Atualize para o Pro

  • Mwimbaji Staa Harmonize amesema May 25,2024 anatarajia kuzindua album yake ya tano katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambayo ameipa jina la ‘Muziki wa Samia’ akiwa na lengo kupongeza na kuunga mkono kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uongozi wake.

    Harmonize amesema album hiyo ni ya mwisho kwake na kusisitiza kuwa ameimba sana kuliko kawaida na ametengezeneza nyimbo 10 ambazo zote zinamlenga Rais Samia hivyo baada ya album hiyo atapumzika na kurefresh huku akiwa anaachia wimbo mmojammoja na sio album tena.

    Harmo amesema siku ya uzinduzi huo itakuwa ni usiku wa mialiko na hakutakuwa na viingilio “Tumekusanya mazuri yote ambayo yanafanywa na Rais Samia na Serikali na kuyaweka kwenye kitabu kimoja cha kumbukumbu ambacho kitaishi milele kinachoitwa Muziki wa Samia”
    #MillardAyoENT
    Mwimbaji Staa Harmonize amesema May 25,2024 anatarajia kuzindua album yake ya tano katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambayo ameipa jina la ‘Muziki wa Samia’ akiwa na lengo kupongeza na kuunga mkono kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uongozi wake. Harmonize amesema album hiyo ni ya mwisho kwake na kusisitiza kuwa ameimba sana kuliko kawaida na ametengezeneza nyimbo 10 ambazo zote zinamlenga Rais Samia hivyo baada ya album hiyo atapumzika na kurefresh huku akiwa anaachia wimbo mmojammoja na sio album tena. Harmo amesema siku ya uzinduzi huo itakuwa ni usiku wa mialiko na hakutakuwa na viingilio “Tumekusanya mazuri yote ambayo yanafanywa na Rais Samia na Serikali na kuyaweka kwenye kitabu kimoja cha kumbukumbu ambacho kitaishi milele kinachoitwa Muziki wa Samia” #MillardAyoENT
    Like
    Love
    8
    8 Comentários ·555 Visualizações
  • Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa taarifa kwa Wanafunzi wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu na umma kuwa inakamilisha malipo ya fedha za kujikimu (Chakula na Malazi) kwa robo ya nne (Quarter IV) na Wanafunzi watarajie kupokea fedha hizo kuanzia kesho Jumatatu May 20, 2024.

    Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia amesema ametoa ufafanuzi huo baada ya maoni na maswali yanayoulizwa na Wanafunzi Wanufaika kupitia barua pepe, mitandao ya kijamii kuhusu hatua ya malipo iliyofikiwa hususan kwa vyuo ambavyo tarehe za malipo (due dates) ya robo ya nne zimefika.

    “Tunawasihi Wanafunzi kuwa watulivu na kuwasiliana na Maafisa Mikopo waliopo katika Vyuo vyote Nchini pale watakapokuwa na maoni au kuhitaji ufafanuzi, katika mwaka wa masomo 2023/2024, Serikali imetenga Tsh. 786 bilioni kwa ajili ya mikopo na ruzuku kwa Wanafunzi zaidi ya 220,000 wanaosoma shahada na stashahada mbalimbali katika Taasisi za elimu Nchini”
    #MillardAyoUPDATES
    Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa taarifa kwa Wanafunzi wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu na umma kuwa inakamilisha malipo ya fedha za kujikimu (Chakula na Malazi) kwa robo ya nne (Quarter IV) na Wanafunzi watarajie kupokea fedha hizo kuanzia kesho Jumatatu May 20, 2024. Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia amesema ametoa ufafanuzi huo baada ya maoni na maswali yanayoulizwa na Wanafunzi Wanufaika kupitia barua pepe, mitandao ya kijamii kuhusu hatua ya malipo iliyofikiwa hususan kwa vyuo ambavyo tarehe za malipo (due dates) ya robo ya nne zimefika. “Tunawasihi Wanafunzi kuwa watulivu na kuwasiliana na Maafisa Mikopo waliopo katika Vyuo vyote Nchini pale watakapokuwa na maoni au kuhitaji ufafanuzi, katika mwaka wa masomo 2023/2024, Serikali imetenga Tsh. 786 bilioni kwa ajili ya mikopo na ruzuku kwa Wanafunzi zaidi ya 220,000 wanaosoma shahada na stashahada mbalimbali katika Taasisi za elimu Nchini” #MillardAyoUPDATES
    Like
    Love
    5
    4 Comentários ·455 Visualizações
  • Thanks for the support from you guys you really mean something to me
    Nawapenda sanaa,
    #socialpop @social pop #millardayo
    Thanks🙏 for the support from you guys you really mean something to me👊💯 Nawapenda sanaa,💗 #socialpop @social pop #millardayo
    Like
    Love
    9
    ·381 Visualizações ·81 Visualizações
  • Dereva wa pikipiki ya Afisa mifugo Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, Abel Adamson Mwaipopo (25) amefariki Dunia baada kumgonga ndege aina ya bundi na kisha pikipiki yake kupoteza mwelekeo na kuanguka na hatimaye kupoteza maisha yake.

    Mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando amesema tukio hilo limetokea mapema leo katika eneo la Sindeni jirani na kona ya PRS ambapo Dereva huyo alikuwa akiendesha pikipiki yenye namba za usajili STM 0232 .

    Msando amesema “Kwanza naomba nitolee ufafanuzi jambo hili kwani aliyefariki sio Afusa mifugo kama wengi walivyosema kwani Afisa mifugo wetu wa Wilaya ni Mwanamke na aliyefariki ni Mwanaume Dereva ambaye anamwendesha Afisa mifugo”

    “Ajali ni kama ajali nyingime lakini akishahusishwa bundi mara zote tayari kunakuwa na hizo imani za kishirikina na hofu kwa Watu kwamba amegonga bundi kafa na yeye mwenye amekufa lakini vilele inawezekana kwa kiasi kikubwa labda alivyomuona bundi katika kujaribu kumkwepa hakuchukua tahadhari akapata ajali ni uwezekano vilevile hakuwa amevaa kofia ngumu hivyo katika kuanguka akajigonga akapata madhara akafariki hivyo inawezekana ikawa ni ajali ya kawaida lakini kwasababu imemuhusisha bundi lazima ita letataharuki kuwa inahusiana na mambo ya kishirikina”

    Msando amesema kama Serikali ngazi ya Wilaya wana amini ni ajali kama ajali nyingine zinazotokea barabarani na hivyo ametoa wito kwa wale wote wanao tumia vyombo vya moto hususa pikipiki kuvaa kofia ngumu na kuchukua tadhari pindi wanapo kuwa barabarani na kutokwenda kwa spidi ili kuweza kuepuka kupata ajali. #MillardAyoUPDATES
    Dereva wa pikipiki ya Afisa mifugo Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, Abel Adamson Mwaipopo (25) amefariki Dunia baada kumgonga ndege aina ya bundi na kisha pikipiki yake kupoteza mwelekeo na kuanguka na hatimaye kupoteza maisha yake. Mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando amesema tukio hilo limetokea mapema leo katika eneo la Sindeni jirani na kona ya PRS ambapo Dereva huyo alikuwa akiendesha pikipiki yenye namba za usajili STM 0232 . Msando amesema “Kwanza naomba nitolee ufafanuzi jambo hili kwani aliyefariki sio Afusa mifugo kama wengi walivyosema kwani Afisa mifugo wetu wa Wilaya ni Mwanamke na aliyefariki ni Mwanaume Dereva ambaye anamwendesha Afisa mifugo” “Ajali ni kama ajali nyingime lakini akishahusishwa bundi mara zote tayari kunakuwa na hizo imani za kishirikina na hofu kwa Watu kwamba amegonga bundi kafa na yeye mwenye amekufa lakini vilele inawezekana kwa kiasi kikubwa labda alivyomuona bundi katika kujaribu kumkwepa hakuchukua tahadhari akapata ajali ni uwezekano vilevile hakuwa amevaa kofia ngumu hivyo katika kuanguka akajigonga akapata madhara akafariki hivyo inawezekana ikawa ni ajali ya kawaida lakini kwasababu imemuhusisha bundi lazima ita letataharuki kuwa inahusiana na mambo ya kishirikina” Msando amesema kama Serikali ngazi ya Wilaya wana amini ni ajali kama ajali nyingine zinazotokea barabarani na hivyo ametoa wito kwa wale wote wanao tumia vyombo vya moto hususa pikipiki kuvaa kofia ngumu na kuchukua tadhari pindi wanapo kuwa barabarani na kutokwenda kwa spidi ili kuweza kuepuka kupata ajali. #MillardAyoUPDATES
    Like
    Love
    Sad
    12
    8 Comentários ·545 Visualizações
  • Shindano linalofanyika kila mwaka liitwalo ‘Space-out’ Nchini Korea Kusini hutumika kusaka aliyekuwa bora kwenye sekta ya ‘kukaa tu bila kufanya kitu chochote’ ambapo Mshiriki haruhusiwi kusinzia, kuangalia simu yake au kuzungumza kwa dakika 90.

    Unaambiwa hadi mapigo ya moyo ya Washiriki hufuatiliwa kwa makini huku Watazamaji wakipewa nafasi ya kuwapigia kura Washiriki 10 wanaowapenda ambapo yeyote aliye na mapigo ya moyo yaliyotulia zaidi kati ya hao 10 anatunukiwa kombe.

    Zaidi ya Watu 4,000 waliomba kushiriki katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Serikali ya jiji la Seoul ambapo Washiriki 117 waliochaguliwa walikuwa kwenye rika la kuanzia mtoto wa darasa la pili hadi watu wenye umri wa miaka 60.

    Tangu shindano la kwanza la ‘Space-out’ lifanyike jijini Seoul mwaka 2014 umaarufu wake umezidi kuwa mkubwa zaidi kimataifa ambako Miji mbalimbali kama vile Beijing nchini China, Rotterdam Uholanzi, Taipei, Hong Kong na Tokyo, Japan yamefanya shindano hilo. #MillardAyoUPDATES
    Shindano linalofanyika kila mwaka liitwalo ‘Space-out’ Nchini Korea Kusini hutumika kusaka aliyekuwa bora kwenye sekta ya ‘kukaa tu bila kufanya kitu chochote’ ambapo Mshiriki haruhusiwi kusinzia, kuangalia simu yake au kuzungumza kwa dakika 90. Unaambiwa hadi mapigo ya moyo ya Washiriki hufuatiliwa kwa makini huku Watazamaji wakipewa nafasi ya kuwapigia kura Washiriki 10 wanaowapenda ambapo yeyote aliye na mapigo ya moyo yaliyotulia zaidi kati ya hao 10 anatunukiwa kombe. Zaidi ya Watu 4,000 waliomba kushiriki katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Serikali ya jiji la Seoul ambapo Washiriki 117 waliochaguliwa walikuwa kwenye rika la kuanzia mtoto wa darasa la pili hadi watu wenye umri wa miaka 60. Tangu shindano la kwanza la ‘Space-out’ lifanyike jijini Seoul mwaka 2014 umaarufu wake umezidi kuwa mkubwa zaidi kimataifa ambako Miji mbalimbali kama vile Beijing nchini China, Rotterdam Uholanzi, Taipei, Hong Kong na Tokyo, Japan yamefanya shindano hilo. #MillardAyoUPDATES
    Like
    Love
    Haha
    Wow
    14
    4 Comentários ·577 Visualizações
  • #millardayo
    #millardayo
    Like
    2
    1 Comentários ·323 Visualizações
  • "Kifuta jasho" ni maneno mawili maarufu sana kuyakuta midomoni mwa Watu ambao wanazitazama kesho zao kwa kuogopa kuadhirika, Watu wanaoogopa kutaabika huko mbeleni na kujutia nguvu za ujana wao, ni herufi kumi na moja ambazo ukizizingatia zinaweza kukupatia kitambaa cha bei ghali zaidi utapofika muda wa kujifuta jasho ambapo bei hiyo kubwa itatokana na maamuzi yako ya leo kwenye swala la kujiwekea akiba.

    Nimeyasema haya baada ya kushuhudia Benki ya NMB ikituletea bidhaa mpya kabisa sokoni katika sekta ya kibenki iitwayo "NMB JIWEKEE" ikiwa ni akaunti maalum ya kidijitali inayolenga kuleta ukombozi wa maisha ya baadaye ya Watu walio nje ya mfumo rasmi wa ajira kama vile Wafanyabiashara wadogo na wa kati, watoa huduma wa sekta ya usafirishaji kwa pikipiki 'bodaboda', Mama na Baba lishe na hata Waajiriwa wanaopenda kujiongezea vyanzo vya akiba ya uzee.

    Uzinduzi wa NMB Jiwekee uliowakutanisha pamoja Watu mbalimbali waliokula kiapo cha 'Chama la Watunza Pesa,' ulifanyika jijini Dar es salaam Jumatatu May 13 na kuzinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Deogratius Ndejembi huku mwenyeji wa hafla hiyo akiwa ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi.

    Akizingumza katika uzinduzi huo uliofanyika kwa mfumo wa kipindi cha runinga kilichoongozwa na Mtangazaji Millard Ayo, Waziri Ndejembi alisema NMB Jiwekee inayoambatana na faida lukuki kwa Wajasiriamali na kada zingine, ni mwendelezo wa juhudi za wazi za Taasisi hiyo kuunga mkono jitihada za Serikali kuyawezesha makundi maalum ya kijamii.

    "Kwa jambo hili Taasisi nyingine zinapaswa kufuata nyayo za NMB kwa kuanzisha huduma bora na rahisi, nafuu na salama kama hizi, sasa NMB ijikite katika kutoa elimu kwa Watanzania juu ya umuhimu wa huduma hii mpya, Serikali haiwezi 'ku-cover' kila kitu ndio maana tunasisitiza nguvu za Wadau hususani Taasisi za fedha katika kuwaunganisha Watanzania na huduma Jumuishi za fedha, zaidi niwapongeze NMB kwa kuwapa uhuru Watumiaji wa NMB Jiwekee wa kuchagua asilimia za kujitunzia kutokana na matumizi ya fedha zilizo kwenye akaunti zao" —— Ndejembi. #MillardAyoUPDATES
    "Kifuta jasho" ni maneno mawili maarufu sana kuyakuta midomoni mwa Watu ambao wanazitazama kesho zao kwa kuogopa kuadhirika, Watu wanaoogopa kutaabika huko mbeleni na kujutia nguvu za ujana wao, ni herufi kumi na moja ambazo ukizizingatia zinaweza kukupatia kitambaa cha bei ghali zaidi utapofika muda wa kujifuta jasho ambapo bei hiyo kubwa itatokana na maamuzi yako ya leo kwenye swala la kujiwekea akiba. Nimeyasema haya baada ya kushuhudia Benki ya NMB ikituletea bidhaa mpya kabisa sokoni katika sekta ya kibenki iitwayo "NMB JIWEKEE" ikiwa ni akaunti maalum ya kidijitali inayolenga kuleta ukombozi wa maisha ya baadaye ya Watu walio nje ya mfumo rasmi wa ajira kama vile Wafanyabiashara wadogo na wa kati, watoa huduma wa sekta ya usafirishaji kwa pikipiki 'bodaboda', Mama na Baba lishe na hata Waajiriwa wanaopenda kujiongezea vyanzo vya akiba ya uzee. Uzinduzi wa NMB Jiwekee uliowakutanisha pamoja Watu mbalimbali waliokula kiapo cha 'Chama la Watunza Pesa,' ulifanyika jijini Dar es salaam Jumatatu May 13 na kuzinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Deogratius Ndejembi huku mwenyeji wa hafla hiyo akiwa ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi. Akizingumza katika uzinduzi huo uliofanyika kwa mfumo wa kipindi cha runinga kilichoongozwa na Mtangazaji Millard Ayo, Waziri Ndejembi alisema NMB Jiwekee inayoambatana na faida lukuki kwa Wajasiriamali na kada zingine, ni mwendelezo wa juhudi za wazi za Taasisi hiyo kuunga mkono jitihada za Serikali kuyawezesha makundi maalum ya kijamii. "Kwa jambo hili Taasisi nyingine zinapaswa kufuata nyayo za NMB kwa kuanzisha huduma bora na rahisi, nafuu na salama kama hizi, sasa NMB ijikite katika kutoa elimu kwa Watanzania juu ya umuhimu wa huduma hii mpya, Serikali haiwezi 'ku-cover' kila kitu ndio maana tunasisitiza nguvu za Wadau hususani Taasisi za fedha katika kuwaunganisha Watanzania na huduma Jumuishi za fedha, zaidi niwapongeze NMB kwa kuwapa uhuru Watumiaji wa NMB Jiwekee wa kuchagua asilimia za kujitunzia kutokana na matumizi ya fedha zilizo kwenye akaunti zao" —— Ndejembi. #MillardAyoUPDATES
    Like
    Love
    Yay
    Angry
    9
    6 Comentários ·569 Visualizações
  • Taarifa ya hali ya dawa za kulevya Duniani ya mwaka 2023 imeonesha kuwa takribani Watu milioni 219 walitumia bangi mwaka 2021, sawa na 4% ya idadi ya Watu duniani ambapo idadi hiyo imeongezeka kwa 21% katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

    Taarifa hiyo ambayo imeandaliwa na Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Nchini (DCEA) na kuwasilishwa Bungeni Jijini Dodoma leo May 16,2024 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenista J. Mhagama inaonesha kuwa matumizi ya bangi yanaendelea kuongezeka kwa kasi duniani kote na kwamba matumizi ya bangi yameendelea kuwa ya juu zaidi Amerika Kaskazini ambapo 17.4% ya Watu wenye umri kati ya miaka 15 hadi 64 walitumia bangi mwaka 2021.

    Barani Afrika taarifa imeonesha kuwa Afrika Kaskazini ni kitovu cha biashara haramu ya bangi iliyosindikwa (cannabis resin) kuelekea Ulaya Magharibi na matumizi ya bangi ni ya juu katika Afrika Magharibi na Kati na kufikia mwaka 2021, karibu 10% ya Watu (milioni 30) waliripotiwa kutumia bangi katika kipindi cha mwaka 2020, hususan katika Nchi ya Nigeria.

    Nchi nyingi Afrika zina uzalishaji wa bangi na imeendelea kuwa moja ya dawa inayosababisha athari kubwa miongoni mwa Watu wanaopatiwa matibabu ya uraibu. #MillardAyoUPDATES
    Taarifa ya hali ya dawa za kulevya Duniani ya mwaka 2023 imeonesha kuwa takribani Watu milioni 219 walitumia bangi mwaka 2021, sawa na 4% ya idadi ya Watu duniani ambapo idadi hiyo imeongezeka kwa 21% katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Taarifa hiyo ambayo imeandaliwa na Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Nchini (DCEA) na kuwasilishwa Bungeni Jijini Dodoma leo May 16,2024 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenista J. Mhagama inaonesha kuwa matumizi ya bangi yanaendelea kuongezeka kwa kasi duniani kote na kwamba matumizi ya bangi yameendelea kuwa ya juu zaidi Amerika Kaskazini ambapo 17.4% ya Watu wenye umri kati ya miaka 15 hadi 64 walitumia bangi mwaka 2021. Barani Afrika taarifa imeonesha kuwa Afrika Kaskazini ni kitovu cha biashara haramu ya bangi iliyosindikwa (cannabis resin) kuelekea Ulaya Magharibi na matumizi ya bangi ni ya juu katika Afrika Magharibi na Kati na kufikia mwaka 2021, karibu 10% ya Watu (milioni 30) waliripotiwa kutumia bangi katika kipindi cha mwaka 2020, hususan katika Nchi ya Nigeria. Nchi nyingi Afrika zina uzalishaji wa bangi na imeendelea kuwa moja ya dawa inayosababisha athari kubwa miongoni mwa Watu wanaopatiwa matibabu ya uraibu. #MillardAyoUPDATES
    Like
    Love
    Wow
    11
    3 Comentários ·526 Visualizações
  • Benki ya NMB imetanua wigo wa kushiriki katika masoko ya mitaji kimataifa kwa kuiorodhesha Hati fungani ya NMB Jamii (NMB Jamii Bond) katika Soko la Hisa la London (LSE) ambapo hatua hii inaifanya NMB kuwa Taasisi ya kwanza Tanzania kuwa na hati fungani katika soko hilo na Benki ya kwanza Afrika Mashariki kuorodhesha Hatifungani ya Uendelevu katika soko la Hisa la London.

    Hati Fungani ya NMB Jamii inalenga kuchochea uwekezaji katika miradi yenye tija kijamii na kimazingira ambapo toleo la Dola za Kimarekani milioni 73 ndio limeorodheshwa kwa Wawekezaji wa soko la Hisa la London huku uzinduzi huo ukifanyika wakati wa ufunguzi wa shughuli za wiki hii za soko la Hisa la London na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mbelwa Kairuki, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, Mhazini wa Benki ya NMB Aziz Chacha, Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la London, Julia Hoggetts na Viongozi wengine waandamizi kutoka Serikali ya Uingereza na Taasisi mbalimbali.

    “Tulianza kwa kuiorodhesha hati fungani hii katika Soko la Hisa la Dar es salaam mwaka jana, pia soko la Luxembourg mwezi uliopita na sasa tunaiorodhesha hapa Soko la Hisa la London ili kuwapa Wawekezaji wanaozingatia uendelevu, fursa ya kuchangia mabadiliko huku wakipata faida nzuri ya uwekezaji wao, Mafanikio haya kipekee yanadhihirisha imani waliyonayo wawekezaji wa Kitanzania na wa Kimataifa katika uthabiti wa Benki ya NMB na dhamira yake ya uendelevu katika utendaji wake, biashara, jamii na masuala ya mazingira” - Ruth Zaipuna alieleza.

    Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna alisema masoko ya kimataifa yanaiwezesha Benki ya NMB kuwa na wigo mpana wa kupata fedha kwa ajili ya kufadhili miradi inayosaidia kuboresha mazingira, kubadilisha jamii na kuwa na mustakabali bora kwa Watu wote. #MillardAyoUPDATES
    Benki ya NMB imetanua wigo wa kushiriki katika masoko ya mitaji kimataifa kwa kuiorodhesha Hati fungani ya NMB Jamii (NMB Jamii Bond) katika Soko la Hisa la London (LSE) ambapo hatua hii inaifanya NMB kuwa Taasisi ya kwanza Tanzania kuwa na hati fungani katika soko hilo na Benki ya kwanza Afrika Mashariki kuorodhesha Hatifungani ya Uendelevu katika soko la Hisa la London. Hati Fungani ya NMB Jamii inalenga kuchochea uwekezaji katika miradi yenye tija kijamii na kimazingira ambapo toleo la Dola za Kimarekani milioni 73 ndio limeorodheshwa kwa Wawekezaji wa soko la Hisa la London huku uzinduzi huo ukifanyika wakati wa ufunguzi wa shughuli za wiki hii za soko la Hisa la London na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mbelwa Kairuki, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, Mhazini wa Benki ya NMB Aziz Chacha, Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la London, Julia Hoggetts na Viongozi wengine waandamizi kutoka Serikali ya Uingereza na Taasisi mbalimbali. “Tulianza kwa kuiorodhesha hati fungani hii katika Soko la Hisa la Dar es salaam mwaka jana, pia soko la Luxembourg mwezi uliopita na sasa tunaiorodhesha hapa Soko la Hisa la London ili kuwapa Wawekezaji wanaozingatia uendelevu, fursa ya kuchangia mabadiliko huku wakipata faida nzuri ya uwekezaji wao, Mafanikio haya kipekee yanadhihirisha imani waliyonayo wawekezaji wa Kitanzania na wa Kimataifa katika uthabiti wa Benki ya NMB na dhamira yake ya uendelevu katika utendaji wake, biashara, jamii na masuala ya mazingira” - Ruth Zaipuna alieleza. Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna alisema masoko ya kimataifa yanaiwezesha Benki ya NMB kuwa na wigo mpana wa kupata fedha kwa ajili ya kufadhili miradi inayosaidia kuboresha mazingira, kubadilisha jamii na kuwa na mustakabali bora kwa Watu wote. #MillardAyoUPDATES
    Like
    Love
    Haha
    8
    3 Comentários ·542 Visualizações
  • PICHA: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewasili Jijini Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Paul Makonda pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama cha Mapinduzi, Vyombo vya ulinzi na usalama katika uwanja wa ndege wa Arusha leo tarehe 16 Mei 2024.

    Rais Dk.Mwinyi kesho tarehe 17 Mei 2024 anatarajiwa kufungua semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha )AICC). #MillardAyoUPDATES
    PICHA: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewasili Jijini Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Paul Makonda pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama cha Mapinduzi, Vyombo vya ulinzi na usalama katika uwanja wa ndege wa Arusha leo tarehe 16 Mei 2024. Rais Dk.Mwinyi kesho tarehe 17 Mei 2024 anatarajiwa kufungua semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha )AICC). #MillardAyoUPDATES
    Like
    Love
    15
    3 Comentários ·592 Visualizações
  • Waziri wa Mambo ya Ndani, Eng. Hamad Masauni amesema kuanzia July, 2023 hadi April, 2024 jumla ya vitambulisho 7,698,819 vimezalishwa na hivyo kufanya jumla ya vitambulisho vilivyozalishwa kufikia 20,578,325 sawa na asilimia 99 ya idadi ya Namba za Utambulisho 20,701,956 zilizozalishwa ambapo ametoa rai kwa Wananchi wote ambao bado hawajachukua vitambulisho vyao vya Taifa kufika katika ofisi za Serikali za Mitaa walipojiandikisha kwa ajili ya kuvichukua.

    Akiwasilisha Bungeni Jijini Dodoma Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2024/2025, Masauni amesema “Katika mwaka 2024/25 Shilingi bilioni 2.9 zimetengwa kwa ajili ya kusajili na kutambua Watu 2,389,290 wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa kila Mwananchi mwenye namba ya Utambulisho Tanzania Bara na Zanzibar anapata Kitambulisho cha Taifa”

    “Hadi Aprili, 2024 NIDA imeunganisha Taasisi 21 katika mfumo wa usajili na utambuzi, hivyo kufanya jumla ya taasisi zilizounganishwa kufikia 107, katika mwaka wa fedha 2024/25 jumla ya Taasisi 35 za umma na binafsi zinatarajiwa kuunganishwa katika mfumo huo ili kuwezesha ushirikishanaji wa taarifa na hivyo kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii, naomba nitumie fursa hii kuwahamasisha watoa huduma kujiunga na Mfumo wa NIDA ili kuwezesha upatikanaji wa taarifa sahihi za Wateja”
    #MillardAyoUPDATES
    Waziri wa Mambo ya Ndani, Eng. Hamad Masauni amesema kuanzia July, 2023 hadi April, 2024 jumla ya vitambulisho 7,698,819 vimezalishwa na hivyo kufanya jumla ya vitambulisho vilivyozalishwa kufikia 20,578,325 sawa na asilimia 99 ya idadi ya Namba za Utambulisho 20,701,956 zilizozalishwa ambapo ametoa rai kwa Wananchi wote ambao bado hawajachukua vitambulisho vyao vya Taifa kufika katika ofisi za Serikali za Mitaa walipojiandikisha kwa ajili ya kuvichukua. Akiwasilisha Bungeni Jijini Dodoma Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2024/2025, Masauni amesema “Katika mwaka 2024/25 Shilingi bilioni 2.9 zimetengwa kwa ajili ya kusajili na kutambua Watu 2,389,290 wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa kila Mwananchi mwenye namba ya Utambulisho Tanzania Bara na Zanzibar anapata Kitambulisho cha Taifa” “Hadi Aprili, 2024 NIDA imeunganisha Taasisi 21 katika mfumo wa usajili na utambuzi, hivyo kufanya jumla ya taasisi zilizounganishwa kufikia 107, katika mwaka wa fedha 2024/25 jumla ya Taasisi 35 za umma na binafsi zinatarajiwa kuunganishwa katika mfumo huo ili kuwezesha ushirikishanaji wa taarifa na hivyo kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii, naomba nitumie fursa hii kuwahamasisha watoa huduma kujiunga na Mfumo wa NIDA ili kuwezesha upatikanaji wa taarifa sahihi za Wateja” #MillardAyoUPDATES
    Like
    Love
    12
    4 Comentários ·419 Visualizações
  • Mtanzania, Denis Mfumbulwa (44) anayedaiwa kujipatia huduma ya kula katika Hoteli ya Serena bila kulipa, ameachiwa huru katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo jijini Dar es salaam kwa sababu hakuna ushahidi wa kuthibitisha kama kesi hiyo dhidi yake ni ya jinai.

    Mfumbulwa ambaye ni Mkazi wa Goba ameachiwa leo na Hakimu Gladness Njau wakati kesi hiyo ilipoitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusikilizwa.

    Mapema Meneja wa Hoteli hiyo, Desdery Doto alifika Mahakamani hapo kutoa ushahidi ambapo alipoulizwa alidai Mshtakiwa alifika hotelini hapo na kupata huduma ya chakula na malazi bila kulipa na kisha akatoweka.

    Kufuatia maelezo hayo, Hakimu Gladness Njau alimuachia huru Mshtakiwa huyo akisema “inaonekana asili ya shauri hili ni la madai na siyo jinai hivyo kama Mlalamikaji ataona inafaa afungue kesi ya madai”

    Katika kesi hiyo Mshtakiwa Mfulumbwa anayeishi Goba Kulangwa anadaiwa kuwa Machi 6,2022 hadi Machi 28,2024 kwa nyakati tofauti katika Hoteli ya Serena Wilaya ya Ilala, Dar es salaam alijipatia huduma ya malazi na chakula yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 21 bila kulipa ambapo baada ya kupatiwa huduma hiyo alitoweka huku akijua kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria.

    Akizungumza nje ya Mahakama Meneja Doto amesema yuko tayari kuendelea na kesi ya madai hivyo anasubiri nakala ya hukumu. #MillardAyoUPDATES
    Mtanzania, Denis Mfumbulwa (44) anayedaiwa kujipatia huduma ya kula katika Hoteli ya Serena bila kulipa, ameachiwa huru katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo jijini Dar es salaam kwa sababu hakuna ushahidi wa kuthibitisha kama kesi hiyo dhidi yake ni ya jinai. Mfumbulwa ambaye ni Mkazi wa Goba ameachiwa leo na Hakimu Gladness Njau wakati kesi hiyo ilipoitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusikilizwa. Mapema Meneja wa Hoteli hiyo, Desdery Doto alifika Mahakamani hapo kutoa ushahidi ambapo alipoulizwa alidai Mshtakiwa alifika hotelini hapo na kupata huduma ya chakula na malazi bila kulipa na kisha akatoweka. Kufuatia maelezo hayo, Hakimu Gladness Njau alimuachia huru Mshtakiwa huyo akisema “inaonekana asili ya shauri hili ni la madai na siyo jinai hivyo kama Mlalamikaji ataona inafaa afungue kesi ya madai” Katika kesi hiyo Mshtakiwa Mfulumbwa anayeishi Goba Kulangwa anadaiwa kuwa Machi 6,2022 hadi Machi 28,2024 kwa nyakati tofauti katika Hoteli ya Serena Wilaya ya Ilala, Dar es salaam alijipatia huduma ya malazi na chakula yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 21 bila kulipa ambapo baada ya kupatiwa huduma hiyo alitoweka huku akijua kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria. Akizungumza nje ya Mahakama Meneja Doto amesema yuko tayari kuendelea na kesi ya madai hivyo anasubiri nakala ya hukumu. #MillardAyoUPDATES
    Like
    Haha
    Love
    10
    5 Comentários ·357 Visualizações
  • Wizara ya Afya imetangaza matokeo ya Mashindano ya Afya na Usafi wa Mazingira kwa kuhusisha Manispaa 19 za Tanzania ambapo Manispaa ya Shinyanga imeibuka kuwa Mshindi wa kwanza.

    Shinyanga imeshika nafasi ya kwanza kwa kupata asilimia 95 ya alama zote ikifuatiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ambayo imepata asilimia 87.

    Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ambayo kwa miaka mingi imekuwa kwenye orodha ya Manispaa safi za Tanzania, mwaka huu imeshika nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 83 ya alama zote. #MillardAyoUPDATES
    Wizara ya Afya imetangaza matokeo ya Mashindano ya Afya na Usafi wa Mazingira kwa kuhusisha Manispaa 19 za Tanzania ambapo Manispaa ya Shinyanga imeibuka kuwa Mshindi wa kwanza. Shinyanga imeshika nafasi ya kwanza kwa kupata asilimia 95 ya alama zote ikifuatiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ambayo imepata asilimia 87. Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ambayo kwa miaka mingi imekuwa kwenye orodha ya Manispaa safi za Tanzania, mwaka huu imeshika nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 83 ya alama zote. #MillardAyoUPDATES
    Like
    Love
    10
    2 Comentários ·359 Visualizações