Wamarekani watatu waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo kwa kushiriki katika jaribio la mapinduzi dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , sasa wamekabidhiwa kwa mamlaka za Marekani na kurejea Nchini kwao ili kutumikia adhabu yao maisha Jela baada ya kupata msamaha wa Rais kufuatia mazungumzo kati ya Serekali ya DR Congo na Marekani.
Msemaji wa Rais wa DRC,Tina Salama, amethibitisha kuwa Raia hao waliondoka Kinshasa siku ya Jana Jumanne majira ya asubuhi, kufuatia jitihada za kidiplomasia zilizoongozwa na Ubalozi wa Marekani Nchini humo. Hatua hiyo imekuja siku chache tu baada ya adhabu zao za kifo kubadilishwa na kuwa kifungo cha maisha jela.
Miongoni mwa waliorejeshwa ni Marcel Malanga, kijana mwenye umri wa miaka 21, ambaye ni Mtoto wa marehemu Christian Malanga ambaye ni Kiongozi wa upinzani aliyepanga jaribio la mapinduzi dhidi ya Serikali ya Rais Félix Tshisekedi mwaka jana. Hata hivyo, jaribio hilo lilishindikana, na Christian Malanga aliuawa wakati wa makabiliano na Maafisa wa usalama. Kwa mujibu wa taarifa, Marcel alidai kuwa alishinikizwa na Baba yake kushiriki katika tukio hilo, akieleza kuwa hakufanya hivyo kwa hiari yake.
Kurejeshwa kwa Raia hao kumetokea wakati ambapo Serikali ya DR Congo inashughulikia makubaliano ya ushirikiano wa kimataifa kuhusu madini na msaada wa kijeshi na Marekani, lengo likiwa ni kuimarisha usalama hususan katika maeneo ya mashariki ya nchi ambayo yamekuwa yakikumbwa na machafuko ya mara kwa mara.

Wamarekani watatu waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo kwa kushiriki katika jaribio la mapinduzi dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩, sasa wamekabidhiwa kwa mamlaka za Marekani 🇺🇸 na kurejea Nchini kwao ili kutumikia adhabu yao maisha Jela baada ya kupata msamaha wa Rais kufuatia mazungumzo kati ya Serekali ya DR Congo na Marekani.
Msemaji wa Rais wa DRC,Tina Salama, amethibitisha kuwa Raia hao waliondoka Kinshasa siku ya Jana Jumanne majira ya asubuhi, kufuatia jitihada za kidiplomasia zilizoongozwa na Ubalozi wa Marekani Nchini humo. Hatua hiyo imekuja siku chache tu baada ya adhabu zao za kifo kubadilishwa na kuwa kifungo cha maisha jela.
Miongoni mwa waliorejeshwa ni Marcel Malanga, kijana mwenye umri wa miaka 21, ambaye ni Mtoto wa marehemu Christian Malanga ambaye ni Kiongozi wa upinzani aliyepanga jaribio la mapinduzi dhidi ya Serikali ya Rais Félix Tshisekedi mwaka jana. Hata hivyo, jaribio hilo lilishindikana, na Christian Malanga aliuawa wakati wa makabiliano na Maafisa wa usalama. Kwa mujibu wa taarifa, Marcel alidai kuwa alishinikizwa na Baba yake kushiriki katika tukio hilo, akieleza kuwa hakufanya hivyo kwa hiari yake.
Kurejeshwa kwa Raia hao kumetokea wakati ambapo Serikali ya DR Congo inashughulikia makubaliano ya ushirikiano wa kimataifa kuhusu madini na msaada wa kijeshi na Marekani, lengo likiwa ni kuimarisha usalama hususan katika maeneo ya mashariki ya nchi ambayo yamekuwa yakikumbwa na machafuko ya mara kwa mara.
0 Kommentare
·0 Anteile
·5 Ansichten