• اقرأ أكثر
    7. Tel Hazor Katika eneo la ekari 200 hivi, eneo hili lililo katika Galilaya ya Juu (sasa ni mbuga ya kitaifa) ndilo kubwa zaidi kati ya “tels” za Israeli, Kulingana na Agano la Kale, Hazori ilikuwa mahali pa ushindi muhimu wa Yoshua katika ushindi wake wa Kanaani baada ya kifo cha Musa; eti aliteketeza jiji hilo kabisa, akisafisha njia kwa ajili ya makazi ya Waisraeli.
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·190 مشاهدة
  • اقرأ أكثر
    Katika hatua mpya ya mzozo unaoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩, kundi la Waasi wa M23 likishirikiana na Muungano wa Mto Congo (AFC) limetangaza kuwa Wanajeshi wa zamani wa Jeshi la DR Congo (FARDC) waliokamatwa au kujisalimisha wamehitimu mafunzo ya kiitikadi na mbinu za kijeshi. Katika taarifa ya Kundi la M23 kwenye mtandao wao wa X leo Februari 18, picha zilionyesha Wanajeshi hao wakiwa na sare na silaha rasmi za wanamgambo hao. Ujumbe uliambatana na chapisho hilo ulieleza: "Wanajeshi wa zamani wa FARDC, waliokamatwa au kujisalimisha, wamemaliza mafunzo ya kiitikadi na mbinu huko Rumangabo Mjini Goma chini ya AFC/M23. Sasa wakiwa na vifaa kamili na wanaolipwa, wametumwa Lubero, ambako wanashiriki kikamilifu muungano wa serikali." Wakati huo huo, Uganda imetangaza kuwa vikosi vyake vya kijeshi vimeanza kuelekea Bunia, DRC, ikiwa ni siku chache baada ya Jeshi la Uganda kutoa muda wa saa 24 kwa Askari waliopo eneo hilo kujisalimisha. Taarifa nyingine kuwa, hapo jana Kundi la Waasi hao wa M23 wamefanikiwa kuteka eneo la Kamanyola na sasa hivi wanajipanga kuelekea Uvira, Fizi kisha Mkoa wa Tanganyika (Kalemie) kabla ya kwenda Mjini Lubumbashi. Kwa mujibu wa Wananchi wa Kamanyala wanasema kuwa Kundi la Wapiganaji wa Wazalendo ambao wanapigana kwa upande wa Serikali waliibwa Silaha zao kisha wakakimbia na kuwaachia M23 kuichukua Kamanyola.
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·236 مشاهدة
  • اقرأ أكثر
    "Wakati tunazilaumu Simba Sports na Azam Football Club Kuukosa Ubingwa,tukumbuke pia Mazingira Yao Magumu ya Kushindana Parameters za Simba Sports na Azam Fc Kuchukua Ubingwa zimebadilika Kabisa na ni tofauti Washindani wenzao Kwenye Ligi Kuna hoja Lazy sana eti Mbona Simba Sports alicheza na Tabora United Dhaifu? Kwenye Mechi zote 2 Tabora wana uwezo wa Ku justifie Kwanini walichezesha Vikosi vile na ukawaelewa vizuri tu. Mechi ya Kwanza n issue ya Vibali,na mechi ya Pili Heritier Makambo alikuwa na Kadi 3 za njano. Yacouba Sogne alikuwa ni Majeruhi.. Kuna hoja Lazy nyingine Kwamba mbona Kikosi bora cha Singida Black Stars Kilifungwa 2-0 na KMC ambayo ilifungwa 6-1 na Yanga? Kwanza Kwenye hiyo hoja hapo wote tumekubaliana Kwamba Singida Black Stars wamepanga Kikosi Dhaifu Pili, Sisi hatusemi Singida Black Stars angepanga Kikosi bora lazima angeshinda dhidi ya Yanga au asingepoteza mechi Mbona ile Mechi ya Kwanza Kule Amani Complex Zanzibar Singida Black Stars waliweka Full Mkoko na bado Yanga alishinda 1-0 bao la Paccome ? Swali ni Sababu ipi ya Singida Black Stars Kubadilisha wachezaji 6 Kutoka Kwenye Kikosi Kilichomfunga Jkt Tanzania 1-0? Mbaya zaidi Kuna wachezaji walichezeshwa Kabisa nje ya Maeneo ya ya asili na wachezaji wenye nafasi zao wakiwa bench Singida black stars Dhaifu ilipigwa 2-0 Kipindi Cha Kwanza na Stars bora ilishinda 1-0 Kipindi cha Pili. Ligi yetu tukufu inachezewa na watu ambao hawana nia njema na Mpira wetu na Kama tusipotwanga sasa hivi tutakuja Kuula Mbichi" - Wilson Orumo, Mchambuzi.
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·213 مشاهدة
  • اقرأ أكثر
    Mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu kutoka Nchini Liberia 🇱🇷, George Weah, amekana kufanya mazungumzo yoyote na Mmiliki wa mtandao wa X Elon Musk kuhusiana na kununua tuzo yake ya Ballon D’or aliyoshinda mwaka 1995 kwa thamani ya Dola bilioni moja (1). Mchezaji huyo amesema kuwa Musk hakuwahi kutaka kununua tuzo hiyo kutoka kwake, kama ilivyoripotiwa mitandaoni hivi karibuni. Pamoja na hayo, Weah ameongeza kuwa Tuzo hiyo haiuzwi hata Watoto wake alishawaambia kuwa Tuzo hiyo ni mali ya Afrika, hata ikitokea wakapatwa na shida, haitakiwi kuuzwa kwa sababu ndio Tuzo pekee bara la Afrika inajivunia.
    Love
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·205 مشاهدة
  • اقرأ أكثر
    Kaka yake, Josh Jones, alisikia sauti za John akilia kwa uchungu. Alipojaribu kumvuta, aligundua kuwa amekwama vibaya sana. John alikuwa amepinda vibaya, kifua chake kimesukumwa dhidi ya mwamba, na hawezi kupumua vizuri. Kila sekunde iliyopita, damu yake ilianza kushindwa kuzunguka mwilini. Josh alipiga mayowe ya msaada, na hivi karibuni, vikosi vya uokoaji vilifika. Lakini walichokiona kilikuwa cha kutisha zaidi ya walivyodhani.
    Love
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·133 مشاهدة
  • اقرأ أكثر
    Rais wa Senegal 🇸🇳, Bassirou Diomaye Faye ametangaza mpango wa kubadilisha majina ya mitaa yenye majina ya enzi za ukoloni na kuyapa majina ya mashujaa wa kitaifa na matukio muhimu ya kihistoria ya Nchi ya Senegal. Mpango huo ulioanzishwa wakati wa mkutano wa hivi karibuni wa Baraza la Mawaziri ni sehemu ya juhudi za kurejesha utambulisho wa kitamaduni wa Nchi hiyo. Mpango huyo utahusu pia kubadilisha majina na kuandika upya historia ya Nchi ya Senegal katika kwa umma, alisema Rais huyo ambapo pia aliongeza kwa kusema “Lazima tuelimishe Vijana wetu kuhusu Watu na matukio yaliyounda na kuijenga Senegal"
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·216 مشاهدة
  • اقرأ أكثر
    Wapiganaji wa kundi la Waasi wa M23 na Askari wanaodhaniwa kuwa ni Rwanda 🇷🇼 wameendelea kusonga mbele katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Hayo ni kwa mujibu wa vyanzo vya eneo hilo pamoja na vya mashirika ya kibinadamu. Miji iliyotekwa ni Ihusi na Kalehe, iliyoko karibu kiliomita sitini (60) kutoka Mji wa Bukavu. Katika taarifa, Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeitisha mkutano wa dharura wa mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutathmini hali hiyo na "kutathmini hali na matokeo ya kitendo hiki kipya cha uchokozi", ikitoa wito wa vikwazo. Rais wa Burundi 🇧🇮, Evariste Ndayishimiye amesema yeyote atakayeishambulia Nchi yake naye atashambuliwa. Wakati huo huo, Viongozi wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Nchini DR Congo na ule wa Kanisa la Kristo la DR Congo umekutana na kundi la Waasi wa M23 Mjini Goma katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kusaka amani na mazungumzo. Walikutana na kiongozi wa kisiasa wa kundi la M23 Corneille Nangaa. (DW Swahili)
    Love
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·227 مشاهدة
  • اقرأ أكثر
    TBT ya Haji Manara "September 2007 nikiwa kijana Mdogo na nikiwa kiongozi wa Chama changu na hapo ni fresh from School kule Beijing China. Kipindi hicho nna madini ya hatari kuhusu taaluma ya Propaganda na Uenezi,enzi ambazo nilikuwa naweza kukuaminisha Jiwe ni Keki 😀😀😀 Enzi ambazo nilikuwa naweza kuwavusha hata kuku barabarani kwa maneno tu😀😀😀, Ni zile zile zama nilizowaaminisha Barcelona haichomoki kwa Mkapa, tena Barcelona kweli ya Xavi ,Iniesta na kina Messi. Taaluma iliyonipa ujasiri wa kusema na kuamini tutafuzu kwa AFCON ya 2019 kule Misri,wakati huo tukiwa chini kwenye msimamo wa kundi letu, na Nchi nzima ikiwa imejikatia tamaa ya kwenda Cairo. Bila kusahau one day kule Paris France niliposahau Passport hotelini na siku hiyo tulisimamishwa na Manjagu njiani nikiwa na wenzangu ambao walikuwa Kamil Gado, Nikazuga kama naitoa kwenye mfuko wa koti, Askari wakaniamini kabla ya kuwaonyesha ,wakaturuhusu kilaini kabisa,inaitwa Blue Propaganda 😀😀😀 Yes: Pembeni yangu katika hiyo picha ni Marehemu Captain Barongo aliyekuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Na hii ilikuwa sherehe ya harusi ya DC wa Temeke hivi sasa Mh Sixtus Mapunda ambae wakati huo alikuwa Katibu wa Umoja wa Vijana ( UV CCM ) Mkoa huu. Hadi leo tumebaki marafiki wakubwa na hakosi mwaliko wowote kwangu 🙏🙏 Nb: Usicheke ukubwa wa koti,miaka ile ilikuwa ndio fashion na wenyewe tuliyaita Majumba 😀😀😀"
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·259 مشاهدة
  • اقرأ أكثر
    Habari iliyobamba kwa sasa kwenye vyombo vya habari ni ndoa ya Stephane Aziz Ki na Hamisa Mobetto, ingawa wapo waliofika mbali na kudai ni kiki tu kwa ajili ya matangazo ya bidhaa fulani na wanatumika tu. Baada ya vuta nkuvute ya stori hii hatimaye mama yake Hamisa, Shufaa Rutanga amefunga na anathibitisha kuwepo kwa ndoa hiyo na kuhusu posa ya Aziz Ki, amesema hakuna posa yoyote iliyofika kwake kutoka kwa nyota huyo wa kimataifa wa Burkina Faso ingawa amepokea nyingi kutoka kwa wanaume tofauti wanaotaka kumuoa mwanaye. “Sasa ngoja nikuambie ukweli, maana nilikuwa nashindwa kutoa majibu sahihi kutokana na baadhi ya ya vitu kuhusu ndoa hii vilikuwa havijakamilika, sasa vimekamilika na ndoa ipo. Kiukweli namshukuru Mungu maombi yangu kwa mwanagu yameitika, nilikuwa kila kukicha naomba apate mtu sahihi watakayependana ili aolewe, kuwa kwenye ndoa ni heshima kubwa sana" - Mama Mobetto Mama Hamisa anasema hekaheka za ndoa hiyo zitaanza Jumamosi Februari 15 na ndiyo siku mahari itatolewa na sherehe itafanyika Februari 19, The Superdome, Masaki, jijini Dar es Salaam. “Kutoka moyoni nimewapa baraka zote mkwe wangu AziZ Ki na mwanagu Hamisa na upendo mwingi sana kwake Aziz Ki kwa kupenda watoto wa Hamisa. Hiki ndiyo sababu kuu iliyonifanya nimpende zaidi Aziz Ki, maana kwa hali ya sasa hivi upate mwanamume atakayekubali kuoa mwanamke mwenye watoto ni wachache sana ila Aziz Ki ameonyesha upendo wa dhati kwa mwanangu Hamisa, kapenda boga na maua yake.” - Mama Mobetto Wakati huohuo mmoja wa viongozi wa Yanga, amethibitisha ni kweli wawili hao watafunga ndoa Ijumaa na kwasasa Aziz yupo kwenye maandalizi ya Ndoa ingawa atakuwepo kwenye mchezo wa Ijumaa. (Mwananchi)
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·329 مشاهدة
  • Hellow cm yangu ilizingua kidg but now am back online
    Nilitaka kuuliza
    Hivi nyie dunia mnaielewa kweli inakoelekea au wameqnza kuharibu bora wangemaliza
    Hellow cm yangu ilizingua kidg but now am back online Nilitaka kuuliza Hivi nyie dunia mnaielewa kweli inakoelekea au wameqnza kuharibu bora wangemaliza
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·123 مشاهدة
  • اقرأ أكثر
    SHEREHEKEENI PAMOJA SIKU YENU Picha inaiieleza kwamba ni ya mwaka 1948, waasisi wa klabu ya Yanga wakiwa na wenzao wa Africa Sports ya Zanzibar. Picha hii inatufundisha kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar haukuwa mwaka 1964 bali zamani sana...mwaka 1964 ulikuwa mkataba tu. Na hata kutengana kuliletwa na wakoloni, wakaweka mipaka na kuigawana ardhi...mjerumani akachukua Bara na mwingereza akachukua Zanzibar. Lakini kabla ya mipaka yao, hii nchi ilikuwa moja tu, na hata mji wa Dar es Salaam ulianzishwa na Sultan Majid wa Zanzibar. Yaani aliamua tu kutoka sehemu moja ya nchi yake na kwenda kuanzisha mji sehemu nyingine ya nchi yake. Lakini hilo lengo la andiko hili... Lengo la kuandika hapa ni kutaka kuwakumbusha watu kwamba waliopo kwenye picha ni waasisi wa Yanga, na pia hawa ndiyo waasisi wa Simba. Na hii ni kwa sababu walioanzisha Simba ni wale wale walioanzisha Yanga, lakini wakajitenga na wenzao. Ni hivi Kulikuwa na timu iliyoitwa New Young, ambayo ilianzishwa mwaka 1935 na kuanza kushiriki ligi mwaka huo huo. Wakati huo ligi ilikuwa moja tu, ya Dar es Salaam...na Dar es Salaam yenyewe ilikuwa wilaya ya jimbo la Mashariki. Hakukuwa na ligi nyingine yoyote nchini, japo miaka michache baadaye wilaya zingine nazo zikaanzisha ligi...ikianza wilaya ya Iringa. Stori yake itakuja siku nyingine. Ligi ya Dar es Salaam ambayo ilianza 1929 ikiwa na daraja moja tu, la kwanza...ilikua na kuongeza daraja la pili kwenye miaka ya 1930. Kwa hiyo New Young ilipojiunga na ligi mwaka 1935, ikaanzia daraja la pili. Ikashinda ubingwa na kupanda daraja la kwanza, mwaka 1936. Hata hivyo ilicheza ligi kwa mtindo wa VIEW ONCE kwani ilishuka mwaka huo huo. Kushuka kwao ndiko kulikoleta mpasuko na wengine kujitenga. Waliojitenga ndiyo hawa ambao sasa ni Simba, na waliobaki wakabadili jina kutoka New Young na kujiita Young Africans ambao ndiyo Yanga. Lakini hawa watu walikuwa pamoja mwaka mmoja tu uliopita...na ndiyo waliopo kwenye picha hii. Kwa hiyo leo inatakiwa hii sherehe iwe yao wote! Happy Birthday Yanga na Simba. Furahieni siku yenu kwa amani. Sisi tunajua nyinyi ni ndugu ila mnatuzuga tu! (Zakazakazi ✍️)
    Love
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·285 مشاهدة
  • اقرأ أكثر
    Hii joint meeting imehudhuriwa na viongozi karibu wote wa SADC na EAC kwa kutambua umuhimu wake kwa usalama eneo la maziwa makuu. Viongozi hawa wanajua kuwa usalama wa eneo hili ni muhimu kwa ustawi wa kanda nzima, hasa ikizingatiwa mizozo ya muda mrefu kama ile ya Mashariki mwa DRC. Lakini pia hata viongozi ambao nchi zao zimekuwa kwenye msuguano kwenye mgogoro wa Congo wamehushuria. Paul Kagame wa Rwanda na Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini wamehudhuria pia. Wote tunakumbuka kwamba hivi karibuni Kagame na Ramaphosa walikuwa kwenye uhasama hawa kwa sababu ya tuhuma zinazoelekewa kwa Rwanda kwamba wanawaunda mkono M23, kundi la waasi linalohusishwa na kuvuruga amani Mashariki mwa DRC. Hata hivyo, Tshisekedi ameshindwa kuona umuhimu wa mkutano huu mpaka kumtuma mwakilishi badala yake? Hii inaashiria kutokuwa na ushirikiano wa kutosha au kutokubaliana na juhudi za kutatua mgogoro huu kwa njia ya kidiplomasia. Is this a sign of deeper political divisions within the DRC or a strategic move to maintain sovereignty?..
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·263 مشاهدة
  • اقرأ أكثر
    #PART4 Lakini cha kushangaza, wanaume wengi hawafanyi hivi. Kwa nini? Kwa sababu mwanaume hapendi kuonekana amefeli. Dogo akimuuliza baba yake, "Kwanini ulimuacha mama?" baba atapata kigugumizi. Hakuna mwanaume anayependa aonekane alishindwa kufanya kitu sahihi. Ndiyo maana wanaume wengi husema mambo mazuri kuhusu mama wa mtoto wao, hata kama waliachana kwa mabaya. Lakini wanawake wengi hawawezi kufanya hivyo. Wengi hujaza chuki kwa mtoto. Wanaangalia maisha yao kwa sasa, wanasahau mtoto atakua na atagundua ukweli wenyewe. 50 Cent ni role model wa wanaume wengi kwa sababu moja kubwa, anajua dunia ilivyo. Ndiyo maana hata Chris Brown, kabla ya kuingia kwenye ndoa, alikwenda kwa 50 Cent kumuuliza ushauri. 50 Cent alimwambia USITHUBUTU!
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·375 مشاهدة
  • اقرأ أكثر
    Katika siasa za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), jina la Corneille Nangaa limepita katika nyanja tofauti. Kutoka kuwa msomi wa uchumi, mtumishi wa Umoja wa Mataifa (UNDP), msimamizi wa uchaguzi mkuu. Hadi sasa kuwa mmoja wa watu wanaoitikisa nchi hiyo kwa kiwango kikubwa. Mwanaume huyu ambaye aliwahi kuwa miongoni mwa watendaji wakubwa wa serikali, sasa anatajwa kuwa nyuma ya moja ya harakati hatari zaidi zinazoendelea katika ardhi ya Congo. Akiwa na historia ndefu ya kushika nafasi za juu serikalini, alifikia hatua ya kuanzisha chama chake cha kisiasa, Action for Change (AFC). Lakini hatua zake zilizoibua taharuki kubwa ni uhusiano wake wa karibu na kundi la waasi la M23, ambalo hivi sasa linatajwa kuwa jeshi lake binafsi. Lakini vipi msomi huyu wa uchumi alihamia kutoka kuongoza uchaguzi hadi kusimamia jeshi la waasi? Corneille Nangaa alianza kama msomi wa uchumi, akipata elimu yake kutoka Chuo Kikuu cha Kinshasa.
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·343 مشاهدة
  • اقرأ أكثر
    Usichanganye hivi vitu viwili, ni tofauti sana. Mapenzi na upendo, hivi ni vitu tofauti. Mapenzi Yana utumwa lakini upendo una uhuru, mapenzi yana visasi lakini upendo una msamaha, mapenzi yanamiliki lakini upendo una utu, mapenzi yana mwisho lakini upendo ni wa milele. Mahusiano ya mwanaume na mwanamke ni mapenzi siyo upendo. Huu ni muungano wa kimaslahi, utake usitake ni maslahi. Kila upande una maslahi yake na siyo upendo. Angalia wanavyohesabiana waliyofanyiana aidha mema au mabaya siku wanapoachana. Upendo huwa hauhesabu na hauna kumbukumbu kabisa. Mtu akikuambia nilikupenda sana, wala usijione na hatia, huyo muongo mkubwa. Neno analotakiwa kusema ni "nilikuwa na hisia kali za mapenzi kwako". Huwezi kumpiga mtu unayempenda, wala huwezi kutamani apatwe na mabaya sababu amekuacha. Mtu unayempenda utamtakia mema hata kama kukuacha kwake kulikuumiza. Siku zote utamuunga mkono kwa lolote linalompa furaha na amani hata kama ni kukuacha. Usichanganye upendo na mapenzi ni vitu tofauti. Upendo ni nishati ya asili inayoishi ndani ya mtu lakini mapenzi ni hisia inayotokana na mvuto wa kimahaba.
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·355 مشاهدة
  • اقرأ أكثر
    #PART8 Kwahiyo wakati mapigano makali yakiendelea huko mashariki mwa Congo baina ya vikundi vya Waasi na wanamgambo wa Maimai, hali ikatulia mjini Kinshasa na Rais Kabila akapata nafasi ya kupumua kidogo. Maadui zako wakipigana wewe utafanya nini zaidi ya kunywa supu na chapati 2 kujipongeza? Lakini alichosahau Kabila ni kwamba Kagame ni Jasusi mwandamizi. Wakati wa kusaini mkataba Lemera, Kagame alimchomekea "watu wake" kwenye kikosi chake cha ulinzi. Mmojawapo ni Luteni Rashid Kasereka, Mtutsi (Banyamulenge) wa Kivu Kusini. Januari 16, 2001, Luteni Kasereka alimfyatulia Rais Kabila risasi 4 za tumbo na kumuua papohapo. Jumuiya ya kimataifa ikamtuhumu Kagame kuhusika, lakini akakanusha na kusema ni madai yasiyo na msingi. Baada ya kifo cha Mzee Kabila, mwanae Joseph akaapishwa kuwa Rais akiwa na miaka 29 tu. Joseph akafanya jitihada mbalimbali za kukomesha vita kwa kushirikisha Jumuiya ya kimataifa. Julai 30, 2002, ukasainiwa Mkataba wa Pretoria (The Pretoria Agreement) uliotaka pande zote kusitisha mapigano. Desemba 17, 2002, ukasainiwa Mkataba mwingine ulioitwa Global &Inclusive Agreement (maarufu kama 2003 Peace Deal). Na hatimaye, Aprili 2, 2003, ukasainiwa Mkataba Maarufu wa Sun City Peace Agreement uliomaliza kabisa vita ya Congo. Pamoja na mambo mengine, mkataba huo ulitaka kuondolewa kwa majeshi yote ya kigeni nchini Congo, kuwepo na utaratibu wa uchaguzi wa kidemokrasia, na kuwaingiza jeshini askari wa vikundi vya waasi. Mkataba huo ulihitimisha Vita vya Pili vya Congo. Vita mbaya mno katika historia. Vita hivi vilibatizwa jina "The Great war of Africa" kwa jinsi vilivyoshirikisha mataifa mengi, na jinsi vilivyoleta madhara makubwa kwa watu ikiwemo vifo vya zaidi ya watu 500,000. Baada ya kumalizika kwa vita hivyo, Congo ikarudi kwenye amani, japokuwa kulikuwa na vikundi vidogo vya wanamgambo katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo, hasa eneo la Kivu lakini makundi makubwa yote ya Waasi yalikubali kuweka silaha chini. Kuanzia mwaka 2003 hadi 2006 hali ikatulia kabisa. Kwa mara ya kwanza raia wa Congo wakalala pasi na kusikia milio ya risasi.! (Malisa GJ)
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·558 مشاهدة
  • Hivi mpira wa miguu (football) maana yake ni nini lakini
    Hivi mpira wa miguu (football) maana yake ni nini lakini 👇😳
    0 التعليقات ·0 المشاركات ·178 مشاهدة
  • اقرأ أكثر
    Kama utafuatilia kwa undani kinachoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩, lazima utagundua kuwa Nchi ya Kongo ilikua na kila sababu kuweza kudhibiti hali ya Mashariki mwa Taifa hilo ila kutokana na mipango mibovu na kutegemea misaada na uthaifu wa Viongozi wa Nchi akiwemo Raisi Félix Tshisekedi ndio maana waliodharauliwa sasa wanasonga mbele kwa namna isiyo ya kawaida. Toka Rais Tshisekedi aingia madarakani mwaka 2018 ni mambo yapi ya kimkakati amefanya ili kuhakikisha anakomesha makundi ya uasi mashariki mwa Kongo utabaini hakuna, yeye anaongoza tu akiwa Kinshasa ukanda wa mashariki ni kama amewasusa hali imezidi kuwa mbaya. Hajafanikiwa kubadili upepo kwa namna yoyote sio kijeshi wala kimazungumzo. Mojawapo ya jukumu kuu la Rais wa Nchi yoyote Duniani ni kuhakikisha usalama na amani ya Raia anaowaongoza, sasa Tshisekedi zaidi ya miaka saba (7) sasa yupo madarakani huku Raia wakiendelea kuteswa na vita Mashariki mwa Nchi hiyo huku yeye akiwa hana jipya alilofanya kama Rais kuwanusuru Raia wake, sasa hapo mnatarajia nini kama sio kuvamiwa? Kilichotokea na kinachoelea kwa sasa hivi Nchini Kongo, Viongozi Wakuu wanapaswa kujilaumu wenyewe, maadui zao wanatumia udhaifu wa kimkakati na kufanikisha ajenda zao.Tshisekedi alipaswa baada ya kutwaa Urais tu angehakikisha nguvu kubwa na mipango anaelekeza Mashariki mwa Nchi kwa sababu kule ndipo kwenye changamoto kubwa Nchini Kongo ila hadi sasa anatoa hotuba za kuilaumu Rwanda tu, yeye hajaja na mpango kwamba amejipanga vipi kukomesha uasi eneo hilo la mashariki na kuweka amani ya kudumu. Inashauriwa kabla ya kutaka uongozi wa juu wa Nchi, jipime kwanza. Je, wanafaa? utaweza majukumu? au unafikiri kuongoza Nchi ni rahisi tu kama kumsukuma Mlevi kwenye shimo! Kwa kumalizia, kama Kongo ingekuwa na uongozi thabiti, wenye maono, nguvu, mipango na mikakati madhubuti kupitia tu Jeshi la ndani ilikua na uwezo wa kukomesha Maadui wote. Mipaka ya Kongo inaimgilika kama maji ya kunywa, misitu kama yote haina uangalizi au ulinzi wowote ule. Tuendelee kuiombea Nchi ya Kongo ipate kwanza Viongozi bora na sio bora Viongozi.
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·399 مشاهدة
  • اقرأ أكثر
    Mkutano wa Kilele wa Marais wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika hivi karibuni umemtaka Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Félix Tshisekedi, kukaa meza moja na Waasi wa M23 kwa ajili ya mazungumzo ya pamoja ili kutafuta suluhu ya amani katika taifa hilo. Taarifa iliyotolewa na Mjumbe wa Mkutano huo, ambaye pia ni Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X (Twitter), ilieleza kuwa Viongozi hao walikutana Januari 29, chini ya Uenyekiti wa Rais wa Kenya, William Ruto, kujadili hali ya usalama Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Miongoni mwa makubaliano ya mkutano huo ni pendekezo la Rais Tshisekedi kushiriki mazungumzo na kundi la M23. Kadhalika, Viongozi hao walikubaliana kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inapaswa kuitisha mkutano wa dharura na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ili kutafuta suluhisho la kudumu kwa mgogoro huo. Museveni aliambatanisha taarifa hiyo na orodha ya Viongozi waliohudhuria mkutano huo, wakiwemo Rais wa Kenya William Ruto, Rais wa Somalia Hassan Mohamud, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, Rais wa Rwanda Paul Kagame, na mwenyeji wao, Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
    Like
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·491 مشاهدة
  • Kwa waliosahau msimamo wa Ligi Kuu ya NBC na Ligi Kuu ya Wanawake.

    Hali ipo hivi

    #paulswai
    📈 Kwa waliosahau msimamo wa Ligi Kuu ya NBC na Ligi Kuu ya Wanawake. Hali ipo hivi 😎 #paulswai
    Love
    1
    · 0 التعليقات ·0 المشاركات ·423 مشاهدة
الصفحات المعززة