• "Ni kweli tunamshikilia Ali Kamwe ambaye ni Msemaji wa Klabu ya Yanga na tunamfanyia mahojiano kwa tuhuma za kutoa maneno machafu kwa Viongozi wa Serikali na tutatoa taarifa rasmi baada ya mahojiano kukamilika" - RPC Richard Abwao, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani wa Tabora.

    "Ni kweli tunamshikilia Ali Kamwe ambaye ni Msemaji wa Klabu ya Yanga na tunamfanyia mahojiano kwa tuhuma za kutoa maneno machafu kwa Viongozi wa Serikali na tutatoa taarifa rasmi baada ya mahojiano kukamilika" - RPC Richard Abwao, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani wa Tabora.
    Like
    1
    · 1 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·6 Views
  • Msemaji wa klabu ya Yanga SC, Ali Kamwe alikamatwa na Jeshi Polisi baada ya mchezo wao dhidi ya klabu ya Tabora United majira ya saa saba na nusu usiku wa kuamkia leo hii. Ali Kamwe alipelekwa kituo kikubwa cha Polisi cha Mkoa na amelala ndani hapo na hadi sasa bado hajaachiwa.

    Viongozi wa Yanga SC bado wanaendelea kufanya jitihada za kumtoa Ali Kamwe hapo haijawekwa bayana makosa aliyoyafanya Msemaji huyo. Taarifa iliyopo ni kuwa, inadaiwa Ali Kamwe alitoa kauli isiyokuwa nzuri kipindi anamjibu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha kabla ya mechi kama sehemu ya utani baada ya Mkuu huyo kutoa ahadi ya Shilingi milioni sitini (60) endapo klabu ya Tabora United ikimfunga Yanga SC ambapo mchezo ulimalizika kwa ushindi wa Yanga SC wa mabao matatu kwa bila (0-3).

    Msemaji wa klabu ya Yanga SC, Ali Kamwe alikamatwa na Jeshi Polisi baada ya mchezo wao dhidi ya klabu ya Tabora United majira ya saa saba na nusu usiku wa kuamkia leo hii. Ali Kamwe alipelekwa kituo kikubwa cha Polisi cha Mkoa na amelala ndani hapo na hadi sasa bado hajaachiwa. Viongozi wa Yanga SC bado wanaendelea kufanya jitihada za kumtoa Ali Kamwe hapo haijawekwa bayana makosa aliyoyafanya Msemaji huyo. Taarifa iliyopo ni kuwa, inadaiwa Ali Kamwe alitoa kauli isiyokuwa nzuri kipindi anamjibu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha kabla ya mechi kama sehemu ya utani baada ya Mkuu huyo kutoa ahadi ya Shilingi milioni sitini (60) endapo klabu ya Tabora United ikimfunga Yanga SC ambapo mchezo ulimalizika kwa ushindi wa Yanga SC wa mabao matatu kwa bila (0-3).
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·13 Views
  • Mke wa Mchezaji wa kimataifa wa Burkina Faso n'a klabu ya Yanga SC, Hamisa Mobetto (Tanzania ) ameingia kwenye orodha ya WAGS (Wives And Girlfriends of Footballers) ambao ni Wake (Wapenzi au Wachumba) wa Wachezaji wenye Wafuasi (followers) wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram Duniani.

    1. @georginagio (Mrs. Ronaldo) :+65.5M
    2. antonelaroccuzzo (Mrs. Messi) : +39.9M
    3. @iambeckyg (Mrs. Sebastian) : +37.2M
    4. @victoriabeckham (Mrs. Beckham) : +32.9M
    5. @perrieedwards (Mrs. Alex) :+19M

    6. @alishalehmann7 (Mrs. Douglas Luiz) : +16.6M
    7. @brunabiancardi (Mrs. Neymar Jr) : +13.6M
    8. @hamisamobetto (Mrs. Aziz Ki) : +12.1M
    9. @pilarrubio (Mrs. Sergio Ramos) : +11.1M
    10. @leighannepinnock (Mrs. Andre Gray) : +10M

    Mke wa Mchezaji wa kimataifa wa Burkina Faso 🇧🇫 n'a klabu ya Yanga SC, Hamisa Mobetto (Tanzania 🇹🇿) ameingia kwenye orodha ya WAGS (Wives And Girlfriends of Footballers) ambao ni Wake (Wapenzi au Wachumba) wa Wachezaji wenye Wafuasi (followers) wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram Duniani. 1. @georginagio (Mrs. Ronaldo) :+65.5M 2. antonelaroccuzzo (Mrs. Messi) : +39.9M 3. @iambeckyg (Mrs. Sebastian) : +37.2M 4. @victoriabeckham (Mrs. Beckham) : +32.9M 5. @perrieedwards (Mrs. Alex) :+19M 6. @alishalehmann7 (Mrs. Douglas Luiz) : +16.6M 7. @brunabiancardi (Mrs. Neymar Jr) : +13.6M 8. @hamisamobetto (Mrs. Aziz Ki) : +12.1M 9. @pilarrubio (Mrs. Sergio Ramos) : +11.1M 10. @leighannepinnock (Mrs. Andre Gray) : +10M
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·208 Views
  • "Marekani mpaka sasa hawajasaini mkataba wa kuilinda Congo mchakato umekuwa mrefu. Jiulize vile vikwazo vya Magharibi walivyoiwekea Rwanda vimeishia wapi

    Kagame anajua anachokifanya ndio maana licha ya ripoti za UN , US na EU kuonyesha Rwanda wanaifadhili M23 plus Vikwazo hakuna kilichobadilika Congo

    Wanachokifanya wanaoibia Congo na Africa ni ile ile mbinu ya wakati wa ukoloni inaitwa "Divided and Rule " yaani wagawanywe uwatawale nakumbuka hii mbinu pia enzi hizo ndio iliyozaa utani wa jadi wa Yanga na Simba

    Oooh Africa " - Zungu, Mchambuzi wa Siasa na Mtangazaji.

    "Marekani mpaka sasa hawajasaini mkataba wa kuilinda Congo mchakato umekuwa mrefu. Jiulize vile vikwazo vya Magharibi walivyoiwekea Rwanda vimeishia wapi 😀😀😀😀 Kagame anajua anachokifanya ndio maana licha ya ripoti za UN , US na EU kuonyesha Rwanda wanaifadhili M23 plus Vikwazo hakuna kilichobadilika Congo 😭😭😭😭 Wanachokifanya wanaoibia Congo na Africa ni ile ile mbinu ya wakati wa ukoloni inaitwa "Divided and Rule " yaani wagawanywe uwatawale nakumbuka hii mbinu pia enzi hizo ndio iliyozaa utani wa jadi wa Yanga na Simba Oooh Africa🌍 😭" - Zungu, Mchambuzi wa Siasa na Mtangazaji.
    Like
    1
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·143 Views
  • Amesema Steve Nyerere.

    "Mstafuuu ,,, Ivi Mama Akipenda kwenda kuangalia Dabi,....Pale uwanja wa Taifa pamoja na Watanzania na mashabiki wa Simba na Yanga Si Itapendeza sana,......Naimani Timu zote zitafurahia kuazimisha Miaka 4 Ya Rais wetu Mpendwa kwa Kucheza Dabi,...Maana ndani ya Miaka 4 Ya Mh @samia_suluhu_hassan Soka Limekuwa kivutio kikubwa sana Na Muanko wa Soka umekuwa mkubwa Baada ya Mh Rais kuhakikisha sekta hii Inapiga hatua,......

    Kuazimisha Miaka 4 Ya kipenzi cha Watanzania Dr Samia Suluhu Hassan Dabi halafu mgeni Rasmi Mama Itapendeza Tutajaaaa balaaa,...Apo vipi.,.," - Steve Nyerere, Mwigizaji wa filamu Tanzania.

    Amesema Steve Nyerere. "Mstafuuu ,,, Ivi Mama Akipenda kwenda kuangalia Dabi,....Pale uwanja wa Taifa pamoja na Watanzania na mashabiki wa Simba na Yanga Si Itapendeza sana,......Naimani Timu zote zitafurahia kuazimisha Miaka 4 Ya Rais wetu Mpendwa kwa Kucheza Dabi,...Maana ndani ya Miaka 4 Ya Mh @samia_suluhu_hassan Soka Limekuwa kivutio kikubwa sana Na Muanko wa Soka umekuwa mkubwa Baada ya Mh Rais kuhakikisha sekta hii Inapiga hatua,...... Kuazimisha Miaka 4 Ya kipenzi cha Watanzania Dr Samia Suluhu Hassan Dabi halafu mgeni Rasmi Mama Itapendeza Tutajaaaa balaaa,...Apo vipi.,.," - Steve Nyerere, Mwigizaji wa filamu Tanzania.
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·145 Views
  • “Sisi tumeitwa na serikali tumekuja kusikiliza ila msimamo wa Klabu upo wazi na unafahamika ila hapa tumekuja kusikiliza na tutayabeba yale ambayo tuna uwezo nayo ambayo hatuna uwezo nayo tutayaacha, ilipofikia sio suala la maslahi ya mpira wa Tanzania bali maslahi ya Klabu yetu kwanza” - Alex Ngai, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Yanga SC.

    “Sisi tumeitwa na serikali tumekuja kusikiliza ila msimamo wa Klabu upo wazi na unafahamika ila hapa tumekuja kusikiliza na tutayabeba yale ambayo tuna uwezo nayo ambayo hatuna uwezo nayo tutayaacha, ilipofikia sio suala la maslahi ya mpira wa Tanzania bali maslahi ya Klabu yetu kwanza” - Alex Ngai, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Yanga SC.
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·130 Views
  • "Sisi Simba tumeitwa kujadili kuhusu soka la Tanzania na maendeleo yake na Waziri, hatujaitwa hapa kujadili kuhusu mchezo wetu dhidi ya Yanga na kama ingekuwa hivyo tungeitwa wote kwa pamoja, wao kama wamejadili kuhusu mchezo huo ni wao sasa ila sisi hatujajadili hilo kwanza hata sifahamu kama Yanga walikuwepo” - Murtaza Mangungu, Mwenyekiti wa klabu ya Simba SC.

    "Sisi Simba tumeitwa kujadili kuhusu soka la Tanzania na maendeleo yake na Waziri, hatujaitwa hapa kujadili kuhusu mchezo wetu dhidi ya Yanga na kama ingekuwa hivyo tungeitwa wote kwa pamoja, wao kama wamejadili kuhusu mchezo huo ni wao sasa ila sisi hatujajadili hilo kwanza hata sifahamu kama Yanga walikuwepo” - Murtaza Mangungu, Mwenyekiti wa klabu ya Simba SC.
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·163 Views
  • Baada ya kikao kilichofanyika leo hii katika ofisi za Baraza la Michezo Tanzania (BMT), ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, imeelezwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, hakuja kutoa maamuzi bali kutafuta suluhisho kuhusu hatima ya Dabi ya Kariakoo, iliyokuwa ipigwe Machi 8, 2025 lakini ikaahirishwa.

    "Mheshimiwa Waziri amekuwa na mwanzo mzuri kwa kueleza kwamba jukwaa hilo siyo la maamuzi, bali ni la kutafuta suluhisho la tatizo lililotokea." - Eng. Hersi Said, Rais wa klabu ya Yanga SC

    Aidha, Rais huyo wa klabu ya Yanga SC amewahakikishia Wanachama wa klabu hiyo kuwa Uongozi wao uko imara na unafanya kila jitihada kuhakikisha maslahi ya klabu yanalindwa.Kikao hicho kimewakutanisha Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) na klabu ya Yanga SC, ambapo pande zote zimepata fursa ya kuwasilisha hoja zao kwa Waziri Kabudi.

    Baada ya kikao kilichofanyika leo hii katika ofisi za Baraza la Michezo Tanzania (BMT), ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, imeelezwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, hakuja kutoa maamuzi bali kutafuta suluhisho kuhusu hatima ya Dabi ya Kariakoo, iliyokuwa ipigwe Machi 8, 2025 lakini ikaahirishwa. "Mheshimiwa Waziri amekuwa na mwanzo mzuri kwa kueleza kwamba jukwaa hilo siyo la maamuzi, bali ni la kutafuta suluhisho la tatizo lililotokea." - Eng. Hersi Said, Rais wa klabu ya Yanga SC Aidha, Rais huyo wa klabu ya Yanga SC amewahakikishia Wanachama wa klabu hiyo kuwa Uongozi wao uko imara na unafanya kila jitihada kuhakikisha maslahi ya klabu yanalindwa.Kikao hicho kimewakutanisha Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) na klabu ya Yanga SC, ambapo pande zote zimepata fursa ya kuwasilisha hoja zao kwa Waziri Kabudi.
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·181 Views
  • Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania , Profesa Palamagamba Kabudi anatarajiwa kukutana na Viongozi wa klabu za Simba SC na Yanga SC kuzungumzia sakata la uamuzi wa klabu ya Simba SC kugomea mechi ya watani wa jadi iliyokuwa ifanyike Machi 8, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

    Pamoja na Viongozi hao wa klabu ya Simba SC na Yanga SC, Wengine ambao wanatarajiwa kushiriki kikao hicho kilichopangwa kufanyika Machi 27 mwaka huu ni Viongozi wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) pamoja na Viongozi kutoka Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara (TPBL).

    Ikumbukwe kwamba klabu ya Simba Sports SC iligomea mchezo huo kwa madai ya ukiukwaji wa Kanuni namba 17(45) ya Kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa zuiliwa kwa Vijana (Mabausa) waliodhaniwa kuwa ni wa klabu ya Yanga SC, ambayo inaruhusu klabu ngeni kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa mechi angalau mara moja kabla ya siku ya mechi.

    Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania 🇹🇿, Profesa Palamagamba Kabudi anatarajiwa kukutana na Viongozi wa klabu za Simba SC na Yanga SC kuzungumzia sakata la uamuzi wa klabu ya Simba SC kugomea mechi ya watani wa jadi iliyokuwa ifanyike Machi 8, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Pamoja na Viongozi hao wa klabu ya Simba SC na Yanga SC, Wengine ambao wanatarajiwa kushiriki kikao hicho kilichopangwa kufanyika Machi 27 mwaka huu ni Viongozi wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) pamoja na Viongozi kutoka Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara (TPBL). Ikumbukwe kwamba klabu ya Simba Sports SC iligomea mchezo huo kwa madai ya ukiukwaji wa Kanuni namba 17(45) ya Kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa zuiliwa kwa Vijana (Mabausa) waliodhaniwa kuwa ni wa klabu ya Yanga SC, ambayo inaruhusu klabu ngeni kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa mechi angalau mara moja kabla ya siku ya mechi.
    Like
    1
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·293 Views
  • Klabu ya Yanga SC imefungua malalamiko kwenye Mahakama ya usuhishi wa michezo Duniani (CAS) baada ya kutoridhishwa na majibu ya TFF. Klabu ya Yanga haina imani na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara na wameshindwa kukubaliana kabisa na majibu ya barua iliyotoka na hivyo wameamuwa kusonga mbele (CAS) ili kudai haki yao.

    Mara ya baada ya kutuma malalamiko yao CAS, klabu ya Yanga SC itasubiri taratibu kutoka katika Mahakama hiyo kisha kesi yao kuanza kusikilizwa.

    Klabu ya Yanga SC imefungua malalamiko kwenye Mahakama ya usuhishi wa michezo Duniani (CAS) baada ya kutoridhishwa na majibu ya TFF. Klabu ya Yanga haina imani na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara na wameshindwa kukubaliana kabisa na majibu ya barua iliyotoka na hivyo wameamuwa kusonga mbele (CAS) ili kudai haki yao. Mara ya baada ya kutuma malalamiko yao CAS, klabu ya Yanga SC itasubiri taratibu kutoka katika Mahakama hiyo kisha kesi yao kuanza kusikilizwa.
    Like
    Haha
    2
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·240 Views
  • "Ile barua ni ya Mwanaukome… Acheni kuijaribu jaribu mamlaka nyie msilete utoto kwenye mambo serious" - Ahmed Ally, Msemaji wa klabu ya Simba SC akiwapiga dongo klabu ya Yanga SC baada ya kuipeleka kesi yao CAS.

    "Ile barua ni ya Mwanaukome…😀😀 Acheni kuijaribu jaribu mamlaka nyie msilete utoto kwenye mambo serious" - Ahmed Ally, Msemaji wa klabu ya Simba SC akiwapiga dongo klabu ya Yanga SC baada ya kuipeleka kesi yao CAS.
    Like
    2
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·207 Views
  • Kwenye barua ambayo Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imewajibu Yanga yenye kumbukumbu namba TPLB/2024/625 ya Machi 16,2025 imewaambia Yanga hawawezi kupewa alama tatu kutokana na kuwa hakuna KANUNI ya Ligi Kuu inayoamuru jambo hilo ambapo TPLB imewapa sababu takribani 10, nitazielezea kwa uchache.

    1. Mchezo ulighairishwa na Bodi majira ya saa8 Mchana ambapo baada ya Bodi huo hapakuwa na Afisa yoyote wa mchezo zaidi ya Watu wa Usalama.

    2. Hakuna taratibu zozote za mchezo zilizofanyika uwanjani kwa mujibu wa Kanuni ya 17 ikiwemo timu kukaguliwa na ili timu ipewe alama tatu na mabao matatu ilipaswa ukaguzi kufanyika na Maafisa ww Mchezo.

    3. Bodi ilishindwa kuruhusu mchezo uchezwe sio kwasababu Simba ALIGOMEA mechi bali kupitia Kamati ya Masaa 72 ikaamuru kupitia sababu mbalimbali za Kikanuni kughairisha mchezo huo baada ya kupokea pia ripoti mbalimbali kutoka Maafisa wa mchezo huo.

    4. Yanga SC wameambiwa kwamba hakuna Kanuni inasema Klabu Mgeni anapaswa kuwataarifu wao kwamba wanakuja kufanya mazoezi, hivyo suala la mawasiliano ni MWONGOZO tu wa Bodi hivyo Simba haikuvunja Kanuni kutowasiliana bali ilivunja MIONGOZO.

    5. Yanga SC wamejibiwa kuwa haitowapa alama tatu kwakuwa sababu za kughairisha mchezo zilikuwa ni za kiusalama, ambapo kulikuwa na tuhuma za rushwa, vitisho na kasoro za Kiusalama hivyo ingekuwa ngumu kuruhusu mchezo uendelee ambao ungeleta kasoro, kabla, wakati na baada ya mchezo.

    6. Yanga SC wanalaumiwa na Bodi kitendo cha kupeleka timu uwanjani wakati mechi imeshaghairishwa ni kinyume na Kanuni ya 47(18) na imeonesha kupingana na Mamlaka.

    7. Kuhusu gharama za mchezo ambazo Yanga wameziingia Bodi inasema itazighulikia Kikanuni.

    8. Bodi imewatakia Yanga maandalizi mema ya mchezo ujao wa Derby ambapo watawapangia rasmi tarehe.
    Etc.

    Kwenye barua ambayo Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imewajibu Yanga yenye kumbukumbu namba TPLB/2024/625 ya Machi 16,2025 imewaambia Yanga hawawezi kupewa alama tatu kutokana na kuwa hakuna KANUNI ya Ligi Kuu inayoamuru jambo hilo ambapo TPLB imewapa sababu takribani 10, nitazielezea kwa uchache. 1. Mchezo ulighairishwa na Bodi majira ya saa8 Mchana ambapo baada ya Bodi huo hapakuwa na Afisa yoyote wa mchezo zaidi ya Watu wa Usalama. 2. Hakuna taratibu zozote za mchezo zilizofanyika uwanjani kwa mujibu wa Kanuni ya 17 ikiwemo timu kukaguliwa na ili timu ipewe alama tatu na mabao matatu ilipaswa ukaguzi kufanyika na Maafisa ww Mchezo. 3. Bodi ilishindwa kuruhusu mchezo uchezwe sio kwasababu Simba ALIGOMEA mechi bali kupitia Kamati ya Masaa 72 ikaamuru kupitia sababu mbalimbali za Kikanuni kughairisha mchezo huo baada ya kupokea pia ripoti mbalimbali kutoka Maafisa wa mchezo huo. 4. Yanga SC wameambiwa kwamba hakuna Kanuni inasema Klabu Mgeni anapaswa kuwataarifu wao kwamba wanakuja kufanya mazoezi, hivyo suala la mawasiliano ni MWONGOZO tu wa Bodi hivyo Simba haikuvunja Kanuni kutowasiliana bali ilivunja MIONGOZO. 5. Yanga SC wamejibiwa kuwa haitowapa alama tatu kwakuwa sababu za kughairisha mchezo zilikuwa ni za kiusalama, ambapo kulikuwa na tuhuma za rushwa, vitisho na kasoro za Kiusalama hivyo ingekuwa ngumu kuruhusu mchezo uendelee ambao ungeleta kasoro, kabla, wakati na baada ya mchezo. 6. Yanga SC wanalaumiwa na Bodi kitendo cha kupeleka timu uwanjani wakati mechi imeshaghairishwa ni kinyume na Kanuni ya 47(18) na imeonesha kupingana na Mamlaka. 7. Kuhusu gharama za mchezo ambazo Yanga wameziingia Bodi inasema itazighulikia Kikanuni. 8. Bodi imewatakia Yanga maandalizi mema ya mchezo ujao wa Derby ambapo watawapangia rasmi tarehe. Etc.
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·253 Views
  • Kutoka kwa Arafati Haji, makamu raisi wa YANGA
    Kutoka kwa Arafati Haji, makamu raisi wa YANGA
    Like
    1
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·118 Views
  • Mchezaji wa klabu ya Yanga SC na Askari, Ibrahim Bacca amepandishwa cheo kutoka kuwa Koplo hadi Sajenti. Mchezaji huyo amepandishwa cheo kutokana na kuonyesha kiwango bora katika klabu yake ya Yanga SC pamoja na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars).

    Mchezaji wa klabu ya Yanga SC na Askari, Ibrahim Bacca amepandishwa cheo kutoka kuwa Koplo hadi Sajenti. Mchezaji huyo amepandishwa cheo kutokana na kuonyesha kiwango bora katika klabu yake ya Yanga SC pamoja na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars).
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·183 Views
  • Kutoka kwa Mchambuzi wetu Jemedari Said.

    HAKUNA ALAMA 3 ZA MEZANI, YANGA YAAMBIWA INAWEZA KUSHUSHWA DARAJA (47:18)

    Bodi ya Ligi Kuu imeijibu klabu ya Yanga barua yake ambayo ilikuwa pamoja na mambo mengine inataka ipewe alama 3 na mabao 3 kwenye mchezo ulioahirishwa wa tarehe 8 Machi,2025. Katika barua ya tarehe 16 Machi,2025 yenye Kumb.Na TPLB/CEO/2024/625, Bodi inasema mechi ILIAHIRISHWA kwa kufuata kanuni na wala sio kwa sababu Simba SC WALIGOMEA kama ambavyo Yanga walisema.

    Katika barua hiyo ya Bodi yenye kurasa 3 na vipengele 12, Bodi imewaambia Yanga mchezo uliahirishwa rasmi saa 8 mchana baada ya hapo hakukuwa na taratibu zozote kuhusu mchezo huo ambazo ziliendelea, na kwamba maafisa wote wa mchezo ambao walikuwa wakifanya shughuli za mechi Benjamin Mkapa waliondoka isipokuwa wale wa usalama pekee.

    Hakukuwa na taratibu zozote za mchezo zilizoendelea kama zinavyoelezwa kwenye kanuni 17 ambazo zilifanywa ili kuipatia timu iliyopo kiwanjani alama 3 na mabao 3 kikanuni, ikiwemo kukagua timu hiyo, inasomeka sehemu ya barua hiyo ya majibu kwa Yanga SC.

    Klabu yako inapaswa kuelewa kwamba kanuni za ligi Kuu namba 17:45 haisemi popote kwamba klabu mgeni (visiting team) inapaswa kuwasiliana na wadau wengine ili kutimiza takwa la kikanuni la wao kwenda kufanya mazoezi kwenye uwanja utakaochezwa mechi. Imesomeka barua hii ya Bodi.

    Bodi aidha imesema waliita kikao cha dharura cha Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi baada ya kupokea ripoti tofauti tofauti Zenue mfululizo wa matukio uliojenga msingi wa mgogoro uliotokea tarehe 7 Machi,2025 pale Benjamin Mkapa wakati Simba wakitaka kufanya mazoezi.

    Kutokana na umuhimu na unyeti wa taarifa zilizopokelewa, zingine zilitishia usalama, vitisho, tuhuma za rushwa, ambazo zinachukuliwa kwa umuhimu na upekee kwenye soka, Kamati iliona umuhimu wa kuhairisha mechi, ili kuepuka changamoto za kiusalama kabla hazijatokea, kabla au baada ya mechi, ili kujipa muda na pengine kuhusisha vyombo vya kitaifa vya uchunguzi, imesema barua hii ya Bodi kwenda Yanga.

    Kamati iliona matokeo hasi ya kuahirishwa mechi ni madogo kuliko matokeo hasi ambayo yangetokea kwa mechi hiyo kuchezwa.Aidha kwa kupeleka timu kiwanjani Yanga wamekiuka kanuni 47:18.

    Kutoka kwa Mchambuzi wetu Jemedari Said. HAKUNA ALAMA 3 ZA MEZANI, YANGA YAAMBIWA INAWEZA KUSHUSHWA DARAJA (47:18) Bodi ya Ligi Kuu imeijibu klabu ya Yanga barua yake ambayo ilikuwa pamoja na mambo mengine inataka ipewe alama 3 na mabao 3 kwenye mchezo ulioahirishwa wa tarehe 8 Machi,2025. Katika barua ya tarehe 16 Machi,2025 yenye Kumb.Na TPLB/CEO/2024/625, Bodi inasema mechi ILIAHIRISHWA kwa kufuata kanuni na wala sio kwa sababu Simba SC WALIGOMEA kama ambavyo Yanga walisema. Katika barua hiyo ya Bodi yenye kurasa 3 na vipengele 12, Bodi imewaambia Yanga mchezo uliahirishwa rasmi saa 8 mchana baada ya hapo hakukuwa na taratibu zozote kuhusu mchezo huo ambazo ziliendelea, na kwamba maafisa wote wa mchezo ambao walikuwa wakifanya shughuli za mechi Benjamin Mkapa waliondoka isipokuwa wale wa usalama pekee. Hakukuwa na taratibu zozote za mchezo zilizoendelea kama zinavyoelezwa kwenye kanuni 17 ambazo zilifanywa ili kuipatia timu iliyopo kiwanjani alama 3 na mabao 3 kikanuni, ikiwemo kukagua timu hiyo, inasomeka sehemu ya barua hiyo ya majibu kwa Yanga SC. Klabu yako inapaswa kuelewa kwamba kanuni za ligi Kuu namba 17:45 haisemi popote kwamba klabu mgeni (visiting team) inapaswa kuwasiliana na wadau wengine ili kutimiza takwa la kikanuni la wao kwenda kufanya mazoezi kwenye uwanja utakaochezwa mechi. Imesomeka barua hii ya Bodi. Bodi aidha imesema waliita kikao cha dharura cha Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi baada ya kupokea ripoti tofauti tofauti Zenue mfululizo wa matukio uliojenga msingi wa mgogoro uliotokea tarehe 7 Machi,2025 pale Benjamin Mkapa wakati Simba wakitaka kufanya mazoezi. Kutokana na umuhimu na unyeti wa taarifa zilizopokelewa, zingine zilitishia usalama, vitisho, tuhuma za rushwa, ambazo zinachukuliwa kwa umuhimu na upekee kwenye soka, Kamati iliona umuhimu wa kuhairisha mechi, ili kuepuka changamoto za kiusalama kabla hazijatokea, kabla au baada ya mechi, ili kujipa muda na pengine kuhusisha vyombo vya kitaifa vya uchunguzi, imesema barua hii ya Bodi kwenda Yanga. Kamati iliona matokeo hasi ya kuahirishwa mechi ni madogo kuliko matokeo hasi ambayo yangetokea kwa mechi hiyo kuchezwa.Aidha kwa kupeleka timu kiwanjani Yanga wamekiuka kanuni 47:18.
    Like
    1
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·286 Views
  • "Masaa 72 Yanga waliowapa TPLB yamekwisha, Sasa tukutane CAS

    Tukumbuke tarehe March 10, 2025.

    Yanga waliandika barua Kwa bodi ya ligi kudai haki Yao ya magoli 3 pamoja na points 3 na fidia ya Tshs million 56,435,000 baada ya uvunjifu wa mchezo ambao ulikuwa ufanyike tarehe 8 March

    Simba waliwashinikiza bodi ya ligi katika hali isiyo ya kawaida bodi ya ligi Kwa kuongozwa na hisia na bila ya kufuata kanuni wanavunja mchezo

    Bodi ya ligi walijulishwa wao wakachagua kukaa kimya bila kujibu madai ya young Africans

    Sasa baada ya saa 72 kutamatika shauri linaenda kwenye mahakama ya usulihisi wa michezo kimataifa CAS

    Hapa hata bodi ya ligi walipanga tarehe mpya ya mchezo hakuna kitakachoendelea Kwa kuwa shauri litakuwa CAS

    Kila la heri Young Africans

    Yanga bingwa" - Mwalimu Yanga, Shabiki kindakindaki wa klabu ya Yanga SC.

    "Masaa 72 Yanga waliowapa TPLB yamekwisha, Sasa tukutane CAS Tukumbuke tarehe March 10, 2025. Yanga waliandika barua Kwa bodi ya ligi kudai haki Yao ya magoli 3 pamoja na points 3 na fidia ya Tshs million 56,435,000 baada ya uvunjifu wa mchezo ambao ulikuwa ufanyike tarehe 8 March Simba waliwashinikiza bodi ya ligi katika hali isiyo ya kawaida bodi ya ligi Kwa kuongozwa na hisia na bila ya kufuata kanuni wanavunja mchezo Bodi ya ligi walijulishwa wao wakachagua kukaa kimya bila kujibu madai ya young Africans Sasa baada ya saa 72 kutamatika shauri linaenda kwenye mahakama ya usulihisi wa michezo kimataifa CAS Hapa hata bodi ya ligi walipanga tarehe mpya ya mchezo hakuna kitakachoendelea Kwa kuwa shauri litakuwa CAS Kila la heri Young Africans Yanga bingwa" - Mwalimu Yanga, Shabiki kindakindaki wa klabu ya Yanga SC.
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·229 Views
  • KAMATI YA SAA 72 YA BODI YA LIGI IMESHINDWA KUKAA NDANI YA SAA 72 KUSHUGHULIKIA SUALA LA DERBY YA SIMBA NA YANGA.

    SASA IMEPITA ZAIDI YA WIKI. VITENDO VYA HILA NA KUPUUZIA KANUNI, VITAHARIBU NA KUSHUSHA THAMANI YA SOKA LETU. WADHAMINI WATAANZA KUKIMBIA.
    KAMATI YA SAA 72 YA BODI YA LIGI IMESHINDWA KUKAA NDANI YA SAA 72 KUSHUGHULIKIA SUALA LA DERBY YA SIMBA NA YANGA. SASA IMEPITA ZAIDI YA WIKI. VITENDO VYA HILA NA KUPUUZIA KANUNI, VITAHARIBU NA KUSHUSHA THAMANI YA SOKA LETU. WADHAMINI WATAANZA KUKIMBIA.
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·241 Views
  • Steve Nyerere agusia sakata la Nicole

    "Mstafuuu,.....Nani mkamilifu katika hii Ardhi Ya Mwenyezi Mungu,..

    Napokea sms Simu swala la Nicole Toka juzi kulia na kushoto lakini nikasema Mungu nitangulie nami nione Mwanga kwenye hili,....Ni Ukweli Usio pingika dada kapuyanga Sana Tena sana Ana Makosa Na Ana Kosa la kujibu, lakini nani mkamilifu,....

    Nicole Ana makosa na kibaya zaidi ni kwenda kuchangisha Watu wenye kujipambania kuitafuta kesho yao, Na kibaya zaidi walikuamini kutokana na bland yake wakiamini kuna matokeo sahihi kupitia Nicole,....

    Nicole ni mtu mzima na mwenye akili timamu Alikuwa Anafanya kitu anacho kijua na kujua matokeo na mwisho wa Matokeo lakini tukienda mbali zaidi limesha tokea naye ni Binadamu,..Sipo hapa kumtetea Mwalifu lakini naandika hapa kujaribu kuona haki ya walio fanyiwa ujinga huu wanaipataje,...Je Nicole kukaaa ndani haki ya wadai Itapatikana Maana siku ya Mwisho Nicole Anatakiwa kuwarudishia FEDHA zao wote walio guswa na yeye Anarudishaje Atajua yeye lakini Akiwa nje kwa dhamana na masharti yenye tija basi Anaweza kumaliza jambo hili.,.

    Lakini Ifike mahara hii michezo ya Magroup Inayogusa FEDHA naomba sana kuwe na Utaratibu wa kumsajiri kijumbe kitambulisho chake na wanachama anao wachangisha waridhie kwa maandishi kuwa wamekubaliana kuanzisha group la kusaidia hii itasaidia sana,.lakini sio mtu anatoka tu huko anaanzisha group mara michango sio sawa.,,.

    Niombe sasa Ni wakati wa kusimama na Nicole Tusiangalie kafanya nini Tuangalie Dhamana yake na jinsi ya kumsaidia,....Haijalishi kala mzigo na nani lakini bado ni mwenzetu,....Anapitia kipindi kibaya sana Ambacho Anahitaji faraja,....

    Tusimame kumuombea Dhamana Tunajua na kutambua sheria na kuheshimu sheria kwenye Taifa letu,......

    Niombe Si muda wa kuliangalia kosa ni Muda wa kulitibu kosa Nani mkamilifu hapa Duniani,..Mimi Binafsi kama STEVEN MENGELE (NYERERE) NIPO TAYARI KUMSAIDIA NICOLE ,..KUTOKA NDANI KWA KUFATA TARATIBU ZOTE,..NA AKIPATA DHAMANA BASI ATAMBUE KULIPA KILA JASHO LA MCHANGAJI KURUDISHIWA NA MAISHA KUENDELEA,....HAKUNA MWANADAMU AMBAYE MKAMILIFU HAPA DUNIANI,...." - Steve Nyerere, Mwigizaji wa filamu Tanzania.

    Steve Nyerere agusia sakata la Nicole "Mstafuuu,.....Nani mkamilifu katika hii Ardhi Ya Mwenyezi Mungu,.. Napokea sms Simu swala la Nicole Toka juzi kulia na kushoto lakini nikasema Mungu nitangulie nami nione Mwanga kwenye hili,....Ni Ukweli Usio pingika dada kapuyanga Sana Tena sana Ana Makosa Na Ana Kosa la kujibu, lakini nani mkamilifu,.... Nicole Ana makosa na kibaya zaidi ni kwenda kuchangisha Watu wenye kujipambania kuitafuta kesho yao, Na kibaya zaidi walikuamini kutokana na bland yake wakiamini kuna matokeo sahihi kupitia Nicole,.... Nicole ni mtu mzima na mwenye akili timamu Alikuwa Anafanya kitu anacho kijua na kujua matokeo na mwisho wa Matokeo lakini tukienda mbali zaidi limesha tokea naye ni Binadamu,..Sipo hapa kumtetea Mwalifu lakini naandika hapa kujaribu kuona haki ya walio fanyiwa ujinga huu wanaipataje,...Je Nicole kukaaa ndani haki ya wadai Itapatikana Maana siku ya Mwisho Nicole Anatakiwa kuwarudishia FEDHA zao wote walio guswa na yeye Anarudishaje Atajua yeye lakini Akiwa nje kwa dhamana na masharti yenye tija basi Anaweza kumaliza jambo hili.,. Lakini Ifike mahara hii michezo ya Magroup Inayogusa FEDHA naomba sana kuwe na Utaratibu wa kumsajiri kijumbe kitambulisho chake na wanachama anao wachangisha waridhie kwa maandishi kuwa wamekubaliana kuanzisha group la kusaidia hii itasaidia sana,.lakini sio mtu anatoka tu huko anaanzisha group mara michango sio sawa.,,. Niombe sasa Ni wakati wa kusimama na Nicole Tusiangalie kafanya nini Tuangalie Dhamana yake na jinsi ya kumsaidia,....Haijalishi kala mzigo na nani lakini bado ni mwenzetu,....Anapitia kipindi kibaya sana Ambacho Anahitaji faraja,.... Tusimame kumuombea Dhamana Tunajua na kutambua sheria na kuheshimu sheria kwenye Taifa letu,...... Niombe Si muda wa kuliangalia kosa ni Muda wa kulitibu kosa Nani mkamilifu hapa Duniani,..Mimi Binafsi kama STEVEN MENGELE (NYERERE) NIPO TAYARI KUMSAIDIA NICOLE ,..KUTOKA NDANI KWA KUFATA TARATIBU ZOTE,..NA AKIPATA DHAMANA BASI ATAMBUE KULIPA KILA JASHO LA MCHANGAJI KURUDISHIWA NA MAISHA KUENDELEA,....HAKUNA MWANADAMU AMBAYE MKAMILIFU HAPA DUNIANI,...." - Steve Nyerere, Mwigizaji wa filamu Tanzania.
    0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·233 Views
  • Afande Sele, Msanii wa muziki Hip-hop Tanzania

    "Tutusa" limeamua kugawa rasilimali muhimu za nchi yake masikini sana kwa Marekani,kusudi Marekani walihakikishie ulinzi wa cheo chake cha urais tu,

    Kuna wakati fulani pale bungeni Dodoma,Mbunge wa Misungwi mdogo wangu Mnyeti,aliwahi kutania kwa kusema vijana wa Congo kama Mayele,badala ya kubaki kwao kulinda nchi yao,kinyume chake wao wanakimbilia nje ya nchi kutetema na kukata mauno

    Baada ya Mnyeti kutania utani huo wa kweli,chakushangaza wabongo lala kama kawaida yetu,tukaacha kujadili hoja yake,badala yake tukaanza kumshambulia mtoa hoja kwasababu za ugonjwa wetu sugu wa usimba na Yanga,

    Ona sasa matokeo yake ndio haya,,nchi yao inauzwa kwa malipo ya kulinda madaraka ya Rais wao ambae hata hivyo hakushinda kihalalii na wakati huo wacongoman wanaendelea kuuza mauno duniani na sio kupaaza sauti zao au kuandamana kupinga ujambazi huo kwa kumshinikiza Rais wao akae kwenye meza ya mazungumzo na ndugu zao wa M23 ili kumaliza mzozo kama Dunia yote inavyomshaurj

    Kinachosikitisha zaidi nj ukweli kwamba Marekani siku zote huwa wanasema hawana rafiki wala Adui wa kudumu,bali wao wanamaslahi ya kudumu,hivyo sio ajabu Marekani wakatumia ufala huo wa Tutusa kuvuna madini kutoka upande wa serekali na upande wa waasi kwa kugawa silaha pande zote kusudi waendelee kupigana na wao Marekani wapate nafasi nzuri ya kuchukua madini ya kila upande kwa Raha zao

    Bila Marekani.

    Each one Teach one
    I Change Nation
    Sina Hatia

    Afande Sele, Msanii wa muziki Hip-hop Tanzania ✍️ "Tutusa" limeamua kugawa rasilimali muhimu za nchi yake masikini sana kwa Marekani,kusudi Marekani walihakikishie ulinzi wa cheo chake cha urais tu,😞 Kuna wakati fulani pale bungeni Dodoma,Mbunge wa Misungwi mdogo wangu Mnyeti,aliwahi kutania kwa kusema vijana wa Congo kama Mayele,badala ya kubaki kwao kulinda nchi yao,kinyume chake wao wanakimbilia nje ya nchi kutetema na kukata mauno🤣 Baada ya Mnyeti kutania utani huo wa kweli,chakushangaza wabongo lala kama kawaida yetu,tukaacha kujadili hoja yake,badala yake tukaanza kumshambulia mtoa hoja kwasababu za ugonjwa wetu sugu wa usimba na Yanga,⚽ Ona sasa matokeo yake ndio haya,,nchi yao inauzwa kwa malipo ya kulinda madaraka ya Rais wao ambae hata hivyo hakushinda kihalalii na wakati huo wacongoman wanaendelea kuuza mauno duniani na sio kupaaza sauti zao au kuandamana kupinga ujambazi huo kwa kumshinikiza Rais wao akae kwenye meza ya mazungumzo na ndugu zao wa M23 ili kumaliza mzozo kama Dunia yote inavyomshaurj💪 Kinachosikitisha zaidi nj ukweli kwamba Marekani siku zote huwa wanasema hawana rafiki wala Adui wa kudumu,bali wao wanamaslahi ya kudumu,hivyo sio ajabu Marekani wakatumia ufala huo wa Tutusa kuvuna madini kutoka upande wa serekali na upande wa waasi kwa kugawa silaha pande zote kusudi waendelee kupigana na wao Marekani wapate nafasi nzuri ya kuchukua madini ya kila upande kwa Raha zao 😜 Bila Marekani.🌚 Each one Teach one🔨 I Change Nation🌎 Sina Hatia⚖️
    Like
    1
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·364 Views
  • "Kupitia kituo cha Wasafi, Kamishna wa mchezo wa Simba na Yanga wa raundi ya kwanza Khalid Bitebo ameomba radhi kuwa aliteleza sio kweli kwamba Yanga walifanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Mkapa kwenye Derby iliyopita, kifupi ameomba radhi kuwa alijichanganya.

    Na huo ndio ukweli ulio wazi kuwa kwenye historia ya Derby hakuna aliyewahi kufanya mazoezi siku moja kabla ya mchezo pale hata Mimi siku ya kwanza ya sakata hili niliripoti kuwa Yanga alifanya mazoezi pale ila sio kweli hawakufanya, Simba na Yanga hata mechi yao iwe Mwanza au Kigoma hawafanyi mazoezi kwenye uwanja wa game, inaenda mbali hadi pitch feeling wanakwepa.

    Wakongwe wa Simba na Yanga pia wakanikumbusha zamani kwanza walikuwa wote wanapakimbia Dar Es Slaaam sio Mgeni wala Mwenyeji wa mechi, mwingine anaenda Pemba mwingine Morogoro, mara Zanzibar mwingine Pemba, timu zinakutana Mjini Mzizima hapa siku ya mbungi na inapigwa kwelikweli ndio utaratibu wao.

    Kwakuwa Kamishna wa mchezo ameomba radhi nadhani ni muhimu ila sio lazima basi na wale waliounga mkono, wakaaminisha Umma kuwa Yanga alifanya mazoezi pale wakaomba radhi pia, ni muhimu ila sio lazima ni katika kuweka kumbukumbu tu sawa, tunakubaliana?" - Farhan JR, Mchambuzi.

    "Kupitia kituo cha Wasafi, Kamishna wa mchezo wa Simba na Yanga wa raundi ya kwanza Khalid Bitebo ameomba radhi kuwa aliteleza sio kweli kwamba Yanga walifanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Mkapa kwenye Derby iliyopita, kifupi ameomba radhi kuwa alijichanganya. Na huo ndio ukweli ulio wazi kuwa kwenye historia ya Derby hakuna aliyewahi kufanya mazoezi siku moja kabla ya mchezo pale hata Mimi siku ya kwanza ya sakata hili niliripoti kuwa Yanga alifanya mazoezi pale ila sio kweli hawakufanya, Simba na Yanga hata mechi yao iwe Mwanza au Kigoma hawafanyi mazoezi kwenye uwanja wa game, inaenda mbali hadi pitch feeling wanakwepa. Wakongwe wa Simba na Yanga pia wakanikumbusha zamani kwanza walikuwa wote wanapakimbia Dar Es Slaaam sio Mgeni wala Mwenyeji wa mechi, mwingine anaenda Pemba mwingine Morogoro, mara Zanzibar mwingine Pemba, timu zinakutana Mjini Mzizima hapa siku ya mbungi na inapigwa kwelikweli ndio utaratibu wao. Kwakuwa Kamishna wa mchezo ameomba radhi nadhani ni muhimu ila sio lazima basi na wale waliounga mkono, wakaaminisha Umma kuwa Yanga alifanya mazoezi pale wakaomba radhi pia, ni muhimu ila sio lazima ni katika kuweka kumbukumbu tu sawa, tunakubaliana?" - Farhan JR, Mchambuzi.
    Like
    1
    · 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·337 Views
Arama Sonuçları