• 10/21 Nguvu za Mungu.

    Huwezi kumuona Mungu ikiwa tu hufanyi mapenzi yake .

    Moja ya mapenzi ya Mungu ni kuona kanisa linamju Mungu katika eneo la msamaha.

    Nguvu za Mungu zinatafutwa na muamini anaye zihitaji .

    Zaburi 105:4

    *Mtakeni BWANA na nguvu zake, Utafuteni uso wake sikuzote*

    Ukiona maandiko yameweka wazi kabisa kwamba nguvu za Mungu ili uzipate lazima uzitake kwa kuomba, kusoma neno na kulitafakari na kuzidi kutenda wema.

    *Watu wengi tunachanganya mambo tunazani ukiokoka tu nguvu za Mungu utakuwa nazo kitu ambacho si kweli .*

    Mitume walio fanya kazi na Yesu bdo yesu aliwapa maelekezo ya kupata nguvu zake kupitia msaada wa roho mtakatifu lakini pia walikutwa wanaomba .

    Walipokea nguvu wakati wakiendelea na maombi.

    Matendo 1:8 SUV
    *Lakini wakati Roho Mtakatifu atakapowashukieni nyinyi, mtapokea nguvu na mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, katika nchi yote ya Yudea na Samaria, na hata miisho ya dunia.”*

    Kumbe maombi ndiyo siri ya kupata nguvu za kuweza kukusaidia hata kishinda majaribu.

    *Kadiri unavyo weza mtafuta Mungu katika kuongezeka nguvu zake ndivyo unavyo jisogeza mbali na majaribu na mitego ya majaribu.*

    Yesu alishinda jaribu kwa kuwa alikuwa mtu wa maombi muda wake wote aliokuwepo duniani.
    Luka 5
    *Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani*
    Kumbe alipata kumshinda shetani katika jaribu zote kwa sababu tu alipata nguvu kipitia zile siku arobaini.

    Sasa kumbe kuna watu sababu ya kukosa nguvu wnazimia kirahisi sana.

    Mithali 24:10
    *Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache.*

    *Wokovu ni zaidi ya hapo kwani lazima uamue kuto kuzimia kabisa .*

    Ukiokoka lazima ujifunze kuzitaka nguvu za Mungu kupitia roho takatifu ili usiweze zimia moyo.

    Ni matumaini yangu maombi yanaweza kuwa maisha yetu ili tupate kumuona Mungu.

    Bila maombi uwezi pokea kwani biblia inasema ili *upokee lazima tuombe*

    Na yesu pia anasema *tukeshe katika maombi*

    Nguvu za Mungu ni muhimu sana ili uufurahie wokovu na ahadi za Mungu.

    *Mtafute bwana naye awe shirika nawe ili upate kuishi mapenzi yake .*

    Ahsante sana naitwa mwl.Sylvester Mwakabende (kutoka build new eden )

    #build new eden
    #Restoremenposition
    10/21 Nguvu za Mungu. Huwezi kumuona Mungu ikiwa tu hufanyi mapenzi yake . Moja ya mapenzi ya Mungu ni kuona kanisa linamju Mungu katika eneo la msamaha. Nguvu za Mungu zinatafutwa na muamini anaye zihitaji . Zaburi 105:4 *Mtakeni BWANA na nguvu zake, Utafuteni uso wake sikuzote* Ukiona maandiko yameweka wazi kabisa kwamba nguvu za Mungu ili uzipate lazima uzitake kwa kuomba, kusoma neno na kulitafakari na kuzidi kutenda wema. *Watu wengi tunachanganya mambo tunazani ukiokoka tu nguvu za Mungu utakuwa nazo kitu ambacho si kweli .* Mitume walio fanya kazi na Yesu bdo yesu aliwapa maelekezo ya kupata nguvu zake kupitia msaada wa roho mtakatifu lakini pia walikutwa wanaomba . Walipokea nguvu wakati wakiendelea na maombi. Matendo 1:8 SUV *Lakini wakati Roho Mtakatifu atakapowashukieni nyinyi, mtapokea nguvu na mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, katika nchi yote ya Yudea na Samaria, na hata miisho ya dunia.”* Kumbe maombi ndiyo siri ya kupata nguvu za kuweza kukusaidia hata kishinda majaribu. *Kadiri unavyo weza mtafuta Mungu katika kuongezeka nguvu zake ndivyo unavyo jisogeza mbali na majaribu na mitego ya majaribu.* Yesu alishinda jaribu kwa kuwa alikuwa mtu wa maombi muda wake wote aliokuwepo duniani. Luka 5 *Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani* Kumbe alipata kumshinda shetani katika jaribu zote kwa sababu tu alipata nguvu kipitia zile siku arobaini. Sasa kumbe kuna watu sababu ya kukosa nguvu wnazimia kirahisi sana. Mithali 24:10 *Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache.* *Wokovu ni zaidi ya hapo kwani lazima uamue kuto kuzimia kabisa .* Ukiokoka lazima ujifunze kuzitaka nguvu za Mungu kupitia roho takatifu ili usiweze zimia moyo. Ni matumaini yangu maombi yanaweza kuwa maisha yetu ili tupate kumuona Mungu. Bila maombi uwezi pokea kwani biblia inasema ili *upokee lazima tuombe* Na yesu pia anasema *tukeshe katika maombi* Nguvu za Mungu ni muhimu sana ili uufurahie wokovu na ahadi za Mungu. *Mtafute bwana naye awe shirika nawe ili upate kuishi mapenzi yake .* Ahsante sana naitwa mwl.Sylvester Mwakabende (kutoka build new eden ) #build new eden #Restoremenposition
    0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·155 Visualizações
  • 6/21 .MTAKATIFU ANAYE ISHI.

    Utakatifu ni kitendo cha kutakaswa. na kutakaswa ni kuwa safi .
    Kiebrania HAGOIS usimama kama maneno ,vitu na watu waliotengwa kwa ajiri ya Mungu.

    1samweli 2:2
    *Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA; Kwa maana hakuna yeyote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu*

    Fasiri stahiki ni kuwa Mungu ana viwango vyake vya utakatifu tofauti na sisi wanadamu .

    Lengo la Mungu kumuumba mwanadamu ilikuwa awe copy yake au mfano wake .
    Mwanzo 2:27
    *Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba*

    Kama sisi tu mfano au mfanano na Mungu wetu kwa asili ni mtakatifu kumbe hata sisi yatupasa kuwa watakatifu.

    Lawi 19:2.
    *Nena na mkutano wote wa wana wa Israeli, uwaambie, Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wenu, ni mtakatifu*

    Kuna watu sababu ya uelewa wao mkubwa utasikia hilo ni agano la kale sisi tuko ndani ya neema .

    Ok Petro mtume na shujaa aliye kabidhiwa kanisa na Kristo mwenyewe ananukuu

    1 Petro 1:15-16
    *Bali mnapaswa kuwa watakatifu katika mwenendo wenu wote, kama vile yule aliyewaiteni ni mtakatifu. Maandiko yasema: “Muwe watakatifu, kwa kuwa mimi alivyo mtakatifu.”*
    Utakatifu ndio unao tusogeza njia ya ukamolifu.
    Yesu mwenyewe anaonyesha
    Mathayo 5:48 NIV
    *Basi, muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.*

    Na ili uwe mkamilifu kama Mungu lazima uwe mtakatifu.

    Utakatifu kwetu si tukio u pendekezo bali ni maisha ya mwamini.

    *Sababu ya kanisa kukosa utakatifu tumezalisha kizazi cha kuombewa kila siku na hata wakati mwingine tunaishi na shida zetu sababu tumeshindwa mlingana mungu.*

    *Utakatifu kwa mwokovu ni swala la lazima na siyo hiari*

    Nakupenda wewe jasiri wa imani ambaye unamtafuta Mungu kuliko chochote kile na mungu lazima atakujibu tu kama hautazimia moyo.

    Kama wafuasi wa maisha ya kristo lazima utuishi katika utakatifu kwani ndiyo toka uumbaji MAPENZI yake MUNGU.

    Neno neema lisikuponze kiasi cha kuona kuwa upaswi kuishi kwa utakatifu ni kujipotezea muda wewe mwenyewe .

    Bwana awezi kuwa mkuu kwako ikiwa wewe uwezi kumuheshimu kiwango anacho stahili.

    Nazungumza na mtu mmoja ambaye ni praise team lakini pia kila weekend anazini kamwe uwezi muona Mungu sawa sawa na mapenzi yake.

    Kaka ukichagua kuokokz lazima uwe mtakatifu unayeishi duniani .

    Ok naitwa Sylvester Mwakabende kutoka BUILD NEW EDEN

    #build new eden
    #restore men position
    6/21 .MTAKATIFU ANAYE ISHI. Utakatifu ni kitendo cha kutakaswa. na kutakaswa ni kuwa safi . Kiebrania HAGOIS usimama kama maneno ,vitu na watu waliotengwa kwa ajiri ya Mungu. 1samweli 2:2 *Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA; Kwa maana hakuna yeyote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu* Fasiri stahiki ni kuwa Mungu ana viwango vyake vya utakatifu tofauti na sisi wanadamu . Lengo la Mungu kumuumba mwanadamu ilikuwa awe copy yake au mfano wake . Mwanzo 2:27 *Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba* Kama sisi tu mfano au mfanano na Mungu wetu kwa asili ni mtakatifu kumbe hata sisi yatupasa kuwa watakatifu. Lawi 19:2. *Nena na mkutano wote wa wana wa Israeli, uwaambie, Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wenu, ni mtakatifu* Kuna watu sababu ya uelewa wao mkubwa🤣 utasikia hilo ni agano la kale sisi tuko ndani ya neema . Ok Petro mtume na shujaa aliye kabidhiwa kanisa na Kristo mwenyewe ananukuu 1 Petro 1:15-16 *Bali mnapaswa kuwa watakatifu katika mwenendo wenu wote, kama vile yule aliyewaiteni ni mtakatifu. Maandiko yasema: “Muwe watakatifu, kwa kuwa mimi alivyo mtakatifu.”* Utakatifu ndio unao tusogeza njia ya ukamolifu. Yesu mwenyewe anaonyesha Mathayo 5:48 NIV *Basi, muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.* Na ili uwe mkamilifu kama Mungu lazima uwe mtakatifu. Utakatifu kwetu si tukio u pendekezo bali ni maisha ya mwamini. *Sababu ya kanisa kukosa utakatifu tumezalisha kizazi cha kuombewa kila siku na hata wakati mwingine tunaishi na shida zetu sababu tumeshindwa mlingana mungu.* *Utakatifu kwa mwokovu ni swala la lazima na siyo hiari* Nakupenda wewe jasiri wa imani ambaye unamtafuta Mungu kuliko chochote kile na mungu lazima atakujibu tu kama hautazimia moyo. Kama wafuasi wa maisha ya kristo lazima utuishi katika utakatifu kwani ndiyo toka uumbaji MAPENZI yake MUNGU. Neno neema lisikuponze kiasi cha kuona kuwa upaswi kuishi kwa utakatifu ni kujipotezea muda wewe mwenyewe . Bwana awezi kuwa mkuu kwako ikiwa wewe uwezi kumuheshimu kiwango anacho stahili. Nazungumza na mtu mmoja ambaye ni praise team lakini pia kila weekend anazini kamwe uwezi muona Mungu sawa sawa na mapenzi yake. Kaka ukichagua kuokokz lazima uwe mtakatifu unayeishi duniani . Ok naitwa Sylvester Mwakabende kutoka BUILD NEW EDEN #build new eden #restore men position
    0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·203 Visualizações
  • MAOMBI YANAYO JIBIWA SEHEMU YAPILI.

    *Mungu huwa awezi kutenda kinyume na neno lake hii ndiyo sababu inatufanya tuombe kwa kumkumbusha ahadi zake.*

    Mungu aliapa kwa neno nafsi yake kumbariki Abraham na mpaka leo islaeri yote huesabika kuwa waendelewa sababu tu ya neno alilo mwapia ibrahimu.

    *Kwanini basi tunapaswa kuomba kwa kutumia neno.*

    1.Tunayajua mapenzi yake kupitia neno lake.

    Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.

    *Kumbe ili usikike kirahisi lazima umkumbushe mapenzi yake kwako kupitia neno lake.*

    Mathayo 6:10. "Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni."

    *Hii ni sehemu ya sala aliyo wafundisha Yesu mwenyewe kuwa wakati wakuomba lazima uyaombe mapenzi ya Mungu yatimilike na hayawezi timilika bila neno lake.*

    Na mapenzi ya Mungu yanapatikana au yanasikika kupitia neno lake.

    2.Neno la mungu lina mamlaka .

    Yohana 1;3-5
    *Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. 4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. 5 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.*

    Neno ndo lenye mamlaka pasipo neno nuru haikuwapo.

    *Mungu mwenyewe katika uumbaji alianza kwanza na neno ndipo ikawa ,*,

    Kumbe neno ndilo utupa mamlaka ya kumkemea muovu na mamlaka .

    *Neno ndio funguo yenye mamlaka ya kupokea au kutokupokea kwani Mungu anapo sikiliza maombi anatazama neno lake linasema nini.*

    Ebrania 4:12-13
    Paulo katika mistali anaonyesha mamlaka na nguvu za neno la Mungu,1.liko hai 2.linanguvu kweli kweli .
    33.ni kali kama kupanga ukatao kuwili .

    *Ok ukisoma mstali kwa mstali ebrania 4;12-13 utoana ni kwa jinsi gani neno la Mungu lina nguvu kweli kweli.*

    Turudi msalabani tumkumbushe Mungu kupitia ahadi zake kupitia neno lake.

    Marko 16:17
    *Nazo ishara hizi zitafuatana na wanaoamini: Kwa Jina langu watatoa pepo wachafu; watasema kwa lugha mpya*

    *Ni neno lake ndilo linalo tuwezesha kupata mamlaka .si kitu kingine chochote.*

    Natamani leo tukiomba tuombe kwa kupitia neno lake ili Mungu Atujibu sawasawa na neno lake.

    Ahsante sana naitwa sylvester Mwakabende kutoka (Build new eden)
    #build new eden
    #restore men position
    MAOMBI YANAYO JIBIWA SEHEMU YAPILI. *Mungu huwa awezi kutenda kinyume na neno lake hii ndiyo sababu inatufanya tuombe kwa kumkumbusha ahadi zake.* Mungu aliapa kwa neno nafsi yake kumbariki Abraham na mpaka leo islaeri yote huesabika kuwa waendelewa sababu tu ya neno alilo mwapia ibrahimu. *Kwanini basi tunapaswa kuomba kwa kutumia neno.* 1.Tunayajua mapenzi yake kupitia neno lake. Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. *Kumbe ili usikike kirahisi lazima umkumbushe mapenzi yake kwako kupitia neno lake.* Mathayo 6:10. "Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni." *Hii ni sehemu ya sala aliyo wafundisha Yesu mwenyewe kuwa wakati wakuomba lazima uyaombe mapenzi ya Mungu yatimilike na hayawezi timilika bila neno lake.* Na mapenzi ya Mungu yanapatikana au yanasikika kupitia neno lake. 2.Neno la mungu lina mamlaka . Yohana 1;3-5 *Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. 4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. 5 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.* Neno ndo lenye mamlaka pasipo neno nuru haikuwapo. *Mungu mwenyewe katika uumbaji alianza kwanza na neno ndipo ikawa ,*, Kumbe neno ndilo utupa mamlaka ya kumkemea muovu na mamlaka . *Neno ndio funguo yenye mamlaka ya kupokea au kutokupokea kwani Mungu anapo sikiliza maombi anatazama neno lake linasema nini.* Ebrania 4:12-13 Paulo katika mistali anaonyesha mamlaka na nguvu za neno la Mungu,1.liko hai 2.linanguvu kweli kweli . 33.ni kali kama kupanga ukatao kuwili . *Ok ukisoma mstali kwa mstali ebrania 4;12-13 utoana ni kwa jinsi gani neno la Mungu lina nguvu kweli kweli.* Turudi msalabani tumkumbushe Mungu kupitia ahadi zake kupitia neno lake. Marko 16:17 *Nazo ishara hizi zitafuatana na wanaoamini: Kwa Jina langu watatoa pepo wachafu; watasema kwa lugha mpya* *Ni neno lake ndilo linalo tuwezesha kupata mamlaka .si kitu kingine chochote.* Natamani leo tukiomba tuombe kwa kupitia neno lake ili Mungu Atujibu sawasawa na neno lake. Ahsante sana naitwa sylvester Mwakabende kutoka (Build new eden) #build new eden #restore men position
    Love
    1
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·321 Visualizações
  • 1/21
    MAOMBI YENYE TIJA MBELE ZA MUNGU.

    tuanze kwa kujua nini maana ya maombi.

    Maombi ni mazungumzo kati ya mtu aliye okoka na Mungu wake .
    Isaya 1:18.
    Haya, *njoni, tusemezane, asema BWANA*. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama damu, zitakuwa kama sufu.

    Maombi ni hali ya kuhitaji kupeleka mahitaji yetu mbele za bwana.
    Filip 4:6
    6 Msifadhaike juu ya jambo lo lote; lakini katika kila jambo mjulisheni Mungu haja zenu, kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru.

    Maombi ndiyo kibali kinacho mpa Mungu nafasi ya kuingilia kati mambo ya watoto wake.

    Mathayo 7:7-8
    *“Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni mlango, nanyi mtafunguliwa. Maana, yeyote aombaye hupewa, atafutaye hupata, na abishaye mlango hufunguliwa.*

    Maombi ni vita .

    Efeso 6:10-12
    Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

    Maombi pia ni ibada .
    Zaburi 42:1-3

    Maombi yanayo jibiwa ni maombi yanayo ambatana na neno la Mungu.

    Mungu anapo jibu maombi anajibu neno lake siyo wewe unasema nini.

    Ili maombi yako yajibiwe lazima uwe na uhakika naye unaye muomba .

    Warumi 10:17
    *Imani chanzo chake ni kusikia ,na kusikia huja kwa neno la kristo.

    Kiwango chako cha kuliamini neno ndicho kinacho amua aina ya majibu unayo yataka.

    Natamani unavyo ingia msimu mpya uombe kama mtu wa mbinguni kwa kila ombi kumkumbusha Mungu neno lake.

    Mfano.
    Unataka kufanikiwa mkumbushe mungu kuwa kwa neno lako umesema madamu muda wa kupanda udumupo wakati wa kuvuna hauta koma.

    Au kwa neno lako *umesema sinta kuwa mkia nitakuwa kichwa*
    Ndipo anza kuingiza haja yako .

    Au kwa neno lako *umesema nitabarikiwa mjini nitabarikiwa shambani* ndipo uendelee na haja zako.

    Ili umpendeze Mungu lazima uwe na neno lake .
    Ebrania 11:6

    Mungu hawezi kwenda kinyume na neno lake hiyo ndiyo sababu ya kuomba kwa neno lake.
    Ebrania 6:16-17
    Yeremia 1:12

    Mungu alimwambia yeremia umenena vema kwa maana mimi Bwana naangalia neno langu hili nitimize.
    Natumaini maombi yetu leo yataongozwa na neno la Mungu.
    #build new eden
    1/21 MAOMBI YENYE TIJA MBELE ZA MUNGU. tuanze kwa kujua nini maana ya maombi. Maombi ni mazungumzo kati ya mtu aliye okoka na Mungu wake . Isaya 1:18. Haya, *njoni, tusemezane, asema BWANA*. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama damu, zitakuwa kama sufu. Maombi ni hali ya kuhitaji kupeleka mahitaji yetu mbele za bwana. Filip 4:6 6 Msifadhaike juu ya jambo lo lote; lakini katika kila jambo mjulisheni Mungu haja zenu, kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru. Maombi ndiyo kibali kinacho mpa Mungu nafasi ya kuingilia kati mambo ya watoto wake. Mathayo 7:7-8 *“Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni mlango, nanyi mtafunguliwa. Maana, yeyote aombaye hupewa, atafutaye hupata, na abishaye mlango hufunguliwa.* Maombi ni vita . Efeso 6:10-12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Maombi pia ni ibada . Zaburi 42:1-3 Maombi yanayo jibiwa ni maombi yanayo ambatana na neno la Mungu. Mungu anapo jibu maombi anajibu neno lake siyo wewe unasema nini. Ili maombi yako yajibiwe lazima uwe na uhakika naye unaye muomba . Warumi 10:17 *Imani chanzo chake ni kusikia ,na kusikia huja kwa neno la kristo. Kiwango chako cha kuliamini neno ndicho kinacho amua aina ya majibu unayo yataka. Natamani unavyo ingia msimu mpya uombe kama mtu wa mbinguni kwa kila ombi kumkumbusha Mungu neno lake. Mfano. Unataka kufanikiwa mkumbushe mungu kuwa kwa neno lako umesema madamu muda wa kupanda udumupo wakati wa kuvuna hauta koma. Au kwa neno lako *umesema sinta kuwa mkia nitakuwa kichwa* Ndipo anza kuingiza haja yako . Au kwa neno lako *umesema nitabarikiwa mjini nitabarikiwa shambani* ndipo uendelee na haja zako. Ili umpendeze Mungu lazima uwe na neno lake . Ebrania 11:6 Mungu hawezi kwenda kinyume na neno lake hiyo ndiyo sababu ya kuomba kwa neno lake. Ebrania 6:16-17 Yeremia 1:12 Mungu alimwambia yeremia umenena vema kwa maana mimi Bwana naangalia neno langu hili nitimize. Natumaini maombi yetu leo yataongozwa na neno la Mungu. #build new eden
    0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·363 Visualizações
  • WAKO WAPI WASHITAKI WAKO ?

    Yohana 8:3-11
    Mafarisayo walimpeleka mwanamke waliye mfumania kwa Yesu ili atoe hukumu .

    *Walipo mpeleka si kwa sababu ya kuwa mwanamke amekosea peke yake walitaka kumjaribu Yesu kupitia yule mwanamke .*

    Lakini wao ambacho hawakujua ni kuwa Yesu yeye ndo anaye tazama mioyo kabla hawajafika.

    *Ukisoma torati ya Musa unaweza dhani walikuwa wameenda kwa nia njema lkn kumbe lengo ni kumtega.*

    *Na kwa sababu walienda kwa mtego Yesu naye akawapa jibu la mtego vile vile kuwa yeyote asiye na dhambi na awe wa kwanza kumpiga huyu mtu.*
    Yohana 8:7
    [7]Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.

    Yes kabla ujamshitaki mwingine lazima ujiangalie vipi kuhusu wewe hawa walikuwa washitaki wazuri lakini kumbe bado na wao ni wadhinifu tu.

    *Jiulize wewe ambaye unajiona malaika vipi wewe una dhambi yeyote kweli ni kweli umevuka zinaa lakini mbona wivu na husda bado unao*

    Baada ya hapo Yesu anampa njia impasayo *wokovu Nenda zako usitende dhambi tena*

    Kumbe njia nzuri si kumuhukumu mtu kwa kumpiga mawe badala yake mpe njia ya kushinda hiyo zinaa.

    Sababu ya kusema wengine kumeharibu mwili w Kristo hasa watu wanao jifanya wana kirohost wakati ni mafarisayo.

    Ukimkuta ndugu yako anadumbukia shimoni msaidie atoke si kwenda kumtangaza na kumbe huyo mtu kaokoka wiki moja mfuate mtie moyo na mpe njia uliyo tumia kushinda dhambi nayeye ajifunze na hapo ndipo tutita Upendo wa kristo.

    *Siyo unapeleka kwa mchungaji arafu nyuma ya pazia unamtega mchungaji akiamua kumfukuza upate la kumsema akimuonya upate la kumsema.*

    *Dada angu usikubali maneno ya watu na mashitaka ya watu yakukosanishe Mungu ni ukianguka mrudie Bwana ambaye atasimama na wewe na kukusamehe na kukupa onyo ,*

    Walokole wengi tumepoteza radha ya wokovu kwa majungu na kujihesabia sana haki kumbe ni sadukayo na farisayo.

    Kukulia machinjioni haimaanishi lazima ujue kuchinjz nyama kumbe hata wewe dada wengine unawaona wamesimama leo ni
    kwasababu waliamua kujifunza nq si kutumia uzoefu..

    Naweza kwambia kuwa Yesu anakuja ni muhimu kutengeneza.

    Ahsante.naitwa Sylvester Mwakabende wa BUILD NEW EDEN

    #RESTORE MEN POSITION
    WAKO WAPI WASHITAKI WAKO ? Yohana 8:3-11 Mafarisayo walimpeleka mwanamke waliye mfumania kwa Yesu ili atoe hukumu . *Walipo mpeleka si kwa sababu ya kuwa mwanamke amekosea peke yake walitaka kumjaribu Yesu kupitia yule mwanamke .* Lakini wao ambacho hawakujua ni kuwa Yesu yeye ndo anaye tazama mioyo kabla hawajafika. *Ukisoma torati ya Musa unaweza dhani walikuwa wameenda kwa nia njema lkn kumbe lengo ni kumtega.* *Na kwa sababu walienda kwa mtego Yesu naye akawapa jibu la mtego vile vile kuwa yeyote asiye na dhambi na awe wa kwanza kumpiga huyu mtu.* Yohana 8:7 [7]Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. Yes kabla ujamshitaki mwingine lazima ujiangalie vipi kuhusu wewe hawa walikuwa washitaki wazuri lakini kumbe bado na wao ni wadhinifu tu. *Jiulize wewe ambaye unajiona malaika vipi wewe una dhambi yeyote kweli ni kweli umevuka zinaa lakini mbona wivu na husda bado unao* Baada ya hapo Yesu anampa njia impasayo *wokovu Nenda zako usitende dhambi tena* Kumbe njia nzuri si kumuhukumu mtu kwa kumpiga mawe badala yake mpe njia ya kushinda hiyo zinaa. Sababu ya kusema wengine kumeharibu mwili w Kristo hasa watu wanao jifanya wana kirohost wakati ni mafarisayo. Ukimkuta ndugu yako anadumbukia shimoni msaidie atoke si kwenda kumtangaza na kumbe huyo mtu kaokoka wiki moja mfuate mtie moyo na mpe njia uliyo tumia kushinda dhambi nayeye ajifunze na hapo ndipo tutita Upendo wa kristo. *Siyo unapeleka kwa mchungaji arafu nyuma ya pazia unamtega mchungaji akiamua kumfukuza upate la kumsema akimuonya upate la kumsema.* *Dada angu usikubali maneno ya watu na mashitaka ya watu yakukosanishe Mungu ni ukianguka mrudie Bwana ambaye atasimama na wewe na kukusamehe na kukupa onyo ,* Walokole wengi tumepoteza radha ya wokovu kwa majungu na kujihesabia sana haki kumbe ni sadukayo na farisayo. Kukulia machinjioni haimaanishi lazima ujue kuchinjz nyama kumbe hata wewe dada wengine unawaona wamesimama leo ni kwasababu waliamua kujifunza nq si kutumia uzoefu.. Naweza kwambia kuwa Yesu anakuja ni muhimu kutengeneza. Ahsante.naitwa Sylvester Mwakabende wa BUILD NEW EDEN #RESTORE MEN POSITION
    0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·546 Visualizações
  • NINAWEKA KIPAUMBELE AMANI YANGU—NA INAHISI KAMA KUJA NYUMBANI

    Siombi tena msamaha kwa kujichagua.

    Kwa muda mrefu zaidi, niliwamwagia wengine huku nikikimbia nikiwa mtupu. Nilitabasamu nikiwa nimechoka. Nilisema "sijambo" wakati roho yangu ilikuwa inauma. Niliendelea kujitokeza—kwa kila mtu isipokuwa mimi mwenyewe. Lakini sivyo tena.

    Sasa, ninachagua kile kinachofanya moyo wangu kuwa mwepesi.
    Ninachagua aina ya amani ambayo haihitaji kuelezewa.
    Aina ya upendo ambayo hauhitaji mimi kuomba tahadhari.
    Aina ya nishati ambayo inaniacha nimejaa, sio kuvunjika.

    Ninatanguliza kile kinachojisikia vizuri kwa roho yangu -
    Asubuhi tulivu. Maneno ya upole. Watu salama.
    Aina ya mazungumzo ambayo hulisha roho yangu, sio kuitenganisha.

    Ninapenda furaha rahisi:
    Kikombe cha joto cha chai. Sauti ya mvua. Kitabu kinachonielewa.
    Hisia ya kuwa peke yangu lakini sio upweke.
    Utambuzi kwamba sio kila ukimya unahitaji kujazwa.

    Ninajifunza kuwa amani ya kweli haipigi kelele.
    Inanong'ona, "Uko salama sasa."
    Ni wakati unapoacha kujaribu kujithibitisha.
    Ni uhuru wa kuwepo, jinsi ulivyo—bila hukumu, bila utendaji, bila uzito.

    Sifukuzi tena mapenzi ambayo yananichanganya.
    Sio kung'ang'ania tena watu wanaokuja tu wakati wanahitaji.
    Sio kuvumilia tena hali zinazonichosha.

    Kwa sababu hatimaye nimekumbuka mimi ni nani.
    Na kwamba kukumbuka? Huo ndio mwanzo wa kila kitu.

    Kwa hivyo hapa ndio msimu huu wa laini.
    Enzi hii ya uponyaji.
    Toleo hili langu ambalo huchagua amani badala ya shinikizo, uwepo juu ya utendakazi, na upendo—upendo wa kweli—ambalo huhisi kama nyumbani.

    Na unajua nini?
    Kwa mara moja, siishi tu ...
    Ninaipenda.
    NINAWEKA KIPAUMBELE AMANI YANGU—NA INAHISI KAMA KUJA NYUMBANI Siombi tena msamaha kwa kujichagua. Kwa muda mrefu zaidi, niliwamwagia wengine huku nikikimbia nikiwa mtupu. Nilitabasamu nikiwa nimechoka. Nilisema "sijambo" wakati roho yangu ilikuwa inauma. Niliendelea kujitokeza—kwa kila mtu isipokuwa mimi mwenyewe. Lakini sivyo tena. Sasa, ninachagua kile kinachofanya moyo wangu kuwa mwepesi. Ninachagua aina ya amani ambayo haihitaji kuelezewa. Aina ya upendo ambayo hauhitaji mimi kuomba tahadhari. Aina ya nishati ambayo inaniacha nimejaa, sio kuvunjika. Ninatanguliza kile kinachojisikia vizuri kwa roho yangu - Asubuhi tulivu. Maneno ya upole. Watu salama. Aina ya mazungumzo ambayo hulisha roho yangu, sio kuitenganisha. Ninapenda furaha rahisi: Kikombe cha joto cha chai. Sauti ya mvua. Kitabu kinachonielewa. Hisia ya kuwa peke yangu lakini sio upweke. Utambuzi kwamba sio kila ukimya unahitaji kujazwa. Ninajifunza kuwa amani ya kweli haipigi kelele. Inanong'ona, "Uko salama sasa." Ni wakati unapoacha kujaribu kujithibitisha. Ni uhuru wa kuwepo, jinsi ulivyo—bila hukumu, bila utendaji, bila uzito. Sifukuzi tena mapenzi ambayo yananichanganya. Sio kung'ang'ania tena watu wanaokuja tu wakati wanahitaji. Sio kuvumilia tena hali zinazonichosha. Kwa sababu hatimaye nimekumbuka mimi ni nani. Na kwamba kukumbuka? Huo ndio mwanzo wa kila kitu. Kwa hivyo hapa ndio msimu huu wa laini. Enzi hii ya uponyaji. Toleo hili langu ambalo huchagua amani badala ya shinikizo, uwepo juu ya utendakazi, na upendo—upendo wa kweli—ambalo huhisi kama nyumbani. Na unajua nini? Kwa mara moja, siishi tu ... Ninaipenda.
    Love
    1
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·336 Visualizações
  • HAKUNA TOFAUTI KATI YA MAMA YANGU NA MOYO WANGU-VYOTE WAMWEKA HAI.

    Yeye sio tu mwanamke aliyenipa maisha-
    Yeye ni maisha yangu.

    Kama mapigo ya moyo wangu, upendo wake ni wa kudumu.
    Kama pumzi yangu, sala zake hazijulikani - lakini zinanibeba kupitia dhoruba.
    Nguvu zake zimekuwa mdundo ambao uliniweka thabiti wakati ulimwengu ulitetemeka chini yangu.

    Alinishikilia nilipokuwa mchanga sana kuelewa ulimwengu ...
    Na bado ananishikilia sasa, ikiwa tu kwa maneno yake, hekima yake, ukimya wake unaosema "Najua."

    Aliacha usingizi kwa ajili ya ndoto zangu, machozi kwa tabasamu langu, faraja kwa faraja yangu.
    Hakuwahi kuuliza chochote kama malipo, lakini alinipa kila kitu.

    Upendo wake? Aina ambayo haina kelele.
    Ni kimya. Imara. Mtakatifu.

    Kwa hivyo ninaposema hakuna tofauti kati ya mama yangu na moyo wangu,
    Namaanisha kila neno.
    Kwa sababu bila yoyote—ningeacha tu kuwa.

    #WeweNdiweMaishaYangu#
    #MamaYanguMoyoWangu#
    #Upendo Usio na Masharti
    #MileleAsante#
    #MamaNiNyumbaYangu#
    #MaishaKwasababuYake#
    HAKUNA TOFAUTI KATI YA MAMA YANGU NA MOYO WANGU-VYOTE WAMWEKA HAI. Yeye sio tu mwanamke aliyenipa maisha- Yeye ni maisha yangu. Kama mapigo ya moyo wangu, upendo wake ni wa kudumu. Kama pumzi yangu, sala zake hazijulikani - lakini zinanibeba kupitia dhoruba. Nguvu zake zimekuwa mdundo ambao uliniweka thabiti wakati ulimwengu ulitetemeka chini yangu. Alinishikilia nilipokuwa mchanga sana kuelewa ulimwengu ... Na bado ananishikilia sasa, ikiwa tu kwa maneno yake, hekima yake, ukimya wake unaosema "Najua." Aliacha usingizi kwa ajili ya ndoto zangu, machozi kwa tabasamu langu, faraja kwa faraja yangu. Hakuwahi kuuliza chochote kama malipo, lakini alinipa kila kitu. Upendo wake? Aina ambayo haina kelele. Ni kimya. Imara. Mtakatifu. Kwa hivyo ninaposema hakuna tofauti kati ya mama yangu na moyo wangu, Namaanisha kila neno. Kwa sababu bila yoyote—ningeacha tu kuwa. #WeweNdiweMaishaYangu# #MamaYanguMoyoWangu# #Upendo Usio na Masharti #MileleAsante# #MamaNiNyumbaYangu# #MaishaKwasababuYake#
    Love
    1
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·500 Visualizações
  • 𝘼 𝙎𝙩𝙤𝙧𝙮 𝙤𝙛 𝙇𝙤𝙫𝙚

    Siku ya harusi yangu, nilimbeba mke wangu mikononi mwangu. Tulipofika kwenye gorofa yetu ndogo, marafiki zangu waliniomba nimbebe ndani. Alikuwa mzito na mwenye haya wakati huo, na mimi nilikuwa bwana harusi mwenye furaha na mwenye nguvu.

    Hiyo ilikuwa miaka kumi iliyopita. Maisha yetu baada ya ndoa yalikuwa rahisi, kama glasi ya maji safi. Tulikuwa na mtoto, na nilifanya kazi kwa bidii ili kukuza biashara yangu. Kadiri nilivyozidi kupata pesa, mapenzi yetu yalififia taratibu. Mke wangu alikuwa mfanyakazi wa serikali, na tulikuwa tukiondoka nyumbani na kurudi wakati uleule kila siku. Mtoto wetu alisoma katika shule ya bweni. Kwa nje, maisha yetu yalionekana kuwa yenye furaha, lakini ndani kabisa, mabadiliko yalikuwa yakitokea.

    Kisha, nilikutana na Dew.

    Ilikuwa ni siku nzuri wakati Dew alinikumbatia kwa nyuma. Nilihisi kupendwa tena. Hata nilikuwa nimemnunulia nyumba. Dew aliwahi kuniambia, "Wewe ni aina ya wanaume wanaowaona wasichana." Maneno yake yalinikumbusha mke wangu. Muda mrefu uliopita, alikuwa amesema kitu kimoja: "Unapofanikiwa, wanawake wengi watavutiwa nawe." Nilihisi hatia, nikijua nilikuwa nikimsaliti, lakini sikuweza kujizuia.

    Nilimuuliza Dew kwenda kuchukua samani wakati nikienda ofisini. Hakufurahi kwa sababu niliahidi kwenda naye. Siku hiyo, wazo la talaka likawa wazi zaidi akilini mwangu. Lakini ilikuwa ngumu kumwambia mke wangu. Alikuwa mke mzuri, akiandaa chakula cha jioni kila wakati na kushiriki jioni tulivu pamoja nami. Hata hivyo, moyo wangu haukuwa naye tena.

    Siku moja, kwa utani, nilimuuliza mke wangu, "Ungefanya nini ikiwa tutaachana?" Hakujibu, kana kwamba ni jambo lisilowezekana kufikiria. Lakini ndani kabisa, nilikuwa nikijiandaa.

    Mke wangu aliponitembelea ofisini kwangu, Dew alikuwa ametoka tu. Watu walimtazama mke wangu kwa huruma. Huenda alikisia kitu lakini akatabasamu kwa upole, ingawa niliona uchungu machoni mwake.

    Umande uliendelea kunisisitiza tuachane. Hatimaye, nilikubali.

    Jioni hiyo, mke wangu alipokuwa akiandaa sahani ya mwisho wakati wa chakula cha jioni, nilimshika mkono na kusema, "Nina jambo la kukuambia." Alikaa kimya, tayari alihisi kuna kitu kibaya. Nikasema, "Nataka talaka." Hakuwa na hasira mwanzoni na akauliza, "Kwa nini?" Nilikwepa kumjibu jambo ambalo lilimkera sana. Alitupa vijiti vyake chini na kupiga kelele, "Wewe si mwanaume!" Alilia usiku huo. Nilijua alikuwa anashangaa mapenzi yetu yameenda wapi, lakini sikuweza kumpa jibu.

    Kwa hatia, niliandika makubaliano ya talaka kumpa nyumba yetu, gari, na sehemu ya kampuni yangu. Aliichana. Kumwona akilia kwa kweli kulinifanya nijisikie raha, kana kwamba ningeweza kusonga mbele.

    Usiku mmoja, nilikuja nyumbani na kumwona akiandika kitu. Asubuhi iliyofuata, alinipa masharti yake ya talaka. Hakutaka chochote kutoka kwangu, lakini alikuwa na ombi moja: kumpa mwezi mmoja kabla ya talaka, na wakati huo, kuishi maisha kwa kawaida iwezekanavyo. Alisema, "Mwana wetu atamaliza mapumziko yake ya kiangazi katika mwezi mmoja. Sitaki aone ndoa yetu ikisambaratika."

    Pia aliomba jambo moja zaidi: "Siku ya harusi yetu, ulinibeba hadi nyumbani kwetu. Tunapoachana, nichukue nje ya chumba cha kulala hadi mlangoni kila asubuhi." Nilikubali, nikidhani ni njia yake ya kuaga kwa utamu fulani.

    Nilipomwambia Dew, alicheka na kudhani ni ujinga. Mwitikio wake ulinisumbua, lakini sikusema chochote.

    Siku ya kwanza, kubeba mke wangu nilijisikia vibaya. Mwana wetu alipiga makofi kwa furaha, akifikiri ilikuwa ya kufurahisha. Kila siku, ikawa rahisi. Niliona mambo ambayo sikuwa nimeona kwa muda mrefu: jinsi alivyoegemea kifua changu, vikumbusho vyake vya upole kuhusu maisha, na kupungua kwa uzito kulikonitia wasiwasi. Alikuwa amekonda sana.

    Kufikia siku za mwisho, niligundua bado ninampenda. Kumbeba mikononi mwangu kila asubuhi kulinikumbusha siku zetu za mapema tukiwa pamoja. Ulaini wake, harufu yake, utunzaji wake wa utulivu kwangu ... niliona yote wazi sasa.

    Siku ya mwisho, nilipomnyanyua, alisema kwa upole, "Laiti ungenibeba hivi hadi tuzeeke." Machozi yalinijaa. Niliendesha gari moja kwa moja hadi kwa Dew na kumwambia, "Sitaachana na mke wangu." Alishtuka na kukasirika, lakini nilijua uamuzi wangu ulikuwa sahihi.

    Nilipokuwa njiani kurudi, nilimnunulia mke wangu maua yake ya kupenda na kuandika kwenye kadi: "Nitakuchukua kila asubuhi hadi tutakapozeeka."
    𝘼 𝙎𝙩𝙤𝙧𝙮 𝙤𝙛 𝙇𝙤𝙫𝙚 Siku ya harusi yangu, nilimbeba mke wangu mikononi mwangu. Tulipofika kwenye gorofa yetu ndogo, marafiki zangu waliniomba nimbebe ndani. Alikuwa mzito na mwenye haya wakati huo, na mimi nilikuwa bwana harusi mwenye furaha na mwenye nguvu. Hiyo ilikuwa miaka kumi iliyopita. Maisha yetu baada ya ndoa yalikuwa rahisi, kama glasi ya maji safi. Tulikuwa na mtoto, na nilifanya kazi kwa bidii ili kukuza biashara yangu. Kadiri nilivyozidi kupata pesa, mapenzi yetu yalififia taratibu. Mke wangu alikuwa mfanyakazi wa serikali, na tulikuwa tukiondoka nyumbani na kurudi wakati uleule kila siku. Mtoto wetu alisoma katika shule ya bweni. Kwa nje, maisha yetu yalionekana kuwa yenye furaha, lakini ndani kabisa, mabadiliko yalikuwa yakitokea. Kisha, nilikutana na Dew. Ilikuwa ni siku nzuri wakati Dew alinikumbatia kwa nyuma. Nilihisi kupendwa tena. Hata nilikuwa nimemnunulia nyumba. Dew aliwahi kuniambia, "Wewe ni aina ya wanaume wanaowaona wasichana." Maneno yake yalinikumbusha mke wangu. Muda mrefu uliopita, alikuwa amesema kitu kimoja: "Unapofanikiwa, wanawake wengi watavutiwa nawe." Nilihisi hatia, nikijua nilikuwa nikimsaliti, lakini sikuweza kujizuia. Nilimuuliza Dew kwenda kuchukua samani wakati nikienda ofisini. Hakufurahi kwa sababu niliahidi kwenda naye. Siku hiyo, wazo la talaka likawa wazi zaidi akilini mwangu. Lakini ilikuwa ngumu kumwambia mke wangu. Alikuwa mke mzuri, akiandaa chakula cha jioni kila wakati na kushiriki jioni tulivu pamoja nami. Hata hivyo, moyo wangu haukuwa naye tena. Siku moja, kwa utani, nilimuuliza mke wangu, "Ungefanya nini ikiwa tutaachana?" Hakujibu, kana kwamba ni jambo lisilowezekana kufikiria. Lakini ndani kabisa, nilikuwa nikijiandaa. Mke wangu aliponitembelea ofisini kwangu, Dew alikuwa ametoka tu. Watu walimtazama mke wangu kwa huruma. Huenda alikisia kitu lakini akatabasamu kwa upole, ingawa niliona uchungu machoni mwake. Umande uliendelea kunisisitiza tuachane. Hatimaye, nilikubali. Jioni hiyo, mke wangu alipokuwa akiandaa sahani ya mwisho wakati wa chakula cha jioni, nilimshika mkono na kusema, "Nina jambo la kukuambia." Alikaa kimya, tayari alihisi kuna kitu kibaya. Nikasema, "Nataka talaka." Hakuwa na hasira mwanzoni na akauliza, "Kwa nini?" Nilikwepa kumjibu jambo ambalo lilimkera sana. Alitupa vijiti vyake chini na kupiga kelele, "Wewe si mwanaume!" Alilia usiku huo. Nilijua alikuwa anashangaa mapenzi yetu yameenda wapi, lakini sikuweza kumpa jibu. Kwa hatia, niliandika makubaliano ya talaka kumpa nyumba yetu, gari, na sehemu ya kampuni yangu. Aliichana. Kumwona akilia kwa kweli kulinifanya nijisikie raha, kana kwamba ningeweza kusonga mbele. Usiku mmoja, nilikuja nyumbani na kumwona akiandika kitu. Asubuhi iliyofuata, alinipa masharti yake ya talaka. Hakutaka chochote kutoka kwangu, lakini alikuwa na ombi moja: kumpa mwezi mmoja kabla ya talaka, na wakati huo, kuishi maisha kwa kawaida iwezekanavyo. Alisema, "Mwana wetu atamaliza mapumziko yake ya kiangazi katika mwezi mmoja. Sitaki aone ndoa yetu ikisambaratika." Pia aliomba jambo moja zaidi: "Siku ya harusi yetu, ulinibeba hadi nyumbani kwetu. Tunapoachana, nichukue nje ya chumba cha kulala hadi mlangoni kila asubuhi." Nilikubali, nikidhani ni njia yake ya kuaga kwa utamu fulani. Nilipomwambia Dew, alicheka na kudhani ni ujinga. Mwitikio wake ulinisumbua, lakini sikusema chochote. Siku ya kwanza, kubeba mke wangu nilijisikia vibaya. Mwana wetu alipiga makofi kwa furaha, akifikiri ilikuwa ya kufurahisha. Kila siku, ikawa rahisi. Niliona mambo ambayo sikuwa nimeona kwa muda mrefu: jinsi alivyoegemea kifua changu, vikumbusho vyake vya upole kuhusu maisha, na kupungua kwa uzito kulikonitia wasiwasi. Alikuwa amekonda sana. Kufikia siku za mwisho, niligundua bado ninampenda. Kumbeba mikononi mwangu kila asubuhi kulinikumbusha siku zetu za mapema tukiwa pamoja. Ulaini wake, harufu yake, utunzaji wake wa utulivu kwangu ... niliona yote wazi sasa. Siku ya mwisho, nilipomnyanyua, alisema kwa upole, "Laiti ungenibeba hivi hadi tuzeeke." Machozi yalinijaa. Niliendesha gari moja kwa moja hadi kwa Dew na kumwambia, "Sitaachana na mke wangu." Alishtuka na kukasirika, lakini nilijua uamuzi wangu ulikuwa sahihi. Nilipokuwa njiani kurudi, nilimnunulia mke wangu maua yake ya kupenda na kuandika kwenye kadi: "Nitakuchukua kila asubuhi hadi tutakapozeeka."
    Like
    Love
    2
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·555 Visualizações
  • "Nafahamu wote kwa pamoja tuna hamu ya kupata matokeo katika mechi hii lakini matokeo haya kuyapata kwa kushinda na kufuzu. Sisi tumeweka mazingira mazuri ambayo yataiwezesha timu yetu kufuzu.”

    “Nipo hapa kuwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa alkini ningependa kutoa taarifa muhimu kwamba tunaendelea kushirikiana na serikali kuimarisha usalama wa siku hiyo. Tunawataka wapenzi wetu kuhakikisha kwamba wanazingatia mazingatio yote ambayo yatawekwa ya usalama. Hatutaruhusu mtu yeyote ambaye sio Mwanasimba kutuharibia shughuli yetu.”

    “Katika mchezo uliopita walisema maneno mengi kwamba kuna wazee wafupi, mbuzi lakini tuwatumie ujumbe kwamba kama mechi aikuhusu wabaki nyumbani na sisi tumejiandaa kuthibiti hilo kama klabu.”- Zubeda Sakuru, CEO wa klabu ya Simba SC.

    "Nafahamu wote kwa pamoja tuna hamu ya kupata matokeo katika mechi hii lakini matokeo haya kuyapata kwa kushinda na kufuzu. Sisi tumeweka mazingira mazuri ambayo yataiwezesha timu yetu kufuzu.” “Nipo hapa kuwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa alkini ningependa kutoa taarifa muhimu kwamba tunaendelea kushirikiana na serikali kuimarisha usalama wa siku hiyo. Tunawataka wapenzi wetu kuhakikisha kwamba wanazingatia mazingatio yote ambayo yatawekwa ya usalama. Hatutaruhusu mtu yeyote ambaye sio Mwanasimba kutuharibia shughuli yetu.” “Katika mchezo uliopita walisema maneno mengi kwamba kuna wazee wafupi, mbuzi lakini tuwatumie ujumbe kwamba kama mechi aikuhusu wabaki nyumbani na sisi tumejiandaa kuthibiti hilo kama klabu.”- Zubeda Sakuru, CEO wa klabu ya Simba SC.
    Like
    1
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·690 Visualizações
  • Wakati mwingine, ninashangaa ikiwa unatambua jinsi ninavyokupenda, ikiwa unaelewa ni kiasi gani ninajali. Huenda usielewe kikamilifu maana ya kupendwa nami, na huenda nisipate kamwe maneno ya kueleza kujitolea kwangu.

    Tangu nilipokutana na wewe, maisha yangu yalibadilika kwa njia ambazo sikuwahi kufikiria. Uwepo wako unazijaza siku zangu na mwanga na usiku wangu kwa amani. Daima jua kwamba kila wakati unapotabasamu, unalia, kila chembe ya furaha unayohisi, na kila hisia unayopata, ninaihisi pia kwa sababu wewe ni moyo wangu, na kukutazama ni kuona roho yangu.

    Kuna wakati maneno hunishinda, ninachoweza kufanya ni kutazama macho yako na kutumaini unaweza kuona undani wa upendo wangu. Nataka ujue kwamba furaha yako ni furaha yangu, na maumivu yako ni maumivu yangu. Mioyo yetu inapiga kama kitu kimoja, iliyounganishwa katika dansi ya zamani kama wakati.

    Katika ulimwengu huu mkubwa, wewe ni nanga yangu, mara kwa mara, na nyumbani. Kila wakati tunaposhiriki ni hazina ninayothamini sana. Upendo wangu kwako hauna kikomo, hauna wakati, na hauteteleki. Ni upendo unaopita maneno, upendo ambao unaweza kuhisiwa tu katika nyakati tulivu tunazoshiriki.

    Jua kwamba mimi ni wako sasa na hata milele na kwamba upendo wangu kwako hautapungua kamwe. Wewe ni kila kitu changu, moyo wangu, roho yangu, mpenzi wangu.
    Wakati mwingine, ninashangaa ikiwa unatambua jinsi ninavyokupenda, ikiwa unaelewa ni kiasi gani ninajali. Huenda usielewe kikamilifu maana ya kupendwa nami, na huenda nisipate kamwe maneno ya kueleza kujitolea kwangu. Tangu nilipokutana na wewe, maisha yangu yalibadilika kwa njia ambazo sikuwahi kufikiria. Uwepo wako unazijaza siku zangu na mwanga na usiku wangu kwa amani. Daima jua kwamba kila wakati unapotabasamu, unalia, kila chembe ya furaha unayohisi, na kila hisia unayopata, ninaihisi pia kwa sababu wewe ni moyo wangu, na kukutazama ni kuona roho yangu. Kuna wakati maneno hunishinda, ninachoweza kufanya ni kutazama macho yako na kutumaini unaweza kuona undani wa upendo wangu. Nataka ujue kwamba furaha yako ni furaha yangu, na maumivu yako ni maumivu yangu. Mioyo yetu inapiga kama kitu kimoja, iliyounganishwa katika dansi ya zamani kama wakati. Katika ulimwengu huu mkubwa, wewe ni nanga yangu, mara kwa mara, na nyumbani. Kila wakati tunaposhiriki ni hazina ninayothamini sana. Upendo wangu kwako hauna kikomo, hauna wakati, na hauteteleki. Ni upendo unaopita maneno, upendo ambao unaweza kuhisiwa tu katika nyakati tulivu tunazoshiriki. Jua kwamba mimi ni wako sasa na hata milele na kwamba upendo wangu kwako hautapungua kamwe. Wewe ni kila kitu changu, moyo wangu, roho yangu, mpenzi wangu. ♥️💘
    Love
    1
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·668 Visualizações
  • "Ni kweli tunamshikilia Ali Kamwe ambaye ni Msemaji wa Klabu ya Yanga na tunamfanyia mahojiano kwa tuhuma za kutoa maneno machafu kwa Viongozi wa Serikali na tutatoa taarifa rasmi baada ya mahojiano kukamilika" - RPC Richard Abwao, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani wa Tabora.

    "Ni kweli tunamshikilia Ali Kamwe ambaye ni Msemaji wa Klabu ya Yanga na tunamfanyia mahojiano kwa tuhuma za kutoa maneno machafu kwa Viongozi wa Serikali na tutatoa taarifa rasmi baada ya mahojiano kukamilika" - RPC Richard Abwao, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani wa Tabora.
    Like
    3
    · 1 Comentários ·0 Compartilhamentos ·426 Visualizações
  • “Kila siku Robo tu , Kocha naye amechangia Dakika ya kwanza tu toa Ateba weka Mukwala , Halftime toa Ngoma weka Mavambo mwarabu alikuwa anakufa” Mwisho wa kunukuu

    Kuna kibanda umiza nipo hapa nimenukuu maneno ya shabiki Ingawa sijafanikiwa kujua ni shabiki wa timu gani" - Shaffih Dauda, Mchambuzi

    “Kila siku Robo tu , Kocha naye amechangia Dakika ya kwanza tu toa Ateba weka Mukwala , Halftime toa Ngoma weka Mavambo mwarabu alikuwa anakufa” Mwisho wa kunukuu Kuna kibanda umiza nipo hapa nimenukuu maneno ya shabiki Ingawa sijafanikiwa kujua ni shabiki wa timu gani" - Shaffih Dauda, Mchambuzi ✍️
    Like
    1
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·404 Visualizações
  • Najua umesalitiwa na wale uliowaamini, umeachwa ulipohitaji kupendwa, na umedhihakiwa wakati ulichotaka ni kuungwa mkono. Najua umechoka. Najua umepigana vita hakuna mtu aliyeona, kulia kimya, na kuvumilia maumivu ambayo maneno hayawezi kuelezea.

    Maisha hayajakuwa sawa kwako. Milango imegongwa usoni mwako. Umewatazama wengine wakiinuka huku wewe ukiwa umekwama katika sehemu moja. Umeomba, kutumaini, na kungoja, lakini hakuna kinachoonekana kubadilika. Inaumiza. Ni chungu. Inachosha.

    Lakini nisikilizeni, na nisikilize kwa makini: USIKATE TAMAA.

    Kila mtu mkubwa unayekuvutia leo alikuwa hapo ulipo sasa. Walihisi kile unachohisi. Walihangaika, walilia, na walitilia shaka wenyewe. Lakini hawakuacha. Hawakuruhusu maumivu yao yawafafanue. Waliendelea kusonga mbele, hata pale nguvu zao zilipopungua. Na ndio maana leo, ulimwengu unawaadhimisha.

    Lazima uelewe ukweli huu: Kadiri hatima yako inavyokuwa kubwa, ndivyo vita yako inavyokuwa kubwa. KILA KIWANGO KIPYA UNACHOFIKIA, KUNA SHETANI MPYA ANAKUSUBIRI. Ulipokuwa maskini, hakuna aliyekuonea wivu. Lakini unapoanza kufanya maendeleo, ghafla, watu wanaanza kukuchukia. Ulipokuwa huna kazi, hakuna aliyezungumza juu yako. Lakini mara tu unapopata kazi nzuri, wanaanza kueneza uvumi. Ulipokuwa ukihangaika, hakuna aliyejali. Lakini wakati unapoanza kufanikiwa, maadui huonekana kutoka popote.

    Ibilisi hapigani na watu ambao hawaendi popote. Sababu ya wewe kukabiliwa na vita vingi ni kwa sababu hatima yako ni kubwa; sababu ya maisha kukujaribu sana ni kwa sababu kesho yako ni kubwa. Huna mateso kwa sababu wewe ni dhaifu. Unateseka kwa sababu wewe ni IMARA, na maisha yanajua kwamba mara tu unapopitia, hautazuilika.

    Kwa hivyo, usikatishwe tamaa na vita unavyokabili sasa. Wao ni ishara kwamba unasonga mbele. Usiruhusu maumivu yakufanye uchungu. Usiruhusu tamaa kuua ndoto zako. Endelea kupigana. Endelea kusukuma. Endelea kuamini. Wakati wako utafika.

    Kuna toleo lako katika siku zijazo ambalo lina nguvu zaidi, busara, na mafanikio zaidi kuliko wewe sasa. Toleo hilo lako linasubiri. Lakini ili kuwa mtu huyo, lazima upitie moto huu. Sio rahisi, lakini nakuahidi, itafaa.

    Lia ikiwa ni lazima, lakini baada ya kulia, futa machozi yako na uendelee kusonga. Lalamika ikibidi, lakini baada ya kulalamika, simama na upigane tena. Jisikie dhaifu ikiwa ni lazima, lakini usiache kujaribu.

    Wakati wako unakuja. Ufanisi wako umekaribia. Maumivu hayatadumu milele. Siku moja, utaangalia nyuma na kugundua kuwa kila kitu ulichopitia kilikufanya kuwa mtu mwenye nguvu, aliyefanikiwa ambaye unakusudiwa kuwa.

    Kwa hivyo, endelea kusonga mbele. Ushindi wako uko njiani.

    Quadic Bangura
    Najua umesalitiwa na wale uliowaamini, umeachwa ulipohitaji kupendwa, na umedhihakiwa wakati ulichotaka ni kuungwa mkono. Najua umechoka. Najua umepigana vita hakuna mtu aliyeona, kulia kimya, na kuvumilia maumivu ambayo maneno hayawezi kuelezea. Maisha hayajakuwa sawa kwako. Milango imegongwa usoni mwako. Umewatazama wengine wakiinuka huku wewe ukiwa umekwama katika sehemu moja. Umeomba, kutumaini, na kungoja, lakini hakuna kinachoonekana kubadilika. Inaumiza. Ni chungu. Inachosha. Lakini nisikilizeni, na nisikilize kwa makini: USIKATE TAMAA. Kila mtu mkubwa unayekuvutia leo alikuwa hapo ulipo sasa. Walihisi kile unachohisi. Walihangaika, walilia, na walitilia shaka wenyewe. Lakini hawakuacha. Hawakuruhusu maumivu yao yawafafanue. Waliendelea kusonga mbele, hata pale nguvu zao zilipopungua. Na ndio maana leo, ulimwengu unawaadhimisha. Lazima uelewe ukweli huu: Kadiri hatima yako inavyokuwa kubwa, ndivyo vita yako inavyokuwa kubwa. KILA KIWANGO KIPYA UNACHOFIKIA, KUNA SHETANI MPYA ANAKUSUBIRI. Ulipokuwa maskini, hakuna aliyekuonea wivu. Lakini unapoanza kufanya maendeleo, ghafla, watu wanaanza kukuchukia. Ulipokuwa huna kazi, hakuna aliyezungumza juu yako. Lakini mara tu unapopata kazi nzuri, wanaanza kueneza uvumi. Ulipokuwa ukihangaika, hakuna aliyejali. Lakini wakati unapoanza kufanikiwa, maadui huonekana kutoka popote. Ibilisi hapigani na watu ambao hawaendi popote. Sababu ya wewe kukabiliwa na vita vingi ni kwa sababu hatima yako ni kubwa; sababu ya maisha kukujaribu sana ni kwa sababu kesho yako ni kubwa. Huna mateso kwa sababu wewe ni dhaifu. Unateseka kwa sababu wewe ni IMARA, na maisha yanajua kwamba mara tu unapopitia, hautazuilika. Kwa hivyo, usikatishwe tamaa na vita unavyokabili sasa. Wao ni ishara kwamba unasonga mbele. Usiruhusu maumivu yakufanye uchungu. Usiruhusu tamaa kuua ndoto zako. Endelea kupigana. Endelea kusukuma. Endelea kuamini. Wakati wako utafika. Kuna toleo lako katika siku zijazo ambalo lina nguvu zaidi, busara, na mafanikio zaidi kuliko wewe sasa. Toleo hilo lako linasubiri. Lakini ili kuwa mtu huyo, lazima upitie moto huu. Sio rahisi, lakini nakuahidi, itafaa. Lia ikiwa ni lazima, lakini baada ya kulia, futa machozi yako na uendelee kusonga. Lalamika ikibidi, lakini baada ya kulalamika, simama na upigane tena. Jisikie dhaifu ikiwa ni lazima, lakini usiache kujaribu. Wakati wako unakuja. Ufanisi wako umekaribia. Maumivu hayatadumu milele. Siku moja, utaangalia nyuma na kugundua kuwa kila kitu ulichopitia kilikufanya kuwa mtu mwenye nguvu, aliyefanikiwa ambaye unakusudiwa kuwa. Kwa hivyo, endelea kusonga mbele. Ushindi wako uko njiani. Quadic Bangura
    Love
    1
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·873 Visualizações
  • JE, UNAMLETEA UHAI MPENZI WAKO, AU UNALETA KISU?

    Upendo unakusudiwa kujenga, sio kuvunja. Uhusiano unakusudiwa kuwa patakatifu, sio kichinjio. Nafsi mbili zinapokutana, zinapaswa kuleta uhai kwa kila mmoja, sio majeraha, sio makovu, sio huzuni. Hata hivyo, ukweli wa kusikitisha ni kwamba watu wengi huingia kwenye mahusiano wakitarajia kupendwa lakini hupokea maumivu. Wanatazamia furaha lakini wanakutana na taabu. Badala ya mwenzi anayeleta uzima, wanajikuta wanaishi na mtu ambaye ana kisu, akipunguza ujasiri wao, amani na heshima. Kwa hiyo, unaleta uhai kwa mpenzi wako, au unaleta kisu? Upendo unakusudiwa kumpa uhai yule unayedai kumpenda. Katika Mwanzo Mungu alimpulizia Adamu pumzi ya uhai, naye akawa nafsi hai. Kwa njia hiyo hiyo, uhusiano unapaswa kupumua maisha ndani ya mtu, sio kukimbia maisha kutoka kwao. Unapomhimiza mwenzako kufuata ndoto zake, unaleta uzima. Unapozungumza maneno ya fadhili, heshima, na uthibitisho, unaleta uzima. Unapovumilia mapungufu yao na kutembea nao katika mapambano yao, unaleta uhai. Wakati uwepo wako ni chanzo cha amani na si chanzo cha msongo wa mawazo, unaleta uhai. Upendo haupaswi kamwe kuhisi kama kutembea kwenye uwanja wa vita, ambapo kila neno, kila kitendo na kila siku huhisi kama kupigania kuishi. Mpenzi wako hapaswi kujisikia salama nje kuliko ndani ya uhusiano. Ikiwa unampenda mtu, anapaswa kustawi chini ya upendo wako, sio kukauka.

    Kisu sio lazima kiwe cha mwili kila wakati. Vidonda vingine huenda zaidi kuliko mwili; wanachoma roho. Baadhi yetu, badala ya kuleta uhai, kuleta kisu. Tunaleta kisu cha maneno makali, kukata ndani ya kujithamini kwa mpenzi wetu. Tunaleta kisu cha kulinganisha, na kuwafanya wahisi kama hawatoshi vya kutosha. Tunakuja na kisu cha kupuuza, na njaa ya upendo na tahadhari wanayotamani. Kwa namna fulani, pia kuja na kisu cha usaliti, ambapo uaminifu wetu ni kwa maneno tu lakini si kwa vitendo. Watu wengine wanakufa kihisia na kiroho kwa sababu ya mtu wanayempenda. Furaha yao inafifia taratibu. Kujiamini kwao kunatoweka. Kicheko chao hakitoki tena moyoni. Kwa nini? Kwa sababu aliyekusudiwa kuwalisha sasa ndiye anayewaangamiza. Je, wewe ni mtoaji wa uzima au mleta maumivu? Je, watu hupata amani mbele yako au wasiwasi wako? Je, unainua au kubomoa? Ikiwa mtu unayempenda anafurahi zaidi wakati haupo kuliko wakati haupo, ni ishara kwamba unaweza kuwa unaleta kisu, sio maisha. Upendo unapaswa kuwa kama bustani ambayo watu wawili hukua pamoja. Lakini upendo unawezaje kukua ikiwa mwenzi mmoja anamwaga maji wakati mwingine anamwaga sumu? Ikiwa mmoja anapanda mbegu wakati mwingine anang'oa? Chagua kusema maneno ya uhai badala ya maneno yanayoua kujiamini. Chagua kukumbatia dosari badala ya kuzitumia kama silaha. Chagua kuunga mkono ndoto badala ya kuzikejeli. Chagua kuwa mahali salama, sio eneo la vita.

    Upendo unapaswa kuwa zawadi, sio mzigo. Baraka, si laana. Nguvu ya uponyaji, sio chanzo cha majeraha. Je, katika maisha ya mwenzako wewe ni mganga au mharibifu? Unaleta uhai au kisu?

    Credit
    Albert Nwosu
    JE, UNAMLETEA UHAI MPENZI WAKO, AU UNALETA KISU? Upendo unakusudiwa kujenga, sio kuvunja. Uhusiano unakusudiwa kuwa patakatifu, sio kichinjio. Nafsi mbili zinapokutana, zinapaswa kuleta uhai kwa kila mmoja, sio majeraha, sio makovu, sio huzuni. Hata hivyo, ukweli wa kusikitisha ni kwamba watu wengi huingia kwenye mahusiano wakitarajia kupendwa lakini hupokea maumivu. Wanatazamia furaha lakini wanakutana na taabu. Badala ya mwenzi anayeleta uzima, wanajikuta wanaishi na mtu ambaye ana kisu, akipunguza ujasiri wao, amani na heshima. Kwa hiyo, unaleta uhai kwa mpenzi wako, au unaleta kisu? Upendo unakusudiwa kumpa uhai yule unayedai kumpenda. Katika Mwanzo Mungu alimpulizia Adamu pumzi ya uhai, naye akawa nafsi hai. Kwa njia hiyo hiyo, uhusiano unapaswa kupumua maisha ndani ya mtu, sio kukimbia maisha kutoka kwao. Unapomhimiza mwenzako kufuata ndoto zake, unaleta uzima. Unapozungumza maneno ya fadhili, heshima, na uthibitisho, unaleta uzima. Unapovumilia mapungufu yao na kutembea nao katika mapambano yao, unaleta uhai. Wakati uwepo wako ni chanzo cha amani na si chanzo cha msongo wa mawazo, unaleta uhai. Upendo haupaswi kamwe kuhisi kama kutembea kwenye uwanja wa vita, ambapo kila neno, kila kitendo na kila siku huhisi kama kupigania kuishi. Mpenzi wako hapaswi kujisikia salama nje kuliko ndani ya uhusiano. Ikiwa unampenda mtu, anapaswa kustawi chini ya upendo wako, sio kukauka. Kisu sio lazima kiwe cha mwili kila wakati. Vidonda vingine huenda zaidi kuliko mwili; wanachoma roho. Baadhi yetu, badala ya kuleta uhai, kuleta kisu. Tunaleta kisu cha maneno makali, kukata ndani ya kujithamini kwa mpenzi wetu. Tunaleta kisu cha kulinganisha, na kuwafanya wahisi kama hawatoshi vya kutosha. Tunakuja na kisu cha kupuuza, na njaa ya upendo na tahadhari wanayotamani. Kwa namna fulani, pia kuja na kisu cha usaliti, ambapo uaminifu wetu ni kwa maneno tu lakini si kwa vitendo. Watu wengine wanakufa kihisia na kiroho kwa sababu ya mtu wanayempenda. Furaha yao inafifia taratibu. Kujiamini kwao kunatoweka. Kicheko chao hakitoki tena moyoni. Kwa nini? Kwa sababu aliyekusudiwa kuwalisha sasa ndiye anayewaangamiza. Je, wewe ni mtoaji wa uzima au mleta maumivu? Je, watu hupata amani mbele yako au wasiwasi wako? Je, unainua au kubomoa? Ikiwa mtu unayempenda anafurahi zaidi wakati haupo kuliko wakati haupo, ni ishara kwamba unaweza kuwa unaleta kisu, sio maisha. Upendo unapaswa kuwa kama bustani ambayo watu wawili hukua pamoja. Lakini upendo unawezaje kukua ikiwa mwenzi mmoja anamwaga maji wakati mwingine anamwaga sumu? Ikiwa mmoja anapanda mbegu wakati mwingine anang'oa? Chagua kusema maneno ya uhai badala ya maneno yanayoua kujiamini. Chagua kukumbatia dosari badala ya kuzitumia kama silaha. Chagua kuunga mkono ndoto badala ya kuzikejeli. Chagua kuwa mahali salama, sio eneo la vita. Upendo unapaswa kuwa zawadi, sio mzigo. Baraka, si laana. Nguvu ya uponyaji, sio chanzo cha majeraha. Je, katika maisha ya mwenzako wewe ni mganga au mharibifu? Unaleta uhai au kisu? Credit Albert Nwosu
    Love
    1
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·857 Visualizações
  • Balozi wa Afrika Kusini Nchini Marekani , Ebrahim Rasool ambaye ametimuliwa na Nchi ya Marekani kutokana na kukosoa sera za Donald Trump, amerejea Afrika Kusini kwa ufakhari mkubwa na kupokewa kwa shangwe na mamia ya Wananchi waliofurika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town Nchini Afrika Kusini.

    Balozi huyo na mkewe, Rosieda, waliwasili jana katika Uwanda wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town baada ya kusafari kutoka Nchini Marekani kupitia Qatar na wamekaribishwa vyema na kwa shangwe na mamia ya Wafuasi wao. Mapema mwezi huu, Balozi Rasool alitangazwa na Serikali ya Marekani kuwa ni Mtu asiyetakiwa kuweko Nchini humo baada ya kukosoa sera za Donald Trump, hatua ambayo inaonesha wazi jinsi madai ya uhuru wa kusema yasivyothaminiwa Nchini Marekani licha ya majigambo makubwa ya Nchi Marekani ya kupigania haki za Binadamu na demokrasia.

    Akiwahutubia mamia ya Mashabiki wake kwenye Uwanja wa Ndege wa Cape Town, Balozi Rasool amesema kwamba ingawa ametakiwa kuondoka huko Marekani lakini jambo hilo limeshindwa kufikia lengo lake kwani Viongozi wa Marekani wanadhani wamemdhalilisha wakati yeye anaona fakhari kwa maneno aliyotoa na Wananchi wa Afrika Kusini nao wanajivunia msimamo huo ndio maana wamejitokea kwa mamia kumpokea kishujaa.

    "Unaporejea nyumbani na kupokewa kwa shangwe na umati kama huu wa watu, mtu unaona fakhari na unajivunia msimamo wako." alisema Rasool.

    Alipoulizwa iwapo diplomasia imeshindwa, amesema ukweli kwamba matamshi yake yamemfanya Trump na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio kuwa makini na hatua ya Serikali ya Marekani ya kumtangaza kuwa ni Mtu asiyetakiwa nchini humo ni ushahidi kwamba ujumbe wake umefika ngazi za juu kabisa za serikali ya Marekani.

    Balozi wa Afrika Kusini 🇿🇦 Nchini Marekani 🇺🇸, Ebrahim Rasool ambaye ametimuliwa na Nchi ya Marekani kutokana na kukosoa sera za Donald Trump, amerejea Afrika Kusini kwa ufakhari mkubwa na kupokewa kwa shangwe na mamia ya Wananchi waliofurika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town Nchini Afrika Kusini. Balozi huyo na mkewe, Rosieda, waliwasili jana katika Uwanda wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town baada ya kusafari kutoka Nchini Marekani kupitia Qatar na wamekaribishwa vyema na kwa shangwe na mamia ya Wafuasi wao. Mapema mwezi huu, Balozi Rasool alitangazwa na Serikali ya Marekani kuwa ni Mtu asiyetakiwa kuweko Nchini humo baada ya kukosoa sera za Donald Trump, hatua ambayo inaonesha wazi jinsi madai ya uhuru wa kusema yasivyothaminiwa Nchini Marekani licha ya majigambo makubwa ya Nchi Marekani ya kupigania haki za Binadamu na demokrasia. Akiwahutubia mamia ya Mashabiki wake kwenye Uwanja wa Ndege wa Cape Town, Balozi Rasool amesema kwamba ingawa ametakiwa kuondoka huko Marekani lakini jambo hilo limeshindwa kufikia lengo lake kwani Viongozi wa Marekani wanadhani wamemdhalilisha wakati yeye anaona fakhari kwa maneno aliyotoa na Wananchi wa Afrika Kusini nao wanajivunia msimamo huo ndio maana wamejitokea kwa mamia kumpokea kishujaa. "Unaporejea nyumbani na kupokewa kwa shangwe na umati kama huu wa watu, mtu unaona fakhari na unajivunia msimamo wako." alisema Rasool. Alipoulizwa iwapo diplomasia imeshindwa, amesema ukweli kwamba matamshi yake yamemfanya Trump na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio kuwa makini na hatua ya Serikali ya Marekani ya kumtangaza kuwa ni Mtu asiyetakiwa nchini humo ni ushahidi kwamba ujumbe wake umefika ngazi za juu kabisa za serikali ya Marekani.
    Love
    Like
    3
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·686 Visualizações
  • USIMSAHAU

    Kabla hajaaga dunia mzee mmoja alimpa maneno ya hekima kwa machozi mtoto wake .Alimuambia haya ,"Mwanangu hali yangu ni mbaya naendea safari ya wasafiri wote duniani lakini ninakuhusia neno hili ,katika maisha yako usije kuwasahau watu wawili wafuatao"

    Wakwanza
    Mwanangu usimsahau mtu yule aliyekaa nawe katika magumu yako.
    Yule aliyesema wewe ni mwema,wengine waliposema wewe ni mbaya.
    Yule aliyesonga mbele akabaki nawe,wengine waliporudi nyuma kuachana nawe.
    Yule uliyemfanyia wema mmoja akautumia huo kupuuza mabaya yako yote.
    Yule ambaye katika giza nene la dhiki zako,akaleta nuru ya faraja ya ulimi wake.
    Yule ambaye katika masika ya mateso yako,alifanyiza hema la mwili wake akukinge usinyeshewe.
    Yule ambaye katika joto kali la kuandamwa na watesi wako alileta baridi kwa tabasamu lake akufariji.
    Yule ambaye kwenye upweke wako ,uwepo wake ukafanyika upo na kundi kubwa.
    USIMSAHAU

    Wapili
    Mwanangu usimsahau mtu aliyekuacha kipindi cha mateso yako.
    Aliyetakiwa akusaidie, akakudhihaki.
    Aliyetakiwa akupe msaada, akageuka mwiba.
    Aliyetakiwa akushukuru akakulaumu.
    Aliyesahau wema wako wote na kukumbuka ubaya wako mmoja.
    Aliyetakiwa akufariji ,akakuletea jeuri.
    Aliyewaona wengine wanakukimbia,akaungana nao.
    Aliyeona upweke wako akakuacha,akijihesabu yeye ni wa muhimu na akuoneshe unamhitaji.
    USIMSAHAU
    Kwaheri mwanangu!!!
    USIMSAHAU😭😭😭 Kabla hajaaga dunia mzee mmoja alimpa maneno ya hekima kwa machozi mtoto wake .Alimuambia haya ,"Mwanangu hali yangu ni mbaya naendea safari ya wasafiri wote duniani lakini ninakuhusia neno hili ,katika maisha yako usije kuwasahau watu wawili wafuatao" Wakwanza Mwanangu usimsahau mtu yule aliyekaa nawe katika magumu yako. Yule aliyesema wewe ni mwema,wengine waliposema wewe ni mbaya. Yule aliyesonga mbele akabaki nawe,wengine waliporudi nyuma kuachana nawe. Yule uliyemfanyia wema mmoja akautumia huo kupuuza mabaya yako yote. Yule ambaye katika giza nene la dhiki zako,akaleta nuru ya faraja ya ulimi wake. Yule ambaye katika masika ya mateso yako,alifanyiza hema la mwili wake akukinge usinyeshewe. Yule ambaye katika joto kali la kuandamwa na watesi wako alileta baridi kwa tabasamu lake akufariji. Yule ambaye kwenye upweke wako ,uwepo wake ukafanyika upo na kundi kubwa. USIMSAHAU Wapili Mwanangu usimsahau mtu aliyekuacha kipindi cha mateso yako. Aliyetakiwa akusaidie, akakudhihaki. Aliyetakiwa akupe msaada, akageuka mwiba. Aliyetakiwa akushukuru akakulaumu. Aliyesahau wema wako wote na kukumbuka ubaya wako mmoja. Aliyetakiwa akufariji ,akakuletea jeuri. Aliyewaona wengine wanakukimbia,akaungana nao. Aliyeona upweke wako akakuacha,akijihesabu yeye ni wa muhimu na akuoneshe unamhitaji. USIMSAHAU Kwaheri mwanangu!!!
    Love
    1
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·671 Visualizações
  • Rais wa Marekani , Donald Trump ametoa siri kuwa Ofisi yake imepokea barua kutoka kwa Rais wa Ukraine , Volodymyr Zelensky, ikisema yuko tayari kwa mazungumzo na Russia na kusaini makubaliano ya madini adimu.

    “Ukraine iko tayari kukaa kwenye meza ya mazungumzo haraka iwezekanavyo ili kuleta amani ya kudumu. Hakuna anayetaka amani zaidi ya Waukraine,” Trump amesema katika hotuba yake bungeni usiku wa kuamkia leo huku akinukuu barua hiyo.

    “Mimi na timu yangu tuko tayari kufanya kazi chini ya uongozi thabiti wa Rais Trump ili kupata amani ya kudumu’,” Trump alinukuu maneno ya Zelenskyy.

    “Si hilo lingekuwa jambo zuri?” aliuliza. “Ni wakati wa kukomesha huu upuuzi. Ni wakati wa kusitisha mauaji. Ni wakati wa kumaliza vita hivi visivyo na maana. Ukitaka kumaliza vita, lazima uzungumze na pande zote mbili,” amesema Trump.

    Kauli hiyo ya Trump imekuja siku chache baada ya mvutano mkali kati yake na Zelenskyy katika Ofisi ya Oval iliyoko Ikulu ya White House, hali iliyosababisha Marekani kusitisha msaada muhimu wa kijeshi kwa Ukraine.

    Rais wa Marekani 🇺🇸, Donald Trump ametoa siri kuwa Ofisi yake imepokea barua kutoka kwa Rais wa Ukraine 🇺🇦, Volodymyr Zelensky, ikisema yuko tayari kwa mazungumzo na Russia 🇷🇺 na kusaini makubaliano ya madini adimu. “Ukraine iko tayari kukaa kwenye meza ya mazungumzo haraka iwezekanavyo ili kuleta amani ya kudumu. Hakuna anayetaka amani zaidi ya Waukraine,” Trump amesema katika hotuba yake bungeni usiku wa kuamkia leo huku akinukuu barua hiyo. “Mimi na timu yangu tuko tayari kufanya kazi chini ya uongozi thabiti wa Rais Trump ili kupata amani ya kudumu’,” Trump alinukuu maneno ya Zelenskyy. “Si hilo lingekuwa jambo zuri?” aliuliza. “Ni wakati wa kukomesha huu upuuzi. Ni wakati wa kusitisha mauaji. Ni wakati wa kumaliza vita hivi visivyo na maana. Ukitaka kumaliza vita, lazima uzungumze na pande zote mbili,” amesema Trump. Kauli hiyo ya Trump imekuja siku chache baada ya mvutano mkali kati yake na Zelenskyy katika Ofisi ya Oval iliyoko Ikulu ya White House, hali iliyosababisha Marekani kusitisha msaada muhimu wa kijeshi kwa Ukraine.
    Like
    1
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·488 Visualizações
  • BOT INAYO DOWNLOAD NYIMBO haraka na kwa mbs kidogo

    Hii ni bot ya telegram ambayo unaipatia maneno kidogo ya muziki unayukumbka inakuletea ngoma nzima pia unaweza kuipa hata sauti ikakuletea wimbo wako, hii inatumika Kudowload nyimbo ni kama shaazam
    Link yake hii hapa https://t.me/Waduduu_musicBot

    Au ingia telegram search Wadudu_musicBot
    BOT INAYO DOWNLOAD NYIMBO haraka na kwa mbs kidogo Hii ni bot ya telegram ambayo unaipatia maneno kidogo ya muziki unayukumbka inakuletea ngoma nzima pia unaweza kuipa hata sauti ikakuletea wimbo wako, hii inatumika Kudowload nyimbo ni kama shaazam Link yake hii hapa https://t.me/Waduduu_musicBot Au ingia telegram search Wadudu_musicBot
    0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·569 Visualizações
  • Ijumaa, tarehe 28 Februari, haikuwa siku rahisi kwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alipofanya ziara katika Ikulu ya White House, Marekani. Kabla hata ya mzozo wa maneno kati yake na mwenyeji wake, Rais Donald Trump, pamoja na Makamu wa Rais JD Vance, tayari kulikuwa na ishara za mivutano.

    Trump alimkaribisha Zelensky mlangoni na kusema kwa utani: “Leo amevalia kweli kweli,” kauli ambayo iliwafanya baadhi ya waandishi wa habari kuiona kama kejeli badala ya pongezi. Wakati huo, Zelensky alikuwa amevalia fulana nyeusi ya mikono mirefu, vazi ambalo amekuwa akilivaa mara kwa mara tangu Ukraine ivamiwe na Urusi mwaka 2022.

    Baadaye, Trump alipompokea Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, alionekana kutazama mavazi yake kwa makini kutoka juu hadi chini, kisha kunong’ona maneno yanayoweza kutafsiriwa kama pongezi kwa suti rasmi aliyovaa Starmer.

    Mjadala kuhusu mavazi ya Zelensky ulizidi kupamba moto wakati wa mkutano wa waandishi wa habari. Brian Glenn, mwandishi kutoka Real America’s Voice—chombo cha habari kinachopendelea mrengo wa kulia—alimtupia swali la moja kwa moja:

    “Kwa nini hauvai suti? Upo katika ofisi ya juu kabisa katika nchi hii, na umegoma kuvaa suti – je, unamiliki hata suti?”

    Kwa utulivu, Zelensky alijibu kwa mshangao mdogo:

    “Nitavaa suti vita hivi vitakapomalizika. Labda suti kama yako, labda bora zaidi, au pengine ya bei nafuu kuliko yako,” alisema kwa utani huku akionyesha msimamo wake wa kuendelea kuvaa mavazi ya kijeshi.

    Swali hilo la Glenn liliibua mjadala mkali mitandaoni. Wengine walimuunga mkono, wakisema kwamba kiongozi wa taifa anapaswa kuvaa mavazi rasmi anapokutana na viongozi wengine, ilhali wengine waliona swali hilo kuwa la dhihaka na lisilo na umuhimu.

    Miongoni mwa waliomkosoa Glenn ni mwandishi maarufu wa Uingereza, Piers Morgan, ambaye pia ni rafiki wa karibu wa Trump. Morgan aliandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter):

    “Swali la kipuuzi. Elon Musk havai suti anapoingia Ikulu.”

    Historia pia inaonyesha kuwa si Zelensky pekee aliyeingia Ikulu ya Marekani bila suti. Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Winston Churchill, alifanya hivyo katika moja ya ziara zake rasmi.
    Ijumaa, tarehe 28 Februari, haikuwa siku rahisi kwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alipofanya ziara katika Ikulu ya White House, Marekani. Kabla hata ya mzozo wa maneno kati yake na mwenyeji wake, Rais Donald Trump, pamoja na Makamu wa Rais JD Vance, tayari kulikuwa na ishara za mivutano. Trump alimkaribisha Zelensky mlangoni na kusema kwa utani: “Leo amevalia kweli kweli,” kauli ambayo iliwafanya baadhi ya waandishi wa habari kuiona kama kejeli badala ya pongezi. Wakati huo, Zelensky alikuwa amevalia fulana nyeusi ya mikono mirefu, vazi ambalo amekuwa akilivaa mara kwa mara tangu Ukraine ivamiwe na Urusi mwaka 2022. Baadaye, Trump alipompokea Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, alionekana kutazama mavazi yake kwa makini kutoka juu hadi chini, kisha kunong’ona maneno yanayoweza kutafsiriwa kama pongezi kwa suti rasmi aliyovaa Starmer. Mjadala kuhusu mavazi ya Zelensky ulizidi kupamba moto wakati wa mkutano wa waandishi wa habari. Brian Glenn, mwandishi kutoka Real America’s Voice—chombo cha habari kinachopendelea mrengo wa kulia—alimtupia swali la moja kwa moja: “Kwa nini hauvai suti? Upo katika ofisi ya juu kabisa katika nchi hii, na umegoma kuvaa suti – je, unamiliki hata suti?” Kwa utulivu, Zelensky alijibu kwa mshangao mdogo: “Nitavaa suti vita hivi vitakapomalizika. Labda suti kama yako, labda bora zaidi, au pengine ya bei nafuu kuliko yako,” alisema kwa utani huku akionyesha msimamo wake wa kuendelea kuvaa mavazi ya kijeshi. Swali hilo la Glenn liliibua mjadala mkali mitandaoni. Wengine walimuunga mkono, wakisema kwamba kiongozi wa taifa anapaswa kuvaa mavazi rasmi anapokutana na viongozi wengine, ilhali wengine waliona swali hilo kuwa la dhihaka na lisilo na umuhimu. Miongoni mwa waliomkosoa Glenn ni mwandishi maarufu wa Uingereza, Piers Morgan, ambaye pia ni rafiki wa karibu wa Trump. Morgan aliandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter): “Swali la kipuuzi. Elon Musk havai suti anapoingia Ikulu.” Historia pia inaonyesha kuwa si Zelensky pekee aliyeingia Ikulu ya Marekani bila suti. Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Winston Churchill, alifanya hivyo katika moja ya ziara zake rasmi.
    Like
    Love
    2
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·790 Visualizações
  • Nikueleze kwa kifupi sana kiini cha mgogoro. Kabla ya mwaka 1991 Ukraine ilikua sehemu ya Urusi kupitia muungano wa kisovieti wa USSR. Baada ya USSR kufa ndipo taifa la Ukraine likazaliwa pamoja na mataifa mengine 14 yaliyokua majimbo ya Urusi.

    Lakini usisahau mwaka 1949 umoja wa kujihami wa nchi za magharibi (NATO) ulianzishwa dhidi ya Urusi (USSR). Makubaliano yao ni kwamba ikiwa Urusi itamgusa mmoja wao basi wote watamvamia. Marekani akiwa kinara.

    Kuanguka kwa USSR kukafanya mataifa 15 mapya kuzaliwa. Baadhi ya Mataifa hayo yakawa na hofu kuwa Urusi inaweza kurudi kuyakalia kimabavu. Kwahiyo yakaomba kujiunga NATO kwa usalama wao. Estonia, Latvia na Lithuania zikapata uanachana wa NATO chap kwa haraka. Ukraine ilipoomba uanachama Urusi ikakataa, kwa sababu ya strategic position ya Ukraine ambayo inaiweka Urusi hatarini.

    Ukraine ilipokosa uanachama NATO ikamua kujilinda kwa kusuka mpango wa nyuklia. Marekani na Urusi zikashtuka. Kwa kutambua hatari ya nyuklia zikamsihi sana Ukraine aachane na mpango huo. Mwaka 1994 ukaandaliwa mkataba uitwao Budapest memorundum, huko Hungary. Mkataba huo ulihusisha nchi 4. Urusi na Ukraine zilisaini kwamba hakuna atakayemvamia mwenzake. Marekani na Uingereza zikasaini kwamba atakayemvamia mwenzake watampiga bila huruma. Pia Marekani na Uingereza zitagharamia fedha na vifaa vyote vya vita. Mkataba ukasainiwa na Ukraine ikasitisha mpango wake wa nyuklia.

    Lakini Mwaka 2014 Urusi ikaivamia Ukraine na kuchukua jimbo lake la Crimea kimabavu. Marekani na Uingereza hazikuipiga Urusi kama mkataba wa Budapest unavyosema. Ukraine akalalamika lakini akapuuzwa. Kwenye vita inayoendelea sasa, Urusi ameshajitwalia majimbo manne Donetsk, Luhansk, Zaporizhzhia na Kherson lakini Marekani na Uingereza ziko kimya.

    Ukraine inaona imesalitiwa. Mkataba wa Budapest ulikua kiini macho. Laiti Ukraine ingekataa kusaini na kuendelea na mpango wake wa nyuklia, leo Urusi isingethubutu kuigusa. Lakini Waliomdanganya sasa wamemgeuka na wanamfokea. Ukraine ingeyajua maneno ya Mzee Jomo Kenyatta "Learn to fight your own battle" isingeachana na mpango wake wa nyuklia mwaka 1994. Wangejifunza kupigana vita yao wenyewe bila kutegemea mtu.!
    (Malisa GJ)

    Nikueleze kwa kifupi sana kiini cha mgogoro. Kabla ya mwaka 1991 Ukraine ilikua sehemu ya Urusi kupitia muungano wa kisovieti wa USSR. Baada ya USSR kufa ndipo taifa la Ukraine likazaliwa pamoja na mataifa mengine 14 yaliyokua majimbo ya Urusi. Lakini usisahau mwaka 1949 umoja wa kujihami wa nchi za magharibi (NATO) ulianzishwa dhidi ya Urusi (USSR). Makubaliano yao ni kwamba ikiwa Urusi itamgusa mmoja wao basi wote watamvamia. Marekani akiwa kinara. Kuanguka kwa USSR kukafanya mataifa 15 mapya kuzaliwa. Baadhi ya Mataifa hayo yakawa na hofu kuwa Urusi inaweza kurudi kuyakalia kimabavu. Kwahiyo yakaomba kujiunga NATO kwa usalama wao. Estonia, Latvia na Lithuania zikapata uanachana wa NATO chap kwa haraka. Ukraine ilipoomba uanachama Urusi ikakataa, kwa sababu ya strategic position ya Ukraine ambayo inaiweka Urusi hatarini. Ukraine ilipokosa uanachama NATO ikamua kujilinda kwa kusuka mpango wa nyuklia. Marekani na Urusi zikashtuka. Kwa kutambua hatari ya nyuklia zikamsihi sana Ukraine aachane na mpango huo. Mwaka 1994 ukaandaliwa mkataba uitwao Budapest memorundum, huko Hungary. Mkataba huo ulihusisha nchi 4. Urusi na Ukraine zilisaini kwamba hakuna atakayemvamia mwenzake. Marekani na Uingereza zikasaini kwamba atakayemvamia mwenzake watampiga bila huruma. Pia Marekani na Uingereza zitagharamia fedha na vifaa vyote vya vita. Mkataba ukasainiwa na Ukraine ikasitisha mpango wake wa nyuklia. Lakini Mwaka 2014 Urusi ikaivamia Ukraine na kuchukua jimbo lake la Crimea kimabavu. Marekani na Uingereza hazikuipiga Urusi kama mkataba wa Budapest unavyosema. Ukraine akalalamika lakini akapuuzwa. Kwenye vita inayoendelea sasa, Urusi ameshajitwalia majimbo manne Donetsk, Luhansk, Zaporizhzhia na Kherson lakini Marekani na Uingereza ziko kimya. Ukraine inaona imesalitiwa. Mkataba wa Budapest ulikua kiini macho. Laiti Ukraine ingekataa kusaini na kuendelea na mpango wake wa nyuklia, leo Urusi isingethubutu kuigusa. Lakini Waliomdanganya sasa wamemgeuka na wanamfokea. Ukraine ingeyajua maneno ya Mzee Jomo Kenyatta "Learn to fight your own battle" isingeachana na mpango wake wa nyuklia mwaka 1994. Wangejifunza kupigana vita yao wenyewe bila kutegemea mtu.! (Malisa GJ)
    Like
    1
    · 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·897 Visualizações
Páginas impulsionada