• "Naona Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amefunga safari hadi Congo kumuona Rais Tshisekedi, sijui ni kipi hasa kinaendelea katika jumuiya ya Afrika mashariki lakini ni kama kuna muungano ndani ya muungano, eeeh kuna muungano kati ya Congo na Burundi ambao unalenga kupambana dhidi ya Rwanda

    Yaani ukiwatazama Congo na Burundi ni kama wameungana kupambana na Rwanda na M23 eeeh ipo wazi na tayari mapigano kati ya majeshi ya Congo Burundi dhidi ya Rwanda na M23 yameshuhudiwa, EAC wasipodhibiti hali ya Congo mzozo huu utaenda kutanuka na kuwa wa kikanda

    Ngoja tuone ila yajayo sio mazuri kwa diplomasia ya EAC , kiufupi ziara ya Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, nchini Congo inalenga kuonana na mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Felix Tshisekedi, huku lengo kuu ikiwa na mazungumzo kuhusu mzozo unaolikumba eneo la mashariki mwa Kongo" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa Siasa.

    "Naona Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amefunga safari hadi Congo kumuona Rais Tshisekedi, sijui ni kipi hasa kinaendelea katika jumuiya ya Afrika mashariki lakini ni kama kuna muungano ndani ya muungano, eeeh kuna muungano kati ya Congo na Burundi ambao unalenga kupambana dhidi ya Rwanda Yaani ukiwatazama Congo na Burundi ni kama wameungana kupambana na Rwanda na M23 eeeh ipo wazi na tayari mapigano kati ya majeshi ya Congo Burundi dhidi ya Rwanda na M23 yameshuhudiwa, EAC wasipodhibiti hali ya Congo mzozo huu utaenda kutanuka na kuwa wa kikanda 😭 Ngoja tuone ila yajayo sio mazuri kwa diplomasia ya EAC , kiufupi ziara ya Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, nchini Congo inalenga kuonana na mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Felix Tshisekedi, huku lengo kuu ikiwa na mazungumzo kuhusu mzozo unaolikumba eneo la mashariki mwa Kongo" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa Siasa.
    0 Comments ·0 Shares ·266 Views
  • Rais wa Marekani , Donlad Trump ametangaza kuwa Nchi yake imedhamiria kununua na kumiliki Ukanda wa Gaza na kuhamisha Wapalestina zaidi ya milioni mbili (2) wanaoishi huko, licha ya pendekezo hilo kupingwa vikali na Jumuiya ya Kimataifa. Rais huyo amewaambia Wanahabari kuwa huenda akaruhusu mataifa ya kiarabu kuhusika katika kukarabati upya sehemu mbalimbali na kuwa atahakikisha Raia wa Palestina wataishi maisha mazuri.

    Mamlaka ya Palestina na kikundi kilicho na silaha cha Hamas ambao wamekuwa vitani kwa miezi (16) na Israel na kusababisha maafa Gaza, wamemjibu wakisema ardhi ya Palestina sio ya kuuzwa''. Lakini waziri Mkuu mkuu wa Israel , Benjamin Netanyahu ameipigia upatu pendekezo hilo la Trump akilitaja ni ''mwamko mpya na bunifu''.

    Haya yamekuja Wiki tatu (3) baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza Huku Kundi la Hamas likiachilia huru baadhi ya Mateka wa Nchi ya Israel inayowazuia ili kubadilishana na Wafungwa wa Palestina walioko katika Magerezani Nchini Israel.

    Wanajeshi wa Israel walianzisha kampeni ya kuvamia na kuharibu Gaza wakijibu shambulizi la kushtukizia la mwezi Oktoba tarehe 7 2023, ambapo watu 1,200 waliuawa na 251 wakatekwa nyara. Zaidi ya Watu 48,180 wameuliwa Gaza tangu mapigano hayo yaanze , hii ni kwa mujibu wa wizara ya afya inayosimamiwa na kundi la Hamas lililokuwa likipigana na Nchi ya Israel.

    Rais wa Marekani 🇺🇸, Donlad Trump ametangaza kuwa Nchi yake imedhamiria kununua na kumiliki Ukanda wa Gaza na kuhamisha Wapalestina zaidi ya milioni mbili (2) wanaoishi huko, licha ya pendekezo hilo kupingwa vikali na Jumuiya ya Kimataifa. Rais huyo amewaambia Wanahabari kuwa huenda akaruhusu mataifa ya kiarabu kuhusika katika kukarabati upya sehemu mbalimbali na kuwa atahakikisha Raia wa Palestina wataishi maisha mazuri. Mamlaka ya Palestina na kikundi kilicho na silaha cha Hamas ambao wamekuwa vitani kwa miezi (16) na Israel na kusababisha maafa Gaza, wamemjibu wakisema ardhi ya Palestina sio ya kuuzwa''. Lakini waziri Mkuu mkuu wa Israel 🇮🇱, Benjamin Netanyahu ameipigia upatu pendekezo hilo la Trump akilitaja ni ''mwamko mpya na bunifu''. Haya yamekuja Wiki tatu (3) baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza Huku Kundi la Hamas likiachilia huru baadhi ya Mateka wa Nchi ya Israel inayowazuia ili kubadilishana na Wafungwa wa Palestina walioko katika Magerezani Nchini Israel. Wanajeshi wa Israel walianzisha kampeni ya kuvamia na kuharibu Gaza wakijibu shambulizi la kushtukizia la mwezi Oktoba tarehe 7 2023, ambapo watu 1,200 waliuawa na 251 wakatekwa nyara. Zaidi ya Watu 48,180 wameuliwa Gaza tangu mapigano hayo yaanze , hii ni kwa mujibu wa wizara ya afya inayosimamiwa na kundi la Hamas lililokuwa likipigana na Nchi ya Israel.
    Like
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·544 Views
  • Kwa mujibu wa The Citizens, zaidi ya kampuni tano (5) za kigeni kutoka Nchini Ufaransa na Misri pamoja na Wawekezaji wa ndani ya Tanzania , wameonyesha nia ya kuwekeza katika usafirishaji wa nyaya yaani "cable" kwa lugha ya Kiingereza. Ili kufanikisha hilo sasa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) inakamilisha Kanuni za Usafiri wa Waya za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini za Mwaka, 2024 katika ngazi ya Serikali.

    Kanuni zingine zinazoendelea zinazopendekezwa ni pamoja na Kanuni za LATRA (Utoaji Leseni kwa Waendeshaji Reli) 2024 na Kanuni ya Utoaji Leseni ya Usafiri (Leseni ya Kipekee ya Usafiri wa Umma), 2024. Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa LATRA, Salum Pazzy ameiambia The Citizen kwamba kampuni mbili kutoka Ufaransa na moja kutoka Misri zimejitokeza zikisubiri idhini ya kuwekeza katika sekta hiyo.

    Kampuni hizi zimewasilisha mapendekezo yao na yanasubiri kuidhinishwa kwa kanuni ili kujihakikishia mazingira mazuri kwani usafiri wa waya unaonekana kuwa fursa kubwa ya kiuwekezaji.

    Kwa mujibu wa The Citizens, zaidi ya kampuni tano (5) za kigeni kutoka Nchini Ufaransa 🇫🇷 na Misri 🇪🇬 pamoja na Wawekezaji wa ndani ya Tanzania 🇹🇿, wameonyesha nia ya kuwekeza katika usafirishaji wa nyaya yaani "cable" kwa lugha ya Kiingereza. Ili kufanikisha hilo sasa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) inakamilisha Kanuni za Usafiri wa Waya za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini za Mwaka, 2024 katika ngazi ya Serikali. Kanuni zingine zinazoendelea zinazopendekezwa ni pamoja na Kanuni za LATRA (Utoaji Leseni kwa Waendeshaji Reli) 2024 na Kanuni ya Utoaji Leseni ya Usafiri (Leseni ya Kipekee ya Usafiri wa Umma), 2024. Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa LATRA, Salum Pazzy ameiambia The Citizen kwamba kampuni mbili kutoka Ufaransa na moja kutoka Misri zimejitokeza zikisubiri idhini ya kuwekeza katika sekta hiyo. Kampuni hizi zimewasilisha mapendekezo yao na yanasubiri kuidhinishwa kwa kanuni ili kujihakikishia mazingira mazuri kwani usafiri wa waya unaonekana kuwa fursa kubwa ya kiuwekezaji.
    Like
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·373 Views
  • #PART4

    Lakini cha kushangaza, wanaume wengi hawafanyi hivi.

    Kwa nini?

    Kwa sababu mwanaume hapendi kuonekana amefeli.

    Dogo akimuuliza baba yake, "Kwanini ulimuacha mama?" baba atapata kigugumizi.

    Hakuna mwanaume anayependa aonekane alishindwa kufanya kitu sahihi.

    Ndiyo maana wanaume wengi husema mambo mazuri kuhusu mama wa mtoto wao, hata kama waliachana kwa mabaya.

    Lakini wanawake wengi hawawezi kufanya hivyo. Wengi hujaza chuki kwa mtoto. Wanaangalia maisha yao kwa sasa, wanasahau mtoto atakua na atagundua ukweli wenyewe.

    50 Cent ni role model wa wanaume wengi kwa sababu moja kubwa, anajua dunia ilivyo.

    Ndiyo maana hata Chris Brown, kabla ya kuingia kwenye ndoa, alikwenda kwa 50 Cent kumuuliza ushauri.

    50 Cent alimwambia USITHUBUTU!
    #PART4 Lakini cha kushangaza, wanaume wengi hawafanyi hivi. Kwa nini? Kwa sababu mwanaume hapendi kuonekana amefeli. Dogo akimuuliza baba yake, "Kwanini ulimuacha mama?" baba atapata kigugumizi. Hakuna mwanaume anayependa aonekane alishindwa kufanya kitu sahihi. Ndiyo maana wanaume wengi husema mambo mazuri kuhusu mama wa mtoto wao, hata kama waliachana kwa mabaya. Lakini wanawake wengi hawawezi kufanya hivyo. Wengi hujaza chuki kwa mtoto. Wanaangalia maisha yao kwa sasa, wanasahau mtoto atakua na atagundua ukweli wenyewe. 50 Cent ni role model wa wanaume wengi kwa sababu moja kubwa, anajua dunia ilivyo. Ndiyo maana hata Chris Brown, kabla ya kuingia kwenye ndoa, alikwenda kwa 50 Cent kumuuliza ushauri. 50 Cent alimwambia USITHUBUTU!
    0 Comments ·0 Shares ·442 Views
  • #PART1

    Katika maisha, kuna mafanikio, kuna mapenzi, na kuna maumivu.

    Lakini maumivu gani yanaweza kuwa makali zaidi ya baba kugombana na damu yake mwenyewe?

    Hii ni stori ya 50 Cent, mwanamuziki, mfanyabiashara, na mtu aliye role model wa mamilioni ya wanaume duniani.

    Jamaa aliinuka kutoka mitaa ya ghetto, akapambana, akawa milionea. Lakini pamoja na pesa zote, hakununua upendo wa mtoto wake wa kwanza.

    Miaka ya nyuma, 50 Cent alikuwa baba mwenye furaha. Alikuwa anampenda mtoto wake kupita maelezo.

    Ilikuwa siyo tu kwa sababu ni damu yake, bali pia alitaka kuhakikisha kijana wake anakuwa na maisha bora zaidi.

    Aliamua kumuandalia mtoto wake maisha mazuri. Akampeleka kwenye shule nzuri ya mpira wa kikapu. Akalipia kila kitu, kutoka ada mpka mavazi.

    Mtoto akapewa kila alichohitaji, maisha ya kifahari yakawa sehemu yake ya kila siku.

    Lakini kitu kimoja hakikumpenda. Mpira wa kikapu haukumpenda.

    Dogo akaamua kuachana na basketball. Baba yake hakukasirika, akamwambia

    "Sawa mwanangu, kama siyo mpira, basi komaa na shule."

    #PART1 Katika maisha, kuna mafanikio, kuna mapenzi, na kuna maumivu. Lakini maumivu gani yanaweza kuwa makali zaidi ya baba kugombana na damu yake mwenyewe? Hii ni stori ya 50 Cent, mwanamuziki, mfanyabiashara, na mtu aliye role model wa mamilioni ya wanaume duniani. Jamaa aliinuka kutoka mitaa ya ghetto, akapambana, akawa milionea. Lakini pamoja na pesa zote, hakununua upendo wa mtoto wake wa kwanza. Miaka ya nyuma, 50 Cent alikuwa baba mwenye furaha. Alikuwa anampenda mtoto wake kupita maelezo. Ilikuwa siyo tu kwa sababu ni damu yake, bali pia alitaka kuhakikisha kijana wake anakuwa na maisha bora zaidi. Aliamua kumuandalia mtoto wake maisha mazuri. Akampeleka kwenye shule nzuri ya mpira wa kikapu. Akalipia kila kitu, kutoka ada mpka mavazi. Mtoto akapewa kila alichohitaji, maisha ya kifahari yakawa sehemu yake ya kila siku. Lakini kitu kimoja hakikumpenda. Mpira wa kikapu haukumpenda. Dogo akaamua kuachana na basketball. Baba yake hakukasirika, akamwambia "Sawa mwanangu, kama siyo mpira, basi komaa na shule."
    0 Comments ·0 Shares ·650 Views
  • Maboresho yaliyofanyika, ikiwemo kubadili mwonekano ni mazuri sana. Yanavutia na yataongeza hamasa.
    Maboresho yaliyofanyika, ikiwemo kubadili mwonekano ni mazuri sana. Yanavutia na yataongeza hamasa.
    Like
    Love
    5
    · 3 Comments ·0 Shares ·271 Views
  • “Ushindi wa CCM katika uchaguzi mwaka huu hauna mjadala. Wagombea watakuwepo wa vyama vingine lakini sioni namna wanavyoweza kuishinda CCM. Lakini sio kwa ujanja ujanja ni kwa sababu yapo mambo mengi mazuri yaliyofanywa na serikali zetu mbili, lakini ni mambo ambayo yana manufaa kwa Watanzania.” – Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Tanzania
    “Ushindi wa CCM katika uchaguzi mwaka huu hauna mjadala. Wagombea watakuwepo wa vyama vingine lakini sioni namna wanavyoweza kuishinda CCM. Lakini sio kwa ujanja ujanja ni kwa sababu yapo mambo mengi mazuri yaliyofanywa na serikali zetu mbili, lakini ni mambo ambayo yana manufaa kwa Watanzania.” – Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Tanzania
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·308 Views
  • Siku ya Jana 18, January na leo 19, January 2025 nimefuatilia kwa ukaribu na Umakini Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Mwaka 2025 uliofanyika Dodoma Hakika umekua wa kipekee na Uliovutia kwa Maandalizi mazuri, Hongera sana Kwa Waandaaji wakiongozwa na Dk @samia_suluhu_hassan Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuli ya muungano wa Tanzania.

    Pamoja na mambo mengine yaliyojadiliwa kwenye Mkutano huu nimeshuhudia Matukio Matatu Muhimu,

    Mosi, Uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Dkt Steven Wasira
    Pili, Marekebisho ya Baadhi ya vipengele muhimu vya Katiba ya CCM ikiwemo kuongezeka kwa wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM kutoka nafasi 6 paka 10 yaani nafasi 5 Zanzibar na Nafasi 5 Bara,
    Tatu, Uteuzi na Uidhinishwaji wa Majina ya wagombea wa Nafasi ya Urais Tanzania na Zanzibar Uchaguzi Mkuu 2025 Yaani Dkt @samia_suluhu_hassan kwa Tanzania na Dkt @dr.hmwinyi Zanzibar

    Nne, kupendekeza na kupitisha Jina la Mgombea mwenza (Makamu wa Rais) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt @nchimbie

    Matukio yote haya Manne yameendelea kuthibitisha kwamba CCM ni chama kilichokomaa Kidemocrasia na Ndio chama pekee kinachofaa kuiongoza nchi hii kwa Amani na Utulivu (Hasa ukizingatia yanayoendelea huko upande wa Pili Mmh)

    Lakini pia imendelea kuthibitisha kiasi Gani chama cha Mapinduzi @ccmtanzania kina hazina ya Watu wanaoweza kuiongoza chama na Serikali wakati wowote ule kuanzia Chama chenyewe na Jumuia zake zote @wazazi_ccm_tz @uwt_taifa , na @uvccm_tz , Hakika CCM idumu milele, Hongera Mwenyekiti @samia_suluhu_hassan kwa Uongozi na Malezi Bora kwa Chama

    Itoshe Kusema @ccmtanzania inatosha na ni kwa matakwa ya kikatiba tu lakini ingewezekana TUSIFANYE UCHAGUZI TUMUACHE MAMA NA SAFU YAKE WAENDELEE KUFANYA KAZI YA KUIJENGA TANZANIA, Kwa Hali inayoendelea na Mfarakano wa huko kwa Majirani naona kabisa ni kupoteza muda. Ni kwasababu ni Takwa la kikatiba tu na CCM tunaheshimu Katiba lakini isingekua Hilo Basi Mama @samia_suluhu_hassan Angeachwa na Safu yake aendelee kuchapa kazi, Aendeleze kazi ya kuijenga Tanzania iliyotukuka

    Hongera Mama @samia_suluhu_hassan, Hongera Dkt @dr.hmwinyi, Hongera Dkt @nchimbie kwa kuaminiwa Tena

    #kaziiendelee

    @ccmtanzania @uvccm_tz @uvccm_tanga
    Siku ya Jana 18, January na leo 19, January 2025 nimefuatilia kwa ukaribu na Umakini Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Mwaka 2025 uliofanyika Dodoma Hakika umekua wa kipekee na Uliovutia kwa Maandalizi mazuri, Hongera sana Kwa Waandaaji wakiongozwa na Dk @samia_suluhu_hassan Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuli ya muungano wa Tanzania. Pamoja na mambo mengine yaliyojadiliwa kwenye Mkutano huu nimeshuhudia Matukio Matatu Muhimu, Mosi, Uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Dkt Steven Wasira Pili, Marekebisho ya Baadhi ya vipengele muhimu vya Katiba ya CCM ikiwemo kuongezeka kwa wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM kutoka nafasi 6 paka 10 yaani nafasi 5 Zanzibar na Nafasi 5 Bara, Tatu, Uteuzi na Uidhinishwaji wa Majina ya wagombea wa Nafasi ya Urais Tanzania na Zanzibar Uchaguzi Mkuu 2025 Yaani Dkt @samia_suluhu_hassan kwa Tanzania na Dkt @dr.hmwinyi Zanzibar Nne, kupendekeza na kupitisha Jina la Mgombea mwenza (Makamu wa Rais) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt @nchimbie Matukio yote haya Manne yameendelea kuthibitisha kwamba CCM ni chama kilichokomaa Kidemocrasia na Ndio chama pekee kinachofaa kuiongoza nchi hii kwa Amani na Utulivu (Hasa ukizingatia yanayoendelea huko upande wa Pili Mmh🙌😂) Lakini pia imendelea kuthibitisha kiasi Gani chama cha Mapinduzi @ccmtanzania kina hazina ya Watu wanaoweza kuiongoza chama na Serikali wakati wowote ule kuanzia Chama chenyewe na Jumuia zake zote @wazazi_ccm_tz @uwt_taifa , na @uvccm_tz , Hakika CCM idumu milele, Hongera Mwenyekiti @samia_suluhu_hassan kwa Uongozi na Malezi Bora kwa Chama Itoshe Kusema @ccmtanzania inatosha na ni kwa matakwa ya kikatiba tu lakini ingewezekana TUSIFANYE UCHAGUZI TUMUACHE MAMA NA SAFU YAKE WAENDELEE KUFANYA KAZI YA KUIJENGA TANZANIA, Kwa Hali inayoendelea na Mfarakano wa huko kwa Majirani naona kabisa ni kupoteza muda. Ni kwasababu ni Takwa la kikatiba tu na CCM tunaheshimu Katiba lakini isingekua Hilo Basi Mama @samia_suluhu_hassan Angeachwa na Safu yake aendelee kuchapa kazi, Aendeleze kazi ya kuijenga Tanzania iliyotukuka Hongera Mama @samia_suluhu_hassan, Hongera Dkt @dr.hmwinyi, Hongera Dkt @nchimbie kwa kuaminiwa Tena #kaziiendelee @ccmtanzania @uvccm_tz @uvccm_tanga
    0 Comments ·0 Shares ·639 Views
  • Maisha ni mazuri unapokuwa na marafiki napenda kukutana na watu wengine kutoka pande zote za dunia. Ikiwa unataka kuzungumza nami, nitumie ujumbe!
    Maisha ni mazuri unapokuwa na marafiki napenda kukutana na watu wengine kutoka pande zote za dunia. Ikiwa unataka kuzungumza nami, nitumie ujumbe!
    0 Comments ·0 Shares ·269 Views
  • “Maandalizi yapo vizuri tunamshukuru mwenyezi Mungu, sisi kama Yanga SC tupo vizuri kabisa kwa mchezo. Tumefanya maandalizi makubwa na yapo sawa tuwaachie tu mashabiki waje uwanjani”

    “Sisi tunataka kwenda robo fainali ya CAF champions League, tunataka tuingie kwenye Top 5 ya klabu bora barani Afrika, kwa mujibu wa taratibu wa renki za klabu kwa ubora barani Afrika tukishinda kesho tunapata point 39 tunataka nafasi ya tano na inakuwa mara ya kwanza klabu ya Tanzania na Afrika mashariki kufika nafasi ya tano, tuna vitu vingi vyakutusukuma kwenda kupambana kesho kupata maatokeo mazuri”

    “Malengo makubwa ambayo viongozi waliyatoa mapema ni kufika tulipofika msimu uliopita yaani tukifika robo fainali tutakuwa tumefikia malengo yetu ya michuano ya kimataifa baada ya hapo gari itakuwa imekata breki ila atakayekuja mbele yeyote yule tutamfokea na kuruka naye sababu itakuwa tayari presha imeshaondoka”

    “Kwanza tumalize mchezo wa kesho kwa wana Yanga njooni tukajaze uwanja,tukamchinje mwarabu, na kuhusu mauzo ya tiketi yanakwenda vizuri” - Ally Kamwe Msemaji wa Klabu ya Yanga SC.

    “Maandalizi yapo vizuri tunamshukuru mwenyezi Mungu, sisi kama Yanga SC tupo vizuri kabisa kwa mchezo. Tumefanya maandalizi makubwa na yapo sawa tuwaachie tu mashabiki waje uwanjani” “Sisi tunataka kwenda robo fainali ya CAF champions League, tunataka tuingie kwenye Top 5 ya klabu bora barani Afrika, kwa mujibu wa taratibu wa renki za klabu kwa ubora barani Afrika tukishinda kesho tunapata point 39 tunataka nafasi ya tano na inakuwa mara ya kwanza klabu ya Tanzania na Afrika mashariki kufika nafasi ya tano, tuna vitu vingi vyakutusukuma kwenda kupambana kesho kupata maatokeo mazuri” “Malengo makubwa ambayo viongozi waliyatoa mapema ni kufika tulipofika msimu uliopita yaani tukifika robo fainali tutakuwa tumefikia malengo yetu ya michuano ya kimataifa baada ya hapo gari itakuwa imekata breki ila atakayekuja mbele yeyote yule tutamfokea na kuruka naye sababu itakuwa tayari presha imeshaondoka” “Kwanza tumalize mchezo wa kesho kwa wana Yanga njooni tukajaze uwanja,tukamchinje mwarabu, na kuhusu mauzo ya tiketi yanakwenda vizuri” - Ally Kamwe Msemaji wa Klabu ya Yanga SC.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·399 Views
  • Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) leo limetangaza kuahirisha Mashindano ya Mataifa ya Afrika ya TotalEnergies (CHAN) yaliyokuwa yafanyike Kenya, Tanzania, na Uganda kuanzia Februari na sasa yatafanyika Agosti 2025.

    Taarifa ya CAF imekiri kwamba kumekuwa na maendeleo makubwa katika ujenzi na ukarabati wa viwanja vya michezo, maeneo ya mazoezi, hoteli, hospitali, na miundombinu mingine muhimu katika nchi hizo tatu kwa ajili ya mashindano hayo.

    Hata hivyo, wataalamu wa kiufundi na miundombinu wa CAF waliopo Kenya, Tanzania, na Uganda wameishauri CAF kwamba muda zaidi unahitajika ili kuhakikisha miundombinu inafikia viwango vinavyohitajika kwa ajili ya kuandaa mashindano yenye mafanikio.

    Rais wa CAF, Dkt. Patrice Motsepe, amesema: "Ninatoa shukrani za dhati kwa Rais William Ruto wa Kenya, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, na Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa uongozi wao, kujitolea, na maendeleo mazuri yaliyopatikana katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya soka. Nimevutiwa na kazi inayoendelea, na nina uhakika kwamba viwanja vya michezo, maeneo ya mazoezi, hoteli, hospitali, na miundombinu mingine itakidhi viwango vya CAF ifikapo Agosti 2025."

    CAF pia imetangaza kwamba droo ya CHAN Kenya, Tanzania, na Uganda 2024 itafanyika jijini Nairobi, Jumatano, Januari 15, 2025, saa mbili usiku kwa saa za Nairobi.

    Tarehe kamili ya kuanza kwa mashindano hayo mwezi Agosti 2025 itatangazwa na CAF katika siku zijazo.

    #neliudcosiah
    Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) leo limetangaza kuahirisha Mashindano ya Mataifa ya Afrika ya TotalEnergies (CHAN) yaliyokuwa yafanyike Kenya, Tanzania, na Uganda kuanzia Februari na sasa yatafanyika Agosti 2025. Taarifa ya CAF imekiri kwamba kumekuwa na maendeleo makubwa katika ujenzi na ukarabati wa viwanja vya michezo, maeneo ya mazoezi, hoteli, hospitali, na miundombinu mingine muhimu katika nchi hizo tatu kwa ajili ya mashindano hayo. Hata hivyo, wataalamu wa kiufundi na miundombinu wa CAF waliopo Kenya, Tanzania, na Uganda wameishauri CAF kwamba muda zaidi unahitajika ili kuhakikisha miundombinu inafikia viwango vinavyohitajika kwa ajili ya kuandaa mashindano yenye mafanikio. Rais wa CAF, Dkt. Patrice Motsepe, amesema: "Ninatoa shukrani za dhati kwa Rais William Ruto wa Kenya, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, na Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa uongozi wao, kujitolea, na maendeleo mazuri yaliyopatikana katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya soka. Nimevutiwa na kazi inayoendelea, na nina uhakika kwamba viwanja vya michezo, maeneo ya mazoezi, hoteli, hospitali, na miundombinu mingine itakidhi viwango vya CAF ifikapo Agosti 2025." CAF pia imetangaza kwamba droo ya CHAN Kenya, Tanzania, na Uganda 2024 itafanyika jijini Nairobi, Jumatano, Januari 15, 2025, saa mbili usiku kwa saa za Nairobi. Tarehe kamili ya kuanza kwa mashindano hayo mwezi Agosti 2025 itatangazwa na CAF katika siku zijazo. #neliudcosiah
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·796 Views
  • Escobares, mji uliyo masikini nchini Marekani.
    Mji wa Escobares katika mpaka Mexico na Marekani haujawahi kuorodheshwa kama moja ya miji masikini zaidi nchini Marekani lakini wakaazi wake wanaishi chini ya dola moja kwa siku.

    Kwa mujibu wa shirika la kukadiria idadi ya watu, 62.4% ya wakaazi 2,512 wa mji huo wanaishi chini ya dola moja kwa siku.

    "Wakati mwingine nakosa chakula hadi nasaidiwa na jamaa zangu," anasema Debora Hernández, raia wa Marekani aliyezaliwa na kulelewa katika mji huo wa mpakani.

    Mji wa Escobares uko mbali na miji iliyo na shughuli nyingi za kiuchumi na wakaazi hawana njia nyingine ya kujikimu kimaisha.
    Watu wanaoishi maeneo ya kusini mwa Marekani wanakabiliwa na viwango vya juu vya umasikini,"Rakesh Kochhar, mtafiti katika kituo cha utafiti cha Pew mjini Washington, aliiambia BBC.

    Kituo hicho kinasema kiwango cha umasikini nchini Marekani kimefikia 12.3%, na takriban watu milioni 40 wameathiriwa.

    Watu masikini zaidi nchini Marekani wanaishi miji ya Mississippi, Louisiana na New Mexico, wengi wao ni watu wa asili ya "Uhispania na Waafrika ambao katika historia ya nchi hiyo wamekabiliwa na umasikini kwa muda mrefu,"anasema mtafiti, Rakesh Kochhar.
    watu wa Escobares wanaishi ndani ya mabogi ya treni au trela ambayo yameguzwa kuwa nyumba ambayo yanawezwa kuhamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
    Wapo watu wengi wanafikiria marekani maisha ni mazuri je ungependa kuishi marekani katika mji huu!?nakaribisha maoni.
    ®jbgw.
    Escobares, mji uliyo masikini nchini Marekani. Mji wa Escobares katika mpaka Mexico na Marekani haujawahi kuorodheshwa kama moja ya miji masikini zaidi nchini Marekani lakini wakaazi wake wanaishi chini ya dola moja kwa siku. Kwa mujibu wa shirika la kukadiria idadi ya watu, 62.4% ya wakaazi 2,512 wa mji huo wanaishi chini ya dola moja kwa siku. "Wakati mwingine nakosa chakula hadi nasaidiwa na jamaa zangu," anasema Debora Hernández, raia wa Marekani aliyezaliwa na kulelewa katika mji huo wa mpakani. Mji wa Escobares uko mbali na miji iliyo na shughuli nyingi za kiuchumi na wakaazi hawana njia nyingine ya kujikimu kimaisha. Watu wanaoishi maeneo ya kusini mwa Marekani wanakabiliwa na viwango vya juu vya umasikini,"Rakesh Kochhar, mtafiti katika kituo cha utafiti cha Pew mjini Washington, aliiambia BBC. Kituo hicho kinasema kiwango cha umasikini nchini Marekani kimefikia 12.3%, na takriban watu milioni 40 wameathiriwa. Watu masikini zaidi nchini Marekani wanaishi miji ya Mississippi, Louisiana na New Mexico, wengi wao ni watu wa asili ya "Uhispania na Waafrika ambao katika historia ya nchi hiyo wamekabiliwa na umasikini kwa muda mrefu,"anasema mtafiti, Rakesh Kochhar. watu wa Escobares wanaishi ndani ya mabogi ya treni au trela ambayo yameguzwa kuwa nyumba ambayo yanawezwa kuhamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine. Wapo watu wengi wanafikiria marekani maisha ni mazuri je ungependa kuishi marekani katika mji huu!?nakaribisha maoni. ®jbgw.
    0 Comments ·0 Shares ·340 Views
  • GEREZA LA GITARAMA: Jehenamu duniani!

    Jiji la Gitarama hupatikana katikati ya nchi ya Rwanda, kwa makadirio kilomita arobaini na tano toka kwenye jiji kubwa nchini humo; jiji la Kigali, jiji pekee lililoitangulia Gitarama kwa ukubwa.

    Kama haitoshi ni hapahapa katika jiji hili ndipo kuna historia kubwa ya makutano yaliyofanyika mwezi wa kwanza; mwaka 1961, Rwanda ikatangazwa rasmi kama jamhuri. Vilevile jiji hili (kipindi hicho mji) likatoa raisi wa kwanza wa Rwanda, bwana Gregoire Kayibanda, ambaye kumbukumbuye mpaka sasa imesimamishwa katikati ya eneo hili.

    Mazuri hayo hayakomei hapo, hapana! Bali pia hili jiji likabarikiwa na kutunukiwa vivutio kadha wa kadha vya utalii na taasisi lukuki za elimu ambazo aidha zaweza jaza ukumbi nikizianisha hapa. Na kwa namna moja ama nyingine nachelea kusema taasisi hizo zilijengwa (zimejengwa) kwa lengo chanya la kuwafanya watu wapate elimu na hatimaye kujikomboa kifikra na kimwili.

    Lakini mbali na taasisi hizo, na aidha vivutio na uzuri wa jiji hili, upande wa pili wa sarafu ukisikia jina hili ‘Gitarama’, yakupasa uhofie na hata kushikwa na huruma kwa namna binadamu kama wewe wanavyotendwa, tena bado wakiwa hai kabisa. Binadamu hao wakiwa wanaishi ndani ya eneo ambalo hakuna binadamu yeyote juu ya uso wa dunia angelipenda kuwamo kwa gharama yoyote ile!

    GITARAMA; ‘JEHANAMU DUNIANI’:

    Sehemu nyingi duniani zimewahi kuitwa jehanamu. Na jina hili lilishamiri zaidi baada ya vita vya pili vya dunia ambapo maeneo kadhaa yalipewa jina hili kuwakilisha maeneo yasiyokalika, hatari na yasiyo na afya stahiki kwa wanadamu. Maeneo hayo mathalani ni Blood Falls (Maanguko ya damu) huko Antarktika, Danakil Depression (bonde la Danakil) huko Ethiopia, Door to Hell (mlango wa kuzimu) huko Turkmenistan, Kamchatka Peninsula huko Russia na kadhalika, na kadhalika.

    Japokuwa sehemu hizo zipo nyingi zikipatikana maeneo mbalimbali, ni dhahiri kuna sifa ambazo hushirikiana na hivyo basi ndio maana huwekwa chini ya mwamvuli mmoja wa ‘jehanamu’.

    Upande wa kusini magharibi mwa jiji la Kigali, ndipo ilipo jela hii Gitarama. Kwa sasa inaitwa jela ya Muhanga ikichukua jina la wilaya ambayo ndiyo makazi yake mpaka sasa. Majengo ya jela hiyo yalikuwa yanamilikiwa na waingereza British housing complex mnamo mwaka 1960 yakiwa yamejengwa kama makazi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.

    Pale kampuni ilipofungwa, eneo hilo likakodiwa na serikali ya kwanza ya Rwanda iliyokuwa imedhamiria kufanya majengo hayo kuwa jela ya kisiasa (political prison). Tangu hapo hakuna chochote kilichobadilika ndani ya jela hiyo isipokuwa tu serikali ya Rwanda ambapo kila serikali iliyoingia madarakani ilionekana kuipatia ama kuitafutia matumizi eneo hilo.

    Kwa mujibu wa gazeti la London Independent mwaka 1995, hii ndiyo jela mbaya zaidi kuwahi kutokea duniani. Pia wanda za tovuti nyingi za mitandao, zinakiri na kuiweka jela hii kwenye kumi, ama tano, ama tatu bora zaidi ya jela hatari mno kuwahi kutokea duniani.

    Gitarama ilijengwa kwa ajili ya kumudu wafungwa mia nne tu, lakini mpaka sasa inabebelea wafungwa elfu saba! Mara kumi na nane kwa makadirio. Hali hii inapelekea mahesabu ya wafungwa wanne kurundikana katika eneo la hatua tatu (three feet). Hili laweza likawa la kawaida sana ukilisoma hapa, lakini ukijaribu kutoka nje ya bandiko hili na kujikuta ukiwa umekaa na watu wengine watatu ndani ya eneo la hatua tatu tu, kidogo waweza kuelewa.

    Hakuna mahali pa kulala, kujilaza, wala pa kuketi. Wafungwa husimama wakikung’utwa na jua na wakipoozwa na mvua kwakuwa jela hii kwa kiasi kikubwa haina paa la kuwakinga wafungwa na jua, mvua wala baridi.

    Kutokana na kutapakaa kwa wafungwa hao kwenye eneo hilo dogo, inakuwa ngumu sana kwa mfungwa kutaka kwenda chooni akafanikiwa kwa muda, hali hii inapelekea wafungwa kujisaidia popote pale na hivyo basi kujaza vinyesi, mikojo na harufu kila eneo. Wafungwa huozeshwa na kumomonywa miili na bakteria mpaka kufa kwasababu ya kujiweka karibu, aidha kwa kulala ama kusimama kwenye vinyesi na uchafu wa kila aina (gangrene).

    Wafungwa wengi hawana vidole, nyayo na miguu kwasababu ya kuoza wakiwa hai. Miguu hubadilika rangi na hata kutoa madonda. Ni kawaida kuona mtu ana wadudu miguuni huku wakitembea.

    Kati ya wafungwa kumi ndani ya jela hii, nane hufa kwa kukosa hewa ama magonjwa mbalimbali. Lakini wanapotoka kwenda kuzikwa, basi huingizwa wafungwa wengine ndani ya mlango mkubwa wenye kutu wenye kutoa malalamiko ya ukuukuu.

    Lakini ajabu na kweli ni kwamba, wafungwa waliomo humo ndani hakuna hata mmoja ambaye amepitia mahakamani akathibitishwa ya kwamba ana makosa na anastahili kufungwa.
    Wengi wao, kama si wote, ni wa Hutu. Na walianza kujazwa humo miaka ya 1990's wakituhumiwa kwa mauaji ya Kimbari yaliyokwapua maisha ya wana Rwanda zaidi ya milioni moja. Na hii huonekana ni sababu kubwa inayofanya serikali kutokujali kabisa jela hiyo achilia mbali aliye madarakani ni mtutsi.

    "Watu wanafanyana vitoweo."

    Si tu kwamba hakuna mahali pa kupumzikia, bali ndani ya jela hii kuna rekodi kadha wa kadha mfungwa kumuua mwenzake kisha kumla kama chakula.

    Mgawo wa chakula ni finyu sana. chakula na maji hutolewa mara moja tu kwa juma, tena kikiwa kibovu na hakitoshelezi; mara nyingine chakula kinakosekana kabisa na hivyo basi kuwalazimu wafungwa kumaliza siku kadha wa kadha pasipo kutia kitu tumboni.

    Kwakuwa kila mtu anataka kuishi, wafungwa wengine huamua kuchukua hatua ya kulinda uhai wao kwa kuwanyonga wenzao, kuwabamiza ukutani mpaka mauti kisha kuwatafuna wakiwa wabichi na wakivuja damu moto.

    Wengine hucheza kamari kabisa, ambapo wahusika huchaguliwa kwa kukurupushwa. Mwisho wa siku wahanga wa Kamari hiyo hupotea isijulikane wameenda wapi ndani ya jela, bali matumboni.

    Kumbuka kwamba yote haya yanawezekana tena kwa urahisi kwa sababu ndani ya jela hii hakuna hata mlinzi anayediriki kuingia, ni wafungwa wenyewe tu ndio ambao hujihudumia wenyewe. Chakula na maji vikiletwa, huachwa mlangoni kabla ya wafungwa wenyewe kunyakuwa na kuanza kujigawia. Ndio maana mtu anaweza akafa mpaka akaoza ndani ya jela hii kabla hajaja tolewa na kwenda kuzikwa kwenye makaburi ya pamoja.

    Kulana wenyewe kwa wenyewe si jambo geni wala la kushhtukiza kwa walinzi wa jela hiyo wala tawala husika.

    Juhudi za kubadilisha hali ya Gitarama:

    Kwa namna moja ama nyingine kuna watu na mashirika yaliyoguswa na hali ya kusikitisha kuhusu Gitarama. Japokuwa kweli waliomo humo wanaweza wakawa ni watu waliofanya makosa mbalimbali, ikiwemo hata kuua, lakini halibadilishi dhana ya kwamba na wao wanahitaji haki za binadamu kama wengineo.

    Shirika la Global Giving, likisukumwa na kiongozi wa projekti hii Karen Tse, ni moja ya shirika lisilonuwia faida lililoguswa na hata kuanzisha kampeni ya kutafuta pesa kwa ajili ya kuwasaidia wafungwa hao. Mpaka sasa shirika hili li wazi na unaweza ukawachangia.

    Pesa waliyoichangisha mpaka sasa ni dola za kimarekani 325 huku wakifadhiliwa na mashirika mawili fadhili na huu ukiwa ni mwaka wa sita sasa wapo moto (active).

    Mbali na hapo wanajitutumua kuwasaidia wafungwa hao kisheria ili kesi zao zipatwe kusikilizwa mahakamani. Japokuwa swala hili linaonekana ndoto zaidi ya uhalisia tangu mkono wa serikali unakuwa mzito sana kutingisha kidole.

    “Hiyo ndiyo Gitarama; jehanamu juu ya uso wa dunia. Ama tuseme tawi dogo la jehanamu duniani.”
    GEREZA LA GITARAMA: Jehenamu duniani! Jiji la Gitarama hupatikana katikati ya nchi ya Rwanda, kwa makadirio kilomita arobaini na tano toka kwenye jiji kubwa nchini humo; jiji la Kigali, jiji pekee lililoitangulia Gitarama kwa ukubwa. Kama haitoshi ni hapahapa katika jiji hili ndipo kuna historia kubwa ya makutano yaliyofanyika mwezi wa kwanza; mwaka 1961, Rwanda ikatangazwa rasmi kama jamhuri. Vilevile jiji hili (kipindi hicho mji) likatoa raisi wa kwanza wa Rwanda, bwana Gregoire Kayibanda, ambaye kumbukumbuye mpaka sasa imesimamishwa katikati ya eneo hili. Mazuri hayo hayakomei hapo, hapana! Bali pia hili jiji likabarikiwa na kutunukiwa vivutio kadha wa kadha vya utalii na taasisi lukuki za elimu ambazo aidha zaweza jaza ukumbi nikizianisha hapa. Na kwa namna moja ama nyingine nachelea kusema taasisi hizo zilijengwa (zimejengwa) kwa lengo chanya la kuwafanya watu wapate elimu na hatimaye kujikomboa kifikra na kimwili. Lakini mbali na taasisi hizo, na aidha vivutio na uzuri wa jiji hili, upande wa pili wa sarafu ukisikia jina hili ‘Gitarama’, yakupasa uhofie na hata kushikwa na huruma kwa namna binadamu kama wewe wanavyotendwa, tena bado wakiwa hai kabisa. Binadamu hao wakiwa wanaishi ndani ya eneo ambalo hakuna binadamu yeyote juu ya uso wa dunia angelipenda kuwamo kwa gharama yoyote ile! GITARAMA; ‘JEHANAMU DUNIANI’: Sehemu nyingi duniani zimewahi kuitwa jehanamu. Na jina hili lilishamiri zaidi baada ya vita vya pili vya dunia ambapo maeneo kadhaa yalipewa jina hili kuwakilisha maeneo yasiyokalika, hatari na yasiyo na afya stahiki kwa wanadamu. Maeneo hayo mathalani ni Blood Falls (Maanguko ya damu) huko Antarktika, Danakil Depression (bonde la Danakil) huko Ethiopia, Door to Hell (mlango wa kuzimu) huko Turkmenistan, Kamchatka Peninsula huko Russia na kadhalika, na kadhalika. Japokuwa sehemu hizo zipo nyingi zikipatikana maeneo mbalimbali, ni dhahiri kuna sifa ambazo hushirikiana na hivyo basi ndio maana huwekwa chini ya mwamvuli mmoja wa ‘jehanamu’. Upande wa kusini magharibi mwa jiji la Kigali, ndipo ilipo jela hii Gitarama. Kwa sasa inaitwa jela ya Muhanga ikichukua jina la wilaya ambayo ndiyo makazi yake mpaka sasa. Majengo ya jela hiyo yalikuwa yanamilikiwa na waingereza British housing complex mnamo mwaka 1960 yakiwa yamejengwa kama makazi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo. Pale kampuni ilipofungwa, eneo hilo likakodiwa na serikali ya kwanza ya Rwanda iliyokuwa imedhamiria kufanya majengo hayo kuwa jela ya kisiasa (political prison). Tangu hapo hakuna chochote kilichobadilika ndani ya jela hiyo isipokuwa tu serikali ya Rwanda ambapo kila serikali iliyoingia madarakani ilionekana kuipatia ama kuitafutia matumizi eneo hilo. Kwa mujibu wa gazeti la London Independent mwaka 1995, hii ndiyo jela mbaya zaidi kuwahi kutokea duniani. Pia wanda za tovuti nyingi za mitandao, zinakiri na kuiweka jela hii kwenye kumi, ama tano, ama tatu bora zaidi ya jela hatari mno kuwahi kutokea duniani. Gitarama ilijengwa kwa ajili ya kumudu wafungwa mia nne tu, lakini mpaka sasa inabebelea wafungwa elfu saba! Mara kumi na nane kwa makadirio. Hali hii inapelekea mahesabu ya wafungwa wanne kurundikana katika eneo la hatua tatu (three feet). Hili laweza likawa la kawaida sana ukilisoma hapa, lakini ukijaribu kutoka nje ya bandiko hili na kujikuta ukiwa umekaa na watu wengine watatu ndani ya eneo la hatua tatu tu, kidogo waweza kuelewa. Hakuna mahali pa kulala, kujilaza, wala pa kuketi. Wafungwa husimama wakikung’utwa na jua na wakipoozwa na mvua kwakuwa jela hii kwa kiasi kikubwa haina paa la kuwakinga wafungwa na jua, mvua wala baridi. Kutokana na kutapakaa kwa wafungwa hao kwenye eneo hilo dogo, inakuwa ngumu sana kwa mfungwa kutaka kwenda chooni akafanikiwa kwa muda, hali hii inapelekea wafungwa kujisaidia popote pale na hivyo basi kujaza vinyesi, mikojo na harufu kila eneo. Wafungwa huozeshwa na kumomonywa miili na bakteria mpaka kufa kwasababu ya kujiweka karibu, aidha kwa kulala ama kusimama kwenye vinyesi na uchafu wa kila aina (gangrene). Wafungwa wengi hawana vidole, nyayo na miguu kwasababu ya kuoza wakiwa hai. Miguu hubadilika rangi na hata kutoa madonda. Ni kawaida kuona mtu ana wadudu miguuni huku wakitembea. Kati ya wafungwa kumi ndani ya jela hii, nane hufa kwa kukosa hewa ama magonjwa mbalimbali. Lakini wanapotoka kwenda kuzikwa, basi huingizwa wafungwa wengine ndani ya mlango mkubwa wenye kutu wenye kutoa malalamiko ya ukuukuu. Lakini ajabu na kweli ni kwamba, wafungwa waliomo humo ndani hakuna hata mmoja ambaye amepitia mahakamani akathibitishwa ya kwamba ana makosa na anastahili kufungwa. Wengi wao, kama si wote, ni wa Hutu. Na walianza kujazwa humo miaka ya 1990's wakituhumiwa kwa mauaji ya Kimbari yaliyokwapua maisha ya wana Rwanda zaidi ya milioni moja. Na hii huonekana ni sababu kubwa inayofanya serikali kutokujali kabisa jela hiyo achilia mbali aliye madarakani ni mtutsi. "Watu wanafanyana vitoweo." Si tu kwamba hakuna mahali pa kupumzikia, bali ndani ya jela hii kuna rekodi kadha wa kadha mfungwa kumuua mwenzake kisha kumla kama chakula. Mgawo wa chakula ni finyu sana. chakula na maji hutolewa mara moja tu kwa juma, tena kikiwa kibovu na hakitoshelezi; mara nyingine chakula kinakosekana kabisa na hivyo basi kuwalazimu wafungwa kumaliza siku kadha wa kadha pasipo kutia kitu tumboni. Kwakuwa kila mtu anataka kuishi, wafungwa wengine huamua kuchukua hatua ya kulinda uhai wao kwa kuwanyonga wenzao, kuwabamiza ukutani mpaka mauti kisha kuwatafuna wakiwa wabichi na wakivuja damu moto. Wengine hucheza kamari kabisa, ambapo wahusika huchaguliwa kwa kukurupushwa. Mwisho wa siku wahanga wa Kamari hiyo hupotea isijulikane wameenda wapi ndani ya jela, bali matumboni. Kumbuka kwamba yote haya yanawezekana tena kwa urahisi kwa sababu ndani ya jela hii hakuna hata mlinzi anayediriki kuingia, ni wafungwa wenyewe tu ndio ambao hujihudumia wenyewe. Chakula na maji vikiletwa, huachwa mlangoni kabla ya wafungwa wenyewe kunyakuwa na kuanza kujigawia. Ndio maana mtu anaweza akafa mpaka akaoza ndani ya jela hii kabla hajaja tolewa na kwenda kuzikwa kwenye makaburi ya pamoja. Kulana wenyewe kwa wenyewe si jambo geni wala la kushhtukiza kwa walinzi wa jela hiyo wala tawala husika. Juhudi za kubadilisha hali ya Gitarama: Kwa namna moja ama nyingine kuna watu na mashirika yaliyoguswa na hali ya kusikitisha kuhusu Gitarama. Japokuwa kweli waliomo humo wanaweza wakawa ni watu waliofanya makosa mbalimbali, ikiwemo hata kuua, lakini halibadilishi dhana ya kwamba na wao wanahitaji haki za binadamu kama wengineo. Shirika la Global Giving, likisukumwa na kiongozi wa projekti hii Karen Tse, ni moja ya shirika lisilonuwia faida lililoguswa na hata kuanzisha kampeni ya kutafuta pesa kwa ajili ya kuwasaidia wafungwa hao. Mpaka sasa shirika hili li wazi na unaweza ukawachangia. Pesa waliyoichangisha mpaka sasa ni dola za kimarekani 325 huku wakifadhiliwa na mashirika mawili fadhili na huu ukiwa ni mwaka wa sita sasa wapo moto (active). Mbali na hapo wanajitutumua kuwasaidia wafungwa hao kisheria ili kesi zao zipatwe kusikilizwa mahakamani. Japokuwa swala hili linaonekana ndoto zaidi ya uhalisia tangu mkono wa serikali unakuwa mzito sana kutingisha kidole. “Hiyo ndiyo Gitarama; jehanamu juu ya uso wa dunia. Ama tuseme tawi dogo la jehanamu duniani.”
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·849 Views
  • Wanaitwa ‘MANTIS SHRIMP’ mwenye pigo sawa na nguvu ya bunduki

    ❇Hawa ni moja kati ya viumbe hatari sana wanaopatikana baharini hasa bahari ya Hindi hapa Tanzania Kitalaam anaitwa “Stamatopoda”
    .
    ❇wana urefu wa cm 20 sawa na inchi 8 na uzitowao ni Gram 90 – 100 lakini mambo yao ni konki
    .Kwa umbo wanamagamba mazuri yenye kuvutia lakini ni moja ya viumbe hatari sana baharini
    .
    ❇wanauwezo wa kupiga sehemu na kuvunja na nguvu yake ni sawa na risasi wanauwezo wa kupasua vile vioo vya mabwawa ya kuhifadhia samaki (aquarims) kwa Single Hit)
    .
    ❇Mantis huwa hawachangani, ni wakali sana hasa kwenye mipaka yao yaani ukiingia bahati mbaya kwenye anga zao umeyatimba
    .
    ❇Huwa wanatoa sauti za chini sana ambazo huwasiliana kama ikitokea wakakutana na nadra sana kuona wanapigana
    .
    ❇Macho yao yako kwa juu kama antena na yana uwezo mkubwa wa kuona na kujua direction ya predators au prey
    .pia yana uwezo wa kwenda direction tofauti tofauti yaani moja kaskazini na moja kusini, Vile vile wanakucha ambazo hutumia kumkamata prey anapokua karibu
    .
    ❇Chakula chao kikuu ni ngadu, Samaki na baadhi ya viumbe vingine na wanakula samaki ambao huwa wakubwa kuliko hata umbo lao
    .
    ❇Huwa wanatumia mechanism tofauti sana pale wanapotaka kutafuta chakula wanauwezo wa kupiga maji yakatengeneza mawimbi makubwa tu kukelekea direction ya prey na kabla ya prey hajafanya maamuzi anapigwa round kick kali sana..
    .
    ❇Wanauwezo wa kugundua Mgonjwa wa cancer kwa macho yao na hii ni kwasabu macho yanauwezo mkubwa sana wakuona na kugundua movement nampangilio wa neurons (Hii ni kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Queensland)
    .
    ❇Kwa kawaida huwa na life partner yaani bebi mmoja tu kwenye maisha yao na muda wa kutaga jike na dume hulalia pamoja mayai mpaka muda wa kupata watoto
    .
    ❇Adui yao mkubwa ni binadamu maana nchi kama Japan na China huwa wanawala sana na wakati mwingine huwa wanaaminishwa na imani fulani kama moja ya viumbe vyenye kuongeza sana nguvu ya mwili kwa kuimarisha seli hai nyeupe (white blood cells).
    Wanaitwa ‘MANTIS SHRIMP’ mwenye pigo sawa na nguvu ya bunduki ❇Hawa ni moja kati ya viumbe hatari sana wanaopatikana baharini hasa bahari ya Hindi hapa Tanzania Kitalaam anaitwa “Stamatopoda” . ❇wana urefu wa cm 20 sawa na inchi 8 na uzitowao ni Gram 90 – 100 lakini mambo yao ni konki .Kwa umbo wanamagamba mazuri yenye kuvutia lakini ni moja ya viumbe hatari sana baharini . ❇wanauwezo wa kupiga sehemu na kuvunja na nguvu yake ni sawa na risasi wanauwezo wa kupasua vile vioo vya mabwawa ya kuhifadhia samaki (aquarims) kwa Single Hit) . ❇Mantis huwa hawachangani, ni wakali sana hasa kwenye mipaka yao yaani ukiingia bahati mbaya kwenye anga zao umeyatimba . ❇Huwa wanatoa sauti za chini sana ambazo huwasiliana kama ikitokea wakakutana na nadra sana kuona wanapigana . ❇Macho yao yako kwa juu kama antena na yana uwezo mkubwa wa kuona na kujua direction ya predators au prey .pia yana uwezo wa kwenda direction tofauti tofauti yaani moja kaskazini na moja kusini, Vile vile wanakucha ambazo hutumia kumkamata prey anapokua karibu . ❇Chakula chao kikuu ni ngadu, Samaki na baadhi ya viumbe vingine na wanakula samaki ambao huwa wakubwa kuliko hata umbo lao . ❇Huwa wanatumia mechanism tofauti sana pale wanapotaka kutafuta chakula wanauwezo wa kupiga maji yakatengeneza mawimbi makubwa tu kukelekea direction ya prey na kabla ya prey hajafanya maamuzi anapigwa round kick kali sana.. 😀 . ❇Wanauwezo wa kugundua Mgonjwa wa cancer kwa macho yao na hii ni kwasabu macho yanauwezo mkubwa sana wakuona na kugundua movement nampangilio wa neurons (Hii ni kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Queensland) . ❇Kwa kawaida huwa na life partner yaani bebi mmoja tu kwenye maisha yao na muda wa kutaga jike na dume hulalia pamoja mayai mpaka muda wa kupata watoto . ❇Adui yao mkubwa ni binadamu maana nchi kama Japan na China huwa wanawala sana na wakati mwingine huwa wanaaminishwa na imani fulani kama moja ya viumbe vyenye kuongeza sana nguvu ya mwili kwa kuimarisha seli hai nyeupe (white blood cells).
    0 Comments ·0 Shares ·564 Views

  • MCHEZAJI MKUBWA KAONGEA KIKUBWA SANA HAPA

    NAPENDA SIMBA WANAVYOCHEZA NAWAOMBEA PIA WASHINDE!

    AUCHO AISIFIA SIMBA NA KUIOMBEA MAZURI KIMATAIFA!
    #paulswai
    MCHEZAJI MKUBWA KAONGEA KIKUBWA SANA HAPA NAPENDA SIMBA WANAVYOCHEZA NAWAOMBEA PIA WASHINDE! AUCHO AISIFIA SIMBA NA KUIOMBEA MAZURI KIMATAIFA! #paulswai
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·479 Views
  • JINSI SHIRIKA LA KIJASUSI LA URUSI FSB {KGB} LILIVYO HATARI....

    Kama waswahili wasemavyo maisha ni safari ndefu na kifo ni Siri, pengine hili ni kweli kutokana na sintofahamu iliyochukua uhai wa Alexander Litvinenko, jasusi wa zamañi wa KGB na baadae FSB ya Urusi ya sasa.

    Tutarudi Sasa tuendelee mwishoni mwa wiki za mwezi wa kumi mwaka 2006 Alexander Litvinenko alipokuwa jijini London alipotorokea baada ya rabsha dhidi ya serikali mjini Moscow, siku hiyo Litvinenko alikuwa ametembelewa na marafiki zake wawili walikuwa wanausalama ndani ya FSB na iliyokuwa KGB Dmitri Kovtun na Andrei Lugovoi, asichokijua ni kwamba wale wawili walikuwa moja ya watu hatari na pia kama wasafirishaji mahiri wa msafiri kama Litvinenko kuliendelea kaburi

    Waliikutana hotelini jijini London wakinywa na kufurahi, siku hiyo Lugovoi na Kovtun wao waliagiza bia wakanywa wakifurahi, unajua nini Litvinenko ye aliagizwa chai ya rangi akanywa huku akiwachekea wasafirishaji wa ule msemo wa kiswahili " maisha ni safari"

    Maskinii Litvinenko alipojichanganya tu Lugovoi na Kovtun wakifanya kazi yao moja waliotumwa na FSB, kumnyamazisha " traitor of the mother Russia"

    Unajua walifanya Nini? Walichukua kemikali hatari sana duniani inayoua taratibu sana jina lake Polonium 210 wakatia katika chai ya Litvinenko. Inavyosemekana alivyorudi walimchekea na kufurahi zaidi kuona Litvinenko alikuwa amesahau mbinu muhimu kabisa ya wanaintelijensia kote duniani ! Kutomwamini mtu hata mama na baba yako.
    Litvinenko alikunywa chai ile

    **********
    Lugovoi na Kovtun walichukua ndege siku tatu baadae haoo Moscow, huko walifanyiwa sherehe ya uhakika wa kazi iliyofanyika isiyo na shaka, Kovtun aliamua kuwa mfanyabiashara mkubwa wakati Lugovoi alipandishwa cheo siku chache baadae.
    ******
    Maskini Litvinenko aliagana na wanyama wale wa kwenye barafu Kama wajiitavyo wao " "bear " lakini akiwapachika majina mazuri yaani marafiki, ndugu, wapenzi kutoka home Russia. Pia aliwauliza vipi watarudi lini kumuona, kimoyomoyo Kovtun na Lugovoi walikua wakicheka na kusikitika kiunafiki,wakijua huyu mtu hana mwezi duniani. Wiki tatu nyingi! atakufa kifo Cha mateso akiwa kitandani amelala.

    ***
    November 1 mwaka 2006 Litvinenko aliugua homa ya ghafla mwili ukiungua kwa namna ya kutisha sana, alipelekwa hospitali mjini London akaishi kwa wiki 3 akiwa hoi kitandani! Wakati akifa akitoa laana kwa Putin akamshutumu amemuua.

    Huo ukawa mwisho wa Litvinenko mtu aliyekuwa ameaminiwa kutunza siri za Russia yeye alizitoa hadharani kwa m16 . Pengine ni chafu sana zenye damu lakini bila shaka kulikuwa pigo kwa vitu hivyo kuwa hadharani. Putin alivuliwa nguo hata asiijifunike.

    Tuzungimzapo Leo ni miaka karibu 12 toka mnyama huyu atutoke.

    Mwaka fulani Putin aliulizwa na mwanahabari mmoja ni kitu gani asichoweza kuvumilia na kusamehe alisema hivi.. Ye ni ngumu sana kuwasamehe wasaliti wa mother Russia.

    Ohh ndo hivyo Litvinenko hakupata bahati ya kusamehewa na Putin hivyo alikwenda.

    Chanzo: na Google
    JINSI SHIRIKA LA KIJASUSI LA URUSI FSB {KGB} LILIVYO HATARI.... Kama waswahili wasemavyo maisha ni safari ndefu na kifo ni Siri, pengine hili ni kweli kutokana na sintofahamu iliyochukua uhai wa Alexander Litvinenko, jasusi wa zamañi wa KGB na baadae FSB ya Urusi ya sasa. Tutarudi Sasa tuendelee mwishoni mwa wiki za mwezi wa kumi mwaka 2006 Alexander Litvinenko alipokuwa jijini London alipotorokea baada ya rabsha dhidi ya serikali mjini Moscow, siku hiyo Litvinenko alikuwa ametembelewa na marafiki zake wawili walikuwa wanausalama ndani ya FSB na iliyokuwa KGB Dmitri Kovtun na Andrei Lugovoi, asichokijua ni kwamba wale wawili walikuwa moja ya watu hatari na pia kama wasafirishaji mahiri wa msafiri kama Litvinenko kuliendelea kaburi Waliikutana hotelini jijini London wakinywa na kufurahi, siku hiyo Lugovoi na Kovtun wao waliagiza bia wakanywa wakifurahi, unajua nini Litvinenko ye aliagizwa chai ya rangi akanywa huku akiwachekea wasafirishaji wa ule msemo wa kiswahili " maisha ni safari" Maskinii Litvinenko alipojichanganya tu Lugovoi na Kovtun wakifanya kazi yao moja waliotumwa na FSB, kumnyamazisha " traitor of the mother Russia" Unajua walifanya Nini? Walichukua kemikali hatari sana duniani inayoua taratibu sana jina lake Polonium 210 wakatia katika chai ya Litvinenko. Inavyosemekana alivyorudi walimchekea na kufurahi zaidi kuona Litvinenko alikuwa amesahau mbinu muhimu kabisa ya wanaintelijensia kote duniani ! Kutomwamini mtu hata mama na baba yako. Litvinenko alikunywa chai ile ********** Lugovoi na Kovtun walichukua ndege siku tatu baadae haoo Moscow, huko walifanyiwa sherehe ya uhakika wa kazi iliyofanyika isiyo na shaka, Kovtun aliamua kuwa mfanyabiashara mkubwa wakati Lugovoi alipandishwa cheo siku chache baadae. ****** Maskini Litvinenko aliagana na wanyama wale wa kwenye barafu Kama wajiitavyo wao " "bear " lakini akiwapachika majina mazuri yaani marafiki, ndugu, wapenzi kutoka home Russia. Pia aliwauliza vipi watarudi lini kumuona, kimoyomoyo Kovtun na Lugovoi walikua wakicheka na kusikitika kiunafiki,wakijua huyu mtu hana mwezi duniani. Wiki tatu nyingi! atakufa kifo Cha mateso akiwa kitandani amelala. *** November 1 mwaka 2006 Litvinenko aliugua homa ya ghafla mwili ukiungua kwa namna ya kutisha sana, alipelekwa hospitali mjini London akaishi kwa wiki 3 akiwa hoi kitandani! Wakati akifa akitoa laana kwa Putin akamshutumu amemuua. Huo ukawa mwisho wa Litvinenko mtu aliyekuwa ameaminiwa kutunza siri za Russia yeye alizitoa hadharani kwa m16 . Pengine ni chafu sana zenye damu lakini bila shaka kulikuwa pigo kwa vitu hivyo kuwa hadharani. Putin alivuliwa nguo hata asiijifunike. Tuzungimzapo Leo ni miaka karibu 12 toka mnyama huyu atutoke. Mwaka fulani Putin aliulizwa na mwanahabari mmoja ni kitu gani asichoweza kuvumilia na kusamehe alisema hivi.. Ye ni ngumu sana kuwasamehe wasaliti wa mother Russia. Ohh ndo hivyo Litvinenko hakupata bahati ya kusamehewa na Putin hivyo alikwenda. Chanzo: na Google
    0 Comments ·0 Shares ·858 Views
  • PICHA NI MKE NA MAMA WATOTO WA MCHEZAJI POGBA

    Picha ni mwadada Mrembo Ambaye ni mke wa Kiungo Fundi Mwenye Asili ya Guinea Paul Labile Pogba ambaye kwa sasa amesimama kujihusisha na Soka kutokana na kutumia madawa yasiyofaa kwenye Michezo.

    Mrembo huyo kwa Majina anaitwa Maria Zulay Salaues amezaliwa kwenye Mji wa Robore, Nchini Bolivia.

    Pogba ni miongoni Mwa wachezaji ambao wanamiliki mwanamke Sahihi na mrembo.

    Zulay amezaliwa mwaka 1994 Pia Amezaa watoto Wawili na Pogba

    Licha ya Yote anayopitia mume wake lakini mwanadada huyo amekua Akiendelea kua Sahihi kwa Pogba.

    Kuna Kauli za Mitaani zinatukiwa Sana na Vijana ambao hawajajipata wakisema kwamba Tafuta Pesa Wanawake Wazuri wapo.

    NIWAAMBIE tu unaweza kua na Pesa na Mwanamke mzuri ulimmliki kwa Sababu Kumiliki Pisi sio kitu Cha Kawaida tangu enzi za manabi na manabi

    Kuna Watu hawana Ela lakini wanamiliki Wanawake Wazuri na waotokea maisha Mazuri kabisa ✍🏽

    Kwahiyo ni kuomba MUNGU akujalie kwenye Kila kitu

    SOMA KITABU CHA MHUBIRI12:1

    Mkumbuke Muumba (MUNGU )wako Siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku Zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka Utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.
    PICHA NI MKE NA MAMA WATOTO WA MCHEZAJI POGBA Picha ni mwadada Mrembo Ambaye ni mke wa Kiungo Fundi Mwenye Asili ya Guinea Paul Labile Pogba ambaye kwa sasa amesimama kujihusisha na Soka kutokana na kutumia madawa yasiyofaa kwenye Michezo. Mrembo huyo kwa Majina anaitwa Maria Zulay Salaues amezaliwa kwenye Mji wa Robore, Nchini 🇧🇴Bolivia. Pogba ni miongoni Mwa wachezaji ambao wanamiliki mwanamke Sahihi na mrembo. Zulay amezaliwa mwaka 1994 Pia Amezaa watoto Wawili na Pogba Licha ya Yote anayopitia mume wake lakini mwanadada huyo amekua Akiendelea kua Sahihi kwa Pogba. Kuna Kauli za Mitaani zinatukiwa Sana na Vijana ambao hawajajipata wakisema kwamba Tafuta Pesa Wanawake Wazuri wapo. NIWAAMBIE tu unaweza kua na Pesa na Mwanamke mzuri ulimmliki kwa Sababu Kumiliki Pisi sio kitu Cha Kawaida tangu enzi za manabi na manabi Kuna Watu hawana Ela lakini wanamiliki Wanawake Wazuri na waotokea maisha Mazuri kabisa ✍🏽 Kwahiyo ni kuomba MUNGU akujalie kwenye Kila kitu SOMA KITABU CHA 📖MHUBIRI12:1 Mkumbuke Muumba (MUNGU )wako Siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku Zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka Utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.
    0 Comments ·0 Shares ·418 Views
  • IFAHAMU SHULE YA BEI KUBWA ZAIDI DUNIANI.

    Shule ya bei kubwa zaidi Duniani inaitwa Instut Le Rosey ambayo ipo Switzerland, ada ya Mwanafunzi mmoja kwa mwaka sio chini ya USD 117,434 ambayo kwa Tsh. ni kama Milioni 272 Unaambiwa ukiachia mazingira mazuri.

    Shule ipo karibu na Ziwa, ina madarasa 50, Maabara 8 za Sayansi, Theater na kila asubuhi Wanafunzi hupata breki ya kula chocolate

    Ukiacha masomo, Wanafunzi hufundishwa kucheza golf, kutumia farasi, wanacho chumba maalum kwa ajili ya muziki na studio kwa ajili ya sanaa nyingine Wanafunzi wanaweza kujifunza kwa lugha mbili ambazo ni Kiingereza na Kifaransa ambapo pamoja na kwamba ni Shule ya bei ghali lakini wanausambaza upendo mwingi kwa Afrika ambako wamejenga Shule kwenye nchi ya Mali
    IFAHAMU SHULE YA BEI KUBWA ZAIDI DUNIANI. Shule ya bei kubwa zaidi Duniani inaitwa Instut Le Rosey ambayo ipo Switzerland, ada ya Mwanafunzi mmoja kwa mwaka sio chini ya USD 117,434 ambayo kwa Tsh. ni kama Milioni 272 Unaambiwa ukiachia mazingira mazuri. Shule ipo karibu na Ziwa, ina madarasa 50, Maabara 8 za Sayansi, Theater na kila asubuhi Wanafunzi hupata breki ya kula chocolate Ukiacha masomo, Wanafunzi hufundishwa kucheza golf, kutumia farasi, wanacho chumba maalum kwa ajili ya muziki na studio kwa ajili ya sanaa nyingine Wanafunzi wanaweza kujifunza kwa lugha mbili ambazo ni Kiingereza na Kifaransa ambapo pamoja na kwamba ni Shule ya bei ghali lakini wanausambaza upendo mwingi kwa Afrika ambako wamejenga Shule kwenye nchi ya Mali
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·543 Views
  • HIVI NDIVYO UNAVYOMSAMEHE ALIYEKUUGUA MOYO.

    Unawasamehe kwa kujipa muda wa kupona. Hii haifanyiki mara moja. Hii haifanyiki mara moja. Ni mwendelezo wa polepole. Unapiga hatua mbili mbele na hatua nne nyuma. Wakati mwingine haitakuwa na maana. Lakini unakua na nguvu kidogo, na ustahimilivu zaidi, kila siku. Hata kama hauoni kila wakati.

    Unawasamehe kwa kuzingatia wewe mwenyewe. Acha kumwaga nishati yako kwenye sumu. Unachomoa. Unaacha kufuata. Fanya mazoezi ya kujitunza. Soma tena vitabu unavyovipenda na utoke pamoja na marafiki zako bora, mkicheka na kukumbuka jinsi mambo yanavyoweza kuwa mazuri wakati unajizunguka kwa chanya. Uambie moyo wako uliovunjika ni sawa kuchukua pumziko ili kukumbuka jinsi ya kutabasamu tena.
    Unawasamehe kwa kujiondoa kwenye hali hiyo. Kadiri unavyokaa ndani yake, katika maumivu ya moyo, ndivyo inavyozidi. Ni ngumu, lakini lazima uiache peke yako. Heshimu hisia zako. Heshimu hisia zako. Lakini usiendelee kuzunguka nyuma. Usiendelee kuhangaikia kilichotokea. Wazia kama puto. Wacha ielee. Mwambie kwaheri. Haiwezi kukuumiza sasa.
    Unawasamehe kwa kukubali walichofanya. Hiyo haimaanishi kuwa maumivu yamefutwa. Hiyo haimaanishi kuwa ghafla unafikiri ni sawa au umewaacha waachane na ndoano. Haimaanishi kwamba hawawajibiki kwa matendo yao au kwamba umesahau kilichotokea. Inamaanisha tu kukubali kile kilichofanywa kimefanywa. Inamaanisha kukubali kuwa hakuna kitufe cha kurejesha nyuma. Unaweza tu kusonga mbele.
    Unawasamehe kwa kurejesha maisha yako. Kwa sababu kuna mengi zaidi ya mtu mmoja tu ambaye alivunja moyo wako.

    ✍Sifa kwa Mwandishi halali
    👩🏻‍🎨Pinterest
    HIVI NDIVYO UNAVYOMSAMEHE ALIYEKUUGUA MOYO. Unawasamehe kwa kujipa muda wa kupona. Hii haifanyiki mara moja. Hii haifanyiki mara moja. Ni mwendelezo wa polepole. Unapiga hatua mbili mbele na hatua nne nyuma. Wakati mwingine haitakuwa na maana. Lakini unakua na nguvu kidogo, na ustahimilivu zaidi, kila siku. Hata kama hauoni kila wakati. Unawasamehe kwa kuzingatia wewe mwenyewe. Acha kumwaga nishati yako kwenye sumu. Unachomoa. Unaacha kufuata. Fanya mazoezi ya kujitunza. Soma tena vitabu unavyovipenda na utoke pamoja na marafiki zako bora, mkicheka na kukumbuka jinsi mambo yanavyoweza kuwa mazuri wakati unajizunguka kwa chanya. Uambie moyo wako uliovunjika ni sawa kuchukua pumziko ili kukumbuka jinsi ya kutabasamu tena. Unawasamehe kwa kujiondoa kwenye hali hiyo. Kadiri unavyokaa ndani yake, katika maumivu ya moyo, ndivyo inavyozidi. Ni ngumu, lakini lazima uiache peke yako. Heshimu hisia zako. Heshimu hisia zako. Lakini usiendelee kuzunguka nyuma. Usiendelee kuhangaikia kilichotokea. Wazia kama puto. Wacha ielee. Mwambie kwaheri. Haiwezi kukuumiza sasa. Unawasamehe kwa kukubali walichofanya. Hiyo haimaanishi kuwa maumivu yamefutwa. Hiyo haimaanishi kuwa ghafla unafikiri ni sawa au umewaacha waachane na ndoano. Haimaanishi kwamba hawawajibiki kwa matendo yao au kwamba umesahau kilichotokea. Inamaanisha tu kukubali kile kilichofanywa kimefanywa. Inamaanisha kukubali kuwa hakuna kitufe cha kurejesha nyuma. Unaweza tu kusonga mbele. Unawasamehe kwa kurejesha maisha yako. Kwa sababu kuna mengi zaidi ya mtu mmoja tu ambaye alivunja moyo wako. ✍Sifa kwa Mwandishi halali 👩🏻‍🎨Pinterest
    Like
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·482 Views
  • Najua mpaka sasa umeisikia sana ile GUSA ACHIA TWENDE KWAO. Ningependa nikupe uhondo wake kidogo, msingi wake ni upi na ufanisi wake unatokana na nini?

    Ally Kamwe kama muasisi wa Gusa twende kwao alijaribu kuaminisha wanaYanga kuwa falsafa ya Ramovic ni pira matokeo, lenye speed, na ufanisi wa hali ya juu huku likiambatana na burudani isiyoisha hamu.

    Je unajua ili GUSA ACHIA TWENDE KWAO iwe na ufanisi kinahitajika nini?

    Kuna watu lazima wawepo nyuma ya hii falsafa. Mtu wa kwanza wa muhimu zaidi baada ya kocha mkuu Ramovic, ni kocha wa utimamu wa mwili (Fitness coach). Hapa namuongelea mtu ambae atawafanya wachezaji wa Yanga wakimbie kama vishada, wafukie mashimo uwanjani, na kuweza kuzimudu dakika 90 bila kuchoka. Mpaka hapa tumeelewana?

    Yanga haijapoteza mechi yoyote ya ligi kuu mpaka sasa tangu Ramovic atue nchini. Na alisema wazi ili falsafa ya soka lake lianze kutoa matunda anahitaji wachezaji wake wote wawe vizuri kwenye fitness. Yanga ikaingia sokoni, kusaka mtaalamu wa kutengeneza utamu wa Ramovic. Yanga ikamshusha mtaalamu ADNAN BEHLULOVIC - Fitness coach wa Yanga.

    Nyuma ya pazia la Ramovic na matokeo mazuri ya ligi kuu mpka sasa huwezi kuacha kumtaja Bwana Adnan.

    Pressing ambayo anasifiwa Yanga, inayofanya wapinzani wanafanya makosa, nyuma yake yupo ADNAN.

    Speed na ufanisi wa Yanga kwenye kushambulia bila kuchoka, nyuma ya hayo yote yupo ADNAN.

    Zinachezwa dakika 90 huioni Yanga kama imechoka, kila mchezaji unaona kuwa bado ana hamu ya kuendelea kutwanga dakika zingine 90. ADNAN hajamaliza hata mwezi tangu aanze operesheni rudisha ufiti ndani ya Yanga, huyu kocha wa Fitness siku akimaliza mwezi Yanga ikafikia asilimia 100 ya ufiti nina uhakika kuna timu zitapasuliwa vifua.

    Side wa kijerumani ataimbwa sana, kwa sababu silaha moja ya timu yoyote ni kuwa fiti. Speed ya Yanga imeniogopesha, Pressing yao imeniogopesha, ubora wa Adnan umeniogopesha.

    Ni follow
    #neliudcosiah
    Najua mpaka sasa umeisikia sana ile GUSA ACHIA TWENDE KWAO. Ningependa nikupe uhondo wake kidogo, msingi wake ni upi na ufanisi wake unatokana na nini? Ally Kamwe kama muasisi wa Gusa twende kwao alijaribu kuaminisha wanaYanga kuwa falsafa ya Ramovic ni pira matokeo, lenye speed, na ufanisi wa hali ya juu huku likiambatana na burudani isiyoisha hamu. Je unajua ili GUSA ACHIA TWENDE KWAO iwe na ufanisi kinahitajika nini? Kuna watu lazima wawepo nyuma ya hii falsafa. Mtu wa kwanza wa muhimu zaidi baada ya kocha mkuu Ramovic, ni kocha wa utimamu wa mwili (Fitness coach). Hapa namuongelea mtu ambae atawafanya wachezaji wa Yanga wakimbie kama vishada, wafukie mashimo uwanjani, na kuweza kuzimudu dakika 90 bila kuchoka. Mpaka hapa tumeelewana? Yanga haijapoteza mechi yoyote ya ligi kuu mpaka sasa tangu Ramovic atue nchini. Na alisema wazi ili falsafa ya soka lake lianze kutoa matunda anahitaji wachezaji wake wote wawe vizuri kwenye fitness. Yanga ikaingia sokoni, kusaka mtaalamu wa kutengeneza utamu wa Ramovic. Yanga ikamshusha mtaalamu ADNAN BEHLULOVIC - Fitness coach wa Yanga. Nyuma ya pazia la Ramovic na matokeo mazuri ya ligi kuu mpka sasa huwezi kuacha kumtaja Bwana Adnan. Pressing ambayo anasifiwa Yanga, inayofanya wapinzani wanafanya makosa, nyuma yake yupo ADNAN. Speed na ufanisi wa Yanga kwenye kushambulia bila kuchoka, nyuma ya hayo yote yupo ADNAN. Zinachezwa dakika 90 huioni Yanga kama imechoka, kila mchezaji unaona kuwa bado ana hamu ya kuendelea kutwanga dakika zingine 90. ADNAN hajamaliza hata mwezi tangu aanze operesheni rudisha ufiti ndani ya Yanga, huyu kocha wa Fitness siku akimaliza mwezi Yanga ikafikia asilimia 100 ya ufiti nina uhakika kuna timu zitapasuliwa vifua. Side wa kijerumani ataimbwa sana, kwa sababu silaha moja ya timu yoyote ni kuwa fiti. Speed ya Yanga imeniogopesha, Pressing yao imeniogopesha, ubora wa Adnan umeniogopesha. Ni follow 👇 #neliudcosiah
    Like
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·682 Views
More Results