DUNIA NA MAAJABU YAKE
(Muundo wa Dunia na Maajabu Yaliyomo)
1. UMRI WA DUNIA
HII Dunia yetu ina historia ndefu mno tangu ilipojiunda angani, miaka takribani bilioni 4.5 iliyopita.
Tarakimu za umri huo wa miaka bilioni 4.5 ni 4,500,000,000, yaani miaka milioni elfu nne na mia tano iliyopita.
Dunia ambayo kwa lugha ya Kiingereza inafahamika vyema kwa jina la 'Earth', pia hujulikana kama 'the World', ikimaanishwa ulimwengu.
Aidha, Dunia ni sayari pekee kwenye himaya ya sayari zilizopo chini ya jua ambayo jina lake halitokani na majina ya "Miungu wa Dola" ya Kigiriki au ya Kirumi.
Asili ya jina la 'earth' ni 'erde' lenye asili ya nchini Ujerumani, na maana yake ni udongo au ardhi.
Mpaka kuweza kupata umri huo wa dunia wanasayansi walifanya kazi ya kutafiti na kisha kuwasilisha matokeo yao kwenye makongamano ya kisayansi duniani, ambapo matokeo hayo yalijadiliwa kwa kina na hatimaye kukubalika kama hivi.
Kumbuka katika majadiliano hayo huwepo mivutano mikali miongoni mwa wanasayansi waalikwa, ambapo pia jopo la wanasayansi wanaowasilisha utafiti husika hujikuta wakitakiwa kujibu hoja mbalimbali za wanasayansi wenzao.
Kuna wakati baadhi ya matokeo ya tafiti kadhaa hukataliwa, huku watafiti husika wakitakiwa kurejea upya tafiti zao.
Wanasayansi hupata umri wa sayari kwa kupima umri wa miamba ya sayari husika, ambapo mwamba wenye umri mkubwa zaidi kuliko miamba yote ndiyo huchukuliwa kuwa umri wa sayari husika.
Itakumbukwa kuwa Msahafu wa Biblia (Sura ya Mwanzo 1) husimulia jinsi Mwenyezi Mungu alivyoumba "mbingu na nchi na vyote vilivyomo kwa siku 6," lakini pia Msahafu huohuo kwenye aya zingine hueleza kuwa miaka elfu moja ya duniani yaweza kuwa sawa na siku moja kwenye ya Makazi ya Mwenyezi Mungu.
Ni dhahiri kuwa binadamu tukiwa hatuna hoja sahihi kwa maelezo ya aina hiyo, ndipo tunaona ni vyema mambo ya Mwenyezi Mungu kumwachia Yeye Mwenyewe Mwenyezi Mungu.
2. KUUMBIKA DUNIA, SAYARI, JUA, NYOTA
Kimsingi, Dunia kama zilivyo sayari zingine zote ilijiunda kutokana na mabaki ya vitu vilivyotumika kuunda Jua.
Jua ambalo ni nyota kama zilivyo nyota zote angani, lilijiunda lenyewe kwenye eneo la anga lijulikanalo kama 'Pillars of Creation' (nguzo za uumbaji) katika ukanda wa anga wenye upana ambao huonekana kutokuwa na mwisho.
Ukanda huo ujulikanao kama 'Solar Nebula,' umegubikwa na mawingu ya vumbi la huko angani pamoja na aina mbalimbali za gesi na hewa, ikiwemo haidrojeni na heliumu.
'Solar' ni jina la nishati itokanayo na joto la jua, na 'Nebula' kwa lugha ya Kilatini ni "wingu" au vumbi la gesi asilia mithili ya ukungu.
Hivyo, 'Solar Nebula' ni ukanda katika anga ya mbali wenye mawingu yaliyosheheni nishati yenye joto, sawa na nishati ya joto la jua.
Sasa basi, tunafahamu vyema kuwa jua hutoa mionzi hatari yenye joto kali mithili ya moto mkali, na ambayo ikiboreshwa kisayansi pia huweza kutoa nishati ya umeme.
Hivyo, kwa muktadha huo, hebu ngoja sasa tuleta pamoja hewa za gesi, zikiwemo haidrojeni na heliumu, mawingu yenye nishati ya umeme wa jua, vumbi la angani na tufani itokanayo na mchafuko mbaya wa hali ya hewa huko anga za mbali.
Na ili kuweza kupata matokeo yanayotakiwa, hebu pia tutambue uwepo wa nguvu kubwa ya asili katika kiwango kijulikanacho kwa jina la "Supernatural Power", ambayo ndiyo huwa kisababishi cha mambo yote.
Kisayansi, "Supernatural Power" ni nguvu kubwa ya asili ambayo huendesha mifumo mbalimbali ya asili, ambapo duniani nguvu hiyo hujulikana kama Nguvu ya Mungu.
Nguvu asili hiyo, yaani Supernatural Power, husababisha tufani ambayo huvurumisha kwa pamoja vitu vyote hivyo, (gesi, hewa, mawingu yenye nishati ya joto na vumbi la angani) ili kuunda tufani yenye umbo la duara.
Duara hiyo ni kama ile itokanayo na kimbunga kikali duniani, na ambacho sasa tutaona kikifungamanisha pamoja vitu vyote hivyo katika mchafuko mkubwa wa hali mbaya ya hewa.
Natumia maneno ya msisitizo kuelezea "ukubwa" wa mchafuko huo wa hali ya hewa katika eneo hilo la anga, kwani katika kuunda sayari au nyota nguvuasili kubwa hutumika.
Aidha, tufani hiyo ya duara itakayoanza kidogo kidogo kama kimbunga kikali, itazidi kukua hadi kuwa na kipenyo cha takribani kilomita 10 hadi 200 au zaidi na kwendelea.
Tufani hiyo ndiyo itavurumisha kwa pamoja gesi na hewa za naitrojeni na heliumu, mawingu ya nishati ya joto na vumbi la angani (kama kifanyavyo kimbunga kikali katika eneo tambarare la duniani).
Pia, wakati mchafuko huo wa hali mbaya ya hewa ukiendelea, hebu ngoja sisi watazamaji tujibanze mahali fulani kwa mbali kushuhudia duara hiyo ya tufani ikijizungusha yenyewe bila kukoma kwa kipindi cha miaka mingi.
Kitakachofuata ni kuanza kuona kiini cha moto kikianza kujiunda katikati ya duara hiyo ya tufani kali, huku pia nje ya duara hiyo vitu kibao vikivutwa kujiunga na mzunguko wa hiyo tufani ya duara.
Vitu hivyo ni pamoja na vumbi zaidi la angani, na gesi zaidi zenye joto kali.
Wakati huohuo kipenyo na mzingo wa duara hiyo vitazidi kuongezeka upana na ukubwa, mfano wa duara yenye umbo sawa na la mpira mkubwa wa miguu.
Hivyo, baada ya miaka takribani milioni moja tutashangaa kuona lile vumbi likigeuka taratibu kuwa miamba ya moto ndani ya kiini cha tufani hiyo ya duara.
Miamba hiyo ni kutokana na lile vumbi la angani ambalo hatimaye limeshikamana pamoja mithili ya zege, na hatimaye kuwa miamba ndani ya tufani ya duara.
Sanjari na kuundika huko ndani ya kitovu cha hiyo tufani ya duara, pia kwelekea nje ya duara hiyo utaundika udongo ambao ardhi, mchanga na mawe.
Kimsingi, vitu hivyo pia ni matokeo ya lile vumbi la angani ambalo lilikusanywa pamoja na kuvutwa na kasi ya mzunguko wa tufani.
Hatua hiyo mpya inatokana na kuwepo mshikamano na mgandamizo wa zile chembechembe za lile vumbivumbi ndani ya tufani.
Vurumai hiyo ya mzunguko wa hiyo tufani ya duara yenye vumbi, itazidi kukua hadi kuunda sumaku ya asili ndani ya kile kitovu cha duara ya tufani.
Kutokana na duara hiyo ya tufani kuongezeka ukubwa, hatimaye sumaku iliyopo kwenye kitovu cha duara hiyo itaishiwa nguvu ya kwendelea kunasa vumbi zaidi kuja kwenye mzingo wa hiyo duara ya tufani.
Kumbuka kuwa wakati huo hiyo duara pia itaunda kimo kutoka kwenye usawa wa ardhi yake kwenda ndani kwenye kitovu chake, na hivyo kuwa duara ya mviringo kama umbo mfano wa mpira mchezo wa miguu.
Baada ya kupita maelfu ya miaka mingi, duara hiyo ambayo hapo awali ilianza kama umbo la tufani na kuzidi kukua huko angani, sasa itakuwa na joto kali kupita kiasi na kuanza kung'aa kama jua.
Jua hilo, ndiyo nyota mojawapo ya zile ambazo huonekana usiku ziking'aa angani.
Lakini pia wakati wa kujiunda nyota hiyo, kama tulivyoona hapo awali, baadhi ya mabaki yake yaliyokuwa yakitawanyika angani wakati ile tufani ya duara ikijizungusha, huweza kujikusanya pamoja na kuunda sayari ambazo huzunguka baadhi ya hizo nyota.
Hivyo ndivyo zilivyojiunda sayari zote ambazo huelea kwa kulizunguka jua letu.
Mathalani, sayari zote ambazo hulizunguka jua, ikiwemo dunia zilijiunda kutokana na mabaki ya vitu kama gesi, michanga na mawe ambavyo vilitawanyika angani wakati jua likijiunda (kama ambavyo imeelezwa hapo awali).
3. KIINI CHA DUNIA
Dunia yetu ambayo wastani wa nusu kipenyo cha umbo lake la duara ni kilomita 6,371, mzingo wake ni kilomita takribani 40,041.
Kama zilivyo sayari zote katika himaya ya jua, dunia nayo ilijiunda wakati jua likijiunda lenyewe.
Yaani kwamba sayari ni mabaki ya vitu vilivyotumika kuliunda jua.
Kadhalika kama zilivyo sayari zingine zote, dunia nayo ina kiini chake ambacho kipo katikati ya ardhi yake.
Kiini hicho kina nguvu kubwa ya sumaku ambayo, pamoja na mambo mengineyo, 'huvuta' umbo hilo la duara kutoka juu ya ardhi kwenda katikati ya kiini hicho.
Muundo huo ndio hulifungamanisha pamoja umbo la duara la dunia, na hivyo kuzuia umbo hilo lisifumke kutoka ardhini na kusambaratika.
Hiyo ni sawa na mpira wa miguu unavyoweza kupasuka na kusambaratika, kama utajazwa upepo kupita kiasi chake.
Kiini hicho ambacho kipo katikati kabisa ya dunia, kinajulikanacho kwa jina la kisayansi la 'Inner Core.'
Kiini hicho kina joto kali la sentigredi 6,230 ambacho ndio kiasi cha joto la jua.
Kiini hicho kina umbo la duara lenye nusu kipenyo cha kilomita 1,250.
Kama ingetokea kuchimba ardhi wima kwenda kwenye kiini hicho, mchimbaji angeanza kukutana na joto la kiini hicho kuanzia kimo cha umbali wa kilomita 5,150 kutoka usawa wa juu ya ardhi tunayotembea.
Katika historia ya uchimbaji ardhi, kina kirefu kilichowahi kuchimbwa ardhini ni mita 12,345 (kilomita 12.345) huko Sakhalini, nchini Urusi, kwa ajili ya uvunaji wa mafuta ya petroli.
Kiini cha dunia kinaundwa na madini mchanganyiko wa nikeli (nickle), chuma (iron) na dhahabu.
Kwa mujibu wa utafiti, inakadiriwa kuwa kama dhahabu hiyo ingechimbwa na kuchomwa mpaka kuwa kimiminika sawa na uji na kisha kumwagwa chini, ingeweza kuifunika dunia yote kwa unene wa sentimeta 45.
Kiini hicho muhimu kwa uhai wa sayari hii ya dunia kiligunduliwa mwaka 1936 na mtaalamu wa matetemeko ya ardhi wa nchini Denmark, mwanamama Dkt. Inge Lehmann.
Dkt. Lehmann alihitimu shahada yake ya kwanza katika fani ya Hisabati mwaka 1910, ya Uzamili mwaka 1920 (zote kutoka Chuo Kikuu cha Copenhagen nchini mwake), na ile ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge nchini Uingereza.
Alifariki kwa uzee mwaka 1993 akiwa na umri wa miaka 104.
4. MAJI DUNIANI
Kupatikana maji kwenye dunia yetu, ni mojawapo ya miundo ambayo haipo katika sayari zingine ambazo tuna taarifa za kitafiti kuzuhusu.
Maji ni muhimili muhimu kwa ajili ya uhai wa viumbe wote na mimea, ambavyo kwa pamoja havipo katika sayari zingine za himaya ya jua.
Kwa mujibu wa tafiti nyingi ambazo zimefanyika kwa miongo mingi ya miaka kujaribu kubaini nini chanzo cha kuwepo maji duniani, hakuna hata utafiti mmoja ulioonesha kwa usahihi matokeo ya kuridhisha.
Miongoni mwa tafiti hizo ni pamoja na ule wa mwaka 2005, ambapo Mkuu wa Idara ya Masomo ya Sayari na Mwezi katika Chuo Kikuu cha Arizona nchini Marekani, Profesa Michael Julian Drake, na mwenzake ambaye ni mtaalamu wa Vimondo, Dkt. Huberto Campins, wa Chuo Kikuu cha Central Florida, walitafiti nini chanzo cha kuwepo maji duniani.
Katika mawasilisho yao kwenye kongamano la kisayansi la Chama cha Wanataaluma wa Maarifa ya Anga za Juu (IAU), watafiti hao walikanusha madai ya uwezekano wa dunia hapo kale kugongwa na kimondo kikubwa na kusababisha maji kulipuka kutoka ardhini.
Wakiwasilisha matokeo ya utafiti wao kwenye mkutano wa kongamano hilo, magwiji hao wa masuala ya sayari walieleza kwenye waraka wao uitwao "Origin of water on the terrestial planets" (chanzo cha kuwepo maji kwenye sayari).
Walidai kuwa maji yaliyopo duniani yaliumbika kwenye ardhi ya dunia tangu mwanzo, wakati ikijiunda angani.
Ikumbukwe kuwa eneo la uso wa dunia likiwa ni jumla ya kilomita za mraba milioni 510, asilimia 70.8 ya eneo hilo imefunikwa na maji na asilimia 29.2 ni nchi kavu, ikiwemo milima, mabonde na ardhi tambarare.
5. HEWA YA OKSIJENI
Muundo mwingine muhimu katika sayari hii ya dunia ni hewa ambazo ni tawala, yaani Naitrojeni ambayo kwa usahihi imeenea kwa asilimia 78.08 ya hewa yote ya dunia, Oksijeni asilimia 20.95, 'Argon' asilimia 0.93, hewa ya Ukaa (Carbon dioxide) asilimia 0.039, na asilimia moja ni hewa mithili ya mvuke wa maji (water vapour).
Hewa ya Oksijeni ambayo ni nguzo muhimu kwa ajili ya uhai wa viumbe wote na pia haipatikani kwenye sayari nyingine chini ya jua, inadhaniwa ilianza kupatikana duniani miaka takribani bilioni 2.5 iliyopita kufuatia "kukomaa kwa kiini cha dunia."
Kwa mujibu wa matokeo ya tafiti mbalimbali na nadharia za kisayansi, inaoneshwa kuwa kukomaa kwa kiini hicho cha dunia hatimaye ndiko kulisababisha kuzuka duniani milipuko ya volikano ambayo pia ilisababisha kuzuka mabonde na milima.
Inaoneshwa kuwa tayari wakati huo maji yaliishakuwepo duniani, na kuwezesha kuzuka chembechembe ndogo sana za kibakteria zijulikanazo kwa jina la kisayansi la 'cyanobacteria' au 'blue-green algae'.
Kwa kutumia mwanga wa jua, maji na hewa ya ukaa, chembechembe hizo ziliweza kuzalisha hewa mbalimbali, ikiwemo 'Carbonhydrates' na Oksijeni.
Kwa kuwa hizo chembechembe ndogo za kibakteria huishi baharini, ilikuwa rahisi kwa oksijeni kutokea baharini kupepea na kuenea katika anga ya dunia na kuzuiliwa hapo na nguvu asili ya uvutano ya dunia ili pia ibaki ikienea pote duniani.
Mpaka wakati wa kuzuka duniani mimea na viumbe hai miaka takribani bilioni 3.5 iliyopita, tayari oksijeni ilikwa ni tele duniani; na hivyo kutumika kudumisha uhai wa viumbe hadi wakati huu.
6. UKANDA WA 'OZONE'
Muundo mwingie muhimu wa asili kwa dunia ni ukanda wa anga ujulikanao kwa jina la 'ozone' ambao umetanda kama 'mwavuli' kwenye anga ya dunia, na kuikinga isidhuriwe na mionzi hatari ya sumu kutoka kwenye Jua.
Ukanda huo maarufu kama 'ozone layer' umetanda kuanzia usawa wa kilometa 15 kutoka ardhini kwenda juu angani mpaka ukomo wa kilomita takribani 50, ambapo huchuja asilimia kati ya 97 na 99 ya mionzi hatari kwenye miale ya joto la jua.
Miongoni mwa matatizo yanayosababishwa na mionzi hiyo hatari kutoka kwenye jua, ni pamoja na magonjwa ya saratani ya ngozi kwa bianadamu.
Pia juu ya ukanda wa tabaka la ozone kuna ukanda mwingine uitwao "atmosphere" ambao ni madhubuti kiasi kwamba vitu vinavyotoka anga za juu na kujaribu kuupenya ili kufika duniani, hukumbana na joto kali na kusambaratishwa kwa kuunguzwa.
Si kwamba tabaka hilo lina joto, isipokuwa kasi ya "kuanguka" vitu hivyo kutoka juu angani kuja dunia husababisha msuguano na chembechembe za gesi katika eneo hilo na kuzalisha joto mithili ya ndimi za moto.
Picha za video za vyombo vya 'Apollo' vikirejea duniani kutoka mwezini vikiwa na wanaanga ndani yake na kupenya tabaka hilo kwa kasi ya kilomita 39,000 kwa saa, huonekana kughubikwa na ndimi za moto wa rangi ya njano na bluu.
Rangi hizo ni ishara ya ukali wa moto huo, lakini kutokana na waundaji wa vyombo hivyo kutumia mchanganyiko wa mabati na plastiki ngumu visivyopenywa na joto, Apollo huonekana kulichana tabaka hilo na kutokea upande wa pili ambao ni anga ya dunia.
Hivyo basi, mfano huo mdogo unaonesha uimara wa tabaka hilo la 'ozone', ambalo kama ambavyo tumeona huchuja mionzi ya sumu kutoka kwenye mwanga wa jua ili kutolete madhara kwa viumbe duniani.
Mwanga huo ukisafiri kutoka juani umbali wa kilomita milioni 150 kwa kasi ya kilomita 299,793, hutua duniani ndani ya dakika 8 na sekunde 19 ukiwa tayari umechujwa wakati ukipenya tabaka hilo.
'Ozone' iligunduliwa mwaka 1913 na wanasayansi wawili wa nchini Ufaransa, Charlest Fabry na Henri Buisson, ambapo kipimo cha kasi ya mwanga kiligunduliwa na mwanasayansia wa anga za juu wa nchini Denmark, Ole Roemer, mwaka 1676.
7. NGUVU ASILI YA UVUTANO
Muundo mwingine wa dunia ni nguvu ya asili ya uvutano ya dunia, maarufu kama 'gravitation', ambayo huvuta vitu kuvirejesha chini duniani pale vinaporushwa kwenda juu au vile vinavyoanguka kutoka juu angani.
Nguvu hiyo ina manufaa makubwa, kwani bila kuwepo duniani binadamu na viumbe wengine wangepeperuka kama karatasi kwenda juu wakati wakitembea juu ya ardhi ya hii.
Kadhalika, nguvu hiyo husaidia kuvuta hewa ya oksijeni na kuiweka karibu na ardhi kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Pia, nguvu hiyo husaidia kuiweka dunia, mwezi, jua na sayari zingine katika uwiano wa umbali usio na madhara kutoka kila moja.
Nguvu hiyo ya asili ndiyo huliweka joto la jua duniani na kubaki kuwa katika kiwango kinachotakiwa, na hivyo kuwezesha viumbe kupata joto la wastani na pia katika kiwango mwanana.
Nguvu hiyo huvuta mvua kuja duniani na kuwezesha maji ya bahari, maziwa na mito kutulia duniani.
Mathalani, bila nguvu asili hiyo kuwepo duniani, maji 'yangemwagika' kutoka duniani kwa kutawanyika kama upepo na kupaa kwenda juu angani na kutoweka kabisa.
Na ndio maana ukirusha maji kwenda juu, hurudi chini ardhini.
Hebu angalia mfano huu kwamba wanaanga waliokwenda mwenzini walilazimika kuvaa mavazi yenye uzito wa kilo 80 hapa duniani, lakini mavazi hayo kule mwezini yakawa na uzito wa kilo 3.
Mavazi hayo, yaani viatu, koti, suruali, na kofia nzito yenye miwani maalumu ya kukinga macho dhidi ya mionzi hatari ya jua, vyote kwa pamoja viliunganishwa na kuwa mfano wa sare za 'ovaroli' za mafundi wa magari.
Mavazi hayo pia mgongoni yakiwa yameunganishwa kwa pamoja na mtungi wa hewa ya oksijeni kwa ajili ya kupumua, yalivaaliwa mahsusi muda mfupi baada ya chombo kutua mwezini.
Hivyo, msomaji wangu tafakari nini kilisababisha mavazi kuwa mazito hapa duniani, lakini yawe mepesi kule mwezini?
Jibu ni kwamba nguvu asili ya uvutano hapa duniani ni kubwa kuliko ya kule mwezini.
Na ndipo tunaona umuhimu wa muundo huo wa nguvu asili ya uvutano, ambapo hapa duniani huvuta vitu kuja chini kwa kasi ya mita 9.81 kwa sekunde, lakini kwa kuwa nguvu ya mwezi ni hafifu, huvuta vitu kwa kasi ndogo ya mita 1.62 kwa sekunde.
Ingawa nguvu hiyo ya asili iligunduliwa kuwepo duniani miaka mingi iliyopta, mwanafizikia bingwa wa Uingereza, Sir Isaac Newton (1642-1727), ndiye anatambulika kama mgunduzi wa hesabu hizo za nguvu asili hiyo.
Anaeleza kuwa vitu vyote vyenye maumbo asili, ikiwemo jua, sayari, dunia, mwezi, na vimondo, kila kimoja kina nguvu hiyo katika viwango tofauti.
Kanuni hiyo, kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wake, hueleza kuwa nguvu hiyo ndiyo hufanya jua kuvuta sayari zake ili kulizunguka, huku pia kila sayari ikitumia nguvu 'binafsi' (na kwa uwiano maalumu) kujihami isivutwe hadi kwenda kuligonga jua au kugongana na sayari zingine au vimondo.
Nguvuasili ya jua ni mita 274 kwa sekunde, ikiwa ni zaidi ya kiasi cha nguvuasili ya kila sayari.
Muundo huo wa kila sayari kujihami kivyake katika mstari wa njia yake hufahamika kisayansi kama "sayari kuhami mazingira ya njia yake"; yaani kwamba 'a planet has to clear the neighbourhood around its orbit.'
Newton akiwa amezaliwa 'mtoto-njiti' na baadaye kuibuka kuwa mwenye akili nyingi kiasi cha kukaribia kuwa sawa na mtu wa miujiza, hakuwahi kuoa kutokana na kinachoelezwa kuwa ni " kutokana na kutingwa na shughuli za kimasomo."
Huoneshwa kuwa muda mwingi alikuwa maabara akifanya tafiti mbalimbali za kisayansi, au akiwa maktaba akijisomea, ama akiandika kitabu, au akifundisha wanafunzi wake.
Alikuwa bingwa mwenye kipaji cha taaluma nyingi, ikiwemo Fizikia, Kemia, Hisabati, Maarifa ya Anga za Juu, Uchumi, Falsafa, na Theolojia ambayo ni taaluma ya masuala ya kiroho.
Kwa mujibu wa historia, mwanasayansi huyo gwiji wa kuigwa alihitimu shahada zake zote mbili za sayansi, yaani 'Bachelor' na 'Masters', mwaka 1665 na 1668 katika Chuo Kikuu cha Cambridge, nchini Uingereza.
Akiwa na umri wa miaka 84, mwanasayansi huyo anayedhaniwa na wengi kuwa bingwa wa hesabu za kisayansi kuliko wote duniani, alifariki mwaka 1727 akiwa usingizini.
Ripoti ya uchunguzi wa mwili wake huonesha kuwa alikuwa na tatizo la figo, lakini pia alikutwa na kiasi kingi cha zebaki.
Zebaki hiyo, yamkini, ni kutokana na kudumu mno kwenye maabara za Kemia na Fizikia, ambazo hutumia kemikali aina mbalimbali, zikiwemo hewa za gesi, katika kufanya majaribio ya kisayansi.

·68 Views