwa Polisi masaa 72 kabla, umeelewa hapo? Ni haki yako ila huja na Wajibu, Kanuni ili ikulinde hakikisha umetekeleza Wajibu, biashara za Mamlaka za soka duniani ni mpira, kutocheza mpira ni kuzitusi, hazikuachi salama.

    Ni haki yako kuja kufanya mazoezi uwanja wa mechi siku moja kabla ila ni Wajibu wako kunijulisha kuwa nakuja, ili nikuandalie mazingira, huenda narekebisha mfumo wa Umeme? Huenda hali ya usalama sio shwari, huenda nimepulizia dawa za dudu zinaweka kukuathiri, yaani ni HAKI yako ila una WAJIBU wako huu ni mfano tu.

    Mnasemaje Watu wangu wa nchini Yemen haya hayawahusu sana, huko kwenu Kivyenu vyenu Wayemen" - Farhan JR, Mchambuzi.

    "Msimu uliyopita Zamalek aligomea mechi dhidi ya Al Ahly, Mamlaka za soka nchini Misri zikampa ushindi Al Ahly wa mabao mawili na alama zake tatu kisha wakailima Zamalek alama tatu na timu ikashuka mpaka nafasi ya 12 kama sikosei, Bodi na Chama wala hakikuwaza mara mbili, ni kesi kubwa sana kwenye dunia ya soka kukacha mechi. Jana, Al Ahly nae kaleta mbwembwe zile zile za masuala ya Kanuni akagomea mchezo, akasahau kanuni ya kutokea Uwanjani na kucheza mechi ndio kanuni yenye maana zaidi kwenye soka, amejikuta anapoteza alama tatu na mabao matatu kwa Zamalek, Kanuni hii inaweza kusema hivi ila Kanuni nyingine ikawa na maelezo mengine. Nikukumbushe tu Al Ahly aliyeadhibiwa ndio Klabu Tajiri zaidi Afrika, Klabu yenye Mashabiki na Wanachama wengi zaidi Afrika, ndio Klabu ya pili kwa Mataji mengi duniani baada ya Real Madrid, ila huko Misri watu hawatazami makunyanzi, ukileta maksudi, Bodi na Chama cha soka zinakufanyia bahati mbaya, Ahly inatajwa pia ina nguvu kubwa sana CAF, sio ya kufikirika ama nadharia ndio uhalisia ila wamepita nayo mapema tu. Nawakumbusha tena Watu wangu HAKI huenda na WAJIBU, mfano Tanzania kwa mujibu wa Katiba kuandamana ni haki yako ila unapaswa kutoa taarifa kwa Polisi masaa 72 kabla, umeelewa hapo? Ni haki yako ila huja na Wajibu, Kanuni ili ikulinde hakikisha umetekeleza Wajibu, biashara za Mamlaka za soka duniani ni mpira, kutocheza mpira ni kuzitusi, hazikuachi salama. Ni haki yako kuja kufanya mazoezi uwanja wa mechi siku moja kabla ila ni Wajibu wako kunijulisha kuwa nakuja, ili nikuandalie mazingira, huenda narekebisha mfumo wa Umeme? Huenda hali ya usalama sio shwari, huenda nimepulizia dawa za dudu zinaweka kukuathiri, yaani ni HAKI yako ila una WAJIBU wako huu ni mfano tu. Mnasemaje Watu wangu wa nchini Yemen haya hayawahusu sana, huko kwenu Kivyenu vyenu Wayemen😀" - Farhan JR, Mchambuzi.
    Like
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·324 Ansichten
  • Sahivi movie zimeoga
    Ni za kutosha
    Niwewe tu na bundle lako
    Nyimgine hii
    Sahivi movie zimeoga Ni za kutosha Niwewe tu na bundle lako Nyimgine hii
    0 Kommentare ·0 Anteile ·184 Ansichten
  • Rais wa Marekani , Donald Trump ametoa siri kuwa Ofisi yake imepokea barua kutoka kwa Rais wa Ukraine , Volodymyr Zelensky, ikisema yuko tayari kwa mazungumzo na Russia na kusaini makubaliano ya madini adimu.

    “Ukraine iko tayari kukaa kwenye meza ya mazungumzo haraka iwezekanavyo ili kuleta amani ya kudumu. Hakuna anayetaka amani zaidi ya Waukraine,” Trump amesema katika hotuba yake bungeni usiku wa kuamkia leo huku akinukuu barua hiyo.

    “Mimi na timu yangu tuko tayari kufanya kazi chini ya uongozi thabiti wa Rais Trump ili kupata amani ya kudumu’,” Trump alinukuu maneno ya Zelenskyy.

    “Si hilo lingekuwa jambo zuri?” aliuliza. “Ni wakati wa kukomesha huu upuuzi. Ni wakati wa kusitisha mauaji. Ni wakati wa kumaliza vita hivi visivyo na maana. Ukitaka kumaliza vita, lazima uzungumze na pande zote mbili,” amesema Trump.

    Kauli hiyo ya Trump imekuja siku chache baada ya mvutano mkali kati yake na Zelenskyy katika Ofisi ya Oval iliyoko Ikulu ya White House, hali iliyosababisha Marekani kusitisha msaada muhimu wa kijeshi kwa Ukraine.

    Rais wa Marekani 🇺🇸, Donald Trump ametoa siri kuwa Ofisi yake imepokea barua kutoka kwa Rais wa Ukraine 🇺🇦, Volodymyr Zelensky, ikisema yuko tayari kwa mazungumzo na Russia 🇷🇺 na kusaini makubaliano ya madini adimu. “Ukraine iko tayari kukaa kwenye meza ya mazungumzo haraka iwezekanavyo ili kuleta amani ya kudumu. Hakuna anayetaka amani zaidi ya Waukraine,” Trump amesema katika hotuba yake bungeni usiku wa kuamkia leo huku akinukuu barua hiyo. “Mimi na timu yangu tuko tayari kufanya kazi chini ya uongozi thabiti wa Rais Trump ili kupata amani ya kudumu’,” Trump alinukuu maneno ya Zelenskyy. “Si hilo lingekuwa jambo zuri?” aliuliza. “Ni wakati wa kukomesha huu upuuzi. Ni wakati wa kusitisha mauaji. Ni wakati wa kumaliza vita hivi visivyo na maana. Ukitaka kumaliza vita, lazima uzungumze na pande zote mbili,” amesema Trump. Kauli hiyo ya Trump imekuja siku chache baada ya mvutano mkali kati yake na Zelenskyy katika Ofisi ya Oval iliyoko Ikulu ya White House, hali iliyosababisha Marekani kusitisha msaada muhimu wa kijeshi kwa Ukraine.
    Like
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·356 Ansichten
  • Ijumaa, tarehe 28 Februari, haikuwa siku rahisi kwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alipofanya ziara katika Ikulu ya White House, Marekani. Kabla hata ya mzozo wa maneno kati yake na mwenyeji wake, Rais Donald Trump, pamoja na Makamu wa Rais JD Vance, tayari kulikuwa na ishara za mivutano.

    Trump alimkaribisha Zelensky mlangoni na kusema kwa utani: “Leo amevalia kweli kweli,” kauli ambayo iliwafanya baadhi ya waandishi wa habari kuiona kama kejeli badala ya pongezi. Wakati huo, Zelensky alikuwa amevalia fulana nyeusi ya mikono mirefu, vazi ambalo amekuwa akilivaa mara kwa mara tangu Ukraine ivamiwe na Urusi mwaka 2022.

    Baadaye, Trump alipompokea Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, alionekana kutazama mavazi yake kwa makini kutoka juu hadi chini, kisha kunong’ona maneno yanayoweza kutafsiriwa kama pongezi kwa suti rasmi aliyovaa Starmer.

    Mjadala kuhusu mavazi ya Zelensky ulizidi kupamba moto wakati wa mkutano wa waandishi wa habari. Brian Glenn, mwandishi kutoka Real America’s Voice—chombo cha habari kinachopendelea mrengo wa kulia—alimtupia swali la moja kwa moja:

    “Kwa nini hauvai suti? Upo katika ofisi ya juu kabisa katika nchi hii, na umegoma kuvaa suti – je, unamiliki hata suti?”

    Kwa utulivu, Zelensky alijibu kwa mshangao mdogo:

    “Nitavaa suti vita hivi vitakapomalizika. Labda suti kama yako, labda bora zaidi, au pengine ya bei nafuu kuliko yako,” alisema kwa utani huku akionyesha msimamo wake wa kuendelea kuvaa mavazi ya kijeshi.

    Swali hilo la Glenn liliibua mjadala mkali mitandaoni. Wengine walimuunga mkono, wakisema kwamba kiongozi wa taifa anapaswa kuvaa mavazi rasmi anapokutana na viongozi wengine, ilhali wengine waliona swali hilo kuwa la dhihaka na lisilo na umuhimu.

    Miongoni mwa waliomkosoa Glenn ni mwandishi maarufu wa Uingereza, Piers Morgan, ambaye pia ni rafiki wa karibu wa Trump. Morgan aliandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter):

    “Swali la kipuuzi. Elon Musk havai suti anapoingia Ikulu.”

    Historia pia inaonyesha kuwa si Zelensky pekee aliyeingia Ikulu ya Marekani bila suti. Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Winston Churchill, alifanya hivyo katika moja ya ziara zake rasmi.
    Ijumaa, tarehe 28 Februari, haikuwa siku rahisi kwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alipofanya ziara katika Ikulu ya White House, Marekani. Kabla hata ya mzozo wa maneno kati yake na mwenyeji wake, Rais Donald Trump, pamoja na Makamu wa Rais JD Vance, tayari kulikuwa na ishara za mivutano. Trump alimkaribisha Zelensky mlangoni na kusema kwa utani: “Leo amevalia kweli kweli,” kauli ambayo iliwafanya baadhi ya waandishi wa habari kuiona kama kejeli badala ya pongezi. Wakati huo, Zelensky alikuwa amevalia fulana nyeusi ya mikono mirefu, vazi ambalo amekuwa akilivaa mara kwa mara tangu Ukraine ivamiwe na Urusi mwaka 2022. Baadaye, Trump alipompokea Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, alionekana kutazama mavazi yake kwa makini kutoka juu hadi chini, kisha kunong’ona maneno yanayoweza kutafsiriwa kama pongezi kwa suti rasmi aliyovaa Starmer. Mjadala kuhusu mavazi ya Zelensky ulizidi kupamba moto wakati wa mkutano wa waandishi wa habari. Brian Glenn, mwandishi kutoka Real America’s Voice—chombo cha habari kinachopendelea mrengo wa kulia—alimtupia swali la moja kwa moja: “Kwa nini hauvai suti? Upo katika ofisi ya juu kabisa katika nchi hii, na umegoma kuvaa suti – je, unamiliki hata suti?” Kwa utulivu, Zelensky alijibu kwa mshangao mdogo: “Nitavaa suti vita hivi vitakapomalizika. Labda suti kama yako, labda bora zaidi, au pengine ya bei nafuu kuliko yako,” alisema kwa utani huku akionyesha msimamo wake wa kuendelea kuvaa mavazi ya kijeshi. Swali hilo la Glenn liliibua mjadala mkali mitandaoni. Wengine walimuunga mkono, wakisema kwamba kiongozi wa taifa anapaswa kuvaa mavazi rasmi anapokutana na viongozi wengine, ilhali wengine waliona swali hilo kuwa la dhihaka na lisilo na umuhimu. Miongoni mwa waliomkosoa Glenn ni mwandishi maarufu wa Uingereza, Piers Morgan, ambaye pia ni rafiki wa karibu wa Trump. Morgan aliandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter): “Swali la kipuuzi. Elon Musk havai suti anapoingia Ikulu.” Historia pia inaonyesha kuwa si Zelensky pekee aliyeingia Ikulu ya Marekani bila suti. Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Winston Churchill, alifanya hivyo katika moja ya ziara zake rasmi.
    Like
    Love
    2
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·604 Ansichten
  • Hii kama sijaielewa hivi.
    Hii kama sijaielewa hivi.
    Like
    Love
    5
    · 1 Kommentare ·0 Anteile ·300 Ansichten
  • 7. Tel Hazor
    Katika eneo la ekari 200 hivi, eneo hili lililo katika Galilaya ya Juu (sasa ni mbuga ya kitaifa) ndilo kubwa zaidi kati ya “tels” za Israeli,

    Kulingana na Agano la Kale, Hazori ilikuwa mahali pa ushindi muhimu wa Yoshua katika ushindi wake wa Kanaani baada ya kifo cha Musa; eti aliteketeza jiji hilo kabisa, akisafisha njia kwa ajili ya makazi ya Waisraeli.
    7. Tel Hazor Katika eneo la ekari 200 hivi, eneo hili lililo katika Galilaya ya Juu (sasa ni mbuga ya kitaifa) ndilo kubwa zaidi kati ya “tels” za Israeli, Kulingana na Agano la Kale, Hazori ilikuwa mahali pa ushindi muhimu wa Yoshua katika ushindi wake wa Kanaani baada ya kifo cha Musa; eti aliteketeza jiji hilo kabisa, akisafisha njia kwa ajili ya makazi ya Waisraeli.
    0 Kommentare ·0 Anteile ·360 Ansichten
  • Katika hatua mpya ya mzozo unaoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , kundi la Waasi wa M23 likishirikiana na Muungano wa Mto Congo (AFC) limetangaza kuwa Wanajeshi wa zamani wa Jeshi la DR Congo (FARDC) waliokamatwa au kujisalimisha wamehitimu mafunzo ya kiitikadi na mbinu za kijeshi.

    Katika taarifa ya Kundi la M23 kwenye mtandao wao wa X leo Februari 18, picha zilionyesha Wanajeshi hao wakiwa na sare na silaha rasmi za wanamgambo hao. Ujumbe uliambatana na chapisho hilo ulieleza:

    "Wanajeshi wa zamani wa FARDC, waliokamatwa au kujisalimisha, wamemaliza mafunzo ya kiitikadi na mbinu huko Rumangabo Mjini Goma chini ya AFC/M23. Sasa wakiwa na vifaa kamili na wanaolipwa, wametumwa Lubero, ambako wanashiriki kikamilifu muungano wa serikali."

    Wakati huo huo, Uganda imetangaza kuwa vikosi vyake vya kijeshi vimeanza kuelekea Bunia, DRC, ikiwa ni siku chache baada ya Jeshi la Uganda kutoa muda wa saa 24 kwa Askari waliopo eneo hilo kujisalimisha.

    Taarifa nyingine kuwa, hapo jana Kundi la Waasi hao wa M23 wamefanikiwa kuteka eneo la Kamanyola na sasa hivi wanajipanga kuelekea Uvira, Fizi kisha Mkoa wa Tanganyika (Kalemie) kabla ya kwenda Mjini Lubumbashi. Kwa mujibu wa Wananchi wa Kamanyala wanasema kuwa Kundi la Wapiganaji wa Wazalendo ambao wanapigana kwa upande wa Serikali waliibwa Silaha zao kisha wakakimbia na kuwaachia M23 kuichukua Kamanyola.

    Katika hatua mpya ya mzozo unaoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩, kundi la Waasi wa M23 likishirikiana na Muungano wa Mto Congo (AFC) limetangaza kuwa Wanajeshi wa zamani wa Jeshi la DR Congo (FARDC) waliokamatwa au kujisalimisha wamehitimu mafunzo ya kiitikadi na mbinu za kijeshi. Katika taarifa ya Kundi la M23 kwenye mtandao wao wa X leo Februari 18, picha zilionyesha Wanajeshi hao wakiwa na sare na silaha rasmi za wanamgambo hao. Ujumbe uliambatana na chapisho hilo ulieleza: "Wanajeshi wa zamani wa FARDC, waliokamatwa au kujisalimisha, wamemaliza mafunzo ya kiitikadi na mbinu huko Rumangabo Mjini Goma chini ya AFC/M23. Sasa wakiwa na vifaa kamili na wanaolipwa, wametumwa Lubero, ambako wanashiriki kikamilifu muungano wa serikali." Wakati huo huo, Uganda imetangaza kuwa vikosi vyake vya kijeshi vimeanza kuelekea Bunia, DRC, ikiwa ni siku chache baada ya Jeshi la Uganda kutoa muda wa saa 24 kwa Askari waliopo eneo hilo kujisalimisha. Taarifa nyingine kuwa, hapo jana Kundi la Waasi hao wa M23 wamefanikiwa kuteka eneo la Kamanyola na sasa hivi wanajipanga kuelekea Uvira, Fizi kisha Mkoa wa Tanganyika (Kalemie) kabla ya kwenda Mjini Lubumbashi. Kwa mujibu wa Wananchi wa Kamanyala wanasema kuwa Kundi la Wapiganaji wa Wazalendo ambao wanapigana kwa upande wa Serikali waliibwa Silaha zao kisha wakakimbia na kuwaachia M23 kuichukua Kamanyola.
    0 Kommentare ·0 Anteile ·522 Ansichten
  • "Wakati tunazilaumu Simba Sports na Azam Football Club Kuukosa Ubingwa,tukumbuke pia Mazingira Yao Magumu ya Kushindana

    Parameters za Simba Sports na Azam Fc Kuchukua Ubingwa zimebadilika Kabisa na ni tofauti Washindani wenzao Kwenye Ligi

    Kuna hoja Lazy sana eti Mbona Simba Sports alicheza na Tabora United Dhaifu?

    Kwenye Mechi zote 2 Tabora wana uwezo wa Ku justifie Kwanini walichezesha Vikosi vile na ukawaelewa vizuri tu.

    Mechi ya Kwanza n issue ya Vibali,na mechi ya Pili Heritier Makambo alikuwa na Kadi 3 za njano. Yacouba Sogne alikuwa ni Majeruhi..

    Kuna hoja Lazy nyingine Kwamba mbona Kikosi bora cha Singida Black Stars Kilifungwa 2-0 na KMC ambayo ilifungwa 6-1 na Yanga?

    Kwanza Kwenye hiyo hoja hapo wote tumekubaliana Kwamba Singida Black Stars wamepanga Kikosi Dhaifu

    Pili, Sisi hatusemi Singida Black Stars angepanga Kikosi bora lazima angeshinda dhidi ya Yanga au asingepoteza mechi

    Mbona ile Mechi ya Kwanza Kule Amani Complex Zanzibar Singida Black Stars waliweka Full Mkoko na bado Yanga alishinda 1-0 bao la Paccome ?

    Swali ni Sababu ipi ya Singida Black Stars Kubadilisha wachezaji 6 Kutoka Kwenye Kikosi Kilichomfunga Jkt Tanzania 1-0?

    Mbaya zaidi Kuna wachezaji walichezeshwa Kabisa nje ya Maeneo ya ya asili na wachezaji wenye nafasi zao wakiwa bench

    Singida black stars Dhaifu ilipigwa 2-0 Kipindi Cha Kwanza na Stars bora ilishinda 1-0 Kipindi cha Pili.

    Ligi yetu tukufu inachezewa na watu ambao hawana nia njema na Mpira wetu na Kama tusipotwanga sasa hivi tutakuja Kuula Mbichi" - Wilson Orumo, Mchambuzi.

    "Wakati tunazilaumu Simba Sports na Azam Football Club Kuukosa Ubingwa,tukumbuke pia Mazingira Yao Magumu ya Kushindana Parameters za Simba Sports na Azam Fc Kuchukua Ubingwa zimebadilika Kabisa na ni tofauti Washindani wenzao Kwenye Ligi Kuna hoja Lazy sana eti Mbona Simba Sports alicheza na Tabora United Dhaifu? Kwenye Mechi zote 2 Tabora wana uwezo wa Ku justifie Kwanini walichezesha Vikosi vile na ukawaelewa vizuri tu. Mechi ya Kwanza n issue ya Vibali,na mechi ya Pili Heritier Makambo alikuwa na Kadi 3 za njano. Yacouba Sogne alikuwa ni Majeruhi.. Kuna hoja Lazy nyingine Kwamba mbona Kikosi bora cha Singida Black Stars Kilifungwa 2-0 na KMC ambayo ilifungwa 6-1 na Yanga? Kwanza Kwenye hiyo hoja hapo wote tumekubaliana Kwamba Singida Black Stars wamepanga Kikosi Dhaifu Pili, Sisi hatusemi Singida Black Stars angepanga Kikosi bora lazima angeshinda dhidi ya Yanga au asingepoteza mechi Mbona ile Mechi ya Kwanza Kule Amani Complex Zanzibar Singida Black Stars waliweka Full Mkoko na bado Yanga alishinda 1-0 bao la Paccome ? Swali ni Sababu ipi ya Singida Black Stars Kubadilisha wachezaji 6 Kutoka Kwenye Kikosi Kilichomfunga Jkt Tanzania 1-0? Mbaya zaidi Kuna wachezaji walichezeshwa Kabisa nje ya Maeneo ya ya asili na wachezaji wenye nafasi zao wakiwa bench Singida black stars Dhaifu ilipigwa 2-0 Kipindi Cha Kwanza na Stars bora ilishinda 1-0 Kipindi cha Pili. Ligi yetu tukufu inachezewa na watu ambao hawana nia njema na Mpira wetu na Kama tusipotwanga sasa hivi tutakuja Kuula Mbichi" - Wilson Orumo, Mchambuzi.
    0 Kommentare ·0 Anteile ·666 Ansichten
  • Mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu kutoka Nchini Liberia , George Weah, amekana kufanya mazungumzo yoyote na Mmiliki wa mtandao wa X Elon Musk kuhusiana na kununua tuzo yake ya Ballon D’or aliyoshinda mwaka 1995 kwa thamani ya Dola bilioni moja (1).

    Mchezaji huyo amesema kuwa Musk hakuwahi kutaka kununua tuzo hiyo kutoka kwake, kama ilivyoripotiwa mitandaoni hivi karibuni. Pamoja na hayo, Weah ameongeza kuwa Tuzo hiyo haiuzwi hata Watoto wake alishawaambia kuwa Tuzo hiyo ni mali ya Afrika, hata ikitokea wakapatwa na shida, haitakiwi kuuzwa kwa sababu ndio Tuzo pekee bara la Afrika inajivunia.

    Mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu kutoka Nchini Liberia 🇱🇷, George Weah, amekana kufanya mazungumzo yoyote na Mmiliki wa mtandao wa X Elon Musk kuhusiana na kununua tuzo yake ya Ballon D’or aliyoshinda mwaka 1995 kwa thamani ya Dola bilioni moja (1). Mchezaji huyo amesema kuwa Musk hakuwahi kutaka kununua tuzo hiyo kutoka kwake, kama ilivyoripotiwa mitandaoni hivi karibuni. Pamoja na hayo, Weah ameongeza kuwa Tuzo hiyo haiuzwi hata Watoto wake alishawaambia kuwa Tuzo hiyo ni mali ya Afrika, hata ikitokea wakapatwa na shida, haitakiwi kuuzwa kwa sababu ndio Tuzo pekee bara la Afrika inajivunia.
    Love
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·311 Ansichten
  • Kaka yake, Josh Jones, alisikia sauti za John akilia kwa uchungu.

    Alipojaribu kumvuta, aligundua kuwa amekwama vibaya sana.

    John alikuwa amepinda vibaya, kifua chake kimesukumwa dhidi ya mwamba, na hawezi kupumua vizuri.

    Kila sekunde iliyopita, damu yake ilianza kushindwa kuzunguka mwilini.

    Josh alipiga mayowe ya msaada, na hivi karibuni, vikosi vya uokoaji vilifika.

    Lakini walichokiona kilikuwa cha kutisha zaidi ya walivyodhani.
    Kaka yake, Josh Jones, alisikia sauti za John akilia kwa uchungu. Alipojaribu kumvuta, aligundua kuwa amekwama vibaya sana. John alikuwa amepinda vibaya, kifua chake kimesukumwa dhidi ya mwamba, na hawezi kupumua vizuri. Kila sekunde iliyopita, damu yake ilianza kushindwa kuzunguka mwilini. Josh alipiga mayowe ya msaada, na hivi karibuni, vikosi vya uokoaji vilifika. Lakini walichokiona kilikuwa cha kutisha zaidi ya walivyodhani.
    Love
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·272 Ansichten
  • Rais wa Senegal , Bassirou Diomaye Faye ametangaza mpango wa kubadilisha majina ya mitaa yenye majina ya enzi za ukoloni na kuyapa majina ya mashujaa wa kitaifa na matukio muhimu ya kihistoria ya Nchi ya Senegal. Mpango huo ulioanzishwa wakati wa mkutano wa hivi karibuni wa Baraza la Mawaziri ni sehemu ya juhudi za kurejesha utambulisho wa kitamaduni wa Nchi hiyo.

    Mpango huyo utahusu pia kubadilisha majina na kuandika upya historia ya Nchi ya Senegal katika kwa umma, alisema Rais huyo ambapo pia aliongeza kwa kusema “Lazima tuelimishe Vijana wetu kuhusu Watu na matukio yaliyounda na kuijenga Senegal"

    Rais wa Senegal 🇸🇳, Bassirou Diomaye Faye ametangaza mpango wa kubadilisha majina ya mitaa yenye majina ya enzi za ukoloni na kuyapa majina ya mashujaa wa kitaifa na matukio muhimu ya kihistoria ya Nchi ya Senegal. Mpango huo ulioanzishwa wakati wa mkutano wa hivi karibuni wa Baraza la Mawaziri ni sehemu ya juhudi za kurejesha utambulisho wa kitamaduni wa Nchi hiyo. Mpango huyo utahusu pia kubadilisha majina na kuandika upya historia ya Nchi ya Senegal katika kwa umma, alisema Rais huyo ambapo pia aliongeza kwa kusema “Lazima tuelimishe Vijana wetu kuhusu Watu na matukio yaliyounda na kuijenga Senegal"
    0 Kommentare ·0 Anteile ·440 Ansichten
  • Wapiganaji wa kundi la Waasi wa M23 na Askari wanaodhaniwa kuwa ni Rwanda wameendelea kusonga mbele katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo . Hayo ni kwa mujibu wa vyanzo vya eneo hilo pamoja na vya mashirika ya kibinadamu. Miji iliyotekwa ni Ihusi na Kalehe, iliyoko karibu kiliomita sitini (60) kutoka Mji wa Bukavu.

    Katika taarifa, Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeitisha mkutano wa dharura wa mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutathmini hali hiyo na "kutathmini hali na matokeo ya kitendo hiki kipya cha uchokozi", ikitoa wito wa vikwazo.

    Rais wa Burundi , Evariste Ndayishimiye amesema yeyote atakayeishambulia Nchi yake naye atashambuliwa. Wakati huo huo, Viongozi wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Nchini DR Congo na ule wa Kanisa la Kristo la DR Congo umekutana na kundi la Waasi wa M23 Mjini Goma katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kusaka amani na mazungumzo. Walikutana na kiongozi wa kisiasa wa kundi la M23 Corneille Nangaa.
    (DW Swahili)

    Wapiganaji wa kundi la Waasi wa M23 na Askari wanaodhaniwa kuwa ni Rwanda 🇷🇼 wameendelea kusonga mbele katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Hayo ni kwa mujibu wa vyanzo vya eneo hilo pamoja na vya mashirika ya kibinadamu. Miji iliyotekwa ni Ihusi na Kalehe, iliyoko karibu kiliomita sitini (60) kutoka Mji wa Bukavu. Katika taarifa, Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeitisha mkutano wa dharura wa mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutathmini hali hiyo na "kutathmini hali na matokeo ya kitendo hiki kipya cha uchokozi", ikitoa wito wa vikwazo. Rais wa Burundi 🇧🇮, Evariste Ndayishimiye amesema yeyote atakayeishambulia Nchi yake naye atashambuliwa. Wakati huo huo, Viongozi wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Nchini DR Congo na ule wa Kanisa la Kristo la DR Congo umekutana na kundi la Waasi wa M23 Mjini Goma katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kusaka amani na mazungumzo. Walikutana na kiongozi wa kisiasa wa kundi la M23 Corneille Nangaa. (DW Swahili)
    Love
    1
    · 0 Kommentare ·0 Anteile ·481 Ansichten
Suchergebnis