• Katika hatua mpya ya mzozo unaoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , kundi la Waasi wa M23 likishirikiana na Muungano wa Mto Congo (AFC) limetangaza kuwa Wanajeshi wa zamani wa Jeshi la DR Congo (FARDC) waliokamatwa au kujisalimisha wamehitimu mafunzo ya kiitikadi na mbinu za kijeshi.

    Katika taarifa ya Kundi la M23 kwenye mtandao wao wa X leo Februari 18, picha zilionyesha Wanajeshi hao wakiwa na sare na silaha rasmi za wanamgambo hao. Ujumbe uliambatana na chapisho hilo ulieleza:

    "Wanajeshi wa zamani wa FARDC, waliokamatwa au kujisalimisha, wamemaliza mafunzo ya kiitikadi na mbinu huko Rumangabo Mjini Goma chini ya AFC/M23. Sasa wakiwa na vifaa kamili na wanaolipwa, wametumwa Lubero, ambako wanashiriki kikamilifu muungano wa serikali."

    Wakati huo huo, Uganda imetangaza kuwa vikosi vyake vya kijeshi vimeanza kuelekea Bunia, DRC, ikiwa ni siku chache baada ya Jeshi la Uganda kutoa muda wa saa 24 kwa Askari waliopo eneo hilo kujisalimisha.

    Taarifa nyingine kuwa, hapo jana Kundi la Waasi hao wa M23 wamefanikiwa kuteka eneo la Kamanyola na sasa hivi wanajipanga kuelekea Uvira, Fizi kisha Mkoa wa Tanganyika (Kalemie) kabla ya kwenda Mjini Lubumbashi. Kwa mujibu wa Wananchi wa Kamanyala wanasema kuwa Kundi la Wapiganaji wa Wazalendo ambao wanapigana kwa upande wa Serikali waliibwa Silaha zao kisha wakakimbia na kuwaachia M23 kuichukua Kamanyola.

    Katika hatua mpya ya mzozo unaoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 馃嚚馃嚛, kundi la Waasi wa M23 likishirikiana na Muungano wa Mto Congo (AFC) limetangaza kuwa Wanajeshi wa zamani wa Jeshi la DR Congo (FARDC) waliokamatwa au kujisalimisha wamehitimu mafunzo ya kiitikadi na mbinu za kijeshi. Katika taarifa ya Kundi la M23 kwenye mtandao wao wa X leo Februari 18, picha zilionyesha Wanajeshi hao wakiwa na sare na silaha rasmi za wanamgambo hao. Ujumbe uliambatana na chapisho hilo ulieleza: "Wanajeshi wa zamani wa FARDC, waliokamatwa au kujisalimisha, wamemaliza mafunzo ya kiitikadi na mbinu huko Rumangabo Mjini Goma chini ya AFC/M23. Sasa wakiwa na vifaa kamili na wanaolipwa, wametumwa Lubero, ambako wanashiriki kikamilifu muungano wa serikali." Wakati huo huo, Uganda imetangaza kuwa vikosi vyake vya kijeshi vimeanza kuelekea Bunia, DRC, ikiwa ni siku chache baada ya Jeshi la Uganda kutoa muda wa saa 24 kwa Askari waliopo eneo hilo kujisalimisha. Taarifa nyingine kuwa, hapo jana Kundi la Waasi hao wa M23 wamefanikiwa kuteka eneo la Kamanyola na sasa hivi wanajipanga kuelekea Uvira, Fizi kisha Mkoa wa Tanganyika (Kalemie) kabla ya kwenda Mjini Lubumbashi. Kwa mujibu wa Wananchi wa Kamanyala wanasema kuwa Kundi la Wapiganaji wa Wazalendo ambao wanapigana kwa upande wa Serikali waliibwa Silaha zao kisha wakakimbia na kuwaachia M23 kuichukua Kamanyola.
    0 Reacties 0 aandelen 201 Views
  • Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Nchi ya Uganda (UPDF), Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amesema Uganda inatoa saa (24) vikosi vyote vilivyopo katika Mji wa Bunia Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuacha kuuwa Raia wa kabila la Bahima (ambalo asili yake ni kutoka Nchini Uganda) lasivyo Jeshi lake litashambulia Mji huo.

    Kainerugaba ametoa kauli hiyo Februari 15 katika mtandao wake wa X. Huku akielezwa kuwa na historia ya kuchapisha maoni ya uchochezi kuhusu sera za kigeni mara kwa mara. Alisema ana mamlaka ya Rais Yoweri Museveni, ambaye pia ni Baba yake Mzazi ambako hata hivyo, alipotafutwa Msemaji wa Jeshi la Uganda alisema hawezi kuzungumzia suala hilo.

    Hata hivyo, kabla ya kusasisha ujumbe huo kwenye mtandao wa X, Jenerali huyo alikuwa alieleza bila kutoa ushahidi, kwamba Watu kutoka kabila la Bahima walikuwa wakiuawa huko Nchini DR Congo.

    Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Nchi ya Uganda 馃嚭馃嚞 (UPDF), Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amesema Uganda inatoa saa (24) vikosi vyote vilivyopo katika Mji wa Bunia Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo 馃嚚馃嚛 kuacha kuuwa Raia wa kabila la Bahima (ambalo asili yake ni kutoka Nchini Uganda) lasivyo Jeshi lake litashambulia Mji huo. Kainerugaba ametoa kauli hiyo Februari 15 katika mtandao wake wa X. Huku akielezwa kuwa na historia ya kuchapisha maoni ya uchochezi kuhusu sera za kigeni mara kwa mara. Alisema ana mamlaka ya Rais Yoweri Museveni, ambaye pia ni Baba yake Mzazi ambako hata hivyo, alipotafutwa Msemaji wa Jeshi la Uganda alisema hawezi kuzungumzia suala hilo. Hata hivyo, kabla ya kusasisha ujumbe huo kwenye mtandao wa X, Jenerali huyo alikuwa alieleza bila kutoa ushahidi, kwamba Watu kutoka kabila la Bahima walikuwa wakiuawa huko Nchini DR Congo.
    Like
    1
    0 Reacties 0 aandelen 134 Views
  • #PART5

    Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite.

    Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo.

    Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba.

    Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay.

    April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha.

    March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa.

    Kumekua na jitihada mbalimbali za kumaliza mgogoro wa DRC kwa njia za kidiplomasia ikiwemo mkutano wa viongozi wakuu wa SADC na EAC uliofanyika leo jijini Dar.

    #MyaTake:
    1. Congo imeponzwa na ukarimu wake. Wakati wa vita vya Rwanda, Congo ilipokea Watutsi wengi na kuwapa hifadhi, akiwemo Kagame. Baada ya utawala wa Habyarimana kuangushwa Wahutu nao wakakimbilia Congo na kupewa hifadhi. Sasa hicho kimekua kigezo cha Rwanda kuingiza majeshi Congo kila mara kwa madai ya kuwatafuta Wahutu wa FDLR. Kwa lugha rahisi vita ya ndugu wawili (Wahutu na Watutsi) iliyopaswa kupiganwa Rwanda sasa inapiganwa Congo.

    2. Congo inateswa na mipaka ya kikoloni. Laiti wakati wa kuchora mipaka jamii yote ya Watutsi ingewekwa Rwanda, leo kusingekuwa na Banyamulenge Congo, kwahiyo Watutsi wasingepata sababu ya kuishi Congo na kujifanya raia. Ni sawa na kukuta Wamasai 1,000 pale Longido, halafu uambiwe kati yao wapo wa Kenya. Utawajuaje? Utawatofautishaje?

    3. Congo inateswa na rasilimali zake. Kama eneo la Kivu lisingekuwa na utajiri, mgogoro usingekuwa mkubwa kama ulivyo. Rejea #Part1 kujua utajiri uliopo Kivu. Kumbuka bila Kivu dunia haina laptop wala smartphones kwa sababu 80% ya coltan yote duniani inatoka Kivu.

    4. Rwanda na Uganda ni Keyplayers kwenye mgogoro wa Congo. Kwa miaka mingi majeshi yao yameigeuza Congo shamba la bibi. Waondoe majeshi yao Congo.

    5. Viongozi wengi wa M23 ni Wanyarwanda. Huu ni udhibitisho kuwa Rwanda ni kinara kwenye mgogoro huu.

    6. Congo ni kubwa sana na hivyo inakosa jeshi imara la kutosha kulinda mipaka yake yote. Congo ni kubwa mara 90 ya Rwanda. Wapo wanaoshauri igawanywe kama njia ya kutatua mgogoro. Kama ambavyo Yugoslavia iligawanywa na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.

    7. Kiongozi wa sasa wa M23 Corneille Nangaa alikua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi 2019 na ndiye aliyemtangaza Tshisekedi kuwa Rais kwa ushindi wa 38%. Lakini alilaumiwa kupunguza kura za Martin Fayulu aliyepata 34%. Huenda kuna ahadi alipewa haikutimizwa ndio maana akaungana na Waasi.

    Sababu hizo hapo juu zikifanyiwa kazi, mgogoro wa Congo unaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Mnaopenda kujifunza zaidi, naandika Kitabu. Get ready to have your copy. MWISHO.!

    (Malisa GJ )

    #PART5 Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite. Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo. Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba. Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay. April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha. March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa. Kumekua na jitihada mbalimbali za kumaliza mgogoro wa DRC kwa njia za kidiplomasia ikiwemo mkutano wa viongozi wakuu wa SADC na EAC uliofanyika leo jijini Dar. #MyaTake: 1. Congo imeponzwa na ukarimu wake. Wakati wa vita vya Rwanda, Congo ilipokea Watutsi wengi na kuwapa hifadhi, akiwemo Kagame. Baada ya utawala wa Habyarimana kuangushwa Wahutu nao wakakimbilia Congo na kupewa hifadhi. Sasa hicho kimekua kigezo cha Rwanda kuingiza majeshi Congo kila mara kwa madai ya kuwatafuta Wahutu wa FDLR. Kwa lugha rahisi vita ya ndugu wawili (Wahutu na Watutsi) iliyopaswa kupiganwa Rwanda sasa inapiganwa Congo. 2. Congo inateswa na mipaka ya kikoloni. Laiti wakati wa kuchora mipaka jamii yote ya Watutsi ingewekwa Rwanda, leo kusingekuwa na Banyamulenge Congo, kwahiyo Watutsi wasingepata sababu ya kuishi Congo na kujifanya raia. Ni sawa na kukuta Wamasai 1,000 pale Longido, halafu uambiwe kati yao wapo wa Kenya. Utawajuaje? Utawatofautishaje? 3. Congo inateswa na rasilimali zake. Kama eneo la Kivu lisingekuwa na utajiri, mgogoro usingekuwa mkubwa kama ulivyo. Rejea #Part1 kujua utajiri uliopo Kivu. Kumbuka bila Kivu dunia haina laptop wala smartphones kwa sababu 80% ya coltan yote duniani inatoka Kivu. 4. Rwanda na Uganda ni Keyplayers kwenye mgogoro wa Congo. Kwa miaka mingi majeshi yao yameigeuza Congo shamba la bibi. Waondoe majeshi yao Congo. 5. Viongozi wengi wa M23 ni Wanyarwanda. Huu ni udhibitisho kuwa Rwanda ni kinara kwenye mgogoro huu. 6. Congo ni kubwa sana na hivyo inakosa jeshi imara la kutosha kulinda mipaka yake yote. Congo ni kubwa mara 90 ya Rwanda. Wapo wanaoshauri igawanywe kama njia ya kutatua mgogoro. Kama ambavyo Yugoslavia iligawanywa na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe. 7. Kiongozi wa sasa wa M23 Corneille Nangaa alikua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi 2019 na ndiye aliyemtangaza Tshisekedi kuwa Rais kwa ushindi wa 38%. Lakini alilaumiwa kupunguza kura za Martin Fayulu aliyepata 34%. Huenda kuna ahadi alipewa haikutimizwa ndio maana akaungana na Waasi. Sababu hizo hapo juu zikifanyiwa kazi, mgogoro wa Congo unaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Mnaopenda kujifunza zaidi, naandika Kitabu. Get ready to have your copy. MWISHO.! (Malisa GJ 鉁嶏笍)
    Like
    1
    0 Reacties 0 aandelen 833 Views
  • Jumuiya ya kimataifa inafuatilia kwa karibu hali inayoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), huku mashirika ya haki za binadamu yakilaani uhalifu wa kivita unaofanywa na pande zote dhidi ya raia.

    Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa maelfu ya watu wamelazimika kuyakimbia makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea, huku ukatili dhidi ya wanawake na watoto ukiongezeka kwa kiwango cha kutisha.

    Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetangaza kuwa inafuatilia kwa karibu mzozo huu na imeonya kuwa yeyote anayehusika na uhalifu wa kivita, dhidi ya binadamu, au mauaji ya halaiki hatosazwa na mkono wa sheria.

    Mgogoro wa DRC ni wa muda mrefu na wenye mizizi mirefu. Tangu miaka ya 1990, taifa hili limepitia machafuko ya mara kwa mara, yakichochewa na rasilimali za madini,ukosefu wa utawala thabiti, na uhusiano tata wa kisiasa kati ya mataifa jirani, hususan Rwanda na Uganda.

    M23, kundi la waasi linalotajwa kupokea msaada kutoka nje, limeendelea kushikilia maeneo muhimu, hususan Goma, na hata kutishia kuuteka mji wa Kinshasa.

    Katika mazingira haya, kama ungekuwa Rais wa DRC, Félix Tshisekedi, ungefanya nini?

    Kwa mtazamo wangu, suluhisho pekee ni mazungumzo na diplomasia.

    Historia imeonyesha kuwa vita dhidi ya makundi ya waasi kama M23 si rahisi kushinda kwa nguvu za kijeshi pekee.

    Licha ya msaada wa kijeshi kutoka kwa MONUSCO (Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC) na majeshi ya kikanda kama vile EACRF (East African Community Regional Force), kundi hili limeendelea kuwa tishio kubwa kwa utawala wa Tshisekedi.

    Ikiwa Rais Tshisekedi ataendelea kulazimisha suluhisho la kijeshi bila mpango wa mazungumzo, hatari ipo kwamba mapigano yatapanuka zaidi, na hata kutishia utulivu wa taifa kwa ujumla.

    Hatua muhimu kwa sasa ni kuitisha mazungumzo ya dhati na kutafuta njia ya kidiplomasia ya kumaliza mgogoro huu kabla hali haijazidi kuwa mbaya.
    Jumuiya ya kimataifa inafuatilia kwa karibu hali inayoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), huku mashirika ya haki za binadamu yakilaani uhalifu wa kivita unaofanywa na pande zote dhidi ya raia. Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa maelfu ya watu wamelazimika kuyakimbia makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea, huku ukatili dhidi ya wanawake na watoto ukiongezeka kwa kiwango cha kutisha. Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetangaza kuwa inafuatilia kwa karibu mzozo huu na imeonya kuwa yeyote anayehusika na uhalifu wa kivita, dhidi ya binadamu, au mauaji ya halaiki hatosazwa na mkono wa sheria. Mgogoro wa DRC ni wa muda mrefu na wenye mizizi mirefu. Tangu miaka ya 1990, taifa hili limepitia machafuko ya mara kwa mara, yakichochewa na rasilimali za madini,ukosefu wa utawala thabiti, na uhusiano tata wa kisiasa kati ya mataifa jirani, hususan Rwanda na Uganda. M23, kundi la waasi linalotajwa kupokea msaada kutoka nje, limeendelea kushikilia maeneo muhimu, hususan Goma, na hata kutishia kuuteka mji wa Kinshasa. Katika mazingira haya, kama ungekuwa Rais wa DRC, Félix Tshisekedi, ungefanya nini? Kwa mtazamo wangu, suluhisho pekee ni mazungumzo na diplomasia. Historia imeonyesha kuwa vita dhidi ya makundi ya waasi kama M23 si rahisi kushinda kwa nguvu za kijeshi pekee. Licha ya msaada wa kijeshi kutoka kwa MONUSCO (Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC) na majeshi ya kikanda kama vile EACRF (East African Community Regional Force), kundi hili limeendelea kuwa tishio kubwa kwa utawala wa Tshisekedi. Ikiwa Rais Tshisekedi ataendelea kulazimisha suluhisho la kijeshi bila mpango wa mazungumzo, hatari ipo kwamba mapigano yatapanuka zaidi, na hata kutishia utulivu wa taifa kwa ujumla. Hatua muhimu kwa sasa ni kuitisha mazungumzo ya dhati na kutafuta njia ya kidiplomasia ya kumaliza mgogoro huu kabla hali haijazidi kuwa mbaya.
    0 Reacties 0 aandelen 426 Views
  • Bunge la Nchi ya Uganda limependekeza Wabunge Wanajeshi kuvaa mavazi rasmi ya Bunge wakiwa Bungeni, badala ya kuvaa sare zao wakati wa mijadala.

    Kamati ya Bunge inayosimamia masuala ya utaratibu na nidhamu imesema si sahihi kwa Wabunge hao wanaowakilisha Wanajeshi kuingia na magwanda yao, kwa kuwa yanaonyesha ishara ya kuwa vitani.

    Ikumbukwe kwamba Nchi ya Uganda ndio Nchi pekee barani Afrika wenye Wabunge Wanajeshi. Wanajeshi hao huteuliwa Jeshini kisha kupigiwa kura na kupatikana Wabunge hao huku Watatu (3) kati yao lazima wawe Wanawake.

    Bunge la Nchi ya Uganda 馃嚭馃嚞 limependekeza Wabunge Wanajeshi kuvaa mavazi rasmi ya Bunge wakiwa Bungeni, badala ya kuvaa sare zao wakati wa mijadala. Kamati ya Bunge inayosimamia masuala ya utaratibu na nidhamu imesema si sahihi kwa Wabunge hao wanaowakilisha Wanajeshi kuingia na magwanda yao, kwa kuwa yanaonyesha ishara ya kuwa vitani. Ikumbukwe kwamba Nchi ya Uganda ndio Nchi pekee barani Afrika wenye Wabunge Wanajeshi. Wanajeshi hao huteuliwa Jeshini kisha kupigiwa kura na kupatikana Wabunge hao huku Watatu (3) kati yao lazima wawe Wanawake.
    Like
    1
    0 Reacties 0 aandelen 121 Views
  • RASMI : Young Africans vs Ken Gold ni Khalid Aucho na Maokoto Day....

    Mashabiki wa klab ya Young Africans wameuomba Uongozi wa klab yao Juu ya kumtaarifu kiungo wao Mkabaji Raia wa Uganda Khalid Aucho 'Doctor' kuwa ndiye watakaye mpa zawadi ya pesa 'Maokoto kwenye kibegi' siku ya Jumatano kwenye mchezo wao wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Klab ya Ken Gold,

    Ameyasema hayo Mkuu wa kitengo cha habari Ali kamwe baada ya kupokea maombi hayo kutoka kwa mashabiki wa klab yao,

    Mashabiki wa klab ya Yanga wamekuwa na utaratibu huo na baadhi ya wachezaji ambao wamepata maokoto hayo ni:

    Bacca
    Kibwana
    Mzize
    Maxi
    Pacome

    Next game:

    馃Young Africans vs Ken Gold
    05-02-2025
    16:00 Hrs
    Kmc Complex
    RASMI : Young Africans vs Ken Gold ni Khalid Aucho na Maokoto Day.... Mashabiki wa klab ya Young Africans wameuomba Uongozi wa klab yao Juu ya kumtaarifu kiungo wao Mkabaji Raia wa Uganda Khalid Aucho 'Doctor' kuwa ndiye watakaye mpa zawadi ya pesa 'Maokoto kwenye kibegi' siku ya Jumatano kwenye mchezo wao wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Klab ya Ken Gold, Ameyasema hayo Mkuu wa kitengo cha habari Ali kamwe baada ya kupokea maombi hayo kutoka kwa mashabiki wa klab yao, Mashabiki wa klab ya Yanga wamekuwa na utaratibu huo na baadhi ya wachezaji ambao wamepata maokoto hayo ni: 馃憠Bacca 馃憠Kibwana 馃憠Mzize 馃憠Maxi 馃憠Pacome Next game: 馃Young Africans vs Ken Gold 馃搶05-02-2025 馃晳16:00 Hrs 鉀矺mc Complex
    Like
    2
    0 Reacties 0 aandelen 494 Views
  • #PART10

    March 23, 2009 Mkataba wa amani uitwao "March 23 Agreement" ukasainiwa huko Goma, kati ya serikali ya Congo na Waasi wa CNDP, wasuluhishi wakiwa mzee Mkapa na mzee Obasanjo. Mapigano yakasitishwa

    Ntaganda na askari wa CNDP wakaingizwa kwenye jeshi la Congo (FARDC). Kukawepo na miaka mitatu ya amani, vita ikakoma kabisa. Lakini ghafla, April 04, mwaka 2012 Bosco Ntaganda alitangaza kujitoa kwenye jeshi la Congo (FARDC) pamoja na baadhi ya askari waliokuwa wanamgambo wa CNDP. Ntaganda alidai Serikali ya Congo imeshindwa kutekeleza mkataba wa amani wa Machi 23, 2009.

    Alisema Makataba huo uliweka masharti ya kutowabughudhi askari 600 wa CNDP waliokataa kujiunga na jeshi la Congo. Lakini serikali ya Congo iliwashughulikia. Baadhi walikamatwa na wengine kuuawa. Pia alidai serikali ya Congo imeshindwa kuwalinda Watutsi (Banyamulenge) waishio mashariki mwa nchi hiyo.

    Ntaganda akatangaza kuanzisha kikundi kipya cha waasi kiitwacho M23. Alidai kutumia jina hilo ili kuikumbusha serikali ya Congo kuheshimu mkataba wa amani wa Machi 23, 2009. Kundi la M23 likapata wafuasi wengi hasa askari wa zamani wa CNDP na Banyamulenge wa Kivu. Mapigano yakaanza upya.

    Rwanda na Uganda zikashutumiwa kuunga mkono waasi hao, lakini zikakataa. Hata hivyo Rwanda ililaumiwa kwa kuruhusu M23 kuwa na kambi za kijeshi katika miji ya Gisenyi na Rusizi. Pia Rwanda ilihusishwa na mgogoro huo kwa sababu Ntaganda hakuwa Mkongomani, bali Mnyarwanda aliyezaliwa na kukulia Rwanda. Ametumikia jeshi la Rwanda kwa miaka mingi, kabla ya kuhamia Congo kupigania haki za Banyamulenge.

    Baada ya mwaka mmoja wa mapigano makali, vikosi vya M23 vikazidiwa nguvu na jeshi la serikali. Machi 18, 2013, Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda na akaenda mwenyewe kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani mjini Kigali. Akasafirishwa kwenda The Heague kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai (ICC).

    Mwaka 2015 kesi yake ikaanza kusikilizwa, na mwaka 2019 akapatikana na hatia katika makosa 18, yakiwemo ubakaji, mauaji ya raia wasio na hatia, na kutumikisha watoto jeshini. Akahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, adhabu ambayo anaitumikia hadi sasa.
    (Malisa GJ)

    #PART10 March 23, 2009 Mkataba wa amani uitwao "March 23 Agreement" ukasainiwa huko Goma, kati ya serikali ya Congo na Waasi wa CNDP, wasuluhishi wakiwa mzee Mkapa na mzee Obasanjo. Mapigano yakasitishwa Ntaganda na askari wa CNDP wakaingizwa kwenye jeshi la Congo (FARDC). Kukawepo na miaka mitatu ya amani, vita ikakoma kabisa. Lakini ghafla, April 04, mwaka 2012 Bosco Ntaganda alitangaza kujitoa kwenye jeshi la Congo (FARDC) pamoja na baadhi ya askari waliokuwa wanamgambo wa CNDP. Ntaganda alidai Serikali ya Congo imeshindwa kutekeleza mkataba wa amani wa Machi 23, 2009. Alisema Makataba huo uliweka masharti ya kutowabughudhi askari 600 wa CNDP waliokataa kujiunga na jeshi la Congo. Lakini serikali ya Congo iliwashughulikia. Baadhi walikamatwa na wengine kuuawa. Pia alidai serikali ya Congo imeshindwa kuwalinda Watutsi (Banyamulenge) waishio mashariki mwa nchi hiyo. Ntaganda akatangaza kuanzisha kikundi kipya cha waasi kiitwacho M23. Alidai kutumia jina hilo ili kuikumbusha serikali ya Congo kuheshimu mkataba wa amani wa Machi 23, 2009. Kundi la M23 likapata wafuasi wengi hasa askari wa zamani wa CNDP na Banyamulenge wa Kivu. Mapigano yakaanza upya. Rwanda na Uganda zikashutumiwa kuunga mkono waasi hao, lakini zikakataa. Hata hivyo Rwanda ililaumiwa kwa kuruhusu M23 kuwa na kambi za kijeshi katika miji ya Gisenyi na Rusizi. Pia Rwanda ilihusishwa na mgogoro huo kwa sababu Ntaganda hakuwa Mkongomani, bali Mnyarwanda aliyezaliwa na kukulia Rwanda. Ametumikia jeshi la Rwanda kwa miaka mingi, kabla ya kuhamia Congo kupigania haki za Banyamulenge. Baada ya mwaka mmoja wa mapigano makali, vikosi vya M23 vikazidiwa nguvu na jeshi la serikali. Machi 18, 2013, Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda na akaenda mwenyewe kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani mjini Kigali. Akasafirishwa kwenda The Heague kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai (ICC). Mwaka 2015 kesi yake ikaanza kusikilizwa, na mwaka 2019 akapatikana na hatia katika makosa 18, yakiwemo ubakaji, mauaji ya raia wasio na hatia, na kutumikisha watoto jeshini. Akahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, adhabu ambayo anaitumikia hadi sasa. (Malisa GJ)
    Like
    1
    0 Reacties 0 aandelen 624 Views
  • #PART9

    Baada ya miaka mitatu ya utulivu, ghafla 2006 Jenerali Laurent Nkunda, aliasi jeshi kwa madai serikali imeshindwa kutekeleza Mkataba wa Amani wa SunCity. Ikumbukwe kabla ya kujiunga na Jeshi, alikua mpiganaji wa RCD - Goma, kundi lililoungwa mkono na Rwanda. Baada ya mkataba wa Suncity waasi wote waliingizwa jeshini akiwemo Nkunda.

    Lakini Juni 29, 2006, Nkunda akaasi jeshi na kuunda kundi la Congrès National pour la Défense du Peuple (CNDP). Madai yake:
    - Askari wa vikundi vya waasi walioingizwa jeshini hawakupewa vyeo.
    - Serikali ya Congo kushindwa kuwatanbua Watutsi (Banyamulenge) waishio mashariki mwa nchi hiyo kama raia wa Congo.
    - Serikali ya Congo kushindwa kuwakamata wanamgambo wa kihutu wa FDLR (Intarahanwe) waliojificha Congo baada ya kufanya mauaji ya kimbari Rwanda 1994.

    Nkunda akasema lengo la kuanzisha kundi la waasi la CNDP ni kupigania haki za Watutsi waishio mashariki mwa Congo (Banyamulenge) na kukabiliana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR. Nkunda akaungwa mkono na Rwanda na Uganda, akapewa silaha, vita ikaanza upyaaaaa (tamka kwa sauti ya mbunge Bwege).

    CNDP ikaua raia wengi wenye asili ya Kihutu ikiwatumu kuwa wafuasi wa FDLR. Serikali ya Burundi ikiongozwa na Piere Nkurunzinza (Mhutu) ikaingiza jeshi Congo kupambana na CNDP ili kulinda raia wake waliokua Congo. Kwa miaka mitatu kukawa na mapigano makali sana mashariki mwa Congo.

    January 2009 Waasi wa CNDP wakazidiwa. Laurent Nkunda akakimbilia Rwanda. Alipofika akakamatwa na kuwekwa kizuizini. Mpaka leo, bado anashikiliwa bila kufikishwa mahakamani. Jenerali Bosco Ntaganda, Mtutsi (Banyamulenge) wa Kivu akateuliwa kuongoza CNDP. Akafanya vitendo vingi vya kikatili kwa raia kuliko mtangulizi wake, kama ubakaji, mauaji ya halaiki, na kutumikisha watoto jeshini.

    Machi 23, 2009 serikali ya Congo na CNDP wakasaini Mkataba wa Amani, ulioitwa "March 23 Agreement" wenye masharti yafuatayo:
    - Kusitisha mapigano kwa pande zote.
    - Kuingiza askari wa CNDP kwenye jeshi la Congo.
    - Kutowashtaki askari wa CNDP kwa makosa waliyofanya wakati wa vita.
    - Wananchi wa Kivu wanufaike na rasilimali zao
    - Kulinda haki za binadamu Kivu
    (Malisa GJ)

    #PART9 Baada ya miaka mitatu ya utulivu, ghafla 2006 Jenerali Laurent Nkunda, aliasi jeshi kwa madai serikali imeshindwa kutekeleza Mkataba wa Amani wa SunCity. Ikumbukwe kabla ya kujiunga na Jeshi, alikua mpiganaji wa RCD - Goma, kundi lililoungwa mkono na Rwanda. Baada ya mkataba wa Suncity waasi wote waliingizwa jeshini akiwemo Nkunda. Lakini Juni 29, 2006, Nkunda akaasi jeshi na kuunda kundi la Congrès National pour la Défense du Peuple (CNDP). Madai yake: - Askari wa vikundi vya waasi walioingizwa jeshini hawakupewa vyeo. - Serikali ya Congo kushindwa kuwatanbua Watutsi (Banyamulenge) waishio mashariki mwa nchi hiyo kama raia wa Congo. - Serikali ya Congo kushindwa kuwakamata wanamgambo wa kihutu wa FDLR (Intarahanwe) waliojificha Congo baada ya kufanya mauaji ya kimbari Rwanda 1994. Nkunda akasema lengo la kuanzisha kundi la waasi la CNDP ni kupigania haki za Watutsi waishio mashariki mwa Congo (Banyamulenge) na kukabiliana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR. Nkunda akaungwa mkono na Rwanda na Uganda, akapewa silaha, vita ikaanza upyaaaaa (tamka kwa sauti ya mbunge Bwege). CNDP ikaua raia wengi wenye asili ya Kihutu ikiwatumu kuwa wafuasi wa FDLR. Serikali ya Burundi ikiongozwa na Piere Nkurunzinza (Mhutu) ikaingiza jeshi Congo kupambana na CNDP ili kulinda raia wake waliokua Congo. Kwa miaka mitatu kukawa na mapigano makali sana mashariki mwa Congo. January 2009 Waasi wa CNDP wakazidiwa. Laurent Nkunda akakimbilia Rwanda. Alipofika akakamatwa na kuwekwa kizuizini. Mpaka leo, bado anashikiliwa bila kufikishwa mahakamani. Jenerali Bosco Ntaganda, Mtutsi (Banyamulenge) wa Kivu akateuliwa kuongoza CNDP. Akafanya vitendo vingi vya kikatili kwa raia kuliko mtangulizi wake, kama ubakaji, mauaji ya halaiki, na kutumikisha watoto jeshini. Machi 23, 2009 serikali ya Congo na CNDP wakasaini Mkataba wa Amani, ulioitwa "March 23 Agreement" wenye masharti yafuatayo: - Kusitisha mapigano kwa pande zote. - Kuingiza askari wa CNDP kwenye jeshi la Congo. - Kutowashtaki askari wa CNDP kwa makosa waliyofanya wakati wa vita. - Wananchi wa Kivu wanufaike na rasilimali zao - Kulinda haki za binadamu Kivu (Malisa GJ)
    0 Reacties 0 aandelen 534 Views
  • #PART7

    Baada ya kundi la RCD kuvunjika, yalizaliwa makundi mawili ambayo ni RCD Goma (liliungwa mkono na Rwanda) na RCD Kisangani (likiungwa mkono na Uganda). Aliyekua Kiongozi wa RCD Ernest Wamba Dia Wamba akaamua kukaa pembeni baada ya kugundua wanatumika kupigana kwa maslahi ya watu wengine.

    Kwahiyo makundi haya yakapata viongozi wapya. RCD-Goma ikaongozwa na Kanali Emile Ilunga na RCD-Kisangani, ikaongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi. Ikumbukwe kabla kundi la RCD halijavunjika, lilikuwa limeshikilia maeneo mengi ya migodi huko Goma, Bukavu, na Katanga. Sasa baada ya kuvunjika, ukatokea mgogoro wa kugawana maeneo. Mgodi upi uende RCD Goma na upi uende RCD Kisangani.

    Kwa hiyo wakaanza kupigana tena wao kwa wao. Ikapigwa vita moja kali sana pale Kisangani, ikabatizwa jina la ‘Six Day War’ maana ilipiganwa kwa siku sita. RCD-Goma, ikawatandika vibaya sana RCD-Kisangani. Tar.10 June 2000 RCD Kisangani ikaachia migodi yote na kukimbia. RCD-Goma wakataka RCD-Kisangani wabadili jina lao maana mji wa Kisangani haukuwa chini yao tena. Hatimaye, RCD-Kisangani wakabadili na kujiita RCD-ML, yaani Rally for Congolese Democracy - Liberation Movement.

    RCD - ML walikimbilia kwenye milima Mikeno karibu na hifadhi ya Virunga kujipanga upya. RCD-Goma wakaendeleza mapigano kuelekea Kinshasa. Lakini kufika Bukavu wakakumbana na upinzani kutoka wanamgambo wa Maï-Maï waliokua wamepewa silaha na serikali za majimbo kupigana na askari yoyote mgeni kwenye ardhi yao.

    Maï-Maï waliongozwa na Kanali Musa Sindi upande wa Kivu Kusini na Sheikh Ntabo Ntaberi kwa Kivu Kaskazini. Kwa hiyo safari ya RCD Goma kwenda Kinshasa kumng’oa Laurent Kabila ikakutana na kizuizi cha Maï-Maï. Wakachapana sana. Watu zaidi ya 1,000 wakapoteza maisha.

    Kwahiyo vita ya kumng'oa Laurent Kabila ikawa ngumu maana vikundi vingi vya waasi vilianza kupigana vyenyewe kwa vyenyewe. Hali hiyo ilifanya vita kuwa ngumu zaidi, maana watu walipigana bila mpangilio. Risasi zikafyatuliwa hovyo hovyo na wananchi wengi wakapoteza maisha.
    (Malisa GJ)

    #PART7 Baada ya kundi la RCD kuvunjika, yalizaliwa makundi mawili ambayo ni RCD Goma (liliungwa mkono na Rwanda) na RCD Kisangani (likiungwa mkono na Uganda). Aliyekua Kiongozi wa RCD Ernest Wamba Dia Wamba akaamua kukaa pembeni baada ya kugundua wanatumika kupigana kwa maslahi ya watu wengine. Kwahiyo makundi haya yakapata viongozi wapya. RCD-Goma ikaongozwa na Kanali Emile Ilunga na RCD-Kisangani, ikaongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi. Ikumbukwe kabla kundi la RCD halijavunjika, lilikuwa limeshikilia maeneo mengi ya migodi huko Goma, Bukavu, na Katanga. Sasa baada ya kuvunjika, ukatokea mgogoro wa kugawana maeneo. Mgodi upi uende RCD Goma na upi uende RCD Kisangani. Kwa hiyo wakaanza kupigana tena wao kwa wao. Ikapigwa vita moja kali sana pale Kisangani, ikabatizwa jina la ‘Six Day War’ maana ilipiganwa kwa siku sita. RCD-Goma, ikawatandika vibaya sana RCD-Kisangani. Tar.10 June 2000 RCD Kisangani ikaachia migodi yote na kukimbia. RCD-Goma wakataka RCD-Kisangani wabadili jina lao maana mji wa Kisangani haukuwa chini yao tena. Hatimaye, RCD-Kisangani wakabadili na kujiita RCD-ML, yaani Rally for Congolese Democracy - Liberation Movement. RCD - ML walikimbilia kwenye milima Mikeno karibu na hifadhi ya Virunga kujipanga upya. RCD-Goma wakaendeleza mapigano kuelekea Kinshasa. Lakini kufika Bukavu wakakumbana na upinzani kutoka wanamgambo wa Maï-Maï waliokua wamepewa silaha na serikali za majimbo kupigana na askari yoyote mgeni kwenye ardhi yao. Maï-Maï waliongozwa na Kanali Musa Sindi upande wa Kivu Kusini na Sheikh Ntabo Ntaberi kwa Kivu Kaskazini. Kwa hiyo safari ya RCD Goma kwenda Kinshasa kumng’oa Laurent Kabila ikakutana na kizuizi cha Maï-Maï. Wakachapana sana. Watu zaidi ya 1,000 wakapoteza maisha. Kwahiyo vita ya kumng'oa Laurent Kabila ikawa ngumu maana vikundi vingi vya waasi vilianza kupigana vyenyewe kwa vyenyewe. Hali hiyo ilifanya vita kuwa ngumu zaidi, maana watu walipigana bila mpangilio. Risasi zikafyatuliwa hovyo hovyo na wananchi wengi wakapoteza maisha. (Malisa GJ)
    Like
    1
    0 Reacties 0 aandelen 740 Views
  • Ukisikia madai ya Rwanda kuvuruga amani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ukarudi kuangalia ramani na takwimu za mataifa hayo hakika utaamini ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi. Kitakwimu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeizidi Rwanda kila kitu ikiwemo ukubwa wa eneo, rasilimali, madini pamoja na idadi ya Watu.

    Eneo la Congo ni karibu mara mia (100) ya eneo la Rwanda. Idadi ya Watu wa Kongo ni takribani mara 10 Watu wa Rwanda. Pamoja na hayo yote Congo wanalalamika kwamba Rwanda ndio inayounga mkono makundi ya waasi mashariki mwa nchi hiyo ambayo yamelemea majeshi ya serikali na kusonga mbele kiasi cha kutwaa miji mikubwa ya kimkakati yenye utajiri mkubwa wa madini.

    Rwanda pamoja na kuzidiwa takwimu hizo ila mipango thabiti na uwekezaji wa kimkakati katika masuala ya kijeshi, ulinzi na usalama katika eneo hilo ndio umeifanya ionekane kama ndio taifa kubwa. Yaani kiufupi ukiwa hujui ramani na takwimu unaweza kudhani Rwanda ndio taifa kubwa ndio maana inalalamikiwa kuionea Kongo. Kiufupi Rwanda inanufaika mno na mipango thabiti ya kiuongozi, wakati Kongo ikiwa na uongozi usio na mipango thabiti ya kikanda na kimkakati kulinda mipaka yake na majimbo ya Mashariki yenye utajiri mkubwa wa madini

    Rwanda ina idadi kubwa ya Watutsi ambao pia wanapatikana Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na wachache Burundi na Uganda. Historia ya watutsi inasemekana walitokea Ethiopia kuja maziwa makuu na sifa yao kuu wanapenda uongozi (kwa mnaowajua mtakua mashahidi). Jamii ya watutsi ni watu ambao huwa hawapendi unyonge wala kuonewa, ni wepesi kujitetea na huwa wanaumoja sana.

    Baada ya Wakoloni kugawa mipaka ndio walisababisha watutsi kujikuta ndani ya nchi nyingi tofauti ila ni wazawa wa maeneo hayo na historia yao katika nchi hizo ni toka zama za kale hivyo ni ngumu kuwaita Wahamiaji. Watutsi ndio waliomsaidia Hayati Laurent Kabila kumpindua Mobutu Seseseko na inasemekana Mama mzazi wa Joseph Kabila alikua Mtutsi pia. Kimsingi Kongo haikupaswa kuilalamikia Rwanda, bali Rwanda ndio ingepaswa kuilalamikia Kongo.

    Ukisikia madai ya Rwanda 馃嚪馃嚰 kuvuruga amani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 馃嚚馃嚛 ukarudi kuangalia ramani na takwimu za mataifa hayo hakika utaamini ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi. Kitakwimu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeizidi Rwanda kila kitu ikiwemo ukubwa wa eneo, rasilimali, madini pamoja na idadi ya Watu. Eneo la Congo ni karibu mara mia (100) ya eneo la Rwanda. Idadi ya Watu wa Kongo ni takribani mara 10 Watu wa Rwanda. Pamoja na hayo yote Congo wanalalamika kwamba Rwanda ndio inayounga mkono makundi ya waasi mashariki mwa nchi hiyo ambayo yamelemea majeshi ya serikali na kusonga mbele kiasi cha kutwaa miji mikubwa ya kimkakati yenye utajiri mkubwa wa madini. Rwanda pamoja na kuzidiwa takwimu hizo ila mipango thabiti na uwekezaji wa kimkakati katika masuala ya kijeshi, ulinzi na usalama katika eneo hilo ndio umeifanya ionekane kama ndio taifa kubwa. Yaani kiufupi ukiwa hujui ramani na takwimu unaweza kudhani Rwanda ndio taifa kubwa ndio maana inalalamikiwa kuionea Kongo. Kiufupi Rwanda inanufaika mno na mipango thabiti ya kiuongozi, wakati Kongo ikiwa na uongozi usio na mipango thabiti ya kikanda na kimkakati kulinda mipaka yake na majimbo ya Mashariki yenye utajiri mkubwa wa madini Rwanda ina idadi kubwa ya Watutsi ambao pia wanapatikana Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na wachache Burundi na Uganda. Historia ya watutsi inasemekana walitokea Ethiopia kuja maziwa makuu na sifa yao kuu wanapenda uongozi (kwa mnaowajua mtakua mashahidi). Jamii ya watutsi ni watu ambao huwa hawapendi unyonge wala kuonewa, ni wepesi kujitetea na huwa wanaumoja sana. Baada ya Wakoloni kugawa mipaka ndio walisababisha watutsi kujikuta ndani ya nchi nyingi tofauti ila ni wazawa wa maeneo hayo na historia yao katika nchi hizo ni toka zama za kale hivyo ni ngumu kuwaita Wahamiaji. Watutsi ndio waliomsaidia Hayati Laurent Kabila kumpindua Mobutu Seseseko na inasemekana Mama mzazi wa Joseph Kabila alikua Mtutsi pia. Kimsingi Kongo haikupaswa kuilalamikia Rwanda, bali Rwanda ndio ingepaswa kuilalamikia Kongo.
    Like
    1
    0 Reacties 0 aandelen 392 Views
  • #PART6

    Alipoingia Ikulu Kabila alifuta jina Zaire na kurudisha Congo (Jamhuri ya kidemokrasia). Baadae alifikiria kuiachia Kivu, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini adimu duniani. Akasema "to hell with Lemera Agreement" akautupilia mbali mkataba wa Lemera. Akasema Kivu itabaki Congo na madini ya Kivu yatajenga Congo. Full stop. Ashakuwa Rais utamfanya nini?

    Kagame hakuamini macho yake. Alishawaza jinsi ambavyo Rwanda ingekuwa Dubai ya Afrika kwa rasilimali za Congo. Lakini ghafla aligeukwa na mshirika wake Laurent Désiré Kabila. Akamfuata "Godfather" wake mzee Museveni. Mzee akasema kama katugeuka tumpige. Wakatafuta kikundi cha Waasi wakiunge mkono. Wakapata Rassemblement Congolais pour la Démocratie (RCD), kilichoongozwa na Jenerali Ernest Wamba dia Wamba. Kikundi kikapewa silaha na fedha kikaanza kumshughulikia Kabila.

    RCD ikaanza kuchapana na jeshi la Congo (FARDC) ikiwa na backup ya Rwanda na Uganda. Vita vikapamba moto. Rwanda na Uganda nao wakaingiza majeshi Congo kusaidia waasi wa RCD. Kabila akaona anazidiwa, akaomba msaada Angola na Chad. Nchi hizo zikaleta vikosi vyake Congo. Mapigano yakawa makali sana. Eneo la mashariki mwa Congo likageuka machinjioni. Watu walikufa kwa wingi, mpaka maiti zikatapakaa barabarani bila kuzikwa, zikawa zinadonolewa na ndege.

    Hii iliitwa Vita ya Pili ya Congo (1998–2002), iliyokua mbaya zaidi katika historia ya vita zote Afrika. Imebatizwa jina "Vita Kuu ya Afrika". Inakadiriwa watu laki tano walipoteza maisha huku mamilioni wakikimbia nchi. Mapigano yaliendelea, huku vikosi vya Rwanda na Uganda vikichota madini. Katikati ya mapigano mgongano wa kimaslahi ukajitokeza.

    Jasin Stearns, katika kitabu chake Dancing in the Glory of Monsters, anasema Kagame alishindwa kuelewana na "godfather" wake Museveni juu ya mgawanyo wa mali. Hali hiyo ilifanya kikundi cha RCD kipasuke na kuzaliwa vikundi viwili. Cha kwanza kikajiita RCD-Goma kikiongozwa na Kanali Emile Ilunga (hiki kilisaidiwa na Rwanda) na cha pili kikajiita RCD-Kisangani, kikiongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi (kikisaidiwa na Uganda).
    (Malisa GJ)

    #PART6 Alipoingia Ikulu Kabila alifuta jina Zaire na kurudisha Congo (Jamhuri ya kidemokrasia). Baadae alifikiria kuiachia Kivu, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini adimu duniani. Akasema "to hell with Lemera Agreement" akautupilia mbali mkataba wa Lemera. Akasema Kivu itabaki Congo na madini ya Kivu yatajenga Congo. Full stop. Ashakuwa Rais utamfanya nini? Kagame hakuamini macho yake. Alishawaza jinsi ambavyo Rwanda ingekuwa Dubai ya Afrika kwa rasilimali za Congo. Lakini ghafla aligeukwa na mshirika wake Laurent Désiré Kabila. Akamfuata "Godfather" wake mzee Museveni. Mzee akasema kama katugeuka tumpige. Wakatafuta kikundi cha Waasi wakiunge mkono. Wakapata Rassemblement Congolais pour la Démocratie (RCD), kilichoongozwa na Jenerali Ernest Wamba dia Wamba. Kikundi kikapewa silaha na fedha kikaanza kumshughulikia Kabila. RCD ikaanza kuchapana na jeshi la Congo (FARDC) ikiwa na backup ya Rwanda na Uganda. Vita vikapamba moto. Rwanda na Uganda nao wakaingiza majeshi Congo kusaidia waasi wa RCD. Kabila akaona anazidiwa, akaomba msaada Angola na Chad. Nchi hizo zikaleta vikosi vyake Congo. Mapigano yakawa makali sana. Eneo la mashariki mwa Congo likageuka machinjioni. Watu walikufa kwa wingi, mpaka maiti zikatapakaa barabarani bila kuzikwa, zikawa zinadonolewa na ndege. Hii iliitwa Vita ya Pili ya Congo (1998–2002), iliyokua mbaya zaidi katika historia ya vita zote Afrika. Imebatizwa jina "Vita Kuu ya Afrika". Inakadiriwa watu laki tano walipoteza maisha huku mamilioni wakikimbia nchi. Mapigano yaliendelea, huku vikosi vya Rwanda na Uganda vikichota madini. Katikati ya mapigano mgongano wa kimaslahi ukajitokeza. Jasin Stearns, katika kitabu chake Dancing in the Glory of Monsters, anasema Kagame alishindwa kuelewana na "godfather" wake Museveni juu ya mgawanyo wa mali. Hali hiyo ilifanya kikundi cha RCD kipasuke na kuzaliwa vikundi viwili. Cha kwanza kikajiita RCD-Goma kikiongozwa na Kanali Emile Ilunga (hiki kilisaidiwa na Rwanda) na cha pili kikajiita RCD-Kisangani, kikiongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi (kikisaidiwa na Uganda). (Malisa GJ)
    Like
    2
    0 Reacties 0 aandelen 610 Views
  • #PART5
    Eneo la Kivu ni eneo la kimkakati sana na mabepari wote duniani wanalitolea macho kutokana na utajiri wake. Kivu ina madini ya Coltan ambayo yanatumika kutengeneza simu na laptop. 80% ya coltan yote duniani inatoka Congo (unaweza kugoogle kama huamini). Yani kwa kifupi bila Congo hakuna smartphones wala laptop duniani.

    Kivu pia kuna madini ya tin yanayotumika kutengenezea solder za kuchomelea vifaa vya kielektroniki kama radio, TV, simu, nk. Kuna madini ya Tungsten yanayotumika kutengenezea silaha. Na pia kuna Cobalt inayotumika kutengeneza betri mbalimbali zikiwemo za magari. Kama haitoshi Kivu kuna dhahabu nyingi mno. Eneo la Kivu ni eneo lenye dhahabu nyingi zaidi duniani ambayo bado haijachimbwa (The most unexplored gold site globally).

    Kagame aliona fursa. Wakati huo Rwanda ilikuwa imetoka kwenye vita na machafuko ya muda mrefu. Akataka rasilimali za jirani. Lakini atazipataje wakati yeye na Mobutu hawaelewani? Akakaamua kumuunga mkono mzee Laurent Kabila. Lakini akaweka masharti. Nikikusaidia kumng'oa Mobutu, eneo la Kivu Kusini, lenye Watutsi wengi (Banyamulenge), litajitenga na Congo na kuwa nchi inayojitegemea.

    Alishapiga hesabu za mbali za kuifanya Kivu kuwa sehemu ya Rwanda baada ya kujitenga DRC. Kabila akasema poa tu. Ashapigana miaka 30 msituni bila mafanikio? Sasa kapata "kamserereko" ka kwenda Ikulu akatae? Kagame nyuma yake walikuwepo Ufaransa na Uingereza akasema twende kwa maandishi. Mkataba ukasainiwa mji mdogo wa Lemera, Kivu Kusini. AFDL ikapewa support ya silaha na pesa, ikaamsha dude kupigana na majeshi ya serikali (FARDC).

    Wakati Mobutu anajaribu kupambana na AFDL, vikaibuka vikundi vingine vya waasi zaidi ya 40 kupigana na majeshi ya serikali. Vita ikiwa imepamba moto, Rwanda ikajitosa rasmi kupigana na serikali ya Mobutu kwa kisingizio cha kuwatafuta wanamgambo wa Intarahamwe waliokimbilia Congo. Uganda nayo ikaingiza jeshi kuwatafuta waasi wa LRA. Mobutu kaona "nini cha kufia" akadaka chopa akatokomea zake Moroco. Kesho yake tar.17 Mei 1997, Laurent Kabila akatangazwa Rais mpya wa Congo. Vita hii ikabatizwa jina vita vya kwanza vya Congo (1996-1997).
    (Malisa GJ)

    #PART5 Eneo la Kivu ni eneo la kimkakati sana na mabepari wote duniani wanalitolea macho kutokana na utajiri wake. Kivu ina madini ya Coltan ambayo yanatumika kutengeneza simu na laptop. 80% ya coltan yote duniani inatoka Congo (unaweza kugoogle kama huamini). Yani kwa kifupi bila Congo hakuna smartphones wala laptop duniani. Kivu pia kuna madini ya tin yanayotumika kutengenezea solder za kuchomelea vifaa vya kielektroniki kama radio, TV, simu, nk. Kuna madini ya Tungsten yanayotumika kutengenezea silaha. Na pia kuna Cobalt inayotumika kutengeneza betri mbalimbali zikiwemo za magari. Kama haitoshi Kivu kuna dhahabu nyingi mno. Eneo la Kivu ni eneo lenye dhahabu nyingi zaidi duniani ambayo bado haijachimbwa (The most unexplored gold site globally). Kagame aliona fursa. Wakati huo Rwanda ilikuwa imetoka kwenye vita na machafuko ya muda mrefu. Akataka rasilimali za jirani. Lakini atazipataje wakati yeye na Mobutu hawaelewani? Akakaamua kumuunga mkono mzee Laurent Kabila. Lakini akaweka masharti. Nikikusaidia kumng'oa Mobutu, eneo la Kivu Kusini, lenye Watutsi wengi (Banyamulenge), litajitenga na Congo na kuwa nchi inayojitegemea. Alishapiga hesabu za mbali za kuifanya Kivu kuwa sehemu ya Rwanda baada ya kujitenga DRC. Kabila akasema poa tu. Ashapigana miaka 30 msituni bila mafanikio? Sasa kapata "kamserereko" ka kwenda Ikulu akatae? Kagame nyuma yake walikuwepo Ufaransa na Uingereza akasema twende kwa maandishi. Mkataba ukasainiwa mji mdogo wa Lemera, Kivu Kusini. AFDL ikapewa support ya silaha na pesa, ikaamsha dude kupigana na majeshi ya serikali (FARDC). Wakati Mobutu anajaribu kupambana na AFDL, vikaibuka vikundi vingine vya waasi zaidi ya 40 kupigana na majeshi ya serikali. Vita ikiwa imepamba moto, Rwanda ikajitosa rasmi kupigana na serikali ya Mobutu kwa kisingizio cha kuwatafuta wanamgambo wa Intarahamwe waliokimbilia Congo. Uganda nayo ikaingiza jeshi kuwatafuta waasi wa LRA. Mobutu kaona "nini cha kufia" akadaka chopa akatokomea zake Moroco. Kesho yake tar.17 Mei 1997, Laurent Kabila akatangazwa Rais mpya wa Congo. Vita hii ikabatizwa jina vita vya kwanza vya Congo (1996-1997). (Malisa GJ)
    Like
    2
    1 Reacties 0 aandelen 707 Views
  • #PART3

    Baadhi ya wanajeshi wa Kitutsi hawakuridhika na ukandamizaji uliofanywa na Habyarimana. Wakajiorganize kupambana. Wakati huo Kagame akiwa askari wa NRA ya Uganda akimsaidia Museveni vita vya msituni. Mwaka 1983 hadi 1985 alienda kozi ya kijeshi TMA, Moduli. Alipohitimu akarudi Uganda kumsaidia Museveni vita vya msituni na hatimaye mwaka 1986 wakafanikiwa kuchukua nchi. NRA ikawa sehemu ya jeshi la Uganda kabla ya kubadilishwa muundo mwaka 1995 kuwa UPDF.

    Kagame akawa mkuu wa intelijensia ya jeshi. Baadae akaenda masomoni Marekani. Akiwa huko RPF ikaanzishwa na Jenerali Fredy Rwigyema kupambana na Serikali ya Habyarimana. Lakini Jenerali Rwigyema akauawa kwa guruneti akiwa uwanja wa vita. Kagame akalazimika kukatisha masomo na kurudi Rwanda kuongoza RPF akishirikiana na Alexis Kanyarwenge. Museveni akampa msaada wa fedha, silaha na chakula. RPF ikaweka kambi Uganda eneo la Kabale, Burundi eneo la Muyinga na Congo maeneo ya Kivu, Uvira na Goma.

    Mwaka 1994, askari wa RPF wakatungua ndege ya Rais Habyarimana ikiwa inakaribia kutua uwanja wa ndege wa Kigali ikitokea Dar es Salaam kwenye mazungumzo ya Amani alikuwa na Rais Cyprien Ntaramira wa Burundi. Wote wawili walikufa papo hapo.

    Kuuawa kwa Rais Habyarimana kuliamsha hasira za Wahutu na kusabisha mauaji ya Kimbari ambapo Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa kikatili kwa kucharangwa mapanga. Hali hiyo ilisababisha Watutsi wengi kukimbia nchi yao. Wapo waliokimbilia Tanzania, Uganda, lakini wengi zaidi walikimbilia eneo la Kivu.

    Kwa kifupi, idadi ya Watutsi eneo la Kivu iliongezeka siku hadi siku. Watutsi walioenda Kivu wengi hawakurudi Rwanda hata baada ya vita kumalizika. Ilikuwa vigumu kutofautisha Mtutsi mwenye asili ya Congo (Banyamulenge) na Mtutsi wa Rwanda, kwa sababu wote wanaongea lugha moja, mila na desturi moja.

    Kwahiyo hisia za Wakongomani kwamba Banyamulenge ni wageni zikaanza kupata nguvu kutokana na uhamiaji mkubwa wa Watutsi maeneo ya Kivu kaskazini na kusini. Wakati huo Congo ikiitwa Zaire Rais Mobutu Sese Seko alikataa kuwatambua Banyamulenge kama raia wake, na akazuia wasipewe vitambulisho vya taifa.
    (Malisa GJ)

    #PART3 Baadhi ya wanajeshi wa Kitutsi hawakuridhika na ukandamizaji uliofanywa na Habyarimana. Wakajiorganize kupambana. Wakati huo Kagame akiwa askari wa NRA ya Uganda akimsaidia Museveni vita vya msituni. Mwaka 1983 hadi 1985 alienda kozi ya kijeshi TMA, Moduli. Alipohitimu akarudi Uganda kumsaidia Museveni vita vya msituni na hatimaye mwaka 1986 wakafanikiwa kuchukua nchi. NRA ikawa sehemu ya jeshi la Uganda kabla ya kubadilishwa muundo mwaka 1995 kuwa UPDF. Kagame akawa mkuu wa intelijensia ya jeshi. Baadae akaenda masomoni Marekani. Akiwa huko RPF ikaanzishwa na Jenerali Fredy Rwigyema kupambana na Serikali ya Habyarimana. Lakini Jenerali Rwigyema akauawa kwa guruneti akiwa uwanja wa vita. Kagame akalazimika kukatisha masomo na kurudi Rwanda kuongoza RPF akishirikiana na Alexis Kanyarwenge. Museveni akampa msaada wa fedha, silaha na chakula. RPF ikaweka kambi Uganda eneo la Kabale, Burundi eneo la Muyinga na Congo maeneo ya Kivu, Uvira na Goma. Mwaka 1994, askari wa RPF wakatungua ndege ya Rais Habyarimana ikiwa inakaribia kutua uwanja wa ndege wa Kigali ikitokea Dar es Salaam kwenye mazungumzo ya Amani alikuwa na Rais Cyprien Ntaramira wa Burundi. Wote wawili walikufa papo hapo. Kuuawa kwa Rais Habyarimana kuliamsha hasira za Wahutu na kusabisha mauaji ya Kimbari ambapo Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa kikatili kwa kucharangwa mapanga. Hali hiyo ilisababisha Watutsi wengi kukimbia nchi yao. Wapo waliokimbilia Tanzania, Uganda, lakini wengi zaidi walikimbilia eneo la Kivu. Kwa kifupi, idadi ya Watutsi eneo la Kivu iliongezeka siku hadi siku. Watutsi walioenda Kivu wengi hawakurudi Rwanda hata baada ya vita kumalizika. Ilikuwa vigumu kutofautisha Mtutsi mwenye asili ya Congo (Banyamulenge) na Mtutsi wa Rwanda, kwa sababu wote wanaongea lugha moja, mila na desturi moja. Kwahiyo hisia za Wakongomani kwamba Banyamulenge ni wageni zikaanza kupata nguvu kutokana na uhamiaji mkubwa wa Watutsi maeneo ya Kivu kaskazini na kusini. Wakati huo Congo ikiitwa Zaire Rais Mobutu Sese Seko alikataa kuwatambua Banyamulenge kama raia wake, na akazuia wasipewe vitambulisho vya taifa. (Malisa GJ)
    Like
    1
    0 Reacties 0 aandelen 513 Views
  • Jeshi la Uganda (UPDF) limesema Wanajeshi wake walioko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , watatafuta mbinu ya kujiimarisha kiulinzi ili kuyazuwia makundi mengine ya Waasi kuingia mashariki mwa Taifa hilo.

    Hali inazidi kuwa tete mashariki mwa Kongo, huku Waasi wa kujndi la M23 wanaosemekana kuungwa mkono na Rwanda wakiendelea kuyadhibiti maeneo kadhaa ya eneo hilo ukiwemo Mji wa Goma, hali iliyoisababisha Uganda kupitia Jeshi lake kusema inataka kujipanga upya kiulinzi, katika eneo inayofanyia operesheni zake hadi mzozo huo wa DR Congo utakapotulia. Imesema nia yake ni kuyazuwia makundi mengine ya Waasi yasitumie mwanya wa vita kuingia mashariki mwa Taifa hilo. 

    Nchi ya Uganda ina jukumu muhimu katika kanda hiyo. Inafanya kazi pamoja na Wanajeshi wa Kongo katika mpango wa Operesheni Shujaa dhidi ya makundi yaliyo na itikadi kali kama Allied Democratic Forces, ADF, ambalo limekuwa likifungamanishwa na kundi la dola la kiislamu. Lakini kando na hayo, Uganda pia imekuwa ikishutumiwa na Wataalamu wa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine kwa kuwaunga mkono Waasi wa M23 kwa kuwaruhusu kutumia ardhi yake kupitisha silaha zake madai ambayo Uganda imeyakanusha vikali.

    Jeshi la Uganda 馃嚭馃嚞 (UPDF) limesema Wanajeshi wake walioko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 馃嚚馃嚛, watatafuta mbinu ya kujiimarisha kiulinzi ili kuyazuwia makundi mengine ya Waasi kuingia mashariki mwa Taifa hilo. Hali inazidi kuwa tete mashariki mwa Kongo, huku Waasi wa kujndi la M23 wanaosemekana kuungwa mkono na Rwanda 馃嚪馃嚰 wakiendelea kuyadhibiti maeneo kadhaa ya eneo hilo ukiwemo Mji wa Goma, hali iliyoisababisha Uganda kupitia Jeshi lake kusema inataka kujipanga upya kiulinzi, katika eneo inayofanyia operesheni zake hadi mzozo huo wa DR Congo utakapotulia. Imesema nia yake ni kuyazuwia makundi mengine ya Waasi yasitumie mwanya wa vita kuingia mashariki mwa Taifa hilo.  Nchi ya Uganda ina jukumu muhimu katika kanda hiyo. Inafanya kazi pamoja na Wanajeshi wa Kongo katika mpango wa Operesheni Shujaa dhidi ya makundi yaliyo na itikadi kali kama Allied Democratic Forces, ADF, ambalo limekuwa likifungamanishwa na kundi la dola la kiislamu. Lakini kando na hayo, Uganda pia imekuwa ikishutumiwa na Wataalamu wa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine kwa kuwaunga mkono Waasi wa M23 kwa kuwaruhusu kutumia ardhi yake kupitisha silaha zake madai ambayo Uganda imeyakanusha vikali.
    0 Reacties 0 aandelen 292 Views
  • Mkutano wa Kilele wa Marais wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika hivi karibuni umemtaka Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Félix Tshisekedi, kukaa meza moja na Waasi wa M23 kwa ajili ya mazungumzo ya pamoja ili kutafuta suluhu ya amani katika taifa hilo.

    Taarifa iliyotolewa na Mjumbe wa Mkutano huo, ambaye pia ni Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X (Twitter), ilieleza kuwa Viongozi hao walikutana Januari 29, chini ya Uenyekiti wa Rais wa Kenya, William Ruto, kujadili hali ya usalama Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo .

    Miongoni mwa makubaliano ya mkutano huo ni pendekezo la Rais Tshisekedi kushiriki mazungumzo na kundi la M23. Kadhalika, Viongozi hao walikubaliana kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inapaswa kuitisha mkutano wa dharura na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ili kutafuta suluhisho la kudumu kwa mgogoro huo.

    Museveni aliambatanisha taarifa hiyo na orodha ya Viongozi waliohudhuria mkutano huo, wakiwemo Rais wa Kenya William Ruto, Rais wa Somalia Hassan Mohamud, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, Rais wa Rwanda Paul Kagame, na mwenyeji wao, Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

    Mkutano wa Kilele wa Marais wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika hivi karibuni umemtaka Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Félix Tshisekedi, kukaa meza moja na Waasi wa M23 kwa ajili ya mazungumzo ya pamoja ili kutafuta suluhu ya amani katika taifa hilo. Taarifa iliyotolewa na Mjumbe wa Mkutano huo, ambaye pia ni Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X (Twitter), ilieleza kuwa Viongozi hao walikutana Januari 29, chini ya Uenyekiti wa Rais wa Kenya, William Ruto, kujadili hali ya usalama Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 馃嚚馃嚛. Miongoni mwa makubaliano ya mkutano huo ni pendekezo la Rais Tshisekedi kushiriki mazungumzo na kundi la M23. Kadhalika, Viongozi hao walikubaliana kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inapaswa kuitisha mkutano wa dharura na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ili kutafuta suluhisho la kudumu kwa mgogoro huo. Museveni aliambatanisha taarifa hiyo na orodha ya Viongozi waliohudhuria mkutano huo, wakiwemo Rais wa Kenya William Ruto, Rais wa Somalia Hassan Mohamud, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, Rais wa Rwanda Paul Kagame, na mwenyeji wao, Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
    Like
    1
    0 Reacties 0 aandelen 460 Views
  • Mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Victor Boniface, anayeichezea Bayer Leverkusen ya Ujerumani, ameachana na mpenzi wake, Rikke Hermine, raia wa Norway. Wawili hao walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa miaka minne, lakini wameamua kuvunja uhusiano wao kutokana na kugundua kuwa Victor kwenye mali zake ameandika majina ya mama yake tu.

    Chanzo cha habari kinaeleza kuwa uamuzi wa Rikke kuachana na Victor ulitokana na kugundua kuwa katika mali zote za mshambuliaji huyo, majina ya mama yake mzazi pekee ndiyo yaliyoandikwa. Hali hii ilimfanya Rikke kuhisi kuwa hakuwa na nafasi ya kutosha katika maisha ya Victor, jambo lililomfanya kuchukua hatua hiyo.

    Aidha, inadaiwa kuwa Rikke alikuwa akishinikiza kufunga ndoa baada ya kuwa wapenzi kwa muda mrefu, huku Victor akiwa tayari kufunga naye ndoa lakini kwa sharti la kusaini mkataba wa awali (prenup).

    Prenup ni Mkataba wa awali kabla ya kufunga ndoa ambao unalenga kulinda mali za pande zote mbili endapo itatokea mkaachana kila mmoja anabaki na alichokuja nacho katika ndoa na sio kugawana mali, ila bibie Rikkie amekuwa mgumu kukubali hilo hivyo kuachana

    #tanzania #kenya #daressalaam #africa #zanzibar #diamondplatnumz #arusha #mwanza #dodoma #uganda #wcb #travel #life #safari #wasafi #love #millardayoupdates #mbeya #nairobi #harmonize #rwanda #eastafrica #kilimanjaro #alikiba #gainwithmchina #serengeti #wasafitv #fashion #wasafimedia #wemasepetu
    Mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Victor Boniface, anayeichezea Bayer Leverkusen ya Ujerumani, ameachana na mpenzi wake, Rikke Hermine, raia wa Norway. Wawili hao walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa miaka minne, lakini wameamua kuvunja uhusiano wao kutokana na kugundua kuwa Victor kwenye mali zake ameandika majina ya mama yake tu. Chanzo cha habari kinaeleza kuwa uamuzi wa Rikke kuachana na Victor ulitokana na kugundua kuwa katika mali zote za mshambuliaji huyo, majina ya mama yake mzazi pekee ndiyo yaliyoandikwa. Hali hii ilimfanya Rikke kuhisi kuwa hakuwa na nafasi ya kutosha katika maisha ya Victor, jambo lililomfanya kuchukua hatua hiyo. Aidha, inadaiwa kuwa Rikke alikuwa akishinikiza kufunga ndoa baada ya kuwa wapenzi kwa muda mrefu, huku Victor akiwa tayari kufunga naye ndoa lakini kwa sharti la kusaini mkataba wa awali (prenup). Prenup ni Mkataba wa awali kabla ya kufunga ndoa ambao unalenga kulinda mali za pande zote mbili endapo itatokea mkaachana kila mmoja anabaki na alichokuja nacho katika ndoa na sio kugawana mali, ila bibie Rikkie amekuwa mgumu kukubali hilo hivyo kuachana #tanzania #kenya #daressalaam #africa #zanzibar #diamondplatnumz #arusha #mwanza #dodoma #uganda #wcb #travel #life #safari #wasafi #love #millardayoupdates #mbeya #nairobi #harmonize #rwanda #eastafrica #kilimanjaro #alikiba #gainwithmchina #serengeti #wasafitv #fashion #wasafimedia #wemasepetu
    Like
    1
    0 Reacties 0 aandelen 2K Views
  • #JeWajua Msako mkali wa wahamiaji uliofanyika nchini Marekani siku ya Jumapili na kusababisha kukamatwa kwa watu 956, idadi hiyo ikiwa kubwa zaidi tangu Donald Trump arejee mamlakani, kulingana na shirika la Uhamiaji na Utekelezaji wa Forodha (ICE).

    Mashirika kadhaa ya serikali yenye mamlaka mapya ya kuwaweka kizuizini wasio na vibali yalihusika katika kamata kamata hiyo kwenye miji kadhaa ikiwa ni pamoja na Chicago, Newark na Miami. Moja ya ahadi alizotoa Donald Trump wakati wa kampeni yake, ni kuwafukuza nchi Marekani wahamiaji wasio na vibali.

    Mtangulizi wake Joe Biden aliwarejesha makwao wastani wa wahamiaji 311 kila siku, kulingana na ICE, wengi wao wakiwa watu ambao walikuwa wamefanya uhalifu. Tangu aingie madarakani, Trump ametekeleza maagizo 21 kurekebisha mfumo wa uhamiaji wa Marekani.

    Huko Miami siku ya Jumapili, vyombo vya kutekeleza sheria vya serikali vilichukua "hatua kadhaa za uhamiaji," Uchunguzi wa Usalama wa jiji hilo ulisema kwenye mitandao ya kijamii.

    #tanzania #kenya #daressalaam #africa #zanzibar #diamondplatnumz #arusha #mwanza #dodoma #uganda #wcb #travel #life #safari #wasafi #love #millardayoupdates #mbeya #nairobi #harmonize #rwanda #eastafrica #kilimanjaro #alikiba #gainwithmchina #serengeti #wasafitv #fashion #wasafimedia
    #JeWajua Msako mkali wa wahamiaji uliofanyika nchini Marekani siku ya Jumapili na kusababisha kukamatwa kwa watu 956, idadi hiyo ikiwa kubwa zaidi tangu Donald Trump arejee mamlakani, kulingana na shirika la Uhamiaji na Utekelezaji wa Forodha (ICE). Mashirika kadhaa ya serikali yenye mamlaka mapya ya kuwaweka kizuizini wasio na vibali yalihusika katika kamata kamata hiyo kwenye miji kadhaa ikiwa ni pamoja na Chicago, Newark na Miami. Moja ya ahadi alizotoa Donald Trump wakati wa kampeni yake, ni kuwafukuza nchi Marekani wahamiaji wasio na vibali. Mtangulizi wake Joe Biden aliwarejesha makwao wastani wa wahamiaji 311 kila siku, kulingana na ICE, wengi wao wakiwa watu ambao walikuwa wamefanya uhalifu. Tangu aingie madarakani, Trump ametekeleza maagizo 21 kurekebisha mfumo wa uhamiaji wa Marekani. Huko Miami siku ya Jumapili, vyombo vya kutekeleza sheria vya serikali vilichukua "hatua kadhaa za uhamiaji," Uchunguzi wa Usalama wa jiji hilo ulisema kwenye mitandao ya kijamii. #tanzania #kenya #daressalaam #africa #zanzibar #diamondplatnumz #arusha #mwanza #dodoma #uganda #wcb #travel #life #safari #wasafi #love #millardayoupdates #mbeya #nairobi #harmonize #rwanda #eastafrica #kilimanjaro #alikiba #gainwithmchina #serengeti #wasafitv #fashion #wasafimedia
    Like
    1
    0 Reacties 0 aandelen 2K Views
  • ...||TANZANIA NJIA NYEUPE KWENYE KUNDI C AFCON 2025.

    Haya hapa Makundi yote ya Afcon 2025,

    KUNDI A
    Morocco
    Comoros
    Zambia
    Mali

    KUNDI B
    Zimbabwe
    Angola
    South Africa
    Egypt

    KUNDI C
    Tanzania
    Uganda
    Tunisia
    Nigeria

    KUNDI D
    Botswana
    Benin
    Dr Congo
    Senegal

    KUNDI E
    Sudan
    Equatorial Guinea
    Burkina Faso
    Algeria

    KUNDI F
    Cameroon
    Mozambique
    Gabon
    Cotê D'Ivoire 馃嚚馃嚠

    Kila la kheri Tanzania
    馃毃...||TANZANIA 馃嚬馃嚳 NJIA NYEUPE KWENYE KUNDI C AFCON 2025. 馃拵Haya hapa Makundi yote ya Afcon 2025, KUNDI A Morocco馃嚥馃嚘 Comoros馃嚢馃嚥 Zambia馃嚳馃嚥 Mali馃嚥馃嚤 KUNDI B Zimbabwe 馃嚳馃嚰 Angola馃嚘馃嚧 South Africa馃嚳馃嚘 Egypt馃嚜馃嚞 KUNDI C Tanzania馃嚬馃嚳 Uganda馃嚭馃嚞 Tunisia馃嚬馃嚦 Nigeria馃嚦馃嚞 KUNDI D Botswana馃嚙馃嚰 Benin馃嚙馃嚡 Dr Congo馃嚚馃嚛 Senegal馃嚫馃嚦 KUNDI E Sudan馃嚫馃嚫 Equatorial Guinea馃嚞馃嚩 Burkina Faso馃嚙馃嚝 Algeria馃嚛馃嚳 KUNDI F Cameroon馃嚚馃嚥 Mozambique馃嚥馃嚳 Gabon馃嚞馃嚘 Cotê D'Ivoire 馃嚚馃嚠 馃拵Kila la kheri Tanzania 馃嚬馃嚳馃嚬馃嚳馃檹馃憡馃挭馃挋馃馃枻
    Like
    1
    0 Reacties 0 aandelen 437 Views
  • GROUP A
    Morocco
    Mali
    Zambia
    Comoros

    GROUP B
    Egypt
    South Africa
    Angola
    Zimbabwe

    GROUP C
    Nigeria
    Tunisia
    Uganda
    Tanzania


    GROUP D
    Senegal
    DR Congo
    Benin Republic
    Botswana


    GROUP E
    Algeria
    Burkina Faso
    Equatorial Guinea
    Sudan


    GROUP F
    Ivory Coast 馃嚚馃嚠
    Cameroon
    Gabon
    Mozambique

    #AFCON2025
    GROUP A Morocco 馃嚥馃嚘 Mali 馃嚥馃嚤 Zambia 馃嚳馃嚥 Comoros 馃嚢馃嚥 GROUP B Egypt 馃嚜馃嚞 South Africa 馃嚳馃嚘 Angola 馃嚘馃嚧 Zimbabwe 馃嚳馃嚰 GROUP C Nigeria 馃嚦馃嚞 Tunisia 馃嚬馃嚦 Uganda 馃嚭馃嚞 Tanzania 馃嚬馃嚳 GROUP D Senegal 馃嚫馃嚦 DR Congo 馃嚚馃嚛 Benin Republic 馃嚙馃嚡 Botswana 馃嚙馃嚰 GROUP E Algeria 馃嚛馃嚳 Burkina Faso 馃嚙馃嚝 Equatorial Guinea 馃嚞馃嚩 Sudan 馃嚫馃嚛 GROUP F Ivory Coast 馃嚚馃嚠 Cameroon 馃嚚馃嚥 Gabon 馃嚞馃嚘 Mozambique 馃嚥馃嚳 #AFCON2025
    Like
    Love
    5
    0 Reacties 0 aandelen 516 Views
  • AFCON Kundi C
    Nigeria
    Tunisia
    Uganda
    Tanzania
    AFCON Kundi C Nigeria馃嚦馃嚞 Tunisia 馃嚬馃嚦 Uganda馃嚭馃嚞 Tanzania馃嚬馃嚳
    Like
    1
    0 Reacties 0 aandelen 201 Views
Zoekresultaten