• Mahakama ya ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) imeanza kusikiliza shauri la Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo dhidi ya Nchi ya Rwanda , ambalo limefunguliwa kwenye mahakama hiyo iliyoko Jijini Arusha Nchini Tanzania .

    Aidha, DR Congo ilifungua kesi dhidi ya Rwanda, Agosti 21 2023, ikiituhumu Nchi hiyo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu. Kupitia kesi namba 007/2023, DR Congo inadai kuwa Nchi ya Rwanda inahusika na mgogoro unaeondelea Mashariki mwa Nchi hiyo hasa Mkoa wa Sud-Kivu.

    Mahakama ya ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) imeanza kusikiliza shauri la Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 dhidi ya Nchi ya Rwanda 🇷🇼, ambalo limefunguliwa kwenye mahakama hiyo iliyoko Jijini Arusha Nchini Tanzania 🇹🇿. Aidha, DR Congo ilifungua kesi dhidi ya Rwanda, Agosti 21 2023, ikiituhumu Nchi hiyo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu. Kupitia kesi namba 007/2023, DR Congo inadai kuwa Nchi ya Rwanda inahusika na mgogoro unaeondelea Mashariki mwa Nchi hiyo hasa Mkoa wa Sud-Kivu.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·170 Views
  • COMPLEX NA VIVY.
    Walipata ajali mbaya ya gari wakitokea Morogoro kwenda Arusha kwenye sherehe ya kumbukizi ya miaka 25 ya ndoa ya wazazi wa Vivian a.k.a Vivy.

    Complex na Vivy walikuwa ni wapenzi waliozaliwa tarehe moja, mwezi mmoja na mwaka mmoja. Walishangaza wengi baada ya wao kufa pamoja tar 21.08.2005.

    Walikutanishwa na mtaalamu Ambwene Yessayah, A.Y. Complex akiwa ni producer wa studio ya Algies Records huku Vivian akiwa Ni mtangazaji wa Clouds FM.

    Kisa Cha kukutana nakuwa Wapenzi Kiko hivi Vivian alifahamiana na A.Y Mkoani Iringa Kipindi A.Y anasoma Ifunda na Vivian alikuwa anasoma Mkwawa.

    Baada ya School, AY alikuja kukutana na Vivian Arusha alipoenda kwenye show akamshawishi Vivian kwa muonekano wake awe Mtangazaji. Vivian akaelewa Mchongo akakutanishwa na Hayati Gardener G Habash pale Clouds akapewa Mchongo wa Utangazaji.

    Simon Sai a.K.a Complex alikuwa anafanya kazi na A.Y

    Kuna ngoma walishirikishana kiufupi walikuwa Maswahiba wakubwa baada ya kufahamiana.

    Simon Sai a.K.a Complex akamuona Vivian pale Clouds FM kupitia A.Y akatokea kumpenda Vivian

    Baada ya hapo kilichofuata ni kuibuka kwa Penzi Zito kati ya Complex na Vivian..

    #BURUDANI #michezoonlineupdates #mahusiano

    Like & follow
    COMPLEX NA VIVY. Walipata ajali mbaya ya gari wakitokea Morogoro kwenda Arusha kwenye sherehe ya kumbukizi ya miaka 25 ya ndoa ya wazazi wa Vivian a.k.a Vivy. Complex na Vivy walikuwa ni wapenzi waliozaliwa tarehe moja, mwezi mmoja na mwaka mmoja. Walishangaza wengi baada ya wao kufa pamoja tar 21.08.2005. Walikutanishwa na mtaalamu Ambwene Yessayah, A.Y. Complex akiwa ni producer wa studio ya Algies Records huku Vivian akiwa Ni mtangazaji wa Clouds FM. Kisa Cha kukutana nakuwa Wapenzi Kiko hivi Vivian alifahamiana na A.Y Mkoani Iringa Kipindi A.Y anasoma Ifunda na Vivian alikuwa anasoma Mkwawa. Baada ya School, AY alikuja kukutana na Vivian Arusha alipoenda kwenye show akamshawishi Vivian kwa muonekano wake awe Mtangazaji. Vivian akaelewa Mchongo akakutanishwa na Hayati Gardener G Habash pale Clouds akapewa Mchongo wa Utangazaji. Simon Sai a.K.a Complex alikuwa anafanya kazi na A.Y Kuna ngoma walishirikishana kiufupi walikuwa Maswahiba wakubwa baada ya kufahamiana. Simon Sai a.K.a Complex akamuona Vivian pale Clouds FM kupitia A.Y akatokea kumpenda Vivian 😊 Baada ya hapo kilichofuata ni kuibuka kwa Penzi Zito kati ya Complex na Vivian.. #BURUDANI #michezoonlineupdates #mahusiano Like & follow 🙏 🙏
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·837 Views
  • Mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Victor Boniface, anayeichezea Bayer Leverkusen ya Ujerumani, ameachana na mpenzi wake, Rikke Hermine, raia wa Norway. Wawili hao walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa miaka minne, lakini wameamua kuvunja uhusiano wao kutokana na kugundua kuwa Victor kwenye mali zake ameandika majina ya mama yake tu.

    Chanzo cha habari kinaeleza kuwa uamuzi wa Rikke kuachana na Victor ulitokana na kugundua kuwa katika mali zote za mshambuliaji huyo, majina ya mama yake mzazi pekee ndiyo yaliyoandikwa. Hali hii ilimfanya Rikke kuhisi kuwa hakuwa na nafasi ya kutosha katika maisha ya Victor, jambo lililomfanya kuchukua hatua hiyo.

    Aidha, inadaiwa kuwa Rikke alikuwa akishinikiza kufunga ndoa baada ya kuwa wapenzi kwa muda mrefu, huku Victor akiwa tayari kufunga naye ndoa lakini kwa sharti la kusaini mkataba wa awali (prenup).

    Prenup ni Mkataba wa awali kabla ya kufunga ndoa ambao unalenga kulinda mali za pande zote mbili endapo itatokea mkaachana kila mmoja anabaki na alichokuja nacho katika ndoa na sio kugawana mali, ila bibie Rikkie amekuwa mgumu kukubali hilo hivyo kuachana

    #tanzania #kenya #daressalaam #africa #zanzibar #diamondplatnumz #arusha #mwanza #dodoma #uganda #wcb #travel #life #safari #wasafi #love #millardayoupdates #mbeya #nairobi #harmonize #rwanda #eastafrica #kilimanjaro #alikiba #gainwithmchina #serengeti #wasafitv #fashion #wasafimedia #wemasepetu
    Mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Victor Boniface, anayeichezea Bayer Leverkusen ya Ujerumani, ameachana na mpenzi wake, Rikke Hermine, raia wa Norway. Wawili hao walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa miaka minne, lakini wameamua kuvunja uhusiano wao kutokana na kugundua kuwa Victor kwenye mali zake ameandika majina ya mama yake tu. Chanzo cha habari kinaeleza kuwa uamuzi wa Rikke kuachana na Victor ulitokana na kugundua kuwa katika mali zote za mshambuliaji huyo, majina ya mama yake mzazi pekee ndiyo yaliyoandikwa. Hali hii ilimfanya Rikke kuhisi kuwa hakuwa na nafasi ya kutosha katika maisha ya Victor, jambo lililomfanya kuchukua hatua hiyo. Aidha, inadaiwa kuwa Rikke alikuwa akishinikiza kufunga ndoa baada ya kuwa wapenzi kwa muda mrefu, huku Victor akiwa tayari kufunga naye ndoa lakini kwa sharti la kusaini mkataba wa awali (prenup). Prenup ni Mkataba wa awali kabla ya kufunga ndoa ambao unalenga kulinda mali za pande zote mbili endapo itatokea mkaachana kila mmoja anabaki na alichokuja nacho katika ndoa na sio kugawana mali, ila bibie Rikkie amekuwa mgumu kukubali hilo hivyo kuachana #tanzania #kenya #daressalaam #africa #zanzibar #diamondplatnumz #arusha #mwanza #dodoma #uganda #wcb #travel #life #safari #wasafi #love #millardayoupdates #mbeya #nairobi #harmonize #rwanda #eastafrica #kilimanjaro #alikiba #gainwithmchina #serengeti #wasafitv #fashion #wasafimedia #wemasepetu
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·2K Views
  • #JeWajua Msako mkali wa wahamiaji uliofanyika nchini Marekani siku ya Jumapili na kusababisha kukamatwa kwa watu 956, idadi hiyo ikiwa kubwa zaidi tangu Donald Trump arejee mamlakani, kulingana na shirika la Uhamiaji na Utekelezaji wa Forodha (ICE).

    Mashirika kadhaa ya serikali yenye mamlaka mapya ya kuwaweka kizuizini wasio na vibali yalihusika katika kamata kamata hiyo kwenye miji kadhaa ikiwa ni pamoja na Chicago, Newark na Miami. Moja ya ahadi alizotoa Donald Trump wakati wa kampeni yake, ni kuwafukuza nchi Marekani wahamiaji wasio na vibali.

    Mtangulizi wake Joe Biden aliwarejesha makwao wastani wa wahamiaji 311 kila siku, kulingana na ICE, wengi wao wakiwa watu ambao walikuwa wamefanya uhalifu. Tangu aingie madarakani, Trump ametekeleza maagizo 21 kurekebisha mfumo wa uhamiaji wa Marekani.

    Huko Miami siku ya Jumapili, vyombo vya kutekeleza sheria vya serikali vilichukua "hatua kadhaa za uhamiaji," Uchunguzi wa Usalama wa jiji hilo ulisema kwenye mitandao ya kijamii.

    #tanzania #kenya #daressalaam #africa #zanzibar #diamondplatnumz #arusha #mwanza #dodoma #uganda #wcb #travel #life #safari #wasafi #love #millardayoupdates #mbeya #nairobi #harmonize #rwanda #eastafrica #kilimanjaro #alikiba #gainwithmchina #serengeti #wasafitv #fashion #wasafimedia
    #JeWajua Msako mkali wa wahamiaji uliofanyika nchini Marekani siku ya Jumapili na kusababisha kukamatwa kwa watu 956, idadi hiyo ikiwa kubwa zaidi tangu Donald Trump arejee mamlakani, kulingana na shirika la Uhamiaji na Utekelezaji wa Forodha (ICE). Mashirika kadhaa ya serikali yenye mamlaka mapya ya kuwaweka kizuizini wasio na vibali yalihusika katika kamata kamata hiyo kwenye miji kadhaa ikiwa ni pamoja na Chicago, Newark na Miami. Moja ya ahadi alizotoa Donald Trump wakati wa kampeni yake, ni kuwafukuza nchi Marekani wahamiaji wasio na vibali. Mtangulizi wake Joe Biden aliwarejesha makwao wastani wa wahamiaji 311 kila siku, kulingana na ICE, wengi wao wakiwa watu ambao walikuwa wamefanya uhalifu. Tangu aingie madarakani, Trump ametekeleza maagizo 21 kurekebisha mfumo wa uhamiaji wa Marekani. Huko Miami siku ya Jumapili, vyombo vya kutekeleza sheria vya serikali vilichukua "hatua kadhaa za uhamiaji," Uchunguzi wa Usalama wa jiji hilo ulisema kwenye mitandao ya kijamii. #tanzania #kenya #daressalaam #africa #zanzibar #diamondplatnumz #arusha #mwanza #dodoma #uganda #wcb #travel #life #safari #wasafi #love #millardayoupdates #mbeya #nairobi #harmonize #rwanda #eastafrica #kilimanjaro #alikiba #gainwithmchina #serengeti #wasafitv #fashion #wasafimedia
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·2K Views
  • Taswira mbalimbali za Serge Pokou akiwa mazoezini leo kwa mara ya kwanza

    #ArushaCamp #midseason #inawezekana
    Taswira mbalimbali za Serge Pokou akiwa mazoezini leo kwa mara ya kwanza 🐆 #ArushaCamp #midseason #inawezekana
    Like
    1
    · 1 Comments ·0 Shares ·351 Views
  • Mchezaji wetu wa kimataifa Wa Tanzania Arthur Bada Mara baada ya kubadili Uraia na kuwa Mtanzania Ameanza mchakato wa kupata kabila

    Sasa Tupo Arusha huku kambini kuna hawa wameru anawaona kila saa naona anang'ang'ania kweli kuwa mmeru

    Sasa Chagueni Aitwe Nani

    Arthur Bada Akyoo
    Arthur Bada Mbisse
    Arthur Bada Mafie
    Arthur Bada Pallangyo
    Arthur Bada kutomari
    Arthur Bada Nnko
    Mchezaji wetu wa kimataifa Wa Tanzania 🇹🇿 Arthur Bada Mara baada ya kubadili Uraia na kuwa Mtanzania Ameanza mchakato wa kupata kabila Sasa Tupo Arusha huku kambini kuna hawa wameru anawaona kila saa naona anang'ang'ania kweli kuwa mmeru Sasa Chagueni Aitwe Nani Arthur Bada Akyoo Arthur Bada Mbisse Arthur Bada Mafie Arthur Bada Pallangyo Arthur Bada kutomari Arthur Bada Nnko
    Love
    1
    · 1 Comments ·0 Shares ·170 Views
  • OPERATION ENTEBBE -4

    Katika sehemmu iliyopita nilieleza namna ambavyo baada ya madege ya kivita ya Lockheed Harcules C-130 kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe na moja ya ndege hizo kwenda moja kwa moja karibu na geti la Terminal huku mlango wa nyuma ukiwa wazi na kutoka gari aina na Mercides pamoja na Land Rover kufanana kabisa na msafara wa Idd Amin atembeleapo uwanja wa ndege, la kini ajabu ni kwamba walijikuta wakinyooshewa bunduki na wanajeshi waliokuwa wanalinda getini…
    Walikuwa hawana taarifa kuwa Amin alikuwa amebadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi kwenda nyeupe kabla ya safari yake ya kwenda Mauritius kwenye kikao cha O.A.U.
    Tuendelee…
    SEHEMU TA NNE
    Wanajeshi hawa wawili wa Uganda waliokuwa getini walinyanyua bunduki zao aina ya Kalashnikov na hawakuonyesha dalili kwamba labda walikuwa wanataka kufanya ukaguzi wa kawaida tu kabla ya kuwaruhusu, walionyesha dhahiri kabisa kwamba walikuwa wanataka kufanya shambulio.
    Kabla wanajeshi hao wa Uganda kufanya lolote lile, Netanyahu na komando mwingine ambao walikuwa ndani ya gari walitumia weledi wao kufanya uamuzi makini wa haraka kwa kufyatua risasi kutoka kwenye bastola zao zenye ‘silencer’ na mara moja wale wanajeshi wawili wa Uganda walienda chini.
    Lakini moja ya wale wanajeshi wa Uganda waliodondoka chini baada ya kufyatuliwa risasi, hakufa mara moja na alikuwa anajitahidi kuinuka. Hii ilisababisha komando mwingine wa Israel kufyatua risasi lakini safari hii huyu komando wa Israel alifyatua risasi kutoka kwenye bunduki ambayo haina ‘silencer’. Hii iliwashitua wanajeshi wengine wa Uganda waliokuwa nje ya Terminal na kuanza kukimbilia walipokuwa wanasikia milio ya risasi inatokea huku wanafyatua risasi.
    Kwa maneno mengine ilikuwa kwa kiasi fulani walichokuwa wamekipanga makomando wa Israel, kufanya shambulio la kushitukiza lakini mpaka muda huu tayari ile ‘element of surprise’ ilikuwa haipo tena, jeshi la Uganda lilikuwa limeshitukia ‘mchezo’.
    Bila kuchelewa sana, makomando wote walikuwa kwenye zile gari mbili (Mercedes na Land Rover) waliruka nje ya gari na kukimbia kuelekea ndani ya terminal.
    Vichwani mwao walikuwa bado hawajaondokewa na kumbukumbu ya oparesheni kama hii iliyotokea miaka miwili iliyopita nchini Israel kwenye mji wa Ma’a lot ambapowatekaji wa KIpalestina baada ya kushituka kuwa kulikuwa na makomando wa Israel wamefika kufanya uokozi, waliwapiga risasi mateka wao 25 ambao kati yao 22 walikuwa ni watoto wadogo.
    Hivyo Netanyahu na wenzake hawakutaka kitu kama hiki kjitokeze tena… Netenyahu na makomando wenzake wa Syeret Matkal kwa ustadi wa hali ya juu walikimbia na kuingia ndani ya terminal na kuwaacha vile vikosi vingine kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliopo nje ya terminal (kama nilivyoeleza juzi namna kikosi kilivyogawanywa kwenye vikundi vidogo kila kimoja kikipewa jukumu lake).
    Mateka wanaeleza kwamba baada ya mpambano ya risasi kuanza huko nje ya terminal waliwaona watekaji kadhaa wakiongozwa na yule aliyeonekana kama kiongozi wao, Wilfred Bose waliingia ndani ya terminal wakiwa wanahaha kama wamechanganyikiwa wasijue wafanye nini, ilionekana dhahiri kuwa walikuwa hawajajiandaa kwa hili shambulio la ghafla, ilionekana dhahiri kwamba katika akili yao walikuwa wanasubiria Israel kutimiza masharti yao ili waweze kuachia mateka.
    Kuna muda Wilfred Bose alionekana kunyoonya bunduki yake kwa mateka kama vile anawataka kuwamininia risasi lakini alikuwa anashindwa kufanya uamuzi huo. Bose aligeuka ghafla baada ya kusikia kishindo cha mlango wa terminal ukifunguliwa.
    Makomando wa Israel walikuwa wametumia weledi na ustadi wao wa hali ya juu kuingia ndani ya terminal kwa muda sahihi kabla ya Wilfred Bose na wenzake kufanya uamuzi wowote wa kuua mateka.
    Makomando wa Israel walipoingia tu ndani ya terminal, mmoja wao mkononi walikuwa na kipaza sauti aina ya ‘megaphone’ na alikuwa anaongeea kwa nguvu kwa lugha ya kihebrania, “Lay down, Lay down. We are Israel soldiers. Lay down. Lay down!!”.
    Mateka wote wa kiisrael hata wale waliokuwa wamekaa kitako walilala chini, hivyo ndani ya sekunde chache tu kila mtu ambaye alibakia amesimama alikuwa ni halali yao kumtandika risasi.
    Kwa bahati mbaya kulikuwa na mateka kadhaa ambao wwalikuwa hawajui kihebreania sawia na hii iliwagharimu sana. Kwa mfano kulikuwa na kijana wa mika 19 aliyeitwa Jean-Jacques Maimoni, huyu alikuwa amehamia Israel siku si nyingi sana kutokea nchini ufaransa. Lilipotolewa tangazo hilo la kila mtu kulala chini hakuelewa na alibakia akiwa amesimama na alitandikwa risasi na makomando wa Israel pamoja na wale watekaji. Kijana huyu hakuwa peke yake, lakini pia kulikuwa na mateka mwingine aliyeitwa Ida Borochovitch, ambaye alihamia Israel kutoka nchini Urusi.
    Risasi zilirindima kwa takribani dakika mbili nzima na baadae ukimya wa kama sekunde 15 ukatawala na moja wa makomando wa kiisrael akauliza kwa kiebrania, “where are the rest of them?” (“wako wapi wengine?”). Mateka wakaonyesha kidole kwenye chumba kidogo kilichopo pembeni.
    Makomando wakarusha mabomu kadhaa ya kutupa kwa mkono na kisha kuingia ndani ya chumba hicho na kuwamiminia risasi wote ambao walikuwa humo.
    Milio ya risasi ndani ya terminal hatimaye ilikuwa imekoma japo bado huko nje walisikia majibizano ya risasi. Mwanajeshi mmoja wa Israel kati ya wale waliopo ndani ya terminal, kwa sauti ya utulivu kabisa na katika lugha ya kihebrania aliwatangazia mateka, “listen guys, we’ve come to take you home!” (“sikilizeni, tumekuja kuwachukua kuwarudisha nyumbani!”).
    Baada ya hapo makomando walianza kuwatoa mateka kutoka kwenye terminal na kuwapakia kwenye ndege kwa tahadhari kubwa huku wale wenzao wengine wakiendelea kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanarusha risasi kutoka kwenye maeneo ya kujificha ndani ya uwanja wa ndege.
    Wakiwa wanaendelea kuwapakia mateka waliowaokoa kwenye ndege, kumbe kulikuwa na mwanajeshi wa Uganda amebakia juu kwenye mnara wa uongozaji (airport control tower). Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibunui kutoka kwa mtoto wa Idd Amin anasema kwamba mwanajeshi huyu alikuwa ni binamu wa Idd Amin. Kutokea hapo kwenye mnara alimimina risasi mfululizo kwa makomando wa Israel na moja ya risasi hizi ilimpaka Koamando Yonatan Netanyahu ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Matkal iliyopo hapoa na alipoteza uhai pale pale.
    Wanajeshi wa Isarel walijibu mapigo kwa kurusha bomu la roketi ndogo ya begani na kusambaratisha kabisa kiota cha mnara na kumuua mwanajeshi wa Uganda aliyekuwa anawashambulia.
    Baada ya hapo waliwapakia kwenye ndege mateka wote ambao waliokolewa pamoja na miili ya Waisrael ambao walifariki kwenye majibizano hayo ya risasi.
    Kisha ili kuhakikisha kuwa hakuna ndege itakayowafuatia nyuma wakiondoka au kushambuliwa, walilipua ndege zote za jeshi la Uganda ambazo zilikuwa uwanjani hapo.
    Oparesheni yote hii ilichukua takribani dakika 53 ambapo dakika 30 pekee ndio zilikuwa za mapigano na 23 zilizosalia zilikuwa za kupakia mateka walio okolewa na kuondoka.
    Mpaka kufikia mwishio mwa oparesheni, jumla ya watekaji wote 7 walikuwa wameuwawa, pia wanajeshi 45 wa jeshi la Uganda walikuwa wameuwawa pia. Lakini pia ndege za kijeshi 11 aina ya MiG-17 na Mig-21 zililipuliwa na makomando wa Isarel. Ikumbukwe kwamba ndege hizi ndizo zilikuwa ni ndege zote za kijeshi ambazo zilikuwa zinamilikiwa na jeshi la anga la Uganda. Hii inaonyesha moja kati ya mapungufu makubwa ya kiuongozi ya Amin. Hakukuwa na busara yoyote au faida yoyote ya kimkakati kuweka ndege zote za jeshi lako la anga kwenye uwanja wa ndege wa kiraia ili kulinda mateka wa tukio ambalo wengine walikuwa wanaweza kuliona kama tukio la kigaidi na kwa namna Fulani kama ugomvi ambao ulikuwa haumuhusu moja kwa moja.
    Katika mateka wote 106 waliobakia (kumbuka nilieleza kuwa kulikuwa na mikupuo miwili ya mateka wasio wa Kiisrael au asili ya Kiyahudi waliachiwa kwa kupelekwa na ndege ufaransa nchini), kwahiyo kati ya wale 106 waliobakio, mateka watatu waliuwawa muda wa mapambano (hawa ndio wale ambao walikuwa hawaelewi kihebrania kwa ufasaha na kwa hiyo hawakulalala chini kama ilivyoamrishwa na makomando wa Israel), na mateka mmoja bibi wa miaka 74 aliyeitwa Dora Bloch aliachwa akiwa Hospitali mjini Entebbe ambako alipelekwa na Amin siku kadhaa nyuma kutokana na kuhitaji uangalizi maalumu wa kidaktari.
    Kati ya Makomando wa Isarel, ni mmoja tu ndiye aliuwawa tena dakika za mwisho (Yonatan Netanyahu) japo pia kuna makomando wengine kama watano ambao walijeruhiwa. Kifo cha kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Mitkal, Yonatan Netanyahu katika oparesheni hii ndio iliyofanya siku kadhaa baadae oparesheni hii pia kubatizwa jina la OPERATION YONATAN kwa heshima yake na ushujaa wake wa kutoa maisha yake ili kutetea na kuooa roho za raia alioapa kuwalinda.
    Baada ya kila kitu kuwekwa sawa na watu wote kupanda ndani ya ndege, waliruka mpaka Nairobi Kenya kwa mapumziko mafupi ili kutibia wale ambao walijeruhiwa (kama ambavyo nilieleza kuwa ile moja ya Boeing 707 iliyotengwa kama ‘hospitali’ ilibaki Nairobi).
    Baada ya matibabu hapo Nairobi, madege yote yaliruka kurudi Israel. Kwa kifupi operation hii was a big SUCCESS.!
    Japokuwa baada ya ulimwengu mzima kutangaziwa juu ya kilichotokea, juu ya ‘umafia’ uliofanywa na Israel, ulimwengu uligawanyika kila nchi ukiunga mkono upande fulani, lakini nchi nyingi ziliunga mkono Israel kwa matumizi ya jeshi katika nchi nyingine, wengi walimlaumu Amin kwa kushindwa kutumia diplomasia kumaliza mzozo huu. Ajabu ni kwamba mwezi huo wa July, Mkuu wa Majeshi wa Iran moja wa mahsimu wa siku zote wa Israel aliandika barua kwa Waziri mkuu wa Israel kumpongeza kuhusu Oparation hiyo na kumpa pole kwa kifo cha Yonatan Netanyahu akimuita Yonatan kumsifu kuwa ni ‘martyr’.
    Vyovyote vile ambavyo unaweza kuitazama oparesheni hii kwenye jicho la kisiasa ua kidiplomasia, kwamba kama ilikuwa ni sahihi au si sahihi lakini katika jicho la kijeshi na ujasusi hii ni moja ya oparesheni murua kabisa kuwahi kufanyika katika historia ya majeshi duniani. Moja ya manguli wa “ulimwengu wa giza”, Bw. Henry Kissinger aliwahi kutamka kuwa hii ilikuwa ni “an immposible mission”!
    Umaridadi wa oparesheni hii umefanya hata vitengo kadhaa vya weledi vya majeshi mbali mbali kutaka kuiga mfano wake lakini bila mafanikio yoyote. Kwa mfano Wamarekani walijaribu kuiga umaridadi wa Oparesheni hii na kufanya ya kwao iliyoitwa Oparation Eagle Claw baada ya kutokea kwa utekeaji kwenye ubalozi wa Iran lakini oparesheni hiyo ilifeli vibaya.
    Sasa hivi kama wewe ni mwanajeshi katika jeshi fulani kwenye kitengo cha weledi (special force) au labda ni jasusi maalumu, lazima katika hatua fulani ya japo hata ‘darasani’ kwenye makaratasi utafundwa kuhusu Oparetion Entebbe na namna ilivyo tekelezwa.
    Oparesheni hii ilimuacha Amin na aibu kubwa kiasi kwamba akaendelea kufanya vitu ambavyo vilidhihirisha udhaifu wake wa kiungozi. Kwa mfano, yule bibi wa miaka 74 aliyeachwa hospitali mjini Entebbe, aliamuru auwawe kinyama. Lakini pia Amin alisimami kuwawa kwa McKenzie yule waziri wa kilimo wa Kenya ambaye alimsaidia Ehud Barak kumshinikiza Mzee Jomo Kenyetta kuruhusu ndege za jeshi la Israel kutumia viwanja vya ndege vya Kenya wakati wa utekelezaji wa OParesheni hiyo na pia kumsaidi kukusanya Intelijensia kwa kutumia ndege yake binafsi.
    McKenzie aliuwawa kwa bomu lililotegwa kwenye gari yake.
    Pia Amin alisimamia ulipuaji kwa bomu moja ya hoteli kubwa Nairobi kipindi hicho ambayo ilikuwa inaitwa The Norfolk Hotel, ambayo ilimilikiwa na moja ya wayahudi mashuhuri nchini Kenya.
    [6/12, 13:48] The Bold: Licha ya ‘fujo’ zote hizi ambazo Amin alizifanya baada ya jeshi lake kudhalilika kutokana na Oeration Entebbe lakini hatupawsi kusahau kwamba chini ya miaka mitatu baadae, yaani baada ya utekelezaji wa opareshini hii, Idd Amin aliondolewa kwa aibu madarakani na majeshi ya Tanzania na kumfanya akimbie nchi yake.

    ......................MWISHO..............
    #TheBOLD_JF
    OPERATION ENTEBBE -4 Katika sehemmu iliyopita nilieleza namna ambavyo baada ya madege ya kivita ya Lockheed Harcules C-130 kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe na moja ya ndege hizo kwenda moja kwa moja karibu na geti la Terminal huku mlango wa nyuma ukiwa wazi na kutoka gari aina na Mercides pamoja na Land Rover kufanana kabisa na msafara wa Idd Amin atembeleapo uwanja wa ndege, la kini ajabu ni kwamba walijikuta wakinyooshewa bunduki na wanajeshi waliokuwa wanalinda getini… Walikuwa hawana taarifa kuwa Amin alikuwa amebadili rangi ya gari yake kutoka nyeusi kwenda nyeupe kabla ya safari yake ya kwenda Mauritius kwenye kikao cha O.A.U. Tuendelee… SEHEMU TA NNE Wanajeshi hawa wawili wa Uganda waliokuwa getini walinyanyua bunduki zao aina ya Kalashnikov na hawakuonyesha dalili kwamba labda walikuwa wanataka kufanya ukaguzi wa kawaida tu kabla ya kuwaruhusu, walionyesha dhahiri kabisa kwamba walikuwa wanataka kufanya shambulio. Kabla wanajeshi hao wa Uganda kufanya lolote lile, Netanyahu na komando mwingine ambao walikuwa ndani ya gari walitumia weledi wao kufanya uamuzi makini wa haraka kwa kufyatua risasi kutoka kwenye bastola zao zenye ‘silencer’ na mara moja wale wanajeshi wawili wa Uganda walienda chini. Lakini moja ya wale wanajeshi wa Uganda waliodondoka chini baada ya kufyatuliwa risasi, hakufa mara moja na alikuwa anajitahidi kuinuka. Hii ilisababisha komando mwingine wa Israel kufyatua risasi lakini safari hii huyu komando wa Israel alifyatua risasi kutoka kwenye bunduki ambayo haina ‘silencer’. Hii iliwashitua wanajeshi wengine wa Uganda waliokuwa nje ya Terminal na kuanza kukimbilia walipokuwa wanasikia milio ya risasi inatokea huku wanafyatua risasi. Kwa maneno mengine ilikuwa kwa kiasi fulani walichokuwa wamekipanga makomando wa Israel, kufanya shambulio la kushitukiza lakini mpaka muda huu tayari ile ‘element of surprise’ ilikuwa haipo tena, jeshi la Uganda lilikuwa limeshitukia ‘mchezo’. Bila kuchelewa sana, makomando wote walikuwa kwenye zile gari mbili (Mercedes na Land Rover) waliruka nje ya gari na kukimbia kuelekea ndani ya terminal. Vichwani mwao walikuwa bado hawajaondokewa na kumbukumbu ya oparesheni kama hii iliyotokea miaka miwili iliyopita nchini Israel kwenye mji wa Ma’a lot ambapowatekaji wa KIpalestina baada ya kushituka kuwa kulikuwa na makomando wa Israel wamefika kufanya uokozi, waliwapiga risasi mateka wao 25 ambao kati yao 22 walikuwa ni watoto wadogo. Hivyo Netanyahu na wenzake hawakutaka kitu kama hiki kjitokeze tena… Netenyahu na makomando wenzake wa Syeret Matkal kwa ustadi wa hali ya juu walikimbia na kuingia ndani ya terminal na kuwaacha vile vikosi vingine kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliopo nje ya terminal (kama nilivyoeleza juzi namna kikosi kilivyogawanywa kwenye vikundi vidogo kila kimoja kikipewa jukumu lake). Mateka wanaeleza kwamba baada ya mpambano ya risasi kuanza huko nje ya terminal waliwaona watekaji kadhaa wakiongozwa na yule aliyeonekana kama kiongozi wao, Wilfred Bose waliingia ndani ya terminal wakiwa wanahaha kama wamechanganyikiwa wasijue wafanye nini, ilionekana dhahiri kuwa walikuwa hawajajiandaa kwa hili shambulio la ghafla, ilionekana dhahiri kwamba katika akili yao walikuwa wanasubiria Israel kutimiza masharti yao ili waweze kuachia mateka. Kuna muda Wilfred Bose alionekana kunyoonya bunduki yake kwa mateka kama vile anawataka kuwamininia risasi lakini alikuwa anashindwa kufanya uamuzi huo. Bose aligeuka ghafla baada ya kusikia kishindo cha mlango wa terminal ukifunguliwa. Makomando wa Israel walikuwa wametumia weledi na ustadi wao wa hali ya juu kuingia ndani ya terminal kwa muda sahihi kabla ya Wilfred Bose na wenzake kufanya uamuzi wowote wa kuua mateka. Makomando wa Israel walipoingia tu ndani ya terminal, mmoja wao mkononi walikuwa na kipaza sauti aina ya ‘megaphone’ na alikuwa anaongeea kwa nguvu kwa lugha ya kihebrania, “Lay down, Lay down. We are Israel soldiers. Lay down. Lay down!!”. Mateka wote wa kiisrael hata wale waliokuwa wamekaa kitako walilala chini, hivyo ndani ya sekunde chache tu kila mtu ambaye alibakia amesimama alikuwa ni halali yao kumtandika risasi. Kwa bahati mbaya kulikuwa na mateka kadhaa ambao wwalikuwa hawajui kihebreania sawia na hii iliwagharimu sana. Kwa mfano kulikuwa na kijana wa mika 19 aliyeitwa Jean-Jacques Maimoni, huyu alikuwa amehamia Israel siku si nyingi sana kutokea nchini ufaransa. Lilipotolewa tangazo hilo la kila mtu kulala chini hakuelewa na alibakia akiwa amesimama na alitandikwa risasi na makomando wa Israel pamoja na wale watekaji. Kijana huyu hakuwa peke yake, lakini pia kulikuwa na mateka mwingine aliyeitwa Ida Borochovitch, ambaye alihamia Israel kutoka nchini Urusi. Risasi zilirindima kwa takribani dakika mbili nzima na baadae ukimya wa kama sekunde 15 ukatawala na moja wa makomando wa kiisrael akauliza kwa kiebrania, “where are the rest of them?” (“wako wapi wengine?”). Mateka wakaonyesha kidole kwenye chumba kidogo kilichopo pembeni. Makomando wakarusha mabomu kadhaa ya kutupa kwa mkono na kisha kuingia ndani ya chumba hicho na kuwamiminia risasi wote ambao walikuwa humo. Milio ya risasi ndani ya terminal hatimaye ilikuwa imekoma japo bado huko nje walisikia majibizano ya risasi. Mwanajeshi mmoja wa Israel kati ya wale waliopo ndani ya terminal, kwa sauti ya utulivu kabisa na katika lugha ya kihebrania aliwatangazia mateka, “listen guys, we’ve come to take you home!” (“sikilizeni, tumekuja kuwachukua kuwarudisha nyumbani!”). Baada ya hapo makomando walianza kuwatoa mateka kutoka kwenye terminal na kuwapakia kwenye ndege kwa tahadhari kubwa huku wale wenzao wengine wakiendelea kuwadhibiti wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanarusha risasi kutoka kwenye maeneo ya kujificha ndani ya uwanja wa ndege. Wakiwa wanaendelea kuwapakia mateka waliowaokoa kwenye ndege, kumbe kulikuwa na mwanajeshi wa Uganda amebakia juu kwenye mnara wa uongozaji (airport control tower). Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibunui kutoka kwa mtoto wa Idd Amin anasema kwamba mwanajeshi huyu alikuwa ni binamu wa Idd Amin. Kutokea hapo kwenye mnara alimimina risasi mfululizo kwa makomando wa Israel na moja ya risasi hizi ilimpaka Koamando Yonatan Netanyahu ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Matkal iliyopo hapoa na alipoteza uhai pale pale. Wanajeshi wa Isarel walijibu mapigo kwa kurusha bomu la roketi ndogo ya begani na kusambaratisha kabisa kiota cha mnara na kumuua mwanajeshi wa Uganda aliyekuwa anawashambulia. Baada ya hapo waliwapakia kwenye ndege mateka wote ambao waliokolewa pamoja na miili ya Waisrael ambao walifariki kwenye majibizano hayo ya risasi. Kisha ili kuhakikisha kuwa hakuna ndege itakayowafuatia nyuma wakiondoka au kushambuliwa, walilipua ndege zote za jeshi la Uganda ambazo zilikuwa uwanjani hapo. Oparesheni yote hii ilichukua takribani dakika 53 ambapo dakika 30 pekee ndio zilikuwa za mapigano na 23 zilizosalia zilikuwa za kupakia mateka walio okolewa na kuondoka. Mpaka kufikia mwishio mwa oparesheni, jumla ya watekaji wote 7 walikuwa wameuwawa, pia wanajeshi 45 wa jeshi la Uganda walikuwa wameuwawa pia. Lakini pia ndege za kijeshi 11 aina ya MiG-17 na Mig-21 zililipuliwa na makomando wa Isarel. Ikumbukwe kwamba ndege hizi ndizo zilikuwa ni ndege zote za kijeshi ambazo zilikuwa zinamilikiwa na jeshi la anga la Uganda. Hii inaonyesha moja kati ya mapungufu makubwa ya kiuongozi ya Amin. Hakukuwa na busara yoyote au faida yoyote ya kimkakati kuweka ndege zote za jeshi lako la anga kwenye uwanja wa ndege wa kiraia ili kulinda mateka wa tukio ambalo wengine walikuwa wanaweza kuliona kama tukio la kigaidi na kwa namna Fulani kama ugomvi ambao ulikuwa haumuhusu moja kwa moja. Katika mateka wote 106 waliobakia (kumbuka nilieleza kuwa kulikuwa na mikupuo miwili ya mateka wasio wa Kiisrael au asili ya Kiyahudi waliachiwa kwa kupelekwa na ndege ufaransa nchini), kwahiyo kati ya wale 106 waliobakio, mateka watatu waliuwawa muda wa mapambano (hawa ndio wale ambao walikuwa hawaelewi kihebrania kwa ufasaha na kwa hiyo hawakulalala chini kama ilivyoamrishwa na makomando wa Israel), na mateka mmoja bibi wa miaka 74 aliyeitwa Dora Bloch aliachwa akiwa Hospitali mjini Entebbe ambako alipelekwa na Amin siku kadhaa nyuma kutokana na kuhitaji uangalizi maalumu wa kidaktari. Kati ya Makomando wa Isarel, ni mmoja tu ndiye aliuwawa tena dakika za mwisho (Yonatan Netanyahu) japo pia kuna makomando wengine kama watano ambao walijeruhiwa. Kifo cha kiongozi wa ‘unit’ ya Sayeret Mitkal, Yonatan Netanyahu katika oparesheni hii ndio iliyofanya siku kadhaa baadae oparesheni hii pia kubatizwa jina la OPERATION YONATAN kwa heshima yake na ushujaa wake wa kutoa maisha yake ili kutetea na kuooa roho za raia alioapa kuwalinda. Baada ya kila kitu kuwekwa sawa na watu wote kupanda ndani ya ndege, waliruka mpaka Nairobi Kenya kwa mapumziko mafupi ili kutibia wale ambao walijeruhiwa (kama ambavyo nilieleza kuwa ile moja ya Boeing 707 iliyotengwa kama ‘hospitali’ ilibaki Nairobi). Baada ya matibabu hapo Nairobi, madege yote yaliruka kurudi Israel. Kwa kifupi operation hii was a big SUCCESS.! Japokuwa baada ya ulimwengu mzima kutangaziwa juu ya kilichotokea, juu ya ‘umafia’ uliofanywa na Israel, ulimwengu uligawanyika kila nchi ukiunga mkono upande fulani, lakini nchi nyingi ziliunga mkono Israel kwa matumizi ya jeshi katika nchi nyingine, wengi walimlaumu Amin kwa kushindwa kutumia diplomasia kumaliza mzozo huu. Ajabu ni kwamba mwezi huo wa July, Mkuu wa Majeshi wa Iran moja wa mahsimu wa siku zote wa Israel aliandika barua kwa Waziri mkuu wa Israel kumpongeza kuhusu Oparation hiyo na kumpa pole kwa kifo cha Yonatan Netanyahu akimuita Yonatan kumsifu kuwa ni ‘martyr’. Vyovyote vile ambavyo unaweza kuitazama oparesheni hii kwenye jicho la kisiasa ua kidiplomasia, kwamba kama ilikuwa ni sahihi au si sahihi lakini katika jicho la kijeshi na ujasusi hii ni moja ya oparesheni murua kabisa kuwahi kufanyika katika historia ya majeshi duniani. Moja ya manguli wa “ulimwengu wa giza”, Bw. Henry Kissinger aliwahi kutamka kuwa hii ilikuwa ni “an immposible mission”! Umaridadi wa oparesheni hii umefanya hata vitengo kadhaa vya weledi vya majeshi mbali mbali kutaka kuiga mfano wake lakini bila mafanikio yoyote. Kwa mfano Wamarekani walijaribu kuiga umaridadi wa Oparesheni hii na kufanya ya kwao iliyoitwa Oparation Eagle Claw baada ya kutokea kwa utekeaji kwenye ubalozi wa Iran lakini oparesheni hiyo ilifeli vibaya. Sasa hivi kama wewe ni mwanajeshi katika jeshi fulani kwenye kitengo cha weledi (special force) au labda ni jasusi maalumu, lazima katika hatua fulani ya japo hata ‘darasani’ kwenye makaratasi utafundwa kuhusu Oparetion Entebbe na namna ilivyo tekelezwa. Oparesheni hii ilimuacha Amin na aibu kubwa kiasi kwamba akaendelea kufanya vitu ambavyo vilidhihirisha udhaifu wake wa kiungozi. Kwa mfano, yule bibi wa miaka 74 aliyeachwa hospitali mjini Entebbe, aliamuru auwawe kinyama. Lakini pia Amin alisimami kuwawa kwa McKenzie yule waziri wa kilimo wa Kenya ambaye alimsaidia Ehud Barak kumshinikiza Mzee Jomo Kenyetta kuruhusu ndege za jeshi la Israel kutumia viwanja vya ndege vya Kenya wakati wa utekelezaji wa OParesheni hiyo na pia kumsaidi kukusanya Intelijensia kwa kutumia ndege yake binafsi. McKenzie aliuwawa kwa bomu lililotegwa kwenye gari yake. Pia Amin alisimamia ulipuaji kwa bomu moja ya hoteli kubwa Nairobi kipindi hicho ambayo ilikuwa inaitwa The Norfolk Hotel, ambayo ilimilikiwa na moja ya wayahudi mashuhuri nchini Kenya. [6/12, 13:48] The Bold: Licha ya ‘fujo’ zote hizi ambazo Amin alizifanya baada ya jeshi lake kudhalilika kutokana na Oeration Entebbe lakini hatupawsi kusahau kwamba chini ya miaka mitatu baadae, yaani baada ya utekelezaji wa opareshini hii, Idd Amin aliondolewa kwa aibu madarakani na majeshi ya Tanzania na kumfanya akimbie nchi yake. ......................MWISHO.............. #TheBOLD_JF
    0 Comments ·0 Shares ·2K Views
  • "SPACE SHUTTLE AU ORBITER " CHOMBO KINACHO KWENDA MWENDO MKALI MARA TISA ZAIDI YA RISASI NA MARA ISHIRINI YA SPIDI YA SAUTI "

    > Hiki chombo kina mwendo mkali, mara 9 zaidi ya risasi au mara20 ya spidi ya sauti pindi kinapotoka hapa duniani.

    Hapa tunaongelea chombo cha anga za mbali au kile kiendacho nje ya dunia. "Space shuttle" au "Orbiter" ambayo ni aina ya ndege maalum.

    "HAPO AWALI"

    Nakumbuka baadhi yetu tulipokuwa tunaona chombo kinapita umbali wa juu huku kikiacha moshi mweupe nyuma tunasema "rocket" lakini leo tunafahamu kuwa ile ni ndege ya kawaida ya abiria na ule moshi mweupe tunao uona nyuma ni matokeo ya kukutana hewa yenye joto itokayo kenye injini na hali ya hewa ya baridi iliyopo usawa ule ambapo "condensation trail" vikikutana vinaganda na kutengeneza lile wingu moshi tulionalo nyuma.
    wanasema hata mawingu yanapatikana kwa njia inayofanana kidogo na hiyo, Kwa mujibu wa wataalam.
    (kumbuka pia hata 'rocket' ina tabia ya kuacha moshi nyuma pale inapokuwa imewashwa).

    "UZITO"

    Chombo hiki 'space shuttle' mara nyingi huwa kinabeba wataalam mbalimbali wa masuala ya anga za juu "Astronauts", vifaa mbalimbali vya ujenzi wa maabara ya nje ya dunia, spare, satelite n.k
    Pia kinabeba hewa yake yenyewe ya oxygen kwasababu ya uhai wa watu waliomo ndani kwaajili ya kuendesha injini zake kinapokuwa nje ya dunia kwasababu huko hakuna hewa."vacuum space"
    Mara nyingi kinafikia jumla ya uzito wa hadi tani 2000 au kg 2,000,000 pindi kinapoondoka hapa duniani.

    "NGUVU"

    Chombo hiki kimeundwa na injini tatu lakini kinaongezewa injini mbili za ziada "Solid Rocket Booster" 'SRB' na ndiyo jina la rocket lilipozaliwa, (picha chini inaonesha rocket booster hizo mbili nyeupe) ambazo ndani hubeba mafuta ya aina yake.

    Lakini pia inabeba tank kubwa la mafuta tumboni lenye rangi ya Orange, ambalo nalo linabeba mamilioni ya lita za mafuta ambayo yote huwa yanaisha ndani ya dakika8 tangu ikianza safari.

    Kutokana na uzito na umbali wa safari yake kwa ujumla injini hizo mbili za Solid Rocket Booster "SRB" zinazalisha nguvu kufikia horse power million44 au linganisha nguvu ya vichwa vya train 14,000.

    Rocket injini hizi na tank la mafuta zikifika umbali fulani hujiachia na kurudi duniani hasa pale yanapoisha mafuta yake na kukiacha chombo kinaendelea chenyewe na injini zake ambapo kinakuwa kimefikishwa umbali ambao hakihitaji tena nguvu kubwa.

    Umbali wa kufikia anga za huko kwenye "Space" au anga za mbali uanzia kilometa 100 kutoka hapa duniani kwenda angani wanasema wataalam wa mambo ya anga.

    "MWENDO"

    Wakati kinawashwa kuondoka kutoka katika sehemu yake "launch pad" ndani ya dakika 8 huwa kinafikia mwendo wa 25000 M/hr au 40,000 k/hr hivyo kufanya kwenda kasi mara9 zaidi ya risasi au mara10 ya kasi ya sauti.
    Mwendo wa sauti ni zaidi ya 1200 k/h.

    "GHARAMA"

    Chombo hiki huwa akiruki mara kwa mara isipokuwa kwa misheni maalum tu.
    Mara nyingi, mara moja kwa miezi miwili au zaidi ya hapo.

    NASA ambao ndiyo Mamlaka ya Usafiri wa Anga za karibu na mbali huko Marekani ndiyo wahusika wakuu kwenye kurusha chombo hiki.

    Pia alikuwa anarusha Mrusi na kuna taarifa za Mchina pia alikuwa na program ya kwenda.

    Marekani ameviita majina vyombo hivyo,
    >Enteprise-kimestaafu zamani
    >Colombia-kilipata ajali kikaua wote
    >Discovery-2011
    >Atlantis-2011
    >Endeavour- 2011 kiliziba nafasi ya challenger
    >Challenge-kilipata ajali kikaua wote

    Mrusi aliita
    >Buran-na kilienda safari moja tu.

    Gharama waliyotoa NASA mwaka 2011 kurusha chombo hiki kwa safari moja ni sawa na bei ya kununua Boeing 787 Dreamliner mbili hadi Tano inategemea na misheni husika.
    Tukumbuke pia sio kila "rocket launch" roketi inayorushwa ni lazima ihusishe chombo hiki, zipo misheni nyengine za anga za mbali ambazo zinapeleka mizigo tu kama satelite n.k pasipo kuwemo watu katika chombo na huwa kinaendeshwa kwa remote control.
    "SPACE SHUTTLE AU ORBITER " CHOMBO KINACHO KWENDA MWENDO MKALI MARA TISA ZAIDI YA RISASI NA MARA ISHIRINI YA SPIDI YA SAUTI " > Hiki chombo kina mwendo mkali, mara 9 zaidi ya risasi au mara20 ya spidi ya sauti pindi kinapotoka hapa duniani. Hapa tunaongelea chombo cha anga za mbali au kile kiendacho nje ya dunia. "Space shuttle" au "Orbiter" ambayo ni aina ya ndege maalum. "HAPO AWALI" Nakumbuka baadhi yetu tulipokuwa tunaona chombo kinapita umbali wa juu huku kikiacha moshi mweupe nyuma tunasema "rocket" lakini leo tunafahamu kuwa ile ni ndege ya kawaida ya abiria na ule moshi mweupe tunao uona nyuma ni matokeo ya kukutana hewa yenye joto itokayo kenye injini na hali ya hewa ya baridi iliyopo usawa ule ambapo "condensation trail" vikikutana vinaganda na kutengeneza lile wingu moshi tulionalo nyuma. wanasema hata mawingu yanapatikana kwa njia inayofanana kidogo na hiyo, Kwa mujibu wa wataalam. (kumbuka pia hata 'rocket' ina tabia ya kuacha moshi nyuma pale inapokuwa imewashwa). "UZITO" Chombo hiki 'space shuttle' mara nyingi huwa kinabeba wataalam mbalimbali wa masuala ya anga za juu "Astronauts", vifaa mbalimbali vya ujenzi wa maabara ya nje ya dunia, spare, satelite n.k Pia kinabeba hewa yake yenyewe ya oxygen kwasababu ya uhai wa watu waliomo ndani kwaajili ya kuendesha injini zake kinapokuwa nje ya dunia kwasababu huko hakuna hewa."vacuum space" Mara nyingi kinafikia jumla ya uzito wa hadi tani 2000 au kg 2,000,000 pindi kinapoondoka hapa duniani. "NGUVU" Chombo hiki kimeundwa na injini tatu lakini kinaongezewa injini mbili za ziada "Solid Rocket Booster" 'SRB' na ndiyo jina la rocket lilipozaliwa, (picha chini inaonesha rocket booster hizo mbili nyeupe) ambazo ndani hubeba mafuta ya aina yake. Lakini pia inabeba tank kubwa la mafuta tumboni lenye rangi ya Orange, ambalo nalo linabeba mamilioni ya lita za mafuta ambayo yote huwa yanaisha ndani ya dakika8 tangu ikianza safari. Kutokana na uzito na umbali wa safari yake kwa ujumla injini hizo mbili za Solid Rocket Booster "SRB" zinazalisha nguvu kufikia horse power million44 au linganisha nguvu ya vichwa vya train 14,000. Rocket injini hizi na tank la mafuta zikifika umbali fulani hujiachia na kurudi duniani hasa pale yanapoisha mafuta yake na kukiacha chombo kinaendelea chenyewe na injini zake ambapo kinakuwa kimefikishwa umbali ambao hakihitaji tena nguvu kubwa. Umbali wa kufikia anga za huko kwenye "Space" au anga za mbali uanzia kilometa 100 kutoka hapa duniani kwenda angani wanasema wataalam wa mambo ya anga. "MWENDO" Wakati kinawashwa kuondoka kutoka katika sehemu yake "launch pad" ndani ya dakika 8 huwa kinafikia mwendo wa 25000 M/hr au 40,000 k/hr hivyo kufanya kwenda kasi mara9 zaidi ya risasi au mara10 ya kasi ya sauti. Mwendo wa sauti ni zaidi ya 1200 k/h. "GHARAMA" Chombo hiki huwa akiruki mara kwa mara isipokuwa kwa misheni maalum tu. Mara nyingi, mara moja kwa miezi miwili au zaidi ya hapo. NASA ambao ndiyo Mamlaka ya Usafiri wa Anga za karibu na mbali huko Marekani ndiyo wahusika wakuu kwenye kurusha chombo hiki. Pia alikuwa anarusha Mrusi na kuna taarifa za Mchina pia alikuwa na program ya kwenda. Marekani ameviita majina vyombo hivyo, >Enteprise-kimestaafu zamani >Colombia-kilipata ajali kikaua wote >Discovery-2011 >Atlantis-2011 >Endeavour- 2011 kiliziba nafasi ya challenger >Challenge-kilipata ajali kikaua wote Mrusi aliita >Buran-na kilienda safari moja tu. Gharama waliyotoa NASA mwaka 2011 kurusha chombo hiki kwa safari moja ni sawa na bei ya kununua Boeing 787 Dreamliner mbili hadi Tano inategemea na misheni husika. Tukumbuke pia sio kila "rocket launch" roketi inayorushwa ni lazima ihusishe chombo hiki, zipo misheni nyengine za anga za mbali ambazo zinapeleka mizigo tu kama satelite n.k pasipo kuwemo watu katika chombo na huwa kinaendeshwa kwa remote control.
    0 Comments ·0 Shares ·680 Views
  • KWANINI WAARABU HUWA HAWATEKI RAIA WA KUTOKA URUSI!????

    Mkwara wa kibabe: Majasusi wa KGB walivyowafanya magaidi wa Hezbollah waliowateka diplomats wao wanne.

    Picha za video za hivi karibuni zilizokuwa zikionesha jinsi wanahabari wa kimarekani bwana James Foley pamoja na Steven sotloff wakikatwa vichwa na magaidi wa ISIS inanikumbusha stori ambayo ilitokea nchini Lebanon mnamo mwaka 1985.

    Mnamo mwezi wa tisa, tarehe 30, mwaka 1985, kundi la watu wenye silaha lilifanikiwa kuwateka nyara wanadiplomasia wanne wa Urusi pamoja na wafanyakazi wa ubalozi wa Urusi nchini Lebanon (Arkady Katkov, Valery Myrikov, Oleg Spirin pamoja na Nikolai Svirsky) katika mji mkuu wa Beirut.

    Wakati wa tukio zima la utekaji nyara huo nje kabisa ya majengo ya ubalozi huo, bwana Katkov alijeruhiwa sehemu ya mguu wake wa kushoto.

    Watekaji nyara hao walijiita ni "Jeshi la Khaled Al-Walid" pamoja na "Islamic Liberation Organization" (ILO). Kulingana na taarifa za idara ya ujasusi wa nje ya Urusi, kanali Yuri Perfilyev, ambaye kwa wakatu huo ndiye aliyekuwa shushushu mkazi (resident spy ama station chief) wa KGB nchini Lebanon, tukio zima la utekaji nyara lilipangwa na kuratibiwa kwa umakini mkubwa na jasusi katili sana wa magaidi wa Hezbollah bwana Imad Mugniyeh kama kujibu mapigo ya wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali ya Syria katika mji wa Tripoli uliopo humo nchini Lebanon. Baada ya kuchukua mateka, magaidi hao wa kishiha wakaitaka kwa nguvu zote serikali ya Urusi kuilazimisha Syria kuacha mara moja kufanya mashambulizi ya kijeshi katika mji wa Tripoli na kuufunga haraka sana ubalozi wake uliopo mjini Beirut.

    Ili kudhihirisha ya kwamba hawakuwa na masihara katika kutaka matakwa yao kutekelezwa, ndani ya siku mbili tu, gaidi mkuu Mugniyeh akamuua bila huruma mwanadiplomasia wa Urusi aliyekuwa amejeruhiwa bwana Katkov kwa kummiminia risasi za kutosha kwa SMG na kisha kuutupa mwili wake kwenye dampo la takataka hapo hapo jijini Beirut.

    KGB station chief bwana Perfilyev kisha akaamua kukutana na bwana mkubwa Ayatollah Muhammad Fadlallah, kiongozi wa kidini wa washiha waishio nchini Lebanon kisha akamwambia;

    "Taifa kubwa kamwe haliwezi kusubiri milele. Tutaacha kusubiri na kutazama na kuamua kuchukua hatua kali zitakazokuwa na madhara yasiyotabirika (mkwara huu......)

    Baada ya kuona ayatollah Fadlallah bado tupo kimya, KGB station chief akazungumza kwa ukali sana safari hii akimwambia;

    " Hatuzungumzii tu kuhusu watu wa Beirut. Ninazungumza kuhusu miji ya Tehran na Qom ambao ni mji mtakatifu wa washiha pamoja na makazi ya Ayatollah Khomeini, ambayo haipo mbali na mpaka wa Urusi.

    Qom ipo karibu sana na Russia na makosa yanaweza kujitokeza na kombora linarusha kwa bahati mbaya. Makosa ya kiufundi yanaweza kutokea kwa bahati mbaya sana na tunaomba Mungu aepushie mbali janga hili"

    Ayatollah Fadlallah ambaye alionekana anatetemeka sana kutokana na mkwara ule wa boss wa KGB akajibu baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu akisema "ninafikiri mambo yote yataenda sawa sawia"

    Baadaye mshauri wa karibu wa Ayatollah Fadlallah bwana Hassan akamwambia KGB boss ya kwamba hakuna mtu aliyewahi kuongea na kiongozi wetu mkuu wa dini kwa ukali wa namna hiyo.

    Kutumia mbinu ya kutishia kushambulia moja kati ya miji kitakatifu sana ya watu wa dhehebu la shiha ilikuwa ni moja tu kati ya mikakati lukuki ya Urusi katika kutaka kuwakomboa diplomats wake, ila baada ya ukimya kuzidi kushika kasi KGB wakaamua kutoa somo la milele kwa magaidi wote wa kiarabu pale mashariki ya kati. Wanaume wa KGB walifanya ushenzi huu mpaka leo wanaogopwa sana na waarabu;

    KGB walimteka mtu waliyejua fika alikuwa ni ndugu wa karibu saaaaana na kiongozi mashuhuri wa Hezbollah. Walimkata vipandevipande vya nyama, kisha wakaweza nyama zile kwenye mfuko na kisha kuvituma kwa viongozi wa juu wa Hezbollah.

    Siku iliyofuata KGB wakakamata ndugu mwingine wa karibu sana wa kiongozi wa Hezbollah, wakamfumua ubongo wake kwa risasi, wakaweka kwenye kiroba, kisha wakapeleka mwili wake kwa viongozi wa magaidi hao.

    Kama hio haitoshi kuonesha ya kwamba wapo serious sana na kazi zao, wababe wa KGB wakawaambia viongozi wa Hezbollah ya kwamba tunajua walipo ndugu zenu wengine wa karibu kabisa na kwamba wategemee vifurushi zaidi vya maiti ndani ya mifuko ya viroba kama wanadiplomasia hao watatu hawataachiwa huru mara moja.

    Baada ya kuonea sasa wamegusa pabaya pasipogusika, viongozi wa Hezbollah wakachukua gari mpya na za kisasa sana aina ya BMW zinazokimbia kwa kasi kubwa sana, wakawabeba wanadiplomasia wale waliobaki hai, kisha kiwapeleka katika ubalozi wa Urusi mjini Beirut.

    Tangia siku hiyo, hakuna mwanadiplomasia wala raia wa Urusi aliyewahi kutekwa nchini Lebanon.

    Hivi ndivyo KGB ilivyokuwa ilifanya kazi. Walikuwa hawaongei mara mbili mbili.

    ****MWISHO****
    KWANINI WAARABU HUWA HAWATEKI RAIA WA KUTOKA URUSI!???? Mkwara wa kibabe: Majasusi wa KGB walivyowafanya magaidi wa Hezbollah waliowateka diplomats wao wanne. Picha za video za hivi karibuni zilizokuwa zikionesha jinsi wanahabari wa kimarekani bwana James Foley pamoja na Steven sotloff wakikatwa vichwa na magaidi wa ISIS inanikumbusha stori ambayo ilitokea nchini Lebanon mnamo mwaka 1985. Mnamo mwezi wa tisa, tarehe 30, mwaka 1985, kundi la watu wenye silaha lilifanikiwa kuwateka nyara wanadiplomasia wanne wa Urusi pamoja na wafanyakazi wa ubalozi wa Urusi nchini Lebanon (Arkady Katkov, Valery Myrikov, Oleg Spirin pamoja na Nikolai Svirsky) katika mji mkuu wa Beirut. Wakati wa tukio zima la utekaji nyara huo nje kabisa ya majengo ya ubalozi huo, bwana Katkov alijeruhiwa sehemu ya mguu wake wa kushoto. Watekaji nyara hao walijiita ni "Jeshi la Khaled Al-Walid" pamoja na "Islamic Liberation Organization" (ILO). Kulingana na taarifa za idara ya ujasusi wa nje ya Urusi, kanali Yuri Perfilyev, ambaye kwa wakatu huo ndiye aliyekuwa shushushu mkazi (resident spy ama station chief) wa KGB nchini Lebanon, tukio zima la utekaji nyara lilipangwa na kuratibiwa kwa umakini mkubwa na jasusi katili sana wa magaidi wa Hezbollah bwana Imad Mugniyeh kama kujibu mapigo ya wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali ya Syria katika mji wa Tripoli uliopo humo nchini Lebanon. Baada ya kuchukua mateka, magaidi hao wa kishiha wakaitaka kwa nguvu zote serikali ya Urusi kuilazimisha Syria kuacha mara moja kufanya mashambulizi ya kijeshi katika mji wa Tripoli na kuufunga haraka sana ubalozi wake uliopo mjini Beirut. Ili kudhihirisha ya kwamba hawakuwa na masihara katika kutaka matakwa yao kutekelezwa, ndani ya siku mbili tu, gaidi mkuu Mugniyeh akamuua bila huruma mwanadiplomasia wa Urusi aliyekuwa amejeruhiwa bwana Katkov kwa kummiminia risasi za kutosha kwa SMG na kisha kuutupa mwili wake kwenye dampo la takataka hapo hapo jijini Beirut. KGB station chief bwana Perfilyev kisha akaamua kukutana na bwana mkubwa Ayatollah Muhammad Fadlallah, kiongozi wa kidini wa washiha waishio nchini Lebanon kisha akamwambia; "Taifa kubwa kamwe haliwezi kusubiri milele. Tutaacha kusubiri na kutazama na kuamua kuchukua hatua kali zitakazokuwa na madhara yasiyotabirika (mkwara huu......) Baada ya kuona ayatollah Fadlallah bado tupo kimya, KGB station chief akazungumza kwa ukali sana safari hii akimwambia; " Hatuzungumzii tu kuhusu watu wa Beirut. Ninazungumza kuhusu miji ya Tehran na Qom ambao ni mji mtakatifu wa washiha pamoja na makazi ya Ayatollah Khomeini, ambayo haipo mbali na mpaka wa Urusi. Qom ipo karibu sana na Russia na makosa yanaweza kujitokeza na kombora linarusha kwa bahati mbaya. Makosa ya kiufundi yanaweza kutokea kwa bahati mbaya sana na tunaomba Mungu aepushie mbali janga hili" Ayatollah Fadlallah ambaye alionekana anatetemeka sana kutokana na mkwara ule wa boss wa KGB akajibu baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu akisema "ninafikiri mambo yote yataenda sawa sawia" Baadaye mshauri wa karibu wa Ayatollah Fadlallah bwana Hassan akamwambia KGB boss ya kwamba hakuna mtu aliyewahi kuongea na kiongozi wetu mkuu wa dini kwa ukali wa namna hiyo. Kutumia mbinu ya kutishia kushambulia moja kati ya miji kitakatifu sana ya watu wa dhehebu la shiha ilikuwa ni moja tu kati ya mikakati lukuki ya Urusi katika kutaka kuwakomboa diplomats wake, ila baada ya ukimya kuzidi kushika kasi KGB wakaamua kutoa somo la milele kwa magaidi wote wa kiarabu pale mashariki ya kati. Wanaume wa KGB walifanya ushenzi huu mpaka leo wanaogopwa sana na waarabu; KGB walimteka mtu waliyejua fika alikuwa ni ndugu wa karibu saaaaana na kiongozi mashuhuri wa Hezbollah. Walimkata vipandevipande vya nyama, kisha wakaweza nyama zile kwenye mfuko na kisha kuvituma kwa viongozi wa juu wa Hezbollah. Siku iliyofuata KGB wakakamata ndugu mwingine wa karibu sana wa kiongozi wa Hezbollah, wakamfumua ubongo wake kwa risasi, wakaweka kwenye kiroba, kisha wakapeleka mwili wake kwa viongozi wa magaidi hao. Kama hio haitoshi kuonesha ya kwamba wapo serious sana na kazi zao, wababe wa KGB wakawaambia viongozi wa Hezbollah ya kwamba tunajua walipo ndugu zenu wengine wa karibu kabisa na kwamba wategemee vifurushi zaidi vya maiti ndani ya mifuko ya viroba kama wanadiplomasia hao watatu hawataachiwa huru mara moja. Baada ya kuonea sasa wamegusa pabaya pasipogusika, viongozi wa Hezbollah wakachukua gari mpya na za kisasa sana aina ya BMW zinazokimbia kwa kasi kubwa sana, wakawabeba wanadiplomasia wale waliobaki hai, kisha kiwapeleka katika ubalozi wa Urusi mjini Beirut. Tangia siku hiyo, hakuna mwanadiplomasia wala raia wa Urusi aliyewahi kutekwa nchini Lebanon. Hivi ndivyo KGB ilivyokuwa ilifanya kazi. Walikuwa hawaongei mara mbili mbili. ****MWISHO****
    0 Comments ·0 Shares ·851 Views
  • Hii ndio ilikuwa Bendera yetu, na katikati ya Bendera ni Ngao ya Jamii (Coat of Arms) ya Nchi yetu enzi tunaitwa Deutsch-Ostafrika (Ujerumani ya Afrika Mashariki) miaka ya 1885 mpaka 1918.

    Wakati huo nchi ilikuwa na eneo la Mita Square 994,996 Km² ndani yake kuna Burundi na Rwanda, na Eneo la Nchi ya Msumbiji lililoitwa Kionga Triangle.

    Je wajua neno la Kiswahili "Shule" limetoka kwenye Neno la Kijerumani "Schule" yote yakimaanisha "School".

    Maeneo mengine yaliitwa hivi:

    • Rombo iliitwa Fischerstadt
    • Nyakanazi iliitwa Friedberg
    • Kisarawe iliitwa Hoffnungshöh
    • Tukuyu iliitwa Langenburg
    • Ushetu iliitwa Marienthal
    • Shume (huko kwa Wapare) kuliitwa Neu-Hornow
    • Mbulu kuliitwa Neu-Trier
    • Sekenke paliitwa Sachsenwald na ilikua ni Mgodi.
    • Lushoto iliitwa Wilhelmsdorf.

    Kipindi hiki ndio tulijengewa Reli iliyoitwa Usambara Railway mwaka 1891 ilijengwa na Wajerumani na ilikuwa na Km 350, ilianzia Mjini Tanga, ikawa na makutano na Kenya Mji wa Kahe, ikapita Moshi mpaka Arusha.

    Wajerumani katika Reli hii walikuwa na vichwa vya Treni 18 (Locomotive) na mabehewa 199, kipindi hicho Reli hii ilikuwa na wafanyakazi 562 huku kati yao 35 tu ndio walikuwa Wajerumani.

    Lengo la Wajerumani kujenga Reli hii ilikuwa ni kuunganisha Bandari ya Tanga na Ziwa Victoria kupitia milima ya Usambara.

    Treni la kwanza lilipita likiwa tupu tarehe 26 September 1911 ili kujaribu safari na kufanikiwa 100%, likapita tena likiwa na Abiria tarehe 4 October 1911 na kufanikiwa 100% Wajerumani wakaamini kweli kitu ni Konki.

    Hivyo ukafanyika uzinduzi wa Reli tarehe 7 February 1912, na baada ya hapo Treni lilikuwa lazima lifanye safari kila siku kutoka Tanga mpaka Buiko na Kurudi, safari ilichukua muda wa masaa 14 na dakika 40.

    Reli hii haikukamilika mpaka Arusha sababu ya Vita ya kwanza ya Dunia, Waingereza ndio Wakaiunganisha.

    #Kutoka_Maktaba
    Hii ndio ilikuwa Bendera yetu, na katikati ya Bendera ni Ngao ya Jamii (Coat of Arms) ya Nchi yetu enzi tunaitwa Deutsch-Ostafrika (Ujerumani ya Afrika Mashariki) miaka ya 1885 mpaka 1918. Wakati huo nchi ilikuwa na eneo la Mita Square 994,996 Km² ndani yake kuna Burundi na Rwanda, na Eneo la Nchi ya Msumbiji lililoitwa Kionga Triangle. Je wajua neno la Kiswahili "Shule" limetoka kwenye Neno la Kijerumani "Schule" yote yakimaanisha "School". Maeneo mengine yaliitwa hivi: • Rombo iliitwa Fischerstadt • Nyakanazi iliitwa Friedberg • Kisarawe iliitwa Hoffnungshöh • Tukuyu iliitwa Langenburg • Ushetu iliitwa Marienthal • Shume (huko kwa Wapare) kuliitwa Neu-Hornow • Mbulu kuliitwa Neu-Trier • Sekenke paliitwa Sachsenwald na ilikua ni Mgodi. • Lushoto iliitwa Wilhelmsdorf. Kipindi hiki ndio tulijengewa Reli iliyoitwa Usambara Railway mwaka 1891 ilijengwa na Wajerumani na ilikuwa na Km 350, ilianzia Mjini Tanga, ikawa na makutano na Kenya Mji wa Kahe, ikapita Moshi mpaka Arusha. Wajerumani katika Reli hii walikuwa na vichwa vya Treni 18 (Locomotive) na mabehewa 199, kipindi hicho Reli hii ilikuwa na wafanyakazi 562 huku kati yao 35 tu ndio walikuwa Wajerumani. Lengo la Wajerumani kujenga Reli hii ilikuwa ni kuunganisha Bandari ya Tanga na Ziwa Victoria kupitia milima ya Usambara. Treni la kwanza lilipita likiwa tupu tarehe 26 September 1911 ili kujaribu safari na kufanikiwa 100%, likapita tena likiwa na Abiria tarehe 4 October 1911 na kufanikiwa 100% Wajerumani wakaamini kweli kitu ni Konki. Hivyo ukafanyika uzinduzi wa Reli tarehe 7 February 1912, na baada ya hapo Treni lilikuwa lazima lifanye safari kila siku kutoka Tanga mpaka Buiko na Kurudi, safari ilichukua muda wa masaa 14 na dakika 40. Reli hii haikukamilika mpaka Arusha sababu ya Vita ya kwanza ya Dunia, Waingereza ndio Wakaiunganisha. #Kutoka_Maktaba
    Like
    2
    · 1 Comments ·0 Shares ·563 Views
  • HOTELI YA NAURA ILIYOPO ARUSHA, KUPIGWA MNADA ALHAMISI TAREHE 12.12.2024
    HOTELI YA NAURA ILIYOPO ARUSHA, KUPIGWA MNADA ALHAMISI TAREHE 12.12.2024
    Like
    5
    · 0 Comments ·0 Shares ·300 Views
  • Ujenzi wa Uwanja mpya wa mpira wa miguu jijini Arusha wazidi kushika kasi.

    Uwanja huu umepewa jina la Raisi wa kwanza mwanamke Tanzania Mh Dr Samia Suluhu Hassan Stadium.

    uwanja huu ni moja kati ya viwanja vitakavyo tumika kwenye mashindano ya AFCON 2027.

    Tanzania itashirikiana na majira zake Kenya na Uganda kwenye mandalizi ya mashindano haya makubwa barani Africa.
    Ujenzi wa Uwanja mpya wa mpira wa miguu jijini Arusha wazidi kushika kasi. Uwanja huu umepewa jina la Raisi wa kwanza mwanamke Tanzania Mh Dr Samia Suluhu Hassan Stadium. uwanja huu ni moja kati ya viwanja vitakavyo tumika kwenye mashindano ya AFCON 2027. Tanzania itashirikiana na majira zake Kenya na Uganda kwenye mandalizi ya mashindano haya makubwa barani Africa.
    Like
    Love
    8
    · 1 Comments ·0 Shares ·401 Views
  • Habar zenu Mimi nikijana nipo tu Sina kazi Mwenye mishe anisaidie na Mimi nipate, Nipo Arusha
    Habar zenu Mimi nikijana nipo tu Sina kazi Mwenye mishe anisaidie na Mimi nipate, Nipo Arusha
    0 Comments ·0 Shares ·277 Views
  • K/KOO DERBY | SIMBA vs YANGA

    MWAMUZI WA KATI
    ELLY SASII (DARES SALAAM)

    MWAMUZI MSAIDIZI 1
    MOHAMED MKONO (TANGA)

    MWAMUZI MSAIDIZI 2
    KASSIM MPANGA (DARES SALAAM)

    MWAMUZI WA AKIBA
    AMINA KYANDO (MOROGORO)

    MTATHMINI WAAMUZI
    SOUD ABDI (ARUSHA)
    K/KOO DERBY | SIMBA vs YANGA MWAMUZI WA KATI ELLY SASII (DARES SALAAM) MWAMUZI MSAIDIZI 1 MOHAMED MKONO (TANGA) MWAMUZI MSAIDIZI 2 KASSIM MPANGA (DARES SALAAM) MWAMUZI WA AKIBA AMINA KYANDO (MOROGORO) MTATHMINI WAAMUZI SOUD ABDI (ARUSHA)
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·250 Views
  • Harmonize Karusha Kijembe Kwa Diamond Platnumz.
    Harmonize Karusha Kijembe Kwa Diamond Platnumz.
    0 Comments ·0 Shares ·408 Views
  • hip hop ngumu,, nai kata kaa utepe!!
    mi zaidi ya sumu,, unaleta za bele 9 nilipe nisepe!!
    Pusha, sema hii yawapi,, ni arusha jamaica au ya dom!!
    Shusha, bei shingapi,, hatuna cha kupoteza home!!
    hip hop ngumu,, nai kata kaa utepe!! mi zaidi ya sumu,, unaleta za bele 9 nilipe nisepe!! Pusha, sema hii yawapi,, ni arusha jamaica au ya dom!! Shusha, bei shingapi,, hatuna cha kupoteza home!!
    0 Comments ·0 Shares ·249 Views
  • hip hop ngumu,, nai kata kaa utepe!!
    mi zaidi ya sumu,, unaleta za bele 9 nilipe nisepe!!
    Pusha, sema hii yawapi,, ni arusha jamaica au ya dom!!
    Shusha, bei shingapi,, hatuna cha kupoteza home!!
    hip hop ngumu,, nai kata kaa utepe!! mi zaidi ya sumu,, unaleta za bele 9 nilipe nisepe!! Pusha, sema hii yawapi,, ni arusha jamaica au ya dom!! Shusha, bei shingapi,, hatuna cha kupoteza home!!
    0 Comments ·0 Shares ·242 Views
  • HIP Hop Hisia Nyingi Ma balz Mingi Napokuwa Narap..
    Najiona Zaidi Dingi Demu Kiganja Napigi Safu..
    Umenipa Nini Hip Hop Nafanya Vingi Juu Yako..
    Bila Shilingi Me Mbavu Najiamini Nikiwa Kwako..
    Nilishakana Kubana Pua Wote Mashoga Bongo Wanazingua..
    Siko Dom Arusha Nakichafua Nakwako Ndo Nimeshatua..
    Hip Hop Nikupe Nini Usiwafate Maemce Shilingi..
    HIP Hop Hisia Nyingi Ma balz Mingi Napokuwa Narap.. Najiona Zaidi Dingi Demu Kiganja Napigi Safu.. Umenipa Nini Hip Hop Nafanya Vingi Juu Yako.. Bila Shilingi Me Mbavu Najiamini Nikiwa Kwako.. Nilishakana Kubana Pua Wote Mashoga Bongo Wanazingua.. Siko Dom Arusha Nakichafua Nakwako Ndo Nimeshatua.. Hip Hop Nikupe Nini Usiwafate Maemce Shilingi..
    0 Comments ·0 Shares ·456 Views
  • Wauni tulio peace hatuishi kwa masifa..
    Naishinao mm mbishi sifa zitakuja siku nikifa..
    Wasionipenda waambieni npo Arusha bado naishi..
    Tena siwawazi nikila nashushia na kushi..
    Manigger mwendokasi xyoo ubitozi..
    Nashangaa wanapanga kikosi kunisaka wamekosa kazi..
    Gari limeshawashwa katikati ya sheli..
    Uvutaji wa sigara ni hatari ukiwa mmbovu wa seli..
    Wauni tulio peace hatuishi kwa masifa.. Naishinao mm mbishi sifa zitakuja siku nikifa.. Wasionipenda waambieni npo Arusha bado naishi.. Tena siwawazi nikila nashushia na kushi.. Manigger mwendokasi xyoo ubitozi.. Nashangaa wanapanga kikosi kunisaka wamekosa kazi.. Gari limeshawashwa katikati ya sheli.. Uvutaji wa sigara ni hatari ukiwa mmbovu wa seli..
    0 Comments ·0 Shares ·275 Views
  • wanasota kutunga rhymes, freestyle nazikatia dengE
    wakinikuta maskani, wanasema ni la wahuni gengE
    au imekuwa kosa sisi Masela kuvuta bangE
    msifananishe mtindo wa Rap na miziki ya WengE
    au Maskani East zoo na Arusha pale KijengE
    ...bundle limemanda but........2B Continued...
    wanasota kutunga rhymes, freestyle nazikatia dengE wakinikuta maskani, wanasema ni la wahuni gengE au imekuwa kosa sisi Masela kuvuta bangE msifananishe mtindo wa Rap na miziki ya WengE au Maskani East zoo na Arusha pale KijengE ...bundle limemanda but........2B Continued...
    Like
    5
    · 1 Comments ·0 Shares ·269 Views
More Results