• World Happiness Report 2025 imetangaza orodha ya Nchi zenye furaha zaidi Duniani huku Nchi ya Finland ikiendelea kushika nafasi ya kwanza kwa mwaka wa nane (8) mfululizo, Tanzania imeshika nafasi ya 136 kati ya Nchi 147, ikishuka kwa nafasi tano kutoka nafasi ya 131 mwaka uliopita. Nafasi ya sasa inaiweka Nchi hiyo kuwa miongoni mwa Nchi 11 za mwisho Duniani kwa viwango vya furaha.

    Cha kushangaza ni kwamba Tanzania , licha ya kuwa na amani na utajiri mkubwa wa maliasili, imepitwa hata na mataifa yenye migogoro kama Somalia . Nchi jirani kama Kenya na Uganda , ambazo mara kwa mara hukumbwa na changamoto za kisiasa na kiusalama, zimepata nafasi za juu zaidi. Hapa chini ni orodha ya Nchi zenye furaha kwa mujibu wa World Happiness Report 2025, kuonyesha kumi bora na zilizoshika mkia. Kwa Afrika Mauritius inaongoza, wakati Lebanon , Sierra Leone na Afghanistan ni Nchi tatu za mwisho Duniani.

    1. Finland
    2. Denmark
    3. Iceland
    4. Sweden
    5. Uholanzi

    6. Costa Rica
    7. Norway
    8. Israel
    9. Luxemborg
    10.Mexico

    78. Mauritius
    79. Libya
    84. Algeria
    115. Kenya
    116. Uganda

    122. Somalia
    136. Tanzania
    145. Lebanon
    146. Sierra Leone
    147. Afghanistan

    World Happiness Report 2025 imetangaza orodha ya Nchi zenye furaha zaidi Duniani huku Nchi ya Finland 🇫🇮 ikiendelea kushika nafasi ya kwanza kwa mwaka wa nane (8) mfululizo, Tanzania imeshika nafasi ya 136 kati ya Nchi 147, ikishuka kwa nafasi tano kutoka nafasi ya 131 mwaka uliopita. Nafasi ya sasa inaiweka Nchi hiyo kuwa miongoni mwa Nchi 11 za mwisho Duniani kwa viwango vya furaha. Cha kushangaza ni kwamba Tanzania 🇹🇿, licha ya kuwa na amani na utajiri mkubwa wa maliasili, imepitwa hata na mataifa yenye migogoro kama Somalia 🇸🇴. Nchi jirani kama Kenya 🇰🇪 na Uganda 🇺🇬, ambazo mara kwa mara hukumbwa na changamoto za kisiasa na kiusalama, zimepata nafasi za juu zaidi. Hapa chini ni orodha ya Nchi zenye furaha kwa mujibu wa World Happiness Report 2025, kuonyesha kumi bora na zilizoshika mkia. Kwa Afrika Mauritius 🇲🇷 inaongoza, wakati Lebanon 🇱🇧, Sierra Leone 🇸🇱na Afghanistan 🇦🇫 ni Nchi tatu za mwisho Duniani. 1. Finland 🇫🇮 2. Denmark 🇩🇰 3. Iceland 🇮🇸 4. Sweden 🇸🇪 5. Uholanzi 🇳🇱 6. Costa Rica 🇨🇷 7. Norway 🇳🇴 8. Israel 🇮🇱 9. Luxemborg 🇱🇺 10.Mexico 🇲🇽 78. Mauritius 🇲🇷 79. Libya 🇱🇾 84. Algeria 🇩🇿 115. Kenya 🇰🇪 116. Uganda 🇺🇬 122. Somalia 🇸🇴 136. Tanzania 🇹🇿 145. Lebanon 🇱🇧 146. Sierra Leone 🇸🇱 147. Afghanistan 🇦🇫
    0 Comments ·0 Shares ·249 Views
  • Adhabu ya Raia kutoka Nchini Kenya ambaye alikuwa anyongwe mpaka kifo baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya cocaine Nchini Vietnam imepunguzwa baada ya jitihada nyingi za Viongozi wa Kenya kuomba sana kwa Serikali hiyo impunguzie adhabu ya Magreth Nduta.

    Kwa sasa adhabu ya Magret Nduta imesogezwa mpaka mwezi June ili kuona kama Vietnam watakubali Magreth kurudishwa ili aje apewe kifungo na nchi yake ya Kenya .

    Ikumbukwe kuwa Vietnam ni moja ya Nchi yenye misimamo mikali sana kuhusu Wauzaji na Wasambazaji wa madawa ya kulevya ambapo adhabu yake ni kufa.

    Adhabu ya Raia kutoka Nchini Kenya 🇰🇪 ambaye alikuwa anyongwe mpaka kifo baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya cocaine Nchini Vietnam 🇻🇳 imepunguzwa baada ya jitihada nyingi za Viongozi wa Kenya 🇰🇪 kuomba sana kwa Serikali hiyo impunguzie adhabu ya Magreth Nduta. Kwa sasa adhabu ya Magret Nduta imesogezwa mpaka mwezi June ili kuona kama Vietnam 🇻🇳 watakubali Magreth kurudishwa ili aje apewe kifungo na nchi yake ya Kenya 🇰🇪. Ikumbukwe kuwa Vietnam 🇻🇳 ni moja ya Nchi yenye misimamo mikali sana kuhusu Wauzaji na Wasambazaji wa madawa ya kulevya ambapo adhabu yake ni kufa.
    0 Comments ·0 Shares ·146 Views
  • Margaret Nduta Macharia (37) ambaye ni Raia wa Kenya aliyekamatwa mwaka 2023 Nchini Vietnam na kilogramu mbili (2) za dawa za kulevya aina ya Cocaine, anatarajiwa kunyongwa hadi kufa kesho Jumatatu Machi 17, 2025.

    Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Nation, Margaret aliyepewa hukumu hiyo Machi 6, 2025 alisema alipewa mzigo huo wa dawa za kulevya na Mwanaume mmoja kutoka Nchini Kenya aliyemtaja kwa jina moja la John. Pia, taarifa hiyo inaeleza kuwa alifanikiwa kupita katika Viwanja vitatu (3) vya Ndege bila kukamatwa, kabla ya kugundulika Nchini Vietnam. Viwanja hivyo ni pamoja na Jomo Kenyatta (Kenya), Bole (Ethiopia) na Hamad (Qatar).

    Hata hivyo, Margaret akijitetea Mahakamani Nchini Vietnam alidai hakufahamu kama mzigo ule ulikuwa ni dawa za kulevya. Taarifa kutoka Nchini Vietnam, Margaret atakula chakula chake cha mwisho kesho saa 1:30 usiku na kisha kunyongwa saa 2:30 za usiku.

    Margaret Nduta Macharia (37) ambaye ni Raia wa Kenya 🇰🇪 aliyekamatwa mwaka 2023 Nchini Vietnam 🇻🇳 na kilogramu mbili (2) za dawa za kulevya aina ya Cocaine, anatarajiwa kunyongwa hadi kufa kesho Jumatatu Machi 17, 2025. Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Nation, Margaret aliyepewa hukumu hiyo Machi 6, 2025 alisema alipewa mzigo huo wa dawa za kulevya na Mwanaume mmoja kutoka Nchini Kenya aliyemtaja kwa jina moja la John. Pia, taarifa hiyo inaeleza kuwa alifanikiwa kupita katika Viwanja vitatu (3) vya Ndege bila kukamatwa, kabla ya kugundulika Nchini Vietnam. Viwanja hivyo ni pamoja na Jomo Kenyatta (Kenya), Bole (Ethiopia) na Hamad (Qatar). Hata hivyo, Margaret akijitetea Mahakamani Nchini Vietnam alidai hakufahamu kama mzigo ule ulikuwa ni dawa za kulevya. Taarifa kutoka Nchini Vietnam, Margaret atakula chakula chake cha mwisho kesho saa 1:30 usiku na kisha kunyongwa saa 2:30 za usiku.
    0 Comments ·0 Shares ·143 Views
  • Jeshi la Polisi katika Kaunti ya Uasin Gishu Nchini Kenya wameanzisha uchunguzi baada ya Mwanamume mmoja kuanzisha kituo kidogo cha Polisi kinyume cha sheria na bila idhini ya mamlaka Nchini humo. Ripoti zinasema kuwa Mwanaume huyo wa Kijiji cha Asis alijipa jukumu la kufungua kituo hicho na kupaka rangi rasmi za Jeshi la Polisi

    Mamlaka bado hazijabaini sababu za Mshukiwa kuanzisha kituo hicho na amekamatwa kwa uchunguzi zaidi huku Wananchi wa eneo hilo wakishindwa kubaini kuwa kituo hicho kilikuwa "feki" badala yake waliendelea kupatiwa huduma wakidhani kuwa Jeshi la Polisi limesogezea huduma hiyo karibu ili kulinda usalama wa eneo hilo.

    Jeshi la Polisi katika Kaunti ya Uasin Gishu Nchini Kenya 🇰🇪 wameanzisha uchunguzi baada ya Mwanamume mmoja kuanzisha kituo kidogo cha Polisi kinyume cha sheria na bila idhini ya mamlaka Nchini humo. Ripoti zinasema kuwa Mwanaume huyo wa Kijiji cha Asis alijipa jukumu la kufungua kituo hicho na kupaka rangi rasmi za Jeshi la Polisi Mamlaka bado hazijabaini sababu za Mshukiwa kuanzisha kituo hicho na amekamatwa kwa uchunguzi zaidi huku Wananchi wa eneo hilo wakishindwa kubaini kuwa kituo hicho kilikuwa "feki" badala yake waliendelea kupatiwa huduma wakidhani kuwa Jeshi la Polisi limesogezea huduma hiyo karibu ili kulinda usalama wa eneo hilo.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·285 Views
  • Nikueleze kwa kifupi sana kiini cha mgogoro. Kabla ya mwaka 1991 Ukraine ilikua sehemu ya Urusi kupitia muungano wa kisovieti wa USSR. Baada ya USSR kufa ndipo taifa la Ukraine likazaliwa pamoja na mataifa mengine 14 yaliyokua majimbo ya Urusi.

    Lakini usisahau mwaka 1949 umoja wa kujihami wa nchi za magharibi (NATO) ulianzishwa dhidi ya Urusi (USSR). Makubaliano yao ni kwamba ikiwa Urusi itamgusa mmoja wao basi wote watamvamia. Marekani akiwa kinara.

    Kuanguka kwa USSR kukafanya mataifa 15 mapya kuzaliwa. Baadhi ya Mataifa hayo yakawa na hofu kuwa Urusi inaweza kurudi kuyakalia kimabavu. Kwahiyo yakaomba kujiunga NATO kwa usalama wao. Estonia, Latvia na Lithuania zikapata uanachana wa NATO chap kwa haraka. Ukraine ilipoomba uanachama Urusi ikakataa, kwa sababu ya strategic position ya Ukraine ambayo inaiweka Urusi hatarini.

    Ukraine ilipokosa uanachama NATO ikamua kujilinda kwa kusuka mpango wa nyuklia. Marekani na Urusi zikashtuka. Kwa kutambua hatari ya nyuklia zikamsihi sana Ukraine aachane na mpango huo. Mwaka 1994 ukaandaliwa mkataba uitwao Budapest memorundum, huko Hungary. Mkataba huo ulihusisha nchi 4. Urusi na Ukraine zilisaini kwamba hakuna atakayemvamia mwenzake. Marekani na Uingereza zikasaini kwamba atakayemvamia mwenzake watampiga bila huruma. Pia Marekani na Uingereza zitagharamia fedha na vifaa vyote vya vita. Mkataba ukasainiwa na Ukraine ikasitisha mpango wake wa nyuklia.

    Lakini Mwaka 2014 Urusi ikaivamia Ukraine na kuchukua jimbo lake la Crimea kimabavu. Marekani na Uingereza hazikuipiga Urusi kama mkataba wa Budapest unavyosema. Ukraine akalalamika lakini akapuuzwa. Kwenye vita inayoendelea sasa, Urusi ameshajitwalia majimbo manne Donetsk, Luhansk, Zaporizhzhia na Kherson lakini Marekani na Uingereza ziko kimya.

    Ukraine inaona imesalitiwa. Mkataba wa Budapest ulikua kiini macho. Laiti Ukraine ingekataa kusaini na kuendelea na mpango wake wa nyuklia, leo Urusi isingethubutu kuigusa. Lakini Waliomdanganya sasa wamemgeuka na wanamfokea. Ukraine ingeyajua maneno ya Mzee Jomo Kenyatta "Learn to fight your own battle" isingeachana na mpango wake wa nyuklia mwaka 1994. Wangejifunza kupigana vita yao wenyewe bila kutegemea mtu.!
    (Malisa GJ)

    Nikueleze kwa kifupi sana kiini cha mgogoro. Kabla ya mwaka 1991 Ukraine ilikua sehemu ya Urusi kupitia muungano wa kisovieti wa USSR. Baada ya USSR kufa ndipo taifa la Ukraine likazaliwa pamoja na mataifa mengine 14 yaliyokua majimbo ya Urusi. Lakini usisahau mwaka 1949 umoja wa kujihami wa nchi za magharibi (NATO) ulianzishwa dhidi ya Urusi (USSR). Makubaliano yao ni kwamba ikiwa Urusi itamgusa mmoja wao basi wote watamvamia. Marekani akiwa kinara. Kuanguka kwa USSR kukafanya mataifa 15 mapya kuzaliwa. Baadhi ya Mataifa hayo yakawa na hofu kuwa Urusi inaweza kurudi kuyakalia kimabavu. Kwahiyo yakaomba kujiunga NATO kwa usalama wao. Estonia, Latvia na Lithuania zikapata uanachana wa NATO chap kwa haraka. Ukraine ilipoomba uanachama Urusi ikakataa, kwa sababu ya strategic position ya Ukraine ambayo inaiweka Urusi hatarini. Ukraine ilipokosa uanachama NATO ikamua kujilinda kwa kusuka mpango wa nyuklia. Marekani na Urusi zikashtuka. Kwa kutambua hatari ya nyuklia zikamsihi sana Ukraine aachane na mpango huo. Mwaka 1994 ukaandaliwa mkataba uitwao Budapest memorundum, huko Hungary. Mkataba huo ulihusisha nchi 4. Urusi na Ukraine zilisaini kwamba hakuna atakayemvamia mwenzake. Marekani na Uingereza zikasaini kwamba atakayemvamia mwenzake watampiga bila huruma. Pia Marekani na Uingereza zitagharamia fedha na vifaa vyote vya vita. Mkataba ukasainiwa na Ukraine ikasitisha mpango wake wa nyuklia. Lakini Mwaka 2014 Urusi ikaivamia Ukraine na kuchukua jimbo lake la Crimea kimabavu. Marekani na Uingereza hazikuipiga Urusi kama mkataba wa Budapest unavyosema. Ukraine akalalamika lakini akapuuzwa. Kwenye vita inayoendelea sasa, Urusi ameshajitwalia majimbo manne Donetsk, Luhansk, Zaporizhzhia na Kherson lakini Marekani na Uingereza ziko kimya. Ukraine inaona imesalitiwa. Mkataba wa Budapest ulikua kiini macho. Laiti Ukraine ingekataa kusaini na kuendelea na mpango wake wa nyuklia, leo Urusi isingethubutu kuigusa. Lakini Waliomdanganya sasa wamemgeuka na wanamfokea. Ukraine ingeyajua maneno ya Mzee Jomo Kenyatta "Learn to fight your own battle" isingeachana na mpango wake wa nyuklia mwaka 1994. Wangejifunza kupigana vita yao wenyewe bila kutegemea mtu.! (Malisa GJ)
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·568 Views
  • Zambia wana Laptop zao zinaitwa NEO, Rwanda wana MARA Phones na Satelite , Uganda wana Simu zao zinaitwa SIMI, Kenya wana Laptop zao zinaitwa TAIFA Wana Starlink pia wana Satelite yao, Tanzania tuna nini ?
    Zambia wana Laptop zao zinaitwa NEO, Rwanda wana MARA Phones na Satelite , Uganda wana Simu zao zinaitwa SIMI, Kenya wana Laptop zao zinaitwa TAIFA Wana Starlink pia wana Satelite yao, Tanzania tuna nini ?
    Like
    Wow
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·533 Views
  • MASHEMEJI DERBY - KENYA.
    MASHEMEJI DERBY - KENYA.
    Like
    Love
    5
    · 0 Comments ·0 Shares ·288 Views
  • Mkojo wa Sungura wageuka dhahabu Nchini Kenya.

    Kumekukuwa na wimbi kubwa la mahitaji ya mkojo wa Sungura Nchini Kenya huku lita moja (1) ikiuzwa kwa Shilingi elfu moja (1,000) ambazo ni takribani Shilingi 19,885 za Kitanzania hali ambayo imepelekea Wakulima wengi kuvutiwa zaidi kuwekeza katika ufugaji wa Wanyama hao.

    Sanjari na kitoweo cha Sungura kuuzwa kwa kati ya Shilingi elfu moja (1,000) na elfu elfu mbili (2,000) za Kenya (39,790 Tsh) kwa kilo, Wakulima sasa wanapata faida kutokana na mkojo wa Mnyama huyo, ambao hutumika kama mbolea ya asili na dawa ya kuua Wadudu wanaoshambulia mimea.

    Mkojo wa Sungura wageuka dhahabu Nchini Kenya. Kumekukuwa na wimbi kubwa la mahitaji ya mkojo wa Sungura Nchini Kenya 🇰🇪 huku lita moja (1) ikiuzwa kwa Shilingi elfu moja (1,000) ambazo ni takribani Shilingi 19,885 za Kitanzania hali ambayo imepelekea Wakulima wengi kuvutiwa zaidi kuwekeza katika ufugaji wa Wanyama hao. Sanjari na kitoweo cha Sungura kuuzwa kwa kati ya Shilingi elfu moja (1,000) na elfu elfu mbili (2,000) za Kenya (39,790 Tsh) kwa kilo, Wakulima sasa wanapata faida kutokana na mkojo wa Mnyama huyo, ambao hutumika kama mbolea ya asili na dawa ya kuua Wadudu wanaoshambulia mimea.
    0 Comments ·0 Shares ·322 Views
  • #PART5

    Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite.

    Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo.

    Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba.

    Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay.

    April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha.

    March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa.

    Kumekua na jitihada mbalimbali za kumaliza mgogoro wa DRC kwa njia za kidiplomasia ikiwemo mkutano wa viongozi wakuu wa SADC na EAC uliofanyika leo jijini Dar.

    #MyaTake:
    1. Congo imeponzwa na ukarimu wake. Wakati wa vita vya Rwanda, Congo ilipokea Watutsi wengi na kuwapa hifadhi, akiwemo Kagame. Baada ya utawala wa Habyarimana kuangushwa Wahutu nao wakakimbilia Congo na kupewa hifadhi. Sasa hicho kimekua kigezo cha Rwanda kuingiza majeshi Congo kila mara kwa madai ya kuwatafuta Wahutu wa FDLR. Kwa lugha rahisi vita ya ndugu wawili (Wahutu na Watutsi) iliyopaswa kupiganwa Rwanda sasa inapiganwa Congo.

    2. Congo inateswa na mipaka ya kikoloni. Laiti wakati wa kuchora mipaka jamii yote ya Watutsi ingewekwa Rwanda, leo kusingekuwa na Banyamulenge Congo, kwahiyo Watutsi wasingepata sababu ya kuishi Congo na kujifanya raia. Ni sawa na kukuta Wamasai 1,000 pale Longido, halafu uambiwe kati yao wapo wa Kenya. Utawajuaje? Utawatofautishaje?

    3. Congo inateswa na rasilimali zake. Kama eneo la Kivu lisingekuwa na utajiri, mgogoro usingekuwa mkubwa kama ulivyo. Rejea #Part1 kujua utajiri uliopo Kivu. Kumbuka bila Kivu dunia haina laptop wala smartphones kwa sababu 80% ya coltan yote duniani inatoka Kivu.

    4. Rwanda na Uganda ni Keyplayers kwenye mgogoro wa Congo. Kwa miaka mingi majeshi yao yameigeuza Congo shamba la bibi. Waondoe majeshi yao Congo.

    5. Viongozi wengi wa M23 ni Wanyarwanda. Huu ni udhibitisho kuwa Rwanda ni kinara kwenye mgogoro huu.

    6. Congo ni kubwa sana na hivyo inakosa jeshi imara la kutosha kulinda mipaka yake yote. Congo ni kubwa mara 90 ya Rwanda. Wapo wanaoshauri igawanywe kama njia ya kutatua mgogoro. Kama ambavyo Yugoslavia iligawanywa na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.

    7. Kiongozi wa sasa wa M23 Corneille Nangaa alikua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi 2019 na ndiye aliyemtangaza Tshisekedi kuwa Rais kwa ushindi wa 38%. Lakini alilaumiwa kupunguza kura za Martin Fayulu aliyepata 34%. Huenda kuna ahadi alipewa haikutimizwa ndio maana akaungana na Waasi.

    Sababu hizo hapo juu zikifanyiwa kazi, mgogoro wa Congo unaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Mnaopenda kujifunza zaidi, naandika Kitabu. Get ready to have your copy. MWISHO.!

    (Malisa GJ )

    #PART5 Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite. Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo. Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba. Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay. April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha. March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa. Kumekua na jitihada mbalimbali za kumaliza mgogoro wa DRC kwa njia za kidiplomasia ikiwemo mkutano wa viongozi wakuu wa SADC na EAC uliofanyika leo jijini Dar. #MyaTake: 1. Congo imeponzwa na ukarimu wake. Wakati wa vita vya Rwanda, Congo ilipokea Watutsi wengi na kuwapa hifadhi, akiwemo Kagame. Baada ya utawala wa Habyarimana kuangushwa Wahutu nao wakakimbilia Congo na kupewa hifadhi. Sasa hicho kimekua kigezo cha Rwanda kuingiza majeshi Congo kila mara kwa madai ya kuwatafuta Wahutu wa FDLR. Kwa lugha rahisi vita ya ndugu wawili (Wahutu na Watutsi) iliyopaswa kupiganwa Rwanda sasa inapiganwa Congo. 2. Congo inateswa na mipaka ya kikoloni. Laiti wakati wa kuchora mipaka jamii yote ya Watutsi ingewekwa Rwanda, leo kusingekuwa na Banyamulenge Congo, kwahiyo Watutsi wasingepata sababu ya kuishi Congo na kujifanya raia. Ni sawa na kukuta Wamasai 1,000 pale Longido, halafu uambiwe kati yao wapo wa Kenya. Utawajuaje? Utawatofautishaje? 3. Congo inateswa na rasilimali zake. Kama eneo la Kivu lisingekuwa na utajiri, mgogoro usingekuwa mkubwa kama ulivyo. Rejea #Part1 kujua utajiri uliopo Kivu. Kumbuka bila Kivu dunia haina laptop wala smartphones kwa sababu 80% ya coltan yote duniani inatoka Kivu. 4. Rwanda na Uganda ni Keyplayers kwenye mgogoro wa Congo. Kwa miaka mingi majeshi yao yameigeuza Congo shamba la bibi. Waondoe majeshi yao Congo. 5. Viongozi wengi wa M23 ni Wanyarwanda. Huu ni udhibitisho kuwa Rwanda ni kinara kwenye mgogoro huu. 6. Congo ni kubwa sana na hivyo inakosa jeshi imara la kutosha kulinda mipaka yake yote. Congo ni kubwa mara 90 ya Rwanda. Wapo wanaoshauri igawanywe kama njia ya kutatua mgogoro. Kama ambavyo Yugoslavia iligawanywa na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe. 7. Kiongozi wa sasa wa M23 Corneille Nangaa alikua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi 2019 na ndiye aliyemtangaza Tshisekedi kuwa Rais kwa ushindi wa 38%. Lakini alilaumiwa kupunguza kura za Martin Fayulu aliyepata 34%. Huenda kuna ahadi alipewa haikutimizwa ndio maana akaungana na Waasi. Sababu hizo hapo juu zikifanyiwa kazi, mgogoro wa Congo unaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Mnaopenda kujifunza zaidi, naandika Kitabu. Get ready to have your copy. MWISHO.! (Malisa GJ ✍️)
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·1K Views
  • Chukua hii.

    Kama utakwenda Nchini Japan na kusikia neno "Johatsu" (じょうはつ) tambua kuwa ni Mtu au Watu waliotoweka (kupotea) kutoka kwenye familia zao kutokana na sababu mbalimbali kama vile migogoro kwenye Ndoa, kushindwa kuoa, kukimbia madeni, kufukuzwa kazi na kadhalika. Watu hao huacha maisha yao na kuishi bila kujulikana wapi walipo kwa muda fulani na inaweze kuwa ni ndani ya Nchi ya Japan au nje Nchi yaani mataifa mengine kama vile Tanzania DR Congo , Burundi , Marekani , Mexico , Kenya ,....

    Pamoja na Watu hao kupotea, lakini wanasaidiwa na Makampuni ambayo yamebobea katika kazi hiyo yaani Watu au Mtu anayehitaji huduma hiyo unalipia kisha kuhamishwa usiku. Makampuni hayo maalumu yanajulikana kwa jina la "Wahamishaji Usiku" huwasaidia Watu kupotea (unaweza kusema kujiteka, kujipoteza,...).

    Haya Mashirika au Makampuni husaidia Watu kutoweka kwa kuwahamisha kwa siri sana na mara nyingi kazi hii hufanyika usiku na wanapokupeleka inakuwa ni siri kubwa yaani kuanzia mahali pa kulala, utakula nini, vitambulisho vipya vya kusafiria Kampuni hizo ndizo zinafanya kila kitu kwa mujibu wa mkataba wenu.

    Pia Kampuni hizi zitahakikisha zinasafisha kumbukumbu zote za Mteja na kusahaulika kwenye Jamii, Nyumbani na Nchi kwa ujumla kisha unaanza mwanzo mpya wa kuanzisha maisha mengine kwenye Nchi au mahali walipo kupeleka.

    Chukua hii. Kama utakwenda Nchini Japan 🇯🇵 na kusikia neno "Johatsu" (じょうはつ) tambua kuwa ni Mtu au Watu waliotoweka (kupotea) kutoka kwenye familia zao kutokana na sababu mbalimbali kama vile migogoro kwenye Ndoa, kushindwa kuoa, kukimbia madeni, kufukuzwa kazi na kadhalika. Watu hao huacha maisha yao na kuishi bila kujulikana wapi walipo kwa muda fulani na inaweze kuwa ni ndani ya Nchi ya Japan au nje Nchi yaani mataifa mengine kama vile Tanzania 🇨🇩 DR Congo 🇨🇩, Burundi 🇧🇮, Marekani 🇺🇸, Mexico 🇲🇽, Kenya 🇰🇪,.... Pamoja na Watu hao kupotea, lakini wanasaidiwa na Makampuni ambayo yamebobea katika kazi hiyo yaani Watu au Mtu anayehitaji huduma hiyo unalipia kisha kuhamishwa usiku. Makampuni hayo maalumu yanajulikana kwa jina la "Wahamishaji Usiku" huwasaidia Watu kupotea (unaweza kusema kujiteka, kujipoteza,...). Haya Mashirika au Makampuni husaidia Watu kutoweka kwa kuwahamisha kwa siri sana na mara nyingi kazi hii hufanyika usiku na wanapokupeleka inakuwa ni siri kubwa yaani kuanzia mahali pa kulala, utakula nini, vitambulisho vipya vya kusafiria Kampuni hizo ndizo zinafanya kila kitu kwa mujibu wa mkataba wenu. Pia Kampuni hizi zitahakikisha zinasafisha kumbukumbu zote za Mteja na kusahaulika kwenye Jamii, Nyumbani na Nchi kwa ujumla kisha unaanza mwanzo mpya wa kuanzisha maisha mengine kwenye Nchi au mahali walipo kupeleka.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·517 Views
  • Nchi ya Kenya imetuma Askari wengine 144 Nchini Haïti, kwa ajili ya kulinda amani na kurejesha utulivu Nchini humo ambao imepotea kwa miaka kadhaa sasa. Askari hao, ambao ni Wanaume 120 na Wanawake 24, wameelekea Haiti asubuhi ya Februari 6, 2025 baada ya kuagwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Kipchumba Murkomen.

    Idadi ya Askari hao kutoka Nchini Kenya inafikisha jumla ya Askari Polisi 744 waliotumwa Nchini Haiti kwa ajili ya kupambana na magenge ya kihalifu yaliyokithiri Nchini humo pamoja na uvunjwaji wa amani.

    Nchi ya Kenya 🇰🇪 imetuma Askari wengine 144 Nchini Haïti🇭🇹, kwa ajili ya kulinda amani na kurejesha utulivu Nchini humo ambao imepotea kwa miaka kadhaa sasa. Askari hao, ambao ni Wanaume 120 na Wanawake 24, wameelekea Haiti asubuhi ya Februari 6, 2025 baada ya kuagwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Kipchumba Murkomen. Idadi ya Askari hao kutoka Nchini Kenya inafikisha jumla ya Askari Polisi 744 waliotumwa Nchini Haiti kwa ajili ya kupambana na magenge ya kihalifu yaliyokithiri Nchini humo pamoja na uvunjwaji wa amani.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·337 Views
  • Rais Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , Felix Tshisekedi na Paul Kagame wa Rwanda, wanatarajia kukutana Jijini Dar es Salaam, Tanzania, Februari 8, 2025 kujadili mustakabali wa hali ya usalama inayoendelea eneo la Mashariki mwa DR Congo.

    Taarifa iliyotolewa na Rais wa Kenya, William Ruto, wawili hao watakutana katika mkutano wa pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), baada ya Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kuridhia Nchi yake ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo.

    Rais Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩, Felix Tshisekedi na Paul Kagame wa Rwanda, wanatarajia kukutana Jijini Dar es Salaam, Tanzania, Februari 8, 2025 kujadili mustakabali wa hali ya usalama inayoendelea eneo la Mashariki mwa DR Congo. Taarifa iliyotolewa na Rais wa Kenya, William Ruto, wawili hao watakutana katika mkutano wa pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), baada ya Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kuridhia Nchi yake ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo.
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·435 Views
  • #PART2

    Baada ya mipaka ya Wakoloni walioangukia Rwanda na Burundi waliendelea kujiita Watutsi, lakini walioangukia Congo hawakujiita Watutsi, kwa sababu ya kukwepa ubaguzi. Ili wasitengwe wakajitambulisha kwa eneo wanalotoka, safu za Milima ya Mulenge. Kwahiyo wakajiita Banyamulenge, yani watu kutoka Mulenge. Lakini ukweli ni Watutsi, wametengwa na wenzao kwa mipaka ya wakoloni.

    Ni sawa na wamassai wa Tanzania na wale wa Kenya. Ni jamii moja ila wametengwa na mipaka ya Wakoloni. Huku Tanzania Wamasai ni wengi kuliko Kenya, lakini serikali ya Kenya haiwezi kuwafukuza wa Kenya waje Tanzania. Itakua dhambi ya ubaguzi. Mipaka ilipowekwa waliojikuta Kenya wakawa raia wa Kenya hivyo, hali kadhalika waliojikuta Tanzania.

    Watutsi wa Congo pamoja na kujiita Banyamulenge, bado wakikumbana na ubaguzi. Hawakupata ushirikiano kutoka kwa jamii nyingine za Kivu. Kwahiyo wakajikuta wameongeza "bond" na Watutsi wa Rwanda. Kukawa na mwingiliano mkubwa kati ya Watutsi wa Rwanda na wale wa Congo (Banyamulenge).

    Mwaka 1959, mfalme wa mwisho wa Rwanda, Mutara III, aliuawa kwa sumu. Baada ya kifo chake, Rwanda iliingia katika machafuko ambapo Wahutu waliokuwa zaidi ya 80% waliwashambulia Watutsi, wakiwatuhumu kupendelewa na Wakoloni wa Kibelgiji. Maelfu ya Watutsi walikimbilia Kivu kwa ajili ya usalama wao. Walipofika huko, waliungana na wenzao (Banyamulenge), idadi ikaongezeka.

    Mwaka 1962, Rwanda ilipata uhuru, na Gregoire Kayibanda akawa Rais. Kwa mara ya kwanza, Wahutu walishika madaraka baada ya utawala wa kifalme wa Watutsi kwa miaka mingi. Kayibanda alikakandamiza Watutsi na kupendelea Wahutu wenzake. Watutsi wengi walikimbilia uhamishoni, hasa maeneo ya Kivu. Wakaenda kuungana na wenzao (Banyamulenge).

    Mwaka 1973, Kayibanda alipinduliwa na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Juvénal Habyarimana, ambaye alijiapiza kuwatokomeza Watutsi. Kwa miaka 21 ya utawala wake, Watutsi waliteswa vikali. Waliondolewa kwenye nafasi za kijeshi, mashirika ya umma, na siasa. Wengi walifungwa gerezani au kuuawa. Hali hii iliwafanya Watutsi wengi zaidi kukimbia Rwanda na kuelekea maeneo mbalimbali ikiwemo Kivu. Walioenda Kivu wakaenda kuongeza idadi ya Banyamulenge.!
    (Malisa GJ)

    #PART2 Baada ya mipaka ya Wakoloni walioangukia Rwanda na Burundi waliendelea kujiita Watutsi, lakini walioangukia Congo hawakujiita Watutsi, kwa sababu ya kukwepa ubaguzi. Ili wasitengwe wakajitambulisha kwa eneo wanalotoka, safu za Milima ya Mulenge. Kwahiyo wakajiita Banyamulenge, yani watu kutoka Mulenge. Lakini ukweli ni Watutsi, wametengwa na wenzao kwa mipaka ya wakoloni. Ni sawa na wamassai wa Tanzania na wale wa Kenya. Ni jamii moja ila wametengwa na mipaka ya Wakoloni. Huku Tanzania Wamasai ni wengi kuliko Kenya, lakini serikali ya Kenya haiwezi kuwafukuza wa Kenya waje Tanzania. Itakua dhambi ya ubaguzi. Mipaka ilipowekwa waliojikuta Kenya wakawa raia wa Kenya hivyo, hali kadhalika waliojikuta Tanzania. Watutsi wa Congo pamoja na kujiita Banyamulenge, bado wakikumbana na ubaguzi. Hawakupata ushirikiano kutoka kwa jamii nyingine za Kivu. Kwahiyo wakajikuta wameongeza "bond" na Watutsi wa Rwanda. Kukawa na mwingiliano mkubwa kati ya Watutsi wa Rwanda na wale wa Congo (Banyamulenge). Mwaka 1959, mfalme wa mwisho wa Rwanda, Mutara III, aliuawa kwa sumu. Baada ya kifo chake, Rwanda iliingia katika machafuko ambapo Wahutu waliokuwa zaidi ya 80% waliwashambulia Watutsi, wakiwatuhumu kupendelewa na Wakoloni wa Kibelgiji. Maelfu ya Watutsi walikimbilia Kivu kwa ajili ya usalama wao. Walipofika huko, waliungana na wenzao (Banyamulenge), idadi ikaongezeka. Mwaka 1962, Rwanda ilipata uhuru, na Gregoire Kayibanda akawa Rais. Kwa mara ya kwanza, Wahutu walishika madaraka baada ya utawala wa kifalme wa Watutsi kwa miaka mingi. Kayibanda alikakandamiza Watutsi na kupendelea Wahutu wenzake. Watutsi wengi walikimbilia uhamishoni, hasa maeneo ya Kivu. Wakaenda kuungana na wenzao (Banyamulenge). Mwaka 1973, Kayibanda alipinduliwa na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Juvénal Habyarimana, ambaye alijiapiza kuwatokomeza Watutsi. Kwa miaka 21 ya utawala wake, Watutsi waliteswa vikali. Waliondolewa kwenye nafasi za kijeshi, mashirika ya umma, na siasa. Wengi walifungwa gerezani au kuuawa. Hali hii iliwafanya Watutsi wengi zaidi kukimbia Rwanda na kuelekea maeneo mbalimbali ikiwemo Kivu. Walioenda Kivu wakaenda kuongeza idadi ya Banyamulenge.! (Malisa GJ)
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·696 Views
  • DRC SAGA - PART 1

    (TAHADHARI: kama wwe ni mpenzi wa udaku au story fupifupi usisome. Hii ni kwa ajili ya watu wenye "solid mind" na wanaopenda kujifunza).
    ______
    Mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umebeba historia ndefu inayohitaji muda mrefu kuielezea, lakini nitajaribu kuifupisha kwa kuangazia mambo machache muhimu.

    Mpelelezi wa Kiingereza, John Speke, katika kitabu chake Journal of the Discovery of the Source of the Nile (1863), aliandika kuwa asili ya Watutsi ni Pembe ya Afrika (Ethiopia, Somalia, Djibouti), na kwamba walihama katika karne ya 12 wakielekea eneo la Maziwa Makuu. Walifanya makazi yao katika maeneo ya kaskazini-magharibi mwa Ziwa Tanganyika, eneo ambalo kwa sasa ni Rwanda, Burundi, na Congo. Walipowasili, walikuta wenyeji ambao Wahutu na Watwa, ambao waliishi nao kwa amani. Wahutu na Watwa walikuwa wakulima, huku Watutsi wakiwa wafugaji.

    Karne ya 18, wakoloni walipofika, waligawa maeneo ya kiutawala bila kuzingatia mipaka ya kijamii iliyokuwepo. Badala yake, walizingatia maslahi yao binafsi, jambo lililosababisha baadhi ya jamii kugawanyika katika mataifa mawili tofauti. Kwa mfano, jamii ya Wamasai iligawanywa kati ya Kenya na Tanganyika. Wahutu waligawanyika kati ya Rwanda na Burundi, huku Watutsi wakigawanyika Rwanda, Burundi na Congo maeneo ya Kivu kusini.

    Watutsi pamoja na kuwa wachache kwa idadi lakini walijikuta wameathirika zaidi kwa kugawanyika maeneo mengi. Waligawanyika katika mataifa matatu tofauti ingawa walikuwa watu wa jamii moja, walioongea lugha moja, wenye mila na desturi zinazofanana.

    Baada ya mipaka kuwekwa Watutsi waliojikuta katika eneo la Kivu (Congo) walitengwa na jamii nyingine za watu wa eneo hilo kama Wabembe, Wavira, na Wanyindu. Kwa kuwa sehemu kubwa ya Watutsi ilikua Rwanda, wale waliojikuta Congo walionekana kama wageni (externals) maana walikua 6% tu ya watu wa Kivu.

    Walishauriwa kuhamia Rwanda, lakini hawakua wanyarwanda. Ni Wakongomani waliozaliwa hapo. Babu zao walifika hapo karne ya 12 kama nilivyoeleza juu. Kabla ya ukoloni Watutsi wote walikua jamii moja. Lakini baada ya mipaka ya wakoloni wakajikuta wamegawanywa katika nchi 3 tofauti. Sasa wafanjeje?
    (Malisa GJ)

    DRC SAGA - PART 1 (TAHADHARI: kama wwe ni mpenzi wa udaku au story fupifupi usisome. Hii ni kwa ajili ya watu wenye "solid mind" na wanaopenda kujifunza). ______ Mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umebeba historia ndefu inayohitaji muda mrefu kuielezea, lakini nitajaribu kuifupisha kwa kuangazia mambo machache muhimu. Mpelelezi wa Kiingereza, John Speke, katika kitabu chake Journal of the Discovery of the Source of the Nile (1863), aliandika kuwa asili ya Watutsi ni Pembe ya Afrika (Ethiopia, Somalia, Djibouti), na kwamba walihama katika karne ya 12 wakielekea eneo la Maziwa Makuu. Walifanya makazi yao katika maeneo ya kaskazini-magharibi mwa Ziwa Tanganyika, eneo ambalo kwa sasa ni Rwanda, Burundi, na Congo. Walipowasili, walikuta wenyeji ambao Wahutu na Watwa, ambao waliishi nao kwa amani. Wahutu na Watwa walikuwa wakulima, huku Watutsi wakiwa wafugaji. Karne ya 18, wakoloni walipofika, waligawa maeneo ya kiutawala bila kuzingatia mipaka ya kijamii iliyokuwepo. Badala yake, walizingatia maslahi yao binafsi, jambo lililosababisha baadhi ya jamii kugawanyika katika mataifa mawili tofauti. Kwa mfano, jamii ya Wamasai iligawanywa kati ya Kenya na Tanganyika. Wahutu waligawanyika kati ya Rwanda na Burundi, huku Watutsi wakigawanyika Rwanda, Burundi na Congo maeneo ya Kivu kusini. Watutsi pamoja na kuwa wachache kwa idadi lakini walijikuta wameathirika zaidi kwa kugawanyika maeneo mengi. Waligawanyika katika mataifa matatu tofauti ingawa walikuwa watu wa jamii moja, walioongea lugha moja, wenye mila na desturi zinazofanana. Baada ya mipaka kuwekwa Watutsi waliojikuta katika eneo la Kivu (Congo) walitengwa na jamii nyingine za watu wa eneo hilo kama Wabembe, Wavira, na Wanyindu. Kwa kuwa sehemu kubwa ya Watutsi ilikua Rwanda, wale waliojikuta Congo walionekana kama wageni (externals) maana walikua 6% tu ya watu wa Kivu. Walishauriwa kuhamia Rwanda, lakini hawakua wanyarwanda. Ni Wakongomani waliozaliwa hapo. Babu zao walifika hapo karne ya 12 kama nilivyoeleza juu. Kabla ya ukoloni Watutsi wote walikua jamii moja. Lakini baada ya mipaka ya wakoloni wakajikuta wamegawanywa katika nchi 3 tofauti. Sasa wafanjeje? (Malisa GJ)
    0 Comments ·0 Shares ·557 Views
  • Mkutano wa Kilele wa Marais wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika hivi karibuni umemtaka Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Félix Tshisekedi, kukaa meza moja na Waasi wa M23 kwa ajili ya mazungumzo ya pamoja ili kutafuta suluhu ya amani katika taifa hilo.

    Taarifa iliyotolewa na Mjumbe wa Mkutano huo, ambaye pia ni Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X (Twitter), ilieleza kuwa Viongozi hao walikutana Januari 29, chini ya Uenyekiti wa Rais wa Kenya, William Ruto, kujadili hali ya usalama Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo .

    Miongoni mwa makubaliano ya mkutano huo ni pendekezo la Rais Tshisekedi kushiriki mazungumzo na kundi la M23. Kadhalika, Viongozi hao walikubaliana kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inapaswa kuitisha mkutano wa dharura na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ili kutafuta suluhisho la kudumu kwa mgogoro huo.

    Museveni aliambatanisha taarifa hiyo na orodha ya Viongozi waliohudhuria mkutano huo, wakiwemo Rais wa Kenya William Ruto, Rais wa Somalia Hassan Mohamud, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, Rais wa Rwanda Paul Kagame, na mwenyeji wao, Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

    Mkutano wa Kilele wa Marais wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika hivi karibuni umemtaka Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Félix Tshisekedi, kukaa meza moja na Waasi wa M23 kwa ajili ya mazungumzo ya pamoja ili kutafuta suluhu ya amani katika taifa hilo. Taarifa iliyotolewa na Mjumbe wa Mkutano huo, ambaye pia ni Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X (Twitter), ilieleza kuwa Viongozi hao walikutana Januari 29, chini ya Uenyekiti wa Rais wa Kenya, William Ruto, kujadili hali ya usalama Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Miongoni mwa makubaliano ya mkutano huo ni pendekezo la Rais Tshisekedi kushiriki mazungumzo na kundi la M23. Kadhalika, Viongozi hao walikubaliana kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inapaswa kuitisha mkutano wa dharura na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ili kutafuta suluhisho la kudumu kwa mgogoro huo. Museveni aliambatanisha taarifa hiyo na orodha ya Viongozi waliohudhuria mkutano huo, wakiwemo Rais wa Kenya William Ruto, Rais wa Somalia Hassan Mohamud, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, Rais wa Rwanda Paul Kagame, na mwenyeji wao, Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·578 Views
  • Kazi ya Bando la Wananchi wa Kenya
    Kazi ya Bando la Wananchi wa Kenya 🇰🇪 😳
    Wow
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·492 Views
  • Mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Victor Boniface, anayeichezea Bayer Leverkusen ya Ujerumani, ameachana na mpenzi wake, Rikke Hermine, raia wa Norway. Wawili hao walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa miaka minne, lakini wameamua kuvunja uhusiano wao kutokana na kugundua kuwa Victor kwenye mali zake ameandika majina ya mama yake tu.

    Chanzo cha habari kinaeleza kuwa uamuzi wa Rikke kuachana na Victor ulitokana na kugundua kuwa katika mali zote za mshambuliaji huyo, majina ya mama yake mzazi pekee ndiyo yaliyoandikwa. Hali hii ilimfanya Rikke kuhisi kuwa hakuwa na nafasi ya kutosha katika maisha ya Victor, jambo lililomfanya kuchukua hatua hiyo.

    Aidha, inadaiwa kuwa Rikke alikuwa akishinikiza kufunga ndoa baada ya kuwa wapenzi kwa muda mrefu, huku Victor akiwa tayari kufunga naye ndoa lakini kwa sharti la kusaini mkataba wa awali (prenup).

    Prenup ni Mkataba wa awali kabla ya kufunga ndoa ambao unalenga kulinda mali za pande zote mbili endapo itatokea mkaachana kila mmoja anabaki na alichokuja nacho katika ndoa na sio kugawana mali, ila bibie Rikkie amekuwa mgumu kukubali hilo hivyo kuachana

    #tanzania #kenya #daressalaam #africa #zanzibar #diamondplatnumz #arusha #mwanza #dodoma #uganda #wcb #travel #life #safari #wasafi #love #millardayoupdates #mbeya #nairobi #harmonize #rwanda #eastafrica #kilimanjaro #alikiba #gainwithmchina #serengeti #wasafitv #fashion #wasafimedia #wemasepetu
    Mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Victor Boniface, anayeichezea Bayer Leverkusen ya Ujerumani, ameachana na mpenzi wake, Rikke Hermine, raia wa Norway. Wawili hao walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa miaka minne, lakini wameamua kuvunja uhusiano wao kutokana na kugundua kuwa Victor kwenye mali zake ameandika majina ya mama yake tu. Chanzo cha habari kinaeleza kuwa uamuzi wa Rikke kuachana na Victor ulitokana na kugundua kuwa katika mali zote za mshambuliaji huyo, majina ya mama yake mzazi pekee ndiyo yaliyoandikwa. Hali hii ilimfanya Rikke kuhisi kuwa hakuwa na nafasi ya kutosha katika maisha ya Victor, jambo lililomfanya kuchukua hatua hiyo. Aidha, inadaiwa kuwa Rikke alikuwa akishinikiza kufunga ndoa baada ya kuwa wapenzi kwa muda mrefu, huku Victor akiwa tayari kufunga naye ndoa lakini kwa sharti la kusaini mkataba wa awali (prenup). Prenup ni Mkataba wa awali kabla ya kufunga ndoa ambao unalenga kulinda mali za pande zote mbili endapo itatokea mkaachana kila mmoja anabaki na alichokuja nacho katika ndoa na sio kugawana mali, ila bibie Rikkie amekuwa mgumu kukubali hilo hivyo kuachana #tanzania #kenya #daressalaam #africa #zanzibar #diamondplatnumz #arusha #mwanza #dodoma #uganda #wcb #travel #life #safari #wasafi #love #millardayoupdates #mbeya #nairobi #harmonize #rwanda #eastafrica #kilimanjaro #alikiba #gainwithmchina #serengeti #wasafitv #fashion #wasafimedia #wemasepetu
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·2K Views
  • #JeWajua Msako mkali wa wahamiaji uliofanyika nchini Marekani siku ya Jumapili na kusababisha kukamatwa kwa watu 956, idadi hiyo ikiwa kubwa zaidi tangu Donald Trump arejee mamlakani, kulingana na shirika la Uhamiaji na Utekelezaji wa Forodha (ICE).

    Mashirika kadhaa ya serikali yenye mamlaka mapya ya kuwaweka kizuizini wasio na vibali yalihusika katika kamata kamata hiyo kwenye miji kadhaa ikiwa ni pamoja na Chicago, Newark na Miami. Moja ya ahadi alizotoa Donald Trump wakati wa kampeni yake, ni kuwafukuza nchi Marekani wahamiaji wasio na vibali.

    Mtangulizi wake Joe Biden aliwarejesha makwao wastani wa wahamiaji 311 kila siku, kulingana na ICE, wengi wao wakiwa watu ambao walikuwa wamefanya uhalifu. Tangu aingie madarakani, Trump ametekeleza maagizo 21 kurekebisha mfumo wa uhamiaji wa Marekani.

    Huko Miami siku ya Jumapili, vyombo vya kutekeleza sheria vya serikali vilichukua "hatua kadhaa za uhamiaji," Uchunguzi wa Usalama wa jiji hilo ulisema kwenye mitandao ya kijamii.

    #tanzania #kenya #daressalaam #africa #zanzibar #diamondplatnumz #arusha #mwanza #dodoma #uganda #wcb #travel #life #safari #wasafi #love #millardayoupdates #mbeya #nairobi #harmonize #rwanda #eastafrica #kilimanjaro #alikiba #gainwithmchina #serengeti #wasafitv #fashion #wasafimedia
    #JeWajua Msako mkali wa wahamiaji uliofanyika nchini Marekani siku ya Jumapili na kusababisha kukamatwa kwa watu 956, idadi hiyo ikiwa kubwa zaidi tangu Donald Trump arejee mamlakani, kulingana na shirika la Uhamiaji na Utekelezaji wa Forodha (ICE). Mashirika kadhaa ya serikali yenye mamlaka mapya ya kuwaweka kizuizini wasio na vibali yalihusika katika kamata kamata hiyo kwenye miji kadhaa ikiwa ni pamoja na Chicago, Newark na Miami. Moja ya ahadi alizotoa Donald Trump wakati wa kampeni yake, ni kuwafukuza nchi Marekani wahamiaji wasio na vibali. Mtangulizi wake Joe Biden aliwarejesha makwao wastani wa wahamiaji 311 kila siku, kulingana na ICE, wengi wao wakiwa watu ambao walikuwa wamefanya uhalifu. Tangu aingie madarakani, Trump ametekeleza maagizo 21 kurekebisha mfumo wa uhamiaji wa Marekani. Huko Miami siku ya Jumapili, vyombo vya kutekeleza sheria vya serikali vilichukua "hatua kadhaa za uhamiaji," Uchunguzi wa Usalama wa jiji hilo ulisema kwenye mitandao ya kijamii. #tanzania #kenya #daressalaam #africa #zanzibar #diamondplatnumz #arusha #mwanza #dodoma #uganda #wcb #travel #life #safari #wasafi #love #millardayoupdates #mbeya #nairobi #harmonize #rwanda #eastafrica #kilimanjaro #alikiba #gainwithmchina #serengeti #wasafitv #fashion #wasafimedia
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·2K Views
  • Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , Félix Tshisekedi na Rais wa Burundi , Evariste Ndayishimiye wamekataa kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioitishwa na Rais wa Kenya , William Ruto, ambao pia ulipangwa kumjumuisha Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye alishasema kuwa yupo tayari kuhudhuria mkutano huo ila kwa kusisitiza, yagusiwe kiini haswa cha ngorongoro uliopo kati ya DR Congo na Waasi.

    Aidha, Tshisekedi amesema kuwa hatoweza kuhudhuria mkutano huo kwa sababu ya ratiba.

    Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩, Félix Tshisekedi na Rais wa Burundi 🇧🇮, Evariste Ndayishimiye wamekataa kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioitishwa na Rais wa Kenya 🇰🇪, William Ruto, ambao pia ulipangwa kumjumuisha Rais wa Rwanda 🇷🇼 Paul Kagame ambaye alishasema kuwa yupo tayari kuhudhuria mkutano huo ila kwa kusisitiza, yagusiwe kiini haswa cha ngorongoro uliopo kati ya DR Congo na Waasi. Aidha, Tshisekedi amesema kuwa hatoweza kuhudhuria mkutano huo kwa sababu ya ratiba.
    0 Comments ·0 Shares ·458 Views
  • Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo linaendelea kupambana na Waasi wa M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Jeshi la Rwanda (Japo Rwanda imeshalikanusha mara nyingi tu). Raia watano pia wameripotiwa kuuawa huko Gisenyi Nchini Rwanda.

    Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais wa Kenya William Ruto, ameitisha mkutano wa Marais wa Jumuiya hiyo hapo kesho Jumatano wa kuutafutia suluhu mzozo huo wa mashariki mwa Kongo licha ya Kigali na Kinshasa kutotoa taarifa rasmi kuwa watashiriki mkutano huo.

    Umoja wa Mataifa ambao umetahadharisha kuwa mzozo huo unaweza kuzusha vita vya kikanda na umeelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya mbaya ya kibinadamu huko Goma ambako mwezi huu pekee, karibu Watu 500,000 wameyahama makazi yao.

    Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo linaendelea kupambana na Waasi wa M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Jeshi la Rwanda (Japo Rwanda imeshalikanusha mara nyingi tu). Raia watano pia wameripotiwa kuuawa huko Gisenyi Nchini Rwanda. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais wa Kenya William Ruto, ameitisha mkutano wa Marais wa Jumuiya hiyo hapo kesho Jumatano wa kuutafutia suluhu mzozo huo wa mashariki mwa Kongo licha ya Kigali na Kinshasa kutotoa taarifa rasmi kuwa watashiriki mkutano huo. Umoja wa Mataifa ambao umetahadharisha kuwa mzozo huo unaweza kuzusha vita vya kikanda na umeelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya mbaya ya kibinadamu huko Goma ambako mwezi huu pekee, karibu Watu 500,000 wameyahama makazi yao.
    0 Comments ·0 Shares ·481 Views
More Results