Upgrade to Pro

  • "Tukiwa katika majonzi na kazi ikiendelea katika kuwatafuta ndugu zetu ambao tunaamini bado wako hai kufuatia kuporomoka kwa jengo eneo la Kariakoo, ninawapongeza vijana wetu Taifa Stars kwa ushindi na kufuzu kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025. Mmeandika historia kwa Taifa letu, ikiwa ni mara yetu ya nne kufikia mafanikio haya makubwa katika kipindi cha zaidi ya miaka arobaini.

    Hongera kwa kazi nzuri nyote tuliowapa dhamana kusimama na vijana wetu kukamilisha jukumu hili katika Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Benchi la Ufundi na Watanzania wote kwa kuendelea kuipenda, kuithamini na kuipa hamasa Timu ya Taifa.

    Baada ya ushindi huu, sasa tujikite katika maandalizi mazuri zaidi kwa mashindano yajayo" - Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania.

    "Tukiwa katika majonzi na kazi ikiendelea katika kuwatafuta ndugu zetu ambao tunaamini bado wako hai kufuatia kuporomoka kwa jengo eneo la Kariakoo, ninawapongeza vijana wetu Taifa Stars kwa ushindi na kufuzu kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025. Mmeandika historia kwa Taifa letu, ikiwa ni mara yetu ya nne kufikia mafanikio haya makubwa katika kipindi cha zaidi ya miaka arobaini. Hongera kwa kazi nzuri nyote tuliowapa dhamana kusimama na vijana wetu kukamilisha jukumu hili katika Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Benchi la Ufundi na Watanzania wote kwa kuendelea kuipenda, kuithamini na kuipa hamasa Timu ya Taifa. Baada ya ushindi huu, sasa tujikite katika maandalizi mazuri zaidi kwa mashindano yajayo" - Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania.
    ·87 Views
  • KABLA HUJATENDA CHOCHOTE KILE JIULIZE HIVI...

    Siku zote katika maisha yako kabla hujatenda kitu chochote, kabla hujasema kitu chochote, jiulize kitu unachotaka kutenda au kitu unachotaka kusema je, kitaleta matokeo chanya kwako au hata kwa wengine?

    Sio kwa sababu unayo nafasi nzuri ya kutenda au kusema hiyo ikawa na maana kwako ufanye au useme tu hata mambo yanayoumiza wengine. Unatakiwa kuwa makini na kuzingatia ni nini matokea ya kile ambacho unakwenda kutenda au kukizungumza.

    Ni dhahiri wapo watu ambao moja kwa moja utawaumiza, kama utatenda au kusema maneno ya hasi, hata kama hujui jinsi unavyowaumiza. Pia uelewe wapo watu utakaowaponya kama utaamua kusema au kutenda matendo chanya ambayo yana msaada mkubwa katika maisha yao kwa ujumla.

    Kila wakati, unayo nafasi nzuri sana ya kutoa mazuri katika dunia, ingawa uamuzi ni wako. Acha kutenda au kusema mara moja kile kinachokujia kichwani mwako, Jipe muda wa kukifikiri kitu hicho na kujua ni nini matokeo yake katika maisha yako na ya wengine.

    Kuanzia leo jifunze kutoa yale mazuri katika hii dunia, jenga utamaduni wa kutoa yale matendo au maneno mazuri iwe sehemu ya utamaduni wako. Ukifanya hivyo dunia itakupa mazuri pia na utafurahia maisha yako kutokana na mazuri unayoyatoa.

    Simama imara katika kuhakikisha hili unalitenda. Kumbuka sana TOA YALE MAZURI KATIKA MAISHA YAKO, GIVE GOODNESS TO LIFE, ukifanikisha hili furaha na mafanikio vitakuwa upande wako.
    KABLA HUJATENDA CHOCHOTE KILE JIULIZE HIVI... Siku zote katika maisha yako kabla hujatenda kitu chochote, kabla hujasema kitu chochote, jiulize kitu unachotaka kutenda au kitu unachotaka kusema je, kitaleta matokeo chanya kwako au hata kwa wengine? Sio kwa sababu unayo nafasi nzuri ya kutenda au kusema hiyo ikawa na maana kwako ufanye au useme tu hata mambo yanayoumiza wengine. Unatakiwa kuwa makini na kuzingatia ni nini matokea ya kile ambacho unakwenda kutenda au kukizungumza. Ni dhahiri wapo watu ambao moja kwa moja utawaumiza, kama utatenda au kusema maneno ya hasi, hata kama hujui jinsi unavyowaumiza. Pia uelewe wapo watu utakaowaponya kama utaamua kusema au kutenda matendo chanya ambayo yana msaada mkubwa katika maisha yao kwa ujumla. Kila wakati, unayo nafasi nzuri sana ya kutoa mazuri katika dunia, ingawa uamuzi ni wako. Acha kutenda au kusema mara moja kile kinachokujia kichwani mwako, Jipe muda wa kukifikiri kitu hicho na kujua ni nini matokeo yake katika maisha yako na ya wengine. Kuanzia leo jifunze kutoa yale mazuri katika hii dunia, jenga utamaduni wa kutoa yale matendo au maneno mazuri iwe sehemu ya utamaduni wako. Ukifanya hivyo dunia itakupa mazuri pia na utafurahia maisha yako kutokana na mazuri unayoyatoa. Simama imara katika kuhakikisha hili unalitenda. Kumbuka sana TOA YALE MAZURI KATIKA MAISHA YAKO, GIVE GOODNESS TO LIFE, ukifanikisha hili furaha na mafanikio vitakuwa upande wako.
    Like
    1
    ·187 Views
  • Rais wa Young Africans SC na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vilabu Afrika Eng. Hersi Said ameshinda Tuzo ya mwanamichezo mwenye mchango kwenye maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika.

    Shamrashamra za kutunuku tuzo hizi za Nigeria-France Sports Awards, zilifanyika juzi jijini Paris, Ufaransa na Tuzo hiyo ya Rais Hersi ilipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Mwakilishi wa Kudumu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Mhe.Ali Jabir Mwadini.

    #timuyawananchi
    #daimambelenyumamwiko.
    Rais wa Young Africans SC na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vilabu Afrika Eng. Hersi Said ameshinda Tuzo ya mwanamichezo mwenye mchango kwenye maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika. Shamrashamra za kutunuku tuzo hizi za Nigeria-France Sports Awards, zilifanyika juzi jijini Paris, Ufaransa na Tuzo hiyo ya Rais Hersi ilipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Mwakilishi wa Kudumu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Mhe.Ali Jabir Mwadini. #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko.
    Like
    Love
    3
    3 Commentarios ·462 Views
  • Ukuta Mkuu wa China: Safari ya Kustaajabisha Kwenye Historia ya Kale

    Ndoto ya kutembelea Ukuta Mkuu wa China imekuwa moyoni mwangu kwa muda mrefu. Ukuta huu mkubwa, unaoenea kwa zaidi ya kilomita 21,000, ni alama ya kuvutia ya historia ya kale ya China na ufundi wa ajabu. Picha za mandhari ya kuvutia na maoni ya kupendeza yamenifanya nitamani kutembea kwenye mawe haya ya zamani na kuhisi ukuu wake kwa karibu.

    Ninafikiria kutembelea sehemu ya Mutianyu ya Ukuta Mkuu. Sehemu hii iko karibu na Beijing na inajulikana kwa mandhari yake nzuri na urahisi wa kufikia. Natumai kupanda hadi kileleni na kufurahia mandhari ya kuvutia ya milima na misitu inayozunguka. Pia napenda kutembelea minara ya ulinzi na kujifunza kuhusu historia ya Ukuta Mkuu na umuhimu wake kwa China.

    Safari hii itakuwa zaidi ya kutembelea tu kivutio maarufu. Ninaamini itakuwa safari ya kugundua utamaduni wa China, historia yake tajiri, na uzuri wake wa asili. Nina hamu ya kukutana na watu wa China, kujaribu vyakula vyao vya kupendeza, na kujifunza kuhusu mila zao za kale.

    Ninaamini Ukuta Mkuu wa China ni mahali pazuri pa kuanza safari yangu ya kugundua China. Nina hakika itakuwa uzoefu usioweza kusahaulika ambao utaniacha na kumbukumbu za kudumu.

    #socialpop #utalii #China #UkutaMkuuwaChina #historia #utamaduni #safari
    Ukuta Mkuu wa China: Safari ya Kustaajabisha Kwenye Historia ya Kale Ndoto ya kutembelea Ukuta Mkuu wa China imekuwa moyoni mwangu kwa muda mrefu. Ukuta huu mkubwa, unaoenea kwa zaidi ya kilomita 21,000, ni alama ya kuvutia ya historia ya kale ya China na ufundi wa ajabu. Picha za mandhari ya kuvutia na maoni ya kupendeza yamenifanya nitamani kutembea kwenye mawe haya ya zamani na kuhisi ukuu wake kwa karibu. Ninafikiria kutembelea sehemu ya Mutianyu ya Ukuta Mkuu. Sehemu hii iko karibu na Beijing na inajulikana kwa mandhari yake nzuri na urahisi wa kufikia. Natumai kupanda hadi kileleni na kufurahia mandhari ya kuvutia ya milima na misitu inayozunguka. Pia napenda kutembelea minara ya ulinzi na kujifunza kuhusu historia ya Ukuta Mkuu na umuhimu wake kwa China. Safari hii itakuwa zaidi ya kutembelea tu kivutio maarufu. Ninaamini itakuwa safari ya kugundua utamaduni wa China, historia yake tajiri, na uzuri wake wa asili. Nina hamu ya kukutana na watu wa China, kujaribu vyakula vyao vya kupendeza, na kujifunza kuhusu mila zao za kale. Ninaamini Ukuta Mkuu wa China ni mahali pazuri pa kuanza safari yangu ya kugundua China. Nina hakika itakuwa uzoefu usioweza kusahaulika ambao utaniacha na kumbukumbu za kudumu. #socialpop #utalii #China #UkutaMkuuwaChina #historia #utamaduni #safari
    Love
    Like
    7
    1 Commentarios ·396 Views
  • Bad granny ( Utakuja uonekane chizi ) ikitokea Umekutananae uso kwa macho .. kabra ya kukimbia .. Toa salamu kwanza Bibi shikamoo .. akikukimbiza ndo ukimbie... sio unajikimbiza kimbiza tu utaonekana chizi bure Huwo ni utamaduni wa kawaida tu ila bado sija jua bado ni kabira gan? hili
    Bad granny 😂😂 ( Utakuja uonekane chizi ) ikitokea Umekutananae uso kwa macho .. kabra ya kukimbia😃 .. Toa salamu kwanza Bibi shikamoo .. akikukimbiza ndo ukimbie😂... sio unajikimbiza kimbiza tu utaonekana chizi bure 😂😂 Huwo ni utamaduni wa kawaida tu 😂😂 ila bado sija jua bado ni kabira gan? hili 🤣🤣🤣
    Love
    Haha
    2
    ·131 Views