• Zambia wana Laptop zao zinaitwa NEO, Rwanda wana MARA Phones na Satelite , Uganda wana Simu zao zinaitwa SIMI, Kenya wana Laptop zao zinaitwa TAIFA Wana Starlink pia wana Satelite yao, Tanzania tuna nini ?
    Zambia wana Laptop zao zinaitwa NEO, Rwanda wana MARA Phones na Satelite , Uganda wana Simu zao zinaitwa SIMI, Kenya wana Laptop zao zinaitwa TAIFA Wana Starlink pia wana Satelite yao, Tanzania tuna nini ?
    Like
    Wow
    2
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·110 Views
  • MASHEMEJI DERBY - KENYA.
    MASHEMEJI DERBY - KENYA.
    Like
    Love
    5
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·88 Views
  • Read more
    Mkojo wa Sungura wageuka dhahabu Nchini Kenya. Kumekukuwa na wimbi kubwa la mahitaji ya mkojo wa Sungura Nchini Kenya 🇰🇪 huku lita moja (1) ikiuzwa kwa Shilingi elfu moja (1,000) ambazo ni takribani Shilingi 19,885 za Kitanzania hali ambayo imepelekea Wakulima wengi kuvutiwa zaidi kuwekeza katika ufugaji wa Wanyama hao. Sanjari na kitoweo cha Sungura kuuzwa kwa kati ya Shilingi elfu moja (1,000) na elfu elfu mbili (2,000) za Kenya (39,790 Tsh) kwa kilo, Wakulima sasa wanapata faida kutokana na mkojo wa Mnyama huyo, ambao hutumika kama mbolea ya asili na dawa ya kuua Wadudu wanaoshambulia mimea.
    0 Commenti ·0 condivisioni ·118 Views
  • Read more
    #PART5 Baada ya M23 kukamata Goma walidai hawana mpango wa kuchukua miji mingine. Jeshi la Congo (FARDC) likarelax. Kumbe ilikua mbinu ya kivita. Ghafla M23 wakavamia na kuuteka mji wa Rutshuru wenye utajiri wa dhahabu, tin na Tungsten na mji wa Masisi wenye utajiri mkubwa wa dhahabu na cassiterite. Mpango wa M23 ni kufika Kinshasa na kuuangusha utawala wa Rais Felix Tshisekedi. Madai ya M23 ni yaleyale ya siku zote, ambayo ni kulinda maslahi ya Watutsi waishio mashariki mwa nchi hiyo, kupambana na wanamgambo wa Kihutu wa FDLR (Interahamwe), na kutaka Banyamulenge watambuliwe kama raia halali wa Congo. Mzozo wa mashariki mwa Congo umegharimu maisha ya mamilioni ya watu toka ulipoanza. Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umepeleka askari wa kulinda amani. Ikumbukwe askari hao hawapigani upande wa serikali wala wa waasi. Kuna watu wanadhani askari wetu wa JWTZ walioko Congo wanapigana upande wa jeshi la serikali (FARDC). Hapana. Hawapigani upande wowote. Wanalinda amani. Lakini ikitokea kuna upande unahatarisha amani utapewa haki yake ya kikatiba. Kwa mfano, mwaka 2012 Umoja wa mataifa uliunda jeshi la kulinda amani Congo (MONUSCO). Ndani yake kulikua na brigedi maalumu ya kunyang'anya silaha makundi ya wapiganaji - Force Intervention Bregade (FIB). Brigedi hiyo iliundwa na askari kutoka Tanzania, Malawi, Afrika Kusini na Uruguay. April 2012, M23 wakashambulia kambi ya FIB iliyokua mji wa Rutshuru na kuua askari watatu. Baada ya shambulio hilo, aliyekua Mkuu FIB, Jenerali James Mwakibolwa alipanga vikosi vyake kujibu mapigo. M23 walichakazwa vibaya ambapo zaidi ya askari 600 wa M23 waliuawa na wengi kujeruhiwa. Walipigwa bila huruma na kuachia miji yote waliyokua wameishikilia ikiwemo Rubaya, Kitchanga na Rutshuru. Askari 16 wa FIB nao walipoteza maisha. March 2013, M23 walisalimu amri na Kiongozi wao Bosco Ntaganda akakimbilia Rwanda kujisalimisha kwenye ubalozi wa Marekani. Alipelekwa ICC akahukumiwa miaka 30 na sasa anatumikia adhabu yake gereza la Leuze-en-Hainaut lililopo Ubelgiji. Moja ya makosa ambayo Ntaganda anayajutia hadi leo ni kuingia kwenye 18 za FIB iliyokua inaongozwa na Jenerali James Aloizi Mwakibolwa. Kumekua na jitihada mbalimbali za kumaliza mgogoro wa DRC kwa njia za kidiplomasia ikiwemo mkutano wa viongozi wakuu wa SADC na EAC uliofanyika leo jijini Dar. #MyaTake: 1. Congo imeponzwa na ukarimu wake. Wakati wa vita vya Rwanda, Congo ilipokea Watutsi wengi na kuwapa hifadhi, akiwemo Kagame. Baada ya utawala wa Habyarimana kuangushwa Wahutu nao wakakimbilia Congo na kupewa hifadhi. Sasa hicho kimekua kigezo cha Rwanda kuingiza majeshi Congo kila mara kwa madai ya kuwatafuta Wahutu wa FDLR. Kwa lugha rahisi vita ya ndugu wawili (Wahutu na Watutsi) iliyopaswa kupiganwa Rwanda sasa inapiganwa Congo. 2. Congo inateswa na mipaka ya kikoloni. Laiti wakati wa kuchora mipaka jamii yote ya Watutsi ingewekwa Rwanda, leo kusingekuwa na Banyamulenge Congo, kwahiyo Watutsi wasingepata sababu ya kuishi Congo na kujifanya raia. Ni sawa na kukuta Wamasai 1,000 pale Longido, halafu uambiwe kati yao wapo wa Kenya. Utawajuaje? Utawatofautishaje? 3. Congo inateswa na rasilimali zake. Kama eneo la Kivu lisingekuwa na utajiri, mgogoro usingekuwa mkubwa kama ulivyo. Rejea #Part1 kujua utajiri uliopo Kivu. Kumbuka bila Kivu dunia haina laptop wala smartphones kwa sababu 80% ya coltan yote duniani inatoka Kivu. 4. Rwanda na Uganda ni Keyplayers kwenye mgogoro wa Congo. Kwa miaka mingi majeshi yao yameigeuza Congo shamba la bibi. Waondoe majeshi yao Congo. 5. Viongozi wengi wa M23 ni Wanyarwanda. Huu ni udhibitisho kuwa Rwanda ni kinara kwenye mgogoro huu. 6. Congo ni kubwa sana na hivyo inakosa jeshi imara la kutosha kulinda mipaka yake yote. Congo ni kubwa mara 90 ya Rwanda. Wapo wanaoshauri igawanywe kama njia ya kutatua mgogoro. Kama ambavyo Yugoslavia iligawanywa na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe. 7. Kiongozi wa sasa wa M23 Corneille Nangaa alikua Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi 2019 na ndiye aliyemtangaza Tshisekedi kuwa Rais kwa ushindi wa 38%. Lakini alilaumiwa kupunguza kura za Martin Fayulu aliyepata 34%. Huenda kuna ahadi alipewa haikutimizwa ndio maana akaungana na Waasi. Sababu hizo hapo juu zikifanyiwa kazi, mgogoro wa Congo unaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Mnaopenda kujifunza zaidi, naandika Kitabu. Get ready to have your copy. MWISHO.! (Malisa GJ ✍️)
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·888 Views
  • Read more
    Chukua hii. Kama utakwenda Nchini Japan 🇯🇵 na kusikia neno "Johatsu" (じょうはつ) tambua kuwa ni Mtu au Watu waliotoweka (kupotea) kutoka kwenye familia zao kutokana na sababu mbalimbali kama vile migogoro kwenye Ndoa, kushindwa kuoa, kukimbia madeni, kufukuzwa kazi na kadhalika. Watu hao huacha maisha yao na kuishi bila kujulikana wapi walipo kwa muda fulani na inaweze kuwa ni ndani ya Nchi ya Japan au nje Nchi yaani mataifa mengine kama vile Tanzania 🇨🇩 DR Congo 🇨🇩, Burundi 🇧🇮, Marekani 🇺🇸, Mexico 🇲🇽, Kenya 🇰🇪,.... Pamoja na Watu hao kupotea, lakini wanasaidiwa na Makampuni ambayo yamebobea katika kazi hiyo yaani Watu au Mtu anayehitaji huduma hiyo unalipia kisha kuhamishwa usiku. Makampuni hayo maalumu yanajulikana kwa jina la "Wahamishaji Usiku" huwasaidia Watu kupotea (unaweza kusema kujiteka, kujipoteza,...). Haya Mashirika au Makampuni husaidia Watu kutoweka kwa kuwahamisha kwa siri sana na mara nyingi kazi hii hufanyika usiku na wanapokupeleka inakuwa ni siri kubwa yaani kuanzia mahali pa kulala, utakula nini, vitambulisho vipya vya kusafiria Kampuni hizo ndizo zinafanya kila kitu kwa mujibu wa mkataba wenu. Pia Kampuni hizi zitahakikisha zinasafisha kumbukumbu zote za Mteja na kusahaulika kwenye Jamii, Nyumbani na Nchi kwa ujumla kisha unaanza mwanzo mpya wa kuanzisha maisha mengine kwenye Nchi au mahali walipo kupeleka.
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·383 Views
  • Read more
    Nchi ya Kenya 🇰🇪 imetuma Askari wengine 144 Nchini Haïti🇭🇹, kwa ajili ya kulinda amani na kurejesha utulivu Nchini humo ambao imepotea kwa miaka kadhaa sasa. Askari hao, ambao ni Wanaume 120 na Wanawake 24, wameelekea Haiti asubuhi ya Februari 6, 2025 baada ya kuagwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Kipchumba Murkomen. Idadi ya Askari hao kutoka Nchini Kenya inafikisha jumla ya Askari Polisi 744 waliotumwa Nchini Haiti kwa ajili ya kupambana na magenge ya kihalifu yaliyokithiri Nchini humo pamoja na uvunjwaji wa amani.
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·157 Views
  • Read more
    Rais Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩, Felix Tshisekedi na Paul Kagame wa Rwanda, wanatarajia kukutana Jijini Dar es Salaam, Tanzania, Februari 8, 2025 kujadili mustakabali wa hali ya usalama inayoendelea eneo la Mashariki mwa DR Congo. Taarifa iliyotolewa na Rais wa Kenya, William Ruto, wawili hao watakutana katika mkutano wa pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), baada ya Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kuridhia Nchi yake ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo.
    Like
    2
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·361 Views
  • Read more
    #PART2 Baada ya mipaka ya Wakoloni walioangukia Rwanda na Burundi waliendelea kujiita Watutsi, lakini walioangukia Congo hawakujiita Watutsi, kwa sababu ya kukwepa ubaguzi. Ili wasitengwe wakajitambulisha kwa eneo wanalotoka, safu za Milima ya Mulenge. Kwahiyo wakajiita Banyamulenge, yani watu kutoka Mulenge. Lakini ukweli ni Watutsi, wametengwa na wenzao kwa mipaka ya wakoloni. Ni sawa na wamassai wa Tanzania na wale wa Kenya. Ni jamii moja ila wametengwa na mipaka ya Wakoloni. Huku Tanzania Wamasai ni wengi kuliko Kenya, lakini serikali ya Kenya haiwezi kuwafukuza wa Kenya waje Tanzania. Itakua dhambi ya ubaguzi. Mipaka ilipowekwa waliojikuta Kenya wakawa raia wa Kenya hivyo, hali kadhalika waliojikuta Tanzania. Watutsi wa Congo pamoja na kujiita Banyamulenge, bado wakikumbana na ubaguzi. Hawakupata ushirikiano kutoka kwa jamii nyingine za Kivu. Kwahiyo wakajikuta wameongeza "bond" na Watutsi wa Rwanda. Kukawa na mwingiliano mkubwa kati ya Watutsi wa Rwanda na wale wa Congo (Banyamulenge). Mwaka 1959, mfalme wa mwisho wa Rwanda, Mutara III, aliuawa kwa sumu. Baada ya kifo chake, Rwanda iliingia katika machafuko ambapo Wahutu waliokuwa zaidi ya 80% waliwashambulia Watutsi, wakiwatuhumu kupendelewa na Wakoloni wa Kibelgiji. Maelfu ya Watutsi walikimbilia Kivu kwa ajili ya usalama wao. Walipofika huko, waliungana na wenzao (Banyamulenge), idadi ikaongezeka. Mwaka 1962, Rwanda ilipata uhuru, na Gregoire Kayibanda akawa Rais. Kwa mara ya kwanza, Wahutu walishika madaraka baada ya utawala wa kifalme wa Watutsi kwa miaka mingi. Kayibanda alikakandamiza Watutsi na kupendelea Wahutu wenzake. Watutsi wengi walikimbilia uhamishoni, hasa maeneo ya Kivu. Wakaenda kuungana na wenzao (Banyamulenge). Mwaka 1973, Kayibanda alipinduliwa na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Juvénal Habyarimana, ambaye alijiapiza kuwatokomeza Watutsi. Kwa miaka 21 ya utawala wake, Watutsi waliteswa vikali. Waliondolewa kwenye nafasi za kijeshi, mashirika ya umma, na siasa. Wengi walifungwa gerezani au kuuawa. Hali hii iliwafanya Watutsi wengi zaidi kukimbia Rwanda na kuelekea maeneo mbalimbali ikiwemo Kivu. Walioenda Kivu wakaenda kuongeza idadi ya Banyamulenge.! (Malisa GJ)
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·518 Views
  • Read more
    DRC SAGA - PART 1 (TAHADHARI: kama wwe ni mpenzi wa udaku au story fupifupi usisome. Hii ni kwa ajili ya watu wenye "solid mind" na wanaopenda kujifunza). ______ Mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umebeba historia ndefu inayohitaji muda mrefu kuielezea, lakini nitajaribu kuifupisha kwa kuangazia mambo machache muhimu. Mpelelezi wa Kiingereza, John Speke, katika kitabu chake Journal of the Discovery of the Source of the Nile (1863), aliandika kuwa asili ya Watutsi ni Pembe ya Afrika (Ethiopia, Somalia, Djibouti), na kwamba walihama katika karne ya 12 wakielekea eneo la Maziwa Makuu. Walifanya makazi yao katika maeneo ya kaskazini-magharibi mwa Ziwa Tanganyika, eneo ambalo kwa sasa ni Rwanda, Burundi, na Congo. Walipowasili, walikuta wenyeji ambao Wahutu na Watwa, ambao waliishi nao kwa amani. Wahutu na Watwa walikuwa wakulima, huku Watutsi wakiwa wafugaji. Karne ya 18, wakoloni walipofika, waligawa maeneo ya kiutawala bila kuzingatia mipaka ya kijamii iliyokuwepo. Badala yake, walizingatia maslahi yao binafsi, jambo lililosababisha baadhi ya jamii kugawanyika katika mataifa mawili tofauti. Kwa mfano, jamii ya Wamasai iligawanywa kati ya Kenya na Tanganyika. Wahutu waligawanyika kati ya Rwanda na Burundi, huku Watutsi wakigawanyika Rwanda, Burundi na Congo maeneo ya Kivu kusini. Watutsi pamoja na kuwa wachache kwa idadi lakini walijikuta wameathirika zaidi kwa kugawanyika maeneo mengi. Waligawanyika katika mataifa matatu tofauti ingawa walikuwa watu wa jamii moja, walioongea lugha moja, wenye mila na desturi zinazofanana. Baada ya mipaka kuwekwa Watutsi waliojikuta katika eneo la Kivu (Congo) walitengwa na jamii nyingine za watu wa eneo hilo kama Wabembe, Wavira, na Wanyindu. Kwa kuwa sehemu kubwa ya Watutsi ilikua Rwanda, wale waliojikuta Congo walionekana kama wageni (externals) maana walikua 6% tu ya watu wa Kivu. Walishauriwa kuhamia Rwanda, lakini hawakua wanyarwanda. Ni Wakongomani waliozaliwa hapo. Babu zao walifika hapo karne ya 12 kama nilivyoeleza juu. Kabla ya ukoloni Watutsi wote walikua jamii moja. Lakini baada ya mipaka ya wakoloni wakajikuta wamegawanywa katika nchi 3 tofauti. Sasa wafanjeje? (Malisa GJ)
    0 Commenti ·0 condivisioni ·439 Views
  • Read more
    Mkutano wa Kilele wa Marais wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika hivi karibuni umemtaka Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Félix Tshisekedi, kukaa meza moja na Waasi wa M23 kwa ajili ya mazungumzo ya pamoja ili kutafuta suluhu ya amani katika taifa hilo. Taarifa iliyotolewa na Mjumbe wa Mkutano huo, ambaye pia ni Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X (Twitter), ilieleza kuwa Viongozi hao walikutana Januari 29, chini ya Uenyekiti wa Rais wa Kenya, William Ruto, kujadili hali ya usalama Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩. Miongoni mwa makubaliano ya mkutano huo ni pendekezo la Rais Tshisekedi kushiriki mazungumzo na kundi la M23. Kadhalika, Viongozi hao walikubaliana kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inapaswa kuitisha mkutano wa dharura na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ili kutafuta suluhisho la kudumu kwa mgogoro huo. Museveni aliambatanisha taarifa hiyo na orodha ya Viongozi waliohudhuria mkutano huo, wakiwemo Rais wa Kenya William Ruto, Rais wa Somalia Hassan Mohamud, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, Rais wa Rwanda Paul Kagame, na mwenyeji wao, Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·487 Views
  • Kazi ya Bando la Wananchi wa Kenya
    Kazi ya Bando la Wananchi wa Kenya 🇰🇪 😳
    Wow
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·372 Views
  • Read more
    Mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Victor Boniface, anayeichezea Bayer Leverkusen ya Ujerumani, ameachana na mpenzi wake, Rikke Hermine, raia wa Norway. Wawili hao walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa miaka minne, lakini wameamua kuvunja uhusiano wao kutokana na kugundua kuwa Victor kwenye mali zake ameandika majina ya mama yake tu. Chanzo cha habari kinaeleza kuwa uamuzi wa Rikke kuachana na Victor ulitokana na kugundua kuwa katika mali zote za mshambuliaji huyo, majina ya mama yake mzazi pekee ndiyo yaliyoandikwa. Hali hii ilimfanya Rikke kuhisi kuwa hakuwa na nafasi ya kutosha katika maisha ya Victor, jambo lililomfanya kuchukua hatua hiyo. Aidha, inadaiwa kuwa Rikke alikuwa akishinikiza kufunga ndoa baada ya kuwa wapenzi kwa muda mrefu, huku Victor akiwa tayari kufunga naye ndoa lakini kwa sharti la kusaini mkataba wa awali (prenup). Prenup ni Mkataba wa awali kabla ya kufunga ndoa ambao unalenga kulinda mali za pande zote mbili endapo itatokea mkaachana kila mmoja anabaki na alichokuja nacho katika ndoa na sio kugawana mali, ila bibie Rikkie amekuwa mgumu kukubali hilo hivyo kuachana #tanzania #kenya #daressalaam #africa #zanzibar #diamondplatnumz #arusha #mwanza #dodoma #uganda #wcb #travel #life #safari #wasafi #love #millardayoupdates #mbeya #nairobi #harmonize #rwanda #eastafrica #kilimanjaro #alikiba #gainwithmchina #serengeti #wasafitv #fashion #wasafimedia #wemasepetu
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·2K Views
  • Read more
    #JeWajua Msako mkali wa wahamiaji uliofanyika nchini Marekani siku ya Jumapili na kusababisha kukamatwa kwa watu 956, idadi hiyo ikiwa kubwa zaidi tangu Donald Trump arejee mamlakani, kulingana na shirika la Uhamiaji na Utekelezaji wa Forodha (ICE). Mashirika kadhaa ya serikali yenye mamlaka mapya ya kuwaweka kizuizini wasio na vibali yalihusika katika kamata kamata hiyo kwenye miji kadhaa ikiwa ni pamoja na Chicago, Newark na Miami. Moja ya ahadi alizotoa Donald Trump wakati wa kampeni yake, ni kuwafukuza nchi Marekani wahamiaji wasio na vibali. Mtangulizi wake Joe Biden aliwarejesha makwao wastani wa wahamiaji 311 kila siku, kulingana na ICE, wengi wao wakiwa watu ambao walikuwa wamefanya uhalifu. Tangu aingie madarakani, Trump ametekeleza maagizo 21 kurekebisha mfumo wa uhamiaji wa Marekani. Huko Miami siku ya Jumapili, vyombo vya kutekeleza sheria vya serikali vilichukua "hatua kadhaa za uhamiaji," Uchunguzi wa Usalama wa jiji hilo ulisema kwenye mitandao ya kijamii. #tanzania #kenya #daressalaam #africa #zanzibar #diamondplatnumz #arusha #mwanza #dodoma #uganda #wcb #travel #life #safari #wasafi #love #millardayoupdates #mbeya #nairobi #harmonize #rwanda #eastafrica #kilimanjaro #alikiba #gainwithmchina #serengeti #wasafitv #fashion #wasafimedia
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·2K Views
  • Read more
    Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩, Félix Tshisekedi na Rais wa Burundi 🇧🇮, Evariste Ndayishimiye wamekataa kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioitishwa na Rais wa Kenya 🇰🇪, William Ruto, ambao pia ulipangwa kumjumuisha Rais wa Rwanda 🇷🇼 Paul Kagame ambaye alishasema kuwa yupo tayari kuhudhuria mkutano huo ila kwa kusisitiza, yagusiwe kiini haswa cha ngorongoro uliopo kati ya DR Congo na Waasi. Aidha, Tshisekedi amesema kuwa hatoweza kuhudhuria mkutano huo kwa sababu ya ratiba.
    0 Commenti ·0 condivisioni ·328 Views
  • Read more
    Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo linaendelea kupambana na Waasi wa M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Jeshi la Rwanda (Japo Rwanda imeshalikanusha mara nyingi tu). Raia watano pia wameripotiwa kuuawa huko Gisenyi Nchini Rwanda. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais wa Kenya William Ruto, ameitisha mkutano wa Marais wa Jumuiya hiyo hapo kesho Jumatano wa kuutafutia suluhu mzozo huo wa mashariki mwa Kongo licha ya Kigali na Kinshasa kutotoa taarifa rasmi kuwa watashiriki mkutano huo. Umoja wa Mataifa ambao umetahadharisha kuwa mzozo huo unaweza kuzusha vita vya kikanda na umeelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya mbaya ya kibinadamu huko Goma ambako mwezi huu pekee, karibu Watu 500,000 wameyahama makazi yao.
    0 Commenti ·0 condivisioni ·348 Views
  • Read more
    Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo linaendelea kupambana na Waasi wa M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Jeshi la Rwanda (Japo Rwanda imeshalikanusha mara nyingi tu). Raia watano pia wameripotiwa kuuawa huko Gisenyi Nchini Rwanda. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais wa Kenya William Ruto, ameitisha mkutano wa Marais wa Jumuiya hiyo hapo kesho Jumatano wa kuutafutia suluhu mzozo huo wa mashariki mwa Kongo licha ya Kigali na Kinshasa kutotoa taarifa rasmi kuwa watashiriki mkutano huo. Umoja wa Mataifa ambao umetahadharisha kuwa mzozo huo unaweza kuzusha vita vya kikanda na umeelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya mbaya ya kibinadamu huko Goma ambako mwezi huu pekee, karibu Watu 500,000 wameyahama makazi yao.
    0 Commenti ·0 condivisioni ·343 Views
  • Read more
    OPERATION ENTEBBE -2 Tayari zilikuwa zimepita siku tatu tangu ndege ya Air France Flight 139 kuondoka Tel Aviv na hatimaye kutekwa baada ya kuruka jijini Athens iliposimama kuchukua abiria. Lakini pia zilikuwa zimepita siku mbili tangu ndege hii kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda. Katika siku zote mbili hizi tangu ndege hii itue uwanjani hapa, rais wa Uganda Idd Amin Nduli Dadaa alikuwa anafika uwanjani hapo kila siku “kuwajulia hali” mateka hao. Kwa muda wa siku hizi zote mbili tangu ndege itue uwanjani hapo, magaidi hawa walioiteka ndege kwa kushirikiana na jeshi la Uganda kuchunguza majina ya kila abiria kama ambavyo yalikuwa yameandikwa kwenye pasport. Lengo lao la kufanya hivi ilikuwa ni kujaribu kufahamu uraia wa kila mateka waliye naye. Baada ya kufanya uchambuzi huu wa passport zote, hatimaye siku hii ya tatu, yaani tarehe 29 June 1976 kiongozi wa magaidi hawa Wilfred Bose akiwa na karatasi mkononi aliingi ndani ya terminal ambayo walikuwa wanaitumia kuwahifadhi mateka na kisha akaanza kusoma majina ya kila abiria. Alichokuwa anakifanya ni kusoma majina ya mateka ambao passport zao zilionyesha walikuwa ni raia wa Israel. Lakini pia alisoma majina ya mateka wengine ambao licha ya passport zao kuonyesha kuwa hawakuwa raia wa Israel lakini walikuwa na majina ya kiyahudi. Pamoja na hao pia mateka wote ambao walikuwa na uraia pacha na uraia huo mmojawapo ukiwa ni Israel basi nao waliunganishwa kwenye list hii. Baada ya kuwatenganisha raia wote wa Israel na kuwaweka kwenye chumba kingine peke yao hapo hapo kwenye terminal, kuna mwanadada raia wa Ufaransa aliyeitwa Jocelyne Monier yeye jina lake halikuitwa kwenye ile list ya wanaotakiwa kutengwa kwenye chumba kingine (Waisrael na Wayahudi). Lakini ‘boyfriend’ wake alikuwa ni Muisrael na aliitwa jina na kutengwa na wengine katika kile chumba kingine. Mwanadada huyu ili kuonyesha kumtia moyo mpenzi wake na kupinga huu ubaguzi uliokuwa unafanywa na hawa magaidi, kwa hiari yake alijipeleka kwenye chumba cha mateka wa Kiisrael. Si mwanadada huyu pekee ambaye alifanya kitendo hiki cha ushujaa, lakini pia kulikuwa na mwanamama mwingine aliitwa Janet Almog (rai wa Marekani) na mateka mwingine aliyeitwa Jean-Jacques Mimouni (raia wa Ufaransa) nao kwenye kuonyesha hali ya kuwaunga mkono wenzao waliotengwa kwenye chumba kingine na kupinga ubaguzi uliokuwa unafanywa na maharamia hawa, nao walijipeleka kwa hiari yao kwenye chumba ambacho mateka hao walikibatiza jina “Chumba cha Waisrael”, ambacho mateka wote walijua fika kwamba kuna jambo baya maharamia hao walikuwa wamepanga kulifanya. Licha ya maharamia kwa kushirikiana na jeshi la Uganda kufanya uchambuzi huu wa kina kuhusu uraia wa kila mateka waliye naye, lakini walifanya kosa kubwa sana ambalo lilkuja kuwagharimu sana hapo baadae. Kwenye uchambuzi wao wote huu walioufanya walishindwa kumng’amua mateka mmoja mwanajeshi wa Israel ambaye alikuwa ana uraia pacha na siku hiyo alikuwa anatumia passport ambayo sio ya Israel. Mateka huyu alikuja kuwa muhimu sana huko mbeleni kuwapatia Mossad Intelijensia mujarabu kabisa kuhusu watekaji, jengo wanaloshikilia mateka, na namana wanavyoshirikiana na jeshi la Uganda. Siku iliyofuata yaani June 30, maharamia haya wakawaachia mkupuo wa kwanza wa mateka wasio raia wa Israel au wayahudi. Katika mkupuo huu wa kwanza waliachia mateka 48 ambao walikuwa ni wazee, watoto na akina mama wenye watoto wadogo. Baada ya mkupuo huu wa kwanza wa kuwaachia mateka hawa wachache, maharamia wakaweka wazi matakwa yao ili waweze kuachia mateka wengine. Kwanza kabisa walitaka walipwe fedha kiasi cha dola za Kimarekani milioni 5. Na pili walitakakuachiwa kwa wafungwa 53 wenye asili ya kipalestina wanaotuhumiwa kwa ugaidi, ambao kati yao 40 walikuwa kwenye jela za Israel na 13 katika nchi nyingine za Ulaya. Watekaji hawa wakatoa ‘ultimutum’ kwamba kama matakwa yao hayatatekelezwa ndani ya masaa ishirini na nne yajayo (mpaka tarehe 1 July saa 8 mchana) basi wataanza kuua raia wa Israel mmoja baada ya mwingine. Dunia nzima ni kama ilisimama kwa masaa kadhaa kutokana na sintofahamu iliyogubika kila mahali. Sintofahamu hii ililetwa na ukweli kwamba, ilikuwa inajulikana wazi kwa miaka yote kwamba Israel wana sera ya kutofanya mazungumzo au makubaliano na Magaidi. Kwahiyo kila mtu alikuwa nafahamu kuwa kuna uwezekano mkubwa ndani ya masaa 24 yajayo ulimwengu ukashuhidia watu zaidi ya 200 wakichinjwa kama kuku. NCHINI ISRAEL: KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI Nchini Israel kikao cha dharura cha baraza la mawaziri kilikuwa kimeitishwa na waziri Mkuu Yitzhak Rabin kujadili kuhusu hatua za kuchukua kuokoa raia wake ambao wameshikiliwa mateka huko uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda. Hali ya kikao ilikuwa tete sana kutokana na kila dakika waliyokuwa wanaitumia kujadili ndivyo ambavyo walikuwa wanaikaribia saa 8 mchana ya tarehe 1 July. Walipowasilana na Ujerumani na Ufaransa ambao nao walikuwa na baadhi ya wafungwa wa Kipalestina ambao watekaji walitaka waachiwe… walipowaomba ushirikiano wao kuhusu kukabali kuachia hao wafungwa, Ujerumani na Ufaransa walikataa katakata kuachia hata mfungwa mmoja wa Kipalestina ambaye alikuwa kwenye magereza zao. Sintofahamu ilizidi kuongezeka. Masaa yalizidi kuyoyoma. Saa 8 mchana ya tarehe 1 July ilizidi kukaribia. Harufu ya damu ilikuwa inabisha hodi mlangoni kwao. Licha ya weledi wao wote walionao lakini mbele yao waliona giza. Inapaswa kukumbukwa kwamba Idd Amin aliwahi kupatiwa mafunzo ya weledi wa kijeshi nchini Isarel (Special Force Training). Kwa hiyo baraza la mawaziri likamuagiza Baruch Bar-Lev, kamanda mstaafu wa IDF ambaye alihusika kumpatia mafunzo ya kijeshi Amin kipindi yuko Israel na kufanikiwa kujenga naye ukaribu. Baraza la Mawaziri likamuagiza Baruck (marafiki zake humuita “Burka”) kufanya mawasiliano na Rais huyo wa Uganda ili kujaribu kumuomba awashawishi magaidi wanaoshikilia mateka kwenye uwanja wake wa ndege wa Entebbe wawaachie mateka hao bila masharti magumu. Kupitia kwa Burka, Israel ilifikia mpaka hatua ya kumuahidi Idd Amin kuwa kama atafanikisha kuachiwa kwa mateka hao basi watatumia ushawishi walionao kuhakikisha kuwa Amin anatunukiwa tuzo ya amani ya Nobel. Lakini Amin hakulegeza msimamo, akaendelea kuwasisitiza kuwa hakuna namna nyingine yeyote ambayo mateka hao wataachiwa bila masharti yaliyotolewa na watekaji kutimizwa. Baada ya juhudi hii ya kumuhonga ‘tuzo’ kugonga mwamba, Waziri Mkuu wa Israel akawasiliana na serikali ya Marekani na kuwaomba wamshawishi Rais wa Misri Anwar Sadat ambaye alikuwa anaheshimiana sana na Amin ili amshawishi kuwaamuru magaidi yaliyoko uwanjani kwake Entebbe waachiemateka bila masharti magumu. Amin bado akashikilia msimamo kwamba hakuna mateka atakayeachiwa pasipo masharti yaliyotolewa kutimizwa. Juhudi hizi za kumshawishi Amin zilikula muda mwingi sana na hatimaye wakajikuta tayari kulikuwa kumekucha asubuhi. Mbele yao kulikuwa kumebakia masaa chini ya manane kabla ya damu ya zaidi ya watu 200 kumwagika. Baraza la mawaziri la Israel likamuomba Amin aongee na watekaji wakubali kusogeza siku mbele ili kuipa serikali ya Israel muda wakutosha kushughulikia lojistiki na kushawishi Ujerumani na Ufaransa ili waweze kutimiza sharti la kuachiwa kwa wafungwa wa kipalestina 53 wanaotuhumiwa kwa ugaidi. Rais Idd Amin baada ya kushawishiwa sana akakubali ombi hili na akaieleza serikali ya Israel kwamba ni siku tatu tu pekee zinaongezwa, yaani ikimaanisha kwamba siku zitaongezwa mpaka tarehe 4 July, saa 8 mchana. Serikali ya Israel ikakubliana na hili. Mchana wa siku hiyo, serikali ilitoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari wakilaani vitendo vya kigaidi na hususani matukio ya utekeji wa raia wasio na hatia, na pia ikaendelea kusisitiza kuhusu sera yake ya kutojadili na magaidi. Lakini taarifa hii ikamalizia kwa kueleza kuwa kwa kujali zaidi uhai wa zaidi ya raia 200 ambao bado wanashikiliwa na magaidi hayo, na kujali maumivu ambayo familia zao na taifa zima linapitia, wamekubali kutimiza sharti la magaidi hao la kuwalipa fedha za kimarekani dola milioni tano pamoja na kuachiwa kwa wafungwa wa kipalestina 53 wenye tuhuma za ugaidi. Ilikuwa ni moja ya matukio machache ambayo yaliishangaza dunia kwa Israel kukubali kushindwa hadharani. Kwa upande wa maadui wa Israel hii ilikuwa ni sherehe kubwa kwao. Na kwa upande wa Isarel na maswahiba zake hii iikuwa ni maombolezo makubwa. Amin na wenzake kule Uganda walikuwa wanasherehekea baada ya taarifa hii kutolewa kwa vyombo vya habari. Walihsi kabisa harufu ya ushindi inanukia kwenye pua zao. Kitu ambacho walikuwa hawafahamu ilikuwa ni kwamba, Israel walikuwa wanawafanyia ‘mchezo’ wa kisaikolojia ili Amin, jeshi lake na watekaji wajiamini kwa kuona kuwa ushindi umeegemea upande wao na hatimaye wajisahau kutokana na kujiamini huku. NYUMA YA PAZIA Huko Tel aviv, makamanda wa IDF na maafisa wa Mossad walikuwa wamekusanyika katika conference room ya mako makuu ya wizara ya ulinzi kuweka mkakati wa oparesheni ya uokozi (rescue mission) wa mateka wanaoshikiliwa katika uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda. Kati ya watu muhimu ambao walikuwepo kwenye kikao hiki alikuwa ni Waziri Mkuu Rabin na Ehud Barak ambaye kipindi hicho alikuwa kamanda wa ngazi za juu kwenye jeshi anayeongoza kitengo cha Intelijensia ya jeshi (Military Intelligence). Moja kati ya vitu muhimu ambavyo viliwasaidia ilikuwa ni taarifa ya intelijensia iliyoletwa na Mossad kwamba uwanja wa ndege wa Entebbe ulijengwa na kampuni ya Kiisrael inayoitwa Solel Boneh. Kwahiyo muwakilishi kutoka katika kampuni hii ya ujenzi naye akaitwa kikaoni kwa ajili ya kuwasilisha michoro kuhusu jengo lote na uwanja wa ndege wa Entebbe ulivyo. Lakini pia wakati huo huo kulikuwa na maafisa wa Mossad ambao walikuwa ufaransa kuwahoji wale mateka ambao walikuwa wameachiwa awali. Mtu muhimu zaidi ambaye alitoa taarifa nzuri kwa Mossad alikuwa ni yule afisa wa jeshi niliyemuelezea awali kwamba alikuwa na uraia wan chi mbili (Israel na Ufaransa) na siku hii alikuwa ametumia passport ya nchi ya ufaransa hivyo watekaji walimuachia pamoja na wenzake wa kundi la kwanza lile la watu 48. Bwana huyu alitoa taarifa muhimu zaidi kuhusu kilichokuwa kinaendelea katika uwanja wa ndege wa Entebbe, kwa kuwa yeye tofauti na wenzake kutokana na uzoefu wake wa jeshi alikuwa aliweza kuwaeleza Mossad kuhusu ni salaha za namna gani watekaji walikuwa nazo, kulikuwa na ndege za aina gani za kijeshi pale uwanjani (Idd Amin aliamuru Air Force ya Uganda kulinda uwanja huo masaa 24), pia aliweza kuwaeleza kuhusu ‘rotation’ ya ulinzi ya jeshi la Uganda pamoja na taarifa nyingine muhimu ambazo abiria wengine wasingeweza kuzitilia maanani au kkuzieleza kwa ufasaha. Baada ya kupata intelijensia ya kutosha, mkakati wa awali ambao ulipendekezwa na jeshi ulikuwa ni kutumia ndege ya kijeshi na kisha kudondosha makomando kwenye ziwa Viktoria na kutoka hapo watatumia boti za mpira kuvuka mpaka nchi kavu na hatimaye kuelekea uwanja wa ndege ambao haukuwa mbali sana na ziwa Viktoria. Mkakati huu ulikuwa ni mzuri lakini ulihairishwa baada ya kupewa taarifa kuwa ziwa Viktoria lilikuwa na mamba wengi na ingeweza kuhatarisha uhai wa hawa makomando kabla hata ya kufika kwenye uwanja wa ndege. Kwahiyo ilikuwa dhahiri kwamba mkakati wowote ambao utawekwa ni lazima uwe wa kuvamia kutokea nchi kavu na ikiwezekana kutoka nchi jirani. Changamoto kubwa zaidi ilikuwa ni usafiri. Yaani kwamba oparesheni hii ilikuwa si tu kwamba makomando wanaotumwa kutekeleza wanaenda kupambana na magaidi wanne tu walioteka ndege, bali ilikuwa ni kana kwamba wanaenda kupambana na jeshi zima la Uganda. Kwa hiyo kikosi cha makomando ambacho kitatumwa kwenda huko lazima kiwe na watu wengi wa kutosha na pia lazima wachukue silaha nzito za kutosha. Ili kufaniskisha safari yenye makomando wengi hivi na vifaa vizito ilikuwa ni lazima kutumia ndege kubwa za kijeshi zenye uwezo mkubwa pia na hakukuwa na chaguo zuri zaid ya kutumia ndege za kijeshi za LOCKHEED C-130 HERCULES. Sasa changamoto ilikuwa inakuja kwamba huwezi kurusha dege kubwa kama hii kwenda na kurudi kutoka Israel mpaka Uganda bila kujaza mafuta tena japo mara moja. Katika kipindi hiki bado Israel walikuwa hawajawa na uwezo wa kufanya ‘Aerial Refuel’, yaani ndege kujazwa mafuta kwa kutumia ndege nyingine ikiwa angani. Lakini pia ilikuwa ni lazima madege hayo yakikaribia Uganda yaruke chini chini ili kukwepa kudunguliwa na kuikwepa rada ya kijeshi. Kwa hiyo ilikuwa ni lazima kupata nchi ndani ya afrika Mashariki ambao watakubali madege hayo ya kijeshi ya Israel kutua kwenye uwanja wake wa ndege na kujaza mafuta lakini pia kujiandaa na kuanzisha operation kutokea hapo na pia anga lao kutumika kuanzisha shambulizi la kijeshi kuelekea Uganda. Sasa japokuwa nchi zote za Afrika Mashariki zilikuwa hazikubaliana na kitendo cha Rais wa Uganda kushirikiana na watekaji, lakini hakukuwa na hata nchi moja ambayo ilikuwa iko tayari kuingia kwenye mzozo na Idd Amin kwa kuruhusu viwanja vya vya ndege kutumika na ndege za jeshi la Israel au wanajeshi kujiandaa kuvamia Entebbe au pia kuruhusu anga lao kutumia na jeshi la Israel. Ndipo hapa ambapo kwa haraka sana siku hiyo hiyo Waziri Mkuu Rabin akamtuma Ehud Barak na maafisa wachache wa Mossad kwenda Kenya kushawishi serikali ya Mzee Jomo Kenyatta iruhusu ndege za jeshi la Isarel kutumia kiwanja chao cha ndege. Ehud barak na wenzake hawakwenda tu moja kwa moja kwa Mzee Kenyatta, bali kwanza walienda kwa Waziri wa kilimo wa kipindi hicho Bw. Bruce McKenzie ambaye huyu aliwahi kuwa afisa wa Idara ya ujasusi ya Uingereza, MI6 na pia alikuwa swahiba mkubwa wa Ehud Barak. Kwa hiyo Israel ikamtumia Bruce McKenzie kumshawishi Mzee Jomo Kenyatta kuruhusu anga la Kenya na viwanjavya ndege kutumiwa na makomando wa Israel na ndege zao. Ehud Barak na maafisa wa Mossad hawakuishia hapa tu, bali pia walifanya vikao vya siri na wafanyabiashara wakubwa nchini Kenya wenye asili ya Israel na wale ambao walikuwa na ‘marafiki’ wa Israel kuwaomba watumie ushawishi wao wa kisiasa na kiuchumi wasaidie kumshawishi Kenyatta kukubali ombi la seriakli ya Israael viwanja vyao kutumika na ndege za kijeshi za Israel na makondo wake. Baada ya mashinikizo haya kutoka kila upande, Mzee Kenyatta hakuwa na chaguo linguine zaidi ya kukubali ombi lao. Bwana huyu McKenzie pia alikuwa na ndege yakebinafsi, na Ehud Barak akaona fursa. Walitumia ndege hii ya kiraia kuruka mpaka Uganda mijini Entebbe na kukatiza juu ya anga la uwanja wa ndege wa Entebbe na walipokuwa wanapita juu ya anga la uwanja wa ndege, Ehud Barak akatumia fursa hii kupiga picha kila eneo la uwanja. Kwa kuwa hii ilikuwa ni ndege ya kiraia, jeshi la Uganda hawakushughulika nayo. Picha hizi zilizopigwa na Ehud Barak zilikuja kuwa na umuhimumkubwa katika maandalizi ya mwisho ya oparesheni ya makomando wa Isarel Kuvamia uwanja huu. Mpaka kufikia hapa maandalizi yote muhimu yalikuwa yamekamilika. WAKATI HUO HUO Upande wa watekaji kule Uganda walikuwa wanasubria mifwedha yao dola milioni 5 za kimarekani. Rais Idd Amin naye baada ya kufikia makubaliano na Israel kuwa masharti ya fedha na wafungwa wa kipalestina kuachiwa tarehe 4 July, naye ‘akarelax’ na akaona huo ndio muda wa kutekeleza majukumu Mengine akisubiria tarehe 4 July ifike. Katika kipindi hiki Idd amin ndiye alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwa kuzingatia utaratibu wa uenyekiti kuzunguka kwa kila nchi kwa mwaka mmoja mmoja na wiki hii alikuwa anatakiwa kwenye kikao cha Umoja wa Afrika kilichokuwa kinafanyika Mauritius. Kwa hiyo Amin akafunga safari kuelekea Mauritius kwenda kukabidhi kijiti cha Uenyekiti. Ehud Barak aliposikia taarifa hii, kwa kutumia akili yake kubwa ya kuzaliwa aliyojaliwa na uzoefu wake wa ujasusi, aliona fursa adhimu kabisa hapa. Akawasiliana na walioko kikaoni huko Tel Aviv na kuwaeleza taarifa ambazo awali wote hawakuielewa. Ehud Barak: “Idd Amin akiwa ndani ya Uganda huwa anatumia Mercedes Limousine katika msafara wake” Waziri Mkuu Rabin: “Ok! Limefanyaje?’ Ehud Barak: “Nataka mtafute gari kama hiyo… Mercedes Limousine” Waziri Mkuu Rabin: “la kazi gani?” Ehud Barak: “siku ambayo kikosi cha makomando wakipanda kwenye ndege kutoka huko Israel kwenda Uganda, gari hilo nataka pia lipakiwe ndani ya ndge!” Kwa dakika kadhaa wote ambao walikuwa wanamsikiliza pale kikaoni kupitia simu hakuna ambaye alielewa nini hasa Ehud Barak alikuwa anapendekeza. Yalikuwa yamebaki masaa machache tu ambapo, weledi, ushujaa na uzalendo uliotukuka ulikuwa unaedna kudhihirika. Itaendelea #TheBOLD_JF
    0 Commenti ·0 condivisioni ·1K Views
  • Read more
    Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) leo limetangaza kuahirisha Mashindano ya Mataifa ya Afrika ya TotalEnergies (CHAN) yaliyokuwa yafanyike Kenya, Tanzania, na Uganda kuanzia Februari na sasa yatafanyika Agosti 2025. Taarifa ya CAF imekiri kwamba kumekuwa na maendeleo makubwa katika ujenzi na ukarabati wa viwanja vya michezo, maeneo ya mazoezi, hoteli, hospitali, na miundombinu mingine muhimu katika nchi hizo tatu kwa ajili ya mashindano hayo. Hata hivyo, wataalamu wa kiufundi na miundombinu wa CAF waliopo Kenya, Tanzania, na Uganda wameishauri CAF kwamba muda zaidi unahitajika ili kuhakikisha miundombinu inafikia viwango vinavyohitajika kwa ajili ya kuandaa mashindano yenye mafanikio. Rais wa CAF, Dkt. Patrice Motsepe, amesema: "Ninatoa shukrani za dhati kwa Rais William Ruto wa Kenya, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, na Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa uongozi wao, kujitolea, na maendeleo mazuri yaliyopatikana katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya soka. Nimevutiwa na kazi inayoendelea, na nina uhakika kwamba viwanja vya michezo, maeneo ya mazoezi, hoteli, hospitali, na miundombinu mingine itakidhi viwango vya CAF ifikapo Agosti 2025." CAF pia imetangaza kwamba droo ya CHAN Kenya, Tanzania, na Uganda 2024 itafanyika jijini Nairobi, Jumatano, Januari 15, 2025, saa mbili usiku kwa saa za Nairobi. Tarehe kamili ya kuanza kwa mashindano hayo mwezi Agosti 2025 itatangazwa na CAF katika siku zijazo. #neliudcosiah
    Like
    1
    · 0 Commenti ·0 condivisioni ·732 Views
  • Michuano ya CHAN yahairishwa, badala ya kufanyika Februari 2025 sasa yatafanyika Agosti 2025. Sababu ni kutokamiliaka kwa ujenzi wa miundombinu ya Viwanja katika Nchi wenyeji (Tanzania, Kenya na Uganda).
    Michuano ya CHAN yahairishwa, badala ya kufanyika Februari 2025 sasa yatafanyika Agosti 2025. Sababu ni kutokamiliaka kwa ujenzi wa miundombinu ya Viwanja katika Nchi wenyeji (Tanzania, Kenya na Uganda).
    Like
    Love
    4
    · 1 Commenti ·0 condivisioni ·643 Views
  • Read more
    OPERATION ENTEBBE -3 Siku ya July 3 mwaka huo 1976 saa 12 na nusu ya jioni takribani masaa kadhaa kabla ya kufikia deadline ya mwisho waliyopewa na watekaji (July 4), Waziri mkuu wa Israel Yitzhak Rabin alitia saini nyaraka ya kuidhinisha oparesheni ya kijeshi ya uokozi (rescue mission) ambayo iliwasilishwa mezani na Meja Jenerali Yekutiel Adam (maarufu kwa jina la “Kuti”) na Brigedia Generali Dan Shomron. Pia kwa mujibu wa nyaraka hiyo iliyosainiwa na Waziri mkuu, Shomron aliteuliwa kuwa Kamanda wa utekelezaji wa Oparesheni. Baada ya oparesheni hii kuidhinishwa rasmi na Baraza la Mawaziri muda huo nilioutaja hapo juu, Meja Jenerali Yekutiel Adam na Brigedia Generali Dan SHomron walikusuka kikosi cha kijeshi kwa ajili ya kutekeleza oparesheni hiyo kama ifuatavyo; The Ground Command Hiki kilikuwa ni kikosi (japo sio kikosi haswa) ambcho kilikuwa na watu wawili tu, Brigedia Generali Dan Shomron na mwakilishi wa jeshi la Anga la Israel Kanali Ami Ayalon na watu wachache wa masasiliano ya jeshi. Kikosi hiki ndicho ambacho kilikuwa na amri ya mwisho juu ya nini wanajeshi walikuwa wanatakiwa kufanya pindi wakakapoanza utekelezaji wa oparesheni. The Asault Team Timu hii ilipewa kazi ya kuvamia jengo la uwanja wa ndege ambalo mateka walikuwa wanashikiliwa na kuokoa mateka wote waliomo humo. Kikosi hiki kilikuwa na wanajeshi 29 ambacho kiliongozwa na Luteni Kanali Yonathan Netanyahu (kaka yake Waziri Mkuu wa sasa wa Israel, Benjamin Netanyahu). Kikosi hiki kilijumuisha makomando wenye weledi wa hali juu kutoka katika kitengo maalumu cha jeshi la Israel kiitwacho SAYERET MATKAL. Nieleze kidogo kuhusu Sayet Matkal. Hiki ni kikosi cha weledi maalumu (special force) ndani ya jeshi la Israel la IDF. Makomando wanofuzu kutumika katika kikosi hiki, licha ya kupata mafunzo yote ya kijeshi kama wanajeshi wengine lakini wanaongezewa mafunzo mengine adhimu zaidi kuwafanya waweze kutekeleza oparesheni hata katika mazingira ambayo kwa akili ya kijeshi ya kawaida inaonekana kwamba hakuna uwezekano wa kufanikiwa kwa oparesheni hiyo. Mfano wa mafunzo haya adhimu ambayo wanapatiwa ni pamoja na ukusanyaji wa intelijensia, kufanya ‘deep recon’ (nimekosa Kiswahili chake) katika uwanja wa vita, upenyezaji wa intelijensia za kimkakati (strategic intelligence) mafunzo adhimu ya counterterrorism pamoja na uokozi wa mateka nje ya mipaka ya Israel. Kwa namna fulani ili kukielewa kikosi hiki unaweza kukifananisha na kikosi cha SAS kwenye jeshi la nchi ya Uingereza japo vinatofauti fulani bado. Ila kwa ufupi huo ndio muonekano wa Sayeret Matkal na shughuli zake. The securing Element Kikosi hiki kiligawanywa katika vikundi vidogo vidogo vitatu ili kuleta ufanisi. 1.Paratroopers – hawa waliongozwa na Kanali Matan Vilnai. Kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha hakuna shughuli zozote zinaendelea ndani ya uwanja wa ndege wa Entebbe qawakati ambao oparesheni hiyo inatekelezwa. Pia walikuwa wanatakiwa kuhakikisha kuwa njia ya kurukia ndege (runway) iko ‘clear’ muda wote. Pamoja na hayo kikosi hiki pia walikuwa ndio wanaowajibika kulinda ndege za kijeshi za Israel muda wote zinatakapo kuwa kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe pamoja na ujazaji mafuta. 2. The Golani Force – kikundi hikicha kijeshi kiliongozwa na Kanali Uri Sagi. Kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa yale madege makubwa aina ya Lockheed Harcules C-130. Pia walitakiwa kuyasogeza madege hayo karibu kabisa na terminal ambayo mateka walikuwepo ili waweze kuwapakia pindi ambapo uokozi ukiwa umefanikiwa. Lakini pia kikundi hiki kilifanya kazi kama ‘kikosi’ cha akiba endapo ambapo kungetoke dharura ya upungufu katika kikosi kingine. 3. The Sayeret Matkal Force – kikosi hiki nacho pia kama ilivyo kwa ‘Assault Team’ ambayo nimeiongelea hapo juu, nacho pia kiliundwa na makomando wa Sayeret Matkal na kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha kuwa hakukuwa na ‘interception’ yoyote kutoka kwenye jeshi la anga la Uganda na kuwa tayari kuwazuia na kuzuia shambulizi lolote la kijeshi ikitokea kwamba wanajeshi wa Uganda walioko uwanja wa ndege wakiomba msaada kutoka kambi ya jeshi iliyoko ndani ya jiji la Entebbe. Kwa ujumla huo ndio ulikuwa muonekano kamili wa Kikosi kizima na majukumu ya wanajeshi wote waliohusia katika oparesheni ya uokozi kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe. USIKU WA TAREHE 3 JULY, 1976 Hatimaye siku ya siku ikawadia, saa lililotarajiwa likafika. Ndege nne kubwa aina ya Lockheed Harcules C-130 zikiwa zimebea zaidi ya makomando 200 pamoja na ile gari Mercedes Limousine (pamoja na gari nyingine aina ya Land Rover) ambayo Ehud Barak alipendekeza waje nayo, ziliruka kutoka kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi ulioko eneo la Sharm El Sheikh mpakani kabisa na Misri. Ndege hizi nne kubwa Lockheed Harcules C-130 zilisindikizwa nyuma na ndege mbili aina ya Boeing 707 ambazo moja ilikuwa imelengwa kutumiwa kama ‘command post’ na nyingine itumike kama hospitali kutibu majeruhi ambao watatokana na mapambano ya risasi ambayo walikuwa wanayategemea kati yao na watekaji pamoja na jeshi la Uganda. Ndege ziliruka katika njia ya kimataifa kupita Red sea na kwa muda mwingi wa safari yake zililazimika kuruka si zaidi ya mita 30 angani (kuna muda inaelezwa kuwa iliwabidi kuruka mpaka futi 35 kutoka ardhini) ili kuepuka kuonekana na rada za Misi, Sudan na Saud Arabia. Safari ilikuwa ngumu haswa hasa ukizingatia kuwa ndege kubwa kama zile zikiruka katika usawa wa karibu hivyo na ardhi mtikisiko unakuwa mkubwa haswa ndani ya ndege. Waliokaribia mchepuko wa kusini wa Red Sea ndege zilikata kona na kupita kusini mwa nchi ya Djibouti. Kutokea hapo walielekea mpaka kutokea kaskazini mashariki mwa Nairobi, Kenya na kisha Somalia na kupita eneo la Ogaden nchini Ethiopia. Kutoka hapo wakapinda magharibi kufuata bonde la ufa ba mpaka kutokea juu ya ziwa Victoria. Ikumbukwe kwamba kati ya ndege zile mbili za Boeing 707 zilizokuwa zinafuatia nyuma na zile Harcules nne, moja ambayo ilipangwa itumike kama hospitali ilitua Nairobi, uwanja wa ndege wa Jomo Kenyetta. Ile nyingine ambayo nimeeleza kwamba ilipangwa itumike kama ‘command post’ ilikuwa inaruka kuzunguka uwanja wa ndege wa Entebbe wakati ndege zile za kijeshi zikitua. Ndege hii (command post) haikutua uwanjani na kamanda mkuu wa oparesheni hii Meja Jenerali Yekutiel Adam alikuwa ndani yake kuwaongoza wenzake walipo ardhini. Mnamo saa 23:00 ndege za kijeshi za Israel zilitua kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe huku milango ya nyuma ya mizigo kwenye ndege ikiwa wazi. Hapa nieleze kidogo… Mbinu kuu ambayo jeshi la Israel walikuwa wanataka kuitumia ili kufanikisha Oparesheni hii ilikuwa ni kufanya shambulio la kushtukiza. ! Kivipi? Katika sehemu iliyopita nilieleza kuwa Ehud Barak baada ya kukusanya intelijensia za kutosha akiwa Kenya, aliwaeleza wenzake kuwa wapakie gari aina ya Mercedes Limousine inayofanana kabisa na ile ambayo inatumiwa na Rais Idd Amin a Uganda ambayo ilikuwa na rangi nyeusi. Kwa kuwa walifahamu Rais Idd Amin alikuwa safarini nchini Mauritius kukabidhi uenyekiti wa O.A.U, hivyo walitaka kuigiza kana kwamba Idd Amin alikuwa anarejea kutoka safarini na alikuwa anaenda kutembelea mateka pale uwanja wa ndege kama ambavyo ilikuwa kawaida yake. Hii ndio sababu ya wao kwenda na ile gari nyeusi aina ya Mercedes Limousine pamoja na Land Rover… ambavyo ndivyo ilikuwa namna ambavyo Idd Amin alikuwa anapenda kwenda kutembelea pale uwanjani…. Mercedes Limousine ambayo ina mbeba yeye na nyuma yake gari aina ya Land Rover iliyo na walinzi wake. Kwa hiyo ndege ya kwanza ya jeshi la Israel ilipotua kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe ambao kwa muda huo wa saa tano usiku kulikuwa na giza tupu taa zote za uwanja wa ndege zikiwa zimezimwa. Ndege ilitua ikiwa imefunguliwa mlango wa nyuma wa mizigo, ambako ilitoka gari aina ya Mercedes Limousine ikiongozana na Landa Rover na moja kwa zikaendeshwa kuelekea kwenye geti la Terminal ambayo mateka walikuwa wamehifadhiwa. Walikuwa wamefaulu kuigiza kabisa msafara wa Idd amin unavyokuwa. Msafara ulikuwa unafanana kabisa na ule wa Idd Amin lakini tofauti ilikuwa kwamba gari hizi ndani yake kuliwa na makomamdo. Jambo la ajabu ni kwamba walipofika mbele ya geti la Terminal badala ya kuruhusiwa kupita, wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanalinda getini waliinua bunduki zao na kuwanyoosha kuelea magari haya. Walichokuwa hawakijua makomando hawa ambacho wanajeshi hawa waliokuwa wanalinda hapa uwanjani walikijua ni kwamba, Siku moja ya kabla ya Idd Amin kwenda Mauritus alibadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi kwenda rangi nyeupe. Kwa hiyo wanajeshi hawa wa Uganda walipoona magari haya walikuwa wanajua fika kuwa huyu hakuwa Rais wao Idd Amin. Itaendelea #TheBOLD_JF
    0 Commenti ·0 condivisioni ·1K Views
Pagine in Evidenza