• AYRA STARR AANDIKA HISTORIA KWENYE YOUTUBE KUPITIA WIMBO WAKE “RUSH”.

    Nyota wa muziki kutoka Nigeria, Ayra Starr, ameweka rekodi ya kipekee na kuandika jina lake kwenye vitabu vya historia ya burudani barani Afrika. Kupitia wimbo wake maarufu Rush, Ayra Starr amekuwa Msanii wa kwanza wa kike barani Afrika kufikisha zaidi ya Watazamaji milioni 500 kwenye mtandao wa YouTube kwa wimbo mmoja wa solo.

    Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Ayra alishiriki furaha yake kwa mafanikio hayo na kusema:

    “Sauti ya Gen-Z kutoka Afrika inasikika! Rush imefanya historia, na hii ni mwanzo tu.”

    Kwa mafanikio haya, Rush imejiunga na orodha ya video tano bora za muziki za Kiafrika zilizotazamwa zaidi kila wakati kwenye YouTube.

    - Calm Down : Rema
    - Jerusalema : Master KG ft. Nomcebo Zikode
    - Love Nwantiti : CKay
    - Magic In The Air : Magic System

    Kinachovutia zaidi ni kwamba, licha ya umaarufu wa Wasanii kama Burna Boy, Wizkid, Davido, pamoja na wakali wa kimataifa kama NBA YoungBoy, Polo G, Lil Tjay, NLE Choppa, na Lil Durk, hakuna hata mmoja wao ambaye amewahi kufikisha Watazamaji zaidi ya milioni 500 kwa wimbo mmoja wa solo kwenye jukwaa la YouTube tofauti na Ayra Starr.

    Rekodi hii inaendelea kuimarisha nafasi ya Ayra Starr kama sauti muhimu ya kizazi kipya cha muziki barani Afrika, hasa kwa kizazi cha Gen-Z, na kuonyesha ukuaji wa ushawishi wa Wanawake kwenye tasnia ya muziki wa kimataifa.

    “Rush is not just a song, it’s a movement.” - Ayra Starr

    Pongezi kwa Ayra kwa kuwakilisha Afrika kwa kishindo duniani!
    AYRA STARR AANDIKA HISTORIA KWENYE YOUTUBE KUPITIA WIMBO WAKE “RUSH”. Nyota wa muziki kutoka Nigeria, Ayra Starr, ameweka rekodi ya kipekee na kuandika jina lake kwenye vitabu vya historia ya burudani barani Afrika. Kupitia wimbo wake maarufu Rush, Ayra Starr amekuwa Msanii wa kwanza wa kike barani Afrika kufikisha zaidi ya Watazamaji milioni 500 kwenye mtandao wa YouTube kwa wimbo mmoja wa solo. Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Ayra alishiriki furaha yake kwa mafanikio hayo na kusema: “Sauti ya Gen-Z kutoka Afrika inasikika! Rush imefanya historia, na hii ni mwanzo tu.” Kwa mafanikio haya, Rush imejiunga na orodha ya video tano bora za muziki za Kiafrika zilizotazamwa zaidi kila wakati kwenye YouTube. - Calm Down : Rema - Jerusalema : Master KG ft. Nomcebo Zikode - Love Nwantiti : CKay - Magic In The Air : Magic System Kinachovutia zaidi ni kwamba, licha ya umaarufu wa Wasanii kama Burna Boy, Wizkid, Davido, pamoja na wakali wa kimataifa kama NBA YoungBoy, Polo G, Lil Tjay, NLE Choppa, na Lil Durk, hakuna hata mmoja wao ambaye amewahi kufikisha Watazamaji zaidi ya milioni 500 kwa wimbo mmoja wa solo kwenye jukwaa la YouTube tofauti na Ayra Starr. Rekodi hii inaendelea kuimarisha nafasi ya Ayra Starr kama sauti muhimu ya kizazi kipya cha muziki barani Afrika, hasa kwa kizazi cha Gen-Z, na kuonyesha ukuaji wa ushawishi wa Wanawake kwenye tasnia ya muziki wa kimataifa. “Rush is not just a song, it’s a movement.” - Ayra Starr Pongezi kwa Ayra kwa kuwakilisha Afrika kwa kishindo duniani!
    0 Comments 0 Shares 1K Views
  • Vurugu mitandaoni! Ned Nwoko amvaa Regina Daniels, asema "ameharibu familia yetu".

    Mitandao ya kijamii imewaka moto kufuatia tuhuma nzito zilizotolewa na Bilionea na mwanasiasa mashuhuri kutoka Nigeria, Prince Ned Nwoko, dhidi ya Mke wake, Mwigizaji maarufu wa filamu za Nigeria (Nollywood) Regina Daniels. Kupitia chapisho la video kwenye ukurasa wake wa Instagram, Nwoko amemshutumu Regina kwa kile alichokiita "vurugu za kupindukia" pamoja na matumizi mabaya ya dawa za kulevya na pombe.

    Katika maneno yake, Ned aliandika: “Hakuwa hivi mwanzo… kile kinachotokea sasa kimeharibu kabisa utulivu wa familia yetu.”

    Nwoko alieleza kuwa ndani ya saa 48, Regina alifanya fujo kubwa nyumbani kwao akiwapiga Wafanyakazi watatu wa ndani, kuharibu mali, na kusababisha uharibifu mkubwa bila sababu ya msingi.

    Kwa mujibu wa chapisho hilo la Instagram: “Nimetoa masharti ya wazi kwake. Lazima akubali kwenda kwenye tiba ya kuacha dawa, iwe ndani au nje ya Nchi. Vinginevyo, naogopa kwa usalama wake.” - Prince Ned Nwoko.

    Katika tuhuma hizo, Ned alimtaja mtu aitwaye Sammy kama Muuzaji mkuu wa dawa kwa Regina, huku pia akilitaja jina la Ann, akisema anahusika katika kile alichokiita “mzunguko wa maovu.”

    Tukio hili limetikisa jamii ya mtandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakionesha mshangao, wengine wakimtetea Regina, na wengi wakitaka ukweli wa kina juu ya maisha ya kifahari ya wawili hao.

    Je, hii ni drama ya ndoa ya Mastaa au kuna jambo kubwa zaidi nyuma ya pazia?
    Vurugu mitandaoni! Ned Nwoko amvaa Regina Daniels, asema "ameharibu familia yetu". Mitandao ya kijamii imewaka moto kufuatia tuhuma nzito zilizotolewa na Bilionea na mwanasiasa mashuhuri kutoka Nigeria, Prince Ned Nwoko, dhidi ya Mke wake, Mwigizaji maarufu wa filamu za Nigeria (Nollywood) Regina Daniels. Kupitia chapisho la video kwenye ukurasa wake wa Instagram, Nwoko amemshutumu Regina kwa kile alichokiita "vurugu za kupindukia" pamoja na matumizi mabaya ya dawa za kulevya na pombe. Katika maneno yake, Ned aliandika: “Hakuwa hivi mwanzo… kile kinachotokea sasa kimeharibu kabisa utulivu wa familia yetu.” Nwoko alieleza kuwa ndani ya saa 48, Regina alifanya fujo kubwa nyumbani kwao akiwapiga Wafanyakazi watatu wa ndani, kuharibu mali, na kusababisha uharibifu mkubwa bila sababu ya msingi. Kwa mujibu wa chapisho hilo la Instagram: “Nimetoa masharti ya wazi kwake. Lazima akubali kwenda kwenye tiba ya kuacha dawa, iwe ndani au nje ya Nchi. Vinginevyo, naogopa kwa usalama wake.” - Prince Ned Nwoko. Katika tuhuma hizo, Ned alimtaja mtu aitwaye Sammy kama Muuzaji mkuu wa dawa kwa Regina, huku pia akilitaja jina la Ann, akisema anahusika katika kile alichokiita “mzunguko wa maovu.” Tukio hili limetikisa jamii ya mtandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakionesha mshangao, wengine wakimtetea Regina, na wengi wakitaka ukweli wa kina juu ya maisha ya kifahari ya wawili hao. Je, hii ni drama ya ndoa ya Mastaa au kuna jambo kubwa zaidi nyuma ya pazia?
    0 Comments 0 Shares 1K Views
  • Meneja wa Paris Saint Germain, Luis Enrique ameweka wazi kuwa Uongozi wa klabu hiyo unamuunga mkono kwenye uamuzi wake wa kuachana na Golikipa Gianluigi Donnarumma kutokuwa sehemu ya kikosi cha Timu hiyo hivyo ataanza kwa kuukosa mchezo wa UEFA Super Cup.

    Kipa huyo raia wa Italia aliachwa nje ya kikosi kilichosafiri hadi Udine kwa mechi ya kirafiki leo dhidi ya Tottenham, huku Magolikipa Lucas Chevalier na Renato Marin wakichaguliwa badala yake.

    Katika chapisho lake kwenye mtandao wake wa Instagram, Donnarumma alisema "amesikitishwa na kuvunjika moyo" kwa kukosekana kwake.
    Nyota huyo alikuwa mmoja wa wachezaji wa PSG walioshinda taji la Ligi ya Mabingwa msimu uliopita na uamuzi huo umekuja kwa mshtuko kutokana na hadhi yake na wasifu wake.

    Enrique alisema uamuzi wake ulikuwa na lengo la kutafuta Golikipa mwenye "wasifu tofauti" na Gigi.

    "Uongozi unaniunga mkono na tunajaribu kutafuta suluhu bora," aliongea kwenye mkutano wa wanahabari Jumanne.

    "Ni uamuzi mgumu, namkubali Donnarumma kwani ni mmoja wa makipa bora na mtu bora zaidi. Lakini tulikuwa tunatafuta wasifu tofauti, na ni vigumu sana kuchukua maamuzi ya aina hii." - alimaliza kwa kusema hivyo.

    #SportsElite
    🚨🚨Meneja wa Paris Saint Germain, Luis Enrique ameweka wazi kuwa Uongozi wa klabu hiyo unamuunga mkono kwenye uamuzi wake wa kuachana na Golikipa Gianluigi Donnarumma kutokuwa sehemu ya kikosi cha Timu hiyo hivyo ataanza kwa kuukosa mchezo wa UEFA Super Cup. Kipa huyo raia wa Italia aliachwa nje ya kikosi kilichosafiri hadi Udine kwa mechi ya kirafiki leo dhidi ya Tottenham, huku Magolikipa Lucas Chevalier na Renato Marin wakichaguliwa badala yake. Katika chapisho lake kwenye mtandao wake wa Instagram, Donnarumma alisema "amesikitishwa na kuvunjika moyo" kwa kukosekana kwake. Nyota huyo alikuwa mmoja wa wachezaji wa PSG walioshinda taji la Ligi ya Mabingwa msimu uliopita na uamuzi huo umekuja kwa mshtuko kutokana na hadhi yake na wasifu wake. Enrique alisema uamuzi wake ulikuwa na lengo la kutafuta Golikipa mwenye "wasifu tofauti" na Gigi. "Uongozi unaniunga mkono na tunajaribu kutafuta suluhu bora," aliongea kwenye mkutano wa wanahabari Jumanne. "Ni uamuzi mgumu, namkubali Donnarumma kwani ni mmoja wa makipa bora na mtu bora zaidi. Lakini tulikuwa tunatafuta wasifu tofauti, na ni vigumu sana kuchukua maamuzi ya aina hii." - alimaliza kwa kusema hivyo. #SportsElite
    0 Comments 0 Shares 1K Views
  • #SportsElite

    - Baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu, hatimaye mshambuliaji hatari wa klabu ya Inter Miami pamoja Nahodha wa timu ya Taifa ya Argentina, Leo Messi.. kupitia katika Ukurasa wake wa Instagram (@leomessi) ‘FIFA BOY’ ame-share picha ya Diogo Jota, ikiwa ni ishara ya KUGUSWA moja kwa moja na msiba huu mzito katika soka. Kudos Legend..!
    .
    .
    - Hakika kwa kuondokewa na mtu kama Diogo Jota, itoshe kusema familia ya mpira tumepata pigo kubwa haswa! 🥹!
    .
    .

    …Endelea kupumzika, Diogo Jota. 🕊
    #SportsElite - Baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu, hatimaye mshambuliaji hatari wa klabu ya Inter Miami pamoja Nahodha wa timu ya Taifa ya Argentina, Leo Messi.. kupitia katika Ukurasa wake wa Instagram (@leomessi) ‘FIFA BOY’ ame-share picha ya Diogo Jota, ikiwa ni ishara ya KUGUSWA moja kwa moja na msiba huu mzito katika soka. Kudos Legend..! 🤝 . . - Hakika kwa kuondokewa na mtu kama Diogo Jota, itoshe kusema familia ya mpira tumepata pigo kubwa haswa! 🥹! . . …Endelea kupumzika, Diogo Jota. 🕊
    0 Comments 0 Shares 1K Views
  • Klabu ya Al Masri ya Misri imesasisha picha hiyo kwenye ukurasa wao wa Instagram na kusema kuwa wamefutahia kukutana na Mashabiki wa klabu ya Yanga SC.

    Ukiangalia chapisho hili la klabu ya Al Masry, utagudua kuwa klabu hiyo wanafuatilia mpira wa Tanzania na wanajua mpinzani wa klabu ya Simba SC ni Yanga SC. Pia wanajua kua Mashabiki wa Yanga watakua Uwanjani kuwashangilia.

    Klabu ya Al Masri ya Misri 🇪🇬 imesasisha picha hiyo kwenye ukurasa wao wa Instagram na kusema kuwa wamefutahia kukutana na Mashabiki wa klabu ya Yanga SC. Ukiangalia chapisho hili la klabu ya Al Masry, utagudua kuwa klabu hiyo wanafuatilia mpira wa Tanzania na wanajua mpinzani wa klabu ya Simba SC ni Yanga SC. Pia wanajua kua Mashabiki wa Yanga watakua Uwanjani kuwashangilia.
    0 Comments 0 Shares 1K Views
  • Mke wa Mchezaji wa kimataifa wa Burkina Faso n'a klabu ya Yanga SC, Hamisa Mobetto (Tanzania ) ameingia kwenye orodha ya WAGS (Wives And Girlfriends of Footballers) ambao ni Wake (Wapenzi au Wachumba) wa Wachezaji wenye Wafuasi (followers) wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram Duniani.

    1. @georginagio (Mrs. Ronaldo) :+65.5M
    2. antonelaroccuzzo (Mrs. Messi) : +39.9M
    3. @iambeckyg (Mrs. Sebastian) : +37.2M
    4. @victoriabeckham (Mrs. Beckham) : +32.9M
    5. @perrieedwards (Mrs. Alex) :+19M

    6. @alishalehmann7 (Mrs. Douglas Luiz) : +16.6M
    7. @brunabiancardi (Mrs. Neymar Jr) : +13.6M
    8. @hamisamobetto (Mrs. Aziz Ki) : +12.1M
    9. @pilarrubio (Mrs. Sergio Ramos) : +11.1M
    10. @leighannepinnock (Mrs. Andre Gray) : +10M

    Mke wa Mchezaji wa kimataifa wa Burkina Faso 🇧🇫 n'a klabu ya Yanga SC, Hamisa Mobetto (Tanzania 🇹🇿) ameingia kwenye orodha ya WAGS (Wives And Girlfriends of Footballers) ambao ni Wake (Wapenzi au Wachumba) wa Wachezaji wenye Wafuasi (followers) wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram Duniani. 1. @georginagio (Mrs. Ronaldo) :+65.5M 2. antonelaroccuzzo (Mrs. Messi) : +39.9M 3. @iambeckyg (Mrs. Sebastian) : +37.2M 4. @victoriabeckham (Mrs. Beckham) : +32.9M 5. @perrieedwards (Mrs. Alex) :+19M 6. @alishalehmann7 (Mrs. Douglas Luiz) : +16.6M 7. @brunabiancardi (Mrs. Neymar Jr) : +13.6M 8. @hamisamobetto (Mrs. Aziz Ki) : +12.1M 9. @pilarrubio (Mrs. Sergio Ramos) : +11.1M 10. @leighannepinnock (Mrs. Andre Gray) : +10M
    0 Comments 0 Shares 2K Views
  • Klabu ya Kengold inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, imeiandikia barua redio ya FURAHA FM kupitia kwa Mwanasheria wake Nicky Ngale wakidai fidia ya Shilingi Billion moja na kuombwa radhi kupitia mitandao ya Kijamii baada ya Radio hiyo kupitia mtandao wake wa Kijamii wa Instagram kuchapisha taarifa kuwa:

    “Kengold yaomba alama 15 atakazokatwa Simba na TFF, wapewe wao alama tatu”

    Kufuatia kuchapisha chapisho hilo, Mwanasheria anadai Mteja wake ameathirika kwa kiasi kikubwa huku jina lao likichafuka kwa kiasi kikubwa, nje na hapo matakwa yao yote yanapaswa kutimizwa ndani ya siku saba (7).

    Klabu ya Kengold inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, imeiandikia barua redio ya FURAHA FM kupitia kwa Mwanasheria wake Nicky Ngale wakidai fidia ya Shilingi Billion moja na kuombwa radhi kupitia mitandao ya Kijamii baada ya Radio hiyo kupitia mtandao wake wa Kijamii wa Instagram kuchapisha taarifa kuwa: “Kengold yaomba alama 15 atakazokatwa Simba na TFF, wapewe wao alama tatu” Kufuatia kuchapisha chapisho hilo, Mwanasheria anadai Mteja wake ameathirika kwa kiasi kikubwa huku jina lao likichafuka kwa kiasi kikubwa, nje na hapo matakwa yao yote yanapaswa kutimizwa ndani ya siku saba (7).
    0 Comments 0 Shares 1K Views
  • MADHARA YA KUVUTA SIGARA NA TIBA YAKE
    ✦Magonjwa ya macho
    ✦Kukunjana kwa ngozi
    ✦Magonjwa ya masikio
    ✦Saratani ya ngozi
    ✦Magonjwa ya meno
    ✦Magonjwa ya mapafu,Mifupa,Kucha kungoka kwenye vidole na miguu.
    ✦Magonjwa ya ngozi.

    𝐈𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐰𝐞𝐰𝐞 𝐧𝐢 𝐦𝐮𝐡𝐚𝐧𝐠𝐚 𝐰𝐚 𝐭𝐚𝐭𝐢𝐳𝐨 𝐡𝐢𝐥𝐨 𝐥𝐚 𝐬𝐢𝐠𝐚𝐫𝐚 𝐧𝐚 𝐡𝐚𝐭𝐚 𝐩𝐞𝐦𝐛𝐞,𝐓𝐰𝐚𝐢𝐛 𝐇𝐞𝐫𝐛𝐬 𝐭𝐮𝐧𝐚 𝐬𝐮𝐥𝐮𝐡𝐢𝐬𝐡𝐨 𝐢𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐮𝐧𝐚𝐡𝐢𝐭𝐚𝐣𝐢 𝐤𝐮𝐚𝐜𝐡𝐚 𝐮𝐯𝐮𝐭𝐚𝐣𝐢 𝐰𝐚 𝐚𝐢𝐧𝐚 𝐲𝐨𝐲𝐨𝐭𝐞 𝐧𝐚 𝐩𝐨𝐦𝐛𝐞.

    #𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈𝐀𝐍𝐀_𝐍𝐀𝐒𝐈
    ✦WHATSAP BUSSNESS CATALOGUE
    https://wa.me/c/255767607724

    ✦Instagram:
    https://www.instagram.com/twaibherbs

    ✦Facebook:
    https://www.facebook.com/twaibherbs

    ✦Google/blog.
    https://www.twaibherbs.blogspot.com
    MADHARA YA KUVUTA SIGARA NA TIBA YAKE ✦Magonjwa ya macho ✦Kukunjana kwa ngozi ✦Magonjwa ya masikio ✦Saratani ya ngozi ✦Magonjwa ya meno ✦Magonjwa ya mapafu,Mifupa,Kucha kungoka kwenye vidole na miguu. ✦Magonjwa ya ngozi. 𝐈𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐰𝐞𝐰𝐞 𝐧𝐢 𝐦𝐮𝐡𝐚𝐧𝐠𝐚 𝐰𝐚 𝐭𝐚𝐭𝐢𝐳𝐨 𝐡𝐢𝐥𝐨 𝐥𝐚 𝐬𝐢𝐠𝐚𝐫𝐚 𝐧𝐚 𝐡𝐚𝐭𝐚 𝐩𝐞𝐦𝐛𝐞,𝐓𝐰𝐚𝐢𝐛 𝐇𝐞𝐫𝐛𝐬 𝐭𝐮𝐧𝐚 𝐬𝐮𝐥𝐮𝐡𝐢𝐬𝐡𝐨 𝐢𝐤𝐢𝐰𝐚 𝐮𝐧𝐚𝐡𝐢𝐭𝐚𝐣𝐢 𝐤𝐮𝐚𝐜𝐡𝐚 𝐮𝐯𝐮𝐭𝐚𝐣𝐢 𝐰𝐚 𝐚𝐢𝐧𝐚 𝐲𝐨𝐲𝐨𝐭𝐞 𝐧𝐚 𝐩𝐨𝐦𝐛𝐞. #𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈𝐀𝐍𝐀_𝐍𝐀𝐒𝐈 ✦WHATSAP BUSSNESS CATALOGUE https://wa.me/c/255767607724 ✦Instagram: https://www.instagram.com/twaibherbs ✦Facebook: https://www.facebook.com/twaibherbs ✦Google/blog. https://www.twaibherbs.blogspot.com
    Love
    1
    0 Comments 0 Shares 2K Views
  • Mtandao wa Threads unaomilikiwa na META (Facebook, Instagram, WhatsApp, ...) ambao ni mshindani wa X(Twitter) umefanya mabadiliko kwenye Wasifu (profile) wa Watumiaji wake. Kwa sasa Threads imefika Watumiaji zaidi ya milioni (300) kwa mwezi.

    Threads imeongeza "tab" mpya ya “Media” ambayo itakuwa ni maalum kwa kuona picha na video ambazo zimepostiwa na akaunti. Pia Threas imeanza kuweka mfumo wa matangazo kwa baadhi ya Watumiaji na mabadiliko haya yameanza kwa Watumiaji wa Nchini Marekani na Japan .

    Mtandao wa Threads unaomilikiwa na META (Facebook, Instagram, WhatsApp, ...) ambao ni mshindani wa X(Twitter) umefanya mabadiliko kwenye Wasifu (profile) wa Watumiaji wake. Kwa sasa Threads imefika Watumiaji zaidi ya milioni (300) kwa mwezi. Threads imeongeza "tab" mpya ya “Media” ambayo itakuwa ni maalum kwa kuona picha na video ambazo zimepostiwa na akaunti. Pia Threas imeanza kuweka mfumo wa matangazo kwa baadhi ya Watumiaji na mabadiliko haya yameanza kwa Watumiaji wa Nchini Marekani 🇺🇸 na Japan 🇯🇵.
    Like
    2
    0 Comments 0 Shares 1K Views
  • Chukua hii

    Toleo jipya la mtandao wa WhatsApp ya iOS toleo la 25.1.10.73 imeanza kuweka sehemu ya kuchagua miziki katika sehemu ya WhatsApp Status. Mabadiliko haya yameanza kama sehemu ya majaribio na tayari Watumiaji wa mfumo wa Android toleo la 2.25.2.5 kuna majaribio haya.

    WhatsApp bado inafanya majaribio ya kuweka mfumo wa kuweka miziki katika WhatsApp Status kama vile ilivyo katika Instagram Stories na Facebook Stories. Watumiaji wataweza kutafuta miziki na kuiweka katika sehemu ya Status.

    Chukua hii Toleo jipya la mtandao wa WhatsApp ya iOS toleo la 25.1.10.73 imeanza kuweka sehemu ya kuchagua miziki katika sehemu ya WhatsApp Status. Mabadiliko haya yameanza kama sehemu ya majaribio na tayari Watumiaji wa mfumo wa Android toleo la 2.25.2.5 kuna majaribio haya. WhatsApp bado inafanya majaribio ya kuweka mfumo wa kuweka miziki katika WhatsApp Status kama vile ilivyo katika Instagram Stories na Facebook Stories. Watumiaji wataweza kutafuta miziki na kuiweka katika sehemu ya Status.
    Like
    Love
    3
    0 Comments 0 Shares 909 Views
  • Chukua hii

    Mtandao wa WhatsApp utaanza kuruhusu kusasisha (kuposti) "Status" zako moja kwa moja kama "Stories" za Facebook au Instagram. Muunganiko huu unatarajiwa kuanza kutumika katika miezi ijayo ambapo WhatsApp itaruhusu Watumiaji wake ambao wameunganisha akaunti zao za WhatsApp kwenye Instagram na Facebook kupata urahisi wa kuweka "Status" zao ambazo wanaziweka kwenye WhatsApp "Status" zitaenda kwenye Instagram "Stories" na Facebook "stories" moja kwa moja.

    Mabadiliko haya yameanza taratibu hivi karibuni na Mtandao huo wa WhatsApp utabadili kwa Watumiaji wote Duniani.

    Chukua hii Mtandao wa WhatsApp utaanza kuruhusu kusasisha (kuposti) "Status" zako moja kwa moja kama "Stories" za Facebook au Instagram. Muunganiko huu unatarajiwa kuanza kutumika katika miezi ijayo ambapo WhatsApp itaruhusu Watumiaji wake ambao wameunganisha akaunti zao za WhatsApp kwenye Instagram na Facebook kupata urahisi wa kuweka "Status" zao ambazo wanaziweka kwenye WhatsApp "Status" zitaenda kwenye Instagram "Stories" na Facebook "stories" moja kwa moja. Mabadiliko haya yameanza taratibu hivi karibuni na Mtandao huo wa WhatsApp utabadili kwa Watumiaji wote Duniani.
    Like
    Love
    2
    0 Comments 0 Shares 986 Views
  • PATA BLUETICK YAKO KWA TSHS 1,300 TU KATIKA INSTAGRAM NA FACEBOOK!

    Kampuni ya Meta inayosimamia Mtandao wa Instagram, Facebook na WhatsApp imeanzisha Mfumo wa Discount (Punguzo la Bei) kwa Account za Biashara (Business Accounts) katika Huduma yake ya Meta Verified (Huduma ya Blue tick za Kulipia).

    Sasa Mtu/Kampuni yenye Account Instagram inaweza Kupata tick ya Blue kwa Ada ya Tshs 1,300 tu! (Elfu Moja na Mia Tatu) kwa Mwezi wa Kwanza, kisha Tshs 19,500 kwa Mwezi unaofuata.

    Huduma ya Meta Verified ni huduma nzuri ikiwa unapenda Kulinda Brand yako Mtandaoni kwani utawapa Mashabiki au Wateja urahisi wa kufahamu ipi ni Account yako Rasmi.



    ZINGATIA:
    Ofa ya Punguzo la Bei ya tiki hizi ipo kwa Account za Biashara pekee katika Instagram na kwa Watumiaji wa Facebook wenye Account zilizo katika Professional Mode. (Si Account zote zinaweza Kuwa na Discount hii).
    PATA BLUETICK YAKO KWA TSHS 1,300 TU KATIKA INSTAGRAM NA FACEBOOK! 🙌 Kampuni ya Meta inayosimamia Mtandao wa Instagram, Facebook na WhatsApp imeanzisha Mfumo wa Discount (Punguzo la Bei) kwa Account za Biashara (Business Accounts) katika Huduma yake ya Meta Verified (Huduma ya Blue tick za Kulipia). Sasa Mtu/Kampuni yenye Account Instagram inaweza Kupata tick ya Blue kwa Ada ya Tshs 1,300 tu! (Elfu Moja na Mia Tatu) kwa Mwezi wa Kwanza, kisha Tshs 19,500 kwa Mwezi unaofuata. Huduma ya Meta Verified ni huduma nzuri ikiwa unapenda Kulinda Brand yako Mtandaoni kwani utawapa Mashabiki au Wateja urahisi wa kufahamu ipi ni Account yako Rasmi. ZINGATIA: Ofa ya Punguzo la Bei ya tiki hizi ipo kwa Account za Biashara pekee katika Instagram na kwa Watumiaji wa Facebook wenye Account zilizo katika Professional Mode. (Si Account zote zinaweza Kuwa na Discount hii).
    Love
    1
    0 Comments 0 Shares 1K Views
  • NJIA MPYA YA KUJIINGIZIA PESA FACEBOOK KUPITIA POSTS ZA MAANDISHI, VIDEO NA REELS.

    October 2, 2024 Facebook Walizindua Programu Mpya waliyoipa Jina “Content Monetization” ambayo imezijumuisha kwa Pamoja category ambazo mwanzo zilijitegemea, Category hizo zilikuwa,

    ⬜️ Ads On Reels
    ⬜️ InStream Ads
    ⬜️ Performance Bonus

    Category hizi kwasasa zimejumuishwa kwa Pamoja na Kupewa Jina “Content Monetization” ambapo Mtu yeyote kwasasa mwenye Page ya Facebook au Account ambayo iko “on Professional Mode” iliyo na Video, Picha, Post au Maudhui yoyote ambayo yatakuwa yanafaa Kulipwa basi Facebook watapachika Matangazo yao na Mhusika ataanza Kulipwa kwa Ukubwa zaidi kuliko Mwanzo. Malipo ni kila Tarehe 21-23 ya Kila Mwezi na kiwango cha Chini cha Kutoa Pesa ni $100 (Tshs 271,500), yaani ikiwa Page au Account yako haijafikisha Kiwango hicho hutoruhusiwa Kutoa mpaka utakapofikisha au kupita kiwango hicho na Ni rahisi kufikisha ikiwa unatengeneza Video zaidi na zinatazamwa zaidi.

    Hii Itawapa Motisha zaidi Content Creators kutengeneza Video zaidi katika Platform hiyo.

    Mfumo huu kwasasa unatolewa kwa Mualiko Pekee, ikiwa Una Page au Account yenye Video au Posts zilizo tazamwa zaidi fuata hatua zifuatazo hapo chini kuomba Mualiko wa Kuunganishwa na Programu hii BURE.

    ⬜️ Ingia >> hapa https://creators.facebook.com/tools/facebook-content-monetization
    ⬜️ Chagua >> I'm Interested
    ⬜️ Jaza Taarifa zako
    ⬜️ Sehemu ya Email Address, Weka Email yako yoyote iliyo hewani (Ni Vizuri ukitumia uliyo Link katika Account yako)
    ⬜️ Sehemu ya Facebook Account URL, Weka Link ya Account au Page yako unayohitaji Iwe na Programu hiyo.
    ⬜️ Sehemu ya Other Social Media Accounts, Weka Link ya Account yako katika Mtandao Mwingine (Hasa Instagram).
    Baadae Bofya LET'S DO THIS


    Utapokea Email ya Uthibitisho baada ya Siku kadhaa ikiwa Account au Page yako imeruhusiwa Kutumia Programu hiyo.

    Programu hii ni Programu nzuri na Bora zaidi kwa Content Creators wadogo, Wakubwa na Wanaochipukia (Upcoming Creators). Ni Programu Rafiki kwa kila Mmoja, itakusaidia Kupata Chochote kupitia Kazi zako.
    NJIA MPYA YA KUJIINGIZIA PESA FACEBOOK KUPITIA POSTS ZA MAANDISHI, VIDEO NA REELS. October 2, 2024 Facebook Walizindua Programu Mpya waliyoipa Jina “Content Monetization” ambayo imezijumuisha kwa Pamoja category ambazo mwanzo zilijitegemea, Category hizo zilikuwa, ⬜️ Ads On Reels ⬜️ InStream Ads ⬜️ Performance Bonus Category hizi kwasasa zimejumuishwa kwa Pamoja na Kupewa Jina “Content Monetization” ambapo Mtu yeyote kwasasa mwenye Page ya Facebook au Account ambayo iko “on Professional Mode” iliyo na Video, Picha, Post au Maudhui yoyote ambayo yatakuwa yanafaa Kulipwa basi Facebook watapachika Matangazo yao na Mhusika ataanza Kulipwa kwa Ukubwa zaidi kuliko Mwanzo. Malipo ni kila Tarehe 21-23 ya Kila Mwezi na kiwango cha Chini cha Kutoa Pesa ni $100 (Tshs 271,500), yaani ikiwa Page au Account yako haijafikisha Kiwango hicho hutoruhusiwa Kutoa mpaka utakapofikisha au kupita kiwango hicho na Ni rahisi kufikisha ikiwa unatengeneza Video zaidi na zinatazamwa zaidi. Hii Itawapa Motisha zaidi Content Creators kutengeneza Video zaidi katika Platform hiyo. Mfumo huu kwasasa unatolewa kwa Mualiko Pekee, ikiwa Una Page au Account yenye Video au Posts zilizo tazamwa zaidi fuata hatua zifuatazo hapo chini kuomba Mualiko wa Kuunganishwa na Programu hii BURE. ⬜️ Ingia >> hapa https://creators.facebook.com/tools/facebook-content-monetization ⬜️ Chagua >> I'm Interested ⬜️ Jaza Taarifa zako ⬜️ Sehemu ya Email Address, Weka Email yako yoyote iliyo hewani (Ni Vizuri ukitumia uliyo Link katika Account yako) ⬜️ Sehemu ya Facebook Account URL, Weka Link ya Account au Page yako unayohitaji Iwe na Programu hiyo. ⬜️ Sehemu ya Other Social Media Accounts, Weka Link ya Account yako katika Mtandao Mwingine (Hasa Instagram). 🔗 Baadae Bofya LET'S DO THIS Utapokea Email ya Uthibitisho baada ya Siku kadhaa ikiwa Account au Page yako imeruhusiwa Kutumia Programu hiyo. Programu hii ni Programu nzuri na Bora zaidi kwa Content Creators wadogo, Wakubwa na Wanaochipukia (Upcoming Creators). Ni Programu Rafiki kwa kila Mmoja, itakusaidia Kupata Chochote kupitia Kazi zako.
    Love
    1
    0 Comments 0 Shares 2K Views
  • "TAARIFA

    Napenda kuwajulisha wanamichezo wote sihusiki na huo uchambuzi hapo juu , kumekuwepo na hali ya wadau hususani wazalisha mahudhui mtandaoni kulitumia jina langu kwenye kujenga hoja zao

    Ni muda sasa vitendo hivi vimekuwa vikijitokeza, nawaomba wadau wangu kufuatilia taarifa zangu rasmi kupitia kwenye platform zangu za mitandao ya kijamii zote ambazo ziko verified ( Instagram na X zamani Twitter)

    Pamoja na vipindi vya michezo" - Shaffih Dauda, Mchambuzi.

    "TAARIFA Napenda kuwajulisha wanamichezo wote sihusiki na huo uchambuzi hapo juu , kumekuwepo na hali ya wadau hususani wazalisha mahudhui mtandaoni kulitumia jina langu kwenye kujenga hoja zao Ni muda sasa vitendo hivi vimekuwa vikijitokeza, nawaomba wadau wangu kufuatilia taarifa zangu rasmi kupitia kwenye platform zangu za mitandao ya kijamii zote ambazo ziko verified ( Instagram na X zamani Twitter) Pamoja na vipindi vya michezo" - Shaffih Dauda, Mchambuzi.
    0 Comments 0 Shares 833 Views
  • https://www.instagram.com/p/DE1_jdII8l4/?igsh=dTBuM2ZlaGd2d2c3#MSUMBIJI: *DANIEL CHAPO AAPISHWA KUWA RAIS MPYA WA MSUMBIJI LEO*
    Msumbiji imemuapisha Daniel Chapo kuwa Rais mpya wa taifa hilo leo Jumatano baada ya miezi kadhaa ya machafuko ya kisiasa kufuatia uchaguzi, ambapo kwa mujibu wa shirika la misaada linadai kuwa imesababisha vifo vya zaidi ya watu 300.
    Chapo ameahidi kwenye kiapo chake hii leo kwamba atatoa nguvu zake zote katika kulinda, kukuza na kuimarisha umoja wa kitaifa.
    Chapo, mwenye umri wa miaka 48, anapanua utawala wa chama cha Frelimo kwa miaka 50 katika nchi hii tajiri kwa gesi.
    Mgombea wa upinzani, Venancio Mondlane, anadai kuwa uchaguzi wa Oktoba ulighushiwa.
    https://www.instagram.com/p/DE1_jdII8l4/?igsh=dTBuM2ZlaGd2d2c3#MSUMBIJI: *DANIEL CHAPO AAPISHWA KUWA RAIS MPYA WA MSUMBIJI LEO* Msumbiji imemuapisha Daniel Chapo kuwa Rais mpya wa taifa hilo leo Jumatano baada ya miezi kadhaa ya machafuko ya kisiasa kufuatia uchaguzi, ambapo kwa mujibu wa shirika la misaada linadai kuwa imesababisha vifo vya zaidi ya watu 300. Chapo ameahidi kwenye kiapo chake hii leo kwamba atatoa nguvu zake zote katika kulinda, kukuza na kuimarisha umoja wa kitaifa. Chapo, mwenye umri wa miaka 48, anapanua utawala wa chama cha Frelimo kwa miaka 50 katika nchi hii tajiri kwa gesi. Mgombea wa upinzani, Venancio Mondlane, anadai kuwa uchaguzi wa Oktoba ulighushiwa.
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 1K Views
  • Sheria za ndani zilizovuja zinaonyesha kuwa Meta (Instagram, Facebook, n.k.) sasa inawaruhusu watumiaji kutusi vikundi kama vile mashoga, watu wanaohama na wahamiaji. Hii inakuja kama sehemu ya mabadiliko ya sera ambayo pia yanasimamisha mpango wa ukaguzi wa ukweli wa kampuni. Kulingana na Mkurugenzi Mtendaji Mehta, lengo ni "kuruhusu uhuru zaidi wa kujieleza kwa kuondoa vikwazo
    Sheria za ndani zilizovuja zinaonyesha kuwa Meta (Instagram, Facebook, n.k.) sasa inawaruhusu watumiaji kutusi vikundi kama vile mashoga, watu wanaohama na wahamiaji. Hii inakuja kama sehemu ya mabadiliko ya sera ambayo pia yanasimamisha mpango wa ukaguzi wa ukweli wa kampuni. Kulingana na Mkurugenzi Mtendaji Mehta, lengo ni "kuruhusu uhuru zaidi wa kujieleza kwa kuondoa vikwazo
    Like
    2
    0 Comments 0 Shares 1K Views
  • Wananchi eh kesho furaha uhakika kwa mujibu wa meneja habari na mawasiliano wa klabu ya Young Africans Ally Kamwe anasema kesho ifike wananchi mfurahi

    #Rafikiwasoka
    #Instagramrafikiwasoka
    📌 Wananchi eh kesho furaha uhakika 🤣 kwa mujibu wa meneja habari na mawasiliano wa klabu ya Young Africans Ally Kamwe anasema kesho ifike wananchi mfurahi #Rafikiwasoka #Instagramrafikiwasoka
    Like
    2
    1 Comments 0 Shares 1K Views