• OPERATION ENTEBBE -2

    Tayari zilikuwa zimepita siku tatu tangu ndege ya Air France Flight 139 kuondoka Tel Aviv na hatimaye kutekwa baada ya kuruka jijini Athens iliposimama kuchukua abiria. Lakini pia zilikuwa zimepita siku mbili tangu ndege hii kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda. Katika siku zote mbili hizi tangu ndege hii itue uwanjani hapa, rais wa Uganda Idd Amin Nduli Dadaa alikuwa anafika uwanjani hapo kila siku “kuwajulia hali” mateka hao.
    Kwa muda wa siku hizi zote mbili tangu ndege itue uwanjani hapo, magaidi hawa walioiteka ndege kwa kushirikiana na jeshi la Uganda kuchunguza majina ya kila abiria kama ambavyo yalikuwa yameandikwa kwenye pasport. Lengo lao la kufanya hivi ilikuwa ni kujaribu kufahamu uraia wa kila mateka waliye naye. Baada ya kufanya uchambuzi huu wa passport zote, hatimaye siku hii ya tatu, yaani tarehe 29 June 1976 kiongozi wa magaidi hawa Wilfred Bose akiwa na karatasi mkononi aliingi ndani ya terminal ambayo walikuwa wanaitumia kuwahifadhi mateka na kisha akaanza kusoma majina ya kila abiria. Alichokuwa anakifanya ni kusoma majina ya mateka ambao passport zao zilionyesha walikuwa ni raia wa Israel. Lakini pia alisoma majina ya mateka wengine ambao licha ya passport zao kuonyesha kuwa hawakuwa raia wa Israel lakini walikuwa na majina ya kiyahudi. Pamoja na hao pia mateka wote ambao walikuwa na uraia pacha na uraia huo mmojawapo ukiwa ni Israel basi nao waliunganishwa kwenye list hii.
    Baada ya kuwatenganisha raia wote wa Israel na kuwaweka kwenye chumba kingine peke yao hapo hapo kwenye terminal, kuna mwanadada raia wa Ufaransa aliyeitwa Jocelyne Monier yeye jina lake halikuitwa kwenye ile list ya wanaotakiwa kutengwa kwenye chumba kingine (Waisrael na Wayahudi). Lakini ‘boyfriend’ wake alikuwa ni Muisrael na aliitwa jina na kutengwa na wengine katika kile chumba kingine. Mwanadada huyu ili kuonyesha kumtia moyo mpenzi wake na kupinga huu ubaguzi uliokuwa unafanywa na hawa magaidi, kwa hiari yake alijipeleka kwenye chumba cha mateka wa Kiisrael. Si mwanadada huyu pekee ambaye alifanya kitendo hiki cha ushujaa, lakini pia kulikuwa na mwanamama mwingine aliitwa Janet Almog (rai wa Marekani) na mateka mwingine aliyeitwa Jean-Jacques Mimouni (raia wa Ufaransa) nao kwenye kuonyesha hali ya kuwaunga mkono wenzao waliotengwa kwenye chumba kingine na kupinga ubaguzi uliokuwa unafanywa na maharamia hawa, nao walijipeleka kwa hiari yao kwenye chumba ambacho mateka hao walikibatiza jina “Chumba cha Waisrael”, ambacho mateka wote walijua fika kwamba kuna jambo baya maharamia hao walikuwa wamepanga kulifanya.

    Licha ya maharamia kwa kushirikiana na jeshi la Uganda kufanya uchambuzi huu wa kina kuhusu uraia wa kila mateka waliye naye, lakini walifanya kosa kubwa sana ambalo lilkuja kuwagharimu sana hapo baadae. Kwenye uchambuzi wao wote huu walioufanya walishindwa kumng’amua mateka mmoja mwanajeshi wa Israel ambaye alikuwa ana uraia pacha na siku hiyo alikuwa anatumia passport ambayo sio ya Israel. Mateka huyu alikuja kuwa muhimu sana huko mbeleni kuwapatia Mossad Intelijensia mujarabu kabisa kuhusu watekaji, jengo wanaloshikilia mateka, na namana wanavyoshirikiana na jeshi la Uganda.
    Siku iliyofuata yaani June 30, maharamia haya wakawaachia mkupuo wa kwanza wa mateka wasio raia wa Israel au wayahudi. Katika mkupuo huu wa kwanza waliachia mateka 48 ambao walikuwa ni wazee, watoto na akina mama wenye watoto wadogo.
    Baada ya mkupuo huu wa kwanza wa kuwaachia mateka hawa wachache, maharamia wakaweka wazi matakwa yao ili waweze kuachia mateka wengine. Kwanza kabisa walitaka walipwe fedha kiasi cha dola za Kimarekani milioni 5. Na pili walitakakuachiwa kwa wafungwa 53 wenye asili ya kipalestina wanaotuhumiwa kwa ugaidi, ambao kati yao 40 walikuwa kwenye jela za Israel na 13 katika nchi nyingine za Ulaya. Watekaji hawa wakatoa ‘ultimutum’ kwamba kama matakwa yao hayatatekelezwa ndani ya masaa ishirini na nne yajayo (mpaka tarehe 1 July saa 8 mchana) basi wataanza kuua raia wa Israel mmoja baada ya mwingine.
    Dunia nzima ni kama ilisimama kwa masaa kadhaa kutokana na sintofahamu iliyogubika kila mahali. Sintofahamu hii ililetwa na ukweli kwamba, ilikuwa inajulikana wazi kwa miaka yote kwamba Israel wana sera ya kutofanya mazungumzo au makubaliano na Magaidi. Kwahiyo kila mtu alikuwa nafahamu kuwa kuna uwezekano mkubwa ndani ya masaa 24 yajayo ulimwengu ukashuhidia watu zaidi ya 200 wakichinjwa kama kuku.

    NCHINI ISRAEL: KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI
    Nchini Israel kikao cha dharura cha baraza la mawaziri kilikuwa kimeitishwa na waziri Mkuu Yitzhak Rabin kujadili kuhusu hatua za kuchukua kuokoa raia wake ambao wameshikiliwa mateka huko uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda.
    Hali ya kikao ilikuwa tete sana kutokana na kila dakika waliyokuwa wanaitumia kujadili ndivyo ambavyo walikuwa wanaikaribia saa 8 mchana ya tarehe 1 July. Walipowasilana na Ujerumani na Ufaransa ambao nao walikuwa na baadhi ya wafungwa wa Kipalestina ambao watekaji walitaka waachiwe… walipowaomba ushirikiano wao kuhusu kukabali kuachia hao wafungwa, Ujerumani na Ufaransa walikataa katakata kuachia hata mfungwa mmoja wa Kipalestina ambaye alikuwa kwenye magereza zao.
    Sintofahamu ilizidi kuongezeka. Masaa yalizidi kuyoyoma. Saa 8 mchana ya tarehe 1 July ilizidi kukaribia. Harufu ya damu ilikuwa inabisha hodi mlangoni kwao. Licha ya weledi wao wote walionao lakini mbele yao waliona giza.
    Inapaswa kukumbukwa kwamba Idd Amin aliwahi kupatiwa mafunzo ya weledi wa kijeshi nchini Isarel (Special Force Training). Kwa hiyo baraza la mawaziri likamuagiza Baruch Bar-Lev, kamanda mstaafu wa IDF ambaye alihusika kumpatia mafunzo ya kijeshi Amin kipindi yuko Israel na kufanikiwa kujenga naye ukaribu. Baraza la Mawaziri likamuagiza Baruck (marafiki zake humuita “Burka”) kufanya mawasiliano na Rais huyo wa Uganda ili kujaribu kumuomba awashawishi magaidi wanaoshikilia mateka kwenye uwanja wake wa ndege wa Entebbe wawaachie mateka hao bila masharti magumu.
    Kupitia kwa Burka, Israel ilifikia mpaka hatua ya kumuahidi Idd Amin kuwa kama atafanikisha kuachiwa kwa mateka hao basi watatumia ushawishi walionao kuhakikisha kuwa Amin anatunukiwa tuzo ya amani ya Nobel.
    Lakini Amin hakulegeza msimamo, akaendelea kuwasisitiza kuwa hakuna namna nyingine yeyote ambayo mateka hao wataachiwa bila masharti yaliyotolewa na watekaji kutimizwa.
    Baada ya juhudi hii ya kumuhonga ‘tuzo’ kugonga mwamba, Waziri Mkuu wa Israel akawasiliana na serikali ya Marekani na kuwaomba wamshawishi Rais wa Misri Anwar Sadat ambaye alikuwa anaheshimiana sana na Amin ili amshawishi kuwaamuru magaidi yaliyoko uwanjani kwake Entebbe waachiemateka bila masharti magumu.
    Amin bado akashikilia msimamo kwamba hakuna mateka atakayeachiwa pasipo masharti yaliyotolewa kutimizwa.
    Juhudi hizi za kumshawishi Amin zilikula muda mwingi sana na hatimaye wakajikuta tayari kulikuwa kumekucha asubuhi. Mbele yao kulikuwa kumebakia masaa chini ya manane kabla ya damu ya zaidi ya watu 200 kumwagika.
    Baraza la mawaziri la Israel likamuomba Amin aongee na watekaji wakubali kusogeza siku mbele ili kuipa serikali ya Israel muda wakutosha kushughulikia lojistiki na kushawishi Ujerumani na Ufaransa ili waweze kutimiza sharti la kuachiwa kwa wafungwa wa kipalestina 53 wanaotuhumiwa kwa ugaidi.
    Rais Idd Amin baada ya kushawishiwa sana akakubali ombi hili na akaieleza serikali ya Israel kwamba ni siku tatu tu pekee zinaongezwa, yaani ikimaanisha kwamba siku zitaongezwa mpaka tarehe 4 July, saa 8 mchana. Serikali ya Israel ikakubliana na hili.
    Mchana wa siku hiyo, serikali ilitoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari wakilaani vitendo vya kigaidi na hususani matukio ya utekeji wa raia wasio na hatia, na pia ikaendelea kusisitiza kuhusu sera yake ya kutojadili na magaidi. Lakini taarifa hii ikamalizia kwa kueleza kuwa kwa kujali zaidi uhai wa zaidi ya raia 200 ambao bado wanashikiliwa na magaidi hayo, na kujali maumivu ambayo familia zao na taifa zima linapitia, wamekubali kutimiza sharti la magaidi hao la kuwalipa fedha za kimarekani dola milioni tano pamoja na kuachiwa kwa wafungwa wa kipalestina 53 wenye tuhuma za ugaidi.
    Ilikuwa ni moja ya matukio machache ambayo yaliishangaza dunia kwa Israel kukubali kushindwa hadharani. Kwa upande wa maadui wa Israel hii ilikuwa ni sherehe kubwa kwao. Na kwa upande wa Isarel na maswahiba zake hii iikuwa ni maombolezo makubwa.
    Amin na wenzake kule Uganda walikuwa wanasherehekea baada ya taarifa hii kutolewa kwa vyombo vya habari. Walihsi kabisa harufu ya ushindi inanukia kwenye pua zao.
    Kitu ambacho walikuwa hawafahamu ilikuwa ni kwamba, Israel walikuwa wanawafanyia ‘mchezo’ wa kisaikolojia ili Amin, jeshi lake na watekaji wajiamini kwa kuona kuwa ushindi umeegemea upande wao na hatimaye wajisahau kutokana na kujiamini huku.

    NYUMA YA PAZIA
    Huko Tel aviv, makamanda wa IDF na maafisa wa Mossad walikuwa wamekusanyika katika conference room ya mako makuu ya wizara ya ulinzi kuweka mkakati wa oparesheni ya uokozi (rescue mission) wa mateka wanaoshikiliwa katika uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda.
    Kati ya watu muhimu ambao walikuwepo kwenye kikao hiki alikuwa ni Waziri Mkuu Rabin na Ehud Barak ambaye kipindi hicho alikuwa kamanda wa ngazi za juu kwenye jeshi anayeongoza kitengo cha Intelijensia ya jeshi (Military Intelligence).
    Moja kati ya vitu muhimu ambavyo viliwasaidia ilikuwa ni taarifa ya intelijensia iliyoletwa na Mossad kwamba uwanja wa ndege wa Entebbe ulijengwa na kampuni ya Kiisrael inayoitwa Solel Boneh.
    Kwahiyo muwakilishi kutoka katika kampuni hii ya ujenzi naye akaitwa kikaoni kwa ajili ya kuwasilisha michoro kuhusu jengo lote na uwanja wa ndege wa Entebbe ulivyo.
    Lakini pia wakati huo huo kulikuwa na maafisa wa Mossad ambao walikuwa ufaransa kuwahoji wale mateka ambao walikuwa wameachiwa awali. Mtu muhimu zaidi ambaye alitoa taarifa nzuri kwa Mossad alikuwa ni yule afisa wa jeshi niliyemuelezea awali kwamba alikuwa na uraia wan chi mbili (Israel na Ufaransa) na siku hii alikuwa ametumia passport ya nchi ya ufaransa hivyo watekaji walimuachia pamoja na wenzake wa kundi la kwanza lile la watu 48.
    Bwana huyu alitoa taarifa muhimu zaidi kuhusu kilichokuwa kinaendelea katika uwanja wa ndege wa Entebbe, kwa kuwa yeye tofauti na wenzake kutokana na uzoefu wake wa jeshi alikuwa aliweza kuwaeleza Mossad kuhusu ni salaha za namna gani watekaji walikuwa nazo, kulikuwa na ndege za aina gani za kijeshi pale uwanjani (Idd Amin aliamuru Air Force ya Uganda kulinda uwanja huo masaa 24), pia aliweza kuwaeleza kuhusu ‘rotation’ ya ulinzi ya jeshi la Uganda pamoja na taarifa nyingine muhimu ambazo abiria wengine wasingeweza kuzitilia maanani au kkuzieleza kwa ufasaha.
    Baada ya kupata intelijensia ya kutosha, mkakati wa awali ambao ulipendekezwa na jeshi ulikuwa ni kutumia ndege ya kijeshi na kisha kudondosha makomando kwenye ziwa Viktoria na kutoka hapo watatumia boti za mpira kuvuka mpaka nchi kavu na hatimaye kuelekea uwanja wa ndege ambao haukuwa mbali sana na ziwa Viktoria.
    Mkakati huu ulikuwa ni mzuri lakini ulihairishwa baada ya kupewa taarifa kuwa ziwa Viktoria lilikuwa na mamba wengi na ingeweza kuhatarisha uhai wa hawa makomando kabla hata ya kufika kwenye uwanja wa ndege. Kwahiyo ilikuwa dhahiri kwamba mkakati wowote ambao utawekwa ni lazima uwe wa kuvamia kutokea nchi kavu na ikiwezekana kutoka nchi jirani.
    Changamoto kubwa zaidi ilikuwa ni usafiri. Yaani kwamba oparesheni hii ilikuwa si tu kwamba makomando wanaotumwa kutekeleza wanaenda kupambana na magaidi wanne tu walioteka ndege, bali ilikuwa ni kana kwamba wanaenda kupambana na jeshi zima la Uganda. Kwa hiyo kikosi cha makomando ambacho kitatumwa kwenda huko lazima kiwe na watu wengi wa kutosha na pia lazima wachukue silaha nzito za kutosha. Ili kufaniskisha safari yenye makomando wengi hivi na vifaa vizito ilikuwa ni lazima kutumia ndege kubwa za kijeshi zenye uwezo mkubwa pia na hakukuwa na chaguo zuri zaid ya kutumia ndege za kijeshi za LOCKHEED C-130 HERCULES. Sasa changamoto ilikuwa inakuja kwamba huwezi kurusha dege kubwa kama hii kwenda na kurudi kutoka Israel mpaka Uganda bila kujaza mafuta tena japo mara moja.
    Katika kipindi hiki bado Israel walikuwa hawajawa na uwezo wa kufanya ‘Aerial Refuel’, yaani ndege kujazwa mafuta kwa kutumia ndege nyingine ikiwa angani. Lakini pia ilikuwa ni lazima madege hayo yakikaribia Uganda yaruke chini chini ili kukwepa kudunguliwa na kuikwepa rada ya kijeshi. Kwa hiyo ilikuwa ni lazima kupata nchi ndani ya afrika Mashariki ambao watakubali madege hayo ya kijeshi ya Israel kutua kwenye uwanja wake wa ndege na kujaza mafuta lakini pia kujiandaa na kuanzisha operation kutokea hapo na pia anga lao kutumika kuanzisha shambulizi la kijeshi kuelekea Uganda.
    Sasa japokuwa nchi zote za Afrika Mashariki zilikuwa hazikubaliana na kitendo cha Rais wa Uganda kushirikiana na watekaji, lakini hakukuwa na hata nchi moja ambayo ilikuwa iko tayari kuingia kwenye mzozo na Idd Amin kwa kuruhusu viwanja vya vya ndege kutumika na ndege za jeshi la Israel au wanajeshi kujiandaa kuvamia Entebbe au pia kuruhusu anga lao kutumia na jeshi la Israel.
    Ndipo hapa ambapo kwa haraka sana siku hiyo hiyo Waziri Mkuu Rabin akamtuma Ehud Barak na maafisa wachache wa Mossad kwenda Kenya kushawishi serikali ya Mzee Jomo Kenyatta iruhusu ndege za jeshi la Isarel kutumia kiwanja chao cha ndege. Ehud barak na wenzake hawakwenda tu moja kwa moja kwa Mzee Kenyatta, bali kwanza walienda kwa Waziri wa kilimo wa kipindi hicho Bw. Bruce McKenzie ambaye huyu aliwahi kuwa afisa wa Idara ya ujasusi ya Uingereza, MI6 na pia alikuwa swahiba mkubwa wa Ehud Barak.

    Kwa hiyo Israel ikamtumia Bruce McKenzie kumshawishi Mzee Jomo Kenyatta kuruhusu anga la Kenya na viwanjavya ndege kutumiwa na makomando wa Israel na ndege zao.
    Ehud Barak na maafisa wa Mossad hawakuishia hapa tu, bali pia walifanya vikao vya siri na wafanyabiashara wakubwa nchini Kenya wenye asili ya Israel na wale ambao walikuwa na ‘marafiki’ wa Israel kuwaomba watumie ushawishi wao wa kisiasa na kiuchumi wasaidie kumshawishi Kenyatta kukubali ombi la seriakli ya Israael viwanja vyao kutumika na ndege za kijeshi za Israel na makondo wake.
    Baada ya mashinikizo haya kutoka kila upande, Mzee Kenyatta hakuwa na chaguo linguine zaidi ya kukubali ombi lao.
    Bwana huyu McKenzie pia alikuwa na ndege yakebinafsi, na Ehud Barak akaona fursa. Walitumia ndege hii ya kiraia kuruka mpaka Uganda mijini Entebbe na kukatiza juu ya anga la uwanja wa ndege wa Entebbe na walipokuwa wanapita juu ya anga la uwanja wa ndege, Ehud Barak akatumia fursa hii kupiga picha kila eneo la uwanja. Kwa kuwa hii ilikuwa ni ndege ya kiraia, jeshi la Uganda hawakushughulika nayo.
    Picha hizi zilizopigwa na Ehud Barak zilikuja kuwa na umuhimumkubwa katika maandalizi ya mwisho ya oparesheni ya makomando wa Isarel Kuvamia uwanja huu.
    Mpaka kufikia hapa maandalizi yote muhimu yalikuwa yamekamilika.
    WAKATI HUO HUO
    Upande wa watekaji kule Uganda walikuwa wanasubria mifwedha yao dola milioni 5 za kimarekani.
    Rais Idd Amin naye baada ya kufikia makubaliano na Israel kuwa masharti ya fedha na wafungwa wa kipalestina kuachiwa tarehe 4 July, naye ‘akarelax’ na akaona huo ndio muda wa kutekeleza majukumu Mengine akisubiria tarehe 4 July ifike.
    Katika kipindi hiki Idd amin ndiye alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwa kuzingatia utaratibu wa uenyekiti kuzunguka kwa kila nchi kwa mwaka mmoja mmoja na wiki hii alikuwa anatakiwa kwenye kikao cha Umoja wa Afrika kilichokuwa kinafanyika Mauritius. Kwa hiyo Amin akafunga safari kuelekea Mauritius kwenda kukabidhi kijiti cha Uenyekiti.
    Ehud Barak aliposikia taarifa hii, kwa kutumia akili yake kubwa ya kuzaliwa aliyojaliwa na uzoefu wake wa ujasusi, aliona fursa adhimu kabisa hapa. Akawasiliana na walioko kikaoni huko Tel Aviv na kuwaeleza taarifa ambazo awali wote hawakuielewa.
    Ehud Barak: “Idd Amin akiwa ndani ya Uganda huwa anatumia Mercedes Limousine katika msafara wake”
    Waziri Mkuu Rabin: “Ok! Limefanyaje?’
    Ehud Barak: “Nataka mtafute gari kama hiyo… Mercedes Limousine”
    Waziri Mkuu Rabin: “la kazi gani?”
    Ehud Barak: “siku ambayo kikosi cha makomando wakipanda kwenye ndege kutoka huko Israel kwenda Uganda, gari hilo nataka pia lipakiwe ndani ya ndge!”
    Kwa dakika kadhaa wote ambao walikuwa wanamsikiliza pale kikaoni kupitia simu hakuna ambaye alielewa nini hasa Ehud Barak alikuwa anapendekeza.
    Yalikuwa yamebaki masaa machache tu ambapo, weledi, ushujaa na uzalendo uliotukuka ulikuwa unaedna kudhihirika.

    Itaendelea
    #TheBOLD_JF
    OPERATION ENTEBBE -2 Tayari zilikuwa zimepita siku tatu tangu ndege ya Air France Flight 139 kuondoka Tel Aviv na hatimaye kutekwa baada ya kuruka jijini Athens iliposimama kuchukua abiria. Lakini pia zilikuwa zimepita siku mbili tangu ndege hii kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda. Katika siku zote mbili hizi tangu ndege hii itue uwanjani hapa, rais wa Uganda Idd Amin Nduli Dadaa alikuwa anafika uwanjani hapo kila siku “kuwajulia hali” mateka hao. Kwa muda wa siku hizi zote mbili tangu ndege itue uwanjani hapo, magaidi hawa walioiteka ndege kwa kushirikiana na jeshi la Uganda kuchunguza majina ya kila abiria kama ambavyo yalikuwa yameandikwa kwenye pasport. Lengo lao la kufanya hivi ilikuwa ni kujaribu kufahamu uraia wa kila mateka waliye naye. Baada ya kufanya uchambuzi huu wa passport zote, hatimaye siku hii ya tatu, yaani tarehe 29 June 1976 kiongozi wa magaidi hawa Wilfred Bose akiwa na karatasi mkononi aliingi ndani ya terminal ambayo walikuwa wanaitumia kuwahifadhi mateka na kisha akaanza kusoma majina ya kila abiria. Alichokuwa anakifanya ni kusoma majina ya mateka ambao passport zao zilionyesha walikuwa ni raia wa Israel. Lakini pia alisoma majina ya mateka wengine ambao licha ya passport zao kuonyesha kuwa hawakuwa raia wa Israel lakini walikuwa na majina ya kiyahudi. Pamoja na hao pia mateka wote ambao walikuwa na uraia pacha na uraia huo mmojawapo ukiwa ni Israel basi nao waliunganishwa kwenye list hii. Baada ya kuwatenganisha raia wote wa Israel na kuwaweka kwenye chumba kingine peke yao hapo hapo kwenye terminal, kuna mwanadada raia wa Ufaransa aliyeitwa Jocelyne Monier yeye jina lake halikuitwa kwenye ile list ya wanaotakiwa kutengwa kwenye chumba kingine (Waisrael na Wayahudi). Lakini ‘boyfriend’ wake alikuwa ni Muisrael na aliitwa jina na kutengwa na wengine katika kile chumba kingine. Mwanadada huyu ili kuonyesha kumtia moyo mpenzi wake na kupinga huu ubaguzi uliokuwa unafanywa na hawa magaidi, kwa hiari yake alijipeleka kwenye chumba cha mateka wa Kiisrael. Si mwanadada huyu pekee ambaye alifanya kitendo hiki cha ushujaa, lakini pia kulikuwa na mwanamama mwingine aliitwa Janet Almog (rai wa Marekani) na mateka mwingine aliyeitwa Jean-Jacques Mimouni (raia wa Ufaransa) nao kwenye kuonyesha hali ya kuwaunga mkono wenzao waliotengwa kwenye chumba kingine na kupinga ubaguzi uliokuwa unafanywa na maharamia hawa, nao walijipeleka kwa hiari yao kwenye chumba ambacho mateka hao walikibatiza jina “Chumba cha Waisrael”, ambacho mateka wote walijua fika kwamba kuna jambo baya maharamia hao walikuwa wamepanga kulifanya. Licha ya maharamia kwa kushirikiana na jeshi la Uganda kufanya uchambuzi huu wa kina kuhusu uraia wa kila mateka waliye naye, lakini walifanya kosa kubwa sana ambalo lilkuja kuwagharimu sana hapo baadae. Kwenye uchambuzi wao wote huu walioufanya walishindwa kumng’amua mateka mmoja mwanajeshi wa Israel ambaye alikuwa ana uraia pacha na siku hiyo alikuwa anatumia passport ambayo sio ya Israel. Mateka huyu alikuja kuwa muhimu sana huko mbeleni kuwapatia Mossad Intelijensia mujarabu kabisa kuhusu watekaji, jengo wanaloshikilia mateka, na namana wanavyoshirikiana na jeshi la Uganda. Siku iliyofuata yaani June 30, maharamia haya wakawaachia mkupuo wa kwanza wa mateka wasio raia wa Israel au wayahudi. Katika mkupuo huu wa kwanza waliachia mateka 48 ambao walikuwa ni wazee, watoto na akina mama wenye watoto wadogo. Baada ya mkupuo huu wa kwanza wa kuwaachia mateka hawa wachache, maharamia wakaweka wazi matakwa yao ili waweze kuachia mateka wengine. Kwanza kabisa walitaka walipwe fedha kiasi cha dola za Kimarekani milioni 5. Na pili walitakakuachiwa kwa wafungwa 53 wenye asili ya kipalestina wanaotuhumiwa kwa ugaidi, ambao kati yao 40 walikuwa kwenye jela za Israel na 13 katika nchi nyingine za Ulaya. Watekaji hawa wakatoa ‘ultimutum’ kwamba kama matakwa yao hayatatekelezwa ndani ya masaa ishirini na nne yajayo (mpaka tarehe 1 July saa 8 mchana) basi wataanza kuua raia wa Israel mmoja baada ya mwingine. Dunia nzima ni kama ilisimama kwa masaa kadhaa kutokana na sintofahamu iliyogubika kila mahali. Sintofahamu hii ililetwa na ukweli kwamba, ilikuwa inajulikana wazi kwa miaka yote kwamba Israel wana sera ya kutofanya mazungumzo au makubaliano na Magaidi. Kwahiyo kila mtu alikuwa nafahamu kuwa kuna uwezekano mkubwa ndani ya masaa 24 yajayo ulimwengu ukashuhidia watu zaidi ya 200 wakichinjwa kama kuku. NCHINI ISRAEL: KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI Nchini Israel kikao cha dharura cha baraza la mawaziri kilikuwa kimeitishwa na waziri Mkuu Yitzhak Rabin kujadili kuhusu hatua za kuchukua kuokoa raia wake ambao wameshikiliwa mateka huko uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda. Hali ya kikao ilikuwa tete sana kutokana na kila dakika waliyokuwa wanaitumia kujadili ndivyo ambavyo walikuwa wanaikaribia saa 8 mchana ya tarehe 1 July. Walipowasilana na Ujerumani na Ufaransa ambao nao walikuwa na baadhi ya wafungwa wa Kipalestina ambao watekaji walitaka waachiwe… walipowaomba ushirikiano wao kuhusu kukabali kuachia hao wafungwa, Ujerumani na Ufaransa walikataa katakata kuachia hata mfungwa mmoja wa Kipalestina ambaye alikuwa kwenye magereza zao. Sintofahamu ilizidi kuongezeka. Masaa yalizidi kuyoyoma. Saa 8 mchana ya tarehe 1 July ilizidi kukaribia. Harufu ya damu ilikuwa inabisha hodi mlangoni kwao. Licha ya weledi wao wote walionao lakini mbele yao waliona giza. Inapaswa kukumbukwa kwamba Idd Amin aliwahi kupatiwa mafunzo ya weledi wa kijeshi nchini Isarel (Special Force Training). Kwa hiyo baraza la mawaziri likamuagiza Baruch Bar-Lev, kamanda mstaafu wa IDF ambaye alihusika kumpatia mafunzo ya kijeshi Amin kipindi yuko Israel na kufanikiwa kujenga naye ukaribu. Baraza la Mawaziri likamuagiza Baruck (marafiki zake humuita “Burka”) kufanya mawasiliano na Rais huyo wa Uganda ili kujaribu kumuomba awashawishi magaidi wanaoshikilia mateka kwenye uwanja wake wa ndege wa Entebbe wawaachie mateka hao bila masharti magumu. Kupitia kwa Burka, Israel ilifikia mpaka hatua ya kumuahidi Idd Amin kuwa kama atafanikisha kuachiwa kwa mateka hao basi watatumia ushawishi walionao kuhakikisha kuwa Amin anatunukiwa tuzo ya amani ya Nobel. Lakini Amin hakulegeza msimamo, akaendelea kuwasisitiza kuwa hakuna namna nyingine yeyote ambayo mateka hao wataachiwa bila masharti yaliyotolewa na watekaji kutimizwa. Baada ya juhudi hii ya kumuhonga ‘tuzo’ kugonga mwamba, Waziri Mkuu wa Israel akawasiliana na serikali ya Marekani na kuwaomba wamshawishi Rais wa Misri Anwar Sadat ambaye alikuwa anaheshimiana sana na Amin ili amshawishi kuwaamuru magaidi yaliyoko uwanjani kwake Entebbe waachiemateka bila masharti magumu. Amin bado akashikilia msimamo kwamba hakuna mateka atakayeachiwa pasipo masharti yaliyotolewa kutimizwa. Juhudi hizi za kumshawishi Amin zilikula muda mwingi sana na hatimaye wakajikuta tayari kulikuwa kumekucha asubuhi. Mbele yao kulikuwa kumebakia masaa chini ya manane kabla ya damu ya zaidi ya watu 200 kumwagika. Baraza la mawaziri la Israel likamuomba Amin aongee na watekaji wakubali kusogeza siku mbele ili kuipa serikali ya Israel muda wakutosha kushughulikia lojistiki na kushawishi Ujerumani na Ufaransa ili waweze kutimiza sharti la kuachiwa kwa wafungwa wa kipalestina 53 wanaotuhumiwa kwa ugaidi. Rais Idd Amin baada ya kushawishiwa sana akakubali ombi hili na akaieleza serikali ya Israel kwamba ni siku tatu tu pekee zinaongezwa, yaani ikimaanisha kwamba siku zitaongezwa mpaka tarehe 4 July, saa 8 mchana. Serikali ya Israel ikakubliana na hili. Mchana wa siku hiyo, serikali ilitoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari wakilaani vitendo vya kigaidi na hususani matukio ya utekeji wa raia wasio na hatia, na pia ikaendelea kusisitiza kuhusu sera yake ya kutojadili na magaidi. Lakini taarifa hii ikamalizia kwa kueleza kuwa kwa kujali zaidi uhai wa zaidi ya raia 200 ambao bado wanashikiliwa na magaidi hayo, na kujali maumivu ambayo familia zao na taifa zima linapitia, wamekubali kutimiza sharti la magaidi hao la kuwalipa fedha za kimarekani dola milioni tano pamoja na kuachiwa kwa wafungwa wa kipalestina 53 wenye tuhuma za ugaidi. Ilikuwa ni moja ya matukio machache ambayo yaliishangaza dunia kwa Israel kukubali kushindwa hadharani. Kwa upande wa maadui wa Israel hii ilikuwa ni sherehe kubwa kwao. Na kwa upande wa Isarel na maswahiba zake hii iikuwa ni maombolezo makubwa. Amin na wenzake kule Uganda walikuwa wanasherehekea baada ya taarifa hii kutolewa kwa vyombo vya habari. Walihsi kabisa harufu ya ushindi inanukia kwenye pua zao. Kitu ambacho walikuwa hawafahamu ilikuwa ni kwamba, Israel walikuwa wanawafanyia ‘mchezo’ wa kisaikolojia ili Amin, jeshi lake na watekaji wajiamini kwa kuona kuwa ushindi umeegemea upande wao na hatimaye wajisahau kutokana na kujiamini huku. NYUMA YA PAZIA Huko Tel aviv, makamanda wa IDF na maafisa wa Mossad walikuwa wamekusanyika katika conference room ya mako makuu ya wizara ya ulinzi kuweka mkakati wa oparesheni ya uokozi (rescue mission) wa mateka wanaoshikiliwa katika uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda. Kati ya watu muhimu ambao walikuwepo kwenye kikao hiki alikuwa ni Waziri Mkuu Rabin na Ehud Barak ambaye kipindi hicho alikuwa kamanda wa ngazi za juu kwenye jeshi anayeongoza kitengo cha Intelijensia ya jeshi (Military Intelligence). Moja kati ya vitu muhimu ambavyo viliwasaidia ilikuwa ni taarifa ya intelijensia iliyoletwa na Mossad kwamba uwanja wa ndege wa Entebbe ulijengwa na kampuni ya Kiisrael inayoitwa Solel Boneh. Kwahiyo muwakilishi kutoka katika kampuni hii ya ujenzi naye akaitwa kikaoni kwa ajili ya kuwasilisha michoro kuhusu jengo lote na uwanja wa ndege wa Entebbe ulivyo. Lakini pia wakati huo huo kulikuwa na maafisa wa Mossad ambao walikuwa ufaransa kuwahoji wale mateka ambao walikuwa wameachiwa awali. Mtu muhimu zaidi ambaye alitoa taarifa nzuri kwa Mossad alikuwa ni yule afisa wa jeshi niliyemuelezea awali kwamba alikuwa na uraia wan chi mbili (Israel na Ufaransa) na siku hii alikuwa ametumia passport ya nchi ya ufaransa hivyo watekaji walimuachia pamoja na wenzake wa kundi la kwanza lile la watu 48. Bwana huyu alitoa taarifa muhimu zaidi kuhusu kilichokuwa kinaendelea katika uwanja wa ndege wa Entebbe, kwa kuwa yeye tofauti na wenzake kutokana na uzoefu wake wa jeshi alikuwa aliweza kuwaeleza Mossad kuhusu ni salaha za namna gani watekaji walikuwa nazo, kulikuwa na ndege za aina gani za kijeshi pale uwanjani (Idd Amin aliamuru Air Force ya Uganda kulinda uwanja huo masaa 24), pia aliweza kuwaeleza kuhusu ‘rotation’ ya ulinzi ya jeshi la Uganda pamoja na taarifa nyingine muhimu ambazo abiria wengine wasingeweza kuzitilia maanani au kkuzieleza kwa ufasaha. Baada ya kupata intelijensia ya kutosha, mkakati wa awali ambao ulipendekezwa na jeshi ulikuwa ni kutumia ndege ya kijeshi na kisha kudondosha makomando kwenye ziwa Viktoria na kutoka hapo watatumia boti za mpira kuvuka mpaka nchi kavu na hatimaye kuelekea uwanja wa ndege ambao haukuwa mbali sana na ziwa Viktoria. Mkakati huu ulikuwa ni mzuri lakini ulihairishwa baada ya kupewa taarifa kuwa ziwa Viktoria lilikuwa na mamba wengi na ingeweza kuhatarisha uhai wa hawa makomando kabla hata ya kufika kwenye uwanja wa ndege. Kwahiyo ilikuwa dhahiri kwamba mkakati wowote ambao utawekwa ni lazima uwe wa kuvamia kutokea nchi kavu na ikiwezekana kutoka nchi jirani. Changamoto kubwa zaidi ilikuwa ni usafiri. Yaani kwamba oparesheni hii ilikuwa si tu kwamba makomando wanaotumwa kutekeleza wanaenda kupambana na magaidi wanne tu walioteka ndege, bali ilikuwa ni kana kwamba wanaenda kupambana na jeshi zima la Uganda. Kwa hiyo kikosi cha makomando ambacho kitatumwa kwenda huko lazima kiwe na watu wengi wa kutosha na pia lazima wachukue silaha nzito za kutosha. Ili kufaniskisha safari yenye makomando wengi hivi na vifaa vizito ilikuwa ni lazima kutumia ndege kubwa za kijeshi zenye uwezo mkubwa pia na hakukuwa na chaguo zuri zaid ya kutumia ndege za kijeshi za LOCKHEED C-130 HERCULES. Sasa changamoto ilikuwa inakuja kwamba huwezi kurusha dege kubwa kama hii kwenda na kurudi kutoka Israel mpaka Uganda bila kujaza mafuta tena japo mara moja. Katika kipindi hiki bado Israel walikuwa hawajawa na uwezo wa kufanya ‘Aerial Refuel’, yaani ndege kujazwa mafuta kwa kutumia ndege nyingine ikiwa angani. Lakini pia ilikuwa ni lazima madege hayo yakikaribia Uganda yaruke chini chini ili kukwepa kudunguliwa na kuikwepa rada ya kijeshi. Kwa hiyo ilikuwa ni lazima kupata nchi ndani ya afrika Mashariki ambao watakubali madege hayo ya kijeshi ya Israel kutua kwenye uwanja wake wa ndege na kujaza mafuta lakini pia kujiandaa na kuanzisha operation kutokea hapo na pia anga lao kutumika kuanzisha shambulizi la kijeshi kuelekea Uganda. Sasa japokuwa nchi zote za Afrika Mashariki zilikuwa hazikubaliana na kitendo cha Rais wa Uganda kushirikiana na watekaji, lakini hakukuwa na hata nchi moja ambayo ilikuwa iko tayari kuingia kwenye mzozo na Idd Amin kwa kuruhusu viwanja vya vya ndege kutumika na ndege za jeshi la Israel au wanajeshi kujiandaa kuvamia Entebbe au pia kuruhusu anga lao kutumia na jeshi la Israel. Ndipo hapa ambapo kwa haraka sana siku hiyo hiyo Waziri Mkuu Rabin akamtuma Ehud Barak na maafisa wachache wa Mossad kwenda Kenya kushawishi serikali ya Mzee Jomo Kenyatta iruhusu ndege za jeshi la Isarel kutumia kiwanja chao cha ndege. Ehud barak na wenzake hawakwenda tu moja kwa moja kwa Mzee Kenyatta, bali kwanza walienda kwa Waziri wa kilimo wa kipindi hicho Bw. Bruce McKenzie ambaye huyu aliwahi kuwa afisa wa Idara ya ujasusi ya Uingereza, MI6 na pia alikuwa swahiba mkubwa wa Ehud Barak. Kwa hiyo Israel ikamtumia Bruce McKenzie kumshawishi Mzee Jomo Kenyatta kuruhusu anga la Kenya na viwanjavya ndege kutumiwa na makomando wa Israel na ndege zao. Ehud Barak na maafisa wa Mossad hawakuishia hapa tu, bali pia walifanya vikao vya siri na wafanyabiashara wakubwa nchini Kenya wenye asili ya Israel na wale ambao walikuwa na ‘marafiki’ wa Israel kuwaomba watumie ushawishi wao wa kisiasa na kiuchumi wasaidie kumshawishi Kenyatta kukubali ombi la seriakli ya Israael viwanja vyao kutumika na ndege za kijeshi za Israel na makondo wake. Baada ya mashinikizo haya kutoka kila upande, Mzee Kenyatta hakuwa na chaguo linguine zaidi ya kukubali ombi lao. Bwana huyu McKenzie pia alikuwa na ndege yakebinafsi, na Ehud Barak akaona fursa. Walitumia ndege hii ya kiraia kuruka mpaka Uganda mijini Entebbe na kukatiza juu ya anga la uwanja wa ndege wa Entebbe na walipokuwa wanapita juu ya anga la uwanja wa ndege, Ehud Barak akatumia fursa hii kupiga picha kila eneo la uwanja. Kwa kuwa hii ilikuwa ni ndege ya kiraia, jeshi la Uganda hawakushughulika nayo. Picha hizi zilizopigwa na Ehud Barak zilikuja kuwa na umuhimumkubwa katika maandalizi ya mwisho ya oparesheni ya makomando wa Isarel Kuvamia uwanja huu. Mpaka kufikia hapa maandalizi yote muhimu yalikuwa yamekamilika. WAKATI HUO HUO Upande wa watekaji kule Uganda walikuwa wanasubria mifwedha yao dola milioni 5 za kimarekani. Rais Idd Amin naye baada ya kufikia makubaliano na Israel kuwa masharti ya fedha na wafungwa wa kipalestina kuachiwa tarehe 4 July, naye ‘akarelax’ na akaona huo ndio muda wa kutekeleza majukumu Mengine akisubiria tarehe 4 July ifike. Katika kipindi hiki Idd amin ndiye alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwa kuzingatia utaratibu wa uenyekiti kuzunguka kwa kila nchi kwa mwaka mmoja mmoja na wiki hii alikuwa anatakiwa kwenye kikao cha Umoja wa Afrika kilichokuwa kinafanyika Mauritius. Kwa hiyo Amin akafunga safari kuelekea Mauritius kwenda kukabidhi kijiti cha Uenyekiti. Ehud Barak aliposikia taarifa hii, kwa kutumia akili yake kubwa ya kuzaliwa aliyojaliwa na uzoefu wake wa ujasusi, aliona fursa adhimu kabisa hapa. Akawasiliana na walioko kikaoni huko Tel Aviv na kuwaeleza taarifa ambazo awali wote hawakuielewa. Ehud Barak: “Idd Amin akiwa ndani ya Uganda huwa anatumia Mercedes Limousine katika msafara wake” Waziri Mkuu Rabin: “Ok! Limefanyaje?’ Ehud Barak: “Nataka mtafute gari kama hiyo… Mercedes Limousine” Waziri Mkuu Rabin: “la kazi gani?” Ehud Barak: “siku ambayo kikosi cha makomando wakipanda kwenye ndege kutoka huko Israel kwenda Uganda, gari hilo nataka pia lipakiwe ndani ya ndge!” Kwa dakika kadhaa wote ambao walikuwa wanamsikiliza pale kikaoni kupitia simu hakuna ambaye alielewa nini hasa Ehud Barak alikuwa anapendekeza. Yalikuwa yamebaki masaa machache tu ambapo, weledi, ushujaa na uzalendo uliotukuka ulikuwa unaedna kudhihirika. Itaendelea #TheBOLD_JF
    0 Comments 0 Shares 292 Views
  • Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) leo limetangaza kuahirisha Mashindano ya Mataifa ya Afrika ya TotalEnergies (CHAN) yaliyokuwa yafanyike Kenya, Tanzania, na Uganda kuanzia Februari na sasa yatafanyika Agosti 2025.

    Taarifa ya CAF imekiri kwamba kumekuwa na maendeleo makubwa katika ujenzi na ukarabati wa viwanja vya michezo, maeneo ya mazoezi, hoteli, hospitali, na miundombinu mingine muhimu katika nchi hizo tatu kwa ajili ya mashindano hayo.

    Hata hivyo, wataalamu wa kiufundi na miundombinu wa CAF waliopo Kenya, Tanzania, na Uganda wameishauri CAF kwamba muda zaidi unahitajika ili kuhakikisha miundombinu inafikia viwango vinavyohitajika kwa ajili ya kuandaa mashindano yenye mafanikio.

    Rais wa CAF, Dkt. Patrice Motsepe, amesema: "Ninatoa shukrani za dhati kwa Rais William Ruto wa Kenya, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, na Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa uongozi wao, kujitolea, na maendeleo mazuri yaliyopatikana katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya soka. Nimevutiwa na kazi inayoendelea, na nina uhakika kwamba viwanja vya michezo, maeneo ya mazoezi, hoteli, hospitali, na miundombinu mingine itakidhi viwango vya CAF ifikapo Agosti 2025."

    CAF pia imetangaza kwamba droo ya CHAN Kenya, Tanzania, na Uganda 2024 itafanyika jijini Nairobi, Jumatano, Januari 15, 2025, saa mbili usiku kwa saa za Nairobi.

    Tarehe kamili ya kuanza kwa mashindano hayo mwezi Agosti 2025 itatangazwa na CAF katika siku zijazo.

    #neliudcosiah
    Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) leo limetangaza kuahirisha Mashindano ya Mataifa ya Afrika ya TotalEnergies (CHAN) yaliyokuwa yafanyike Kenya, Tanzania, na Uganda kuanzia Februari na sasa yatafanyika Agosti 2025. Taarifa ya CAF imekiri kwamba kumekuwa na maendeleo makubwa katika ujenzi na ukarabati wa viwanja vya michezo, maeneo ya mazoezi, hoteli, hospitali, na miundombinu mingine muhimu katika nchi hizo tatu kwa ajili ya mashindano hayo. Hata hivyo, wataalamu wa kiufundi na miundombinu wa CAF waliopo Kenya, Tanzania, na Uganda wameishauri CAF kwamba muda zaidi unahitajika ili kuhakikisha miundombinu inafikia viwango vinavyohitajika kwa ajili ya kuandaa mashindano yenye mafanikio. Rais wa CAF, Dkt. Patrice Motsepe, amesema: "Ninatoa shukrani za dhati kwa Rais William Ruto wa Kenya, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, na Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa uongozi wao, kujitolea, na maendeleo mazuri yaliyopatikana katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya soka. Nimevutiwa na kazi inayoendelea, na nina uhakika kwamba viwanja vya michezo, maeneo ya mazoezi, hoteli, hospitali, na miundombinu mingine itakidhi viwango vya CAF ifikapo Agosti 2025." CAF pia imetangaza kwamba droo ya CHAN Kenya, Tanzania, na Uganda 2024 itafanyika jijini Nairobi, Jumatano, Januari 15, 2025, saa mbili usiku kwa saa za Nairobi. Tarehe kamili ya kuanza kwa mashindano hayo mwezi Agosti 2025 itatangazwa na CAF katika siku zijazo. #neliudcosiah
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 188 Views
  • Michuano ya CHAN yahairishwa, badala ya kufanyika Februari 2025 sasa yatafanyika Agosti 2025. Sababu ni kutokamiliaka kwa ujenzi wa miundombinu ya Viwanja katika Nchi wenyeji (Tanzania, Kenya na Uganda).
    Michuano ya CHAN yahairishwa, badala ya kufanyika Februari 2025 sasa yatafanyika Agosti 2025. Sababu ni kutokamiliaka kwa ujenzi wa miundombinu ya Viwanja katika Nchi wenyeji (Tanzania, Kenya na Uganda).
    Like
    Love
    4
    1 Comments 0 Shares 405 Views
  • OPERATION ENTEBBE -3

    Siku ya July 3 mwaka huo 1976 saa 12 na nusu ya jioni takribani masaa kadhaa kabla ya kufikia deadline ya mwisho waliyopewa na watekaji (July 4), Waziri mkuu wa Israel Yitzhak Rabin alitia saini nyaraka ya kuidhinisha oparesheni ya kijeshi ya uokozi (rescue mission) ambayo iliwasilishwa mezani na Meja Jenerali Yekutiel Adam (maarufu kwa jina la “Kuti”) na Brigedia Generali Dan Shomron. Pia kwa mujibu wa nyaraka hiyo iliyosainiwa na Waziri mkuu, Shomron aliteuliwa kuwa Kamanda wa utekelezaji wa Oparesheni.
    Baada ya oparesheni hii kuidhinishwa rasmi na Baraza la Mawaziri muda huo nilioutaja hapo juu, Meja Jenerali Yekutiel Adam na Brigedia Generali Dan SHomron walikusuka kikosi cha kijeshi kwa ajili ya kutekeleza oparesheni hiyo kama ifuatavyo;
    The Ground Command
    Hiki kilikuwa ni kikosi (japo sio kikosi haswa) ambcho kilikuwa na watu wawili tu, Brigedia Generali Dan Shomron na mwakilishi wa jeshi la Anga la Israel Kanali Ami Ayalon na watu wachache wa masasiliano ya jeshi. Kikosi hiki ndicho ambacho kilikuwa na amri ya mwisho juu ya nini wanajeshi walikuwa wanatakiwa kufanya pindi wakakapoanza utekelezaji wa oparesheni.
    The Asault Team
    Timu hii ilipewa kazi ya kuvamia jengo la uwanja wa ndege ambalo mateka walikuwa wanashikiliwa na kuokoa mateka wote waliomo humo.
    Kikosi hiki kilikuwa na wanajeshi 29 ambacho kiliongozwa na Luteni Kanali Yonathan Netanyahu (kaka yake Waziri Mkuu wa sasa wa Israel, Benjamin Netanyahu). Kikosi hiki kilijumuisha makomando wenye weledi wa hali juu kutoka katika kitengo maalumu cha jeshi la Israel kiitwacho SAYERET MATKAL.
    Nieleze kidogo kuhusu Sayet Matkal.
    Hiki ni kikosi cha weledi maalumu (special force) ndani ya jeshi la Israel la IDF. Makomando wanofuzu kutumika katika kikosi hiki, licha ya kupata mafunzo yote ya kijeshi kama wanajeshi wengine lakini wanaongezewa mafunzo mengine adhimu zaidi kuwafanya waweze kutekeleza oparesheni hata katika mazingira ambayo kwa akili ya kijeshi ya kawaida inaonekana kwamba hakuna uwezekano wa kufanikiwa kwa oparesheni hiyo.
    Mfano wa mafunzo haya adhimu ambayo wanapatiwa ni pamoja na ukusanyaji wa intelijensia, kufanya ‘deep recon’ (nimekosa Kiswahili chake) katika uwanja wa vita, upenyezaji wa intelijensia za kimkakati (strategic intelligence) mafunzo adhimu ya counterterrorism pamoja na uokozi wa mateka nje ya mipaka ya Israel.
    Kwa namna fulani ili kukielewa kikosi hiki unaweza kukifananisha na kikosi cha SAS kwenye jeshi la nchi ya Uingereza japo vinatofauti fulani bado. Ila kwa ufupi huo ndio muonekano wa Sayeret Matkal na shughuli zake.
    The securing Element
    Kikosi hiki kiligawanywa katika vikundi vidogo vidogo vitatu ili kuleta ufanisi.
    1.Paratroopers – hawa waliongozwa na Kanali Matan Vilnai. Kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha hakuna shughuli zozote zinaendelea ndani ya uwanja wa ndege wa Entebbe qawakati ambao oparesheni hiyo inatekelezwa. Pia walikuwa wanatakiwa kuhakikisha kuwa njia ya kurukia ndege (runway) iko ‘clear’ muda wote. Pamoja na hayo kikosi hiki pia walikuwa ndio wanaowajibika kulinda ndege za kijeshi za Israel muda wote zinatakapo kuwa kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe pamoja na ujazaji mafuta.
    2. The Golani Force – kikundi hikicha kijeshi kiliongozwa na Kanali Uri Sagi. Kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa yale madege makubwa aina ya Lockheed Harcules C-130. Pia walitakiwa kuyasogeza madege hayo karibu kabisa na terminal ambayo mateka walikuwepo ili waweze kuwapakia pindi ambapo uokozi ukiwa umefanikiwa. Lakini pia kikundi hiki kilifanya kazi kama ‘kikosi’ cha akiba endapo ambapo kungetoke dharura ya upungufu katika kikosi kingine.
    3. The Sayeret Matkal Force – kikosi hiki nacho pia kama ilivyo kwa ‘Assault Team’ ambayo nimeiongelea hapo juu, nacho pia kiliundwa na makomando wa Sayeret Matkal na kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha kuwa hakukuwa na ‘interception’ yoyote kutoka kwenye jeshi la anga la Uganda na kuwa tayari kuwazuia na kuzuia shambulizi lolote la kijeshi ikitokea kwamba wanajeshi wa Uganda walioko uwanja wa ndege wakiomba msaada kutoka kambi ya jeshi iliyoko ndani ya jiji la Entebbe.
    Kwa ujumla huo ndio ulikuwa muonekano kamili wa Kikosi kizima na majukumu ya wanajeshi wote waliohusia katika oparesheni ya uokozi kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe.
    USIKU WA TAREHE 3 JULY, 1976
    Hatimaye siku ya siku ikawadia, saa lililotarajiwa likafika. Ndege nne kubwa aina ya Lockheed Harcules C-130 zikiwa zimebea zaidi ya makomando 200 pamoja na ile gari Mercedes Limousine (pamoja na gari nyingine aina ya Land Rover) ambayo Ehud Barak alipendekeza waje nayo, ziliruka kutoka kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi ulioko eneo la Sharm El Sheikh mpakani kabisa na Misri.
    Ndege hizi nne kubwa Lockheed Harcules C-130 zilisindikizwa nyuma na ndege mbili aina ya Boeing 707 ambazo moja ilikuwa imelengwa kutumiwa kama ‘command post’ na nyingine itumike kama hospitali kutibu majeruhi ambao watatokana na mapambano ya risasi ambayo walikuwa wanayategemea kati yao na watekaji pamoja na jeshi la Uganda.
    Ndege ziliruka katika njia ya kimataifa kupita Red sea na kwa muda mwingi wa safari yake zililazimika kuruka si zaidi ya mita 30 angani (kuna muda inaelezwa kuwa iliwabidi kuruka mpaka futi 35 kutoka ardhini) ili kuepuka kuonekana na rada za Misi, Sudan na Saud Arabia.
    Safari ilikuwa ngumu haswa hasa ukizingatia kuwa ndege kubwa kama zile zikiruka katika usawa wa karibu hivyo na ardhi mtikisiko unakuwa mkubwa haswa ndani ya ndege.
    Waliokaribia mchepuko wa kusini wa Red Sea ndege zilikata kona na kupita kusini mwa nchi ya Djibouti. Kutokea hapo walielekea mpaka kutokea kaskazini mashariki mwa Nairobi, Kenya na kisha Somalia na kupita eneo la Ogaden nchini Ethiopia.
    Kutoka hapo wakapinda magharibi kufuata bonde la ufa ba mpaka kutokea juu ya ziwa Victoria.
    Ikumbukwe kwamba kati ya ndege zile mbili za Boeing 707 zilizokuwa zinafuatia nyuma na zile Harcules nne, moja ambayo ilipangwa itumike kama hospitali ilitua Nairobi, uwanja wa ndege wa Jomo Kenyetta. Ile nyingine ambayo nimeeleza kwamba ilipangwa itumike kama ‘command post’ ilikuwa inaruka kuzunguka uwanja wa ndege wa Entebbe wakati ndege zile za kijeshi zikitua. Ndege hii (command post) haikutua uwanjani na kamanda mkuu wa oparesheni hii Meja Jenerali Yekutiel Adam alikuwa ndani yake kuwaongoza wenzake walipo ardhini.
    Mnamo saa 23:00 ndege za kijeshi za Israel zilitua kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe huku milango ya nyuma ya mizigo kwenye ndege ikiwa wazi.
    Hapa nieleze kidogo…
    Mbinu kuu ambayo jeshi la Israel walikuwa wanataka kuitumia ili kufanikisha Oparesheni hii ilikuwa ni kufanya shambulio la kushtukiza. !
    Kivipi?
    Katika sehemu iliyopita nilieleza kuwa Ehud Barak baada ya kukusanya intelijensia za kutosha akiwa Kenya, aliwaeleza wenzake kuwa wapakie gari aina ya Mercedes Limousine inayofanana kabisa na ile ambayo inatumiwa na Rais Idd Amin a Uganda ambayo ilikuwa na rangi nyeusi.
    Kwa kuwa walifahamu Rais Idd Amin alikuwa safarini nchini Mauritius kukabidhi uenyekiti wa O.A.U, hivyo walitaka kuigiza kana kwamba Idd Amin alikuwa anarejea kutoka safarini na alikuwa anaenda kutembelea mateka pale uwanja wa ndege kama ambavyo ilikuwa kawaida yake. Hii ndio sababu ya wao kwenda na ile gari nyeusi aina ya Mercedes Limousine pamoja na Land Rover… ambavyo ndivyo ilikuwa namna ambavyo Idd Amin alikuwa anapenda kwenda kutembelea pale uwanjani…. Mercedes Limousine ambayo ina mbeba yeye na nyuma yake gari aina ya Land Rover iliyo na walinzi wake.
    Kwa hiyo ndege ya kwanza ya jeshi la Israel ilipotua kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe ambao kwa muda huo wa saa tano usiku kulikuwa na giza tupu taa zote za uwanja wa ndege zikiwa zimezimwa. Ndege ilitua ikiwa imefunguliwa mlango wa nyuma wa mizigo, ambako ilitoka gari aina ya Mercedes Limousine ikiongozana na Landa Rover na moja kwa zikaendeshwa kuelekea kwenye geti la Terminal ambayo mateka walikuwa wamehifadhiwa.
    Walikuwa wamefaulu kuigiza kabisa msafara wa Idd amin unavyokuwa. Msafara ulikuwa unafanana kabisa na ule wa Idd Amin lakini tofauti ilikuwa kwamba gari hizi ndani yake kuliwa na makomamdo.
    Jambo la ajabu ni kwamba walipofika mbele ya geti la Terminal badala ya kuruhusiwa kupita, wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanalinda getini waliinua bunduki zao na kuwanyoosha kuelea magari haya.
    Walichokuwa hawakijua makomando hawa ambacho wanajeshi hawa waliokuwa wanalinda hapa uwanjani walikijua ni kwamba, Siku moja ya kabla ya Idd Amin kwenda Mauritus alibadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi kwenda rangi nyeupe.
    Kwa hiyo wanajeshi hawa wa Uganda walipoona magari haya walikuwa wanajua fika kuwa huyu hakuwa Rais wao Idd Amin.

    Itaendelea
    #TheBOLD_JF
    OPERATION ENTEBBE -3 Siku ya July 3 mwaka huo 1976 saa 12 na nusu ya jioni takribani masaa kadhaa kabla ya kufikia deadline ya mwisho waliyopewa na watekaji (July 4), Waziri mkuu wa Israel Yitzhak Rabin alitia saini nyaraka ya kuidhinisha oparesheni ya kijeshi ya uokozi (rescue mission) ambayo iliwasilishwa mezani na Meja Jenerali Yekutiel Adam (maarufu kwa jina la “Kuti”) na Brigedia Generali Dan Shomron. Pia kwa mujibu wa nyaraka hiyo iliyosainiwa na Waziri mkuu, Shomron aliteuliwa kuwa Kamanda wa utekelezaji wa Oparesheni. Baada ya oparesheni hii kuidhinishwa rasmi na Baraza la Mawaziri muda huo nilioutaja hapo juu, Meja Jenerali Yekutiel Adam na Brigedia Generali Dan SHomron walikusuka kikosi cha kijeshi kwa ajili ya kutekeleza oparesheni hiyo kama ifuatavyo; The Ground Command Hiki kilikuwa ni kikosi (japo sio kikosi haswa) ambcho kilikuwa na watu wawili tu, Brigedia Generali Dan Shomron na mwakilishi wa jeshi la Anga la Israel Kanali Ami Ayalon na watu wachache wa masasiliano ya jeshi. Kikosi hiki ndicho ambacho kilikuwa na amri ya mwisho juu ya nini wanajeshi walikuwa wanatakiwa kufanya pindi wakakapoanza utekelezaji wa oparesheni. The Asault Team Timu hii ilipewa kazi ya kuvamia jengo la uwanja wa ndege ambalo mateka walikuwa wanashikiliwa na kuokoa mateka wote waliomo humo. Kikosi hiki kilikuwa na wanajeshi 29 ambacho kiliongozwa na Luteni Kanali Yonathan Netanyahu (kaka yake Waziri Mkuu wa sasa wa Israel, Benjamin Netanyahu). Kikosi hiki kilijumuisha makomando wenye weledi wa hali juu kutoka katika kitengo maalumu cha jeshi la Israel kiitwacho SAYERET MATKAL. Nieleze kidogo kuhusu Sayet Matkal. Hiki ni kikosi cha weledi maalumu (special force) ndani ya jeshi la Israel la IDF. Makomando wanofuzu kutumika katika kikosi hiki, licha ya kupata mafunzo yote ya kijeshi kama wanajeshi wengine lakini wanaongezewa mafunzo mengine adhimu zaidi kuwafanya waweze kutekeleza oparesheni hata katika mazingira ambayo kwa akili ya kijeshi ya kawaida inaonekana kwamba hakuna uwezekano wa kufanikiwa kwa oparesheni hiyo. Mfano wa mafunzo haya adhimu ambayo wanapatiwa ni pamoja na ukusanyaji wa intelijensia, kufanya ‘deep recon’ (nimekosa Kiswahili chake) katika uwanja wa vita, upenyezaji wa intelijensia za kimkakati (strategic intelligence) mafunzo adhimu ya counterterrorism pamoja na uokozi wa mateka nje ya mipaka ya Israel. Kwa namna fulani ili kukielewa kikosi hiki unaweza kukifananisha na kikosi cha SAS kwenye jeshi la nchi ya Uingereza japo vinatofauti fulani bado. Ila kwa ufupi huo ndio muonekano wa Sayeret Matkal na shughuli zake. The securing Element Kikosi hiki kiligawanywa katika vikundi vidogo vidogo vitatu ili kuleta ufanisi. 1.Paratroopers – hawa waliongozwa na Kanali Matan Vilnai. Kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha hakuna shughuli zozote zinaendelea ndani ya uwanja wa ndege wa Entebbe qawakati ambao oparesheni hiyo inatekelezwa. Pia walikuwa wanatakiwa kuhakikisha kuwa njia ya kurukia ndege (runway) iko ‘clear’ muda wote. Pamoja na hayo kikosi hiki pia walikuwa ndio wanaowajibika kulinda ndege za kijeshi za Israel muda wote zinatakapo kuwa kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe pamoja na ujazaji mafuta. 2. The Golani Force – kikundi hikicha kijeshi kiliongozwa na Kanali Uri Sagi. Kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa yale madege makubwa aina ya Lockheed Harcules C-130. Pia walitakiwa kuyasogeza madege hayo karibu kabisa na terminal ambayo mateka walikuwepo ili waweze kuwapakia pindi ambapo uokozi ukiwa umefanikiwa. Lakini pia kikundi hiki kilifanya kazi kama ‘kikosi’ cha akiba endapo ambapo kungetoke dharura ya upungufu katika kikosi kingine. 3. The Sayeret Matkal Force – kikosi hiki nacho pia kama ilivyo kwa ‘Assault Team’ ambayo nimeiongelea hapo juu, nacho pia kiliundwa na makomando wa Sayeret Matkal na kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha kuwa hakukuwa na ‘interception’ yoyote kutoka kwenye jeshi la anga la Uganda na kuwa tayari kuwazuia na kuzuia shambulizi lolote la kijeshi ikitokea kwamba wanajeshi wa Uganda walioko uwanja wa ndege wakiomba msaada kutoka kambi ya jeshi iliyoko ndani ya jiji la Entebbe. Kwa ujumla huo ndio ulikuwa muonekano kamili wa Kikosi kizima na majukumu ya wanajeshi wote waliohusia katika oparesheni ya uokozi kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe. USIKU WA TAREHE 3 JULY, 1976 Hatimaye siku ya siku ikawadia, saa lililotarajiwa likafika. Ndege nne kubwa aina ya Lockheed Harcules C-130 zikiwa zimebea zaidi ya makomando 200 pamoja na ile gari Mercedes Limousine (pamoja na gari nyingine aina ya Land Rover) ambayo Ehud Barak alipendekeza waje nayo, ziliruka kutoka kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi ulioko eneo la Sharm El Sheikh mpakani kabisa na Misri. Ndege hizi nne kubwa Lockheed Harcules C-130 zilisindikizwa nyuma na ndege mbili aina ya Boeing 707 ambazo moja ilikuwa imelengwa kutumiwa kama ‘command post’ na nyingine itumike kama hospitali kutibu majeruhi ambao watatokana na mapambano ya risasi ambayo walikuwa wanayategemea kati yao na watekaji pamoja na jeshi la Uganda. Ndege ziliruka katika njia ya kimataifa kupita Red sea na kwa muda mwingi wa safari yake zililazimika kuruka si zaidi ya mita 30 angani (kuna muda inaelezwa kuwa iliwabidi kuruka mpaka futi 35 kutoka ardhini) ili kuepuka kuonekana na rada za Misi, Sudan na Saud Arabia. Safari ilikuwa ngumu haswa hasa ukizingatia kuwa ndege kubwa kama zile zikiruka katika usawa wa karibu hivyo na ardhi mtikisiko unakuwa mkubwa haswa ndani ya ndege. Waliokaribia mchepuko wa kusini wa Red Sea ndege zilikata kona na kupita kusini mwa nchi ya Djibouti. Kutokea hapo walielekea mpaka kutokea kaskazini mashariki mwa Nairobi, Kenya na kisha Somalia na kupita eneo la Ogaden nchini Ethiopia. Kutoka hapo wakapinda magharibi kufuata bonde la ufa ba mpaka kutokea juu ya ziwa Victoria. Ikumbukwe kwamba kati ya ndege zile mbili za Boeing 707 zilizokuwa zinafuatia nyuma na zile Harcules nne, moja ambayo ilipangwa itumike kama hospitali ilitua Nairobi, uwanja wa ndege wa Jomo Kenyetta. Ile nyingine ambayo nimeeleza kwamba ilipangwa itumike kama ‘command post’ ilikuwa inaruka kuzunguka uwanja wa ndege wa Entebbe wakati ndege zile za kijeshi zikitua. Ndege hii (command post) haikutua uwanjani na kamanda mkuu wa oparesheni hii Meja Jenerali Yekutiel Adam alikuwa ndani yake kuwaongoza wenzake walipo ardhini. Mnamo saa 23:00 ndege za kijeshi za Israel zilitua kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe huku milango ya nyuma ya mizigo kwenye ndege ikiwa wazi. Hapa nieleze kidogo… Mbinu kuu ambayo jeshi la Israel walikuwa wanataka kuitumia ili kufanikisha Oparesheni hii ilikuwa ni kufanya shambulio la kushtukiza. ! Kivipi? Katika sehemu iliyopita nilieleza kuwa Ehud Barak baada ya kukusanya intelijensia za kutosha akiwa Kenya, aliwaeleza wenzake kuwa wapakie gari aina ya Mercedes Limousine inayofanana kabisa na ile ambayo inatumiwa na Rais Idd Amin a Uganda ambayo ilikuwa na rangi nyeusi. Kwa kuwa walifahamu Rais Idd Amin alikuwa safarini nchini Mauritius kukabidhi uenyekiti wa O.A.U, hivyo walitaka kuigiza kana kwamba Idd Amin alikuwa anarejea kutoka safarini na alikuwa anaenda kutembelea mateka pale uwanja wa ndege kama ambavyo ilikuwa kawaida yake. Hii ndio sababu ya wao kwenda na ile gari nyeusi aina ya Mercedes Limousine pamoja na Land Rover… ambavyo ndivyo ilikuwa namna ambavyo Idd Amin alikuwa anapenda kwenda kutembelea pale uwanjani…. Mercedes Limousine ambayo ina mbeba yeye na nyuma yake gari aina ya Land Rover iliyo na walinzi wake. Kwa hiyo ndege ya kwanza ya jeshi la Israel ilipotua kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe ambao kwa muda huo wa saa tano usiku kulikuwa na giza tupu taa zote za uwanja wa ndege zikiwa zimezimwa. Ndege ilitua ikiwa imefunguliwa mlango wa nyuma wa mizigo, ambako ilitoka gari aina ya Mercedes Limousine ikiongozana na Landa Rover na moja kwa zikaendeshwa kuelekea kwenye geti la Terminal ambayo mateka walikuwa wamehifadhiwa. Walikuwa wamefaulu kuigiza kabisa msafara wa Idd amin unavyokuwa. Msafara ulikuwa unafanana kabisa na ule wa Idd Amin lakini tofauti ilikuwa kwamba gari hizi ndani yake kuliwa na makomamdo. Jambo la ajabu ni kwamba walipofika mbele ya geti la Terminal badala ya kuruhusiwa kupita, wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanalinda getini waliinua bunduki zao na kuwanyoosha kuelea magari haya. Walichokuwa hawakijua makomando hawa ambacho wanajeshi hawa waliokuwa wanalinda hapa uwanjani walikijua ni kwamba, Siku moja ya kabla ya Idd Amin kwenda Mauritus alibadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi kwenda rangi nyeupe. Kwa hiyo wanajeshi hawa wa Uganda walipoona magari haya walikuwa wanajua fika kuwa huyu hakuwa Rais wao Idd Amin. Itaendelea #TheBOLD_JF
    0 Comments 0 Shares 548 Views
  • OPERATION ENTEBBE -4

    Katika sehemmu iliyopita nilieleza namna ambavyo baada ya madege ya kivita ya Lockheed Harcules C-130 kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe na moja ya ndege hizo kwenda moja kwa moja karibu na geti la Terminal huku mlango wa nyuma ukiwa wazi na kutoka gari aina na Mercides pamoja na Land Rover kufanana kabisa na msafara wa Idd Amin atembeleapo uwanja wa ndege, la kini ajabu ni kwamba walijikuta wakinyooshewa bunduki na wanajeshi waliokuwa wanalinda getini…
    Walikuwa hawana taarifa kuwa Amin alikuwa amebadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi kwenda nyeupe kabla ya safari yake ya kwenda Mauritius kwenye kikao cha O.A.U.
    Tuendelee…
    SEHEMU TA NNE
    Wanajeshi hawa wawili wa Uganda waliokuwa getini walinyanyua bunduki zao aina ya Kalashnikov na hawakuonyesha dalili kwamba labda walikuwa wanataka kufanya ukaguzi wa kawaida tu kabla ya kuwaruhusu, walionyesha dhahiri kabisa kwamba walikuwa wanataka kufanya shambulio.
    Kabla wanajeshi hao wa Uganda kufanya lolote lile, Netanyahu na komando mwingine ambao walikuwa ndani ya gari walitumia weledi wao kufanya uamuzi makini wa haraka kwa kufyatua risasi kutoka kwenye bastola zao zenye ‘silencer’ na mara moja wale wanajeshi wawili wa Uganda walienda chini.
    Lakini moja ya wale wanajeshi wa Uganda waliodondoka chini baada ya kufyatuliwa risasi, hakufa mara moja na alikuwa anajitahidi kuinuka. Hii ilisababisha komando mwingine wa Israel kufyatua risasi lakini safari hii huyu komando wa Israel alifyatua risasi kutoka kwenye bunduki ambayo haina ‘silencer’. Hii iliwashitua wanajeshi wengine wa Uganda waliokuwa nje ya Terminal na kuanza kukimbilia walipokuwa wanasikia milio ya risasi inatokea huku wanafyatua risasi.
    Kwa maneno mengine ilikuwa kwa kiasi fulani walichokuwa wamekipanga makomando wa Israel, kufanya shambulio la kushitukiza lakini mpaka muda huu tayari ile ‘element of surprise’ ilikuwa haipo tena, jeshi la Uganda lilikuwa limeshitukia ‘mchezo’.
    Bila kuchelewa sana, makomando wote walikuwa kwenye zile gari mbili (Mercedes na Land Rover) waliruka nje ya gari na kukimbia kuelekea ndani ya terminal.
    Vichwani mwao walikuwa bado hawajaondokewa na kumbukumbu ya oparesheni kama hii iliyotokea miaka miwili iliyopita nchini Israel kwenye mji wa Ma’a lot ambapowatekaji wa KIpalestina baada ya kushituka kuwa kulikuwa na makomando wa Israel wamefika kufanya uokozi, waliwapiga risasi mateka wao 25 ambao kati yao 22 walikuwa ni watoto wadogo.
    Hivyo Netanyahu na wenzake hawakutaka kitu kama hiki kjitokeze tena… Netenyahu na makomando wenzake wa Syeret Matkal kwa ustadi wa hali ya juu walikimbia na kuingia ndani ya terminal na kuwaacha vile vikosi vingine kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliopo nje ya terminal (kama nilivyoeleza juzi namna kikosi kilivyogawanywa kwenye vikundi vidogo kila kimoja kikipewa jukumu lake).
    Mateka wanaeleza kwamba baada ya mpambano ya risasi kuanza huko nje ya terminal waliwaona watekaji kadhaa wakiongozwa na yule aliyeonekana kama kiongozi wao, Wilfred Bose waliingia ndani ya terminal wakiwa wanahaha kama wamechanganyikiwa wasijue wafanye nini, ilionekana dhahiri kuwa walikuwa hawajajiandaa kwa hili shambulio la ghafla, ilionekana dhahiri kwamba katika akili yao walikuwa wanasubiria Israel kutimiza masharti yao ili waweze kuachia mateka.
    Kuna muda Wilfred Bose alionekana kunyoonya bunduki yake kwa mateka kama vile anawataka kuwamininia risasi lakini alikuwa anashindwa kufanya uamuzi huo. Bose aligeuka ghafla baada ya kusikia kishindo cha mlango wa terminal ukifunguliwa.
    Makomando wa Israel walikuwa wametumia weledi na ustadi wao wa hali ya juu kuingia ndani ya terminal kwa muda sahihi kabla ya Wilfred Bose na wenzake kufanya uamuzi wowote wa kuua mateka.
    Makomando wa Israel walipoingia tu ndani ya terminal, mmoja wao mkononi walikuwa na kipaza sauti aina ya ‘megaphone’ na alikuwa anaongeea kwa nguvu kwa lugha ya kihebrania, “Lay down, Lay down. We are Israel soldiers. Lay down. Lay down!!”.
    Mateka wote wa kiisrael hata wale waliokuwa wamekaa kitako walilala chini, hivyo ndani ya sekunde chache tu kila mtu ambaye alibakia amesimama alikuwa ni halali yao kumtandika risasi.
    Kwa bahati mbaya kulikuwa na mateka kadhaa ambao wwalikuwa hawajui kihebreania sawia na hii iliwagharimu sana. Kwa mfano kulikuwa na kijana wa mika 19 aliyeitwa Jean-Jacques Maimoni, huyu alikuwa amehamia Israel siku si nyingi sana kutokea nchini ufaransa. Lilipotolewa tangazo hilo la kila mtu kulala chini hakuelewa na alibakia akiwa amesimama na alitandikwa risasi na makomando wa Israel pamoja na wale watekaji. Kijana huyu hakuwa peke yake, lakini pia kulikuwa na mateka mwingine aliyeitwa Ida Borochovitch, ambaye alihamia Israel kutoka nchini Urusi.
    Risasi zilirindima kwa takribani dakika mbili nzima na baadae ukimya wa kama sekunde 15 ukatawala na moja wa makomando wa kiisrael akauliza kwa kiebrania, “where are the rest of them?” (“wako wapi wengine?”). Mateka wakaonyesha kidole kwenye chumba kidogo kilichopo pembeni.
    Makomando wakarusha mabomu kadhaa ya kutupa kwa mkono na kisha kuingia ndani ya chumba hicho na kuwamiminia risasi wote ambao walikuwa humo.
    Milio ya risasi ndani ya terminal hatimaye ilikuwa imekoma japo bado huko nje walisikia majibizano ya risasi. Mwanajeshi mmoja wa Israel kati ya wale waliopo ndani ya terminal, kwa sauti ya utulivu kabisa na katika lugha ya kihebrania aliwatangazia mateka, “listen guys, we’ve come to take you home!” (“sikilizeni, tumekuja kuwachukua kuwarudisha nyumbani!”).
    Baada ya hapo makomando walianza kuwatoa mateka kutoka kwenye terminal na kuwapakia kwenye ndege kwa tahadhari kubwa huku wale wenzao wengine wakiendelea kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanarusha risasi kutoka kwenye maeneo ya kujificha ndani ya uwanja wa ndege.
    Wakiwa wanaendelea kuwapakia mateka waliowaokoa kwenye ndege, kumbe kulikuwa na mwanajeshi wa Uganda amebakia juu kwenye mnara wa uongozaji (airport control tower). Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibunui kutoka kwa mtoto wa Idd Amin anasema kwamba mwanajeshi huyu alikuwa ni binamu wa Idd Amin. Kutokea hapo kwenye mnara alimimina risasi mfululizo kwa makomando wa Israel na moja ya risasi hizi ilimpaka Koamando Yonatan Netanyahu ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Matkal iliyopo hapoa na alipoteza uhai pale pale.
    Wanajeshi wa Isarel walijibu mapigo kwa kurusha bomu la roketi ndogo ya begani na kusambaratisha kabisa kiota cha mnara na kumuua mwanajeshi wa Uganda aliyekuwa anawashambulia.
    Baada ya hapo waliwapakia kwenye ndege mateka wote ambao waliokolewa pamoja na miili ya Waisrael ambao walifariki kwenye majibizano hayo ya risasi.
    Kisha ili kuhakikisha kuwa hakuna ndege itakayowafuatia nyuma wakiondoka au kushambuliwa, walilipua ndege zote za jeshi la Uganda ambazo zilikuwa uwanjani hapo.
    Oparesheni yote hii ilichukua takribani dakika 53 ambapo dakika 30 pekee ndio zilikuwa za mapigano na 23 zilizosalia zilikuwa za kupakia mateka walio okolewa na kuondoka.
    Mpaka kufikia mwishio mwa oparesheni, jumla ya watekaji wote 7 walikuwa wameuwawa, pia wanajeshi 45 wa jeshi la Uganda walikuwa wameuwawa pia. Lakini pia ndege za kijeshi 11 aina ya MiG-17 na Mig-21 zililipuliwa na makomando wa Isarel. Ikumbukwe kwamba ndege hizi ndizo zilikuwa ni ndege zote za kijeshi ambazo zilikuwa zinamilikiwa na jeshi la anga la Uganda. Hii inaonyesha moja kati ya mapungufu makubwa ya kiuongozi ya Amin. Hakukuwa na busara yoyote au faida yoyote ya kimkakati kuweka ndege zote za jeshi lako la anga kwenye uwanja wa ndege wa kiraia ili kulinda mateka wa tukio ambalo wengine walikuwa wanaweza kuliona kama tukio la kigaidi na kwa namna Fulani kama ugomvi ambao ulikuwa haumuhusu moja kwa moja.
    Katika mateka wote 106 waliobakia (kumbuka nilieleza kuwa kulikuwa na mikupuo miwili ya mateka wasio wa Kiisrael au asili ya Kiyahudi waliachiwa kwa kupelekwa na ndege ufaransa nchini), kwahiyo kati ya wale 106 waliobakio, mateka watatu waliuwawa muda wa mapambano (hawa ndio wale ambao walikuwa hawaelewi kihebrania kwa ufasaha na kwa hiyo hawakulalala chini kama ilivyoamrishwa na makomando wa Israel), na mateka mmoja bibi wa miaka 74 aliyeitwa Dora Bloch aliachwa akiwa Hospitali mjini Entebbe ambako alipelekwa na Amin siku kadhaa nyuma kutokana na kuhitaji uangalizi maalumu wa kidaktari.
    Kati ya Makomando wa Isarel, ni mmoja tu ndiye aliuwawa tena dakika za mwisho (Yonatan Netanyahu) japo pia kuna makomando wengine kama watano ambao walijeruhiwa. Kifo cha kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Mitkal, Yonatan Netanyahu katika oparesheni hii ndio iliyofanya siku kadhaa baadae oparesheni hii pia kubatizwa jina la OPERATION YONATAN kwa heshima yake na ushujaa wake wa kutoa maisha yake ili kutetea na kuooa roho za raia alioapa kuwalinda.
    Baada ya kila kitu kuwekwa sawa na watu wote kupanda ndani ya ndege, waliruka mpaka Nairobi Kenya kwa mapumziko mafupi ili kutibia wale ambao walijeruhiwa (kama ambavyo nilieleza kuwa ile moja ya Boeing 707 iliyotengwa kama ‘hospitali’ ilibaki Nairobi).
    Baada ya matibabu hapo Nairobi, madege yote yaliruka kurudi Israel. Kwa kifupi operation hii was a big SUCCESS.!
    Japokuwa baada ya ulimwengu mzima kutangaziwa juu ya kilichotokea, juu ya ‘umafia’ uliofanywa na Israel, ulimwengu uligawanyika kila nchi ukiunga mkono upande fulani, lakini nchi nyingi ziliunga mkono Israel kwa matumizi ya jeshi katika nchi nyingine, wengi walimlaumu Amin kwa kushindwa kutumia diplomasia kumaliza mzozo huu. Ajabu ni kwamba mwezi huo wa July, Mkuu wa Majeshi wa Iran moja wa mahsimu wa siku zote wa Israel aliandika barua kwa Waziri mkuu wa Israel kumpongeza kuhusu Oparation hiyo na kumpa pole kwa kifo cha Yonatan Netanyahu akimuita Yonatan kumsifu kuwa ni ‘martyr’.
    Vyovyote vile ambavyo unaweza kuitazama oparesheni hii kwenye jicho la kisiasa ua kidiplomasia, kwamba kama ilikuwa ni sahihi au si sahihi lakini katika jicho la kijeshi na ujasusi hii ni moja ya oparesheni murua kabisa kuwahi kufanyika katika historia ya majeshi duniani. Moja ya manguli wa “ulimwengu wa giza”, Bw. Henry Kissinger aliwahi kutamka kuwa hii ilikuwa ni “an immposible mission”!
    Umaridadi wa oparesheni hii umefanya hata vitengo kadhaa vya weledi vya majeshi mbali mbali kutaka kuiga mfano wake lakini bila mafanikio yoyote. Kwa mfano Wamarekani walijaribu kuiga umaridadi wa Oparesheni hii na kufanya ya kwao iliyoitwa Oparation Eagle Claw baada ya kutokea kwa utekeaji kwenye ubalozi wa Iran lakini oparesheni hiyo ilifeli vibaya.
    Sasa hivi kama wewe ni mwanajeshi katika jeshi fulani kwenye kitengo cha weledi (special force) au labda ni jasusi maalumu, lazima katika hatua fulani ya japo hata ‘darasani’ kwenye makaratasi utafundwa kuhusu Oparetion Entebbe na namna ilivyo tekelezwa.
    Oparesheni hii ilimuacha Amin na aibu kubwa kiasi kwamba akaendelea kufanya vitu ambavyo vilidhihirisha udhaifu wake wa kiungozi. Kwa mfano, yule bibi wa miaka 74 aliyeachwa hospitali mjini Entebbe, aliamuru auwawe kinyama. Lakini pia Amin alisimami kuwawa kwa McKenzie yule waziri wa kilimo wa Kenya ambaye alimsaidia Ehud Barak kumshinikiza Mzee Jomo Kenyetta kuruhusu ndege za jeshi la Israel kutumia viwanja vya ndege vya Kenya wakati wa utekelezaji wa OParesheni hiyo na pia kumsaidi kukusanya Intelijensia kwa kutumia ndege yake binafsi.
    McKenzie aliuwawa kwa bomu lililotegwa kwenye gari yake.
    Pia Amin alisimamia ulipuaji kwa bomu moja ya hoteli kubwa Nairobi kipindi hicho ambayo ilikuwa inaitwa The Norfolk Hotel, ambayo ilimilikiwa na moja ya wayahudi mashuhuri nchini Kenya.
    [6/12, 13:48] The Bold: Licha ya ‘fujo’ zote hizi ambazo Amin alizifanya baada ya jeshi lake kudhalilika kutokana na Oeration Entebbe lakini hatupawsi kusahau kwamba chini ya miaka mitatu baadae, yaani baada ya utekelezaji wa opareshini hii, Idd Amin aliondolewa kwa aibu madarakani na majeshi ya Tanzania na kumfanya akimbie nchi yake.

    ......................MWISHO..............
    #TheBOLD_JF
    OPERATION ENTEBBE -4 Katika sehemmu iliyopita nilieleza namna ambavyo baada ya madege ya kivita ya Lockheed Harcules C-130 kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe na moja ya ndege hizo kwenda moja kwa moja karibu na geti la Terminal huku mlango wa nyuma ukiwa wazi na kutoka gari aina na Mercides pamoja na Land Rover kufanana kabisa na msafara wa Idd Amin atembeleapo uwanja wa ndege, la kini ajabu ni kwamba walijikuta wakinyooshewa bunduki na wanajeshi waliokuwa wanalinda getini… Walikuwa hawana taarifa kuwa Amin alikuwa amebadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi kwenda nyeupe kabla ya safari yake ya kwenda Mauritius kwenye kikao cha O.A.U. Tuendelee… SEHEMU TA NNE Wanajeshi hawa wawili wa Uganda waliokuwa getini walinyanyua bunduki zao aina ya Kalashnikov na hawakuonyesha dalili kwamba labda walikuwa wanataka kufanya ukaguzi wa kawaida tu kabla ya kuwaruhusu, walionyesha dhahiri kabisa kwamba walikuwa wanataka kufanya shambulio. Kabla wanajeshi hao wa Uganda kufanya lolote lile, Netanyahu na komando mwingine ambao walikuwa ndani ya gari walitumia weledi wao kufanya uamuzi makini wa haraka kwa kufyatua risasi kutoka kwenye bastola zao zenye ‘silencer’ na mara moja wale wanajeshi wawili wa Uganda walienda chini. Lakini moja ya wale wanajeshi wa Uganda waliodondoka chini baada ya kufyatuliwa risasi, hakufa mara moja na alikuwa anajitahidi kuinuka. Hii ilisababisha komando mwingine wa Israel kufyatua risasi lakini safari hii huyu komando wa Israel alifyatua risasi kutoka kwenye bunduki ambayo haina ‘silencer’. Hii iliwashitua wanajeshi wengine wa Uganda waliokuwa nje ya Terminal na kuanza kukimbilia walipokuwa wanasikia milio ya risasi inatokea huku wanafyatua risasi. Kwa maneno mengine ilikuwa kwa kiasi fulani walichokuwa wamekipanga makomando wa Israel, kufanya shambulio la kushitukiza lakini mpaka muda huu tayari ile ‘element of surprise’ ilikuwa haipo tena, jeshi la Uganda lilikuwa limeshitukia ‘mchezo’. Bila kuchelewa sana, makomando wote walikuwa kwenye zile gari mbili (Mercedes na Land Rover) waliruka nje ya gari na kukimbia kuelekea ndani ya terminal. Vichwani mwao walikuwa bado hawajaondokewa na kumbukumbu ya oparesheni kama hii iliyotokea miaka miwili iliyopita nchini Israel kwenye mji wa Ma’a lot ambapowatekaji wa KIpalestina baada ya kushituka kuwa kulikuwa na makomando wa Israel wamefika kufanya uokozi, waliwapiga risasi mateka wao 25 ambao kati yao 22 walikuwa ni watoto wadogo. Hivyo Netanyahu na wenzake hawakutaka kitu kama hiki kjitokeze tena… Netenyahu na makomando wenzake wa Syeret Matkal kwa ustadi wa hali ya juu walikimbia na kuingia ndani ya terminal na kuwaacha vile vikosi vingine kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliopo nje ya terminal (kama nilivyoeleza juzi namna kikosi kilivyogawanywa kwenye vikundi vidogo kila kimoja kikipewa jukumu lake). Mateka wanaeleza kwamba baada ya mpambano ya risasi kuanza huko nje ya terminal waliwaona watekaji kadhaa wakiongozwa na yule aliyeonekana kama kiongozi wao, Wilfred Bose waliingia ndani ya terminal wakiwa wanahaha kama wamechanganyikiwa wasijue wafanye nini, ilionekana dhahiri kuwa walikuwa hawajajiandaa kwa hili shambulio la ghafla, ilionekana dhahiri kwamba katika akili yao walikuwa wanasubiria Israel kutimiza masharti yao ili waweze kuachia mateka. Kuna muda Wilfred Bose alionekana kunyoonya bunduki yake kwa mateka kama vile anawataka kuwamininia risasi lakini alikuwa anashindwa kufanya uamuzi huo. Bose aligeuka ghafla baada ya kusikia kishindo cha mlango wa terminal ukifunguliwa. Makomando wa Israel walikuwa wametumia weledi na ustadi wao wa hali ya juu kuingia ndani ya terminal kwa muda sahihi kabla ya Wilfred Bose na wenzake kufanya uamuzi wowote wa kuua mateka. Makomando wa Israel walipoingia tu ndani ya terminal, mmoja wao mkononi walikuwa na kipaza sauti aina ya ‘megaphone’ na alikuwa anaongeea kwa nguvu kwa lugha ya kihebrania, “Lay down, Lay down. We are Israel soldiers. Lay down. Lay down!!”. Mateka wote wa kiisrael hata wale waliokuwa wamekaa kitako walilala chini, hivyo ndani ya sekunde chache tu kila mtu ambaye alibakia amesimama alikuwa ni halali yao kumtandika risasi. Kwa bahati mbaya kulikuwa na mateka kadhaa ambao wwalikuwa hawajui kihebreania sawia na hii iliwagharimu sana. Kwa mfano kulikuwa na kijana wa mika 19 aliyeitwa Jean-Jacques Maimoni, huyu alikuwa amehamia Israel siku si nyingi sana kutokea nchini ufaransa. Lilipotolewa tangazo hilo la kila mtu kulala chini hakuelewa na alibakia akiwa amesimama na alitandikwa risasi na makomando wa Israel pamoja na wale watekaji. Kijana huyu hakuwa peke yake, lakini pia kulikuwa na mateka mwingine aliyeitwa Ida Borochovitch, ambaye alihamia Israel kutoka nchini Urusi. Risasi zilirindima kwa takribani dakika mbili nzima na baadae ukimya wa kama sekunde 15 ukatawala na moja wa makomando wa kiisrael akauliza kwa kiebrania, “where are the rest of them?” (“wako wapi wengine?”). Mateka wakaonyesha kidole kwenye chumba kidogo kilichopo pembeni. Makomando wakarusha mabomu kadhaa ya kutupa kwa mkono na kisha kuingia ndani ya chumba hicho na kuwamiminia risasi wote ambao walikuwa humo. Milio ya risasi ndani ya terminal hatimaye ilikuwa imekoma japo bado huko nje walisikia majibizano ya risasi. Mwanajeshi mmoja wa Israel kati ya wale waliopo ndani ya terminal, kwa sauti ya utulivu kabisa na katika lugha ya kihebrania aliwatangazia mateka, “listen guys, we’ve come to take you home!” (“sikilizeni, tumekuja kuwachukua kuwarudisha nyumbani!”). Baada ya hapo makomando walianza kuwatoa mateka kutoka kwenye terminal na kuwapakia kwenye ndege kwa tahadhari kubwa huku wale wenzao wengine wakiendelea kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanarusha risasi kutoka kwenye maeneo ya kujificha ndani ya uwanja wa ndege. Wakiwa wanaendelea kuwapakia mateka waliowaokoa kwenye ndege, kumbe kulikuwa na mwanajeshi wa Uganda amebakia juu kwenye mnara wa uongozaji (airport control tower). Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibunui kutoka kwa mtoto wa Idd Amin anasema kwamba mwanajeshi huyu alikuwa ni binamu wa Idd Amin. Kutokea hapo kwenye mnara alimimina risasi mfululizo kwa makomando wa Israel na moja ya risasi hizi ilimpaka Koamando Yonatan Netanyahu ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Matkal iliyopo hapoa na alipoteza uhai pale pale. Wanajeshi wa Isarel walijibu mapigo kwa kurusha bomu la roketi ndogo ya begani na kusambaratisha kabisa kiota cha mnara na kumuua mwanajeshi wa Uganda aliyekuwa anawashambulia. Baada ya hapo waliwapakia kwenye ndege mateka wote ambao waliokolewa pamoja na miili ya Waisrael ambao walifariki kwenye majibizano hayo ya risasi. Kisha ili kuhakikisha kuwa hakuna ndege itakayowafuatia nyuma wakiondoka au kushambuliwa, walilipua ndege zote za jeshi la Uganda ambazo zilikuwa uwanjani hapo. Oparesheni yote hii ilichukua takribani dakika 53 ambapo dakika 30 pekee ndio zilikuwa za mapigano na 23 zilizosalia zilikuwa za kupakia mateka walio okolewa na kuondoka. Mpaka kufikia mwishio mwa oparesheni, jumla ya watekaji wote 7 walikuwa wameuwawa, pia wanajeshi 45 wa jeshi la Uganda walikuwa wameuwawa pia. Lakini pia ndege za kijeshi 11 aina ya MiG-17 na Mig-21 zililipuliwa na makomando wa Isarel. Ikumbukwe kwamba ndege hizi ndizo zilikuwa ni ndege zote za kijeshi ambazo zilikuwa zinamilikiwa na jeshi la anga la Uganda. Hii inaonyesha moja kati ya mapungufu makubwa ya kiuongozi ya Amin. Hakukuwa na busara yoyote au faida yoyote ya kimkakati kuweka ndege zote za jeshi lako la anga kwenye uwanja wa ndege wa kiraia ili kulinda mateka wa tukio ambalo wengine walikuwa wanaweza kuliona kama tukio la kigaidi na kwa namna Fulani kama ugomvi ambao ulikuwa haumuhusu moja kwa moja. Katika mateka wote 106 waliobakia (kumbuka nilieleza kuwa kulikuwa na mikupuo miwili ya mateka wasio wa Kiisrael au asili ya Kiyahudi waliachiwa kwa kupelekwa na ndege ufaransa nchini), kwahiyo kati ya wale 106 waliobakio, mateka watatu waliuwawa muda wa mapambano (hawa ndio wale ambao walikuwa hawaelewi kihebrania kwa ufasaha na kwa hiyo hawakulalala chini kama ilivyoamrishwa na makomando wa Israel), na mateka mmoja bibi wa miaka 74 aliyeitwa Dora Bloch aliachwa akiwa Hospitali mjini Entebbe ambako alipelekwa na Amin siku kadhaa nyuma kutokana na kuhitaji uangalizi maalumu wa kidaktari. Kati ya Makomando wa Isarel, ni mmoja tu ndiye aliuwawa tena dakika za mwisho (Yonatan Netanyahu) japo pia kuna makomando wengine kama watano ambao walijeruhiwa. Kifo cha kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Mitkal, Yonatan Netanyahu katika oparesheni hii ndio iliyofanya siku kadhaa baadae oparesheni hii pia kubatizwa jina la OPERATION YONATAN kwa heshima yake na ushujaa wake wa kutoa maisha yake ili kutetea na kuooa roho za raia alioapa kuwalinda. Baada ya kila kitu kuwekwa sawa na watu wote kupanda ndani ya ndege, waliruka mpaka Nairobi Kenya kwa mapumziko mafupi ili kutibia wale ambao walijeruhiwa (kama ambavyo nilieleza kuwa ile moja ya Boeing 707 iliyotengwa kama ‘hospitali’ ilibaki Nairobi). Baada ya matibabu hapo Nairobi, madege yote yaliruka kurudi Israel. Kwa kifupi operation hii was a big SUCCESS.! Japokuwa baada ya ulimwengu mzima kutangaziwa juu ya kilichotokea, juu ya ‘umafia’ uliofanywa na Israel, ulimwengu uligawanyika kila nchi ukiunga mkono upande fulani, lakini nchi nyingi ziliunga mkono Israel kwa matumizi ya jeshi katika nchi nyingine, wengi walimlaumu Amin kwa kushindwa kutumia diplomasia kumaliza mzozo huu. Ajabu ni kwamba mwezi huo wa July, Mkuu wa Majeshi wa Iran moja wa mahsimu wa siku zote wa Israel aliandika barua kwa Waziri mkuu wa Israel kumpongeza kuhusu Oparation hiyo na kumpa pole kwa kifo cha Yonatan Netanyahu akimuita Yonatan kumsifu kuwa ni ‘martyr’. Vyovyote vile ambavyo unaweza kuitazama oparesheni hii kwenye jicho la kisiasa ua kidiplomasia, kwamba kama ilikuwa ni sahihi au si sahihi lakini katika jicho la kijeshi na ujasusi hii ni moja ya oparesheni murua kabisa kuwahi kufanyika katika historia ya majeshi duniani. Moja ya manguli wa “ulimwengu wa giza”, Bw. Henry Kissinger aliwahi kutamka kuwa hii ilikuwa ni “an immposible mission”! Umaridadi wa oparesheni hii umefanya hata vitengo kadhaa vya weledi vya majeshi mbali mbali kutaka kuiga mfano wake lakini bila mafanikio yoyote. Kwa mfano Wamarekani walijaribu kuiga umaridadi wa Oparesheni hii na kufanya ya kwao iliyoitwa Oparation Eagle Claw baada ya kutokea kwa utekeaji kwenye ubalozi wa Iran lakini oparesheni hiyo ilifeli vibaya. Sasa hivi kama wewe ni mwanajeshi katika jeshi fulani kwenye kitengo cha weledi (special force) au labda ni jasusi maalumu, lazima katika hatua fulani ya japo hata ‘darasani’ kwenye makaratasi utafundwa kuhusu Oparetion Entebbe na namna ilivyo tekelezwa. Oparesheni hii ilimuacha Amin na aibu kubwa kiasi kwamba akaendelea kufanya vitu ambavyo vilidhihirisha udhaifu wake wa kiungozi. Kwa mfano, yule bibi wa miaka 74 aliyeachwa hospitali mjini Entebbe, aliamuru auwawe kinyama. Lakini pia Amin alisimami kuwawa kwa McKenzie yule waziri wa kilimo wa Kenya ambaye alimsaidia Ehud Barak kumshinikiza Mzee Jomo Kenyetta kuruhusu ndege za jeshi la Israel kutumia viwanja vya ndege vya Kenya wakati wa utekelezaji wa OParesheni hiyo na pia kumsaidi kukusanya Intelijensia kwa kutumia ndege yake binafsi. McKenzie aliuwawa kwa bomu lililotegwa kwenye gari yake. Pia Amin alisimamia ulipuaji kwa bomu moja ya hoteli kubwa Nairobi kipindi hicho ambayo ilikuwa inaitwa The Norfolk Hotel, ambayo ilimilikiwa na moja ya wayahudi mashuhuri nchini Kenya. [6/12, 13:48] The Bold: Licha ya ‘fujo’ zote hizi ambazo Amin alizifanya baada ya jeshi lake kudhalilika kutokana na Oeration Entebbe lakini hatupawsi kusahau kwamba chini ya miaka mitatu baadae, yaani baada ya utekelezaji wa opareshini hii, Idd Amin aliondolewa kwa aibu madarakani na majeshi ya Tanzania na kumfanya akimbie nchi yake. ......................MWISHO.............. #TheBOLD_JF
    0 Comments 0 Shares 754 Views
  • TARABUSHI - KOFIA ZA KIHISTORIA.

    Leo hii ni aghalabu sana kukutana na mtu aliyevaa tarabushi kutokana na kutoweka kwa kofia hizi. Ni watu wachache sana wenye nazo, hususani wazee au wenye umri wa makamo, kwa kutaja wachache ni mbunge wa Musoma vijijini, Mh. Nimrod Mkono, na msanii wa maigizo, marehemu 'mzee small.

    Hizi ni kofia zenye rangi hasa nyekundu zikiwa na shada ya nyuzi nyeusi. Kwa kingereza zikijulikana kama 'Fez', kwa kiarabu 'Tarboosh' huku waswahili tukiita Tarabushi. Katika kuelezea historia ya Tarabushi, yanipasa kurudi miaka mia mbili iliyopita, pale ambapo Sultan Mahmud II wa dola ya Ottoman alipotangaza kofia za Fez/tarabushi kutumika kama vazi rasmi la dola hiyo. Sultani alifanya hivyo kufuatia kampeni yake ya kuboresha 'empire' ambapo alitamani watu wa Ottoman kuwa na utambulisho wao utakaowatofautisha na watu wengine.

    Kufuatia kampeni hiyo, tarabushi zilipata umaarufu mkubwa ndani na nje ya Ottoman ambapo watu wengi walianza kuvaa. Mwaka 1829, Mfalme Mahmud II alipitisha sheria kwamba tarabushi zianze kutumika katika jeshi lake, hivyo kwanzia siku hiyo tuliona wanajeshi wa Ottoman Empire wakienda kwenye uwanja wa vita wakiwa wamevaa tarabushi.

    Kabla ya wazo la kutumia Tarabushi, Sultani Mahmud II alichagua aina fulani ya kofia zenye asili ya Uingereza ambazo zina umbo la pembe tatu. Lakini watu wake wa karibu walimshauri kutotumia kofia hizo, kwasababu waliona hiyo pembe tatu humaanisha 'utatu mtakatifu' hivyo isingeleta tafsiri nzuri kwa watu wa Ottoman ambao asilimia kubwa ni waislamu. Wakristo huamini katika "utatu mtakatifu" yaani Mungu, Mwana na Roho mtakatifu.

    Wakati Sultani anaendelea kuwaza mbadala wa kofia, ikatokea siku mabaharia wa Ottoman walikuwa wanarudi kutoka Morroco. Kichwani wakiwa wamevaa kofia nyekundu zenye shada ya nyuzi nyeusi. Sultani akavutiwa na kofia hizo na hapo ndio chanzo cha kuzichagua kutumika kama utamaduni wa Ottoman Empire. Morroco ndipo zilipokuwa zinatengenezwa kwa wingi kwasababu rangi ya kutengeneza kofia hizo ilikuwa inatokana na matunda fulani ambayo yalistawi kwa wingi hapo Morroco katika mji wa Fez. Ndio maana hata jina la kofia hizo 'Fez', limetokana na mji huo ambao hadi mwaka 1912 ndio ulikuwa mji mkuu wa Morroco.

    Umaarufu wa kofia hizi uliendelea kutapakaa kote ulimwenguni, ukizingatia kwamba dola ya Ottoman ilikuwa ni dola kubwa iliyoenea sehemu nyingi. Hivyo baadhi ya nchi zikaanza kutumia kofia hizi hususani katika majeshi yao-mfano Cyprus, Ugiriki, Albania. Pia India, Misri, Ufaransa n.k.

    Kwa huku kwetu Afrika Mashariki, umaarufu wa kofia hizi ulikuja baada ya ujio wa ukoloni. Hiyo ni kutokana na ukweli kwamba katika kipindi cha Uingereza, waAfrika walijumuishwa katika jeshi la kikoloni ambalo lilikuja kuitwa 'King's African Rifles KAR' wakivaa sare za rangi ya khaki na kichwani walivaa Fez/ tarabushi. Jeshi hili lilianzishwa mwaka 1902 huko Kenya na baadae kuenea katika nchi zingine za Afrika Mashariki na hata kujumuishwa kwenye vita ya kwanza ya Dunia mwaka 1914.

    Pia katika makoloni ya Ujerumani, Tanganyika ikiwemo, kuliundwa jeshi la kikoloni 'Schutztruppe' ambapo waAfrika wengi walijumuishwa humo na kuwa Askari wa kikoloni 'Polizei-Askari', ambao sare zao zilikuwa za rangi ya khaki pamoja na kofia za tarabushi.

    Umaarufu wa kofia hizi za ulikuja kupungua mara baada kuanguka kwa dola ya Ottoman na kuzaliwa kwa nchi ya Uturuki ambapo mwaka 1925 Rais wa kwanza wa Uturuki bwana *Mustapha Kemal Artatuk,* alipiga marufuku kofia hizo. Hiyo ni katika hatua ya kuanzisha Uturuki mpya isiyo na mabaki ya kisultani. Pia huko Misri, mwaka 1956 Mara baada ya Gamer Abdel Nasser kumpindua mfalme, alipiga marufuku kofia za Tarboosh.

    Pia hata huku kwetu Afrika Mashariki, muda mfupi kidogo baada ya kupata uhuru, serikali ziliamua kubadilisha sare za majeshi yetu ambapo kofia zingine zilianza kutumika badala ya Tarabushi ambazo zilionekana ni kama za kikoloni. Na huo ndio ukawa mwanzo wa kupotea kwa kofia za Tarabushi japokuwa kuna baadhi ya watu waliendelea kubaki nazo.

    TARABUSHI - KOFIA ZA KIHISTORIA. Leo hii ni aghalabu sana kukutana na mtu aliyevaa tarabushi kutokana na kutoweka kwa kofia hizi. Ni watu wachache sana wenye nazo, hususani wazee au wenye umri wa makamo, kwa kutaja wachache ni mbunge wa Musoma vijijini, Mh. Nimrod Mkono, na msanii wa maigizo, marehemu 'mzee small. Hizi ni kofia zenye rangi hasa nyekundu zikiwa na shada ya nyuzi nyeusi. Kwa kingereza zikijulikana kama 'Fez', kwa kiarabu 'Tarboosh' huku waswahili tukiita Tarabushi. Katika kuelezea historia ya Tarabushi, yanipasa kurudi miaka mia mbili iliyopita, pale ambapo Sultan Mahmud II wa dola ya Ottoman alipotangaza kofia za Fez/tarabushi kutumika kama vazi rasmi la dola hiyo. Sultani alifanya hivyo kufuatia kampeni yake ya kuboresha 'empire' ambapo alitamani watu wa Ottoman kuwa na utambulisho wao utakaowatofautisha na watu wengine. Kufuatia kampeni hiyo, tarabushi zilipata umaarufu mkubwa ndani na nje ya Ottoman ambapo watu wengi walianza kuvaa. Mwaka 1829, Mfalme Mahmud II alipitisha sheria kwamba tarabushi zianze kutumika katika jeshi lake, hivyo kwanzia siku hiyo tuliona wanajeshi wa Ottoman Empire wakienda kwenye uwanja wa vita wakiwa wamevaa tarabushi. Kabla ya wazo la kutumia Tarabushi, Sultani Mahmud II alichagua aina fulani ya kofia zenye asili ya Uingereza ambazo zina umbo la pembe tatu. Lakini watu wake wa karibu walimshauri kutotumia kofia hizo, kwasababu waliona hiyo pembe tatu humaanisha 'utatu mtakatifu' hivyo isingeleta tafsiri nzuri kwa watu wa Ottoman ambao asilimia kubwa ni waislamu. Wakristo huamini katika "utatu mtakatifu" yaani Mungu, Mwana na Roho mtakatifu. Wakati Sultani anaendelea kuwaza mbadala wa kofia, ikatokea siku mabaharia wa Ottoman walikuwa wanarudi kutoka Morroco. Kichwani wakiwa wamevaa kofia nyekundu zenye shada ya nyuzi nyeusi. Sultani akavutiwa na kofia hizo na hapo ndio chanzo cha kuzichagua kutumika kama utamaduni wa Ottoman Empire. Morroco ndipo zilipokuwa zinatengenezwa kwa wingi kwasababu rangi ya kutengeneza kofia hizo ilikuwa inatokana na matunda fulani ambayo yalistawi kwa wingi hapo Morroco katika mji wa Fez. Ndio maana hata jina la kofia hizo 'Fez', limetokana na mji huo ambao hadi mwaka 1912 ndio ulikuwa mji mkuu wa Morroco. Umaarufu wa kofia hizi uliendelea kutapakaa kote ulimwenguni, ukizingatia kwamba dola ya Ottoman ilikuwa ni dola kubwa iliyoenea sehemu nyingi. Hivyo baadhi ya nchi zikaanza kutumia kofia hizi hususani katika majeshi yao-mfano Cyprus, Ugiriki, Albania. Pia India, Misri, Ufaransa n.k. Kwa huku kwetu Afrika Mashariki, umaarufu wa kofia hizi ulikuja baada ya ujio wa ukoloni. Hiyo ni kutokana na ukweli kwamba katika kipindi cha Uingereza, waAfrika walijumuishwa katika jeshi la kikoloni ambalo lilikuja kuitwa 'King's African Rifles KAR' wakivaa sare za rangi ya khaki na kichwani walivaa Fez/ tarabushi. Jeshi hili lilianzishwa mwaka 1902 huko Kenya na baadae kuenea katika nchi zingine za Afrika Mashariki na hata kujumuishwa kwenye vita ya kwanza ya Dunia mwaka 1914. Pia katika makoloni ya Ujerumani, Tanganyika ikiwemo, kuliundwa jeshi la kikoloni 'Schutztruppe' ambapo waAfrika wengi walijumuishwa humo na kuwa Askari wa kikoloni 'Polizei-Askari', ambao sare zao zilikuwa za rangi ya khaki pamoja na kofia za tarabushi. Umaarufu wa kofia hizi za ulikuja kupungua mara baada kuanguka kwa dola ya Ottoman na kuzaliwa kwa nchi ya Uturuki ambapo mwaka 1925 Rais wa kwanza wa Uturuki bwana *Mustapha Kemal Artatuk,* alipiga marufuku kofia hizo. Hiyo ni katika hatua ya kuanzisha Uturuki mpya isiyo na mabaki ya kisultani. Pia huko Misri, mwaka 1956 Mara baada ya Gamer Abdel Nasser kumpindua mfalme, alipiga marufuku kofia za Tarboosh. Pia hata huku kwetu Afrika Mashariki, muda mfupi kidogo baada ya kupata uhuru, serikali ziliamua kubadilisha sare za majeshi yetu ambapo kofia zingine zilianza kutumika badala ya Tarabushi ambazo zilionekana ni kama za kikoloni. Na huo ndio ukawa mwanzo wa kupotea kwa kofia za Tarabushi japokuwa kuna baadhi ya watu waliendelea kubaki nazo.
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 252 Views
  • MJUE JASUSI(intelejinsia) PAUL KAGAME SIMBA WA VITA.
    (Aliyeiweka Uganda Kiganjani Mwake).

    Unaposikia jina Paul Kagame kama mwana diplomasia mbobezi lazima ushtuke, Huyu jamaa ni mtu hatari sana katika uwanja wa vita. Ni moja ya majasusi wachache wanao ingia mapambanoni wenyewe bila kuangalia vyeo vyao.
    Ikumbukwe kwamba Paul Kagame alikuwa na ushawishi mkubwa kwenye jeshi la Uganda kutokana na umahiri wake wa intelejinsia. Kwann ipo hivi? Kagame ndie aliyeshiriki kumuondoa Idd Amin na ndie aliyeshiriki Kumuweka madarakani Museveni na pia ndie aliyeshiriki kuliasisi na kuliunda jeshi la Uganda Kwa hiyo yeye ndo alkuwa anawashauri nani anafaa kuwa Rais au hafai. Haya sasa twende.

    Baada ya vita ya Kagera, Tanzania wakamsimika Yusuf Lule kuwa Rais wa nchi ya Uganda. Kina Museveni wakaanzisha chombo chao cha kijeshi National Consultative Commission(NCC) hiki chombo ndo walikifanya kuwa na maamuzi ya mwisho ya nchi. Miezi miwili tu baada ya Tanzania kumsimika Yusufu Lule kuwa Rais kukatokea mvutano kati yake na NCC. NCC ya kina Museveni waliona Rais anavuka mipaka yake huku Rais Lule hatak nch iongozwe kijeshi.

    Hatimaye june 10 1979 Kwa ushawishi wa Museveni kiongozi wa NCC wakamuondoa Lule na kumuweka Godfrey Binaisa kuwa Rais wa nchi. Kimsingi Binaisa alikuwa km kikaragosi tu lakini maamuzi yote ya nchi yanatoka kwa NCC. Lakini Binaisa utamu wa Urais ulimkolea akavimba kichwa akamfukuza manadhimu mkuu wa jeshi Ojok baada ya kuhisi atapinduliwa. Kitendo hiki kiliwaumiza sana NCC na wakamuondoa Godfrey Binaisa na kuunda tume maalum iliyoitwa Presidential commission iliyofanya kazi kuongoza nchi baadala ya Rais.

    Baada ya migogoro mingi hapo ndipo umahiri wa Kagame ukaonekana kwa mara nyingine tena baada ya ule wa Kagame aliyeshiriki kumuondoa Dikteta Idd Amin Dada. Maana Kagame aliona Vita ya Panzi furaha kwa kunguru. Pia kumbuka yote yanatokea bado Kagame alkuwa na ushauri mkubwa wa kijeshi Uganda kutokana na umahiri wake wa kiintelejinsia.

    Milton Obote baada ya kushinda Urais 1980 kina Museveni hawakufurahia ushindi wake, ndipo Yoweri Museveni na Paul kagame Wakajitenga NCC na UNLA japokuwa walikuwa na ushawishi mkubwa juu ya vyombo hivyo. Ndipo Yoweri Museveni, Paul Kagame, Fred Rwigyema na waganda wengine 37 walianzisha chombo chao cha kijeshi kilichoitwa National Resistance Army(NRA) ili wampindue Rais.

    Kikundi hiki kilikimbilia msituni na kuanzisha mapigano makali kwa miaka sita dhidi ya majeshi ya serikali, pamoja na udogo wake(japo baadae waliongezeka arobaini wa awali) lakini kiliyachosha majeshi ya serikali kwa miaka sita. Miaka hii sita ya mapambano dhidi ya majeshi ya serikali yalidhihirisha unguli wa Paul Kagame nguli wa 'Physical Werfare' pia baadae ulidhihirika kweny mauaji ya kimbari, baada, nikipata uhai nitaelezea.

    Kwa miaka yote ya vita Paul Kagame alikuwa kiungo muhimu sana na aliheshimika sana na wapiganaji wenzake kuliko hata Museveni mwenyewe. Nyadhifa zao NRA zilikaribia kwenye usawa mmoja.

    Majeshi ya serikali yalikuwa na hali tete kupelekea askari wa miguu kuomba serikali isitishe mapigano maana walikuwa wanakufa wengi Lakini serikili ikanya ngumu kukakataa kusikiliza askari wake. Wanasema la kuvunda halina ubani. Desemba 1980 Mkuu wa majeshi ya Uganda jenerali Oyite Ojok alikufa kwa ajali ya ndege ambayo kuna kila dalili ya mkono wa Kagame.

    Baada ya Jenerali kufariki aliyetegemewa sana na Rais Obote badala ya kumteua waliotegemewa Tito Okello au Bazilio Olara okello ambaye alishiriki kumuondoa Idd Amin hatimaye akamteua askari wa chini kabisa anayetoka nae kabila moja. Hali hii iliwauzi Jeshi la serikali na waganda Na ndipo miaka 2 baadae jeshi likampindua Milton Obote na jeshi kushika nchi na kuanzisha mapambano dhidi ya vikundi vya msituni kila kimoja kikitaka kuongoza nchi. Ndipo yalifanyija maongezi nchini Kenya baina ya vikundi vyote vya msituni na serikali chini ya Rais Daniel Arap Moi ili kuleta Suluhu na kuweka muelekeo mpya wa nchi ya Uganda.

    29 januari 1986 Yoweri Kaguta Museveni akaapishws kuwa Rais mpya wa Uganda. Paul Kagame akateuliwa na Rais kuwa Chief Millitary Intelligence(Mkuu wa usalama wa Jeshi Uganda) na swahiba wake Fred Rwigyema kuwa waziri wa ulinzi. Kutokana na ushawishi wa kagame uganda ilipelekea baraza la mawaziri kujaa watusi kabila la kagame. Kwa maana nyingine twasema Kagame aliiweka Uganda kiganjani mwake japo hakuwa Rais. Mtandao mkubwa alioujenga ndani ya serikal ya Uganda, baraza la mawaziri na jeshi alikuwa na nguvu kumzidi Rais Yoweri Museveni. Uzuri ni kwamba Museveni aliujua umahiri wa kagame kijasusi na hakutaka mvutano nae maana alijua lengo lake lipi. Kagame hakuwa na nia ya Urais wa Uganda wala kuendelea kuliendesha jeshi la uganda. Bali alitaka kuwakomboa ndugu zake watusi waliokuwa wanateseka Rwanda.

    Na sasa alikuwa amekamilika kila kitu. Alikuwa na uzoefu wa kutosha, alikuwa na weledi wa kutosha. Tunathubutu kusema kwamba kwa kipindi hiki hakuna ambaye aliyekuwa anaweza kufikia daraja la juu la umahiri wa Kagame katika masuala ya Ujasusi Afrika Mashariki na Kati. Pia alikuwa na ushawishi katika nchi za kimkakati zinazopakana na Rwanda kama Kongo aliwapeleka wapiganaji wa NRA kupata mafunzo ya Special Force kipindi cha mapigano cha miaka 6 msituni dhidi ya majeshi ya serikali Obote.

    Pia alikuwa na ushawishi Tanzania(mtoto wetu tuliyemfunza wenyewe Ujasusi na alitusaidia sana kwenye vita ya Kagera).

    Mbele yake alikuwa na jambo moja tu kabla ya kuondoka kwenye uso wa Dunia ni kuiweka Rwanda mikononi mwake.

    NOTE: Mungu akinipa uhai nitawaletea Harakati za Kagame kuyamaliza mauaji ya Wahutu na watusi, kimbali hadi Kuwa Rais wa Rwanda.

    Ahsante kwa Utiifu Wako.
    MJUE JASUSI(intelejinsia) PAUL KAGAME SIMBA WA VITA. (Aliyeiweka Uganda Kiganjani Mwake). Unaposikia jina Paul Kagame kama mwana diplomasia mbobezi lazima ushtuke, Huyu jamaa ni mtu hatari sana katika uwanja wa vita. Ni moja ya majasusi wachache wanao ingia mapambanoni wenyewe bila kuangalia vyeo vyao. Ikumbukwe kwamba Paul Kagame alikuwa na ushawishi mkubwa kwenye jeshi la Uganda kutokana na umahiri wake wa intelejinsia. Kwann ipo hivi? Kagame ndie aliyeshiriki kumuondoa Idd Amin na ndie aliyeshiriki Kumuweka madarakani Museveni na pia ndie aliyeshiriki kuliasisi na kuliunda jeshi la Uganda Kwa hiyo yeye ndo alkuwa anawashauri nani anafaa kuwa Rais au hafai. Haya sasa twende. Baada ya vita ya Kagera, Tanzania wakamsimika Yusuf Lule kuwa Rais wa nchi ya Uganda. Kina Museveni wakaanzisha chombo chao cha kijeshi National Consultative Commission(NCC) hiki chombo ndo walikifanya kuwa na maamuzi ya mwisho ya nchi. Miezi miwili tu baada ya Tanzania kumsimika Yusufu Lule kuwa Rais kukatokea mvutano kati yake na NCC. NCC ya kina Museveni waliona Rais anavuka mipaka yake huku Rais Lule hatak nch iongozwe kijeshi. Hatimaye june 10 1979 Kwa ushawishi wa Museveni kiongozi wa NCC wakamuondoa Lule na kumuweka Godfrey Binaisa kuwa Rais wa nchi. Kimsingi Binaisa alikuwa km kikaragosi tu lakini maamuzi yote ya nchi yanatoka kwa NCC. Lakini Binaisa utamu wa Urais ulimkolea akavimba kichwa akamfukuza manadhimu mkuu wa jeshi Ojok baada ya kuhisi atapinduliwa. Kitendo hiki kiliwaumiza sana NCC na wakamuondoa Godfrey Binaisa na kuunda tume maalum iliyoitwa Presidential commission iliyofanya kazi kuongoza nchi baadala ya Rais. Baada ya migogoro mingi hapo ndipo umahiri wa Kagame ukaonekana kwa mara nyingine tena baada ya ule wa Kagame aliyeshiriki kumuondoa Dikteta Idd Amin Dada. Maana Kagame aliona Vita ya Panzi furaha kwa kunguru. Pia kumbuka yote yanatokea bado Kagame alkuwa na ushauri mkubwa wa kijeshi Uganda kutokana na umahiri wake wa kiintelejinsia. Milton Obote baada ya kushinda Urais 1980 kina Museveni hawakufurahia ushindi wake, ndipo Yoweri Museveni na Paul kagame Wakajitenga NCC na UNLA japokuwa walikuwa na ushawishi mkubwa juu ya vyombo hivyo. Ndipo Yoweri Museveni, Paul Kagame, Fred Rwigyema na waganda wengine 37 walianzisha chombo chao cha kijeshi kilichoitwa National Resistance Army(NRA) ili wampindue Rais. Kikundi hiki kilikimbilia msituni na kuanzisha mapigano makali kwa miaka sita dhidi ya majeshi ya serikali, pamoja na udogo wake(japo baadae waliongezeka arobaini wa awali) lakini kiliyachosha majeshi ya serikali kwa miaka sita. Miaka hii sita ya mapambano dhidi ya majeshi ya serikali yalidhihirisha unguli wa Paul Kagame nguli wa 'Physical Werfare' pia baadae ulidhihirika kweny mauaji ya kimbari, baada, nikipata uhai nitaelezea. Kwa miaka yote ya vita Paul Kagame alikuwa kiungo muhimu sana na aliheshimika sana na wapiganaji wenzake kuliko hata Museveni mwenyewe. Nyadhifa zao NRA zilikaribia kwenye usawa mmoja. Majeshi ya serikali yalikuwa na hali tete kupelekea askari wa miguu kuomba serikali isitishe mapigano maana walikuwa wanakufa wengi Lakini serikili ikanya ngumu kukakataa kusikiliza askari wake. Wanasema la kuvunda halina ubani. Desemba 1980 Mkuu wa majeshi ya Uganda jenerali Oyite Ojok alikufa kwa ajali ya ndege ambayo kuna kila dalili ya mkono wa Kagame. Baada ya Jenerali kufariki aliyetegemewa sana na Rais Obote badala ya kumteua waliotegemewa Tito Okello au Bazilio Olara okello ambaye alishiriki kumuondoa Idd Amin hatimaye akamteua askari wa chini kabisa anayetoka nae kabila moja. Hali hii iliwauzi Jeshi la serikali na waganda Na ndipo miaka 2 baadae jeshi likampindua Milton Obote na jeshi kushika nchi na kuanzisha mapambano dhidi ya vikundi vya msituni kila kimoja kikitaka kuongoza nchi. Ndipo yalifanyija maongezi nchini Kenya baina ya vikundi vyote vya msituni na serikali chini ya Rais Daniel Arap Moi ili kuleta Suluhu na kuweka muelekeo mpya wa nchi ya Uganda. 29 januari 1986 Yoweri Kaguta Museveni akaapishws kuwa Rais mpya wa Uganda. Paul Kagame akateuliwa na Rais kuwa Chief Millitary Intelligence(Mkuu wa usalama wa Jeshi Uganda) na swahiba wake Fred Rwigyema kuwa waziri wa ulinzi. Kutokana na ushawishi wa kagame uganda ilipelekea baraza la mawaziri kujaa watusi kabila la kagame. Kwa maana nyingine twasema Kagame aliiweka Uganda kiganjani mwake japo hakuwa Rais. Mtandao mkubwa alioujenga ndani ya serikal ya Uganda, baraza la mawaziri na jeshi alikuwa na nguvu kumzidi Rais Yoweri Museveni. Uzuri ni kwamba Museveni aliujua umahiri wa kagame kijasusi na hakutaka mvutano nae maana alijua lengo lake lipi. Kagame hakuwa na nia ya Urais wa Uganda wala kuendelea kuliendesha jeshi la uganda. Bali alitaka kuwakomboa ndugu zake watusi waliokuwa wanateseka Rwanda. Na sasa alikuwa amekamilika kila kitu. Alikuwa na uzoefu wa kutosha, alikuwa na weledi wa kutosha. Tunathubutu kusema kwamba kwa kipindi hiki hakuna ambaye aliyekuwa anaweza kufikia daraja la juu la umahiri wa Kagame katika masuala ya Ujasusi Afrika Mashariki na Kati. Pia alikuwa na ushawishi katika nchi za kimkakati zinazopakana na Rwanda kama Kongo aliwapeleka wapiganaji wa NRA kupata mafunzo ya Special Force kipindi cha mapigano cha miaka 6 msituni dhidi ya majeshi ya serikali Obote. Pia alikuwa na ushawishi Tanzania(mtoto wetu tuliyemfunza wenyewe Ujasusi na alitusaidia sana kwenye vita ya Kagera). Mbele yake alikuwa na jambo moja tu kabla ya kuondoka kwenye uso wa Dunia ni kuiweka Rwanda mikononi mwake. NOTE: Mungu akinipa uhai nitawaletea Harakati za Kagame kuyamaliza mauaji ya Wahutu na watusi, kimbali hadi Kuwa Rais wa Rwanda. Ahsante kwa Utiifu Wako.
    0 Comments 0 Shares 462 Views
  • ELIMU; HISTORIA NA SIFA ZA ZIWA VICTORIA .
    _______________________________

    Ziwa hili kabla ya kuitwa Victoria, lilikuwa na majina mengi yaliyotokana na wakazi walioishi kando kando yake, mfano; Kule Uganda liliitwa "Nnalubaale" kwa lugha ya Luganda, Nchini Kenya Waluo wao waliliita "Nam Lolwe" na huku Tanzania lilijulikana kama "Nyanza" kwa lugha za makabila ya wabantu.

    Baadae lilipewa jina la Malkia wa Uingereza aliyeitwa Alexandrina Victoria aliyeitawala Uingereza kuanzia mwaka 1837 hadi 1901.

    Wakati wa Ukoloni, Malkia huyu alituma wapelelezi wake kuja Afrika na ndipo Bw. John Hanning Speke na Richard Francis Burton waliamua kufanya chunguzi wa kina dhidi ziwa hili lote toka kasikazini hadi wakafanikiwa kufika katika fukwe za ng'ambo ya kusini mwaka 1858, Na wakawa ndio wazungu wa kwanza kuandika taarifa juu ya ziwa hili.
    Baada ya uchunguzi waliwasilisha ripoti kwa Malkia ambaye ndiye aliyewezesha shughuli nzima ya upelelezi na serikali ya Uingereza ikaamua kuliita kwa jina la Victoria kama sehemu ya heshima ya kumuenzi Kiongozi huyo kama ilivyo kwa maeneo mengine yanavyopewa majina ya viongozi na watu mashuhuri.


    SIFA ZAKE:
    1. Ziwa hili lina upana wa kilomita za mraba 69, 584 Japo eneo lote linalopatikana maji ni kilomita za Mraba 169, 858

    2. Victoria inakadiriwa kuwa na Urefu wa kina kuanzia mita 80 hadi mita 84 ambazo ni sawa na futi 262 hadi futi 276. Lakini maeneo mengi yana wastani wa kina cha mita 40 ambazo ni sawa na futi 130.

    3. Ziwa Victoria limegawanyika katika Nchi tatu; Tanzania, Kenya na Uganda.
    Upande wa Tanzania ziwa lina ukubwa wa kilomita za mraba 33,700 sawa na 49% ya ziwa lote, Nchini Uganda ziwa lina ukubwa wa kilomita za mraba 31, 000 sawa na 45% ya ziwa lote na Nchini Kenya ziwa lina ukubwa wa kilomita za mraba 4,100 sawa na 6% ya ziwa lote.

    4. Ziwa Victoria linakadiriwa kuwa na aina zaidi ya 500 za Samaki japo tafiti zinasema kwamba 40% ya aina zote za Samaki ziko mbioni kutoweka kabisa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kibinadamu na zile za asili.

    5. Ziwa hili lina zaidi ya visiwa 100 ambavyo hukaliwa na watu na vingine hatukaliwi na watu

    5. Ziwa hili ni la kwanza kwa ukubwa Barani Afrika na la pili kwa eneo lenye maji baridi Duniani baada ya Ziiwa Superior la Marekani, Lakini pia ni la tatu kwa ukubwa katika maziwa yote Duniani

    6. Shughuli kuu zifanyikazo katika ziwa hili ni Uvuvi, Usafirishaji, Utalii, Uvunaji wa maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali n.k.

    7. Ziwa hili hupokea maji kutoka mito mikubwa kama vile Mto Kagera, Mto Mara n.k. mbali na hapo Ziwa hili humwaga maji yake katika Mto Nile.
    ELIMU; HISTORIA NA SIFA ZA ZIWA VICTORIA . _______________________________ Ziwa hili kabla ya kuitwa Victoria, lilikuwa na majina mengi yaliyotokana na wakazi walioishi kando kando yake, mfano; Kule Uganda liliitwa "Nnalubaale" kwa lugha ya Luganda, Nchini Kenya Waluo wao waliliita "Nam Lolwe" na huku Tanzania lilijulikana kama "Nyanza" kwa lugha za makabila ya wabantu. Baadae lilipewa jina la Malkia wa Uingereza aliyeitwa Alexandrina Victoria aliyeitawala Uingereza kuanzia mwaka 1837 hadi 1901. Wakati wa Ukoloni, Malkia huyu alituma wapelelezi wake kuja Afrika na ndipo Bw. John Hanning Speke na Richard Francis Burton waliamua kufanya chunguzi wa kina dhidi ziwa hili lote toka kasikazini hadi wakafanikiwa kufika katika fukwe za ng'ambo ya kusini mwaka 1858, Na wakawa ndio wazungu wa kwanza kuandika taarifa juu ya ziwa hili. Baada ya uchunguzi waliwasilisha ripoti kwa Malkia ambaye ndiye aliyewezesha shughuli nzima ya upelelezi na serikali ya Uingereza ikaamua kuliita kwa jina la Victoria kama sehemu ya heshima ya kumuenzi Kiongozi huyo kama ilivyo kwa maeneo mengine yanavyopewa majina ya viongozi na watu mashuhuri. SIFA ZAKE: 1. Ziwa hili lina upana wa kilomita za mraba 69, 584 Japo eneo lote linalopatikana maji ni kilomita za Mraba 169, 858 2. Victoria inakadiriwa kuwa na Urefu wa kina kuanzia mita 80 hadi mita 84 ambazo ni sawa na futi 262 hadi futi 276. Lakini maeneo mengi yana wastani wa kina cha mita 40 ambazo ni sawa na futi 130. 3. Ziwa Victoria limegawanyika katika Nchi tatu; Tanzania, Kenya na Uganda. Upande wa Tanzania ziwa lina ukubwa wa kilomita za mraba 33,700 sawa na 49% ya ziwa lote, Nchini Uganda ziwa lina ukubwa wa kilomita za mraba 31, 000 sawa na 45% ya ziwa lote na Nchini Kenya ziwa lina ukubwa wa kilomita za mraba 4,100 sawa na 6% ya ziwa lote. 4. Ziwa Victoria linakadiriwa kuwa na aina zaidi ya 500 za Samaki japo tafiti zinasema kwamba 40% ya aina zote za Samaki ziko mbioni kutoweka kabisa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kibinadamu na zile za asili. 5. Ziwa hili lina zaidi ya visiwa 100 ambavyo hukaliwa na watu na vingine hatukaliwi na watu 5. Ziwa hili ni la kwanza kwa ukubwa Barani Afrika na la pili kwa eneo lenye maji baridi Duniani baada ya Ziiwa Superior la Marekani, Lakini pia ni la tatu kwa ukubwa katika maziwa yote Duniani 6. Shughuli kuu zifanyikazo katika ziwa hili ni Uvuvi, Usafirishaji, Utalii, Uvunaji wa maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali n.k. 7. Ziwa hili hupokea maji kutoka mito mikubwa kama vile Mto Kagera, Mto Mara n.k. mbali na hapo Ziwa hili humwaga maji yake katika Mto Nile.
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 158 Views
  • KHALID AUCHO WABONGO WAMEKUITA DAKTARI!!!

    Aucho amecheza soka katika vilabu mbalimbali, kama vile Halmashauri ya Manispaa ya Jinja F.C. kutoka 2009 hadi 2010, Water F.C kutoka Uganda kutoka 2010 hadi 2012, Simba FC kutoka Uganda, Tusker kutoka Kenya, Gor Mahia kutoka Kenya, na Baroka kutoka Ligi Kuu ya Soka ya Afrika Kusini.

    Kipindi kile anasajiliwa jangwani, mwaka mmoja nyuma alikuwa anawindwa na klabu moja kubwa hapa nchini lakini dili lake halikukaa sawa na panapo muda kuwadia, akatua mizigo yake Jangwani!

    Mpaka hivi sasa ndiye kiungo wa kati wa Kigeni aliyedumu nchini kwa Ubora usiomithilika licha ya sasa kasi yake kuonekana inapungua na hii ni changamoto ya kucheza michezo msimu mzima bila kupata msaidizi halisi!..

    Kabla Hujaniuliza kwanini nimemsifia huyu AUCHO kutoka kwa Wananchi njoo apa uniambie kwani Aucho kijana wa watu Aliwahi kukukosea wapi ili Tujue kabla hatujakutafsiri kama mtu mwenye nongwa binafsi!

    Yess,, Utani upo lakini sio kila wakati!

    Unyamani namuona akija FABRICE NGOMA licha naye bado hajajisimika vizuri kwenye mwendelezo bora wa kila msimu...!!!

    SEMA "WABONGO" KILA MTU KWAO #DAKTARI
    Khalid Aucho8
    #UkweliUnaumaSana馃
    #neliudcosiah

    KHALID AUCHO WABONGO WAMEKUITA DAKTARI!!! 馃 Aucho amecheza soka katika vilabu mbalimbali, kama vile Halmashauri ya Manispaa ya Jinja F.C. kutoka 2009 hadi 2010, Water F.C kutoka Uganda kutoka 2010 hadi 2012, Simba FC kutoka Uganda, Tusker kutoka Kenya, Gor Mahia kutoka Kenya, na Baroka kutoka Ligi Kuu ya Soka ya Afrika Kusini. Kipindi kile anasajiliwa jangwani, mwaka mmoja nyuma alikuwa anawindwa na klabu moja kubwa hapa nchini lakini dili lake halikukaa sawa na panapo muda kuwadia, akatua mizigo yake Jangwani! Mpaka hivi sasa ndiye kiungo wa kati wa Kigeni aliyedumu nchini kwa Ubora usiomithilika licha ya sasa kasi yake kuonekana inapungua na hii ni changamoto ya kucheza michezo msimu mzima bila kupata msaidizi halisi!.. Kabla Hujaniuliza kwanini nimemsifia huyu AUCHO kutoka kwa Wananchi njoo apa uniambie kwani Aucho kijana wa watu Aliwahi kukukosea wapi ili Tujue kabla hatujakutafsiri kama mtu mwenye nongwa binafsi! Yess,, Utani upo lakini sio kila wakati! Unyamani namuona akija FABRICE NGOMA licha naye bado hajajisimika vizuri kwenye mwendelezo bora wa kila msimu...!!! SEMA "WABONGO" KILA MTU KWAO #DAKTARI 馃ぃ鉁嶏笍 Khalid Aucho8馃嚭馃嚞 #UkweliUnaumaSana馃馃 #neliudcosiah
    Like
    2
    0 Comments 0 Shares 344 Views
  • Hujambo kaka...Mie jina langu Mike kutoka Nairobi Kenya natafuta mchumba kwa mahusiano ambayo yatatuelekeza kwenye ndoa.Nina umri wa miaka 30 hivi awe na umri sawa na wangu au awe mdogo kwangu.Nambari yangu ya whatsapp ni +254713168463.
    Hujambo kaka...Mie jina langu Mike kutoka Nairobi Kenya 馃嚢馃嚜 natafuta mchumba kwa mahusiano ambayo yatatuelekeza kwenye ndoa.Nina umri wa miaka 30 hivi awe na umri sawa na wangu au awe mdogo kwangu.Nambari yangu ya whatsapp ni +254713168463.
    Like
    Love
    4
    1 Comments 0 Shares 194 Views
  • Nyumbu ( wildebeest) uzito 140 hadi 220 kulingana na afya yake, hupendelea kula nyasi ndogo ndogo zinazochipua, kama hatopata suluba huishi hadi miaka 17 na kidogo.uzee ukimzidi akishindwa kufanya safari kutafta malisho na wenzake basi hufa kwa njaa, eidha ufanywa kitoweo cha jioni na mtawala wa eneo hilo (simba)

    Kundi LA nyumbu huwa kati ya 10,000 hadi 90,000. Endapo majani yapo yakutosha nyumbu huongezeka idadi hadi kufikia 100,000 na zaidi.vipindi vya mvua nyingi ndipo nymbu huzaliana kwa kasi zaidi,

    Nyumbu wa Serengeti hula na kuzaliana nyakati za masika tu.endapo kiangazi kitaingia nyumbuwote hufunga safari na kuelekea hifadhi jilani ya Kenya (masaimar). Nyakati hizo huko kenya huwa kunamalisho yakutosha, nyumbu hukaa miezi isiyopungua 6 ndipo hufanya safari zao.

    Nyumbu ni mnyama wa tofauti kidogo na wanyama wengine kimaumbile, yaani nyumbu amebeba muonekano wa wanyama wasiopungua 7, ngoja nikujuze,

    Nywele za shingoni; SIMBA
    Mkia: FARASI
    Ndevu:MBUZI
    Mapaja ya nyuma; PUNDA MILIA
    Mgongo :ng'ombe
    Miguu ya mbele milefu yanyuma mifupi ; FISI

    Watu husema nyumbu ni mwoga na mzembe

    Nyumbu wakiwa katika kundi huwa ni waoga saaaana, yaani at a mtoto wa duma mwenye mwezi mmoja anaweza kutishia kundi LA nyumbu 20000 na wakakimbia, na asiwepo nyumbu wa kudinda ata kugeuka nyuma.

    Ila nyumbu akiwa mwenyew huwa haogopi .ni mala chache mno nyumbu aliye pekeake kumkimbia adui yake, nyumbu akiwa mwenyewe huwa anajiona kama tembo au kifaru, huwa ni hatari zaidi ata duma hutegea wawe kwenye kundi ndio wavamie.

    Nyumbu wakiwa safarini hawajawai kupisha kitu chochote kilichopo mbeleyao. Wakiwa katika mwendo wa mchaka mchaka wakiluka mabonde na mapolomoko, wakivuka mito mikubwa mithiri ya wanajeshi wakiwa mafunzoni.

    Katika safari yao nyumbu hawajawahi kumsubiri nyumbu mwezao aliyepata ajali, aliejisahau eidha alikuw anakul majan, aliyezaa wala aliyekamatwa na mnyama mlanyama, msafala wao huwa hausubiri kitu wala hauna fea.

    Pia nyumbu hawana mda wa kumtetea mwenzao aliyedhibitiwa na mnyama mla mnyama.
    Nyumbu ( wildebeest) uzito 140 hadi 220 kulingana na afya yake, hupendelea kula nyasi ndogo ndogo zinazochipua, kama hatopata suluba huishi hadi miaka 17 na kidogo.uzee ukimzidi akishindwa kufanya safari kutafta malisho na wenzake basi hufa kwa njaa, eidha ufanywa kitoweo cha jioni na mtawala wa eneo hilo (simba) Kundi LA nyumbu huwa kati ya 10,000 hadi 90,000. Endapo majani yapo yakutosha nyumbu huongezeka idadi hadi kufikia 100,000 na zaidi.vipindi vya mvua nyingi ndipo nymbu huzaliana kwa kasi zaidi, Nyumbu wa Serengeti hula na kuzaliana nyakati za masika tu.endapo kiangazi kitaingia nyumbuwote hufunga safari na kuelekea hifadhi jilani ya Kenya (masaimar). Nyakati hizo huko kenya huwa kunamalisho yakutosha, nyumbu hukaa miezi isiyopungua 6 ndipo hufanya safari zao. Nyumbu ni mnyama wa tofauti kidogo na wanyama wengine kimaumbile, yaani nyumbu amebeba muonekano wa wanyama wasiopungua 7, ngoja nikujuze, Nywele za shingoni; SIMBA Mkia: FARASI Ndevu:MBUZI Mapaja ya nyuma; PUNDA MILIA Mgongo :ng'ombe Miguu ya mbele milefu yanyuma mifupi ; FISI Watu husema nyumbu ni mwoga na mzembe Nyumbu wakiwa katika kundi huwa ni waoga saaaana, yaani at a mtoto wa duma mwenye mwezi mmoja anaweza kutishia kundi LA nyumbu 20000 na wakakimbia, na asiwepo nyumbu wa kudinda ata kugeuka nyuma. Ila nyumbu akiwa mwenyew huwa haogopi .ni mala chache mno nyumbu aliye pekeake kumkimbia adui yake, nyumbu akiwa mwenyewe huwa anajiona kama tembo au kifaru, huwa ni hatari zaidi ata duma hutegea wawe kwenye kundi ndio wavamie. Nyumbu wakiwa safarini hawajawai kupisha kitu chochote kilichopo mbeleyao. Wakiwa katika mwendo wa mchaka mchaka wakiluka mabonde na mapolomoko, wakivuka mito mikubwa mithiri ya wanajeshi wakiwa mafunzoni. Katika safari yao nyumbu hawajawahi kumsubiri nyumbu mwezao aliyepata ajali, aliejisahau eidha alikuw anakul majan, aliyezaa wala aliyekamatwa na mnyama mlanyama, msafala wao huwa hausubiri kitu wala hauna fea. Pia nyumbu hawana mda wa kumtetea mwenzao aliyedhibitiwa na mnyama mla mnyama.
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 148 Views
  • Hii ndio ilikuwa Bendera yetu, na katikati ya Bendera ni Ngao ya Jamii (Coat of Arms) ya Nchi yetu enzi tunaitwa Deutsch-Ostafrika (Ujerumani ya Afrika Mashariki) miaka ya 1885 mpaka 1918.

    Wakati huo nchi ilikuwa na eneo la Mita Square 994,996 Km² ndani yake kuna Burundi na Rwanda, na Eneo la Nchi ya Msumbiji lililoitwa Kionga Triangle.

    Je wajua neno la Kiswahili "Shule" limetoka kwenye Neno la Kijerumani "Schule" yote yakimaanisha "School".

    Maeneo mengine yaliitwa hivi:

    • Rombo iliitwa Fischerstadt
    • Nyakanazi iliitwa Friedberg
    • Kisarawe iliitwa Hoffnungshöh
    • Tukuyu iliitwa Langenburg
    • Ushetu iliitwa Marienthal
    • Shume (huko kwa Wapare) kuliitwa Neu-Hornow
    • Mbulu kuliitwa Neu-Trier
    • Sekenke paliitwa Sachsenwald na ilikua ni Mgodi.
    • Lushoto iliitwa Wilhelmsdorf.

    Kipindi hiki ndio tulijengewa Reli iliyoitwa Usambara Railway mwaka 1891 ilijengwa na Wajerumani na ilikuwa na Km 350, ilianzia Mjini Tanga, ikawa na makutano na Kenya Mji wa Kahe, ikapita Moshi mpaka Arusha.

    Wajerumani katika Reli hii walikuwa na vichwa vya Treni 18 (Locomotive) na mabehewa 199, kipindi hicho Reli hii ilikuwa na wafanyakazi 562 huku kati yao 35 tu ndio walikuwa Wajerumani.

    Lengo la Wajerumani kujenga Reli hii ilikuwa ni kuunganisha Bandari ya Tanga na Ziwa Victoria kupitia milima ya Usambara.

    Treni la kwanza lilipita likiwa tupu tarehe 26 September 1911 ili kujaribu safari na kufanikiwa 100%, likapita tena likiwa na Abiria tarehe 4 October 1911 na kufanikiwa 100% Wajerumani wakaamini kweli kitu ni Konki.

    Hivyo ukafanyika uzinduzi wa Reli tarehe 7 February 1912, na baada ya hapo Treni lilikuwa lazima lifanye safari kila siku kutoka Tanga mpaka Buiko na Kurudi, safari ilichukua muda wa masaa 14 na dakika 40.

    Reli hii haikukamilika mpaka Arusha sababu ya Vita ya kwanza ya Dunia, Waingereza ndio Wakaiunganisha.

    #Kutoka_Maktaba
    Hii ndio ilikuwa Bendera yetu, na katikati ya Bendera ni Ngao ya Jamii (Coat of Arms) ya Nchi yetu enzi tunaitwa Deutsch-Ostafrika (Ujerumani ya Afrika Mashariki) miaka ya 1885 mpaka 1918. Wakati huo nchi ilikuwa na eneo la Mita Square 994,996 Km² ndani yake kuna Burundi na Rwanda, na Eneo la Nchi ya Msumbiji lililoitwa Kionga Triangle. Je wajua neno la Kiswahili "Shule" limetoka kwenye Neno la Kijerumani "Schule" yote yakimaanisha "School". Maeneo mengine yaliitwa hivi: • Rombo iliitwa Fischerstadt • Nyakanazi iliitwa Friedberg • Kisarawe iliitwa Hoffnungshöh • Tukuyu iliitwa Langenburg • Ushetu iliitwa Marienthal • Shume (huko kwa Wapare) kuliitwa Neu-Hornow • Mbulu kuliitwa Neu-Trier • Sekenke paliitwa Sachsenwald na ilikua ni Mgodi. • Lushoto iliitwa Wilhelmsdorf. Kipindi hiki ndio tulijengewa Reli iliyoitwa Usambara Railway mwaka 1891 ilijengwa na Wajerumani na ilikuwa na Km 350, ilianzia Mjini Tanga, ikawa na makutano na Kenya Mji wa Kahe, ikapita Moshi mpaka Arusha. Wajerumani katika Reli hii walikuwa na vichwa vya Treni 18 (Locomotive) na mabehewa 199, kipindi hicho Reli hii ilikuwa na wafanyakazi 562 huku kati yao 35 tu ndio walikuwa Wajerumani. Lengo la Wajerumani kujenga Reli hii ilikuwa ni kuunganisha Bandari ya Tanga na Ziwa Victoria kupitia milima ya Usambara. Treni la kwanza lilipita likiwa tupu tarehe 26 September 1911 ili kujaribu safari na kufanikiwa 100%, likapita tena likiwa na Abiria tarehe 4 October 1911 na kufanikiwa 100% Wajerumani wakaamini kweli kitu ni Konki. Hivyo ukafanyika uzinduzi wa Reli tarehe 7 February 1912, na baada ya hapo Treni lilikuwa lazima lifanye safari kila siku kutoka Tanga mpaka Buiko na Kurudi, safari ilichukua muda wa masaa 14 na dakika 40. Reli hii haikukamilika mpaka Arusha sababu ya Vita ya kwanza ya Dunia, Waingereza ndio Wakaiunganisha. #Kutoka_Maktaba
    Like
    2
    1 Comments 0 Shares 278 Views
  • Kwa mujibu wa Willy Paul, Diamond Platnumz hakulipwa dola milion moja bali ni Shilingi million 12 za Kenya.
    Kwa mujibu wa Willy Paul, Diamond Platnumz hakulipwa dola milion moja bali ni Shilingi million 12 za Kenya.
    0 Comments 0 Shares 268 Views
  • Diamond Platnumz amefunguka kulipwa Dola milioni moja ($1 million) ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 2.3 za Kitanzania ili kutumbuiza katika harusi inayofanyika leo hii huko Mjini Mombasa Nchini Kenya .

    Aidha, Wahudhuriaji wa harusi hiyo na mashabiki wameonesha furaha yao kukutana uso kwa uso na Msanii huyo namba moja Nchini Tanzania na Afrika Mashariki.

    Pamoja na Diamond Platnumz kulipwa fedha hizo, Wasanii wengine wakubwa wenye hadhi ya kidunia akiwemo Beyonce, Rihanna, Justin Bieber, Katty Perry, Pitbull walipotumbuiza katika harusi za Matajiri walitoza pesa kubwa ili kulinda hadhi zao za muziki zisionekane ni za kutumbuiza katika harusi ili hata Waandamanaji wa matamasha makubwa waendelee kuwaweka viwango vya juu watakapowahitaji kwenye "show".

    “$1M For Wedding Show In Mombasa ” - Diamond Platnumz via Instagram.

    Diamond Platnumz amefunguka kulipwa Dola milioni moja ($1 million) ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 2.3 za Kitanzania ili kutumbuiza katika harusi inayofanyika leo hii huko Mjini Mombasa Nchini Kenya 馃嚢馃嚜. Aidha, Wahudhuriaji wa harusi hiyo na mashabiki wameonesha furaha yao kukutana uso kwa uso na Msanii huyo namba moja Nchini Tanzania na Afrika Mashariki. Pamoja na Diamond Platnumz kulipwa fedha hizo, Wasanii wengine wakubwa wenye hadhi ya kidunia akiwemo Beyonce, Rihanna, Justin Bieber, Katty Perry, Pitbull walipotumbuiza katika harusi za Matajiri walitoza pesa kubwa ili kulinda hadhi zao za muziki zisionekane ni za kutumbuiza katika harusi ili hata Waandamanaji wa matamasha makubwa waendelee kuwaweka viwango vya juu watakapowahitaji kwenye "show". “$1M For Wedding Show In Mombasa 馃嚢馃嚜” - Diamond Platnumz via Instagram.
    0 Comments 0 Shares 356 Views
  • Meneja wa Diamond Platnumz, Sallam SK amefunguka kuhusu Diamond Platnumz kushindwa kutumbuiza huko Nchini Kenya usiku wa kuamkia leo. Hii baada ya Msanii wa kenya Willy Paul kudai kuwa Wasanii wa Tanzania wanapendelewa zaidi Nchini humo huku akimtaja Diamond Platnumz kutaka kutumbuiza kabla yake.

    “Nadhani ifike mahali wasanii muwekeze bidii
    kwenye kazi, kufeki story sababu ya fame ya kulazimisha bifu ili kutrend haisaidii, Msanii aitwae Willy aseme ukweli alikuwa anabishana na mtoto wa kike ( Zuchu ) aliblock njia Zuchu asipande kwenye steji akisema alikuwepo tokea mwanzo hivyo anataka pande yeye, ilhali wakati zamu yake allitwa apande kwenye stage aligoma na kusema hawezi kupanda yeye ni Headliner anataka Afunge show Mwisho, baada ya kuona wenzake wanapata shangwe akawa anforce kupanda kwenye Muda wa Zuchu na wala sio Diamond. Regarding why Diamond hajapanda is between us and organizer has nothing to do na msanii yoyote. Bless Up” - Sallam SK

    Toa maoni yako
    Meneja wa Diamond Platnumz, Sallam SK amefunguka kuhusu Diamond Platnumz kushindwa kutumbuiza huko Nchini Kenya usiku wa kuamkia leo. Hii baada ya Msanii wa kenya Willy Paul kudai kuwa Wasanii wa Tanzania wanapendelewa zaidi Nchini humo huku akimtaja Diamond Platnumz kutaka kutumbuiza kabla yake. “Nadhani ifike mahali wasanii muwekeze bidii kwenye kazi, kufeki story sababu ya fame ya kulazimisha bifu ili kutrend haisaidii, Msanii aitwae Willy aseme ukweli alikuwa anabishana na mtoto wa kike ( Zuchu ) aliblock njia Zuchu asipande kwenye steji akisema alikuwepo tokea mwanzo hivyo anataka pande yeye, ilhali wakati zamu yake allitwa apande kwenye stage aligoma na kusema hawezi kupanda yeye ni Headliner anataka Afunge show Mwisho, baada ya kuona wenzake wanapata shangwe akawa anforce kupanda kwenye Muda wa Zuchu na wala sio Diamond. Regarding why Diamond hajapanda is between us and organizer has nothing to do na msanii yoyote. Bless Up” - Sallam SK Toa maoni yako
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 397 Views
  • Ujenzi wa Uwanja mpya wa mpira wa miguu jijini Arusha wazidi kushika kasi.

    Uwanja huu umepewa jina la Raisi wa kwanza mwanamke Tanzania Mh Dr Samia Suluhu Hassan Stadium.

    uwanja huu ni moja kati ya viwanja vitakavyo tumika kwenye mashindano ya AFCON 2027.

    Tanzania itashirikiana na majira zake Kenya na Uganda kwenye mandalizi ya mashindano haya makubwa barani Africa.
    Ujenzi wa Uwanja mpya wa mpira wa miguu jijini Arusha wazidi kushika kasi. Uwanja huu umepewa jina la Raisi wa kwanza mwanamke Tanzania Mh Dr Samia Suluhu Hassan Stadium. uwanja huu ni moja kati ya viwanja vitakavyo tumika kwenye mashindano ya AFCON 2027. Tanzania itashirikiana na majira zake Kenya na Uganda kwenye mandalizi ya mashindano haya makubwa barani Africa.
    Like
    Love
    8
    1 Comments 0 Shares 299 Views
  • NGORONGORO HEROES HAWAPOI

    鈿斤笍 Valentino Mashaka
    鈿斤笍 Sheikhan Hamis

    TANZANIA U20 [2]-1 KENYA U20
    #paulswai
    NGORONGORO HEROES HAWAPOI 馃敟 鈿斤笍 Valentino Mashaka 鈿斤笍 Sheikhan Hamis 馃嚬馃嚳 TANZANIA U20 [2]-1 KENYA U20馃嚢馃嚜 #paulswai
    Like
    3
    0 Comments 0 Shares 83 Views
  • Jamaa ameamua kujiuzulu. Kenya ipo tofauti sana.
    Jamaa ameamua kujiuzulu. Kenya ipo tofauti sana.
    Like
    1
    0 Comments 0 Shares 175 Views
  • Kenya#uganda#burundi..socialpo.com
    Kenya#uganda#burundi..socialpo.com
    Like
    3
    0 Comments 0 Shares 142 Views
  • Kwa mujibu wa JamiiForums, kampuni ya Meta imesema kuwa kuanzia mwezi huu wa Agosti 2024 itakuwa inawalipa Watayarishi wa maudhui (Content Creator) waliopo Nchini Tanzania kupitia mitandao yake ya kijamii ambayo ni Facebook na Instagram.

    Pia mwezi huu kampuni hiyo ya Meta imerudisha mfumo na utaratibu wa kulipa Waandaji wa maudhui Nchini Kenya baada ya kusitisha utaratibu huo mwezi wa tano.

    Hata hivyo, bado Kampuni ya Meta haijatoa taarifa yoyote ile kuhusiana na kuwalipa Watengenezaji wa maudhui Nchini Tanzania lakini habari hii itakuwa ni nzuri kwa Afrika Mashariki kwa sababu itakuza soko la maudhui na kuleta faida kwa Watengenezaji hao.
    Kwa mujibu wa JamiiForums, kampuni ya Meta imesema kuwa kuanzia mwezi huu wa Agosti 2024 itakuwa inawalipa Watayarishi wa maudhui (Content Creator) waliopo Nchini Tanzania kupitia mitandao yake ya kijamii ambayo ni Facebook na Instagram. Pia mwezi huu kampuni hiyo ya Meta imerudisha mfumo na utaratibu wa kulipa Waandaji wa maudhui Nchini Kenya 馃嚢馃嚜 baada ya kusitisha utaratibu huo mwezi wa tano. Hata hivyo, bado Kampuni ya Meta haijatoa taarifa yoyote ile kuhusiana na kuwalipa Watengenezaji wa maudhui Nchini Tanzania lakini habari hii itakuwa ni nzuri kwa Afrika Mashariki kwa sababu itakuza soko la maudhui na kuleta faida kwa Watengenezaji hao.
    Like
    Love
    3
    2 Comments 0 Shares 331 Views
More Results