Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili hali ya usalama na kibinadamu Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku hali ikizidi kuzorota. Mwakilishi Maalum wa Umoja huo (UN) Nchini DR Congo, Bintou Keita, amesema Waasi wa kundi la M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda sasa wanadhibiti maeneo makubwa ya Mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini na kutishia kupanua mashambulizi yao hadi Mkoani Tshopo na Maniema.
"Hivi karibuni M23 imesimika utawala wake kwa kuteua gavana, makamu gavana na meya huko Bukavu, Kivu Kusini," amesema Keita.
Ameeleza kuwa mgogoro huo unahusiana na unyonyaji wa madini mashariki mwa DR Congo na kuzua wasiwasi wa kikanda. Pia amegusia hali mbaya ya kibinadamu, akisema kumekuwa na ongezeko la ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, utekaji nyara na ajira ya kulazimishwa kwa Vijana, wakiwemo Watoto.
Licha ya makubaliano ya hivi karibuni kati ya Marais wa Rwanda na DR Congo Nchini Qatar , amani bado haijapatikana. Keita ametoa wito wa kuteuliwa kwa mpatanishi wa Umoja wa Afrika ili kuongoza juhudi za kusitisha mapigano.
Balozi wa DR Congo katika Baraza la Umoja wa kimataifa (UN), Zénon Mukongo Ngay, ameishutumu Rwanda kwa kutotekeleza usitishaji mapigano, huku Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe, akisema Nchi yake itaendelea kuchukua "hatua za ulinzi" mpaka kuwe na mfumo wa kudumu wa usalama.
Wakati huo huo, imeripotiwa kuwa DR Congo inakabiliwa na janga kubwa zaidi la njaa kuwahi kutokea, ambapo Watu zaidi ya milioni 27.7 wanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na vita na ukosefu wa utulivu mashariki mwa Nchi hiyo.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili hali ya usalama na kibinadamu Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 huku hali ikizidi kuzorota. Mwakilishi Maalum wa Umoja huo (UN) Nchini DR Congo, Bintou Keita, amesema Waasi wa kundi la M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Nchi ya Rwanda 🇷🇼 sasa wanadhibiti maeneo makubwa ya Mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini na kutishia kupanua mashambulizi yao hadi Mkoani Tshopo na Maniema.
"Hivi karibuni M23 imesimika utawala wake kwa kuteua gavana, makamu gavana na meya huko Bukavu, Kivu Kusini," amesema Keita.
Ameeleza kuwa mgogoro huo unahusiana na unyonyaji wa madini mashariki mwa DR Congo na kuzua wasiwasi wa kikanda. Pia amegusia hali mbaya ya kibinadamu, akisema kumekuwa na ongezeko la ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, utekaji nyara na ajira ya kulazimishwa kwa Vijana, wakiwemo Watoto.
Licha ya makubaliano ya hivi karibuni kati ya Marais wa Rwanda na DR Congo Nchini Qatar 🇶🇦, amani bado haijapatikana. Keita ametoa wito wa kuteuliwa kwa mpatanishi wa Umoja wa Afrika ili kuongoza juhudi za kusitisha mapigano.
Balozi wa DR Congo katika Baraza la Umoja wa kimataifa (UN), Zénon Mukongo Ngay, ameishutumu Rwanda kwa kutotekeleza usitishaji mapigano, huku Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe, akisema Nchi yake itaendelea kuchukua "hatua za ulinzi" mpaka kuwe na mfumo wa kudumu wa usalama.
Wakati huo huo, imeripotiwa kuwa DR Congo inakabiliwa na janga kubwa zaidi la njaa kuwahi kutokea, ambapo Watu zaidi ya milioni 27.7 wanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na vita na ukosefu wa utulivu mashariki mwa Nchi hiyo.
0 Kommentare
·0 Anteile
·76 Ansichten