• Read more
    PICHA YA SIMBA HUYU NI FUNZO MAISHANI: ------------------------------------------------------ Hivi ndivyo mfalme wa pori anavyoonekana akiwa kwenye siku za mwisho za maisha yake. Jinsi alivyokonda, kujua idadi ya mbavu zake hata huitaji msaada wa calculator. Hii picha ilipigwa na "Larry Pannell." Alifanikiwa kupata picha ya Simba aliyekuwa kwenye hitimisho la kuvuta pumzi za mwisho. Katika huu ulimwengu wenye mafungamano na dhambi. "Larry Pannell" anasema: Nilimkuta huyu simba amelala kwenye majani. Akiwa amechoka, miguu ikionekana kumnyima ushirikiano wa kutembea. Sikuwa na lakufanya zaidi ya kusimama mita kadhaa. Macho yakifanya ushuhuda wa kutazama, "King of savannah" akipoteza uhai chini ya kivuli cha mti. Nikiwa nimesimama kimya. Nilishusha chini camera yangu. Tulitazamana na simba, tukafumba macho yetu pamoja. Jinsi mfalme wa nyika alivyokuwa akihangaika kuhema. Pumzi zilionekana kuwa bidhaa hadimu kwenye duka la mapafu yake. Kifua chake kilikuwa kikipanda na kushuka. Ishara ya kuonyesha anavuta pumzi za mwisho, kabla ya kukipa ruhusa kifo kiondoke na roho yake. Ghafla eneo alilolala Simba ukazaliwa ukimya. Mfalme wa pori akawa haemi wala kutikisika. Mauti ikawa imehitimisha simulizi ya ubabe wake mbugani. Hakika maisha ya binadamu na wanyama ni simulizi fupi sana." Haijalishi una nguvu kiasi gani. Kuna nyakati zitafika nguvu zitafanya mgomo wa kuishi mwilini mwako. Zitaupisha udhaifu uchukue nafasi ya kukutawala. Udhaifu nao ukikutawala, utayaita maradhi. Bila hiyari utajikuta umekigeuza kitanda kuwa rafiki." Kuna shule ya bure hapa: Nguvu tulizonazo ni kitu cha kupita. Hata uzuri umpao kiburi mwanamke una ukomo. Licha ya kujidanganya kwa make up na wanja. Lakini hawezi kuzuia muanguko wa mashavu, uzee unapoanza kumuondoa kwenye kundi la warembo. "Chini ya jua kila kitu kina mwanzo na mwisho." Hivyo katika maisha tusisahau kuvipa kipaumbele vitu hivi. Utu, wema, ukarimu, heshima, na unyenyekevu. Tusaidie wenye maradhi, tuwajali wasiojiweza, na viongozi tusitumie madaraka vibaya. Tutende mema tukiamini. Kuna siku pumzi zitamaliza mkataba wa kuishi ndani ya matundu ya pua zetu. Baada ya hapo sisi wote tutalala mauti." Imeandikwa na Green Osward
    0 Comments ·0 Shares ·55 Views
  • Read more
    "Najisikia vibaya namna watu wanavyoniona na kuanza kuniita Yesu, wanafikia hata kutundika picha zangu katika nyumba zao, mimi ni mwigizaji tu, mimi ni mtu" - Jonathan Roumie(50), mwigizaji wa Marekani Aidha, Jonathan Roumie katika mahojiano amesema maisha yake binafsi alikuwa na hali mbaya kiuchumi hakuwa na uhakika siku inayofuata atakula nini, alikuwa mwigizaji ila kiuchumi alikuwa bado hajafanikiwa. Baada ya mambo kuzidi kuwa magumu siku moja ni kama alikuwa anamuomba Mungu kuhusu hali anayopitia ili mambo yake yakae sawa Baada ya miezi kama mitatu ndio akapata nafasi ya kuigiza kama Yesu katika series ya "The Chosen" iliyoanza kuoneshwa 2017 ambayo imejipatia umaarufu mkubwa sana hadi sasa imetazamwa na watu zaidi ya milioni 250 na misimu mipya inafuata huku ikipongezwa kwa kinachoonekana kuigizwa Umaarufu wa uhusika wake kama Yesu umempa umaarufu mkubwa na fursa nyingi ikiwemo katika mikutano na makongamano makubwa ya kidini na app za dini ya kikiristo Jonathan ambaye ni mkatoliki, alipoulizwa na New York Times, je ni tukio gani gumu analokumbuka ambalo alishakutana nalo baada ya kuigiza kama Yesu, amejibu kwa kusema kuna kipindi alikuwa katika mkutano kwenye uwanja wenye watu takribani 40,000 baadaye alishuka stejini akaenda kwenye chumba fulani uwanjani hapo, mmoja wa walinzi alikuja akamwambia nje kuna mwanamke ana mtoto kwenye kiti cha magurudumu anaomba kusalimiana na wewe Jonathan alitoka akaonana na mwanamke husika na mwanae ambaye kwa ufupi alieleza jinsi Yesu alivyoponya mtu katika hiyo series ya "The Chosen" na kusema angependa mwanae pia apone yaani akimtaka Jonathan amponye mtoto wake. Ilibidi Jonathan amueleze ukweli kwamba yeye sio mponyaji wala mhubiri bali ni mwigizaji tu. Jonathan akamueleza wafanye maombi wote ilichukua kama dakika moja, walipomaliza maombi wakafurahi na kushukuru kisha Jonathan akarudi alipokuwa huku akitokwa na machozi akihisi amewaangusha matarajio waliyokuwa nayo kwake ila amesema ni bora waujue ukweli kuwa yeye sio Yesu wala mponyaji bali ni mwigizaji tu Ukiacha hayo ya uhusika wake wa Yesu na dini, Jonathan Roumie amegusia pia kwamba alishafika Tanzania na Rwanda sababu kuna watoto kadhaa wanaoishi katika mazingira magumu huwa anawasaidia na familia zao Jonathan Roumie pia ameweka wazi kwamba anatamani watu pia wawe wanamuona katika nyuma ya pazia(behind the scene) anayopitia katika kujiandaa na uigizaji wake kama Yesu ili watu wengine waelewe wajue kumtofautisha katika maisha halisi na kisanaa KUMBUKA, zipo filamu nyingine miaka ya nyuma kuhusu Yesu zilizohusisha waigizaji wengine kabla ya sasa Jonathan Roumie kupata umaarufu na uhusika wa Yesu katika series maarufu ya "The Chosen" (Swahili Word)
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·136 Views
  • Read more
    “Wazazi wangu waliniita N’golo kwa sababu ni jina la mfalme wa zamani huko Mali. Mfalme ambaye alianza kutoka chini kushinda ufalme. Nilikuwa nakusanya taka. Leo nacheza mpira na wananitazama kwenye TV. Hadithi yangu pia ni nzuri, nilianzia chini.” - N'golo Kante, Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa mwenye asili ya Mali.
    0 Comments ·0 Shares ·139 Views
  • Read more
    "Sijui kama mnaona jinsi Trump na Marekani yake wanavyocheza na Dunia kupitia ugomvi au migogoro ya Dunia ili kuipatia faida Marekani kwa kisingizio cha kutafuta amani huku nyuma ya pazia Marekani ikipata faida kupitia migogoro au vita. Tazama Makubaliano ya Madini pale Ukraine Ambapo Marekani watafaidika na Rasilimali za madini za Ukraine, yani ili Marekani waisadie Ukraine ni lazima Ukraine kuipatia madini yake Marekani Congo nayo inakaribia kusaini mkataba wa kuipatia Marekani madini ili Marekani iipatie ulinzi hapo tunazungumzia rasimali za Congo amabzo zinaenda kutumika kama faida kwa Marekani kisa tu ni ugomvi wa Afrika wenyewe kwa wenyewe na hapo hapo Trump katupiga Bao Huko Gaza napo mpango wa kuwahamisha wakazi wa Gaza kwa kisingizio cha kuijenga upya Gaza umeiva, Trump haijengi Gaza bure anafahamu fika kuwa chini ya ardhi ya Gaza kuna utajiri mkubwa wa maliasili ya Gesi na mafuta Huyo ndiye Trump mfanyabiashara kutoka White House ambaye anaenda sambamba na ule msemo unaosema "no free lunch in America" yaani hakuna chakula cha mchana cha bure Marekani, ukiona unapewa cha bure ujue badae utalipia tu!!" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa Siasa.
    0 Comments ·0 Shares ·139 Views
  • Read more
    VITABU VYENYE NGUVU DUNIANI AMBAVYO HAUTAFUNDISHWA SHULENI: SIRI KUBWA YA UTAJIRI WA ULIMWENGU! Je, umefundishwa katika dini yako kuwa Biblia na Quran ndio vitabu pekee vyenye nguvu na maajabu? Ni kweli vitabu hivi ni miongoni mwa vitabu vyenye maajabu, ila kuna baddhi ya vitabu vinavyofichwa kutokana na nguvu zake za kubadili maisha ya watu, kwa utajiri ama wakawa masikini wa kutupwa na hata kuwa wenye mikosi mikubwa. Dunia imejawa siri ambazo wachache wanazitumia kujinufaisha na kujitajirisha, huku wakiwadanganya wengine Kuwa ili ufanikiwe basi wafaa upate muda wa kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa, uwe mvumilivu, Ufanye kazi kwa bidii na mambo mengine mengi, lakini hawakuambii mambo ya siri wanayoyafanya na vitabu vya siri wanavyosoma ili kukuza utajiri wao na mvuto wao katika ulimwengu. Leo hii nimekuletea vitabu vya siri zaidi ya Biblia na Quran, vyenye nguvu sana, na vinavyotumika kubadili maisha ya Matajiri wa dunia hii, na imebakia kuwa siri kwao, wakiificha kwa nguvu zote na kuhakikisha wachache wanaifahamu, huku wengi wakitiwa hofu ya kuiogopa siri hii na kuviona vitabu hivi kama vya mashetani. 1. The Book of Abramelin the Mage – Kitabu cha kale cha uchawi kinachoeleza njia za kuwasiliana na malaika na nguvu za kichawi. Kitabu hiki kina nguvu za kukufundisha ushirikina na upeo wa juu unaopita uwezo wa kawaida wa mwanadamu. 2.The Lesser Key of Solomon (Lemegeton) – Kitabu cha uchawi kinachodaiwa kuwa na mafundisho ya mfalme Sulemani kuhusu majini na roho. Ni kitabu kinachosadikika kuandikwa na mfalme wa Israel ajulikanaye kama sulemani, kikiwa kimejaa elimu ya kiroho, na namna ya kuyatumia majini katika shughuli za kila siku bila kutumia nguvu kubwa. 3.Picatrix – Kitabu cha uchawi wa Kiarabu kinachoeleza jinsi ya kutumia nyota na sayari kwa utajiri. Masomo mengi yanayohusiana na nyota pamoja na bahati, hutolewa katika kitabu hiki cha ajabu. Kuna matamshi ya kiarabu katika kitabu hiki yenye nguvu ya kuleta maajabu usiyotarajia, ambayo sitayasema katika makala hii kwa kuwa sifundishi uchawi, nafunua siri zilizofichwa na mabeberu wachache ili waendelee kuitawala dunia hii kiuchumi na kuwa na nguvu ya ushawishi. 4.The Kybalion – Kitabu cha Hermeticism kinachofundisha sheria saba za ulimwengu zinazodaiwa kuwa na nguvu za kimetafizikia, zinazoleta mvuto kwa watu wanaokutazama, ushawishi kwa wanaokusikiliza na Nguvu ya fedha. 5. The Secret (Rhonda Byrne) – Kitabu kinachoelezea sheria ya mvutano (Law of Attraction) na jinsi ya kutumia mawazo kuvutia mafanikio na utajiri. Kitabu hiki ni cha ajabu maana kimejawa na siri zenye uwezo wa Kubadili uchumi wako. 6. Necronomicon – Ingawa ni kitabu cha kubuniwa na H.P. Lovecraft, kimekuwa na hadithi nyingi zinazodai kuwa kina maelezo ya siri za ulimwengu. Usisome kitabu hiki maana kinaweza kuleta shida maishani mwako bila kupata mwongozo kamili. 7.The Voynich Manuscript – Kitabu cha ajabu kilichoandikwa kwa lugha isiyojulikana na hakijafasiriwa hadi sasa. Kimekosa tafsiri yake kutokana na ukweli kuwa kiliandikwa katika lugha ambayo haipo hapa duniani, ama ilikuwapo ila imepotea. Vitabu hivi ndivyo vinavyowafanya watu kuwa na mvuto, na utajiri mkubwa duniani. Kwa kweli huwezi kuwa na mvuto mkubwa ama utajiri mkubwa duniani pasina kusoma vitabu hivi na kufuata kanuni zake, wenda kama utakuwa tajiri kijijini kwenu lakini si duniani. Nikiwa namalizia, kuna Vitabu vyenye nguvu ya kukutajirisha, vyenye nguvu ya kukulaani na hata kukuletea mikosi isiyokoma, ambavyo vimekuwa vikihifadhiwa kwa siri sana, ili kutumiwa na wachache kwa malengo mahususi. Wapo watu kadhaa wanaopinga nguvu ya maandishi katika vitabu wakiidharau na kuyaona maandishi kama herufi za kawaida sana, lakini ukweli ni kuwa kuna nguvu katika vitabu, kuna maajabu katika vitabu na kuna watu waliofunga maisha yao kwa kusoma vifungu fulani kimakosa katika vitabu. Hebu kuwa makini na kila kitabu unachosoma. Hakikisha kwanza kitabu usomacho ni salama, maana kuna vitabu kama vile "Necronomicon, The book of Soyga, The grand Grimoire, n.k" vinavyoweza kukuletea shida na hata mikosi maishani mwako.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·184 Views
  • Read more
    "Simba walitumia kanuni ya 17 (45) kuto kuja uwanjani ila hiyo kanuni ina muongozo wake ambao uliwataka Simba kutoa faarifa ya kutumia uwanja. Kwa kigezo hicho hakukuwa na sababu ya Simba kutoleta timu uwanjani✍️ Leo nimetazama kiwango cha Simba,wachezaji walikuwa sharp,walikuwa na utashi na uwezo wa kufanya mambo yatokee,nahisi wangeweza kushinda hata goli 10. Nyie msimu huu Simba wana timu na sielewi kwanini waliogopa kuleta timu uwanjani siku ya tarehe 8🙌 Sielewi tarehe 8 kwanini hawakuleta timu uwanjani,sielewi,sielewi🖐️" - Hans Rafael, Mchambuzi. FT': Simba SC 6-0 Dodoma Jiji
    0 Comments ·0 Shares ·171 Views
  • Read more
    MAISHA YANAKUWA RAHISI USIPOKERWA NA MAONI YAO ... Tunaishi katika ulimwengu ambamo watu wanahangaikia zaidi jinsi mambo yanavyoonekana badala ya jinsi yalivyo kiukweli. Ulimwengu ambamo mazishi ni makubwa kuliko maisha utayokuwa ukiishi, ambapo ndoa husherehekewa zaidi ya upendo unaopaswa kudumishwa, ambapo uzuri wa nje unaabudiwa huku roho ikipuuzwa. Tunaishi katika kizazi ambacho kinathamini ufungashaji juu ya maudhui, lakini jambo la kusikitisha zaidi ni hili: wengi wamenaswa katika udanganyifu huu, wakijitahidi kila mara kukidhi matarajio ya ulimwengu ambao hautatosheka. Ikiwa unataka kuishi kweli na kupata amani, acha kuwa na wasiwasi juu ya maoni ya watu. Kwa sababu ukweli ni kwamba, hata ufanye nini, mtu atakuwa na la kusema kila wakati. Ukifanikiwa, watasema ulikuwa na bahati. Ukishindwa watasema ulikuwa mjinga. Ukikaa kimya watasema wewe ni dhaifu. Ukiongea watasema unaongea sana. Sasa unaona jinsi inavyochosha kuishi kwa maoni ya watu? Umewahi kuona kuwa mtu akiwa hai hakuna mwenye muda naye ila anapofariki watu hukimbilia kuandaa mazishi ya fujo? Watatumia mamilioni kwenye kasha lakini hawakuweza kumpa chakula alipokuwa na njaa. Wataandika heshima ndefu, lakini hawakuwahi kumwambia "Nakupenda" alipokuwa hai. Kwa nini? Kwa sababu tunaishi katika ulimwengu unaothamini utendakazi kuliko uwepo, mwonekano juu ya uhalisi, na tambiko juu ya ukweli. Hii ndio sababu haupaswi kuishi kwa makofi. Usife ukijidhihirisha kwa watu ambao watalia kwenye mazishi yako lakini haujawahi kukujali maishani. Watu wale wale wanaokusifia leo watakukosoa kesho. Midomo hiyo hiyo inayopiga kelele "Hosana!" baadaye atapiga kelele "Msulubishe!" . Hata Yesu, Mwana wa Mungu, hakuepuka asili ya watu wenye nyuso mbili. Wewe ni nani basi hata ufikirie kuwa utafanya hivyo? Katika jamii yetu ya leo, watu huwekeza zaidi kwenye harusi kuliko kwenye ndoa yenyewe. Wenzi wa ndoa wanaweza kutumia mamilioni ya pesa kwenye arusi ili kuuvutia umati, lakini baada ya miezi michache ndoa hiyo inavunjika. Kwa nini? Kwa sababu tunatanguliza sherehe kuliko msingi. Wengi hawaoi kwa ajili ya mapenzi tena; wanaoa kwa hadhi, kwa kujionyesha, na kwa maoni ya jamii. Lakini harusi nzuri si sawa na ndoa yenye furaha. Sherehe ya kupendeza haihakikishii nyumba yenye amani. Tunaishi katika nyakati ambapo uzuri ni sarafu, ambapo kuonekana kwa nje huamua hali ya kijamii. Lakini ni nini thamani ya uso mzuri na roho tupu? Je, ni thamani gani ya kuvutia kimwili wakati hakuna kina cha tabia? Katika ulimwengu wetu wa leo, watu hutumia pesa nyingi kutazama sura lakini wanasahau kulisha roho zao. Wanaongeza miili yao lakini wanapuuza tabia zao. Wanachuja picha zao lakini wanaacha mioyo yao bila kuchujwa. Usidanganywe. Uzuri hupotea, lakini tabia inabaki. Sura inaweza kuvutia watu kwako, lakini maadili yako pekee ndiyo yatawahifadhi. Watu wanaweza kustaajabia uso wako, lakini ni kina cha nafsi yako ambacho hakika kitaathiri maisha. Kwa hiyo, wekeza kwenye kile kinachodumu. Kuza akili yako. Imarisha imani yako. Jenga uadilifu wako. Acha kufukuza uthibitisho kutoka kwa watu ambao wenyewe wamevunjika na kuchanganyikiwa. Hukuumbwa ili ufanane na matarajio ya wanadamu; uliumbwa ili kutimiza kusudi la kimungu. Mikopo; @Fr. Albert Nwosu'
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·212 Views
  • Read more
    "Msimu uliyopita Zamalek aligomea mechi dhidi ya Al Ahly, Mamlaka za soka nchini Misri zikampa ushindi Al Ahly wa mabao mawili na alama zake tatu kisha wakailima Zamalek alama tatu na timu ikashuka mpaka nafasi ya 12 kama sikosei, Bodi na Chama wala hakikuwaza mara mbili, ni kesi kubwa sana kwenye dunia ya soka kukacha mechi. Jana, Al Ahly nae kaleta mbwembwe zile zile za masuala ya Kanuni akagomea mchezo, akasahau kanuni ya kutokea Uwanjani na kucheza mechi ndio kanuni yenye maana zaidi kwenye soka, amejikuta anapoteza alama tatu na mabao matatu kwa Zamalek, Kanuni hii inaweza kusema hivi ila Kanuni nyingine ikawa na maelezo mengine. Nikukumbushe tu Al Ahly aliyeadhibiwa ndio Klabu Tajiri zaidi Afrika, Klabu yenye Mashabiki na Wanachama wengi zaidi Afrika, ndio Klabu ya pili kwa Mataji mengi duniani baada ya Real Madrid, ila huko Misri watu hawatazami makunyanzi, ukileta maksudi, Bodi na Chama cha soka zinakufanyia bahati mbaya, Ahly inatajwa pia ina nguvu kubwa sana CAF, sio ya kufikirika ama nadharia ndio uhalisia ila wamepita nayo mapema tu. Nawakumbusha tena Watu wangu HAKI huenda na WAJIBU, mfano Tanzania kwa mujibu wa Katiba kuandamana ni haki yako ila unapaswa kutoa taarifa kwa Polisi masaa 72 kabla, umeelewa hapo? Ni haki yako ila huja na Wajibu, Kanuni ili ikulinde hakikisha umetekeleza Wajibu, biashara za Mamlaka za soka duniani ni mpira, kutocheza mpira ni kuzitusi, hazikuachi salama. Ni haki yako kuja kufanya mazoezi uwanja wa mechi siku moja kabla ila ni Wajibu wako kunijulisha kuwa nakuja, ili nikuandalie mazingira, huenda narekebisha mfumo wa Umeme? Huenda hali ya usalama sio shwari, huenda nimepulizia dawa za dudu zinaweka kukuathiri, yaani ni HAKI yako ila una WAJIBU wako huu ni mfano tu. Mnasemaje Watu wangu wa nchini Yemen haya hayawahusu sana, huko kwenu Kivyenu vyenu Wayemen😀" - Farhan JR, Mchambuzi.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·237 Views
  • Read more
    Unakuja wakati katika maisha wakati kila kitu kinaonekana kuwa kibaya na kisicho na tumaini. Familia yako haikuamini tena. Marafiki zako wanakutazama kwa huruma. Wengine hata hucheka nyuma yako. Wanasema hutafanikiwa kamwe. Na ndani kabisa, umeanza kuwaamini kwa sababu, umejitahidi, umefanya kazi kwa bidii, na umefanya kila kitu unachoweza, lakini hakuna kinachoonekana kubadilika. Unawatazama wengine wakifanikiwa huku wewe ukiwa umekwama katika sehemu moja. Inahisi kama maisha yamekusahau. Usiku, wakati hakuna mtu anayekutazama, unalia. Unalia kwa sababu unahisi umepotea. Unalia kwa sababu unahisi kushindwa. Unalia kwa sababu umechoka, umechoka kujaribu, umechoka kutumaini, umechoka kusubiri upenyo ambao hauji. Nisikilize. USIKATE TAMAA. Shikilia kwa muda mrefu kidogo. Hata kama barabara ni ngumu, endelea kutembea, endelea kupigana na endelea kujiamini, hata kama hakuna mtu anayekuamini. Siku moja, utaangalia nyuma na kutambua kwamba kila kitu ulichopitia kilikuwa muhimu ili kukufikisha pale ulipokusudiwa kuwa. Na siku hiyo hao hao waliokutilia shaka ndio watakupigia makofi. Kwa hiyo usikate tamaa. Hadithi yako bado haijaisha. WAKATI WAKO UTAKUJA! Credit: Quadic Bangura
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·183 Views
  • Read more
    "Mimi sio Mcameroon mimi ni mfaransa, wakati naanza kucheza mpira, wakati nikiwa bado sijulikani Baba yangu aliwasiliana na Fecafoot(shirikisho la mpira la Cameroon) ili wanipe nafasi ya kucheza timu ya taifa ya Cameroon, lakini waliomba kiasi kikubwa sana cha fedha kwetu ndo mimi nipate nafasi ya kucheza" "Baba yangu alichukizwa na huo mtazamo wao akaamua kwenda kuomba Ufaransa, Ufaransa walinipa nafasi ili niionyeshe dunia ni kipi nilichonacho, leo hii nimekua mchezaji ghali duniani ndipo Cameroon wananiita na kunisifia kwa uraia usio wakwangu, mimi ni mfaransa na nitabaki kuwa Mfaransa" - Kilyan Mbappé, Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Real Madrid.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·248 Views
  • Read more
    Kwa mwanamke ambaye anatamani mtoto, anayetazama wengine wakisherehekea watoto zao huku yeye akifuta machozi kimya kimya, wakati wako utafika. Siku moja, utamshika mtoto wako mikononi mwako, na miaka ya kusubiri haitakuwa na maana tena. Kwa mwanamke ambaye ameumizwa katika mapenzi, ambaye ameutoa moyo wake tu kuvunjika, sio kosa lako. Wewe sio kwamba hufai. Mtu sahihi, ambaye atakupenda na kukuthamini, atakupata. Kwa mwanamke anayejitahidi kifedha, ambaye anaamka kila siku anashangaa jinsi ya kulipa bili, jinsi ya kulisha watoto wake, jinsi ya kuishi, hii sio mwisho. Milango ambayo imefungwa usoni mwako itafunguliwa siku moja. Endelea kusukuma. Endelea kuamini. Hadithi yako itabadilika. Kwa mwanamke anayepambana na ugonjwa, ambaye mwili wake unahisi kama gereza la maumivu na uchovu, shikilia. Una nguvu kuliko unavyofikiria. Hata katika wakati wako dhaifu, bado wewe ni mpiganaji. Uponyaji utakuja. Kwa mwanamke ambaye amedhihakiwa, kuchekwa, na kudhalilishwa, tembea na kichwa chako juu. Wanaocheka leo siku moja watakaa kimya wakikutazama ukiinuka. Mungu hawasahau waliovunjika. Kwa mwanamke ambaye amehukumiwa na jamii, yule wanayemdharau; wanasema unaruka kutoka kwa mwanaume mmoja kwenda kwa mwingine, hawajui hadithi yako. Hawajui huzuni ya moyo, upweke, tamaa ambazo umekabiliana nazo. Wewe sio kile wanachokuita. Wewe sio makosa yako. Wewe ni zaidi ya wanachokiona. Kwa mwanamke aliyejipoteza, ambaye hajui tena yeye ni nani, jipate tena. Bado unastahili. Bado wewe ni mrembo. Bado unapendwa. Maisha yamejaribu kukuvunja, lakini bado uko hapa. Na hiyo inamaanisha kuwa hadithi yako bado haijaisha. Siku moja, maumivu yatakuwa na maana. Siku moja, machozi yatageuka kuwa kicheko. Siku moja, maombi yatajibiwa. Siku moja, utaangalia nyuma na kutambua msimu huu wa maisha yako ulikuwa unakutayarisha kwa jambo kubwa zaidi. Lakini hadi wakati huo, endelea kushikilia. Endelea kupigana. Endelea kuamini. Wakati wako utafika. Anza safari yako ya ukuaji. credit: Quadic Bangura HERI YA SIKU YA WANAWAKE KIMATAIFA!
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·264 Views
  • Read more
    Maisha yatakujaribu. Yatakusukuma hadi ukingoni. Yatakufanya uhoji kila kitu: thamani yako, kusudi lako, nguvu zako. Utalia. Utaanguka. Utajisikia kukata tamaa. Lakini nisikilize: usikate tamaa. Usiruhusu mapambano ya leo yakushawishi kuwa kesho haitakuwa bora. Usiruhusu maumivu yako yanyamazishe ndoto zako. Una nguvu kuliko unavyofikiria. Una nguvu zaidi kuliko mapambano yako. Umeokoka kila siku mbaya uliyodhani itakuangamiza. Na utaokoka hii pia. Futa machozi yako, nyoosha mgongo wako, na tembea mbele kwa ujasiri. Maumivu yako si jela yako; ni mafuta yako. Hukuumbwa kuvunjika. Uliumbwa kushinda. Simama kwa urefu. Endelea kusonga mbele. Waache wakutie shaka. Waache wazungumze juu yako. Lakini kamwe, kamwe waache wakuzuie. Siku bora zinakuja, endelea kuwa na nguvu na ENDELEA KUPIGANA. Vikwazo vyako si mwisho wako; wao ni vijiwe vya kukanyaga kwenye kitu kikubwa zaidi. Kila dhoruba unayovumilia inakutengeneza, hukusafisha na kukutayarisha kwa ushindi ulio mbele yako. Maumivu unayoyasikia leo ni kujenga nguvu utakazohitaji kesho. Amini mchakato, jiamini, na amini kuwa kila pambano linakufanya ushindwe kuzuilika. Hukuwekwa katika dunia hii kuishi kwa hofu au kusitasita katika uso wa dhiki. Ulikusudiwa kuinuka, kuangaza, kuhamasisha. Moto ulio ndani yako ni mkubwa kuliko vikwazo vilivyo mbele yako. Kwa hivyo pumua kwa kina, nyamazisha mashaka yako, na ujikumbushe wewe ni nani: shujaa, mwokoaji, mpiganaji. Na wapiganaji hawaachi. Ulimwengu unaweza usione thamani yako kila wakati, lakini hiyo haimaanishi kuwa wewe sio wa thamani. Ndoto zako ni muhimu. Sauti yako ni muhimu. Wewe ni muhimu. Kwa hivyo simama, jitokeze, na ujithibitishie kuwa hakuna changamoto kubwa kuliko roho yako. Endelea kuamini, endelea kusukuma, na tazama jinsi maisha yanavyokuegemeza. Anza safari yako ya ukuaji.
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·234 Views
  • Read more
    *🔥 NAFASI YA AJABU!* *TubePesa* - Jukwaa jipya kwa *YouTube* 🎯 *Pata Pesa kwa Kutazama Video!* 🎥 • Pata TSh20,625 bonasi ya kukaribishwa • Tazama video kila siku = Pata pesa kila siku 💰 • Malipo ya papo hapo ⚡ *Jiunge SASA!* ⬇️ https://mpesawatch.site/ref/yaredsimonkayir?s=wa&ch=undefined ✅ Jukwaa rasmi la Youtube 🔒 Salama & Inayoaminika
    Love
    1
    · 1 Comments ·0 Shares ·184 Views
  • Read more
    *🔥 NAFASI YA AJABU!* *TubePesa* - Jukwaa jipya kwa *YouTube* 🎯 *Pata Pesa kwa Kutazama Video!* 🎥 • Pata TSh20,625 bonasi ya kukaribishwa • Tazama video kila siku = Pata pesa kila siku 💰 • Malipo ya papo hapo ⚡ *Jiunge SASA!* ⬇️ https://mpesawatch.site/ref/yaredsimonkayir?s=wa&ch=undefined ✅ Jukwaa rasmi la Youtube 🔒 Salama & Inayoaminika
    PayTube - Earn Money Online
    mpesawatch.site
    Join PayTube and start earning money today! Sign up now to access our market research network and earn up to $20 per day. Get a $8 sign-up bonus!
    0 Comments ·0 Shares ·183 Views
  • Read more
    "Siamini na sitakaa niamini kama TFF kupitia kamati yake inakwenda kumfungia Ali Kamwe kama tetesi zinavyosema, nataka kuamini huenda wanaanzisha jambo kuangalia mapokeo ya watu” “Maoni yangu kama kuna jambo ambalo TFF linapaswa kulitazama ni hili la kuanza kuwaandama wasemaji wa vilabu haswa klabu ya Yanga, kwa taarifa niliyonayo na ninayoifahamu alifungiwa Hassan Bumbuli, Antonio Nugaz, nimefungiwa mimi (Jerry Muro),amefunguwa Haji Manara na sasa wanataka kumfungia Ali Kamwe watu watano katika kipindi cha miaka mitano sitaki kusema kama hawa waliofungiwa wamefanya makosa kuliko wengine” “Wasemaji ni sehemu ya familia ya mpira japo sio main actors kwenye mpira sio wachezaji,sio benchi la ufundi, sio mwenyekiti wala makatibu hawa ni familia ya mpira,nachotaka kuwashauri kabla ya kuwafungia wasemaji sasa ni wakati wa TFF kutengeneza kanuni na miongozo na taratibu zinazosimamia eneo la usemaji kama zinavyotengenezwa kanuni za chama cha marefa au soka la wanawake” - Jerry Muro.
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·336 Views
  • Read more
    BOT INAYO DOWNLOAD NYIMBO haraka na kwa mbs kidogo Hii ni bot ya telegram ambayo unaipatia maneno kidogo ya muziki unayukumbka inakuletea ngoma nzima pia unaweza kuipa hata sauti ikakuletea wimbo wako, hii inatumika Kudowload nyimbo ni kama shaazam Link yake hii hapa https://t.me/Waduduu_musicBot Au ingia telegram search Wadudu_musicBot
    0 Comments ·0 Shares ·319 Views
  • Read more
    Ijumaa, tarehe 28 Februari, haikuwa siku rahisi kwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alipofanya ziara katika Ikulu ya White House, Marekani. Kabla hata ya mzozo wa maneno kati yake na mwenyeji wake, Rais Donald Trump, pamoja na Makamu wa Rais JD Vance, tayari kulikuwa na ishara za mivutano. Trump alimkaribisha Zelensky mlangoni na kusema kwa utani: “Leo amevalia kweli kweli,” kauli ambayo iliwafanya baadhi ya waandishi wa habari kuiona kama kejeli badala ya pongezi. Wakati huo, Zelensky alikuwa amevalia fulana nyeusi ya mikono mirefu, vazi ambalo amekuwa akilivaa mara kwa mara tangu Ukraine ivamiwe na Urusi mwaka 2022. Baadaye, Trump alipompokea Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, alionekana kutazama mavazi yake kwa makini kutoka juu hadi chini, kisha kunong’ona maneno yanayoweza kutafsiriwa kama pongezi kwa suti rasmi aliyovaa Starmer. Mjadala kuhusu mavazi ya Zelensky ulizidi kupamba moto wakati wa mkutano wa waandishi wa habari. Brian Glenn, mwandishi kutoka Real America’s Voice—chombo cha habari kinachopendelea mrengo wa kulia—alimtupia swali la moja kwa moja: “Kwa nini hauvai suti? Upo katika ofisi ya juu kabisa katika nchi hii, na umegoma kuvaa suti – je, unamiliki hata suti?” Kwa utulivu, Zelensky alijibu kwa mshangao mdogo: “Nitavaa suti vita hivi vitakapomalizika. Labda suti kama yako, labda bora zaidi, au pengine ya bei nafuu kuliko yako,” alisema kwa utani huku akionyesha msimamo wake wa kuendelea kuvaa mavazi ya kijeshi. Swali hilo la Glenn liliibua mjadala mkali mitandaoni. Wengine walimuunga mkono, wakisema kwamba kiongozi wa taifa anapaswa kuvaa mavazi rasmi anapokutana na viongozi wengine, ilhali wengine waliona swali hilo kuwa la dhihaka na lisilo na umuhimu. Miongoni mwa waliomkosoa Glenn ni mwandishi maarufu wa Uingereza, Piers Morgan, ambaye pia ni rafiki wa karibu wa Trump. Morgan aliandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter): “Swali la kipuuzi. Elon Musk havai suti anapoingia Ikulu.” Historia pia inaonyesha kuwa si Zelensky pekee aliyeingia Ikulu ya Marekani bila suti. Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Winston Churchill, alifanya hivyo katika moja ya ziara zake rasmi.
    Like
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·512 Views
  • Read more
    "Nimetazama Interview ya Rais wa Marekani na Rais wa Ukraine pale Oval Office ndani ya Ikulu ya Marekani, nimekuja kugundua Rais wa Ukraine anahisi anajadiliana na Mwanasiasa mwenzake ila anachosahau Trump ni Mfanyabiashara na hawezi kufanya kitu cha bure ambacho Taifa lake Marekani halinufaiki na chochote, ndio maan anamsukumia sana kuwa amalizane na Urusi wasaini mkataba wa amani. Pale Ukraine kuna madini adimu sana duniani, Mrusi hapigani Kichwa kichwa ndio maana maeneo ya Donbass na Zaporizhia yanabaki kuwa maeneo ya Kimkakati sana kwa Mrusi, hata Marekani hawapo kichwa kichwa maana Secretary Rubio wa Marekani alimwambia Rais wa Ukraine akubali kusaini mkataba wa madini ili wao waendelee kumlinda, Mrusi na Mmarekani wapo rada sana eneo lile na kila mmoja yupo Kitalaam. Kwa akili ya kawaida Marekani hataki kuendelea kugharamikia vita hivyo bila faida. Juzi kuna website nilisoma ya taarifa za Kiuchunguzi ni kuwa Marekani, China na Urusi kwasasa wapo meza moja na wazo lao kubwa wamekubaliana juu ya MULTIPOLAR WORLD ORDER ambapo Mataifa zaidi ya mawili yanakuwa na nguvu sawa ama yanakaribiana, kwa ufupi sana mataifa haya matatu yanataka kuitawala dunia bila kugusana. Ndio maana Trump alivyoingia madarakani akapush agenda chap ya BRICS kuachana na wazo lao la kuibadili dola ya Marekani kuwa sio sarafu rasmi kwenye umoja wao, ndio maana alipoingia wamerudi mezani kwa mengi ikiwemo Trump na Putin wote kukiri kuwa watashirikiana na Trump atasafiri kuelekea Urusi kwenye sherehe za Mei 9, ambapo watakutana Marais wote watatu yani Putin, Xi Jinping na Trump. Kifupi sana Marekani ya Donald Trump ina Approach tofauti sana, ndio maana hata Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Stearmer alipofika White House kukutana na Trump kwenye mazungumzo yao akalisifia sana Jeshi la Uingereza ila kuna sehemu akampiga kwa kumwambia huwezi kuichukua Urusi peke yako, hata leo amesisitiza Ukraine wakubali amani nje na hapo bila msaada wake hawamuwezi Mrusi, huyo ndio Donald Trump" - Farhan JR, Mchambuzi.
    0 Comments ·0 Shares ·456 Views
  • Read more
    Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA), leo hii litakutana kuchakata kanuni mpya nne (4) ambazo zinaweza kuanza kutumika Julai 1, 2025 endepo zitapitishwa. 1. Kanuni ya Arsene Wenger: Mchezaji atahesabiwa kuwa yuko "offside" ikiwa mwili wake mzima utapita Mchezaji wa mwisho. Ikumbukwe kwamba "offside" ya sasa ni kuwa Mchezaji anahesabiwa kuwa yupo "offside" endapo sehemu yake ndogo ya mwili au mwili mzima itampita Mchezaji wa mwisho. 2. Waamuzi (Refarii) kutoa ufafanuzi wa maamuzi yao kwa Watazamaji Uwanjani kwa kutumia kipaza sauti (Microphone): Baada ya kushirikiana na VAR, Waamuzi wataelezea maamuzi yao kwa kutumia kipaza sauti kwa Watazamaji wote waliopo Uwanjani. 3. Challenge System: Kila Kocha Mkuu wa Timu ataruhusiwa kuomba kutumia VAR wakati wa mchezo ili kupitia tukio wanaloona kuwa lina utata. NB : Wataweka idadi maalumu ya kuomba kutumia VAR na sio muda wote. 4. Waamuzi kusimamisha muda: Waamuzi wataweza kusimamisha saa ili kuchunguza tukio lenye utata au wakati wa majeraha makubwa. Lengo: kuepuka kupoteza muda mwingi katika mpira wa miguu na kuhakikisha muda halisi wa kucheza unatumika. NB : Hii itamika pia kwa wale Wachezaji ambao hupenda kupoteza muda kipindi anatolewa Uwanjani ili Mchezaji mwingine aingie.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·376 Views
  • Read more
    "Naona Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amefunga safari hadi Congo kumuona Rais Tshisekedi, sijui ni kipi hasa kinaendelea katika jumuiya ya Afrika mashariki lakini ni kama kuna muungano ndani ya muungano, eeeh kuna muungano kati ya Congo na Burundi ambao unalenga kupambana dhidi ya Rwanda Yaani ukiwatazama Congo na Burundi ni kama wameungana kupambana na Rwanda na M23 eeeh ipo wazi na tayari mapigano kati ya majeshi ya Congo Burundi dhidi ya Rwanda na M23 yameshuhudiwa, EAC wasipodhibiti hali ya Congo mzozo huu utaenda kutanuka na kuwa wa kikanda 😭 Ngoja tuone ila yajayo sio mazuri kwa diplomasia ya EAC , kiufupi ziara ya Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, nchini Congo inalenga kuonana na mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Felix Tshisekedi, huku lengo kuu ikiwa na mazungumzo kuhusu mzozo unaolikumba eneo la mashariki mwa Kongo" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa Siasa.
    0 Comments ·0 Shares ·397 Views
More Results