Upgrade to Pro

  • Mnamo Mwaka 2006, wiki kadhaa baada ya kustaafu nafasi ya ukatibu mkuu, Kofi Annan alienda nchini Italia kwa ajili ya mapumziko.

    Akiwa huko, Siku moja aliamua kutoka nje kidogo na kwenda kununua gazeti, lakini ghafla akashangaa Watu wengi wanamzonga. Lengo lao ni kutaka sahihi kutoka kwake. (Kama uonavyo nyota wa filamu au wachezaji mpira, wanavyochora sahihi zao kwenye mashati ya wafuasi).

    Lakini kumbe, Watu hao walimfananisha Kofi Annan na yule nyota wa filamu wa marekani bwana Morgan Freeman .

    Ila, kwa kutotaka kuwaangusha Watu hao, Kofi Annan alichora sahihi kwa kutumia jina la Freeman.

    (Angalia picha zao)

    Koffi Anan, alifaliki akiwa na umri wa miaka 80 huko nchini Switzerland.

    Alihudumu nafasi ya ukatibu mkuu kwanzia Mwaka 1997 hadi 2006, akiwa ndiye mwafrika mweusi wa kwanza kushika nafasi hiyo.

    RIP koffi Annan.
    Mnamo Mwaka 2006, wiki kadhaa baada ya kustaafu nafasi ya ukatibu mkuu, Kofi Annan alienda nchini Italia kwa ajili ya mapumziko. Akiwa huko, Siku moja aliamua kutoka nje kidogo na kwenda kununua gazeti, lakini ghafla akashangaa Watu wengi wanamzonga. Lengo lao ni kutaka sahihi kutoka kwake. (Kama uonavyo nyota wa filamu au wachezaji mpira, wanavyochora sahihi zao kwenye mashati ya wafuasi). Lakini kumbe, Watu hao walimfananisha Kofi Annan na yule nyota wa filamu wa marekani bwana Morgan Freeman . Ila, kwa kutotaka kuwaangusha Watu hao, Kofi Annan alichora sahihi kwa kutumia jina la Freeman. (Angalia picha zao) Koffi Anan, alifaliki akiwa na umri wa miaka 80 huko nchini Switzerland. Alihudumu nafasi ya ukatibu mkuu kwanzia Mwaka 1997 hadi 2006, akiwa ndiye mwafrika mweusi wa kwanza kushika nafasi hiyo. RIP koffi Annan.
    Like
    2
    ·47 Views
  • BAPHOMET: SANAMU LA SHETANI LILILOLETA UTATA NCHINI MAREKANI.

    Binadamu tangu zama za kale amekuwa akijenga, kuchonga na kuweka sanamu za aina nyingi kwa sababu mbalimbali.
    Baadhi hutumiwa kuwaenzi watu maarufu na kuwakumbuka, na nyingine huabudiwa kama miungu. Kwa muda mrefu hata hivyo imekuwa ni nadra kuona sanamu ambayo moja kwa moja inahusishwa na shetani au ibilisi. Lakini ukifika Marekani, mambo ni tofauti. Kuna sanamu moja kubwa ya shaba ambayo inahusishwa na ushetani. Ni sanamu ya, Baphomet ni kiumbe mwenye kichwa kinachofanana na cha mbuzi lakini ameongezwa maungo ya ajabu. Ni kiumbe mwenye mabawa, na kwenye sanamu hiyo inayotumiwa kwa sasa huoneshwa akiwa na watoto wawili wanaotabasamu.

    Sanamu inayotumiwa kwa sasa ina urefu wa karibu futi 9, na iligharimu $100,000 (£64,000) kuitengeneza. Sanamu hii imekuwa ikitumiwa kuwapiga vita wale walio na imani za Kikristo kiislamu na imani nyingine zenye kumcha Mungu mmoja. Ni sanamu hii ambayo imekuwa ikitumiwa kuendesha vita dhidi ya kuwekwa kwa sanamu za Kikristo na dini nyingine katika majengo maarufu, bustani na maeneo ya umma nchini Marekani. Agosti 17, sanamu hiyo ya kiumbe anayefahamika kama Baphomet ilipelekwa katika jimbo la Arkansas anakotoka Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton. Wanaotumia sanamu hiyo ni watu wa kundi linalofahamika kama Satanic Temple (Hekalu la Shetani) ambalo ni kundi la 'kidini' na kisiasa ambalo hupinga kuingizwa kwa dini katika masuala ya Serikali.

    Kundi hilo liliandaa maandamano ya watu 150 waliyojumuisha waabudu shetani, watu wasioamini Mungu yupo, na Wakristo pia.
    Maandamano hayo yalifanyika nje ya jengo lililo Makao Makuu ya jimbo la Arkansas katika mji wa Little Rock. Walikuwa wamekerwa na hatua ya kuweka sanamu ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu katika uwanja wa Makao Makuu hayo. Satanic Temple walisema sanamu hiyo inakiuka Sheria ya Kwanza ya Marekebisho ya Katiba nchini Marekani ambayo huzungumzia uhuru na haki za kidini. "Ikiwa utakubaliana na kuwepo kwa sanamu ya dini moja basi kunafaa kuwa na uhuru kwa wengine kuweka sanamu za kidini, na ukizuia basi kusiwe na sanamu yoyote ile," mwanzilishi mwenza wa tawi la Satanic Temple katika jimbo la Arkansas, Ivy Forrester, alinukuliwa na wanahabari siku hiyo ya maandamano.

    Ndoto yao ni kuwa na sanamu ya kudumu, lakini siku hiyo hawakuruhusiwa na sheria kuiweka kwa muda mrefu. Kuna sheria ya Arkansas ya mwaka 2017 inayohitaji sanamu ya kuwekwa maeneo ya Serikali iwe na udhamini wa Mbunge ambaye atawasilisha mswada iidhinishwe kupitia Bunge. Sanamu hiyo ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu ilidhaminiwa na mwanasiasa wa Republican, Seneta Jason Rapert. Hata hivyo, chini ya saa 24 baada ya kuwekwa, mwanamume mmoja alivurumisha gari na kuugonga mnara huo na kuubomoa. Maandamano ya Satanic Temple Arkansas yalisababisha kuandaliwa kwa maandamano mengine ya kuwapinga yaliyoandaliwa na makundi ya Kikristo na Wanachama wa Republican. Wakristo walikuwa wamebeba karatasi zilizokuwa na ujumbe kutoka kwenye Biblia. Satanic Temple waliwasilisha ombi la kushirikishwa kwenye kesi ya kupinga mnara huo wa Amri Kumi za Mungu iliyowasilishwa na shirika la haki za kiraia la American Civil Liberties Union, lakini kundi hilo limewasilisha ombi kutaka wasishirikishwe kwenye kesi hiyo.

    Sanamu hiyo ya Baphomet ilizinduliwa mara ya kwanza katika mji wa Detroit, Michigan. Mipango ya kuuweka nje ya Makao Makuu ya jimbo la Oklahoma ambapo kulikuwa kumewekwa mnara mwingine wa Amri Kumi za Mungu mwaka 2015. Mnara huo ulizinduliwa Julai 25 Mwaka huo, ambapo kupitia taarifa yao, Satanic temple walisema: "Tulichagua Baphomet kwa sababu ni kiumbe ambaye huhusishwa na Shetani na maana inayohusishwa naye inafaa sana akiwekwa kando na Sanamu inayowakilisha dini nyingine." Sherehe ya kuizindua ilikuwa ya faragha, na ukumbi uliotumiwa uliwekwa siri kubwa kwani Wakristo walikuwa wameandamana awali kuipinga mjini. Picha zilizopakiwa kwenye Facebook zilionyesha uzinduzi wake ulifanyika karibu na Mto wa Detroit. Kabla ya uzinduzi huo kufanyika, waumini takriban 200 walihudhuria ibada ya misa katika kanisa la St. Joseph mjini humo kupinga sanamu hiyo. Wengine 50 walifanya maombi mjini katika eneo ambalo awali Satanic Temple walikuwa wamepanga kuuzindulia mnara huo hapo.

    Mwanamume yule yule aliyeuharibu mnara wa Arkansas anadaiwa kufanya vivyo hivyo na kuubomoa mnara mwingine kama huo wa Amri Kumi za Mungu nje ya Makao Makuu ya jimbo la Oklahoma.
    Satanic Temple walisitisha juhudi zao za kutaka kuweka sanamu ya Baphomet huko baada ya Mahakama ya Juu ya Oklahoma kuamua kwamba Sanamu ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu ilikuwa imewekwa kinyume cha sheria, hivyo wakawa wameshinda vita bila kupigana. Mahakama ilisema ni kinyume cha sheria kutumia mali ya umma kwa manufaa ya dini yoyote ile.

    Jina hili Baphomet, asili yake ni enzi ya kukomesha uasi katika Kanisa Katoliki katika miaka ya 1100, kwa Kiingereza "Inquisition", na kuteswa kwa wapiganaji wa kidini kwa jina la "Knights Templar" waliokuwa wanateswa ili wafichue siri zao na wakubali kuifuata dini kwa mujibu wa viongozi wa kanisa wa wakati huo. Kwa mujibu wa waandishi wa enzi za vita vya kidini maarufu kama Crusade, wapiganaji hao walikiri kumuabudu Mungu wa wapagani kwa jina la Baphometh.

    Baadhi ya wasomi hata hivyo huamini kwamba "Baphometh" ni upotoshaji wa jina "Mahomet" - ambalo hutumiwa kumrejelea Nabii Muhammad, jambo linalozua utata zaidi. Lakini kadiri miaka ilivyosonga na mafumbo na siri kuhusu Utata wa Knights Templar kuzidi, ndivyo ufafanuzi wa neno hilo na maana yake ulivyozidi kutofautiana. Moja ya tafsiri ya neno hilo inapatikana katika kitabu cha "Da Vinci Code" cha ,Dan Brown, ambapo, neno Baphomet limefafanuliwa na kutafsiriwa kama "Sophia" au busara.

    Picha maarufu zaidi ya Baphomet ilichorwa na mzungu wa Ufaransa aitwaye , Eliphas Levi, mwaka 1856 katika kitabu chake cha Transcendental Magic: Its Doctrine and Ritual. Alichora kiumbe mwenye mabawa na mwenye pembe na mwenge ulio katikati ya pembe hizo kichwani. Kuna mchoro pia wa pembe nane kwenye paji la uso. Mikononi kumeandikwa maneno ya Kilatino SOLVE (tenganishwa) na COAGULA (fungamanisha) - ambazo ni nguvu za kuunganisha na kutenganisha ambazo zilitwaliwa kutoka kwa Mungu. Mchoro wa Levi ulihamasisha zaidi sanamu inayotumiwa na Satanic Temple.

    Ni jinsia mbili kwa pamoja, nusu mnyama na nusu binadamu.anapiga saluti ya vidole viwili Sanamu hiyo ina vidole viwili vilivyoelekezwa juu mkono wa kulia na viwili vinavyoelekezwa chini mkono wa kushoto, maana yake "kama ilivyo juu, na chini iwe pia". Maneno hayo na ishara hiyo ya vidole ni maarufu miongoni mwa wenye kuamini katika mizungu na mafumbo. Chanzo chake ni kazi za kale za msomi Hermes Trismegistus, ambaye vitabu vyake vilikuwa maarufu sana enzi ya Kipindi cha mwamko wa sanaa na mageuzi ya kidini, maarufu kama "Renaissance and Reformation" barani Ulaya. Maneno hayo pia hutumiwa kuhusiana na sayansi, vitu vyote na Mungu, lakini Levi aliandika kwamba kwa kutumia ishara hiyo, Baphomet wake alikuwa anaashiria kuwiana sawa kwa fadhila na haki. Lakini maana yake halisi ni kwamba ,shetani anatawala duniani na Mungu anatawala juu.

    Lucien Greaves, msemaji wa Satanic Temple anasema "lengo lao ni kwamba watoto watatazama kazi hiyo ya sanaa kama kwa usalama, ni sanamu isiyofaa kuzua wasiwasi wowote. "Sura ya mbuzi huyo haioneshi chochote. Si ya kishetani wala ya kutisha - kama wanavyodai baadhi ya watu - ukiitazama bila kuongozwa na mzigo wa utamaduni."
    "Sifikiri watoto wanaokutana na sanamu hii watatiwa hofu na propaganda wanaweza wasione chochote cha kuwatia wasiwasi," anasema Greaves. "Lakini si kwamba tunapinga kuwaingiza watoto kwenye mitazamo ya kidini. Mara nyingi watoto hulazimishwa kuingia kwenye dini. Hilo ni jambo hatutaki kulifanya kamwe."

    Kwenye tumbo la Baphomet kuna ishara ya kale ya Kigiriki ya nyoka wawili walio kwenye fimbo - fimbo ambayo ilibebwa na Hermes na maafisa wa kueneza matangazo au kutoa matangazo rasmi waliotumiwa kutoa matamko rasmi. Ishara hiyo kwenye sanamu hiyo inaashiria biashara, mashauriano na kutendeana, na iliingizwa kwenye Baphomet na Levi. "Kwetu ni ishara ya maridhiano ya vitu viwili tofauti - kwa mfano kuwa na sanamu ya Kishetani karibu na sanamu ya Kikristo," anasema Greaves. "Tunafikiri ni ujumbe wenye nguvu sana kuwa na sanamu hii ikiwa karibu na sanamu ya Amri Kumi za Mungu. Unaweza kuwa na mambo mawili tofauti kwa pamoja bila mzozo." Baphomet wa Levi alikuwa ni mwenye maziwa, lakini "tuliyaondoa maziwa hayo" anasema Greaves. Anasema hatukutaka wajipachike kwenye mdahalo kuhusu jinsia ya kiumbe huyo wao jambo ambalo lingewafanya watu kupoteza maana halisi. Badala yake anasema watoto wawili, mvulana na msichana, ndio wanaowakilisha jinsia. Kwa maana iliyojificha Greaves anashindwa kusema kwamba watoto hao wawili wa kike na kiume wanawakilisha ulimwengu wote na hawa ni Adam na Hawa,

    Kwenye paji la uso la Baphomet na kwenye kiti cha enzi alichokikalia kuna mchoro wa nyota ya pembe tano, ishara ambayo mara nyingi hutambuliwa kama ishara ya shetani. Mara nyingi huonekana ikiwa imepinduliwa. Msalaba wa Peter pia hupinduliwa. Greaves anasema lengo lao ni kuwafanya watu wabadilishe mtazamo wao na kuacha kuongozwa na waliyofunzwa na utamaduni wao. Waangazie mambo kwa kuzingatia ushahidi uliopo. Anasema mtazamo huo huwazuia watu kuchukua msimamo huru kuhusu masuala kama vile ndoa za wapenzi wa jinsia moja na haki za kutoa mimba pamoja na huduma nyingine za uzazi wa mpango. "Mwenge wa maarifa ndio kama upembe wa kati na inatukuza juhudi za kutafuta elimu na maarifa. Tunathamini hilo sana," anasema Greaves.

    Levi mwenyewe aliandika kwamba mwenge wa maarifa uolikuwa unawaka katikati ya pembe za Baphomet ni mwanga wa kusawazisha vitu vyote. Ni taswira ya roho iliyo juu ya vitu vyote vinavyoonekana, kama zilivyo ndimi za moto, ingawa bado imeunganishwa na vitu hivyo, mfano moto unavyoendelea kung'aa juu ya mafuta au kijiti. Kulikuwa na mpango wa kuongeza maandiko kwenye mchoro wa nyota ya pembe tano ya moja ya nguzo saba kuu za Satanic Temple: "moyo wa huruma, busara na haki unafaa daima kuongoza zaidi ya neno lililoandikwa au kutamkwa." Nyuma ya sanamu hiyo, kutakuwa na nukuu kutoka kwa kitabu cha Cain chake Lord Byron unaosema: "Kisha, nani alikuwa Ibilisi? Yule hangekuruhusu wewe uishi milele, au yule ambaye angelikuumba uishi milele, katika raha na nguvu za elimu na maarifa?"

    Kwa mujibu wa tovuti yao Satanic Temple wanaamini kwamba "kimsingi watu kuteseka au kuumia ni vibaya, na chochote kile kinachopunguza madhila na mateso ni kizuri." Hawaamini katika kutenda mabaya. Wanasema: "Huwa tunakumbatia kukufuru kama njia halali ya kujieleza na kuonyesha uhuru wa mtu binafsi dhidi ya imani za kitamaduni zisizo na tija." "Msimamo wa Satanic Temple ni kwamba dini inaweza, na inafaa kutenganishwa na ushirikina. Hivyo basi, huwa hawaendelezi imani katika Shetani binafsi. "Kukumbatia jina la Shetani ni kukumbatia mtazamo wa kutumia fikira na kujiondoa kutoka katika mfumo wa kuamini katika nguvu za kipekee za kutoka nje ya dunia na utamaduni uliopitwa na wakati wenye msingi wake katika ushirikina."
    BAPHOMET: SANAMU LA SHETANI LILILOLETA UTATA NCHINI MAREKANI. Binadamu tangu zama za kale amekuwa akijenga, kuchonga na kuweka sanamu za aina nyingi kwa sababu mbalimbali. Baadhi hutumiwa kuwaenzi watu maarufu na kuwakumbuka, na nyingine huabudiwa kama miungu. Kwa muda mrefu hata hivyo imekuwa ni nadra kuona sanamu ambayo moja kwa moja inahusishwa na shetani au ibilisi. Lakini ukifika Marekani, mambo ni tofauti. Kuna sanamu moja kubwa ya shaba ambayo inahusishwa na ushetani. Ni sanamu ya, Baphomet ni kiumbe mwenye kichwa kinachofanana na cha mbuzi lakini ameongezwa maungo ya ajabu. Ni kiumbe mwenye mabawa, na kwenye sanamu hiyo inayotumiwa kwa sasa huoneshwa akiwa na watoto wawili wanaotabasamu. Sanamu inayotumiwa kwa sasa ina urefu wa karibu futi 9, na iligharimu $100,000 (£64,000) kuitengeneza. Sanamu hii imekuwa ikitumiwa kuwapiga vita wale walio na imani za Kikristo kiislamu na imani nyingine zenye kumcha Mungu mmoja. Ni sanamu hii ambayo imekuwa ikitumiwa kuendesha vita dhidi ya kuwekwa kwa sanamu za Kikristo na dini nyingine katika majengo maarufu, bustani na maeneo ya umma nchini Marekani. Agosti 17, sanamu hiyo ya kiumbe anayefahamika kama Baphomet ilipelekwa katika jimbo la Arkansas anakotoka Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton. Wanaotumia sanamu hiyo ni watu wa kundi linalofahamika kama Satanic Temple (Hekalu la Shetani) ambalo ni kundi la 'kidini' na kisiasa ambalo hupinga kuingizwa kwa dini katika masuala ya Serikali. Kundi hilo liliandaa maandamano ya watu 150 waliyojumuisha waabudu shetani, watu wasioamini Mungu yupo, na Wakristo pia. Maandamano hayo yalifanyika nje ya jengo lililo Makao Makuu ya jimbo la Arkansas katika mji wa Little Rock. Walikuwa wamekerwa na hatua ya kuweka sanamu ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu katika uwanja wa Makao Makuu hayo. Satanic Temple walisema sanamu hiyo inakiuka Sheria ya Kwanza ya Marekebisho ya Katiba nchini Marekani ambayo huzungumzia uhuru na haki za kidini. "Ikiwa utakubaliana na kuwepo kwa sanamu ya dini moja basi kunafaa kuwa na uhuru kwa wengine kuweka sanamu za kidini, na ukizuia basi kusiwe na sanamu yoyote ile," mwanzilishi mwenza wa tawi la Satanic Temple katika jimbo la Arkansas, Ivy Forrester, alinukuliwa na wanahabari siku hiyo ya maandamano. Ndoto yao ni kuwa na sanamu ya kudumu, lakini siku hiyo hawakuruhusiwa na sheria kuiweka kwa muda mrefu. Kuna sheria ya Arkansas ya mwaka 2017 inayohitaji sanamu ya kuwekwa maeneo ya Serikali iwe na udhamini wa Mbunge ambaye atawasilisha mswada iidhinishwe kupitia Bunge. Sanamu hiyo ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu ilidhaminiwa na mwanasiasa wa Republican, Seneta Jason Rapert. Hata hivyo, chini ya saa 24 baada ya kuwekwa, mwanamume mmoja alivurumisha gari na kuugonga mnara huo na kuubomoa. Maandamano ya Satanic Temple Arkansas yalisababisha kuandaliwa kwa maandamano mengine ya kuwapinga yaliyoandaliwa na makundi ya Kikristo na Wanachama wa Republican. Wakristo walikuwa wamebeba karatasi zilizokuwa na ujumbe kutoka kwenye Biblia. Satanic Temple waliwasilisha ombi la kushirikishwa kwenye kesi ya kupinga mnara huo wa Amri Kumi za Mungu iliyowasilishwa na shirika la haki za kiraia la American Civil Liberties Union, lakini kundi hilo limewasilisha ombi kutaka wasishirikishwe kwenye kesi hiyo. Sanamu hiyo ya Baphomet ilizinduliwa mara ya kwanza katika mji wa Detroit, Michigan. Mipango ya kuuweka nje ya Makao Makuu ya jimbo la Oklahoma ambapo kulikuwa kumewekwa mnara mwingine wa Amri Kumi za Mungu mwaka 2015. Mnara huo ulizinduliwa Julai 25 Mwaka huo, ambapo kupitia taarifa yao, Satanic temple walisema: "Tulichagua Baphomet kwa sababu ni kiumbe ambaye huhusishwa na Shetani na maana inayohusishwa naye inafaa sana akiwekwa kando na Sanamu inayowakilisha dini nyingine." Sherehe ya kuizindua ilikuwa ya faragha, na ukumbi uliotumiwa uliwekwa siri kubwa kwani Wakristo walikuwa wameandamana awali kuipinga mjini. Picha zilizopakiwa kwenye Facebook zilionyesha uzinduzi wake ulifanyika karibu na Mto wa Detroit. Kabla ya uzinduzi huo kufanyika, waumini takriban 200 walihudhuria ibada ya misa katika kanisa la St. Joseph mjini humo kupinga sanamu hiyo. Wengine 50 walifanya maombi mjini katika eneo ambalo awali Satanic Temple walikuwa wamepanga kuuzindulia mnara huo hapo. Mwanamume yule yule aliyeuharibu mnara wa Arkansas anadaiwa kufanya vivyo hivyo na kuubomoa mnara mwingine kama huo wa Amri Kumi za Mungu nje ya Makao Makuu ya jimbo la Oklahoma. Satanic Temple walisitisha juhudi zao za kutaka kuweka sanamu ya Baphomet huko baada ya Mahakama ya Juu ya Oklahoma kuamua kwamba Sanamu ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu ilikuwa imewekwa kinyume cha sheria, hivyo wakawa wameshinda vita bila kupigana. Mahakama ilisema ni kinyume cha sheria kutumia mali ya umma kwa manufaa ya dini yoyote ile. Jina hili Baphomet, asili yake ni enzi ya kukomesha uasi katika Kanisa Katoliki katika miaka ya 1100, kwa Kiingereza "Inquisition", na kuteswa kwa wapiganaji wa kidini kwa jina la "Knights Templar" waliokuwa wanateswa ili wafichue siri zao na wakubali kuifuata dini kwa mujibu wa viongozi wa kanisa wa wakati huo. Kwa mujibu wa waandishi wa enzi za vita vya kidini maarufu kama Crusade, wapiganaji hao walikiri kumuabudu Mungu wa wapagani kwa jina la Baphometh. Baadhi ya wasomi hata hivyo huamini kwamba "Baphometh" ni upotoshaji wa jina "Mahomet" - ambalo hutumiwa kumrejelea Nabii Muhammad, jambo linalozua utata zaidi. Lakini kadiri miaka ilivyosonga na mafumbo na siri kuhusu Utata wa Knights Templar kuzidi, ndivyo ufafanuzi wa neno hilo na maana yake ulivyozidi kutofautiana. Moja ya tafsiri ya neno hilo inapatikana katika kitabu cha "Da Vinci Code" cha ,Dan Brown, ambapo, neno Baphomet limefafanuliwa na kutafsiriwa kama "Sophia" au busara. Picha maarufu zaidi ya Baphomet ilichorwa na mzungu wa Ufaransa aitwaye , Eliphas Levi, mwaka 1856 katika kitabu chake cha Transcendental Magic: Its Doctrine and Ritual. Alichora kiumbe mwenye mabawa na mwenye pembe na mwenge ulio katikati ya pembe hizo kichwani. Kuna mchoro pia wa pembe nane kwenye paji la uso. Mikononi kumeandikwa maneno ya Kilatino SOLVE (tenganishwa) na COAGULA (fungamanisha) - ambazo ni nguvu za kuunganisha na kutenganisha ambazo zilitwaliwa kutoka kwa Mungu. Mchoro wa Levi ulihamasisha zaidi sanamu inayotumiwa na Satanic Temple. Ni jinsia mbili kwa pamoja, nusu mnyama na nusu binadamu.anapiga saluti ya vidole viwili Sanamu hiyo ina vidole viwili vilivyoelekezwa juu mkono wa kulia na viwili vinavyoelekezwa chini mkono wa kushoto, maana yake "kama ilivyo juu, na chini iwe pia". Maneno hayo na ishara hiyo ya vidole ni maarufu miongoni mwa wenye kuamini katika mizungu na mafumbo. Chanzo chake ni kazi za kale za msomi Hermes Trismegistus, ambaye vitabu vyake vilikuwa maarufu sana enzi ya Kipindi cha mwamko wa sanaa na mageuzi ya kidini, maarufu kama "Renaissance and Reformation" barani Ulaya. Maneno hayo pia hutumiwa kuhusiana na sayansi, vitu vyote na Mungu, lakini Levi aliandika kwamba kwa kutumia ishara hiyo, Baphomet wake alikuwa anaashiria kuwiana sawa kwa fadhila na haki. Lakini maana yake halisi ni kwamba ,shetani anatawala duniani na Mungu anatawala juu. Lucien Greaves, msemaji wa Satanic Temple anasema "lengo lao ni kwamba watoto watatazama kazi hiyo ya sanaa kama kwa usalama, ni sanamu isiyofaa kuzua wasiwasi wowote. "Sura ya mbuzi huyo haioneshi chochote. Si ya kishetani wala ya kutisha - kama wanavyodai baadhi ya watu - ukiitazama bila kuongozwa na mzigo wa utamaduni." "Sifikiri watoto wanaokutana na sanamu hii watatiwa hofu na propaganda wanaweza wasione chochote cha kuwatia wasiwasi," anasema Greaves. "Lakini si kwamba tunapinga kuwaingiza watoto kwenye mitazamo ya kidini. Mara nyingi watoto hulazimishwa kuingia kwenye dini. Hilo ni jambo hatutaki kulifanya kamwe." Kwenye tumbo la Baphomet kuna ishara ya kale ya Kigiriki ya nyoka wawili walio kwenye fimbo - fimbo ambayo ilibebwa na Hermes na maafisa wa kueneza matangazo au kutoa matangazo rasmi waliotumiwa kutoa matamko rasmi. Ishara hiyo kwenye sanamu hiyo inaashiria biashara, mashauriano na kutendeana, na iliingizwa kwenye Baphomet na Levi. "Kwetu ni ishara ya maridhiano ya vitu viwili tofauti - kwa mfano kuwa na sanamu ya Kishetani karibu na sanamu ya Kikristo," anasema Greaves. "Tunafikiri ni ujumbe wenye nguvu sana kuwa na sanamu hii ikiwa karibu na sanamu ya Amri Kumi za Mungu. Unaweza kuwa na mambo mawili tofauti kwa pamoja bila mzozo." Baphomet wa Levi alikuwa ni mwenye maziwa, lakini "tuliyaondoa maziwa hayo" anasema Greaves. Anasema hatukutaka wajipachike kwenye mdahalo kuhusu jinsia ya kiumbe huyo wao jambo ambalo lingewafanya watu kupoteza maana halisi. Badala yake anasema watoto wawili, mvulana na msichana, ndio wanaowakilisha jinsia. Kwa maana iliyojificha Greaves anashindwa kusema kwamba watoto hao wawili wa kike na kiume wanawakilisha ulimwengu wote na hawa ni Adam na Hawa, Kwenye paji la uso la Baphomet na kwenye kiti cha enzi alichokikalia kuna mchoro wa nyota ya pembe tano, ishara ambayo mara nyingi hutambuliwa kama ishara ya shetani. Mara nyingi huonekana ikiwa imepinduliwa. Msalaba wa Peter pia hupinduliwa. Greaves anasema lengo lao ni kuwafanya watu wabadilishe mtazamo wao na kuacha kuongozwa na waliyofunzwa na utamaduni wao. Waangazie mambo kwa kuzingatia ushahidi uliopo. Anasema mtazamo huo huwazuia watu kuchukua msimamo huru kuhusu masuala kama vile ndoa za wapenzi wa jinsia moja na haki za kutoa mimba pamoja na huduma nyingine za uzazi wa mpango. "Mwenge wa maarifa ndio kama upembe wa kati na inatukuza juhudi za kutafuta elimu na maarifa. Tunathamini hilo sana," anasema Greaves. Levi mwenyewe aliandika kwamba mwenge wa maarifa uolikuwa unawaka katikati ya pembe za Baphomet ni mwanga wa kusawazisha vitu vyote. Ni taswira ya roho iliyo juu ya vitu vyote vinavyoonekana, kama zilivyo ndimi za moto, ingawa bado imeunganishwa na vitu hivyo, mfano moto unavyoendelea kung'aa juu ya mafuta au kijiti. Kulikuwa na mpango wa kuongeza maandiko kwenye mchoro wa nyota ya pembe tano ya moja ya nguzo saba kuu za Satanic Temple: "moyo wa huruma, busara na haki unafaa daima kuongoza zaidi ya neno lililoandikwa au kutamkwa." Nyuma ya sanamu hiyo, kutakuwa na nukuu kutoka kwa kitabu cha Cain chake Lord Byron unaosema: "Kisha, nani alikuwa Ibilisi? Yule hangekuruhusu wewe uishi milele, au yule ambaye angelikuumba uishi milele, katika raha na nguvu za elimu na maarifa?" Kwa mujibu wa tovuti yao Satanic Temple wanaamini kwamba "kimsingi watu kuteseka au kuumia ni vibaya, na chochote kile kinachopunguza madhila na mateso ni kizuri." Hawaamini katika kutenda mabaya. Wanasema: "Huwa tunakumbatia kukufuru kama njia halali ya kujieleza na kuonyesha uhuru wa mtu binafsi dhidi ya imani za kitamaduni zisizo na tija." "Msimamo wa Satanic Temple ni kwamba dini inaweza, na inafaa kutenganishwa na ushirikina. Hivyo basi, huwa hawaendelezi imani katika Shetani binafsi. "Kukumbatia jina la Shetani ni kukumbatia mtazamo wa kutumia fikira na kujiondoa kutoka katika mfumo wa kuamini katika nguvu za kipekee za kutoka nje ya dunia na utamaduni uliopitwa na wakati wenye msingi wake katika ushirikina."
    ·294 Views
  • MUONEKANO WA NABII ISSA MIAKA HIYO ULIKUWAJE ?

    Karibu kila mtu ana dhana fulani kuhusu muonekano wa Yesu Kristo.
    Ndiye mtu aliyechorwa zaidi katika sanaa ya Magharibi. Picha zake hutambuliwa kwa urahisi, ambapo huoneshwa akiwa na nywele na ndevu, akiwa amevalia vazi lefu lenye mikono mirefu linalofanana na kanzu ( la rangi nyeupe), na pia akiwa amejifunga joho (la rangi ya samawati). Muonekano wa Yesu umefahamika sana na wengi kiasi kwamba unaweza kutambuliwa ukiwa hata kwenye mikate au biskuti.

    Picha za sasa za Yesu zinatokana na enzi ya Byzantine, himaya iliyokuwa na mji mkuu wake Constantinople. Ni picha iliyoanza kutumika karne ya nne hivi. Michoro ya Yesu ya wakati wa utawala wa Byzantine ilikuwa ya ishara, na si muonekano wake. Wasanii waliangazia zaidi maana na si kumfananisha na Yesu mwenyewe.
    Picha zao ziliongozwa na dhana ya Yesu kama mtawala, kwenye kiti cha enzi, kama anavyoonyeshwa kwenye mchoro ulio kwenye altari ya kanisa la Santa Pudenziana jijini Roma.

    Yesu anaoneshwa akiwa amevalia mgolole wa rangi ya dhahabu.
    Ndiye mtawala wa dunia yote aliyetoka mbinguni, mfanano wa picha yake ni ule wa sanamu ya Zeus wa Olympus anayeonyeshwa akiwa na nywele ndefu za ndevu kwenye kiti cha enzi. Ni sanamu iliyokuwa maarufu sana wakati huo kiasi kwamba Mfalme Augustus wa Roma alishurutisha naye atengenezewe sanamu kama hiyo, lakini yake ikiwa bila nywele ndefu na ndevu, Wasanii wa Byzantine, walitaka kumuonyesha Kristo kama mtawala kutoka mbinguni, mfalme wa aina yake, na hivyo wakachora wakimuonyesha kama Zeus, lakini akiwa mdogo kidogo wa umri.

    Kilichotokea kadiri miaka ilivyosonga ni kwamba kuonyeshwa huku kwa Kristo kama mtawala kutoka mbinguni - ambapo wakati mwingine ameonyeshwa hata akiwa kama 'hippie' au 'superstar' (kama ilivyo kwenye mchoro huu hapa chini) - ndiko kumekuwa kama kigezo chetu cha Yesu alivyokuwa. Hebu tuchanganue kutoka kichwani hadi vidole vya miguuni. Wakristo wa nyakati za kwanza wakati walipokuwa wanamwonyesha Kristo si kama mtawala kutoka mbinguni, walimuonyesha kama binadamu wa kawaida tu - akiwa hana ndevu na hana nywele ndefu.

    Lakini pengine, kama msomi wa aina yake aliyekuwa akisafiri kutoka eneo moja hadi jingine, Yesu pengine alikuwa na ndevu, kwa sababu hakuwa akienda kwa vinyozi. Kwa kawaida, kuwa mchafu kiasi na kuwa na ndevu ndefu ni sifa ambazo zilihusishwa na wanafalsafa, wasomi wa ngazi ya juu, na kuwatenganisha na watu wa kawaida.
    Mwanafalsafa maarufu wa kundi la Stoic (Wanafalsafa wa Kigiriki waliofuata mafundisho ya mwanzilishi wao Zeno wa Citium mjini Athens mapema karne ya 3 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu) Epictetus aliamini "ilifaa hivyo kwa mujibu wa maumbile." Mambo yalibadilika katika karne ya 1 baada ya kuzaliwa kwa Yesu, wakati wa enzi za Warumi na Wagiriki, ambapo kuwa na nywele fupi na kunyoa ndefu ndiyo mambo yaliyochukuliwa kuwa yafaayo na ya kistaarabu.

    Kuwa na nywele ndefu na ndevu ni mambo ambayo yaliachiwa miungu pekee, si ya watu wa kawaida. Hata wanafalsafa enzi hizo walikuwa na nywele fupi. Ndevu pia hazikuwa sifa za kuwatambulisha Wayahudi enzi hizo. Ukweli ni kwamba moja ya changamoto ambazo waliotaka kuwatesa Wayahudi vipindi mbalimbali katika historia walihangaika sana kuwatofautisha na watu wengine. Hii ni kwa sababu wote walifanana (jambo ambalo limegusiwa katika kitabu cha Wamakabayo). Hata hivyo, picha za wanaume wa Kiyahudi zilizokuwa kwenye sarafu za Judea Capta ambazo zilitolewa na utawala wa Roma baada ya kutekwa kwa mji wa Yerusalemu mwaka 70 baada ya kuzaliwa kwa Yesu zinawaonesha wanaume wakiwa na ndevu, lakini nywele zao si ndefu.

    Kwa hivyo, Yesu, kama mwanafalsafa wa muonekano wa kawaida, kuna uwezekano alikuwa na ndevu lakini si ndefu sana, sawa na wanaume hao walioonyeshwa kwenye sarafu za Judaea Capta, lakini nywele zake basi hazikuwa ndefu sana pia.
    Kama ingetokea kwamba awe na nywele ndefu hata kidogo tu kuliko kawaida, basi angezua mtafaruku Wanaume wa Kiyahudi waliokuwa na ndevu ambazo hazikuwa zimetunzwa vyema na nywele ambazo zilikuwa ndefu kidogo kuliko kawaida walitambulika mara moja kama watu waliokuwa wamekula kiapo cha kuwa Wanazari (Nazarite).

    Hii ilikuwa na maana kwamba wangejitoa wakfu kwa Mungu kwa kipindi fulani, ambapo hawangekunywa vileo wala kuzikata nywele zao. Mwisho wa kipindi hicho, wangenyolewa nywele zao katika sherehe maalum hekaluni Jerusalem (kama inavyoelezwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Sura ya 21, aya ya 24).
    Lakini Yesu hakuwa amekula kiapo cha kuwa Mnazari, kwa sababu mara nyingi tunamsikia kwenye Biblia akinywa divai - wakosoaji wake hata wakati mwingine wanamshutumu kwa kunywa divai sana, kupita kiasi (Matayo Sura ya 11, aya ya 19). Kama angekuwepo na nywele ndefu, na kuonekana kama Mnazari, tungelitarajia basi kuwepo na tamko pahala fulani kuhusu tofauti ya muonekano wake na matendo aliyokuwa akiyafanya ambayo hayakuendana na Unazari. Hali kwamba alikuwa akinywa divai yenyewe ingekuwa tatizo kubwa.

    Wakati Yesu alipoishi, matajiri walizoea kuvalia kanzu na majoyo ya vitambaa vya thamani, kuonyesha hadhi yao katika jamii. Katika moja ya mahubiri yake, Yesu anasema : "Jihadharini na walimu wa sheria (waandishi). Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu (stolai), na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Pia wao hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kupewa nafasi za heshima katika karamu." Mafundisho haya ya Yesu kwa kawaida huchukuliwa kama yenye maelezo ya kuaminika zaidi kwenye Injili, hivyo tunaweza kuwa na msingi kuamini kwamba Yesu hakuvalia mavazi kama hayo marefu. Kwa jumla, mwanamume wakati huo wa Yesu angevalia gwanda au kanzu fupi hivi, na mwanamke angevalia vazi lililomfika kwenye kifundo cha mguu.

    Kwa hivyo, katika karne ya 2 kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume, Paul na Thecla, inapotokea kwamba Thecla ambaye ni mwanamke anavalia kanzu fupi kama mwanamume, hilo ni jambo linaloshangaza sana. Kanzu hizi kwa kawaida zingekuwa na ukanda au mstari wa rangi tofauti kutoka kwenye bega hadi kwenye pindo sehemu ya chini. Ni vazi ambalo lingeshonwa au kufumwa kama kipande kimoja cha vazi. Juu ya kanzu hiyo, ungejifunga joho au vazi jingine la nje, na tunajua kwamba Yesu alivalia vazi kama hilo kwa sababu ndilo lililoguswa na mwanamke aliyetaka kuponywa naye. (Marko 5:27): Alikuwa amesikia habari za Yesu, naye akaja kwa nyuma yake kwenye umati wa watu, akaligusa vazi lake, kwa maana alisema moyoni mwake, 'Kama nikiweza kuligusa vazi lake tu, nitaponywa.') Vazi hilo la nje lilifumwa kwa manyoya, lakini halikuwa zito sana na ndipo ili uhisi joto ingemlazimu mtu kuvalia mavazi mawili kama hayo.

    Vazi hilo lingevaliwa kwa njia nyingi, na wakati mwingine lingening'inia hadi chini ya magoti na kulifunika lile kanzu fupi la ndani. (Baadhi ya wanafalsafa walizoea kuvalia vazi hilo la nje pekee bila kuvalia ile kanzu ya ndani na kuacha sehemu ya bega au kifua ikiwa wazi). Mamlaka na hadhi ya mtu ni vitu ambavyo vilidhihirishwa kupitia ubora, ukubwa na rangi ya mavazi hayo ya nje. Rangi ya zambarau na baadhi ya aina za rangi ya buluu (samawati) ni rangi zilizoashiria utajiri, hadhi na kujionea fahari. Zilikuwa ni rangi za kifahari kwa sababu viungo vya kutengeneza rangi hizo vilikuwa adimu na ghali sana.

    Lakini rangi pia huashiria kitu kingine tofauti. Mwanahistoria Josephus, anawaeleza walokole waliofahamika kama Zealots (kundi la Wayahudi wa itikadi kali waliotaka kuwafurusha Warumi kutoka Judea) kama kundi la wahalifu wauaji waliovalia mavazi ya nje yaliyopakwa rangi kwa jina - mavazi anayoyaita chlanidia - kuashiria kwamba yalikuwa ni kama mavazi yaliyovaliwa na wanawake. Hii inaashiria kwamba wanaume kamili, kama hawakuwa na cheo cha juu zaidi katika jamii, walifaa kuvalia mavazi yasiyopakwa rangi.
    Yesu hakuvalia mavazi meupe hata hivyo. Haya yalikuwa mavazi ya kipekee na yalihitaji kupaushwa mara kwa mara (kufanywa meupe tena) au kupakwa chokaa. Judea, mavazi kama hayo meupe yalihusishwa na kundi lililofahamika kama Essenes - ambao ni watu waliofuata ufasiri mkali wa sheria za Kiyahudi. Tofauti kati ya mavazi ya Yesu na mavazi mengine ya rangi nyeupe ya kung'aa inaelezwa kwenye sura ya 9 ya Marko ambapo anaandamana na mitume watatu mlimani.

    Yesu aliwachukua "Petro, Yakobo na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao. Mavazi yake yakawa na weupe wa kuzima macho, meupe kuliko ambavyo mtu yeyote duniani angaliweza kuyangʼarisha. Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Yesu." Marko anaeleza kwamba mavazi ya Yesu yaligeuka rangi yakawa meupe sana, hapa anarejelea vazi la ndani na si la nje. Kabla ya kugeuka sura huku kwa Yesu, anaoneshwa na Marko kama mwanamume wa kawaida, aliyevalia mavazi ya kawaida, ambayo ni ya rangi ambayo haijapaushwa. Katika hali ambayo ndipo yang'ae na kuangaza unahitaji kumpelekea fundi.

    Tunaelezwa zaidi kuhusu mavazi ya Yesu wakati wa kusulubiwa kwake, pale wanajeshi wa Kirumi wanapoyakata mavazi yake ya nje vipande vinne (Yohana19:23: Askari walipokwisha kumsulubisha Yesu, walichukua nguo zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. Ila walikubaliana wasilichane lile vazi lake kwa maana lilikuwa halina mshono bali limefumwa tangu juu hadi chini.) Kuna uwezekano mavazi hayo ya nje yalikuwa mavazi mawili.

    Moja ya vazi hili huenda lilikuwa ni tallith, ambalo ni vazi la kujifunga Kiyahudi wakati wa maombi. Vazi hili lenye shada (tzitzith) limetajwa moja kwa moja na Yesu katika kitabu cha Mathayo 23:5 anapozungumza kuhusu walimu wa sheria na Mafarisayo (Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao). Lilikuwa ni vazi la nje lisilo zito, ambalo kawaida lilitengenezwa kwa kitambaa cha manyoya na lilikuwa la rangi ya malai hivi (krimu), na pengine lilikuwa na ukanda au mstari wa rangi ya nili (bluu iliyoiva).

    Miguuni, Yesu angevalia ndara (kandambili au malapa). Kila mtu wakati huo alivalia ndara. Katika mapango yaliyo jangwani karibu na Bahari ya Chumvi (Bahari Mfu) na Masada, ndara za wakati alipoishi Yesu zimegunduliwa, na tunaweza kutazama ndara ambazo huenda alivaa zilivyoonekana. Zilikuwa hazijafanyiwa kazi nyingi sana ya kiufundi. Soli (nyayo au kikanyagio) zake zilikuwa vipande vigumu vya ngozi vilivyoshonwa pamoja, na juu kulikuwa ni kanda za ngozi ambazo mbele zingeingizwa katikati ya vidole, kama malapa tu ya siku hizi.

    Yesu (Nabii Issa) Alikuwa Myahudi, na uso wake pia bila shaka ungefanana na Wayahudi wa wakati huo. Hali kwamba Yesu alikuwa Myahudi (au Mjudea) ni jambo linalorejelewa katika vitabu vingi, zikiwemo barua za Mtume Paulo. Na katika barua yake kwa Waebrania, anaandika: "Kwa maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika uzao wa Yuda" (Sura ya 7:14) Kwa hivyo, Myahudi wa wakati huo, mwanamume wa miaka 30 hivi alipoanza kueneza Injili kwa mujibu wa Luka 3, pia akiwa ni mwenye ngozi nyeusi kama ilivyokuwa kwa wayahudi wengi zama zile waliokuwa wakitembeleana na ndugu zao wa Misri (Kushi) kemet.

    Mwaka 2001 mwanaantholopojia (mtaalamu wa elimu ya binadamu hasa elimu ihusuyo habari zinazohusu asili na maendeleo yake ya awali) Richard Neave alitengeneza mfano wa mwanamume wa Galilaya wa zama za Yesu ambao ulitumiwa kwa jina Son of God (Mwana wa Mungu). Alitumia fuvu lililopatikana katika eneo hilo. Hakusema kwamba huo ulikuwa muonekano wa uso wa Yesu. Mfano ulikuwa tu wa kuchochea hisia na kuwafanya watu kumfikiria Yesu kama mwanamume wa zama hizo na eneo hilo, kwa sababu hakuna mchoro wala maelezo yaliyopo ya kina kuhusu muonekano wake halisi.

    Ingawa tunaweza kupata viashiria kutoka kwa teknolojia na kutumia mifupa ya watu wa kale, kiashiria cha karibu sana kuhusu pengine Yesu alionekana vipi labda kinaweza kutokana na mchoro wa Musa kwenye ukuta wa sinagogi ya karne ya 3 ya Dura-Europos, kwani mchoro huo unaonesha jinsi Myahudi wa hekima alidhaniwa kuwa wakati wa utawala wa Wagiriki na Warumi. Musa anaoneshwa akiwa na mavazi ambayo hayajapaushwa, na moja ya vazi lake la nje ni tallith.

    Katika mchoro huo wa Dura wa Musa akitenganisha maji kwenye Bahari ya Sham ili Waisraeli wapite, unaweza kuziona shada (tzitzith) kwenye kona za vazi hilo. Kwa kiwango kikubwa, picha hiyo pengine inatoa msingi bora zaidi wa kumfikiria Yesu alivyokuwa badala ya picha za sasa zinazoongozwa na busara na mawazo ya enzi ya Byzantine - alikuwa na nywele fupi, ndevu fupi, na alikuwa amevalia kanzu fupi lenye mikono mifupi, na alikuwa na joho au vazi la nje.

    Makala hii chimbuko lake ni makala ya Kiingereza ya Joan Taylor ambaye ni profesa wa kitivo cha Asili ya Ukristo na Hekalu la Pili la Wayahudi katika Chuo Kikuu cha King's College London na ndiye mwandishi wa kitabu kwa jina The Essenes, the Scrolls and the Dead Sea.
    MUONEKANO WA NABII ISSA MIAKA HIYO ULIKUWAJE ? Karibu kila mtu ana dhana fulani kuhusu muonekano wa Yesu Kristo. Ndiye mtu aliyechorwa zaidi katika sanaa ya Magharibi. Picha zake hutambuliwa kwa urahisi, ambapo huoneshwa akiwa na nywele na ndevu, akiwa amevalia vazi lefu lenye mikono mirefu linalofanana na kanzu ( la rangi nyeupe), na pia akiwa amejifunga joho (la rangi ya samawati). Muonekano wa Yesu umefahamika sana na wengi kiasi kwamba unaweza kutambuliwa ukiwa hata kwenye mikate au biskuti. Picha za sasa za Yesu zinatokana na enzi ya Byzantine, himaya iliyokuwa na mji mkuu wake Constantinople. Ni picha iliyoanza kutumika karne ya nne hivi. Michoro ya Yesu ya wakati wa utawala wa Byzantine ilikuwa ya ishara, na si muonekano wake. Wasanii waliangazia zaidi maana na si kumfananisha na Yesu mwenyewe. Picha zao ziliongozwa na dhana ya Yesu kama mtawala, kwenye kiti cha enzi, kama anavyoonyeshwa kwenye mchoro ulio kwenye altari ya kanisa la Santa Pudenziana jijini Roma. Yesu anaoneshwa akiwa amevalia mgolole wa rangi ya dhahabu. Ndiye mtawala wa dunia yote aliyetoka mbinguni, mfanano wa picha yake ni ule wa sanamu ya Zeus wa Olympus anayeonyeshwa akiwa na nywele ndefu za ndevu kwenye kiti cha enzi. Ni sanamu iliyokuwa maarufu sana wakati huo kiasi kwamba Mfalme Augustus wa Roma alishurutisha naye atengenezewe sanamu kama hiyo, lakini yake ikiwa bila nywele ndefu na ndevu, Wasanii wa Byzantine, walitaka kumuonyesha Kristo kama mtawala kutoka mbinguni, mfalme wa aina yake, na hivyo wakachora wakimuonyesha kama Zeus, lakini akiwa mdogo kidogo wa umri. Kilichotokea kadiri miaka ilivyosonga ni kwamba kuonyeshwa huku kwa Kristo kama mtawala kutoka mbinguni - ambapo wakati mwingine ameonyeshwa hata akiwa kama 'hippie' au 'superstar' (kama ilivyo kwenye mchoro huu hapa chini) - ndiko kumekuwa kama kigezo chetu cha Yesu alivyokuwa. Hebu tuchanganue kutoka kichwani hadi vidole vya miguuni. Wakristo wa nyakati za kwanza wakati walipokuwa wanamwonyesha Kristo si kama mtawala kutoka mbinguni, walimuonyesha kama binadamu wa kawaida tu - akiwa hana ndevu na hana nywele ndefu. Lakini pengine, kama msomi wa aina yake aliyekuwa akisafiri kutoka eneo moja hadi jingine, Yesu pengine alikuwa na ndevu, kwa sababu hakuwa akienda kwa vinyozi. Kwa kawaida, kuwa mchafu kiasi na kuwa na ndevu ndefu ni sifa ambazo zilihusishwa na wanafalsafa, wasomi wa ngazi ya juu, na kuwatenganisha na watu wa kawaida. Mwanafalsafa maarufu wa kundi la Stoic (Wanafalsafa wa Kigiriki waliofuata mafundisho ya mwanzilishi wao Zeno wa Citium mjini Athens mapema karne ya 3 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu) Epictetus aliamini "ilifaa hivyo kwa mujibu wa maumbile." Mambo yalibadilika katika karne ya 1 baada ya kuzaliwa kwa Yesu, wakati wa enzi za Warumi na Wagiriki, ambapo kuwa na nywele fupi na kunyoa ndefu ndiyo mambo yaliyochukuliwa kuwa yafaayo na ya kistaarabu. Kuwa na nywele ndefu na ndevu ni mambo ambayo yaliachiwa miungu pekee, si ya watu wa kawaida. Hata wanafalsafa enzi hizo walikuwa na nywele fupi. Ndevu pia hazikuwa sifa za kuwatambulisha Wayahudi enzi hizo. Ukweli ni kwamba moja ya changamoto ambazo waliotaka kuwatesa Wayahudi vipindi mbalimbali katika historia walihangaika sana kuwatofautisha na watu wengine. Hii ni kwa sababu wote walifanana (jambo ambalo limegusiwa katika kitabu cha Wamakabayo). Hata hivyo, picha za wanaume wa Kiyahudi zilizokuwa kwenye sarafu za Judea Capta ambazo zilitolewa na utawala wa Roma baada ya kutekwa kwa mji wa Yerusalemu mwaka 70 baada ya kuzaliwa kwa Yesu zinawaonesha wanaume wakiwa na ndevu, lakini nywele zao si ndefu. Kwa hivyo, Yesu, kama mwanafalsafa wa muonekano wa kawaida, kuna uwezekano alikuwa na ndevu lakini si ndefu sana, sawa na wanaume hao walioonyeshwa kwenye sarafu za Judaea Capta, lakini nywele zake basi hazikuwa ndefu sana pia. Kama ingetokea kwamba awe na nywele ndefu hata kidogo tu kuliko kawaida, basi angezua mtafaruku Wanaume wa Kiyahudi waliokuwa na ndevu ambazo hazikuwa zimetunzwa vyema na nywele ambazo zilikuwa ndefu kidogo kuliko kawaida walitambulika mara moja kama watu waliokuwa wamekula kiapo cha kuwa Wanazari (Nazarite). Hii ilikuwa na maana kwamba wangejitoa wakfu kwa Mungu kwa kipindi fulani, ambapo hawangekunywa vileo wala kuzikata nywele zao. Mwisho wa kipindi hicho, wangenyolewa nywele zao katika sherehe maalum hekaluni Jerusalem (kama inavyoelezwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Sura ya 21, aya ya 24). Lakini Yesu hakuwa amekula kiapo cha kuwa Mnazari, kwa sababu mara nyingi tunamsikia kwenye Biblia akinywa divai - wakosoaji wake hata wakati mwingine wanamshutumu kwa kunywa divai sana, kupita kiasi (Matayo Sura ya 11, aya ya 19). Kama angekuwepo na nywele ndefu, na kuonekana kama Mnazari, tungelitarajia basi kuwepo na tamko pahala fulani kuhusu tofauti ya muonekano wake na matendo aliyokuwa akiyafanya ambayo hayakuendana na Unazari. Hali kwamba alikuwa akinywa divai yenyewe ingekuwa tatizo kubwa. Wakati Yesu alipoishi, matajiri walizoea kuvalia kanzu na majoyo ya vitambaa vya thamani, kuonyesha hadhi yao katika jamii. Katika moja ya mahubiri yake, Yesu anasema : "Jihadharini na walimu wa sheria (waandishi). Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu (stolai), na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Pia wao hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kupewa nafasi za heshima katika karamu." Mafundisho haya ya Yesu kwa kawaida huchukuliwa kama yenye maelezo ya kuaminika zaidi kwenye Injili, hivyo tunaweza kuwa na msingi kuamini kwamba Yesu hakuvalia mavazi kama hayo marefu. Kwa jumla, mwanamume wakati huo wa Yesu angevalia gwanda au kanzu fupi hivi, na mwanamke angevalia vazi lililomfika kwenye kifundo cha mguu. Kwa hivyo, katika karne ya 2 kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume, Paul na Thecla, inapotokea kwamba Thecla ambaye ni mwanamke anavalia kanzu fupi kama mwanamume, hilo ni jambo linaloshangaza sana. Kanzu hizi kwa kawaida zingekuwa na ukanda au mstari wa rangi tofauti kutoka kwenye bega hadi kwenye pindo sehemu ya chini. Ni vazi ambalo lingeshonwa au kufumwa kama kipande kimoja cha vazi. Juu ya kanzu hiyo, ungejifunga joho au vazi jingine la nje, na tunajua kwamba Yesu alivalia vazi kama hilo kwa sababu ndilo lililoguswa na mwanamke aliyetaka kuponywa naye. (Marko 5:27): Alikuwa amesikia habari za Yesu, naye akaja kwa nyuma yake kwenye umati wa watu, akaligusa vazi lake, kwa maana alisema moyoni mwake, 'Kama nikiweza kuligusa vazi lake tu, nitaponywa.') Vazi hilo la nje lilifumwa kwa manyoya, lakini halikuwa zito sana na ndipo ili uhisi joto ingemlazimu mtu kuvalia mavazi mawili kama hayo. Vazi hilo lingevaliwa kwa njia nyingi, na wakati mwingine lingening'inia hadi chini ya magoti na kulifunika lile kanzu fupi la ndani. (Baadhi ya wanafalsafa walizoea kuvalia vazi hilo la nje pekee bila kuvalia ile kanzu ya ndani na kuacha sehemu ya bega au kifua ikiwa wazi). Mamlaka na hadhi ya mtu ni vitu ambavyo vilidhihirishwa kupitia ubora, ukubwa na rangi ya mavazi hayo ya nje. Rangi ya zambarau na baadhi ya aina za rangi ya buluu (samawati) ni rangi zilizoashiria utajiri, hadhi na kujionea fahari. Zilikuwa ni rangi za kifahari kwa sababu viungo vya kutengeneza rangi hizo vilikuwa adimu na ghali sana. Lakini rangi pia huashiria kitu kingine tofauti. Mwanahistoria Josephus, anawaeleza walokole waliofahamika kama Zealots (kundi la Wayahudi wa itikadi kali waliotaka kuwafurusha Warumi kutoka Judea) kama kundi la wahalifu wauaji waliovalia mavazi ya nje yaliyopakwa rangi kwa jina - mavazi anayoyaita chlanidia - kuashiria kwamba yalikuwa ni kama mavazi yaliyovaliwa na wanawake. Hii inaashiria kwamba wanaume kamili, kama hawakuwa na cheo cha juu zaidi katika jamii, walifaa kuvalia mavazi yasiyopakwa rangi. Yesu hakuvalia mavazi meupe hata hivyo. Haya yalikuwa mavazi ya kipekee na yalihitaji kupaushwa mara kwa mara (kufanywa meupe tena) au kupakwa chokaa. Judea, mavazi kama hayo meupe yalihusishwa na kundi lililofahamika kama Essenes - ambao ni watu waliofuata ufasiri mkali wa sheria za Kiyahudi. Tofauti kati ya mavazi ya Yesu na mavazi mengine ya rangi nyeupe ya kung'aa inaelezwa kwenye sura ya 9 ya Marko ambapo anaandamana na mitume watatu mlimani. Yesu aliwachukua "Petro, Yakobo na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao. Mavazi yake yakawa na weupe wa kuzima macho, meupe kuliko ambavyo mtu yeyote duniani angaliweza kuyangʼarisha. Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Yesu." Marko anaeleza kwamba mavazi ya Yesu yaligeuka rangi yakawa meupe sana, hapa anarejelea vazi la ndani na si la nje. Kabla ya kugeuka sura huku kwa Yesu, anaoneshwa na Marko kama mwanamume wa kawaida, aliyevalia mavazi ya kawaida, ambayo ni ya rangi ambayo haijapaushwa. Katika hali ambayo ndipo yang'ae na kuangaza unahitaji kumpelekea fundi. Tunaelezwa zaidi kuhusu mavazi ya Yesu wakati wa kusulubiwa kwake, pale wanajeshi wa Kirumi wanapoyakata mavazi yake ya nje vipande vinne (Yohana19:23: Askari walipokwisha kumsulubisha Yesu, walichukua nguo zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. Ila walikubaliana wasilichane lile vazi lake kwa maana lilikuwa halina mshono bali limefumwa tangu juu hadi chini.) Kuna uwezekano mavazi hayo ya nje yalikuwa mavazi mawili. Moja ya vazi hili huenda lilikuwa ni tallith, ambalo ni vazi la kujifunga Kiyahudi wakati wa maombi. Vazi hili lenye shada (tzitzith) limetajwa moja kwa moja na Yesu katika kitabu cha Mathayo 23:5 anapozungumza kuhusu walimu wa sheria na Mafarisayo (Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao). Lilikuwa ni vazi la nje lisilo zito, ambalo kawaida lilitengenezwa kwa kitambaa cha manyoya na lilikuwa la rangi ya malai hivi (krimu), na pengine lilikuwa na ukanda au mstari wa rangi ya nili (bluu iliyoiva). Miguuni, Yesu angevalia ndara (kandambili au malapa). Kila mtu wakati huo alivalia ndara. Katika mapango yaliyo jangwani karibu na Bahari ya Chumvi (Bahari Mfu) na Masada, ndara za wakati alipoishi Yesu zimegunduliwa, na tunaweza kutazama ndara ambazo huenda alivaa zilivyoonekana. Zilikuwa hazijafanyiwa kazi nyingi sana ya kiufundi. Soli (nyayo au kikanyagio) zake zilikuwa vipande vigumu vya ngozi vilivyoshonwa pamoja, na juu kulikuwa ni kanda za ngozi ambazo mbele zingeingizwa katikati ya vidole, kama malapa tu ya siku hizi. Yesu (Nabii Issa) Alikuwa Myahudi, na uso wake pia bila shaka ungefanana na Wayahudi wa wakati huo. Hali kwamba Yesu alikuwa Myahudi (au Mjudea) ni jambo linalorejelewa katika vitabu vingi, zikiwemo barua za Mtume Paulo. Na katika barua yake kwa Waebrania, anaandika: "Kwa maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika uzao wa Yuda" (Sura ya 7:14) Kwa hivyo, Myahudi wa wakati huo, mwanamume wa miaka 30 hivi alipoanza kueneza Injili kwa mujibu wa Luka 3, pia akiwa ni mwenye ngozi nyeusi kama ilivyokuwa kwa wayahudi wengi zama zile waliokuwa wakitembeleana na ndugu zao wa Misri (Kushi) kemet. Mwaka 2001 mwanaantholopojia (mtaalamu wa elimu ya binadamu hasa elimu ihusuyo habari zinazohusu asili na maendeleo yake ya awali) Richard Neave alitengeneza mfano wa mwanamume wa Galilaya wa zama za Yesu ambao ulitumiwa kwa jina Son of God (Mwana wa Mungu). Alitumia fuvu lililopatikana katika eneo hilo. Hakusema kwamba huo ulikuwa muonekano wa uso wa Yesu. Mfano ulikuwa tu wa kuchochea hisia na kuwafanya watu kumfikiria Yesu kama mwanamume wa zama hizo na eneo hilo, kwa sababu hakuna mchoro wala maelezo yaliyopo ya kina kuhusu muonekano wake halisi. Ingawa tunaweza kupata viashiria kutoka kwa teknolojia na kutumia mifupa ya watu wa kale, kiashiria cha karibu sana kuhusu pengine Yesu alionekana vipi labda kinaweza kutokana na mchoro wa Musa kwenye ukuta wa sinagogi ya karne ya 3 ya Dura-Europos, kwani mchoro huo unaonesha jinsi Myahudi wa hekima alidhaniwa kuwa wakati wa utawala wa Wagiriki na Warumi. Musa anaoneshwa akiwa na mavazi ambayo hayajapaushwa, na moja ya vazi lake la nje ni tallith. Katika mchoro huo wa Dura wa Musa akitenganisha maji kwenye Bahari ya Sham ili Waisraeli wapite, unaweza kuziona shada (tzitzith) kwenye kona za vazi hilo. Kwa kiwango kikubwa, picha hiyo pengine inatoa msingi bora zaidi wa kumfikiria Yesu alivyokuwa badala ya picha za sasa zinazoongozwa na busara na mawazo ya enzi ya Byzantine - alikuwa na nywele fupi, ndevu fupi, na alikuwa amevalia kanzu fupi lenye mikono mifupi, na alikuwa na joho au vazi la nje. Makala hii chimbuko lake ni makala ya Kiingereza ya Joan Taylor ambaye ni profesa wa kitivo cha Asili ya Ukristo na Hekalu la Pili la Wayahudi katika Chuo Kikuu cha King's College London na ndiye mwandishi wa kitabu kwa jina The Essenes, the Scrolls and the Dead Sea.
    ·182 Views

  • MADA: KUWA AMBAYE MUNGU ANATAKA UWE, SIYO ANAYETAKA UWE...

    Ulimwengu daima utakuwa na sauti elfu zinazozungumza mara moja. Wengine watapiga kelele zaidi kuliko wengine, kila mmoja akijaribu kukuunda katika toleo ambalo linalingana na matarajio yao. Jamii itachora mistari na kujenga ua, ikikupa njia inayoonekana kuwa ya kawaida na salama, lakini salama haimaanishi sawa kila wakati. Utapewa mapendekezo, na utaonyeshwa barabara tofauti. Mtasikia sauti, na mtapewa dalili. Ninachotaka ujue ni kwamba kuna njia ambazo zinaonekana kuwa sawa, lakini mara nyingi zinakuongoza vibaya. Kwangu mimi, ukuaji wa kweli hauanzii katika faraja ya kuiga bali katika ujasiri wa kuamini sauti yako ya ndani; sauti ya Mungu. Wakati mwingine, sauti hii inaweza isikuambie unachotaka kusikia; bali inazungumza uzima katika maisha yako. Kuna moto unaowaka kipekee ndani yako, taa ambayo hakuna mtu mwingine anayeibeba, lakini unahitaji kumsikiliza mtu wako wa ndani ili uweze kuwa mwanaume/mwanamke. Kuiga kunaweza kuhisi kama kimbilio, lakini kunakuweka kwenye vivuli vya uzuri wa mtu mwingine. Ubinafsi wako ndio uwezo wako mkuu. Usiruhusu mtu yeyote akufanye ufanane naye; baadhi yao hata hawana furaha na wao wenyewe, lakini wanataka wewe kuwa kama wao. Jifunze kuwa mtu ambaye Mungu anataka uwe, si vile wao wanvyotaka uwe.

    Hakuna mtu mwingine kwenye sayari hii yote anayetazama maisha kupitia lenzi sawa na wewe. Makovu yako, ushindi wako, vita vyako vya kimya kimya, na ndoto zako zenye sauti kubwa ni vipande vya fumbo ambalo hakuna mtu mwingine anayeweza kulikamilisha. Ulimwengu unaweza kujaribu kukufanya unafaa, lakini kufaa kamwe haikuwa dhamira yako, Bali kusimama nje ya kufaa . Ninakutia moyo leo, "thubutu kuwa tofauti." Sisitiza uhalisi wako. Sema ukweli wako hata kama sauti yako inatetemeka. Tembea njia ambazo wengine huepuka. Ukuaji hutokea si wakati unalingana lakini wakati unapochanua, bila msamaha, katika ngozi yako mwenyewe. Njia ambayo watu husafiri kidogo inaweza kuhisi upweke wakati fulani, lakini ni kwenye barabara hii ambapo utakutana na utimilifu wa yule unayekusudiwa kuwa. Kuchanganya ndani ni kuishi, lakini kusimama nje ni kuishi. Kwa hiyo, kukua. Inuka zaidi ya kuiga na tegemea upekee wako. Ulimwengu unahitaji zawadi yako, toleo la kweli, lisilochujwa na lisiloweza kurudiwa. Tembea kwa ujasiri. Ongea bila woga. Na ukue kwenye nuru ambayo wewe tu unaweza kutupwa. Usiruhusu mtu yeyote akuinamishe na kuwa mtu mbaya, asiye na moyo, shetani,pepo, mwovu au asiye na maana; uwe yule ambaye Mungu alikuita uwe. Ikiwa watu hawapendi hivyo, wanaweza kuwa yeyote wapendavyo, lakini usiruhusu maoni yao matupu yakufanye uache njia ambayo Mungu amekutengenezea.

    Credit:
    Fr. Albert Nwosu
    MADA: KUWA AMBAYE MUNGU ANATAKA UWE, SIYO ANAYETAKA UWE... Ulimwengu daima utakuwa na sauti elfu zinazozungumza mara moja. Wengine watapiga kelele zaidi kuliko wengine, kila mmoja akijaribu kukuunda katika toleo ambalo linalingana na matarajio yao. Jamii itachora mistari na kujenga ua, ikikupa njia inayoonekana kuwa ya kawaida na salama, lakini salama haimaanishi sawa kila wakati. Utapewa mapendekezo, na utaonyeshwa barabara tofauti. Mtasikia sauti, na mtapewa dalili. Ninachotaka ujue ni kwamba kuna njia ambazo zinaonekana kuwa sawa, lakini mara nyingi zinakuongoza vibaya. Kwangu mimi, ukuaji wa kweli hauanzii katika faraja ya kuiga bali katika ujasiri wa kuamini sauti yako ya ndani; sauti ya Mungu. Wakati mwingine, sauti hii inaweza isikuambie unachotaka kusikia; bali inazungumza uzima katika maisha yako. Kuna moto unaowaka kipekee ndani yako, taa ambayo hakuna mtu mwingine anayeibeba, lakini unahitaji kumsikiliza mtu wako wa ndani ili uweze kuwa mwanaume/mwanamke. Kuiga kunaweza kuhisi kama kimbilio, lakini kunakuweka kwenye vivuli vya uzuri wa mtu mwingine. Ubinafsi wako ndio uwezo wako mkuu. Usiruhusu mtu yeyote akufanye ufanane naye; baadhi yao hata hawana furaha na wao wenyewe, lakini wanataka wewe kuwa kama wao. Jifunze kuwa mtu ambaye Mungu anataka uwe, si vile wao wanvyotaka uwe. Hakuna mtu mwingine kwenye sayari hii yote anayetazama maisha kupitia lenzi sawa na wewe. Makovu yako, ushindi wako, vita vyako vya kimya kimya, na ndoto zako zenye sauti kubwa ni vipande vya fumbo ambalo hakuna mtu mwingine anayeweza kulikamilisha. Ulimwengu unaweza kujaribu kukufanya unafaa, lakini kufaa kamwe haikuwa dhamira yako, Bali kusimama nje ya kufaa . Ninakutia moyo leo, "thubutu kuwa tofauti." Sisitiza uhalisi wako. Sema ukweli wako hata kama sauti yako inatetemeka. Tembea njia ambazo wengine huepuka. Ukuaji hutokea si wakati unalingana lakini wakati unapochanua, bila msamaha, katika ngozi yako mwenyewe. Njia ambayo watu husafiri kidogo inaweza kuhisi upweke wakati fulani, lakini ni kwenye barabara hii ambapo utakutana na utimilifu wa yule unayekusudiwa kuwa. Kuchanganya ndani ni kuishi, lakini kusimama nje ni kuishi. Kwa hiyo, kukua. Inuka zaidi ya kuiga na tegemea upekee wako. Ulimwengu unahitaji zawadi yako, toleo la kweli, lisilochujwa na lisiloweza kurudiwa. Tembea kwa ujasiri. Ongea bila woga. Na ukue kwenye nuru ambayo wewe tu unaweza kutupwa. Usiruhusu mtu yeyote akuinamishe na kuwa mtu mbaya, asiye na moyo, shetani,pepo, mwovu au asiye na maana; uwe yule ambaye Mungu alikuita uwe. Ikiwa watu hawapendi hivyo, wanaweza kuwa yeyote wapendavyo, lakini usiruhusu maoni yao matupu yakufanye uache njia ambayo Mungu amekutengenezea. Credit: Fr. Albert Nwosu
    Like
    Love
    2
    1 Comments ·156 Views
  • Mtandao wa Instagram kwa sasa unaruhusu kupanga ujumbe wako (DM) ujitume lini na saa ngapi yaani tarehe na saa maalum. Ili kufanikisha hilo, ni kwa kushikilia kwa muda mrefu kitufe cha “Send” kisha utapata "option" ya kuchagua tarehe na saa ambayo unataka message ijitume.

    Kipengele hiki kimeanza kwenye ujumbe wa maandishi pekee, lakini sio katika ujumbe (meseji) wa kutuma picha, video, na GIF. Kipengele hiki pia kinaruhusu kupanga hadi siku (29) mbele na kinaonyesha idadi ya ujumbe uliopangwa kwenye mazungumzo.

    Instagram imeongeza pia vipengele vingine kama kuhariri ujumbe, kuchora kwenye picha, na kutuma au kuonyesha mahali ulipo "Live Location".
    Mtandao wa Instagram kwa sasa unaruhusu kupanga ujumbe wako (DM) ujitume lini na saa ngapi yaani tarehe na saa maalum. Ili kufanikisha hilo, ni kwa kushikilia kwa muda mrefu kitufe cha “Send” kisha utapata "option" ya kuchagua tarehe na saa ambayo unataka message ijitume. Kipengele hiki kimeanza kwenye ujumbe wa maandishi pekee, lakini sio katika ujumbe (meseji) wa kutuma picha, video, na GIF. Kipengele hiki pia kinaruhusu kupanga hadi siku (29) mbele na kinaonyesha idadi ya ujumbe uliopangwa kwenye mazungumzo. Instagram imeongeza pia vipengele vingine kama kuhariri ujumbe, kuchora kwenye picha, na kutuma au kuonyesha mahali ulipo "Live Location".
    ·146 Views
  • Yamesemwa na Raya, Mke wa Barnaba Classic

    "Nimechoka nimechoka Mwanaume kila siku jipya ukiuliza kisa umeolewa na msanii? Hapana kwa kwel ifike muda nifanye maamuzi yangu binafsi mm sio wa kukuta dm za wasanii wakubwa wa kike ambao niliokua nacheka nao na kuheshimiana nao kumbe walikua wakinichora na kuninafikia hapana kwa kwel nimechoka nimechoka napitia mambo mengi sana napambana nayo ??

    Nimekuvumilia toka si lolole tulivumiliana kwa shida na raha na hata nilipokua nazo ulitumia sasa hivi umepata hela unaniona mm sio kitu ! Yani nimejifunza sitakuja kuanza tena na mwanaume chini tena Navumilia mambo mengi sana mpaka naitwa mgumba na bado nimekuvumilia umekua nani ww ?

    Unachelewa kurud kwasababu ya hao wanawake ifike pahala niseme imetosha nimechoka nimechoka kwa akili zangu timamu nasema hivi kwanzia leo mm na ww basi nimefika mwisho ukurasa nimeufunga nakuacha na maisha yako ya kua huru ufanye uhuni wako kwa amani Naona Heshima ya kuoa bado hujaijua ww ulikurupuka ww ni hayo tu Barnaba imetosha

    am official singleeeeeeeeeeeeeeeeeee Talaka yangu unajua pa kuipeleka Mama Kimbo mama angu ulikua ukiniambia kila siku lakini leo nimejionea imetosha sasa ! I’m single ready to mingleeeeeeeeeeeeeeeeeee"
    Yamesemwa na Raya, Mke wa Barnaba Classic "Nimechoka nimechoka Mwanaume kila siku jipya ukiuliza kisa umeolewa na msanii? Hapana kwa kwel ifike muda nifanye maamuzi yangu binafsi mm sio wa kukuta dm za wasanii wakubwa wa kike ambao niliokua nacheka nao na kuheshimiana nao kumbe walikua wakinichora na kuninafikia hapana kwa kwel nimechoka nimechoka napitia mambo mengi sana napambana nayo ?? Nimekuvumilia toka si lolole tulivumiliana kwa shida na raha na hata nilipokua nazo ulitumia sasa hivi umepata hela unaniona mm sio kitu ! Yani nimejifunza sitakuja kuanza tena na mwanaume chini tena Navumilia mambo mengi sana mpaka naitwa mgumba na bado nimekuvumilia umekua nani ww ? Unachelewa kurud kwasababu ya hao wanawake ifike pahala niseme imetosha nimechoka nimechoka kwa akili zangu timamu nasema hivi kwanzia leo mm na ww basi nimefika mwisho ukurasa nimeufunga nakuacha na maisha yako ya kua huru ufanye uhuni wako kwa amani Naona Heshima ya kuoa bado hujaijua ww ulikurupuka ww ni hayo tu Barnaba imetosha am official singleeeeeeeeeeeeeeeeeee Talaka yangu unajua pa kuipeleka Mama Kimbo mama angu ulikua ukiniambia kila siku lakini leo nimejionea imetosha sasa ! I’m single ready to mingleeeeeeeeeeeeeeeeeee"
    Like
    1
    ·246 Views
  • Maana za Tattoo:
    Watu, Miungu na viumbe vya kubuni

    Watu, iwe ni uso tu au mwili kamili, ni tattoo maarufu sana. Watu wengine huchora tattoo za mashujaa wao, wakati wengine huchagua viumbe vya hadithi na takwimu za kidini ambazo zina maana zaidi
    Maana za Tattoo: Watu, Miungu na viumbe vya kubuni Watu, iwe ni uso tu au mwili kamili, ni tattoo maarufu sana. Watu wengine huchora tattoo za mashujaa wao, wakati wengine huchagua viumbe vya hadithi na takwimu za kidini ambazo zina maana zaidi
    ·170 Views
  • Maana au ujumbe wa tattoo umewekwa kwa kuzingatia sehemu au mahali iliyochorwa hiyo tattoo, rangi iliyotumika kuichora hiyo tattoo, na mtindo uliotumika kuchora kwa tattoo husika
    Kabla hatujachambua orodha yetu ya tattoo maarafu na maana zake, unahitaji kujua mambo mengine ambayo ni muhimu
    1. Sehemu ambayo tattoo imechorwa au imekaa kwenye mwili ina maana kubwa, hasa kama ikiwa imewekwa au kuchorwa mahali fulani kwa ishara kama vile juu ya moyo, nyuma ya sikio au katika sehemu ya siri ya mwili.
    2. Rangi iliyotumika kuchora hiyo tattoo - rangi ya tattoo inaweza kubadilisha kabisa maana. Ua rose nyekundu inaashiria upendo wa kimapenzi na shauku, wakati Ua rose la bluu mara nyingi hutumika kuashiria upendo usioweza kupatikana.
    3. Mtindo uliotumika kuchora tattoo ina maana zaidi. Mfano tattoo ya simba dume kuwakilisha nguvu....au inaweza tu kuwa heshima.

    Huwezi kutambua maana halisi ya tattoo kwa kuiangalia pekee. Ni vyema ukauliza maana kwa mtu mwenye tattoo hiyo ilikupata majibu sahihi na maana sahihi.
    Ikiwa watajibu vyema, endelea na uulize kuhusu maana ya tattoo walizochora. Ikiwa hawaonekani na nia ya kuzungumza juu ya tattoo zao, usilazimishe zaidi.
    Tattoo zinaweza kushikilia maana na kumbukumbu za kina sana, na hata machungu ambayo watu wanapendelea kuweka faragha au siri.
    Maana au ujumbe wa tattoo umewekwa kwa kuzingatia sehemu au mahali iliyochorwa hiyo tattoo, rangi iliyotumika kuichora hiyo tattoo, na mtindo uliotumika kuchora kwa tattoo husika Kabla hatujachambua orodha yetu ya tattoo maarafu na maana zake, unahitaji kujua mambo mengine ambayo ni muhimu 1. Sehemu ambayo tattoo imechorwa au imekaa kwenye mwili ina maana kubwa, hasa kama ikiwa imewekwa au kuchorwa mahali fulani kwa ishara kama vile juu ya moyo, nyuma ya sikio au katika sehemu ya siri ya mwili. 2. Rangi iliyotumika kuchora hiyo tattoo - rangi ya tattoo inaweza kubadilisha kabisa maana. Ua rose nyekundu inaashiria upendo wa kimapenzi na shauku, wakati Ua rose la bluu mara nyingi hutumika kuashiria upendo usioweza kupatikana. 3. Mtindo uliotumika kuchora tattoo ina maana zaidi. Mfano tattoo ya simba dume kuwakilisha nguvu....au inaweza tu kuwa heshima. Huwezi kutambua maana halisi ya tattoo kwa kuiangalia pekee. Ni vyema ukauliza maana kwa mtu mwenye tattoo hiyo ilikupata majibu sahihi na maana sahihi. Ikiwa watajibu vyema, endelea na uulize kuhusu maana ya tattoo walizochora. Ikiwa hawaonekani na nia ya kuzungumza juu ya tattoo zao, usilazimishe zaidi. Tattoo zinaweza kushikilia maana na kumbukumbu za kina sana, na hata machungu ambayo watu wanapendelea kuweka faragha au siri.
    ·371 Views
  • Tattoo/Alama kwenye mwili sio mbaya ila waliochora tattoo wengi wao wanafanya mambo ambayo jamii inatafsiri ni mabaya, karibu ujifunze na kutambua maana ya tattoo maarufu tafsiri zake na asili zake.
    Tattoo/Alama kwenye mwili sio mbaya ila waliochora tattoo wengi wao wanafanya mambo ambayo jamii inatafsiri ni mabaya, karibu ujifunze na kutambua maana ya tattoo maarufu tafsiri zake na asili zake.
    ·159 Views
  • Balbu ya taa inayoelea :
    Taa hii inayoelea angani hukuikiwa inawaka inatoka #HCNT ni taa ya #LED inayowaka bila waya na inazunguka angani. Inatumia nguvu za sumaku kupepea juu ya msingi wake bila waya. Taa hii ni mapambo ya kipekee kwa meza au chumba. Ni zawadi nzuri kwa watu wanaopenda vitu vya kipekee.

    Hora Tech | jiunge Nasi Telegram kwa habari zaidi ...
    Telegram Channel : https://t.me/+kZVHb14mRuJjYmVk
    #kai #teknolojia #socialpop
    💡 Balbu ya taa inayoelea : Taa hii inayoelea angani hukuikiwa inawaka inatoka #HCNT ni taa ya #LED inayowaka bila waya na inazunguka angani. Inatumia nguvu za sumaku kupepea juu ya msingi wake bila waya. Taa hii ni mapambo ya kipekee kwa meza au chumba. Ni zawadi nzuri kwa watu wanaopenda vitu vya kipekee. ⚙️Hora Tech | jiunge Nasi Telegram kwa habari zaidi ... Telegram Channel : https://t.me/+kZVHb14mRuJjYmVk #kai #teknolojia #socialpop
    Like
    1
    1 Comments ·504 Views ·6 Views
  • Tayari zimetangazwa glavu mpya
    unapotumia glavu hizi wakati wa kucheza game, utaweza kuhisi kama unashika na kushikilia vitu au watu ndani ya mchezo huo.

    Tizama Zaidi
    Hapa https://t.me/Hora_Tech/297
    #HoraTech
    😍🧤 Tayari zimetangazwa glavu mpya unapotumia glavu hizi wakati wa kucheza game, utaweza kuhisi kama unashika na kushikilia vitu au watu ndani ya mchezo huo. Tizama Zaidi Hapa https://t.me/Hora_Tech/297 #HoraTech
    Like
    Love
    5
    1 Comments ·342 Views ·57 Views
  • Helmeti ya Dola 400,000 kwa Marubani wa Ndege za Kivita

    Collins Aerospace wamezindua kizazi cha tatu cha helmeti kwa marubani wa ndege za kivita za F-35, iitwayo "Genesis III" na inagharimu dola 400,000.

    F-35 ina kamera sita zilizowekwa nje ambazo hutoa muonekano wa kidijitali wa mazingira yote kwa rubani, akiona pande zote kwa nyuzi 360. Pia, kuna kamera za infrared kwenye mwili wa ndege, kuruhusu kuona hata gizani.

    Mifumo ya ndani ya helmeti inamruhusu rubani kuongoza ndege kwa kutumia macho tu, bila kuhitaji mikono. Pia, kila helmeti ni ya kibinafsi kwa rubani, huwezi kutumia helmeti ya mwenzako, na hairuhusiwi kubadilisha hata mtindo wa nywele zako.

    Ukaguzi unafanywa kila baada ya siku 120 ili kuhakikisha kuwa kichwa na helmeti vinakuwa sawa, ili kuhakikisha kuwa mfumo wa kuonyesha ni wa kuaminika.

    #Hora_Tech | It's Home
    #F35 #Helmeti #Teknolojia #Kivita
    Helmeti ya Dola 400,000 kwa Marubani wa Ndege za Kivita 🇺🇸 🎭Collins Aerospace wamezindua kizazi cha tatu cha helmeti kwa marubani wa ndege za kivita za F-35, iitwayo "Genesis III" na inagharimu dola 400,000. 🛫F-35 ina kamera sita zilizowekwa nje ambazo hutoa muonekano wa kidijitali wa mazingira yote kwa rubani, akiona pande zote kwa nyuzi 360. Pia, kuna kamera za infrared kwenye mwili wa ndege, kuruhusu kuona hata gizani. ♻️Mifumo ya ndani ya helmeti inamruhusu rubani kuongoza ndege kwa kutumia macho tu, bila kuhitaji mikono. Pia, kila helmeti ni ya kibinafsi kwa rubani, huwezi kutumia helmeti ya mwenzako, na hairuhusiwi kubadilisha hata mtindo wa nywele zako. 🔎 Ukaguzi unafanywa kila baada ya siku 120 ili kuhakikisha kuwa kichwa na helmeti vinakuwa sawa, ili kuhakikisha kuwa mfumo wa kuonyesha ni wa kuaminika. ✱ #Hora_Tech | It's Home #F35 #Helmeti #Teknolojia #Kivita
    Like
    2
    ·902 Views
  • Samsung Yazindua Pete ya Kipekee ya Galaxy Ring!

    Samsung imezindua Galaxy Ring, pete ya kisasa inayofuatilia usingizi, kiwango cha msongo, ubora wa chakula, kalori unazoweza kula kwa siku, na mahitaji ya maji ya mwili. Pete hii inakuja na AI inayohesabu kalori zilizotumika na index ya uzito wa mwili (BMI).

    🖱 Pete inapatikana kwa rangi tatu: silva, nyeusi, na dhahabu. Inaweza kufanya kazi bila kuchajiwa kwa siku 7 na inachajiwa kwa kutumia kituo maalum cha kuchajia kilichojumuishwa kwenye kifurushi.

    #Hora_Tech
    #Samsung #GalaxyRing #Pete
    💍 Samsung Yazindua Pete ya Kipekee ya Galaxy Ring! 🌟 💣 Samsung imezindua Galaxy Ring, pete ya kisasa inayofuatilia usingizi, kiwango cha msongo, ubora wa chakula, kalori unazoweza kula kwa siku, na mahitaji ya maji ya mwili. Pete hii inakuja na AI inayohesabu kalori zilizotumika na index ya uzito wa mwili (BMI). 🖱 Pete inapatikana kwa rangi tatu: silva, nyeusi, na dhahabu. Inaweza kufanya kazi bila kuchajiwa kwa siku 7 na inachajiwa kwa kutumia kituo maalum cha kuchajia kilichojumuishwa kwenye kifurushi. ➤ #Hora_Tech #Samsung #GalaxyRing #Pete
    Like
    2
    ·569 Views
  • Hatari za Kiusalama:
    Wadukuzi na Teknolojia za Kisasa

    Maisha yetu yanabadilika na kuwa ya kiteknolojia kila siku. Wadukuzi sasa wanaweza kusikiliza mazungumzo yako kupitia AirPods za Apple kwa kutumia vipaza sauti. Pia, wanaweza kupata ufikiaji wa mbali kwenye vifaa vya kuchaji simu na kuzidisha nguvu za umeme, na kusababisha simu kulipuka wakati wa kuchaji.

    Udukuzi huu unajulikana kama BadPower, na unaweza kushambulia simu yoyote yenye teknolojia ya kuchaji haraka kama iPhones, Samsung Galaxy, na simu nyingi za kisasa. Hii inamaanisha kwamba watu wenye nia mbaya wanaweza kuingilia teknolojia zetu na kuzitumia vibaya, hata kutoka umbali mrefu.

    🛡Jihadharini na vifaa vyako vya kiteknolojia na kuwa makini na usalama wao!

    #Hora_Tech
    #Hatari #Wadukuzi #BadPower #teknolojia
    🔐 Hatari za Kiusalama: Wadukuzi na Teknolojia za Kisasa 🌐 😎 Maisha yetu yanabadilika na kuwa ya kiteknolojia kila siku. Wadukuzi sasa wanaweza kusikiliza mazungumzo yako kupitia AirPods za Apple kwa kutumia vipaza sauti. Pia, wanaweza kupata ufikiaji wa mbali kwenye vifaa vya kuchaji simu na kuzidisha nguvu za umeme, na kusababisha simu kulipuka wakati wa kuchaji. 🚨 🦠 Udukuzi huu unajulikana kama BadPower, na unaweza kushambulia simu yoyote yenye teknolojia ya kuchaji haraka kama iPhones, Samsung Galaxy, na simu nyingi za kisasa. Hii inamaanisha kwamba watu wenye nia mbaya wanaweza kuingilia teknolojia zetu na kuzitumia vibaya, hata kutoka umbali mrefu. 🛡Jihadharini na vifaa vyako vya kiteknolojia na kuwa makini na usalama wao! ➤ #Hora_Tech #Hatari #Wadukuzi #BadPower #teknolojia
    Like
    1
    ·1K Views
  • Kamera Mpya
    Inayoweza Kuona Kupitia Karatasi ya 1cm

    Wanasayansi wameunda kamera mpya inayoweza kuona kupitia vipande vya karatasi hadi unene wa 1 cm. Hii inamaanisha unaweza kuona kilicho upande wa pili wa karatasi bila kuiondoa karatasi, kama vile kuchunguza vitu vilivyofichwa nyuma ya karatasi au sanduku. Teknolojia hii inaruhusu uchunguzi kupitia vifaa vya kawaida vya kila siku, bila kutumia mionzi hatari kama X-ray.

    #Hora_Tech
    #camera #ugunduzi #Karatasi #XRay
    📷 Kamera Mpya Inayoweza Kuona Kupitia Karatasi ya 1cm 🚨 Wanasayansi wameunda kamera mpya inayoweza kuona kupitia vipande vya karatasi hadi unene wa 1 cm. Hii inamaanisha unaweza kuona kilicho upande wa pili wa karatasi bila kuiondoa karatasi, kama vile kuchunguza vitu vilivyofichwa nyuma ya karatasi au sanduku. Teknolojia hii inaruhusu uchunguzi kupitia vifaa vya kawaida vya kila siku, bila kutumia mionzi hatari kama X-ray. ➤ #Hora_Tech #camera #ugunduzi #Karatasi #XRay
    Like
    1
    ·920 Views
  • K9 GEN4:
    Teknolojia Mpya kwa Mbwa Mashujaa

    USA, wametengeneza kofia mpya, aina ya K9 GEN4, zenye taa za mbele kwa mbwa. Kofia hii inawalinda dhidi ya kelele kali na mwangaza mkali. Hii inawaruhusu hawa mashujaa wa manyoya kufanya kazi kwa ufanisi hata katika mazingira magumu sana.

    #Hora_Tech
    #USA #Teknolojia #Mbwa #shujaa
    🐾 K9 GEN4: Teknolojia Mpya kwa Mbwa Mashujaa USA, wametengeneza kofia mpya, aina ya K9 GEN4, zenye taa za mbele kwa mbwa. Kofia hii inawalinda dhidi ya kelele kali na mwangaza mkali. Hii inawaruhusu hawa mashujaa wa manyoya kufanya kazi kwa ufanisi hata katika mazingira magumu sana. ➤ #Hora_Tech #USA #Teknolojia #Mbwa #shujaa
    Like
    Love
    2
    ·637 Views
  • Teknolojia Mpya:
    Spacetop G1 na Uhalisia wa Ongezeko

    Kompyuta ya Spacetop G1 inabadilisha jinsi tunavyoona teknolojia ya uhalisia. Ikiwa na miwani ya AR, unaweza kujionea skrini kubwa ya inchi 100 ikionekana hewani, ingawa kompyuta yenyewe haina skrini ya kawaida. Teknolojia hii inaleta uzoefu mpya wa matumizi ya kompyuta kwa njia ya kipekee na ya kisasa.

    #Hora_Tech
    #Spacetop #Computer #AR #Uhalisia
    🌐 Teknolojia Mpya: Spacetop G1 na Uhalisia wa Ongezeko 💻 Kompyuta ya Spacetop G1 inabadilisha jinsi tunavyoona teknolojia ya uhalisia. Ikiwa na miwani ya AR, unaweza kujionea skrini kubwa ya inchi 100 ikionekana hewani, ingawa kompyuta yenyewe haina skrini ya kawaida. Teknolojia hii inaleta uzoefu mpya wa matumizi ya kompyuta kwa njia ya kipekee na ya kisasa. ➤ #Hora_Tech #Spacetop #Computer #AR #Uhalisia
    Like
    Love
    2
    ·861 Views
  • 🖥 Computer Kama Bunduki

    Mwanafunzi mwenye kipaji kutoka Thailand ametengeneza casing ya kipekee kwa ajili ya kompyuta yake ya michezo, inayofanana na bunduki ya kisasa ya mtafuta shabaha. Alikusanya mashine hii kwa ajili ya shindano la Cooler Master, ambapo washiriki wanashindania taji la casing ya kipekee zaidi.

    Ingawa sifa kamili za kompyuta hiyo hazijafichuliwa, inajulikana kuwa zina ubora wa juu kabisa. Mtengenezaji huyu ametumia $2700 (sawa na takriban TZS 6,345,000) kwa ajili ya kuunda Computer hii. Ikiwa atashinda shindano hilo, atapata zawadi ya $5000 (takriban TZS 11,750,000).

    #Hora_Tech
    #Computer #Thailand #mwanafunzi
    🖥 Computer Kama Bunduki 😱 Mwanafunzi mwenye kipaji kutoka Thailand ametengeneza casing ya kipekee kwa ajili ya kompyuta yake ya michezo, inayofanana na bunduki ya kisasa ya mtafuta shabaha. Alikusanya mashine hii kwa ajili ya shindano la Cooler Master, ambapo washiriki wanashindania taji la casing ya kipekee zaidi. 💾 Ingawa sifa kamili za kompyuta hiyo hazijafichuliwa, inajulikana kuwa zina ubora wa juu kabisa. Mtengenezaji huyu ametumia $2700 (sawa na takriban TZS 6,345,000) kwa ajili ya kuunda Computer hii. Ikiwa atashinda shindano hilo, atapata zawadi ya $5000 (takriban TZS 11,750,000). ➤ #Hora_Tech #Computer #Thailand #mwanafunzi
    Like
    Love
    2
    ·642 Views
  • Mgonjwa wa Kwanza wa Neuralink Aeleza Uzoefu Wake

    🎙Katika mahojiano, mgonjwa wa kwanza aliyewekewa kipandikizi cha Neuralink ameeleza uzoefu wake. Mgonjwa huyu, ambaye ni kiwete kutoka shingo kushuka chini, sasa anaweza kudhibiti vifaa kwa nguvu ya mawazo yake. Wakati wa kuwekewa kipandikizi kwa mara ya kwanza, kilitoka kwa sababu wanasayansi hawakuzingatia harakati za ubongo ndani ya kipenyo cha milimita moja, na ilibidi wafanye upasuaji tena.

    Sasa, mgonjwa huyu anaweza kuvinjari TikTok, kuwasiliana kupitia Twitter, kufanya manunuzi mtandaoni, na kucheza michezo ya kompyuta kwa kuunganisha kipandikizi kwenye kompyuta kupitia Bluetooth na programu maalum. Amebainisha kuwa kipandikizi hicho hakileti maumivu wala hali ya kutojisikia vizuri.

    #Hora_Tech
    #Neuralink #mahojiano #Bluetooth
    🧠 Mgonjwa wa Kwanza wa Neuralink Aeleza Uzoefu Wake 🌐 🎙Katika mahojiano, mgonjwa wa kwanza aliyewekewa kipandikizi cha Neuralink ameeleza uzoefu wake. Mgonjwa huyu, ambaye ni kiwete kutoka shingo kushuka chini, sasa anaweza kudhibiti vifaa kwa nguvu ya mawazo yake. Wakati wa kuwekewa kipandikizi kwa mara ya kwanza, kilitoka kwa sababu wanasayansi hawakuzingatia harakati za ubongo ndani ya kipenyo cha milimita moja, na ilibidi wafanye upasuaji tena. 🥸 Sasa, mgonjwa huyu anaweza kuvinjari TikTok, kuwasiliana kupitia Twitter, kufanya manunuzi mtandaoni, na kucheza michezo ya kompyuta kwa kuunganisha kipandikizi kwenye kompyuta kupitia Bluetooth na programu maalum. Amebainisha kuwa kipandikizi hicho hakileti maumivu wala hali ya kutojisikia vizuri. ➤ #Hora_Tech #Neuralink #mahojiano #Bluetooth
    Like
    Love
    2
    ·846 Views
  • System inatukuza na kuishi maisha yanayo ongozwa na malengo mnafki ishi nae kinafki.Vaa miwani akizani umuoni kumb unamchora tu

    #Sizophumelela
    #nimuhimu
    #likeforlikes
    System inatukuza na kuishi maisha yanayo ongozwa na malengo mnafki ishi nae kinafki.Vaa miwani akizani umuoni kumb unamchora tu📌 #Sizophumelela #nimuhimu #likeforlikes
    Like
    4
    ·482 Views
More Results