Mahakama Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imebatilisha hukumu ya kifo waliyopewa Raia watatu (3) wa Marekani kwa makosa ya jinai, ugaidi na kujaribu kuipindua Serikali ya Nchi hiyo.
Shirika la Habari la Reuters, limeripoti leo Aprili 2,2025, kuwa taarifa ya Ikulu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeeleza watatu hao sasa hawatotumikia adhabu ya kifo badala yake watatumikia kifungo cha maisha jela. Walikuwa miongoni mwa Watu (37) waliohukumiwa kifo Septemba mwaka jana (2024) na Mahakama ya Kijeshi Nchini DR Congo katika mashitaka hayo ambayo hata hivyo waliyakanusha.
Watatu hao ambao ni Mtoto wa Raia wa Marekani mwenye asili ya DR Congo, Christian Malanga, Marcel Malanga Malu, Rafiki zake Tylor Thomson na Zalman Polun Benjamin, walipewa msamaha kutoka kwa Rais Felix Tshisekedi. Walishtakiwa kwa kuongoza genge la uhalifu lililotekeleza shambulio dhidi ya ikulu na makazi ya Mshirika wa Rais wa Nchi nchi hiyo, Mei, 2024.
Katika Taarifa iliyosomwa na Msemaji wa Rais Félix Tshisekedi, Tyna Salama kwenye Televisheni ya Taifa, imesema kuwa Rais Tshisekedi ametoa msamaha huo kwa kubatilisha hukumu ya kifo kwa Rais hao na kuwa ya kifungo cha maisha Jela kwa sababu ya kudumisha mahusiano mazuri kimataifa na Nchi ya Marekani.
Kubatilishwa kwa hukumu hiyo kunakuja kabla ya ziara ya Mshauri mpya Mwandamizi wa Marekani barani Afrika, Massad Boulos. Ambapo ziara hiyo ililenga kwenda DR Congo.
Read more

Mahakama Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 imebatilisha hukumu ya kifo waliyopewa Raia watatu (3) wa Marekani 🇺🇸 kwa makosa ya jinai, ugaidi na kujaribu kuipindua Serikali ya Nchi hiyo.
Shirika la Habari la Reuters, limeripoti leo Aprili 2,2025, kuwa taarifa ya Ikulu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeeleza watatu hao sasa hawatotumikia adhabu ya kifo badala yake watatumikia kifungo cha maisha jela. Walikuwa miongoni mwa Watu (37) waliohukumiwa kifo Septemba mwaka jana (2024) na Mahakama ya Kijeshi Nchini DR Congo katika mashitaka hayo ambayo hata hivyo waliyakanusha.
Watatu hao ambao ni Mtoto wa Raia wa Marekani mwenye asili ya DR Congo, Christian Malanga, Marcel Malanga Malu, Rafiki zake Tylor Thomson na Zalman Polun Benjamin, walipewa msamaha kutoka kwa Rais Felix Tshisekedi. Walishtakiwa kwa kuongoza genge la uhalifu lililotekeleza shambulio dhidi ya ikulu na makazi ya Mshirika wa Rais wa Nchi nchi hiyo, Mei, 2024.
Katika Taarifa iliyosomwa na Msemaji wa Rais Félix Tshisekedi, Tyna Salama kwenye Televisheni ya Taifa, imesema kuwa Rais Tshisekedi ametoa msamaha huo kwa kubatilisha hukumu ya kifo kwa Rais hao na kuwa ya kifungo cha maisha Jela kwa sababu ya kudumisha mahusiano mazuri kimataifa na Nchi ya Marekani.
Kubatilishwa kwa hukumu hiyo kunakuja kabla ya ziara ya Mshauri mpya Mwandamizi wa Marekani barani Afrika, Massad Boulos. Ambapo ziara hiyo ililenga kwenda DR Congo.
0 Comments
·0 Shares
·11 Views